Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

TIMU YA SEVILLA FC YAJINOA KWA MECHI YA SIMBA SC LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Timu ya Sevilla FC leo wamefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Timu ya Simba SC hapo kesho May 23, 2019 mchezo utakaopigwa kuanzia majira ya Saa 1 usiku.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 22.05.2019

SERIKALI KUTUMIA BILIONI 2.9 KUMALIZA TATIZO LA MAJI SUMBAWANGA

$
0
0
Serikali imepanga kutumia zaidi ya Shilingi bilioni 2.9 kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Maji wa Ikozi ikiwa ni miongoni mwa Miradi ya Maji 6 inayotekelezwa chini ya Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Maji awamu ya Pili (WSDP II) katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa yenye lengo la kutatua kero ya upatikanjai wa maji kwa wananchi.
Akizungumza na wananchi wa Ikonzi mara baada ya kutembelea baadhi ya miradi ya Wilaya ya Sumbawanga, Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) amesema Serikali imejipanga kutekeleza na kusimamia mradi huo kwa ufanisi na kuwa mradi wa ujenzi wa bwawa wa mfano kwa kuzingatia viwango vya ubora na usalama kwa wananchi walio karibu na mradi huo.
Profesa Mbarawa amesema miradi mingi ya mabwawa nchini imekuwa ikitekelezwa chini ya viwango na ikishindwa kutimiza lengo halisi, akisisitiza wizara itasimamia kwa ukaribu utaratibu mzima na maendeleo ya ujenzi wa bwawa hilo ili liweze kuwa mfano wa kuigwa nchini.
‘‘Mradi huu ulianza Novemba, 2018 chini ya mkandarasi wa Kampuni ya Emirate Builders Ltd kwa gharama ya Shilingi bilioni 2,943,086,780 na ameshalipwa asilimia 15 ya malipo ya awali Shilingi 441,463,017 unatarajiwa kukamilika mwezi Julai, 2019’’, Profesa Mbarawa ameeleza.
‘‘Mkataba wa mradi huu unahusisha ujenzi wa bwawa la ujazo wa lita 436,015,120 pamoja na kazi nyingine na awamu ya kwanza unatarajia kuhudumia Vijiji (3) vya Ikozi, Kazwila na Chituo vyenye jumla ya wakazi 14,395 na baada ya hapo huduma itasogezwa mpaka  Kijiji cha Tentula chenye idadi ya wakazi 2,452’’, Profesa Mbarawa amesema.
Mhandisi wa Maji Wilaya ya Sumbawanga, Patrick Ndimbo amesema usimamizi wa kazi ni mzuri, mkandarasi amekuwa akitumia muda mwingi akiwa site na kazi hiyo inaendelea vizuri akitegemea kukabidhiwa kazi hiyo ifikapo mwezi Julai kama mkataba unavyoonyesha.
Awali, Profesa Mbarawa  alitembelea Mradi wa Maji wa mji mdogo wa Laela na kutoridhishwa na mkandarasi anayetekeleza awamu ya pili ya mradi huo na kuagiza aonane na mkandarasi huyo amuone, ili wapange pamoja upya mpango kazi wa utekelezaji wa mradi huo uliotegemewa kukamilika baada ya miezi minne jambo ambalo waziri huyo amelikataa.
Akiwa katika mradi huo ameagiza chanzo kipya cha mserereko (gravity) cha Kimenyanze kitumike baadala ya chanzo cha awali, kwa kuwa nguvu ya umeme wa nishati ya jua (solar) zilizokuwa zimefungwa kushindwa kusukuma maji kutoka kwenye chanzo hicho cha awali kwenda kwenye tenki na kuyasambaza kwa wananchi.
Profesa Mbarawa amesema jumla ya gharama za mradi huo ni zaidi ya Shilingi bilioni 1.7 na zaidi Shilingi bilioni 1.4 sawa na asilimia 80 zimeshalipwa, akatoa miezi miwili tu mradi huo uwe umekamilika.
 Sehemu ya mradi
 Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiomngea na wataalamu huko Ikonzi akiwa katika kutembelea baadhi ya miradi ya maji Wilaya ya Sumbawanga.

Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiomngea na wataalamu huko Ikonzi akiwa katika kutembelea baadhi ya miradi ya maji Wilaya ya Sumbawanga.

SERIKALI YAAHIDI MAWASILIANO KWA KWA WAKAZI WA WINYENZELE, KIBAKWE

$
0
0

Na Innocent Mungy, Dodoma
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mheshimiwa Atashasta Nditiye (Mb) ameutaka Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote nchini, UCSAF, kufanya tathmini ya kuwezesha wananchi wa Winyenzele katika jimbo la Kibakwe kupata mawasiliano ya uhakika.
Akizungumza na wananchi baada ya kukagua usikivu wa mawasiliano ya simu za mkononi katika kijiji cha Winyenzele, Mh. Nditiye aliwaeleza wananchi hao kuwa kwa tathmini ya haraka iliyofanywa na Mfuko wa Mawasiliano, imeonekana kuna tatizo kubwa la mawasiliano na kuahidi kuwa Serekali kupitia Mfuko wa Mawasiliano itafanya tathmini ya uhakika ili kuhakikisha eneo hilo linapata mawasiliano haraka.
“Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua wazi kuhusu suala zima la mawasiliano kwa Watanzania, nawaelekeza UCSAF waje hapa na kuhakikisha kabla ya mwezi Disemba mwaka huu wananchi hawa wanapata mawasiliano kama Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inavyoelekeza kuhusu mawasiliano kwa wote” alisema Mheshimiwa Nditiye.
Akizungumza katika Mkutano huo baada ya kukagua usikivu wa mawasiliano kijijini hapo, Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mh. George Simbachawene aliiomba Serikali kupitia Wizara ua Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuwasaidia wananchi hao kupata mawasiliano kwani wanapata shida sana kuwasiliana na wananchi wenzao, ndugu jamaa na marafiki.
“Mheshimiwa Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli amehamishia Makao Makuu ya Nchi Jijini Dodoma ambako ni mwendo wa saa moja na nusu kutoka hapa. Lakini wananchi hawa wanashindwa kupata hata mawasiliano kupeleka mayai ya kuku wa kienyeji, mazao mbalimbali na biashara zingine kwani hawana mawasiliano ya simu kama wenzao wanaoagizwa kwa simu oda mbalimbali na kulipwa kwa miamala ya kifedha kupitia simu za mkononi. Naomba Serikali iwawezeshe na wao waweze kuchangia jitihada za Serekali kuhamia Dodoma,” alisema Mheshimiwa Simbachawene.
Wananchi wa Winyenzele walisoma risala iliozungumzia ugumu wa mawasiliano katika eneo hilo na kumuomba mbunge wao aiombe Serikali iwasaidie wapate mawasiliano. Aidha katika kuupokea ugeni wa Mh. Naibu Waziri Nditiye aliyekuwa ziarani kikazi kukagua usikivu wa mawasiliano katika jimbo la Kibakwe, wananchi walimpokea kwa ngoma, nyimbo na maelezo ya kuonesha jinsi wanavyopata shida ya mawasiliano.
“Tunaishukuru Serikali kwa kutuletea umeme, maji na hospitali hapa Winyenzele, lakini tunaiomba Serikali ituletee mawasiliano” waliimba wanavikundi wa Kwaya ya amani na ngoma ya wazee wa kijijini hapo kwa nyakati tofauti.
Mh. Waziri aliwasihi wananchi hao kuwa wavumilivu na kuwaahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imesikia kilio chao na watapata mawasiliano.
“Rais wetu mpendwa kama mnavyomjua ni mtu wa vitendo, nilipokuwa nakuja huku nilimuaga Mh. Waziri Mkuu na anawasalimia sana. Najua lazima atatoa taarifa hizi huko juu na sisi watumishi wenu, tutahakikisha tunamsaidi Rais wetu kutekeleza ahadi za Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Mtapata mawasiliano” alisisitiza Mh. Nditiye.
Serikali kupitia mfuko wa Mawasiliano Nchini (UCSAF) umewezesha Zaidi ya vijiji 500 kupata minara ya mawasiliano kwa kutoa ruzuku kwa makampuni ya simu kujenga minara maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara. Katika maadhimisho ya miaka 10 ya UCSAF, Mfuko huo ulielezea kuwa takribani 94% ya nchi inapata mawasiliano na maeneo machacheyaliyobaki yatafanyiwa tathmini ili kupatiwa mawasiliano ya uhakika.

 Mh. George Simbachawene (Kulia) ambae ni Mbunge wa Kibakwe akimkaribisha Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Atashasta Nditiye (Kushoto) kuzungumza na wananchi wa Winyenzele, Kibakwe.
 Mheshimiwa George Simbachawene Mbunge wa Kibakwe pamoja na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Atashasta Nditiye wakisikiliza risala ya wananchi wa Winyenzele wakiomba huduma ya Mawasiliano kijijini hapo.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Atashasta Nditiye akizungumza na wananchi wa Winyenzele Kibakwe ambapo aliwaahidi wananchi hao kuwa Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano Kwa Wote nchini (UCSAF) utapeleka Mawasiliano eneo hilo.
Wazee wa Kijiji cha Winyenzele walifanya maombi ya Kimila kwa kumpa Mbunge wao Mh. George Simbachawene  kigoda na fimbo na kumuomba awasaidie wapate mawasiliano. 

HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI IMETOA MIKOPO SH MILIONI 400 KWA VIKUNDI 128

$
0
0
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imetoa mikopo siyo kuwa na riba ya yenyt Sh milioni 400 kwa vikundi 128 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Akizungumza leo katika hafla kukabidhi mikopo hiyo amau ya pili, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Ng’wilabuzu Ludigija, amesema kwa mwaka 2018/2019 walipanga kutoa mikopo ya Sh milioni 537.1.

Amesema katika awamu ya kwanza zilitolewa Sh milioni 250 kwa vikudi 97 na awamu ya pili zimetolewa Sh milioni 150 kwa vikundi 31.
“Kwa kuzingatia sera na maelekezo ya Serikali tumekuwa tukitenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kuyawezesha makundi haya.

“Walionufaika wahakikishe wanarejesha fedha hizi kwa wakati ili kujitengenezea nafasi ya kupata mikopo mingine,” amesema Ludigija.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, amesema kumekuwa na mabadiliko makubwa ya mapato katika halmashauri hiyo kutoka Sh bilioni 3 hadi kufikia Sh bilioni 6 hatua iliyowezesha kuongezeka kwa vikundi vinavyopatiwa mikopo.

“Tulipotoa awamu ya kwanza ya mikopo hakukuwa na vijana waliojitokeza fedha zote walikabidhiwa kinamama na wenye ulemavu. Je, vijana wenzangu mnakwama wapi?
“Vijana ndio nguvu kazi ya Taifa hivyo, changamkieni fursa hizi mjikwamue kiuchumi,” amesema Sara.
Kati ya vikundi 128 vikundi 92 ni vya wanawake, 28 vya vijana na vinane vya watu wenye ulemavu.Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri (katikati) akizungumza na wajasiriamali katika hafla ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa vikundi mbalimbali leo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni,Ng’wilabuzu Ludigija akizungumza na wajasiriamali katika hafla ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa vikundi mbalimbali leo jijini Dar es Salaam ambapo aliwaomba kurejesha mikopo yao kwa wakati.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv) Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri akiamkabidhi cheki Katibu wa kikundi cha Wateule Group,Johaim Sasila leo katika hafla ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa vikundi mbalimbali leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu Wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri akitoa amekabidhi Vitambulisho vya Matibabu ya Bure kwa wazee Katika awamu hii ya kwanza zaidi ya wazee 1000 ndio wamekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA JIMBO LA XUZHOU LA CHINA

$
0
0
Na Ramadhani Ali - Maelezo Zanzibar
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed ameiomba Jamhuri ya Watu wa China kurejesha utaratibu wa madaktari wa nchi hiyo wanaokuja kufanyakazi Zanzibar kukaa miaka miwili badala ya mwaka mmoja wa sasa. 

Alisema tokea kuanzisha uhusiano wa madaktari wa China kuja Zanzibar mwaka 1965 walikuwa wakikaa kipindi cha miaka miwili lakini utaratibu huo ulibadilika miaka ya hivi karibuni na hivi sasa wanakaa mwaka mmoja.

Waziri wa Afya alitoa ombi hilo alipokutana na Ujumbe wa wataalamu wa afya kutoka Mji wa Xuzhou ambao upo nchini kufanya tathmini ya Madaktari wanaokuja kufanyakazi Zanzibar katika hospitali ya Abdlala Mzee Mkoani na Mnazimmoja.

Aliueleza ujumbe huo kwamba utaratibu wa zamani wa timu za madaktari wa China kukaa miaka miwili ulikuwa unatoa fursa nzuri kwa madaktari wa Zanzibar kujenga uzoefu na kujifunza mambo mengi ya kitaalamu kutoka kwao.

Alisema madaktari wa Zanzibar wanapopata uzoefu kwa vitendo kutoka kwa madaktari wa China inawasaidia kufanya vizuri wanapopata nafasi ya masomo ya juu nje ya nchi.

Waziri Hamad aliushauri ujumbe huo kuwaelekeza madaktari wa China waliopo Zanzibar kuwapa mafunzo madaktari wa Hospitali ya Abdalla Mzee ya kutumia mashine mpya zilizowekwa katika hospitali hiyo na kuitafsiri teknolojia iliyotumika ili baada ya kuondoka waweze kuzitumia.

Aidha Waziri wa Afya aliwahimiza madaktari wazalendo kuwa tayari kujifunza utaalamu kutoka madaktari wa China ambao wamekuwa wakifanya matibabu ya kitaalamu na kuwashirikisha.

Kiongozi wa ujumbe huo Zhou Guangchum alimuhakikishia Waziri wa Afya kwamba nchi yake itaendelea kuisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuongeza msaada wake hasa katika sekta ya afya.

Aliahidi kuwa atalifikisha nchini kwake ombi la kurejesha utaratibu wa zamani wa madaktari wanaokuja Zanzibar kukaa kwa kipindi cha miaka miwili ili waweze kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ndugu zao.
 Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akizungumza na ujumbe kutoka Mji wa Xuzhou Nchini China uliokuja kufanya tathmini ya Madaktari wa nchi hiyo wanaokuja kufanya kazi Zanzibar Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akiagana na Kiongozi wa ujumbe kutoka Mji Xuzhou Nchini China Zhou Guangchum baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ofisini kwake. Picha na Makame Mshenga.

NMB YAWEZESHA MJADALA WA MAONI KUKUZA UKUSANYAJI MAPATO JIJI LA DAR

$
0
0


Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge akizungumza na wadau mbalimbali (hawapo pichani) katika mkutano wa kupokea maoni toka kwa wadau anuai ili kuboresha sekta ya ukusanyaji mapato kwenye mkoa huo.
Ofisa Mwandamizi Wateja wa Serikali, Bi. Vicky Bishubo kutoka NMB Makao Makuu (kulia) akizungumza katika mkutano wa kupokea maoni toka kwa wadau mbalimbali ili kuboresha ukusanyaji mapato Mkoa wa Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd ambao ni wadhamini wa mkutano huo.
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge akizungumza na wadau mbalimbali (hawapo pichani) katika mkutano wa kupokea maoni toka kwa wadau anuai ili kuboresha sekta ya ukusanyaji mapato kwenye mkoa huo. Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd ambao walidhamini mkutano huo.
Mwakilishi kutoka Chuo cha Kodi TRA, Emmanuel Masalu akiratibu majadiliano katika mkutano wa kupokea maoni toka kwa wadau anuai ili kuboresha sekta ya ukusanyaji mapato ya jiji la Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd ambao ni wadhamini wa mkutano huo.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa kupokea maoni toka kwa wadau mbalimbali jijini Dar es Salaam ili kuboresha ukusanyaji mapato kwenye mkoa huo.
Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (kushoto) akizungumza jambo na Ofisa Mwandamizi Wateja wa Serikali, Bi. Vicky Bishubo kutoka NMB Makao Makuu kwenye mkutano huo.

USAJILI WA BIASHARA UMEONGEZEKA KUTOKA MAKAMPUNI 62 KWA MWEZI HADI KUFIKIA 700-BRELLA

$
0
0

Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini(Brella) Bakari Mketo wakati akizungumza na wadau wa biashara Jijini Tanga waliohudhuria mafunzo ya namna ya urasimishaji kuwapa uwezo wajasriamali ili waweze kujua namna ya kusajili na kuongeza thamani ya bidhaa.
Afisa kutoka Kitengo cha Ubunifu wa Wakala wa Biashara na Leseni (BRELLA) ambaye pia ni Mkufunzi wa Mafunzo kwa Kanda ya Kaskazini anayefundisha namna ya mfumo unavyofanya kazi Suzana Senso akizungumza wakati wa mafunzo hayo ambapo alisema zoezi la uelimishaji limeanza kutoka mwaka jana desemba walianzia Nyanda za Juu, kanda ya Ziwa,Kanda ya Magharibi na Kanda ya Kati na sasa wapo kanda ya Kaskazini.
Sehemu ya wafanyabiashara walioshiriki mafunzo hayo wakifuatilia matukio mbalimbali
Sehemu ya wafanyabiashara walioshiriki mafunzo hayo wakifuatilia matukio mbalimbali
MWAMKO wa watanzania kusajili biashara zao kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA) umeongezeka kutoka makampuni 62 kwa mwezi hadi kufikia 700 hali inayosababisha na kuwepo kwa mfumo rafiki wa kuweza kuwafikia kupitia mtandao ambao umekuwa mkombozi kwao. 

Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Brella Bakari Mketo wakati akizungumza na wadau wa biashara Jijini Tanga waliohudhuria mafunzo ya namna ya urasimishaji kuwapa uwezo wajasriamali ili waweze kujua namna ya kusajili na kuongeza thamani ya bidhaa.

Alisema hatua hiyo ni mzuri kwa sababu inaonyeshwa namna watanzania hususani wafanyabiashara walivyokuwa mstari kujisajili kupitia wakala huu na kuweza kutambulika ambapo alisema idadi hiyo ilitokea makampuni hayo 62 kwenda 200 na baadae sasa kufikia 700 huku wakiweka mipango ya kuhakikisha wanazidi kuongeza wigo mpaka ili kuongeza idadi ya makampuni yatakayojisajili

“Baada ya mfumo wa kutoka kwa vitambulisho vya Taifa na kutakiwa kutumia namba ya vitambulisho idadi ya makampuni yanayosajiliwa umeongezeka na kufikia idadi hiyo lakini bado tutaendelea kukutana na wadau kwa kutoa elimu kuweza kuongeza wigo mpaka “Alisema.

Aidha alisema malengo yao ni kuhakikisha wanapanua wigo mpaka na kufikia idadi ya watu 1000 kwa mwezi ili kumhakikisha kila mdau wao anafikia na huduma yao kwa wakati hali itakayopelekea kumpunguzia mzigo mzito mwananchi na hivyo pia kuondoa gharama za kufuata huduma hiyo.

‘Usajili kabla ya mfumo ulikuwa ni mkubwa sana lakini ulikuwa unawagharmi wateja wetu kutokana na kwamba wengi walikuwa wakiibiwa na vishoka kwa sababu wanasafiri kutoka Tanga kwenda Dar kutokana na kwamba hapo awali kutokuwa na matawi na hivyo kupelekea kuingia gharama na kuwapelekea mzigo mkubwa hivyo kwa kuliona hilo tukatambulisha mfumo huo wa kusajili kupitia online na mwamko kabla ya mfumo na baada ya mfumo mwamko umekuwa mkubwa sana”Alisema

Awali akizungumza wakati wa mafunzo hayo kutoka Kitengo cha Ubunifu wa Wakala wa Biashara na Leseni (BRELLA) ambaye pia ni Mkufunzi wa Mafunzo kwa Kanda ya Kaskazini anayefundisha namna ya mfumo unavyofanya kazi Suzana Senso alisema zoezi la uelimishaji limeanza kutoka mwaka jana desemba walianzia Nyanda za Juu, kanda ya Ziwa,Kanda ya Magharibi na Kanda ya Kati na sasa wapo kanda ya Kaskazini.

Alisema kwenye maeneo ambayo tayari wamepita mwamko umekuwa mkubwa sana kutokana na wafanyabiashara kueleza namna ya mfumo huo unavyofanya kazi ikiwemo kukutana na maafisa biashara hivyo kuwa chachu ya ongezeko la usajili na uelewa umeongezeka sana.

Hata hivyo alisema baada ya kutoka mkoani Tanga wataekelea kwenye mikoa ya Kanda ya kaskazini mingine ikiwemo Kilimanjaro,Arusha na Manyara huku akitoa wito kwa watu watakaosikia wakala huo wapo kwenye mikoa yao watumie fursa hiyo kupata darasa ambalo litawapa uelewa mkubwa.



SERIKALI YADHAMIRIA KUMLINDA MTEJA KUANGALIA GHARAMA ZA WAKANDARASI - NAIBU WAZIRI MGALU

$
0
0
NA SAMIA CHANDE, RUFIJI

NAIBU Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu amewasha umeme katika vijiji vya Muhoro Mashariki na Magharibi wilayani Rufiji Mkoani Pwani leo Mei 22, 2019 ikiwa ni muendelezo wa Serikali kuhakikisha watanzania wote wakiwemo wa vijijini wanapata umeme.

Akiwaelimisha wananchi kuhusu gharama za kuunganishiwa umeme wakati wa hafla hiyo iliyofanyika shule ya msingi Nyampapu iliyoko kijiji cha Muhoro Mashariki, Naibu Waziri alisema serikali inaowajibu wa kumlinda mlaji na mtumiaji wa huduma mbalimbali ndio maana katika swala la umeme vijijini imeshusha gharama za kuunganishiwa umeme hadi shilingi 27,000/= tu.

“Awali gharama za kuunganishiwa umeme zilikuwa ni shilingi 177,000, lakini Serikali kwa vile inawajali wananchi wake imelipa shilingi 150,000/= kwa kila anayeweka umeme, na kazi ya mwananchi ni kulipia kiasi kidogo tu cha shilingi 27,000/=, tofauti na hapo awali.” Alisema Mhe. Naibu Waziri Mgalu katika hafla hiyo ambapo takriban Kaya 26 zimefaidika na zoezi hilo.

Alisema anatambua wapo wananchi wapo karibu na miundombinu ya njia ya umeme na sio kwamba wanashindwa kulipa shilingi elfu 27,000/= bali wanashindwa na gharama ya kutandaza umeme ndani ya nyumba (wiring) inayofanywa na wakandarasi.(mafundi).

“Alisema gharama hizo za wiring zimeonekana kuwa ndio changamoto kwa wananchi na serikali imepokea changamoto hiyo na kwamba itafanyia kazi.” Alisema.

Alitoa wito kwa wakandarasi wanaofanya kazi ya wiring wazingatie vipato vya watanzania wenzao, watakapoweka bei kubwa watapata wateja wachache lakini wakiweka bei ya kawaida, wateja wengi ambao serikali imelenga kuwaunganishia umeme watawapata.Aidha Mhe. Naibu Waziri Subira Mgalu, aliwataka wananchi wa Wilaya ya Rufiji kuchangamkia fursa za kutoa huduma kwa wafanyakazi wanaojenga mradi wa umeme wa maji wa Mto Rufiji.

“Vijana nendeni Ngarambe, Mloka na Mwasemi, ajira ziko za kutosha, akina mama ntilie, wanatakiwa vibarua, lakini pia kunachangamoto ya nyumba za kulala wageni, kwa hivyo ziko fursa nyingi katika maeneo ya mradi.” Alisema.

Alisema kuna mahitaji mbalimbali ya vyakula kama vile mbogamboga, kitoweo, mahitaji ya bidhaa hizo yamekuwa makubwa na kutoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Rufiji kuhcngamkia fursa hiyo.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu (mwenye hijab mbele), akizunhgumza baada ya zoezi la kuwasha umeme kwenye vijiji vya Muhoro Mashariki na Magharibi wilayani Rufiji Mkoani Pwani leo Mei 22, 2019. Takriban Kata 26 zimefaidika na zoezi hilo.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, (aliyesimama), akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika vijiji vya Muhoro Masharki na Magharibi iliyofanyika shule ya msingi Nyampapu wilayani Rufiji Mkoani Pwani leo Mei 22, 2019. Mwenye shati la bluu ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Mhe. Juma Njwayo.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, (wapili kulia), akiongozana na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Rufiji baada ya hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, (kushoto), akipokea zwadi kutoka kwa akina mama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), baada ya kuhutubia wananchi katika hafla ya kuwasha umeme iliyofanyika shule ya msingi Nyampapu iliyopo Muhoro Mashariki wilayani Rufiji Mkoani Pwani leo Mei 22, 2019. (PICHA NA SAMIA CHANDE).

ISACA TANZANIA CHAPTER 2019 annual Conference

IFAD KUENDELEA KUISAIDIA TANZANIA KUENDELEZA SEKTA YA KILIMO

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha, Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bw. Gilbert Fossoun Houngbo, baada ya Mkutano ulioangazia maendeleo ya sekta ya kilimo nchini na namna ya kutatua changamoto zake, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma. 
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akipeana mkono na mgeni wake Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bw. Gilbert Fossoun Houngbo, katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma. 
Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bw. Gilbert Fossoun Houngbo, akiipongeza Serikali ya Tanzania kwa ukuaji wa Sekta ya Kilimo kwa takribani asilimia 6, kiwango ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na nchi nyingi za Afrika, wakati wa Mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), kushoto ni Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Rubuga. 
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa sita kushoto) na Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bw. Gilbert Fossoun Houngbo (wa sita kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania na IFAD, baada ya kumalizika kwa mkutano ulioangazia Maendeleo ya Sekta ya Kilimo kikiwemo kilimo cha umwagiliaji, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma. 


Na Peter Haule, WFM, Dodoma 

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bw. Gilbert Houngbo, na kuiomba Taasisi hiyo kusaidia kuendeleza zaidi Sekta ya Kilimo kupitia mpango wake mpya wa awamu ya 11 wa kuendeleza kilimo nchini. 

Dkt. Mpango ameyataja baadhi ya maeneo ya kipaumbele kuwa ni uzalishaji wa mbegu bora, kusaidia kilimo cha umwagiliaji, kutafuta masoko ya uhakika ya mazao ya wakulima, kusaidia upatikanaji wa mitaji kwa wakulima na kuanzisha taasisi za utafiti wa kilimo za kikanda. 

Aidha, Dkt. Mpango alimwomba kiongozi huyo kusaidia pia mbinu za kupunguza upotevu wa mazao wakati na baada ya mavuno ili kuchochea na kuongeza tija katika sekta ya kilimo ambayo amesema inaajiri zaidi ya asilimia 66 ya Watanzania. 

”Takiribani asilimia 66 ya watanzania wanategemea kilimo na kilimo ndio mwajiri mkuu hivyo kwa kuwa IFAD ina program mpya, tumeamua kushauriana ili wajue vipaumbele vya Serikali na fedha tutakazo zipata tuzielekeze katika maeneo hayo”, alieleza Dkt. Mpango. 

Dkt. Mpango alisema kuwa Serikali inaunda kikosi kazi kitakacho husisha Wizara ya Kilimo, Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ili kuweka nguvu ya pamoja kwa kuangalia maeneo ya vipaumbele ambavyo Mfuko wa IFAD utasaidia. 

Kwa upande wake Rais wa IFAD Bw. Gilbert Houngbo, alisema kuwa Taasisi yake itashirikiana na Tanzania katika jitihada zake za kupunguza umasikini wa wananchi kupitia kilimo kwa kuyapatia ufumbuzi masuala kadhaa ikiwemo changamoto ya upatikanaji wa mbolea na mbegu bora za kilimo na mifugo, masoko ya bidhaa, upatikanaji wa mitaji, kuongeza ujuzi wa wakulima, kuendeleza kilimo cha umwagiliaji na kuwashawishi vijana wengi kujihusisha na kilimo. 

Alielezea kufurahishwa kwake na mwamko pamoja na mwitikio wa baadhi ya wakulima na wafugaji walionufaika na awamu zilizotangulia za uendelezaji sekta ya kilimo na mifugo kupitia taasisi yake aliowatembelea, ambao amesema wanamtazamo mzuri wa kilimo cha kibiashara kinachozingatia uongezaji wa mnyororo wa thamani, suala ambalo ni moja ya lengo la Mfuko huo katika kuendeleza Sekta hiyo. 

Mfuko wa IFAD ulianza kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi ya maendeleo ya kilimo kuanzia mwaka 1978, ambapo hadi sasa imesaidia miradi 15 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 385.80 na katika awamu mpya ya miaka mitatu kuanzia mwaka 2019/2021, IFAD imetenga zaidi ya dola za Marekani milioni 58.8 kwa ajili ya kuendeleza Sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi nchini. 

Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na kuwasaidia wakulima kutumia teknolojia ya kisasa ya kilimo na mifumo ya masoko, kuhamasisha Sekta binafsi katika uwekezaji na kuwasaidia wakulima wadogo na wavuvi kuongeza kipato na kupunguza umasikini kwa kuzingatiakuongeza mnyororo wa thamani ya mazao husika. 

Sekta ya Kilimo nchini inachangia asilimia 30.1 ya jumla ya pato la ndani (GDP), asilimia 26 ya mapato ya kigeni, ajira takribani asilimia 65.5, inachangia malighafi za viwandani kwa takribani asilimia 65 na inachangia kwenye mahitaji ya chakula kwa asilimia 100.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MEI 23,2019

ZIMEBAKI SIKU SABA KUFIKIA MWISHO WA MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI

UTPC kuongoza Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Afrika na Karibiani

$
0
0
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), umekamilisha taratibu za kulichukua Shirikisho la Klabu za Waandishi wa Habari katika nchi za Afrika na Karibiani (African and Caribbean Press Club-ACP) ambapo makao makuu yake yatakuwa jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa UTPC Abubakar Karsan aliyasema hayo jana wakati akihitimisha mafunzo ya sheria mbalimbali za habari kwa waandishi wa habari wa Vyombo vya Habari Mbadala (Alternative Media) yaliyofanyika Morena Hoteli jijini Dodoma kwa siku mbili kuanzia Mei 21, 2019.


“Waambieni Watanzania jambo hilo.. .Waambieni watu wasioijua UTPC jambo hilo, waambieni watu wenye mashaka na UTPC jambo hilo, kwamba sasa tunaisimamia “Federation” (shirikisho) ya nchi zaidi ya 160” alisema Karsan akisisitiza kwamba hilo si jambo dogo bali ni hatua kubwa.


Aidha Karsan alitumia nafasi hiyo kushukru uwepo wa mradi wa DDA ambapo alisisitiza washiriki wake kutimiza wajibu wao ipasavyo ili kuhakikisha matarajio yanafikiwa na kuondokana na changamoto ya kutotimiza makubaliano jambo ambalo limekuwa likisababisha taasisi nyingi ikiwemo za waandishi wa habari kuvunjika.


Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari (APC), Claude Gwandu alisisitiza kwamba klabu hiyo itahakikisha mradi huo unafanikiwa na kwamba haitasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayetaka kukwamisha mradi huo lengo likiwa ni kuleta mabadiliko katika jamii na taifa kwa ujumla.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) kupitia mradi wa utetezi na ushawishi wa haki za binadamu kwa kutumia takwimu (DDA), Midraji Ibrahim alisema mafunzo hayo yatawasaidia kupiga hatua katika majukumu yao ikiwa kila mmoja atafanyia kazi yale aliyojifunza huku akiishukru taasisi ya Freedom House kwa ushirikiano wake.


Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) unafadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka jana 2018 ambapo kwa waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) unasimamiwa na UTPC kupitia APC.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Vyombo Vya Habari Mbadala (Alternative Media), wakinasa matukio jana jijini Dodoma wakati Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan akihitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi hao kuhusu sheria mbalimbali za habari ili kutekeleza kwa weledi mradi wa Utetezi na Ushawishi kwa kutumia Takwimu (Data Driven Advocacy-DDA), unaosimamiwa na UTPC kupitia Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC) kwa ufadhili wa taasisi ya Freedom House.
Picha na Kadama Malunde, Malunde 1 Blog
Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan akizungumza kwenye kwenye kilele cha mafunzo ya siku mbili kuanzia Mei 21-22, 2019 kwa waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Altenative Media) yaliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan aliwahimiza waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) kutimiza wajibu wao ipasavyo ili kuhakikisha mategemeo ya mradi huo wa utetezi na ushawishi kwa kutumia takwimu yanatimia.
Wakili James Marenga ambaye alikuwa Mkufunzi wa Mafunzo hayo akitoa salamu zake.
Afisa Program kutoka UTPC, Victor Maleko akitoa ufafanuzi kwenye kilele cha mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) kupitia mradi wa utetezi na ushawishi kwa kutumia takwimu (DDA), Midraji Ibrahim akitoa salamu zake kwenye kilele cha mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa Arusha Press Club, Claude Gwandu akitoa salamu zake kwenye hitimisho la mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada kutoka kwa Wakili James Marenga.
Washiriki wa mafunzo hayo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Tazama BMG Online TV hapa chini

MUONEKANO WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE TERMINAL lll, KUKABIDHIWA WIKI IJAYO


BENKI YA EXIM YAFUTURISHA WATEJA WAKE WA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na kati wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Andrew Lyimo (kulia) akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa huduma za reja reja wa benki hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na kati wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Andrew Lyimo (kulia) sambamba na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo walioudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa huduma za reja reja wa benki hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na kati wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Andrew Lyimo (kulia) akizungumza wateja wa benki hiyo waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa huduma za reja reja wa benki hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam jana.
Mmoja wa wateja wa benki ya Exim Tanzania kutoka taasisi Ahmadiyya Muslim Jamaat Tanzania, Bw Abdulrahman Mohamed Ame akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wateja wa benki hiyo waliohudhuria hafla ya futari iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam jana.

KIONGOZI BARAZA LA WAWAKILISHI UINGEREZA LEADSOM AACHIA NGAZI

$
0
0
Na Ripota Wetu

KIONGOZI wa Baraza la Wawakilishi nchini Uingereza Andrea Leadsom amejiuzulu kwa madai kuwa hana imani na tena na njia anayotumia Waziri Mkuu Theresa May kama inaweza kuufanikisha mchakato wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya ama Brexit.

Hatua hiyo inaongeza shinikizo kwa Waziri Mkuu May ambapo Leadsom anayetambulika zaidi kwa kuunga mkono Brexit amemuandikia barua May akimtolea mwito wa kuchukua uamuzi sahihi kwa ajili ya maslahi ya taifa, serikali na chama chao.

Kwa mujibu wa mtandao wa DW -Swahili ni kwamba kujiuzulu kwake kunakuja siku moja kabla ya Uingereza kushiriki uchaguzi wa Bunge la Ulaya.

Wakati hayo yakiendelea  May hapo jana aliendelea kupuuza ongezeko la miito ya kumtaka ajiuzulu, licha ya kuongezeka kwa upinzani kutoka kwa wabunge na mawaziri wa chama chake cha Conservative kuhusu mpango wake wa karibuni wa Brexit.

PENTAGON YADAIWA KUWA NA MPANGO WA KUONGEZA WANAJESHI 5000 MASHARIKI YA KATI

$
0
0
Na Ripota Wetu

WIZARA ya Ulinzi ya Marekani imesema kwa sasa inapitia ombi la jeshi la nchi hiyo la kutaka kupeleka wanajeshi zaidi ya 5,000 Mashariki ya Kati, wakati wasiwasi ukiongezeka kati yake na Iran.

Taarifa inaeleza kuwa kulingana na maofisa wawili waliozungumza na Shirika la Habari la Reuters kwa masharti ya kutotajwa majina, ombi hilo limewasilishwa na makao makuu ya jeshi la Marekani, lakini bado haiko wazi iwapo wizara hiyo italiidhinisha. 

Mmoja wa maofisa hao amesema wanajeshi hao wanapelekwa kwa ajili ya kujihami na hilo linatajwa kama ombi la karibuni zaidi la kuongezwa kwa wanajeshi katika kile ambacho Marekani inakitaja kama kitisho dhahiri kutoka kwa Iran dhidi Marekani na maslahi yake katika ukanda wa Mashariki ya Kati.

Hata hivyo, wizara hiyo ilipoulizwa iwapo kuna ombi hilo ilikataa kuzungumzia mipango yake ya usoni.

SHIRIKISHO LA SOKA DUNIANI LAKATAA KUONGEZA IDADI YA TIMU KOMBE LA DUNIA

$
0
0
SHIRIKISHO la Soka Duniani (FIFA) limekataa kuongeza idadi ya timu zitakazoshiriki kwenye michuano ya Kombe la Dunia ya 2022 itakayofanyika Qatar, kutoka timu 32 hadi 48 kama ambavyo ilikuwa imependekezwa.

Kwa mujibu wa FIFA imesema kuwa baada ya majadiliano ya kina na wadau wote muhimu sasa  imeamua kwamba chini ya mazingira ya sasa haitaweza kulitekeleza pendekezo hilo kwa wakati huu.

Hivyo michuano hiyo sasa itasalia na timu 32 za awali na hakutakuwa na pendekezo litakalowasilishwa kwenye kongamano lijalo la FIFA litakalofanyika Juni 5.

Uamuzi huo wa mwisho wa FIFA umetolewa mapema tofauti na ilivyotarajiwa kwamba yangetolewa wakati wa kongamano hilo litakalofanyika Paris nchini  Ufaransa kabla ya michuano ya Kombe la Dunia ya wanawake.

Rais wa FIFA, Gianni Infantino aliunga mkono pendekezo hilo, na maamuzi haya yanatajwa kuwa pigo kubwa kwake.

VILABU SITA UINGEREZA VYASAKA SAINI YA MSHAMBULIAJI MBWANA ALLY SAMATA

$
0
0
MSHAMBULIAJI nyota katika Ligi ya Ubelgiji anayekipiga Klabu ya Genk na nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mbwana Samatta huenda akatua Ligi Kuu ya England (EPL) msimu ujao.

Samatta anayejulikana zaidi kwa jina Samagoal, amedokeza hadi sasa kuna vilabu sita vya Ligi ya Primia ambavyo vinapigana vikumbo kumsajili nyota huyo ambapo mwenyewe amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akieleza kuwa hayupo katika wakati mzuri kusema klabu gani anaweza kwenda.

Mchezaji huyo amefafanua kutoka Hispania kuna timu mbili ambazo zimekuwa zikiisaka saini yake lakini ndoto yake kubwa ni kucheza katika Ligi Kuu ya England. Hata hivyo inaelezwa si mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kudaiwa kuwindwa na vilabu vya Ligi ya Premia. CHANZO -BBC
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images