Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWASILI NCHINI AFRIKA KUSINI KWAAJILI YA SHEREHE YA UAPISHO WA RAIS MTEULE WA NCHI HIYO MHE.CYRIL RAMAPHOSA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa OR Tambo Nchini Afrika Kusini kwaajili ya kuhudhuria Sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa nchi hiyo Mhe.Cyril Ramaphosa ambaye anatarajiwa kuapishwa Mei 25,2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa kwenye ndege ya Shirika la ndege la Tanzania (Air Tanzania) wakielekea Nchini Afrika Kusini kwaajili ya Sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa nchi hiyo Mhe.Cyril Ramaphosa ambaye anatarajiwa kuapishwa Mei 25,2019. PICHA NA IKULU.

WAZIRI HASUNGA AWATAKA WATUMISHI KUPAMBANA NA RUSHWA MAHALA PA KAZI

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) sambamba na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe wakiimba wimbo wa mshikamano wakati akifungua  mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo tarehe 24 Mei 2019, wengine pichani ni viongozi wa TUGHE na RAAWU. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akitoa maelezo ya awali wakati akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo tarehe 24 Mei 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua  mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo tarehe 24 Mei 2019, wengine pichani ni viongozi wa TUGHE na RAAWU.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe wakiwa katika picha ya pamoja na  wafanyakazi wa wizara ya Kilimo ambao ni wajumbe wa Baraza la wafanyakazi lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo tarehe 24 Mei 2019, wengine pichani ni viongozi wa TUGHE na RAAWU.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma


Awamu ya Tatu ya Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa (2017-2022 ina mtizamo mpya unaolenga kuhakikisha kuwa rushwa inaondolewa nchini kwa kutumia mbinu mpya na zinazotekelezeka kwa kuweka mkazo katika sekta zenye mazingira shawishi ya rushwa.


Utekelezaji wa Mkakati huo unalenga kupunguza na kudhibiti rushwa katika sekta/ maeneo muhimu ya kimkakati ambayo ni pamoja na manunuzi ya umma, ukusanyaji wa mapato, utoaji wa haki, maliasili na utalii, madini, nishati, mafuta na gesi, afya, elimu na ardhi.


Rushwa ni adui wa haki, Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akifungua  mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo tarehe 24 Mei 2019 amekemea na kuwataka watumishi kupambana na rushwa katika sehemu za kazi.


Amewataka watumishi kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma kwa kutoshiriki katika kutoa au kupokea rushwa. “Napenda kusisitiza kuwa yeyote atakayejihusisha na kubainika kupokea au kutoa rushwa hatua stahiki na kali zitachukuliwa dhidi yake” Alikaririwa Mhe Hasunga


Waziri Hasunga amesema kuwa bado wizara inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yake kutoa huduma kwa umma ikiwemo ukosefu wa rasilimali fedha na rasilimali watu wa kutosha, hali inayosababisha kutofikiwa kwa malengo. “Niwahakikishie kuwa, Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kutatua changamoto hizo. Ni matumaini yangu kuwa, mkiwa kama Wataalamu mtatumia uwezo wenu katika kuibua mikakati itayosaidia kuwezesha Kilimo kuwa chenye tija na cha kibiashara” Alisisitiza


Kadhalika, amewataka watumishi wote kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Maadili katika Utumishi wa Umma.


Mhe Hasunga amesema kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kwa Mtumishi yoyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na vitendo vinavyokiuka maadili ya Utumishi wa Umma.


Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli inayo dhamira ya dhati ya kuondoa uzembe na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma na hivyo mtumishi anaruhusiwa kudai haki zile za msingi kwa kuzingatia Kanuni, Sheria  na Taratibu za Utumishi wa umma wakati wa kutekeleza wajibu wake wa msingi kwa Mwajiri na kwa kutumia lugha ya staha.


Vilevile serikali inatambua umuhimu wa kuwepo kwa ushirikiano kati ya Mwajiri na watumishi kwani pasipokuwa na ushirikiano wa pande hizo mbili, ni vigumu Taasisi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Umuhimu huu wa mashirikiano, umetiliwa mkazo kupitia Sera, Sheria na Kanuni zinazosimamia uendeshaji Taasisi za Umma.


Amesema kuwa ili kuweza kutafsiri dhana hiyo, ni muhimu pia kwa pande zote mbili kutambua haki na wajibu katika utekelezaji wa majukumu ya kazi, kwani umekuwepo utamaduni wa baadhi ya watumishi kudai haki bila kutimiza wajibu wao kwa Mwajiri.


MWISHO

KILUWA GROUP LTD WASAINI MKATABA NA KAMPUNI YA KUTOKA CHINA INAYOTAKA KUJENGA KIWANDA CHA SUKARI ,KILIMO

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimewakaribisha Watanzania wazalendo kutembelea katika ofisi za kituo hicho kwa lengo la kujua taarifa mbalimbali na fursa za uwekezaji zilizopo kwenye maeneo tofauti. 

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Idara ya Uhamasishaji TIC John Mathew kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe katika hafla ya kutia saini mikataba ya makubaliano ya uwekezaji kati ya kampuni za Tanzania na China ambapo amesema huu ndio wakati wa vijana kuwa karibu na kituo hicho ili kupata taarifa za kila siku juu ya uwezekaji. 

Amefafanua kuwa Kampuni ya Kiluwa Group inafanya kazi kubwa ya kuzungumza na wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali hasa China ambapo leo wanashuhudia utiwaji saini mkataba wa mwakubaliano ili kuanzisha kiwanda cha sukari nchini. 

"Wachina hawa baada ya kuvutiwa na mikataba hii watavutia wawekezaji wengine ndani na nje ya nchi, Kampuni ya Kiisu Minyuan International Trading Ltd inataka kuwekeza katika kiwanda cha kutengeneza sukari, hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza idadi ya uzalishaji wa bidhaa hii muhimu kwa maendeleo ya nchi,,"amesema Mathew. 

Ameongeza wadau wengine wajitokeze ili wasaidiwe namna bora ya kuunganisha kampuni kutoka nje na kampuni za ndani ili kuhakikisha kunapatikana urahisi katika baadhi ya masuala. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiluwa Group, Mohammed Kiluwa amesema mara nyingi anapokuwa katika mikutano ya kimataifa inayohusu uwekezaji amekuwa akijitahidi kuhakikisha anavuta wawekezaji wakubwa kuja kuwekeza nyumbani Tanzania. 

"Hivi karibuni nilikuwa katika mkutano wa One Belt One Road, nikauza fursa za uwekezaji, wengi walipenda na baadhi yao ni hawa tuliotiliana nao saini. Sisi ndio wajenga nchi na hasa katika kipindi hiki ambapo Rais Dk. John Magufuli ameamua kwa dhati kuifanya nchi kuwa na uchumi wa kati kwa kutegemea viwanda. 

"Hivyo, viwanda vingi iwezekanavyo vinahitajika. Kwa mfano kwa uwekezaji huu sisi tutahitaji eneo lenye ukubwa wa hekta 30,000 na hili si eneo moja bali tutaweza kuwa na uwekezaji katika mikoa mbalimbali. 

"Kama mnavyofahamu kiwanda cha sukari uzalishaji wake una mambo mengi, muwa unapoingizwa kiwandani unakuwa na vitu vingi hivyo tutakuwa na Industrial Park za kutosha,"amesema Kiluwa. 

Pia amewataka Watanzania kushirikiana katika kutangaza fursa zilizokuwepo nchini kwenye uwekezaji, anadai anajiona yuko peke yake wengi hawachangamkia nafasi za kutangaza maeneo ya nchi kwenye uanzishwaji viwanda kwa faida ya taifa. 

Wakati huo huo Rais wa kampuni ya Kiisu Minyuan International Trading Ltd, Yu Liang amesema amevutiwa na namna Tanzania inavyothamini wageni hasa wawekezaji. Anaamini watakuwa na muda mzuri wakiwa nchini kwenye shughuli za kukuza uchumi wa Afrika na China. 

"Udugu kati ya China na Tanzania ni wa kupigiwa mfano, tumezunguka maeneo mengi ambayo bwana Kiluwa alitueleza tukiwa China na sasa tumeamini hakika Tanzania inayo nafasi kubwa ya kukua katika sekta ya viwanda,,"amesema Liang.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Group, Mohammed Kiluwa akitiliana saini na Rais wa kampuni ya Kiisu Minyuan International Trading Ltd, Yu Liang kuhusu mkataba wa makubaliano ya uwekezaji wa kujenga kiwanda cha sukari na kilimo. Makubaliano hayo yamefanyika leo katika ofisi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Group, Mohammed Kiluwa akipeana mkono mara baada ya kutiliana saini na Rais wa kampuni ya Kiisu Minyuan International Trading Ltd, Yu Liang kuhusu mkataba wa makubaliano ya uwekezaji wa kujenga kiwanda cha sukari na kilimo. Makubaliano hayo yaliyoshuhudiwa na Mkurugenzi Idara ya Uhamasishaji TIC John Mathew kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe, yamefanyika leo katika ofisi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya mashahidi Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Group Naima Kiluwa na Mwakilishi wa kampuni ya Kiisu Minyuan International Trading Ltd, wakitia saini makubaliano kama sehemu ya Mashahidi wa tukio hilo 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Group, Mohammed Kiluwa akizungumza jambo mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wawekezaji kutoka nchini China,mara baada ya kutiliana saini kuhusu mkataba wa makubaliano ya uwekezaji wa kujenga kiwanda cha sukari na kilimo.
Mkurugenzi Idara ya Uhamasishaji TIC John Mathew kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe, (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wawekezaji wa nchini Tanzania na China mara baada ya kumaliza kusaini makubaliano yao,leo katika ofisi hizo jijini Dar
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Group, Mohammed Kiluwa akipeana mikono na Wabia wake mara baada ya kusaini makubaliano yao leo jijini Dar

WAFANYAKAZI WAWILI WA CAMEL WAFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA UTAKATISHAJI FEDHA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii 

MFANYAKAZI wa Kampuni ya mafuta ya Camel David Leole na mwenzake Khalid Said, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashitaka matatu likiwemo la utakatishaji fedha zaidi ya Sh. milioni 181.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Serikali Groly Mwenda amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Maira Kasonde kuwa kati ya Januari 2016 hadi Machi 2018 katika sehemu tofauti ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, washitakiwa walikula njama ya kutenda kosa la wizi wakiwa watumishi wa kampuni hiyo.

Imedaiwa kuwa siku na mahali hapo, washitakiwa hao waliiba Sh.181,181,350 iliyoingia mikononi mwao kutokana na nafasi zao za kuajiliwa.

Aidha ,washitakiwa hao wanadaiwa kutakatisha kiasi hicho cha fedha kwa kuziingiza katika akaunti ya Leole ya benki ya NMB huku wakijua fedha hizo zimetokana na zao la kosa la wizi.

Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 28 mwaka huu itakapotajwa tena. Washitakiwa wote wamerudishwa rumande kwa kuwa kosa la utakatishaji fedha halina dhamana.


NAIBU SPIKA AFUNGUA MAFUNZO YA WABUNGE WANAWAKE

$
0
0


Naibu Spika wa Bunge, Mhe.Dkt. Tulia Ackson akifungua mafunzo kwa wajumbe wa Chama Cha Wabunge Wanawake (TWPG) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa TWPG, Mhe. Magreth Sitta na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa TWPG, Mhe. Susan Lyimo.


Benki ya CRDB yapata tuzo ya "International transfers 2018"

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) akipokea tuzo ya Benki ya CRDB kuwa benki salama na ya uhakika katika huduma ya kutuma na kupokea miamala ya kimataifa (International transfers) 2018 kutoka kwa Makamu wa Rais wa Citi Bank Afrika Mashariki, Mary Sabwa, aliyemtembelea ofisini kwake, jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts.

SERIKALI KUWAJENGEA UWEZO MAFUNDI SANIFU (MAJENGO) NA MAFUNDI MICHUNDO KUPITIA MIRADI INAYOTEKELEZWA NCHINI.

$
0
0
Na. Paschal Dotto-MAELEZO 

Serikali Kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, imesema kuwa itaendelea kuwajengea uwezo na uzoefu mafundi sanifu na mafundi Michundo, ili waendelee kutekeleza kazi zao kwa ufanisi na kuongeza wataalam katika kada hiyo kwani fani hizo zina watu wachache. 

Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Wasanifu Majengo na mafundi Michundo, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Dkt. Elius Mwakalinga alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imejikita katika kuhakikisha kuwa ujenzi wa miundombinu unafanikiwa kwa kiasi kikubwa. 

“Serikali imedhamiria kujenga miundombinu ili kuwezesha ukuaji wa Sekta ya Viwanda nchini, hivyo Mafundi sanifu wanategemewa sana katika kuwezesha miundombinu hii, ili Tanzania iweze kufikia ndoto ya kuwa kwenye uchumi wa kati kupitia viwanda, na katika kutekeleza hilo mwaka wa Fedha 2019/2020, Wizara ya Ujenzi imejikita katika ajenda tatu ikiwemo kuwajengea uwezo wasanifu na wahandisi wote nchini”, Alisema Dkt. Mwakalinga. 

Dkt. Mwakalinga alisema kuwa Serikali inahakikisha watalaam chini ya Taaluma ya Uhandisi, Usanifu Majengo, Ukadiriaji Majenzi na kada zingine katika sekta ya ujenzi wanaongezeka kiidadi na kujengewa ujuzi mahsusi ili kuwa na uwezo na kumudu mahitaji ya nchi ya wataalam hao. 

Aidha, Dkt. Mwakalinga aliwathibitishia kuwa serikali inaendelea kushirikiana na bodi mbalimbali za taaluma za kihandisi kwa kutoa miradi inayotekelezwa nchini ili kuwawezesha watalaam hao kupata uzoefu na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa na kazi hiyo itaanza rasmi mwaka wa fedha 2019/2020, Julai Mosi. 

“Napenda niwadhihirishie kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya uongozi wa Rais Magufuli, inayo dhamira ya dhati ya kuendeleza fani ya usanifu kwa kutumia miradi yake inayotekelezwa, kama vile ujenzi wa Reli ya kisasa, SGR, Ujenzi wa Interchange Ubungo, Ujenzi wa Bwawa kubwa la kuzalisha umeme mto Rufiji, na ujenzi wa Daraja la Selander, kwa hiyo miradi hii itaweza kutoa uzoefu mkubwa kwa wataalum wetu”, alisema Dkt. Mwakalinga. 

Katika kuongeza uzoefu wa watalaam hao, Dkt Mwakalinga amesema ni lazima kuwepo na maarifa na vitendea kazi ambavyo kwa sasa ni uwepo wa miradi ya kimaendeleo ambayo inatekelezwa na Serikali na sasa mafundi sanifu wanahitajika ili kuiwezesha miradi hii kutekelezwa pasipo gharama kubwa. 

Akaongeza kuwa Serikali inapoendelea na zoezi la kuwapa uwezo watalaam hao inawaomba wawe waadilifu, wenye kujituma na wenye weledi mkubwa maana kazi yao hiyo ni kubwa sana kuliko kazi zingine za kihandisi. 

“ Kama nilivyosema hapo awali tutaendelea kuwajengea uwezo watalaam wetu kwa kutumia miradi tuliyonayo, lakini kujenga uwezo kuna uhusiano mkubwa na masuala ya kujituma, kuijitoa kwa moyo kwa taifa, kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa, hii ndiyo itakuwa tiketi ya kupata kazi na tutachagua watalaam kulingana na vigezo hivyo,”Alisisitiza Mwakalinga. 

Akizungumzia kuhusu changamoto za uhaba wa wataalam hao, Dkt. Mwaklinga aliainisha kuwa, kwa takwimu za Shirika la kazi duniani, ILO, zinabaini kuwa Mhandisi mmoja anapaswa kufanya kazi na Mafundi Sanifu watano, na Mafundi Stadi 25, na kuongeza kuwa hiyo inaonyesha umuhimu wa wasanifu na mafundi stadi katika sekta ya ujenzi. 

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB), Prof. Ninatubu Lema, alisema kuwa Wasanafi wanahitajika kijituma ili kuanzisha viwanda vidogovidogo vya kutengeneza vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kuuzwa nchini. 

“Mnatakiwa Mafundi Sanifu kuwa wabunifu katika kujenga na kutengeneza uwezo kwa kufanya wajasiriamali wa kujenga viwanda vidogovidogo, ili mtu mmoja aajiri watu watano, watu sita au watu 10 na kutengeneza vitu vidogovidogo vya kuuzwa hapa nchini, … tuko tayari kuratibu na kwenda kwenye nchi za wenzetu kama India, China kutazama hivyo viwanda vidogovidogo.”, Alisema, Prof.Lema.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 25,2019


WANAHABARI WAPEWA ELIMU KWA VITENDO ENEO LA MRADI WA UMWAGILIAJIAKWA NJIA YA MATONE

$
0
0
  Pichani ni eneo la mradi wa umwagiliaji kwa njia ya matone katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Naliendele. (PICHA NA FATNA MWINYIMKUU)
 Kaimu mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Naliendele Dk. Fortunatus Kapinga aliyekaa kati kati hivi karibuni akitoa elimu kwa vitendo kwenye eneo la mradi wa umwagiliaji kwa njia ya matone katika Taasisi hiyo kwa waandishi wa habari kutoka Lindi na Mtwara na watafiti walioshiriki mafunzo hivi karibuni ya Sayansi na Teknolojia, kulia kwake ni kaimu mkurugenzi kutoka Tume ya Taifa ya  Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk. Msangi Bakari, mwigine ni mtafiti wa mazao ya mafuta katika Taasisi hiyo Joseph Nzunda (PICHA NA FATNA MWINYIMKUU) 

WAUGUZI WA HOSPITALI ZA JAKAYA KIKWETE NA BENJAMIN MKAPA WAPEWA MAFUNZO NA HOSPITALI YA SUNNING HILL YA AFRIKA KUSINI

$
0
0

Mtaalamu wa chumba cha upasuaji mdogo wa moyo kupitia tundu dogo kwa kutumia mtambo wa Cath Lab kutoka Hospitali ya Sunning Hill iliyopo Johannes Burg nchini Afrika ya Kusini Fill Longano akiwafundisha wauguzi na mafundi sanifu wa moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) pamoja na Hospitali ya Aga khan namna ambavyo wanapaswa kuwahudumia wagonjwa wa moyo wanaopata matibabu ya moyo kwa kutumia mtambo wa Cath Lab leo katika Hoteli ya Protea Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wauguzi na mafundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia mafunzo ya namna ya kumhudumia mgonjwa wa moyo anayepata matibabu kupitia mtambo wa Cath Lab yaliyotolewa na Mtaalamu wa chumba cha upasuaji mdogo wa moyo kupitia tundu dogo kwa kutumia mtambo wa Cath Lab kutoka Hospitali ya Sunning Hill iliyopo Johannes Burg nchini Afrika ya Kusini leo katika Hoteli ya Protea Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wauguzi na mafundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) wakifuatilia mafunzo ya namna ya kumhudumia mgonjwa wa moyo anayepata matibabu kupitia mtambo wa Cath Lab yaliyotolewa na Mtaalamu wa chumba cha upasuaji mdogo wa moyo kupitia tundu dogo kutoka Hospitali ya Sunning Hill iliyopo Johannes Burg nchini Afrika ya Kusini leo katika Hoteli ya Protea Jijini Dar es Salaam
Maafisa Uuguzi na mafundi sanifu wa moyo wanaotoa huduma katika chumba cha upasuaji mdogo wa moyo kupitia tundu dogo kwa kutumia mtambo wa Cath kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) pamoja na Hospitali ya Aga khan katika picha ya pamoja baada ya mafunzo ya siku mbili ya namna ya kumuhudumia mgonjwa wa moyo anayepata matibabu kwa kutumia mtambo wa cath lab.
Picha na: Genofeva Matemu – JKCI

NEMC YAWAONDOA HOFU WADAU WA VIWAMJA VYA NDEGE

$
0
0

Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Manchare Heche akiwaonesha wadau wanaotoa huduma
mbalimbali kwenye Kiwanja cha Ncdege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) moja ya mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku kuendelea kutumika nchini ifikapo Juni Mosi, 2019 katika mkutano uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Watu Mashuhuri (VIP). 
Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Manchare Heche (aliyenyanyua mikono) akisisitiza jambo wakati akiongea na wadau wanaotoa huduma mbalimbali kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), juu ya katazo la mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku kuendelea kutumika nchini ifikapo Juni Mosi mwaka huu. Wapili kulia ni Mkurugezi wa JNIA, Paul Rwegasha na wa kwanza kushoto ni mkuu wa kitengo cha Mazingira cha TAA, Maxmilian Mahangila.
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha (aliyesimama) akielezea mikakati iliyowekwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), ya namna ya kutekeleza agizo la serikali la katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki kwa watumiaji wa viwanja vya ndege nchini. Wapili kushoto ni Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Manchare Heche.



BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), leo limewaondolea hofu wadau wanaoendesha huduma mbalimbali kwenye Viwanja vya ndege, katikamkutano ulioitishwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), uliofanyika kwenye Ukumbi wa Watu Mashuhuri (VIP), kuhususiana na katazo la matumizi yamifuko ya plastiki ambalo litaanza rasmi Juni Mosi, 2019.

Mwanasheria wa NEMC, Manchare Heche amesema kwa upande wa viwanja vya ndege ipo mifuko, ambayo itaendelea kutumika kwa mujibu wa Kanuni namba tisa (9) ya sheria ya kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki ya mwaka 2019, lakini baada ya kutumika inatakiwa ihifadhiwe sehemu maalum na kupekekwa mahali itakapoteketezwa. 

“Kweli katazo linahusu Watanzania wote na wageni na hapa Airport wapo wanaotumia nikiwa na maana ya wafanyakazi na wateja wakiwemo abiria, lakini katika sheria ukiangalia kanuni ya tisa 9 ipo mifuko ya vifungashio ambayo haijazuiwa ni kama ile ya kuhifadhi vyakula, dawa, kilimo na inayohifadhia takataka, mfano korosho au keki wanazopewa abiria kwenye ndege mfuko wake upo katika kipengele cha chakula, hivyo itaendelea kutumika lakini baada ya matumizi tu itahuifadhiwa sehemu iliyoelekezwa tayari kwa kwenda kuteketezwa,” alisisitiza Heche.

Alisema kwa upande wa plastiki zinazofungia mizigo ya abiria wanaosafiri kutoka ndani na nje ya nchi kwa usafiri wa ndege itatakiwa kuondolewa abiria anapofika nchini, na zitakusanywa na kuhifadhiwa maeneo maalum kabla ya kupelekwa eneo lililotengwa kwa ajili ya kuziteketeza.

Hatahivyo, kutokana na matumizi makubwa ya mifuko ya plastiki nchini imesababisha uharibifu mkubwa wa mazingira ikiwemo ya kuziba kwenye mifereji ya maji, kuua wanyama, na kuharibu ardhi, Heche amesema kufuatia katazo hilo serikali imefuta leseni za viwanda vinavyotengeneza mifuko ya plastiki na pia haijawapa tena leseni wale wote leseni zao zilizomaliza muda, ili kuhakikisha sheria na kanuni ya kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki namba 394 ya mwaka 2019.

Heche ametoa angalizo kwa wale wote wanaohusika na ukamataji wa watumiaji wa mifuko hiyo, kutotumia nguvu ili kuepusha mikwaruzano na kutoelewana.
Hatahivyo, amewataka wadau hao kuhakikisha wanadai vitambulisho kwa wale wote watakaofika kwenye maeneo yao ya kazi kudai wanakagua endapo wanaendelea kuuza au kutumia mifuko ya plastiki.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha amesema tayari kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wameshatoa taarifa inayokwenda kwenye vituo vyote vya Kimataifa, ambapo kuna shirika la ndege linaloleta abiria Tanzania, ikitaarifu juu ya katazo la mifuko ya plastiki.

“Hii taarifa inajulikana kitaalam kama ‘timatic pre-information’ ambayo inatumwa kwenye centre zote duniani, ambapo kuna shirika la ndege ambalo linaleta abiria Tanzania itakuwa rahisi wao kupata taarifa ya katazo hilo na kuwafanya wasibebe mifuko hiyo,” amesema Rwegasha.

Pia amewataka wadau wote wanaofanya shughuli mbalimbali kwenye viwanja vya ndege kutoa ushirikiano mkubwa kuwaeleza abiria juu ya katazo hilo, na kuwaelekeza watumie mifuko mbadala, ambayo itakuwa ikipatikana kwenye maduka yaliyopo kwenye majengo ya Kwanza na Pili ya JNIA.

Kwa mujibu wa NEMC imesema watumiaji wa kawaida endapo watakamatwa na mifuko hiyo watatozwa faini ya Tshs. 30,000, kifungo cha siku saba, au vyote kwa pamoja; wakati kwa muuzaji anapigwa faini ya Tshs 100,000 haizidi Tshs 500,000, kifungo cha miezi mitatu; na watengenezaji watapigwa faini ya kuanzia Tshs milioni 20 na haitazidi bilioni moja na kifungo cha miaka miwili.

ICS ,SERIKALI WAANZA KUTENGENEZA MPANGO MKAKATI WA KUTOKOMEZA UKATILI KWA WANAWAKE NA WATOTO SHINYANGA

$
0
0



Shirika la Kimataifa (ICS) linalojishughulisha na masuala ya kuboresha malezi na makuzi bora ya watoto na kuwaimarishia ulinzi na usalama,kuimarisha uchumi wa kaya,masuala ya UKIMWI kwa vijana na afya ya uzazi, kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wa Shinyanga limefadhili kuanza kutengenezwa kwa mpango mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.


Mpango mkakati huo umeanza kutengenezwa leo Mei 24, 2019 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga, kwa kuhusisha maofisa maendeleo, ustawi wa jamii, dawati la jinsia na watoto, wachumi, wanasheria, waratibu wa afya ya uzazi, maofisa elimu, pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali ambapo washiriki hao wanatoka katika halmashauri zote sita za mkoa huo. 

Akizungumza kwenye kikao hicho,Meneja wa Shirika hilo la ICS Tanzania Kudely Sokoine Joram, alisema mwaka jana (2018) walishirikiana na serikali ya mkoa wa Shinyanga kuunda kamati ya mkoa ya ulinzi na usalama kwa watoto na wanawake, ambapo ilipewa mafunzo ya siku tatu na wizara ya afya kwa kushirikiana na ICS juu ya masuala ya MTAKUWWA, kwa ajili ya kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto. 

Amesema baada ya kutolewa mafunzo hayo ndipo ikaazimiwa kutengenezwa mpango mkakati wa mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kushughulikia masuala hayo ya kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto ili kufanikisha mpango wa Serikali (MTAKUWWA) wa kutokomeza ukatili huo kutoka asilimia 37 hadi asilimia 10 ifikapo 2022.

 “Kikao cha leo ni cha kwanza ambacho tunatengeza mpango mkakati wa kutokomeza masuala ya ukatili kwa wanawake na watoto mkoani Shinyanga pamoja na kuunda timu ya wataalamu itakayo kwenda kuanza kazi ya kukamilisha utengenezaji wa mpango mkakati mara moja ili kutokomeza ukatili huo,”amesema Kudely. 

“Mbali na kushirikiana na Serikali ya mkoa wa Shinyanga pia tumehusisha na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo ni SAVE THE CHILDREN, AMREF, JHPIEGO, TVMC, AGAPE, WORDVISSION, NA JSI ,kwa lengo la kuunganisha nguvu ya pamoja kutokomeza masuala ya ukatili kwa wananawake na watoto mkoani hapa,”ameongeza. 

Naye mgeni rasmi kwenye kikao hicho katibu tawala msaidizi utumishi na utawala mkoani Shinyanga Amos Machilika, akimwakilisha katibu tawala wa mkoa huo, alisema mpango huo mkakati utaleta matokeo chanya ya kupungunza ukatili mkoani humo dhidi ya wanawake na watoto likiwamo na suala la mimba na ndoa za utotoni. Aidha amesema mkoa wa Shinyanga bado unaongoza kwa masuala ya ndoa za utotoni kwa asilimia 59,ikifuatiwa Tabora 58, na Dodoma 51, ambapo pia kwa mwaka jana kuanzia Julai hadi Disemba jumla ya matukio 31 ya ndoa za utotoni yaliripotiwa. 

Pia ametaja takwimu za mimba za utotoni mkoani Shinyanga kuwa ni asilimia 34 kwa mujibu wa takwimu za viashiria vya hali ya kiafya nchini (TDHS) ya Mwaka 2016, ikitanguliwa na Katavi 45, Tabora,43, Dodoma 39, na Mara 37, ambapo wastani wa kitaifa ni asilimia 27, huku kwa kipichi cha miaka mitatu jumla ya wanafunzi 351 walipewa ujauzito na kuacha masomo mkoani humo.

 Nao baadhi ya washiriki wa kikao hicho wakiwasilisha mada akiwamo Afisa Ustawi wa Jamii Kahama Mji Ibrahimu Nuru, amesema ili kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto mkoani humo kuondoa kwanza tatizo la mila na desturi Kandamizi pamoja na kuimarisha uchumi wa kila Kaya. 
Meneja wa Shirika la kimataifa ICS Tanzania Kudely Sokoine Joram, akizungumza kwenye kikao cha mpango mkakati wa kupanga kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto mkoani Shinyanga. Alisisitiza ushirikiano uwepo wa kuunganisha nguvu ya pamoja kati ya mashirika yasiyo ya kiserikali na Serikali ya mkoa wa Shinyanga, kwa ajili ya kupambana kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog Afisa ustawi wa jamii wa halmashauri ya Kahama Mji Ibrahimu Nuru, akiwasilisha mada ya mpango mkakati wa Serikali wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) kwenye kikao hicho, na kubainisha moja ya changamoto ambayo inatakiwa kushughulikiwa ili kufikia malengo yake ni kutokomeza mila na desturi kandamizi pamoja na kuimarisha uchumi wa kaya. Kaimu mkurugenzi wa Shirika la Save The Children Mkoani Shinyanga Alex Enock akichangia mada kwenye kikao hicho cha kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga. Washiriki wakiwa kwenye kikao cha kupanga mpango wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga. Washiriki wakiwa kwenye kikao cha kupanga mpango wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga. Washiriki wakiwa kwenye kikao cha kupanga mpango wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga. Washiriki wakiwa kwenye kikao cha kupanga mpango wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga. Washiriki wakiwa kwenye makundi ya kila halmashauri sita za mkoa wa Shinyanga wakiandaa mpango mkakati wa mkoa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Washiriki wakiwa kwenye makundi ya kila halmashauri sita za mkoa wa Shinyanga wakiandaa mpango mkakati wa mkoa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Washiriki wakiendelea kupanga mapango mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga. Washiriki wakiendelea kupanga mapango mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.

Washiriki wakiwa kwenye makundi ya kila halmashauri sita za mkoa wa Shinyanga wakiandaa mpango mkakati wa mkoa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga. Picha zote na Marco Maduhu-Malunde 1 Blog

SHULE YA VIZIWI BUGURUNI KUSHIRIKI LIGI YA MPIRA WA MIGUU

$
0
0
Yapewa vifaa vya michezo vya zaidi ya shilingi laki tatu

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

SHULE ya msingi ya watu wenye mahitaji maalumu Buguruni viziwi inataraji kushiriki mashindano ya michezo ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu yanayoshirikisha shule za jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa elimu Manispaa ya Ilala Elizabeth Thomas amesema kuwa wamejiandaa kutetea vikombe vyote katika ligi hiyo kwa watu wenye mahitaji maalumu, amesema kuwa wataingia kambini kwa siku 10 ili kupata timu ya Wilaya.

Amesema kuwa changamoto kubwa kwa sasa ni upungufu wa jezi, mipira pamoja na viatu na amewaomba wadau mbalimbali kujitokokeza na kuwasaidia watoto hao.

Kwa upande wake mkuu wa shule ya msingi Buguruni viziwi Mirembe Kurwa ameshukuru kwa msaada huo na kuahidi ushindi kwa Manispaa ya Ilala, na kusema kuwa wataendelea kushiriki michezo kupitia UMITASHUMTA kila mwaka.

Pia amesema kuwa watoto wenye ulemavu ni sawa na watoto wengine hivyo hatuna budi kuwalinda na kutetea haki zao pamoja na kuwafanya wajisikie kama watoto wengine.

Kwa upande wake meneja masoko Said Adinan kutoka X-TIGI mobile amesema kuwa wametoa zawadi chache ili kuweza kuwasaidia na kuwainua vijana hao kimichezo na kuwataka wadau wengine kuwaangalia watoto wenye mahitaji ya aina hiyo.

Adinan amesema kuwa wao kama ofisi wataangalia namna ya kuwasaidia watoto hao kwa kuanza na mshindi atakayeibuka katika mashindano hayo.
Mashindano hayo ya watoto wenye mahitaji maalumu yatashirikisha shule zote zenye mahitaji maalumu.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Buguruni ya viziwi ,Milembe Kulwa akipokea vifaa michezo kutoka kwa  Meneja Masoko wa X-TIGI,Said Adinan vyenye thamani ya zaidi ya laki tatu leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Wanafunzi wa shule ya msingi Viziwi Buguruni wakionesha  Vipaji vyao vya kucheza mpira.
Picha ya pamoja.

Je, ni Barcelona au Valencia bingwa wa Copa del Rey leo?

$
0
0
Kampuni ya Star Media (T) Ltd imetangaza kuonyesha mchezo wa fainali ya Kombe la mfalme wa Uhispania maarufu kama Copa del Rey. Mchezo huo utakaozihusisha timu za Barcelona na Valencia utapigwa Jumamosi hii saa 4:00 Usiku.

Barcelona ambao wamenyakua kombe la La Liga kwa msimu huu bado wana kazi ya kuwaridhisha mashabiki wao ambao bado wana majonzi ya kutolewa kwenye ligi ya mabingwa baada ya kuongoza kwa goli 3 katika mchezo wa kwanza na kuruhusu goli 4 kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Liverpool.

Mbali na morali kuwa chini Barcelona wana orodha ndefu sana ya majeruhi ambao miongoni mwao ni wachezaji wa kikosi cha kwanza, mshambuliaji Luis Suarez, golikipa Ter Stegen (maumivu ya goti), Ousmane Dembele (maumivu ya misuli ya nyuma ya goti ‘hamsring’) na kiungo wa kati Arthur (maumivu ya nyonga).

Hata hivyo Barcelona bado wana kikosi kizuri sana licha ya majeruhi walionao. Nahodha Lionel Messi amekuwa kwenye kiwango bora kabisa msimu huu baadaya kupachika mabao 36 katika ligi na kuisaidia timu yake kushinda taji hilo.
Kwa Valencia hii ni fainali yao ya 16 katika Kombe la Mfalme huku wakiwa wamefanikiwa kulichukua mara 7 na kupoteza fainali 9. Mara ya mwisho Valencia kuwafunga Barcelona katika fainali za Copa delo Rey ilikuwa mwaka 1958 ambapo walishinda 3-0.

Kwa mashabiki wa soka nchini Tanzania mchezo huu utaoneshwa kupitia king’amuzi cha StarTimes katika chaneli ya ST World Football LIVE kuanzia saa 4:00 Usiku siku ya Jumamosi tarehe 25 Mei.
Chaneli ya ST World Football inapatikana katika kifurushi cha SMART kwa watumiaji wa Dish na kifurushi cha UHURU kwa wateja wa Antenna.

NEMC yawaondoa hofu wadau Viwanja vya Ndege

$
0
0
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), leo limewaondolea hofu wadau wanaoendesha huduma mbalimbali kwenye Viwanja vya ndege, katika mkutano ulioitishwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), uliofanyika kwenye Ukumbi wa Watu Mashuhuri (VIP), kuhususiana na katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki ambalo litaanza rasmi Juni Mosi, 2019.

Mwanasheria wa NEMC, Manchare Heche amesema kwa upande wa viwanja vya ndege ipo mifuko, ambayo itaendelea kutumika kwa mujibu wa Kanuni namba tisa (9) ya sheria ya kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki ya mwaka 2019, lakini baada ya kutumika inatakiwa ihifadhiwe sehemu maalum na kupekekwa mahali itakapoteketezwa.

“Kweli katazo linahusu Watanzania wote na wageni na hapa Airport wapo wanaotumia nikiwa na maana ya wafanyakazi na wateja wakiwemo abiria, lakini katika sheria ukiangalia kanuni ya tisa 9 ipo mifuko ya vifungashio ambayo haijazuiwa ni kama ile ya kuhifadhi vyakula, dawa, kilimo na inayohifadhia takataka, mfano korosho au keki wanazopewa abiria kwenye ndege mfuko wake upo katika kipengele cha chakula, hivyo itaendelea kutumika lakini baada ya matumizi tu itahuifadhiwa sehemu iliyoelekezwa tayari kwa kwenda kuteketezwa,” alisisitiza Heche.

Alisema kwa upande wa plastiki zinazofungia mizigo ya abiria wanaosafiri kutoka ndani na nje ya nchi kwa usafiri wa ndege itatakiwa kuondolewa abiria anapofika nchini, na zitakusanywa na kuhifadhiwa maeneo maalum kabla ya kupelekwa eneo lililotengwa kwa ajili ya kuziteketeza.

Hatahivyo, kutokana na matumizi makubwa ya mifuko ya plastiki nchini imesababisha uharibifu mkubwa wa mazingira ikiwemo ya kuziba kwenye mifereji ya maji, kuua wanyama, na kuharibu ardhi, Heche amesema kufuatia katazo hilo serikali imefuta leseni za viwanda vinavyotengeneza mifuko ya plastiki na pia haijawapa tena leseni wale wote leseni zao zilizomaliza muda, ili kuhakikisha sheria na kanuni ya kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki namba 394 ya mwaka 2019.  

Heche ametoa angalizo kwa wale wote wanaohusika na ukamataji wa watumiaji wa mifuko hiyo, kutotumia nguvu ili kuepusha mikwaruzano na kutoelewana. 
Hatahivyo, amewataka wadau hao kuhakikisha wanadai vitambulisho kwa wale wote watakaofika kwenye maeneo yao ya kazi kudai wanakagua endapo wanaendelea kuuza au kutumia mifuko ya plastiki.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha amesema tayari kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wameshatoa taarifa inayokwenda kwenye vituo vyote vya Kimataifa, ambapo kuna shirika la ndege linaloleta abiria Tanzania, ikitaarifu juu ya katazo la mifuko ya plastiki.

“Hii taarifa inajulikana kitaalam kama ‘timatic pre-information’ ambayo inatumwa kwenye centre zote duniani, ambapo kuna shirika la ndege ambalo linaleta abiria Tanzania itakuwa rahisi wao kupata taarifa ya katazo hilo na kuwafanya wasibebe mifuko hiyo,” amesema Rwegasha.

Pia amewataka wadau wote wanaofanya shughuli mbalimbali kwenye viwanja vya ndege kutoa ushirikiano mkubwa kuwaeleza abiria juu ya katazo hilo, na kuwaelekeza watumie mifuko mbadala, ambayo itakuwa ikipatikana kwenye maduka yaliyopo kwenye majengo ya Kwanza na Pili ya JNIA.
Kwa mujibu wa NEMC imesema watumiaji wa kawaida endapo watakamatwa na mifuko hiyo watatozwa faini ya Tshs. 30,000, kifungo cha siku saba, au vyote kwa pamoja;  wakati kwa muuzaji anapigwa faini ya Tshs 100,000 haizidi Tshs 500,000, kifungo cha miezi mitatu; na watengenezaji watapigwa faini ya kuanzia Tshs milioni 20 na haitazidi bilioni moja na kifungo cha miaka miwili. 
 Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Manchare Heche (aliyenyanyua mikono) akisisitiza jambo wakati akiongea na wadau wanaotoa huduma mbalimbali kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), juu ya katazo la mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku kuendelea kutumika nchini ifikapo Juni Mosi mwaka huu. Wapili kulia ni Mkurugezi wa JNIA, Paul Rwegasha na wa kwanza kushoto ni mkuu wa kitengo cha Mazingira cha TAA, Maxmilian Mahangila.
 Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha (aliyesimama) akielezea mikakati iliyowekwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), ya namna ya kutekeleza  agizo la serikali la katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki kwa watumiaji wa viwanja vya ndege nchini. Wapili kushoto ni Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Manchare Heche.
 Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Joachim Philipo akitoa ushauri kwenye mkutano wa wadau wanaotoa huduma mbalimbali JNIA ulioitishwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), na kuhusisha Wataalam kutoka Baraza ka Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), ambao walitoa maelezo mbalimbali juu ya katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki litakaloanza rasmi Juni Mosi, 2019 kwa mujibu wa sheria.
 Mmoja wa wadau wanaotoa huduma kwenye Jengo la Kwanza la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNI-TBI), Uyeka Rumbyambya akiongea katika mkutano ulioitishwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) leo kwenye Ukumbi wa Watu Mashuhuri (VIP), na kuwashirikisha Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), katazo hilo la matumizi ya mifuko ya plastiki litakaloanza rasmi Juni Mosi, 2019.
 Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji, Anna Mushi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), leo akizungumza katika mkutano wa wadau wanaotoa huduma mbalimbali JNIA katika mkutano ulioitishwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), na kuwahusisha Wataalam kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutokana na katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki ifikapo Juni Mosi, 2019.
Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Manchare Heche akiwaonesha wadau wanaotoa huduma mbalimbali kwenye Kiwanja cha Ncdege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) moja ya mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku kuendelea kutumika nchini ifikapo Juni Mosi, 2019 katika mkutano uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Watu Mashuhuri (VIP).  

ATAKAEKUTWA NA MFUKO WA PLASTIKI KUANZIA JUNI MOSI KULIPA FAINI 30,000-BYARUGABA

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA 

HALMASHAURI ya Mji wa Kibaha ,imeweka bayana kuwa kwa jamii kuwa,mtu yeyote atakaekutwa na mfuko wa plastiki kuanzia Juni mosi ,mwaka huu ,atatakiwa kulipa faini ya sh .30,000. 

Aidha halmashauri hiyo,imeendelea kutoa rai kwa wafanyabiashara na wananchi kuzingatia katazo la serikali la kutoendelea na matumizi ya mifuko hiyo ya plastiki kufungia bidhaa ifikapo siku hiyo. 

Ofisa Mawasiliano, Habari na Uhusiano wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Innocent Byarugaba ,akiongelea juu ya suala hilo kwa waandishi wa habari alieleza, katazo hili ni kwa mujibu wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004, sura 191. 

Alisema, wafanyabishara, wanunuzi na wachuuzi wengine wametakiwa kutumia mifuko rafiki wa mazingira hasa inayotengenezwa na wajasiliamali wadogo ili kulinda mazingira na kuinua kipato chao. 

Katika hatua nyingine ,ofisa mawasiliano huyo anabainisha, halmashauri hiyo pia imeanza ujenzi wa machinjio ya kisasa eneo la Mtakuja itakayogharimu sh.bilioni 1.968.505.1. 

“Kampuni iliyochukua kandarasi hiyo ni PETRA ya jijini Dar-es-Salaam kwa gharama ya sh.bilioni 1,858,505,115. na gharama ya mtaalam mshauri milioni.120 ambaye ni AMUL ARCHITEC”,:”Fedha hizi ni ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia mfuko wa uboreshaji na uendelezaji miji (ULGSP)”aliongezea kusema. 

Byarugaba alisema, lengo la halmashauri ya mji wa Kibaha ni kulinda afya za walaji kwa kuhakikisha kuwa wananchi wanakula kitoweo 
kilichoandaliwa kwenye mazingira safi kiafya.
Ofisa Mawasiliano, Habari na Uhusiano wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Innocent Byarugaba 

HALMASHAURI IGENI MFUMO WA JIJI LA DODOMA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akikabidhi hundi ya mfano kwa kiongozi wa kikundi cha Walemavu Chacha Marwa wakati wa hafla ya utoaji wa mikopo kwa vikundi vya Wanawake, vijana na walemavu katika Jiji la Dodoma. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akitembelea mabanda ya wajasiriamali wakati wa hafla ya utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake,vijana na walemavu katika Jiji la Dodoma. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akiwa na viongozi wa Mkoa na Wilaya ya Dodoma wakati wa hafla ya utoaji mikopo kwa vikundi Jijini Dodoma. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo katika picha na viongozi pamoja na baadhi ya wawakilishi wa vikundi vya wanawake walipata mikopo isiyo na riba toka Halmashauri ya Jiji la Dodoma. 
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi akitoa taarifa ya utoaji mikopo wakati wa hafla ya utoaji mikopo kwa vikundi katika Jiji la Dodoma 
………………………….. 

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amezitaka halmashauri zote nchini kuiga mfano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika utoaji wa mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye walemavu. 

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya mfano yenye thamani ya zaidi ya shilingi bil 1.06 (1,062,500,000) kutoka katika mapato ya ndani ya Jiji la Dodoma kwa mwaka wa Fedha 2018/19 kwa vikundi 201. 

Alisema kuwa halmashauri zingine zihakikishe kuwa asilimia 10 ya mapato yao ya ndani inapelekwa moja kwa moja kwenye vikundi vya wanawake na vijana na watu wenye ulemavu ili kuwainua kiuchumi. 

“ Jiji la Dodoma limekuwa la mfano katika mambo mengi kuanzia ukusanyaji wa mapato wameongoza katika pato ghafi na leo hii wametekeleza kwa vitendo Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura Na, 290 kifungu 37A na kanuni zake za utoaji na usimamizi wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu za mwaka 2019. 

Jafo aliongeza: “ Kukusanya mapato ni jambo moja na utoai wa mikopo ni jambo jingine, halmashauri inaweza kukusanya lakini isitoe mikopo hii kwa vikundi, sasa Dodoma wameyafanya yote haya kwa umakini na ufanisi mkubwa niwapongeze Jiji la Dodoma na niwatake Halmashauri zingine waje kujifunza na kuiga mfano wenu mnafanya kazi nzuri. 

Wakati huo huo, Jafo ameutaka uongozi wa Jiji la Dodoma kukaa pamoja na wadau kubuni na kuunzisha mradi mkubwa ambao utaweza kuwanufaisha makundi maalumu ambao utatekelezwa na asimilia 10 ya mapato ya ndani. 
“Unajua wananchi wetu wanataka kufanikiwa katika biashara na pia wanapendelea biashara kubwa hivyo mkibuni mradi mkawatengenezea vizuri kisha mkawakabidhi kama sehemu ya mkopo itawajenga na kubadilisha maisha yao kuliko kila siku kuwapa fedha ni vyema wakati mwingine mkawapa vitega uchumi,” aliongeza Jafo. 

Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe amesema Jiji la Dodoma pamoja na kutoa mikopo hii wameenda mbali zaidi kwa kuhakikisha wanatafuta vyuo vya kutoa ujuzi na maarifa zaidi kwa wanufaika wa Mikopo ili iweze kuwa na tija zaidi. 

Pia alisema katika siku zijazo wanatarajia kutoa vifaa na vitendea kazi vya biashara zao kuliko kuwapa fedha ili kuwaepusha na vishawishi vinavyoweza kutokea kutokana na kushika fedha mkononi. 

Naye Mkurugenzi wa Jiji hilo, Godwin Kunambi alisema kuwa Jiji la Dodoma limeanza kutoa mikopo kwa vikundi kuanzia mwaka wa fedha wa 2015/16 hadi Desemba 2018 ambapo jumla ya shilingi 2,434,757,316 ziko kwenye mzunguko wa mikopo ya vikundi. 

Aliongeza kuwa kiasi cha zaidi ya Sh bilioni 2.6 (2,606,645,760) zilitengwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2018/19 huku kiasi cha shilingi 1,796,730,000 kimeshatolea katika kipindi cha mwezi Julai hadi Disemba 2018. 

“Fedha za vikundi unazokabidhi leo kiasi cha shilingi 1,062,500,000 zinaifanya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mwaka wa fedha 2018/19 kutoa mikopo ya jumla ya shilingi 2,859,230,000 sawa na asilimia 109.6 ya malengo tuliyojiwekea” alisema Kunambi. 

Jumla ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu vilivyokwishanufaika na mikopo ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuanzia mwaka 2015/16 mpaka sasa ni 1,020 vyenye jumla ya Wanachama 10,200 vikiwa na mzunguko wa jumla ya shilingi 3,497,257,316.

ATSOKO WAADHIMISHA MIAKA 7 TANGU KUANZISHWA KWAKE NCHINI

$
0
0
*Yajivunia kutoa ajira kwa wanawake, Balozi Sweden ahaidi kuzidi kishirikiana na Tanzania

BALOZI wa Sweden nchini Anders Sjoberg amesema kuwa  ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Sweden utazidi kudumishwa na hiyo ni katika kushirikiana katika masuala ya kiuchumi na kijamii.

Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 7 tangu kuanzishwa kwa kampuni ya Kiswedish Atsoko iliyoanza mwaka 2012 kwa duka moja lililopo Mikocheni hadi kufikia maduka 7 ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa sasa ambayo yanapatikana  Mikocheni, Slipway-Masaki, Mbezi Beach - Shoppers, Mlimani City, City Mall, Samora Avenue na Quality Centre Anders amesema kuwa wanasherekea miaka 7 ya Atsoko ikiwa na maendeleo lukuki na bado wanaendelea kuangalia njia zaidi za kutoa fursa kwa watanzania kupitia Atsoko.

Amesema kuwa nchini Tanzania soko ni zuri na kumekuwa na ushindani mkubwa hali inayowapa moyo katika kutoa fursa zaidi ili kujenga nchi ya viwanda na kuhusu kutoa ajira Balozi Anders amesema kuwa wamekuwa wakitoa vipaumbele kwa wanawake katika ajira na hiyo ni katika kuwainua zaidi katika suala zima la kiuchumi.

Amesema kuwa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili utazidi kuimarika zaidi huku akihaidi kuendelea kushiriki katika kuendeleza shughuli za kijamii na kiuchumi.

Kwa upande wake Meneja mkuu wa Atsoko Tanzania Rehema Julias amesema kuwa, kusheherekea miaka 7 pia  wamezindua bidhaa mpya ya Makeup inayoitwa Note. Ni bidhaa nzuri kutoka Uturuki ambayo inakidhi viwango vya kimataifa na imetengenezwa kwa ajili ya soko la Afrika.

Amesema kuwa kupitia Atsoko vijana na wanawake wamepata ajira na kujiajiri wenyewe huku akiwahakikishia watanzania ubora kwa bidhaa hizo kimatumizi.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Anders Sjöberg akizungumza na wateja pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Atsoko Tanzania wakati wa hafla ya kusherekea miaka 7 ya kuanzishwa kwa kampuni hiyo hapa Tanzania iliyofanyika katika duka lao Mlimani City jijini Dar ee Salaam.
Meneja mkuu wa Atsoko Tanzania, Rehema Julius akizungumza kwenye hafla ya kusherekea  miaka saba ya kuanzishwa kwa kapuni hiyo ya vipodozi hapa nchini iliyofanyika katika Duka lao Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya  wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi wa Atsoko wakifuatilia yanayoendelea kujili kwenye  hafla ya kusherekea  miaka saba ya kuanzishwa kwa kapuni hiyo ya vipodozi hapa nchini iliyofanyika katika Duka lao Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AJUMUIKA KATIKA FUTARI NA WANANCHI WA MKOA WA KUSINU UNGUJA

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja katika futari aliyowaandalia katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA)kushoto Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hassan Khatib Hassan.
WANANCHI wa Mkoa wa Kusini Unguja wakiwa katika ukumbi wa SUZA Tunguu Mkoa wa Kusini katika futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.
WANANCHI wa Mkoa wa Kusini Unguja wakijumuika na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, katika futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, kwa Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja iliofanyika katika ukumbi wa Uhamiaji Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja katika futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk Ali Mohamed Shein, iliofanyika ukumbi wa Idara ya Uhamiaji Tunguu.

WANANCHI wa Mkoa wa Kusini Unguja wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja akitowa neno la shukrani baada ya kumaliza hafla hiyo ya futari iliofanyika ukumbi wa SUZA Tunguu Zanzibar.
MKUU wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hassan Khatib Hassan, akitowa neno la shukrani kwa Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, iliofanyika katika ukumbi wa SUZA Tunguu Zanzibar.
WANANCHI wa Mkoa wa Kusini Unguja wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliofanyika katika ukumbi wa SUZA Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia dua ikisoma na Sheikh Abubakary Ally, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Shein, kwa Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja,iliofanyika katika ukumbi wa SUZA Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja baada ya kumalizika hafla ya futari maakum aliyowaandaliwa katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Tunguu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na kuagana na Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe.Kitwana Idrisa Mustafa, wakifurahia jambo, wakiwa katika viwanja vya Chuo Kikuu cha SUZA Tunguu, kushoto Mwakilishi wa Tunguu Mhe. Simai Mohammed Said na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hassan Khatib Hassan na kulia Sheikh Abubakary Ally. Picha na Ikulu, Zanzibar.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZUNGUMZA KATIKA FUTARI ILIYO ANDALIWA NA BANK YA NMB

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Albert Jonkergouw katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa Masheikh wa Mikoa ya Kanda ya Kati, Wazee wa Dodoma, Wabunge, Viongozi wa Dini, Wananchi, wawakilishi wa Taasisi mbalimbali na wafanyakazi wa NMB kwenye hoteli ya Dodoma, Mei 24, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa Masheikh wa Mikoa ya Kanda ya Kati, Wazee wa Dodoma, Wabunge, Viongozi wa Dini, Wananchi, wawakilishi wa Taasisi mbalimbali na wafanyakazi wa NMB kwenye hoteli ya Dodoma, Mei 24, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa Masheikh wa Mikoa ya Kanda ya Kati, Wazee wa Dodoma, Wabunge, Viongozi wa Dini, Wananchi, wawakilishi wa Taasisi mbalimbali na wafanyakazi wa NMB kwenye hoteli ya Dodoma, Mei 24, 2019.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania watumie Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kudumisha amani na mshikamano na kuwaombea viongozi wa kitaifa.

“Mwezi huu tuna majukumu makubwa ya kufanya ibada, kutubu dhambi zetu na kuomba rehma kwa Mwenyezi Mungu pamoja na kudumisha mshikamano na kuwa wavumilivu.”

Waziri Mkuu alitoa wito huo jana jioni (Ijumaa, Mei 24, 2019) aliposhiriki hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya NMB iliyofanyika katika Hoteli ya Dodoma. Alisema kila wananchi aendelee kuliombea Taifa lizidi kudumisha amani na mshikamano. “Tuhakikishe tunatenda matendo mema yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu.”

Kadhalika, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuipongeza benki ya NMB kwa huduma bora wanazozitoa kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuwa na matawi mengi hadi vijijini.

Awali, Mkurugenzi wa benki ya NMB, Albert Jonkergouwalisema lengo la kuandaa hafla hiyo ya futari ni kuimarisha ushirikiano uliopo baina yao na wateja wao. Mkurugenzi huyo alisema katika kipindi hiki Waislamu wanapaswa kumrudia Muumba wao na kumshukuru kwa mema yote anayowajalia waja wake. 

“Mwezi wa Ramadhan ni kipindi muafaka cha kufuturu pamoja hivyo, nawashukuru wateja wetu kwa kujumuika nasi nawaomba muendelee kutumia huduma zetu.”

Alisema mkusanyiko huo unadhihirisha kuwa wao ni sehemu ya jamii ya Watanzania wote, hivyo aliwasisitiza wateja wa benki hiyo waendelee kutumia zaidi huduma za kidijitali.

Hafla hiyo ilihudhuliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Mashekhe wa Mikoa ya Kanda ya Kati (Dodoma, Singida na Manyara).


Wengine ni Wazee wa Dodoma, Waheshimiwa Wabunge , Viongozi wa dini, wananchi, Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali na Wafanyakazi wa NMB.
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images