Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

NITABAKI KUWA MWANACHAMA MWADILIFU WA CHAMA CHA MAPINDUZI NA SERIKALI YAKE- Amos Makalla

$
0
0
Aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Katavi Amos Makala (kulia)  hii leo amekabidhi rasmi ofisi kwa mkuu wa mkoa mpya Mh Juma Homera aliyepewa nafasi hiyo baada ya Makalla kutenguliwa  nafasi ya ukuu wa mkoa huo na Rais Dkt John Magufuli hivi karibuni.

======  ======   ======== ======

- Asema Amekitumia Chama cha mapinduzi na Umoja wa vijana kwa Muda mrefu na  vipaji, uzoefu alionao atandelea kuwa Kada wa mstari wa Mbele  wa Chama cha Mapinduzi

- Amemshukuru Rais Dr John  Pombe Magufuli kwa kumuamini kwa nafasi ya Ukuu wa Mkoa kwa miaka 4

Amesema mwaka 2015 Alipokosa Ubunge ilitosha yeye kubaki mwananchi na mwana ccm tu huko Mvomero  Rais wa awamu ya 4  mhe Jakayla Kikwete alimteua kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na  Rais Dr John Magufuli alimteua kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya  na baadaye Katavi

- Amewashukuru wananchi na viongozi wa ngazi zote dini na serikali kwa kumpa ushirikiano katika Kipindi cha miezi 10 alipokuwa mkuu wa mkoa wa Katavi na Amewaomba wananchi na viongozi wampe ushirikiano wa kutosha mkuu wa mkoa Mpya Juma Homela

MATUKIO MBALIMBALI YA MECHI YA SIMBA NA SEVILLA

Polisi Ubungo waendesha mafunzo kwa madereva

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Mkuu wa kituo cha ukaguzi wa Magari katika kituo cha Mabasi Ubungo Terminal Ibrahim Samwix ameendesha mafunzo kwa madereva wa Magari makubwa kwa lengo la kufanya utambuzi wa gari n breki.

Akizungumza na Madareva hao jana jijini Dar Es Salaam.katika.kituo hicho cha Ubungo Terminal alisema mafunzo hayo ni endelevu kwa madereva ili kuwajengea uwezo wa kutambua mifumo ya gari jinsi linavyojiendesha.

 Alisema mafunzo hayo ni bure na wataendelea kuyatoa Mara kwa Mara kwa madereva wa mikoani  na nje ya nchi kwa lengo kupumbunguza au kuondoa ajari za barabarani.

Ibrahim alisema madereva watapewa vyeti baada ya kufanya mafunzo hayo Mara kwa Mara na yeye kama mkufunzi amefanya kazi hiyo kwa kujitoa zaidi.

"Nafanya kazi hii kwa kujitolea ili kuhakikisha madereva wanapata uelewa na kuepuka kugombana na askari wa barabarani Mara kwa Mara." Alisema Ibrahim.

Pia alitoa rai kwa madereva kuepuka kufanya mashindano barabarani kwani kufanya hivyo nimuhatarisha usalama wao na usalama wa abiria waliowabeba.

 Ibrahimu alisisitiza kwa kuwataka maderava kuhakikisha wanashiriki kikamilifu mafunzo hayo ili waweze kupata uelewa zaidi na kufanya kazi yao kwa kujiamini zaidi.
 Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi cha Mabasi Ubungo wa Kikosi cha Usalama Barabarani Ibrahim Samwix akiendesha mafunzo kwa madereva ikiwa ni hatua ya kupunguza ajali za Barabarani zitokanazo na makosa ya kibinadamu.
 Madereva wakipata elimu kabla ya kuanza safari
Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Ibrahim Samwix akionesha madereva namna ya matumizi ya Blake katika mafunzo hayo yaliyofanyika ofisini saa 10 alfajiri.

UJENZI WA INTERCHANGE YA UBUNGO WAFIKIA PATAMU

$
0
0
--
 Nguzo ya Katikati ya ya Makutano ya Barabara ya Morogoro ,Sam Nujoma na Mandela  ikiwa tayari imesimama kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa barabara za juu ambazo zitasaidia kupunguza msongamano katika jiji la Dar es Salaam.
 Sehemu ya Nguzo za upande wa pili ya barabara ya Mandela pamoja na mitambo ya ujenzi yakionekana katika picha .
Wafanyakazi wa kampuni ya Ujenzi ya China Civil Inayojenga barabara za juu katika Makutano ya Ubungo 

BALOZI FINLAND AIPONGEZA WIZARA YA ELIMU KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI

$
0
0
Balozi wa Finland Pekka Makka ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa utekelezaji wa miradi ya Sekta ya Elimu inayofadhiliwa na Finland ambayo imewezesha uboreshaji katika maeneo mbalimbali ya sekta hiyo.

Balozi Makka ametoa pongezi hizo jijini Dodoma alipofika ofisi za Wizara na kukutana na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha kwa lengo la kushukuru kwa ushirikiano pamoja na kuaga baada ya kumaliza muda wake ambapo amesema kupitia utekelezaji wa miradi hiyo wameiona sekta ya elimu ikiboreshwa.

Makka amesema Wizara ya elimu imeboresha miundombinu katika shule mbalimbali nchini na kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kujifunza, huku akipongeza walimu kwa kuboresha mbinu za ufundishaji. 

Balozi huyo amesema Finland itaendelea kushirikiana na Tanzania katika uboreshaji wa sekta ya elimu hususan katika maeneo ya Elimu ya Ufundi, Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ili kupanua wigo wa upatikanaji wa mafunzo nchini.

“Tumeona maboresho makubwa katika sekta ya elimu, nasi kama wafadhili tumefarijika na hakika tunaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuendelea kuboresha sekta hii muhimu, na ninaahidi kuwa Balozi anayekuja kunipokea ataendeleza ushirikiano huu,” amesema Makka.

Naye Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ameishukuru Finland kwa ufadhili wa Euro milioni 52 kwa ajili ya miradi, ambapo amesema kupitia ufadhili huo Tanzania imeshirikiana na Finland kuongeza fursa za elimu na mafunzo kwa elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, hususan kwa kuwajengea uwezo watekelezaji wa mpango wa ‘Intergrated Post Primary Education (IPPE)’ na mpango wa ‘Intergrated Programme for Out of School Adolescents (IPOSA)’. 

Miradi mingine aliyoitaja ambayo imefadhiliwa na Finland ni pamoja elimu ya afya na michezo katika vyuo vya ualimu ambayo ililenga kuwajengea maarifa na ujuzi wakufunzi na walimu tarajali waweze kufundisha shuleni kwa kuzingatia umuhimu wa michezo shuleni na kwa maendeleo ya taifa, mradi wa Tehama, (TANZAICT) unaotekelezwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), mradi ambao umewezesha kuwepo na mifumo ya kukuza ubunifu na kuwezesha mfuko wa kufadhili wabunifu wadogo.

Aidha, Naibu Waziri amesema ushirikiano kati ya Wizara na Finland utakaoendelea unalenga zaidi katika Mafunzo ya Ufundi na Ubunifu na kwamba umekuja kwa wakati sahihi ambapo nchi inaelekea katika uchumi wa kati kupitia viwanda.

“Ili kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda ni lazima tuwe na rasilimaliwatu ya kutosha iliyoelimika na yenye maarifa na ujuzi kwa ajili ya viwanda na pia itakayoweza kujiajiri,” amesisitiza Ole Nasha.

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 23.05.2019

We are getting closer to Hilton’s 100th Birthday we invite you to book yourself room nights for an irresistible offer of 100USD per night for single/double occupancy.

VIJANA WAMKUNA WAZIRI HASUNGA WAENDELEA KUSHAWISHIKA NA KUJIUNGA KWENYE SEKTA YA KILIMO

$
0
0
Waziri wa Kilimo, Mhe Japheth Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua Jukwaa la Fikra la Mwananchi, lililofanyika katika ukumbi wa Milleinum Tower Jijini Dar es Salaam, tarehe 23 Mei 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo, Mhe Japheth Hasunga (Wa nne kulia) akifatilia mada mbalimbali mara baada ya kufungua Jukwaa la Fikra la Mwananchi, lililofanyika katika ukumbi wa Milleinum Tower Jijini Dar es Salaam, tarehe 23 Mei 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe Japheth Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua Jukwaa la Fikra la Mwananchi, lililofanyika katika ukumbi wa Milleinum Tower Jijini Dar es Salaam, tarehe 23 Mei 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe Japheth Hasunga (Wa nne kulia) akifatilia mada mbalimbali mara baada ya kufungua Jukwaa la Fikra la Mwananchi, lililofanyika katika ukumbi wa Milleinum Tower Jijini Dar es Salaam, tarehe 23 Mei 2019.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Kumekuwa na mwamko mkubwa na muitikio mahusiusi wa vijana kuingia katika shughuli za kilimo tofauti za siku za nyuma ambapo ilikuwa ni vigumu kukuta vijana wakishawishika kuingia katika kilimo. 

Takwimu za mwaka 2014 za Integrated Labour Force Survey chini zinaonesha kwamba vijana ni asilimia 56 ya nguvu kazi ya Taifa. Hivyo, wakihusishwa na kuwezeshwa ipasavyo kwa kuwavutia kwa kuzingatia mahitaji yao ya msingi katika kuwekeza katika kilimo, vijana hawa watalifikisha Taifa katika maendeleo chanya.

Waziri wa Kilimo, Mhe Japheth N. Hasunga (Mb) ameyasema hayo Leo Tarehe 23 Mei 2019 wakati akifungua Jukwaa la Fikra la Mwananchi, lililofanyika katika ukumbi wa Milleinum Tower Jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa Wizara ya Kilimo ina Mkakati wa Taifa wa Vijana wa kuwawezesha kushiriki katika kilimo kwa kuzingatia malengo makuu kumi (10) yakiwemo upatikani wa ardhi, upatikanaji wa mitaji, mafunzo ya ujasiriamali na uhakika wa masoko ya bidhaa zao. 

“Swali kubwa na msingi hapa ni je, sisi wadau wote kwa ujumla tunayatekeleza haya ili kuwavutia vijana kuweza kushiriki uwekezaji katika kilimo kupitia mnyororo wa thamani? Kwani tunakwama wapi?” Aliuliza Mhe Hasunga

Alisema kuwa ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya 2025 ya kufikia uchumi wa kati wa viwanda kunahitajika kilimo bora kitakachowezesha upatikanaji wa malighafi za kutosha kutumika katika viwanda. 

Vilevile, Kilimo chenye tija pia kitawezesha kipato cha wakulima kuongezeka na hivyo kuwezesha wananchi wengi kufikia kipato cha kati. “Nina uhakika ifikapo mwaka 2025 tunaweza kufikia uchumi wa kati na pengine na kuzidi kiwango hicho tulichojiwekea na hapo tutaiona Tanzania mpya yenye neema” Alisema

Mhe Hasunga alieleza kuwa Wizara ya Kilimo imeanza kufanya marekebisho ya Sera ya Kilimo na kutunga Sheria ya Kilimo, hatua ambazo zitaimarisha usimamizi na kutoa mwongozo wa maendeleo ya sekta ya kilimo kwa ujumla.

Kongamano hilo pla Jukwaa la Fikra au Mwananchi Thought Leadership Forum (MTLF) lilirushwa mubashara na Kituo cha Matangazo cha ITV pamoja na Radio One Sterio likiwa na lengo la kujadili masuala yanayowagusa Watanzania moja kwa moja kwa lengo la kuyatafutia suluhisho kwa pamoja kupitia mijadala iliyotolewa.

Alisema tangu majukwaa ya namna hiyo yalipoanza mwaka 2018 yakihusisha pia IPP Media (ITV, Radio na Capital Radio) masuala kadhaa yamejadiliwa ikiwa pamoja na mada za kuvutia kama vile "Magonjwa Yasiyoambukiza", mada ya "Tanzania ya Viwanda" na masuala ya Mazingira. Kupitia jukwa hili, Mamilioni ya Watanzania wamefaidika kwa kutoa na kusikiliza maoni katika Nyanja hizo kupitia mitandao ya jamii, televisheni, radio na magazeti. 

Mhe Hasunga alisisitiza kuwa Serikali haiwezi kufikia malengo yake bila kuwashirikisha wadau, aliwakaribisha wananchi na wadau wote kujadili na kutoa mawazo yatakayo iwezesha wizara ya kilimo kutoka katika hali iliyopo na kwenda hali nyingine ya kuboresha kilimo katika nyanja za masoko, upatikanaji wa pembejeo, wataalamu na zana bora za kilimo. 

Waziri Hasunga aliongeza kuwa Pamoja na umuhimu wa sekta ya kilimo katika kuchangia uchumi kwa asilimia kubwa zaidi kuliko sekta zingine, kuajiri watu wengi zaidi kuliko sekta nyingine, kuwezesha upatikanaji wa chakula cha kutosha hapa nchini na ziada kuuza nje ya nchi, kuchangia fedha nyingi za kigeni na kuwa moja ya sekta mama katika pato la Taifa na nguzo kuu ya uchumi, bado kilimo hakijaweza kukuza uchumi wetu kwa namna inavyostahili kutokana na umuhimu wake. 

“Tunatambua kihistoria kuwa nchi nyingi duniani zilianzia maendeleo kwenye mapinduzi ya kilimo, kwenda mapinduzi ya viwanda, huduma na baadaye teknolojia. Pengine hatuwezi kukwepa kufanya mapinduzi hayo ya kilimo hapa nchini. Tutakachoweza kufanya ni mapinduzi ya kasi zaidi kwa sababu tuna mifano mingi ya kuiga hapa duniani” Alikariiriwa Mhe Hasunga

How to INVEST in Tanzania: w/Mr. Mwambe, Dir. Tanzania Investment Centre

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK LEo

Polisi Ubungo waendesha mafunzo kwa madereva

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Mkuu wa kituo cha ukaguzi wa Magari katika kituo cha Mabasi Ubungo Terminal Ibrahim Samwix ameendesha mafunzo kwa madereva wa Magari makubwa kwa lengo la kufanya utambuzi wa gari n breki.

Akizungumza na Madareva hao jana jijini Dar Es Salaam.katika.kituo hicho cha Ubungo Terminal alisema mafunzo hayo ni endelevu kwa madereva ili kuwajengea uwezo wa kutambua mifumo ya gari jinsi linavyojiendesha.

Alisema mafunzo hayo ni bure na wataendelea kuyatoa Mara kwa Mara kwa madereva wa mikoani na nje ya nchi kwa lengo kupumbunguza au kuondoa ajari za barabarani.

Ibrahim alisema madereva watapewa vyeti baada ya kufanya mafunzo hayo Mara kwa Mara na yeye kama mkufunzi amefanya kazi hiyo kwa kujitoa zaidi."Nafanya kazi hii kwa kujitolea ili kuhakikisha madereva wanapata uelewa na kuepuka kugombana na askari wa barabarani Mara kwa Mara." Alisema Ibrahim.

Pia alitoa rai kwa madereva kuepuka kufanya mashindano barabarani kwani kufanya hivyo nimuhatarisha usalama wao na usalama wa abiria waliowabeba.

Ibrahimu alisisitiza kwa kuwataka maderava kuhakikisha wanashiriki kikamilifu mafunzo hayo ili waweze kupata uelewa zaidi na kufanya kazi yao kwa kujiamini zaidi.
 Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi cha Mabasi Ubungo wa Kikosi cha Usalama Barabarani Ibrahim Samwix akiendesha mafunzo kwa madereva ikiwa ni hatua ya kupunguza ajali za Barabarani zitokanazo na makosa ya kibinadamu.
 Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Ibrahim Samwix akionesha madereva namna ya matumizi ya Blake katika mafunzo hayo yaliyofanyika ofisini saa 10 alfajiri.
 Madereva wakipata elimu kabla ya kuanza safari
Mafunzo kwa madereva yakiendelea

UVIKASA WAKABIDHI AHADI YA MIPIRA KWA RC GAGUTI.

$
0
0

Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV - Karagwe 

Katika kuelekea Fainali ya Mashindano ya Mpira wa Miguu yanayozishirikisha Timu 16 za waendesha Bodaboda kutoka vituo mbalimbali ndani ya Manispaa ya Bukoba, maarufu kama JPM BODABODA CUP 2019 KAGERA, Umoja Wa Vijana Karagwe Saccos (UVIKASA), umekabidhi zawadi ya mipira 16 kwa Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti ikiwa ni juhudi za kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Mkuu huyo wa Mkoa wa Kagera katika kuwainua Vijana.

Zawadi hiyo imekabidhiwa Mapema Mei 23, 2019 na Mwenyekiti wa Saccos hiyo Yahya Salim Kateme, Kwa Mkuu wa Mkoa Mhe.Gaguti wakati alipofika katika Ofisi za UVIKASA kusalimia, akiwa katika ziara ya Kikazi Wilayani humor, ikiwa ni ahadi iliyotolewa na Mwenyekiti Yahya mapema baada ya kuanza kwa mashindano hayo, ambayo sasa yanaelekea ukingoni kwa michezo miwili iliyosalia ambayo ni mshindi wa tatu, na mchezo wa fainali, ambapo mipira hiyo itagawiwa kwa Timu zilizoshiriki.

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa Mwenyekiti Yahya ameeleza kuwa Kama vijana wamekuwa wakiona juhudi za Mhe. Gaguti toka alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, kwa jinsi ambavyo amekuwa bega kwa bega kuhakikisha Vijana wanajikwamua Kiuchumi katika masuala mbalimbali, na hivyo kupitia Mashindano ya JPM BODABODA CUP, wameona ni vyema kuunga mkono kwa kutoa hicho kidogo kiongozwe katika zawadi za Timu zinazoshiriki Ligi hiyo.

Kwa upande wake Mhe. Gaguti katika shukrani zake ameahidi kuendelea kutoa Ushirikiano kwa SACCOS hiyo pale itakapokwama, na pia amefurahishwa na ubunifu wa Mwenyekiti huyo ambaye licha ya SACCOS hiyo inayoendelea kutoa Mikopo ya Riba nafuu kwa ajili ya kuinua vijana Wilayani Karagwe, pia tayari wamebuni miradi mingine ikiwemo ya Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji, Mbuzi na Ng’ombe, mradi wa mikopo ya Pikipiki kwa Vijana.
 Mwenyekiti wa UVIKASA Ndg. Yahya Salim akikabidhi Sare ya Umoja wa Vijana Karagwe Saccos, kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Gaguti, kama ishara ya Kumbukumbu ya ujio wake katika Ofisi hiyo.
 Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe. Gaguti akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi za UVIKASA mjini Kayanga Wilayani Karagwe kwa ajili ya Kusalimia na Kuona Saccso hiyo hiyo inayojishughulisha na kuinua Uchumi wa Vijana Karagwe.
Pichani Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akipokea zawadi ya Mipira kutoka kwa Ndg. Yahya S. Kateme, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Karagwe Saccos (UIKASA) mara baada ya Kutembelea ofisi ya Saccos Hiyo, katikati ni Mkuu wa Wilaya Karagwe Mh. Godfrey Mheluka.

MREMBO WA DUNIA WA UANDISHI WA HABARI ATEMBELEA BUNGE

$
0
0
Mrembo wa Dunia wa Uandishi wa Habari (Miss World Journalism 2018) Nina Yevtushenko kutoka Nchini Ukraine atembelea Bunge na kujionea namna Vikao vinavyoendeshwa hii leo Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge)

RC GAGUTI AZINDUA RASMI MSIMU WA KAHAWA 2019 KAGERA

$
0
0

Anaadika Abdullatif Yunus, Michuzi Tv – Karagwe .

Wananchi na wakulima wa zao la Kahawa Mkoani Kagera wameombwa kufanya maandalizi mazuri, ikiwa ni pamoja na kuvuna kahawa iliyokomaa, kuikausha vizuri katika mazingira safi ili kuweza kupata daraja bora na bei bora katika Soko la Dunia.

Akizungumza na Wakulima pamoja na wadau wa Zao la hilo, katika uzinduzi wa msimu mpya wa Kahawa Wilayani Karagwe Mkoani Kagera, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, amewataka wakulima kuzingatia sana vigezo vya Kahawa bora ili kupata bei nzuri sokoni, ambapo kama Mkoa kwa Msimu uliopita Kahawa iliyokusanywa ni Kilo Milioni 58.9 sawa na asilimia 50 ya Kahawa yote ya Tanzania.

Katika salaam zake Mhe. Gaguti ametoa angalizo na kusisitiza kwa wale wote wanaofikiria kufanya magendo ya Kahawa kwa kuuza Nchi jirani, kutojihusisha na magendo hayo na kukumbusha kuwa tayari Serikali inazidi kuweka mazingira mazuri ya Bei nzuri ya zao hilo itakayomnufaisha Mkulima na kuinua kipato chake na Taifa kwa ujumla.

Katika kuhakikisha suala la magendo linakomeshwa hasa kuanzia msimu huu ulioanza Mei Mosi, Mhe. Gaguti ameanzisha kampeni ya ukomeshwaji magendo hayo, ambapo kwa yeyote atakayesaidia kukamatwa kwa Magendo hayo, atapewa 30% ya mauzo ya kahawa hiyo mara baada ya kutaifishwa na Kikundi kitapewa 50% ya mauzo ya Kahawa itakayotaifishwa. 

Awali Mkuu huyo wa Mkoa Mhe. Gaguti amekutana na Menjimenti ya KDCU pamoja na Bodi ya KDCU na kuweka mustakabari wa pamoja katika kuelekea kuanza kukusanya kahawa hiyo ambapo Tarehe rasmi ya kuanza kukusanaya kahawa itatangazwa Rasmi mwezi ujao. 

Uzinduzi wa Msimu Mpya wa Kahawa umefanyika rasmi katika Kijiji cha Kituntu Wilayani Karagwe, Mei 23, 2019 katika Shamba la mfano la Mkulima wa Kituntu Ndg. Kajoki, ambapo kijiji cha Kituntu wamekuwa kinara wa uzalishaji Kahawa kwa Msimu uliopita.
 Mkuu wa Mkoa Kagera, Mhe. Gaguti akiwa shambani kwa Mkulima Bwana Kajoki alievaa (kofia), pamoja na Mkuu wa wilaya Karagwe Mhe. Godfrey Mheluka wakishikiria moja kati ya miche ya mibuni ya zao la Kahawa Kama ishara ya Uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa Kahawa 2019 Mkoani Kagera.
 Pichani ni Kahawa inayoelekea katika hatua ya kukomaa tayari kuvunwa kwa ajili ya msimu mpya ulioanza Mei Mosi, kama ilivyokutwa shambani kwa Ndg. Mutawajjib Kajoki wa Kijiji cha Kituntu Wilayani Karagwe
 pichani ni RC Gaguti akizungumza na wananchi, wakulima na wadau wa Kahawa kijiji Kituntu kabla ya Uzinduzi wa Msimu mpya wa zao hilo la Kahawa Mkoani  Kagera

picha ya pamoja ya Mhe. RC Gaguti, Mkuu wa Wilaya Karagwe Mhe. Mheluka, Mwenyekiti wa CCM Karagwe Mhe. Mutafungwa pamoja na Menejimenti ya KDCU

Muamko Wa Elimu Kwa Viziwi Tabora Bado Upo Chini

$
0
0
Na Editha Edward-Michuzi TV,Tabora 

Wizara ya Elimu, sayansi na teknolojia imesema inaendelea kuweka mikakati itakayosaidia Kukabiliana na Changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwemo Viziwi ili waweze kupata haki ya msingi ya Elimu sawa na watu Wengine

Yamebainishwa hayo na naibu katibu Mkuu wa wizara ya Elimu sayansi na teknolojia katika semina maalumu ya kujadili Changamoto mbalimbali zinazowakabili Viziwi iliyoandaliwa na chuo Kikuu cha Askofu Mkuu MIHAYO mjini Tabora

Akizungumza katika semina hiyo naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu sayansi na teknolojia anayeshughulikia Elimu msingi Dk. Evamaria Semakavu amesema kuna haja ya kuweka mazingira wezeshi kwa wenye Ulemavu hasa Viziwi 

"Wapo maprofesa wasioona Lakini inapofika kwa Viziwi Tanzania bado kuna Changamoto na sisi kama wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Tanzania ambao tumepewa jukumu la kusimamia suala la sera viwango na Mustakabali mzima na Sekta ya Elimu bado tunasema uziwi bado ni tatizo inapokuja kwenye Elimu ambapo tunahitaji kukusanya wadau wote ili kufanikisha hili"Amesema Dk. Semakavu

Paul Luzoka ambae ni Askofu Mkuu wa Jimbo kuu Catholic Tabora amesema anaomba serikali iongeze juhudi katika kuhakikisha inawajali kipekee zaidi Watoto wenye Ulemavu wa Kusikia

Aidha mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amesema watu wa Tabora wanatakiwa kumshukuru Mungu kwa kuona kuwa wadau wa Elimu kwa pamoja wanakubali kuweka mazingira wezeshi kwa watu wenye mahitaji maalumu 

Hata hivyo Muamko wa Elimu kwa Viziwi Mkoani Tabora bado upo chini ni jukumu la wazazi, Wadau wa Elimu na jamii kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia watu hao wenye mahitaji maalumu ili kuwawezesha kuzifikiri ndoto zao.
 Ni mmoja kati ya watu wenye mahitaji maalumu akifuatilia jambo wakati wa mkutano.
Pichani ni naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dk. Evamaria Semakavu akizungumza na wadau katika semina Maalumu ya kujadili changamoto zinazowakabili Viziwi.

 Pichani ni wadau wa mkutano wa Elimu kutoka Sekta mbalimbali ndani na nje ya nchi

Balozi Seif akutana na Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama kutoka Nchini India

$
0
0
Na Othman Khamis/Rashida Abdi, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amekutana kwa mazungumzo ya Timu ya Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama kutoka Chuo cha Kijeshi Nchini India.

Timu hiyo iliyoongozwa na Balozi Mdogo wa India aliyepo Zanzibar Bwana T.B Barual ipo Tanzania kujifunza mambo mbali mbali ikiwemo masuala ya Historia ya Uhuru wa Tanganyika na Ukombozi wa Zanzibar.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ukumbi wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar Balozi Seif  aliushauri Uongozi wa Timu hiyo kuandaa utaratibu maalum wa kuwapatia Mafunzo ya muda mfupi ama mrefu Maafisa na Wapiganaji wa Vikosi Maalum vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema India na Tanzania ikiwemo Zanzibar kwa ujumla Zina historia  ndefu katika masuala ya Kisiasa, Uchumi, Utamaduni na Biashara ambayo kwa sasa upo umuhimu wa kuelekeza nguvu hizo katika masuala ya Ulinzi ili Amani iendelee kutawala ndani ya Ukanda wa Bahari ya Hindi.

Nao kwa upande wao Makamanda hao kutoka Chuo cha Kijeshi cha India wameelezea faraja yao kutokana na mapokezi mazuri waliyoyapata ndani ya Vikosi vya Ulinzi vya Tanzania pamoja na Wananchi wenyewe kwa ujumla.

Walisema ukarimu walioupata Tanzania na Visiwa vya Zanzibar kwa ujumla umewapa matumaini makubwa ya kuwa na fikra na muelekeo wa kuitambelea tena Tanzania katika kipindi chengine kijacho.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Makamanda wa Vikosi mbali mbali vya Ulinzi na Usalama Kutoka Nchini India hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Makamanda wa Vikosi mbali mbali vya Ulinzi na Usalama Kutoka Nchini India hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
 Baadhi ya Makamanda wa Vikosi vya India na wale wenyeji wao wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ} wakifuatilia maelezo ya Balozi Seif hayupo pichani wakati wa mazungumzo yao.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akipokea zawadi maalum kutoka kwa Makamanda wa Vikosi mbali mbali vya Ulinzi na Usalama Kutoka Nchini India.

 Baadhi ya Makamanda wa Vikosi vya India na wale wenyeji wao wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ} wakifuatilia maelezo ya Balozi Seif hayupo pichani wakati wa mazungumzo yao.
 Baadhi ya Makamanda wa Vikosi vya India na wale wenyeji wao wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ} wakifuatilia maelezo ya Balozi Seif hayupo pichani wakati wa mazungumzo yao.
 Baadhi ya Makamanda wa Vikosi vya India na wale wenyeji wao wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ} wakifuatilia maelezo ya Balozi Seif hayupo pichani wakati wa mazungumzo yao.
 Makamanda wa Vikosi vya India na wale wenyeji wao wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania { JWTZ} wakifuatilia maelezo ya Balozi Seif wakati wa mazungumzo yao.
 
 Balozi Seif  akiwa katika picha ya pamoja na Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama kutoka Nchini India mara baada ya kufanya mazungumzo nao Ofisini kwake Vuga.

Balozi Seif  akiagana na Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama kutoka Nchini India mara baada ya kufanya mazungumzo nao Ofisini kwake Vuga.
Balozi Seif  akiagana na Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama kutoka Nchini India mara baada ya kufanya mazungumzo nao Ofisini kwake Vuga.
Balozi Seif  akiagana na Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama kutoka Nchini India mara baada ya kufanya mazungumzo nao Ofisini kwake Vuga. Picha na OMPR – ZNZ.

RC CHALAMILA AYASHUKIA MAKAMPUNI YA UNUNUZI WA TUMBAKU.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akisaini kitabu maalumu kuashiria uzinduzi rasmi wa soko la Tumbaku Msimu wa 2018/19 Kimkoa katika Wilaya ya Chunya.
Mkuu wa Mkoa Mbeya Mh .Albert Chalamila akizugumza na wananchi wa Kijiji Cha Mtande Halmashauri ya Wilaya ya Chunya (Hawapo Pichani)Mara baada ya kuzindua soko la Tumbaku Msimu wa 2018/19, ambapo pia uliendana na uwekaji wa Jiwe la Msingi Chama cha Ushirika Cha Msingi Mtande Chunya 
Meckfason Moshi Mteuzi wa Tumbaku Mbeya na Iringa akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mbeya Mh .Albert Chalamila (Katikati) Mara baada ya kuzindua rasmi soko la Tumbaku msimu wa 2018/19 ,Kulia Mkuu wa Wilaya ya Chunya Merryprisca Mahundi.


SERIKALI Mkoani Mbeya imeyataka Makampuni ya ununuzi wa zao la tumbaku Wilayani Chunyani Mkoani Mbeya kuacha tabia ya kuwalalia wakulima wa zao hilo kwa kununua bei ndogo ambayo hainendani na gharana za uzalishaji.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Albert Chalamila wakati akizindua Soko la Tumbaku Kimkoa msimu wa 2018/2019 uzinduzi ambao umefanyika katika kijiji Cha Mtande Wilayani Chunya..

Amesema yapo baadhi ya makampuni ya ununuzi wa zao hilo la tumbuka yamekuwa yakiwalalia wakulima kwa kununua bei ndogo hasa kutokana na wakulima wengi kutokuwa na elimu pamoja uelewa mdogo kuhusu soko.

“inawezekana ndani ya makampuni hayo wapo wanaofaidika moja kwa moja wao binafsi na wala sio kuifadisha Kampuni wala wakulima kwa ujumla wake kwa makusudi huku wakijua kuwa ni uonezi kwa Mkulima ambapo unaweza kukuta hata watumishi wa serikali wapo .”Amesema 

Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa amekemea tabia ya baadhi ya wakulima kuuza tumbaku yao nje vyama vya ushirika kwasabau imekuwa mzigo kwa wanachama wengine kulipa madeni ya wakulima ambao wamekopa pembejeo za kilimo.

Pia ameitaka Kamati ya ulinzi na Usalama Halmashauri ya Wilaya Chunya pamoja na Chama cha Wakulima wa Tumbaku kuhakikisha inafnya msako wa wale wote wanajihusisha na tabia hiyo ya uuzaji wa tumbaku nje ya ushirika hata kama ni watumishi wa serikali.

Naye Mrajisi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Mbeya Angel Maganga amesema changamoto kubwa ni Kuondoka kwa Makampuni mengi ambayo yaliingia Mkataba kwa ajili ya uzalishaji wa zao hilo.

IUCEA AWARDS US$1 MILLION TO ESTABLISH INCUBATION CENTERS AT AFRICA CENTERS OF EXCELLENCE

$
0
0

Kampala, May 22nd, 2019:  The Inter-University Council for East Africa (IUCEA), a Regional Facilitation Unit for the World Bank-supported Africa Centers of Excellence for East and Southern Africa Project (ACE II) has completed the process of selection of Incubation Centers to be hosted at four of the Africa Centers of Excellence (ACEs). Each Center will receive a financial award of US$250,00, from a World Bank grant, as seed funds for the establishment of these regional Incubation Centers for East and Southern Africa. The ACEs selected to host the Incubation Centers are: 
  1. ACEESD – African Center of Excellence in Energy for Sustainable Development, University of Rwanda
  2. CREATES – Center for Research Advancement, Teaching Excellence and Sustainability in Food and Nutrition Security, Nelson Mandela African Institution of Science and Technology, Tanzania
  3. PHARMBIOTRAC – Center for Pharm-Bio Technology and Traditional Technology, Mbarara University of Science and Technology, Uganda
  4. PTRE - Center of Excellence in Phytochemicals, Textile and Renewable Energy based at Moi University, Kenya 
IUCEA received 15 proposals in response to a call that was issued in June 2018. The call invited any African Center of Excellence participating in the ACE II Project to submit proposals to host Incubation Centers through a co-financing arrangement in the four priority areas of the ACE II Project which include health, industry, agriculture, and education/applied statistics. The proposals were evaluated through a rigorous 3-step process by an international team of experts with extensive experience in business incubation, start-ups creation and successful commercialization of innovations and covered a diverse array of important topics -- such as energy for sustainable development, innovative drugs development, food and nutrition security, among others -- that are critical to the development of the region. 

In the evaluation process priority was given to ACEs that already had good enough products that may require improvement, promotion for wider markets and potential for business incubation, i.e. the process of nurturing of early stage ventures to success. Another key criterion considered was the capacity to source additional sources of co-financing for the Center, to ensure the long-term financial sustainability of the incubation center.

According to Dr. K. A. Appiah, a member of the Regional Steering Committee of the ACE II project who chaired the Independence Selection Panel, "the quality of the proposals that were submitted was quite high, and it was a difficult decision to have to select only 4 out of the 15 proposals submitted,” he said.  He added, “We hope that more funding can be made available by host governments and other institutions to fund other incubation centers. Our international team of experts were very impressed and eager to work with the selected ACEs to ensure that the selected incubation centers are successful in commercializing research innovations towards job creation and economic growth."

The selection panel recommended that although the fifth selected institution, Center for Innovative Drugs Development and Therapeutic Trials for Africa (CDT-Africa) could not be funded, the proposal “was one of the best and needed to be considered as a non-funded Incubation Center.”  

The IUCEA and the World Bank believe that such incubation centers will help build important linkages between academia and industry to help galvanize business growth in these priority areas that are critical to long-term growth and development of the region.

The World Bank believes strongly in the innovation potential of African research, as a key lever in the continued economic development of the continent, and these incubations centers will serve as important hubs where the impact of research can be transformed to commercial opportunities. We hope these centers will be the first among many to follow,” said Dr. Roberta Malee Bassett, Senior Education Specialist, World Bank and Task Team Leader for ACE II Project.

The Eastern and Southern Africa Higher Education Centers of Excellence (ACE II) Project supports the governments of Ethiopia, Kenya, Malawi, Mozambique, Rwanda, Tanzania, Uganda, and Zambia in strengthening selected African Centers of Excellence (ACEs) to deliver quality post-graduate education and build collaborative research capacity in the priority areas of (i) Industry, (ii) Agriculture, (iii) Health, (iv) Education, and (v) Applied Statistics.

For more information contact:
Agnes Asiimwe Okoth
Information and Communication Officer
Mob: +256-783 724-489
http://www.ace2.iucea.org/

Introducing "Kinaombeka" Official Video by The COCODO BAND

WAKULIMA WA ALIZETI WALIA NA MASHARTI YA MIKOPO KATIKA TAASISI ZA FEDHA

$
0
0
Kaimu katibu tawala anayeshughulikia masuala ya Kilimo,Uchumi na uwezeshaji mkoa wa Songwe ,Evance Kakulanga akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la siku tatu kwa wadau wa zao la Alizeti liliofanyika mkaoni Mbeya. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Programu ya kuendeleza Mifumo ya Masoko ya Kilimo Tanzania (AMDT) Michael Kirumba akizungumza wakati wa Kongamano hilo la siku tatu .
Baadhi ya washiriki wakifuatili mada zilizokuwa zikitolewa katika Kongamano hilo. 
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo wakichangia mada wakati wa mijadala katika Kongamano hilo. 
Washiriki wa kongamano la mafunzo lililoandaliwa na Programu ya kuendeleza Mifumo ya Masoko ya Kilimo Tanzania (AMDT) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kongmano hilo lililofanyika mkoani Mbeya. 



Na Dixon Busagaga wa Michuzi TV .

MASHARTI ya mikopo yanayotolewa na taasisi za fedha nchini kwa ajili ya wakulima yanatajwa kuwa kikwazo kwa baadhi ya wakulima wa zao la Alizeti nchini kushindwa kufanya kilimo chenye tija kwa zao hilo.

Moja ya Masharti hayo ni pamoja na wakulima kujiunga katika vikundi ili kurahisisha upatikanaji wa mikopo jambo ambalo wakulima wengi wa Alizeti wameshindwa kutumiza sharti hilo kutokana na kuamua kufanya shughuli za kilimo bila ya kuwa kwenye kikundi.

Kutokana na hali hiyo tayari Wakulima wa zao la Alizeti nchini wameshauriwa kujiunga katika vikundi ikiwa ni pamoja na kuanzisha vyama vya ushirika ambavyo vitasaidia katika kuanzisha mchakato wa kupata mikopo pamoja na pembejeo za kilimo kwa ajili ya zao hilo.

Ushauri huo umetolewa wakati wa Kongamano la mafunzo liloandaliwa na Taasisi ya Kuendeleza Mifumo ya Masoko ya Kilimo Tanzanina (AMDT),kongamano lililofanyika mkoani Mbeya likiwahusisha wadau mbalimbali wa zao la Alizeti kutoka mikoa 16 ya Tanzania bara.

Wakati wa mijadala katika kongamano hilo baadhi ya wakulima na wadau wa zao la Alizeti walisema kumekuwepo na changamoto ya upatikanaji wa mikopo kwa wakulima, hali ambayo wameitaja kuwa ni kikwazo katika kumsaidia mkulima mdogo wa zao hilo.

“Ni ukweli usiopingika wengi wetu licha ya kuvutiwa na kilimo cha Alizeti, kutokana na hamasa na elimu ambayo tumekuwa tukiipata kutoka kwa wadau wetu wa kilimo lakini tunashindwa kufanya kilimo chenye tija kutokana na uwezo wetu kuwa mdogo” alisema Anita Mwakyoma ambaye ni msindikaji wa mafuta ya Alizeti.

Alisema pamoja na ugumu wa upatikanaji wa mikopo, bado wakulima wengi wameshindwa kumudu bei za mbegu bora za Alizeti zinazopatikana sokoni na hivyo kulazimika kutumia mbegu zisizokuwa na ubora ambazo zimekuwa hazitoi mbegu za kutosha hali ambayo inayomfanya mkulima asinufaike na kilimo.

“Pamekuwepo na jitihada kubwa sana inayofanya na wadau wa kilimo na hasa maafisa ugani katika kutuhamasisha juu ya umuhimu wa matumizi ya mbegu bora ambazo hutoa mazao mengi wakati wa mavuno, lakini kutokana na gharama kubwa ya mbegu hizi wengi wetu tunashindwa.”alisema Mwakyoma.

Naye Mkulima wa Alizeti katika mkoa wa Songwe Sophia Mwanandenga aliziomba mamlaka zinazohusika na Kilimo hususani upande wa Pembejeo kuangalia namna zitakavyomsaidia mkulima kupata mbegu bora kwa bei nafuu. 

Akijibu hoja ya upatikanaji wa mikopo kwa wakulima wadogo, mwakilishi wa Benki ya Posta Nchini Tawi la Mbeya,Leonard Katamba alisema kwa muda mrefu mkulima mdogo amekuwa hakopesheki kutokana na kushindwa kufikia vigezo vilivyowekwa na baadhi ya taasisi za fedha.

“Kwa kutambua mchango wa mkulima katika ukuaji wa uchumi nchini, TPB tumeanzisha mpango maalumu wa kuwahamasisha wakulima kujiunga na vikundi, hatua ambayo itakuwa ni msaada kwa mkulima kuweza kupata mikopo pindi atakapokuwa anahitaji.”alisema Katamba.

“Kwa sasa tunawahamasisha wajiunge katika vikundi ili waweze kufikiwa kwa urahisi na wadau mbalimbali walioko katika mnyororo wa thamani wa zao la Alizeti , na tayari tumeanza kuyaona mafanikio katika maeneo ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Iringa na Mkoa wa Njombe”aliongeza Katamba . 
Alisema katika maeneo hayo tayari wakulima wamehamasishwa kuanzisha vikundi ambavyo hadi sasa licha ya kusubili mikopo kutoka benki tayari wameanza utamaduni wa kujiwekea akiba jambo ambalo linatajwa kma hatua njema.

“Hii kwetu ni hatua nzuri maana kwa kujiwekea akiba mkulima hata lazimika kuchukua mikopo bila sababu ya msingi maana tayari wanakuwa na akiba ambayo inaweza kuwasaidia katika hatua mbalimbali wakati wa kilimo.”alisema Katamba.

Kwa Upande wake mtafiti wa mbegu kutoka taasisi ya utafiti wa mbegu nchini (TARI) Samweli Mwenda alisema taasisi yao mpaka sasa inaendelea na tafiti mbalimbali ambazo zimelenga kumsaidia mkulima kupata mbegu bora na ambayo itakuwa na tija kwa mkulima wa Alizeti nchini.

“Sisi kama taasisi ya serikali jukumu letu ni kuhakikisha kuwa tunapata mbegu bora na zenye tija na mpaka sasa tunaendelea na tafiti mbalimbali ili kuleta mbegu mpya pamoja na kusafisha au kuboresha mbegu mbalimbali zilizopo sokoni ili mkulima aweze kupata mavuno mengi na yenye tija. alisema Mwenda.

Naye Meneja wa zao la Alizeti kutoka taasisi ya Taasisi ya Kuendeleza Mifumo ya Masoko ya Kilimo Tanzanina AMDT, Martin Mgallah amesema kuwa wao kama taasisi ambayo imekusudia kumuinua mkulima wa zao la Alizeti nchini itaendelea kwa kushirikiana na wadau wake kuhakikisha wakulima wanakuwa katika vikundi ili viweze kuwa na sifa ya kukopesheka hatua ambayo itakuwa ndio mkombozi kwa mkulima.

Taasisi ya Kuendeleza Mifumo ya Kimasoko Katika Kilimo Tanzania,AMDT imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali katika mikoa 15 nchi ambapo mpaka sasa zaidi ya wakulima 150,000 wamekwisha fikiwa kupitia mradi huu ambao lengo lake kubwa ni kumwezesha mkulima mdogo kupata tija katika kilimo hicho kwa kulima na kuzingatia kanuni bora za kilimo.
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images