Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI NA RAIS MSTAAFU KIKWETE WAONDOKA NCHINI KUUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA RAIS MPA WA AFRIKA YA KUSINI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea Afrika ya Kusini asubuhi hii ambapo kesho atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa mjini Pretoria.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakati wakiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kuelekea Afrika ya Kusini asubuhi hii ambapo kesho watahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa mjini Pretoria.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameongoza na na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula wakipanda kwenye ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam tayari kuelekea Afrika ya Kusini asubuhi hii ambapo kesho watahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa mjini Pretoria. Picha na IKULU

SEVILLA YAICHAPA SIMBA BAO 5-4, YACHUKUA KIKOMBE CHA URAFIKI

$
0
0
 Beki wa pembani wa Simba SC, Zana Coulibaly akijaribu kumpita Mchezaji wa Sevilla FC kwenye mchezo uliomalizika usiku huu kwa Simba SC kukubali kipigo cha bao 5-4.
 Kikosi cha Sinba SC kilichoanza leo kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Sevilla FC
 Hekaheka za mtanange huo kati ya Simba SC dhidi Sevilla FC
 Mashabiki wa Simba SC wakishangilia moja ya bao lillilofungwa na timu yao katika mchezo wa kirafiki dhidi Sevilla FC ya Hispania, Simba SC imekubali kichapo cha bao 5-4.
 Kikosi cha Sevilla FC kilichoanza leo mchezo dhidi ya Simba SC.
 Wachezaji wa Simba SC, Maddie Kagere na Clotous Chama wakipongezana baada timu yao kupata bao, pembeni ni Beki wa timu hiyo, Zana Coulibaly akiteta jambo na Haruna Niyonzima. Simba SC ilikubali kipigo cha bao 5-4 kutoka kwa Sevilla FC ya Hispania.

 Nyota wa Simba SC, Cloutous Chama akijaribu kuwatoka Wachezaji wa Sevilla FC katika mchezo wa kirafiki ulimalizika usiku huu kwa Simba SC kukubali kichapo cha bao 5-4.
 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Mchezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akikabidhi Kombe la Ushindi kwa Nahodha wa Sevilla FC, Jesus Navas pamoja na Wachezaji wengine wa timu hiyo baada yakuondoka na Ushindi wa bao 5-4 mbele ya Simba SC. (Picha zote na Mohammed Ibrahim, Michuzi TV)









Benki ya NMB Pemba yafutarisha Wateja Wake na Wananchi.

$
0
0
WAFANYAKAZI wa Bank ya NMB Kisiwani Pemba, wananchi na wateja wao wakiwa katika sala ya pamoja, iliyofanyika Chake Chake kuelekea kwenye futari maalumu iliyoandaliwa na Banke ya NMB kwa wateja wake
AFISA Mdhamini Wizara ya Fedha na Mipango Ibrahim Saleh Juma (katikati) akipata uji wakati wa futari maalumu iliyoandaliwa na bank ya NMB kwa wateja wake, kulia ni meneja wa benk hiyo kanda ya Dar es Salam na Zanzibar Badru Iddi na kushoto ni Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Mahmoud Mussa Wadi, futari hiyo imefanyika Chake Chake Pemba 
MENEJA wa Bank ya NMB kanda ya Dar es Salam na Zanzibar Badru Iddi, akichukua futari maalumu iliyoandaliwa na benk hiyo kwa wateja wake Kisiwani Pemba na kufanyika mjini Chake Chake
BAADHI ya wateja wa Bank ya NMB na wananchi wa Kisiwa cha Pemba, wakichukua futari maalumu iliyoandaliwa na Bank hiyo kwa wateja wake na kufanyika mjini Chake Chake'
AFISA Mdhamini Wizara ya Fedha na Mipango Ibrahim Saleh Juma (katikati) akipata uji wakati wa futari maalumu iliyoandaliwa na bank ya NMB kwa wateja wake, kulia ni meneja wa benk hiyo kanda ya Dar es Salam na Zanzibar Badru Iddi na kushoto ni Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Mahmoud Mussa Wadi, futari hiyo imefanyika Chake Chake Pemba
VIONGOZI wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kusini Pemba, wakiongoza na Kamanda wa Polisi Mkoa huo Hassan Nassir Ali wa pili kutoka kulia, akifuatiwa na Kamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania 14KJ Khamis, wakipata futari maalumu iliyoandaliwa na Bank ya NMB kwa wateja wao na kufanyika Mjini Chake Chake
BAADHI ya wafanyakazi wa NMB, wateja wao na wananchi wa Kisiwa cha Pemba, wakichukuwa futari maalumu iliyoandaliwa na benk hiyo kwa wateja wao Kisiwani hapa
BAADHI ya wateja wa Banki ya NMB na wananchi akipata futari maalumu, iliyoandaliwa na benk hiyo kwa wateja wao na kufanyika mjini Chake Chake
MENEJA wa Bank ya NMB Kisiwani Pemba Ahmed Nassor, akitoa shukurani kwa wananchi na wateja wao waliohudhuria futari maalumu, iliyoandaliwa na Bank hiyo kwa wateja wao na kufanyika mjini Chake Chake
MENEJA wa NMB kanda ya Dar es Salam na Zanzibar Badru Iddi, akizungumzia juu ya mikakati ya NMB kwa wateja wake mara baada ya kumalizika kwa futari Maalumu iliyoandaliwa na benk hiyo na kufanyika mjini Chake Chake.
AFISA mdhamini Wizara ya Fedha na Mipango Pemba Ibrahim Saleh Juma, akizungumza na wananchi na wateja wa NMB kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, mara baada ya kumalizika kwa futari maalumu iliyoandaliw ana bank hiyo kwa wateja wao na kufanyka mjni Chake Chake.

(Picha na Abdi Suleiman - Pemba).

Jafo atoa Neno kwa Plan International

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(Mb) amelitaka Shirika la Plan International kutekeleza miradi yake hapa nchini kwa weledi na umakini ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea kupata ufadhili.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa kufunga warsha ya Shirika hilo iliyokuwa na lengo la kufanya tathimini na kuweka mipango ya Shirika iliyofanyika Jijini Dodoma.

Alisema kuwa ni vyema Shirika la Plan International kutekeleza majukumu na miradi yake kwa ufanisi mkubwa ili kushika nafasi ya kwanza kwa utendaji kazi kwa Nchi zinazotekeleza miradi yake mashariki na kusini mwa Africa (RESA).
“Ninyi wataalamu wa Shirikia la Plan International mnatakiwa kuchapa kazi kwa weledi wa hali juu ili kushika nafasi ya kwanza na kuwa katika nafasi nzuri ya kupata ufadhili wa utekelezaji wa malengo ya Shirika.”

Jafo aliongeza: “Ujue ufadhili ndio kila kitu katika Shirika, mkifanya kazi vizuri mtapata fedha za kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali na hapo mtaweza kuwafikia wanufaika wengi katika achi yetu na kuzidi kuwainua na kuleta matumaini mapya katika jamii yetu,” Alisema Jafo.
“mkizidi kupata ufadhili ndipo na nyie mtapata mishahara mizuri na marupurupu hivyo ufadhili sio kwa sababu ya wananchi pekee bali ni kwa faida yenu  kama watendaji wakuu wa shirika hili”

Aidha, Jafo alitumia fursa hiyo kuwapongeza Plan International kwa namna wanavyofanya kazi zao jambo ambalo linachangia utoaji wa huduma bora kwa jamii.
“Mimi nimefanya kazi Plan International na umahiri wangu na weledi katika utendaji kazi umetokana na kufanya kazi katika Shirika hili limenijenga katika misingi ambayo mpaka kazi imekuwa ni sehemu ya masiha yangu na wala sichoki kufanya kazi hii ndio Plan International”Alisema Jafo.

“Watu wengi wamekuwa wakinishangaa kwa kazi nyingi ninazozifanya kwa siku na bado nazifanya kwa umakini na umahiri mkuwa msingi huu niliupata Plan Internatioinal na bado  nawaelekeza watumishi wa Wizara yangu kufanya kazi kwa bidii wakati wote ndio maana unaona mabadiliko makubwa ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI.
Naye Meneja Ufadhili wa Plan International Nicodemus Gachu alisema kuwa mpaka sasa Shirika lina watoto rafiki elfu 30 ambao wanapata huduma mbalimbali kutoka Plan International.

Gachu alisema kwa sasa Plan Internationa imekuja na mpango wa kutoa Bima ya Afya iliyoboreshwa kwa watoto rafiki wa shirika hilo, ambao unatarajia kuzinduliwa hivi karibuni kwa kuwakabidhi watoto hao Bima za Afya katika kila Mkoa ambako wana watoto rafiki.
Gachu alitumia fursa hiyo kuanisha kazi ambazo Shirika limezifanya kuwa ni pamoja na kujenga miundombinu ya Afya katika baadhi ya hospital na vituo vya Afya kama Buguruni, ujenzi wa miundombinu ya Elimu, ujenzi wa  miundombinu ya Maji, kuwawezesha vijana kiuchumi na kuwajengea uwezo watoto kuzifahamu hazi zao.

Naye Neema Moris ambaye ni Meneja ya Uniti ya Kisarawe amesema kupitia warsha hiyo ya siku nne wameweza kujitathmini utendaji kazi wa shirika, namna ya kutatua changamoto wanazokabiliana nazo katika maeneo ya kazi na kuweka malengo ya utekelezaji wa kazi za Shirika.
Ikumbukwe kuwa Waziri Jafo alianzia kazi katika Shirika la Plan Internationa akiwa kama Meneja wa Uniti ya Kisarawe kabla ya kuwa Mbunge wa Kisarawe kisha kuteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo (Mb) akifunga warsha ya Shirika la Plan International ya kufanya tathimini na kuweka mipango ya Shirika hilo inayofanyika Jijini Dodoma.
Meneja Ufadhili wa Plan International Nicodemus Gachu akitoa mada kwa washiriki wa warsha ya tathimini na mipango ya Shirika la Plan International.
 Wataalam wa Shirika la Plan International wakiendelea na warsha ya tathimini na kuweka malengo ya Shirika hilo inayofanyika Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo (Mb) katika picha ya pamoja na Meneja wa Uniti ya Kisarawe katika warsha ya Shirika la Plan International inayofanyika Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo (Mb) katika picha ya pamoja na wataalam wa shirika la Plan International wakati wa warsha ya tathimini na mipango.

SETH ARUHUSIWA NA MAHAKAMA KUONANA NA WAKILI WAKE AKIWA MAGEREZA

$
0
0
Na Karama Kenyunko Michuzi TV

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewaamuru maofisa wa Magereza anapokaa mshitakiwa Harbinder Seth anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, kumruhusu kuonana na wakili wake kwa sababu ni haki yake ya masingi.

Amri hiyo imetolewa Mei 23, 2019 baada ya mshtakiwa Seth kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa ana miezi sita hajaonana na wakili wake kwa sababu maofisa wa magereza wanamkatalia kufanya hivyo.

Seth amedai,  anataka kuonana na wakili wake ili waweze kuzungumzia masuala ya kesi hiyo hivyo anaomba kibali cha mahakama aweze kuruhusiwa kuonana na wakili wake.

Mapema kabla ya kutolewa kwa amri hiyo, wakili wa Serikali, Wankyo Simon alidai  kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi bado haujakamilika hivyo ameomba tarehe nyingine kwa ya kutajwa.

Kufuatia hayo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 10, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande.

Mbali na Seth mshitakiwa mwengine ni mfanyabiashara  James Rugemalira ambapo wote kwa  pamoja wanaokabiliwa na mashtaka 12 yakiwemo ya utakatishaji fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27 kwa mara ya kwanza walifikishwa mahakamani hapo Juni 19, 2017. 

Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa Oktoba 18, 2011 na Machi 19 , 2014 jijini Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ili kutenda kosa.

Aidha, inadaiwa katika mashitaka ya kujipatia fedha kwamba  kati ya  Novemba 28 na 29, 2011 na Januari 23,2014 katika Makao makuu ya Benki ya Stanbic Kinondoni  na Benki ya Mkombozi tawi la Mtakatifu Joseph,  kwa ulaghai washitakiwa hao walijipatia kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Dola za Marekani  22,198,544.60 na Sh 309, 461,300,158.27.  

Pia washitakiwa wote wanadaiwa kuisababishia serikali hasara ambapo inadaiwa walitenda makosa hayo Novemba 29, 2013 katika Benki ya Stanbic tawi la  kati kinondoni, kwa vitendo vyao waliisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 22, 198, 544.60 na Sh. 309,461,300,158.27.

Kati ya Novemba 29,2013 na Januari 23, 2014 maeneo tofauti Dar es Salaam kwa pamoja walitenda kosa la kutakatisha fedha kwa kuchukua fedha kutoka BoT ambazo ni dola za Marekani milioni 22.1 na Sh bilioni 309.4  wakati wakijua fedha hizo ni zao la kujihusisha na genge la uhalifu.

Washitakiwa hao wapo rumande kwa kuwa mashitaka hayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.

WANAKIJIJI CHIKONGO WASHUPALIA MAPATO NA MATUMIZI

$
0
0
Kamati ndogo ya kuchunguza mapato na matumizi imeundwa katika mkutano wa hadhara wa kijiji cha Chikongo baada ya Wananchi kuchachamaaa kwa kuikataa taarifa ya Serikali ya kijiji.

Sakata hilo limeibuka kwenye mkutano wa robo ya tatu ya mwaka katika Kijiji cha Chikongo kilichopo kata ya Mkoreha mbele ya Afisa Tarafa ya Mihambwe Gavana Emmanuel Shilatu baada ya Wananchi kutokuwa na imani na ripoti iliyosomwa kutowaridhisha .

Kutokana na tafran hiyo Afisa Tarafa ya Mihambwe Emmanuel Shilatu aliagiza mara moja iundwe kamati ndogo itakayopitia mapato na matumizi ya Kijiji hicho jambo ambalo liliungwa mkono na Wananchi.

Gavana huyo alitaka kamati hiyo ihusishe viongozi wa kata, Serikali ya Kijiji, baadhi ya Wananchi na wajumbe wa kamati ya ujenzi ili kumaliza utata huo na ukweli ujulikane

"Yapo madai ya mkutano mkuu wa kijiji hauitishwi kwa mujibu wa kalenda, Wananchi hawasomewi mapato na matumizi, Madai hayo ni ukiukaji wa sheria. Napendekeza iundwe kamati hapa hapa. Ipekue hesabu kisha ije na majibu ya kuridhisha" Alisema Gavana Shilatu.

Katika hatua nyingine Gavana Shilatu kupitia mkutano huo aliwataka Wakulima kuendelea na kazi zao za kilimo na wajasiliamali kuendelea kupatiwa vitambulisho vya shughuli zao.

"Mkulima ahakikishe analima, Mjasiriamali apatiwe kitambulisho. Tunahitaji kila Mwananchi awe mlinzi wa amani. Wote tukifanya kazi ndipo tutakapoinua uchumi wa nchi." alieleza Gavana Shilatu.

Katika mkutano huo wa Kijiji ulihudhuliwa na Afisa Tarafa Mihambwe, Diwani kata ya Mkoreha, Mtendaji kata na Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Chikongo.

HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA YAANZA KUTOA UCHUNGUZI NA MATIBABU YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

WANANCHI MBULU KUNUFAIKA NA BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA

$
0
0
WANANCHI wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, waliokuwa wanafuata huduma ya Baraza la ardhi na nyumba Wilayani Babati, wataondoka na tatizo hilo baada ya viongozi wa wilaya hiyo kupanga mikakati ya kuanzisha katika eneo hilo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Joseph Mandoo aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo.

Mandoo alisema wameshapata jengo litakalokuwa linatumika katika mashauri mbalimbali ya baraza hilo litakalokuwa kwenye kata ya Dongobesh.

Alisema baada ya jengo hilo kupatikana hivi sasa wanajipanga ili lianze kutumika na wananchi waliokuwa wanakwenda mbali hadi wilaya ya Babati kufuata huduma hiyo, sasa itakuwa karibu tofauti na mwanzo.

"Tutawachukua wazee wa baraza hilo kutoka kwenye kata mbalimbali za jirani ikiwemo Dongobesh, Tumati na nyinginezo kuliko kuwachukulia waliopo mbali na eneo ofisi ilipo," alisema Mandoo.

Hata hivyo, mbunge wa jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Massay alisema changamoto kubwa inayosababisha kutoanzishwa kwa baraza hilo ni watumishi hasa wapiga chapa. "Kama mkurugenzi angeweza kufanikisha tupate hata wapiga chama wa halmashauri mashauri yangeanza kusikilizwa ila muda siyo mrefu shughuli ya baraza hilo itaanza," alisema Massay.

Awali, diwani wa viti maalum wa Tarafa ya Dongobesh, Ester Joel (CCM) aliuliza swali juu ya jambo linalokwamisha uanzishaji wa shughuli za baraza la ardhi na nyumba kwenye halmashauri hiyo.

Joel alisema hivi karibuni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi aliwateua wenyeviti wa wilaya wa mabaraza ya ardhi na nyumba wa wilaya hivyo ofisi ya Mbulu nayo ianze kazi.

Mkazi wa kijiji cha Dongobesh, John Matle aliipongeza serikali kwa kufanikisha uanzishwaji wa baraza hilo kwani wengi wanaofuata huduma hiyo mjini Babati wanalazimika kutumia gharama kubwa.

"Wengine walikuwa wanalazimika kulala Babati ili kusikiliza mashauri yao na gharama za kupeleka mashahidi nazo ni nyingi ila kuwepo hapa Dongobesh itapunguza muda na gharama," alisema Matle.
  Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Gregory Maasay akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
 Diwani wa viti maalum wa Tarafa ya Dongobesh Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, Ester Joel akisoma taarifa ya utekelezaji wa kamati ya fedha, uongozi na mipango, juu ya uanzishwaji wa baraza la ardhi na nyumba la wilaya hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Stanley Kamoga akizungumzia kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo, kushoto ni Mwenyekiti wake, Joseph Guulo Mandoo.

WANANCHI DODOMA WATEKELEZA AGIZO LA MATUMIZI YA MIFUKO MBADALA

Dhahabu ya Bilioni 34.3 imeuzwa katika kipindi cha mwezi mmoja - Biteko.

SHILINGI ML 400 KUJENGA KITUO CHA AFYA MAPERA MBINGA

$
0
0
JUMLA ya shilingi Milioni 400 zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Mapera kata ya Mapera Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ambrose Mtarazaki amesema hayo jana wakati akifungua kikao cha Baraza la robo ya tatu cha Baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Umati Mjini Mbinga.

Alisema, ujenzi wa kituo hicho utakapokamilika utasaidia sana kuwaondolea wananchi wa kata ya Mapera na Bonde zima la Hagati kusafiri umbali mrefu hadi Hospitali ya wilaya iliyopo Mbinga Mjini au Hospitali ya Misheni Litembo kufuata matibabu.

Mtarazaki ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kutoa fedha hizo ambazo zitakwenda kukamilisha kazi hiyo na kuimarisha huduma za Afya kwa wananchi hasa ikizingatia kuwa, lengo la kujenga kituo cha Afya Mapera ni la muda mrefu hata hivyo walishindwa kutokana na ukosefu wa fedha.

Amewaomba wananchi wa Mapera na kata jirani kuhakikisha wanashiriki vema katika ujenzi wa miundombinu kwa kupeleka mchanga ,tofali na mahitaji mengine ili kazi hiyo ikamilike kwa wakati badala ya kuiachia Serikali jambo linalo weza kuchelewesha kazi hiyo.

Aidha Mtarazaki, ametaka fedha hizo zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na kuwaonya watendaji wa Serikali kanzia ngazi ya kijiji hadi wilaya kutothubutu kwa namna yoyote kujaribu kutumia fedha hizo kinyume na malengo.

Katika hatua nyingine Mtarazaki alisema, katika kipindi cha robo ya tatu ya Mwaka wa Fedha 2019/2020 Halmashauri ya wilaya imeweza kutekeleza na kufuatilia miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo mbalimbali hatua iliyochochea sana upatikanaji wa huduma bora za kijamii kwa Wananchi.

lisema, katika kipindi hicho Halmashauri ya wilaya imetoa shilingi Milioni 261 kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa na Upimaji na usimamizi wa matumizi Bora ya Ardhi katika vijiji mbalimbali.

Mtarazaki alisema, pia Halmashauri ya wilaya imetoa jumla ya shilingi milioni 198 kama mkopo kwa makundi maalum ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu pamoja na shilingi milioni285 zilizotengwa kwa ajli ya ununuzi wa magari mawili ili kurahisisha utendaji wa watumishi na utoaji huduma Bora kwa wananchi.

Alisema, sambamba na hilo Halmashauri imefanikiwa kupata hati safi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG),na amewataka watumishi wa Halmashauri ya kuendelea kufanya kazi kwa weledi na madiwani kuhakikisha wanasimamia kikamilifu vyanzo vyote vya mapato ili fedha zinazokusanywa ziende kufanya kazi ya kumaliza changamoto na upatikanaji wa huduma za kijamii.

Pi aliwaeleza madiwani kuwa,hadi kufikia mwezi April mwaka huu Halmashauri imeshakusanya asilimia 85 ya mapato yake ya ndani.

Hata hivyo alisema, licha ya mafanikio hayo bado kuna tatizo kubwa kwa baadhi ya watendaji wachache kushindwa kutumia mashine za POS kwa ajili ya kukusanya mapato ya Halmashauri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga Juma Mnwele akifafanua jambo kwa wajumbe wa Baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika jana katika Ukumbi wa Umati Mbinga,katikati Mwenyekiti wa halmashauri Ambrose Mtarazaki.

WABUNGE WAPEWA SEMINA YA BAJETI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti Mhe. Andrew Chenge akichania jambo katika semina ya mapitio ya Bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2018/2019 iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Wajumbe wa Kamati ya Bajeti wakifuatila jambo katika semina ya mapitio ya Bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2018/2019 iliyotolewa na Ndg. Cliff Muga kwenye Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.(Picha na Ofisi ya Bunge)

Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani Awasha umeme ndani ya Vijiji vya Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha

$
0
0
 Waziri wa Medard Kalemani alivyowasili kwenye nyumba ya mzee Ambilikile Mwaisapile (babu wa Loliondo) tayari kwa kuwasha umeme katika tarafa ya  Samunge wilaya ya Ngorongoro,kulia kwake ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
 Babu wa Loliondo Ambilikile Mwaisapile akiushukuru viongozi waliotembelea nyumbani kwake na kuwasha umeme,Kulia kwake ni Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kaleman,Naibu wa Elimu Nishati na Teknolojia William Olenasha,mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro.
 Waziri wa Nishati Dkt Medadi Kalemani akiwa katika wilaya ya Ngorongoro makao makuu ya wilaya hiyo Loliondo,Kata ya Samunge tayari kwa kuwasha Umeme kulia kwake ni mbunge wa Ngorongoro William Olenasha ambae pia niNaibu  waziri wa Elini ,kushoto kwake ni Ambilikile Mwaisapile( babu wa loliondo) ambapo umeme unawashwa leo
 Diwani wa Kata ya Samunge Kajurus Stivin akiongea kumkaribisha mhe Waziri wa Nishati Dkt.Kalemani katika kata hiyo tayari kwa kuwasha umeme
 Mbunge wa Ngorongoro ambaye pia ni Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia akizungumza katika kata ya samunge tayari kumkaribisha waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalema kuwasha umeme ambapo tangia kupata uhuru kijiji hichi hakijapata umeme unawashwa kwa mara ya kwanza,digodigo na Ngorongoro.
Waziri wa Nishati Medard Kalemani akisalimiana na wanafunzi wa shule ya msingi Bisikene iliyopo wilaya ya Ngorongoro kata ya samunge   yenye  darasa la kwanza hadi la nne ambapo amekwenda kuwasha umeme leo.
Wanafunzi wa shule ya msingi Bisikeni iliyopo wilaya ya Ngorongoro kata ya Samunge wakimkaribisha Waziri wa Nishati leo.
 Wananchi wa kata ya digodigo,kata ya digodigo,tarafa ya Sale wilayani Ngorongoro
Wakazi wa Kijiii cha Digodigo ,Kata ya Digodigi Tarafa Sale wilaya ya Ngorongoro wakiwa tayari kumsikiliza waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani leo.

Naibu Waziri wa Nishati, aagiza TANESCO na REA kutatua sintofahamu ya nguzo mkoani Morogoro

$
0
0
Na Teresia Mhagama
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, ametoa Wiki Moja kwa wasimamizi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini mkoani Morogoro kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na TANESCO kuhakikisha kuwa wanatatua changamoto ya nguzo za umeme mkoani Morogoro.

Naibu Waziri alitoa agizo hilo, tarehe 23 Mei, 2019 mkoani Morogoro wakati alipofanya ziara ya kukagua kazi ya usambazaji umeme vijijini wilayani Mvomero na Gairo na kuwasha umeme katika Kijiji cha Dibamba wilayani Mvomero na Kijiji cha Sanganjeru wilayani Gairo.

Agizo la Naibu Waziri limekuja baada ya sampuli ya nguzo za mkandarasi wa umeme mkoani Morogoro kupimwa na wataalam wa TANESCO na kuonekana kuwa hazina vigezo huku mkandarasi huyo akidai kuwa sehemu ya nguzo zake zinafaa kwa matumizi ya umeme.

" Hatutaki kuona mivutano kati ya wakandarasi na wasimamizi wa miradi ya umeme vijijini kwani inachelewesha upelekaji umeme kwa wananchi hivyo nawaagiza mtatue suala hili kwa kupima nguzo zote na Wizara ipate taarifa ndani ya Wiki Moja."alisema Naibu Waziri

Kuhusu kasi ya mkandarasi anayesambaza umeme vijijini mkoani Morogoro, kampuni ya State Grid, alisema kuwa, bado haridhishwi na kasi ya mkandarasi huyo na kutoa onyo kuwa Serikali itamchukulia hatua endapo hatatekeleza kazi kwa mujibu wa mkataba.

Aidha alitoa agizo kwa wazalishaji wa vifaa vya umeme, wasambazaji na wakandarasi wa umeme vijijini kutatua changamoto zao kwa haraka mara zinapojitokeza ili kutochelewesha miradi ya umeme vijijini.

Akieleza kuhusu hatua zilizofikiwa na Serikali katika kazi ya usambazaji umeme vijijini, alibainisha kuwa hadi sasa asilimia 57 ya vijiji nchini tayari vimesambaziwa umeme kati ya Vijiji 12,268 huku kazi hiyo ikiendelea na kwamba Tanzania ndiyo inayoongoza katika nchi za Afrika Mashariki kwa usambazaji umeme vijijini.

" Wakati Serikali ya Awamu ya Tano, inaingia madarakani ilikuta vijiji 8783 havina umeme kati ya Vijiji 12,268, ndio ikaanza safari ya kufikisha umeme kwenye vijiji hivyo kupitia miradi mbalimbali ikiwemo huu wa REA Awamu ya Tatu mzunguko wa kwanza, mradi wa ujazilizi Awamu ya Pili mzunguko wa kwanza na miradi mingine," alisema Mgalu

Kuhusu bei ya umeme aliendelea kusisitiza agizo la Serikali kuwa ni elfu 27,000 tu, awe anasambaza mkandarasi wa umeme vijijini au TANESCO ili kuleta usawa wa utoaji huduma kwa wananchi.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akiwasha umeme katika Kijiji cha Dibamba wilayani Mvomero, Mkoa wa Morogoro.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Tabuhoteli wilayani Gairo Mkoa wa Morogoro wakati alipofika kukagua kazi ya usambazaji umeme vijijini. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe na kulia ni Msimamizi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Ahmed Chinemba.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akikata utepe kuashia uwashaji umeme katika Kijiji cha Sanganjeru wilayani Gairo Mkoa wa Morogoro. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe.
 Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akitoa maelezo kuhusu kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) kwa wananchi wa Kijiji cha Sanganjeru wilayani Gairo Mkoa wa Morogoro wakati alipofika kijijini hapo kukagua kazi ya usambazaji umeme na kuwasha rasmi umeme.
Wataalam kutoka Wizara ya Nishati, TANESCO na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) wakati akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Tabuhoteli wilayani Gairo, Mkoa wa Morogoro.

BENKI YA NMB KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA WANANCHI

$
0
0
Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Ndugai akikata utepe baada ya kukabidhiwa Mabati kwa ajili ya Shule ya Sekondari Chiwe yaliyotolewa na Benki ya NMB tukio lililofanyika leo katika Shule ya Sekondari Mnyakongo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Ndg. Margaret Ikongo
Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimshukuru Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Ndg. Margaret Ikongo baada ya kukabidhiwa Mabati kwa ajili ya Shule ya Sekondari Chiwe yaliyotolewa na Benki hiyo tukio lililofanyika leo katika Shule ya Sekondari Mnyakongo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.Picha na Alex Sonna
Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Ndugai akikata utepe baada ya kukabidhiwa viti na meza kwa ajili ya Shule ya Sekondari Mnyakongo zilizotolewa na Benki ya NMB tukio lililofanyika leo katika Shule ya Sekondari Mnyakongo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. Kuanzia Kushoto ni Meneja wa NMB Benki tawi la Kongwa, Ndg. Tuntufye Mwakatika, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Ndg. White Zuberi, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Ndg. Margaret Ikongo, Afisa Mkuu wa Kitengo cha Digitali, Mifumo na Bidhaa kutoka NMB Benki, Ndg. Pete Novert na Meneja wa NMB Benki Kanda ya Kati, Ndg. Nsolo Mlozi
Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Afisa Mkuu wa Kitengo cha Digitali, Mifumo na Bidhaa kutoka NMB Benki, Ndg. Pete Novert walipokutana leo katika Shule ya Sekondari Mnyakongo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. Katikati ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Ndg. Margaret Ikongo na Meneja wa NMB Benki Kanda ya Kati, Ndg. Nsolo Mlozi
Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiteta jambo na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Ndg. Margaret Ikongo (katikati) na Afisa Mkuu wa Kitengo cha Digitali, Mifumo na Bidhaa kutoka NMB Benki, Ndg. Pete Novert walipokutana leo katika Shule ya Sekondari Mnyakongo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Ndugai akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnyakongo alipowatembelea leo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Meneja wa NMB kanda ya kati Nsolo Mlozi,akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnyakongo baada ya kwenda kukabidhi Viti,Meza na Mabati wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Shule ya Mnyakonga Mpokeeni Sanga,akitoa taarifa ya shule yake baada ya kupokea Viti,Meza kutoka benki ya NMB wilayani Kongwa Mkoani Dodpoma.

Diwani wa Kata ya Kongwa Mhe.White Zuber akitoa neno la shukrani kutoka kwa benki ya NMB mara baada ya kukabidhi Viti,Meza kwa shule ya Sekondari Mnyakongo pamoja mabati 250 kwa shule ya Chiwe zote za wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma
Mjumbe bodi ya wakurugenzi Benki ya NMB Margaret Ikongo akitoa semina kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari Mnyakongo na Chiwe baada ya kufanya ziara ya kukabidhi Viti,Meza na Mabati wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnyakongo wamsikiliza Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Ndugai (hayupo kwenye picha) akizungumza baada ya kuitembelea Shule hiyo leo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.

Na.Alex Sonna,Kongwa.

SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameiomba Benki ya NMB kutoa elimu kwa wananchi ili wajue jinsi ya kutunza fedha za mikopo yao.

Ndugai ameyasema hayo wakati wa NMB ilipofanya ziara ya kukabidhi viti na meza 63 vyote vikiwa na idadi hiyo kwa Shule ya Mnyakongo pamoja na mabati 250 kwa Shule ya Chiwe zilizopo Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.
Spika amesema kuwa NMB wanakila sababu ya kutoa elimu ya utunzaji fedha kwa wananchi kama wanavyofanya kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari ili wawe na ujuzi zaidi.Aidha amesema kuwa watu wengi wanakopa fedha lakini hawajui wafanyie nini baada ya kuzichukua.

‘’Yaani unashangaa muda mchache ukikutana na watu hao hakuna cha maana walichofanyia badala yake wanarudi katika maisha ya chini badala ya kusonga mbele kimaisha’’amesema Ndugai.

Spika Ndugai amesema kutokana na hilo kuna sababu ya elimu hiyo kutolewa kwa wananchi ili wakope fedha huku wakijua wanakwenda kuzifanyia nini.Ndugai amefafanua kuwa ameshakutana na kesi hizo nyingi kwa ndugu jamaa na marafiki ambao wamekopa bila ya kupata mafanikio yoyote.

‘’Kwa kweli kwa hilo naomba mlifanyie kazi kwani limekuwa likiwaumiza wananchi na kupelekea kurudi nyumba kimaendeleo badala ya kwenda mbele katika maisha kupitia fedha walizokopa’’amesisitiza Ndugai.Kwa upande wake Meneja wa NMB kanda ya kati Nsolo Mlozi amesema kuwa wataendelea kuiunga mkono Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli hivyo wametenga maeneo manne kwa ajili ya kusaidia jamii.

Mlozi ameyataja amaeneo hayo ni Elimu,Afya,Kilimo na utunzaji Fedha kwa vijana mpaka watu wa rika la juu kwa lengo la kuwainua kiuchumi kwa kunufaika kwa kupitia NMB.

Hata hivyo amesema kuwa mpaka sasa tayari milioni 400 zimeshatolewa kwa ajili ya misaada katika shule na hospitli ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa.Mlozi amesema kuwa NMB iko pamoja na serikali kuhakikisha wanafikia malengo waliojiwekea.

Naye Mkuu wa Shule ya Mnyakonga Mpokeeni Sanga amesema kuwa walikua na upungufu wa madawati 70 na wanaishukuru NMB kuwapa viti 63 na meza 63 na ambavyo wanaamini vitasaidia kupunguza uhaba waliokuwa nao.Sanga amewahakikishia NMB kuwa vitu hivyo watavitunza ili hapo wanafunzi wengine waje kuvitumia hapo mbeleni na amewaomba waendelee na moyo huo wa kusaidia jamii kwani wamekuwa mfano wa kuigwa nchini.

Mkuu wa shule ya Chiwe Aron Mango amesema kuwa mabati hayo waliopewa yatawasaidia kuezeka mabweni ya wasichana ambayo yanajengwa shuleni hapo

RAIS DKT.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI IKULU NDOGO KIBWENI ZANZIBAR

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akifuatilia maelezo ya Utekelezaji wa Mpango Kazi waWizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa kipindi cha Mwezi Julai 2018 hadi March 2019, ikisomwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu, kushoto, katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar leo.24-5-2019.

 MAOFISA wa Idara mbalimbali za Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, wakifuatilia mkutano huo wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa kipindi cha mwezi Julai 2018 hadi March 2019, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Ndogo ya Kibweni Zanzibar,24-5-2019
 Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Diaspora Zanzibar Ndugu Adila Hilal Vuai,akizungumza wakati mkutano huo wa Utekelezaji wa Mpangio Kazi kwa kipindi cha mwezi Julai 2018 hadi March 2019, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
 KATIBU wa Rais wa Zanzibar Ndg. Haroub Shaib akizchangia wakati wa hafla ya mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi Wizara ya Nchi Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa kipindi cha mwezi Juali 2018 hadi March 2019, uliofanyika Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar
 KATIBU Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ndg. Salum Maulid, akiwasilisha Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar leo.24-5-2019. 
 KATIBU Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee akizungumza wakati wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa kipindi cha mwezi Julai 2018 hadi March 2019, uliofanyika kjatika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, katika mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi, kwa kipindi cha mwezi Julai 2018 hadu March 2019,uliofanyika Ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar leo.24-5-2019.
(Picha na Ikulu)

LAKWETU CONCERT 2019 KUTIKISA MWANZA KWA KISHINDO

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya jamii
       
LILE tamasha kubwa la Muziki wa Injili Mkoani Mwanza Liitwalo Lakwetu Concert linatarajia kufanyika kwa Kishindo Jijini humo tarehe 9 Juni Mwaka huu. Akizungumza na Waandishi wa Habari Meneja wa Famara Promotion waandaji wa Lakwetu Concert Bi Catherine Mniko alisema kuwa tamasha la Mwaka huu litakuwa kubwa kutokana Maandalizi yaliyofanywa na Kamati ya uratibu.

Catherine alisema Kamati imejiandaa vya kutosha kuratibu kila kitu na wanaamini tamasha la mwaka huu litakuwa kubwa tofauti ya miaka miwili iliyopita toka lianzishwe Jijini Mwanza.

"Toka Lakwetu Concert lianzishwe tumeona ukuaji mkubwa wa tamasha, watu wameanza kutuelewa na kulipenda tamasha letu" alisema Bi Catherine.

"Mwaka huu tumeanza Maandalizi mapema Sana toka mwezi wa pili na hadi kilele chake tunaamini kusudi letu litakuwa limefikia hatua nzurii zaidi" 

"Tumepita kwenye makanisa Saba Jijini Mwanza kwa kuandaa matamasha ya kuimba  kwa kuzileta kwaya mbalimbali kutoka madhehebu yote, waimbaji wa bendi na waimbaji binafsi kwa ajili ya kumsifu Mungu pamoja na kujiandaa na kilele Cha tamasha letu la Grand Finale"

Bi Catherine alisema tamasha la finali la Lakwetu Concert litakuwa na Mambo Mbalimbali mazuri Sana kupita miaka miwili iliopita . Alisema tamasha hilo litafanyika Katika Uwanja wa CCM Kirumba tarehe 9 Juni Mwaka huu kwa vikutanisha Vikundi zaidi ya arobaini kutoka Mikoa mbalimbali Nchini.

Pia watakuwepo washiriki wa Shindano la Rock City Gospel Search 2019 siku hiyo na watazamaji watapata nafasi ya kuwaona ili wawafahamu na kuviona vipaji walivyonavyo. Tamasha la Lakwetu Concert ni Kongamano kubwa la Kuimba na kusifu lililobuniwa makusudi kuwaleta waimbaji wa Muziki wa Injili pamoja ili kumsifu Mungu kwa Nyimbo na tenzi, linalozunguka Mikoa mbalimbali Nchini.

BABUTALE AFICHUA SIRI YA MAFANIKIO YA WASAFI, DINI HAINA NAFASI

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya jamii

MENEJA wa msanii Diamond platinum  Khamis Tale Tale a.k.a Babu Tale amempongeza msanii Harmonize kwa alipofikia. Aidha, tale amesema harmonize alikua msanii wa kwanza kusainiwa katika kundi hilo .

"Alikuja wasafi hajui Kiingereza kutokana na kutengenezwa na kuwa msanii wa kimataifa ilimlazimu ajifunze kingereza kuwafikia mashabiki wa kila Kona ya afrika,"

Hata hivyo tale amesema harmonize ni msanii ambae anatambulika vizuri na muziki wake unapendwa na wengi kutokana na nidhamu yake ya kazi na kukipigania kile anachokifanya.

Pia ameweka wazi  sababu zinazofanya wasanii wa kundi hilo rayvan,lavalava,queen darling,mboso , harmonize pamoja na diamond platinum kufanikiwa na kipeperusha bendera nchi zingine ni kutokana na viongozi wa kundi hilo kuwalea kwenye misingi mizuri.

"WCB ni kundi ambalo maadili, nidhamu, upendo na uchapakazi ni miongoni mwa vitu vinavyopewa kipaumbele sana, hivyo Swala la kabila na dini halina nafasi katika kundi la wasafi japo msanii rayvan peke yake ndio dini nyingine lakini kutokana na viongozi wanawalea kwa usawa imekua ngumu kuona utofauti miongoni mwao"

Pia ametoa rai kwa wasanii wengine na makundi mengine kuwa na uvumilivu,b usara na hekima kwa sababu licha ya kundi la wasafi kupitia changamoto za kibiashara kuanzia kutopigwa kwa nyimbo zao kwa baadhi ya vyombo vya habari lakini waliweza kusimama na kuamini ipo siku watasonga mbele.

ZIMEBAKI SIKU TANO USAJILI WA MAGARI YANAYOSAMBAZA MAJISAFI

Hakuna mipaka tena katika mawasiliano

$
0
0
Kampuni ya Halotel Tanzania imekuja na huduma mpya ya mawasiliano iitwayo ‘MPANGO MZIMA’ ambayo pamoja na faida zake nyingine inamuwezesha mtumiaji wa simu wa mtandao wa Halotel kupata unafuu katika huduma mbalimbali za simu.

Kuanzishwa kwa huduma ya Mpango Mzima ni muendelezo wa kampeni mbalimbali zinazoendelea kufanywa na Halotel katika kumrahisishia mteja wake kupata huduma bora za mawasiliano zikiwemo za kutumia Intaneti bila kikomo, kupiga simu matandao yote bila kikomo, kutuma ujumbe mfupi wa maneno(sms),

Akiziungumza kuhusu ‘Mpango Mzima’ Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son alisema ujio wa huduma hiyo mpya na ‘Kijanja’ imelenga kumwezesha mtumiaji wa mtandao huo kutumia intaneti yenye kasi na ukubwa wa (GB 5) bila kikomo.

Pamoja na Intaneti hiyo mtumiaji wa mtandao huo pia ataweza kupiga simu kwenda mitandao yote bure kwa kila dakika 5 za kwanza pamoja kuzawadiwa sms 5000 atakazozitumia katika kipindi cha mwezi mzima.

“Huu ni muendelezo wa mpango wa mapinduzi ya kimawasiliano wa Halotel kuwa karibu na kuwajali wateja wetu kwa huduma bora. Kuanzishwa kwa Mpango Mzima kutamwezesha mteja wetu wa Halotel kutumia intaneti ya kasi kubwa , kupiga simu bila kikomo kwa mitandao yote bure kila dakika 5 za mwanzo na hivyo kumuondolea hofu ya simu kukatika kabla hajamaliza maongezi” amesema Son.

Amesema ili mteja aweze kufaidika na huduma hiyo mpya anapaswa kujiunga kwa kupiga *148*66# na kuchagua Mpango Mzima ambapo ataweza kujiunga na kuwa tayari kwa kuanza kufurahia unafuu huo mahususi kwa ajili ya watumiaji wa mtandao wa Halotel.

Mkurugenzi huyo Bw. Nguyen Van Son amesema huduma ya Mpango Mzima ni mpya kuwahi kutolewa na mtandao mwingine wowote wa simu hapa nchini na kuwaambia watumiaji wa Halotel kuwa hiyo ni zawadi kwao hivyo wanapaswa kuifurahia na kuitumia wakati wote.

Aidha Mkurugenzi huyo Bw. Nguyen Van Son wa alisema Halotel pia imeweza kuunganisha Optic Fiber zenye urefu wa zaidi ya Kilomita 20,000 katika maeneo yenye miundombinu yake kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa data kwa maeneo mapya na hivyo kuiwezesha kuwa chaguo la kwanza kwa wateja pale linapokuja suala la huduma za Internet.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images