Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

UTURUKI YAAMUA KUKUNUA MFUMO WA KUJILINDA URUSI

$
0
0
Na Ripota Wetu

WAZIRI wa Ulinzi nchini Uturuki Hulusi Akar amesema nchi yake inajiandaa kwa vikwazo vya Marekani baada ya kuendelea na mpango wake wa kununua mfumo wa kujilinda na makombora kutoka Urusi.

Katika taarifa iliyosambazwa jana Jumatano, Akar amesema wametuma watu wake nchini Urusi kupewa mafunzo ya kutumia mfumo huo wa S-400, yatakayoanza siku chache zijazo na kuendelea kwa miezi kadhaa.

Inadaiwa kuwa Ikulu ya White House ilitishia kuiwekea vikwazo Uturuki, chini ya sheria ya vikwazo inayozuia shughuli za kibiashara na sekta ya intelijensia na ulinzi ya Urusi.

Hata hivyo Marekani, inataraji kuiongezea mbinyo Uturuki, ambayo ni mshirika wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO ili kununua mfumo wa Marekani, lakini Uturuki imekataa kuachana na ununuzi wa mfumo huo wa Urusi.

CHANZO -DW SWAHILI

IGP SIRRO AFANYA ZIARA YA UKAGUZI KIWANJA CHA NDEGE TERMINAL III

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (wapili kushoto), akiongozwa na Mhandisi Msimamizi wa Ujenzi wa jengo la kiwanja cha ndege Terminal III, Barton Komba, wakati alipofanya ukaguzi wa kuona maendeleo ya mradi huo ambao hadi sasa umekamilika kwa asilimia 99.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akitoka kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanja cha ndege terminal III jijini Dar es salaam, ambapo IGP Sirro alisema Jeshi la Polisi limejipanga kuimarisha usalama kiwanjani hapo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akikagua gwaride aliloandaliwa kwa ajili yake wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika Kikosi cha Kutuliza Ghasia FFU Ukonga Dar es salaam, ambapo katika ukaguzi wake IGP Sirro alizungumza na maofisa na askari wa kikosi hicho.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati) akitoa maelekezo kwa maofisa wa Jeshi hilo wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika Kikosi cha Kutuliza Ghasia FFU Ukonga Dar es salaam, kulia ni kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas. Picha na Jeshi la Polisi.

Airtel yatangaza punguzo kabambe kwa wateja wake kupiga simu Mitandao Yote

$
0
0
 Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano na Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isaack Nchunda wakionyesha bango baada ya  ya Airtel kuzindua huduma mpya inayojulikana kama ‘TAMBA MITANDAO YOTE’, huduma hiyo ina lengo la kuwapa wateja wake suluhisho na uhuru wa kuchagua huduma ya mawasiliano ambayo ni nafuu zaidi wakati wowote hata kama mteja hajajiunga na bando. 
 Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam baada ya Airtel kuzindua huduma mpya inayojulikana kama ‘TAMBA MITANDAO YOTE’, huduma hiyo ina lengo la kuwapa wateja wake suluhisho na uhuru wa kuchagua huduma ya mawasiliano ambayo ni nafuu zaidi wakati wowote hata kama mteja hajajiunga na bando. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isaack Nchunda.



· Punguzo Pekee kutoka Airtel, uhuru wa kuongea

· Airtel sasa yawezesha wateja kupiga simu mitandao yote kwa 1TZS bila bando 

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeendelea kuwapa wateja wake huduma kabambe na za kipekee ikiwa ni jibu na itikio la mahitaji ya wateja wao kwa kuzindua huduma mpya inayojulikana kama ‘TAMBA MITANDAO YOTE’, huduma hiyo ina lengo la kuwapa wateja wake suluhisho na uhuru wa kuchagua huduma ya mawasiliano ambayo ni nafuu zaidi wakati wowote hata kama mteja hajajiunga na bando.

Huduma hii mpya ya TAMBA MITANDAO YOTE inakuja wakati muafaka na kuwapa wateja wa Airtel uhuru wa kupiga simu kwenda mtandao wowote nchini kwa punguzo la kiasi cha 1TZS tu kwa kila sekunde hata kama mteja hajajiunga na bando au kuishiwa bando.

Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isaack Nchunda akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuthibitisha kuzinduliwa kwa huduma hiyo ya TAMBA MITANDAO YOTE kwa niamba ya Mkurugenzi Mkuu, alisema ‘Tunayo furaha kubwa kuzindua huduma hii ambayo inawapa wateja wa Airtel uhakika wa kupiga simu kwenda mtandao wowote hapa nchini kwa gharama nafuu ya 1TZS kwa sekunde, tunaamini kupitia Tamba Mitandao Yote mteja wetu ataona thamani ya pesa yake na kufurahia uhuru wa kuongea wakati wowote. 

 Nchunda aliongeza kuwa wateja wa Airtel watafurahia pia punguzo la vifurushi vya intaneti kutoka TZS172 kwa MB mpaka TZS40 kwa MB ikiwa hajajiunga na bando lolote, pia mteja atafurahia kutumia TZS10 tu kwa MB ikiwa mteja alikuwa na kifurushi cha bando ambacho hakijaisha muda wake huku punguzo la gharama za ujumbe mfupi zikishuka kutoka TZS 69 kwa kila ujumbe mpaka TZS 10 kwa kila ujumbe’.

”TAMBA MITANDAO YOTE” ni huduma ambayo inampa mteja wa Airtel huduma bora, huru na nafuu kwani hata kama mteja atakuwa hajajiunga na bando yoyote bado anaweza kupiga simu kwenda mtandao wowote nchini kwa gharama ndogo ya 1TZS kwa sekunde. Tunaamini hii ni hatua kubwa sana kwenye sekta ya mawasiliano ambapo vikwazo vyote vimeondolewa na kuwapa Watanzania unafuu wa kupiga simu bila kujali kipato chake,’ alisema Nchunda.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema ‘Kulingana na taarifa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), idadi ya wateja wanaotumia simu za mkononi kwa kupiga kati ya mwaka 2017 na 2018 imeongezeka kutoka milioni 40 mpaka 43. Idadi ya wateja wetu imeongezeka pia kwa kipindi cha robo mbili za mwaka uliopita na hii imetokana na hudumu zetu zenye ubunifu na unafuu wa hali ya juu. Tunaamini huduma yetu itawawezesha wateja wetu kupata uhuru wa kupiga na kuongea ,wakiokoa fedha zao na kuziweka kwenye maendeleo ya kiuchumi. 

Airtel imekuwa mstari wa mbele kwenye kuleta huduma nafuu na zenye ubunifu ambazo zinakidhi matakwa ya wateja wetu kama vile huduma za kifedha, SMS, kupiga simu na hata kwenye huduma za intaneti.

‘Airtel inaendelea kukuza wigo wa mtandao wake nchini ambapo kwa sasa tuna maduka ya Airtel Money Branches zaidi ya 650 ambapo mteja anaweza kupata bidhaa na huduma mbalimbali kama za kifedha, kuunganisha kwenye vifurushi vya intaneti pamoja na kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole’, aliongeza Singano.

Utabiri wa Hali ya Hewa wa Siku Tano na Athari Zinazoweza Kutokea

MREMBO WA DUNIA WA UANDISHI WA HABARI ATEMBELEA BUNGE

$
0
0
Mrembo wa Dunia wa Uandishi wa Habari (Miss World Journalism 2018) Nina Yevtushenko kutoka Nchini Ukraine atembelea Bunge na kujionea namna Vikao vinavyoendeshwa hii leo Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge)

Uchaguzi Malawi: Kiongozi wa upinzani Lazarus Chakwera achukua uongozi wa mapema

$
0
0
Kiongozi wa upinzani nchini Malawi amechukua uongozi wa mapema katika uchaguzi mkuu uliofanyika mnamo mwezi Mei 21, kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo.

Lazarus Chakwera , kiongozi wa chama cha upinzani cha Malawi Congress Party MCP amejipatia kura 533,217 ambayo ni sawa na asilimia 37.65.

Anafuatiwa kwa karibu na rais wa sasa Peter Mutharika ambaye ana kura 524,247 ikiwa ni asilimia 37.1 huku makamu wa rais Saulos Chilima wa United Transformation Movement akiwa wa tatu na kura 293,978 ambayo ni asilimia 20.76.

Kiongozi wa chama cha zamani zaidi nchini Malawi Lazarus Chakwera amesema kuwa matokeo hayo ya mapema yanampatia uongozi katika uchaguzi huo.

Amesema kwamba kuna jaribio la baadhi ya watu wasiojulikana kuingilia matokeo ya uchaguzi huo yanayopeperushwa moja kwa moja katika kituo kikuu cha uchaguzi mjini Blantyre akiapa kwamba hatokubali uchakachuaji wowote.

Lakini tume ya uchaguzi nchini humo imetoa wito wa kuwepo kwa utulivu ikisisitiza kuwa ndio yenye uwezo wa kutangaza matokeo hayo.

Uchaguzi huo umekumbwa na ushindani wa karibu kati ya rais Peter Mutharika , makamu wake Saulos Chilima na Chakwera ambaye anakiongoza chama cha Malawi Congress party.

Katika uchaguzi wa 2014 , Chakwera alipoteza kwa karibu dhidi ya rais Mutharika na akashindwa kupinga uchaguzi huo mahakamani.

Tume ya uchaguzi ina hadi siku nane kutangaza matokeo hayo .

Hatahivyo imekiri kwamba inakabiliwa na changamoto za kiufundi katika utangazji wa matokeo hayo.Hatahivyo inasema kuwa ina imani kwamba itatoa matokeo yalio huru na haki.

Takriban raia milioni 6.8 wa Malawi walisajiliwa kushiriki katika uchaguzi huo kumchagua rais mpya , mbunge mpya na madiwani.

WAHARIRI MNA NAFASI KUBWA YA KUELIMISHA JAMII ILI KUPUGUZA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA-UNICEF

$
0
0
Shirika la kuhudumia watoto duniani (UNICEF) Tanzania limesema vifo vya watoto wachanga na mama wajawazito ni miongoni mwa changamoto inayozikumba nchi nyingi duniani, ikiwemo Tanzania.
Kufuatia hali hii, shirika hilo limesema wadau, wakiwemo wahariri ,waandishi wa habari na jamii kwa ujumla wana nafasi ya kuelemisha jamii, ili kusaidia mama wajawazito na watoto wachanga kuepuka vifo zisivyo vya lazima wakati na baada ya kujifungua.

Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Tanzania, Usiah Mkoma amesema katika semina ya wahariri, iliyoandaliwa na kampuni ya True Vision Production kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na UNICEF katika hoteli ya Regency iliyopo Mikocheni, Dar es Salaam kuwa wahariri kutoka vyombo vya habari nchini wanaweza kutumia nafasi zao na kalamu zao katika kusaidia kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kumsaidia mama mjamzito kwenda kliniki ili avuke salama yeye na mtoto atakayemzaa.

Umbali, hali duni ya miasha, ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi, mila na desturi potofu ni miongoni mwa sababu zinazopelekea vifo hivyo, kwa mujibu wa Agnes Mgaya, ambaye anakaimu nafasi ya uratibu wa Afya ya Mtoto mkoa wa Dar es Salaam. Mkoma amesema akina mama wajawazito 8,200 hufa kila mwaka wakati wakijifungua na asilimia 50 ya watoto walio chini ya miaka 5 hufa pia kila mwaka ndani ya mwezi mmoja baada ya kuzaliwa kwa changamoto mbalimbali.

Hivyo amesema wahariri wana wajibu wa kuelimisha jamii, kutumia kalamu zao kuelezea umuhimu wa kwenda kliniki wakati wa ujauzito na hata baada ya kujifungua.

“Muhimu ni kuhakikisha ndani ya siku 42 baada ya kujifungua, mama aendelee kuwa chini ya uangalizi wa wataalam wa afya ili waweze kukabiliana na changamoto zinazoweka kujitokeza kama vile kifafa cha mimba,’ amesema Nkoma.

“Tutumie vyombo vyetu vya habari kuchochea habari zinazowahusu mama mjamzito na mtoto mchanga ili kupunguza vifo vyao visivyo vya lazima,”
“Kwa kufanya hivyo, tutawafanya watunga sera na watendaji wachukue hatua za haraka”, amesema Mkoma.
“Mbali na vyombo vya habari mnavyoviongoza, pia nawaomba mtumie akaunti zenu binafsi za mitandao ya jamii kuwa sehemu ya kampeni ya kuzuia vifo zinavyotokea hapa nchini,” ameongeza.

Kwa mujibu wa takwimu, Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 duniani zinazoongoza katika vifo vya mama wajawazito na watoto vinavyotokana na changamoto mbalimbali za uzazi, zikiwemo kutokwa na damu nyingi wakati na baada ya kukifungua, ukosefu wa chanjo na umbali wa vituo vya afya katika baadhi ya maeneo.

Nchi nyingine ni India, Bangladesh, Nigeria, Jamhuri ya Watu wa Congo, Ethiopia, China na Palestina.
Amesema kutokana na takwimu kuonyesha vifo vipo juu, UNICEF Tanzania inashirikiana na wadau , ikiwemo serikali, taasisi na mashirika katika kuhakikisha mama na mtoto wanavuka salama katika kipindi cha uzazi.
Akizungumza katika semina hiyo, mmoja wa wahariri na waandishi wakongwe, Theophil Makunga amesema takwimu za vifo vya mama wajawazito na watoto zinatisha, hivyo ni muhimu waandishi wakatumia kalamu zao kuhakikisha vifo hivyo havitokei.

“Kazi ya waandishi wa habari ni kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, hivyo katika maeneo haya matatu, kuelimisha jamii ni kazi yetu,”
“Hivyo nadhani wajibu wa waandishi sio tu kuandika habari mbaya, bali pia wajibu kuandika habari zinazohusu maendeleo ya jamii na kutoa suluhisho la matatizo yanayojitokeza ili hatua zichukuliwe na jamii, watendaji na watunga sera,” amesema Makunga.

Pili Mtambalike, miongoni mwa waandishi wakongwe aliyewahi kushika nafasi mbalimbali katika Baraza la Habari Tanzania (MCT) amesema ana imani mtazamo wa vyombo vya habari katika kuandika habari zinazowahusu mama wajawazito na watoto utabadilika, baada ya semina hii.

“Siku zote, habari zinazohusu siasa, watu maarufu zimekuwa zikichukua nafasi sana katika vyombo vyetu vya habari, lakini, nina Imani, semina hii itasidia kubadilisha fikra za wahariri wengi na kutoa kipaumbele pia katika habari zinazowahusu mama wajawazito na watoto katika maeneo yao ya kazi,” amesema Mtambalike.
TVP, kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na UNICEF, imeandaa semina tatu kwa kada tofauti katika kuhakikisha jamii inaelimishwa juu ya umuhimu wa kuwasaidia mama wajawazito na watoto wavuke salama.

Takwimu zinaonesha asilimia 50 ya watoto walio chini ya miaka 5 nchini Tanzania hufariki ndani ya mwezi mmoja baada ya kuzaliwa. Wanawawake wajawazito 8,200 hufariki kwa mwaka wakati wakijifungua.
Moja ya malengo ya Kampeni ya ‘Jiongeze Tuwavushe Salama’ ni kupunguza vifo vya wanawake wajawazito, kutoka 556 mpaka 292, kama sio kumaliza kabisa ifikapo mwaka 2020.

Pia kampeni imeweka malengo ya kuokoa vifo vya watoto wachanga kutoka 43, mpaka 25 kwa vizazi hai 1,000 ifikapo mwakani.
Baada ya semina ya wahariri, kesho (23/04/2019) kutakuwa na semina itakayohusisha viongozi wa dini katika ukumbi wa hoteli ya Regency, iliyopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam. Semina ya mwisho itafanyika Ijumaa, ikiwahusisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini.

Kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama ni kampeni ya Taifa, iliyozinduliwa na Makamu wa Rais, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan mjini Dodoma, mwezi Novemba mwaka jana, ukiwa ni mwongozo kutoka Wizara ya Afya kwa wakuu wote wa mikoa Tanzania Bara kuchukua hatua za kuzuia vifo vya mama na mtoto katika mikoa yao.

Madhumuni ya Serikali ni kuhamasisha viongozi wake, viongozi wa dini, mashirika yasiyo ya serikali, wadau wa maendeleo, watoa huduma za afya, familia na jamii kwa ujumla kuanza kuchukua hatua za kuzuia vifo hivyo.
Mtaalam wa Mawasiliano kutoka UNICEF Tanzania, Usiah Nkoma akitoa mada katika semina ya wahariri iliyofanyika katika Hoteli ya Regency kwa ajili ya kusaidia kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama yenye lengo la kuzuia vifo vya mama wajawazito na watoto.

 Kaimu Mratibu Wa Afya ya Mtoto katika mkoa wa Dar as Salaam, Agnes Mgaya akitoa mada katika semina ya wahariri juu ya kusaidia kuokoa Vigo vya mama na mtoto.
 Mmoja wa wahariri, Peter Nyanje akichangia katika semina ya wahariri  iliyokuwa inahusu kusaidia kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama yenye lengo la kuzuia vifo vya mama wajawazito na watoto.
 
 Baadhi ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika semina iliyokuwa inahusu kusaidia kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama yenye lengo la kuzuia vifo vya mama wajawazito na watoto.
Mtaalam wa Mawasiliano wa UNICEF Tanzania Usiah Nkoma, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa semina iliyokuwa inahusu kusaidia kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama yenye lengo LA kuzuia vifo vya mama wajawazito na watoto.

KITENGO CHA LISHE WIZARA YA AFYA ZANZIBAR CHAWATAKA WANAHABARI NA WALIMU WA MADRASA KUSAIDIA KUHAMASISHA JAMII

$
0
0
Wilaya ya Kaskazini B imetajwa kuwa Wilaya iliyo chini zaidi katika kutekeleza zoezi la kuwapatia Watoto wao Vitamin A na Dawa za Minyoo hivyo juhudi zinahitajika zaidi kuondosha tatizo hilo.

Afisa Lishe Kitengo cha Lishe wa Subira Bakari Ame amebainisha hayo wakati akitoa takwimu za zoezi lililofanyika Mwezi Disemba mwaka jana kwa Waandishi wa habari na Wadau wengine wa afya katika ukumbi wa Hospital ya Wagonjwa wa akili Kidongo chekundu.

Amesema hali hiyo inatokana na sababu mbali mbali ikiwemo uelewa mdogo wa elimu ya afya na ushirikiano hafifu wanaoupata kutoka kwa Wadau tofauti wa Wilaya hiyo.

Hivyo amesema ipo haja kufanyika kwa mjadala wa pamoja kubaini chanzo cha tatizo ili kuifanya Wilaya hiyo kufikia viwango sawa na Wilaya nyingine.

Kwa upande wao washiriki wa Mkutano huo walipedekeza kutengenezwe Bajeti maalum ya kuongeza elimu ya Afya kwa Wilaya hiyo.

Aidha wamesema ipo haja ya kuishirikisha jamii yote ikiwemo Wazee na Walimu wa Madrsa badala ya kuwaachia Masheha na Wajumbe wao kusimamia zoezi la kuhamasisha jamii kutekeleza zoezi hilo.
 Afisa Lishe Kitengo cha Lishe Wizara ya Afya Subira Bakari Ame akitoa takwimu za utoaji wa Vitamin A kwa watoto na dawa za minyoo pamoja na mikakati ya kuboresha zoezi la mwezi wa sita katika Mkutano uliofanyika Kitengo Shirikishi cha mama na mtoto Kidongochekundu.
 Maalim wa Madrasatul Nuru Imani ya Taveta Bi. Asha Uwesu Abdalla akichangia kitu katika Mkutano wa kutafuta nyia sahihi yakuwahamasisha wakina mama kuwapeleka watoto wao kupewa matone ya vitamin A.
 Afisa Lishe Wilaya ya Mjini Fatma Ally Said akitoa elimu ya matone ya Vitamin A kwa Wandishi wa Habari na walimu wa Madrasa ili kusaidia kutoa elimu hiyo kwa wanachi. Picha na Makame Mshenga.

RAIS DKT.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR IKULU NDOGO KIBWENI ZANZIBAR

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza wakati wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi, wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, uliofanyika Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar, 22-5-2019.
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Mohammed Aboud Mohammed, akiwasilisha maelezo ya Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa kipindi cha mwezi wa Julai 2018 hadi March 2019 wa Wizara yake uliofanyika Ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar leo.22-5-2019 kulia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na kushoto Naibu Waziri Mhe. Mihayo Juma N'hunga.
 WATENDAJI wa Idara za Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, wakifuatilia mkutano huo wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa kipindi cha mwezi Julai 2018 hadi Marchi 2019, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Ndg.Seif Shaban Mohamed,akiwasiliza ripoto ya Matumizi na Mapato ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, katika mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Ofisi hiyo, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MNapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiongoza Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa kipindi cha mwezi Julai 2018 hadi March 2019, Ofisi ya Makamu wa Pili wac Rais wa Zanzibar, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni leo,22-5-2019, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na Ikulu)
RAIS WA ZANZIBAR DKT.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR IKULU NDOGO KIBWENI ZANZIBAR

WATAKIWA KUCHANGIA ASILIMIA 10 KWA AJILI YA MFUKO WA WANAWAKE ,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAMAVU

$
0
0
Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Iringa, Lucas Kambelenje akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi wakati wa kikao maalum cha baraza la madiwani wa halmashauri Mji wa Mafinga wakijadili hoja za CAG
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Francis Maghembe akizungumza wakati wa kikao maalum cha baraza la madiwani wa halmashauri Mji wa Mafinga wakijadili hoja za CAG 






NA FREDY MGUNDA,MAFINGA.

MKUU wa mkoa wa Iringa, Ally Hapi ameiagiza Halmashauri ya Mji Mafinga kuhakikisha wanatenga na kuchangia asilimia 10 ya fedha zinazotokana na mapato ya ndani kwa ajili ya Mfuko wa Wanawake ,Vijana na watu wenye Ulemamavu. 

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa, Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Iringa, Lucas Kambelenje wakati wa kikao maalum cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 37A(1) cha Sheria ya Fedha za Serika|i za Mitaa (marekebisho 2018) sura ya 290, suala la kuchangia asi|imia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kukopesha vikundi vya Wanawake, vijana na Watu wenye ulemavu vilivyosajiliwa ni la Kisheria kuanzia Julai, 2018. 

Alisema kuwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mwaka 2017/2018, inaonesha kuwa, Halmashauri ya Mji Mafinga ilichangia kwenye Mfuko huo ,kiasi cha shilingi milioni 90,000,000 tu badala ya shilingi 250,088,994 zilizopaswa kutolewa kutokana na kiasi cha shilingi 2,500,889,940 zilizokusanywa kama mapato ya ndani ya Halmashauri. Hivyo, halmashauri ilishindwa kuchangia shilingi 160,088,994 katika Mfuko wa Wanawake na Vijana 

Kambelenje alisema kuwa matumaini serikali kwa halmashauri hiyo ni kutumia ushirikiano mzuri uliopo kuhakikisha kuwa, hoja zote za ukaguzi zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na zile za Mkaguzi ndani, zinashughulikiwa ipasavyo, ili ziweze kuhakikiwa na kufungwa kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na maelekezo ya Serikali. 

“Naamini kuwa, mafanikio haya mazuri yametokana na uwepo wa ushirikiano Mzuri baina yenu Waheshimiwa Madiwani, Watendaji na Wadau mbalimbali wa Halmashauri. Wito wangu kwenu ni kuwa, muendelee kudumisha ushirikiano huu, ili Halmashauri iendelee kupata Hati Safi katika kaguzi zote kila mwaka na pia kuendelea kutoa huduma bora kwa Wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga.”

alisema kuwa licha ya hoja ya kutenga fedha kwa ajili ya wanawake, vijana na walemavu kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizoishia tarehe 30 Juni, 2018, Halmashauri ya mji Mafinga ina jumla ya hoja 38 ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi.

Aidha alitoa wito kwa Halmashauri iweze kuwa na mifumo bora na imara udhibiti wa ndani, itakayosaidia kulinda na kusimamia ipasav matumizi sahihi ya rasilimali na mapato ya Halmashauri, naiagi Halmashauri ihakikishe kuwa, inakiimarisha kitengo chake Ukaguzi wa ndani kwa kukiwezesha kuwa na wataalam ‘ kutosha na vitendea kazi vya kutosha, ili kiweze kutekele majukumu yake ipasavyo kwa wakati na ukamilifu unaostahili. 

Aliitaka halmashauri ihakikishe kuwa, inasimamia mali zote kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali iliyopo ikiwa kwa kwa mujibu wa agizo la 45(1) la Memoranda ya Fedha za Serikali la Mitaa ya Mwaka 2009 ambayo inaeleza kuwa kuwa, Mali zote ambazo hazitumiki hususan zilizochakaa zitambuliwe na kuwasilishwa kwenye Kamati ya Fedha pamoja na Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupata idhini ya kutumwa Wizara ya Fedha ili kuundiwa Bodi ya kuvikagua kwa hatua ya kuvifuta na kuviondosha kama kanuni ya 254 ya kanuni za fedha za mwaka 2001 inavyoelekeza.

Kambelenje aliongeza kuwa halmashauri ihakikishe kuwa, inaweka utaratibu wa kulipa madeni yanayofikia kiasi cha shilingi milioni 510,042,225 ambayo yametokana na madai ya wakandarasi, watoa huduma mbalimbali na watumishi kama ilivyobainishwa katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2017/2018. 

“Naagiza kuwa, madeni yote yanayostahili kulipwa na fedha za makusanyo ya ndani yahakikiwe na yalipwe mara moja na yale yanayostahili kulipwa na Serikali Kuu, Halmashauri ifanye ufuatiliaji kuhakikisha fedha hizo zinatolewa na kulipwa”” alisema

Aidha, alitoa wito kwa Halmashauri kuacha kulimbikiza au kuongeza madeni hivyo ni vema malipo ya huduma zinazotolewa kwenye Halmashauri ihakikishe kuwa fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo zinatumika baada ya kupata idhini ya kamati ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo.

Akizungumzia hoja hizo makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Francis Maghembe alisema kuwa watahakikisha hoja zote zinafanyiwa kazi ili kusijitokeze hoja nyingine au kuongezeka kwa madeni ambayo halmashauri inadaiwa.

BALOZI WA SWEDEN NCHINI AFIKA OFISINI KWA SPIKA KUMUAGA

$
0
0
 Balozi wa Sweden nchini Bi. Florence Tinguely Mattli (aliyesimama) akitambulishwa Bungeni na Spika wa Bunge Job Ndugai (hayupo pichani). Balozi huyo alifika Ofisini kwa Spika kumuaga baada ya kumaliza muda wake.
 Spika wa Bunge Job Ndugai akifurahia jambo na Balozi wa Sweden nchini Bi. Florence Tinguely Mattli aliyefika Ofisini kwake kumuaga baada ya kumaliza muda wake.
  Spika wa Bunge Job Ndugai akimueleza jambo Balozi wa Sweden nchini Bi. Florence Tinguely Mattli aliyefika Ofisini kwake kumuaga baada ya kumaliza muda wake .
 Spika wa Bunge Job Ndugai katika picha ya pamoja na Balozi wa Sweden nchini Bi. Florence Tinguely Mattli aliyefika Ofisini kwake kumuaga baada ya kumaliza muda wake.
Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai akisalimiana na Balozi wa Sweden nchini Bi. Florence Tinguely Mattli aliyefika Ofisini kwa Spika kumuaga baada ya kumaliza muda wake. PICHA NA BUNGE

UJENZI WA FLY OVER UBUNGO WAENDELEA KWA KASI

$
0
0
 Nguzo ya Katikati ya Makutano ya Barabara ya Morogoro, Sam nujoma na Mandela Ubungo, ikiwa tayari imesimama kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa barabara za juu ambazo zitasaidia kupunguza msongamano katika jiji la Dar es Salaam.
 Sehemu ya Nguzo za upande wa pili ya barabara ya Mandela pamoja na mitambo ya ujenzi yakionekana katika picha .
Wafanyakazi wa kampuni ya Ujenzi ya China Civil Inayojenga barabara za juu katika Makutano ya Ubungo 

TOZO ZINAZOKWAMISHA BIASHARA NCHINI KUFUTWA-MAJALIWA

$
0
0
*Ni baada ya Serikali kusikia kilio kutoka kwa wafanyabiashara

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeanza jitihada za kufuta tozo zote ambazo zinakwamisha mazingira ya ufanyaji wa biashara nchini zikiwemo za kwenye pembejeo ili kuwawezesha wafanyabiashara kuzifikisha hadi ngazi ya kijiji kwa wakulima.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Mei 23, 2019) Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Madaba, Kizito Mhagama katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu. Mbunge huyo alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kupunguza tozo kwa maduka yanayouza pembejeo ili kumwezesha mkulima kupata pembejeo.

Waziri Mkuu amesema Serikali imepokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo na wauzaji wa pembejeo juu ya tozo mbalimbali katika uendeshaji wa shughuli nzima wa biasharazao.

“Serikali imesikia vilio vyenu na sasa inafanya mapitio ya tozo hizo na itakapofikia hatua nzuri itawajulisha na kuwashirikisha kujua ni aina gani ya tozo ambayo itaondolewa au kuibadilisha ili muendelee kufanya biashara zenu katika mazingira rahisi.”

Waziri Mkuu amesema kazi kubwa inayofanywa na Serikali kwa sasa ni kufanya mapitio ya tozo zote kuanzia kwa wakulima hadi kwa wafanyabiashara na kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya biashara nchini, ikiwemo ya pembejeo ili kuzifikisha kiurahisi kwa wakulima.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kwamba tayari Mawaziri wa kisekta wenye dhamana ambao wana tozo mbalimbali kwenye wizara zao zinazokwamisha ufanyaji biashara katika mazingira rafiki wameshakutana kwa ajili ya kujadili namna ya kulipatia ufumbuzi suala hilo.

“Hata juzi nilikuwa na mawaziri hao kupata taarifa zao kwa pamoja kuona maeneo yote waliyoyapitia na tozo zote zinazokusudiwa kupitiwa upya na kazi hiyo ikikamilika watakutana na Kamati ya Bajeti ya Bunge, Wizara ya Fedha ili kuona namna nzuri ya kuondoa tozo hizo. Lakini baadaye suala hilo litaenda kwenye mamlaka inayotoa ridhaa ya kuondoa au kupunguza tozo.”

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema miradi mingi ya maji ambayo inatekelezwa kwenye maeneo mbalimbali nchini baadhi yake haitekelezwi kwa viwango vilivyokusudiwa, hivyo haiwiani na thamani halisi ya kiasi cha fedha kinachotolewa.

Hata hivyo Waziri wa Maji wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2019/2020 alieleza hatua mbalimbali zilizochukuliwa dhidi ya miradi yote ambayo haiwiani na kiasi cha fedha kilichotolewa pamoja na hatua zilizochukuliwa dhidi ya miradi yote.

“Moja kati ya hatua ambazo amezifanya ni pamoja na kuunda timu inayopita kukagua miradi yote nchini na kujiridhisha kama matengenezo yake yanakidhi thamani ya fedha iliyotolewa katika mradi huo na kama haukidhi hatua kali zinachukuliwa kwa wahusika.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la mbunge wa Korogwe Mjini Mary Chatanda aliyetaka kujua Serikali kama ipo tayari kuchunguza na kuchukua hatua kwa watendaji walioshindwa kusimamia miradi ya maji na kuisababishia hasara pamoja na wananchi kukosa huduma waliyokusudiwa.

RIDHIWANI KIKWETE AKABIDHI MSIKITI WA MASJID SWAFIYA, KITONGOJI CHA MAGOME, KATA YA PERA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE
MBUNGE wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani ,Ridhiwani Kikwete amekabidhi msikiti wa Masjid Swafiya uliojengwa kwa msaada wake kwa kushirikiana na Taasisi ya Miraji Islamic Center.

Akizungumza wakati akikabidhi msikiti huo, kata ya Pera kitongoji cha Magome ,aliwataka waislamu ,kutumia nafasi ya kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kuiombea serikali pamoja na kuwaombea viongozi mbalimbali ili waendelee kuwaletea maendeleo.

Aidha mbunge huyo alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ,kwa juhudi zake anazozifanya katika utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa ufanikishaji wa maendeleo kwa wananchi wanyonge na kuinua uchumi.

Hata hivyo ,Kikwete alisisitiza ,mwezi huu wa Ramadhani ni mwezi ambao tunasisitizwa kusoma Qur'an kwasababu mwezi huu wa Ramadhan ndio Qur'an ilimshukia Mtume ili uwe muongozo kwa watu hapa duniani, pia usomaji huo unamalipo makubwa kwa Mungu.

"Kipindi kama hiki cha mfungo tunatakiwa kumcha mungu na kusaidia masikini kwani funga inamaana kubwa sana ,hivyo kila muislamu aliyefanikiwa kupata nafasi hapa duniani ni lazima amsaidie mwenzake japo futali"alisema Kikwete.

Nae Shekhe Mohammed ,alimpongeza mbunge huyo kwa kutambua thamani ya uislamu na hata kujitolea kwa ari na mali katika ufanikishaji wa ujenzi wa msikiti huo .

Hivyo anamwakikishia Kikwete kuwa wao kama viongozi wa dini wataendelea kuliombea Taifa ili liondokane na majanga ya aina yeyote

NEC yawataka wasimamizi wa uchaguzi kuzingatia katiba na sheria kusimamia uchaguzi mdogo kata 32

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Mbarouk Salum Mbarouk amewataka  wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba na Sheria zinazosimamia uchaguzi nchini katika kusimamia uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 32 unaotarajiwa kufanyika Juni 15 mwaka huu.

Jaji Mbarouk ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya usimamizi wa uchaguzi kwa wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kutoka kata 32 na halmashauri 20 za Tanzania Bara zinazotarajia kushiriki katika uchaguzi huo, yanayofanyika jijini Dodoma.
Alisema pamoja na baadhi ya wasimamizi kuwa na uzoefu katika kusimamia chaguzi mbalimbali, aliwasisitiza kuzingatia maelekezo watakayopewa na Tume katika kusimamia uchaguzi huo badala ya kusimamia kwa mazoea kwani NEC imewaamini kuwa wanaweza kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia matakwa ya Katiba na Sheria.

“Ndugu washiriki mnatakiwa kutambua kuwa mmeaminiwa na kuteuliwa kwa sababu mnao uwezo wa kufanya kazi hii jambo la muhimu ni kujiamini na kujitambua na kwamba mtapaswa kuzingatia sheria, miongozo, kanuni na maelekezo yanayotolewa na Tume kwa ajili ya kuendesha na kusimamia chaguzi” alisema Jaji Mbarouk.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Dkt. Athumani Kihamia aliwataka wasimamizi hao wa uchaguzi kuwepo muda wote wakati wa kutekeleza majukumu ya uchaguzi na hata pale inapotokea dharura wahakikishe anakuwepo msimamizi atakayetekeza majukumu yao.
“Ni vyema mkafahamu kwamba kipindi hiki ambacho mmeshateuliwa na kuapa kuwa wasimamizi wa uchaguzi, wewe unakuwa mtumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa muda huo.Kwa hiyo ni vyema ukawa ofisini muda wote ukiondoa dharura” alisema Dkt. Kihamia.

Alifafanua kuwa suala hilo limetolewa muongozo katika Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2015 sehemu ya 4 (1), watendaji wote wa uchaguzi katika kipindi cha uteuzi wa wagombea, katika kipindi cha upigaji kura na katika hatua yoyote ya mchakato wa uchaguzi.
Katika mafunzo hayo, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi walikula kiapo cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa mbele ya Hakimu Arnold Kirekiano ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa kuhusu hatua mbalimbali za mchakato wa uchaguzi.
 Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R ) Mbarouk Salum Mbarouk wakati wa kifungua mafunzo ya usimamizi wa uchaguzi kwa wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kutoka kata 32 na halmashauri 20 za Tanzania Bara zinazotarajia kushiriki katika uchaguzi huo, yanayofanyika jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia akizungumza wakati wa kifungua mafunzo ya usimamizi wa uchaguzi kwa wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kutoka kata 32 na halmashauri 20 za Tanzania Bara zinazotarajia kushiriki katika uchaguzi huo, yanayofanyika jijini Dodoma.
 Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wakila kiapo mbele ya Hakimu Arnold Kirekiano wakati wa kifungua mafunzo ya usimamizi wa uchaguzi kwa wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kutoka kata 32 na halmashauri 20 za Tanzania Bara zinazotarajia kushiriki katika uchaguzi huo, yanayofanyika jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R ) Mbarouk Salum Mbarouk (wa pili kushoto) akiwa na Wajumbe wa Tume Jaji (Mst.) Mary Longway na Mhe. Asina Omari (kulia) wakiwa an Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia (kushoto) wakifuatilia mada. Picha na NEC

WAZIRI MKUU AZUNGUMZA NA MABALOZI WA FINLAND NA SWITZERLAND NCHINI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Finland nchini,  Mhe. Pekka Hukka kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Mei 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Finland nchini, Mhe. Pekka Hukka, ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Mei 23, 2019. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Switzerland nchini, Mhe.  Florence Tinguely Mattli kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma, Mei 23, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Switzerland nchini, Mhe. Florence Tinguely Mattli, ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Mei 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Watoa Huduma wa NHIF achene udanganyifu- Gambo

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo akifungua Mkutano wa Wadau wa NHIF, Mkoa wa Arusha.

Na Mwandishi Wetu, Arusha

SERIKALI imewataka Watoa Huduma waliosajiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kuachana na udanganyifu katika utoaji wa huduma kwa wanachama wake kwa kuwa jambo hilo ni kurudisha nyuma maendeleo ya Mfuko ambao ni nguzo kubwa katika utoaji wa huduma za matibabu.

Akifungua kikao cha Wadau wa NHIF, Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo amesema kuwa udanganyifu katika huduma ni adui mkubwa wa uimarishaji wa chombo hicho ambacho kwa sasa kinahudumia wananchi wengi na wanaohitaji huduma ambazo gharama zake ni kubwa.

“Niwaombe sana wadau wote hususan wanachama wa Mfuko, ni vyema kila mmoja kwenye nafasi yake akawa mlinzi wa huduma anazopata ili Mfuko huu uwe imara zaidi na uendelee kuhudumia wananchi, mimi binafsi nikiri tu kwamba bila ya kuwa na kadi ya NHIF nisingeweza kumudu gharama za matibabu, nimemuuguza Mama yangu na alihitaji matibabu yenye gharama kubwa lakini kwa kuwa na kadi ya NHIF ilinisaidia kwa kiasi kikubwa sana, hivyo ili Mfuko huu uendelee kuwepo ni lazima sote kwa pamoja tuulinde,” alisema Bw. Gambo.

Kwa upande wa watoa huduma aliwataka kuwa wakweli na kuwa wazalendo katika vipimo na dawa wanazowaandikia wanachama ili Mfuko uweze kulipa gharama halisi na sio kulipa fedha ambazo huduma zake hazikuwa sahihi.

“Lengo la Serikali inayoongozwa na Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli ni kuona kila wilaya nchini inakuwa na Hospitali na kata inakuwa na kituo cha Afya na Kijiji kinakuwa na Zahanati ili upatikanaji wa huduma za matibabu uwe rahisi na bora zaidi na kwa kutumia mfumo wa Bima ya Afya wananchi watakuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wote,” alisema Bw. Gambo.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne Makinda amesema kuwa Mfuko umejipanga kuhakikisha mpaka ifikapo mwakani zaidi ya asilimia 50 ya Watanzania iwe inahudumiwa na Mfuko na kwa upande wa huduma, Mfuko umejipanga kuhakikisha wanachama wake wanapata huduma katika maeneo yao na kwa ubora unaotakiwa.

Awali akizungumza kwenye mkutano huo Mkurugenzi wa NHIF, Bw.Bernad Konga amebainisha kuwepo kwa mifumo mizuri ya udhibiti wa udanganyifu ambayo mpaka sasa imeleta matokeo makubwa kwa kuokoa zaidi ya shilingi Bilioni 4 ambazo zingeweza kulipwa kutokana na vitendo vya udanganyifu vya baadhi ya watoa huduma.
Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Mama Anne Makinda akitoa salaam za Bodi kwa wadau wa Mfuko huo.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Bernard Konga akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji ya Mfuko kwa wadau wake.
Meneja wa NHIF Mkoa wa Arusha Bw. Isaya Shekifu akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Mkoa.
Wadau wa NHIF wakifuatilia taarifa mbalimbali za Mfuko.
Sehemu ya Wadau wa Mfuko wakiwa kwenye mkutano huo.
Sehemu ya Wadau wakifuatilia uwasilishwaji wa Mada.
Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu Dkt. David Mwanesano (kulia) akiwa na Meneja Uhusianoi wa Mfuko Bi. Anjela Mziray.

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA NCHI OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akijiandaa kuaza Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi,wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ kwa kipindi cha mwezi wa Julai 2018 hadi March 2019, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akizungumza wakati wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar, kulia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum, Haji Omar Kheri.
 WAKUU wa Vikosi vya Idara Maalum vya SMZ wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, wakati wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai 2018 hadi March 2019, kwa  Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar leo, 23-5-2019.
 KATIBU Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bi. Radhia Rashid Hussein Haroub, akisoma maelezo ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa kipindi cha mwezi Julai 2018 hadi March 2019, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar leo.23-5-2019.
 MAOFISA wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, wakifuatilia  mkutano huo, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akizungumza katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar leo,23-5-2019.
 MKURUGENZI Mtendaji wa Ofisi ya Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar Dkt.Hussein  Hussein Khamis Shaban, akizungumza wakati wa mkutano huo wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar leo.23-5-2019. 
 KATIBU Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Bi. Radhia Rashid Haroub, akiwasilisha ripoti ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wac Wizara yake,wakati wa mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar kulia Wakuu wa Mikoa ya Unguja na Pemba, wakifuatilia mkutano huo.

WAKUU wa Wilaya za Unguja na Pemba wakiwa katika mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ,uliofanyika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.(Picha na Ikulu)

HUYU HAPA MMILIKI WA KFC, ALIANZA KWA KUUZA KUKU BARABARANI

$
0
0

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MGAHAWA wa pili wa ukubwa duniani KFC "Kentucky Fried Chicken" umepata umaarufu duniani zaidi kwa bidhaa zake zinazopendwa na wengi zikiwemo kuku wa kukaanga ambao ndio wamebeba jina la mgahawa huo pamoja na bidhaa nyingine kama vile; vibanzi, kifungua kinywa, vinywaji pamoja na maziwa.

Ukiwa na makao makuu huko Lovisville umekuwa  mgahawa wa pili kwa ukubwa duniani  kwa kipimo cha mauzo baada ya McDonald's ambapo KFC imeenea katika maeneo zaidi ya 22,621 duniani na nchi zaidi ya 136 kwa tafiti za mwaka 2018 na una huduma maarufu za Pizza Hut, Taco Bell na Wing Street.

Historia ya mwanzilishi wa KFC inawasisimua wengi kutokana na mapito yake kuelekea mafanikio yake,  Colonel Harland Sanders alizaliwa mwaka 1890 akiwa anaishi na baba yake na alipotimiza miaka 6 tuu baba yake alifariki dunia na kumwachia majukumu ya kupika na kulea ndugu zake, akiwa Sekondari aliacha shule na kurudi nyumbani na kujihusisha na shughuli za kilimo.

Akiwa na miaka 16 Sanders  alidanganya umri ili aweze kujiunga na jeshi na aliachishwa baada ya kugundulika mwaka moja baadaye.

Baada ya kuachana na shughuli za jeshi alipata kibarua katika shirika la reli na alifukuzwa baada ya kugombana na mfanyakazi mwenzake, Licha ya kubahatika kusoma sheria  akiwa kibarua katika shirika la reli  alipoteza sifa ya fani hiyo baada ya kugombana tena hali iliyomlazimu arudi kwa mama yake ambapo alipata kazi katika kampuni ya bima ambapo alifukuzwa kazi hiyo kwa udanganyifu ila hakukata tamaa.

Mwaka 1920 alianzisha kampuni ya usafirishaji wa majini lakini haikidumu, akiwa na miaka 40 alianza kuuza kuku katika vituo, hoteli, barabarani na migahawa ya jirani, na alipoanza kutangaza biashara hiyo alipata upinzani mkubwa miaka 4 baadaye alinunua hoteli ambayo vita vya pili vya dunia vilipelekea kufungwa kwa hoteli hiyo.

Baada ya vita alianza kutangaza biashara yake na ilikataliwa mara 1,009 na hapo ilikiwa tayari na chapa ya KFC na huduma zikiwa zimeboreshwa kwa hali ya juu.

Baada ya kushindwa kote huko Sanders alifanikiwa kushika soko la dunia akiwa anapata mapato ya dola milioni 23 kwa mwaka 2013.

Akiwa na Miaka 90 Sanders alifariki dunia kwa ugonjwa wa Pumu akiacha KFC ikiwa imeenea katika maeneo 6000 duniani na nchi 48.

Article 3

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu ch Dar es Salaam, Prof Rwekaza Mukandala akizungumza na Waandishi kuhusu mada ya leo katika kigoda cha mwalimu ilihusu kuwawezesha watotokupata elimu na kupingana na ajira za mapema wakiwa katika umri wa kwenda shuleni.
 Mkurugenzi wa Haki Elimu Tanzania, Dr.John Kallage akizungumza na Wanazuoni waliofika katika Kigoda cha Mwalimu Nyerere,Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
 Mjumbe wa bodi wa LHRC, Felister Mahuya  akizungumza katika Kigoda Cha Mwalimu Nyerere kilichofanyika jijini Dar es Salaam
 Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu ch Dar es Salaam, Prof Rwekaza Mukandala , akiwa na Jaji Damiani Lubuva wakifatilia Mjadala wa kujadili elimu kwa watoto wadogo
 Wachambuzi  wa mada katika kigoda cha Mwalimu Nyerere , wakiwa katika Panelist
 Washiriki wa Kongamano la Kigoda cha Mwalimu Nyerere wakinyooosha mikono Kuchangia mada

Msanii wa Muziki wa Kughani kutoka Mjomba Bendi , Mrisho Mpoto akiwa amezungukwa na Wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya  kutoka Mjomba Bendi, Ismail akiongoza Burudani katika kigoda cha Mwalimu
 Sehemu ya Washiriki wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere Katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images