Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

mandela kuzikwa kijijini kwake Qunu siku ya Jumapili Desemba 15, 2013

$
0
0
Rais Jacob Zuma ametangaza muda mfupi uliopita kwamba mazishi ya Nelson Mandela yatafanyika siku ya Jumapili, Desemba 15 kijijini kwake Qunu, katika jimbo la Eastern Cape.
Rais Zuma pia ametangaza siku 10 za maombolezo kitaifa na bendera zitapeperushwa nusu mlingoti katika muda wote huo.  Na ameitangaza siku ya Jumapili ya Desemba 8, 2013 kuwa siku maalumu ya kitaifa ya maombolezo na kumkumbuka Madiba nchi nzima.
 Tayari msisimko wa mazishi hayo yanayotarajiwa kuwa ya kihistoria umekamata dunia nzima, ambapo tayari Rais Obama wa Marekani, mstaafu Bill Clinto na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ni baadhi tu ya viongozi ambao wamethibitisha kushiriki. 
 Sala ya mazishi imepangwa kufanyika katika uwanja wa Taifa wa  FNB  Desemba 10, 2013  jijini Johanesburg.
Mwili wake utawekwa jengo la serikali liitwalo Union Buildings kuanzia  Desemba 11 hadi 13,   kwa kupewa heshima za mwisho, kabla ya kupelekwa kijijini Qunu kwa mazishi

 Uwanja wa Taifa wa michezo wa Johannesburg ambako sala rasmi ya Kitaifa ya mazishi itafanyika  siku ya Jumapili ya Desemba 10, 2013
 Jengo la Union Buildinga ambapo mwili wake utawekwa kwa ajili ya kupewa heshima za mwisho kuanzia Desemba 11 hadi 13, 2013
Ulinzi mkali katika nyumba ya familia ya Madiba kijijini kwake Qunu ambako atapumzishwa katika nyumba yake ya milele Desemba 15, 2013.

JUMA NATURE NA 'DOGO'

TUMUENZI NELSON MANDELA KWA VITENDO

$
0
0
Uongozi na wanachama wa asasi ya vijana ya Tanzania Youth Vision Association(TYVA) kwa masikitiko makubwa tunaungana na watu wengine kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya hayati Nelson Mandela, wananchi wa Afrika Kusini, watu wote wa bara la Afrika na dunia yote kwa ujumla kwa msiba huu mkubwa.

Ni wazi dunia nzima ipo kwenye majonzi makubwa kwa kuondokewa na kiongozi shupavu, Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini(1994-1999), mtu jasiri asiyeogopa kufa akisimamia ndoto yake ya kupigania uhuru, asiye na uchu wa madaraka, mtu makini, mwerevu, mwenye wingi wa hekima, mtu aliyejali wengine kuliko kujijali mwenyewe, mwenye kuamini katika umoja, mwenye roho ya kusamehe waliomuonea na kumfunga jela kwa miaka ishirini na saba(27), mtetezi wa wanyonge kwa vitendo na sio tu kwa maneno, hayati Nelson Mandela.

Bila shaka alikuwa ni nguzo imara iliyobakia katika kizazi cha viongozi waliopigania uhuru sio tu wa nchi moja moja bali Afrika nzima na dunia yote, akishirikiana na wengineo walioamini kuwa "kiongozi bora ni yule anayetetea maslahi ya wananchi anaowaongoza bila ubaguzi wa aina yoyote, iwe wa rangi, jinsia, ama udini".

Mwisho kabisa, tunatoa wito kwa vijana wenzetu na jamii nzima, tuwe wazalendo na kujiuliza "tutakumbukwa kwa lipi jema?" na watu wa nchi yetu ya Tanzania, Afrika na dunia kwa ujumla kwani alisema hayati Mandela; "sisi pekee tunaweza kuifanya dunia mahali bora pa kuishi".

MUNGU AILAZE ROHO YA HAYATI NELSON MANDELA MAHALI PEMA PEPONI, AMEN!
Wenu katika kujenga taifa,

Naamala Samson,
Makamu Mwenyekiti,
Tanzania Youth Vision Association(TYVA).

MAKAMU WA RAIS DKT. BILALA, MGENI RASMI KWENYE MAHAFALI YA KWANZA CHUO KIKUU BAGAMOYO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye mahafali ya kwanza ya chuo kikuu cha Bagamoyo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo Retired Bishop Elinasa Sendoro wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo hicho yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.
Sehemu ya wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo Retired Bishop Elinasa Sendoro kulia na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Costa Ricky Mahalu katikati, wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo hicho yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata keki ya mahafali ya kwanza ya chuo kikuu cha Bagamoyo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013, kulia Mkuu wa Chuo hicho Retired Bishop Elinasa Sendoro, kushoto Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Costa Ricky Mahalu.Picha na OMR

WATANZANIA WAASWA KUHESHIMU HAKI ZA MTOTO

$
0
0
DSC_0960
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania (THBUB), Jaji Mstaafu Amir Manento akizungumza na waandishi wa habari wakati mdahalo wa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu kuelekea maadhimisho ya siku hiyo ambayo hufanyika tarehe 10 mwezi Disemba kila mwaka.
DSC_0885
Meza Kuu kati kati ni msimamizi (moderator) Dkt Khoti Kamanga toka UDSM, kushoto kwake ni Bw, Godfrey Mulisa toka UN, kushoto mwisho ni Mwakilishi Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Bw, Harold Sungusia na kulia kwa msimamizi ni Francis Nzuki kutoka Tume ya Sheria na Haki za Binadamu na Utawala Bora na mwisho kulia ni Bi, Felistas Mushi toka Wizara ya Sheria na Katiba.

IN LOVING MEMORIAL OF MAMA ROSE SHOMARI

$
0
0
It is Dec 7, 2013 and 8 years since you departed Mama its hard to believe ,because we loved you more than anything in our lives, but the lord loved you more.
As it dawns another year, the lonely hours of thinking thoughts of you are ever near. 
You will always be remembered by your sons Mbwana, Franco, Terry, Sunday and your beloved daughter Mwanahija and Lulu also your grand kids Hamisi, Kisaka, Siwa, Rose, Talia, Terry Shomari Jr, Melvin and Rose. 
The Girl guide Association and the entire Upanga community.  We thank God for your wonderful care, parenthood, your advice, your great smile and the wonderful years we spent with you. We miss you dearly. May the Lord rest your soul in eternal bliss. Amen.

STARS YATINGA NUSU FAINALI CECAFA 2013

$
0
0

Inline image 1


TIMU ya Kilimanjaro Stars imefanikiwa kusonga mbele hatua ya Nusu Fainali baada ya kuwatoa Mabingwa watetezi wa Kombe hilo Uganda kwa ushindi wa changamoto ya penalti 3-2 katika michuano ya kombe la Chalenji inayoendelea jijini Nairobi, shujaa akiwa kipa Ivo Mapunda .
Katika mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Manispaa ya mji wa Mombasa,  Uganda ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza likifungwa na Daniel Sserunkuma katika dakika ya 16 akimalizia krosi ya Khamis Kiiza, bao ambalo halikudumu sana kabla ya Mrisho Ngassa kuisawazishia Stars kwa shuti kali  nje ya 18.
Baada ya bao hilo Stars walikuja juu na kufanikiwa kupata bao la pili likifungwa na Ngassa tena kwa mpira wa adhabu uliojaa wavuni katika dakika ya 39, matokeo ambayo yalidumu mpaka mwisho wa kipindi hicho cha kwanza.

Kipindi cha pili Stars inayofundishwa na kocha Kim Poulsen, raia wa Denmark, ilipata pigo katikati ya kipindi hicho baada ya kiungo wake Salum Abubakar 'Sure Boy' kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kucheza rafu, ambapo nafasi hiyo iliwapa nguvu Uganda kupata bao la kusawazisha kupitia Martin Mpuga matokeo ambayo yalibaki hivyo mpaka mwisho wa mchezo na kuzipeleka mpaka kwenye matuta.

Katika mikwaju ya penalti Ivo alikuwa shujaa baada ya kucheza penalti mbili za Waganda ya beki  Khalis Alucho na  ile ya mwisho iliyopigwa na Sserunkuma ambayo ndiyo iliyoivusha stars.
Ifuatayo ni orodha ya waliopiga penalti katika mchezo huo.

Kilimanjaro Stars                                              Uganda
Erasto Nyoni (kakosa)                     Godfrey Walusimbi (kakosa)
Mbwana Samatta (kakosa)                Emanuel Okwi (kapata)
 Amri Kiemba (kapata)                      Khalis Alucho (kakosa)
Athuman Idd (kapata)                        Hamis Kiiza (kapata)
Kelvin Yondani (kapata)                    Sserunkuma (kakosa)

Ziara ya nyota wa filamu Hemedi na wanasoka toka mbeya nchini Zambia

$
0
0
 Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Grace MUJUMA na afisa wake bi Justa Nyange (kusho) walipokutana na waigizaji wa filamu Hemed kutoka Tanzania (kulia) na Bi. Cassie Kabwita wa Zambia. Waigizaji hao wanategemea kutengeneza filamu mpya pamoja nchini Zambia
 Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Grace MUJUMA akiwa na afisa wa Ubalozi Bw. Jeswald Majuva (kulia) wakati walipokutana na waigiza sinema Hemed kutoka Tanzania na Cassie Kabwita wa ZAMBIA
 Muigiza sinema wa Tanzania Hemed akiwa na muigizaji sinema wa Zambia Cassie Kabwita wakati walipotembelea Ofisi Za Ubalozi w Tanzania Lusaka Zambia Jana tarehe 6 desemba 2013. Msanii Huyu wa Tanzania yuko nchini Zambia  akishirikiana na Kabwita katika kutengeneza filamu mpya
Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Grace MUJUMA (katikati) akiwa na maafisa wake Bi. Justa Nyange (wa nne kushoto ju)  na bw Jeswald Majuva mwenye tai kulia  wakiwakaribisha wacheza mpira wa Miguu kutoka Mbalizi, Mbeya, katika ziara Yao ya michezo Kadhaa na wenzao nchini hapa.timu hiyo ya mbalizi imealikwa nchini Zambia  na mtanzania aitwaye Greenwell Mwahalende anayeishi na kufanya Biashara Zake huko.

Makamu wa Rais wa Shirika la Microsoft akutana na Balozi Seif Ali Idd

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikiongoza kikao cha pamoja kati ya Uongozi wa Shirika la Microsoft na Watendaji wa Mawasiliano, Sayansi na Elimu ya Juu wa SMT Na SMZ kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo ndani ya jengo la Bunge Mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Shirika la Microsoft lenye Makao Makuu yake Mjini Seattle Nchini Marekani Bw. David Tennenhouse wa tatu kutoka kulia aliyevaa miwani akielezea mipango itakayofanywa na shirika lake kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania { Costec }.Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

MHE CHIKAWE KATIKA MAHAFALI YA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA

$
0
0
Waziri wa Katiba Mheshimiwa Mathias Chikawe (Mb), jana tarehe 6/12/2013 amewatunuku Stashahada na Astashahada ya  Sheria jumla ya wahitimu 896 wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama, Lushoto katika Mahafali ya 13 ya Chuo hicho. Kati ya Wahitimu hao 267 ni wa Stashahada ya Sheria na wahitimu 629 ni wa Astashahada ya Sheria kwa Kampasi ya Lushoto na Mwanza.

Kabla ya kuwatunuku wahitimu hapo, mheshimiwa Chikawe kwa niaba ya Serikali aliwapongeza wajumbe wa Baraza la Uongozi wa Chuo na Menejimenti ya Chuo kwa kukiendesha Chuo na aliwahakikishia kuwa Serikali inatambua mchango wanaoutoa katika kutoa elimu ya fani ya sheria na kwamba wahitimu wa Chuo wamechangia kwa kiasi kikubwa uboreshwaji wa utoaji wa haki hapa nchini.

Mhe Chikawe alisisitiza kuwa Serikali inaridhishwa na heshima ambayo Chuo imejijengea hapa nchini na kwamba nidhamu inayoonyeshwa na wanachuo kwa miaka yote ni kielelezo tosha cha namna gani wakufunzi na uongozi wa chuo unawajibika ipasavyo kuwaelimisha wanachuo. Na kwamba inaridhiswa na nidhamu ya wahitimu wa Chuo wanaoajiriwa katika sehemu mbalimbali. 

Mhe Chikawe aliwaambia wahitimu kuwa Sekta ya sheria ni sekta muhimu sana kwa maendeleo na mustakabali wa nchi yetu na kwamba Bila utii wa sheria na utawala bora Tanzania haiwezi kuendelea kisiasa,  kiuchumi na kijamii. Sekta hii inahitaji watumishi wenye maadili na kwamba bila kuwa na wanasheria na watumishi wenye maadili ya juu,  sekta hii itakuwa mwanzo wa migogoro badala ya kuwa mtatuzi wa migogoro. 

Mhe Chikawe alitumia fursa hiyo kukemea vitendo vyote vya ukosefu wa maadili wa watumishi katika sekta ya sheria na kuahidi kuwa vitendo hivyo havitavumiliwa kwa kuwa vinawafanya wananchi wakose imani na vyombo vya kutoa haki na waichukie Serikali na hivyo kuongezeka kwa kutotii sheria na kujichukulia sheria mkononi. Alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua zinazostahili ili kuhakikisha sekta hii inabaki na watumishi wenye maadili. 

Mhe Chikawe alikipongeza Chuo kwa kupata Ithibati ya NACTE na aliwahimiza kukamilisha zoezi la uhuishaji wa Mitaala. Aliuhakikishia Uongozi wa Chuo kuwa atashirikiana na Mahakama ya Tanzania katika kutatua changamoto mbalimbali zinazokikabili Chuo.

Pamoja na kutoa Shahada na Astashahada ya Sheria, Chuo cha Uongozi wa Mahakama kwa kupitia kurugenzi yake ya Mafunzo endelevu ya Kimahakama hutoa na kuendesha mafunzo ya muda mfupi watumishi wote wa Mahakama na watumishi wa Sekta ya sheria kwa ujumla.
Mhe Mathias Chikawe, Waziri wa Katiba na Sheria akitoa hotuba yake wakati wa Mahafali ya 13 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama kabla ya kuwatunuku wahitimu 896 wa Chuo wa Stashahada na Astashahada ya Sheria.
Jaji Mstaafu John Mroso, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama akitoa maelezo ya maendeleo ya Chuo hicho kwa Mhe. Chikawe.
Jaji Ferdinand Wambali, Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama akitoa maelezo kuhusu chuo na wahitimu ambao wametunukiwa Stashahada na Astashahada ya Sheria na Waziri wa Katiba na Sheria.
Baadhi ya wahitimu wa Stashahada ya Sheria wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto wakifuatilia mahafali ya 13 ya Chuo hicho jana tarehe 6/12/2013.

MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU KUFANA, WANANCHI WAOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI

$
0
0
Zikiwa zimebaki siku mbili Tanzania iadhimishe miaka 52 ya Uhuru, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadick ametoa wito kwa watanzania kusherehekea maadhimisho hayo kwa kuenzi , kulinda na kudumisha mafanikio makubwa yaliyopatikana tangu Uhuru.

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam Meck Sadiki amesema kuwa Tanzania katika kipindi cha miaka 52 ya Uhuru imepata mafanikio makubwa ya kiuchumi, ulinzi, usalama pamoja na uhusiano wa kimataifa na kuongeza kuwa mafanikio hayo yanatokana na umoja na mshikamano ulioonyesha tangu kuasisiwa kwa taifa la Tanzania.

“Kipindi chote cha miaka 52 ya Uhuru tumepata mafanikio makubwa sana na ya kujivunia kiuchumi, ulinzi na usalama pamoja na uhusiano wa kimataifa, tuna kila sababu ya kuendeleza mafanikio haya”.

Amesema maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru kwa mwaka 2013 kitaifa yatafanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete chini ya kauli mbiu isemayo “Vijana ni Nguzo ya Rasilimali Watu, Tuwaamini, Tuwawezeshe na Tuwatumie kwa Manufaa ya Taifa Letu”.

Ameongeza kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi na kupambwa na burudani za vikundi vya ngoma za asili kutoka bara na visiwani,Gwaride maalum la vikosi vya ulinzi na Usalama, kwaya mbalimbali, bendi za muziki, maonyesho ya ndege za kijeshi na halaiki maalum.

Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi na kuwahi mapema wakati wa maadhimisho hayo na kubainisha kuwa kutokana na maadalizi mazuri yaliyofanyika milango ya uwanja wa Uhuru itakuwa wazi kuanzia saa 12:30 Asubuhi.
Vikosi vya majeshi ya Ulinzi na Usalama vya Tanzania vikiendelea na maadalizi ya maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru na gwaride maalum leo jijini Dar es salaam.

TANZANITE YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA AFRIKA KUSINI YALALA BAO 4-1

$
0
0
 Nahodha wa timu ya taifa ya Wanawake ya Tanzania 'Tanzanite' Fatma Issa akisalimiana na nahodha wa Basetsana, Kaylin Swart kabla ya mchezo wa kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake wenye umri chini ya miaka 20 uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Afrika Kusini ilishinda 4-1.
 Vumilia Seleiman akimtoka mchezaji wa Afrika Kusini, Nomonde Nomtsheke.
 Mshambuliaji wa timu ya taifa ya wanawake wenye umri chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’, Shelda Boniface akimtoka beki wa timu ya Afrika Kusini ‘Besetsana’, Tiisetso Makhubela  katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia la wanawake wa umri huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Afrika Kusini ilishinda 4-1.

 Kumiliki mpira.
 Shelda Boniface akimiliki mpira mbele ya beki wa Afrika Kusini, Meagan Newman.
 Kikosi cha timu ya Afrika Kusini kiimba wimbo wa taifa.
 Kikosi cha Tanzanite kikiimba wimbo wa taifa.
 Wachezaji wa timu ya Afrika Kusini walioanza katika kipindi cha kwanza.
 Wachezaji wa timu ya Tanzanite walioanza katika kipindi cha kwanza.

MAMA SALMA KIKWETE AKIFUNGA RASMI MKUTANO WA MAWAZIRI WA NCHI ZA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA KUHUSU ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA VIJANA

$
0
0
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Botswana na Mjumbe wa High Level Group Dr. Festus Mogae wakati wa kikao cha Mawaziri wa Elimu na Afya kutoka nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika unaofanyika Cape Town nchini Afrika Kusini tarehe 7.12.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na viongozi waandamizi waliohudhuria mkutano wa High Level Group hukom Cape Town wakisimama kwa dakika moja kwa ajili ya kumkumbuka hayati Rais Nelson Mandela. Kutoka kushoto ni Bwana Enver Surty, Waziri wa Elimu ya Msingi wa Afrika Kusini, Dr. Festus Mogae, Rais Mstaafu wa Botswana, Mama Salma, Bwana Luiz Loures, Naibu Mkurugenzi Mtendaji, UNAIDS, Dr. Julitha Onabanjo, Naibu Mkurugenzi Mkuu, UNFPA, Bwana Qian Tang, Naibu Mkurugenzi Mkuu-Elimu- UNESCO, Bwana Geeta Rao Gupta, Naibu Mkurugenzi Mtendaji, UNICEF.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dr. Hussein Mwinyi akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa High Level Group unaofanyika huko Cape Town kuzungumzia elimu ya afya ya uzazi na ukimwi kwa vijana katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha na Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Bwana Michel Sidibe wakionyesha umuhimu wa dhana nzima ya mkutano wa High Level Group ( YOUNG PEOPLE TODAY, TIME TO ACT NOW) kuhusiana na masuala ya elimu ya afya ya uzazi kwa vjijana katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WAZIRI MKUU AZIPA NOTISI NEMC, MANISPAA MOROGORO

$
0
0
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ametoa mwezi mmoja kwa Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) iwe imetoa mapendekezo kwa Serikali kuhusu matumizi ya maji machafu yanayotokea kwenye viwanda vinne vya ngozi, magunia, nguo na maturubali (canvas).

Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumamosi, Desemba 7, 2013) mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kwenye kiwanda cha nguo cha 21st Century kilichopo eneo la Kihonda Viwandani nje kidogo ya mji wa Morogoro.

Akizungumza na uongozi wa mkoa, wilaya, kiwanda hicho pamoja na NEMC  ya mara baada ya kutembelea eneo ambalo limeathirika na maji yanayotiririka kutoka kwenye viwanda hivyo, Waziri Mkuu alisema tatizo lililopo linachangiwa na kutokuwepo kwa mtu au taasisi maalum ya kusimamia mabwawa ya mfumo wa majitaka (waste management ponds).

“Viwanda hivi vilibinafsishwa lakini mfumo wa usafishaji majitaka haukubinafsishwa... NEMC iishauri Serikali nini kinapaswa kifanyike. Ifanye utafiti kuhusu matumizi ya majitaka yanayotoka kwenye viwanda hivi na ilete uchambuzi huo Serikalini,” alisema.

Tatizo la Watoto wenye ugonjwa wa vichwa vikubwa na mgongo wazi laongezeka

$
0
0
Afisa Muuguzi msaidizi wa taasisi ya tiba ya mifupa,mishipa ya fahamu na upasuaji wa Ubongo(MOI)katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,akitoa ushauri kwa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kitengo cha huduma kwa wateja kuhusina na kula vyakula vyenye fuliki acid ya kutosha kama vile mboga za majani,Matunda,Maharage na Viazi,wakati wafanyakazi hao walipofika kutoa msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Tsh Milioni nane(8,000,000)kwa ajili ya watoto wenye ugonjwa wa kichwa vikubwa na mgongo wazi.
Katibu wa chama cha wazazi wa watoto wenye matatizo ya mgongo wazi na kichwa kikubwa (ASBAHT)Bi.Hidaya Juma (kulia)akielezea jinsi mirija inavyoingizwa kichwani wakati wa matibabu ya watoto wenye matatizo hayo kwa baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kitengo cha huduma kwa wateja wakati wafanyakazi hao walipofika kutoa msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Tsh Milioni nane(8,000,000)kwa ajili ya watoto wenye matatizo ya kichwa vikubwa na mgongo wazi.


President Kikwete Speaks at the End of the Elysee Summit in Paris, france

$
0
0
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete speaks during a joint press conference at the end of the Elysee Summit for Peace and Security held in Paris and ended this afternoon. The Summit discussed among other things, Peace and Security in Africa, The Economic partnership and Development and Climate Change. Others in the pictures from left The UN Secretary General Ban Ki Moon, The host French President Francois Hollande and right is Senegal’s President Macky Sall(photos by Freddy Maro).

KINANA AKUTANA NA WASOMI CCM VYUO VYA ELIMU YA JUU, NJOMBE LEO.

$
0
0
Pichani kati ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akifafanua jambo mbele ya wananfunzi hao (hawapo pichani) baada ya kueleza kero zao. wengine kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa NJombe na Mbunge wa Njombe Kaskazini,Mh.Deo Sanga kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mbunge Mteule, Dk. Asha-Rose Migiro.

Ndugu Kinana na Ujumbe wake leo amekutana na Wanafunzi mbalimbali wa vyuo vya elimu ya juu mkoani humo na kusikiliza changamoto na kero zao mbalimbali na namna ya kuzifanyia kazi ikiwemo na kuzitatua.Kinana amefanya ziara maalum ya kikazi katika mkoa huo wa Njombe,baada ya kumaliza ziara yake ndefu ya mkoa wa Ruvuma na Mbeya,akiwa ameambatana na Wajumbe wa kamati kuu ya CCM,Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asha-Rose Migiro pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

Kama vile haitoshi leo jioni kabla ya kurejea jijini Dar kwa njia ya Treni ya TAZAR kutokea Makambako, Ndugu Kinana alishiriki uzinduzi wa albamu ya kikundi cha Sanaa za Vichekesho cha mjini Njombe.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wanafunzi hao jioni ya leo katika chuo cha Maendeleo ya Jamii,kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakumba,mkoani Njombe.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe,Mh,Sarah Dumba akitoa sehemu ya ufafanuzi kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazokwamisha maendeleo katika chuo cha Uuguzi Kibena,Mkoani Njombe wakati wa kujibu maswali ya wanafunzi wa chuo hicho kama waonekanavyo pichani.
Mmoja wa Wanafunzi wa Chuo cha Iringa akielezea changamoto mbalimbali zinazowakabiri mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake aliokuwa ameambatana nao.PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

ZIFF 2014 DEADLINE LOOMING, CHRISTMAS AND NEW YEAR WISHES

$
0
0

    A reminder to all filmmakers and film enthusiasts. The deadline for the ZIFF festival competition is 31st January 2014. The festival is proudly supported by ZUKU with a 10-year grant as Event sponsor. Please see more by clicking below...

    http://www.ziff.or.tz/2013/09/04/ziff2014-film-entry-now-open/ 

    BEST WISHES from ZIFF

    On Behalf of the Management and Board of Directors of ZIFF the Chairman Mahmoud  Thabit Kombo sends his good wishes for the Festive Season to all ZIFF visitors and stalwarts.

    “While this is a busy time for everybody please do not forget to send in your films and start planning your visit to ZIFF 2014.
    The 17th edition of ZIFF will be bigger, with more training workshops, more awards and new programs. Watch this space!”

    taswira za siku ya amani mkoani arusha

    $
    0
    0
      Wadau wa amani wakiwa jukwaa kuu wakiwa wanafuatilia matukio mbali mbali ya maadhimisho ya kuutakia amani mkoa wa Arusha baada ya kukumbwa na matukio mbali mbali yaliotokea baada ya uchaguzi mkuu na mabomu kwenye kanisa la Joseph mfanyakazi olasit na Soweto mkutano ulioandaliwa na msajili wa vyama vya siasa na vyama vya siasa mkoani hapa na kufanyika  kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini hapa.
     Mmoja wa washiriki akiwaonyesha viongozi na wananchi wa jiji la Arusha hawapo pichani waliohudhuria hafla hiyo bango lisemalo amani kwanza vyama baadae ujumbe ulioendana na siku hiyo mbele ya msajili wa vyama vya siasa jaji Francis Mutungi na mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo na viongozi wa vyama vya siasa na dini mkoani hapa.
     Sehemu ya umati mkubwa wa wananchi na wakazi wa mkoa wa Arusha walioshiriki kuiombea amani mkoa wa Arusha wakifuatilia matukio mbali mbali yaliokuwa yakiendelea uwanjani
     Mchungaji Christopher Mwakasege akiombea amani ya mkoa wa Arusha kwenye siku hiyo ya kusahau tofauti na matukio yaliotokea kwenye mkoa huu wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwenye uwanja wa sheikh Amri Kaluta Abeid
     Juu na chini wanaonekana viongozi mbali mbali wa serikali, vyama vya siasa na dini mkoani Arusha Pamoja na mgeni Rasmi Jaji Francis Mutungi Msajili wa Vyama vya siasa wakiwa kwenye maombi yaliokuwa yakiombwa na mwalimu na mchungaji Christopher Mwakasege kwenye uwanja wa sheikh Amri Kaluta Abeid.
    Picha zote na Mahmoud Ahmad wa Globu ya Jamii, Arusha)

    Sugar rays yaifunga MWanza city Veterans 3-2 uwanja wa Kirumba

    $
    0
    0
    Na Ripota wetu Kanda ya Ziwa
    Kikosi kabambe cha Sugar Ray cha Mikocheni, Dar es salaam, kikiwa tayari kupambana na Mwanza ity CVeterans katika uwanja wa CCM Kirumba Jumamosi ambapo Sugar Ray waliibuka washindi kwa bao 3-2. 
     Mabao ya washindi yalifungwa na Abbas Haki "Fumo" dakika ya 10 baada ya kupokea pande safi toka kwa kiungo mchezeshaji anayewaniwa na TP Mazembe, Issa Batenda. 
    Mshambuliaji mkongwe Saidi Tully (yuko katika form kama Suarez) aliye-podoksi kea free kick nje ya box baada ya Abbasi kufanyiwa madhambi dakika ya 40. 
     Bao la tatu kafunga Clement Sanga baada ya kupokea pasi murua toka kwa yule yule mgawaji Issa Batenga. Baada ya hapo Mwanza City Veterans wakaja juu, na kufanya mabadiliko ya subs 9, na kufanikiwa kupata magoli mawili, moja likiwa la off side kabisa.
    Sugar Rays wakijiandaa na mtanage uwanja wa CCM Kirumba dhidi ya Mwanza City Veterans
     Sugar Rays na Mwanza City Veterans wakisalimiana kabla ya mchezo huo.
     Ni wakati wa mapumziko na wachezaji wa Sugar Rays wakipoza rejeta zao
     Nyota wa Sugar rays Clement Sanga na Saidi Tully wakila pozi huku jamaa akidandia kwa nyuma
     Kiungo mchezeshaji Issa Batenda anayesakwa na TP Mazembe na mwenzie Matare wakitoka uwanjani baada ya gemu. Maajaneti wa timu hiyo ya Congo DRC inasemekana wako Mwanza kujaribu kumchukua Issa, lakini yeye anasita kwa sababu Yanga, Simba na Azam zinamtaka pia.
    Hapa wakiwa kambini hoteli ya Isamilo walikofikia kabla ya mchezo. Baadaye meneja wao (huyo dada ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja) akawahamishia hoteli ya Gold Crest kama zawadi ya ushindi.
    Sugar Rays wakisherehekea ushindi usiku huu hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza. Safari yao hii imedhaminiwa na Michuzi Blog....
    Viewing all 109996 articles
    Browse latest View live


    Latest Images