Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA DKT. MPOKI ULISUBISYA KUWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI CANADA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Mpoki Ulisubisya kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 20, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshuhudia Dkt. Mpoki Ulisubisya akiweka sahihi baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 20, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi nyenzo za kazi Dkt. Mpoki Ulisubisya baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 20, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshuhudia Dkt. Mpoki Ulisubisya akila kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 20, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Mzee Ulisubisya Mwasumbi baba mzazi wa Dkt. Mpoki Ulisubisya baada ya kumuapisha mwanae kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 20, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mke wa Dkt. Mpoki Ulisubisya baada ya kumuapisha mumewe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 20, 2019. Wengine ni Baba na wana familia ya Balozi huyo mpya.  PICHA NA IKULU

Picha mtaani leo

$
0
0
Mmoja wa Wakazi wa Dar es Salaam eneo la Kitunda akipambana kupitisha mkokoteni wake kwenye barabara ambayo imejaa maji kama anavyoonekana,Hali hii ya barabra kutopitika ipo kwa sehemu kubwa kwa barabara za pembezoni ambazo zimeharibiwa na mvua zinaendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.

WAITARA AZIKARIBISHA AZAKI ZA KIRAIA KUTOA MAONI YAO SERIKALINI

$
0
0
 Na Humphrey Shao, Globu ya Jamiii

Naibu Waziri Tamisemi, Mwita Waitara ameziomba Tasisi na Azaki mbalimbali zinazojishughulisha na elimu kuacha na kujifungua na kujitokeza hadharani kutoa maoni juu ya uboreshaji wa elimu nchini.

Waitara amesema hayo akizungumza na wadau wa Maendeleo na Viongozi wa Azaki Mbalimbali katika hafla ya kusherehekea Ushindi wa Haki Elimu katika tuzo ya umahiri wa tasisi za kiaraia Barani Afrika .

Waitara amesema licha ya shirika la Haki Elimu Kuibuka mshindi wa jumla pia ilikuwa mshindi katika vipengele vingine viwilivya umahiri wa kimkakati na unyumbufu yaani Strategic Ability and Adaptability pamoja na uwezo wa uongozi na utawala ,hii inaakisi namna shirika linalojiongoza na kuzingatia misingi iliyowekwa .

"nitoe wito kwa tasisi nyingi za kiraia nchini Tanzania kujifunza kutoka mafanikio ya Haki Elimu ili kufanikisha zaidi kazi zaidi ya kuboresha maisha ya jamii ya watanzania na kuiletea sifa nchi yetu kimataifa hivyo nitafurahi kuona asasi zingine za kiraia zinaibuka vinara kwenye mashindano kama haya" Amesema Waitara.

Alimaliza kwa kusema kuwa uwezo na utayari wa Haki Elimu kufanya kazi na wadau mbalimbali ndio uliowawezesha kupata mafanikio haya na ni imanai yangu kuwa shirika litaendelea kushirikiana na serikali katika harakati za kueleta maendeleo katika sekta ya elimu hapa nchini.
 Naibu Waziri Tamisemi, Mwita Waitara akizungumza na wadau wa Maendeleo na Viongozi wa Azaki Mbalimbali katika hafla ya kusherehekea Ushindi wa Haki Elimu katika tuzo ya umahiri wa tasisi za kiaraia Barani Afrika .
 Mkurugenzi wa Tasisi ya Haki Elimu Nchini, Dk. John Kallage akieleza namna tasisi hiyo ilivyoweza kuibuka mshindi katika kategori mbili pamoja na kuepewa ushindi wa jumla wa tuzo hizo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Haki Elimu Nchini, Richard Mabalaakitoa shukrani wa kwa wafanyakazi wa Haki Elimu na wadau wengine kwa kuwapa sapoti.
 Naibu Waziri Tamisemi, Mwita Waitara,akigonga Chiazi na Baadhi ya Wadau na Wafanyakazi wa Haki Elimu
 Wafanyakazi na Wadau wa Haki Elimu wakifungau Shampeni katika sherehe ya kupongezwa kupata tuzo ya Azaki bora barani Afrika.
Mgeni Rasmi na Viongozi wa Meza Kuu wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Azaki Mbalimbali.

MASHINDANO YA KEKI YAMFUNGULIA FURSA ZENA, VIJANA WAASWA KUTOCHAGUA KAZI

$
0
0
   Na.Khadija seif ,Globu ya jamii

MSIMU wa pili wa mashindano  ya keki  yazinduliwa rasmi jijini Dar es salaam.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa  muandaaji wa mashindano hayo zena Sharif amesema washiriki wameimarika na kwa msimu huu wapili washiriki wamekuwa wengi.

"Msimu wa pili tumefanikiwa kupata takribani washiriki 40 ambao watashindana kupika keki na mmoja kati yao ataibuka mshindi"

Zena amesema mashindano yapo mengi lakini swala la keki huwa halipewi kipaumbele sana kutokana na lilivojengeka katika jamii na kutopewa thamani lakini hakuna sherehe inayokosa keki.

Aidha,amesema mbali na vitabu ambavyo alivizindua mwaka jana kwenye msimu wa kwanza wa mashindano hayo kwa msimu wa pili ataweza kuleta kitu cha tofauti ambacho kitaendelea kuwa kama chachu kwa vijana hususani wasichana wenye umri mdogo kujituma na kutumia kazi za mikono kuongeza kipato.

Mashindano hayo wameweza kumkutanisha na watu mbalimbali huku wahitaji wa keki kuwa wengi kutokana na ubora wa keki za washiriki hao.

Hata hivyo kwa mshindi wa kwanza msimu wa kwanza Alexander Alex ambae aliibuka mshindi kutokana na ubora wa keki zake amesema mashindano hayo ni muhimu vijana kujitokeza na kushiriki kikamilifu na kutochagua kazi za kufanya.

"Mashindano ya keki yamenifungulia wigo mpana wa wateja na kuhimarika zaidi na kujifunza njia za washiriki wenzangu ambao walishiriki "

Pia ametoa wito kwa vijana hasa wa kiume kutochagua kazi za kufanya kwani kupika keki hakuchagui jinsi kwani ni anaingiza kipato kupitia kazi hiyo.

MIKOA YA SONGWE NA NJOMBE YAPEWA MAFUNZO BORA YA KILIMO.

$
0
0
Kampuni ya mbolea ya OCP  imeendelea kutoa mafunzo ya kilimo bora katika mikoa ya Songwe na Njombe.Mafunzo hayo yanatolewa bure sambamba na upimaji wa afya ya udongo yanayotarajiwa kuwafikia wakulima zaidi ya 20,000 katika awamu yake ya kwanza.
Mmoja wa wakulima akitoa shukrani kwa niaba ya wakulima wa mikoa ya Songwe na Njombe mara baada ya mafunzo ya kilimo bora yaliyotolewa jana na Kampuni ya mbolea ya OCP.
Wakulima wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mafunzo hayo jana.

MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA NA CHANGAMOTO YA MIUNDOMBINU MAENEO MBALIMBALI

$
0
0
Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika  maeneo mbalimbali barabara  za wilaya ya Mkuranga mko wa Pwani zimekata mawasiliano na kufanya baadhi huduma za kijamii kushindwa kufanyika  kama zinavyo onekana katika picha. Barabara zilizokata mawasiliano ni barabara ya   kata ya Kimanzichana,Kata ya Lukanga,Kisayani Mlela kata ya Mbezi.
 Muonekano wa Daraja la  mto Mlonga likiwa limekatikatika ambalo lipo kati ya Kiparang’anda Kutokana na mvua zinazoendelea katika kunyesha katika  maeneo mbalimba barabara  za wilaya ya Mkuranga mko wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tiv.
 Muonekano wa barabara  kata ya Kimanzinchana   wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani kama ionekanavyo vyone  katika picha.

  Muonekano wa barabara  kata ya Kimanzichana   wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani kamainevyone  katika picha.
Muonekano wa barabara  kata wa barabara ya  Kata ya Lukanga.


Wananchi wa Kisayani Mlela kata ya Mbezi wakivuka mto baada ya Kalvati kukatika Kutokana na mvua zinazoendelea katika kunyesha katika  maeneo mbalimba barabara  za wilaya ya Mkuranga mko wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tiv.

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mhe. Kangi Lugola akisisitiza kuhusu agizo lake lakuwataka askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini kuzingatia sharia wanapowachukulia hatua waendesha bodaboda kote nchini leo Bungeni Jijini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. Dkt. Angelina Mabula akieleza mikakati ya Serikali kuimarisha utendaji wa watumishi wa sekta ya ardhi nchini leo Bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Job Ndugai akisisitiza jambo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.
  Mbunge wa Mtama mhe Nape Nnauye akisisitiza umuhimu wa kuimarisha sekta ya kilimo hapa nchini hasa mazao ya kimkakati kama korosho leo Bungeni jijini Dodoma wakati wa mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Kilimo.
 Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa Waziri wa habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na Mwanasheria mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilangi (Katikati) leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Sehemu ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanaosoma masomo ya Sayansi ya Siasa wakiwa Bungeni kwa ziara ya mafunzo leo Jijini Dodoma.
Sehemu ya wabunge wakiwasili katika Viwanja vya Bunge leo Jijini Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Bunge unaoendelea Bungeni Jijini Dodoma. (Picha zote na Frank  Mvungi- MAELEZO)

RAIS DKT. SHEIN AONGOZA WANANCHI WA ZANZIBAR KATIKA MAZIKO YA WAZIRI WA ZAMANI MAREHEMU ALI JUMA SHAMUHUNA KIJIJI CHA DONGE MKOA WA KASKAZINI UNGUJA LEO

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hassan Khatib alipowasili katika hafla ya maziko ya aliyekuwa Waziri wa Zamani wa SMZ Marehe Ali Juma Shamuhuna, kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri, alipowasili katika Kijiji cha Donge Imiyani.(Picha na Ikulu)
 BAADHI ya Wananchi kutoka sehemu mbalimbali Zanzibar wakijumuika katika hafla ya maziko ya Marehemu Ali Juma Shamuhuna yaliofanyika katika Kijiji cha Donge Imiyani Mkoa wa Kaskazini Unguja leo, 20-5-2019.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.,Dk. Ali Mohamed Shein, akishiriki katika Sala ya kuusalia Mwili wa Marehemu Ali Juma Shamuhuna, maziko yaliofanyika katika Kijiji chao Donge Imiyani Mkoa wa Kaskazini Unguja.leo 20-5-2019.(Picha na Ikulu)
 WANANCHIna Waumini wa Dini ya Kiislam wakiitikia dua baada ya kumalizika Sala ya kuuombea mwili wa Marehemu Ali Juma Shamuhuna iliofanyika katika msikiti wa Donge Imiyani Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.20-5-2019
 WANANCHI wakiwa wamebeba jeneza likiwa na mwili wa Marehemu Ali Juma Shamuhuna wakati wa maziko hayo yaliofanyika Kijijini kwao Donge Imiyani Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.
 VIJANA wa Chama Cha Mapinduzi walioandaliwa kwa ajili ya kubeba jeneza la Marehemu Ali Juma Shamuhuna wakati wa maziko hayo wakielekea katika eneo lililotengwa kwa maziko hayo katika Kijiji cha Imiyani Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Ali Juma Shamuhuna wakati wa maziko hayo yaliofanyika katika Kijiji cha Imiyani Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.20-5-02019
 MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Ali Juma Shamuhuna
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akisoma wasifu wa Marehemu Ali Juma Shamuhuna, baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya maziko iliofanyika katika Kijiji cha Donge Imiyani Mkoa wa Kaskazini Unguja
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, na Wananchi wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa Sala ya kuusalia mwili wa marehemu iliofanyika kjatika Masjid ya ilioko Kijiji Kwao Donge Imiyani Mkoa wa Kasakazini Unguja leo.20-5-2019.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akitowa mkono wa pole na kuifariji familia ya Marehemu Ali Juma Shamuhuna,wakati wa msiba huo uliofanyika Kijiji kwao Donge Imiyani Mkoa wa Kaskazini Unguja leo
RAIS wa Zabnzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia dua ikisomwa na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi, wakati wa hafla hiyo ya maziko ya Marehem,Ali Juma Shamuhuna yaliofanyika Kijiji kwao Donge Imiyani Mkoa wa Kaskazini Unguja leo. (Picha na Ikulu)

WIZARA YA ARDHI YAANDAA MPANGO WA KUENDELEZA MAENEO YA UKANDA WA SGR

$
0
0
Na Grace Semfuko,MAELEZO

Wizara ya ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi  inaandaa mpango maalum wa uendekezaji wa Ukanda wa reli ya kisasa ya Standard Gauge (SGR) inayotoka Dar Es Salaam hadi Kigoma unaolenga kuwawezesha wakazi waishio kando ya Reli hiyo kunufaika kiuchumi kupitia ardhi zao kwa kufanya biashara zitakazopangwa kwenye maeneo hayo na ambazo wananchi wataamua kuzifanya.

Lengo la mpango huo  ni kutoa mwongozo wa namna matumizi ya ardhi yatakavyofanyika katika ukanda mzima wa SGR ambao utasaidia kuondoa matumizi yasiyokusudiwa na pia  utasaidia kuondoa migogoro ya adhi na kuibua fursa ambazo bado hazijajulikana na Wakazi wa maeneo hayo.
Hayo yalibainishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi wakati akizungumza na wakazi wa Vijiji vya Kwala na Soga vilivyopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani kuhusu mpango bora wa matumizi ya ardhi kwenye ukanda wa Reli ya Kisasa ya SGR.

“kila mahali kutakuwa na fursa za kiuchumi zinazopatikana mahali husika, haimaanishi tunaipanga ile ardhi ili ichukuliwe na serikali, hapana!  wananchi wenyewe watayatumia maeneo yao kwa mpango maalum,  tunataka wananchi wanufaike na ardhi yao” alisema Waziri Lukuvi.
Waziri Lukuvi aliwatoa hofu wakazi wa Maeneo yote ya SGR kuwa Serikali haina mpango na kuchukua ardhi zao na kuwataka pia kutouza ardhi hizo kwani tayari Serikali imeshazipandisha hadhi na thamani.

“serikali inapanga matumizi bora ya ardhi yote katika Wilaya zote ambapo SGR inapita, tunataka kuwa na ukanda wa maendeleo ya kiuchumi , yaani mtu akifika hapa anajua kitu gani anakipata wapi, ukanda huu unaopitiwa na SGR sasa utapangwa rasmi, hatuwezi kuwa na reli ya kisasa yenye gharama kubwa kama hii lakini uendelezaji wa ardhi ni mbovu,mtu hataruhusiwa kufanya shughuli isiyoruhusiwa, hapa lazima ardhi ipangwe vizuri na tuwe na mpango mzuri  wa kiuchumi” alisema Lukuvi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Miji wa Wizara ya Ardhi Immaculata Senje alisema pamoja na kuinua pato la wakazi waishio kando ya reli hiyo mpango huo pia unalenga kulinda mazingira na kupendezesha maeneo hayo na wameshaanza maandalizi ya awali ya kukusanya taarifa za mpango huo.

 “Utakuwa ni mpango shirikishi kuanzia ngazi za vijiji hadi Taifa, mpaka sasa timu ya wataalamu imeundwa na imeshaanza maandalizi ya awali kwa kukusanya taarifa muhimu ambazo zitasaidia kuutekeleza mpango huu, tutafanya kazi na wote, lengo la mpango huu ni kutoa mwongozio wa namna matumizi ya ardhi yatakavyofanyika katika ukanda mzima” alisema Senje

DKT. MWANJELWA AFUNGUA SEMINA YA KUZIJENGEA UWEZO NCHI WANACHAMA WA KAMISHENI YA UMOJA WA AFRIKA

$
0
0
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akifungua Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji  wa Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala na Utoaji wa taarifa Barani Afrika iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akifuatilia maelezo ya Mwakilishi wa Mkurugenzi anayeshughulikia Masuala ya Siasa Umoja wa Afrika, Bw. Issaka Garba Abdou wakati wa Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji wa Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala na Utoaji wa taarifa Barani Afrika, iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
 Washiriki wa Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji  wa Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala na Utoaji wa taarifa Barani Afrika wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipokuwa akifungua semina hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe kutoka Tanzania, Bwana Gubas Vyagusa akizungumza kwenye Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji wa Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala na Utoaji wa taarifa Barani Afrika, iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji  wa Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala na Utoaji wa taarifa Barani Afrika iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.


WASHINDI WA MASHINDANYO YA KUHIFADHI QURAAN WAPEWAZ PESA ZAO NA AMANA BANK

$
0
0
Mshindi wa kwanza wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Quraan Kijana Mohamed  Diallo kutoka nchini Senegal akipokea kitita cha shilingi milioni 20 kutoka katika benki ya Amana wadhamini wakuu wa mashindano hayo, makabidhiano hayo yamefanyika leo katika Tawi la Benki hiyo lililopo katika Jengo la Diamond Plaza, jijini Dar es salaam.
Mshindi wa pili wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Quraan Kijana Furuq Kabiru Yakubu kutoka nchini Nigeria akipokea kitita cha shilingi milioni 10 kutoka katika benki ya Amana wadhamini wakuu wa mashindano hayo.
Mshindi wa tatu wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Quraan Kijana Shamsuddin Hussein Ali kutoka Tanzania Zanzibar nae akipokea zawadi yake kutoka katika benki ya Amana wadhamini wakuu wa mashindano hayo.
Mkuu wa idara ya Masoko kutoka Amana Bank ndugu, Dasu Mussa akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari katika tukio la kuwakabidhi washindi walio shinda mashinano ya kusoma na kuhifadhi Quraan kwa mwaka huu.

IGP SIRRO AONGOZA ZOEZI LA USAJILI KWA KUTUMIA ALAMA ZA VIDOLE

MTANZANIA MARTIN BEATUS SEGEJA ALAMBA NONDOZZ YA MECHANICAL ENGINEERING KATIKA CHUO KIKUU CHA TEXAS CHRISTIAN, MJINI DALLAS

$
0
0
Martin Beatus Segeja mtanzania pekee aliyemaliza degree ya Mechanical Engineering katika chuo Kikuu Cha Texas Christian University (TCU) , mjini Dallas Fortworth, Marekani tarehe 11 Mei, 2019 . Kwa kipindi chote hicho ndugu Martin ameipeperusha vyema bendera ya Tanzania na miaka yote 4 amekuwa balozi Mzuri mpaka alitengenezewa scaff ya bendera ya Tanzania.
Martin Beatus Segeja mtanzania pekee aliyemaliza degree ya Mechanical Engineering katika chuo Kikuu Cha Texas Christian University (TCU) , mjini Dallas Fortworth, Marekani akiwa pamoja na marafiki zake waliofika kumpongeza kwa kulamba nondozz yake hiyo.
Nondozz ya Martin Beatus Segeja
Furaha ya kulamba Nondozz akiwa pamoja na wazazi.
Martin Beatus Segeja katikati akiwa na wazazi wake, na ndugu wengine wa familia siku ya graduation yake tarehe 11 Mei, 2019. Kulia ni Baba Mzazi Bw. Beatus Segeja na Kulia ni Mama mzazi Bi. Violeth Segeja. Wengine kwenye picha ni ndugu Abdallah Juma, Consolata Nyaki, Patricia Segeja na Father Msula.

RC MAKONDA AZIKONGA NYOYO ZA MAIMAMU NA MASHEKHE KUTOKA MISIKITI ZAIDI YA 1,000, AWAPATIA SHEHENA YA FUTARI YA NGUVU.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Mhe. Paul Makonda leo amewakabidhi shehena ya viungo vya kutengeneza futari kwa maimamu, mashehe na viongozi wa Dini ya Kislamu kutoka Misikiti zaidi ya 1,000 kama sehemu ya sadaka na shukrani ya Amani na Utulivu ndani ya mkoa huo.

Miongoni mwa vitu alivyokabidhi RC Makonda ni Mchele, Sukari, Unga, Maharage, Mafuta na vitu mbalimbali kwaajili ya kuwawezesha viongozi hao kufurahia futari majumbani mwao.

RC Makonda amewashukuru viongozi wa dini kwa kuwa wasimamizi wazuri wa Amani na mshikamano ndani ya mkoa huo jambo linalofanya mkoa huo kuendelea kuwa kisima cha Amani.

Hata hivyo RC Makonda amewaeleza Viongozi wa Dini kuwa namna bora ya kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli na kumuombea ni kuhakikisha waumini wao wanajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili wachague viongozi wa serikali za mitaa wanaochukia Rushwa.

Aidha RC Makonda amemshukuru Balozi wa Falme za Kiarabu kwa kumkabidhi misaada hiyo huku akiwasihi waislamu kutumia mfungo huu Kuliombea taifa na viongozi pamoja na kuwahimiza wazazi kuwalea watoto katika malezi bora.

Kwa upande wake Balozi mdogo wa Falme za Kiarabu amesema wameamua kumuunga mkono RC Makonda kwakuwa wanamuamini akipokea kitu kinawafikia walengwa na amekuwa mtu wa kuwasaidia watu wasiojiweza bila kujali dini wala kabila.

Filamu fupi ya Utunzaji wa Rasilimali Maji


WACHUNGAJI WALA NONDOZZZZ MINNESOTA, MAREKANI

$
0
0
Wachungaji watatu kutoka KKKT DMP na mmoja kutoka KKKT Dayosisi ya Ziwa Victoria  Shinyanga Wamehitimu katika Chuo Kikuu cha Luther Seminary Minnesota USA tarehe 19/05/2019 kama ifuatavyo:-  Rev. Dr. Ernest William Kadiva ametunukiwa Phd - Doctor of Ministry,  Wengine wametunukiwa Master of Arts degree nao ni Rev. Kishe Dismas Mhando - na Rev. Kaanasia Geofrey Msangi, pia Rev. Martha Ernest Ambarang'u wa Dayosis ya Ziwa Victoria Shinyanga ametunukiwa Masters of Arts degree katika mahafali ya 150 iliyofanyika hapa Central Lutheran Church, Minneapolis na kuhudhuriwa na mamia ya wageni kutoka nchi mbalimbali na kutoka majimbo mbalimbali ya Marekani.  Picha kwa hisani ya Noah William Kadiva akiwa Minnesota, Marekani.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 20.05.2019

Introducing "NIMENASA" (Official Video) by AMINI x LINAH -

WAZIRI JAFO ARIDHISHWA NA UJENZI WA HOSPITALI WILAYA YA KILOLO MKOANI IRINGA

$
0
0
Haya ni baadhi ya majengo yaliyojengwa katika hospitali ya wilaya ya kilolo mkoani Iringa ambayoWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameridhishwa na kasi ya ujenzi wake 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiongea na waandishi wa habari juu ya kuridhishwa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya kilolo mkoani Iringa
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akieleza jinsi gani atakavyo hakikisha wanawasimamia vilivyo wakandarasi wa wanaojenga hospitali hiyo ili kusitokee kasoro zozote zile

NA FREDY MGUNDA, IRINGA.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa unaotekelezwa kwa kutumia zilizotolewa na Rais Dkt. John Magufuli katika kuboresha sekta ya afya nchini.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya kukagua hospitali hiyo Waziri Jafo amesema kuwa kasi ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kilolo inaridhisha na baada ya kukamilika kwake itawasaidia wananchi wengi wa maeneo hayo pamoja na kupunguza msongamano katika hospitali ya rufaa.

“Niwahakikishieni viongozi wa wilaya na mkoa kuwa nimeridhishwa na kasi hii ya ujenzi wa hospitali hii kwa kuwa mnasimamia vilivyo kwa kuhakikisha fedha za serikali zinatumia vizuri hivyo niwapongeze sana” alisema Jafo

Jafo alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano ipo makini katika kuhakikisha wananchi wa chini wanapata huduma muhimu bila kizifuata kama ilivyokuwa awali na amehaidi kuwa atazifukisha salamu kwa Mheshimiwa Rais juu ya hatua ambazo zinaendelea katika hospitali hiyo

“Leo naweza kuwapongeza mmefanya kazi kubwa ya kusimamia ujenzi huu ambao umekuwa ukienda vizuri kila hatua ambayo nimekuwa nikifuatia hatua kwa hatua hadi hii leo naona matunda yake” alisema Jafo

Aidha Jafo aliwataka viongozi kuhakikisha wanawasimamia vilivyo wakandarasi wa majengo hayo kumalizia vizuri ili kuondokana na kasoro mbalimbali ambazo zimekuwa zimejitokeza hasa kwenye milando bado kunashida kuhatajikajia kurekebishwa.

“Nimetembea kwenye majengo haya yamejengwa vizuri kwa kufuata vigezo stahili lakini tatizo ambalo nimelibaini ni kuwa mirango haijakaa vizuri inahitajika kutolewa na kuwekwa milango mipya hivyoa naombeni hakikisheni mnasimamia” alisema Jafo

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi alisema kuwa wataendelea kuwasimamia wakandarasi hao ili kuhakikisha wanarekebisha kasoro zote ambazo zimejitokeza katika hatua hizo za umaliziaje wa ujenzi huo wa hospitali hiyo ya wilaya ya Kilolo.

“Mheshimiwa waziri tumezipokea pokea kasoro hizo ambazo umetuagiza tumsimamie waha wakandarasi na sisi tutazisimamia vilivyo ili kupata hospitali iliyo bora kwa kila kitu na kuwa mfano wa kuigwa kwa hospitali nyingine” alisema Hapi

Hapi alimuomba waziri Jafo kuhakikisha anawafikishia shukrani kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli kwa kuwapa fedha nyingi za kutekeleza miradi mbalimbali ya mkoa wa Iringa.

“Kwa kweli tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli kuendelea kutuletea fedha kwenye miradi mingi ya kimkakati hivyo tunashukuru sana” alisema Hapi

Naye mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah alisema kuwa atahakikisha kila uchwao anaendelea kusimamia ujenzi wa hospitali hiyo kwa kuwa ipo katika wilaya yake.

“Mimi nitaendelea kusimamia kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kila kitu kinaenda kama ilivyokusudiwa na kuwa hospitali ya mfano hata nchini hivyo nikuahidi nimeyachukua kwa umakini mkuwbwa maagizo yako” alisema Abdalah

KUMBILAMOTO ATEMBELEA UKARABATI MACHINJIO YA VINGUNGUTI

$
0
0
 Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala,Omary Kumbilamoto akimueleza Gavana wa Tarafa ya Ukonga namna ukarabati wa soko la Vingunguti unavyoendelea .
Kaimu meya Manispaa ya Ilala akionesha sehemu ambayo haijakarabatiwa na maji yanatuwama, hivyo kumtaka Wakandarasi wa eneo hilo kufanya haraka kukamilisha ujenzi.

Mafundi ujenzi wanaendelea na ukarabati katika Machinji ya Vingunguti ambapo kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti Omary Kumbilamoto alitembelea ujenzi huo kuangalia ni hatua gani imefikiwa
--
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images