↧
Mdau Francis na Winnie wameremeta
↧
ngoma azipendazo ankal
Ngoma ya Johnny Clegg (na Nelson Mandela) ya 'Asimbonanga' inakufanya utoe chozi
↧
↧
miondoko ya kumeremeta kwenye mnuso
↧
Mhe. Angela Kairuki atajwa kuwa miongoni mwa wanawake vijana 20 wenye nguvu barani Afrika 2013
Mhe. Kairuki |
Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Angela Jasmine Kairuki (37) ametajwa katika jarida la kimataifa la Forbes kuwa ni mmoja wanawake vijana 20 wenye nguvu barani Afrika mwaka huu.
Katika toleo lake la hivi karibuni chini ya kichwa cha habari ‘The 20 Young Power Women in Africa 2013’, jarida la Forbes linamuorodhesha Mhe Kairuki sambamba na wanawake wengine 19 kama vijana wa kike wenye nguvu kwa nafasi zao kikazi na kibiashara.
Kutajwa kwa Mhe Kairuki katika orodha hiyo kumezua msisimko katika mawasiliano ya mtandao wa 'twitter' ambapo Watanzania wengi wamekuwa wakielezea furaha na fahari zao kwa kuona Mtanzania mwenzao, tena mwanamke kijana, anatambulika kimataifa kwa utendaji wake.
Mhe. Angela Kairuki akitembelea Jeshi la Magereza katika mojawapo ya shughuli zake za kikazi |
Wanawake wengine waliotajwa na jarida hilo ni Mimi Alemayehou (Ethiopia) Makamu wa RAis Mtendaji wa Overseas Private Investment Corporation (OPIC), Vera Songwe(Cameroon) Mkurugenzi Mkazi World Bank Senegal, na Tara Fela-Durotoye (Nigeria) Mwanzilishi wa House Of Tara.
Wengine ni Rapelang Rabana (Afrika Kusini) Mjasiriamali, Claire Akamanzi (Rwanda) Afisa Mtendaji Mkuu wa Rwanda Development Board, Valentina da Luz Guebuza (Msumbiji) Mwekezaji, Hadeel Ibrahim (Sudan) wa Mo Ibrahim Foundation, Alengot Oromait (Uganda) Mbunge, na Monica Musonda, (Zambia) Afisa Mtendaji Mkuu na MWanzilishi wa kampuni ya Java Foods.
Wengine ni NoViolet Bulawayo (Zimbabwe) Mtunzi wa vitabu, Minoush Abdel-Meguid (Misri) Mwekezaji, mjasiriamali na mwendesha benki, Ola Orekunrin (Nigeria) Daktari na Mwanzilishi wa The Flying Doctors, Sibongile Sambo (Afrika Kusini) Afisa Mtendaji Mkuu na Mwanzilishi wa SRS Aviation, Lupita Nyong’o (Kenya) Mwigizaji na mtengeneza filamu, Amini Kajunju (Congo DRC) Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Africa-America Institute na Folake Folarin-Coker (Nigeria) Mbunifu wa mitindo.
Wengine katika orodha hiyoni Lindiwe Mazibuko (Afrika Kusini) Mwanasia na Kiongozi wa chama cha Democratic Alliance (DA) bungeni, Minoush Abdel-Meguid (Misri) Mwekezaji, Mjasiriamali na mwendesha benki, Sibongile Sambo (Afrika Kusini), Wangechi Mutu, (Kenya) Msanii na mchongaji.
↧
Mhe Zitto Kabwe akisoma ripoti ya kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali (PAC) leo
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe Zitto Kabwe akito taarifa ya mahesabu ya serikali a huu Bungeni Dodoma leo Novemba 7, 2013
↧
↧
TASWIRA YA BARABARA YA MABASI YAENDAYO HARAKA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM
↧
news alert: meli ndogo ya mizigo yazama kilwa masoko, mtu mmoja hajulikani aliko
Na Abdulaziz Video, Kilwa
Mtu mmoja aliefahamika kwa Jina la Nice Mtega fundi mkuu wa Meli ndogo ya mizigo iitwayo MV MERCI II inayomilikiwa na Semuhungu Shingiro anahofiwa kufa maji baada ya kutoweka kwa zaidi ya masaa 36 toka kuzama kwa meli hiyo katika bandari ya Kilwa masoko.
Akiongea na Globu ya Jamii hii iliyofika katika eneo hilo, meneja wa Bandari ya Kilwa, Bw. Iddi Omary, alieleza kuwa Meli hiyo iliyofunga gati jana jioni ikitokea songosongo na kupakia tani 30 za mchanga na tani 30 za maji ilizama majira ya saa 6 usiku wa kuamkia leo ambapo Nahodha wa Meli hiyo Captain Charles Kalinga na wasaidizi wake 3 walifanikiwa kutoka ila Nice Mtega aliekuwepo ndani hajaonekana hadi sasa. Juhudi za kumtafuta na kuinua meli hiyo zinaendelea. Sababu ya kuzama kwake bado hazijajulikana
Meli hiyo ikiwa imezama majini katika gati la Kilwa Masoko
Sehemu ya chini ya meli
MERCI III kabla ya kuzama
Meli ikiwa majini
↧
Makamu wa Rais mgeni rasmi Mbio za Uhuru Marathon leo
↧
shairi la maya angelou kwa madiba
Here is a poem that Maya Angelou wrote and delivered as a tribute to the great Nelson Mandela, who died Thursday at the age of 95. Watch it. It is worth the four minutes and 40 seconds it will take to listen.
↧
↧
WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA AZINDUA JIMBO LA KANISA LA SABATO JIJINI DAR
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aizungumza wakati alipozindua Jimbo la Kusini mwa Tanzania la Kanisa la Waadventista wa sabato kwenye uwanja wa maonyesho wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Desemba 7, 2013. Wengine pichani ni Maaskofu kwa kanisa hilo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na maaskjofu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato baada ya kuzindua Jimbo la Kusini kwa Tanzania la Kanisa hilo kwenye uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Desemba 7, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na maaskofu wa kanisa la Waadventista wa Sabato baada ya kuzindua Jimbo la Kusini mwa Tanzania kwenye uwanja wa maonyesho wa Mwali Nyerere jijini Dar es salaam Desemba 7, 2013.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nisahati na Madini, Eliakim Maswi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
↧
IGP MWEMA ATEUA MAKAMANDA WA MWANZA, MBEYA NA SIMIYU
↧
Rais Kikwete arejea nchini akitokea Ufaransa
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni wakati aliposimama kwa muda katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi akiwa njiani kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano unaohusu Amani na usalama na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Bara la Africa na Ufaransa.Kulia aliyesimama ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Amina Mohamed na kushoto ni afisa itifaki.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Amina Mohamed wakati aliposimama kwa muda katika uwanja wa ndege jijini Nairobi, Kenya alipokuwa akirejea nyumbani akitokea Paris Ufaransa ambapo alihudhuria Mkutano uliohusu Amani,Usalama na Ushirikiano wa kiuchumi kati ya Ufaransa na bara la Afrika.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Mec Sadik akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere muda mfupi baada y kuwasili akitokea Paris Ufaransa ambapo alihudhuria Mkutano wa Amani,Usalama na Ushirikianokati ya Afrika na Ufaransa uliomalizika jana.(picha na Freddy Maro)
↧
Mbio za Uhuru Marathon zafana sana jijini Dar leo,Makamu wa Rais,Dkt. Bilal Mgeni Rasmi
Mshindi wa Kwanza wa Mbio ndefu za KM 42 katika Mashindano ya Uhuru Marathon,Jamin Ikai (kutoka nchini Kenya) akiwasili kwenye viwanja vya Leaders Club wakati akimaliza mbio hizo,zilizofanyika leo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania.![]()

Washindi wa Mbio ndefu za KM 42 katika Mashindano ya Uhuru Marathon wakiwa wamesimama mbele ya mgeni rasmi,mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao.Mshindi wa Kwanza ni Jamin Ikai (kutoka Kenya),Steven Selevestor (kutoka Jeshi la Magereza Tanzania) pamoja na Aley Sanka (Tanzania).
Washindi wa Mbio ndefu za KM 42 (wanawake) wakiwa wakiwa wamesimama mbele ya mgeni rasmi,mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao.Mshindi wa wa Kwanza ni Thabita Kibet (kutoka Kenya),Naum Jerkosgei (Kenya) pamoja na Banoela Brigton.![]()

Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Mbio za Uhuru Marathon,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa hotuba yake wakati wa maadhimisho mbio hizo zilizofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo,ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania.
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenella Mukangara akisoma hotuba yake kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi,wakati wa maadhimisho mbio hizo zilizofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo,ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania.
↧
↧
TCME WASHIRIKIANA NA VETA KATIKA KUTOA MAFUNZO YA UCHIMBAJI MADINI KWA WAZAWA
Mgeni Rasmi katika sherehe za mwaka za Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (Tanzania Chamber of Minerals and Energy) Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akizugumza kwa niaba ya Waziri kwa wageni waalikwa na mabalozi.(Picha na Zainul Mzige)
↧
BONDIA FRANSIC MIYEYUSHO KUPAMBANA NA DAVID CHALANGA WA KENYA
BONDIA Fransic Miyeyusho wa Tanzania amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika mchezo wake dhidi ya David Chalanga kutoka Kenya utakaofanyika Desemba 31 katika kwenye ukumbi wa Msasani Klabu,mchezo huo wa kufunga mwaka na kufungua mwaka utakuwa wa raundi nane.
Itakuwa chachu kwa mabondia hao wanaotamba Afrika Mashariki kugombea mikanda mikubwa ya ubingwa na kujiongezea rekodi ya ushindi wa mpambano huo unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki wa mchezo wa masumbwi kila kona ya tanzania.
akizungumzia mpambano huo miyeyusho amesema yeye yupo fiti wakati wowote ule
kama mpinzani wake yuko tayali yeye yupo kwa ajili ya kupigana katika mpambano huo.
Katika mpambano huo,kutakuwa na Mapambano ya Utangulizi kati ya bondia Iddy Mnyeke atakaeoneshana ubabe na Cosmasi Cheka,Antony Mathias akizipiga na Fadhili Majiha Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akizichapa na Mohamed Kashinde.
↧
LORI LAPOROMOKA NA KUINGIA SHIMONI,WILAYANI RUANGWA
↧
TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO
↧
↧
WATANZANIA JIJINI NEW YORK NA VITONGOJI VYAKE WALIVYOSEREBUKA MIAKA 52 YA UHURU WA TANGANYIKA
Jumuiya ya Watanzania Jijini New York na Vitongoaji vyake jana Jumamosi imesherehekea miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika, katika Hafla iliyojaa nderemo, shamrashamra zikiambatana na muziki, chakula, vinywaji na maonyesho ya nguo zilizokuwa na maudhui ya utamaduni na desturi ya mtanzania. Sherehe hizo zilitanguliwa na mchezo wa mpira wa miguu kati ya Timu ya New York na Timu ya ....... ambako timu ya New York iliibuka kidedea.
Mgeni Rasmi katika sherehe hizo zilifana kianina yake alikuwa ni Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Balozit Tuvako Manongi ambaye alifuatana na Naibu wake Balozi Ramadhan Mwinyi na tukaungwa mkono na Balozi wa Somalia katika Umoja wa Mataifa . Watanzania hawa alisimama kwa sekunde Moja, kumukumbuka na kumwombea Marehemu Rais wa Kwanza wa Afrika ya Kusini Huru, Mzee wetu Nelson Mandera.
katika Salamu zake fupi alizozitoa kwa watanzania hao wa Jiji la New York na Vitongoji vyake, pamoja na kuishukuru Jumuia hiyo ya Watanzania kwa maandalizi mazuri ya sherehe hizo, Balozi Tuvako Manongi amewaasa watanzania hao kuendeleza na kujenga misingi ya utaifa, uzalengo, kupendana na kuheshimiana.
Akasema kila mtanzania anayohaki ya kuwa mfuasi wa chama chochote kile cha siasa, lakini jambo kubwa na la msingi linalowaunganisha watanzania popote pale walipo si itiakadi za vyama bali ni utanzania wao ambao umejengekea katika misingi ya utaifa, uzalendo, kuheshimiana, kupendana , kusaidiana ikiwa ni pamoja na kuitetea nchi yao.
Kwa upande wao, Jumuiya hiyo ya Watanzania katika Salamu zao kwa Serikali kupitia Balozi Manongi, wameomba suala la uraia wa nchi mbili lipewe umuhimu wa pekee katika mwenendo mzima wa mchakato wa Katiba mpya unaoendelea.
Joy na Maurus wakiwaongoza watanzania kuimba wimbo wa Taifa.
Mhe. Balozi Tuvako Manongi akizungumza machache.
↧
Ujumbe wa Wataalam kutoka Jimbo la Nanjing China wakutana na Rais Shein wa Zanzibar
Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Ujumbe wa Wataalam kutoka Idara ya Afya ya Jimbo la Nanjing,nchini China,waliofika Ikulu Mjini Zanzibar,wakiongozwa na Kiongozi wao Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Afya Wang Hua,(wa pili kulia).![A2015]()

Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akiwa katika picha na Ujumbe wa Wataalam kutoka Idara ya Afya ya Jimbo la Nanjing,nchini China,waliofika Ikulu Mjini Zanzibar,leo asubuhi.[Picha na REamadhan Othman Ikulu.]
↧
SIKU YA WANAFAMILIA WA NBC YAFANA JIJINI DAR LEO
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo na familia zao wakati wa sherehe za Siku ya Wanafamilia wa NBC kwenye Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi na wanafamilia wa NBC wakichuana katika mchezo wa soka ili kumpata mshindi katika hafla hiyo leo.
Hapa wakionyesha umahiri wa kucheza mpira wa kikapu katika sherehe hizo jijini humo leo.
Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara wakifurahia kuogelea ndani ya bwawa la kuogelea katika hoteli hjiyo jijini Dar es Salaam leo.
Kulikuwa na aina mbalimbali za vyakula kukidhi haja ya kila mmoja aliyehudhuria sherehe ya Siku ya Wanafamilia wa NBC jijini Dar es Salaam leo.
Manahodha’ wa timu za michezo za benki hiyo wakionyesha umahiri wao kusakata rumba katika hafla iliyowakutanisha wafanyakazi na familia zao jijini Dar es Salaam leo.
↧