Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

BASI LAGONGA TEMBO WILAYANI KARAGWE USIKU WA KUAMKIA LEO

$
0
0
Basi la kampuni ya Fikoshi linalofanya Safari zake kati ya Karagwe na Mwanza limegonga tembo usiku wa kuamkia leo katika eneo la Byenturege Kitengure Wilayani Karagwe lilipokuwa likitokea Mwanza. 

Eneo hilo ni linatambulika kuwa ni Sehemu ambapo Wanyama tofauti kama Swala, Simba, Tembo ambao hupenda kukatiza Barabara wakati wakijitafutia chakula, licha ya kuwepo kwa alama na Vibao vya Tahadhali, lakini Magari yamekuwa yakipita kwa kasi katika eneo hilo na inaelezwa ndio sababu ya basi hilo kugonga Tembo. Hakuna binadamu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo zaidi ya Tembo na Basi kuumia. Tutaendelea kukuletea taarifa zaidi hapo baadae.
 Basi la Fikoshi linalofanya Safari zake kati ya Karagwe na Mwanza limegonga tembo usiku wa Jana  eneo la Byenturege Kitengure Wilayani Karagwe likitokea Mwanza. Hakuna madhara mengine zaidi ya Basi kuumia. Tunaendelea kufuatilia.


NYOTA WA ZAMANI WA TAIFA STARS JELLAH MTAGWA YU HOI KITANDANI, ANAHITAJI MSAADA WAKO

$
0
0
Mchezaji kandanda wa zamani wa Taifa Stars na Yanga na Pan African Jellah Mtagwa yupo kitandani akiugua kiharusi na anahitaji msaada wa matibabu pamoja na kujikimu kimaisha.

Mtagwa, ambaye hivi sasa amepooza nusu ya mwili wake, anaishi Manzese Friend's Corner  jijini Dar es salaam pamoja na familia yake akiwa hana hili wala lile kutokana na maradhi hayo na ufukara.

Wadau na mashabiki wa mpira wa miguu wameelezea masikitiko yao kwa hali kama hiyo kumkumba aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya Taifa Stars ambaye picha yake iliwekwa kwenye stempu kutokana na mchango wake uliotukuka kwa nchi.

Wengi wanahoji endapo kama Shirika la Posta lilimlipa mchezaji huyo mrabaha wa kuwekwa sura yake mwenye stempu, na kama Shirikisho la Mpira nchini (TFF) wana taarifa zake na kama wanamsaidia kwa choche.

Hivi tunavoongea umoja wa wachezaji soka wa zamani  (UMSOTA) wameanzisha harambee ya kumsaidia mwenzao huyo kwa kuchangishana ili kumsaidia.

Tayari umoja huo umetoa ombi la msaada kwa wasamaria wema kumsaidi Jellah Mtagwa kwa kutangaza namba yake ya simu Namba 0755 693330 kwa yeyote atakayeguswa.


 Baadhi ya wachezaji soka wa zamani wakiwa wamemtembelea Jellah Mtagwa nyumbani kwake Manzese Friend's Corner jijini Dar es salaam kumjulia hali na kumpatia msaada

 Baadhi ya wachezaji soka wa zamani wakiwa wamemtembelea Jellah Mtagwa nyumbani kwake Manzese Friend's Corner jijini Dar es salaam kumjulia hali na kumpatia msaada

 Baadhi ya wachezaji soka wa zamani wakiwa  na wanafamilia baada ya kumtembelea Jellah Mtagwa nyumbani kwake Manzese Friend's Corner jijini Dar es salaam kumjulia hali na kumpatia msaada

Stempu iliyowekwa picha ya Jellah Mtagwa
Jellah Mtagwa akisimulia adha ya maradhi yake

Viongozi wa dini watakiwa kuwaeleza wananchi ukweli

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,  Jerry Muro akizungumza katika kongamano la viongozi wa dini lililofanyika jana katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu, Patandi. ambapo alisemakuwa niwajibu wa kila mchungaji kuwaamasisha waumini wao kufanya kazi. 
Mtume Sekela Lolandi wa Huduma ya Ngurumo ya Upako akitoa neno katika Kongamano la Vingozi wa Dini, lililofanyika jana katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu, Patandi. 
baadhi ya viongozi wa dini wakiwa wanasikiliza kwa makini wakati mkuu wawilaya ya meru akiongea nao.

Na Woinde Shizza - Michuzi Tv, Arusha

Viongozi wa dini wametakiwa kuwaeleza wananchi wao umuhimu wa kufanya kazi kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza tatizo la umaskini linalowakabili wananchi wengi. 

Hayo yalibainishwa jana na mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro wakati akizungumza katika kongamano la viongozi wa dini lililofanyika jana katika ukumbi wa chuo cha ualimu patandi ambapo alisemakuwa niwajibu wa kila mchungaji kuwaamasisha waumini wao kufanya kazi. 

Alisema kuwa kumekuwa na tabia ya wananchi wengi kulalamika hali ngumu ya kimaisha lakini ukiwachunguza zaidi unakuta hawana kazi yeyote wanaofanya zaidi ya kulalamika tu hali ngumu ya Maisha

"napenda kuwaomba viongozi wangu wadini mtusaidie hawa waumini wenu wakija uko kutaka kuwaombea wachunguzeni kwanza kama wanakazi kama hawana wahamasisheni wafanye kazi nasio wakae tu bure na kulalamika hali ngumu ya kimaisha "alisema Muro

Aidha Muro aliwasihi viongozi hao wa dini kuendelea kuombea amani ya nchi yetu, pamoja na kuombea viongozi wa nchi yetu. 

Wakati huo huo Watanzania wametakiwa kuendeleza kuenzi upendo, mshikamano, na amani tulioasisi na baba wa Taifa kwani amani hii ikipotea kuirudisha ni kazi na itatugarimu. 

Hayo yameelezwa na mtume Sekela Lolandi  wa Huduma ya ngurumo ya upako  iliopo ndani ya wilaya ya Arumeru,wakati akiongea Katika kongamano la wachungaji la kuombea wilaya ,mkoa ,Taifa na viongozi wa serikali  kongamano lililoandaliwa na mkuu  wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro ambapo walisema kuwa ni wajibu wa kila wananchi kuenzi amani tuliachia. 

Alisema kuwa  niwajibu wa kila mtanzania kuenzi amani na upendo pamoja na ushirika tulioasisiwa na wazee wetu kwani amani hii ikitoweka tutakuwa tumepoteza kitu kikubwa mno ambacho itakuwa ni ngumu kuirejesha. 

"watanzania tunatakiwa tuwe na umoja upendo ili tuendelee kulinda amani ya nchi yetu, na katika swala la upendo tunatakiwa sisi kama viongozi wa kanisa pamoja na kanisa tuanze na sisi kupendana na kiwahimiza wananchi kudumisha amani tulionayo na ili taifa liwe na nguvu lazima tuenzi na kulinda amani tulionayo"alisema mchungaji Orche Mgonja kutoka kanisa la Pentekoste la lift him up.

Aidha pia viongozi hao wadini walimpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli pamoja na mkuu wa wilaya ya Arumeru  Jerry cornel Muro kwa jinsi wanafanya kazi na kuwajali wananchi wa chini pia waliwapongeza serikali ya magufuli kwa jinsi wanavyowaheshimu viongezi wa dini. 

Kipaumbele cha Wizara ni kupeleka nishati kwa wananchi - DKT.KALEMANI

$
0
0
Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani( katikati), Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( wapili kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamis Mwinyimvua( wa pili kulia) wakiwa wameshikana mikono wakiimba wimbo wa mshikamano daima wakati wa Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa wizara ya nishati, mkutano huo umefanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa wizara ya nishati wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,(hayupo pichani) wakati wa mkutano wa baraza la wafanyakazi uliofanyika jijini Dodoma.

Na Zuena Msuya, Dodoma

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewaeleza watumishi wa Wizara ya Nishati kuwa kipaumbele cha Wizara ni kupeleka nishati kwa wananchi ikiwamo ya Umeme na Gesi hivyo amewaasa kushirikiana kwa pamoja na kufanya kazi kwa weledi.

Dkt. Kalemani alitoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Nishati uliofanyika jijini Dodoma, Mei 17,2019 "Watanzania wote wanahitaji huduma ya Umeme, hii tuichukulie kama fursa kwa kuwaunganisha wananchi hao nishati hiyo ili pia kuliongezea Taifa mapato," alisisitiza Dkt. Kalemani.

Kuhusu kuboresha maslahi ya wanyakazi, Dkt. Kalemani aliziagiza Idara husika hasa ile ya utumishi kuhakikisha inawapandisha vyeo watumishi wanaostahili kwani ni moja ya masuala yanayoleta morali ya kufanya kazi kwa bidii.

Aidha, alisema kuwa, kwa watumishi ambao hawajapandishwa vyeo,  waelezwe sababu  ili waweze kujirekebisha ili  kuondoa malalamiko na matabaka sehemu za kazi. 

Sambamba na hilo, alitaka kuwepo na utaratibu wa kuwatambua wafanyakazi wanaofanya kazi vizuri zaidi kwa kuwapa tuzo maaalum, kwa lengo la kuinua ari ya wafanyakazi na kuongeza tija katika utendaji kazi wao.

Katika hotuba yake, Waziri Kalemani, alizitaka Idara za Manunuzi na Utawala katika Sekta ya Nishati kuzingatia sheria za utumishi wa umma na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maslahi ya taifa na si mtu binafsi. 

Mkutaano huo  ulihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati,  Subira Mgalu ambaye aliwataka wafanyakazi kufanya kazi kwa kasi, ari na kujituma kwa kuwa wao ndiyo nguzo muhimu katika kuwafikishia wananchi huduma  ya Umeme. 

Alisisitiza kuwa, watumishi watambue kuwa wizara ya Nishati ni muhimili muhimu kwa Taifa katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuingia katika Uchumi wa Kati hivyo  kuna jukumu la kusambaza Umeme viwandani na kwa wananchi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua aliwaeleza wajumbe wa Baraza hilo kuwa,katika kipindi cha mwaka 2018/2019 watumishi 41 wamepandishwa vyeo ,watumishi 3 wamebadilishwa kada na watumishi wapya 10 wameajiriwa. 

Aliongeza kuwa, watumishi wameendelea kupewa stahiki zao mbalimbali na kuendelea kuboreshwa kwa mazingira ya kazi na makazi. 

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, katika Wizara,  Frank Mrema alishukuru uongozi wa Wizara kwa kusimamia stahiki za watumishi pamoja na upandishaji wa madaraja kwa watumishi wenye sifa. 

Aidha, aliiomba Wizara kuendelea kuboresha maslahi ya watumishi kwa kuzingatia mfumo wa maisha uliopo sasa.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AONGOZA KIKAO KAZI CHA WAKUU WA MAGEREZA YOTE TANZANIA BARA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiongoza Kikao kazi cha Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara Mei 18, 2019 katika Ukumbi wa Magereza Mkoani Morogoro. Kushoto ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiwa meza kuu pamoja na Makamishna na Manaibu Kamishna wa Jeshi la Magereza wakifuatilia uwasilishaji wa mada mbalimbali wa kikao kazi cha Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara Mei 18, 2019 katika Ukumbi wa Magereza Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo katika Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Charles Novart akitoa ufafanuzi katika Kikao cha Wakuu wa Magereza.
Baadhi ya Wakuu Magereza wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Kamishna Jenerali wa Magereza katika kikao hicho.
Meneja Biashara toka Benki ya CRDB Tawi la Mkoa wa Morogoro, Bi. Theofora Madilu akitoa maelezo ya huduma mbalimbali za kifedha zinazotolewa na Benki ya CRDB katika Kikao kazi cha Wakuu wa Magereza Tanzania Bara(Picha na Jeshi la Magereza).

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AJUMUIKA KATIKA FUTARI ALIYOWAANDALIA WANANCHI WA KIJIJI CHA MKANYAGENI WILAYA YA MKOANI KISIWANI PEMBA

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba, katika futari aliyowaandalia katika viwanja vya Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua, kushoto Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na kulia Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri, wakiwa katika hafla hiyo.
WANANCHI wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba wakijumuika katika hafla ya Futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa ajili yao iliofanyika katika Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua.
WANANCHI wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Hemed Suleiman, akitowa neno la shukrani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,.Dk. Ali Mohamed Shein, baada ya kumaliza hafla hiyo ya futari iliofanyika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuika na Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni katika futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa Wananchi hao iliofanyika katika Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba kulia Mshauri wa Rais Afisi ya Rais Pemba Mhe.Dkt. Maud Abeid Daftari.
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Hemed Suleiman, akitowa neno la shukrani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kwa Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni wakati wa hafla ya futari walioandaliwa katika Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua.
WANANCHI wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Hemed Suleiman, akitowa neno la shukrani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,.Dk. Ali Mohamed Shein, baada ya kumaliza hafla hiyo ya futari iliofanyika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kushoto Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na kulia Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Mhe. Mmanga Mjengo Mjawi, wakiitikia dua ikisomwa na Mzee wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Kisimwani Pemba Bw,Khamis Amour, baada ya kumaliza hafla hiyo ya futari iliofanyika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Mzee Khamis Amour, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dk. Shein, kwa wWananchi wa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa hafla ya Futari iliofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari aliowaandalia Wananchi, iliofanyika katika Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua.(Picha na Ikulu, Zanzibar)

MKANDARASI WA REA TANGA KUKATWA MSHAHARA

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (mwenye kinasa sauti) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Vuo wilayani Mkinga, Mkoa wa Tanga, baada ya kuwasha umeme kijijini hapo akiwa katika ziara ya kazi Mei 18, 2019. Kushoto kwa Waziri ni Mbunge wa Jimbo la Mkinga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dustan Kitandula.

Na Veronica Simba - Tanga

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, ameuagiza uongozi wa juu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kukata asilimia 10 ya malipo ya Mkandarasi anayetekeleza miradi ya umeme vijijini mkoani Tanga, endapo itabainika hana sababu za msingi kuchelewesha mradi.

Alitoa maagizo hayo Mei 18 mwaka huu katika Kijiji cha Vuo, Wilaya ya Mkinga, mkoani Tanga akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme.

Akizungumza na wananchi wa Vuo, kabla ya kuwawashia rasmi umeme, Dkt. Kalemani alisema kasi ya mkandarasi hairidhishi maana ni ndogo sana hivyo akawataka watendaji wa TANESCO kufuatilia ili kujiridhisha endapo kuna sababu za msingi za ucheleweshaji huo wa mradi.

Mkurugenzi TANESCO fuatilia; ukikuta kuna uzembe, wakate asilimia 10 ya mshahara wao maana wanataka kutucheleweshea mradi.

Sambamba na agizo hilo, Waziri alielekeza mkandarasi huyo kuwa na Mpango-Kazi wenye mchanganuo wa kuwasha umeme katika vijiji vitatu kila wiki.

Kufuatia agizo hilo, alimtaka Meneja wa TANESCO wa Wilaya, kumwandikia barua ya kusitisha mkataba wake, Mkandarasi husika endapo atashindwa kuwasha umeme katika vijiji vitatu kila wiki.

Aidha, Waziri alimtaka Meneja huyo pamoja na Mkandarasi kuwasilisha maelezo ndani ya siku moja sababu za kusuasua kwa utekelezaji wa mradi.

“Meneja wewe ndiye wa kumsimamia Mkandarasi. Kama kasi yake ni duni, inamaanisha hata wewe utendaji wako siyo mzuri,” alisema Waziri.

Katika hatua nyingine, Dkt. Kalemani alibainisha kuwa moja ya sababu za Mkandarasi kuwa na kasi ndogo yawezekana kuwa ni uhaba wa vibarua alioanao. Alimtaka kuongeza idadi ya vibarua mara moja na kwamba vibarua hao watoke eneo husika na awalipe ujira wao kwa wakati.

“Ni marufuku kuajiri vibarua nje ya eneo unakotekelezwa mradi. Vibarua wote wawe wa eneo husika ili wanufaike kwa uwepo wa mradi katika eneo lao.”

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika maeneo mbalimbali ya Wilaya za Mkinga, Pangani na Muheza, ambako alikagua utekelezaji wa miradi ya umeme pamoja na kuwasha umeme katika vijiji kadhaa; Waziri Kalemani alitoa hamasa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kulipia gharama za kuunganishiwa umeme ambazo ni shilingi 27,000 tu.

Aidha, aliwataka wale ambao tayari wameunganishiwa umeme, kuutumia kwa kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi ili wanufaike kwa kuinua kipato na kuboresha maisha yao.

Waziri alitoa zawadi ya vifaa vya Umeme Tayari (UMETA), kwa wananchi katika maeneo yote aliyotembelea ili kuwahamasisha kuchangamkia fursa ya uwepo wa mradi wa umeme vijijini na hivyo kujitokeza kwa wingi kulipia na kuunganishiwa nishati hiyo.

Katika Shule ya Sekondari Bushiri wilayani Pangani, Waziri alikabidhi vifaa 40 vya UMETA kwa wanafunzi na walimu, ili vifungwe katika vyumba vya madarasa, maabara, ofisi, nyumba za waalimu, vyoo na barabara zote za shule ili pamoja na mambo mengine kuhakikisha usalama wa watoto, hususan wa kike.

Waziri anaendelea na ziara yake mkoani Tanga ambapo anatarajiwa kuhitimisha kwa kutembelea Wilaya ya Korogwe.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Vuo wilayani Mkinga, Mkoa wa Tanga, kabla ya kuwasha umeme kijijini hapo akiwa katika ziara ya kazi Mei 18, 2019.
Mbunge wa Jimbo la Mkinga, Dustan Kitandula, akizungumza wakati wa Hafla ya kuwasha umeme katika kijiji cha Vuo, wilayani Mkinga, Mkoa wa Tanga. Tukio hilo lilifanywa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kutoka kushoto), Mei 18, 2019 akiwa katika ziara ya kazi.
Mkandarasi anayetekeleza mradi wa umeme vijijini mkoani Tanga, Ahmed Hemed kutoka kampuni ya JV RADI Services Njarita & Aguila (kushoto), akizungumza na wamiliki wa nyumba inayoonekana pichani, Sabasaba Hassan na mama yake, muda mfupi baada ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) kuiwashia umeme, akiwa katika ziara ya kazi, Mei 18, 2019.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akitoa maelekezo kwa watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), alipokuwa katika ziara kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme, wilayani Mkinga, Mkoa wa Tanga, Mei 18, 2019.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bushiri, wilayani Pangani, Mkoa wa Tanga, alipofika kuwawashia umeme shuleni hapo, akiwa katika ziara ya kazi, Mei 18, 2019.


Taswira ya baadhi ya nyumba za wakazi wa Wilaya za Mkinga, Pangani na Muheza mkoani Tanga, kama zilivyonaswa wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Mei 18 mwaka huu. Waziri aliziwashia umeme nyumba hizo na kusisitiza kwamba ni marufuku kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini kubagua aina ya nyumba wakati wa kuunganisha umeme.
Sehemu ya wataalamu kutoka Wizara ya Nishati, pamoja na viongozi na wataalamu wengine mbalimbali wa Serikali, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Vuo, Wilaya ya Mkinga, Mkoa wa Tanga, akiwa katika ziara ya kazi, Mei 18, 2019.

LHRC YAWATAKA WANAWAKE WA KIGOMA WANAOINGILIWA NA TEREZA KUTOA TAARIFA KWENYE VYOMBO VYA USALAMA HARAKA.

$
0
0
Na Editha Karlo,Michuzi TV -Kigoma

KITUO cha sheria na haki za binaadamu(LHRC)kimewataka wakazi wa Mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na serikali za mitaa kuunda vikosi vya ulinzi mitaani kwaajili ya kuwalinda wanawake wasifanyiwe ukatili wa kingono.

Mkurugenzi mtendaji wa LHRC Anna Henga ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wasaidizi wa sheria na waangalizi wa haki za binaadamu kanda ya Magharibi.

Anna amesema pamoja kuundwa kwa vikosi hivyo vya ulinzi,lakini pia wanawake wanaofanyiwa vitendo hivyo nao wanapaswa kutoa taarifa katika vyombo vya usalama haraka pale wanapopatwa na tatizo.

"Hapa Kigoma kuna kitu wanaita tereza,yaani wanaume wanajipaka mafuta ya mawese afu wanawaingilia wanawake kingono kwa nguvu,wanapiga,wanawajeruhi,wanawaibia na wakiwashika wanateleza baada ya kujipaka hayo mafunzo,Nimefika Kigoma mwenyewe ili niweze kujionea mwenyewe maana awali nilikuwa nasikia tu hizi habari za tereza,lakini nimeamini hili jambo lipo na baadhi ya waathirika waliofanyiwa vitendo hivyo nimeongea nao naamini tukishirikiana hili jambo litaisha"Alisema

Alisema kitendo wanachofanyiwa baadhi ya wanawake wa Kigoma mjini hasa maeneo ya Mwanga na Katubuka cha kuingiliwa kinguvu kingono,kupigwa na kuibiwa mali zao ni kitendo kibaya mno na hakiwezi kuvumiliwa.

"Mimi kazi yangu kutetea wanawake na watoto,kwa hapa Kigoma hiki kitendo ni kibaya ninawaomba wanawake watakaofanyiwa vitendo hivyo vya ukatili na hao akina tereza kutoa taarifa mara moja kwenye vyombo vya usalama ili waweze kupata msaada ikiwemo kuwakamata na hao waalifu"alisema

Naye Ofisa mratibu wa masuala ya ulinzi na usalama kutoka LHRC Renatha Selemani alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watetezi wa haki za binaadam baada ya kuona kuna hatari nyingi za kiusalama zinawakabili.

Zawadi Jacob mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo amesema wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya jamii kutokujua sheria na haki zao,na kusema mafunzo hayo yatamsaidia katika kazi zake pamoja na kuelimisha jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binaadamu(LHRC)Anna Henga akizungumza na Waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wasaidizi wa sheria na waangalizi wa haki za binaadamu kanda ya Magharibi.

MILIONI 10 ZADAIWA KUTAFUNWA UJENZI WA VYOO SHULE YA MSINGI MAPAMBANO.

$
0
0
Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo Kata ya Iyela (WDC) Jijini Mbeya wamehoji Ofisi ya afisa Mtendaji Kata hiyo juu Matumizi ya Fedha kiasi cha Shilingi Milioni 10 namna ambavyo zimetumika katika ujenzi wa Vyoo katika Shule ya Msingi Mapambano jijini Mbeya .

Aidha wameitaka Ofisi hiyo kutoa Maelezo ya Kina juu ya kusuasua kwa ujenzi wa vyoo hivyo ambao umedumu kwa zaidi ya mwaka mmoja licha ya kutolewa fedha hizo kutoka Halmashauri ya Jiji kupitia Mfuko wa Jimbo na michango ya Wananchi wakiwemo wadau wa maendeleo.

Hatua hiyo inakuja mara baada Wananchi wa Kata ya Iyela pamoja na wadau mbalimbali wanao unga mkono juhudi za Maendeleo katika Kata hiyo kuhoji juu ya Maendeleo ya ujenzi wa Vyoo kuchukua muda mrefu zaidi ya Mwaka mmoja licha Fedha kutolewa.

Akizingumza katika kikao cha Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo (WDC) Kata ya Iyela Mwenyekiti wa Shule ya Mapambano George Gidion amesema Wanafunzi wamekuwa wakipata adha kubwa kutokana na kuto kamilika kwa ujenzi wa vyoo hivyo hali ambayo ineleta hofu kwa afya za wanafunzi.

“Ujenzi wa vyoo hivi ni changamoto kubwa sana na tatizo kubwa lipo kwa Kamati ya Ujenzi pamoja na Ofisi ya Mtendaji kwani fedha ya ujenzi ilikwisha tolewa Shilingi mil 10 pamoja wadau mbalimbali kuchangia akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila,Naibu Spika Dkt .Tulia Ackson pamoja na Ndele Mwanselela Mdau wa Maendeleo.”Amesema Mwenyekiti huyo .

Naye Paul Mwangwiki Mwenyekiti wa Iyela 2

amesema kuna dalili kubwa ya ufisadi katika ujenzi wa vyoo hivyo kwani hata vifaa vya ujenzi vinavyotumika kuwa na uchakavu hivyo ametaka serikali ingilie Kati ili kuchunguza suala hilo.

Kwa upande wake mmoja wa wadau wa Maendeleo ambao wametoa mchango wao katika ujenzi wa Vyoo hivyo Ndele Mwanselela amesema kwa asilimia kubwa lawama zinatakiwa ziende kwa Mwenyekiti wa Mtaa huo pamoja na Kamati nzima ya Ujenzi kwani wao ndio wasimamizi wakubwa wa Mradi huo.

“Kinacho onekana hapa nikwamba ofisi ya Afisa mtendaji na Mwenyekiti wa Mtaa huu hakuna Mawasiliano kwasababu kila mmoja anaonesha kutolifahamu suala hili wakati wao ndio wasimamizi wakubwa wa mradi huu ,lakini Mimi kama Mdau wa maendelo siwezi lifumbia macho suala hili lazima hatua zichukuliwe kama itabainika kuna ufisadi.”Amesema Ndele Mwanselela.

Akizungungumzia hali hiyo Afisa Elimu Kata ya Iyela Dickson Sinkwembe amesema Fedha za ujenzi zilitolewa kwa kufuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kutangaza zabuni kwa ajili ya kumpata Mkandarasi hivyo kusuasua kwa ujenzi huo kunatokana na usimamizi mbovu kwa Kamati ya Ujenzi .

Ujenzi wa Choo hicho umeanza toka 2018 ambapo Halmashauri kupitia mfuko wa jimbo walitoa kiasi cha Shilingi Milioni 10 pamoja na wadau mbalimbali kuchangia ujenzi wa vyoo hivyo ambapo Zaidi ya wanafunzi Mia900 Shule ya Msingi Mapambano wanategemea vyoo hivyo .

 Vyoo vya shule ya Msingi Mapambano Kata ya Iyela Jijini Mbeya ambao Ujenzi wake unadaiwa kuchukua muda mrefu pamoja na kutumia Shilingi Mil10
 Mdau wa Maendeleo Jijini Mbeya Ndele Mwaselela akichangia jambo Mbele ya wajumbe wa Kamati ya Maendeleleo Kata ya Iyela Jijini (Hawapo ) ambao waliketi kujadili maendeleo ya Ujenzi wa vyoo vya Shule ya Msingi Mapambano Jijini Mbeya .
 Afisa Elimu Kata ya Iyela Mbeya Dickson Simkwembe akizungumza katika Kikao cha Cha Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo Jijini Mbeya kilicho Keti Leo Mei 18 ,2019 katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Mapambano.
George Gidioni Mwenyekiti wa Shule ya Msingi Mapambano jijini Mbeya akizungungumza katika Kikao cha Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo (WDC) Kata ya Iyela Leo  Mei 18 katika Shule ya Msingi Mapambano Jijini Mbeya .
 Wajumbe wa Mkutano

Swedish Minister for International Development Cooperation H.E. Peter Eriksson visits Tanzania 19-21 May

$
0
0
The current development cooperation strategy, which has been guiding Swedish collaboration with Tanzania since 2013 is coming to an end in December. The purpose of Minister Eriksson’s visit is to engage in dialogue regarding the next steps in the bilateral relations.

As part of this process, the Swedish Government has instructed the Swedish Development Cooperation Agency, Sida, to begin preparations for a new strategy with Tanzania.

While in Tanzania, H.E. Peter Eriksson will engage in talks with representatives of the Government, civil society and beneficiaries of the programs Sweden supports.

A renewed Swedish engagement brings an opportunity to realign the cooperation in accordance with changes that have occurred both in Tanzania and in Sweden over the past seven years.

Ahead of his visit, Minister Eriksson stated that: “We need to ensure that Swedish development cooperation contributes effectively to improved opportunities for better living conditions for people living in poverty in Tanzania.

Environment and climate related issues are possible new areas of cooperation with particular focus on biodiversity and access to renewable energy.

A guiding principle is continued focus on reducing poverty and leaving no one behind while being firmly anchored in universal values of equality, democracy and human rights.”

Sida will report back to the Government in September this year.

RIDHIWANI KIKWETE ATOA MISAADA KATA YA UBENA ZOMOZI HUKO CHALINZE

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE 

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ametoa msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya saruji 20 na matofali 3,000 kwa ajili ya uanzishwaji ujenzi wa shule ya msingi katika kitongoji cha Choza .

Aidha amemkabidhi msaada wa baiskeli ya miguu mitatu (wheel Chair),mkazi wa Zomozi-Ubena mzee Cosmas Alphonce Chongwe ambae ni mlemavu wa miguu.

Katika hatua nyingine ,Ridhiwani alitoa fimbo nne maalum kwa ajili ya walemavu wa macho,kadi 23 za afya kwa ajili ya matibabu ya wazee, vyote vikiwa na thamani zaidi ya sh.milioni tano.

Mbunge huyo alitoa misaada hiyo baada ya kumaliza kikao chake alichofanya pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Ubena-Zomozi.

Ridhiwani alieleza, msaada huo alioutoa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Ilani ya uchaguzi na maombi mbalimbali ya wananchi katika kata hiyo. 

Pamoja na hayo, alikutana na wanachama mbalimbali wa vikundi vya maendeleo katika kata hiyo, ambapo aliwahimiza kuendelea kujiunga vikundi ili kuweza kupata mikopo kirahisi na kuwezeshwa kuliko kuwa mmoja mmoja. 

Hakusita kusema, ataendelea kusaidia makundi maalum na kusimamia kero zinazowakabili wananchi wa jimbo la Chalinze. 
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh.Ridhiwani Kikwete akimkabidhi msaada wa Baiskeli ya Miguu mitatu (Wheel Chair),Mkazi wa Zomozi-Ubena Mzee Cosmas Alphonce Chongwe ambaye ni mlemavu wa miguu,leo baada ya Mbunge huyo kumaliza kikao chake alichofanya pamoja na Wajumbe wa Mkutano mkuu wa CCM wa Kata ya Ubena-Zomozi,Chalinze.Mh.Ridhiwani amekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya saruji 20 kwa ajili ya uanzishwaji ujenzi wa shule ya Msingi katika kitongoji cha Choza,Matofali Elfu tatu,fimbo nne maalum kwa ajili ya walemavu wa macho,Kadi 23 za Afya kwa ajili ya matibabu ya wazee, vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi Milioni tano
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh.Ridhiwani Kikwete akimuelekeza Mkazi wa Zomozi-Ubena Mzee Cosmas Alphonce Chongwe ,ambaye ni mlemavau wa Miguu namna ya kutumia Baiskeli ya Miguu mitatu (Wheel Chair),aliyomkabidhi kama msaada.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh.Ridhiwani Kikwete akimkabidhi fimbo maalum kwa ajili ya walemavu wa macho,Josephat Mgonge,ambaye ni mlemavu wa macho
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh.Ridhiwani Kikwete akikabidhi mfuko wa saruji kwa uongozi wa chama cha CCM,ambapo Mh.Mbunge msaada wa mifuko ya saruji 20 na matofali 3,000 kwa ajili ya uanzishwaji ujenzi wa shule ya msingi katika kitongoji cha Choza .
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh.Ridhiwani Kikwete akikabidhi kadi ya matibabu maalum kwa Wazee,Mzee Ally Gola,ambapo kadi 25 zilitolewa kwa Wazee.
Mmoja wa Wazee akimshukuru Mbunge Ridhiwani Kikwete kwa kuwapatia msaada wa kadi za matibabu,kulia ni Diwani wa Kata ya Ubena-Zomozi,Nicholaus Muyuwa akishuhudia.

RAIS DKT. MAGUFULI ASALI IBADA YA DOMINIKA YA TANO YA PASAKA KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU PETRO PAROKIA YA OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na waumini wengine wa Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay wakishiriki Ibada ya Dominika ya Tano ya Pasaka katika Kanisa hilo jijini Dar es Salaam leo tarehe 19 Mei 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mtoto ambaye ni muumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam mara baada ya Ibada Kanisani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mtoto ambaye ni muumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam mara baada ya Ibada Kanisani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Padre Dkt. Alister Makubi pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro mara baada ya Ibada katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

SEMINA ENDELEVU YA WATALAAM WA SEKTA YA UJENZI YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Dk.Boniface Bulamile akizungumza na watalaam wa sekta ya ujenzi (hawapo pichani) wakati akifungua semina endelevu ya watalaam wa Sekta ya ujenzi nchini ya kuwajengea uwezo watalaam wa sekta hiyo na kujadili mikataba ambayo inawaongoza katika utekelezaji wa majukumu yao iliyofanyika jijini Dar es Salaam (kulia) QS Albert munuo. Kaimu Msajili wa Bodi hiyo. 
(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON)
Watalaam wa ujenzi wakifuatilia mada mbali mbali katika semina endelevu kwa ajili ya kujadili mikataba ambayo inawaongoza katika utekelezaji wa majukumu yao ilioandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu na Wakadiriaji Majenzi (AQRB),
Baadhi ya Watalaam wa ujenzi wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa semina endelevu kwa ajili ya kujadili mikataba ambayo inawaongoza katika utekelezaji wa majukumu yao ulioandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu na Wakadiriaji Majenzi (AQRB)

MAKUMBUSHO YA TAIFA YAJIPANGA KUTUMIA MITANDAO KUITANGAZA

$
0
0

KAIMU Mkurugenzi mkuu wa Kijiji cha Makumbusho ya Taifa Agnes Robart amesema ili kuendena na mabadiliko ya teknolojia wao kama Makumbusho ya Taifa wamejipanga kikamilifu kutumia mitandao mbalimbali ili kuendelea kuitangaza Makumbusho hiyo. 

Amesema wamejipanga vizuri huku akiwataka wazazi kuhamasika kutembelea Makumbusho kwa lengo la kuendelea kurithi tamaduni mbalimbali hususani za kale. 

Agnes ameyasema hayo leo hii jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari katika kilele cha siku ya Makumbusho Duniani ambapo amesema lazima tuendelee kuenzi tamaduni za asili nchini. 

" Hii Makumbusho inaazimishwa kila ifikapo Mei 18 kila mwaka na lengo nikujifunza Mila na desturi ambazo wazee wetu wametuachia "amesema Agnes 

Akizungumzia Makumbusho ya Taifa amesema Makumbusho hiyo imeandaa tamasha la mama na mwana ambalo linalenga wazazi na watoto kujifunza juu ya kurithi wao. 

Pia katika kauli mbiu ya mwaka huu ni Makumbusho ni" kitovu cha utamaduni :Hatma ya mila na Desturi " na katika jijini cha Makumbusho wanafanya mambo mengi. 

Mkurugenzi Agnes amesema katika kijiji cha Makumbusho vitu vingi vya kiutamaduni ikiwa pamoja nyumba za makabila mbalimbali kama vile Wangoni,wasukuma,wakwere,wachaga,na makabila mengine. 

Pia amesema kuna shughuli mbalimbali za kitamaduni zinafanywa kama vile vyakula vya asili ,maharagwe yanayoungwa kwa nazi,mboga za majani,ugari wa muhogo,na mambo mengine mbalimbali. 

Pia ametoa wito kwa watanzania kujitokeza katika Makumbusho hayo kwa lengo la kuona mambo mbalimbali yaliyopo ndani ya kijiji hicho cha Makumbusho nakwamba kufanya hivyo ni kuendelea kulinda na kujifunza utamaduni wa Taifa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kijiji cha Makumbusho ya Taifa Agnes Robart( kushoto) aliyevaa kofia akisikiliza Maswali Kutoka Mwandishi wa Habari Bakari Lulela katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Makumbusho Duniani.yanayoendelea sasa katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar Es Salaam.

TCRA yafunika Kampeni ya Mnada kwa Mnada mkoani Morogoro.

$
0
0
 Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na wananchi katika Mnada mkoani Morogoro.
Baadhi ya wadau mawasiliano wakiwa katika Mnada wa mkoani Morogoro.

 Afisa wa Mamlaka ya Vitambulusho vya Taifa akiwapa maelezo wananchi walipotembelea Banda hilo katika Mnada mkoani Morogoro.
 Wananchi wakiwa katika foleni ya usajili wa Vitambulusho vya Taifa katika Mnada mkoani Morogoro ikiwa ni Kampeni ya TCRA ya kutoa elimu ya usajili wa simu kwa njia ya alama za vidole.. 
 Meneja wa Duka la Vodacom mkoani Morogoro Ntugwa Jidayi akiwapa maelezo Watendaji wa TCRA walipitembelea Duka hilo.
 Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano kwa Watumiaji Mawasiliano Thadayo Ringo akitoa maelezo kwa wananchi katika Mnada mkoani Morogoro ikiwa ni Kampeni ya TCRA ya Mnada kwa Mnada wa utoaji elimu ya usajili wa simu kwa njia ya alama za Vidole.

WAZIRI LUGOLA AWATULIZA MADEREVA WALIOTAKA KUGOMA NCHINI, AAGIZA WAMILIKI WA MAGARI KUTOA MIKATABA YA KAZI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Bwalo la JKT Umwema, mjini Morogoro, leo. Waziri Lugola amewatuliza madereva wa vyombo vya moto waliotaka kugoma kutokana na kutopewa mikataba ya kazi, matumizi mabaya ya tochi pamoja na ulipaji wa faini na kusimamishwa hovyo na matrafiki mabarabarani. Lugola mewataka wamiliki wa vyombo vya moto nchini kutoa mikataba ya kazi kwa madereva na wafanyakazi mbalimbali katika makampuni yao. Katikati ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbrod Mutafungwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kushoto), akifurahi jambo wakati alipokua anamsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji Nchini, Chuki Shaban alipokuwa akizungumza katika kikao cha Wadau wa usafirishaji kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bwalo la JKT Umwema, mjini Morogoro, jana. Waziri Lugola amewatuliza madereva wa vyombo vya moto waliotaka kugoma kutokana na kutopewa mikataba ya kazi, matumizi mabaya ya tochi pamoja na ulipaji wa faini na kusimamishwa hovyo na matrafiki mabarabarani. Kushoto ni Naibu Waziri wa kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kushoto), akifurahi jambo wakati alipokua anamsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji Nchini, Chuki Shaban alipokuwa akizungumza katika kikao cha Wadau wa usafirishaji kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Bwalo la JKT Umwema, mjini Morogoro, jana. Waziri Lugola amewatuliza madereva wa vyombo vya moto waliotaka kugoma kutokana na kutopewa mikataba ya kazi, matumizi mabaya ya tochi pamoja na ulipaji wa faini na kusimamishwa hovyo na matrafiki mabarabarani. Kushoto ni Naibu Waziri wa kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde. 

Hospitali ya Benjamin Mkapa Kuendesha Kambi Upasuaji wa Matundu Madogo (Endoscopic Surgery)

$
0
0
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) itaendesha kambi kwa ajili ya upasuaji wa matundu madogo (Endoscopic Surgery) kuanzia tarehe 7 mpaka 21 mwezi Juni, 2019.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Januarius Hinju, anasema kambi hiyo ya wiki mbili itaendeshwa kwa ushiriano kati ya madaktari bingwa wa BMH na wenzao kutoka Marekani.

“Tunawakaribisha watanzania na hasa wakazi wa Dodoma na mikoa ya jirani wenye matatizo ya uzazi, kutokushika mimba, ngiri (hernia) waje BMH kuanzia sasa kwa ajili ya uchunguzi ili watakaokutwa na matatizo wapangiwe huduma hiyo ya upasuaji wakati wa kambi hiyo,” anasema Dkt Hinju, ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa BMH.

Dkt. Hinju anasema upasuaji wa matundu madogo ni upasuaji wa kisasa ambao una faida kubwa kwa mgonjwa kulinganisha na upasuaji wa kawaida. 

Alitaja baadhi ya faida hizo kuwa ni pamoja na muda mchache anaotumia mgonjwa kupona baada ya upasuaji, maumivu kidogo pamoja na mgonjwa kutokutokwa na damu nyingi wakati wa upasuaji. 

BMH inaendesha kambi hii yenye lengo la kuimarisha huduma za kibingwa kwa mwaka wa pili mfululizo katika Hospitali hiyo. Kambi ya kwanza ilifanyika Julai mwaka jana.

Imetolewa na Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano
Hospitali ya Benjamin Mkapa
 Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Akinamama Wakifanya Upasuaji wa Kutumia Matundu Madogo (Endoscopic Surgery)  Katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Hivi Karibuni.


Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Akinamama Wakifanya Upasuaji wa Kutumia Matundu Madogo (Endoscopic Surgery)  Katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Hivi Karibuni.

VIJANA WILAYANI MUHEZA WATAKIWA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO VIDOGO

$
0
0
KATIBU Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mlingano Jimbo la Muheza wilayani Muheza Waziri Mohamed amewataka vijana wilayani humo kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt John Magufuli.

Waziri ambaye pia ni Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Tanga aliyasema hayo wakati aliofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Mlingano Jimbo la Muheza aliyoijenga kwa kutumia kiasi cha milioni 7.4
Kwa mujibu wa Katibu huyo ameamua kujenga ofisi hiyo kutokana na kwamba kata hiyo kutokuwa nayo kwa muda mrefu na hivyo kuona haja ya kuhakikisha ujenzi huo unafanyika ili kuwawezesha viongozi kutekeleza wajibu wao wa kukijenga chama hicho.

Aidha alisema pia iwapo vijana watatumia muda wao kufikiria namna ya kujikita kwenye uanzishwaji wa viwanda hivyo utawasaidia kuweza kujiajiri na kuweza kuisaidia jamii kwa kutoa ajira kwa wenzao na hivyo kuchangia pato la mkoa na Taifa kwa ujumla.

“Lakini pia vijana wenzangu tuunge mkono juhudi za serikali kwa kushiriki kwenye miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yetu kwa kujitoa na hivyo kuchochea kasi ya ukuaji maendeleo katika jamii zinazotuzunguka “Alisema.
Muonekano wa Jengo la Ofisi ya CCM kata ya Mlingano wilayani Muheza ambalo limejengwa na KATIBU Mwenezi wa Kata ya Mlingano Jimbo la Muheza ambaye pia ni Katibu Hamasa Chipukizi wa UVCCM Mkoa wa Tanga Waziri Mohamed Waziri kwa asilimia 90 ambapo mpaka kukamilika kwake ametumia kiasi cha milioni 7.4
KATIBU Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mlingano wilayani Muheza Waziri Mohamed ambaye pia ni Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Tanga

MAHAKAMA YA AFRIKA KUHAMASISHA WADAU NCHINI DJIBOUTI

$
0
0
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) yenye makao yake makuu jijini Arusha itafanya ziara ya kikazi nchini Djibouti ili kukutana na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali kwa lengo la kuiitangaza Mahakama hiyo ya Umoja wa Afrika (AU). 

Ujumbe wa ziara hiyo inayoanza Mei 21 hadi Mei 24 pia unatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu wa Djibouti, Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri wa Sheria na Spika wa Bunge . 

Rais wa Mahakama ya Afrika, Mheshimiwa Jaji Sylvain Ore’, alisema wakati wa ziara hiyo itaendeshwa semina inayolenga kukuza uelewa wa wadau hao juu ya uwepo wa Mahakama na jinsi inavyoendesha shughuli zake ikiwemo kupokea mashauri. 

Kwa mujibu wa Jaji Ore’,Uelewa wa wadau hao kuhusu uwepo wa AfCHPR pia utaleta hamasa kwa nchi nyingi zaidi za AU kuridhia itifaki iliyoanzisha mahakama hiyo na kutoa tamko rasmi la kutambua na kukubali mamlaka ya Mahakama hiyo kuweza kupokea kesi za watu binafsi na Mashirika yasiyo ya kiserikali(NGOs). 

“Ili Mahakama iweze kufanikisha malengo yake na pia kuimarisha mfumo wa Haki za Binadamu barani Afrika,nchi nyingi za Umoja wa Afrika hazina budi kuridhia itifaki iliyounda Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kwa mujibu wa kifungu cha 34(6)”,Alisisitiza Jaji Ore’. 

Tangu mwaka 2010,Mahakama hiyo ya Afrika imefanikiwa kuendesha programu mbalimbali zinazolenga kutoa elimu ya uwepo wa AfCHPR pamoja na shughuli zake katika baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Chad,Ethiopia,Afrika ya Kusini,Ghana,Malawi,Kenya,Uganda,Zambia,Morroco na Tunisia.Nchi nyingine ni IvoryCoast,Cape Verde,Jamhuri ya Kiarabu ya Sahrawi,Misri na GuineaBissau. 

AfCHPR ilianzishwa mwaka 2006 na ilianza shughuli zake rasmi mwaka 2008.
 African Court in Arusha, Tanzania
Rais wa Mahakama ya Afrika, Mheshimiwa Jaji Sylvain Ore’,

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU ULIPAJI WA BILI YA HUDUMA YA MAJI KILA MWEZI.

Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images