Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

AWAMU YA KWANZA YA UHAKIKI WA JUMUIYA ZA KIJAMII NA TAASISI ZA KIDINI WAANZA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Kaimu Msajili wa Jumuiya za Kijamii na Taasisi za Kidini kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jesca Shengena akitoa maelekezo kwa Makamu Mwenyekiti wa Kanisa la Mungu Mfalme, Makange Kitua (kushoto), wakati wa zoezi la Uhakiki  wa  Jumuiya  za  Kijamii na Taasisi za Kidini linaloendelea katika Ofisi Ndogo ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Afisa  wa  Kitengo  cha  Jumuiya  za  Kijamii  na  Taasisi  za  Kidini kutoka Wizara  ya  Mambo  ya  Ndani ya Nchi, Neema Ngalawa akihakiki taarifa za Taasisi ya Kidini ya Peaceful Life Ministries wakati wa zoezi hilo linaloendelea Ofisi  Ndogo  ya  wizara  hiyo  jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mchungaji Msaidizi  wa  Kanisa  hilo, Paskazia Makofi.
 Makamu Mwenyekiti wa Kanisa la Mungu Mfalme, Makange Kitua akitoa maelezo ya  taasisi  yake  kwa  Afisa wa Kitengo cha Jumuiya za Kijamii na Taasisi za Kidini kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Neema Ngalawa (kulia),  wakati  wa  zoezi la uhakiki linalofanyika Ofisi Ndogo ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Afisa  wa  Kitengo  cha  Jumuiya  za  Kijamii  na  Taasisi  za  Kidini kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Thomas Sanira akimsikiliza  Katibu Mtendaji  wa  Jumuiya  ya  Istiqama, Issa  Suleiman(kulia), wakati wa zoezi la uhakiki wa taasisi hizo linaloendelea Ofisi Ndogo ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Marekani yalegeza vikwazo dhidi ya kampuni ya Huawei

$
0
0

Serikali ya Marekani imeondoa kwa muda vikwazo vya kibiashara ilivyoweka wiki iliyopita dhidi ya kampuni ya simu ya China Huawei.
Hatua  hiyo inayolenga kupunguza hali ya kuvurugwa wateja wake wanaotumia simu za kampuni hiyo.


Mwasisi wa kampuni hiyo anayesema kuwa Huawei ilikuwa imejiandaa kwa hatua ya Marekani.


Wizara ya Biashara ya Marekani itairuhusu kampuni ya Huawei kununua bidhaa zinazotengenezwa Marekani kwa siku nyingine 90 ili kudumisha mitandao iliyopo na kutoa programu tumishi mpya kwa simu za sasa za Huawei.


Kampuni hiyo kubwa kabisa duniani ya kutengeneza vifaa vya mawasiliano ya simu bado imezuiwa kununua vifaa kutoka nchini Marekani vya kutengenezea bidhaa mpya bila idhini za leseni ambazo kuna uwezekano kuwa zitakataliwa.

Angola kuuzika upya mwili wa Savimbi

$
0
0

Mabaki ya mwili wa aliyekuwa kiongozi wa waasi wa Angola, Jonas Savimbi, yatazikwa tena kwenye mji wake wa Lopitanga mwezi ujao.

Taarifa iliyotolewa jana (Mei 20) na Waziri wa Nchi hiyo Pedro Sebastiao ilieleza kuwa mazishi hayo yangelifanyika baada ya vipimo vya vinasaba kuthibitisha kuwa mabaki hayo ni ya Savimbi.


Savimbi, ambaye alipigana dhidi ya serikali ya Kisoshalisti ya Angola katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 27, aliuawa Februari 22 mwaka  2002 katika mapambano dhidi ya vikosi vya MPLA.


Kifo chake kilifungua njia ya kufikiwa makubaliano ya amani ambayo yalimaliza moja kati ya mizozo ya muda mrefu kabisa Barani Afrika, ambao ulizuka baada ya Angola kupata uhuru wake kutoka Ureno mwaka 1975.


Savimbi alizikwa siku moja baada ya kuuawa katika Jimbo la Mashariki la Moxico.Vipimo vya vinasaba vilivyofanyika katika Maabara za Afrika Kusini, Argentina, Ureno na Angola vilithibitisha kuwa mabaki hayo ni ya mwili wa Savimbi.

Maofisa wa Kenya waenda Dubai kufuatilia kashfa ya dhahabu bandia

$
0
0
Maofisa wa Idara ya Ujasusi nchini Kenya wanaelekea Dubai ili kuchukuwa taarifa ya mwakilishi wa Umoja wa Falme za Kiarabu kuhusiana na sakata la dhahabu bandia linalochunguzwa.

Wakati huohuo, pirikapirika zinaripotiwa Bungeni za kusaka saini ili kumtimua Waziri wa Usalama wa Taifa, Fred Matiangi, kwa madai ya kuwalinda watuhumiwa wa kashfa hiyo. 

Jeshi la Polisi la nchini humo linawashikilia maofisa Polisi waliokuwepo kwenye eneo ilikopatikana dhahabu hiyo bandia wakiwa wanawalinda wanadiplomasia na wala sio wahalifu. 

Maofisa wa Idara ya Ujasusi walitazamiwa kusafiri jioni ya leo Jumanne (21 Mei) kuelekea Dubai ili kuchukuwa taarifa ya mwakilishi wa Umoja wa Falme za Kiarabu kuhusu sakata hilo la dhahabu bandia linalochunguzwa. 

Majasusi hao walitazamiwa kumhoji Ali Zandi anayemuwakilisha Sheikh Mohammed Bin Rashid Al Maktoum na kampuni ya Zlivia inayofanya biashara ya dhahabu Dubai.

WAZIRI WA AFYA AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA JIMBO LA XUZHOU LA CHINA

$
0
0
Na Ramadhani Ali - Maelezo Zanzibar
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed ameiomba Jamhuri ya Watu wa China kurejesha utaratibu wa madaktari wa nchi hiyo wanaokuja kufanyakazi Zanzibar kukaa miaka miwili badala ya mwaka mmoja wa sasa.

Alisema tokea kuanzisha uhusiano wa madaktari wa China kuja Zanzibar mwaka 1965 walikuwa wakikaa kipindi cha miaka miwili lakini utaratibu huo ulibadilika miaka ya hivi karibuni na hivi sasa wanakaa mwaka mmoja.

Waziri wa Afya alitoa ombi hilo alipokutana na Ujumbe wa wataalamu wa afya kutoka Mji wa Xuzhou ambao upo nchini kufanya tathmini ya Madaktari wanaokuja kufanyakazi Zanzibar katika hospitali ya Abdlala Mzee Mkoani na Mnazimmoja.

Aliueleza ujumbe huo kwamba utaratibu wa zamani wa timu za madaktari wa China kukaa miaka miwili ulikuwa unatoa fursa nzuri kwa madaktari wa Zanzibar kujenga uzoefu na kujifunza mambo mengi ya kitaalamu kutoka kwao.

Alisema madaktari wa Zanzibar wanapopata uzoefu kwa vitendo kutoka kwa madaktari wa China inawasaidia kufanya vizuri wanapopata nafasi ya masomo ya juu nje ya nchi.

Waziri Hamad aliushauri ujumbe huo kuwaelekeza madaktari wa China waliopo Zanzibar kuwapa mafunzo madaktari wa Hospitali ya Abdalla Mzee ya kutumia mashine mpya zilizowekwa katika hospitali hiyo na kuitafsiri teknolojia iliyotumika ili baada ya kuondoka waweze kuzitumia.

Aidha Waziri wa Afya aliwahimiza madaktari wazalendo kuwa tayari kujifunza utaalamu kutoka madaktari wa China ambao wamekuwa wakifanya matibabu ya kitaalamu na kuwashirikisha.

Kiongozi wa ujumbe huo Zhou Guangchum alimuhakikishia Waziri wa Afya kwamba nchi yake itaendelea kuisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuongeza msaada wake hasa katika sekta ya afya.

Aliahidi kuwa atalifikisha nchini kwake ombi la kurejesha utaratibu wa zamani wa madaktari wanaokuja Zanzibar kukaa kwa kipindi cha miaka miwili ili waweze kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ndugu zao.
 Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akizungumza na ujumbe kutoka Mji wa Xuzhou Nchini China uliokuja kufanya tathmini ya Madaktari wa nchi hiyo wanaokuja kufanya kazi Zanzibar Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akiagana na Kiongozi wa ujumbe kutoka Mji Xuzhou Nchini China Zhou Guangchum baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ofisini kwake. Picha na Makame Mshenga.

MAGUFULI AZUNGUMZA NA WAKUU WA MIKOA MINNE KWA NJIA YA 'VIDEO COMFERENCE' AKIWA DAR ES SALAAM

$
0
0
  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli amezungumza na wakuu wa mikoa minne nchini na kuwauliza maswali ya papo kwa papo akiwa Makao Makuu Shirika la Simu Tanzania(TTCL) jijini Dar es Salaam kwa kutumia mfumo wa  "Video Conference".

Wakuu wa mikoa ambao Rais Magufuli amezungumza nao kwa mfumo huo ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Songwe na Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Rais Magufuli amezungumza nao leo Mei 21,2019 ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa mfumo wa mawasiliano wa 'Video Conference' ambao umeunganishwa kwa wakuu wa mikoa yote nchini  ili kuweza kufanya kikao na Rais.

Akizungumza wakati anazungumza na wakuu hao wa mikoa pamoja na mambo mengine aliuliza kuhusu hali ya mvua na upatikanaji wa mazao kwa msimu huu wa kilimo ambapo wakuu hao wa mikoa wamemhakikisha Rais pamoja na uhaba wa mvua lakini wakulima wameanza kuvuna mazao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe,amemwambia Rais Magufuli kuwa Mkoa huo mazao yamepatikana ya kutosha licha ya kuwepo kwa uhaba wa mvua lakini Mkoa wao walipata mvua za kutosha.

Rais Magufuli alimuuliza ni mazao gani yamepatikana kwa wingi ambapo alijibu ni mahindi,mpunga,maharagwe na mazao mengine ya chakula na biashara.

Wakati Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella alimwambia Rais kwa Mwanza iko salama na kwamba leo wanaadhamisha miaka 23 tangu kuzama kwa meli ya MV Bukoba iliyozama katika Ziwa Victoria," amesisitiza.

 Rais alimuuliza kuhusu ujenzi wa meli ya kisasa iwapo mkandarasi ameanza kazi ambapo Mongella amejibu mkandarasi tayari ameanza kazi.

"Mheshimiwa Rais mkandarasi ameanza kazi na ana mwezi mmoja sasa.Kazi inakwenda vizuri sana

Hata hivyo Rais Magufuli alitaka kufahamu kuhusu ujenzi wa Kituo cha Afya Ukara wilayani Ukerewe,Mongella amejibu ujenzi umefika hatua nzuri kwani wanatarajia kuanza kuwekamilango na madirisha.

Rais Magufuli pia alitaka kujua hali ikoje kwa TTCL Mkoa wa Mwanza ,amejibiwa kuwa shirika hilo linakwenda vizuri na idadi ya wateja ni kubwa na hivyo kuweza kuchangia pato la Taiga.

Wakati huo huo Rais Magufuli amezungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri ambapo Rais aliuliza kuhusu mvua ambapo alijibiwa kwamba Mkoa huo kuna ukame na hivyo hali ya kilimo sio nzuri sana.

 Hata hivyo Rais alimuuliza Mwanri iwapo ataomba chakula ,amejibu hawezi kuomba chakula kwani wamejipanga na ukame.ambapo ameuzungumzia sio mkubwa sana na kufafanua wanaendelea kuhamasisha wananchi kutunza chakula na kulima mazao yanayostahimili ukame.

"Kuomba chakula siwezi kuruhusu hilo.Kwa sasa tunaendelea kuhifadhi chakula kutokana na ukame.Tunawahimiza wananchi kulima mazao yanayostahimili ukame," amesema Mwanri.

Wakati huo huo Rais alitaka kujua kuhusu ujenzi wa barabara ya lami kutoka Nzega hadi Tabora ,ambapo Mwanri amesema ujenzi unakwenda vizuri.

Baada ya kuzungumza na wakuu hao wa mikoa minne,Rais Magufuli ametumia nafasi hiyo kuwaomba wakuu wa mikoa yote nchini kuitangaza TTCL kwani ni shirika la Watanzania.

"Niwaombee Watanzania tuendelee kulitumia shirika la TTCL,ni shirika letu na lazima wote tuliunge mkono kwani kwa kufanya hivyo ni kumue zi kwa vitendo Baba wa Taiga Mwalim Julisu Nyerere kwa kua zisha shirika hilo," amesema Rais Magufuli.

SHEIKH KIPOZEO AKUTANA NA RAIS DK. MAGUFULI, AMWAMBIA ' I LOVE YOU SO MUCH'

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

I love you so much!Hivyo Sheikh Hilaly Makakara maarufu Sheikh Kipozeo alivyomwambia Rais Dk.Joh Magufuli baada ya kukutana naye jijini Dar es Salaam wakati wa Shirika la Simu Tanzania(TTCL) likikabidhi gawio kwa Serikali.

Sheikh Kipozeo amepata nafasi hiyo leo Mei 21,2019 wakati alipopata nafasi ya kuomba dua kabla ya kuanza kwa tukio la utoaji gawio kwa Serikali kutoka Shirika la Simu Tanzania(TTCL) ambapo Rais Magufuli alikuwa mgeni rasmi.

Wakati anaitwa kusoma dua ,Mshereheshaji wa tukio hilo Tom Mushi ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TTCL amesema Sheikh huyo amekuwa akitamani kumuona Rais Magufuli kwa karibu.

Mushi alisema " Sheikh Kipozeo amekiwa akionekana mitandaoni mara kwa mara akisema anatamani siku moja aonane na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli kwani kuna jambo anataka kumueleza.Sheikh Kipozeo karibu umwambie Rais unachotaka kumwambia.",

Baada ya ukaribisho huo Sheikh Kipozeo alianza kwa kuomba dua na kisha akamwambia Rais Magufuli kwamba "I love you. Mimi ni sheikh wa Rufiji huko, na Rais wangu anatoka Mwanza.Narudia tene I love you," amesema Sheikh huyo mbele ya Rais.

Amesema anayo sababu kubwa ya kumpenda Rais Magufuli na mojawapo ni namna ambavyo Rais amekuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo kwa ajili ya nchi yetu akitolea mfano ununuzi wa ndege nane. 

"Hatukuwa na ndege hata moja lakini Rais Magufuli amenunua ndege nane na binafsi nimezionja ,nimepanda kwenda Mwanza na kurudi na nimepanda kwenda Burundi.Tunakushukuru Rais kwa namna ambavyo unaitumikia nchi yetu kwa uzalendo mkubwa.

" Kazi yetu ni kuhakikisha tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu ili uwe na afya njema kuendelea kulitumia taifa letu la Tanzania,"amesema Sheikh Kipozeo na kusisitiza amefurahi sana kumuona Rais Magufuli kwa karibu zaidi kwani ilikuwa ndoto yake ya siku nyingi.

BENKI YA BARCLAYS YAWAANDALIA FUTARI WATEJA WAKE

$
0
0
 Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Barclays Tanzania kwa wateja wake jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

 Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays, Aron Luhanga (kushoto), akizungumza na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia), pamoja na Mkurugenzi wa Habari katika Ofisi ya Shehe wa Mkoa, Tabu Kawambwa katika hafla hiyo.  
 Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Barclays Tanzania, Hellen Siria (kulia), akisaidia kugawa mlo wa futari kwa baadhi ya waalikwa katika hafla hiyo. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed (katikati), pamoja na baadhi ya wageni waalikwa wakifuturu katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wao jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Baadhi ya wageni waalikwa wakishiriki mlo wa futari uliondaliwa na Benki ya Barclays Tanzania jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

RAIS DK. MAGUFULI APOKEA GAWIO LA SH. BILIONI 2.1 KUTOKA TTCL

$
0
0
*Asema mashirika yasiyotoa gawio yahakikishe yanatoa kabla ya kumalizika kwa Julai

*Asema watakaoshindwa kuchukuliwa hatua , atoa maagizo kwa ofisi za umma

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli ameagiza mashirika yote 253 yaliyopo nchini ambayo Serikali ina hisa yawe yametoa gawio kabla ya kumaliza Julai mwaka huu huku akisisitiza wote ambao hawajatoa waandikiwe barua kwani ni lazima waliopewa jukumu watimize wajibu wao.

Amesema haiwezekani mashirika 24 tu ndio yawe yametoa gawio la Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 huku akisisitiza mashirika kutoa gawio kwa Serikali fedha hizo ndizo ambazo zinatumika kwa ajili ya shughuli za maendeleo nchini ikiwemo ya ujenzi wa kituo vya afya pamoja na miundombinu mingine.

Rais Magufuli amesema hayo leo Mei 21,2019 wakati Shirika la Simu Tanzania(TTCL) likitoa gawio kwa Serikali ambapo limekabidhi gawio la Sh.Bilioni 2.1.

"Nipowapongeze TTCL kwa namna ambavyo mmekuwa mstari katika kutoa gawio kwa Serikali.Ni uzalendo huu ambao mmeuonesha na naamini mwakani tarehe kama ya leo mtanialika tena kuchukua gawio la Serikali," amesema Rais Dk.John Magufuli.

Wakati huo huo ,Rais Magufuli ametumia nafasi hiyo kutoa maagizo kwa mashirika yote ambavyo hajatoa gawio la Serikali kutoa gawio kabla ya kumalizika Julai mwaka huu na kumtaka Msajili wa Hazina kuyaandikia barua mashirika hayo na kufafanua kati ya mashirika hayo ni 24 tu ndio yamelipa gawio.

Rais Magufuli amesema mashirika yatoe gawio na lazima yabanwe kwani kutoa gawio ni takwa la kisheria huku akisisitiza haiwezekani mashirika yasitoe gawio kwa kisingizo cha kutopata faida.

"Ni lazima yatoe gawio na kabla mwezi huu kwisha nipate majina ya mashirika ambavyo yatakuwa hajatoa ,kama hayapati faida kwanini wanaendelea kuwepo na hata namna ambavyo waliyapata mashirika ni sasa na bure," amesema.

Wakati huo huo Rais Magufuli amesema amesikitishwa na taarifa ya ofisi nyingi za Serikali kutotumia mawasiliano ya simu ya TTCL licha ya kwamba yeye mwenyewe alitoa maagizo mwaka jana.

Amesema amesikitika zaidi baada ya kusikia hata Ofisi ya Rais Ikulu nayo haikutajwa na TTCL kuwa miongoni kwa wanaotumia mawasiliano hayo. Ameagiza ofisi za Serikali zote ikiwemo ofisi yake kuhakikisha zinatumia laini za TTCL na kwamba yeye anayo laini ya TTCL ambavyo anailipia kwa fedha zake mwenyewe.

Amesisitiza wakuu wa idara pamoja na watumishi wengine wa Serikali kuhakikisha wanakuwa na laini za TTCL na kwamba amemwambia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Waziri Waziri Kindamba kumuandalia orodha ya wakurugenzi ambao wanatumia laini za shirika hilo.

"Nataka uniandikie majina ya wakurugenzi ambao wanatumia laini za TTCL na sio kwamba wanazo tu nataka nione zinatumika.Sio kwamba msiwe na laini za kampuni nyingine hapan,Ila nataka hizi ambazo Serikali inatoa fedha kwa ajili ya mawasiliano basi ziende kwa shirika hili ambao ni la kwetu Watanzania na lazima tulijengee uwezo ili lijiendeshe," amesema Rais Magufuli.

Pia ametumia nafasi hiyo kuzungumzia fedha ambazo Shirika hilo inalipa kwa ajili ya kulipia minara  ambapo amesema umefika wakati kuwa na minara yake kwani haoni sababu ya kuendelea kuona TTCL inatumia fedha nyingi kulipia gharama ya minara ya simu.

Awali Waziri Kindamba ametumia nafasi hiyo kuelezea mafanikio ambayo Shirika la TTCL wameyapaya bado wanahitaji fedha zaidi kujiendesha na hivyo amekumbusha kupatiwa fedha ambazo Serikali iliahidi ambapo Rais Magufuli ameagiza Wizara ya Fedha kutoa fedha hizo kwa shirika hilo.

Ameongeza kuwa gawio la Sh.bilioni 2.1 ambalo wamelitoa kwa Serikali inatokana na kazi  nzuri ambayo inafanywa na wahasibu wao katika kuandaa hesabu na kisha kupitiwa na mkaguzi wa ndani na baada ya hapo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).

Amesema kutolewa kwa gawio hilo ni baada ya kupitiwa kwa hesabu na kisha faida ambayo wameipata sehemu ya fedha ndio hilo gawio ambalo ni ongezeko la Sh.milioni 600 ukilinganisha na mwaka jana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Gawio la Serikali kiasi cha Shilingi Bilioni 2.1 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Waziri Kindamba, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Omar Nundu katika hafla fupi iliyofanyika katika makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam

ZIMAMOTO YATOA UFAFANUZI KUHUSU MAFUNZO YA KINGA NA TAHADHARI DHIDI YA MAJANGA YA MOTO KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

SPIDI YA SIMBA YAMKOSHA MASANJA MKANDAMIZAJI NA SASA ANASUBIRI KOMBE

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MCHEKESHAJI maarufu nchini Masanja Mkandamizaji amesema spidi ya timu ya soka ya Simba inampa raha na kwamba mashabiki wa timu hiyo kwa sasa wanasubiri kombe lao.

Masanja ambaye ni shabiki mkubwa wa timu ya Simba , amesema hayo wakati anazungumzia uwezo wa timu hiyo kisoka ambapo amesema kuwa Simba inaleta raha na hasa kutokana na aina ya kandanda safi ambalo wachezaji wanalionesha wawapo uwanjani.

"Kwa kweli timu ya Simba iko vizuri sana, wanacheza kandanda la kuvutia na ukweli tumebakisha hatua moja tu kuchukua kombe,"amesema Masanja.

Mchekeshaji huyo ambaye pia ni Mchungaji , amesema amekuwa akifuatilia kwa karibu uchambuzi wa soka na anavutiwa zaidi na mchambuzi Mwalim Kashasha ambaye ana aina yake ya kuchambua mpira.

"Navutia sana na Mwalimu Kashasha , anaswaga ya kuvutia sana kiasi cha kuleta hamu ya kumsikiliza,"amesema Masanja huku akisisitiza Simba iko kwenye spida ya kuchukua ubingwa tu.

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA GAWIO LA SERIKALI KIASI CHA SHILINGI BILIONI MBILI TTCL

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Waziri Kindamba wakati akiwasili katika Makao Makuu ya Ofisi za Shirika hilo katika Gorofa la Extelecom Posta jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa Mikoa minne nchini kwa njia ya Simu ya Video Conference mara baada ya kuwasili katika   Makao Makuu ya Ofisi za Shirika hilo la TTCL lililopo katika Gorofa la Extelecom Posta jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Gawio la Serikali kiasi cha Shilingi Bilioni 2.1 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Waziri Kindamba, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe pamoja na  Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Omar Nundu katika hafla fupi iliyofanyika katika makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vitendea kazi mbalimbali katika makumbusho iliyopo ndani ya Ofisi za Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali waliofika katika hafla ya upokeaji wa Gawio kwa Serikali kutoka kwa Shirika la Mawasiliano TTCL jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Waziri Kindamba mara baada ya kuwasili katika eneo la utoaji wa Gawio katika ofisi za Shirika hilo jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa TTCL mara baada hafla ya upokeaji wa Gawio la Serikali katika Ofisi hizo za TTCL. PICHA NA IKULU

VIDEO YA NIMENASA YA AMINI, NA LINA SASA YAINGIA MTAANI

$
0
0
VIDEO ya wimbo mpya wa msanii maarufu nchini Amini Mwinyimkuu a.k.a Amini unaofahamika kwa jina la Nimenasa ambao amemshirikisha mwanadada Lina Sanga imeingia mtaani. 

Akipiga stori ya Michuzi Blog leo Mei 21, 2019 jijini Dar es Salaam Amini amesema video ya wimbo huo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya na sasa imekamilika kwani tayari ameiachia na iko mtaani na hasa katika mtandao wa youtube . 

"Video yangu mpya ya wimbo ya Nimenasa tayari imekamilia na leo ipo mtaani kwa maana ya link yake ipo mitandaoni.Ni video ambayo ina tofauti kubwa na video zangu za zamani kutokana na aina ya mazingira ambayo nimerekodia. 

"Katika kuhakikisha video yangu inakuwa tofauti nimeamua kwenda kurekodi katika hifadhi ya Msitu wa Magamba ambako ni tulivu na kuna mazingira mazuri. Hivyo kuna tofauti kubwa na mashabiki nimewapa kile ambacho walikuwa wanakihitaji kutoka kwangu,"asema Amini. 

Ametumia nafasi hiyo kufafanua ujumbe wake kwa Watanzania kwanza wahakikishe wanaiangalia video ya wimbo huo na kisha wajenge tabia ya kufanya utalii wa ndani kwani sehemu ya video ya Nimenasa amerekodi akiwa katika hifadhi ya msitu wa Magamba. 

Pia amesema hadi kufikia hatua ya kukamilika kwa video hiyo na kuiingiza mtaani, anatoa shukrani zake kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) kwani aliwaomba sehemu ya kwenda kurekodia na akukabuliwa."Nawashakuru kwani niliwafikia na wakanisaidia sana TFS."

MAGANGA: TUTACHEZA KWA NIDHAMU DHIDI YA MTIBWA SUGAR HAPO KESHO HUKU TUKIISAKA ALAMA 3 MUHIMU.

$
0
0
 Na Agness Francis, michuzi Tv. 

MABINGWA  wa Afrika Mashariki na kati Azam fc kesho watashuka dimbani kuvaana na wakatamiwa wa Morogoro Mtibwa Sugar katika mchezo wa 37  mzunguko wa pili Ligi soka Tanzania bara. 

Afisa habari na msemaji wa klabu ya Azam fc Jaffary Maganga amezungumza leo Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa mtanange huo Utapigwa katika dimba la uwanja wa Azam Complex Chamazi majira ya saa mbili usiku. 

"Baada ya kupoteza mchezo wetu uliopita dhidi ya Simba kwa kutoka  suluhu ya bila kufungana sasa tunashuka tena dimbani kuwakaribisha  Mtibwa Sugar ambapo tunajua kuwa ni timu kongwe na yenye uzoefu iliyopo ligi kuu muda mrefu"amesema Jaffary. 

Maganga amesema kuwa mchezo huo utakuwa wa ushindani kwao hivyo wanahitaji kucheza kwa utulivu na nidhamu ya hali ya juu ili kuhakikisha wanashinda gemu hiyo. 

"Tunakumbuka mchezo wa kwanza Mtibwa walifanikiwa mutufunga mabao 2-0 Sasa na sisi tutapambana  kutafuta ushindi wa nyumbani ukizingatia walimu walipata nafasi nzuri ya kuweza kuandaa timu kwa muda mrefu"amesema Msemaji huyo. 

Aidha ameeleza kuwa kikosi chao hakina majeruhi wachezaji wote wako fiti wapo tayari kwa ajili ya kupambania ushindi mnono wa alama 3 wakiwa nyumbani.

Azam anashuka dimbani akiwa nafasi ya 3 alama 69 akiwa ameshacheza michezo 36,huku yanga wakiwa juu yao kwa alama 83 wakiwa na michezo sawa, ambapo wekundu wa msimbazi Simba akiwa kinara wa Ligi kuu soka Tanzania bara akiwa na alama 88 na michezo 35.

MAJALIWA AIWAKILISHA SERIKALI KATIKA MAZISHI YA ASKOFU MSTAAFU WA JIMBO KATOLIKI LA MTWARA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki la Mtwara, Mhashamu Gabriel Mmole katika mazishi yaliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Watakatifu Wote Mjini Mtwara, Mei 21, 2019. Kulia ni Askofu wa Jimbo la Geita na  Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Flavian Kasalla.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza katika  Mazishi ya Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki la Mtwara,Mhashamu Gebriel Mmole kwenye Kanisa Kuu la Watakatifu Wote mjini Mtwara, Mei 21, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Askofu wa Jimbo Katoliki la Mtwara, Titus Joseph Mdoe katika mazishi ya Askofu Mstaafu wa Jimbo Katolki la Mtwara, Mhashamu Gabriel Mmole yaliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Watakatifu Wote mjini Mtwara, Mei 21, 2019.
 Waombolezaji wakiuweka kaburini mwili wa Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki la Mtwara, Mhashamu Gabriel Mmole katika mazishi yaliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Watakatifu  Wote mjini Mtwara, Mei 21, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka udongo  kwenye kaburi la Askofu Mstaafu wa Jimbo la Mtwara, Mhashamu Gebriel Mmole katika mazishi yaliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Watakatifu Wote mjini  Mtwara, Mei 21, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin Mkapa  wakishiriki katika Ibada ya mazishi ya Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoloki la Mtwara, Mhashamu, Gabriel Mmole  iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo la Mtwara,Titus  Mdoe (kushoto)  kwenye Kanisa Kuu la Watakatifu Wote mjini Mtwara, Mei 21, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiweka shada la maua kwenye kaburi la Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki la Mtwara, Mhashamu, Gabriel Mmole katika mazishi yaliyofanyika kwenye Kanisa la Watakatifu Wote mjini Mtwara, Mei 21, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 21.05.2019

EWURA CCC YATOA ELIMU ZAIDI YA WANAFUNZI 70 CHUO KIKUU HURIA TANZANIA TAWI LA ARUSHA.

$
0
0
 Getrudi Mbilingi Afisa Utawala na Utumishi Ewura CCC Makao Makuu Dar es salaam akitoa ufafanuzi kuhusiana na haki ya mtumiaji wa Nishati na Maji.
 Lukingo Lukingo Afisa Menejimenti na Huduma kwa Wateja Ewura CCC akiwa anatoa ufafanuzi kuhusiana na kazi zinazofanywa na Taasisi hiyo ya serikali.
Said Mremi Afisa Uhusiano Tanesco Mkoani Arusha ;ni lazima mteja anapoluja kuomba kuunganishiwa umeme wakati anajaza fomu ya maombi lazima ajaze kwa usahihi,ahainishe idadi ya vifaa ambavyo anahitaji kuvitumia ili ikitokea hitilafu shirika liweze kuona namna ya kulipa fidia kwa mteja huyo
Jennifer Daniel Katibu wa kamati ya watumiaji huduma ya mkoa wa Arusha  (RCC) akiwasilisha mada kwa wanafunzi wa Chuo kikuu huria Nchini Tanzania tawi la Arusha  namna ya kutoa malalamiko kwa njia sahihi ili mteja aweze kulipwa stahiki zake 

 Dkt.Peter Kashingo Mwenyekiti RCC Mkoani Arusha.Aizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu huria nchini Ranzania tawi la Arusha 
baadhi ya washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Taasisi ya kiserikali ya EWURA CCC mkoa wa Arusha iliyowajumuisha wanafunzi wa Chuo kikuu huria Tanzania tawi la Arusha 
Gerald sambayuka Mjumbe wa kamati ya watumiaji wa mkoa ambayo ipo chini ya EWURA CCC mkoani Arusha
Washiriki wa semina kutoka Chuo kikuu huria nchini Tanzania tawi la Arusha wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali  zinazowasilishwa katika mafunzo yaliyoandandiliwa na Baraza la uUshauri la watuamiaji wa huduma ya a Nishati na Maji  Ewura CCC 
Injinia Raymond David ambae ni Mhazini wa RCC Arusha akitoa ufafanuzi wa sheria kwa watumiaji wa wa huduma za Nishati na Maji .
 Getrudi Mbilingi Afisa Utawala na Utumishi Ewura CCC Makao Makuu Dar es salaam akitoa ufafanuzi kuhusiana na haki ya mtumiaji wa Nishati na Maji.
 Kutoka katikati ni Lugiko Lugiko Afisa Menejimenti na Huduma kwa wateja  Ewura CCC Jijini Arusha,wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ewura CCC Dkt.Peter Kashingo,kulia kwake ni Mhazini wa RCC Arusha Raymond David,Kutoka kulia ni Jennifer Daniel Katibu RCC Arusha,kulia kwake ni Gerald sambayuka Mjumbe wa kamati ya watumiaji wa mkoa ambayo ipo chini ya EWURA ccc mkoani Arusha


Na.Vero Ignatus,Arusha.

Baraza la uUshauri la watuamiaji wa huduma ya a Nishati na Maji EwuraCCC imeendesha programu ya mafunzo kwa wanafunzi zaidi ya sabini wa Chuo Kikuu Huria Tanzania katika tawi la Arusha.

Lukingo Lugiko ni Afisa Menejimenti na Huduma kwa wateja Ewura CCC amesema semina hiyo ni sehemu ya uelimishaji ambazo wanalenga kuifikia jamii ya watanzania hususani watumiaji wa huduma za Nishati na Maji. 
Lukingo amesema lengo kubwa ninkuwafundisha watumiaji wa huduma hizo kuzitambua haki zao kwani watu wengi hawajui haki na wajibu wao kama walaji. 

"Watanzania wengi wanatabia ya kunung'unika badala ya kulalamika kwa maandishi ili wahusika waweze kutatua matatizo yao yananyowakabili wao kama walaji" alisema Lugingo

Getrudi Mbilingi Afisa Utawala na Utumishi Ewura CCC Makao Makuu Dar es salaam akitoa ufafanuzi kuhusiana na haki ya mtumiaji wa Nishati na Maji amesema kuwa taasisi inayo dawati kwa uelimishaji kwa umma kuhakikisa taarifa zinafika kwa kushirikiana na watoa huduma na watendaji wa serikali za vijiji na mitaa ammbao wanafanya nao kazi kwa ukaribu

Said Mremi ni Afisa uhusiano kutoka Tanesco ambaye alimuwakilisha meneja amesema kuwa mteja kabla ya kuomba kunganishwiwa huduma ya umeme ni vyema akajaza fomu kwa usahihi sambamba na idadi ya vifaa amabavyo mteja atavitumia ili tatizo litakapotokea iwe rahisi kutatuliwa au kupewa fidia kwa mteja husika.

"Kama mteja ana madai ya fidia anayohisi yamesababishwa na tanesco swala la utaratibu la ulipaji wa fidia tanesco wanadawati la fidia,vyema mteja husika alete malalamiko yake kwa maandishi na awe na uhakika kwamba anachokileta ni kile alichokijaza kwenye fomu maana kuna baadhi ya wateja ni waongo na wanataja taarifa za uongo"alisema Mremi

Akijibu swali la mmoja wa washiriki wa semina hiyo kuhusiana na tatizo la kukatikakatika kwa umeme na kwanini tanesco hawalipi fidia Mremi amesema kuwa yapo matatizo ya umeme ambayo tanesco wananyapanga na wanatoa taarifa kwa wateja wao, matatizo mengine yanatokea kwa dharura siyo kwa kupanga ambayo yapo nje ya uwezo wa Tanesco.

"Mfano limepita gari lina vyuma likakata nyaya na umeme ukakatika,mtu amekata mti huko ukaangukia nyaya umeme ukakatika huwezi kuja kuidai tanesco kisa samaki zako zimeharibika,mtu amegonga nguzo akakimbia wananchi wamechelewa kutoa taarifa hilo halowezi kuwa kosa letu hilo ni tatizo la umeme la dharura" alisema Mremi

Dkt.Peter Kashingo ni Mwenyekiti wa kamati ya RCC mkoa amesema kutumia teknolojia mpya ambayo inaweza kupunguza matumizi ya umeme majumbani kutoka 50%-70% kwa kuthibiti muda ambao taa huwaka bila sababu za msingi.

"Utumiaji wako mzuri wa huduma ya umeme ni moja ya njia sahihi ya haraka za kupungiza bili yako ya Nishati." Alisema Dkt.Peter Kashingo.
Injinia Raymond David ni Mhazini wa Ewura RCC ambapo amesema kuwa mtoa huduma anatakiwa kuhakikisha hatuabanazochukua dhidi ya mteja aliyeshindwa kulipa bili ni sahihi na siyo za kibaguzi

"Hakuna mteja atakayekatiwa huduma kama notisi ya siku 30 haijatolewa" alisema Raymond.Ewura CCC ni Taasisi ya Kiserikali iliyoanzishwa kwa lengo ka kutetea na kulinda maslahi ya watumiaji wa Nishati na Maji katika sura 414 ya sheria ya Ewura kifungu cha 30

Waziri Kabudi akutana na Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID)

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID) Bi. Jane Edmondson alipomtembelea na baadhi ya wajumbe wake katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam Mei 21, 2019 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimwelezea jambo Bi. Jane Edmondson pamoja na ujumbe alioambatana nao 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID) Bi. Jane Edmondson 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID) Bi. Jane Edmondson (wa pili kutoka kushoto) pamoja na wajumbe alioambatana nao, wa kwanza kushoto ni Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Tunsume Mwangolombe 

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK LEO

WACHUNGAJI WALA NONDOZZZZ MINNESOTA, MAREKANI

$
0
0
Wachungaji watatu kutoka KKKT DMP na mmoja kutoka KKKT Dayosisi ya Ziwa Victoria  Shinyanga Wamehitimu katika Chuo Kikuu cha Luther Seminary Minnesota nchini Marekani tarehe 19/05/2019 kama ifuatavyo:-  Rev. Dr. Ernest William Kadiva ametunukiwa Phd - Doctor of Ministry,  Wengine wametunukiwa Master of Arts degree nao ni Rev. Kishe Dismas Mhando - na Rev. Kaanasia Geofrey Msangi, pia Rev. Martha Ernest Ambarang'u wa Dayosis ya Ziwa Victoria Shinyanga ametunukiwa Masters of Arts degree katika mahafali ya 150 iliyofanyika hapa Central Lutheran Church, Minneapolis na kuhudhuriwa na mamia ya wageni kutoka nchi mbalimbali na kutoka majimbo mbalimbali ya Marekani.  Picha kwa hisani ya Noah William Kadiva akiwa Minnesota, Marekani.
   Ndugu, jamaa na marafiki wakifurahia baada ya Rev. Dr. Ernest William Kadiva kutunukiwa Phd - Doctor of Ministry, na wengine waliotunukiwa Master of Arts degree Rev. Kishe Dismas Mhando - na Rev. Kaanasia Geofrey Msangi, pia Rev. Martha Ernest Ambarang'u wa Dayosis ya Ziwa Victoria Shinyanga 

Rev. Dr. Ernest William Kadiva akitunukiwa Phd - Doctor of Ministry baada ya kuhitimu katika Chuo Kikuu cha Luther Seminary Minnesota kwenye sherehe zilizofanyika Central Lutheran Church, Minneapolis,    nchini Marekani
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images