Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110129 articles
Browse latest View live

TUTUMIE MWEZI WA RAMADHANI KWA KUDUMISHA AMANI-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa Masheikh wa Mikoa ya Kanda ya Kati, Wazee wa Dodoma, Wabunge, Viongozi wa Dini, Wananchi, wawakilishi wa Taasisi mbalimbali na wafanyakazi wa NMB kwenye hoteli ya Dodoma, Mei 24, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa Masheikh wa Mikoa ya Kanda ya Kati, Wazee wa Dodoma, Wabunge, Viongozi wa Dini, Wananchi, wawakilishi wa Taasisi mbalimbali na wafanyakazi wa NMB kwenye hoteli ya Dodoma, Mei 24, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Albert Jonkergouw katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa Masheikh wa Mikoa ya Kanda ya Kati, Wazee wa Dodoma, Wabunge, Viongozi wa Dini, Wananchi, wawakilishi wa Taasisi mbalimbali na wafanyakazi wa NMB kwenye hoteli ya Dodoma, Mei 24, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa Masheikh wa Mikoa ya Kanda ya Kati, Wazee wa Dodoma, Wabunge, Viongozi wa Dini, Wananchi, wawakilishi wa Taasisi mbalimbali na wafanyakazi wa NMB kwenye hoteli ya Dodoma, Mei 24, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

………………………………………………… 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania watumie Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kudumisha amani na mshikamano na kuwaombea viongozi wa kitaifa. 

“Mwezi huu tuna majukumu makubwa ya kufanya ibada, kutubu dhambi zetu na kuomba rehma kwa Mwenyezi Mungu pamoja na kudumisha mshikamano na kuwa wavumilivu.” 

Waziri Mkuu alitoa wito huo jana jioni (Ijumaa, Mei 24, 2019) aliposhiriki hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya NMB iliyofanyika katika Hoteli ya Dodoma. 

Alisema kila wananchi aendelee kuliombea Taifa lizidi kudumisha amani na mshikamano. “Tuhakikishe tunatenda matendo mema yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu.” 

Kadhalika, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuipongeza benki ya NMB kwa huduma bora wanazozitoa kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuwa na matawi mengi hadi vijijini. 

Awali, Mkurugenzi wa benki ya NMB, Albert Jonkergouwalisema lengo la kuandaa hafla hiyo ya futari ni kuimarisha ushirikiano uliopo baina yao na wateja wao. Mkurugenzi huyo alisema katika kipindi hiki Waislamu wanapaswa kumrudia Muumba wao na kumshukuru kwa mema yote anayowajalia waja wake. 

“Mwezi wa Ramadhan ni kipindi muafaka cha kufuturu pamoja hivyo, nawashukuru wateja wetu kwa kujumuika nasi nawaomba muendelee kutumia huduma zetu.” 

Alisema mkusanyiko huo unadhihirisha kuwa wao ni sehemu ya jamii ya Watanzania wote, hivyo aliwasisitiza wateja wa benki hiyo waendelee kutumia zaidi huduma za kidijitali. Hafla hiyo ilihudhuliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Mashekhe wa Mikoa ya Kanda ya Kati (Dodoma, Singida na Manyara). 

Wengine ni Wazee wa Dodoma, Waheshimiwa Wabunge , Viongozi wa dini, wananchi, Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali na Wafanyakazi wa NMB.

RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA RAIS WA AFRIKA KUSINI CYRIL RAMAPHOSA JIJINI PRETORIA LEO

$
0
0




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe.Cyril Ramaphosa Muda mfupi mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo katika uwanja wa Michezo wa Loftus Versfeld Jijini Pretoria Afrika kusini.Mei 25, 2019.
Umati mkubwa wa wananchi unalipuka kwa shangwe na chereko wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili katika uwanja wa michezo wa Loftus Versfeld jijini Pretoria kuhudhuria sherehe za kuaishwa kwa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa leo Jumamosi Mei 25, 2019 

WANACHUO WATAKIWA KUJIWEKEA MALENGO KATIKA MATUMIZI YA FEDHA

$
0
0

Mkurugenzi wa UNILIFE CAMPAS, Dosi Said Dosi wakati akitoa somo la kujitambua kwa wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ajili ya kuwajengea uwezo wa kujiwekea akiba yaliyoandaliwa na UNILIFE CAMPAS jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wakifuatilia.

 Meneja wa Benki ya NBC tawi la Muhimbili Alphonce Musiba akitoa nasaha zake kwa wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa fedha mapema leo wakati wakitoa masomo kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kujiwekea akiba yaliyoandaliwa na UNILIFE CAMPAS jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi wa Smart Me App, Innocent Mathias amewataka vijana wenzake kuwa msitari wa mbele kuweka malengo yao katika masomo huku wakijiwekea akiba katika kipato cha fedha wanazopata.
Mwanzilishi mwenza wa Smart Me App, Edger Lwambano nnocent akiongea machache.

Afisa Mauzo wa Benki ya NBC tawi la Muhimbili, Jane Haule akitoa machache kwa wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
 Wanafunzi wakipata maelezo mbali mbali juu ya kufungua akaunti.
 Kila mmoja busy na kazi...
 Afisa Mauzo wa Benki ya NBC tawi la Muhimbili Jane Haule akiwafungulia akaunti ya malengo wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
 Majadiliano kidogo yakiendelea...
Na Cathbert Kajuna - Kajunason - Kajunason/MMG.
Wanafunzi wa vyuo wametakiwa kuweka malengo katika matumizi yao ili waweze kufanikiwa katika maisha yao.
Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Unilife Campas, Dosi Said Dosi wakati akitoa somo la kujitambua kwa wanachuo wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam.
Dosi amesema kuwa ipo haja ya wanafunzi kuanza kujiwekea akiba ya fedha na kujihusisha na miradi midogo midogo itakayoweza kuwavusha hata pindi watakapomaliza chuo.
"Wakati umefika kila mmoja wetu kujiwekea akiba ya kile kidogo ambacho unakipata sasa maana huko mbeleni ukimaliza chuo utakuta umeweka kidogo kuliko kumaliza akiba yote," amesema Dosi.
Ameongeza pia kuwakaribisha vijana wanachuo na waliomaliza kufika ofisi za Unilife Campus kuweza kuwapatia elimu ya namna ya kuanzisha kampuni za aina mbalimbali bure ili waweze kujiajiri.
Kwa upande wake wa Meneja wa Benki ya NBC tawi la Muhimbili Alphonce Musiba amewaomba vijana kuendelea kuwa wabunifu wa kubuni miradi huku wakijiwekea akiba kwa pesa kidogo wanazozipata.
"Ukiwa chuo unakuwa na nafasi nyingi za kupata fedha hasa kwa wazazi, walezi na wengineo sasa ni vyema kuwa na adabu nazo ili zikuvushe katika maisha yako," amesema .
Ameongeza kuwa kwa sasa benki ya NBC wameanzisha akaunti ya kuwawezesha wanafunzi kujiwekea akiba kidogo kidogo ili waweze kufikia malengo yao.
Nae mwanzilishi wa Smart Me App, Innocent Mathias amewataka vijana wenzake kuwa msitari wa mbele kuweka malengo yao katika masomo huku wakijiwekea akiba katika kipato cha fedha wanazopata.
"Binafsi nimefanikiwa kujiwekea akiba mpaka leo nimefika hapa nilipo kwa ajili ya adabu na heshima katika matumizi ya fedha ninazopata nikiwa chuo, tuweke akiba hata ikiwa shilingi 500 baadae unakuwa na kiasi kikubwa tu. Hivyo nawaasa wanafunzi wafungue akaunti ya kuhifadhi fedha pamoja kupitia SmartMe ili ziweze kuwanufaisha baadae.

HALMASHAURI YA MJI WA MAFINGA YAPATA HATI SAFI KUTOKA KWA CAG

$
0
0
Makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Zakaria Vang’ota akiwa sambamba na kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Francis Maghembe waalisema kuwa kupatikana kwa hati safi katika Halmashauri hiyo kutachochea zaidi kasi ya utendaji kazi ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa
Baadhi ya madiwani na watendaji wa halmasahuri ya Mji wa Mafinga wakifuatilia kwa umakini ripoti ya CAG wakati wa baraza maalum la halmashauri hiyo




NA FREDY MGUNDA,MAFINGA.

HALMASHAURI ya mji wa Mafinga imefanikiwa kupata hati safi kutokana na utendaji bora,usimamizi wa miradi ukusanyaji mapato kwenye vyanzo vyake vya ndani katika kipindi cha mwaka 2018-2019.

Akizungumza kwenye kikao maalumu cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kwa lengo la kusoma rasmi taarifa ya CAG kwa niaba ya mkuu wa mkoa, Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Iringa, Lucas Kambelenje alisema Halmashauri hiyo imeweza kupata hati safi katika kipindi cha mwaka 2018 -2019 kutokana na watendaji wake wakiwemo madiwani kufanya kazi kwa ushirikiano katika suala zima la kuhakikisha mapato yanakusanywa kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na kipindi cha nyuma. 
‘’Nawapongeza watendaji wa Halmashauri na madiwani kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na kufanikiwa kupata hati safi, hivyo nawapongeza muongeze kasi zaidi kiutendaji na kamwe msibweteke,’’alisema

Aidha aliwataka kufuata misingi imara itayowawezesha kudhibiti mapato na matumizi ya halmashauri kwa kuondoa mapungufu yaliyojitokeza katika kipindi cha nyuma kama kuchelewa kuwasilisha mahesabu kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG) ,kuchelewa kuwasilisha taarifa za matumizi bila ya kuwa na viambatanishi vya malipo .

‘’Pia epukeni kulipa madeni hewa kwa watumishi ama waliokufa,kuacha kazi ama watumishi watoro sehemu za kazi, kwani kufanya hivyo kutapelekea halmashauri kupata hati chafu.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Zakaria Vang’ota alisema kuwa kupatikana kwa hati safi katika Halmashauri hiyo kutachochea zaidi kasi ya utendaji kazi ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.‘’Ni dhahiri kila diwani atatekeleza majukumu yake ili kuweza kudhibiti mapato na matumizi ya halmashuari ma kuweza kufanya vizuri zaidi,‘’alisema Vang’ota.

Hata hivyo Vang’ota aliwahimiza madiwani kufanya kazi kwa ushirikiano na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea na kuwataka kuwatendea haki wananchi ambao wamewachagua kwa kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi kwa kuwatataulia kero zinazowakabilia.Akizungumzia hoja hizo kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Francis Maghembe alisema kuwa watahakikisha hoja zote zinafanyiwa kazi ili kusijitokeze hoja nyingine au kuongezeka kwa madeni ambayo halmashauri inadaiwa. 

MAKAMPUNI MATATU YATAKAYOSAFIRISHA MASHABIKI WA SOKA KULEKEA MISRI NA TAIFA STARS YATANGAZWA

$
0
0
Mkurugenzi wa Michezo Yusuph Singo, akizungmza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani), leo Jumamosi, 25 Mei 2019, kuhusu Kutoa kibali kwa Makampuni matatu yatakayosafirisha watanzania kwenda kuiunga mkono Timu ya Taifa (Taifa Stars) katika Michuano ya Mataifa ya Africa (AFCON) Nchini Misri June 21, 2019 hadi Julai 19, 2019, kulia kwake ni Mwakilisha wa kampuni ya Clouds Media Group (CMG), Shafii Dauda na Mwakilishi kutoka World Link, Zaki Admani 
Mwakilishi wa kutoka kampuni ya Clouds Media Group, Shafii Dauda akieleza jambo kuhusu namna ya kuwasafirisha watanzania watakajitokeza kwenda kuiunga mkono Timu ya Taifa (Taifa Stars) katika Michuano ya Mataifa ya Africa (AFCON) Nchini Misri June 21, 2019 hadi Julai 19, 2019, baada CMG kupata kibali hicho kutoka kwa Serikali, Kushoto ni Mwakalishi kutoka Kampuni ya Travel Link, Ephrem Mtuya, Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Singo na Mwakilishi kutoka World Link, Zaki Admani 
Mwakilishi kutoka World Link, Zaki Admani akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu namna ya kuwasafirisha watanzania watakajitokeza kwenda kuiunga mkono Timu ya Taifa (Taifa Stars) katika Michuano ya Mataifa ya Africa (AFCON) Nchini Misri June 21, 2019 hadi Julai 19, 2019, Baada ya Kampuni hiyo kupata kibali hicho kutoka kwa Serikali, Kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo Yusuph Singo 
Mwakalishi kutoka Kampuni ya Travel Link, Ephrem Mtuya, akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu namna ya kuwasafirisha watanzania watakajitokeza kwenda kuiunga mkono Timu ya Taifa (Taifa Stars) katika Michuano ya Mataifa ya Africa (AFCON) Nchini Misri June 21, 2019 hadi Julai 19, 2019, Baada ya Kampuni hiyo kupata kibali hicho kutoka kwa Serikali Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu kutoka Travel Link, Doreen Gafoor na kulia ni Mkurugenzi wa Michezo Yusuph Singo. 

(Picha na Paschal Dotto-MAELEZO) 

…………………………………………………………………. 

MAELEZO-DAR ES SALAAM 

SERIKALI kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Nchini (TFF) imeyataja Makampuni matatu yatakayotumika kusafirisha Mashabiki wa Soka na Watanzania kwa ajili ya kuishangilia Timu ya Soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wakati wa Michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Mwezi Juni, mwaka huu nchini Misri. 

Akizungumza na Waandishi wa Vyombo ya Habari leo Jumamosi (Mei 25, 2019), Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo aliyataja Makampuni hayo kuwa ni pamoja na Clouds Entertainment Group Ltd, Travel Link na World Link, ambayo yalishinda mchakato wa ushindani na makampuni mengine kutokana na kukidhi vigezo mbalimbali vilivyoanishwa. 

Kwa mujibu wa Singo alisema Serikali na kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Nchini (TFF) waliamua kusimamia mchakato wa kupata makampuni hayo ili kuzuia aina yoyote ya utapeli kwa Watanzania hususani Mashabiki wa Soka wa hapa nchini watakaojitokeza kwenda Nchini Misri kuipa nguvu ya ushingiliaji Taifa Stars. 

“Katika miaka ya nyuma kulikuwa na utapeli katika haya makampuni ya usafirishaji, hivyo Serikali kwa kushirikiana na TFF tumeyapata Makampuni matatu, bei zao zitakuwa rahisi na wamepanga kuwa na nembo ya pamoja ambayo wataitangaza ili iweze kujulikana na Watanzania” alisema Singo. 

Aidha Singo alisema kuhusu utaratibu wa visa za kusafiri makampuni hayo kwa kushirikana na TFF yatatoa taarifa ya jinsi Mashabiki wa Soka watavyoweza kupata huduma hiyo kabla ya kuanza kwa michuano hiyo inayotarajia kuanza kutimua vumbi tarehe 21 Juni mwaka huu. 

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Kampuni ya Clouds Entertainment Group Ltd, Shaffih Dauda alisema Kampuni yao imejipanga vyema kuhakikisha kuwa inatoa huduma zote muhimu kwa Watanzania watakaosafiri kwenda Nchini Misiri kuishangalia Taifa Stars ikiwemo visa, usafiri wa ndani, malazi katika kipindi cha siku 10 za mechi tatu za makundi itayocheza Taifa Stars. 

“Clouds Entertainment Ltd kila mwaka tuna msimu wa kulevya wa soka, mwaka jana tulikuwa na Msimu wa kulevya wa Kombe la Dunia kule nchini Urusi, na sasa tunarudi Afrika na tutawahudumia vyema mashabiki watakaojitokeza kwa kiasi cha Dola za Kimarekani 1650 na pia tutaoa ofa ya Mashabiki hao kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini Misri” alisema Dauda. 

Aliongeza kuwa katika kutoa urahisi wa huduma kwa Watanzania hususani suala la malazi, Kampuni yao tayari kwa kushirikiana na wakala wao aliyopo nchini Misri, wamepata mmoja wa Mitaa maarufu nchini Misri ujulikanao Kilimanjaro ambapo utawezesha Mashabiki wa Watanzania kupata huduma zote muhimu kuwafanya Mashabiki hao huko kujiona kuwa wapo nyumbani. 

Kwa upande wake, Meneja Maendeleo ya Masoko wa Kampuni ya World Link, Zaki Admani alisema kampuni hiyo itatoza kiasi cha Dola za Kimarekani 1550 kwa Mashabiki wa Soka, ambayo watasafiri kuelekea Nchini Misri pamoja na kutoa ofa ya kuchagua mechi moja yoyote ambayo mshabiki wa Soka atapenda kuingalia katika timu zitakazochuana na Taifa Stars. 

Aliongeza kuwa kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo Kampuni hiyo itatoa kifurushi kitakachomwezesha Shabiki wa Soka hapa nchini kuweza kuchagua idadi ya mechi ambazo atapenda kuziangalia wakati akiwa na Timu ya Taifa Stars nchini Misri. 

“Wapo wengine watapenda kuangalia mechi moja, na hili tumeliangalia na mapema wiki ijayo kuanzia jumatatu tutatoa utaratibu wake wa namna ya kuwasaidia mashabiki wa aina hii” alisema Admani. 

Naye Meneja Utawala wa Kampuni ya Travel Link, Ephrem Mtuya alisema kuwa kwa miaka 15 sasa Kampuni hiyo imekuwa ikifanya kazi pamoja na TFF kwa ajili ya kuwasifirisha wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania katika nchini mbalimbali na hivyo amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kusafiri na Kampuni hiyo ili kwenda kuipa nguvu Timu ya Taifa ya Tanzania ikiwa nchini Misri. 

Alisema Kampuni imeweka kiwango cha Dola za Kimarekani 1300 pekee kwa Mtanzania yotote atayapenda kusafiri na Timu hiyo hususani Mashabiki wa Soka ikihusisha Gharama za Tiketi ya Ndege, usafiri, pamoja na huduma za malazi.

WAFANYABIASHARA NCHINI WATAKIWA KUBORESHA VIFUNGASHIO-BRELLA

$
0
0
Msajili Msaidizi Kitengo cha Ubunifu (Brella) Suzana Senso akisisitiza jambo kwa Kaimu Afisa Forodha wa Kituo cha Horohoro Nsajigwa Mwambegele katikati ni Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA) Bakari Mketo
Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA) Bakari Mketo katikati akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakati wa ziara hiyo kushoto ni Msajili Msaidizi Kitengo cha Ubunifu (Brella) Suzana Senso kulia ni Kaimu Afisa Forodha wa Kituo cha Horohoro Nsajigwa Mwambegele
Kaimu Afisa Forodha wa Kituo cha Horohoro Nsajigwa Mwambegele katikati akiteta jambo kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA) Bakari Mketo kulia ni Msajili Msaidizi Kitengo cha Ubunifu (Brella) Suzana Senso
Msajili Msaidizi Kitengo cha Ubunifu (Brella) Suzana Senso kushoto akitetaa jambo na Kaimu Afisa Forodha wa Kituo cha Horohoro Nsajigwa Mwambegele wakati wa ziara hiyo
Msajili Msaidizi Kitengo cha Ubunifu (Brella) Suzana Senso kulia akiwa na Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA) Bakari Mketo
Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA) Bakari Mketo katikati akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya ziara hiyo kushoto ni Afisa Mfawidhi wa Forodha wa Kituo cha Horohoro Bakari Athumani kulia ni Msajili Msaidizi Kitengo cha Ubunifu (Brella) Suzana Senso
Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA) Bakari Mketo kulia akimkabidhi vipeperushi Afisa Mfawidhi wa Forodha wa Kituo cha Horohoro Bakari Athumani kushoto mara baada ya ziara hiyo
Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA) Bakari Mketo akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya kufika ofisi ya Forodha kituo cha Horohoro mpakani mwa Tanzania na Kenya wakati wa ziara yake wakati zoezi la Uhamasishaji wa utengenezaji wa bidhaa bora katika soko hilo ambapo alisema bidhaa bora ni lazima ziwe kwenye kifunganisho ambacho pia kitaonyesha taswira halisi ya thamani.
Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA) Bakari Mketo kulia aakiteta jambo na Kaimu Afisa Forodha wa Kituo cha Horohoro Nsajigwa Mwambegele
Kaimu Afisa Forodha wa Kituo cha Horohoro Nsajigwa Mwambegele kushoto akiteta jambo na Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA) Bakari Mketo wakati wa ziara yake wakati zoezi la Uhamasishaji wa utengenezaji wa bidhaa bora katika soko hilo ambapo alisema bidhaa bora ni lazima ziwe kwenye kifunganisho ambacho pia kitaonyesha taswira halisi ya thamani.



WAFANYABIASHARA wa Kati na Wakubwa nchini wametakiwa kuboresha vifungashio vya bidhaa zao katika soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuepuka kupoteza ubora na bidhaa wanazotengeneza kutokana na kukosekana kwa hali hiyo

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA) Bakari Mketo wakati alipofanya ziara ya kutembelea mpaka wa Horohoro unaotengenisha ya Tanzania na Kenya.

Ziara hiyo ilikuwa ni zoezi la Uhamasishaji wa utengenezaji wa bidhaa bora katika soko hilo ambapo alisema bidhaa bora ni lazima ziwe kwenye kifunganisho ambacho pia kitaonyesha taswira halisi ya thamani.

Aidha alisema kwamba lazima wafanyabiashara wahakikisha wanakuwa bora kwenye kuzipa thamani bidhaa zao kwani vifungashio sio kupaki tu bali hata ujumbe uliopo na nembo ya bidhaa anuani na eneo ambalo unapatikana ili kurahisisha upatikanaji wake.

“Isije kutokea watu wanakaa na vifungishio vya nchi jirani kuliko vya hapa nchini inafanya wakati mtu anaponunua bidhaa za ndani hajisikii kukaa na bidhaa hiyo kuliko ilivyokuwa vya nje kwenye soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo lazima tuingie kwenye ushindani tukiwa na ubora wa vifungashio”Alisema, 

Mkurugenzi huyo alisema walichokuwa wakiangalia kwenye ziara hiyo ni namna gani brella wanaweza kupata huduma ya boda linki kwa kuhusanisha na kituo hicho cha horohoro ili kuhakikisha wadau wao hawapati usumbufu kwenye urasimishaji wa biashara zao .

Naye kwa upande wake Msajili Msaidizi Kitengo cha Ubunifu (Brella) Suzan Senso alisema mpaka sasa wamekwisha kutembelea mikoa 17 ambapo sehemu kubwa ya wafanyabiashara wamehamasika na kuanza kusajili biashara zao ili kukuza thamani ya bidhaa wanazozalisha.

Alisema pamoja na mambo mengine watawaelimisha waafanyabiashara kuhusu mfumo wa usajili wa ORS hivyo wanaimani kubwa mwitikio wa wafanyabiashara kujisali utaongezekana kutokana na kupata uelewa wa masuala mbalimbali .

DKT. KALEMANI:SERIKALI IMETENGA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 40 KWAAJILI YA UMEME NGORONGORO

$
0
0
Waziri wa Nishati Medard Kalemani akionyesha moja ya Mita ambazo zinaweza kutumika kwa mwananchi wa kawaida katika matumizi ya nyumbani ikiwemo kutumika kwenye taa,jiko,friji na matumizi mwengine ambayo alikwenda nazo za bure 
Waziri wa Nishati Medard Kalemani akiwa amezungukwa na wananchi wa Digodigo kama inavyoonekana kwenye picha ,pembeni yake anaonekana Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Willium Tate Olenasha ambae pia ni Mbunge wa Ngorongoro.
Waziri wa Nishati Medard Kalemani akionyesha moja ya Mita ambazo zinaweza kutumika kwa mwananchi wa kawaida katika matumizi ya nyumbani ikiwemo kutumika kwenye taa,jiko,friji na matumizi mengine hapa akimkabidhi mwananchi mita hiyo bure.
Waziri wa Nishati akitolea ufafanuzi jambo kwa wananchi wa Dogodigo.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Tate Olebasha akisalimia na wananchi wa Digodigo kama inavyoonekana pichani. 
Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalimani akisalimiana na wananchi wa Digodigo wilayani Ngorongoro ambapo alikwenda huko kwaajili ya uzinduzi wa awamu ya tatu ya umeme wa Rea umefanyika Kimkoa katika Mkoa wa Arusha. 
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na wananchi wa Digodigo wilayani Ngorongoro ambapo umeme wa Rea awamu ya tatu umezinduliwa Kimkoa na Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani.
Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha Injinia Herini Mhina 
Mhandisi wa Miradi ya REA Nchini John Kitonga
Kutoka kulia ni Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha Herini Mhina akifiatiwa na Meneja wa Tanesco wilaya ya Ngorongoro Domonic Shahid walipokuwa wakitambulishwa kwa wananchi katika Kata ya Dogodigo ,kijiji cha digodigo wilaya ya Ngorongoro. 
Kutoka kulia ni Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha Herini Mhina akifiatiwa na Meneja wa Tanesco wilaya ya Ngorongoro Domonic Shahid,Msimamizi wa Rea Tanesco Gesto Jindwa, walipokuwa wakitambulishwa kwa wananchi katika Kata ya Dogodigo ,kijiji cha digodigo wilaya ya Ngorongoro
Kutoka kulia ni Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha Herini Mhina akifiatiwa na Meneja wa Tanesco wilaya ya Ngorongoro Domonic Shahid,Msimamizi wa Rea Tanesco Gesto Jindwa, Wengine ni wakandarasi Wakandarasi wa kampuni ya Nipo Group wanaotekelea mradi huo walipokuwa wakitambulishwa kwa wananchi katika Kata ya Dogodigo ,kijiji cha digodigo wilaya ya Ngorongoro
Waziri wa Nishati Medard Kalemani akiwahutubia wananchi wa Kata ya Digodigo wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha alipokwenda kuwasha umeme awamu ya tatu wa Rea ambapo uzinduzi huo umefanyika kimkoa.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Digodigo wakimpokea Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani alipotembelea Shuleni hapo.
Waziri wa Nishati Dkt Mesard Kalemani akizungumza na wanagunzi wa Shule ya Sekondari Digodigo ambapo amewataka kusoma kwa bidii muda na wasichezee Elimu kwani muda wa mapenzi kwao bado sana.Habari/ Picha na Vero Ignatus -Michuzi TV.



Na.Vero Ignatus,Ngorongoro.

Ni zaidi ya kilometa 400 kutoka Arusha Mjini hadi kufikia kata ya Digodigo iliyopo wilaya ya ngorongoro ambayo umezinduliwa umeme wa awamu ya Tatu REA Kimkoa na kuwashwa katika maeneo mbalimbali wilayani humo.

Akizindua Mradi huo waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani amesema serikali imetoa zaidi ya Sh.bilioni 40 kwa ajili ya umeme, hivyo vema kila mwananchi ahakikishe anawasha nyumbani kwake umeme kabla ya kulazimishwa,kwani umeme huo umepelekwa kupitia Wakala wa umeme vijijini REA.

"Serikali imetumia fedha nyingi hizi sasa sio mchezo watu tuache kuunganisha umeme katika nyumba zenu msisubiri tuwalazimishe,"alisema tutatumia zaidi ya Sh.bilioni 20 katika miradi hiyo ya umeme.Dkt.Kalemani ametoa agizo kwa wakandarasi wa kampuni ya Nipo Group kuongeza kasi katika utendaji wasibweteke kwani mradi huko awali ulisuasua hivyo ifikapo 30 ndiyo mwisho wa kazi zao maeneo hayo.Amewaagiza kuhakikisha vijiji vyote na vitongoji vinapata umeme,amesema kisirukwe kijiji hata kimoja bila kupata umeme na utekelezaji ufanyike chini ya uangalizi wa mwenyekiti wa kijiji husika na kitongoji. 

Dkt.Kalemani amemtaka Meneja wa mkoa wa Tanesco Mhandisi Herini Mhina kuhakikisha anatatua malalamiko ya kukatika kwa umeme katika Jiji la Arusha mara kwa mara na kuhakikisha kila wilaya umeme unafika nyumba hadi nyumba.Pia aliagiza Wakandarasi hao kuajiri vibarua wasiopungua 60 ili kazi niende kwa haraka na wakati huo watasaidia Serikali kuboresha maisha ya wananchi.

"Serikali imewalipa na nyie waajiri watu wa maeneo haya na muwalipe ili kuboresha maisha yao,"alisema.Kuhusu nguzo kutoza wananchi gharama alipiga marufuku kwa kampuni hiyo na Mameneja wa Tanesco kusimamia hilo.Mrisho Gambo ni Mkuu wa mkoa wa Arusha amesema kuwa tangia kupata uhuru wilaya ya ngorongoro haijawahi kuwa na hospitali ya wilaya ila sasa inajengwa ambapo mil.400 zimetengwa kwaajili hiyo,barabara kiwango cha lami kwa sasa imeanzwa kutengenezwa km 50 ikiwa itekelezaji wa majukumu ya serikali ya awamu ya tano.

Gambo amewataka wananchi waweze kutandaza nyaya kwenye nyumba zao ili wapate huduma ya umeme kwa bei nafuu ya elfu 27 kwani wakichelewa watakuja kufungiwa kwa bei kubwa zaidi.

Naye Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Willium Ole Nasha ameishukuru Serikali kupeleka umeme Ngorongoro na kuzindua rasmikwani katika kipindi cha Serikali ya sasa imejitahidi kupeleka maendeleo mengi katika Wilaya hiyo ambayo hawajawahi kutekelezwa tangu Uhuru kupatikana.

Amesema katika hali ya kawaida Ngorongoro hawakuwahi kufikiria kama watapata umeme.hivyo yeye kama mbunge wao anewataka wananchi hao kujitahidi kutumia umeme huo kujiletea maendeleo.Kwa upande wake Ambilikile Mwasapila (Babu wa Kikombe) alishukuru Serikali kumwashia umeme nyumbani kwake."Lakini hii ishara ya kutimia kwa ndoto zake anayoonyeshwa na Mungu kila mara kuwa Tanzania ni kioo cha Afrika sasa hizi ndizo ishara zimeanza kuonekana,"alisema.

Mbali na kuwasha umeme nyumbani kwa Babu wa kikombe,pia aliwasha Kituo cha Afya Digodigo,Shule ya Msingi Bisikene iliyopo Kata ya Digodigo na Ofisi ya Afisa Tarafa Digodigo

DC MBONEKO AMWAGA VIFAA VYA SHULE KWA WATOTO WENYE UALBINO BUHANGIJA

$
0
0

Na Marco Maduhu - Malunde1 blog Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, ametoa msaada wa vifaa vya shule kwenye kituo cha kulea watoto wenye ulemavu ualbino Buhangija Jumuishi kilichopo manispaa ya Shinyanga, kwa ajili ya kuwapatia hamasa ya kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao.

Mboneko ametoa msaada huo leo Mei 25, 2019 akiongozana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, pamoja na Ofisa Maendeleo ya Jamii manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone, kwa kutoa msaada huo wa vifaa vya shule kwa watoto hao.

Amesema msaada wa vifaa hivyo vya shule ameshirikiana na marafiki zake wa Kikundi Cha Computer Digital Women cha Jijini Dar es salaam, ambapo wameguswa na watoto hao wenye ualbino, na kuamua kuwasaidia vifaa hivyo,ili kutoa hamasa kwao ya kusoma kwa bidii.

“Vifaa hivi vya Shule nimeshirikiana na marafiki zangu wa kikundi cha Computer Digital Women cha jijini Dar es salaam, ambapo wameguswa na ninyi na kuamua kuwasaidia ili msome kwa bidii na kutimiza ndoto zenu,”alisema Mboneko.“Vifaa vya shule ambavyo nitawapatia ni madaftari, Counter Book, kalamu za penseli na wino, vifutio, vichongeo, rula, soksi, nguo za ndani kwa watoto wa kike na wa kiume, pamoja na zawadi zingine kama pipi na biskuti,” aliongeza.

Pia aliwapongeza walezi wa kituo hicho kwa kwahudumia watoto hao vizuri na kuwalea kama watoto wao, huku akiwataka waendelea kuboresha hali ya usafi kituoni hapo ili kuwaepusha na magonjwa ya mlipuko.Naye mkuu wa kituo cha Polisi Shinyanga Mjini (OCS) Grace Salia, aliwahakikisha ulinzi na usalama watoto hao kwenye kituo hicho, ambapo siku zote wamekuwa wakilindwa na askari.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Buhangija Seleman Kipanya ambaye ndiye mlezi mkuu wa kituo hicho, akizungumza kwa niaba ya watoto hao alimpongeza mkuu huyo wa wilaya kwa kutoa vifaa hivyo vya shule pamoja na marafiki zake, ambavyo vitawasaidia katika masomo yao.

Alitaja jumla ya watoto ambao wanalelewa kwenye kituo hicho kuwa wapo 230, wasiosikia 74,Wasioona 36, pamoja na wenye ualbino 140 ambao ndiyo wengi zaidi, na kutoa wito kwa wadau wengine kuendelea kujitokeza ili kuwatatulia baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwataka watoto wenye ualbino wanaolelewa kwenye kituo cha Buhanghija Jumuishi Shinyanga Mjini wasome kwa bidii ili kutimiza Ndoto zao. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Askari Alphonce Bandya (ASP) kwa niaba ya Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga (RPC) Richard Abwao, akiwasisitiza watoto hao kupenda sana elimu ambayo ndiyo itakuwa mkombozi wa maisha yao.
Mkuu wa kituo cha Polisi Shinyanga Mjini (OCS) Grace Salia, akiwahakikisha ulinzi na usalama watoto hao wenye ualbino.
Watoto wenye Ualbino wakisikiliza nasaha za viongozi juu ya kusoma kwa bidiii.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule kwa watoto wenye Ualbino.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule kwa watoto wenye Ualbino.
Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akigawa vifaa vya Shule kwa watoto wenye Ualbino.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akigawa vifaa vya shule kwa watoto wenye Ualbino.
Zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule likiendelea kwa watoto hao wenye Ualbino.
Watoto wenye Ualbino wakionyesha vifaa vya Shule ambavyo wamepewa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Watoto wenye Ualbino wakionyesha Soksi kwa ajili ya kuvalia kwenye viatu vya shuleni.
Muonekano wa vifaa vya shule.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwaaga watoto hao wenye Ualbino mara baada ya kumaliza kutoa zawadi ya vifaa vya Shule na kuahidi Serikali itaendelea kuwa nao pamoja katika kuwatatulia changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili.
Mwalimu mkuu wa Shule ya Buhanghija Selemani Kipanya ambaye pia ndiye mlezi mkuu wa watoto hao wenye Ualbino akishukuru kwa msaada huo wa vifaa vya shule ambavyo vitawasaidia watoto hao katika masomo yao.Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

PROF. MCHOME AKAGUA UTOAJI WA MSAADA WA KISHERIA MKOANI SINGIDA

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Prof.Sifuni Mchome akitia saini kitabu cha wageni kaoka Ofisi ya Katibu Tawala mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi aliekaa mbele akimuangalia.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Prof.Sifuni Mchome akiangalia Moja ya machapisho ambayo yapo katika KITUO Cha msaada wa sheria Singida alipokitembelea kituo kwa ukaguzi.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Prof.Sifuni Mchome akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa kituo cha msaada wa sheria Singida alipokitembelea kituo hicho kwa ukaguzi.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Prof.Sifuni Mchome akiwa katika picha ya pamoja na watoa huduma ya msaada wa sheria mkoani Singida alipokuwa mkoani humo kwa ziara ya ukaguzi.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Prof.Sifuni Mchome akizungumza na watendaji wa KITUO Cha msaada wa sheria Singida juu ya huduma za msaada wa sheria kwa wannachi alipofika kuangalia eneo wanalotumia kutoa msaada huo kwa wananchi.

*************************************************

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome atembelea mkoa wa Singida kukagua utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi. Prof Mchome yuko katika ziara ya ukaguzi wa huduma na maeneo yanayotolewa msaada wa kisheria ili kuona kama inaendana na matakwa ya Sheria ya Msaada wa Kisheria No 1. ya 2017.

Katika ziara hiyo Prof. Mchome ambaye ameambatana na Msajili wa Watoa Msaada wa Kisheria nchini bibi Felistas Mushi, amezungumza na wanufaika wa huduma ya msaada wa kisheria katika mkoa wa Singida ambao wameelezea kuridhishwa kwako na huduma hiyo ambayo wamesema imewezesha kutatua matatizo yaliyokuwa yakiwakabili na hivyo kupata haki zao.

Ziara hiyo ya ukaguzi ni utekelezaji wa Sheria ya Msaada wa Kisheria No.1 ya 2017 ambayo inamtaka msimamizi wake kuvitembelea vituo vinavyotoa huduma ya msaada wa kisheria ili kuona maeneo wanakotolea huduma na aina ya huduma wanayoitoa kwa mujibu wa sheria hiyo.

Akizungumza na watoa msaada kutoka wilaya za Singida, Iramba, Mkalama Prof. Mchome amewataka kuzingatia kuwa msaada wa kisheria ni huduma muhimu ambayo wananchi wanahitaji kupewa kwa kuwa sio kila mwananchi anao ufahamu wa sheria.

Amewataka kuhakikisha wanatoa msaada wa kisheria ili kuwawezesha wananchi kutatua matatizo yanayowakabili na hivyo kuokoa muda ambao wangeutumia kujishughulisha kwa ajili ya maendeleoyao na taifa kwa ujumla.

Amesema matatizo mengi yanatatuliwa na sheria mbalimbali na ndio maana mtu akipata mtaalamu wa sheria anakuwa amepata njia sahihi na salama ya kutatua tatizo lake na kuokoa muda kwani atakuwa amerahisisha mambo mengi.

“Sheria ni kama uzio ambao una milango inayotakiwa kufunguliwa ili kuweza kujua njia sahihi ya kupita na kupitia msaada wa kisheria mtaweza kuwaonyesha njia sahihi wananchi wenye shida na hivyo kutatua matatizo yao,” alisema Prof. Mchome na kuongeza kuwa sheria zikitumiwa vizuri huleta jamii zenye amani na furaha nakufanya jamii hizo kupata maendeleo.

WALIMU WA SHULE YA WASIOONA BUIGIRI WAPATIWA MAFUNZO YA HEDHI SALAMA

$
0
0
Baadhi ya washiriki ambao ni walemavu wasioona wanaohudhuria mafunzo ya hedhi salama kwa watoto wa kike na makundi maalum ya walemavu, mafunzo hayo yanaendeshwa na Shirika la Kimataifa la Water Supplies Corraboration Council katika Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma. 


Jamii imetakiwa kuchukua hatua ikiwemo ya kutoa elimu sahihi katika makundi mbalimbali ikiwemo ya walemavu wa aina zote hususan wasioona. 

Hayo yamesemwa leo na muelimishaji mwandamizi wa masuala ya hedhi salama Bi.Dhahia Mbaga kutoka shirika la kimataifa la Water Suppliers Sanitation Corraborative Council wakati wa mafunzo kwa walimu na walezi wa shule maalum ya watoto wasioona ya Buigiri iliyopo wilayani hapa katika kuelekea maadhimisho ya siku ya hedhi salama duniani. 

Bi.Mongi amesema malengo ya mafunzo hayo ni kuongeza maarifa na kuweka mazingira rafiki kwenye vyoo ambapo vinatakiwa kuwa na usafi, maji yanayotiririka pamoja na chumba maalumu kwa ajili ya watoto wanaopevuka kwa kubadilisha vifaa vya hedhi. 

Aidha, amesema katika chumba maalum kunatakiwa kuwe na sanduku la huduma ya kwanza ambayo itakua na dawa za kutuliza maumivu pindi wanapopata maumivu kutokana na hedhi. Pia Bi. Mbaga amesema wanaokuwa na maumivu makali wanatakiwa wapelekwe kwenye kituo cha huduma za afya kupata matibabu. 

Hata hivyo aliongeza kuwa kufika katika shule hiyo ni pamoja na kuibua changamoto za hedhi salama kwani ni nyingi. ”kwani tunapokuwa na watoto waliopevuka na wenye ulemavu kunakuwa na changamoto nyingi zikiwemo za kuwa na vyoo vyenye kuwawezesha walemavu wa macho ambapo kuna ujenzi maalumu ambayo imeanishwa kwenye miongozo ya kitaifa ya shule kwenye masuala ya maji na masuala ya mazingira”. Alisisitiza Mbaga. 

Vilevile alisema mafunzo katika shule hiyo watawafundisha walimu na wanafunzi kuweza kutengeneza taulo za kike kwa kutumia vifaa ambavyo vinapatikana katika eneo hilo na kwa bei rahisi. 

Kwa upande wa unyanyapaa muelimishaji huyo alisema kuwa linakuja kutokuwa na taarifa sahihi hususani kwa wanaume kwani wanapaswa kujua ni jambo la kawaida na wapo baadhi ya wanaume hawana taarifa sahihi kwani na wanaume nao wanapevuka kwahiyo hayo ni mabadiliko ambayo hayawezi kuzuiliwa. 

Maadhimisho ya siku ya hedhi salama duniani mwaka huu kitaifa yanatarajiwa kufanyika jijini Dodoma tarehe 28 mwezi Mei na kauli mbiu ya maadhimisho hayo “Ni wakati wa kuchukua hatua ili kuhakikisha hedhi salama kwa msichana/mwanamke”.

NAMBA ZA SIMU KUHUSU KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI

SHERIA YA MSAADA WA SHERIA IMETUNGWA KUWATAMBUA WASAIDIZI WA SHERIA NCHINI

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Sifuni Mchome akiangalia moja ya machapisho aliyoyakuta katika kituo cha msaada wa sheria cha NILIKO Cha mkoani Geita alipofanya ziara ya ukaguzi wa watoa msaada wa sheria mkoani humo. 
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Sifuni Mchome akipokea taarifa ya utoaji msaada wa sheria mkoani Geita kutoka kwa Mona ya taasisi zinazotoa msaada wa sheria kwa wananchi mkoani Geita. 
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Sifuni Mchome akizungumza na watoa msaada wa sheria mkoani Geita. 
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Sifuni Mchome katika picha ya pamoja na watoa msaada wa sheria kwa wananchi mkoani Geita

………………… 
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Sifuni Mchome amewataka wasaidizi wa sheria nchini kufanya kazi zao kwa umakini kwa kuwa wanatambulika kwa mujibu wa Sheria ya Msaada wa Sheria No.1 ya 2017. 

Prof.Mchome ametoa kauli hiyo mjini Geita alipokutana na wasaidizi wa sheria wanaotoa huduma ya msaada wa sheria kwa wananchi mkoani Geita ambako yuko katika ziara ya kuangalia kama utoaji wa msaada wa sheria unaendana na matakwa ya Sheria ya Msaada wa Sheria ya mwaka 2017. 

“Sheria ya Msaada wa Sheria No.1 ya 2017 ilitungwa rasmi ili kuwatambua wasaidizi wa sheria, sasa ni jukumu lenu kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi kwani mnatambulika kisheria”,alisema Prof.Mchome. 

Amewataka kufanya kazi iliyokusudiwa na kutokujiingiza katika siasa na uanaharakati kwakuwa sheria ni msumeno na haiangalii itikadi, dini , jinsia ,sura wala rangi. 

Amesema utoaji sahihi wa msaada wa sheria kwa wananchi ukizingatiwa kikamilifu utatoa nafuu kwa wananchi na hivyo kupata jamii salama na kujiletea maendeleo.

NYONGO ASHUHUDIA JIWE LA ALMASI LA UZITO WA “CT” 512.15 LIKIUZWA KWA BILION 3, 262, 149, 332

$
0
0
Naibu waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akionyesha jiwe la madini ya Almasi lenye uzito wa “ct” 512.15 leneye thamani Tsh. Bilion 3, 262, 149, 332.75 mali ya mchimbaji mdogo bwana Joseph mkazi wa Shinyanga. Kushoto kwake ni Kamishna wa Madini Prof. Mruma na kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko. 
Kamishna wa Tume ya Madini Prof. Mruma akimuonyesha jambo Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo jiwe la madini ya Almasi lenye uzito wa “ct” 512.15 leneye thamani Tsh. Bilion 3, 262, 149, 332.75 wakati wa mauzo yake yaliyofanyika katika soko la Madini la mkoa wa Shinyanga. 
Bi. Dorcas Moshi, Mchambuzi na Mthamini wa Madini ya Vito na Almasi kutoka tume ya Madini akiifunga rasmi Almasi ya Josephy Temela mara baada ya kukamilika kwa taratibu za uthaminishaji na kupata ghara halisi huku ikishuhudiwa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo mwenye suti ya Blue. 
Bw. Joseph Temba mchimbaji mdogo ambae ameuza jiwe lake la madini ya Almasi lenye uzito wa “ct” 512.15 leneye thamani ya Tsh. Bilion 3, 262, 149, 332.75 wakati wa mauzo yake yaliyofanyika katika soko la Madini la mkoa wa Shinyanga. 


Na: Issa Mtuwa (Wizara ya Madini) – Shinyanga 

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, ameshuhudia mchimbaji
mdogo wa madini ya almasi bwana Joseph akijizolea fedha, dola za
kimarekani (USD) milioni 1, 418,510.82 ambazo sawa na Tsh. bilioni 3,
262,149,332.75 kutokana na mauzo ya jiwe moja lenye uzito wa Kareti
(ct)512.15. Shuguli ya mauzo ya Almas hiyo imefanyika leo tarehe
25/05/2019 katika soko la Madini la mkoa wa Shinyanga na kushuhudiwa
pia na Kamishna wa Tume ya Madini Prof. Mruma na vyombo mbalimbali
vya usalama na wawakilishi wa benki ya CRDB Shinyangai. 

Akiongea wakati wa kushuhudia mauzo hayo , Naibu waziri Nyongo
amesema, kutokana na mauzo hayo serikali itapata USD 103,551.29 sawa
na Tsh. milioni 238,136,901.61. Ameongeza na kusisitiza kuwa, adhima ya
serikali ya awamu ya tano ni kuwezesha shuguli za wachimbaji wadogo na
wadau wote wa sekta ya madini kufanyika kwa utaratibu unao eleweka
kwa faida yao na ya serikali. 

“Nimpongeze bwana Joseph ambae anauza almasi yake hapa leo kwenye
soko hili la madini, kila kitu kinakuwa wazi mbele ya serikali, polisi, watu wa
usalama na wawakilishi wa Bank ya CRDB, bila usumbufu wowote, na hiki
ndicho tunachokitaka sisi kama serikali, wachimbaji wote kufuata utaratibu
tuliouweka.

Niwaombe wachimbaji kwa mara nyingine, acheni kuuza madini
mchochoroni haita wasaidia zaidi ni kuhatarisha usalama wenu, na pengine
hata kupunjwa kutokana na kuto kujua thamani halisi na bei ya madini yenu
igeni mfano wa bwana Joseph, na niwaambie ukweli ukikamatwa unauza
madini nje ya soko madini hayo yanataifishwa, hivyo utakuwa umekula
hasara na utachukuliwa hatua za kisheria.” amesema Nyongo. 

Kwa upande wake Afisa msaminishaji madini kutoka tume ya Madini Bi.
Dorcas Moshi, Mchambuzi na Mthamini wa Madini ya Vito na Almasi
kutoka tume ya Madini aliekuwa anafanya shuguli nzima ya uthaminishaji
wa Almasi hiyo, amefafanua kuwa fedha iliyopata serikali, Milioni
238,136,901.61 inajumuisha Mrabaha wa USD 85,110.65 sawa na Tsh.
Milioni 195,728,959.97, Ada ya ukaguzi ni USD 14,185.11 sawa na Tshs.
32, 621, 493, .33 na Mrabaha wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu ilikotokea Almasi hiyo (Service Levy) ni USD 4,255.53 sawa na Tsh. 9,
786,448. 

Kwa upande wake Kamishina wa Madini prof. Mruma amewasisitiza
wachimbaji wadogo kuzingatia sheria na taratibu hususani kuchimba
kihalali kwa kuhakikisha wanakuwa na leseni za uchimbaji na kulipa tozo
zote za serikali kwani serikali ipo kwa ajili yao hivyo hawana sababu ya
kuikwepa. 

Kwa upande wake bwana Joseph mmiliki wa almasi hiyo, ameishukuru
Wizara ya madini na Tume ya madini kwa utaratibu waliouweka katika
kutoa muongozo na usimamizi wa namna ya mauzo ya madini
unavyotakiwa kufanyika, ulinzi wa madini yao pindi wanapoyapata na
ametoa wito kwa wachimbaji wadogo wenzake kuwa hakuna sababu ya
kuyakimbia masoko yaliyoanzishwa na serikali kwani yanafaida nyingi
ikiwemo usalama, ulinzi, uwazi na utambuzi wa thamani halisi ya madini
kitu ambacho nadra sana kwenye masoko yasiyo rasmi.

BABU WA LOLIONDO AUNGANISHWA NA UMEME WA REA

$
0
0


Na Ahmed Mahmoud Ngorongoro

MCHUNGAJI mstaafu wa kanisa la KKKT, ambae kwa sasa anatoa huduma ya matibabu ,Ambilikile Mwaisapile, ameipongeza serikali kwa kuwasha umeme nyumbani kwake na kusema kuwa sasa amepata mwanga atafanya kazi zake hata nyakati za usiku tofauti na hali ilivyokuwa kabla ya kupata umeme.

Mchungaji Mwaisapile maarufu babu Kikombe wa Samunge, wilayani Ngorongoro,ameyasema hayo jana nyumbani kwake mara baada ya waziri wa Nishati Dakta Medadi Kalemani, kuwasha umeme wa REA nyumbani kwake.

Mwaisapile, amesema hakutegemea kama kuna siku angelipata Umeme lakini sasa ameishukuru serikali kwa kumuwashia umeme wa Rea, nyumbani kwake.

Amesema kutokana na serikali kutekeleza miradi ya umeme Vijiji Tanzania itakuwa ni kioo cha maendeleo barani Afrika.

Akizindua na kuwasha umeme huo Waziri wa Nishati,Dakta Kalemani, amesema serikali ipo katika kutekleza miradi ya umeme vijijini kupitia REA,na kurejea maelekezo yake kwa wakandarasi kuhakikisha hakuna Kitongoji ,Kijiji,Kata ambayo nyumba haitapata umeme hata kama ipo chini ya miti lazima ipatiwe umeme.

Amesema Mwaisapile ameitangaza Samunge na Tanzania Ulimwenguni kutokana na tiba yake kwa watu mbalimbali ambao huwa wanafika nyumbani kwake kupnywa kikombe cha dawa.

Amesema mradi huo wa umeme wa REA ulofungwa nyumbani kwa Mwaisapile,unatokea kijiji cha Wasso,wilayani Ngorongoro umbali wa kilometa 335 .

Amewahakikishia wananchi wilayani Ngorongoro kuwa kila mmoja atapata umeme nyumbani kwake kabla ya Desema 30 mwakani.

Ametoa muda wa mwezi mmoja kwa Mkandarasi wa umeme wa REA kampuni ya Nipoco, kuhakikisha Vijiji na Vitongoji vyote wilayani humo vinapata umeme huo wa REA bila kusahau au kuacha au kuruka nyumba hata moja.

Ameongeza kuwa mwisho wa wakandarasi nchini kusambaza umeme Vijijini nchini kote ni Desemba 31 mwaka huu kulingana na mikataba yao hivyo lazima waongeze kasi ya usambazaji umeme.

Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Ngorongoro Willium ole Nasha, ameipongeza serikali kwa mafankio hayo ya kusambaza umeme vijijini katika kipindi cha miaka mitatu na kuiwezesha wilaya hiyo katika kipindi hicho kuwa na maendeleo makubwa .

Nasha,ambae pia ni Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia,amesema kutokana na kupatikana kwa umeme tayari serikali imeshatoa shilingi milioni 800 kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha ufundi VETA, na kitaanza rasmi Augosti mwaka huu .

MRADI WA BOMBA LA KUSAFIRISHA MAFUTA GHAFI KUTOKA UGANDA KUNUFAISHA VIJIJI LITAKAPOPITA

$
0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizindua mpango wa natumizi bora ya ardhi kwa viijiji 226 vinavyopitiwa na Bomba la Mafuta katika kijiji cha Sojo kata ya Igusule wilaya ya Nzega mkoani Tabora, kulia kwa Lukuvi ni Naibu Waziri Nishati Subira Mgalu. 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi , Naibu Waziri Nishati Subira Mgalu na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri wakicheza ngoma wakati wa uzindizi mpango wa natumizi bora ya ardhi kwa viijiji 226 vinavyopitiwa na Bomba la Mafuta katika kijiji cha Sojo kata ya Igusule wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Picha na Wizara ya ardhi. 

**************************************** 

Na Munir Shemweta, NZEGA 

Wananchi wanaoishi vijiji linakopita Bomba la kusafirisha Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanzania sasa watanufaika na mradi huo kufuatia Serikali kutangaza mradi wa kupanga matumizi bora ya ardhi katika vijiji 226 linapopita bomba hilo. 

Aidha, ilielezwa kuwa wakati wa utekelezaji mradi wa kupanga matumizi bora ya ardhi mwananchi hawatatozwa gharama yoyote na wale ambao maeneo yao yametwaliwa watalipwa fidia. 

Hayo yalibainishwa tarehe 25 Mei 2019 katika kijiji cha Sojo kata ya Igusule wilaya ya Nzega mkoani Tabora na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi wakati wa uzinduzi Mradi wa Upangaji Matumizi bora ya Ardhi katika vijiji vinavyopitiwa na bomba la kusafirisha Mafuta ghafi -EACOP alipozungumza na wananchi wa kijiji hicho kuwaelezea mpango wa Wizara yake kupanga matumizi bora ya ardhi ili kuendana na fursa za kiuchumi. 

” Vijiji vyote 226 ambavyo Bomba la Mafuta linapita ardhi yao itafanyiwa matumizi bora ya ardhi ili kutoa fursa za kiuchumi kwa wananchi wanaoishi katika vijiji hivyo” alisema Lukuvi. 

Akiwa na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu na baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi na Maliasili Waziri Lukuvi alisema, uzinduzi uliofanyika ni kwa niaba ya vijiii 226 na wilaya 24 zilizoko katika mikoa nane inapopita bomba hilo na kubainisha kuwa fedha kwa ajili ya mpango huo zishatengwa. 

Waziri Lukuvi alitoa onyo kwa wananchi watakaojipenyeza au kufanya maendelezo katika eneo la ekari 144 lililotwaliwa na serikali na kusema tayari picha ya anga imechukuliwa katika eneo lote litakalojengwa kituo wezeshi cha kuunganisha mabomba ya mradi. 

Kwa mijibu wa Lukuvi, mradi wa upangaji matumizi ya ardhi katika viiji vinavyopitiwa na bomba la mafuta utakuwa shirikishi kwa kuwahusisha wananchi wanaoishi maeneo hayo. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi Dkt Stephen Nindi alisema kazi ya upangaji matumizi bora ya ardhi imeanza katika vijiji, miji na miji midogo inayopitiwa na bomba la kusafirisha mafuta ghafi ambapo kazi hiyo imeanza katika wilaya 13 kati ya 24 zilizopangwa kufanyiwa matumizi bora ya ardhi. 

Kwa mujibu wa Dkt. Nindi uandaji mpango wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji hivyo unafanyika kwa sababu kuna fursa na kuanisha kuwa katika kijii cha Sojo pekee kiasi cha bilioni 600 zitawekezwa kwa kuwa kituo katika kijiji hicho itakuwa kituo kikuu cha kuunganisha mabomba na hivyo kutoa fursa za kiuchumi na kijamii hivyo wananchi wajiandae namna warakavyobua fursa. 

Aidha, alisema upangaji matumizi bora ya ardhi utasaidia kuepuka migogoro ya ardhi ambapo kwa kiasi kikubwa mradi huo utahusisha wananchi na kusaidia ulinzi na usimamizi wa bomba la mafuta sambamba kulinda maeneo yenye rasilimali kama misitu na maeneo Oevu. 

Meneja wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha Mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanzania Martin Tiffen alisema kazi kubwa ya kuunganisha mabomba ya mradi itafanyika kwa lengo la kupunguza joto itafanyika katika kijiji hicho na kubainisha kuwa mradi huo utaboresha miundombinu ya barabara ili wananchi wanufaike. 

Bomba la kusafirisha mafuta ghafi kwa upande wa Tanzania litapita katika mikoa nane ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Manyara, Dodoma na Tanga sambamba na kujumuisha wilaya 24 na vijiji 226 ambapo vijiji 30 viko katika mkoa wa Tabora.

SIKU YA AFRIKA YAADHIMISHWA KWA VIJANA KUPATA SOMO KUTOKA KWA WAZEE

$
0
0
* Rais Magufuli atawala mdahalo apewa sifa katika kuongoza mapambano ya kiuchumi

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MAADHIMISHO ya siku ya Afrika yanayoadhimishwa kila tarehe 25 mwezi Mei, kwa mwaka huu yameadhimishwa kwa jukwaa la tafakuri lenye kauli mbiu ya "Uafrika wetu na rasilimali za Bara letu ni urithi wetu" huku vijana wakipata somo kutoka kwa wazee na wapigania uhuru wa taifa.

Akizungumza katika tafakuri  hiyo ya pili Waziri wa Habari, sanaa, vijana utamaduni na michezo Dkt. Harison Mwakyembe amesema kuwa viongozi wa Afrika watakumbukwa kwa mengi waliyoyafanya pamoja na juhudi na jitihada walizozifanya zitaishi daima na kumbukumbu zao zitahifadhiwa daima na hadi sasa  zaidi ya kumbukumbu 256 zimehifadhiwa na amewataka vijana kujifunza kutoka kwa watetezi hao.

Mwakyembe amesema kuwa wao kama wizara wataendelea kuhifadhi mazuri yote yaliyofanywa pamoja na kuyaendeleza na hiyo ni pamoja na kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa Lugha inayounganisha bara la Afrika.

Aidha amesema kuwa vijana lazima wawe nguzo imara na wazalendo katika kuhakikisha rasilimali zinanufaisha jamii za kiafrika.

Akizungumza katika halfa hiyo Mkurugenzi mtendaji mkuu wa makampuni ya Uhuru ambao ni waandaaji wa jukwaa hilo Ernest Sungura amesema kuwa imepita miaka 56 tangu nchi za Afrika kujikomboa na ni muhimu sana kwa vijana kurithi mawazo na fikra pana kutoka kwa wazee na watetezi wa taifa.

Amesema kuwa baada ya kujikwamua kisiasa sasa ni wakati wa kujikwamua kiuchumi ambapo Rais wa awamu ya tano Rais Dkt.John Magufuli anaonesha nguvu na nia ya kujikomboa kiuchumi, amesema kuwa Rais Magufuli atakumbukwa na kushukuriwa daima kwa uthubutu na ujasiri wake katika kupambana na masuala yanayokwamisha kukua kwa uchumi ikiwemo kupinga ufisadi, rushwa na ulevi wa madaraka.

Sungura amesema kuwa  kupitia jukwaa hilo matokeo yanayotarajiwa na pamoja na kuona uhifadhi wa historia, tamaduni na rasilimali, ukombozi wa kisiasa na kiuchumi katika zama hizi mpya pamoja na kulinda haki na usawa hasa kwa wanyonge.

Kwa upande mwenyekiti mstaafu wa Bunge la Afrika Mashariki, Getrude Mongella amesema kuwa jambo linalofanya Afrika kubaki tegemezi hasa kwa wanawake ni kwamba; wanaume waliopewa jukumu la kuongoza Afrika walituangusha hivyo vijana wa sasa wawe shupavu ili kuwatoa wanaafrika kutoka sehemu moja kwenda yenye matumaini zaidi.

Getrude amesema kuwa huu ni wakati wa kazi tuu na sio  wakati wa kuoneshana vidole bali wakae na kufikiri ni wapi pamekwama pamoja na kujitambua na kujituma katika kutumia rasilimali katika kujikwamua kiuchumi.

 Mwenyekiti wa kigoda cha Mwalimu Nyerere Profesa. Rwekaza Mukandala amesema kuwa historia ya siku hiyo ya Afrika  ni muhimu kwa vijana katika kurithi yaliyo mema kutoka kwa wazee na hasa uzalendo na ushujaa katika kuleta maendeleo.

Mukandala amesema kuwa mwaka 1963 tarehe kama ya leo takribani nchi 32 zilikuwa huru na ndipo umoja wa nchi huru za Afrika(OAU) ulianzishwa.

Mukandala amesema kuwa mapambano ya kisiasa yalipita na kwa sasa hatuna budi kutumia rasilimali zetu ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kujitegemea kupitia uchumi wetu.

Kwa upande wake balozi mstaafu Christopher Liundi amesema kuwa uzalendo hasa kwa vijana ni lazima kuzingatia elimu za aina tatu zikiwemo elimu kutoka nyumbani, elimu ya darasani na elimu dunia, amesema kuwa malezi bora huanzia nyumbani na ndio huzaa uzalendo.

Amesema kuwa vijana lazima wasome ili waweze kutofautisha mazuri na mabaya pamoja na kulitumikia taifa kwa moyo wote.

Aidha imeelezwa kuwa kitu kinachokwamisha muunganiko huo wa Afrika ni pamoja na ulafi wa madaraka na ubinafsi huku Tanzania ikitolewa mfano kwa kuwa nchi inayofuata misingi ya demokrasia na uongozi.
 Waziri wa habari, sanaa, vijana, utamaduni na michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza katika jukwaa la tafakuri katika maadhimisho ya siku ya Afrika duniani ambapo amewataka vijana kujituma na kuwa wazalendo katika kuhakikisha rasilimali zinalindwa na kutumika ipasavyo, leo jijini Dar es Salaam.

 Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda akitoa majumuisho ya mdahalo huo ambapo ameeleza kuwa hakuna budi kudhibiti rasilimali za asili kwa umakini na kuweka sera elekezi za biashara katika rasilimali hizo, leo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Misri Nchini Tanzania Gaber Mohamed akitoa neno katika mjadala huo, amehimiza umoja na mshikamano miongoni mwa nchi za Afrika, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi mtendaji mkuu wa makampuni ya Uhuru Media ambao pia ni waandaaji wa jukwaa hilo Ernest Sungura akizungumza wakati wa jukwaa hilo na kusema kuwa wanategemea matokeo chanya na ya kujenga kupitia mdahalo huo, leo jijini Dar es Salaam.
 Balozi mstaafu Christopher Liundi akichangia mada katika jukwaa hilo, Balozi Liundi amesema kuwa malezi bora yanajenga uzalendo na kuwataka vijana  kujituma katika kazi, leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa magazeti ya serikali Zanzibar Mahfoudha Hamid akichangia mada katika mjadala huo, leo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti mstaafu wa bunge la Afrika Mashariki Getrude Mongella akichangia mada katika jukwaa hilo ambapo amewataka vijana kuwa wazalendo na kubeba taifa kuelekea mafanikio, leo jijini Dar es Salaam.











 Baadhi ya mabalozi pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia mada

TVP, UNICEF NA WIZARA YA AFYA ZAHITIMISHA SEMINA ZA ‘JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA’ KWA WADAU WA JAMII

$
0
0

Semina tatu zilizoandaliwa na Kampuni ya True Vision Production (TVP) kwa kushirikiana na UNICEF Tanzania na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto za kampeni ya ‘Jiongeze Tuwavushe Salama’ kwa wahariri, viongozi wa dini na waandishi wa habari zimemalizika katika Hotel ya Regency, jijini Dar es Salaam.

Semina hizo zilikuwa na lengo la kuelimisha makundi haya matatu (wahariri, viongozi wa dini na waandishi) juu ya umuhimu wao wa kushiriki katika kampeni ya ‘Jiongeze Tuwavushe Salama’ yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto. Tahseen Alam, Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka UNICEF Tanzania amesema serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau imekuwa ikifanya jitihada kubwa katika miaka 10 iliyopita ya kuokoa vifo vya mama na mtoto, ikiwemo eneo la chanjo ambapo watoto wengi na mama wajawazito wanapatiwa.

Lakini kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Mtaalamu wa Mawasiliano mwenzake kutoka UNICEF, Usia Nkoma, Tanzania bado ina safari ndefu ya kutokomeza vifo hivyo kwa sababu ni nchi ya tisa kati ya nchi 10 duniani zinazoongoza kwa vifo vya mama wajawazito na watoto.
Takwimu zinaonyesha mama wajawazito wasiopungua 6000 (wastani 8,000)  wanakufa kila mwaka wakati wanajifungua, sawa na wanawake 556 kwa kila vizazi hai 100,000.

Pia asilimia 50 ya watoto walio chini ya miaka mitano (5) pia wanakufa ndani ya mwezi mmoja baada ya kuzaliwa, asilimia 40 kati ya hawa wakiwa watoto wachanga. Wakizungumza tofauti tofauti katika semina hizi, mmoja wa waandishi na wahariri wakongwe nchini, Theophil Makunga amasema takwimu hizi zinatisha, hivyo kuna haja kwa wahariri kuzipa kipaumbele habari zinazohusu wanawake wajawazito na watoto ili kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kuchukua hatua kupunguza vifo hivi.

Naye Sheikh Hamid Jongo wa msikiti wa Manyema amesema kuna haja ya kuwafunda watumishi wa afya , kwani baadhi yao inasemekana hawana lugha rafiki kwa wagonjwa. Kauli yake imeungwa mkono na Christosiler Kalata, mchungaji kutoka KKKT, Dayosisi ya Mashariki na Pwani, ambaye amehimiza wahudumu wa Afya kuzingatia miiko ya taaluma yao  ili kuhakikisha vifo vya mama wajawazito na watoto vinaisha.

“Tutahakikisha, kama waandishi wa habari tunabadili mtazamo wa kazi zetu kwa kuzipa kipaumbele habari zinazohusu afya ya mama wajawazito na watoto, kama ilivyo kwa habari nyingine,” amesema Tumaini Msowoya, kutoka gazeti la Mwananchi.

Washiriki wote wa semina hizi tatu wameishukuru kampuni ya True Vision Production, UNICEF Tanzania na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kwa kuhakikisha kampeni ya ‘Jiongeze Tuwavushe Salama’ inafanikiwa, kwani jukumu la kupunguza vifo na kila mmoja katika jamii.

Kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama ni kampeni ya Taifa, iliyozinduliwa na Makamu wa Rais, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan mjini Dodoma, mwezi Novemba mwaka, ukiwa ni mwongozo kutoka Wizara ya Afya kwa wakuu wote wa mikoa Tanzania Bara kuchukua hatua za kuzuia vifo vya mama na mtoto katika mikoa yao.

Madhumuni ya Serikali ni kuhamasisha viongozi wake, viongozi wa dini, mashirika yasiyo ya serikali, wadau wa maendeleo, watoa huduma za afya, familia na jamii kwa ujumla kuanza kuchukua hatua za kuzuia vifo hivyo.
 Mtaalam wa Mawasiliano kutoka UNICEF, Tahseen Alam akitoa mada katika semina ya kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama
 Kaimu Mratibu wa Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto mkoa wa Dar es Salaam, Agnes Mgaya akiwasilisha mada katika semina ya  kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama iliyomalizika.
 Sehemu ya masheikh , akiwemo Hamid Jongo( kushoto), Imamu wa msikiti wa Manyema na Mwakilishi kutoka Baraza LA Waislam nchini Bakwata wakifuatilia semina ya Jiongeze Tuwavushe Salama
 Waandishi wa Habari na watangazaji kutoka mikoa mbalimbali wakiwa katika semina ya Jiongeze Tuwavushe Salama iliyomalizika.
Waandishi wa Habari, viongozi wa UNICEF na Wizara ya Afya wakiwa katika Picha ya pamoja baada ya semina ya Jiongeze Tuwavushe Salama iliyomaliza.

HARUSI YA MDAU DOMINIUS NA PROSCOVIA YAFANA MKOANI KAGERA

$
0
0

Mkuu wa MKoa wa Kagera Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti. akikabidhi zawadi kwa maharusi . 
 Pichani RC Gaguti akiongoza Wageni waalikwa kutoa zawadi kwa Maharusi, kisha kupiga picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuondoka pale.
 Pichani akiwasili Mhe. Naibu waziri wa Kilimo na Mbunge Jimbo la Karagwe Innocent Bashungwa pamoja na msafara wake wakiingia Ukumbini.
 Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti Ukiingia Ukumbini kuungana na Wageni wengine waalikwa.
 Ukafika muda wa kukata utepe na kufungua sherehe rasmi, kama inavyooneka katika Picha
 Bango la shughuli nzima
 Muonekano wa Jukwaa la Maharusi likiwa limenakishiwa vyema na Mapambo mazuri na Kazi Nzuri kutoka Mama Lily Decoration wa Kayanga Karagwe.
Keki iliyoandaliwa rasmi kwa ajili ya maharusi na makundi mbalimbali wakiwemo wazazi wa maharusi, kama inavyoonekana katika Picha. 
 Kati ya washereheshaji waliohakikisha kila kitu kinakaa sawa ni pamoja Mshereheshaji Tajiri wa Kigoma maarufu Brother K wa Futuhi, kama anavyoonekana akiwajibika.
 Wazazi wazaa chema wa Bwana Harusi Dominius wakiingia Ukumbini
 Burudan kidogo ikachukua nafasi yake na sehemu ya waalikwa wakijimwaga uwanjani kunyoosha miguu kama inavyoonekana.
 Katika Picha hii anaonekana Mtumishi wa Mungu akikabidhi Msalaba kwa Baba Mzazi wa Dominius ambae ni Mwenyekiti wa CCM-Kyerwa, kama ishara ya Kubariki eneo la kufugia (Farm) ambapo sherehe za Harusi zimefanyika. 
 Wapendao Hawa Dominius na Proscovia wakapata nafasi ya kukata na kula keki

 Maharusi wakijimwaya mwaya wakati wakiingia eneo la sherehe  
 Pichani waaonekana wakicheza kwa furaha na shangwe paina kulazimishwa, Maharusi Dominus na Proscovia wakiwa wanameremeta.
 Wapambe wa maharudi wakiserebuka uwanjani
Wapendao Hawa Dominius na Proscovia wakapata nafasi ya kukata na kula keki
 Wapendao Hawa Dominius na Proscovia mara baada ya kulishana keki 
 Wasaidizi wa Maharusi wakiingia Ukumbini. 
 Ilikuwa furaha na kutabasamu kwa maharusi hao

 Wazazi wazaa chema wa Bwana Harusi Dominius wakiingia Ukumbini
Wapambe wa Maharusi wakiingia kwa mbwembwe na bashasha kubwa wakionekana kucheza kwa shangwe.

 
Pichani, Burudani kutoka Kikundi cha Sanaa Chanika Karagwe ikichukua nafasi yake, 
 Pichani Ni moja kati ya  Kaunta sita za Vinywaji zilisheheni vinywaji Vilaini na Vikali, kama vinavyoonekana, mpaka Harusi inatamatika Vinywaji vilibaki Kaunta zote.
 Kama ilivyokuwa katika Vinywaji pia upande wa nyama choma na Kuku nako hivyohivyo, majiko manne kwa ajili ya michomo

SHULE YA MSINGI HOLILI YAPEWA MIFUKO YA SARUJI 300 KUFANIKISHA UJENZI WA MADARASA 10, NYUMBA ZA WALIMU

$
0
0
Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Godwin Kamando (kushoto), akikabidhi msaada wa mifuko 300 ya saruji yenye thamani zaidi ya shs Milioni 3,388,488 kwa Ofisa Mtendaji wa kata ya Holili, Fadhili Buzebuze (Ward Executive Officer) (watatu kulia) na Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Holili, Paschal Ntomola kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba 10 vya madarasa, Ofisi 2 na nyumba 2 za walimu wa Shule ya Msingi Holili iliyopo wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro. Hafla ya makabidhiano ilifanyika kiwandani hapo Pongwe, Tanga jana.Wengine ni Maofisa wa kampuni hiyo.
Meneja Afya, Usalama na Mazingira wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Emmanuel Ntoma (wa pili kushoto), akikabidhi msaada wa mifuko 300 ya saruji yenye thamani zaidi ya shs 3,388,488 kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Holili, Paschal Ntomola (kulia) kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba 10 vya madarasa, Ofisi 2 na nyumba 2 za walimu wa Shule ya Msingi Holili iliyopo wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro. Hafla ya makabidhiano ilifanyika kiwandani hapo Pongwe, Tanga jana.Wapili kulia ni Ofisa Mtendaji wa kata ya Holili, Fadhili Buzebuze na Wengine ni maofisa wa kampuni hiyo.
Meneja Ugavi wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Livin Masawe (wa pili kushoto), akikabidhi msaada wa mifuko 300 ya saruji yenye thamani zaidi ya shs Milioni 3,388,488 kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Holili, Paschal Ntomola (wapili kulia) kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba 10 vya madarasa, Ofisi 2 na nyumba 2 za walimu wa Shule ya Msingi Holili iliyopo wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro. Hafla ya makabidhiano ilifanyika kiwandani hapo Pongwe, Tanga jana.Watatu kulia ni Ofisa Mtendaji wa kata ya Holili, Fadhili Buzebuze na Wengine ni Maofisa wa kampuni hiyo.



Na Ripota Wetu,Michuzi TV

KAMPUNI ya Tanga Cement (TCPLC), imetoa msaada wa mifuko 300 ya saruji kwa Shule ya Msingi ya Holili yenye thamani ya Sh.3,388,488 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali kuimarisha sekta ya elimu.

Makabidhiano ya msaada huo yamefanyika katika kampuni hiyo iliyopo eneo la Pongwe mkoani Tanga ambapo viongozi wa ngazi mbalimbali Kata ya Holili na maofisa wa kiwanda hicho wameshuhudia makabidhiano hayo.

Akizungumza leo wakati wa kukabidhi msaada huo, Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Tanga Cement Godwin Kamando amesema lengo lao ni kusaidia maendeleo ya Kata ya Holili na wameona haja ya kusaidia sekta elimu kwa kutoa mifuko hiyo ya saruji kwa ajili ya Shule ya Msingi Holili.

"Msaada huu wa mifuko ya saruji ambayo tumeitoa katika Kata ya Holili ni kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Shule ya Msingi Holili na hasa kwa kuitumia kujenga nyumba mbili za walimu, ofisi mbili za shule na ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa 10,"amesema Kamando.

Ameongeza moja ya mkakati wao ni kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii ya Watanzania kwa kusaidia shughuli za maendeleo na msaada huo ni maalumu kwa ajili ya eneo hilo la Holili ambalo wao wamekuwa wakipata sehemu ya malighafi kwa shughuli za uzalishaji wa saruji.

" Malighafi inayopatikana eneo la Holili ni madini aina ya Pozzolana ambayo ni muhimu sana katika kutengeneza moja ya aina ya saruji,"amesema na kuongeza wanaamini msaada huo utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Kamando amefafanua pamoja na kusaidia katika shule hiyo, wamekuwa wakisaidia katika shughuli nyingine za kimaendeleo na hasa ya ujenzi wa miundombinu katika afya, elimu na mazingira na hadi sasa ndani ya kata hiyo wameshatoa jumla ya mifuko ya saruji 1150. 

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Kata wa Holili Fadhili Buzebuze amesema wanashukuru kupata msaada huo wa mifuko ya saruji na kufafanua watahakikisha mifuko hiyo inatumika kwa ajili ya malengo yaliyokusudiwa.

Mpango wa Matumizi bora ya ardhi katika mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi wazinduliwa

$
0
0
Na Teresia Mhagama, Tabora

Serikali imezindua Mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa Vijiji, Wilaya na Mikoa itakayopitiwa na mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) ikiwa ni hatua nyingine katika utekelezaji wa mradi huo.

Mpango huo umezinduliwa katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilayani Nzega, Mkoa wa Tabora tarehe 25/5/2019 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi aliyeambatana na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry na Meneja Mradi wa EACOP, Mantin Tiffen.

Akizungumza na wananchi wa Sojo, Waziri Lukuvi, alisema kuwa, mpango huo wa matumizi ya ardhi unahusisha Mikoa Nane, Wilaya 24 na Vijiji 226 ambapo vijiji 30 vipo katika Mkoa wa Tabora.

" Mpango huu unazinduliwa katika Kijiji cha Sojo kwa niaba ya Vijiji vyote nchini kwa kuwa hapa Sojo ndipo patakuwa na kituo kikubwa cha kutoa huduma katika mradi wa bomba la Mafuta kuliko vituo vingine kwani kutakuwa na Kambi Kuu na kiwanda cha kutayarisha mabomba yatakayotumika kusafirisha mafuta kitajengwa hapa." alisema Lukuvi.

Katika hatua nyingine, Waziri Lukuvi, alitoa onyo kwa wavamizi wa ardhi iliyotengwa kwa ajili ya mradi huo kuwa, tayari mkuza wote ulishapigwa picha za anga hivyo fidia itatolewa kwa wananchi wanaostahili tu.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, alisema kuwa, kazi za mradi wa EACOP zilizopangwa kufanyika katika Kijiji hicho cha Sojo zina uwekezaji wa shilingi bilioni 600 na matarajio ni kuwa kazi hizo zitaanza mwezi wa Tisa mwaka huu.

Alisema kuwa, kutakuwa na ajira zitakazozalishwa hivyo alitoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa zitakazojitokeza kutokana na uwekezaji huo.

Aliongeza kuwa, mpaka sasa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi umeshatoa ajira zaidi ya 200 na matarajio ni kuwa utaendelea kutoa ajira zaidi kwa watanzania.

Kuhusu umeme, alieleza kuwa, Wizara iko katika Mpango wa kusambaza umeme kwenye Vijiji vyote vinavyopitiwa na mkuza huo kwa gharama ya shilingi elfu 27,000 tu ili kuweka mazingira wezeshi ya kutekeleza mradi husika.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, alisema kuwa, Mkoa huo utaweka mazingira wezeshi ili mradi huo wa Bomba ufanyike kwa ufanisi na ameahidi kusimamia matumizi bora ya ardhi iliyotengwa kwa ajili ya mradi husika.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Tanzania, Salum Mnuna, alisema kuwa, Rais John Pombe Magufuli amefanya jitihada mbalimbali zilizowezesha mradi huo kuanza kutekelezwa nchini hivyo ni muhimu kwa wanachi wakafanya bidii kuchangamkia fursa zinazotokana na mradi.

Aliongeza kuwa, mradi huo licha ya kutoa ajira za ujuzi wa juu, kati, chini na vibarua, utaboresha pia baadhi ya miundombinu kama vile Reli na Barabara pamoja na huduma za kijamii katika maeneo ambayo mradi utapita.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (wa tano kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mpango wa Matumizi bora ya ardhi katika mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi (EACOP). Wa Nne kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, wa Tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri na wengine ni watendaji kutoka Wizara zinazohusika na mradi huo, EACOP, Mkoa na Wilaya ya Nzega.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) na Meneja Mradi wa EACOP, Mantin Tiffen wakizungumza mara baada ya kumaliza uzinduzi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika mradi wa bomba la Mafuta katika Kijiji cha Sojo, wilayani Nzega.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (kulia), Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri (wa pili kushoto) na Mratibu wa Mradi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki, Salum Mnuna (wa kwanza kushoto), wakizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika mradi wa bomba la Mafuta katika Kijiji cha Sojo, wilayani Nzega.
Wataalam kutoka Wizara ya Nishati, wakifuatilia uzinduzi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika mradi wa bomba la Mafuta katika Kijiji cha Sojo, wilayani Nzega.
Meneja Mradi wa EACOP, Mantin Tiffen akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika mradi wa bomba la Mafuta katika Kijiji cha Sojo, wilayani Nzega.
Viewing all 110129 articles
Browse latest View live




Latest Images