Na Moshy Kiyungi
Muziki wa Country hapa nchini si maarufu sana kama ilivyo mingine. Naandika makala haya huku nafsi ikinisuta mbele ya msomaji wai wa gazeti hili, huenda akawa haufahamu muziki huo. Kazi kubwa ya vyombo vya habari ni kupasha habari na kuburudisha. Kwa matinki hiyo, sina bundi kukujuza au kukumbusha kwa wewe uliyesahau enzi za ujana wako alivyokuwa akifuarahia burudani.
Katika makala ya leo hapana shaka mzee mwenye zaidi ya umri wa miaka 50, akisoma majina ya Jim Reeves, atakuwa umeguswa vilivyo. Jim Reeves alikuwa mwanamuziki toka nchini Marekani, aliyekuwa amejikita katika miondoko ya muziki wa ‘Country’ na muziki wa kawaida akiwa mtunzi halikadhalika uimbaji.
Katika maisha yake ya muziki, aliweza kuweka rekodi ya kuupandisha ‘chati’ muziki wake kati ya miaka ya 1950 hadi ya 1980. Nyimbo za Jim Reeves husikika sana katika baaadhi ya sherehe zinazowajumuisha wazee hususani katika mikoa ya Nyanda za Kaskazini, nyakati za sikukuu za Krismasi na mwaka mpya.
Reeves alipata kuwa maarufu na akajulikana kama mwanamuziki wa midundo ya ‘Nashville’ (ambayo ni mchanganyiko wa muziki wa zamani wa Country na ule wa kisasa). Wasifu wa nguli huyo unaonesha kuwa majina lake halisi alikuwa ikiitwa James Travis aka “Jim”.
Mwanamuziki huyu alizaliwa Agosti 20, 1923, katika kitongoji cha Galloways huko Texas, nchini Marekani. Reeves alikuwa akitoka katika jamii ya watu waliokuwa nje ya mji karibu na Carthage.
Aidha Jim alitambulika ‘Muungwana Jim’ Alifariki kwa ajali ya ndege Julai 31, 1964 akiwa na umri mdogo wa miaka 40 katika ajali ya ndege binafsi. Nyimbo zake ziliendelea kupanda chati kwa miaka kadhaa hata baada ya kifo chake. Jim Reeves alikuwa mwanachama wa muziki wa ‘Country’ na pia ule wa Texas Country Halls of Fame.
Alifanikiwa kupata nafasi ya kwenda kusoma msomo ya juu ‘Scholarship’ ambapo alijisajili kusomea masuala ya kuhutubia na maigizo. Baada ya miezi sita katika masomo hayo, aliachana nayo akaamua kwenda kufanya kazi katika Yadi ya kutengeneza Meli huko Houston, huko huko Marekani.
Licha ya kuwa na weledi katika muziki, Reeves pia alikuwa mwanariadha aliyewahi kuchezea ligi za Semi- Professional kabla hajaingia mkataba na St. Louis Cardinals, timu ya shamba. Mwaka 1944 alicheza kama right- handed Pitcher.
Aidha alicheza ligi ndogo kwa miaka mitatu kabla hajaumia na kupata maumivu katika misuli iliyohitimisha juhudi zake za kuendelea na michezo. Reeves alianzia kufanya kazi kama mtangazaji wa redio. Kila wimbo umalizikapo kuupiga redioni, yeye akawa anaimba wimbo huo.
Mwishoni mwa miaka ya 1940, aliingia mikataba na baadhi ya Makampuni madogo ya kurekodi, huko Texas, lakini hakupata mafanikio. Muziki wa Magharibi ulimfanya kuhamasika sana hususani alipokuwa akiwasikia wanamuziki kama Jimmie Rodgers na Moon Mullicann. Waimbaji wengine maarufu wakati huo aliokuwa akiwatamani ni akina Bing Crosby, Eddy Arnold na Frank Sinatra.
Mapenzi hayo makubwa katika muziki yalimpelekea kuwa mwanachama wa bendi ya Moon Mulican. Jim aliweza kucheza mitindo ya mwanzoni ya bendi ya Mullican, ambapo nyimbo zake kama ‘Each Beat of My Heart’ na ‘My Heart’s Like a Welcome Mat’ mnamo miaka ya 1940 mwishoni na mwanzoni 1950, zilitamba wakati huo.
Aliweza ‘kukopi’ akiimba nyimbo za mwanamuziki mkongwe walomtangulia katika tasnia hiyo kama ‘Mexican Joe’. Nyimbo ambazo zilishika namba moja mwaka 1953. Kutoka mwaka 1955 mpaka mwaka 1969 Reeves akiwa na nyimbo zake hizo, ziliendelea kushika ‘ukanda’ hata baada ya yeye kufariki.
Nyimbo zake za kwanza za ‘Country’ zilizompa mafanikio zilikuwa ni pamoja na ‘I Love You’ aliouimba akishirikiana na Ginny Wright, na ‘Mexican Joe’ ‘Bimbo’ Jim aliafanikiwa kufyatua albamu yake katika studio za Abbott Records, ikatoka Novemba, 1955 iliyojulikana ‘Jim Reeves Sings’.
Mapema mwaka 1955, Reeves aliingia mkataba wa miaka 10 na Kampuni ya RCA Victor chini ya Steve Sholes. Katika mkataba huo, alitoa rekodi za kwanza za Reeves akitumia Kampuni ya RCA na pia akasaini mkataba na mwanamuziki Elvis Presley, katika Kampuni hiyohiyo.
Alipokuwa akirekodi mwanzoni akiwa na Kampuni ya RCA, Reeves bado alikuwa anaimba kwa mtindo wa sauti ya juu ambapo ilionekana ndio kipimo cha nyimbo za ‘Country’ Wanamuziki wa Magharibi kwa wakati huo. Jim alisaidia sana kuanzisha mtindo mpya ya muziki wa ‘Country’ akitumia ‘violin’ na ‘mpangilio wa kupendeza wa background ikijulikana kama ‘Nashville’ sound.
Baadae alianza kupunguza sauti yake wakati akiimba na kutumia ‘Pitch’ ya chini akiimba huku midomo yake ikikaribia kugusa kipaza sauti, ingawaje waliokuwa wanamrekodi (RCA) walikuwa wanailalamikia hali hiyo. Mwaka 1957 kwa maelekezo ya ‘Produysa’ wake Chet Arkins, alitumia mtindo huo katika toleo la wimbo wa maonesho wa ‘Penzi lililopotea’ uliokusudiwa uimbwe na mwimbaji wa kike.
Katika kipindi chote miaka yote ya 1950 na hadi 1960 mwanzoni, Jim Reeves alifanikiwa kuachia nyimbo zake kali zizoshika ‘chati’ za ‘Anna Marie’ na ‘Blue Boy’ No. 2 za mwaka 1958. Nguli huyo alifyatua vibao vingine vya ‘Billy Bayo’ mwaka 1959 na ‘He will have to go’ wa mwaka 1960, ‘Adious Amigo’ (namba mbili, 1962), ‘Welcome to my World’ (namba mbili, 1964) na ‘I guess I’m crazy’ (namba moja kwa wiki saba, 1964).
Pia alikuwa na kikosi na idara ya nyimbo za dini katika jukwaa lake. Wimbo wake, ‘Danny Boy’ akijitambulisha kwamba wazazi wake wametokea Irish. Wimbo ‘But You Love Me Daddy’ ukirekodiwa wakati mmoja akiwepo ‘Steve’. Huyo alikuwa ni mtoto wa umri wa miaka minane. Mtoto huyo alikuwa ni wa mpiga gitaa la besi, Bob Moore.
Wimbo huo uliingia katika ishirini bora huko Ulaya baada ya miaka kumi. Rekodi za Reeves mara nyingi zilikuwa na utamanifu wa kipekee, kama ‘I Love you Because’ na ‘I won’t forget You’. Zote hizo zilikuwa katika chati huko Ulaya kwa wiki 39 mfululizo.
Alipata umaarufu kama muimbaji wa kiume mwenye sauti ya kupendeza na nzito kiasi na yenye madaha. Nyimbo kama ‘Adios Amigo’ ‘Welcome to My World’ na ‘Am I Losing You’ zinaonesha hilo. Reeves nyimbo zake za Chrismasi zikijirudia rudia na kupendwa sana hasa zikiwa ni pamoja na ‘Chrismasi’, ‘Blue Chrismas’ na ‘An Old Chrisimasi Card’.
Hali kadhalika alikuwa hodari kwa kuukweza na kuzipa umaarufu nyimbo nyingi za ‘Injili’ kama. Alizipa kipaumbele nyimbo hizo za ‘We Thank Thee’ ‘Take My Hand, Precious Lord’ ‘Across The Bridge’ ‘Where We’ll Never Grow Old’ na nyingine nyingi.
Reeves aliibua na mafanikio makubwa baada ya ‘kujaladia’ kuimba utunzi za Joe Allison, ukiwemo wa ‘He’ll have to Go’. Katika nyimbo za ‘Country’ ambazo ziligonga vichwa vya watu kuanzia February 08, 1960 na kuendelea kwenye chati kwa wiki 14 mfululizo.
Mwana historia wa muziki wa Country, Bill Malone alionesha kwamba ni katika namna nyingi Reeves aliendeleza utamu na ubora katika muziki wa ‘Country’ kimpangilio na ‘melodi’ safi na ujumbe unaogusa mioyo ya watu.
Kwa nyongeza, Malone alimsifia Reeves kwa staili yake ya kuimba ambayo anaishusha chini sauti yake, inakuwa kama ya kubembeleza na ndio maana watu wengi wanatamka kwamba Jim Reeves alikuwa mwimbaji mwenye sauti ya mguso.
July 31, 1964, Reeves na mshirika mwenzake wa kibiashara, Meneja Dean Manuel waliondoka Batesville, Arkansas kupitia Nashville wakitumia ndege ya injini moja akiwa Reeves anaendesha. Wawili hao walikuwa wamepata ‘dili’ ya kununua shamba huko Deadwood Texas, Kaskazini mwa Galloway ambayo ni sehemu aliyozaliwa Reeves.
Wakati wanapaa juu kwa ndege akiwa na Brentwood, Tennessee, walikutana na dhoruba ya upepo mkali na mvua kubwa. Katika uchunguzi ilionekana ndege hiyo ndogo ilinaswa katika dhoruba na Reeves alipata mstuko ikaanguka na wao wakafariki.
Mjane wa marehemu, Mary Reeves alianzusha uvumi kwamba Reeves alikuwa akiendesha juu chini na aliongeza spidi ili kukwepa dhoruba. Hata hivyo kulingana na Larry Jordan, maelezo ya mjane wake kwamba Reeves alikuwa anaendesha chini juu haikuwa sahihi.
Kutokana na watu walioiona ajali hiyo jinsi ndege ilivyoanguka na maelezo yaliyomo kwenye tape iliyorekodi mwenendo wa ndege, na pia maelezo ya ripoti ya ajali, kwamba Reeves alikata kushoto katika jitihada zake za kuipata Franklin road, ili afike uwanja wa ndege aweze kutua.
Katika jitihada yake hiyo akazidi kuelekea kule kwenye mvua kubwa. Katika kuhangaika ili akakipate kiwanja ili kutua, spidi ya ndege ikawa ipo chini hivyo akaikwaza ndege.
Reeves alitegemea zaidi hisia zake katika kumuongoza na hakutumia maarifa aliyofundishwa chuoni kuikabili hali kama hiyo. Baada ya masaa 42 mabaki ya ndege yalionekana ikiwa mbele, yaani usoni pamoja na injini vimejikita ardhini. Reeves na mwenzake walikutwa tayari wamekwisha fariki.
Jim Reeves alizikwa katika kipande cha ardhi maalum ubavuni mwa ‘Highway 79’ Texas. Licha ya kufariki Jim Reeves bado umaarufu wake haukupotea, kwa hakika mauzo ya kazi zake yameongezeka baada ya kufariki.
Tangu kipindi cha kifo cha Jim Reeves kulipotokea, Mary alipatwa na matatizo ya kuugua kabla hayajamzidia. Mjane huyo Mary Reeves alifariki akiwa na umri wa miaka 70, Novemba 11, 1999. Iliripotiwa kuwa alikufa akiwa peke yake katika nyumba ya kuuguza wagonjwa.
Kabla ya kifo chake Mary Reeves Davis alishindwa kusimamia mali za Jim kutokana na ugonjwa, zikauzwa kwa ‘United Show of America’ mwaka 1997 kwa thamani ya Dola za Kimarekani milioni 7.3 Jim Reeves aliwekwa kwenye kundi la mwimbaji nyota wa kiume ambaye ametokeza katika midundo ya ‘Nashville Sound’.
Sauti yake laini ya kidume yenye madaha imeendelea kusikika hadi wakati leo. Mungu ailaza roho yake pahala pema peponi, Amina.
Mwandishi wa makala haya anapatikana kwa namba 0784331200, 0713331200, 0736331200 na 0767331200