Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

WANAFUNZI WA KIKE KUPATA MIMBA NI VIASHIRIA TOSHA VYA KUWEPO MAAMBUKIZI MAPYA YA VIRUSI VYA UKIMWI-UNAIDS

$
0
0

Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (uNIDS) Dkt. Leo Zekeng,(kulia Mwenye ) akizungumza na mtoa Muuguzi Mara baada ya kutembelea Kituo cha afya Halmashauri ya Busokelo ambacho pia kinatoa huduma za dawa kwa wagonjwa wa HIV ,kulia Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti UKIMWI  Tanzania (TACAIDS),Dkt.Leonard Maboko ambaye ameambatana na Mkurugenzi huyo 
 Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti UKIMWI  Tanzania (TACAIDS),Dkt.Leonard Maboko akizungumza na wajumbe wa kamati ndogo za kudhibiti Ukimwi Ngazi ya Kata Halmashuri ya Busokelo Mkoaani Mbeya.
 Wajumbe wa kamati ndogo za kudhibiti na kupambana na UKIMWI katika Halmashauri ya Busokelo Mkoani Mbeya wakimsikiliza Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (uNIDS) Dkt. Leo Zekeng (hayupo pichani) katika semina ya kuwajengea uwezo wajumbe hao ambayo inafadhiliwa na shirika hilo.
 Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNIDS) Dkt. Leo Zekeng,akizungumza na  wajumbe wa kamati ndogo za kudhibiti na kupambana na UKIMWI katika Halmashauri ya Busokelo Mkoani Mbeya (hawapo pichani) Leo Mei 20,19.




SHIRIKA la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa(UNAIDS), limesema ongezeko la watoto wa kike walio chini ya umri miaka kati ya 15-25 ni viashiria tosha vya uwepo wa maambukizo mapya ya virusi vya ugonjwa wa UKIMWI. 

Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika hilo, Dkt. Leo Zekeng, alipotembelea na kuzungumza na wajumbe wa kamati ndogo za kudhibiti na kupambana na UKIMWI katika Halmashauri ya Busokelo Mkoani Mbeya. 

Amesema, jamii inapaswa kutambua kuwa kitendo cha mwanafunzi wa kike kupata mimba ni viashiria tosha vya uwepo wa maambukizo ya virusi vya ugonjwa wa ukimwi hivyo jitihada zaidi zinahitajika katika kuwalinda watoto na jamii nzima. 

Aidha, ameitaka jamii kuondokana na vitendo vya kuwanyanyapaa watu wanaoishi na virusi vya ugonjwa wa UKIMWI ili kupunguza kasi ya maambukizo mapya. 

“Watu wanaogopa kwenda kupima afya zao kwani wanaamini kwamba endapo watagundulika kuwa wamepata maambukizo na kuanza kutumia dawa basi jamii itawatenga, hali inayochangia kwa kiasi kikubwa kutofanikisha malengo ya serikali na mashirika binafsi ya kupunguza au kutokomeza ugonjwa huo,”amesema. 

Hata hivyo, akizungumzia hilo, Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), amesema ofisi hiyo inazitegemea sana kamati hizo katika kufikisha elimu kwa jamii kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji na mitaa hivyo ni vema wakajituma na kuliweka suala la UKIMWI kuwa ni agenda ya kudumu. 

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 21,2019

Tigo yaendesha zoezi la usajili wa laini Wizara ya Mambo ya Ndani

$
0
0
 Afisa huduma kwa wateja kutoka Kampuni ya Tigo Obrien Kinunda, akimsajilia  laini ya simu Mkuu wa Nidhamu wa Jeshi la Polisi Oscar Mushi kwa kutumia mfumo mpya wa usajili unatumia alama za vidole katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam jana.

Afisa huduma kwa wateja wa kampuni ya Tigo Nimzihirwa Elias, akimsajilia laini ya simu mmoja wa wateja wa kampuni hiyo ambaye ni mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kutumia utaratibu mpya wa usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole zoezi lililofanyika makao makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam jana.
 Afisa huduma kwa wateja wa kampuni ya Tigo Nimzihirwa Elias, akimsajilia laini ya simu mmoja wa wateja wa kampuni hiyo ambaye ni mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kutumia utaratibu mpya wa usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole zoezi lililofanyika makao makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam jana.




Afisa huduma kwa wateja wa kampuni ya Tigo Pendo Stephen, akimsajilia laini ya simu mmoja wa wateja wa kampuni hiyo ambaye ni mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kutumia utaratibu mpya wa usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole zoezi lililofanyika makao makuu yan Wizara hiyio jijini Dar es Salaam jana.

WAJUMBE WA BODI YA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA HAWA HAPA.

TODAY IS THE 23rd ANNIVERSARY OF THE MV BUKOBA DISASTER!!!

$
0
0




Today, Tanzania marks 23 years since the tragic MV BUKOBA accident.

On the morning of May, 21, 1996, a ship christened MV BUKOBA, carrying more than 1000 passengers as well as cargo, overturned and sank 30 nautical miles off Mwanza, in Lake Victoria, just an hour before docking at Mwanza port.

MV BUKOBA was built in 1979 and had a capacity for 850 tons of cargo and 430 passengers only.

The then Tanzania's President, HE Ben Mkapa, declared three days of national mourning and formed a probe commission headed by Mr. Justice ROBERT KISANGA.

According to a report issued by the probe commission, over 700 people perished while 114 others, were lucky to survive the accident. One ABU UBAIDAH AL- BASHIR, who was then second in command of Al Qaeda, was one of those who died in the disaster. 

A tower of memories was built at Igoma on the outskirts of Mwanza town were victims were buried in a mass grave.

Mr. GOFREY NYAISA SIMANGO, hitherto a Prison warder at Ukonga Maximum prison but now working with the Bank of Tanzania, was one of the lucky survivors of the worst marine transport accident in Tanzania.

Inspired by the burning desire to tell the world what happened before and after the ship capsized, a few years ago, Mr. NYAISA wrote a Swahili book "SITASAHAU MV BUKOBA" in which he chonicled the horror as it unfolded during that fateful morning. As a great lover of books, I really enjoyed reading this book!.

This is a true heartbreaking story, a depiction of how negligence, complacency, greed and corruption on the part of the establishment, could cost the nation very dearly. This unique and unputdownable book by Mr. NYAISA, prefaced by  Prof. HAROUB OTHMAN, is A MUST- READ and is readily available in all major bookshops across the country. For the sake of preserving history and the love of our nation, I recommend it as one of Tanzania's Best Sellers!. The following quote from NYAISA's book evidences what I have stated above(Translation mine):

"Tickets were available through the back door, even if you came late. Multitudes jammed the dock with their belongings as if fleeing a war zone!. Those who failed to board hurriedly hired taxis in order to catch up with the vessel at Kemondo bay. All hell broke loose when the ship swayed violently as we were sipping our soft drinks. The refrigelators droped on the floor with a loud bang! Bottles of beer and soda broke into pieces and littered the floor! I honestly feared for my dear life!. 

The ship tilts to the left, then right and then makes about turn, she has overturned! Good God, my life is over...I am dead! My mind veered off from the swaying ship and reached my home village in Musoma. I saw my younger siblings screaming and wailing after my body is brought home from the accident scene!.  When Mv Bukoba was swaying, someone grabbed my underpants as we hussled for lifebuoys.

 I felt relieved because when you are under the water, your clothes are nothing but a heavy burden!. I was thus completely naked, am telling you!. The only thing I was wearing was my watch. When the rescue boats arrived, we were given clothes but most of us rejected them. 

Men and women sat together, all naked, we didnt care!. It was a frightening scenario but no authority, not even the Tanzania Railways Authority which  operated the vessel, came foward to quell this  manmade storm", narrates Mr. NYAISA.

Thereafter, four TRC officials including Mr. JUMANNE MWIRU, the Captain of MV BUKOBA, were subsequently charged with 159 counts of the offence of Manslaughter contrary to section 195 of the Penal Code, Cap 16 of the Laws before Mr. Justice JUXTON MLAY in criminal case no. 22/1998.

The high court of Tanzania at Mwanza commenced hearing on the case on 14th May 2001 and on the 22nd November 2002, Judge MLAY acquitted all the accused persons stating:

"Our mourning people and nation respect and live under the rule of law which presumes every individual to be innocent no matter how grave the offence may be until proved by credible and clear evidence that he is guilty. The prosecution evidence has not established the guilt of any accused person beyond reasonable doubt. In our system of criminal justice, they are entitled to be acquitted of all charges".

Ms FLAVIANA MATATA, Tanzania's world famous model based in the US, who lost her mother in the shocking accident, has been, for many years, hosting various events to commemorate the death of her mother:
"I lost my mother when I was only 8 years old. Losing my mother has left a deep scar on my life. For several years I have wanted to transform this loss and pain into something more meaningful, which is why I have launched the Flaviana Matata Foundation. For me this was not only a way to give back to the community but more importantly a way to pay tribute to my mother who was one of the most generous women I have ever known.

 She used to pay school fees of many children, and particularly, young girls. I decided to do something connected to the MV BUKOBA tragedy and to the memory of my mother. I thus personally got in touch with a manufacturer of life vests and ordered 500 life vests and shipped them to Tanzania and delivered in Mwanza city. 

I am now looking foward to every future 21st May with a different perspective. No longer is my heart heavy and no more do I think of it in dread, but I look foward to making every 21st May meaningful not only to me but to the people of Tanzania and to future passengers", said former Miss Universe Tanzania on 26th May 2011.

This morning, Mr. GODFREY SIMANGO NYAISA and 114 people who were lucky to survive the accident on 21st May 1996 and who are still alive together with other Tanzanians, will be commemorating the 23rd anniversary of the sinking of MV BUKOBA, in remembrance of those who perished with it. This is a historical event which must not be allowed to die. It must be told again and again for everyone to get to know their role and responsibility towards protecting lives. 

As we mark 23 years of MV BUKOBA accident, we should come together as a nation and set strong strategies that will help us to end marine accidents in the country. The preface by Prof. HAROUB OTHMAN, in NYAISA's book, tells it all. He criticises the then Ministry of Communication and Transport's inability to rein in corruption, negligence and inefficiency in the TRC.

My heart goes out for all families that lost their loved ones, for the kids who lost their parents and adults who lost their life partners. May the Almighty God continue strengthening you.




Tanzanzania kuwa kitovu cha kuzalisha chakula Afrika.

$
0
0
Serikali ya Ufaransa kupitia Balozi yake nchini Tanzania imeahidi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA na wadau wengine kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha uzalishaji wa chakula na malighafi zingine katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. 

Hayo yamesemwa na Balozi wa Ufaransa nchi Tanzania Mhe. Balozi Fredrick Clavier wakati wa ziara yake chuoni hapo iliyolenga kujifunza kuhusu Mradi wa Kilimo Hifadhi unaofadhiliwa na Ubalozi wa Ufaransa kwa kushirikiana na Shirika la Misaa la Switzerland (SWISSAID) na kutekelezwa na timu ya watafiti wa SUA, SAT na TOAM ambapo Ubalozi huo umechangia kiasi cha EURO 850,000. 

“Mradi huu ni wa miaka mitano unalenga kuboresha maisha ya wakulima wadogo wapatao 6000 na kuhifadhi bayoanuai na mazingira kupitia uzalishaji kwa kutumia kilimo hai, matumizi sahihi ya mnyororo wa thamani wa kilimo hai, kuimarisha vikundi 269 vya wakulima wadogowadogo taasisi mwamvuli za vyama hivyo na kuweka kumbukumbu mbinu za kilimo hai zilizokubaliwa na wakulima ili kusaida utetezi wa kitaifa na kimataifa” Alisema Balozi Fredrick Clavier. 

Balozi huyo aliongeza kuwa katika mikakati yake anataka kuona kunakuwa na ushirikiano mkubwa kati ya wataalamu wa SUA na vyuo vingine kutoka nchini Ufaransa ambapo pamoja na mambo mengine wataalamu hao waweze kutembeleana wakiwashirikisha wanafunzi kwa lengo la kubadilishana uzoefu. 

Aidha, Balozi huyo amewataka wataalamu wa SUA, FAO, IRD na SWISSAID kukaa pamoja na kuangalia maeneo mawili au matatu ya mashirikiano katika utafiti na kuandika mradi wa pamoja na kisha kuuwasilisha kwake ili aweze kuuombea fedha kwenye Serikali yake maana hela ipo. 

Awali akitoa taarifa fupi ya kazi za SUA, Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda alisema kuwa Serikali ya Ufaransa ina historia ya muda mrefu ya SUA kwani imefadhili baadhi ya miradi hususani Mradi wa Kilimo Bustani na ujenzi wa jengo la kufundishia. 

“Ujio huu wa Balozi ni faraja kwa Chuo kwani ni hatua muhimu ya kufungua milango ya ushirikiano zaidi baina ya chuo na Serikali ya Ufaransa katika nyanja za utafiti na maendeleo katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano ambayo inahimiza uwekezaji na kazi ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025” Alisema Prof. Chibunda. 

Kwa upande wake Muwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Bw. Fred Kafeero alisema kuwa FAO Tanzania wapo tayari kuingia kwenye ushirikiano huo na kwamba atatuma wataalamu kutoka ofisi yake ili waweze kukaa na timu ya watu watakaoteuliwa kuandaa mradi huo wa ushirikiano. 

Naye Mwakilishi Mkazi wa SWISSAID Tanzania bwana Blaise Burnier alisema wao wamesaidia wanafunzi wawili wa Shahada ya Uzamivu kwenye utafiti wao unaolenga masuala ya kilimo hifadhi ambao wanasoma SUA. 
Balozi wa Ufaransa nchi Tanzania Mhe. Balozi Fredrick Clavier (katikati) akiongea na Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda (kushoto).
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda (kushoto) akizungumza na Muwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Bw. Fred Kafeero (kulia) wakati wakimsubiri Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania.
Balozi wa Ufaransa nchi Tanzania Mhe. Balozi Fredrick Clavier (katikati), Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda (kushoto), Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Bw. Fred Kafeero (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji kutoka Ubalozi wa Ufaransa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo.

LUKUVI ATANGAZA KUPANGWA MAENEO ITAKAPOPITA RELI YA MWENDOKASI (SGR)

$
0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ametangaza kupangwa kwa maeneo yote itakapopita reli ya Mwendokasi (SGR) ili shughuli zitakazofanyika katika wilaya na vijiji inapopita reli hiyo kwenda sambamba shughuli za kiuchumi za mradi wa reli hiyo.

Aidha, Lukuvi alisema wakati wa kupanga maeneo hayo hakuna mwananchi yeyote atakayenyang'anywa eneo lake bali maeneo hayo yatapangwa kimji na kuainishwa matumizi yake kama vile ujenzi wa Viwanda na Mahoteli hivyo kuwataka wananchi wanaotaka kufanya uendelezaji mdogo mdogo kusubiri mpango huo.

Waziri Lukuvi alisema hayo tarehe 18 Mei 2019 katika vijiji vya Kwala na Soga vilivyopo Kibaha mkoa wa Pwani alipozungumza na wananchi wa maeneo hayo kuwaelezea mpango wa Wizara yake kupanga na kupima maeneo yote inapopita reli ya SGR ili kuendana na fursa za kiuchumi za mradi wa reli hiyo.

" Wilaya na vijiji vyote reli ya SGR itapita ardhi yao itapangwa na wale wananchi walio kando ya reli itakapopita wasubiri wasiwe na wasiwasi ardhi ya maeneo yao itengenezewe mpango na muongozo kuhusiana na maeneo hayo utatolewa" alisema Lukuvi.

Alisema, lengo la serikali kupanga maeneo hayo ni kutaka mpango mzima wa uendelezaji ukanda wa kiuchumi katika maeneo hayo ufahamike kitaifa na kimataifa ili kuvutia wawekezaji watakaotaka kuja kuwekeza na kubainisha kuwa fedha kwa ajili ya mpango huo zishatengwa.

Aliwatahadharisha wananchi wa vijiji hivyo kutokubali kuanza kuuza maeneo yao kwa kuwa baada ya kupangwa kwa maeneo hayo thamani ya ardhi itapanda na tayari baadhi ya watu wajanja kutoka nje ya vijiji hivyo washaanza kutafuta maeneo kwa ajili ya fursa hiyo.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, si vyema kila wilaya ikawa na mpango wake wa uendelezaji maeneo itakapopita reli hiyo bali serikali inachotaka ni kuwa na mpango wa kitaifa utakaotoa muongozo kwa wilaya zote kusisitiza kuwa ardhi katika maeneo hayo itasimamiwa na wilaya husika.

" Tukiacha maeneo ya kandokando ya reli bila kupanga na kupima kutafanyika vitu vya ajabu reli hii ina faida kubwa hivyo lazima kupanga maeneo inakopita ili kwenda sambamba na shughuli za kiuchumi za maeneo hayo" alisema Lukuvi.

Kwa mijibu wa Lukuvi, kuna timu imeundwa kwa ajili ya Mpango wa Uendelezaji Ukanda wa kiuchumi katika eneo inakopita reli ya SGR na timu hiyo inashirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kama vile za Nishati, Uchukuzi, Reli na Mawasiliano lengo likiwa kuwa na mpango utakaokidhi mahitaji ya uendelezaji ukanda kiuchumi katika eneo linakopita reli ya SGR.

Mapema akiwa katika eneo inapojengwa Bandari Kavu kijiji cha Kwala Kibaha vijijini, Mkuu wa wilaya ya Kibaha Asumpta Mshana alimueleza Waziri Lukuvi kuwa wilaya yake ilipanga kuitumia fursa ya reli hiyo pamoja na Bandari Kavu katika eneo la Kwala kwa ujenzi wa Hoteli, Maduka makubwa (Malls) , Nyumba za kupangisha (Apartments) ili wale wote watakaoitumia bandari hiyo kutoka maeneo tofauti waweze kupata malazi.

Akiwa katika Kijiji cha Soga Waziri Lukuvi aliwaambia wananchi wa kijiji hicho kuwa, eneo lao lishapandishwa hadhi na kuwa Mji hivyo ujenzi holela hautaruhusiwa na hati miliki za ardhi zitakazotolewa eneo hilo ni miaka 99 na aliwataka wakazi wake kuitumia fursa ya reli ya SGR kujiendeleza kiuchumi. 

Mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa alimueleza Waziri Lukuvi kuwa zoezi la kuandaa mpango katika maeneo hayo liende sambamba na uboreshaji miundo mbinu katika vijiji hivyo ili kuwawezesha watu watakaoenda katika maeneo hayo kutokumbana na changamoto kama vile barabara, maji na umeme.

BASI LA KAMPUNI YA ARUSHA EXPRESS LATEKETEA KWA MOTO,ABIRIA WANUSURIKA KIFO

$
0
0

Basi LA Abiria Kampuni ya Arusha Express linalofanya safari zake Arusha, Bukoba lenye Namba za Usajili T 222 ABF limewaka moto na kuteketea sehemu kubwa ya Gari hilo, Ajali hiyo imetokea leo asubuhi eneo la kwa Kagambo Kilometa Mbili toka Stendi Bukoba. Abiria wote wamenusurika huku chanzo cha kuwaka moto kikibainishwa kuwa ni hitilafu ya Umeme kwenye gari hilo. 


ISACA TANZANIA CHAPTER 2019 annual Conference

RAIS Dkt Magufuli amelipatia heshima kubwa Taifa kuwa na Paspoti yenye ubora wa Kimataifa -Uhamiaji

$
0
0
Na Francis Godwin ,Iringa 

Ofisa uhamiaji mkoa wa Iringa Tunu Ng'ondya amesema amepongeza jitihada mbali mbali zinazoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli katika kuboresha idara hiyo na kupelekea kuliletea Taifa heshima kubwa katika dunia kwa kuwa na hati ya kusafiria nje ya Tanzania yenye ubora wa kimataifa .

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake kuhusu kujaza fomu ya Maombi ya Pasipoti kwa njia ya Kielektroniki akiwa mahali popote Ng'ondya alisema kuwa kabla ya jitihada za serikali ya awamu ya tano kufanyika pass hiyo ya kusafiria ilikuwa katika hali ya ubora wa chini ila baada ya kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha idara ya uhamiaji hivi sasa kati ya hati bora za kusafiria duniani hati ya Tanzania ni miongoni na hivyo imeweza kuingia katika ubora wa ulimwengu .

Hata hivyo aliwataka wananchi kufika katika ofisi za uhamiaji kukata pass za kusafiri ili kuweza kuchangamkia fursa mbali mbali za kibiashara nje ya Tanzania kwa kwenda kufuata bidhaa na kuja kuuza nchini ama kupeleka bidhaa zinazozalishwa na watanzania kuuza nje ya Tanzania.

Alisema serikali imeweka utaratibu mzuri wa kila mwenye sifa ya kuwa na hati ya kusafiria kuweza kumiliki pasipo usumbufu wowote na kuwa suala la maombi na malipo ya gharama za kupata pass hiyo yanafanyika kwa njia ya mtandao na kuwa ofisi yake haipokei fedha yoyote taslim kutoka kwa mwombaji isipo kuwa mwombaji anapaswa kufika ofisini akiwa na viambatanishi vya vinavyohitaji baada ya kufanya maombi kupitia mtandao 

" Kama kuna mtu ataombwa fedha taslimu na ofisa yeyote atakapofika ofisini kwangu naomba achukue jina la mhusika na kuniletea ili achukuliwe hatua kali za kinidhamu kwani hatupokei fedha yoyote ile "

Alisema hakuna usumbufu wowote wa kupata hati hiyo kwani ndani ya wiki tatu pekee kwa waombaji wa mikoani wanaweza kupata pass zao baada ya kukamilisha taratibu zote na wale wanaohitaji hati ya haraka wanaweza kupewa ndani ya muda mfupi zaidi .

Ng'ondya alisema mwombaji anayehitaji kupata hati hiyo hatua ya kwanza anapaswa kuingia katika tovuti ya Idara ya Uhamiaji www.immigration.go.tz na kisha kwenda katika kitufe cha e-Services.

wakati atua ya pili mwombaji atapaswa kuchagua fomu ya maombi ya hati tatu, kuchagua ombi jipya, nne, atatakiwa kutiki kiboksi kukubaliana na maelekezo na tano anaanza kujaza taarifa zake kwa ukamilifu ukifuata maelekezo na mpangilio katika kila kipengele.

Baada ya mwombaji kukamilisha kujaza taarifa zake, atafahamishwa ya kwamba usajili umekamilika na kupatiwa namba ya ombi, ambayo ni muhimu aiandike pembeni na kuihifadhi kwa kumbukumbu za baadae.

Kuwa mwombaji atapewa namba ya kumbukumbu ya malipo na kutakiwa kwenda kulipia malipo ya awali Sh20,000.

Hata hivyo alisema baada ya mwombaji kumaliza hatua hiyo, ukurasa huo, ataingia katika menu ya M-Pesa/Tigopesa (*150*00#/*150*01#).

Amesema baada ya hapo atatakiwa kubonyeza namba 4 (lipa kwa M-Pesa) au kubonyeza namba 4 (kulipia bili)-Tigo na baada ya kuchagua mtandao wa malipo, atatakiwa kuingiza namba ya kampuni 888999 na mwombaji atatakiwa kuingiza kumbukumbu namba (Ingiza Control Number inayoanzia na 99109…….), kisha kiasi (kama ilivyo elekezwa mfano: 20,000), atapata maelezo kuwa unalipa pesa NMB, baada ya hapo ataingiza namba ya siri, atahakiki na kupata ujumbe mfupi wa maneno kutoka M-Pesa/Tigopesa kama muamala umekubalika.

kuwa baada ya hatua hiyo mwombaji atapata ujumbe kutoka kwenye mfumo namba 15200 kama muamala umekubalika, kisha kurudi katika ombi linaloendelea na mwisho ataingiza namba ya ombi au simu na namba ya risiti na hapo atapakua fomu yake ya maombi na baada ya kuwa amepata fomu atatakiwa kuiwasilisha katika ofisi ya Uhamiaji wilaya ya Mufindi ,Ilula kwa wilaya ya Kilolo ama makao makuu ya mkoa mjini Iringa .
Picha; Afisa wa idara ya uhamiaji mkoa wa Iringa Tunu Ng'ondya akionyesha hati mbali mbali za kusafiria nje ya Tanzania jana wakati alipozungumza na wanahabari kuhusu kujaza fomu ya Maombi ya Pasipoti kwa njia ya Kielektroniki akiwa mahali popote(picha na Francis Godwin)

MKURUGENZI MKUU NEMC ATEMBELEA KIWANDA CHA UZALISHAJI MIFUKO MBADALA AMBACHO KINAFANYA UZALISHAJI KWA MIAKA 10 SASA.

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mhandisi, Dkt. Samuel Gwamaka ametembelea kiwanda kinachojishughulisha na uzalishaji wa mifuko mbadala ili kujionea kiasi cha uzalishaji na uhakika wa upatikanaji wa mifuko hiyo.

Dkt. Gwamaka alifurahia ufanyaji kazi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na watanzania, kwasababu asilimia 90 ya malighafi wanazotumia zinatoka hapahapa Tanzania. Vilevile tayari kimeajiri watu zaidi ya 25, na vibarua zaidi ya 45. Aliongeza kuwa kwasasa Serikali ipo tayari kuwasaidia wale wote ambao wanataka kujikita kwenye uzalishaji wa mifuko mbadala.Alimalizia kwakuwatoa wasiwasi wananchi kuhusu upatikanaji wa mifuko mbadala nakusema kuwa wananchi wafate sharia kwasababu katazo la mifuko ya plastiki ni kwaajili ya kulinda mazingira na afya zao pia.

Kwa upande wa waendeshaji wa kiwanda hicho, wamesema kuwa wamefurahia katazo la mifuko ya plastiki kwani wanaamini kutokana na mahitaji ya mifuko mbadala kuwa mingi watazidi kuongeza ajira kwa kinamama na vijana ukizingatia uzalishaji wa mifuko hiyo hauhitaji elimu kubwa ya darasani.
Dkt. Gwamaka akipatiwa maelezo na wahusiki wa kiwanda cha mifuko mbadala namna ambavyo wanaweza kutengeneza mifuko mbadala ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba vitu vyenye asili ya maji maji. 
Dkt. Gwamaka akipewa maelezo na namna ambayo mashine zinavyofanya kazi. 
Dkt. Gwamaka akipewa maelezo na namna ambayo mashine zinavyofanya kazi. 

MABONDIA WA KULIPWA NA RIDHAA KUCHAPANA JUNI DAR ES SALAAM

$
0
0
Pambano la Ngumi za kulipwa na Ridhaa litakaloshirikisha Mabondia mbalimbali nchini wakiwemo wa Jeshi la Kujenga Taifa na Ngome linatarajia kupigwa Juni 7 Mwaka huu katika Ukumbi wa Club 361 Mwenge Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mratibu wa Ufundi wa pambano hilo Yassin Abdalah Ustaadh alisema upinzani wa JKT na Ngome ni wa kihistoria hivyo watu waje waaangalie burudani Nzuri ya Ngumi.

“ Mabondi wazuri wa Ngumi za kulipwa ni wale walioanzia Ngumi za Ridhaa na Kuwepo kwa JKT na Ngome katika Pambano hilo ni hatua muhimu na Mchango Mkubwa wa jeshi katika Kuendelelea Ngumi na michezo kwa Ujumla.” Alisema Ustaadh.

Aliwataka mabondia wa Ngumi za kulipwa kuwa ni Nassib Ramadhani atakayezichapa na Mohamed Kashinde wakati Kiasi Ally ananyukana na Shadrack Ignas wakati Kudura Tamimu atazichapa na Baina Mazola.

Aliongeza kuwa pambano lingine ni la kuvutia lenye lengo la kuvunja Historia ya Japhet Kaseba kumkaribisha katika Ngumi Mchezaji wa Ngumi na mateke Jeremia Jackson atakayecheza na Hashim Masungo.

Kwa upande wa Kocha wa Ngome Mteule daraja la pili Hassan mzonge alisema wamejiandaa vyema na Mmoja wa mabondi watakopambana katika uzito wa Kilo 81 ni Koplo Selemani Kidunda na kutuma salamu kwa JKT.

Kwa Upande wake katibu wa kamisheni ya Ngumi za kulipwa nchini Yahaya Poli alipongeza waaandaji kutekeleza sera ya kamisheni kuchanganya mapambano ya kulipwa na Ridhaa na Kibali kimetolewa kwa ajili ya kufanyika kwa Pambano hilo.

Kwa Upande wa Wadhamini wa pambano hilo kampuni ya Euromax kupitia kwa Afisa masoko wake Forgiver Tito aliahidi wapenzi wa Ngumi kuwa kuwa Wataendelea kusaidia kukuza mchezo huo kwani ni sehemu ya Ajira na kuwataka wadhamini wengine kujitokeza.

Naye Mratibu wa Pambano hilo Beatrice Ntahona alisema Maandalizi yote yamekamilika na watakahikisha unapatikana ulingo mzuri na mandhari yatakuwa mazuri kuhakikisha mabondia wanacheza vizuri na kupata mshindi halali.

Mapambano hayo ya Ngumi yasiyo ya Ubingwa yanalengo la kuendeleza vipaji vya ngumi za kulipwa nchini sambamba na kuwa sehemu ya Matayarisho kwa Vilabu vya ngumi za Jeshi zinazojiandaa na Mashindano mbalimbali ndani na Nje ya Nch

UWANJA WA NDEGE TERMINAL 3 WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 99.5

$
0
0
*Majaribio yaanza kufanyika, Mhandisi Kamwele afurahishwa na kasi aipongeza TAA

* Ujenzi daraja la Salender wakamilika kwa asilimia 9.5, ujenzi kuanza mwisho wa mwezi huu

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwele amefanya ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa jengo jipya  la 4  la abiria (Terminal 3) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  Julius Nyerere (JNIA) leo jijini Dar es Salaam na kuonesha kuridhishwa na usimamizi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamwele amesema kuwa kasi ya ujenzi huo ni nzuri na hadi sasa uwanja umekamilika na upo katika majaribio na utakabidhiwa rasmi tarehe 29 mwezi huu badala ya tarehe 31 na hiyo ni baada ya uwanja huo kukamilika kwa asilimia kubwa.

Amesema kuwa majaribio kwa ajili ya uwanja huo wa terminal 3 unaendelea huku akiwahimiza wazawa kutumia fursa ya kutumia nafasi maalumu zilizowekwa kwa ajili ya kuuza chakula (canteen) ili waweze kujiongezea kipato.

Aidha ameipongeza Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini kwa kusimami vyema mradi huo na amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa kuleta maendeleo yenye tija kwa kuwa kupitia uwanja huo watalii wengi wanatarajia kuingia nchini huku akieleza kuwa hali ya ulinzi uwanjani hapo ni salama kwa kila mmoja atakaye kuwepo uwanjani hapo.

Kuhusiana na ujenzi wa daraja la Salender Kamwele amesema kuwa kasi inaenda vyema na barabara ya muda inajengwa na mwisho wa mwezi huu ujenzi rasmi utaanza rasmi.

Amesema kuwa ujenzi wa daraja hilo lenye mita 1030 umekamilika kwa asilimia 9.5 na tayari mitambo na nguzo zimewasili kwa ajili ya kazi hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini Mhandisi. Julius Ndyamukama amesema kuwa uwanja wa Terminal 3  una uwezo wa kubeba zaidi ya watu milioni 6 kwa mwaka, kupaki ndege kubwa 13 umekamilika na kazi za majaribio zinaendelea ikiwemo kufunga mitambo kutoka mamlaka za  uhamiaji, mabenki, shirika la simu la TTCL na wadau wakubwa katika uwanja huo.

Amesema kuwa zaidi wa wananchi 2900 ambao ni sawa na asilimia 70 wamenufaika na ajira kupitia mradi huo na ameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kasi katika usimamizi wa miradi ya kimaendeleo na kuahidi kuendelea kutekeleza miradi ya namna hiyo kwa wakati.

Tafiti zinaonesha  kuwa Uwanja wa Terminal 1 una uwezo wa kubeba watu laki tano kwa mwaka, Terminal 2 una uwezo wa kubeba watu zaidi ya milioni mbili na nusu  kwa mwaka na ujenzi wa uwanja wa terminal 3 unataraji  kubeba watu zaidi ya milioni 6 kwa mwaka na umekuja baada uwanja wa terminal 2 kuzidiwa na idadi kubwa ya watu na hii ni kutokana na kukua kwa uchumi na shughuli za kitalii ambapo watu wengi hutumia usafiri wa anga.

Mradi huo wa ujenzi wa uwanja wa terminal 3 umewekezwa hadi mwaka 2035 kimatumizi huku viwanja vingine 9 vikitarajiwa kujengwa katika Mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Ruvuma na Mara.
 Msimamizi wa mradi kutoka TANROAD Mhandisi. Burton Komba (kulia) akitoa maelezo kwa waziri Kamwele kuhusiana na namna uwanja huo utakavyofanya kazi,  leo jijini Dar es Salaam
 Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Isack Kamwele akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua ujenzi wa mradi wa terminal 3 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa  Julius Nyerere ambapo amesema kuwa kasi na ubora wa ujenzi wa uwanja huo inaridhisha na majaribio yanaendelea, leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Isack Kamwele akizungumza na watendaji na wasimamizi wa mradi huo, kulia na msimamizi wa mradi kutoka TANROAD Mhandisi Burton Komba na katikati ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini Mhandisi Julius Ndyamukama, leo jijini Dar es Salaam.

RAIS DKT. SHEIN AHUDHURIA FUTARI ILIOANDALIWA NA PBZ HOTELI YA VERDE MTONI ZANZIBAR

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Wafanyakani wa Benki ya Watu wa Zanzibar na Wananchi katika futari ilioandaliwa na PBZ, katika hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar jana 20-5-2019.(Picha na Ikulu)
 WAZIRI wa Biashara na Viwanda Zanzibar kushoto Mhe. Balozi Amina Salum Ali, akiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Bi. Khadija Shamte, wakipata futali ilioandaliwa na PBZ kwa Wateja wao na Wananchi iliofanyika katika ukumbii wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar jana 20-5-2019.
 MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar Bi. Kidawa Himid. Saleh, akijumuika na Wananchi katika Futari maalum ilioandaliwa na PBZ katika hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.
 WAGENI waalikwa wakipata futari katika hoteli ya Verd Mtoni Zanzibar ilioandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd.(PBZ)
 .
 WANANCHI wa Zanzibar wakijumuika na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, katika Futari ilioandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) katika Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi mbalimbali meza kuu kushoto Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Balozi Mohamed Ramia, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na kulia Mjumbe wa Bodi ya PBZ Yakout Hassan Yakout , Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, wakimsikiliza Sheikh Abdalla Talib akitowa nasaha baada ya kumalizika hafla hiyo ya futari katika ukumbi wa hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar
 MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akitowa neno la shukrani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa hafla hiyo ya futari ilioandaliwa na PBZ katika hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia dua ikisomwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Othman Hassan Ngwali, baada ya kumalizika hafla ya futari ilioandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar katika Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Ameir Hafidh baada ya kumalizika kwa hafla ya Futari iliofanyika katika Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar katikati Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Balozi Mohammed Ramia Abdulwawa.(Picha na Ikulu)

KIKAO CHA BARAZA LA WAWAKILISHI CHAENDELEA ZANZIBAR

$
0
0
 Mwakilishi wa Jimbo la Shaurimoyo Hamza Hassan Juma akichangia Hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala bora Haroun Ali Suleiman katika kikao cha baraza la Wawakilishi kinachoendelea Mbweni Zanzibar.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Nadir Abdul-latif Yussuf katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni Zanzibar.
 Mwakilishi wa Jimbo la Chakechake Suleiman Sarahan Said akichangia Hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala bora Haroun Ali Suleiman katika kikao cha baraza la Wawakilishi kinachoendelea Mbweni Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

HER INITIATIVE YARATIBU UENDESHAJI WA PROGRAMU YA PANDA 2019 YENYE LENGO LA KUWAWEZESHA WASICHANA KIUCHUMI

$
0
0
WASICHANA zaidi ya 30 wameungana na sera ya taifa katika kukuza uchumi wao kupitia programu ya mafunzo ya uandaaji na utoaji huduma katika jamii yao ili kujikwamua kiuchumi Programu ya PANDA yenye lengo la kuwawezesha wasichana Kati ya miaka 18-25 kufikia maendeleo kiuchumi, imeanza rasmi katika vipengele vinne (upambaaji, mapishi, uteengenezaji wa kucha na kilimo) pamoja na elimu ya fedha.

Lengo la Programu hii ya Panda ni kuwawezesha wasichana kwa kuwapatia ujuzi na muongozo ili waweze kujiajiri na hapo baadae kuweza kuwaajiri wengine lakini pia kupata muongozo/usimamizi wa kimawazo katika biashara kwa walio watangulia katika vipengele walivyochagua ili waweza kuendesha biashara zao vizuri na kukabiliana na ushindani katika soko.

Kauli mbiu ya Programu hii ni Anza, Kimbia, kaza kwa lengo la kuwapa hamasa wasichana kuanzisha biashara zao na kuwatia moyo katika kuziendeleza biashara hizo vizuri ili kuyafikia malengo waliojiwekea ya kukabiliana na umaskini lakini pia kufikia usawa wa kijinsia.

Programs hii ni ya miezi sita na itaambatana na shughuli mbalimbali; mafunzo kwa vitendo, miezi mitatu ya usimamizi wa kimawazo kwa biashara zao, warsha kwa siku mbili itakaolenga kuwakutanisha wasichana wajasiriamali wachanga pamoja na sekta binafsi kama taasisi za fedha.

Katika utoaji wa mafunzo haya tunashiriaka na DOT, Lavy_product,Mkulima smart,Mama peridot, rachel’s choice na EFM.Tunakaribisha mashirika/watu binafsil ama taasisi yoyote yenye lengo la kumuinua mtoto wa kike( msichana) kiuchumi kuungana nasi katika kuendesha na kuienndeleza programu hii.

HER INITIATIVE ni shirika lisilo la kiserikali na si la kibiashara.Shirika hili limeanzishwa kwa lengo la kuwaelimisha wasichana katika jamii ili waweze kujitambua na kushiriki katika harakati zozote za kijamii zinazohusu au kugusa maisha yao. Dhamira kuu ya shirika ikiwa ni kuwaelimisha na kuwapa wasichana kipaumbele katika jamii ili kuchochea maendeleo ya usawa.
Majaji siku ya usahili ambao pia ni washirika (partners) katika mradi huu wa Panda kutoka Rachel choice event, DOT,mama Peridot na Lavy Product Panda katika kila kipengele cha mradi (Mapambo, Eimu ya fedha, chakula na kucha), wakimsikiliza msichana aliyekua anajielezea katika usaili.
Baadhi ya wasichana waliokuja kwenye usaili, wakijielezea mbele ya majaji.
Mwanzilishi wa Her Initiative akijadiliana masuala mbalimbali na baadhi ya wasichana waliokuja kwenye usaili.
Timu nzima ya Her Initiative pamoja na wasichana waliokuja kwenye usaili wakiwa katika picha ya pamoja.

HASUNGA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA IFAD

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza na Gilbert Houngbo, Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (International Fund for Agriculture Development – IFAD walipokutana jana Tarehe 20 Mei 2019 Jijini Dodoma. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) jana Tarehe 20 Mei 2019 alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Mfuko wa Kimataifa na Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Gilbert Houngbo.

Katika mazungumzo hayo Houngbo alisema mfuko huo umetenga zaidi ya sh Billion 127.3 kwa ajili ya kufadhili miradi ya kilimo nchini kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2020.

Alimpongeza Rais Dk John Magufuli pamoja na serikali yake kwa juhudi kubwa alizozifanya katika kukuza uchumi ikiwemo utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na mfuko huo.

Katika mazungumzo yake na Rais Magufuli kabla ya kuzuru Jijini Dodoma Rais huyo wa IFAD alimueleza Dkt Magufuli kuwa baada ya kutenga fedha hizo mfuko huo unasubiri upande wa Tanzania kuainisha maeneo mahususi ya miradi ya kilimo ambako fedha zitaelekezwa.

Kadhalika, alieleza kuwa ana matumaini makubwa kuwa miradi hiyo itafanikiwa kwa kuzingatia Tanzania ni nchi yenye amani na namna serikali ilivyo na dhamira ya maendeleo.

Naye Waziri Hasunga alimuhakikishia kuwa fedha hizo zitakazoelekezwa katika maeneo yenye maslahi mapana ya sekta ya kilimo ikiwemo kuwezesha matumizi ya zana za kilimo katika uzalishaji, kuzalisha mbegu bora za mazao, kutatua changamoto za masoko ya mazao pamoja na kuboresha ufugaji zitakuwa chachu ya kuimarisha kilimo nchini.

Mhe Hasunga alisema kuwa tayari Bajeti ya Matumizi ya kawaida ya wizara ya Kilimo imepitishwa na wabunge hivyo kupitia Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP II) umesisitizia mapinduzi ya viwanda na umeitambua Sekta ya Kilimo kuwa muhimili imara kwa ajili ya upatikanaji wa malighafi za viwanda. 

Alisema kiasi hicho kilichotengwa na IFAD itakuwa chachu na chagizo katika kuboresha mustakabali wa kilimo. 

Alisema kupitia Miongozo hiyo ya Kitaifa, pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 na Sera ya Kilimo ya mwaka 2013, inayotekelezwa na Wizara kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) ambayo inalenga kuleta mageuzi katika Sekta ya Kilimo na kwa kutambua umuhimu wa kuongeza mitaji, teknolojia na ubunifu, Sekta Binafsi inashirikishwa kikamilifu katika utekelezaji wa ASDP II wakulima nchini wataelimika kupitia mbinu bora za kilimo na uzalishaji wenye tija.

IFAD imekuwa katika ushirikiano na serikali ya Tanzania kufuatia uhusiano ulioanza mwaka 1978 na kudumishwa kwa maslahi ya Watanzania.

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA KILIMO MALIASILI MIFUGO NA UVUVI IKULU NDOGO KIBWENI ZANZIBAR

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzui Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akiongoza Kikao cha Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar kwa mwezi Julai 2018 hadi March 2019, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar 21-5-2019, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na kulia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri.(Picha na Ikulu)
  MAOFISA wa Idara za Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiongoza Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Kilimo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar leo 21-5-2019.
 WAZIRI wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji Mpango Kazi ya Wizara yake wakati wa mkutano huo uliofanyika Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.
 BAADHI ya Maofisa wa Idara za Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar, wakifuatilia mkutano huo wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai 2018 hadi March 2019, uliofanyika Ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar leo.
KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Bi. Maryam Juma Abdalla Mabodi, akiwasilisha Taarifa ya Matumizi na Mapato ya Wizara yake wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi Julai 2018 hadi March 2019, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Matreka Zana za Kilimo Zanzibar Ndg. Afani Othman Maalim, akichangia wakati wa mkutano huo wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar. (Picha na Ikulu)

WATATU WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA SHITAKA LA UHUJUMU UCHUMI,WAKUTWA NA VIPANDE VINNE VYA MENO YA TEMBO

$
0
0

WATU watatu, wakazi wa jijini Dar es Salaam,  wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shitaka la uhujumu uchumi kwa kukutwa na nyara za serikali na utakatishaji wa vipande vinne vya meno ya tembo yenye thamani ya zaidi ya  Sh. Milioni 69.

Wakili wa serikali Candid Nasua amewataja washtakiwa hao kuwa ni, Godlisten Mtui, mfanyabiashara, Frank Lucas dereva wa pikipiki na Mhando Shomary, Mkulima

Mbele ya Hakimu Mkazi Maila Kasonde imedaiwa,  Mei 7 mwaka huu, huko katika eneo la Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, washtakiwa, walikutwa na vipande vinne vya meno ya tembo vya USD 30000 ambazo ni sawa na Sh. 69,025,000 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Aidha washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka la utakatishaji, ambapo wanadaiwa kumiliki vipande hivyo vya meno ya tembo huku wakijua wakielewa fika kuwa, vipande vivyo vya meno ya tembo vimetokana na kosa la uwindaji haramu.


Hata hivyo, washitakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kw kuwa, mahakama ya Kisutu  haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hadi Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), atakavyoelekeza vinginevyo.

Washitakiwa wote wamerudishwa rumande hadi Juni 4 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

MADIWANI MANYARA WALALAMIKIA KUKATWA POSHO ZAO

$
0
0
MADIWANI wa Mkoa wa Manyara, wamesikitishwa na kitendo cha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwahoji kila mara na kuagiza warudishe posho walizochukua jambo linalosababisha wavunjike moyo wa kufanya kazi zao.

Wakizungumza mjini Babati kwenye kikao cha jumuiya ya serikali za mitaa (Alat) cha mkoa huo, madiwani hao wameazimia kuonana na mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ili kuongelea jambo hilo.

Mwenyekiti wa Alat wa mkoa wa Manyara, George Bajuta alisema kitendo cha Takukuru kuwahoji madiwani na kuagiza warudishe posho walizochukua siyo sahihi kwani jambo hilo lingepaswa kuachwa.

Bajuta alisema kasoro zilizojitokeza kwenye baadhi ya halmashauri zisitumike kuwaadhibu madiwani wengine ambao hawastahili kwani hata posho zenyewe zinazotolewa kwao ni kidogo.

"Wabunge wanapatiwa mishahara mikubwa na posho nzuri sasa baadhi walipendekeza kuwa madiwani wanafuja fedha hivyo kusababisha hali hii ya udhalilishaji kujitoleza," alisema.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Jackson Sipitieck alisema kuna haja ya mkuu wa mkoa huo, katibu tawala wa mkoa, kamanda wa Takukuru na mkuu wa usalama wa taifa wa mkoa, kukutana nao ili kujadili tatizo hilo. Mjum

be wa Alat wa mkoa huo, Daines Peter alisema maslahi na haki ya madiwani ibaki palepale kwani wana majukumu mengi kwa ajili ya kutumikia wananchi. Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Lairumbe Mollel alisema maslahi ya madiwani ni madogo lakini wanajitolea ila suala hilo linawavunja moyo.

wenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Babati, Nicodemus Tarmo alisema hata Rais John Magufuli aliwahi kusema kwenye kikao cha Alat Taifa kuwa posho za vikao wanazopokea madiwani kupitia utaratibu uliowekwa uachwe.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu vijijini, Joseph Mandoo alisema vikao vya madiwani vya vyama na vya kumchagua Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya wanapaswa kulipwa kwani ni maandalizi ya kikao cha baraza la madiwani.

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Mbulu, Gidishanga alisema wabunge hawatetei tena maslahi ya madiwani ila mbunge wa jimbo la Chemba, Juma Nkamia amekuwa akiwasemea madiwani bungeni.

Katibu tawala msaidizi wa mkoa huo (serikali za mitaa) Kenedy Kaganda alisema kila diwani anapatiwa posho zake kulingana na stahili zake ikiwemo fedha za kujikimu.

Hata hivyo, kaimu mkuu wa Takukuru mkoani Manyara, Isdory Kyando alisema madiwani waliotakiwa kurudisha posho ni wale waliochukua miaka iliyopita na sasa bila kustahili kuzichukua.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Jackson Leskar Sipitieck (katikati) akiandika yanayozungumzwa kwenye kikao cha Alat cha mkoa huo, kilichofanyika mjini Babati, kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Joseph Guulo Mandoo.
 Mwenyekiti wa Alat wa Mkoa wa Manyara, George Bajuta akizungumza wakati akifungua kikao cha Alat cha mkoa huo kilichofanyika mjini Babati.
Baadhi ya wajumbe wa Alat wa Mkoa wa Manyara, wakifuatilia kikao chao kilichofanyika mjini Babati.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images