Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

VODACOM YASAJILI WANAFUNZI MFUMO MPYA WA ALAMA ZA VIDOLE JIJINI DODOMA

$
0
0
 Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania Plc Michael Mhando na Emmanuel Medukenya wakisajili wanafunzi kwa kutumia mfumo mpya wa alama za vidole katika viwanja vya chuo kikuu cha Dodoma, jijini humo. Hivi karibuni kampuni hiyo imewezesha wafanyakazi wake na vifaa vya kusajilia kwa kutumia alama za vidole ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wateja wake popote nchini.


DKT. MWANJELWA AFUNGUA SEMINA YA KUZIJENGEA UWEZO NCHI WANACHAMA WA KAMISHENI YA UMOJA WA AFRIKA

$
0
0

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akifungua Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji  wa Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala na Utoaji wa taarifa Barani Afrika iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akifuatilia maelezo ya Mwakilishi wa Mkurugenzi anayeshughulikia Masuala ya Siasa Umoja wa Afrika, Bw. Issaka Garba Abdou wakati wa Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji wa Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala na Utoaji wa taarifa Barani Afrika, iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
 Washiriki wa Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji  wa Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala na Utoaji wa taarifa Barani Afrika wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipokuwa akifungua semina hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe kutoka Tanzania, Bwana Gubas Vyagusa akizungumza kwenye Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji wa Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala na Utoaji wa taarifa Barani Afrika, iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji  wa Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala na Utoaji wa taarifa Barani Afrika iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AONGOZA WANANCHI KATIKA MAZIKO YA WAZIRI WA ZAMANI MAREHEMU ALI JUMA SHAMUHUNA KIJIJI CHA DONGE MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

$
0
0

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hassan Khatib alipowasili katika hafla ya maziko ya aliyekuwa Waziri wa Zamani wa SMZ Marehe Ali Juma Shamuhuna, kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri, alipowasili katika Kijiji cha Donge Imiyani.(Picha na Ikulu)
 BAADHI ya Wananchi kutoka sehemu mbalimbali Zanzibar wakijumuika katika hafla ya maziko ya Marehemu Ali Juma Shamuhuna yaliofanyika katika Kijiji cha Donge Imiyani Mkoa wa Kaskazini Unguja leo, 20-5-2019.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.,Dk. Ali Mohamed Shein, akishiriki katika Sala ya kuusalia Mwili wa Marehemu Ali Juma Shamuhuna, maziko yaliofanyika katika Kijiji chao Donge Imiyani Mkoa wa Kaskazini Unguja.leo 20-5-2019.(Picha na Ikulu)
 WANANCHIna Waumini wa Dini ya Kiislam wakiitikia dua baada ya kumalizika Sala ya kuuombea mwili wa Marehemu Ali Juma Shamuhuna iliofanyika katika msikiti wa Donge Imiyani Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.20-5-2019
 WANANCHI wakiwa wamebeba jeneza likiwa na mwili wa Marehemu Ali Juma Shamuhuna wakati wa maziko hayo yaliofanyika Kijijini kwao Donge Imiyani Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.
 VIJANA wa Chama Cha Mapinduzi walioandaliwa kwa ajili ya kubeba jeneza la Marehemu Ali Juma Shamuhuna wakati wa maziko hayo wakielekea katika eneo lililotengwa kwa maziko hayo katika Kijiji cha Imiyani Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Ali Juma Shamuhuna wakati wa maziko hayo yaliofanyika katika Kijiji cha Imiyani Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.20-5-02019
 MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Ali Juma Shamuhuna
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akisoma wasifu wa Marehemu Ali Juma Shamuhuna, baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya maziko iliofanyika katika Kijiji cha Donge Imiyani Mkoa wa Kaskazini Unguja
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, na Wananchi wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa Sala ya kuusalia mwili wa marehemu iliofanyika kjatika Masjid ya ilioko Kijiji Kwao Donge Imiyani Mkoa wa Kasakazini Unguja leo.20-5-2019.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akitowa mkono wa pole na kuifariji familia ya Marehemu Ali Juma Shamuhuna,wakati wa msiba huo uliofanyika Kijiji kwao Donge Imiyani Mkoa wa Kaskazini Unguja leo
RAIS wa Zabnzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia dua ikisomwa na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi, wakati wa hafla hiyo ya maziko ya Marehem,Ali Juma Shamuhuna yaliofanyika Kijiji kwao Donge Imiyani Mkoa wa Kaskazini Unguja leo. (Picha na Ikulu)

KAFULILA AELEZEKA MPANGOKAZI WA USAIDIZI WA KISHERIA UKAMILIKE HARAKA

$
0
0
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila akinukuu baadhi ya maoni ya wadau katika kikao cha wadau wa msaada wa kisheria kwa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini inayojumuisha mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa na Songwe, kulia kwake ni Msajili wa Mashirika na taasisi zinazotoa Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Felista Joseph

Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila ameelekeza kuwa mpango kazi wa kuratibu taasisi na mashirika yanayotoa msaada wa kisheria kwa wananchi ukamailike haraka ili wananchi wapate huduma ya usaidizi wa kisheria kwa ufanisi.

Kafulila ametoa maelekezo hayo jana wakati akifungua kikao cha wadau wa msaada wa kisheria kwa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini inayojumuisha mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa na Songwe

“Watu wengi wamepoteza haki zao kwa kutokujua sheria au kutokuwa na fedha za kumudu gharama za mawakili lakini serikali imetengeneza utaratibu wa kuratibu taasisi ambazo zinatoa msaada wa kisheria bila malipo ili wananchi wengi zaidi wasiojiweza waweze kupata msaada wa kisheria na wasikose haki zao”, amesema Kafulila.

Amesema kuwa mpango kazi wa kuziratibu taasisi zinazotoa msaada wa kisheria uwe unapimika na hasa uwe na lengo la kutoa elimu kwa wananchi ili wajue kuwa hata kama hawana fedha za kugharimia mawakili wa kuwatetea ili wapate haki zao au hawana elimu juu ya sheria mbalimbali, zipo taasisi ambazo zinatoa huduma hiyo bila malipo.

Naye Msajili wa Mashirika na taasisi zinazotoa Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Felista Joseph amesema kuwa elimu kwa umma itapewa kipaumbele katika mpango kazi huo na ni jambo la msingi ili wananchi wafahamu uwepo wa taasisi hizo

“Katika wiki ya msaada wa kisheria tunatoa elimu kwa wananchi kupitia vipeperushi, radio mbalimbali, tunazungumza nao katika maeneo mbalimbali pia orodha ya taasisi hizo huwekwa katika maeneo yote muhimu ili wananchi wajue kuna taasisi ambazo hutoa msaada wa kisheria pale ambapo watakuwa na uhitaji”, amesema Joseph.

Kwa upande wake Mratibu wa shirika la Gender and Social Reform Steward Shiwuga amesema shirika lake limekuwa likipata vikwazo katika kutoa msaada wa kisheria bila gharama yoyote na pia baadhi ya watendaji wamekuwa hawatoi ushirikiano kwao.

“Wananchi wakisikia huduma ya msaada wa kisheria tunaitoa bure wengine haamini wamezoa kutozwa fedha lakini pia baadhi ya watendaji wamekuwa hawatoi ushirikiano kwetu lakini tunaendelea kuwaelimisha wananchi na watendaji na matokeo tunayaona kwa sasa angalau ushirikiano umeanza kuongezeka na wananchi wanakuja kupata msaada”, amesema Shiwuga. 

Msajili Msaidizi wa Taasisi za Msaada wa kisheria kwa Wilaya ya Ileje Rodrick Sengela ameeleza kuwa hapo awali taasisi hizo zilijiendesha bila kuratibiwa pia baadhi ya watu wasio waaminifu walikuwa wakiwarubuni wananchi na kuwatoza fedha nyingi pale wanapohitaji msaada wa kisheria lakini kwa sasa wananchi wataelimisha mahali sahihi pa kupata msaada wa kisheria bila malipo.

Sevilla FC ya Italy kutua Dar leo, kukipiga na Simba SC Alhamisi Uwanja wa Taifa

$
0
0


Mabingwa wa soka katika michuano ya Ligi Kuu ya Hispania, LaLiga, timu ya Sevilla Fútbol Club  maarufu kama Sevilla FC inatarajiwa kuwasili nchini leo kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya  Simba ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya  kwa timu hiyo kucheza nchini  Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana, timu hiyo ambayo iliundwa January 25, 1890 (ina umri wa miaka 129 sasa)  hiyo inatarajiwa kuwasili jioni hii katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius  Nyerere jijini Dar es salaam.

Kulingana na taarifa hiyo mechi hiyo itakuwa ni maalum kwa vinara hao wa LaLiga ambao wanadhaminiwa na  SportPesa na akaongeza  kwamba ziara itahusisha matukio kadhaa ya   jamii na michezo ikiwemo kliniki namafunzo mbalimbali.
 "Kama ushindani wa kimataifa unakutana na dhamira ya LaLiga kuwa karibu na mashabiki wake. Kwa kweli kwamba mashabiki wetu wa Tanzania wataweza kupata furasa ya  kuangalia karibu  klabu kubwa kama Sevilla FC inamaanisha kuwa ni fursa kubwa kwa kila mtu," alisema Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kimataifa katika Ligi ya La Liga, Oscar Mayo.
  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Tarimba Abbas, kampuni yao  imeshirikiana na baadhi ya taasisi za soka za kubwa  ulimwenguni  baada ya kuna kuna haja ya  kuleta uzoefu  huu mkubwa  kwa Tanzania.
 "Ili kufurahia kuona moja ya klabu  kubwa za  mpira wa miguu  Ulaya, Sevilla FC. Kwa makubaliano yetu na LaLiga ambayo ni ligi bora duniani, tutaweza kuonyesha vipaji vyetu  na kuboresha kiwango cha soka  nchini ", alisema Talimba.
 Alisema kwamba mechi hiyo ni sehemu ya mradi wa 'LaLiga duniani  ambao unalenga kueneza soka  la  Hispania kimataifa na  kueneza pia sera ya 'Marca España', kuleta karibu mashabiki wa  LaLiga na  kukuza klabu nje ya nchi yetu.

Hii itakuwa ni klabu ya pili Ulaya kufanya ziara Afrika Mashariki, baada ya mwaka 2017 Everton FC kucheza  na  Gor Mahia  nchini  Kenya, ingawa  sio mara ya lkwanza kwa  Sevilla kutua katika bara hili kwani  mwaka  2015  ilikuwa nchinbi  Morocco ambao ilicheza mechi ya kuajindaa na  LaLiga dhidi ya timu ya   Hassania Union Sport d'Agadir.

ISACA TANZANIA CHAPTER 2019 annual Conference

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MEI 22,2019

SEVILLA FC YA HISPANIA YATUA DAR,KUCHEZA NA SIMBA SC KESHO UWANJA WA TAIFA

$
0
0
Msafara wa wachezaji 18 na viongozi wa Klabu ya Sevilla FC umetua nchini usiku wa kumkia leo . 

Sevilla wametua nchini chini ya uratibu wa Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya SportPesa pamoja na Laliga. Sevilla wakiwa hapa nchini watacheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya Simba kesho kutwa Alhamisi utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya Sevilla kutua, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas amesema kuwa anafurahia ujio wa Sevilla ambao utaongeza utalii nchini.

Tarimba aliwatahadharisha Sevilla kwa kuwaambia kuwa wajiandae wanacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mabingwa wa Ligi Kuu Bara.
“Ninawaambia kuwa jiandaeni kupambana na mabingwa wa ligi hapa nchini ambao ni Simba.” Ni timu nzuri iliyojiandaa kuhakikisha inapata ushindi kutokana na ubingwa walioupata,”amesema Tarimba.

Lakini pia mara baada ya kuwasili nchini,kikosi hicho kililakiwa na burudani sana kabisa kabisa kutoka kwa kundi la Ngoma za asili linaloongozwa na Msanii mahiri wa kughani Mrisho Mpoto,ama kwa hakina walikunwa na uchezaji ngoma na kujikuta nao wakiinuka kujimwaya mwaya kwa pamoja.

WAZIRI WA AFYA AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA JIMBO LA XUZHOU NCHINI CHINA

$
0
0

Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akizungumza na ujumbe kutoka Mji wa Xuzhou Nchini China uliokuja kufanya tathmini ya Madaktari wa nchi hiyo wanaokuja kufanya kazi Zanzibar Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar. 
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akiagana na Kiongozi wa ujumbe kutoka Mji Xuzhou Nchini China Zhou Guangchum baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ofisini kwake. Picha na Makame Mshenga. 

 

Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar 

Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed ameiomba Jamhuri ya Watu wa China kurejesha utaratibu wa madaktari wa nchi hiyo wanaokuja kufanyakazi Zanzibar kukaa miaka miwili badala ya mwaka mmoja wa sasa. 

Alisema tokea kuanzisha uhusiano wa madaktari wa China kuja Zanzibar mwaka 1965 walikuwa wakikaa kipindi cha miaka miwili lakini utaratibu huo ulibadilika miaka ya hivi karibuni na hivi sasa wanakaa mwaka mmoja. 

Waziri wa Afya alitoa ombi hilo alipokutana na Ujumbe wa wataalamu wa afya kutoka Mji wa Xuzhou ambao upo nchini kufanya tathmini ya Madaktari wanaokuja kufanyakazi Zanzibar katika hospitali ya Abdlala Mzee Mkoani na Mnazimmoja. 

Aliueleza ujumbe huo kwamba utaratibu wa zamani wa timu za madaktari wa China kukaa miaka miwili ulikuwa unatoa fursa nzuri kwa madaktari wa Zanzibar kujenga uzoefu na kujifunza mambo mengi ya kitaalamu kutoka kwao. 

Alisema madaktari wa Zanzibar wanapopata uzoefu kwa vitendo kutoka kwa madaktari wa China inawasaidia kufanya vizuri wanapopata nafasi ya masomo ya juu nje ya nchi. 

Waziri Hamad aliushauri ujumbe huo kuwaelekeza madaktari wa China waliopo Zanzibar kuwapa mafunzo madaktari wa Hospitali ya Abdalla Mzee ya kutumia mashine mpya zilizowekwa katika hospitali hiyo na kuitafsiri teknolojia iliyotumika ili baada ya kuondoka waweze kuzitumia. 

Aidha Waziri wa Afya aliwahimiza madaktari wazalendo kuwa tayari kujifunza utaalamu kutoka madaktari wa China ambao wamekuwa wakifanya matibabu ya kitaalamu na kuwashirikisha. 

Kiongozi wa ujumbe huo Zhou Guangchum alimuhakikishia Waziri wa Afya kwamba nchi yake itaendelea kuisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuongeza msaada wake hasa katika sekta ya afya. 

Aliahidi kuwa atalifikisha nchini kwake ombi la kurejesha utaratibu wa zamani wa madaktari wanaokuja Zanzibar kukaa kwa kipindi cha miaka miwili ili waweze kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ndugu zao.

RAIS MAGUFULI ATOA SIKU 30 KWA VIONGOZI NA WATENDAJI WAKUU WA SERIKALI KUTUMIA HUDUMA ZA KAMPUNI YA TTCL.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo kuhusu uzalendo na kuunga mkono Shirika la Mawasiliano TTCL jijini Dar es Salaam.


Na Paschal Dotto,MAELEZO 

RAIS Dkt.John Magufuli siku 30 Ofisi ya Rais-IKULU, Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara pamoja na Viongozi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma,kutum kutumia huduma za Kampuni ya Mawasiliano ya Simu Nchini (TTCL)ikiwemo laini, ili kupanua huduma za mawasiliano ya Mtandao wa Kampuni hiyo nchini. 

Akizungumza wakati wa Hafla ya kukabidhi gawio kwa Serikali la Tsh Bilioni 2.1 kutoka TTCL, Rais Magufuli alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa TTCL kumuorodheshea nam,ba za simu za Viongozi na Watendaji wote wa Serikali ikiwemo Mawaziri na Makatibu Wakuu kuona kama wanatumia laini za simu za TTCL. 

Aliongeza kuwa tangu atoe agizo lake mwaka jana, kuhusu matumizi ya huduma za mawasiliano ya TTCL katika Ofisi mbalimbali za Umma, hakuna Ofisi yoyote ilitekeleza agizo hilo ukiondoa baadhi ya Taasisi chache ikiwemo Jeshi la Wananchi Tanzania na Jeshi la Polisi Nchini. 

“Nimefurahi alipokuwa akitaja Taasisi na Mashirika ambayo yamejiunga moja kwa moja na kutumia huduma za TTCL, nilisikitika sana niliposikia Ofisi yangu haikutajwa, pia Ofisi ya Chama changu cha mapinduzi, sasa kama wamesikia na wako hapa nataka kipindi cha mwezi mmoja tuanze kutumia simu za TTCL”, Rais Magufuli. 

Aidha Rais Magufuli alizitaka Ofisi zingine za Serikali kutumia huduma za Kampuni ya Mawasiliano Nchini ili kuinua na kuimarisha utendaji kazi wake katika nyanja mbalimbali za maendeleo nchini na kuzitaka Taasisi zingine ziige huo kwa vitendo na siyo maneno. 

“Si Ofisi ya Makamu wa Rais, Si Ofisi ya Waziri Mkuu, Si Ofisi ya Rais, Si Wizara ya Fedha, hata Wizara yako ya Mawasiliano na Uchukuzi nayo haijatajwa hapa, nataka kusema tusipounga Mkono, vyetu tutachezewa mno, tusipowaimarisha hawa TTCL, hawatafika mbali, lakini wakipata ushirikiano matokeo tutayaona”, Rais Magufuli. 

Rais Magufuli alieleza kuwa kabla ya Shirika hilo halijarudishwa Serikalini, katika kipindi cha miaka 15 kutoka mwaka 2001 TTCL ilikuwa ikipata hasara ya Tsh Bilioni 15 kila mwaka, huku likishindwa kutoa gawio lolote kwa Serikali. 

“Wakati Shirika hili likiendeshwa na Wabia wetu, lilikuwa halitoi gawio lolote, lakini pia lilikuwa likipata hasara ya Bilioni 15 kwa mwaka, kwa hiyo mnaweza mkaelewa hii ina maana gani kwenye uchumi wa nchi, hivyo basi kuweza kufikia hatua hii ya kupata faida ya Tsh.bilioni 8.3, na kuweza kutoa gawio la Serikali Tsh.bilioni 2.2 ni mafanikio makubwa’ alisema Rais Dkt Magufuli. 

Pia Rais Magufuli alisema kuwa Sekta ya Mawasiliano kwa sasa imepanuka nchini na kuwezesha sekta nyingine kufanya kazi kwa ufanisi kwani katika sekta mbalimbali kwa sasa sekta hii inahitajika sana. 

“Sekta ya Mawasiliano imesaidia kukua kwa sekta nyingine kama sekta ya fedha, ambapo mwaka jana miamala ya fedha ilifanyika kwa njia ya kimtandao ilikuwa na thamani ya Tsh Trilioni 139.2 sawa na Trilioni 11.6 kwa mwezi, lakini pia sekta ya mawasiliani ni kichocheo kikubwa kwa Sekta za Elimu, Afya, Biashara, Kilimo, Viwanda Ufugaji, Utalii na Ujenzi”, Rais Magufuli. 

MAKAMBA AWAAGIZA WENYEVITI WA MITAA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU MARUFUKU MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI

$
0
0
Serikali imetoa wito kwa Watanzania kuwa ni kosa kisheria pindi watakapokutwa na mifuko ya Plastiki kuanzia Juni mosi mwaka huu.

Wito huo umetolewa leo Jumanne May 21, 2019 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba wakati akizungumza kwenye kikao cha viongozi na watendaji wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwemo Wenyeviti wa Mitaa yote ya Mkoa huo na agenda kuu ikiwa ni marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki.

Waziri Makamba amesema ni vyema watendaji wote wa Mkoa wa Dar es Salaam wakahamasisha wananchi wao ili waweze kutekeleza agizo hilo kwani adhabu mbalimbali ikiwemo faini au kifungo gerezani zitahusika kwa atakayekiuka katazo hili kulingana na Kanuni za “Marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki za Mwaka 2019” zilizoandaliwa chini ya Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004.

Akizungumza katika mkutano huo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mwita Waitara amezielekeza Mamlaka ya Serikali za Mitaa kote nchini kuhakikisha wanatenga maeneo maalum ya kuhifadhia mifuko ya plastiki itakayosalia ifikapo Juni mosi mwaka huu na wananchi wa maeneo husika kujulishwa.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakari Mussa Kunenge akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ameeleza mikakati ambayo Mkoa wanaifanya ya kudhibiti taka zinazozalishwa jijini ikiwemo mfumo mzuri wa uratibu na usimamizi kwa viongozi katika zoezi hilo.

Baadhi ya watendaji wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao wameshiriki kwenye kikao hicho wameeleza kuwa ni vyema ikaendelea kutolewa elimu kwa wananchi ili waweze kutii agizo hilo kwa wakati uliopangwa.

Bidhaa ambazo hazitaathiriwa na katazo hili ni pamoja na vifungashio vya bidhaa kama vile vifungashio vya madawa, vifungashio vya vyakula kama vile: maziwa, korosho, n.k bidhaa za viwandani, kilimo na ujenzi. Hata hivyo, vifungashio ni lazima vikidhi viwango vilivyowekwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira January Makamba kizungumza kwenye mkutano na viongozi na watendaji wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwemo Wenyeviti wa Mitaa yote ya mkoa na agenda kuu ikiwa ni marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki,jana Jumanne Mei 21, 2019 katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche akizungumza na wadau mbalimbali wa Mazingira ambapo amesema ni kosa kisheria pindi watakapokutwa na mifuko ya Plastiki kuanzia Juni mosi mwaka huu jana Jumanne Mei 21, 2019 katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Baadhi ya viongozi na watendaji wa mkoa wa Dar es Salaam wakiwemo wenyeviti wa Mitaa yote ya mkoa wakiwa katika mkutano uliofanyika leo May 21, 2019 kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Muonekano wa vifungashio vilivyo ruhusiwa kisheria kama vinavyo onekana katika picha.

HALMASHAURI YAVUNJA MKATABA WA UJENZI MRADI WA MAJI SAWALA

$
0
0
Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imevunja mkataba wa ujenzi wa mradi mkubwa wa Maji maarufu kama mradi wa Maji Sawala katika Kata ya Mtwango wenye thamani ya shilingi Bilioni 1.8 uliyokuwa ukitekelezwa kwa pamoja na Kampuni za Siha Enterprise Co. LTD na Mavonda Co. LTD za Jijini Dar Es Salaam.

Halmashauri imelazimika kuvunja mkataba huo baada ya Mkandarasi kuonesha uwezo mdogo wa kutekeleza kazi hiyo, kwani tangu asaini Kandarasi ya ujenzi mnamo mwezi Januari 2018, katika hali ya kusikitisha ametekeleza jukumu hilo kwa asilimia 30 pekee licha ya kulipwa Fedha ya awali zaidi ya shilingi Milioni 270.

Aidha, Mkandarasi huyo anatakiwa kuilipa Halmashauri kiasi cha shilingi Milioni 413, ambapo kati ya hizo shilingi Milioni 254 ni faini wakati Milioni 159 ni bakaa ya Fedha ya utangulizi ambayo alilipwa baada ya kusaini mkataba.

Uongozi wa Halmashauri unaomba radhi kwa wananchi wa Kata ya Mtwango kwa kutopata huduma muhimu ya Maji kwa wakati, hata hivyo, uongozi unawahakikishia kuwa mradi utatekelezwa kama ilivyokusudiwa kwani taratibu za kumpata Mkandarasi mwenye uwezo na utashi wa kuujenga zimeanza.

Mnamo mwaka 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ilitiliana saini na Kampuni za Siha Enterprise Co. LTD pamoja na Mavonda Co. LTD kwa kandarasi ya miezi 12 ya kujenga na kuyafikisha Maji katika makazi ya watu kwenye Vijiji nne vya Sawala, Mtwango, Lufuna na Kibao kwa shabaha ya kuhudumia watu elfu 14.

Netho Ndilito
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi

RAIS DKT. SHEIN AKUJUMUIKA NA WANANCHI KATIKA FUTARI ALIOWAANDALIA CHUO CHA AMALI MKOKOTONI

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.Mhe Haji Omar Kheri, alipowasili katika viwanja vya Chuo Cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.21-5-2019.
 WANANCHI wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakijumuika na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, katika futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Unguja.(Picha na Ikulu)
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja katika futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Dk. Ali Mohamed Shein, katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja katika futari Maalum aliyowaandalia katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na kushoto Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe Vuai Mwinyi
 WANANCHI wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakijumuika katika Futari Maalum walioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Vuai Mwinyi akitowa shukrani kwa Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini baada ya kumalizika hafla ya Futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya futari iliofanyika Mkoa wa Kaskazini Unguja, kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.Mhe. Haji Omar Kheri na kushoto Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe Vuai Mwinyi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu.
 WANANCHI wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu)


 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na kuagana na Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Unguja.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Wananchi wa Mkoa wa Kaskaziuni Unguja baada ya kumaliza futari aliyowaandalia katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu)

RAIS DKT.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA UJENZI MAWASILIANO NA USAFIRISHAJI ZANZIBAR IKULU NDOGO KIBWENI

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar, katika mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara hiyo iliofanyika Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na kulia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Dkt. Sira Ubwa.
 WAZIRI wa Ujenzi Mawasiliani na Usafirishaji Zanzibar Dkt. Sira Ubwa akiwasilisha Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara yake wakati wa mkutano huo uliofanyika Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.
 KATIBU Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Ndg. Mustafa Aboud Jumbe akiwasilisha Vifungu vya Matumizi na Mapato ya Wizara yake wakati wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai 2018 hadi March 2019, katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
 BAADHI ya Maofisa wa Idara za Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji wakifuatilia mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.(Picha na Ikulu)

NEC YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATIKA KATA 32 ZA TANZANIA BARA

$
0
0
Na Subira Kaswaga (Afisa Habari NEC)

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza tarehe 15, Juni mwaka huu kuwa ni siku ya kufanyika kwa Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika kata 32 zilizopo katika halmashauri ishirini (20) za Tanzania Bara. 

Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaam Makamu, Mwenyekiti wa NEC Jaji (R) Mbarouk S. Mbarouk amesema kuwa, Tume imetangaza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya serikali za Mitaa, juu ya uwepo wazi wa nafasi 31 za Udiwani katika Kata 31 za Tanzania Bara kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kujiuzulu na vifo.

Aidha, amesema kuwa, Tume imetangaza kufanyika kwa Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika kata ya Kitangiri Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela jijini Mwanza sambamba na kata hizo 31, baada ya Mahakama ya Rufaa kuondoa maombi ya mapitio yaliyowasilishwa katika Mahakama hiyo, kufuatia kutenguliwa kwa matokeo ya Uchaguzi wa Udiwani katika kata hiyo.

Jaji (R) Mbarouk amesema kuwa, fomu za uteuzi wa Wagombea zitatolewa kati ya tarehe 27 hadi 31 Mei, uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 31 Mei, kampeni za uchaguzi zitaanza tarehe 01 Juni hadi 14 Juni mwaka huu na tarehe 15 Juni, mwaka huu ndiyo itakuwa siku ya uchaguzi.
Amezitaja kata zitakazofanya uchaguzi huo kuwa ni Mto wa Mbu, Mkuyuni na Majengo zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Kata za Ganako, Daa, Mbulumbulu, Oldeani na Kanssay zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Karatu mkoani Arusha. Kata ya Likuyuseka iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Kata za Kinyasiti kati iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na Kata ya Kikombo iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma mkoani Dodoma, Kata ya Itenka iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi, Kata za Ipole na Pangale zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge na Kata ya Itumba iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Igunga  za mkoani Tabora.

Nyingine ni Kata ya Boma iliyopo Halmashauri ya Mji wa Mafinga mkoani Iringa, Kata za Tandika na Chikongola zilizopo Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara, Katika Mkoa wa Dar es Salaam zip Kata za Bonyokwa iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Kata ya Tungi iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni na Kata ya Chang’ombe iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.

Pia Kata ya Ruangwa iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, Kata za Mkula na Lamadi zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Kata za Kibosho Magharibi na Uru Shimbwe zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi za mkoani Kilimanjaro, Kata ya Murangi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Musoma mkoa wa Mara na Kata ya Siuyu iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

Pamoja na Kata za Kyaitoke, Mugajale na Ruhunga zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera na Kata ya Kitangiri iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
Aidha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imevikumbusha vyma vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni, maadili ya Uchaguzi, taratibu, miongozo na maelekezo yanayotolewa na Tume wakati wote wa kipindi cha Uchaguzi huu mdogo.

COSTECH yaendesha mafunzo kwa wadau katika utafiti

$
0
0
 Mafunzo ya Siku mbili ambayo yameandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia yamefugwa rasmi June 21 mwaka huu Mkoani Mtwara ambayo yalikuwakutanisha Watafiti,Waandishi Wa Habari na Wataalam kutoka taasisi mbalimbali  za utafiti kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara zikiwemo VETA na SIDO pamoja  Taasisi za elimu ya juu na kilimo.

Akifunga Mafunzo hayo Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Tume hiyo Dr Bakari Msangi amewapongeza washiriki kwa Kuhudhuria na kuwataka kuyafanyia kazi yale waliyojifunza ili ilete tija kwa Jamii Husika 

Dr.Msangi amesema pia kazi ya Tume ni kuratibu na kushauri hivyo amewaomba Watafiti kutoa matokeo ya Utafiti wao nje na njia bora ni kwa kuwatumia Wanahabari Kama daraja kwa Jamii

Kwa upande mwingine ameahidi kuwatunikia vyeti vilivyosainiwa nakurugenzi Mkuu wahitimu wote Wa Mafunzo Kama sehemu ya kutambua na kuthamini mchango wao 

Kwa upande wake Afisa Habari Wa Mkoa Wa Mtwara Bw.Evarist Masuha ameishukuru COSTECH na kuwaomba kushirikiana na Mkoa katika mambo mbalimbali yanayohusu Sayansi teknolojia na Ubunifu.
 Mwakilishi wa mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya sayansi na Teknolojia COSTECH Dkt.Bakari Msangi  (katikati) akifunga mafunzo ya siku  mbili ambayo yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia yamefugwa rasmi June 21 mwaka huu Mkoani Mtwara ambayo yalikuwakutanisha Watafiti,Waandishi Wa Habari na Wataalam kutoka taasisi mbalimbali  za utafiti kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara zikiwemo VETA na SIDO pamoja  Taasisi za elimu ya juu na kilimo.
 Afisa habari mkoa wa Mtwara akiishukuru COSTECH kwa kuona umuhimu wa kuleta mafunzo mkoani Mtwara 
Baadhi ya washiriki katika mafunzo ya siku  mbili ambayo yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia yamefugwa rasmi June 21 mwaka huu Mkoani Mtwara ambayo yalikuwakutanisha Watafiti,Waandishi Wa Habari na Wataalam kutoka taasisi mbalimbali  za utafiti kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara zikiwemo VETA na SIDO pamoja  Taasisi za elimu ya juu na kilimo.

HALMASHAURI ZA MKOA WA RUVUMA ZATAKIWA KUDHIBITI BIDHAA ZA CHAKULA, VIPODOZI NA DAWA ZISIZO NA UBORA NA USALAMA

$
0
0
Waganga wakuu wa halmashauri katika mkoa wa Ruvuma wameagizwa kusimamia kwa karibu  ubora na usalama wa chakula,dawa na vipodozi uliokasimiwa kwao  na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini(TFDA).
Agizo hili limetolewa jana mjini Songea na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Edmund Siame wakati alipofungua kikao kazi kati ya watendaji wa TFDA na halmashauri nane za Ruvuma

Siame amesema kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Chakula na Dawa Kanda ya Kusini imeonyesha halmashauri za Ruvuma zimeshindwa kutekeleza kwa ufanisi usimamizi wa majukumu yaliokasimiwa kwao kwa mujibu wa makubaliano kati ya Wizara ya Afya na TAMISEMI
Sheria ya Chakula ,Dawa na Vipodozi  Sura 209 na kanuni zake za mwaka 2015 ilikasimu baadhi ya majukumu kwa halmashauri  nchini kote ili kudhibiti bidhaa zisizo na ubora na salama.

Amezitaja changamoto zilizokwamisha utekelezaji wa majukumu ya TFDA kuwa ni kushindwa kutenga bajeti ya fedha zinazotokana na makusanyo ya ada na tozo za vibali vya TFDA ili ziweze kutumika katika udhibiti wa bidhaa na kufanya ukaguzi.
“Ni kosa kwa halmashauri kushindwa  kufanya vikao vya robo mwaka vya kamati za chakula na dawa kwani kunasababisha bidhaa zisizo na ubora na usalama kuingia mitaani na kuweza kusababisha madhara kwa wananchi” alisema Siame

Halmashauri hizo pia zimeshindwa kuwasilisha taarifa za za utendaji kazi kwa kila robo mwaka kama ambavyo imeelekezwa kwenye kanuni
Siame ameagiza waganga wakuu wa halmashauri za Ruvuma kuanzia sasa kurekebisha mara moja upungufu na kuhakikisha lengo la TFDA na serikali kulinda afya ya jamii linatimizwa .
Kaimu Katibu Tawala huyo wa Mkoa ametaka kuwepo ushirikiano wa karibu kati ya TFDA na wilaya ili kuepusha madhara kwa walaji na kuepusha uchumi wa nchi kushuka.

“Bidhaa za chakula,dawa,vipodozi na vifaa tiba visipodhibitiwa ipasavyo zinaweza kusababisha madhara ya vifo na kudhoofisha uchumi wa nchi yetu”alisisitiza Siame
Kwa upande wake Meneja wa TFDA kanda ya Kusini, Juma Bukuku amezishauri halmashauri za mkoa wa Ruvuma kuacha kutoza ada na tozo kwa maeneo ambayo hayakukasimiwa kwao mfano maduka ya vipodozi na maduka ya dawa ya jumla.

Akizunguzia tatizo la bajeti Mganga Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru Dkt .Wendy Robert amesema tatizo la ukosefu wa bajeti  lilisababisha washindwe kufanya ufuatiliaji wa shughuli za udhibiti na ubora wa chakula na dawa kwenye baadhi ya maeneo pembezoni.
Naye Dkt.Aron Hyera kutoka halmashauri ya wilaya ya Nyasa ameshukuru kwa TFDA kuratibu kikao kazi hiki kwani kimesaidia kuweka uwelewa na mipaka ya utendaji kazi kati ya TFDA na halmashauri kwenye usimamizi wa majukumu.

Mwisho.
Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Ruvuma

NEC YAFANYA UTEUZI WA MADIWANI WAMAWAKE WA VITI MAALUM

$
0
0
Na Subira Kaswaga (Afisa Habari NEC)

Tume ya Taifa ya  Uchaguzi (NEC) imefanya uteuzi wa Madiwani Wanawake wa Viti Maalum saba (07) katika Hamlashauri za Manispaa za Sumbawanga na Tunduma, Halmashauri za Wilaya za Tandahimba, Korogwe na Rombo.

Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji (R) Mbarouk S. Mbarouk amesema kuwa,  uteuzi huo umefanyika baada ya  Tume kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa juu ya uwepo wazi wa nafasi za Madiwani Wanawake wa Viti Maalum katika halmashauri hizo kutokana na sababu mbalimbali.

Amezitaja sababu hizo kuwa ni pamoja na waliokuwa Madiwani katika Halmashauri hizo kufariki dunia, kujiuzulu na kuvuliwa uanachama na hivyo nafasi zao kuwa wazi. 

Jaji (R) Mbarouk S. Mbarouk amewataja Madiwani walioteuliwa na vyama wanavyotoka kuwa ni Regina  Willbard Lyakurwa na Beatrisi Revocatus Silayo Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Regina Abiudi Liffi Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na Agness Atanazi Chilulumo Halmashauri ya Manispaa ya Tunduma wote wanatoka CHADEMA.

Wengine ni Shahara A. Alfani na Mey R. Dadi Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kutoka CUF na Mwajuma Waziri Kitumpa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe  kutoka CCM.

WATU WANNE WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 27 KWA KOSA LA KUSAFIRISHA MENO YA TEMBO YENYE THAMANI YA ZAIDI YA YA MILIONI 32

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

WATU wanne wakazi wa jijini Dar es Salaam wamehukumiwa kutumikia kifungo cha jumla ya miaka 27 gerezani baada ya kupatikana na hatia katika makosa matatu likiwemo la kupatikana na vipande sita vya meno ya tembo vyenye thamani ya USD 15000 ambazo ni zaidi ya Sh. Milioni 32.5

Aidha mahakama imeamuru kutaifishwa kwa gari aina ya Funcargo yenye namba za usajili T.540 DDS ambayo ilitumika kubebea meno ya Tembo hayo.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Maria Kasonde wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi 11 ulioletwa na upande wa mashtaka pamoja na vielelezo viwili katika kuthibitisha kesi hiyo.

Washtakiwa waliohukumiwa kifungo hicho ni Solomon Mtenya, Siasa Athumani, Musa Ligagabile, Omary Sabo.

Kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 31 iliendeshwa na mawakili wa Serikali, Salum Msemo na Constantine Kakula. Akisoma hukumu Hiyo, Hakimu Kasonde amesema, "Mahakama imeridhika na ushahidi wa uliotolewa na upande wa mashtaka na mahakama inawahukumu kutumikia kifungo  cha miaka 27 gerezani ili iwe fundisho kwao na kwa wengine wenye nia ya kutenda makosa kama hayo.

Akifafanua adhabu hizo, Hakimu Kasonde amesema, katika shtaka la kwanza washtakiwa Mtenya, Athumani na Sabo, wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani huku
katika shtaka la pili la kujihusisha na nyara za serikali washtakiwa wote wamehukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani. Aidha katika shtaka la tatu la kusafirisha nyara hizo, washtakiwa  wote wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 gerezani.

Hata hivyo, Mahakama imesema kuwa adhabu zote hizo zitaenda kwa pamoja hivyo watuhumiwa wote watakaa gerezani kwa miaka 20 pekee.

Katika kesi hiyo, watuhumiwa wanadaiwa, Juni 23, 2016 huko Kimara, katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao kwa pamoja walikutwa wakisafirisha vipande sita vya meno ya tembo vya USD 15,000 ambazo ni sawa na shilingi 32,565,000.

MAMA JANETH MAGUFULI ATOA FUTARI KWA AJILI YA FAMILIA ZENYE UHITAJI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Janeth Magufuli, amewasihi Waislamu nchini kuendelea kuliombea Taifa muda wote, hususan katika kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, na kuendeleza mshikamano bila kujali dini ama kabila tabaka zao.

Mama Magufuli ametoa wito huo leo tarehe 22 Mei, 2019 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji.

Vyakula alivyotoa ni tani 5 za mchele, tani 3 za sukari na tende. Hafla hiyoimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu Mruma, Mkurugenzi wa Hijja wa BAKWATA Shekhe Haidary Kambwile na wawakilishi wa vikundi mbali mbali vya wenye uhitaji.

Mama Magufuli pia amemuomba Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema, azikubali funga za Waislamu wote na kuwalipa malipo stahiki wakati wakitekeleza moja ya nguzo muhimu za Dini ya Kiislamu.

“Kipindu cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni kipindi cha toba. Ni kipindi cha kutenda matendo mema na kujizuia na vitendo viovu” amesema Mama Magufuli.

Mama Magufuli amesema licha ya kwamba Tanzania ina watu wa imani za Dini tofauti lakini siku zote wananchi wake wamekuwa wakishirikiana nyakati za dhiki na za raha bila ubaguzi.

Ametoa mfano kuwa licha ya tofauti za kidini zipo baadhi ya familia ambazo Baba Muislamu na Mama ni Mkristo zinaishi kwa amani na kus

hirikiana katika masuala yote ya kifamilia na kwamba sifa hii ni moja nguzo muhimu za umoja wa Watanzania. “Binafsi nakumbuka zamani nikiwa mdogo tulikuwa tunatafuta Mwislamu aje atuchinjie kuku ama mbuzi ama ng’ombe” , alisema na kuongezea: “Ni kutokana na utamaduni huo uliojengeka miongoni mwa Watanzania , leo nimeguswa kutoa sadaka yangu kwa ajili ya ndugu zangu wenye uhitaji…”
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli, akiongea machache wakati wa hafla ya kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli, akimsiliza Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu Muma akitoa shukurani wakati wa kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli, akimkabidhi Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu Muma msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 019
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli, akimkabidhi Mkurugenzi wa Hija wa BAKWATA Shekhe Haidary Kambwile msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli katika picha ya kumbukumbu na Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu Mruma, Mkurugenzi wa Hijja wa BAKWATA Shekhe Haidary Kambwile pamoja na wawakilishi wa vikundi mbali mbali vya wenye uhitaji baada ya hafla ya kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli, akimkabidhi mmoja wa wawakilishi msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images