Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

RAIS DKT MAGUFULI MGENI RASMI MASHINDANO MAALUMU YA 20 YA QUR-AAN TUKUFU AFRIKA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia Bw. Mohamed El Moujabba Diallo wa Senegal baada ya kuzoa Alama 99.88 na kuibuka mshindi wa Kwanza wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu Afrika
yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia Bi. Sumayyah Juma Abdallah wa Tanzania baada ya kupata alama 98.66 na kuibuka mshindi wa tano wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalum ya 20 ya Qur’aan Tukufu Afrika yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia Bw. Idrissa Ousmane wa Niger baada ya kupata Alama 98.67 na kunyakua ushindi wa nne wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalumuya 20 ya Qur’aan Tukufu Afrika yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia Bw. Shamshuddin Hussein Ali wa Zanzibar baada ya kuzoa Alama 98.83 na kuibuka mshindi wa tatu wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalumuya 20 ya Qur’aan Tukufu Afrika
yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya waumini wa Kiislamu na wadau wengine wakati akihitimisha mashindano maalumuya 20 ya Qur’aan Tukufu Afrika yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei
19, 2019.PICHA NA IKULU


RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN ASHIRIKI KATIKA MAZIKO YA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA ZFA MAREHEMU ALI FEREJ TAMIM KATIKA MAKABURI YA MWANAKWEREKWE ZANZIBAR

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka mchanga katika kaburi la Mareheme Ali Ferej, aliyekuwa Mwenyekiti wa ZFA yaliofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar leo 19-5-2019
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Wananchi na Wanamichezo katika maziko ya Marehemu Ali Ferej Tamim , aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Zanzibar(ZFA) yaliofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akitowa mkono wa Pole kwa Watoto wa Mareheme Ali Ferej Tamim, baada ya kumalizika maziko hayo yaliofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapijnduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwafariji na kutowa mkono wa Pole kwa Familia ya Marehemu Ramadhan Abdalla Shaban, alipofika nyumbani kwa Kijiji cha Uzini Wilaya ya Kati Unguja leo 19-5-2019
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwafariji na kutowa mkono wa Pole kwa Wajane wa Marehemu Ramadhan Abdalla Shaban, aliofika Kijiji kwao Uzini leo kutowa mkono wa pole kwa familia

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia dua ikisomwa na Katibu wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga alipofi kutowa mkono wa pole na kuifariji familia ya Marehemu Ramadhan Abdalla Shaban , kijiji kwa Uzini Wilaya ya Kati Unguja leo 19-5-2019.(Picha na Ikulu)

TCRA yaendelea kutoa elimu kwenye minada mbalimbali nchini

$
0
0
Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV Morogoro

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA), imeendelea na kampeni yake ya kutoa elimu kwenye minada lengo likiwa ni kusogeza karibu huduma kwa wananchi hasa katika kipindi hiki cha usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole.

Akizungumza katika mnada wa sabasaba uliopo Manispaa ya Morogoro Mkuu wa kitengo cha kushughulikia masuala ya watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano TCRA Thadayo Ringo amesema kupitia elimu hiyo wananchi wanapata nafasi ya kujua mambo mbali mbali yanayohusu masuala ya mawasiliano.

Aliwataja wadau wengine wanaoshirikiana nao katika kutoa elimu kuwa ni pamoja na makampuni ya simu ambao wamekuwa wakitoa huduma ya kusajili laini kwa kutumia alama za vidole, jeshi la Polisi ambao wamekuwa wakipokea taarifa za uharifu kwa njia ya mtandao na wizi wa simu na makampuni ya visimbusi.

Kwa upandewa wake Afisa usajili wa vitambulisho kutoka Nida mkoani hapa James Malimo alisema kuwa wananchi wengi hawana uelewa kuhusu usajili wa vitambulisho vya Taifa hali ambayo imekuwa ikisababisha malalamiko hasa pale wanapoambiwa kuwa hawajakamilisha nyaraka muhimu za usajili.

Amesema kuwa kumekuwa na malalamiko mengi ambapo wananchi wanadai Nida wamekuwa wakiwasumbua kwa kuwazungusha hata hivyo alifafanua kuwa NIDA haina nia mbaya ya kuwapa usumbufu wananchi bali ni kutaka kupata uhakika wa nyaraka muhimu zinazotakiwa kwenye usajili.

Hata hivyo alisema kuwa wale waliopata namba za vitambulisho vyao wanaweza kupata huduma ya kusajili laini zao za simu kwa kutumia namba hizo wakati wakisubiri vitambulisho.

Naye mkuu wa kitengo cha makosa ya mitandao kutoka jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro Inspekta David Kamugisha alisema kuwa yeyote anayepoteza ama kuibiwa simu iliyo na laini lazima afike kwenye kitengo chake ili aweze kutoa taarifa na baadaye apewa nyaraka muhimu itakayomruhusu kurudishiwa laini yake.

Alisema kuwa mbali na kutoa huduma lakini kitengo hicho kimekuwa kikitoa elimu kwa wananchi ya kuepukana na utapeli unaofanya kwa kutumia mitandao na pia kuepukana na makosa yanayofanywa kwa kutumia mitandao hasa mitandao ya kijamii.

Aidha Mkuu wa Kanda ya mashariki mhandisi Lawi Odiero alisema kuwa lengo ni kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kuhusu maswala yote yanayohuau Mawasiliano pamoja na muhumu wa usajili wa line za simu kwa kutumia alama za vidole.

Aliwashauri wananchi kuendelea kujiitokeza ili waweze kusajili line zao kwa kutumia alama za vidole na kwamba ni fulsa kwao.
 Wananchi wakiwa katika foleni kwa ajili ya kusajili ili kuweza vitambulisho vya Taifa na kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero akitoa akizungumza na waandishi Habari katika Mnada mkoani Morogoro kuhusiana na usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole.
 Mwananchi akitia saini ya kidole kwa ajili ya kupata kitambulusho cha Taifa kinachotolewa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika Mnada ulioandaliwa na TCRA  kwa kushirikiana na wadau hao ili kuwa na vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole katika Mnada uliofanyika mkoani Morogoro.
 Mkuu wa Kitengo cha Kushughulikia Masuala ya Huduma za Bidhaa za Mawasiliano wa TCRA Thadayo Ringo akizungumza na waandishi wa habari katika Mnada mkoani Morogoro namna wanavyotoa elimu ya Mawasiliano kwa kutumia minada hiyo.
 Afisa wa TCRA Kanda ya Mashariki Vaoleth Iseko akimpa mteja maelezo namna ya kusajili  laini za simu kwa kutumia alama za vidole katika Mnada uliofanyika mkoani Morogoro.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero akihakikisha usajili wake kwa Mtoa huduma wa Kampuni ya Airtel katika Mnada uliofanyika mkoani Morogoro.
 Afisa Usajili wa Vitambulisho vya Taifa NIDA Mkoa wa Morogoro James Malimo akitoa elimu ya usajili wa Vitambulisho katika Mnada uliofanyika mkoani Morogoro.

Stanbic Bank Tanzania conducted a pension fund workshop to its customers in Dodoma

$
0
0
Stanbic Bank Head of Trading, Eric Chijoriga, speaking to the bank's customers during a Pensions Fund workshop held in Dodoma recently. Graced by the regulators from BoT and Social Security Regulatory Authority (SSRA), the workshop provided the customers with an understanding of Debt Market, Transactional banking with a focus on Custody Services and an opportunity to network and exchange ideas with industry peers and experts. 
Stanbic Bank Head Investor Services, Andrew Mgunda speaking to the bank's customers during a Pensions Fund workshop held in Dodoma recently. Graced by the regulators from BoT and Social Security Regulatory Authority (SSRA), the workshop provided the customers with an understanding of Debt Market, Transactional banking with a focus on Custody Services and an opportunity to network and exchange ideas with industry peers and experts.

BARAZA LA HABARI TANZANIA LATAJA MITANDAO YA HABARI INAYOONGOZA KUATHIRIKA WAKATI WA UCHAKATAJI HABARI

$
0
0
Baraza la Habari Tanzania (MCT), limetaja mitandao ya habari inayoongoza kupata madhila/kuathirika/kuathiriwa zaidi wakati wa utafutaji, uandaaji na uchapishaji wa habari kuwa ni Print Media ikifuatiwa na Televisheni.

Hayo yameelezwa mwishono mwa wiki na Programu Ofisa wa Baraza la Habari(MCT), Humphrey Mtuy, katika mkutano wa Baraza hilo uliofanyika Mjini Morogoro na kukutanisha wadau wa habari, wanasheria na Mabalozi wa ukiukwaji wa uhuru wa habari.

Alisema, print media inaongoza kwa kuathiriwa zaidi na madhila hayo ya ukiukwaji wa uhuru wa habari ikifuatiwa na Television, Redio na Tv Online.

Aidha, aisema Tv online ni mtandao wa kijamii mkubwa ambao upo kwenye hatari ya kuathirika au kuathirika kwa wakati ujao.

Kutokana na hali hiyo, Mtuy amewataka waandishi na wadau wa habari kuwa makini zaidi wakati wa utendaji kazi ikiwa na kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na misingi ya kihabari wakati wa utendaji kazi.
Wa kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mkajanga, akisikiliza mkutano wa wadau na mabalozi wa ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanyika Mjini Morogoro, lengo likiwa ni kujenga na kupeana uzoefu kuhusu madhila kwa wanahabari.

VIONGOZI MBALIMBALI WA DINI WAHITIMU MAFUNZO YA UDEREVA KUDHIBITI AJALI

$
0
0
Baadhi ya Viongozi Wa Dini Mkoani Arusha Wahitimu Mafunzo Ya Usalama Barabarani


Na Vero Ignatus,Arusha.

Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa dini kutoka katika baadhi ya makanisa Mkoani Arusha wamehitimu mafunzo ya udereva lengo likiwa ni kudhibiti ajali zinazosababisha vifo na majeruhi,ambapo yametolewa na Chuo cha Wide Institute of Driving.

Faustine Matina ni Mkufunzi wa Chuo hicho amesema kuwa mafunzo hayo ya Usalama barabarabi yamefanyika kwa umakini mkumbwa kwa viongozi hao ili waweze kuwa mabalozi wa masuala ya usalama barabarani na kuokoa maisha ya watu.

Viongozi hao wa dini wamehitimu mafunzo hayo na kupatiwa vyeti hivyo kukidhi matakwa ya serikali ya kuwataka madereva kuwa na vyeti vya shule ya udereva pamoja na leseni kama vigezo muhimu kwa madereva.

Joseph Bukombe ni Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha ambapo amewataka viongozi hao wa dini kuhubiri masuala ya usalama barabarani katika makanisa yao ili kuokoa maisha ya waumini wao ambao wengi ni madereva.

“Nawaomba msikae kimya mkazungumze huko makanisani badala ya kusema nendeni kwa amani muwaambie kuwa wasisahau kufunga mkanda wanapokua kwenye magari yao kwa kufanya hivyo tutaokoa maisha yao” Alisema Bukombe.

Aidha Bukombe amewataka pia Wanasiasa kuwaambia ukweli madereva bodaboda kutii sheria za usalama barabarani badala ya kuwatetea bila kuwaambia ukweli kwani ajali nyingi zinazotokea mkoa wa Arusha zinasababishwa na bodaboda.

Namsemba Mwakatobe ni muwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ambaye ni Mrakibu wa polisi Makao Makuu ya polisi Arusha amesema kuwa jeshi la polisi litashirikiana na viongozi wa dini katika kutatua changamoto za usalama barabarani sambamba na kutoa elimu kwa wananchi.

Askofu Stanley Hotay ni Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa Mkoani Arusha amekiri kuwa mafunzo hayo yatawasaidia Viongozi hao kuwa na uelewa mkubwa na kujifunza vitu vingi ambavyo walikua hawavijui kuhusu usalama barabarani.

TIRA yazindua kanuni za bima kupitia benki

$
0
0
Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zimezindua Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki (Bancassurance regulations).

Akizindua rasmi kanuni hizo Jijini Dar es Salaam, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Yamungu Kayandabila amezitaka taasisi za fedha na benki nchini kuzizingatia katika utoaji wa huduma zao ili kuongeza ufanisi wa shughuli zao.

Alisema kanuni hizo zitasaidia kusambaza huduma ya bima nchini kwani watu wengi bado hawajafikiwa.

“Ujio wa Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki nchini Tanzania umechelewa kidogo hivyo wadau wana kila sababu ya kuzingatia kwa manufaa ya pande zote watoa huduma na wanufaika,” alisema

Alisema endapo wadau watazizingatia kanuni hizo mapato katika sekta hiyo kiujumla yataongezeka kwa taifa, watoa huduma na watu wengi zaidi watafikiwa na huduma za bima. 
Aidha kwa upande wake 

akizungumza katika hafla hiyo alisema licha ya manufaa lukuki ya uzinduzi wa kanuni hizo pia unalenga kueneleza ajenda ya TIRA ya kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za bima nchini yaani bima kwa wote.

"Tunahitaji kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za Bima (access) nchini kwa kuongeza aina mbalimbali za bima kwa mahitaji mbalimbali, mfano mbadala wa uuzaji na usambazaji wa huduma za bima ikiwemo kutumia benki,” alisema

Kamishna huyo aliongeza kuwa inahitajika teknolojia rahisi na rafiki kwa ajili ya kusambaza bima, kununua bima, kuuza bima, kulipa mafao/madai ya bima, kusikiliza maoni na mahitaji ya wananchi, kuchakata na kuandikisha maombi ya bima," alisema Dk. Saqware.

Aliongeza kuwa kuanzishwa kwa kanuni hizo ni muhimu katika kuendeleza sekta ya kifedha nchini na kusisitiza kuwa pato la taifa, hasa ukizingatia faida nyingi ambazo zitapatikana kwa benki zenyewe na watumiaji wa huduma za bima.

 Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali serekalini, makampuni ya bima, taasisi za kifedha, mawakala mbalimbali na wadau wa sekta ya bima na kudhaminiwa na BoT, Reliance Insurance, Heritage Insurance, Zanzibar Insurance, Chama Cha Watoa Huduma za Bima (ATI), NMB, CRDB Insurance, Metropolitan Life Tanzania, Jubilee Insurance, FSDT, Stanbic Bank, Smart Policy, Alliance Insurance, TPB Bank na Shirika la Bima la Taifa (NIC).

 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dr Yamungu Kayandabila akizidua rasmi Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki (Bancassurance regulations) Jijini Dar es Salaam huku wageni wengine wakishuhudia.Uzinduzi huo uliandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT). 
 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dr Yamungu Kayandabila akizungumza wakati wa uziduzi wa rasmi Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki (Bancassurance regulations) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Kamishna wa TIRA, Dk. Baghayo Saqware akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki (Bancassurance regulations) uliofanyika jijini Dar es Salaam

Baadhi ya wadau waalikwa wakifuatilia uzinduzi huo.

RAIS DKT. MAGUFULI MGENI RASMI KWENYE MASHINDANO MAALUMU YA 20 YA QUR-AAN AFRIKA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM JUMAPILI MEI 19, 2019

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kaongozana na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry bin Ally akiwasili kuwa mgeni rasmi kwenye mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kwenye mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Raisi wa Taasisi ya Al Hikma Foundation Sheikh Shariff Abdulqadir (kushoto) na Waziri wa TAMISEMI wa Saudi Arabia Sheikh Dkt. Swaleh al Sheikh mara alipowasili kuwa mgeni rasmi kwenye mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kwenye mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Mohamed Ghalib Bilali mara baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kwenye mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu wa viongozi wengine wakati wa mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry bin Ally  wakati wa mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
 Sehemu ya maelfu ya waumini waliohudhuria kwenye mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
 Sehemu ya wadau wakati wa mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Maelfu ya waumini waliohudhuria kwenye mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akwa meza kuu na  Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa,  Rais MStaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Raisi wa Taasisi ya Al Hikma Foundation (kushoto kwake) na Waziri wa TAMISEMI wa Saudi Arabia Sheikh Dkt. Swaleh al Sheikh (wa tatu kulia) akifuatilia  mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Rais wa Taasisi ya Al Hikma Foundation (kushoto)wakati wa mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  na meza kuu wakimsikiliza  Sheikh Nurdeen Kishk, Mratibu Mkuu wa mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
 Sehemu ya Wafadhili wakuu wa Mshindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Taasisi ya Al Hikma Foundation Sheikh Shariff Abdulqadir akihutubuia kwenye mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Wafadhili wakuu wa wakitambulishwa baada ya kufanikisha mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akihutubia maelfu ya waumini wa Kiislamu na wadau wengine wakati akihitimisha mashindano maalumuya 2o ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akihutubia maelfu ya waumini wa Kiislamu na wadau wengine wakati akihitimisha mashindano maalumuya 2o ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akihutubia maelfu ya waumini wa Kiislamu na wadau wengine wakati akihitimisha mashindano maalumuya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akifuatilia mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akifuatilia mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akihutubia maelfu ya waumini wa Kiislamu na wadau wengine wakati akihitimisha mashindano maalumuya 2o ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akihutubia maelfu ya waumini wa Kiislamu na wadau wengine wakati akihitimisha mashindano maalumuya 2o ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akihutubia maelfu ya waumini wa Kiislamu na wadau wengine wakati akihitimisha mashindano maalumuya 2o ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akihutubia maelfu ya waumini wa Kiislamu na wadau wengine wakati akihitimisha mashindano maalumuya 2o ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akielekea sehemu ya kutolea zawadi  baada ya mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akipungia maelfu ya waumini wa Kiislamu na wadau wengine baada ya mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiislamu ya Amana Dr. Muhsin Salim Masoud ambapo Benki hiyo ndiyo ilikuwa wadhamini wakuu wa mashindano maalumuya 2o ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia Mwakilizshi wa Kituo cha Televisheni cha ZBC Bw. Mehbooud Al Haddad kwa kuwa mmoja wa wadhamini  mashindano maalumuya 2o ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi kwa kuwa mlezi wa mashindano hayo ya Qur’aan Tukufu Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa kwa kuwa mdau mkubwa wa mashindano hayo ya Qur’aan Tukufu Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry bin Ally  wakati wa mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia Bi. Sumayyah Juma Abdallah wa Tanzania baada ya kupata alama 98.66 na kuibuka mshindi wa tano wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalum ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa baada ya kumzawadia Bi. Sumayyah Juma Abdallah wa Tanzania alitepata  alama 98.66 na kuibuka mshindi wa tano wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalum ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia Bw. Idrissa Ousmane wa Niger   baada ya kupata Alama 98.67 na kunyakua ushindi wa nne wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalumuya 2o ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia Bw. Shamshuddin Hussein Ali wa Zanzibar baada ya kuzoa Alama  98.83 na kuibuka mshindi wa tatu wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalumuya 2o ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia Bw. Faruq Kabiru Yakubu wa Nigeria  baada ya kuzoa Alama  98.91 na kuibuka mshindi wa Pili wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalumuya 2o ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaidiana na    Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiislamu ya Amana Dr. Muhsin Salim Masoud  (kulia) akimzawadia Bw. Mohamed El Moujabba Diallo wa Senegal  (wa pili kushoto) zawadi ya shilingi milioni 20 baada ya kuzoa Alama  99.88 na kuibuka mshindi wa Kwanza wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalumuya 2o ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpatia pesa taslimu shilingi milioni moja Bi Sumayyah Juma Abdallah wa Tanzania ikiwa ni zawadi kutoka kwa Rais Dkt. Magufuli baada ya kupata alama 98.66 na kuibuka mshindi wa tano wa Washindi wa Kuhifadhi Juzuu 30 katika mashindano maalum ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwa na viongozi wengine wakiwa katika dua baada ya mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwa na viongozi wengine pamoja na washiriki pamoja na wajumbe wa kamati kuu ya maandalizi ya mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwa na viongozi wengine pamoja na kamati kuu ya maandalizi ya mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiagana na Sheikh Nurdeen Kishk, Mratibu Mkuu wa mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiaga maelfu ya waumini wa Kiislamu na wadau wengine baada ya mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiaga maelfu ya waumini wa Kiislamu na wadau wengine baada ya mashindano maalumu ya 20 ya Qur’aan Tukufu yaliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Jumapili Mei 19, 2019. 
PICHA ZOTE NA IKULU

WACHIMBAJI WA MADINI WILAYA YA TUNDURU WACHUNGUZWA UGONJWA WA KIFUA KIKUU

$
0
0
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Majimaji wilaya ya Tunduru waliojitokeza kwa ajili ya uchunguzi wa vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu wakati wa kampeni ya uchunguzi wa ugonjwa huo kwenye vijiji vinavyozungukwa na machimbo ya madini na maeneo ya machimbo iliyoendeshwa na Shirika lisilo la Serikali ya MDH kwa kushirikiana na Hospitali ya wilaya ya Tunduru.
Baadhi ya watoto wa kijiji cha Majimaji wakiwa katika mstari wakisubiri kufanyiwa uchunguzi wa vimelea vya ugonjwa wa Tb wakati wa zoezi la uchunguzi wa ugonjwa huo kwa vijiji na maeneo yanayzungukwa na machimbo ya madini wilayani Tunduru chini ya usimamizi wa Shirika la MDH kwa kushirikiana na Hospitali ya wilaya ya Tunduru.

Na Mwandishi wetu, Tunduru

SHIRIKA lisilo la Kiserikali la MDH kwa kushirikiana na Hospitali ya wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma limeanza Kampeni ya kupima  ugonjwa wa kifua kikuu kwa wananchi wa vijiji vinavyozungukwa na machimbo kama hatua  ya kumaliza  ugonjwa huo. Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma inatajwa kuwa miongoni mwa wilaya ambazo zimeathirika kwa kiwango kikubwa na ugonjwa huo hapa Nchini.

Kampeni hiyo iliwahusu wananchi wa vijiji vya Majimaji,Muhesi na Magomeni ambapo watu wanaojihusisha na uchimbaji wa madini wanatajwa kuwa kundi mojawapo  ambalo  limeathirika sana na ugonjwa wa kifua kikuu.

Kampeni hiyo inafanywa na Shirika linalojihusisha na uborehaji wa Huduma za Afya(MDH)  kwa kushirikiana na Hospitali ya wilaya ya Tunduru  chini ya kitengo cha Kifua kikuu na Ukoma  na inalenga kuwafikia   watu wote wanaoishi katika  maeneo ya machimbo  na vijiji  vyote vinavyozungukwa na shughuli za uchimbaji.

  Afisa mradi wa Uibuaji wa wagonjwa wa Kifua Kikuu katika Jamii kutoka Shirika la MDH mkoa wa Ruvuma  Dkt Nixson John alisema,zoezi la uchunguzi wa Wagonjwa wachimbaji  wa Madini pamoja na vijiji vinavyozunguka maeneo hayo linafanyika katika wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma.

Kwa mujibu wa Dkt Nixson zoezi hilo lilianza  tarehe 12 hadi 17 Mwezi Mei  ambapo katika  wilaya ya Tunduru uchunguzi ulifanyika  kwenye machimbo ya wachimbaji wadogo katika kata ya Muhesi na Majimaji ambapo idadi ya wahisiwa wa ugonjwa  wa kifua kikuu 202 ,na  sampuli 200 za makohozi zilikusanywa.

Alisema, mpaka sasa watu waliogundulika na maambukizi ya vimelea vya kifua kikuu ni 9 kati ya sampuli zilizokwishapimwa  kati yao  mtoto mmoja yeye alianzishiwa dawa kutokana na kukidhi vigezo na mtu mzima mmoja nae alianzishiwa kwa kuwa na dalili za kifua kikuu nje ya  mapafu na zoezi la upimaji wa sampuli  bado unaendelea.

Dkt Nixson alisema, wataalam walioshiriki katika kazi hiyo ni kutoka Hospitali ya wilaya ya Tunduru wakiongozwa na Mratibu wa Kifua kikuu na Ukoma Dkt Mkasange Kihongole ambapo shirika la MDH ni watekelezaji wa Mradi chini ya ufadhili wa  mfuko wa Dunia wa  Mapambano ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu,Malaria na Ukimwi(Global Fund).

Kwa upande wake Mratibu wa Kifua kikuu na Ukoma wa Hospitali ya wilaya ya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole alisema, watu wanaoishi katika vijiji  vinazungukwa na machimbo na wale wanaoishi katika maeneo ya machimbo wako katika hatari zaidi kupata ugonjwa.

Alisema, hali hiyo inatokana  na muingiliano wa mara kwa mara  na mkusanyiko mkubwa wa watu kutoka katika maeneo mbalimbali ambao baadhi tayari wamepata maradhi ya Kifua kikuu  hivyo ni rahisi  wale waliopata ugonjwa huo kuambukiza Watu wengine.

Dkt Kihongole alisema, kampeni  ya uchunguzi wa vimelea vya ugonjwa huo   katika wilaya ya Tunduru imefanyika katika vijiji vitatu vya Muhesa,Majimaji na Magomeni ambapo jumla ya sampuli zilizochukuliwa kwa ajili ya  kufanyiwa  uchunguzi  ni  200 na mpaka sasa zilizopimwa na kupata majibu ni wagonjwa 9 na zoezi la upimaji bado linaendelea.

Alisema, ugonjwa wa kifua kikuu ni miongoni mwa magonjwa kumi Duniani ambayo yanaongoza kwa kuuwa watu,ndiyo maana kwa kutambua ukubwa wa tatizo  Serikali kwa kushirikiana na mfadhili Shirika la MDH limeanza  uchunguzi na upimaji kwa wananchi kwa kuwafuata vijijini kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa vimelea vya TB badala ya kuwasubiri ofisini.

Alisema,  kimsingi  hatua  hiyo itasaidia  kuwafikia watu wengi na hivyo kuokoa maisha na kusisitiza kuwa,ugonjwa wa TB unatibika na kuwataka wananchi kuwa na mazoea ya kufanya uchunguzi wa Afya zao mara kwa mara.

Kihongole  alibainisha kuwa, ugonjwa huo huambukiza sehemu mbalimbali za mwili wa Binadamu kama vile Uti wa mgongo,Tumbo,Figo,Utumbo,mifupa,Ubongo,Macho na Ngozi ambapo mtu mmoja mwenye kifua kikuu anaweza kuambikiza mpaka watu wengine 15.

Alisema, vimelea vya kifua kikuu huishi katika sehemu za giza na zisizo ingiza Hewa vizuri,mfano Nyumba yenye msongamano na isio na madirisha,Darasa lenye madirisha machache n ahata kwenye gari ambalo halina hewa ya kutosha.

Alisema, kwa watoto wadogo  dalili mojawapo ya kifua kikuu ni kikohozi kwa wiki mbili au zaidi,Homa za mara kwa mara,kupungua uzito/kutoongezeka uzito,  zaidi ya siku tatu,kutokwa na jasho.

Mmoja wa watoa huduma ngazi ya jamii  anayeishi katika kijiji cha Majimaji kata ya Majimaji Ismail Sitambuli alisema, kampeni hiyo itawasaidia wananchi wengi wanaoishi na kifua kikuu bila kujitambua kujielewa na kuanza matibabu haraka.

Alisema, katika mpango huo Wananchi pia wataokoa rasilimali fedha na muda wanaoutumia kutembea umbali mrefuhadi Hospitali kufuata huduma.

Hata hivyo ameiomba Serikali kuwa,huduma ya uchunguzi wa vimelea vya Kifua kikuu n ahata magonjwa mengine ni vema iwe endelevu kwa sababi itasaidia kwa kiwango kikubwa kuokoa maisha ya Watanzania hasa wale wanaoishi maeneo ya vijiji na machimbo ya madini ambao wanakabliwa na tatizo kubwa la kufikiwa kwa Huduma za Afya.

MASELE AFIKA MBELE YA KAMATI YA BUNGE YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE JIJINI DODOMA LEO

$
0
0
Mbunge wa Shinyanga Mjini, Mhe. Stephen Masele akielekea mbele ya kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazomkabili za utovu wa nidhamu tukio lililofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

Mbunge wa Shinyanga Mjini, Mhe. Stephen Masele akifika mbele ya kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazomkabili za utovu wa nidhamu kabla ya kikao kilichofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Mhe. Emmanuel Mwakasaka akiongoza kikao cha utovu wa nidhamu.
Mbunge wa Shinyanga Mjini, Mhe. Stephen Masele akihojiwa mbele ya kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa tuhuma za utovu wa nidhamu katika kikao kilichofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge wakiwa kwenye kikao cha tuhuma za utovu wa nidhamu dhidi ya Mbunge wa Shinyanga Mjini, Mhe. Stephen Masele kilichofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Sevilla FC kutua Dar kesho

$
0
0
VINARA wa soka katika michuano ya Ligi Kuu ya Hispania, LaLiga, timu ya Sevilla FC inatarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya  Simba ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya  kwa timu hiyo kucheza nchini  Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jijini  Dar es Salaam, timu hiyo inatarajiwa kuwasili kesho jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius  Nyerere.

Kulingana na taarifa hiyo mechi hiyo itakuwa ni maalum kwa vinara hao wa 'LaLiga ambao wanadhaminiwa na  SportPesa' na akaongeza  kwamba ziara itahusisha matukio kadhaa ya   jamii na michezo ikiwemo kliniki namafunzo mbalimbali.

 "Kama ushindani wa kimataifa unakutana na dhamira ya LaLiga kuwa karibu na mashabiki wake. Kwa kweli kwamba mashabiki wetu wa Tanzania wataweza kupata furasa ya  kuangalia karibu  klabu kubwa kama Sevilla FC inamaanisha kuwa ni fursa kubwa kwa kila mtu," alisema Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kimataifa katika Ligi ya La Liga, Oscar Mayo.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Tarimba Abbas, kampuni yao  imeshirikiana na baadhi ya taasisi za soka za kubwa  ulimwenguni  baada ya kuna kuna haja ya  kuleta uzoefu  huu mkubwa  kwa Tanzania.

 "Ili kufurahia kuona moja ya klabu  kubwa za  mpira wa miguu  Ulaya, Sevilla FC. Kwa makubaliano yetu na LaLiga ambayo ni ligi bora duniani, tutaweza kuonyesha vipaji vyetu  na kuboresha kiwango cha soka  nchini ", alisema Talimba.

 Alisema kwamba mechi hiyo ni sehemu ya mradi wa 'LaLiga duniani  ambao unalenga kueneza soka  la  Hispania kimataifa na  kueneza pia sera ya 'Marca España', kuleta karibu mashabiki wa  LaLiga na  kukuza klabu nje ya nchi yetu.

Hii itakuwa ni klabu ya pili Ulaya kufanya ziara Afrika Mashariki, baada ya mwaka 2017 Everton FC kucheza  na  Gor Mahia  nchini  Kenya, ingawa  sio mara ya lkwanza kwa  Sevilla kutua katika bara hili kwani  mwaka  2015  ilikuwa nchinbi  Morocco ambao ilicheza mechi ya kuajindaa na  LaLiga dhidi ya timu ya   Hassania Union Sport d'Agadir.

IGP SIRRO ASJILI LAINI YAKE YA AIRTEL KWA ALAMA ZA VIDOLE

$
0
0
 Wafanyakazi wa Airtel wakimuhudumia Inspecta Jenerali wa Polisi (IGP) Saimon Sirro ili kuhakiki usajili wa laini yake ya Airtel kwa kutumia Alama za vidole leo katika Makao makuu ya polisi  jijini Dar es salaam ambapo Airtel inaendelea na zoezi la usajili na uhakiki wa laini za simu kwa kutumia Alama za vidole kama ilivyoagizwa na mamlaka ya mawasiliano TCRA kuwa hadi kufikia Dec 2019 laini zisizohakikiwa kwa mfumo wa alama za vidole (Biometria) zitafungwa.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA WAZIRI WA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA NA MAENDELEO WA SWEDEN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Peter Erikkson, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Sweden alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 20, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Peter Erikkson, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Sweden alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 20, 2019. Kushoto ni Balozi wa Sweden nchini Tanzania Andres Sjoberg.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimzawadia picha ya kuchorwa Peter Erikkson, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Sweden alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 20, 2019. Kushoto ni Balozi wa Sweden nchini Tanzania Andres Sjoberg.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kaatika picha ya pamoja na Peter Erikkson, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Sweden na ujumbe wake pamoja na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wa baada ya kukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 20, 2019. Kushoto ni Balozi wa Sweden nchini Tanzania Andres Sjoberg. PICHA NA IKULU

Rais Magufuli akutana na Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo( IFAD) Ikulu jijini Dar es Salaam

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Gilbert Houngbo, Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (International Fund for Agriculture Development - IFAD - ) , alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 20, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Gilbert Houngbo, Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (International Fund for Agriculture Development - IFAD - ) , alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 20, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Gilbert Houngbo, Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (International Fund for Agriculture Development - IFAD - ) , alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 20, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Gilbert Houngbo, Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (International Fund for Agriculture Development - IFAD - ) , na ujumbe wake pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na maafisa wa serikali baada ya kukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 20, 2019.

Shabiki wa Real Madrid ashinda Sh 208.5 milioni za M-Bet

$
0
0
Shabiki wa Real Madrid ashinda Sh 208.5 milioni za M-Bet

Dar es Salaam. Mkazi wa Ifakara, mkoani Morogoro, Gadi Mwajeka (37) ambaye pia shabiki wa timu ya Real Madrid ameshinda kiasi cha Sh 208, 574, 790 baada ya kubashiri kwa usahihi mchezo wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi, Mwajeka alisema kuwa hakuamini mara baada ya kupigiwa simu kuambiwa kushinda kiasi kikubwa cha fedha.

Mwajeka ambaye ni mfanya biashara ya rangi za mkeka Ifakara mjini alisema kuwa ushindi huo ni faraja kubwa sana kwake kwani utamwezesha kuipanua biashara yake na kuanzisha nyingine.

“Sikuamini kama nimeshinda kiasi kikubwa cha fedha, nimetumia kiasi cha sh1,000 tu kubashiriki na kuingia kiasi kikubwa cha fedha. Nimefarijika sana,” alisema Mwajeka.

Alisema kuwa ameshiriki kubashiri muda mrefu mpaka kushinda kiasi kikubwa cha fedha. Alisema kuwa amecheza kwa miaka mitatu kucheza na hakukata tamaa.

“Mke wangu ni nesi, nilikuwa nachukua madaftari yake kuandika timu na kuanza kuzipigia mahesabu. Nitatumia fedha hizi kwa ushauri wa wazazi wangu kuona ninafanya biashara gani,” alisema.

Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi kuwa Mwajeka ni mshindi wa tano tokea kuanza mwaka huu kushinda zawadi nono.

Mushi alisema kuwa M-Bet itaendelea kuwa nyumba ya mabingwa na kuwaomba mashabiki wa soka kubashiri na kampuni yao ili kuweza kubadili maisha.

“M-Bet ni nyumba za mabingwa na mabingwa wote wanapatikana kupitia michezo ya kubahatisha ya kampuni yetu na kujitajirisha vile vile vile kuichangia nchi yao kwani asilimia 20 ya fedha ukatwa kama kodi ya kusaidia maendeleo ya nchi katika sekta mbalimbali,” alisema Mushi.

Naye, Shabani Mwanga, Mkuu wa Kitengo cha Kodi za Michezo ya Kubahatisha (TRA), mkoa wa kodi wa Ilala alimpongeza Mwajeka kwa ushindi na pia kuipongeza kampuni ya M-Bet kwa kuwa walipa kodi wazuri kwa serikali.
Meneja Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (Kulia) akimkabidhi mfano wa hundi mshindi wa droo ya Perfect 12, Gadi Mwajeka(Katikati) kutoka Ifakara, mkoani Morogoro aliyejishindia Sh 208.5 milioni baada ya kubashiri matokeo ya mechi 12 kwa usahihi. Kushoto ni Shabani Mwanga, Mkuu wa Kitengo cha Kodi za Michezo ya Kubahatisha (TRA), mkoa wa kodi wa Ilala.

Upanuzi Chuo cha Ualimu Patandi Kupunguza Changamoto ya Walimu wa Elimu Maalum

$
0
0
Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

Serikali imekamilisha upanuzi wa Chuo cha Ualimu Patandi ili kukiongezea uwezo wa kudahili walimu wenye taaluma ya elimu maalum wanaohitajika nchini ili kupunguza changamoto ya walimu hao.

Hayo yameelezwa leo Bungeni, Jijini Dodoma na Mhandisi Stella Manyanya alipokuwa akijibu swali la Mhe. Grace Victor Tendega Mbunge wa Viti Maalum kwa niaba ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako juu ya mpango wa Serikali katika kuhakikisha walimu wenye weledi wa watu wenye ulemavu wanatosheleza nchini.

"Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali katika kukabiliana na changamoto ya upungufu wa walimu wenye Taaluma ya Elimu Maalum. Changamoto hii inasababishwa na ongezeko la uandikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu kutokana na mabadiliko chanya ya kimtazamo na uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa elimu kwa watu wenye ulemavu," amesema Mhandisi Manyanya.

Ameendelea kusema, mahitaji ya walimu wa elimu maalum nchini ni walimu 8,882 katika shule maalum na vitengo vinavyopokea wanafunzi wenye mahitaji maalum 706, ambapo hadi kufikia Disemba 2018 walimu 5,556 wenye Taaluma ya Elimu Maalum ngazi ya Astashahasa, Stashahada na Shahada walihitimu katika vyuo mbalimbali nchini vikiwemo Chuo cha Ualimu Patandi na Chuo Kikuu Dodoma.

Aidha amesema, hatua ya Serikali ya kuanzisha kozi ya elimu maalum katika ngazi ya Astashahada Chuo cha Ualimu Patandi kwa walimu tarajali kwa mwaka wa masomo 2018/19 itaongeza idadi wa walimu wanaojiunga na mafunzo ya Ualimu wa Elimu Maalum ili kupunguza changamoto ya walimu wenye elimu hiyo wanaohitajika nchini.

BENDI YA MSONDO NGOMA ILIKOTOKA

$
0
0
 Na Moshy Kiyungi, Dar es Salaam

Yawezekana baadhi ya watu wameshau kwamba kabla na baada ya Uhuru wa Tanganyika zilikuwepo bendi nyingi humu nchini zilizokuwa zikitoa burudani katika sherehe mbalimbali.

Lakini mara baada ya kupatikana kwa Uhuru, kuliundwa bendi iliyopewa jina la NUTA Jazz ambayo kwa sasa ndiyo iliyo kongwe miongoni mwa bendi zilizopo hapa nchini.

Mwaka huu ni miaka 55 tangu ianzishwe mwaka 1964 katika jiji la Dar es Salaam, ikiwa chini ya ummiliki wa Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania (National Union of Tanzania) kwa kifupi NUTA.

Mwaka huohuo wa 1964 Muhidini Gurumo aliitwa kujiunga na bendi hiyo ya NUTA Jazz akitokea katika bendi ya Rufiji Jazz, na kuwa mmoja wa waasisi wa bendi hiyo.

Gurumo aliungana na wanamuziki wengine akina Hamis Sama, Mnenge Ramadhani na Wilfred Boniface. Nyimbo zake za kwanza kurekodi akiwa na NUTA Jazz zilikuwa Baba Nyerere wimbo uliokuwa ukimsifia Mwalimu Nyerere kwa kuleta Uhuru wa Tanganyika. Nyingine zilikuwa Kilimo ni kazi yetu na Mwengele.

Mwaka 1966 mwanamuziki mwingine mahiri John Simon alijiunga na bendi hiyo ya NUTA Jazz. Mpiga gitaa la solo Amed Omar ndiye liyechaguliwa kuwa kiongozi wa bendi pia ndiye aliyetamba mno katika wimbo wa Mwangele.

Jumuiya hiyo ilipobadili majina kuwa ‘Organization of Tanzania Trade Unions’ kwa kifupi OTTU, bendi nayo ikawa OTTU Jazz. Baada ya kipindi kingine kupita Jumuiya hiyo ikabadili majina kuwa Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania, kwa kifupi JUWATA.

Wakati wa uhai wake marehemu Gurumo aliwahi kusema kuwa mpiga solo Ahmed Omar kuwa ndiye aliyechagualiwa kuwa kiongozi wa NUTA Jazz wakati huo. Mzee Gurumo ambaye ndiye aliye asisi mtindo wa Msondo, ukiwa ni wa asili ya kabila la Kizaramo, aliweza kutamba katika nyimbo.

Baadhi ya nyimbo zilizorekodiwa wakati huo zilikuwa za ‘Baba Nyerere’ , uliokuwa ukimsifia Mwalimu Nyerere kuleta Uhuru wa Tanganyika. Nyingine ni ‘Kilimo ni Kazi yetu’ , ‘Mwengele’ , Mpenzi Sofia, Tumeishi toka zamani, na Walinicheka. Zingine zilikuwa Aziza, Tukiwa na Monica shuleni, Sakina, Maneno ya Nyerere, Mipacha Ngui na nyingine nyingi. Wakati huo huo mpiga Solo Saidi Mabera alichaguliwa kuwa kiongozi wa bendi hiyo.

Baadhi ya wanamuziki waliounda Juwata Jazz ni pamoja waimbaji Muhidini Gurumo, Wengine ni Hassan Rehani Bichuka, na mpiga Kinanda Waziri Alli ambaye hivi sasa ni mmoja kati ya viongozi wa bendi ya The Kilimanjaro Band (Wana Njenje).

Waziri kabla ya kujiunga katika bendi hiyo, alikuwa katika bendi ya taarabu ya Lucky Star ya mjini Tanga. Alifika katika jiji la Dar es Salaam akiwa na nia ya kwenda nchini Marekani kujifunza muziki. Juhudi zake hazikufanikiwa akapelekwa na nduguze kwenda kujiunga katika bendi hiyo. Alipotuwa alikabidhiwa kupiga Kinanda.

Miaka hiyo ya 1980 hadi 1990, takribani kila bendi ilikuwa na wapiga vinanda. Ikumbukwe katika bendi ya Maquis du Zaire, alikuwa akibofya Mbuya Makonga ‘Adios’, alikuwepo mwanamama pekee Asia Darwesh aliyekuwa akikipapasa kinanda hususani katika bendi ya MK Group, iliyokuwa ikiga muziki wake katika ukumbi wa Bandari Grill, kwenye hotel ya New Africa, ya jijini Dar es Salaam.

Vijana Jazz walikuwa na Hassan Shaw, ambaye hivi sasa yupo Ughaibuni akipiga muziki katika kumbi mbalimbali za Kitalii. Bima Lee Orchestra walikuwa na Kassimu Magati wakati Abdul Salvador ‘Father Kidevu’ alikuwa akipata ‘ulaji’ ala hiyo.

Ushindani kati ya bendi za muziki wa dansi ulipoongezeka, wanamuziki mwaka 1978 wanamuziki Muhidini Gurumo na Hassan Reheni Bichuka walihamia bendi ya Mlimani Park Orchestra.

Gurumo alipofika katika bendi hiyo akawa kiongozi wa bendi sanjari na kuasisi mtindo wa ‘Sikinde ngoma ya ukae’. Mtindo huo ambao aliwahi kuelezea ni wa asili ya ngoma za kabila lake la Kizaramo. Baada ya muda mfupi Hassani Bichuka naye aliindoka bendi hiyo Juwata kwenda kuungana na Gurumo katika bendi ya Mlimani Park Orchestra.

Baada ya Bichuka kupondoka, uongozi ukamchukuwa mwimbaji aliyekuwa akishabihiana naye kwa sauti, Shaaban ‘Kamchape’ akitokea katika bendi ya Dodoma International ya mjini Dodoma.

Gurumo alirejea tena katika bendi yake ya Juwata mwaka 1991, akapewa wadhifa wa kuwa kiongozi wa bendi hiyo, baada ya kupiga muziki katika bendi hiyo ya Mliamani Park Orchestra pamoja na Orchestra Safari Sound (OSS) kwa nyakati tofauti.

Nyimbo walizotoka nazo zilikuwa za Nidhamu ya kazi, Ete, Queen Kasse, Mariamu ninakujibu, Usia wa baba, Msafiri kafiri, Tupa tupa, Ndugu Kassimu na nyingine lukuki.

Baadaye bendi hiyo ilibadilishwa jina na kuwa OTTU Jazz kufuatia kubadilika kwa jina la Chama cha Wafanyakazi kuwa OTTU. Hakuna ubishi kwamba bendi ya OTTU Jazz au kwa jina lingine wakajiita ‘Baba ya Muziki’, ilitikisa jiji la Dar es Salaam na nchi nzima kwa ujumla wakipigia kwa mtindo wa wa ‘Msondo Ngoma, magoma Kitakita’ au ‘Mambo hadharani’.

Wakati huo ilikuwa katikati ya wimbo wapenzi na mashabiki wa Msondo walikuwa wakiimbishwa kibwagizo cha “Msondo yee Msondo Waa…” wapenzi na walikuwa wakiitikia “Afyaaaa”. Bendi hiyo ilikuwa ikipiga muziki wake katika ukumbi wa Amana uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, ikipakana na hospitali ya Amana.

Katika kipindi hicho bendi hiyo ilikuwa imesheheni wengi wenye vipaji vinavyotofautiana. Wanamuziki hao walikuwa akina Joseph Lusungu, Mnenge Ramadhani, Muhiddin Maalim, Hassan Rehani Bitchuka, Saidi Mabera na TX Moshi William. Wengine ni pamoja na

Nicko Zengekala, Selemani Mbwembwe, Joseph Maina, Mustapha John Ngosha, Suleimani Mwanyiro ‘Computer’, Tino Maselenge (Masinge) ‘Arawa’ Abdull Ridhiwan Pangamawe, Roman Mng’ande ‘Romario’ na Athumani Momba. Wengine ni Salehe Bangwe ‘Mwana Kigoma’, na bila kuwasahau Huruka Uvuruge na Said Mabera mpiga solo mahiri ambaye tangia ajiunge katika bendi hiyo hajathubutu kuiondoka.

Kufuatia Hospitali ya Ilala kupanuka, OTTU Jazz walitakiwa kuondoka kwa kile kilichodaiwa ni kuwabughudhi wagonjwa kwa makelele ya vyombo vya muziki wao. Hivyo walilazimika kuhamia katika ukumbi wa AfriCenter uliopo barabara ya Kigogo, ambako nako hawakudumu kipindi kirefu na hivi sasa wanapiga muziki wao popote wanapoalikwa hususan wamiliki wa Baa, ambapo huwa hakuna kiingilio ili kununua kinywaji chako.

Baadhi ya nyimbo ‘zilizogongwa’ na OTTU Jazz zilikuwa za Kicheko, Mawifi mnanionea, Ndoa Ndoana, Nimezama katika dimbwi, Mti mkavu na Mizimu. Zingine ni Wabakaji, Tabu, Pricila, Penzi la mlemavu, Piga ua talaka utatoa, Tuma, Wapambe, Asha mwana Sefu, Ajali, Mtanikumbuka, Barua ya kusikitisha, Mwana mkiwa, Kalunde, Kaza moyo, Jesca, Kwenye penzi, Binti maringo, Dalili na nyingine nyingi.

Chama cha Wafanyakazi Tanzania baadaye kijiondoa katika ufadhili wa bendi hiyo, kikawaachia vyombo wajitegemee. Walijikusanya kutengeneza mikakati na kuamua kuipa jina la bendi kuwa Msondo Ngoma ikiwa imesheheni wanamuziki wengi wakiwemo wa zamani na wapya.

Msondo Ngoma ina jumla ya wanamuziki 18 na fundi mitambo mmoja. Kiongozi wao ni Said Mabera ambaye pia ni mpigaji wa gita la Solo. Waimbaji wa bendi hiyo ni akaina Juma Katundu, Fresh Jumbe, Shaaban Dede, Twaha Mohamed, Hassan Moshi William ‘TX Junior’ na Hussein Kalembo.

Wakung’utaji magita ni akina Abdull Ridhiwani Pangamawe ambaye ni bingwa wa kupiga kinanda, Solo na Rhythm, Huruka Uvuruge naye pia ni mpigaji wa Solo na Rhythm, Kassimu Mponda, Mustafa Hamis ‘Pishuu’ na Zahoro Bange wakicharaza gitaa la rhythm.

Kwa upande wa gita zito la besi wapo Ally Lindunga na Saad Ally ‘Sure Boy’. Drums huchanganywa na Saad Ally ‘Mashine’ na Arnold Kang’ombe.

Tarumbeta hupulizwa na kijana machachari Roman Mng’ande ‘Romari’ na Hamis Mnyupe. Dorice George hupiga Tumba, Drums ambaye pia ni Mwimbaji wakati Amiri Said Dongo naye ni mpigaji wa Tumba. Mtunzi na mwimbaji mahiri Shabani Dede ‘Kamchape’ alirejea tena katika bendi hiyo akitokea bendi ya Mlimani Park Orchestra ‘Wana Sikinde’.

Talanta za kutunga na kuimba za marehemu TX Moshi William, ambaye inasemekana yeye ndiye alikuwa mtunzi mkuu katika bendi hiyo. Inaaminika kuwa katika albamu moja waliokuwa wakiifyatua, TX alikuwa katunga nyimbo 8 hadi 9 wakati zilizobaki zinatungwa na Jumuiya.

Tofauti kabisa na miaka ya nyuma upinzani kati ya bendi za Mlimani Park na Msondo Ngoma Classic uliokuwa ukishihudiwa nyakati zile, umepungua kwa kiasi kikubwa. Bendi hizo hufikia kuandaa siku ya kupiga muziki kwa pamoja katika viwanja vya TTC Chang’ombe, jijini Dar es Salaam.

Bendi ya Msondo Ngoma Classic bado ipo ikiwa na makao yake katika baa ya Dimax iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanamuziki wanaotajwa katika makala hii wamekwisha tangulia mbele za mungu akiwemo Mzee Muhidini Gurumo.

Wengine ni TX Moshi William, Nicko Zengekala, Selemani Mbwembwe, Joseph Maina, Hamis Kitambi, Mustafa John Ngosha, Suleiman Mwanyiro, Tino Maselenge ‘Arawa’, Athuman Momba na wapulizaji wa saxophone Mnenge Ramadhani na Alli Rashidi aliyefariki dunia siku ambayo bendi hiyo ikitimiza miaka 50, Oktoba 10, 2014.

Mungu azipumzishe roho zao pahala pema peoni, Amina.

Mwandishi wa makala haya anapatikana kwa namba:
0784331200, 0767331200, 0736331200 na 0713331200

Halotel, Visa waungana kuwezesha malipo salama kwa njia ya simu Tanzania

$
0
0
- Idadi ya watumiaji wa Halopesa imeongezeka kwa asilimia 71.76 katika kipindi cha mwaka 2018. Kampuni ilifunga mwaka 2017 ikiwa na jumla watumiaji wa Halopesa wapatao 780,000. Idadi hiyo imeongezeka Kwa kiasi kikubwa hadi kufikia jumla ya watumiaji milioni 1.3 mwishoni mwa mwaka 2018.

Kampuni za Halotel Tanzania na Visa zimesaini mkataba wa kimkakati ambao utawawezesha watumiaji wa Halopesa kufanya malipo kwa njia ya Visa kupitia simu zao.

Ushirikiano kati ya kampuni hizo utawezesha watumiaji wa Halopesa kutumia huduma ya Visa kwenye simu zao kwa kufanya malipo ya bidhaa na kuweka pesa na kutoa kwa mawakala wa huduma ya Visa.

Takwimu kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) iliyotoa mwaka 2018 inasema kuwa Halopesa ni huduma ya malipo kwa njia ya simu inayokua kwa kasi sana hapa Tanzania.

Idadi ya wateja waliojisajili kwa huduma ya Halopesa imeongezeka kwa kiasi cha asilimia 71.76 katika kipindi cha mwaka 2018. Kampuni ilifunga mwaka 2017 ikiwa na jumla watumiaji wa Halopesa wapatao 780,000. Idadi hiyo imeongezeka kwa kiasi kikubwa hadi kufikia jumla ya watumiaji milioni 1.3 mwishoni mwa mwaka 2018.

“Kwa ukuaji mkubwa wa idadi ya wateja wa Halotel na kuwa ni mtandao wa simu unaokua kwa haraka hapa Tanzania tangu tuanze kutoa huduma hapa nchini, tuna imani kwamba idadi ya watumiaji wa Halopesa pia itaendelea kuongezeka,” amesema Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Tien Dung.

Bw. Dung amesema kuwa kwa sasa Halopesa ina zaidi ya mawakala 40,000 na kwamba nguvu ya huduma ya Visa inaipa Halopesa thamani na uwezo zaidi wa kuwezesha wateja kufanya manunuzi kwa njia ya Visa kupitia simu zao.

“Kupitia ushirikiano huu, Halopesa itawapa wateja kulipa kwa muuzaji kwa kutumia msimbo (code) iliyoko kwenye huduma ya Visa kwenye simu zao. Huduma hii ya Visa katika simu huwezesha wateja kupata fedha zao moja kwa moja kutoka katika akaunti zao za benki kupitia simu zao na kulipia bidhaa kwa wauzaji, kutuma pesa bila gharama yoyote, kuweka pesa au kutoa pesa kupitia wakala yeyote wa huduma ya Visa,” amesema na kuhitimisha Bw. Son.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Visa nchini Tanzania Olive Njoroge, ameelezea kuwa ushirikiano huo unalenga zaidi katika kuunganisha Watanzania kwenye huduma ya Visa na kuleta usalama wa fedha zao kufanya malipo fanisi kwa huduma na bidhaa.

‘Tunafarijika kwa ushirikiano huu kati yetu na kampuni muhimu ya huduma za mawasiliano ya simu kama Halotel. Ushirikiano wetu na Halotel utawafanya Watanzania kulipa kwa kutumia Visa katika simu zao kupitia zaidi ya wachuuzi wapya 40,000. Pia itawasaidia kupanuka kwa wigo wa Watanzania wanaotumia huduma za kifedha hapa nchini,” amesema Bi. Njoroge.

Kupitia huduma ya Visa, muuzaji atapewa msimbo (QR code) pamoja na namba maalum ya wakala ambayo mteja ambaye simu yake ina huduma ya Visa ataitumia kwa ajili ya malipo kupitia simu yake.

Ushirikiano huu unadhihirisha nia ya dhati ya VISA kutanua wigo wa malipo kupitia Huduma za kifedha kwa njia ya simu Ulimwenguni kote.
 Naibu Mkurugenzi wa kampuni ya Halotel, Nguyen Tien Dung akiongea na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya HALOPESA VISA ON MOBILE katika makao makuu ya Ofisi za Halotel Dar es salaam. Huduma hiyo itawawezesha wateja wote wa Halopesa kuweza kulipia bidhaa, au kufanya miamala ya kifedha kupitia Visa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Visa Nchini Tanzania Olive Njoroge, kulia ni Mkuu wa kitengo cha Halopesa Magesa Wandwi.
 Naibu Mkurugenzi wa kampuni ya Halotel Nguyen Tien Dung , Mkurugenzi wa Visa nchini Tanzania Olive Njoroge, kwa pamoja wa akisaini Mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara kati ya Halopesa na Visa. Akishuhudia, Kulia ni Meneja Kitengo cha biashara Halopesa Magesa Wandwi.
 Naibu Mkurugenzi wa kampuni ya Halotel Nguyen Tien Dung na Mkurugenzi wa Visa nchini Tanzania Olive Njoroge wakikabidhiana mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara kati ya Halopesa na Visa, ambapo wateja wa Halopesa nchini wataweza kulipia bidhaa na kufanya miamala ya kupitia Visa .
Afisa wa kitengo cha malipo ya kidigitali Halopesa, Emmanuel Mwaisoloka (Kushoto) akilipia bidhaa dukani kupitia Halopesa Visa on Mobile ikiwa ni mfano jinsi mteja yeyote wa Halopesa anavyoweza kulipia bidhaa kupitia Halopesa Visa on Mobile. 

TAARIFA YA UFAFANUZI KUHUSU KUWEPO KWA DAWA ZA VIDONGE ZINAZODHANIWA KUTIBU HOMA YA DENGUE (DENGUE FEVER).

TIMU ya sevilla kuwasili kesho jijini Dar es salaam

$
0
0
TIMU ya sevilla kuwasili kesho jijini Dar es salaam kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Simba.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Utawala na udhibiti wa kampuni ya sportpesa Abas Tarimba amesema kampuni hiyo inayochezesha michezo ya kubahatisha inaenda kuandika historia kwa mara ya pili kuileta timu ya kimataifa sevilla.

"Mbali na ujio wao timu ya sevilla itaweza kufanya shughuli mbalimbali zenye lengo la kuinua sekta ya michezo nchini kwa vijana "
Tarimba ameeleza kuwa timu hiyo ya kimataifa itapata nafasi ya kutoa  mafunzo kwa timu ya vijana bom bom fc huku kwa baadhi ya maofisa wa klabu ya sevilla wataendesha mafunzo kwa viongozi wa vilabu pamoja na shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) na washiriki wake ili wapate kuhimarika kitaaluma na uelewa jinsi ya kuongeza vipato vya vilabu.

Kwa upande wa msemaji mkuu wa klabu ya wekundu wa msimbazi Haji Manara ameeleza wazi kuwa ujio wao utaleta manufaa makubwa katika sekta ya michezo hasa mpira wa miguu huku taifa likiwa limepata heshima kubwa na Pato la taifa kuongeza.

"Mechi ya sevilla dhidi ya Simba fc itaongeza Pato la taifa kutokana na tayari tiketi zimeshanunuliwa kwa wingi na zinaendelea kununuliwa"

Hata hiyo amesema maandalizi yanaendelea vizuri,kwa sasa timu imeelekea singida kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya singida united hapo kesho .

"Uchovu wa mechi za ligi kuu sio kigezo cha kutokufanya vizuri katika mechi dhidi ya sevilla tutapambana na kuhakikisha tunaitangaza nchi yeti kwa ushindi "

Pia ametoa rai kwa mashabiki wa Simba na timu zingine kujitokeza kuishangilia timu ya Simba ili kwani ndio nafasi pekee ya kwa wachezaji wakitanzania kujitangaza kimataifa kama klabu  na kupata fursa nchi zingine kuwekeza katika sekta ya mpira.
Mkurugenzi wa utawala na udhibiti wa kampuni ya michezo ya kubahatisha nchini (SPORTPESA) Abas Tarimba akizungumza na waandishi wa habari kufatia ujio wa timu ya kimataifa sevilla kutoka nchini Hispania kuwasili kesho kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Simba FC
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>