Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

Benki ya CRDB yafuturisha wateja wake Dodoma, Spika Ndugai aimwagia sifa

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, ameipongeza Benki ya CRDB kwakuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za ujenzi wa taifa kupitia miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa mradi wa ufuaji umeme wa Stiglers gogle na mingine mingi.

Spika Ndugai aliyasema hayo wakati wa futari maalum iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dodoma.

“Tuna imani kubwa na Benki ya CRDB. Siku zote nimekuwa nikisisita kuwa Benki hii ndio kioo halisi cha mabenki yetu nchini. Mafanikio ya Benki ya CRDB yana akisi hali halisi ya uchumi wa taifa na mtanzania mmoja mmoja. Hivyo basi, sisi kama Bunge tutaendelea kuwapa kila ushirikiano unaohitajika. Watanzania wanajisikia fahari kuona Benki yao ya kizalendo kiendelea kuimarika.”

Kwa niaba ya wageni waalikwa ambao walihusisha Mawaziri, Wabunge na wateja wa benki ya CRDB, Mheshimiwa Ndugai aliishukuru Benki ya CRDB kwa kuundaa futari hiyo maalum jijini Dodoma. “Tunawashukuru benki ya CRDB kwa kuona umuhimu wa kuandaa futari kwa ajili ya wateja wadau wake hapa Dodoma. Sisi watu wa Dodoma tunaona ufahari kwa kitendo hiki kwani kinaonesha kuwa mnatujali, Ahsanteni sana” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela aliwashukuru wageni waalikwa kwa kuhudhuria futari hiyo na kuwaahidi kuendelea kuboresha huduma za benki ya CRDB ili kufikia matarajio yao. “Kipekee kabisa niwashukuru wageni wote mliofika hapa leo.

 Benki ya CRDB tumejiwekea utaratibu kila mwaka wa kushiriki katika futari  ili kuungana na ndugu zetu wa kiislamu katika kuomba dua pamoja na kuomba yaliyo mema. Nichukue nafasi kuwaahidi kuwa tutaendelea kuwa wabunifu huku tukiongeza utumiaji wa mifumo ya kidijitali ili tuweze kuwapa huduma zitakazokidhi matarajio yenu. Sisi benki ya CRDB tunandelea kuwaahidi huduma bora zaidi na ahadi yetu kwenu ni kuwa TUPO TAYARI KUWAHUDUMIA”.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela baada ya hafla ya Iftar iliyoandalia na Benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wa Jijini Dodoma, iliyofanyika katika Hoteli ya Morena, jana Mei 29, 2019. Kulia ni Katibu wa Bunge, Steven Kigaigai na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakimsikiliza, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi baada ya hafla ya Iftar iliyoandalia na Benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wa Jijini Dodoma, iliyofanyika katika Hoteli ya Morena, jana Mei 29, 2019. 
























































Dkt.Abass:Tanazani kuleta historia katika usimamizi wa madini Afrika na Duniani.

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamiii

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt.Hassan Abass amesema serikali imekuwa matokeo mazuri katika mapato kutokana mabadiliko ya mifumo mipya pamoja na mabadiliko ya Sheria katika sekta ya madini.

Abass ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi habari ikiwa ni utaratibu wa kila mwezi kutoa taarifa za serikali.

Amesema serikali imepata kodi inayotokana na madini sh.bilioni 300 kwa mwaka wa Fedha 2018/2019.Amesema mapato hayo ya kodi yanatokana na matokeo ya utungaji wa sheria za madini na kufanya Tanzania kunufaika na sekta hiyo.

Amesema pamoja na sheria hiyo pamoja na serikali kuagiza kuanzisha kwa masoko ya madini kilo zimeongezeka ikilinganishwa na miaka nyuma.

Abass amesema Geita kabla ya soko walikuwa wanapata kilogram za Madini 259 baada ya soko kuanzisha ni kilogram 312 na maeneo mengine yameendelea kufanya vizuri katika masoko ya madini.

Amesema kabla ya ukuta wa merelani kujengwa zilikuwa zinapatikana kilogram 164 hadi kufikia kilo 781 baada ya ukuta kujengwa.Dkt. Abass amesema Tanzania inakwenda katika mageuzi ya kiuchumi katika sekta ya Madini katika Afrika na Dunia kwa ujumla.

Amesema wale wanaopinga kwa kutumia mitandao katika juhudi za serikali wanaumbuliwa na matokeo yanayotokea.

Amesema baada ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kupokea mtambo wa TTMS kwa serikali imepata mapato zaidi ya sh.bilion 97 katika miamala ya machi watanzania walitumiana miamala ya Fedha zaidi ya sh. Bilioni Moja.

Hata hivyo katika mfumo wa malipo ya huduma mbalimbali za serikali zaidi taasisi 400 zimejiunga.

Amesema shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) tangu kujiunga imeokoa sh.bilioni 38 huku wakala wa Vipimo wakifikia bilioni mbili kutoka bilioni Moja na Aridhi kutoka sh.milioni 70 hadi sh.milioni 100.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt.Hassan Abass akizungumza na waandishi habari kuhusiana na masala mbalimbali yaliyotokea Serikalini jijini Dar es Salaam.

FORUMCC, HALMASHAURI YA LALA YAWAKUTANISHA WADAU KUDAJILI CHANGAMOTO ZA KIMAZINGIRA

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Forum CC Rebecca Muna akizungumza leo kuhusu umuhimu wa wadau wa mazingira kuwa na jukwaa la pamoja la kujadiliana na kufikia makubakiano ya namna bora ya kukabiliana na changamoto zilizopo katika eneo la mazingira nchini.
Mchokoza mada Samuel Bubegwa akichangia wakati wa majadiliano ya wadau wa mazingira katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Dar es Salaam ambapo emetumia nafasi hiyo kushauri uwepo wa jukwaa la majadiliano ambalo litajikita kuweka mikakati ya kuondoa taka zikiwemo taka ngumu.
Mchokoza mada Samuel Bubegwa akichangia wakati wa majadiliano ya wadau wa mazingira katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Dar es Salaam ambapo emetumia nafasi hiyo kushauri uwepo wa jukwaa la majadiliano ambalo litajikita kuweka mikakati ya kuondoa taka zikiwemo taka ngumu.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omar Kumbilatomo akizungumza kwa niaba ya Meya wa manispaa hiyo akizungumza wakati akifungua kikao cha majadiliano  kiichowakutanisha wadau wa mazingira na ForumCC.
 Moja ya wadau wa mazingira Kahana Lukumbuzya akichangia mada wakati wa kikao cha majadiliano kuhusu uboreshaji wa mazingira ya Halmashauri ya Ilala jijini Dar es Salaam.
 Wadau wa mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wakifuatilia majadiliano yaliyohusu kuwekwa mikakati ya kuweka mazingira safi ya manispaa hiyo.

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SHIRIKA la FORUMCC kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wamewakutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la kujadili changamoto za kimazingira na kutafuta ufumbuzi wake kwa hamashauri hiyo.


Mjadala huo unafanyika chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya(EU) kupitia Mradi wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi. EU wamekuwa wakishirikiana kuandaa mijadala na makongamano yanayohusu kujadili mabadiliko ya tabianchini na hali ya mazingira nchini kwa ujumla.


Akizungumza wakati wa akifungua majadiliano hayo Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Omari Kumbilamoto amesema ni jambo muhimu wadau kukutana na kuweka mikakati itakayosaidia kuweka mazingira safi.

“Tunashukuru kwa uwepo wa majadiliano haya yanayohusisha sekta binafsi na Serikali kwa kuangalia namna gani wanaweza kukabiliana na taka ngumu.Mjadala umekuja wakati muafaka hasa kwa kuzingatia tayari Serikali imetoa tamko la kuzuia plastiki ambalo binafsi na Halmashauri ya Ilala tunaunga mkono katazo hilo,”amesema.


Amesema Manispaa ya Ilala imekuwa na jitihada mbalimbali katika utunzaji mazingira kwa kuweka mbinu na mifumo sahihi za usafi mazingira huku akisisitiza kutambua mchango wa sekta binafsi katika jitihada hizo.


Pia ameshauri kampuni ambazo zipo Manispaa ya Ilala na zinatoa huduma za kubeba taka ngumu pamoja na kufanya vizuri maeneo ya kati ya Jiji ni vema pia wakaweka nguvu kubwa katika kuzoa taka maeneo ya pembezoni.

“Ni lazima kuwepo na mipango madhubuti ya kuzoa taka katika Manispaa ya Ilala.Pia niwakumbushe wenye kampuni za kuzoa taka kuendelea kushirikiana na wananchi na vema nikaeleza gharama ya Sh.3000 ya taka nayo inaonekana kuwa changamoto kwa wananchi walio wengi, hivyo mtaangalia namna ya kufanya.


“Tunatarajia majadiliano ya leo yatakuwa na ufumbuzi mzuri katika kumaliza changamoto za taka na kuweka mazingira safi lakini nikiri bado tunayo changamoto ya dampo na kwa bahati nzuri wenzetu wa Jiji wameahidi kutafuta ufumbuzi kwa kuwa na dampo la kisasa,”amesema Kumbilamoto.


Pia amesema pamoja na Manispaa ya Ilala kukusanya mapato mengi yatokanayo na vyanzo mbalimbali vya fedha lakini ifahamike kuwa imekiwa ikitumia fedha nyingi kwa ajili ya masuala mbalimbali yakiwamo ya sekta ya afya na kufafanua Ilala tayari imetenga Sh.milioni 52 kukabiliana na Dengue na wakati huo huo kuna viashiria vya magonjwa ya mlipuko ,”amesema Kumbilamoto.


Wakati wa majadiliano hayo imefafanuliwa katika katika eneo la taka ngumu bado kunachangamoto kubwa na hivyo wadaua wameamua kuweka mikakati ambayo itasaidia kuondoa taka hizo.Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa ForumCC Rebecca Muna amesema lengo la kuwakutanisha wadau hao ni kuhakikisha kunakuwa na makubaliano ya pamoja katika kukabiliana na changamoto ya uwepo wa taka ngumu.

Amesema wanatambua dhamira njema ya Serikali ya kuondoa taka hizo ikiwemo mifuko ya Plastiki, hivyo Forum CC kwa kushirikiana na wadau wengine wa mazingira wanawajibu kuwa sehemu ya kufanikisha malengo ya Serikali.


 Pia ametumia nafasi hiyo kusisitiza umuhimu wa uwajibikaji kwa kuhakikisha kila mmoja wetu kwa maana ya Serikali, wadau na mtu mmoja moja anakuwa sehemu ya kufanikisha mazingira yanakuwa salama.


“Forum CC ni shirika ambalo si la kiserikali ambalo limekuwa likiandaa majadiliano yanayohusu mabadiliko ya tabianchi.Kwa kuwa tunatambua tunaingia kwenye katazo la mifuko ya plastiki tukaona iko haja ya kukutanisha wadau kuweka mikakati ambayo itsaidia kuondosha plastiki ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa kimazingira,”amesema Muna.


Amefafanua uchafuzi wa mazingira una madhara makubwa yakiwemo ya kutumia fedha nyingi kukabiliana na magonjwa ya mlipuko, hivyo ni vema wadau wakaendelea kuweka mikakati ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi,”amesema.


Hata hivyo amesema kuwa kikubwa ambacho kinahitaji ni kuweka uwajibikaji ambao utakuwa na tija kwa kila mmoja kutekeleza majukumu yao iwe kwa upande wa serikali au wadau wa mazingira.


Mmoja wa wachokozi wa mada Samuel Bubegwa wakati akichangia majadiliano hayo amefafanua kwa Manispaa ya Ilala wamekuwa na mfumo mzuri katika kuweka mfumo wa uzoaji taka na kuweka mazingira safi na kuomba ni vema Ilala ikaangalia namna ya kukutana na viongozi wa ngazi za juu serikalini ili kuwaelimisha namna wanavyofanya katika eneo la mazingira.


Pamoja na mambo mengine sehemu kubwa ya taka ngumu zilikuwa zinatokana na plastiki na saas kuondolewa kutasaidia kimazingira huku akishauri uwepo wa jukwaa kati ya wakandarasi, wadau  na Serikali katika uondoshaji wa taka.


Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kwa manispaa ya Ilala taka ambazo zinazalishwa kila siku ni tani 2000 na hivyo ni jukumu la wadau mbalimbali kushirikiana katika kuondoa taka hizo na Ilala imekuwa ikijitahidi katika kuweka mazingira safi.


Kwa upande wake Ofisa Mazingira Mkuu wa Baraza la Mazingira la Taifa(NEMC) Mhandisi Benjamin Mchwampaka amesema suala la uwepo wa uchafuzi wa mazingira linatokana na tabia na hivyo ni vema wananchi wakabadili tabia.


Amesema kuna kila sababu ya taka kuwekwa kulinana na aina ya taka zenyewe, ikiwemo taka zinazooza, taka ngumu pamoja na taka zenye kemikali za sumu na kila familia ikiweza kutenganisha taka uwezekano wa kudhibiti taka ngumu utafanikiiwa.

Mwisho  



RAIS DKT MAGUFULI AREJEA NCHINI AKITOKEA AFRIKA KUSINI, NAMIBIA NA ZIMBABWE

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Brigedia Jenerali Abdallah M. Alphonce na wafanyakazi wa ubalozi huo Bi. Alice Madele na Bi Joyce Makoye katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe jijini Harare, kabla ya kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kurejea nyumbani akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitelemka kutoka katika ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Mei 30, 2019 akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna wa Polisi Diwani Athumani baada ya kutelemka kutoka katika ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo alhamisi Mei 30, 2019 akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo alhamisi Mei 30, 2019 akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mhe. Dkt. Emmerson Mnangagwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe jijini Harare leo alhamisi Mei 30, 2019 baada ya kuhitimisha ziara yake ya Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi PICHA NA IKULU

TSHISEKEDI KUZIKWA RASMI NCHINI KONGO

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MWILI wa aliyekuwa kiongozi wa upinzani wa Jamuhuri ya watu wa Kongo Etienne Tshisekedi ambaye pia ni Rais wa sasa wa nchi hiyo Felix Tshisekedi umewasili nchini humo leo baada ya kuhifadhiwa nchini Ubelgiji baada ya kufikwa na umauti takribani miaka miwili iliyopita.

Wanafamilia wameeleza kuwa kuwa mwili utawasili kutoka Ubelgiji na kuzikwa kwa heshima nchini humo, Etienne alifariki mwaka 2017 Februari huko Brussels huko Ubelgiji akiwa na miaka 84 na mwili wake kuhifadhiwa huko kwa wasiwasi wa kiusalama.

Imeelezwa kuwa mwili wake utazikwa kwa heshima na maandalizi ya mazishi hayo yamekamilika.

Mazishi hayo yatahudhuriwa na marais mbalimbali huku ikielezwa kuwa atazikwa kama shujaa.

Mwanaye wa kiume Felix Tshisekedi aliapishwa kuwa Rais wa nchi hiyi Januari 24 mwaka huu akifuata nyayo za baba yake ambaye alikuwa mkosoaji  mkubwa dhidi ya dikteta Mobutu Sese Seko.

MBATIA AJA NA WAZO LA KUANZISHWA SOMO LA MAJANGA MASHULENI

$
0
0
Anaripoti Dixon Busagaga
MBUNGE wa Jimbo la Vunjo,  James Mbatia amesema anakusudia kupaza sauti juu ya kuanzishwa kwa somo linalohusu kujiandaa na Majanga “ Disaster Preparedness”  katika shule za msingi,sekondari na vyuo ili kuwaandaa wanafunzi kuweza kukabiliana na majanga pindi yanapotokea.

Kauli ya Mh Mbatia ambaye pia ni mtaalamu wa Majanga inakuja siku chache baada ya Mabweni mawili katika shule ya sekondari ya wasichana ya Ashira iliyopo Marangu mkoani Kilimanjaro kuungua moto na kuteketeza vitu mbalimbali yakiwemo magodoro,shuka na nguo za wanafunzi.

Tayari wadau mbalimbali wameendelea kujitokeza kutoa msaada wa kibinadamu kwa wanafunzi 73  ,waathirika wa ajali hiyo ya moto miongoni mwao ni Mbunge wa jimbo la Vunjo na Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia aliyekabidhi msaada wa mabegi 73 kwa ajili ya kuhifadhi nguo za wanafunzi hao.
 Mbunge wa Jimbo la Vunjo,James Mbatia akiwa ameongozana na Mkuu wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Ashira , Elizabeth Abdalah alipofika kutoa pole pamoja na msaada kwa wanafunzi waliathirika na ajali ya moto iliyoteketeza Sehemu ya Mabweni mawili katika shule katika shule ya sekondari ya wasichana ya Ashira iliyopo Marangu mkoani Kilimanjaro.



 Sehemu ya Mabweni ya Japan na Muungano yaliyoungua Moto hivi karibuni katika shule ya sekondari ya wasichana ya Ashira iliyopo Marangu mkoani Kilimanjaro.
 Mabaki ya nguo na vifaa mbalimbali vya wanafunzi baada ya moto kutekekeza sehemu ya Mabweni Katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya Ashira iliyopo Marangu mkoani Kilimanjaro.
 Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akikabidhi msaada wa Mabegi kwa ajili ya kuhifadhi nguo kwa wanafunzi walioathirika na ajali ya moto katika shule ya sekondari ya wasichana ya Ashira iliyopo Marangu mkoani Kilimanjaro.

  Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Ashira wakati akitoa pole kwa wanafunzi hao


WANANCHI WATAKIWA KUTEMBELEA OFISI ZA TRA KUWASILISHA MAONI NA KERO ZA KIKODI

$
0
0
Na Peter Haule, WFM, Dodoma
Serikali imetoa wito kwa wananchi kutembelea ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zilizopo katika maeneo yao na kuhudhuria vikao vinavyoitishwa na wakuu wa Mikoa na Wilaya ili kuwasilisha maoni na kero zao zinazohusu kodi.

Wito huo umetolewa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Jaku Hashimu Ayoub, alietaka kujua ni lini TRA itakaa na Wafanyabiashara kusikiliza vilio vyao kwa kuwa kila mkoa una ofisi za Mamlaka hiyo.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, TRA ina ofisi katika mikoa yote ya Tanzania pamoja na baadhi ya wilaya zake, na baadhi ya mikoa ina vituo maalum vya huduma za kodi (Tax Centres), hususani Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya, pia kila Mkoa una Mwanasheria na Afisa Elimu ya Kodi  kwa ajili ya kutoa elimu, kusikiliza na kutatua kero za walipakodi.

“TRA imeweka utaratibu kwa meneja wa mikoa ya kikodi kukutana na walipakodi kila Alhamisi ili kusikiliza kero zao na kuzitatua, hatua ambayo ina lengo la kujenga imani , kutatua kero na kukuza ridhaa ya ulipaji kodi kwa hiari”, alieleza Dkt. Kijaji.

Alisema kuwa miongoni mwa kazi za kila siku za TRA ni kusikiliza na kutatua kero za wafanyabiashara ili kuwawezesha kufanya biashara zao bila usumbufu, hivyo hufanya biashara katika ngazi ya wilaya, mikoa na Taifa ili kutoa elimu, na pia hurusha vipindi maalum katika runinga na redio kuhusu elimu ya kodi kwa wananchi na kujibu kero za wafanyabiashara.

Dkt. Kijaji alieleza kuwa Wenyeviti wa Kamati za Mapato za Mikoa na Wilaya ambao ni wakuu wa mikoa na wilaya wamekuwa wakisikiliza kero za walipa kodi kwa kushirikiana na TRA na kwamba Mamlaka hiyo hubuni na kuanzisha mifumo, vituo na vilabu rafiki vya kikodi ili kujibu vilio vya wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.

Aidha Dkt. Kijaji alikanusha kuwepo kwa usumbufu wa utoaji wa mizigo kutoka Zanzibar ikilinganishwa na mizigo mingine inayopitia bandari ya Dar es Salaam kwenda nchi za nje kama Zambia, Uganda, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo akifafanua kuwa bidhaa zote zinatakiwa kufuata utaratibu wa forodha.

Alisema bidhaa zinazoingia Tanzania Bara kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Kusini mwa Afrika (SADC), hupata msamaha wa ushuru wa Forodha lakini hulipiwa Kodi ya Ongezeko la Thamani pamoja na ushuru wa bidhaa.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)

AKINA MAMA 191 HUFARIKI ZANZIBAR KUTOKANA NA UZAZI - UNICEF

$
0
0
Vifo vitokanavyo na uzazi vimeongezeka Zanzibar, ikiwa ni nje ya mategemeo ya vifo vilivyotegemewa kutokea, kwa mujibu wa ripoti ya mwaka jana.

Kwa mujibu wa Abdulrahman Kwaza, Msaidizi wa  Mkuu wa Kitengo Cha Elimu ya Afya Zanzibar, wanawake 191 wanapoteza maisha kati ya vizazi hai 100,000, kinyume na matarajio ya vifo 110 kati ya vizazi hai 100,000 ambavyo zilitegemewa.

Hayo aliyasema wakati akiwasilisha mada katika semina ya ‘Jiongeze Tuwavushe Salama’ kwa viongozi wa dini wa Zanzibar.

Semina hii, ambayo imeratibiwa na kampuni ya True Vision Production (TVP) kwa kushirikiana na UNICEF Tanzania na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ni sehemu ya mwendelezo wa semina nyingine tatu zilizofanyika Tanzania Bara hivi karibuni na kuhusisha pia viongozi wa dini tofauti, waandishi wa habari na wahariri.

Kwaza amesema vifo hivyo vinasababishwa na mambo mengi, ikiwemo umbali wa vituo vya afya, ukosefu wa wahudumu wenye utaalamu wa  kuzalisha na ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi, vikichangiwa na membo mengine mengi.

Amesema ushiriki wa jamii katika afya ya uzazi umekuwa mdogo, huku akitoa wito wa kuimarisha huduma za kujifungua chini ya wataalamu wa afya, uboreshwaji wa vituo vya afya na kuweka msisitizo katika lishe ya mama akiwa mjamzito na ya mtoto baada ya kuzaliwa.

Amesema kitaalamu mama anatakiwa kumnyonyesha mtoto wake miezi 6 tangu anapozaliwa, kwani maziwa ya mama yanavirutubisho tosha vya kumlinda mtoto.

Amesema jitihada zimekuwa zikifanyika, huku akiongeza kuwa huduma za afya ya uzazi wa mpango zinapatikana katika vituo vingi, lakini bado kuna changamoto kwani baadhi ya vituo hivyo havitoi huduma za upasuaji mdogo.

Mtaalamu wa mawasiliano kutoka UNICEF, Usia Nkoma amesema jamii kwa ujumla ina wajibu wa kuhakikisha mama mjamzito anakwenda kliniki na kujifungua katika kituo cha afya na anatakiwa awe chini ya uangalizi wa wataalam wa afya masaa 48 baada ya kujifungua.

Sheikh Fadhil Soraga, ambaye ni katibu wa Mufti wa Zanzibar amesema viongozi wa dini wana dhamana ya kuhakikisha wanaelimisha jamii juu ya umuhimu wa kuokoa vifo vitokanavyo na uzazi.

Amesema Qur-an, kitabu cha Waislam, kina sisitiza juu ya afya ya uzazi, kikimtaka mama aliyejifungua kumnyonyesha mtoto wake miaka miwili iliyotimia ili awe na afya njema.
Naye Farashuu Khamis Musa kutoka ofisi ya Mufti amewashukuru waandaaji wa semina, akisema wataleta chachu ya kuokoa vifo hivyo.

“Viongozi wa dini wana wafuasi wengi, hivyo naamini watafanikiwa katika vita hii’, amesema Farashuu.
Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka UNICEF Usia Nkoma akichangia mada katika semina ya Jiongeze Tuwavushe Salama iliyofanyika Zanzibar
 Katibu wa Mufti - Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akizungumza katika semina ya Jiongeze Tuwavushe Salama iliyofanyika Zanzibar
 Abdulrahman Kwaza,Msaidizi Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Afya Zanzibar akichangia mada katika semina ya Jiongeze Tuwavushe Salama iliyofanyika Zanzibar
Farashuu Khamis Musa kutoka ofisi ya Mufti Zanzibar akichangia hoja katika semina ya Jiongeze Tuwavushe Salama iliyofanyika Zanzibar hivi karibuni


Uhamiaji watakiwa kuwa makini suala zima la ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi

$
0
0
Maafisa waandamizi na watendaji wa Idara ya Uhamiaji wametakiwa kuwa makini katika suala zima la ulinzi pamoja na usalama wa mipaka ya nchi ili kuliepusha Taifa kuvamiwa na wageni wasiokuwa waaminifu.

Kufanya hivyo kutalisaidia Taifa pamoja na wakazi wake kuendelea kuishi katika mazingira salama muda wote na kufanya kazi zao bila ya hofu.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd.Shaaban Seif Mohamed alieleza hayo wakati akizungumza na maafisa na watendaji wa idara ya Uhamiaji katika ukumbi wa Ofisi hizo zilizopo Kilamani Mjini Zanzibar.

Alisema Idara ya Uhamiaji ni taasisi muhimu na nyeti katika kuhakikisha mipaka ya nchi inakuwa salama hivyo kuna haja ya kufanya Doria au ukaguzi kwa uwaangalifu katika mipaka ya Nchi kavu na baharini ili kuweka udhibiti wa wahamiaji haramu,na kufanya uvamizi.

“Nitoe mfano kuna changamoto ya bandari bubu zinazopokea wageni bila ya kuwepo maafisa kutoka idara ya Uhamiaji jambo ambalo ni hatari na linafaa kuachwa mara moja”. Alisema Katibu Mkuu Shaaban.

Nd. Shaaban alifahamisha kwamba suala la ulinzi wa mipaka katika ndani ya nchi linahitaji ushirikiano wa pamoja kati ya idara hiyo na wananchi wake sambamba na watendaji kutoka Serikali Kuu.

Akijibu baadhi ya Changamoto zinazoikabili idara hiyo Katibu Mkuu alisema viongozi wanaosimamia majukumu mbali mbali wanapaswa kuzisemea Changamoto hizo kwa viongozi wanaohusika ili ziweze kupatiwa ufumbuzi na aliwahidi maafisa hao kwa yale yanayoweza kupatiwa ufumbuzi Serikali itayachukulia hatua.

Akisoma taarifa ya Idara ya Uhamiaji Naibu Kamishna utawala na Fedha Ali Suleiman Nassor alimuelezea Katibu Mkuu Shaaban kuwa idara ya uhamiaji Zanzibar imefanikisha kuwakamata wageni 205 na kuchukuliwa hatuwa za kisheria ambapo kati yao 26 waliondoshwa nchini na 109 walilipia vibali,15 walishtakiwa Mahakamani ,21 waliachiwa Huru baada ya uchunguzi na wageni 34 bado uchunguzi unaendelea .

Naibu Kamishna Ali alieleza idara ua Uhamiaji katika Kuimarisha Ulinzi na Usalama imewatambua na kuwaoredhesha wahamiaji walowezi 1, 281, Unguja na Pemba kati ya hao 668 wameshasajiliwa .

Vile vile alieleza katika suala zima la utoaji wa vibali , Idara imetoa jumla ya vibali 1,116 kwa wageni kwa shughuli mbali mbali ikijumuisha vibali 143 vya daraja A, 536 vya daraja B, 437 vya daraja C, 225 hati za ufuasi na 250 hati za msamaha.

Alisema katika mwaka wa Fedha 2018/2019 Idara ilipangiwa kukusanya Shillingi 30,001,727,413/- kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Machi 2019 ambapo hadi sasa imekusanya Jumla ya Shillingi 26,104,134, 382.42/- sawa na asilimia 87% ya malengo ya Makusanyo yote.

Akigusia Changamoto zinazoikabili Idara hiyo Naibu Kamishna alizitaja Changamoto hizo ikiwemo Ufinyu wa Afisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharibi ,kukwama kwa utaratibu wa kumalizia upatikanaji wa eneo la Kitogani kwa ajili ya Ujenzi wa eneo la Chuo cha Uhamiaji pamoja na ukosefu wa boti kwa ajili ya kufanyia doria.

Wakichangia katika Kikao hicho Maafisa wamemtaka Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuzitembelea Afisi nyengine za Wilaya Unguja na Pemba ili kujionea hali halisi ya Mazingira ya Kazi .
 Naibu Kamishna utawala na Fedha Ali Suleiman Nassor Kushoto akimpokea Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ndugu Shaaban Seif Mohamed aliyefika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji Zanzibar kuzungumza na Makamanda na Watendaji wa Jeshi hilo.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ndugu Shaaban Seif Mohamed akitia saini kitabu cha Wageni alipofika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji Zanzibar kuzungumza na Makamanda.
 Naibu Kamishna utawala na Fedha wa Uhamiaji Zanzibar Ali Suleiman Nassor akitoa Taarifa ya uwajibikaji wa Jeshi hilo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ndugu Shaaban Seif Mohamed alipofika kuzungumza nao.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ndugu Shaaban Seif akizungumza na Makamanda na Watendaji wa Jeshi la Uhamiaji Makao Makuu yao Kilimani Mjini Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ.

Watoto wa Kike zaidi ya 2,454 wapewa mimba

$
0
0
Na, Editha Edward-Tabora 

Zaidi ya Watoto 2,454 wenye umri wa chini ya Miaka 20 katika Halmashauri ya Wilaya  Nzega mkoani Tabora watoto hao wanapata mimba za utotoni kwa takwimu za Mwaka 2018 huku robo yao mwezi wa kwanza hadi wa tatu 2019 mimba chini ya miaka 20 zilikuwa 603 huku sababu zikielezwa kuwa ni umasikini pamoja na ukatili wa kijinsia

Takwimu hizo zimetolewa katika kikao kilichokutanisha wadau mbalimbali mjini Nzega  na shirika lisilo la Kiserikali la World Vision linaloendesha kampeni hii ya kupambana na Mimba na ndoa za utotoni likishirikiana  na Serikali ili kutokomeza janga hili ambalo linakwamisha ndoto za Watoto wa kike

Bertha Mtesigwa ambaye ni Mratibu wa shirika la world Vision amesema Mradi huo una miaka saba ukitekelezwa na shirika hilo Lakini tatizo hilo linendelea kupungua japo amesema chngamoto haziishi

"Mimba hizi zimechangiwa na Sababu mbalimbali ikiwemo ya kwanza ni umasikini uliokithiri kutoka katika jamii zetu za watu wa Nzega Lakini kumekuwa na uelewa mdogo kuhusu suala la Malezi Makuzi ya mtoto na mila potofu ambazo zimechangia sana kuongezeka kwa mimba za utotoni "Amesema Mtesigwa

Meneja wa shirika la world Vision John Masenza amesema vyombo vya dola vinaendelea kupambana na tatizo hilo na amewaomba Wananchi Kushirikiana na shirika hilo ili kukomesha mimba za utotoni

Aidha idadi kubwa ya wanaopata mimba za utotoni ni wanafunzi wa shule za Msingi na shule za Sekondari.

WIZARA YA MAMBO YA NJE YAWASILISHA BAJETI BUNGENI LEO

$
0
0
Baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha Nchi zao hapa Nchini Tanzania wakifuatilia uwasilishaji wa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyowasilishwa na Waziri Profesa Palamagamba John Kabudi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. May 30, 2019
Baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia uwasilishaji wa hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo iliyowasilishwa na Waziri Profesa Palamagamba John Kabudi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. May 30, 2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi akipongezana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro mara baada ya kuwasilisha bajeti ya Wizara hiyo katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. May 30, 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe akiwa na Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje, Zanzibar Balozi Mohamed Hamza(kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Mwinyi. May 30, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (kushoto) wakijadiliana jambo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro (katikati) pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Augustine Mahiga(kulia). May 30, 2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi  akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro wakisikiliza hoja za Wabunge wakati wa uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni mjini Dodoma. May 30, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi  akiwa katika picha ya pamoja nje ya Bunge na baadhi ya Mabalozi wanaoziwasilisha Nchi zao hapa Nchini. May 30, 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe akipongezwa na Mwakilishi wa Ubalozi wa China hapa Nchini Bw Lin Liang. May 30, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi akipongezwa na Dkt. Detlef Wrätcher Balozi wa Ujerumani hapa Nchini mara baada ya Waziri kuwasilisha hotuba ya Bjaeti ya Wizara yake. May 30, 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe akibadilishana mawazo na baadhi ya Mabalozi wanaoziwasilisha Nchi zao hapa Nchini mara baada ya kuwasilishwa hotuba ya bajeti ya wizara hiyo Bungeni Mjini Dodoma. May 30, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi akiwa pamoja na baadhi ya wazazi na watoto walioshinda katika mashindano ya uandishi wa insha kwa nchi za Afrika ya Mashariki,watatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraji Mnyepe,May 30, 2019

WFT YAZINDUA MRADI KUWEZESHA UTEKELEZAJI MPANGO WA KITAIFA KUZUIA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

$
0
0


Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT) linalofanya shughuli za utetezi wa haki za wanawake na ujenzi wa tapo ya wanawake Tanzania lenye makao yake jijini Dar es salaam limetambulisha rasmi Mradi wa Kuwezesha Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 

Mradi huo wa “Support for the implementation Fund for National Plan of Action to End Violence Against Women and Children” umezinduliwa na kutambulishwa rasmi leo Alhamis Mei 30,2019 wakati wa Kikao cha Wadau wa Haki za Wanawake na Watoto na upingaji wa ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wilaya ya Shinyanga kilichofanyika katika Ukumbi wa Karena Hoteli Mjini Shinyanga.

Akizindua Mradi huo,Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo,alisema mradi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

“Tunawashukuru sana Women Fund Tanzania kwa kutuletea mradi huu katika halmashauri yetu,ninachoweza kusema huu ni mfuko wezeshi kwa jamii,sisi kama serikali tutatoa ushirikiano,kinachotakiwa sasa ni kuwa na mawasiliano kati ya Women Fund Tanzania na wadau watakaowezeshwa/ watakaopata ruzuku,toeni taarifa serikalini”,alisema Chambi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Progamu kutoka Women Fund Tanzania, Carol Francis Mango alisema mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu kama majaribio katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

“Tumeichagua halmashauri hii iwe ya mfano kwa sababu kuna matukio mengi ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto,ili kufanikisha mradi huu tutatoa ruzuku kwa mashirika ya wanawake na wasichana kwa ajili ya utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya ukombozi wa mwanamke na msichana”,alieleza Mango.

“Miongoni mwa Watekelezaji wa mpango wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto na ambao ndio walengwa wa mradi huo ni Halmashauri,Mashirika,taasisi na asasi zisizo za kiserikali ‘NGOs’,mabaraza ya watoto na jamii kwa ujumla”,aliongeza.

Aidha alisema lengo la WFT ni kuchangia harakati za kutetea haki za wanawake,kuwawezesha na kuendeleza mikakati ya ujenzi wa vuguvugu la utetezi wa nguvu za pamoja ili kukuza haki na usawa wa wanawake kimapinduzi nchini.

“Sisi ni mfuko wa kwanza na pekee unaolenga kutoa ruzuku kwa ajili ya kuendeza shughuli za utetezi wa haki za wanawake hususani waliopo kwenye ngazi ya jamii.Tunataka kuchangia katika kujenga tapo la wanawake imara nchini Tanzania kwa kufadhili na kuimarisha uwezo wa wanawake kwa njia ya kuendeleza mikakati ya kuunganisha nguvu za pamoja na kutafuta rasilimali”,aliongeza.

Aidha alisema shirika hilo liko mbioni kufungua ofisi mkoani Shinyanga ili kurahisisha uratibu wa shughuli za mradi huo mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Boniface Chambi akitambulisha na kuzindua Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga unaotekelezwa na Shirika la Kijamii la Women Fund Tanzania. Kushoto ni Mkuu wa Progamu kutoka Women Fund Tanzania,Carol Francis Mango,kulia ni Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Deus Mhoja . Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Sehemu ya Wadau wa Haki za Wanawake na Watoto wilaya ya Shinyanga wakiwa katika Ukumbi wa Karena Hoteli Mjini Shinyanga.
Mkuu wa Progamu kutoka Women Fund Tanzania,Carol Francis Mango akitoa wasilisho la Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa Progamu kutoka Women Fund Tanzania,Carol Francis Mango akielezea kuhusu Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wakimsikiliza Mkuu wa Progamu kutoka Women Fund Tanzania,Carol Francis Mango.
Mratibu wa Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akielezea malengo ya kikao cha wadau wa haki za wanawake na watoto.
Wadau wakiwa ukumbini.
Wadau wakifuatilia matukio ukumbini.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Ngasa Mboje akilishukuru shirika la Women Fund Tanzania kupeleka mradi katika halmashauri yao na kuahidi kutoa ushirikiano wakati wa utekelezaji wa mradi.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume akitoa neno la shukrani kwa Women Fund Tanzania na kueleza kuwa uongozi wa mkoa wa Shinyanga umepokea mradi huo na wapo tayari kutoa ushirikiano wote kufanikisha malengo ya mradi huo unaolenga kuwakomboa wanawake na watoto.
Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Mhoja akiwahamasisha wadau wa haki za wanawake na watoto kuchangamkia fursa ili kuhakikisha jamii inaondokana na mambo maovu.
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Mgeni Rasmi Maadhimisho miaka 50 ya TPDC

BOZI BOZIANA ATOKA NA ‘ADROIDI’.

$
0
0

Na Moshy Kiyungi,Dar es Salaam.

Wahenga walilonga kuwa “Kimya kingi kina mshindo mkuu” msemo huu ameudhihirisha nguli wa miondoko ya rhumba Bozi Boziana.

Nguli huyu amerudi tena kwenye dimba la muziki, hivi sasa hupo bize studio akitayarisha ngoma mpya yenye jina la ‘Android’.

Kwenye ngoma hiyo amemshirikisha Ferre Gola ‘Le Padre’, mwanamuziki ambaye hivi sasa ni gumzo katika jiji la Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa uhodari wa kuimba na kunengua.

Kabla ya ngoma hiyo, nguli huyo awali alifanya onesho kabambe akishirikiana na wakali wenzake, akina General Defao, Scola Miel, MJ 30 na Celenzino.Bozi alikuwa kimya pasipo kupakua wimbo wowote kwa kipindi kirefu, akijiandaa kufanya makubwa.

Licha ya umri wake wa miaka wa miaka 67, bado anao uwezo mkubwa wa kutunga na kuimba nyimbo za muziki wa dansi.Bozi Boziana alijipatia umaarufu wakati akisikika akirap maneno ya “Nzawisaa, Nzawisaaa maama Nzawisaaa..Yelooh!!!” kwenye nyimbo za bendi yake.

Ukimuita kwa jina la Mbenzu Ngamboni Boskill, hautakuwa umekosea kabisa kwa kuwa ndiyo aliyopewa na wazazi wake baada ya kuzaliwa.
Bozi Boziana alizaliwa mwaka 1952 huko Jamhuri ya Kidemkokrasia ya Kongo.

Katika hatua za kutafuta mafanikio, Boziana alipitia katika bendi nyingi kubwa na ndogo nchini mwake zikiwa ni pamoja na Bamboula de Papa Noel, Minzoto Sangela, Zaiko Langa Langa, Isifi Lokole, Yoka Lokole, Langa Langa Stars na Choc Stars.

Baadhi ya wapenzi wakampachika jina bandia la ‘Mzee Benzi’ ambalo limekuwa maarufu.Katika kutafuta njia ya kujikwamua kimaisha, Bozi Boziana aliamua kuunda bendi yake ya Orchestra Anti-Choc, ambayo anaiongoza hadi sasa.

Licha ya utunzi na uimbaji, pia ni mkung’utaji mzuri wa gitaa na kulishambulia jukwaa akishirikiana na akina dada wawili Betty na Scolla Miell.

Mzee Benzi alianzia muziki wa Afro-Pop katika bendi ya Air Marine. Lakini alianza kuyaona mafanikio ya kazi zake ilipotimu mwaka 1974 alipojiunga na bendi ya Zaiko Langa Langa, hivi sasa bendi hiyo inaongozwa na Nyoka Longo.

Zaiko LangaLanga ilikuwa na waimbaji mashuhuri wakati huo wakiongozwa na mkongwe Papa Wemba na mwezake Evoloko Jocker.

Lakini haikuzidi mwaka, Papa Wemba na Evoloko waliondoka bendi hiyo baadae hata Bozi Boziana aliwafuata kwenda kuanzisha bendi mpya ikaitwa Isifi Lokole.

“ Fahari wawili hawakai zizi moja” usemi huo ulijidhirisha baada ya wanamuziki hao kushindwa kukubaliana katika maswala mbalimbali ya msingi yaliyopelekea wanamuziki wake akina Papa Wemba, Boziana, Mavuela Somo na wengine kuondoka bendi ya Isifi Lokole.

Walienda kuunda bendi yao mpya iliyopewa jina la Yoka Lokole.

Bendi ya Yoka Lokole ilipata mafanikio makubwa mwaka 1976, japokuwa ilipotimu mwinshoni mwa mwaka huo, Papa Wemba aliiacha bendi hiyo, akaenda kuanzisha bendi ya Viva la Musica.

Bozi Boziana mwaka 1977 naye aliicha bendi hiyo ya Yoka Lokole, licha ya bendi hiyo kuwa maarufu kwa kipindi kifupi.

Kwa miezi michache Boziana alishirikiana na mwanamuziki Efonge Gina, ambaye naye alikuwa katika bendi ya Zaiko Langa Langa.

Walirekodi nyimbo kadhaa kama vile Selemani iliyotungwa na Bozi Boziana na Libanko Ya Ngai utunzi wake Gina.

Mwanamuziki aliyekuwa na uwezo mkubwa wa fedha Kiamuangana Mateta ‘Verkies’ mwaka 1981, aliibadilisha bendi ya Soukous Super Group na kuiita Langa Langa Stars.

Bendi hiyo ilikuwa imesheheni vipaji vya wanamuziki kaiwemo Evoloko Jocker, Dindo Yogo na wengine wengi.

Bozi Biziana alialikwa kujiunga na vijana hao, pasipo kusita akaukubali na kuicha Zaiko Langa kwa mara ya pili.

Langa Langa Stars ilidumu kwa miaka michache iliyofuatia kabla na Boziana naye akaondoka kwenda kujiunga na bendi kubwa nchini humo ya Choc Stars, aliyokuwa chini Ben Nyamabo ambako alipiga hadi mwezi Novemba 1985.

Akiwa na bendi hiyo ya Choc Stars, Boziana alirekodi baadhi ya nyimbo ambazo zilikuja kuwa maarufu za Sandu Kotti, Alena, Mbuta-Mutu na Retrouvailles a Paris.

Choc ilikuwa na wanamuziki wengi wenye vipaji lukuki wakiwemo akina Fifi Mofude, Djo Nolo, Koffi Alibaba, Wally Ngonda, Rigo Star, Ngouma Lokito, Deesse Mukangi, Marthe Lamugenia, Ngimbi Yespe na Maoussi Solange.

Mpiga gita wa kwanza katika bendi hiyo alikuwa Matou Samuel ambaye kwa sasa anaimba muziki wa Injili na nafasi yake ilishikwa na Dodoly ambaye kabla ya kujiunga humo alitokea katika bendi ya mwanamuziki Lita Bembo ya Orchestre Stukas.

Dodoly alipachikwa jina bandia la ‘The sewing machine’ kwa umahiri wake wa kutumia vidole vyake kucharaza nyuzi kwa kasi kubwa.Tokea miaka ya 1980 Boziana aliendelea katika bendi yake ya Anti-Choc ikiwa ni pamoja na kurekodi nyimbo akishirikiana na wanamuziki wengine mahiri.

Boziana aliwahi kushinda zawadi ya Kora All-African kwa album yake kuwa bora toka nchi za Afrika ya Kati.

Wapenzi wa muziki hapa nchini watamkumbuka Bozi jinsi alivyoziteka nyioyo za wapenzi katika maonesho kadhaa aliyoyafanya hapa nchini.

Alifanya maonesho kadhaa akishirikiana na wasanii wake wa kike Deesse Mukangi na Joly Detta walivyokuwa wakiimba na kulishambulia jukwaa kwa mtindo wao wa ‘Nzawisa’ katika nyimbo za Tembe na Tembe, Palpitation na zingine nyingi zilifanya watu kuviacha viti vyao kwenda kuwatuza.

Bozi Boziana mwenye sauti nzuri yakupendeza, kuna kipindi alibadili dini yake na kuwa muislamu, akapewa jina la Abubakar.

Baadhi ya nyimbo alizowahi kufyatua ni pamoja na Masumu Akey, Mitshuri, Mbuza, Ba Bokilo, Benson Nostalgique, Mon Mari Est Gabonais na Pere Noelle Confiance.

Zingine ni Fiko Fikolo, Chama Chiko, Mya , Ka Munu Ve’, Mifune, Popy Bopase ya mwaka 1998 na Tembe na Tembe.Zingine ni Bana DRC, Riana, Anytha, Sonto ya 1989, Makambo Evelyn ya mwaka 1989, Pot Pourri , Mfumu na Alena.

Bozi alachia vibao vingine vya Sisina, Doukoure, Switzerland, Wakamba, Mansanga na Betlem.Mzee Benzi alifyatua vibao vingi mno vilivyompa sifa nyingi ukiwemo wa La reine de Sabah, Lelo Makambo Lobi na Fleur de Lys ambazo alimshirikisha mwimbaji wa kike Joly Delta.

Watanzania watamkumbuka alivyofanya mambo makubwa katika muziki kwa mara ya mwisho alipokuja humu nchini kwa mwaliko wa Kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET) iliyo chini ya uongozi wa Mkurugenzi Asha Baraka.

Bozi Boziana ni mfano wa kuigwa jinsi anavyoweza kutulia, baadaye anatoka na nyimbo zainazokubalika na kudumu masikioni mwa wapenzi wa muziki huo.

Hii ni tofauti sana na wanamuziki na wasanii wetu, ambao ‘huopoa chakula watu wale hata kabla hakijaiva!.

United States Disburses Grants Worth $750,000 to Create Jobs for Rural Youth

$
0
0
Ms. Abella Bateyunga (right) from the Tanzani a Bora Initiative receives Advancing Youth grant for 209,057,674 TZ shillings. Ms. Bateyunga is accompanied, from left to right, by Mbeya Regional Commissioner, J. Chalamila; PO-RALG Minister, Selemani Jafo; USAID Mission Director, Andrew Karas; and USAID Private Sector and Youth Project Management Specialist Joyce Mndambi. (Photo: Courtesy of U.S Embassy).



USAID Mission Director, Andy Karas addresses a Feed the Future meeting in Mbeya on Wednesday. (Photo: Courtesy of U.S Embassy).

***********************************

Mbeya, Tanzania – On May 29, 2019, the United States Government disbursed grants worth a total of $750,000 to nine institutions that support job creation, entrepreneurship, leadership, and healthy living among youth.



The grants are supported by the Feed the Future Tanzania Advancing Youth activity, funded by the United States Government through the United States Agency for International Development (USAID), and are expected to create 950 jobs for youth in 700 new or improved youth-led enterprises across the regions of Iringa, Mbeya, and Zanzibar.

The Mission Director for USAID, Andrew Karas, and Honorable Suleiman Jafo, the Minister for the President’s Office Regional Administration and Local Government (PO-RALG), presented the grants to the local institutions.
During his remarks, Mr. Karas noted that “Investing in youth leadership in Tanzania is a priority for USAID and the Government of Tanzania. Tanzania is a young country, and its population is expected to double in the next 25 to 30 years. Deliberate efforts are needed by the government, private sector, and communities to ensure that the energy, talents, and
optimism of today’s youth, as well as the next generation, make Tanzania a place of promise and prosperity for all.”

The Advancing Youth activity encourages rural youth to engage in Tanzania’s agriculture sector and supports increased economic opportunities for young people aged 15–35 while promoting leadership and healthy lifestyles. Through its grants program, Feed the Future Tanzania Advancing Youth transforms challenges into opportunities for rural youth to drive and advance Tanzania’s economic growth.

ALIYEFUKUA KABURI LA BABA YAKE KUCHUKUA BLANKETI ALIWAKIMBIA ASKARI MAHAKAMANI.

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akitoa maelekezo kwa wajumbe wa Bodi mpya ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Magereza, kabla ya kuizindua Bodi hiyo, jijini Dodoma, leo. Wapili kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Phaustine Kasike.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akizungumza kabla ya Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola (wapili kushoto) kuizindua Bodi mpya ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Magereza, jijini Dodoma, leo. Wapili kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Phaustine Kasike, akitoa historia fupi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi hilo, kabla ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) kuizindua Bodi hiyo, Jijini Dodoma, leo. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu.
Mwenyekiti wa Bodi Mpya ya Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza, Meja Jenerali Mstaafu, Raphaeli Muhuga, akitoa neno la shukrani baada ya uzinduzi wa Bodi hiyo, jijini Dodoma leo. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu (wapili kulia), Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike (kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi mpya ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Magereza, baada ya uzinduzi wa Bodi hiyo, jijini Dodoma leo.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
………………..

Na EZEKIEL NASHON, DODOMA.
Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola ameiagiza bodi mpya ya Shirika la uzalishaji mali la Jeshi la Magereza nchini, ndani ya miezi miwili ihakikishe maeneo yote yaliyochini ya miliki ya Jeshi hilo kuhakikisha yamepimwa na kuwa na hati miliki pamoja na nyaraka zote.

Sambamba na hilo bodi ihakikishe inakuja na mipango thabiti ya kuimarisha shirika hilo, ikiwa ni pamoja na Jeshi la Magereza linajitegemea kwa kila kitu bila kutegemea Serikali kuu.

Waziri Kangi Lugola umetoa maagizo hayo Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa bodi ya Shirika la uzalishaji mali la jeshi la Magereza iliyoundwa kusimamia miradi yote iliyochini ya Shirika hilo ili iweze kuleta tija kwa Jeshi na jamii.

Amesema bodi hiyo ihakikishe ndani ya miezi miwili kwa kushirikiana na wataalamu ndani ya Jeshi hilo maeneo yote yanayomilikiwa na jeshi la magereza yawe yemepimwa na kuwa na hati miliki halali, kwa sababu kumekuwa na migogoro mingi katika maeneo hayo kwa sababu hayana hati miliki na kushindwa kuendelezwa.

“Niwaagize bodi mpya ndani ya miezi miwili muhakiki mnakuja na mpango mkakati wa kuhakikisha shirika hili linainuka kutoka hapa lilipo na kufikia kujitegemea kwa kila kitu bila kutegemea hata senti moja kutoka serikali kuu”,

“Maeneo mengi ya magereza hayaendelezwi na niliambiwa kuwa shida ni kwamba maeneo mengi hayana hati miliki sasa niagize bodi hii mhakikishe maeneo hayo yanapimwa na kuwa na hati miliki pamoja na nyaraka” amesema Lugola.

Ameitaka bodi hiyo kuhakikisha inatatua changamoto zote ambazo zinaikabili shirika hilo ambazo zilikuwa zinasababisha shirika hilo kuto kuendelea na kuleta tija kama malengo ya kuanzishwa kwake ikiwa ni pamoja na kupunguza msongamano wa mahabusu.

Ameagiza maeneo yote yanayomilikiwa na jeshi la magereza ambayo yatakuwa hayatumiki kwa matumizi yoyote yapandwe miti na kuhakikisha kila mfungwa katika magereza apande miti ya kuzalisha mbao ili isaidie katika viwanda vinavyoanzishwa na shirika hilo.

Pia ameitaka bodi hiyo kuja na suruhu ya kuhakikisha taasisi zote zinazodaiwa na shirika hilo ambayo kwa sasa deni hilo linafikia shilingi bilioni 6.45, amesema fedha hizo zikipatikana zitasaidia kuinua shirika hilo.

Kwa upande wake kamishna wa Jeshi la Magereza Nchini Faustine Kasike amesema shirika hilo lipo chini ya jeshi la magereza na lilianzishwa mwaka 1983 kwa mujibu wa sheria ya bunge ya mashirika na 23 ya mwaka 1974.
Amesema shirika lilianzishwa kwa lengo la kujiendesha kiuchumi na kibiashara baada ya miradi ya jeshi la magereza iliyokuwa ikiendeshwa kwa kutegemea fedha za serikali kushindwa kujiendesha kutokana na fedha hizo kutokufika kwa wakati.

Nae Katibu mkuu wa Wizara hiyo Jacob Kingu amesema kuzinduliwa kwa bodi hiyo ni historia kwani mda mrefu sana shirika hilo limefanya kazi bila ya kuwa na bodi na kusababisha kusuasua katika utendaji kazi wake.
Amesema katika Magereza kumi(10) ya kimkakati yaliyotengwa ametembelea Magereza saba(7) amesema hayo yote yamefanya vizuri, katika miradi mbalimbali inayotekelezwa katika magereza hayo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi hiyo Meja Jenerali mstaafu Raphael Muhuge, amesema bodi hiyo itatimiza majukumu yote iliyopewa na kuhakikisha inasimamia shirika hilo kikamilifu ili kuleta tija, ameahidi kuhakikisha shirika hilo linatoa gawio kwa serikali.

“Ni kuhakikishie mheshimiwa bodi hii itafanya kazi kwa ueledi mkubwa na kuhakikisha linaleta tija kwa jamii, ikiwa ni pamoja na kutimiza majukumu yote iliyopewa, na nikuhakikishie tutahakikisha shirika hili linatoa gawio kwa serikali”, amesema.

DKT. ABBASI: MAONO NA MTAZAMO WA RAIS MAGUFULI YAZIDI KUPAISHA MAKUSANYO YA MAPATO YA MADINI

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari ( hawapo pichani), kuhusu utekelezaji wa Serikali kwenye sekta mbalimbali, katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi 30. Mei. 2019. 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, Akizungumza na Waandishi wa Habari, kuhusu utekelezaji wa Serikali kwenye sekta mbalimbali, katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi 30. Mei. 2019. 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akionyesha nakala ya Jarida la Nchi yetu lililochapisha habari za (Sekta ya Madini) linalotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni, kwa Waandishi wa Habari katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi 30. Mei. 2019.
(Picha na Paschal Dotto-MAELEZO). 

……………………………………………………… 

Na Mwandishi Wetu,- MAELEZO- DAR ES SALAAM 

SERIKALI imesema maono na mtazamo yakinifu wa Rais Dkt. John Magufuli katika usimamizi na ufuatiliaji wa sekta ya madini, umewezesha ongezeko maradufu la makusanyo ya mapato ya sekta hiyo kutoka Tsh Bilioni 210 mwaka 2015/16 hadi kufikia Tsh Bilioni 302 kwa mwaka 2018/19 na kuifanya Tanzania kuzidi kujijenga Kiuchumi. 

Akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari leo Alhamisi (Mei 30, 2019) Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, alisema Serikali ya Awamu ya Tano inafanya kazi kisayansi na itahakikisha rasilimali za nchi zinaendelea kulindwa ili ziweze kuleta manufaa kwa Watanzania wote. 

Dkt. Abbasi alisema mara baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani Novemba 2015, ilifanya mageuzi mbalmbali katika usimamizi na ufuatiliaji wa rasilimali za madini, kwani huko nyuma Serikali ilikuwa ikipoteza kiasi kikubwa cha fedha na kuamua kuchukua hatua stahiki ikiwemo kufanya mabadiliko katika Sheria ya Madini ya mwaka 2010. 

“Tulipofanya marekebisho katika sheria yetu ya madini mwaka 2017, matokeo tumeanza kuyaona kwani tumedhibiti mianya yote ya upotevu wa mapato yetu na kuanza kusimamia kwa umakini mkubwa utoroshaji mkubwa wa madini ambapo ilisababisha Serikali kupoteza kiasi kikubwa cha mapato” alisema Dkt. Abbasi. 

Akitolea mfano Dkt. Abbasi alisema kufuatia agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kuanzishwa kwa masoko ya madini ambayo ni utekelezaji wa sheria ya madini ya mwaka 2017, hadi sasa kuna jumla ya masoko 24 ambayo yamekuwa yakithibiti ubora, thamani na takwimu za madini nchini, ambapo soko la kwanza lilianzishwa Mkoani Geita, mwezi Machi mwaka huu. 

Aidha Dkt. Abbasi alisema Takwimu za jumla za uzalishaji wa dhahabu katika kipindi cha miezi miwili , mkoani Geita kuanzia mwezi Machi hadi Mei, mwaka huu zinaonyesha kuwa uzalishaji umeongezeka kwa kiasi kikubwa na kufikia kilo 312.65 za dhahabu ukilinganisha na uzalishaji wa dhahabu kilo 259.12 zilizokuwa zikizalishwa kabla ya masoko hayo. 

“Mwezi April, pekee uliweka rekodi ya Geita kwa kuzalisha kilo 200 ambazo hazijapata kufikiwa mkoani humo kwa wachimbaji wadogo na wa kati na kwa Takwimu za Mei mwezi mwaka huu zinazidi kuthibitisha kuwa Watanzania wanapaswa kuendelea kumuombea na kumuunga mkono Rais Magufuli” alisema Dkt Abbasi. 

Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema eneo lingine la mageuzi yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika sekta ya madini ni pamoja na maamuzi iliyochukua ya kujenga ukuta kuzunguka eneo la wachimbaji wa Madini ya Tanzanite Mkoani Manyara ambao Serikali iliweka mifumo ya masoko na ukaguzi, na hivyo kuchangia ongezeko la mapato ya wachimbaji wadogo na Serikali kwa ujumla. 

Akifafanua zaidi Dkt. Abbasi alisema uzalishaji wa madini ya Tanzanite kutoka kwa wachimbaji wadogo ulioripotiwa kwa mwaka 2016 ulikuwa kilo 164.6 na kilo 147 kwa mwaka 2017, ambapo Serikali iliweka kukusanya kiasi cha Tsh Milioni 71 (2016) na Tsh Milioni 166 (2017), lakini uzalishaji huo uliongezeka maradufu mara baada ya Serikali kujenga ukuta huo. 

“Uzalishaji uliongeza sana mara baada ya ujenzi wa ukuta kwani Kilo 781.2 zilizalishwa mwaka 2018 na kuiingizia Serikali mapato ya Tsh Bilioni 1.43 na uzalishaji kwa mwaka 2019 katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Mei ulikuwa kilo 1086.05 zenye thamani ya Tsh Bilioni 1.422” alisema Dkt. Abbasi. 

Aliongeza kuwa mabadiliko hayo yameanza kuleta faida kwa nchi ambapo kwa sasa nchi nyingi za Afrika zimeanza kuiga mageuzi yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ikiwemo kupitia upya mikataba na wawekezaji na pia watafiti mbalimbali wanairejea Tanzania inayogeuza “laana” ya madini kuwa “Baraka” ya Madini.

Watoto Wa Kike Zaidi Ya 2,454 Wapewa Mimba

$
0
0

Na, Editha Edward-Tabora 

Zaidi ya Watoto 2,454 wenye umri wa chini ya Miaka 20 katika Halmashauri ya Wilaya  Nzega Mkoani Tabora Watoto hao wanapata mimba za utotoni kwa takwimu za Mwaka 2018 Huku robo yao mwezi wa kwanza hadi wa tatu 2019 mimba chini ya miaka 20 zilikuwa 603 Huku Sababu zikielezwa 
Kuwa ni umasikini pamoja na ukatili wa kijinsia 

Takwimu hizo zimetolewa katika kikao kilichokutanisha wadau mbalimbali mjini Nzega  na shirika lisilo la Kiserikali la World Vision linaloendesha kampeni hii ya kupambana na Mimba na ndoa za utotoni likishirikiana  na Serikali ili kutokomeza janga hili ambalo linakwamisha ndoto za Watoto wa kike 

Bertha Mtesigwa ambaye ni Mratibu wa shirika la world Vision amesema Mradi huo una miaka saba ukitekelezwa na shirika hilo Lakini tatizo hilo linendelea kupungua japo amesema chngamoto haziishi 

"Mimba hizi zimechangiwa na Sababu mbalimbali ikiwemo ya kwanza ni umasikini uliokithiri kutoka katika jamii zetu za watu wa Nzega Lakini kumekuwa na uelewa mdogo kuhusu suala la Malezi Makuzi ya mtoto na mila potofu ambazo zimechangia sana kuongezeka kwa mimba za utotoni "Amesema Mtesigwa

Meneja wa shirika la world Vision John Masenza amesema vyombo vya dola vinaendelea kupambana na tatizo hilo na amewaomba Wananchi Kushirikiana na shirika hilo ili kukomesha mimba za utotoni 

Aidha idadi kubwa ya wanaopata mimba za utotoni ni wanafunzi wa shule za Msingi na shule za Sekondari.
 Wadau mbalimbali wakiwa katika kikao kilichoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la world Vision linalopambana na mimba za utotoni.
John Masenza meneja wa shirika la world Vision akizungumza na wadau.

MIFUKO YA PLASTIKI MWISHO LEO MEI 31, 2019-MKURUGENZI KIGAMBONI

$
0
0
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni,Ng’wilabuzu Ludigija (wa mbele) akiwa ambeamatana na watendanji wa Manispaa hiyo kuwaelimisha wananchi mwisho wa matumizi ya mifuko ya plastiki  kuwa ni leo Mei 31, 2019,amesema ni marufuku kutengeneza, kuingiza, kuuza na kutumia mifuko ya plastiki  kwa ajili ya kubebea bidhaa za aina yoyote  katika Manispaa hiyo.Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Meneja wa Mkuu wa Green Waste,Allan Sudi akimkabidhi  Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni,Ng’wilabuzu Ludigija makasha ya kukusanya kata za mifuko ya plastiki kuunga mkono katazo la Serikalui la kupiga marufuku matumizi  ya mifuko ya plastiki.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni,Ng’wilabuzu Ludigija akizungumza na wananchi wa kigamoni juu ya mwisho wa matumizi ya mifuko ya plastiki  ni leo Mei 31, 2019.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni,Ng’wilabuzu Ludigija (kulia) akiwa maeambana na watendanji wa Manispaa hiyo wakiangalia mifuko iliyopo katika soko kuu  la kigambani na kuwapa elimu wanachi juu ya mwisho wa matumizi ya mifuko ya plastiki  ni leo Mei 31, 2019.
 Wananchi wakiweka mifuko ya plastiki katika makasha ya kukusanya kata.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ferry,Juma Mwingamno (watatu kulia) akitoa elimu kwa wananchi wa Kigamboni kuhusu  kosa kisheria pindi watakapokutwa na mifuko ya Plastiki.

DC MBONEKO AFUNGA MASHINDANO YA UMISSETA MKOANI SHINYANGA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, amefunga rasmi mashindano ya michezo kwa shule za Sekondari (UMISSETA 2019) Mkoani Shinyanga, na kuwataka washindi watakaoungana na kuwa timu moja ya mkoa, wakashiri kikamilifu katika mashindano hayo ngazi ya kitaifa huko Mtwara, na kupata ushindi wa makombe mengi.

Mashindano hayo ya (UMISSETA) yalifunguliwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack Mei 27, 2019 ambapo yamefungwa leo Mei 30 na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kwenye viwanja vya CCM Kambarage mjini humo, ambapo washindi wamepewa zawadi za makombe. 

Mashindano yalishirikisha timu mbalimbali kutoka halmashauri ya Kahama Mji, Msalala, Ushetu, Kishapu, Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga kwa kuchezwa mpira wa miguu, kikapu, pete,tenesi, wavu, riadha, kucheza ngoma, pamoja na kuimba kwaya. Akizungumza wakati akifunga mashindano hayo,Mboneko amewataka washiriki ambao watachaguliwa kuwa timu moja za kwenda kushiriki (UMISSETA) ngazi ya kitaifa, wawe kitu kimoja na kutobaguana kuwa huyo anatoka halmashauri nyingine, bali washindane kama timu moja ambayo inatoka mkoani Shinyanga na hatimaye kuibuka na ushindi. 

“Nawapongeza wanafunzi wote mlioshiriki kwenye mashindano haya ya (UMISSETA) ambapo mmeonyesha vipaji vyenu na wote ni washindi, lakini hamtaweza wote wanafunzi 704 kwenda kushiriki ngazi ya kitaifa, bali tutachagua wanafunzi 120 ili wakatuwakilishe na tunataka mrudi na makombe mengi,” amesema Mboneko. “Na mtakapokuwa kambini muwe timu moja na kutobaguana kuwa huyu anatoka halmashauri hii, sitaki kitu kama hicho bali nataka muwe ndugu kwani nyie wote mnatoka Shinyanga, na mkashindane kweli kweli kwa kuonyesha vipaji vyenu na kuupatia sifa mkoa wetu,”ameongeza.

 Pia amewataka washindi ambao watachaguliwa kwenda kushiriki mashindano hayo ngazi ya kitaifa, wakaonyeshe nidhamu ya hali ya juu na siyo kwenda kuchafua sifa ya mkoa. Naye Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahundi, amewataka wanafunzi hao pindi watakapokuwa huko Mtwara, waonyeshe vipaji vyao ikiwa michezo ni ajira kwa sasa. 

Aidha washindi waliopatikana kwenye mashindano hayo ya (UMISSETA) Mwaka 2019 mkoani Shinyanga, mpira wa miguu wavulana ni halmashauri ya Msalala, wasichana halmashauri ya Shinyanga, mpira wa mikono (Handball) wavulana Manispaa ya Shinyanga, wasichana Kishapu, Volleyball Manispaa ya Shinyanga, wasichana halmashauri ya Shinyanga. 

Kwa upande wa mpira wa kikapu wavulana na wasichana washindi ni kutoka halmashuri hya Shinyanga, mpira wa pete Kahama Mji, Tenesi mshindi wavulana na wasichana ni Halmashauri ya Shinyanga , riadha wavulana Shinyanga, wasichana Kishapu, ngoma kutoka Ushetu, kwaya Kahama Mji, usafi na nidhamu wavulana Kahama Mji, wasichana Shinyanga.

 Hata hivyo katika mashindano hayo ya UMISSETA (2019) Mshindi wa jumla alitoka halmashauri ya Shinyanga , huku kauli mbiu ya mwaka huu inasema ‘MICHEZO NA SANAA KWA ELIMU BORA NA AJIRA.’ TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akifunga rasmi mashindano ya michezo ya UMISSETA 2019 na kuwataka washindi ambao wamechaguliwa kushiriki ngazi ya kitaifa wakawe kitu kimoja na kupata ushindi wa makombe mengi. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog Afisa elimu mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahundi akiwataka wanafunzi ambao wamechaguliwa kwenda Mtwara kwenye mashindano hayo ya (UMISSETA) wakaonyeshe nidhamu ya hali ya juu. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akifungua fainali ya mashindano ya (UMISSETA 2019) kati ya timu ya mpira wa miguu Kahama Mji na Msalala huku kwa upande wa wasichana ni Kahama Mji na Shinyanga , na kuwataka wacheze kwa nidhamu kwa kuonyesha vipaji vyao. Fainali ikiendelea kuchezwa kati ya timu ya Kahama Mji wenye jezi ya njano pamoja na Msalala wenye jezi nyekundu, ambapo hadi dakika 90 zinakamilika walitoka sare ya kufungana goli moja kwa moja na hatimaye kwenda kwenye matuta ili mshindi aweze kupatikana. Msalala waliibuka na ushindi wa magoli 4 kwa matatu dhidi ya Kahama Mji na hatimaye kuwa mabingwa rasmi kwa mpira wa miguu katika UMISSETA Mwaka (2019) Mkoani Shinyanga. Mchezo wa Fainali wa mpira wa miguu ukichezwa kati timu ya wasichana ya Shinyanga wenye Jezi ya Lightblue, na Kahama Mjini wenye Orange, ambapo Shinyanga waliibuka na ushindi wa goli moja na kuwa mabingwa. Wanafunzi kutoka halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama wakiangalia fainali ya michezo ya mpira wa miguu kwa wasichana na wavulana kwenye hitimisho la mashindano ya (UMISSETA) 2019 Mkoani Shinyanga. Wanafunzi kutoka shule mbalimbali mkoani Shinyanga pamoja na walimu wao wakiwa wanaangalia fainali ya mpira wa miguu ya wasichana na wavulana kwenye hitimisho la mashindano ya michezo ya (UMISSETA) mkoani Shinyanga. Wanafunzi kutoka shule mbalimbali mkoani Shinyanga wakiwa wanaangalia fainali ya mpira wa miguu ya wasichana na wavulana kwenye hitimisho la mashindano ya michezo ya (UMISSETA). Wanafunzi kutoka Ushetu wakitoa burudani ya ngoma. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikabidhi Kombe kwa mshindi wa mpira wa miguu kutoka halmashauri ya Msalala. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikabidhi kombe kwa washindi wa mpira wa miguu kwa upande wa wasichana kutoka halmashauri ya Shinyanga. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikabidhi Kombe kwa mshindi wa jumla kwenye hitimisho la mashindano hayo ya michezo ya UMISSETA Kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Awali makombe yakiandaliwa tayari kwa kukabidhiwa washindi wa mashindano ya michezo ya UMISSETA mkoani Shinyanga mwaka 2019. Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images