Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MAREHEMU BRIGEDIA JENERALI MSTAAFU ATHUMANI HASSAN NGWILIZI LUGALO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiandika katika kitabu cha maombolezo mara baada ya kuwasili katika Hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam Mei 22,2019 kwaajili ya kuaga mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Athuman Hassan Ngwilizi aliyefariki dunia hospitalini hapo Mei 20,2019.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Athuman Hassan Ngwilizi katika Hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam Mei 22,2019 ,Marehemu alifariki dunia hospitalini hapo Mei 20,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Shekhe Mkuu wa Dsm Alhaji Mussa Salum baada ya kuwasili katika Hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam Mei 22,2019 kwaajili ya kuaga mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Athuman Hassan Ngwilizi aliyefariki dunia hospitalini hapo Mei 20, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Athuman Hassan Ngwilizi katika Hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam Mei 22,2019 ,Marehemu alifariki dunia hospitalini hapo Mei 20, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameungana na Viongozi wengine na ndugu kusindikiza kwenye gari mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Athuman Hassan Ngwilizi kutoka katika Hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam Mei 22,2019 kuelekea Mlalo Lushoto Mkoani Tanga kwaajili ya mazishi ,Marehemu alifariki dunia hospitalini hapo Mei 20,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa Mjane wa Marehemu mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Athuman Hassan Ngwilizi katika Hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam Mei 22,2019 ,Marehemu alifariki dunia hospitalini hapo Mei 20, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa Familia ya  Marehemu mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Athuman Hassan Ngwilizi katika Hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam Mei 22,2019 ,Marehemu alifariki dunia hospitalini hapo Mei 20, 2019.

PICHA NA IKULU

MAMA JANETH MAGUFULI ATOA FUTARI KWA AJILI YA FAMILIA ZENYE UHITAJI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, amewasihi Waislamu nchini kuendelea kuliombea Taifa muda wote, hususan katika kipindi hiki cha  Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, na kuendeleza mshikamano bila kujali dini ama kabila tabaka zao.

Mama Magufuli ametoa wito huo leo tarehe 22 Mei, 2019 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji.

Vyakula alivyotoa ni tani 5 za mchele, tani 3 za sukari na tende. Hafla hiyoimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu Mruma, Mkurugenzi wa Hijja wa BAKWATA Shekhe Haidary Kambwile na wawakilishi wa vikundi mbali mbali vya wenye uhitaji.

Mama Magufuli pia amemuomba Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema, azikubali funga za Waislamu wote  na kuwalipa malipo stahiki wakati wakitekeleza moja ya nguzo muhimu za Dini ya Kiislamu.

“Kipindu cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni kipindi cha toba. Ni kipindi cha kutenda matendo mema na kujizuia na vitendo viovu” amesema Mama Magufuli.

Mama Magufuli amesema licha ya kwamba Tanzania ina watu wa imani za Dini tofauti lakini siku zote wananchi wake wamekuwa wakishirikiana nyakati za dhiki na za raha bila ubaguzi.

Ametoa mfano kuwa licha ya tofauti za kidini zipo baadhi ya familia ambazo Baba Muislamu na Mama ni Mkristo zinaishi kwa amani na kushirikiana katika masuala yote ya kifamilia na kwamba sifa hii ni moja nguzo muhimu za umoja wa Watanzania.



“Binafsi nakumbuka zamani nikiwa mdogo tulikuwa tunatafuta Mwislamu aje atuchinjie kuku ama mbuzi ama ng’ombe” , alisema na kuongezea: “Ni kutokana na utamaduni huo uliojengeka miongoni mwa Watanzania , leo nimeguswa kutoa sadaka yangu kwa ajili ya ndugu zangu wenye uhitaji…”
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akiongea machache wakati wa hafla ya kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019

 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akimsiliza Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe  Nuhu Muma akitoa shukurani wakati wa kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019


 Wawakilishi waliohudhuria wakiitikia dua baada ya kupokea msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019
 Wawakilishi waliohudhuria wakiitikia dua baada ya kupokea msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akiitikia dua baada ya kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akimkabidhi Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe  Nuhu Muma msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 019

 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akimkabidhi Mkurugenzi wa Hija wa BAKWATA Shekhe Haidary Kambwile  msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akimkabidhi muwakilishi wa watototo msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019

 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akimkabidhi muwakilishi wa wazee msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019

 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akimkabidhi muwakilishi wa kinamama msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019

 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli katika picha ya kumbukumbu na   Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu Mruma, Mkurugenzi wa Hijja wa BAKWATA Shekhe Haidary Kambwile pamoja na wawakilishi wa vikundi mbali mbali vya wenye uhitaji baada ya hafla ya kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji.

 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akiagana na wawakilishi baada ya kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019

 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akiagana na wawakilishi baada ya kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akiagana na wawakilishi baada ya kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akiagana na wawakilishi baada ya kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akiagana na  Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu Mruma, Mkurugenzi wa Hijja wa BAKWATA Shekhe Haidary  baada ya kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019

MUFTI MKUU TANZANIA AIPONGEZA BENKI YA NMB KWA KUIJALI NA KUITHAMINI JAMII,AITABIRIA MAKUBWA

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Albert Jonkergouw (kulia) akimkaribisha Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (kushoto) wakati wa Futari iliyoandaliwa na NMB katika Hotel ya Serena. Katikati ni Meneja wa NMB kanda ya Dar es Salaam Id Badru 
Mkurugenzi Mtendaji wa Beni ya NMB, Albert Jonkergouw akizungumza na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (kushoto) , Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum na Meneja wa NMB kanda ya Dar es Salaam Id Badru. 
Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi wa Benki ya NMB, Omari Mtiga, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kabwe na Mkurugenzi wa ndni wa benki hiyo, Juma Kimori wakiwaongoza wageni kuchukua futari iliyoandaliwa na benki ya NMB iliyodanyika kwenye Hoteli ya Flomi Morogoro. 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Steven Kebwe akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB katika Hoteli ya Flomi mkoani Morogoro. 
Shekhe Mkuu Mkoa wa Mtwara, Nurdin Mangochi akiwa kwenye iftari iliyoandaliwa na Benki ya NMB jana. 
Mkurugenzi wa ndani wa Benki ya NMB Juma Kimori, akizungumza wakati futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB katika Hoteli ya Flomi mkoani Morogoro. 


MUFTI Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir, ameitabiria makubwa Benki ya NMB, kutokana na utamaduni chanya walionao wa kuijali, kuithamini na kuipa kipaumbele jamii chini ya mwamvuli wa kaulimbiu yao ya Karibu Yako.

Mufti Zubeir alitoa mtazamo huo wakati akizungumza na waaalikwa wa hafla ya pili ya benki ya NMB kufuturisha waumini wa Dini ya Kiislamu tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu 2019.

Ukiondoa Mufti Zubeir, hafla hiyo iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam, ikishirikisha waumini wa Kiislamu, wateja na waalikwa wengine, ilihudhuriwa pia na Sheikh Mkuu wa Mkoa, Alhad Mussa Salum na Meya wa Jiji, Issaya Mwita.

“Niwapongeze kwa uamuzi huu wa NMB kufuturisha waumini wa Kiislamu, hasa ukizingatia mnahudumia makundi mbalimbali wakiwemo Wakristo na wasio na dini. Hii inatoa tafsiri moja tu kuwa NMB inajali makundi na kada mbalimbali za jamii, jambo ambalo litawapa mafanikio.

Aliongeza ya kwamba walichofanya NMB ni jambo kubwa, linalojenga mahusiano makubwa baina ya Waislamu na wasio Waislamu, na kila mmoja kuitazama NMB kama taasisi inayojali makundi yote ya watu na kwa namna hiyo wanazivuta nyoyo za wengi kuona inafaya kazi kwa weledi.

“Mtu akiwa mwema kiasi hicho ama hata taasisi, Mwenyezi Mungu humlipa ama huilipa, hii maana yake ni kuwa kwa utamaduni huu, NMB itapata mafanikio makubwa kutokana na namna mnavyojali makundi mbalimbali ya jamii,” alisema Mufti Zubeir.

Aliitaka NMB kutoacha tamaduni ya kufungamanisha makundi kwa kufuturisha waumini wa Kiislamu na kuutaka uongozi kuufanya utamaduni huo kuwa wa kudumu ili pindi awamu moja ya uongozi inapomaliza muda wake, iache alama kwa jamii.

Awali akimkaribisha Mufti Zubeir, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Albert Jonkergouw, alisema benki yake inajisikia furaha kuungana na Waislamu katika kutimiza moja ya nguzo muhimu za dini yao, huku akiahidi kuwa NMB itaendelea kusapoti na kushirikia na jamii.

Alisema tukio hilo ni la pili tangu kuanza kwa mfungo wa Ramadhani mwaka huu, baada ya kukutanisha, kufuturisha na kujadiliana kwa ufupi na Waislamu wa Jiji la Tanga na kwamba wamepanga kufuturisha katika miji kadhaa Tanzania Bara na Visiwani.

“Tukio kama hili leo linafanyika mjini Iringa, awali lilifanyika Tanga na sasa tunaelekea Zanzibar (Unguja na Pemba), na pia mikoa ya Mtwara, Mwanza na kwingineko kulingana na ratiba itakavyoturuhusu,” alisema Jonkergouw.

Akijibu wito wa Mufti Zubeir, aliyeomba muendelezo wa hafla za kufuturisha, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, alisema NMB itaendelea na utaratibu wa kufuturisha waumini wa Kiislamu na kwamba wamefanya hivyo mara nyingi na wataendelea.

BENKI YA POSTA KUISAIDIA SERIKALI KUFIKIA UCHUMI WA KATI

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

BENKI ya Posta Tanzania (TPB) imesema kuwa imeanza kutekeleza mkakati wa serikali kusaidia kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa kati kupitia utekelezaji wa uchumi wa viwanda.

Mwenyekiti wa bodi ya TPB,Dk.Edmund Mndolwa alisema hayo katika futari ya mwezi mtukufu wa ramadhani iliyoandaliwa na benki hiyo kwa viongozi wa serikali na wateja wa benki hiyo wa mkoani Kigoma.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imeazimia kupitia dira ya taifa 2000 - 2025 ya kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa kati na kwa namna ya usimamizi unaofanywa na Raisi John Magufuli ni wazi kila sekta lazima ijipange kuhakikisha inatekeleza majukumu ili kufikia lengo jambo ambalo TPB imeshaanza kulitekeleza.

Alisema kuwa moja ya mambo muhimu katika kutekeleza hilo ni kutoa mikopo kwa wateja ambayo itawafanya wawekezaji wa ndani na nje kushiriki kikamilifu kwenye mipango mbalimbali ya kiuchumi na tayari TPB inao mpango kabambe ambao utawawezesha Watanzania kupata mikopo ya aina mbalimbali ili kutekeleza shughuli zao za kiuchumi.

"Maboresho makubwa yaliyofanywa na serikali katika benki hii imeifanya benki kukua kimtaji, kiuendeshaji na imeongeza wateja kwa kiasi kikubwa na kwa sasa ni benki ya tisa nchini kati ya mabenki ambayo yanajiendesha kwa faida, hivyo ni wakati mzuri kwa wateja kuitumia benki hii kwa kuwa na akaunti lakini pia kuchukua mikopo yenye masharti nafuu ambayo itawasaidia kuendesha shughuli zao za kiuchumi,"Alisema Dk.Mndolwa.

Akizungumza katika futari hiyo kwa wateja wa TPB mkoani Kigoma, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi alisema kuwa benki imeboresha huduma zake kwa kiwango kikubwa na ndiyo msingi wa ongezeko kubwa la wateja na kuifanya benki hiyo ifanye kazi zake kwa tija.

Moshingi alisema kuwa kwa kuthamini hilo ndiyo maana benki imekuwa ikiandaa hafla mbalimbali ambazo zinawakutanisha viongozi waandamizi wa benki hiyo na wateja na wadau wake ili kuweza kupokea maoni na ushauri mbalimbali ambao wanauchukua na kuufanyia kazi ikiwa ni sehemu ya kufanyia maboresho utoaji huduma katika benki hiyo. 

Mkuu wa mkoa Kigoma Brigedia mstaafu Emanuel Maganga alisema kuwa TPB ni benki kongwe ambayo haina budi kuungwa mkono na Watanzania wote kwani sehemu kubwa ya watumishi wa serikali kwa miaka ya nyuma ilikuwa inategemea benki hiyo. 

Maganga aliwakumbusha wateja wa benki hiyo waliohudhuria futari hiyo kwamba msingi wa kukua kwa biashara na shughuli za kiuchumi ni pamoja na kuchukua mikopo ambayo benki ya Posta imerahisisha kwa kuweka masharti nafuu kuweza wateja wake kupata mikopo hiyo.

Shekhe wa mkoa Kigoma, Alhaji Hassan Iddi Kiburwa amesema kuwa kitendo kilichofanywa na benki hiyo kufuturisha waislam na wasio wa islam kwa kupata chakula cha pamoja na kitendo cha kiimani kuwatendea wema wote hivyo kusanyiko hilo la futari limepata baraka za Mwenyezi mungu ambazo zinazidi kuifanya benki hiyo kufany vizuri kwenye shughuli zake.
Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya posta(TPB)Sabasaba Moshingi akizungumza baada ya futari pamoja na waumini wa dini ya kiislam na wateja wao wa Mkoa wa Kigoma futari iliyoandaliwa na benki hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kigom Brigedia Mstaafu Emanuel Maganga akizungumza jambo na waumini wa dini ya kiislamu pamoja na wateja wa benki ya posta(TPB)kwenye futari iliyoandaliwa na bank hiyo Mkoani Kigoma.
Shekhe wa mkoa wa Kigoma Hassan Iddi Kiburwa akiwaongoza waumini wa dini ya kiislam na wateja wa benki ya TPB katika futari iliyoandaliwa na banki hiyo

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Buyungu, Mhandisi Christopher Chiza, Bungeni jijini Dodoma, Mei 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Hanang, Dkt. Mary Nagu, Bungeni jijini Dodoma, Mei 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Kibiti, Ally Ungando kwenye viwanja vyua Bunge jijini Dodoma, Mei 22, 2019.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Reader Rabbits ya jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 22, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Biharamulo, Oscar Mukasa kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 22, 2019. 

WAKALA WA CHAKULA DAWA NA VIPODOZI WAGUNDUA BIDHAA ZILIZOINGIZWA KINYUME NA UTARATIBU ZANZIBAR

$
0
0
 Mkaguzi wa Chakula Dawa na Vipodozi Abrahman Hamadi Mussa akionesha kwa Waandishi wa Habari Bidhaa ya Majani ya Chai yalioingizwa nchini kinyume na Utaratibu ambayo imegunduliwa katika Ghala lililopo Mikunguni sheli mjini Unguja.
 Mkaguzi wa Chakula Dawa na Vipodozi Abrahman Hamadi Mussa akionesha kwa Waandishi wa Habari tarehe na mahala inapotengenezwa Bidhaa ya Majani ya Chai ambapo ilionekana inatengenezwa Zanzibar wakati bidhaa hio inatengenezwa Dare es salaam na kuingizwa Nchini kinyume na Utaratibu ambayo imegunduliwa katika Ghala lililopo Mikunguni sheli mjini Unguja.
 Mkaguzi wa Chakula Dawa na Vipodozi Abrahman Hamadi Mussa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na kugundua Bidhaa ya Majani ya chai ilioingizwa Nchini kinyume na Utaratibu iliogunduliwa katika Ghala lililopo Mikunguni sheli mjini Unguja.
 Mwanasheria wa Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozo Khadija Abdalla Abasi akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na kugundua Bidhaa ya Majani ya chai ilioingizwa Nchini kinyume na Utaratibu iliogunduliwa katika Ghala lililopo Mikunguni sheli mjini Unguja.
Bidhaa ya majani ya chai yalioingizwa kinyume na utaratibu ikiingizwa katika Gari kwa ajili ya kwenda kuangamizwa ambayo imegunduliwa katika Ghala lililopo Mikunguni sheli mjini Unguja.

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge la Jamhuriya Muungano wa Tanzania mhe. Job Ndugai akisisitiza jambo kwa wabunge leo Jijini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.
  Mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha mhe. Amina Mollel akisisitiza jambo leo Bungeni Jijini Dodoma baada ya kipindi cha maswali na majibu.
 Naibu Waziri wa Maji mhe. Jumaa Aweso akisisitiza kuhusu mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa wananchi wote wanafikiwa na huduma ya maji leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi mhe.  Luhaga Mpina akisisitiza kuhusu mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa  haki za wanyama zinazingatiwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala akisisitiza jamb oleo Bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI mhe Selemani Jaffo akisisitiza jambo kwa  Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Kassim Majaliwa leo Bungeni Jijini Dodoma.
(Picha na MAELEZO)

RAIS DKT.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA VIJANA MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA ZANZIBAR IKULU NDOGO KIBWENI

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza wakati wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Vijana Michezo Utamaduni na Sanaa Zanzibar katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar leo 22-5-2019(Picha na Ikulu)
 NAIBU Waziri Wizara ya Vijana Michezo Utamaduni na Sanaa Zanzibar Mhe. Lulu Msham, akwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara yake katika mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar leo,22-5-2019, kushoto Mshauri wa Rais Masuala ya Utamaduni Zanzibar Mhe. Chimbeni Kheri.
 KATIBU Mkuu Wizara ya Vijana Michezo Utamaduni na Sanaa Zanzibar Ndg. Omar Hassan King akiwasilisha viwangu vya Matumizi na Mapato ya Wizara wakati wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi, uliofanyika Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar, kushoto Mshauri wa Rais Afisi ya Rais Pemba Mhe. Maua Abeid Daftari na Mshauri wa Rais Masuala yac Uwezeshaji Mhe. Abdulrahaman Mwinyijumbe. 
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee akizungumza wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Vijana Michezo Utamaduni na Sanaa Zanzibar, uliofanyikia katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar leo 22-05-2019.


MAOFISA wa Idara za Wizara ya Vijana Michezo Utamaduni na Sanaa Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar, wakifuatilia Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa kipindi cha mwezi Julai 2018 hadi March 2019.(Picha na Ikulu)

JUMUIKO LA MALIASLI TANZANIA WAIPONGEZA SERIKALI KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI, YATOA USHAURI

$
0
0
Mmoja wa viongozi kutoka mashirika yaliyoungana kuzungumzia masuala yanayohusu maliasili nchini Tanzania akitoa shukrani kwa waandishi wa habari kwa kushiriki mafunzo ya kuwajengewa uwezo kwani anaamini umafunzo hayo yatakuwa chachua kaika kuandika habari.

Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF) Zakaria Faustine akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya siku mbili ya kujengewa uelewa kuhusu masuala yanayohusu maliasili ikiwemo ardhi.Mafunzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam.

Mtoa mada katika mafunzo hayo Mary Ndaro ambaye pia ni Mratibu wa programu ya Ardhi Yetu (AYP) kutoka Care Tanzania akielezea umuhimu wa waandishi wa habari kuandika habari za ardhi na hasa kwa kuangalia usawa wa kijinsia.
Waandishi wa habari wakiendelea kupata mafunzo kuhusu namna bora ya kuandika habari zinazohusua maliasili nchini kutoka kwa watoa mada.
Wakili Masalu Luhula kutoka Jumuiko la Maliasili Tazanzia  akifafanua masuala mbalimbali ya kisheria katika sekta ya ardhi nchini ambapo pia alitumia mafunzo hayo kueleza namna sheria za ardhi zinavyofanya kazi na umuhimu wake katika kutatua migogoro katika jamii.
Mwandishi wa Habari kutoka gazeti la The Citezen akitoa maelezo kuhusu uzoefu wake katika kuandika habari zinazohusu ardhi na maliasili nchini.




Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


JUMUIKO la Maliasili Tanzania limeishauri Serikali kujiikita katika kuendelea kutatua migogoro ya ardhi nchini huku wakitoa pongezi zao kwa Serikali kwa namna inavyochukua hatua kwa kuhakikisha migogoro iliyopo inapata ufumbuzi wa kudumu.

Pia Jumuiko hilo limesema kuna kila sababu ya mikataba mibovu ambayo ipo kwenye ardhi kufumuliwa kama ambavyo Rais Dk.John Magufuli alivyofumua mikataba mibovu iliyoingiwa kwenye sekta ya madini huku wakisisitiza wao wako tayari kusaidiana na Serikali katika hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF) Zakaria Faustine amesema Jumuiko hilo na mashariki mengine zaidi ya 18 wamekuwa wakishirikiana katika eneo la maliasili na hasa ardhi na wanaona kazi nzuri inayofanywa na Rais na Serikali katika kutafuta utatuzi wa migogoro ya ardhi.

"Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF) pamoja na Tanzania Land Alliance (TALA)tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli kwa hatua inazochukua kutataa kero za wananchi wa maeneo mbalimbali.

"Kwetu sisi ni faraja kubwa lakini nitumie nafasi hii kutoa rai kwa Serikali tunafahamu bado kuna migogoro katika sekta ya ardhi na hivyo ni vema hatua zaidi zikafanyika kupata ufumbuzi wake.

"Binafsi natamani kuona Rais wetu anaagiza kuangaliwa upya mikataba ambayo imeingiwa katika ardhi na ile ambayo itaonekana hafai basi ifumuliwe kwa maslahi ya Watanzania wote,"amesema Faustine.

Akifafanua zaidi wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Jumuiko hilo kwa kushirikiana na TALA kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu kuandika habari za ardhi, amesema wamefurahishwa pia na hatua ya Serikali kuyarejesha kwa wananchi baadhi ya mashamba makubwa.

Hata hivyo amefafanua pamoja na Serikali kutangaza baadhi ya mashamba makubwa yaliyokuwa yanamilikiwa na watu binafsi wakiwamo wawekezaji, kwa mujibu wa Faustine ni kwamba mashamba hayo bado hajayakabidhiwa kwa wananchi.

"Tunashukuru nia na dhamira njema ya Rais wetu katika kuhakikisha baadhi ya mashamba yanarudishwa kwa wananchi wa maeneo husika baada ya Serikali kutangaza kuyarejesha.Hata hivyo wananchi hawajapewa mashamba hayo kwasababu mlolongo wa kisheria nao ni mrefu na ili mashamba hayo yakabidhiwe kwa wananchi kuna hatua za kisheria ambazo zinapaswa kuchukuliwa.

"Tuko tayari kushirikiana na Serikali kuhakikisha mashamba ambayo yametangazwa kuwa yamerudishwa kwa wananchi kweli yanawafikia ili yatumike kwa shughuli za maendeleo ya Taifa letu,"amesema Faustine.

Amesisitiza Jumuiko la Maliasili Tanzania pamoja na TALA kwa muda mrefu wamekuwa wakishiriki kikamilifu keulimisha jamii kuhusu ardhi na namna nzuri ya kutatua migogo lakini changamoto kubwa hakukuwa na uchukuliwaji hatua wa haraka kama ilivyo sasa.

Kuhusu waandishi wa habari nchini katika kuandika habari zinazohusu ardhi na masuala mengine ya maliasili, Faustine amesema bado kuna changamoto kubwa kwani habari za ardhi hazipewi kipaumbele kama ambavyo inafanyika katika habari nyingine, hivyo wakaona njia sahihi ni kuwaita waandishi wa habari na kisha kuwajengea uwezo.

"Baada ya kuona kuna pengo la waandishi wa habari zinazohusu Maliasili tumeona vema tukaandaa mafunzo alau ya siku mbili ili tuwajengee uwezo. Hivyo tumeamua kutoa mafunzo kwa waandishi zaidi16 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini kutoka mikoa tofauti tofauti,"amesema Faustine.

Wakati huo huo waandishi wa habari nchini wamehimizwa kujikita kuandika habari za uchunguzia na hasa zinazohusu maliasili kwa maslahi ya Taifa ambapo Mwandishi mkongwe nchini Deodatus Mfugali alitumia nafasi hiyo kueleza hatua zinazopaswa kufuatwa wakati wa kuandika habari za uchunguzi.

Akifafanua zaidi wakati akitoa mada iliyohusu namna bora ya kuandika habari za uchunguzi, Mfugale amesema ili waandishi waisaidie nchi yao katika kutatua migogoro ya ardhi wanayo nafasi ya kujikita kuandika habari za uchunguzi."Changamoto kubwa iliyopo waandishi wengi haaandiki habari za uchunguzi kuhusu ardhi na maliasili za nchini.Tumebaki tu kuandika habari za matukio.

"Nitoe rai kwa waandishi wa habari nchini mkiwemo mliopatiwa mafunzo haya jikiteni kuandika habari za uchunguzi kwa kutafuta vyanzo sahihi na kwa kuangalia maslahi mapana ya nchi yetu badala ya kuangalia maslahi binafsi,"amesisitiza Mfugale.

Waandishi hao wakiwa kwenye mafunzo hayo pia wameelezwa kuwa nchini Tanzania nafasi ya mwanamke kumiliki ardhi bado ni ndogo sana na hivyo inahitajika jitihada za kutoa elimu na hamasa itakayowezesha wanawake kuwa sehemu ya wanaomiliki ardhi.

Mtoa mada katika mafunzo hayo Mary Ndaro ambaye pia ni Mratibu wa programu ya Ardhi Yetu (AYP) kutoka Care Tanzania ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuelimsha jamii kuwa mwanamke anayo nafasi ya kumiliki kipande cha ardhi.

"Kuna sababu nyingi ambazo zinachangia wanawake wengi kutomiliki ardhi zikiwemo za masuala ya mila, desturi na tamaduni kwani wapo baadhi ya wanawake kutokana na tamaduni zao hata wakipewa ardhi wanakataa kwa madai kuwa ardhi inamilikiwa na wanaume .

"Hii ni changamoto na ni jukumu letu sote kutoa elimu.Tunashukuru kuna maeneo ambayo tumekwenda huko vijijini wanawake wameanza kuona umuhimu wa kuwa na ardhi kwani ndio kila kitu ikiwemo kwa shughuli za kilimo,"amesema Ndaro.

FREDERIC PECHIER, DAKTARI ALIYEWAPA SUMU WAGONJWA ILI KUONESHA UJUZI WAKE KATIKA KUWAOKOA

$
0
0
Je, unatumiaje fani yako? Kama Daktari Pechier?  manufaa yanayoletwa na ujuzi wako  katika jamii ni yapi? hasi au chanya?

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
DAKTARI mmoja nchini Ufaransa Frederic Pechier (47) ameshtakiwa nchini humo kwa tuhuma za kuwapa sumu zaidi ya wagonjwa 17 ikiwa bado yupo katika  uchunguzi wa vifo vya watu 9 alivyosababisha kwa wagonjwa wakati akifanya upasuaji.

Kwa mujibu wa jarida la DailyMail imeelezwa kuwa daktari huyo amekuwa na tabia ya kuwapa sumu wagonjwa hao kwa malengo ya kuonesha ujuzi wake wa namna anavyoweza kuokoa maisha ya wagonjwa hao.

Daktari huyo anayefanya kazi katika hospitali moja huko Mashariki mwa Mji wa Besancon anashukiwa kwa kuwapa sumu wagonjwa hao wakati akiwafanyia upasuaji kwa kuwapa dawa zilizoathiri mfumo wa moyo na baadaye kujaribu kuwatibu ili kuokoa maisha yao.

Pechier amehusishwa na matukio 24 kati ya 66 na bado yupo chini ya ulinzi licha ya kukana madai hayo ambayo tayari ushahidi umetolewa kwa vifo 9 vilivyotokea na matukio 24 kati 66 yamethibitishwa kutokea.

GAVANA BOT AWAAGIZA WAHASIBU KUZINGATIA WELEDI, MAADILI KATIKA KAZI ZAO ZA KIHASIBU

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT)Profesa Florence Luoga amewaagiza wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya kazi ikiwa ni pamoja na kusimama katika weledi ili kuepuka malalamiko ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakiikumba kada hiyo.

Ameyasema hayo leo Mei 22,2019 alipokuwa akifungua mkutano wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa mahesabu hapa nchini(NBAA)unaondelea jijini Arusha na kuongeza kwa kufanya hivyo kutaongeza imani ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu kwa jamii na taasisi wanazozihudumia.

"Ni vema wahasibu kote nchini kuhakikisha kuwa malipo yote yanayofanyika yapitie katika taasisi za kifedha,ikiwemo mabenki taasisi hizo ziweze kujiendesha na serikali iweze kujiongezea kipato kwa lengo la kukuza pato la Taifa,"amesema Profesa Luoga.

Ameongeza endapo watafuata utaratibu huo utasaidia kuondokana na changamoto ya malipo hewa pamoja na kukabiliana na tatizo kubwa la uingizwaji na uzagaaji wa fedha haramu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi yaTaifa ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu(NBAA),Pius Maneno amesema lengo la mkutano huo wa siku tatu ni kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu.

Ameongeza katika mkutano huo mada 11 zitawasilishwa na kujadiliwa zikiwemo za fedha,Tehama,uadilifu pamoja na muongozo wa wahasibu na wakaguzi wa mahesabu kuhusu suala zima la fedha haramu ikiwemo kanuni za nidhamu.

"Bodi ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu hapa nchini imeendelea kuwaelimisha wahasibu na wakaguzi wa mahesabu hapa nchini kuhusu kufanya kuzingatia wajibu na weledi pindi watekelezapo majukumumu yao,"amesema.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema bodi yake imetunga muongozo ulioanza kutumika tarehe 1aprili mwaka huu kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kuhakikisha wanakagua mahesabu yao lengo likiwa ni kuongeza kodi na Mei 1 mwaka huu umeanza kutumika muongozo wa fedha hamu na Juni 15 zitaanza kutumika kanuni za uadilifu.

Amesema mkutano huu unashirikisha watu 300 ambao ni wahasibu na wakaguzi wa hesabu za kutoka taasisi na mashirika mbalimbali, maofisa kutoka Benki Kuu(BOT),na benki nyingine,wataalamu wa fedha na taasisi za Bima.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bodi yaTaifa ya wahasibu na wakaguzi wa Mahesabu (NBAA),Pius Maneno akizungumza na Waandishi wa habari hii leo
Baadhi ya washiriki pamoja na viongozi wakiwa katika picha ya pamoja

MTOTO WA MIAKA MIWILI AFARIKI DUNIA ARUSHA BAADA YA NYUMBA YAO KUTEKETEA KWA MOTO

$
0
0
Na Woinde Shizza, Michuzi Tv, Arusha

MTOTO mwenye umri wa miaka miwili Mercy Nyari amefariki dunia baada ya mwili wake kuteketea kwa moto baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kuungua. 

Nyumba hiyo ya Eliud Nyari iliyoko eneo la Loita Nkwamala katika kata ya Nkwandrua wilayani Meru mkoani Arusha imeungua leo asubuhi na kusababisha kifo hicho.

Akizungumza kuhusu kuungua kwa nyumba hiyo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Loita  Dikson Kaaya amesema mtoto huyo aliachwa nyumbani mwenyewe na mama yake mzazi , kitu kilichomsababishia kifo maana alikosa msaada wakati moto huo ulivyokuwa unawaka.

"Wakati moto unawaka katika nyumba hiyo hakukuwa na mtu yeyote na mtoto alikuwa ameachwa ndani na mama yake, hivyo alikosa msaada wa mtu wa kumsaidia ndio maana umauti ulimkuta,na kwa kweli ukiangalia mwili wake umeteketea kabisa,"amesema.

Amefafanua moto huo umewaka leo asubuhi pasipo kujulikana chanzo kutokana  na nyumba hiyo kutokuwa na umeme au kitu chochote kinachohusisha hatari ya kuwepo kwa moto hali iliyoleta taharuki kwa familia.

Mmoja wa majirani wa nyumba hiyo Mchungaji Tegemea Mbise amesema  wao walishangaa kuona moto huo umeanza kuwaka gafla. Pia amesema  kinachowashangaza zaidi nyumba hiyo iliyoungua haina umeme, hivyo ni jambo  linalotia hofu zaidi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arumeru  Jerry Muro akiambatana na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na usalama walifika eneo la tukio na kukuta tayari moto huo umeshateketeza nyumba hiyo na kuanguka chini huku mali zote zikiwa zimeteketea na kusababisha familia ya watu saba kukosa makazi .

Muro mbali na kutoa pole amesema Serikali ya Wilaya kwa kushirikiana na wadau wamejitolea kuijenga nyumba nyingine ndogo kwa ajili ya familia hiyo na kutoa chakuka cha kuwasaidia kwa muda wa wiki moja.

Pia  Muro amewataka wananchi kutowaacha watoto na watu wasiojiweza majumbani pasipo kuwa na watu wa kuwasaidia ili kuepeshua madhara yanayoweza kujitokeza.

Hata hivyo kutokana na mwili huo kuharibiwa , familia ya mtoto huyo pamoja na Serikali wameamua kuuzika mwili huo na kisha kuacha hatua za uchunguzi ziendelee.
 Baadhi ya wananchi waliojitokeza kuangalia tukio hilo la moto lilillosababisha kifo cha mtoto mmoja

 

MASHABIKI SIMBA WAOMBWA KUUJAZA UWANJA KATIKA MECHI YAO DHIDI YA SEVILLA FC YA SPAIN

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MASHABIKI na wapenzi wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam wameombwa kujitokeza kwa wingi na kuujaza uwanja katika mechi ya kirafiki kati ya timu hiyo na Sevilla FC inayoshiriki Ligi ya Laliga ya nchini Hispania.

Tayari timu hiyo imewasili nchini usiku wa jana ikiwa na wachezaji 18 na wanatarajia kukipiga na Simba kesho Alhamis ya Mei 23,2019 saa moja jioni katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mmiliki wa Klabu ya Simba Mohamed Dewj 'MO' amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi ili kuujaza uwanja huo kwani kucheza na timu ya Sevilla FC ni heshima kubwa kwao ambayo wamepewa na Sportpesa.

"Klabu ya Sevilla ni kubwa na inafanya vizuri katika Laliga. Mashabiki wa Simba njooni tuujaze uwanja kama tulivyokuwa tukiujaza kwenye mechi za Klabu Bingwa Afrika.Huenda bahati ikawa kwetu tukaifunga Sevilla na tukaandika historia katika madani ya soka la Tanzania.

"Tunafahamu ujio wa Sevilla nchini umegharimu fedha nyingi lakini Sportpesa wameamua kutumia fedha hizo kwa ajili ya kuhakikisha Simba tunacheza na timu hiyo.Ni lazima tuoneshe heshima tuliyopewa na Sportpesa kwa kuujaza uwanja hapo kesho,"amesema MO.

Amesema kujitokeza kwa wingi uwanjani pia itakuwa sehemu ya kuonesha ishara ya furaha ambayo Wana Simba wanayo kwa msimu huu ambao kwao umekuwa mzuri kutokana na timu yao kufanya vema katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa kutwaa ubingwa lakini pia katika Ligi ya Klabu Bingwa Afrika kwa kufika hatua ya robo fainali.

MO DEWJ ATOA YA MOYONI UBINGWA WA SIMBA...AWEKA HADHARANI MIKAKATI YAO

$
0
0
*Hatma ya Kocha kufahamika wiki ijayo ila bodi imemkubali 

*Asema kuhusu usajili wa wachezaji wanasubiri taarifa ya Kocha


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BAADA ya timu ya Simba kutangazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Mmilikiwa klabu hiyo Mohamed Dewji 'MO' ametangaza mikakati mbalimbali ya kuisuka timu hiyo ili iwe yenye ushindani zaidi kwa msimu ujao.

Pia ametumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa wachezaji, benchi la ufundi pamoja na Kocha wao kwa kufanikisha kutwaa ubingwa huo kutokana na kazi nzuri ambayo wameifanya katika msimu huu.

Akizungumza leo Mei 22 , 2019 jijini Dar es Salaam, MO ambaye pia ni mfanyabishara maarufu nchini amesema baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa sasa wanajipanga kwa ajili ya kuweka mikakati ya msimu unaokuja hasa kwa kuzingatia ligi itakuwa yenye ushindani mkubwa.


ALICHOSEMA KUHUSU KOCHA 


Kuhusu kocha wao MO amesema kwanza wanampongeza Kocha Patrick Aussems kwa namna ambavyo amefanikiwa kutimiza malengo aliyopewa wakati anakabidhiwa timu.Kocha alitakiwa kuhakikisha anatetea ubingwa wa Ligi Kuu lengo ambalo amelitimiza.

Na kwamba alitakiwa kuipeleka timu hiyo hatua ya mzunguko katika Michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika ambapo yeye ameifikisha Simba hatua ya robo faina ambayo ni mafanikio makubwa kwao.

" Kocha amefikisha malengo kwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ameiwezesha timu kuingia hatua ya robo fainali michuano ya Klabu Bingwa Afrika.Baada ya wiki moja tutazungumza naye ili kumuongeza mshahara.

"Bodi ya wakurugenzi imejiridhisha na uwezo wa kocha na bahati nzuri kwa muda ambao amekaa tayari amefahamu mazingira ya soka la Tanzania na wakati huo huo anajua kabisa wana Simba wanataka nini?

"Tutaingia naye mkataba wa kuendelea kuinoa timu yetu maana anastahili kwa hatua ambayo ametufikisha kwani ametufanya Simba tuwe na msimu mzuri,"amesema MO.


VIPI KUHUSU WACHEZAJI?

MO hakusita kueleza wazi jukumu la kuingia mikataba na wachezaji kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu itategemea na mapendekezo ya kocha baada ya kutoa taarifa yake kwa Bodi ya Wakurugenzi na wale ambao atataka kuendelea nao tutawapa mkataba mpya.

Amefafanua wataingia mkataba mipya na wachezaji wa ndani ambao watabaki katika Klabu ya Simba na wachezaji wengine watawapaleka kwa mkopo katika timu nyingi zinazoshiriki Ligi Kuu.

Pia MO amesema kwa wachezaji 10 wa kimataifa nalo wanamuachia Kocha atoe mapendekezo yake ya nani anataka abaki na nani aondoke. "Kocha atatoa mapendekezo na Bodi ya Wakurugenzi watayafanyia kazi."

Amefafanua leo usiku wanatarajia kupata taarifa ya Kocha kuhusu wachezaji ambao watabaki kwa ajili ya msimu ujao na wakati huo huo ameeleza kuna wachezaji wengine wapya watasajiliwa kwa ajili ya kuongeza nguvu hasa kwa kuzingatia ligi ijayo itakuwa ngumu na wakati huo huo wana mashindano makubwa ya Klabu Bingwa Afrika.


MAANDALIZI MSIMU UJAO SI MCHEZO

Wakati huo huo MO amesema baada ya kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu Bara kwa mwaka 2018/2019 pamoja na kuweka mikakati ya kusuka kikosi cha Simba, pia wanatarajia katika kipindi cha kuelekea msimu ujao wa ligi timu yao itakwenda nje ya nchi kujiandaa.

MO amesema tayari amefanya mazungumzo na baadhi ya timu kubwa zilizoko Marekani na hivyo wanaweza kwenda kuweka kambi huko au wanaweza kwenda Ureno kwani nako kuna mazungumzo yanaendelea kufanyika na itakupowa tayari watatoa taarifa ya wapi wanakwenda kupiga kambi.

Amefafanua kuwa timu ya Simba katika kujiandaa na msimu huu wa Ligi Kuu ambao umemalizika walienda kuweka kambi nchini Uturuki na mwaka juzi walikwenda Afrika Kusini , hivyo kwa mwaka huu wanajiandaa kwenda katika moja ya nchi hizo kama sio Marekani basi Ureno.


VIPI KUHUSU UBINGWA?

MO ameeleza wazi kuwa amefurahishwa na timu yao kufanikiwa kutwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo na kwamba kila mchezaji atapewa pikipiki yenye thamani ya Sh.milioni 2.5 kama ahsante yake ambapo anaamini pikipiki hizo kwa kila moja itaingiza Sh.milioni tano kwa mwaka.

"Nilifanya kikao cha siri na wachezaji na katika kuwatia moyo ili kuhakikisha tunachukua ubingwa, niliwaambia kila mchezaji atapata pikipiki .Lengo langu ni kwamba pikipiki hiyo itakuwa kitega uchumi na ndani ya mwaka mmoja mchezaji anaweza kumpa ndugu yake akawa anamletea Sh.15000 kila siku.

"Baada ya mwaka mmoja atakuwa amepata Sh.milioni tano na kisha pikipiki hiyo kumuachia ndugu yake ili naye aweze kujipatia kipato.Hivyo taarifa za kwamba nitawapa Sh.milioni tano kila mchezaji naweza kusema si sahihi au sahihi lakini binafsi niliahidi pikipiki,"amesema MO.

TFS-SHAMBA LA SAOHILI LAPEWA SIFA LUKUKI KWA JUHUDI ZA UHIFADHI MISITU, UKUSANYAJI MAPATO

$
0
0

Na Ripota Wetu, Michuzi TV

VIONGOZI wa Serikali kutoka Mkoa wa Ruvuma wameupongeza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS kupitia Shamba la Miti Sao Hill kwa uhifadhi misitu uliotukuka na ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa kiwango kikubwa hatimae kutekeleza Tanzania ya Viwanda kwa utoaji malighafi endelevu ya mazao ya misitu kwa faida ya kizazi cha sasa na Vizazi vijavyo ikiwa ni pamoja na kuchangia kukuza uchumi wa Taifa.

Pongezi hizo zimetolewa mapema leo hii na ugeni uliotembelea shamba la miti Sao Hill ukiongozwa na Wakuu wa Wilaya za Songea, Namtumbo na Nyasa, Makatibu Tawala wa Wilaya, Madiwani, Wakurugenzi wa Halmashauri, Watendaji wa Kata, Vijiji na Wenyeviti wa vijiji sanjari na Wataalamu wa Misitu kutoka Shamba la Miti Mpepo waliotembelea shamba hili kwa lengo la kujifunza.

Akizungumza Ofsini kwake wakati wa mapokezi, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi David William amesema kuwa shamba la miti Sao Hill limekuwa chachu kubwa ya uchumi wa wilayani Mufindi na Taifa kwa ujumla kwani limekuwa likikusanya mapato ya Serikali kupitia mazao ya misitu kwa kiasi kikubwa.

Ameongeza kuwa shamba hilo limekuwa likiendelea kuweka uhusiano mzuri na jamii inayozunguka shamba ili kuondokana na changamaoto zinazoweza kujitokeza kama vile moto wa msituni na migogoro ya ardhi.

Mkuu wa Wilaya ya Nyansa Isabela Chilumba ambae pia ndie kiongozi wa Msafara huo akieleza malengo ya ziara amesema wameona ni vema kuja kujifunza katika Shamba la Miti Sao Hill kwani ni Shamba mama na ni shamba kubwa linalofanya vizuri hapa Tanzania.

Ameongeza kuwa ziara hiyo ni muhimu kwani wamejifunza kwa kuona namna ya shughuli za uvunaji zinavyofanyika, ufugaji wa nyuki na uchakataji wa asali, na kuona namna shamba linavyotoa ajira za muda mrefu na mfupi kwa jamii inayozunguka shamba sanjari na huduma za kijamii zinavyotolewa kwa jamii inayozunguka shamba.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema amesema Shamba hilo limekuwa la mfano wa kuigwa kwani limeweza kukusanya fedha zaidi ya Sh.bilioni 47 katika uvunaji wa miti kwa mwaka wa fedha 2017/2018 na zaidi ya Sh.Milioni 700 kuanzia Julai 2018 hadi sasa katika zao la utomvu na hilo si jambo dogo.

Akisoma taarifa ya Shamba Kaimu Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill Bwana Daniel Silima alieleza kuwa shamba limeweza kukusanya zaidi ya Sh.bilioni 319 kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2008 hadi sasa na Tsh bilioni 6 kama CESS kuanzia mwaka 2010 hadi disemba 2018 kwa Halmashauri za Wilaya ya Mufindi, Mji wa Mafinga na Kilombero.

Aidha ameeleza Shamba limekuwa likichangia katika shughuli mbalimbali zinazotekelezwa katika jamii inayozunguka shamba kila mwaka kupitia utoaji wa miche ya miti bure kwa wananchi.

Ambapo kwa mwaka huu wa upandaji takribani miche ,Milioni 1 imegawiwa bure kwa wananchi wa mufindi na taasisi mbalimbali lakini pia , ujenzi wa barabara, madawati na kuchangia huduma nyingine za kijamii.

Katika ziara hiyo wageni kutoka Mkoa wa Ruvuma wamepata pia fursa ya kutembelea maeneo ya Shamba la Miti Sao Hill hususani katika maeneo ya ufugaji nyuki, eneo la uchakati wa asali, mnara wa mawasiliano kwaajili ya ulinzi wa msitu dhidi ya moto, bustani ya miche, na hatimaye kutembelea maeneo yanayovunwa utomvu kwa majaribio.

Shamba la Miti Sao Hill ndilo Shamba kubwa kuliko Mashamba yote 24 ya miti ya kupandwa ya serikali ambapo lina ukubwa wa hekta 135,903 ambazo zimehifadhiwa kwaajili ya upandaji wa miti na uhifadhi wa mazingira.

Shughuli za upandaji miti katika shamba hili zililianza kwa majaribio mnamo mwaka 1939 na kuonesha matokeo mazuri mwaka 1951 hivyo upandaji wa miti kwa kiwango kikubwa ulianza rasmi kuanzia mwaka 1960 hadi mapema miaka ya 1980.
 Wakuu wa Wilaya ya Namtumbo, Nyasa na Songea za mkoani Ruvuma walioambatana na wadau wa Shamba la Miti Mpepo lililopo mkoani humo kwenye ziara ya kikazi katika Shamba la Miti Saohill wakipata maelezo kuhusu namna ambavyo miti inaandaliwa kabla ya kupandwa katika shamba hilo.
 Wakuu wa Wilaya ya Namtumbo, Nyasa na Songea za mkoani Ruvuma walioambatana na wadau wa Shamba la Miti Mpepo lililopo mkoani humo kwenye ziara ya kikazi katika Shamba la Miti Saohill wakipata maelezo kuhusu shamba hilo.
 Sehemu ya miti ambayo imepandwa katika Shamba la Saohili
Msafara wa Wakuu wa Wilaya ya Nyasam Namtumbo na Songea mkoani Ruvuma wakielekea katika Shamba la Mitu Saohili ambako wamekwenda kuona namna ambavyo shamba hilo linavyosimamiwa kama sehemu ya kujifunza na kubadilisha uzoefu

Ujumbe wa Benki ya Dunia Waridhishwa na utekelezaji wa Mradi wa ERPP

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akiongoza kikao kazi cha majumuisho ya ujumbe kutoka Benki ya Dunia kuhusu ufuatiliji wa utekelezaji wa Mradi wa kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga (Expanding Rice Production project), Kilichofanyika Jijini Dar es salaam tarehe 22 Mei 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akiongoza kikao kazi cha majumuisho ya ujumbe kutoka Benki ya Dunia kuhusu ufuatiliji wa utekelezaji wa Mradi wa kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga (Expanding Rice Production project), Kilichofanyika Jijini Dar es salaam tarehe 22 Mei 2019.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe ameengoza kikao kazi cha majumuisho ya ujumbe kutoka Benki ya Dunia kuhusu ufuatiliji wa utekelezaji wa Mradi wa kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga (Expanding Rice Production project), mradi ambao unatekelezwa Tanzania bara na Zanzibar. 

Kikao hicho cha majumuisho kimefanyika leo leo Tarehe 22 Mei 2019 katika ukumbi wa ofisi ndogo za Wizara ya Kilimo maarufu kama Kilimo 1 Jijini Dar es salaam.

Ujumbe huo kutoka Benki ya Dunia ukiongozwa na Bi Sarah Simons umeeleza kuridhishwa na kasi ya utendaji kazi katika utekelezaji wa kazi za mradi huo kulingana na malengo yaliyowekwa kwa kipindi cha miezi 6 iliyopita. 

Ujumbe huo ulianza kazi ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mradi huo wa ERPP tarehe 19-21 Mei 2019 ambapo walitembelea Tanzania bara na Zanzibar na walikutana katika wizara ya Kilimo (Bara) na Wizara ya kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi (Zanzibar) na wameshukuru ushirikiano walioupata kwa watendaji wanaosimamia mradi huo.

Aidha ujumbe huo pamoja na kusisitiza kasi ya utekelezaji na ukamilishaji wa kazi za Mradi huo pia waliridhishwa na namna ambavyo mradi umekuwa ukiripoti kuongezeka kwa uzalishaji wa mpunga kwa hatua za awali baada ya wakulima kutumia mbegu bora katika mfumo wa kilimo shadidi (SRI). 

Pia maendeleo mazuri katika maandalizi ya ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji na Maghala kwa kipindi cha miezi sita iliyopita na wamekuwa na matumaini kuwa Ujenzi wa miradi hiyo na kazi zingine zitakamilika kabla ya tarehe ya mwisho ya mradi huo. 

Mhandisi Mtigumwe (Katibu Mkuu Kilimo Tanzania bara) ameushukuru ujumbe huo na kuwaeleza kuwa wataendelea kwa kasi kutekeleza shughuli zilizobaki za mradi huo ili tija kwa wakulima na nchi ionekane. 

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Maliasili, Mifugo na Uvuvi Bi Mansura Kassim aliushukuru Ujumbe huo kwa ufuatiliaji wao na kueleza kuwa Kwa upande wao wataendelea kukamilisha kazi zilizobakia katika mradi na kusimamia mradi huo ipasavyo.

RAIA WA SOMALIA KORTINI KWA TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii

MFANYABIASHARA wa mafuta ambaye ni raia wa Somalia anayeishi jijini Nairobi nchini Kenya, Abshir Afrah (56), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na tuhuma za mashitaka matatu likiwemo shtaka la kukwepa kodi ya Sh. bilioni 8.1.

Akisoma mashitaka, leo Mei 22, 2019, Wakili wa Serikali Wankyo Simon amedai, mshitakiwa anakabiliwa na tuhuma za kesi ya uhujumu uchumi, yenye mashtaka matatu ambayo ni kukwepa kodi, kuisababishia TRA hasara na utakatishaji wa fedha.

Imedaiwa, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Janeth Mtega kiwa, kati ya mwaka 2015 na 2018 ndani ya jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa Afrah alikwepa kodi ya kusambaza mafuta ya Sh 8,107,509,385.48 kinyume na sheria ya kodi ya mwaka 2015.

Pia imedaiwa kati ya 2015 na 2018 maeneo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), jijini Dar es Salaam, kinyume na sheria mshtakiwa aliisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh. bilioni 8.1 kwa kukwepa kulipa kodi.

Aidha siku na mahali hapo mshtakiwa huyo alitakatisha fedha na kujipatia Sh.bilioni 8.1 kwa kukwepa kulipa kodi wakati akijua fedha hizo ni zao la uhalifu wa kosa la kukwepa kodi akiwa na nia ya kuficha ukweli wa fedha hizo

Hata hivyo, mshitakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa sababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi hadi ipate kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo waliomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 4, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na mshitakiwa amerudishwa rumande kwa sababu mashitaka hayo hayana dhamana.


MFANYABIASHARA wa mafuta,raia wa Somalia anayeishi jijini Nairobi nchini Kenya, Abshir Afrah (56),  akitoka katika chumba cha  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,  baada ya kusomewa  mashitaka matatu katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili ambapo mashtaka hayo ni kukwepa Kodi, kuisababishia TRA hasara na utakatishaji wa fedha zaidi ya sh. Bil, 8.1

JWTZ YAPELEKA WANAJESHI KULINDA AMANI DARFUR

VOA SWAHILI: Duniani Leo May 22, 2019.

SEVILLA FC ARRIVE IN TANZANIA AHEAD OF LALIGA WORLD CLASH WITH SIMBA SC

$
0
0
\Sevilla Fs Arrived in Dar es Salaam, Tanzania on Tuesday ahead of a post-season match against Simba as part of the LaLiga World Challenge programme. 
The Squad, accompanied by the technical, club president Jose Castro and Sporting Director Ramon Rodriguez 'Monchi' landed late on Tuesday afternoon at Julius Nyerere International Airport where they were received by local authorities, SportPesa-LaLiga regional partners -representatives and the Spaish Consul in Tanzania, Teresa Martin. Upon Arriving at the airport, the team enjoyed a welcome ceremony and traditional Tanzania dances. 
 Sevilla will face local heavyweight Simba Sc on Thursday 23rd May at 7pm (local Tanzania time) as part of the 'LaLiga World SportsPesa Challenge' at Tanzania National Main Stadium. The Match will be broadcasting locally in Tanzania on Safari TV, on SuperSports across Africa and on beIN LaLiga, LaLiga TV and SFC TV in Spain. 
 Sevilla FC: Founded over one hundred years ago in the Andalusian capital, Sevilla FC are one of just nine clubs to have ever won the LaLiga title (1945/46). Boasting an impressive list of honours, the club have also won five Copa del Rey titles (1935,1939,1948, 2017,2014, 2015, 2016), and one UEFA Super Cup (2006), One of Spain's ,most iconic clubs now know across the world thanks to impressive international success, Sevilla have won nine of their 13 this century. 
 Simba SC: Dar es Salaam side Simba SC are one of Tanzanian football's most historic and successful club. Founded in 1936 as 'Queens,' Simba have won 19 Tanzanian Premier League titles, an almost unmatched record. 
Currently managed by Belgian Coach Partrick Aussems, the current side boasts of a lethal  attacking line led by Rwandan stricker Meddie Kagere and fed by Zambian midfielder Clatous Chota Chama, Simba recently drew international acclaim by reaching the quarter-finals of the CAF Champions League on 2019 for the first time in 25 years, beating the likes of continental heavyweight Al-Ahly of Egypt and AS Vita of Congo along the way. 
 The Sevilla squad to have traveled to Tanzania to face Simba SC in as Follows: 1. Tomas Vaclik 2. Sergi Gomez 3. Simon Kjoer 4. Ibrahim Amadou 5. Roque Mesa 6. Manuel Agudo 'Nolito' 7. Wissam Ben Yedder 8. Ever Banega 9. Juan Sariano 10. Aleix Vidal 11. Sergio Escudero 12. Munir El Haddadi 13. Quincy Promes 14. Franco Vazquez 15. Guiherme Arana 16. Joris Gnagnon 17. Bryan Gil
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images