Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

MBUNGE MALEMBEKA AHAMASISHA WATANZANIA KUPENDA KWENDA HIFADHI ZA UTALII

$
0
0

Na Heri Shaban,Dodoma 

MWENYEKITI wa Taasisi ya Utalii 255  ambaye pia ni   Mbunge wa Mkoa wa kaskazini Unguja Angelina Malembeka  ,amewahamasisha Watanzania  kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi za Mbunga za Utalii, zilizopo nchini ili  kujifunza utalii wa ndani na kuona vivutio vilivyopo.

Mbunge Malembeka aliyasema hayo Bungeni Dodoma leo  wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada kupokea wageni wake ,Wahamasishaji wa Kundi la Utalii 255 kutoka Tanzania Bara leo walishiriki kusikiliza kikao cha maswali na majibu Bungeni Dodoma.

Alisema ziara ya Wahamasishaji wa Utalii wa 255 Kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar wapo katika ziara ya siku tatu ,wameanza kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kesho Mei 4 ziara inaelekea kutembelea Mbuga ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangile Mkoa wa Mnyara.

"Hii ni sehemu ya  kampeni ya kutangaza Utalii wa ndani ,kundi la Utalii 255 linawataka Watanzania kuweka mazoea ya kutembelea hifadhi za Taifa kuangalia mambo mbalimbali  ikiwemo wanyama kama sehemu ya kujifunza"alisema Malembeka

Alisema Utalii 255 ilianzishwa hivi karibuni,ikiwa na lengo la kuwahamasisha na kuwakumbusha Watanzania kuweza kujiwekea utaratibu wa kutembelea Hifadhi na Vivutio vya Utalii vilivyopo Nchini, Ziara hii imewashirikishaka Vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar. 



DHANA YA AFYA MOJA KUTUMIKA KUDHIBITI MAGONJWA AMBUKIZI MAENEO YA MIPAKANI

$
0
0
Dhana ya Afya moja ambayo hujikita katika kujumuisha sekta zote za Afya katika kujiandaa, kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayomuathiri binadamu imeendelea kufundishwa kwa Wataalamu wa sekta hizo za Afya, ikiwa ni Sekta ya Afya  ya Binadamu, Wanyamapori, Mifugo, Kilimo na Mazingira, ili wataalamu hao watumie dhana hiyo kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama  ambayo hutokea mara kwa mara katika maeneo ya mipakani kutokana na kuwepo kwa  mwingiliano mkubwa kati ya  watu na wanyama katika mazingira yao.

Pamoja na Mwingiliano huo wenye faida kubwa kiuchumi lakini pia unasababisha kuenea kwa vimelea   kwa uharaka zaidi na kusababisha magonjwa kwa binadamu, wanyama na mimea katika mazingira yao, hivyo ili kuimarisha Afya ya binadamu, Shirika la Chakula na Kilimo  la Umoja wa Mataifa (FAO), pamoja  na watalaamu kutoka Wizara ya Mifugo na  Uvuvi, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine wamewapa mafunzo wataalamu wa sekta za Afya wanao toka katika Halmashauri za Mkoa wa Mbeya na Songwe zilizo mipakani juu ya namna ya kujiandaa na kukabili magonjwa ambukizi kama  vile Ugonjwa wa Kimeta kwa kutumia Dhana ya Afya  moja.

Akiongea wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika kuanzia tarehe 29 Aprili hadi,tarehe 3 Mei, 2019, Mkoani Songwe, Mkurugenzi wa Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, ambaye aliwakilishwa na Mratibu Kitaifa, Dawati la Kuratibu Afya Moja, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka,  alibainisha kuwa ushirikiano wa wataalam na sekta za Afya  kwa kutumia dhana ya Afya Moja hivi sasa ni agenda ya dunia nzima. Aidha, alieleza kuwa Dhana hiyo imekusudiwa kutumika maeneo ya mipakani   ambapo mwingiliano huo huchochewa na wasafiri kutoka eneo moja kwenda jingine, ongezeko la watu duniani, mabadiliko ya tabia nchi,  utandawazi, ongezeko la mahitaji ya maji na chakula.

Awali akiongea katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo nchini, Dkt. Hezron Nonga alibainisha kuwa  sekta za Afya zikishirikiana katika Kudhibiti magojwa zitasaidia kuimarisha Afya ya Binadamu kwa kuwa kila sekta itakuwa inachukuwa tahadhri kwa wakati. Aidha alibainisha kuwa  vimelea vingi vinavyo sabababisha magonjwa kwa binadamu asilimia (60%) vinatoka  kwa wanyama pori na mifugo na maambukizi yanatokea pale binadamu anapoingilia maskani ya wanyama hao bila tahadhari, hivyo Afya moja ikitumika maeneo ya mipakani itasaidia kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi yanayotokana na shughuli za mwingiliano wa wanyama na binadamu zinazofanyika sana maeneo ya mipakani.

Katika kuhakikisha watalaam hao kutoka sekta za Afya wanaweza kutumia Dhana  hiyo katika kudhibiti magonjwa katika maeneo ya mipakani wameweza kujengewa uwezo wa namna ya kutoa taarifa za milipuko ya magonjwa ambukizi kama vile ugonjwa wa Kimeta, pindi unapotokea maeneo ya mipakani, Namna ya kuunda vikosi vya kufuatilia na kukabili Ugonjwa, Mawasiliano wakati wa kufuatilia na kukabili magonjwa hayo kwa kutumia Dhana ya Afya moja,  pamoja na masuala ya kutumia vifaa Kinga Binafsi vya Kitaalamu.

Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughuli za Afya moja nchini. Kwa kutambua umuhimu huo  Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja  kwa kushirikiana Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) waliandaa na kuratibu mafuzo hayo.
 Mwezeshaji wa Mafunzo ya kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama, kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Profesa, Rudovick Kazwala, akifundisha kwa vitendo namna ya kutumia Vifaa vya kitaalam vya Kinga Binafsi, wakati wa mafunzo hayo kwa wataalamu wa sekta za Afya  kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya katika Halmashauri zilizopo mipakani, Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe.
 Baadhi ya wataalamu wa sekta za Afya  kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya kwa Halmashauri zilizopo mipakani wakiwa wamevaa vifaa vya Kitaalamu vya Kinga Binafsi, wakati wa  Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe.
 Mratibu wa Kitaifa, Dawati la Afya moja, lililopo Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka, akisisitiza  umuhimu wa sekta za Afya kushirikiana wakati wa mafunzo ya kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama kwa wataalamu wa sekta za Afya  kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya katika Halmashauri zilizopo mipakani, Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe
 Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo nchini, Dkt. Hezron Nonga akisisitiza  umuhimu wa kutumia Dhana ya Afya moja wakati wa mafunzo ya kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama kwa wataalamu wa sekta za Afya  kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya katika Halmashauri zilizopo mipakani, Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe
 Mwezeshaji wa Mafunzo ya kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama, kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, Niwael Mtui,  akifundisha namna ya kudhibiti magonjwa ambukizi maeneo ya mipakani wakati wa mafunzo hayo kwa wataalamu wa sekta za Afya  kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya katika Halmashauri zilizopo mipakani, Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe.
 Baadhi ya wataalamu wa sekta za Afya  kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya katika Halmashauri zilizopo mipakani, wakiwa katika makundi ya majadiliano wakati wa mafunzo ya Kuimarisha Udhibiti wa magonjwa ambukizi kwa kutumia Dhana ya Afya moja kwa maeneo ya mipakani, Mafunzo  hayo yamefadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe.
 Mwezeshaji wa Mafunzo ya kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama, kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Emmanuel Swai, akifundisha namna ya kudhibiti magonjwa ambukizi maeneo ya mipakani, wakati wa mafunzo hayo kwa wataalamu wa sekta za Afya  kutoka Mkoa wa Songwe na Mbeya katika Halmashauri zilizopo mipakani, Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe.
Washiriki wa Mafunzo ya Kuimarisha Udhibiti  wa  magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama kwa kutumia Dhana ya Afya moja wakiwa katika picha ya pamoja. Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa na Kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Dawati la Kuratibu Afya moja, tarehe 29 Aprili hadi 3Mei, 2019, mkoani Songwe.


Waganga Wakuu wa Mikoa wapewa Siku 30 kutathmini utendaji wa Kamati za afya za Mikoa na Wilaya

$
0
0
Waganga wakuu wa Mikoa Tanzania Bara wamepewa mwezi mmoja kuhakikisha kuwa wanazifanyia tathmini ya kina kamati za Uendeshaji Huduma za Afya za Mikoa na wilaya zao kuona kama zinaendana na kasi ya mabadiliko yanayokusudiwa na Serikali ya awamu ya tano.
Agizo hilo limetolewa jana mjini Songea na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt.Dorothy Gwajima wakati akizungumza  na wajumbe wa kamati ya Uendeshaji Huduma za Afya ya Mkoa wa Ruvuma pamoja za Halmashauri za wilaya ya  Namtumbo na Songea pamoja na Manispaa ya Songea.

Amesema anawapa siku 30 Waganga wakuu wa Mikoa yote kuhakikisha kuwa wanafanya tathmini ya wajumbe waliopo katika ofisi zao kama wanatosha kuendelea na nyadhifa zao za kusimamia jukumu la uendeshaji huduma za afya katika mikoa na halmashauri zao.
Dkt Gwajima ameongeza kuwa endapo itabainika kuwa baadhi ya wajumbe wa kamati hizo hawana sifa zinazowafanya kushindwa kutekeleza majukumu yao ya usimamizi na uendeshaji huduma za afya katika maeneo yao, waganga wakuu wa mikoa watalazimika kuwaweka pembeni wajumbe hao na kuunda upya kamati ambazo zitaweza kuiendeleza agenda ya mabadiliko katika sekta ya afya.

“Kinyume na hapo katika ziara hizi ninazoendelea kuzifanya mikoani nikikuta yupo Mganga Mkuu ambaye ametulia tu, mapungufu katika vituo bado yapo na amewezeshwa na serikali, ajue wazi kuwa wa kutokutosha wa kwanza atakuwa yeye,” amesema Dkt Gwajima na kuongeza:
“Haiwezekani tukute mapungufu madogo kabisa katika vituo, ambayo yangeweza kuonwa na wao walioko huko eti hayaonekani hadi tuje sisi kutoka Tamisemi ndiyo mapungufu hao yafanyiwe kazi,”amesisitiza Dkt Gwajima.
Naibu Katibu Mkuu huyo ameonya tabia iliyojengeka miongoni mwa wajumbe wa kamati za uendeshaji huduma ya afya kukimbilia kuomba msamaha pindi zinaposhindwa kutekeleza majukumu yake kwa makusudi.

Amesema huu ni wakati wa kuboresha sekta ya afya katika vituo vya afya na zahanati kwa kuhakikisha kuwa mazingira ya utoaji huduma yanaboreshwa ili yaweze kuwavutia wananchi wengi kukimbilia kupata huduma katika zahanati na vituo vya afya vinavyomilikiwa na serikali.
Dkt Gwajima amesema kuwa kamwe hatawapa nafasi wajumbe wa kamati za uendeshaji huduma za afya wa mikoa na wilaya ambao siku zote wamekuwa ni watu wa visingizio vya kuomba kusamehewa ama kupewa muda kuwa wamefahamu mapungufu yao.
Amesema angependa kuona kamati za uendeshaji huduma za afya katika  mikoa na halmashauri zikijikita katika kuongelea mambo makubwa yanayolenga kuishirikisha sekta na serikali kuu.

“Hivi vitu vidogo vidogo vya kitaalamu tubebe sisi wenyewe, wananchi wametuunga mkono, tumeweza kushirikiana nao kujenga zahanati na vituo vya afya katika mikoa na halmashauri zetu hivyo ni jukumu letu sasa kuhakikisha kuwa tunatoa huduma bora za afya kwa wananchi,” amesema.
Kwa mujibu wa Dkt.Gwajima, katika ziara zake alizokwisha zifanya katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Njombe na Ruvuma amejionea mapungufu mbalimbali ya utoaji wa huduma bora za afya katika vituo vya afya na zahanati.

Ameongeza kuwa mapungufu hayo ambayo ameyashuhudia kwenye vituo vya afya na zahanati zinazomilikiwa na umma yametokana na watendaji hao  kutopata usimamizi unaostahili kutoka kwa kamati za usimamizi  na uendeshaji wa huduma za afya za mikoa na halmashauri husika.
Dkt Gwajima anaamini kuwa kushindwa kwa kamati za uendeshaji ndiko kulikopelekea kukithiri kwa uchafu katika majengo ya vituo vya afya na zahanati nchini licha ya vituo hivyo kuwa na fedha za uendeshaji wake.

Sambamba na kuwataka waganga wakuu wa mikoa kuzitathmini kamati hizo, Dkt Gwajima amewataka waganga wakuu wote kutambua kuwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Magufuli ana agenda moja tu ya kuleta mabadiliko katika sekta ya afya.
 “Hatutapimwa kwa idadi ya semina au vituo vya afya tulivyojenga bali kwa ubora wa kazi za kuhudumia wananchi,” amesema.
Dkt Gwajima amebainisha mapungufu kadhaa aliyoyaona kwenye ziara yake kuwa ni pamoja kuwepo kwa malalamiko toka kwa wagonjwa na  kukosekana kwa takwimu sahihi za utendaji kazi 

Akiwa katika kituo cha afya Mjimwema Manispaa ya Songea Naibu Katibu Mkuu Dkt.Gwajima alipokea kero za wagonjwa kuhusu uwepo wa kauli mbaya toka kwa wauguzi na tatizo la ukosefu dawa hususan  akina mama wajawazito 
“Hapa Mjimwema nimebaini kasoro nyingi mojawapo kauli mbaya za watumishi na tatizo la dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa ” Dkt .Gwajima alionya.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt.Jairy Khanga ameahidi  kuchukua hatua za mapema kufanya mabadiliko ya utendaji kazi wa kamati za usimamizi wa huduma za afya katika mkoa wa Ruvuma .

 Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI (Afya) Dkt. Dorothy Gwajima akiongea na wajumbe wa kamati za usimamizi huduma za Afya mkoa na wilaya za Namtumbo,Songea na Songea Manispaa jana katika ukumbi wa mikutano uliopo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Songea.
  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt. Jairy Khanga akiongea wakati wa kikao cha Naibu Katibu Mkuu -TAMISEMI anayeshughulikia Afya alipofanya kikao na kamati za usimamizi wa huduma za afya wilaya za Songea,Namtumbo na Songea Manispaa  
 Sehemu ya wajumbe wa kamati za usimamizi wa huduma za afya mkoa na zile za Halmashauri za Songea ,Namtumbo na Songea Manispaa wakifuatilia maelekezo ya Naibu Katibu Mkuu-OR-TAMISEMI (Afya) Dkt.Dorothy Gwajima(hayupo pichani).Kikao hiki kilifanyika mjini Songea jana.
 Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI (Afya) Dkt.Dorothy Gwajima wa kwanza kulia akiongea na ndugu wa wagonjwa kusikiliza kero zao alipotembelea na kukagua kituo cha Afya Mjimwema Manispaa ya Songea jana. Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma.

TAARIFA YA UTEUZI

Ujenzi wa Chuo cha VETA Rukwa kuondoka na vigogo wa VETA na Wizara ya Elimu

$
0
0
Waziri wa Elimu nchini Prof. Joyce Ndalichako amethibisha kuunda kamati itakayoshughulikia namna mkandarasi anayeendelea na ujenzi wa chuo cha Ufundi Stadi (VETA) mkoani Rukwa alivyopata zabuni na kumtaka mkandarasi huo ajieleze sababu zilizopelekea kuidanganya serikali katika mkataba wake ulioonyesha uwepo wa vifaa vya kazi katika eneo la ujenzi huku eneo hilo likiwa tupu na kazi zake kufanyika bila ya wataalamu na vifaa vilivyoorodheshwa kwenye mkataba.

Ameongeza kuwa Kamati hiyo pia itashughulikia kuona endapo thamani ya fedha iliyotolewa na serikali inaendana na majengo yaliyojengwa katika eneo hilo ambalo yalitakiwa kujengwa majengo 22 ambapo hadi sasa ni majengo 13 tu kikiwepo kibanda cha mlinzi ndio yameanza kuinuka. Wakati mkandarasi hiyo akitakiwa kukabidhi majengo hayo mwezi Septemba 2019 hadi sasa ujenzi huo umefikia asilimia 25 tofauti na makubaliano ya mkataba aliotakiwa kufikia asilimia 61 hadi mwezi Mei.

Katika kuhakikisha wahusika wanashughulikiwa Prof Ndalichako alimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa VETA nchini kuwachukulia hatua wale wote waliohusika na kumuidhinisha mkandarasi (post qualification) aliyepewa zabuni pamoja na kumtaka kumchukulia hatua Mkurugenzi wa VETA kanda ya nyanda za juu kusini kwa kuonyesha kumtetea mkandarasi ambaye hana uwezo wa kazi.

“Wakandarasi wanaofanya kazi na Wizara ya Elimu badilikeni, kwakweli miradi yangu yote nitaendelea kuipitia na nitaendelea kuchukua hatua kali kwa wale wakandarasi ambao wanapata kazi kwa kiujanja ujanja, kwanza nitashughulika na watu wangu wa kitengo cha manunuzi, hebu angalia vifaa kama hivyo, kuna Afisa wa wizara ambae anapata mshahara ate serikali na alikwenda akathibitisha akasema vifaa viko vizuri akaandika na ripoti, naoma Mkurugenzi Mkuu anza na hao waliofanya “post qualification” kabla y ahata kamati haijaja kufanya kazi wengine ambao watakumbwa sasa ni baada ya kamati kufanya kazi, lakini Mkurugenzi wako wa Kanda hakufai kwasababu anaonekana yeye ni dalali wa Mkandarasi” Alisisitiza.

Amesema hayo baada ya kutembelea ujenzi wa chuo cha ufundi Stadi VETA katika eneo hilo la Kashai lililopo katika Manispaa ya Sumbawanga na kuonyesha kutoridhishwa na kuelekeza kuwa kabla ya kuendelea na ujenzi huo lazima vifaa vinavyotumika katika ujenzi vipimwe kuonyesha kama vinastahili ama vinginevyo viondolewe katika eneo la ujenzi na mkandarasi huyo kuleta vifaa vingine kwa gharama yake.

Awali wakati akisoma taarifa ya ujenzi wa chuo hicho Mkurugenzi wa Kanda wa chuo cha VETA Justine Rutta alisema kuwa changamoto kubwa iliyokuwapo ni mkandarasi huyo kucheleweshewa malipo yake na hivyo anaidai serikali shilingi 51,039,153.59 hali iliyosababisha kuchelewa kuendelea na ujenzi.

“Kwahiyo kwenye hela nayotakiwa kulipwa inaongezeka deni hilo ambalo ni kwaajili ya kucheleweshewa ulipaji, hali ya malipo kwa mshauri wa mradi, ameshalipwa tayari shilingi 1,051,144,000 tangu aanze kufanya kazi hii na nyingine alitakiwa kulipwa mara atakapofikia hatua ya kuweka sakafu, kwahiyo hatudai fedha yoyote mpaka sasa, changamoto katika mradi huu ndio kubwa mradi umeweza kuchelewa kwasababu ya kuchelewa kulipwa kwa mkandarasi,” alisema.

Katika hatua nyingine, Prof. Ndalichako alibaini uwepo wa kampuni nyingine mbili zinazohusika na ujenzi wa chuo hicho, kampuni ambazo serikali haikuingia nazo mkataba na baada yakuulizwa mhandisi wa ujenzi huo (site engineer) aliyefahanmika kwa jina la Jin alisema kuwa kampuni hizo zilisaini mkataba na Tender International kwaajili ya kuwapata vijana wa kufanya kazi, kuwasimamia pamoja na kusimamia malipo ya vijana hao.

Prof. Ndalichako alisikitishwa na kitendo cha mkandarasi huyo kuingia mikataba na kampuni nyingine ambazo hazikidhi viwango vya utekelezaji wa miradi ya serikali kwani kati ya kampuni hizo moja inayoitwa Aricom Building Constractors limited ilikuwa na daraja 7 na nyingine Laicom Building Construcors ilikuwa na daraja 4. Na aliyagundua hayo baada ya kutaka kuonyesha mikataba ya wafanyakazi wa ujenzi huo.

Tarehe 31/8/2019 mkandarasi Tender International alikabidhiwa kiwanja kwaajili ya kuanza ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) katika Manispaa ya Sumbawanga ambapo mshauri Elekezi wa Mradi huo ni Sky Architect Consultancy Ltd na mradi huo kutegemewa kukamillika mwezi Septemba 2019 huku gharama za mradi huo ikiwa shilingi 10,700,488,940.05 na tarehe 22/11/2018 alilipwa shilingi 1,272,138,424.64. na tarehe 11/4/2019 alilipwa shilingi 835,598,299.01 na kufanya jumla ya Shilingi 2,107,736,723.65 ya malipo kwa Mkandarasi huyo ambayo ni sawa na asilimia 25 ya malipo yote.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akikagua moja ya gari lililoorodheshwa kwenye mkataba wa ujenzi kuwa ni tipa la tani 7 jambo ambalo ni kinyume na uhalisia.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako na wataalamu mbalimbali kutoka Chuo cha VETA taifa pamoja na Mkoa wakiangalia miongoni mwa matipa 11 yaliyoorodheshwa kwenye mkataba wa ujenzi baina ya Tender Internattional na Chuo Cha Ufundi VETA yakiwa hayafanyi kazi.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimtahadharisha mhandisi wa ujenzi Site engineer) aliyejilikana kwa jina la Jin ambaye mkataba hauonyeshi mtu huyo kuhusika na ujenzi huo

SPIKA NDUGAI AONGOZA HARAMBEE UJENZI WA VYOO SHULE YA MSINGI KARUME MKOANI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai akizungumza na wananchi wa Kibaigwa wakati wa harambee kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi wa Shule ya Msingi Karume iliyopo Kibaigwa Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. Katika harambee hiyo mifuko 763 ya Saruji ilipatikana, fedha kiasi cha Sh. 2, 645, 900 viliziweza kuchangwa ambapo taslimu ilikuwa ni 1,225, 900 na Ahadi 1, 420, 000/=
 Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa,. Job Ndugai (wa pili kushoto) akiongozana  na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa wakati alipowasili na kwenda kukagua ujenzi wa vyoo vya wanafunzi wa Shule ya Msingi Karume iliyopo Kibaigwa Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
 Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (wa tatu kulia) akimsikiliza Afisa elimu Kata ya Kibaigwa, Ndg. Adilla Muna wakati akikagua ujenzi wa vyoo vyaF wanafunzi wa Shule ya Msingi Karume iliyopo Kibaigwa Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
 Wananchi Mbali mbali wa Kibaigwa wakimsikiliza Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (hayupo kwenye picha) wakati wa harambee kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi wa Shule ya Msingi Karume iliyopo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. Katika harambee hiyo mifuko 763 ya Saruji ilipatikana, fedha kiasi cha Sh. 2, 645, 900 viliziweza kuchangwa ambapo taslimu ilikuwa ni 1,225, 900 na Ahadi 1, 420, 000/=

Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (wa pili kulia)akipokea zawadi ya mfuko wa saruji kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa, Ndg. Elisante Maleko (wa pili kushoto) tukio lililofanyika leo katika Shule ya Msingi Karume iliyopo Kibaigwa Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. Shirika la Bima la Taifa lilitoa mifuko 530 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi wa Shule ya Msingi Karume.

JAFO AMEZINDUA MADARASA MATATU KATIKA S/MSINGI MASANGANYA HUKO KISARAWE

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Suleiman Jafo amezindua vyumba vya madarasa matatu, katika shule ya msingi Masanganya ,kata ya Kibuta, wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Akizindua madarasa hayo ambayo yamejengwa na mkandarasi anayejenga reli ya kisasa SGR kupitia kampuni ya Yapi Merkezi kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC ) ,ameipongeza kampuni hiyo kwa kujenga madarasa hayo na kukarabati vyumba vingine vitano vya madarasa.

Jafo ,aliyataka makampuni mengine yaliyowekeza mkoani humo kuiga mfano uliofanywa na Yapi Merkezi kwa kupitia TRC kwani mkoa bado una changamoto mbalimbali kwenye sekta ya elimu .

Nae mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alieleza, mkoa huo bado unakabiliwa na changamoto kubwa ya upungufu wa vyumba vya madarasa 3,600.

Ndikilo, aliwataka walimu na wanafunzi kutunza miundombinu hiyo ili iweze kudumu kwa kipindi kirefu.

Akitolea ufafanuzi, hali ya kielimu kimkoa, alibainisha kwamba inazidi kuimarika kwani matokeo ya darasa la la saba kwa mwaka 2017 mkoa ulishika nafasi ya 19 kati ya mikoa 26 na kwa mwaka 2018 mkoa ulishika nafasi ya 11. 

Rais Dkt. Shein atowa Salamu za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akitowa Risara ya kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuaza wiki.(Picha na Ikulu)

MAKAMU WA RAIS MSTAAFU DKT BILAL AHANI MSIBA WA DKT REGINALD MENGI LEO KINONDONI JIJINI DAR

$
0
0
Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwasili kutoa pole na kuwafariji wafiwa nyumbani kwa marehemu Dkt Reginald Mengi Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Mwili wa Marehemu Dkt .Mengi unatarajiwa kuwasili kesho Jumatatu saa nane Mchana Katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere. 

VIONGOZI MBALIMBALI WAMIMINIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU DR REGINALD MENGI KUTOA SALAMU ZA POLE KWA FAMILIA

$
0
0
 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akitia saini katika kitabu cha Maombolezo ya Msiba wa Dk , Regnald Mengi nyumbani kwa Marehemu Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Humphrey Polepole, akisaini kitabu cha Maombolezo wa msiba wa Dr. Reginald Mengi Kinondoni Jijini Dar es Salaam
  Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akitoa pole kwa mmoja ya Wafiwa wa Msibani kwa Marehemu Dr. Reginald Mengi
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luaga Mpina akitoa pole kwa mmoja ya Wafiwa wa Msibani kwa Marehemu Dr. Reginald Mengi
 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akizungumza jambo na Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulya
 Mwenyekiti wa Wazalendo kwanza, Steve Nyerere akizungumza na Mkurugenzi wa Global Publisher Erick Shigongo Msibani kwa marehemu Mengi
Balozi Juma Mwapachu akizungumza na Mbunge Hawa Ghasia mara alipowasili kwenye Msiba wa Marehemu Dr. Reginald Mengi Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Wasanii wa Kundi la Uzalendo kwanza wakiteta jambo msibani kwa Marehemju Dr Reginald Mengi Kinondoni Jijini Dar es Salaam

DR MSHINDO MSOLLA AMBWAGA DR TIBOROHA KWA KISHINDO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Zoezi la kuhesabu kura za uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Yanga umemalizika na Dr Mshindo Msolla kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga kwa jumla ya kura 1276 katika Uchaguzi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Msolla amembwaga mpinzani wake Dkt Jonas Tiboroha aliyepata kura 60 huku kura 5 zikiwa zimeharibika.Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Fredirick Mwakalebela amefanikiwa kushinda nafasi hiyo baada ya kupata jumla ya kura 1206 kati ya kura 1341.

Mwakalebela amewapiku wenzake wanne ambao wote walikuwa wanawania nafasi hiyo kwa kura nyingi.Wagombea hao Titus Osoro alipata kura 17, Yono Kevela kura 31, Chota kura 12 na Janeth Mbeni akipata kura 61 na kura 21 zikiwa zimeharibika.

 Katika nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji waliochaguliwa ni Hamad Islam 1206, Engineer Mwaseba 1174, Dominick Ikute 1088, Kamugisha Kalokola 1072, Arafat Haji 1024, Salum Ruvila 976,Saad Khimji 788 na Rodgers Gumbo 776

Uchaguzi Mkuu wa Yanga umefanyika leo kwenye ukumbi wa Police Officers Mess Oysterbay na jumla ya wanachama 1341 walijitokeza kupiga kura.
Dr Mshindo Msolla Mwenyekiti mteule wa Klabu ya Yanga

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YAOMBWA KUHARAKISHW AMCHAKATO WA KUREKEBISHA SHERIA YA USALAMA BARABARANI

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamiii

Wito umetolewa kwa Serikali na watunga sera kuhakikisha wanapitia upya na kufanya mabadiliko katika sheria ya usalama barabarani hili kuweza kudhibiti ajali zinazotokana na uzembe wa watu kwa makusudi.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam leo na Kaimu Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA),Mary Richard alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani kwa umoja wa mataifa.

 "sheria hiyo kwa sasa ina mapungufu mengi kiasi mtu akikutwa na kosa adhabu zake ni za kawaida na makosa mengi yamebainishwa katika kanuni badal aya sheria yenyewe ametaja sheria hii inamtaja mtu aliyekaa siti ya mbele na Dereva ndio wanapaswa kufunga mkanda wakati kanuni inataja abiria wote wafunge mkanda jambo ambalo lina ukakasi kidogo"amesema Mary.

Mary ametaja kuwa sheria hii ya Sasa inaseama Dereva wa pikipiki ndio anapswa kuvaa kofia ngumu peke yake wakati sasa jeshi la Polisi ketengo usalama barabarani wameweka kanuni Dereva na abairia ndio wanapaswa kuvaa kofia hivyo ni bora vitu vyote hivi vingewekwa kwenye sheria hivyo tunaomba mamlaka zinazousika pamoja na Wizara ya Mambo ya ndani waangalie utaratibu wa kubadilisha sheria hii.

kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma , Fatma Toufiq amesema kuwa ajali za barabarani zinaepikika kama watanzania wote wataweza kufata sheria na kuwa makini pindi wanapoendesha vyombo vya moto.

amesema kuwa yeye kama mbunge anayeshiriki katika kutunga sheria atasimama kidete kuhakikisha sheria hii mpya ya usalama barabarani inapatikana hli tuweze kupunguza takwimu za ajali na walemavu wakudumu wanaotokana na ajali za barabarani
 Kaimu Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA),Mary Richard akizungumza na Waandishi juu wiki ya usalama barabarani 
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma , Fatma Toufiq, akieleza ushuhuda wake kwa waandishi wa habari juu ya ajali ilivyoweza kumletea cahangamoto ya utendaji katika kazi


Mratibu wa Usalama Barabarani kutoka shirika la umoja wa Mataifa la WHO,Mary Kessy akizungumza mpango wa shirika lake katika kudhibiti usalama barabarani
 
Muwakilishi wa Mabalozi wa Usalama Barabarani(RSA),John Seka akieleza namna taasisi yao ilivyojipanga na inavyoshirikiana na jeshi la Polisi kutoa taharifa za watu wanaokiuka sheria za Usalama Barabarani
Sehemu ya Waandishi wa habari walioshiriki Mkutano kuhusu Masuala ya Usalama barabarani leo jijini Dar es Salaam uliofanyika katika ukumbi wa Tamwa

LALA MASIKINI UAMKE TAJIRI,CHEZA NA USHINDE SASA BAHATI NASIBU YA BIKO

WAKAZI WA DAR ES WATAKIWA KUACHA POROJO NA KUFANYA KAZI

$
0
0
Na Humphrey Sahao, Globu ya Jamii.


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wakazi wa jiji hilo kuacha kutumia muda mwingi kuongelea mambo ya watu na kutumia muda huo kufanya kazi na kuzalisha hili kusaidia uchumi wa taifa hili.


Makonda amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa mbagala wakati wa kuhitimisha Tamasha la Shika Ndinga linaloendeshwa na kituo cha Radio cha EFM cha Jijini Dar es Salaam.


“kumekuwa na tabia ya ajabu sana katika mkoa huu watu wanatumia muda mwingi kuzungumza mbambo ya watu na kuacha kufanya kazi hali inayofanya wageni kutoka mikoa mingine kufika hapa na kufanya maendeleo na kuchukua fursa zilizopo huku wenyeji wakibaki kulalamika vibarazani”amesema Rc Makonda.


Ametaja kuwa Jiji la Dar es Dasalaam ndio jiji linaloongoza kwa fursa nyingi za kujipatia kipato lakini wazaliwa wa hapa wamebaki kuwa maskini kutokana na kufanya mambo yao kwa mazoea hivyo kuwataka sasa waamke na kutumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo.


Aidha makonda alitumia fursa ya kusanyiko hilo kuwakumbusha Vijana kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha katika Daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za Mitaa.


Pia amewataka Vijana kutumia muda huu kujitokeza kuchukua fomu na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.


 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na Wakazi wa Mbagala Zakhem wakati wa kuhitimisha fainali za shika ndinga jijini Dar es Salaam zinazoa andaliwa na kituo cha Radio  ya Efm.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akikabidhi zawadi ya gari kwa mshindi wa kike ambaye ametokea mkoa wa Mtwara.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikabidhi zawadi ya gari kwa Mshindi wa kiume ambaye ametokea mkoa wa Dodoma.
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambo sasa akieleza hali ya Usalama
 Washiriki wakiwa katika hatua ya kufungua Toelet Pepa 
 Washiriki wakiwa katikahatua ya kukimbia na kitenesi  
 Majaji wa shindano la shika ndinga wakiwa makini kusimamia mchuano katika Viwanja vya Zakhem 
 Washiriki wakiwa hatua ya fainali hili waweze kuchukua gari 
 Washiriki wakiwa hatua ya fainali hili waweze kuchukua gari
 Wageni wa Meza wa Meza kuu wakisuhudia washiriki wakiwa hatua ya fainali hili waweze kuchukua gari
 Eneo la uwanja wa mshindano ya shika ndinga linavyoonekana kwa juu 

--

RAIS WA ZANZIBAR ALHAJ Dk. Ali Mohamed Shein Atowa Salamu zac Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein amewanasihi wafanyabiashara kuwa waadilifu katika kuwafanyia wanunuzi tahafifu za bei za bidhaa na huduma nyenginezo hasa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alhaj Dk. Shein aliyasema hayo katika risala maalum aliyoitoa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari katika kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika mwaka huu wa 1440 Hijria sawa na mwaka 2019 Miladia.

Katika risala yake hiyo, Alhaj Dk. Shein aliwataka wafanyabiashara kukumbuka kwamba kwa kufanya hivyo hawatokula hasara bali watazidi kupata fadhila mbali mbali za Mola wao Mlezi zinazoambatana na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Aidha, aliwataka wakulima waendelee na ustaarabu pamoja na utamaduni wao ule ule wa ustahamilivu na uadilifu kwa kujiepusha na tabia ya uvunaji na uuzaji wa mazao machanga.

Rais Dk. Shein aliongeza kuwa lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar si kumkomoa mtu kwa sababu Serikali huwa haiwakomoi wananchi wake bali dhamira yake ni kuwalinda na kuona kwamba hawafikwi na matatizo ambayo yanaweza kuepukika na kujikinga nayo. 

Pamoja na hayo, Alhaj Dk. Shein alitoa nasaha zake kwa wale ambao si Waislamu na wale ambao watakuwa na dharura zinazowazuwia wasifunge kuwa wasifanye vitendo vitakavyoathiri wanaofunga.

Alhaj Dk. Shein alisisitiza haja ya kuhimizana zaidi kuisoma Qur-an kwa wingi ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na kujitahidi kufahamu mantiki ya maelekezo yake.

Aliwataka waumini kuhimizana kuhudhuria darsa katika misikiti ndani ya mwezi wa Ramadhani na kuepuka kutumia muda kwa kufanya mambo yasiyo na manufaa katika mwezi huo ambayo yanapingana na mafunzo ya Uislamu na silka zao.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein aliwatakia kila la heri Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi wakiongozwa na Spika Zubeir Ali Maulid katika Mkutano wao wa 14 wa Baraza la Tisa la Wawakilishi utakaojadili Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha wa 2019-2020.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein

MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 6,2019

The 5th UDSM Research Week Exhibitions, 6th to 8th May 2019.

MATUKIO YA PICHA MBALIMBALI KUFUATIA HALI YA MVUA KUNYESHA KATI YA JIJI LA DAR NA MKOA WA PWANI

$
0
0
 Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika maeneo mengi hapa jijini Dar es Salaam na mkoa wa Pwani kutokana na Mvua  kubwa iliyonyesha jana, ambapo  barabara nyingi za Dar zilijaa maji hali iliyosababisha baadhi ya magari  kuharibika na pia kusabaisa foleni kubwa ya magari,lakini pia inaonesha mitaro mingi ya kupitisha maji machafu kati kati ya jiji imeziba,hali inayochangia pia kutuama kwa maji.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi  Tv)






Limezima anasubiriwa fundi
 Gari likiwa limehariika katikati ya barabara ya Kilwa kata ya Mandege mkoa wa Pwani.
 Kama ionekanavyo pichani hapa wananchi  wakisukuma gari baada ya kukwama kwenye matope kufuatia Mvua zilizoanza kunyesha wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi  Tv)

BUNGE LA AFRIKA KUSHIRIKIANA NA BUNGE LA UMOJA WA FALME ZA KIARABU ( U.AE.)

$
0
0
Makamu wa Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akipokelewa na mwenyeji wake,Balozi wa UAE,nchini Afrika Kusini Mahash Saeed Alhameli kabla ya kikao cha majadiliano ya ushirikiano baina ya ujumbe wa Bunge la Afrika na ujumbe kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates- UAE) jana Mei 5,2019 jijini Pretoria,Afrika Kusini.
Kushoto ni Makamu wa Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza tete-a-tete na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates- UAE),nchini Afrika Kusini Mahash Saeed Alhameli.
Makamu wa Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akiongoza kikao cha majadiliano kuhusu ushirikiano wa bunge la Afrika na Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates- UAE) ambapo Ujumbe wa Bunge la UAE umeongozwa na Spika wa Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates- UAE), Dk. Amal Abdulla Al Qubaisi ,kwa pamoja wamekubaliana mambo ya msingi ya kushirikiana baina ya mabunge hayo.
Makamu wa Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele akiagana na mwenyeji wake,Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates- UAE),nchini Afrika Kusini Mahash Saeed Alhameli.

AGPAHI YAADHIMISHA SIKU YA MKUNGA DUNIANI KWA KUCHUNGUZA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA AKINA MAMA

$
0
0


Shirika lisilokuwa la kiserikali Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limeshiriki maadhimisho ya siku ya mkunga duniani kwa kutoa huduma ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama pamoja na upimaji wa Virusi Vya Ukimwi (VVU) mkoani Simiyu.


Maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika Mei 5, 2019 kwenye uwanja wa michezo wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile akimwakilisha Makamu wa Rais,Mhe. Samia Suluhu Hassan. 

Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoa wa Simiyu Dafrosa Charles,alisema shirika la AGPAHI limeshiriki maadhimisho ya siku ya mkunga duniani kwa kutoa huduma ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama pamoja na upimaji wa Virusi Vya Ukimwi (VVU). 

Amesema kati ya akina mama 205 waliowafanyia uchunguzi wa saratani hiyo ya mlango wa kizazi, wawili waligundulika kuwa na tatizo hilo na wamepatiwa rufaa ya kwenda kutibiwa kwenye hospitali ya rufaa Bugando Jijini Mwanza, huku 166 waliowapima VVU, mmoja kati yao amebainika kuwa ana maambukizi ya VVU na ameanzishia huduma ya dawa za kupunguza makali ya VVU. 

Aliongeza kuwa Saratani hiyo ya mlango wa kizazi kwa sasa ndiyo imekuwa ikisababisha vifo vingi vya akina mama wakati wa kujifungua kutokana na kuvuja damu kwa wingi na kuwataka akina mama wajenge tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili waweze kupata matibabu mapema na ili kumaliza vifo hivyo. Baadhi ya akina mama waliopatiwa huduma kwenye banda la Shirika la AGPAHI akiwemo Pendo Mboje, wamelipongeza Shirika hilo kwa kuwapelekea huduma hiyo, ambapo walikuwa hawajui visababishi vya kuugua saratani ya mlango wa kizazi pamoja na athari zake na kuahidi kujilinda zaidi na kwenda kutoa elimu kwa wenzao.

Maadhimisho hayo ya siku ya mkunga dunia kitaifa hapa nchini yamefayika mkoani Simiyu yakiwa na kaulimbiu isemayo,”Wakunga watetezi wa haki za wanawake”. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile alimewataka wakunga kuendelea kutoa huduma nzuri kwa akina mama wajawazito na kuwaasa kuacha tabia ya kuwatolea lugha chafu ili kuongeza idadi kubwa ya wanawake kupenda kujifungulia kwenye vituo vya afya hali ambayo itapunguza tatizo la vifo vitokanavyo na uzazi.

 “Licha ya Serikali kupunguza tatizo la vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi bado hali siyo ya kuridhisha ambapo awamu hii ya tano tumedhamiria kabisa kumaliza changamoto hiyo kwa kuhakikisha tunaendelea kuboresha huduma za afya hasa za mama na mtoto,”aliongeza. Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Feddy Mwanga, alisema kilianzishwa mwaka 1992 kwa lengo la kuunganisha wakunga wasajiliwa nchini ili kuwa na nguvu moja katika kupambana kumaliza tatizo la vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi wakati wa kujifugua. 

“Hapa mkoani Simiyu Chama cha Wakunga Tanzania kimeadhimisha siku hii kuanzia Mei 3 hadi leo Mei 5,2019 kwa kushirikiana na wadau wenzetu ambao wametoa huduma mbalimbali za afya ukiwamo upimaji wa VVU, huduma za uzazi wa mpango na uchuguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na matiti,”alisema Mwanga. Naye katibu tawala wa mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini alisema takwimu za vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi kuwa vimepungua ambapo mwaka 2017 vilikuwa 48 ambapo mwaka 2018 vilitokea vifo 40 na kubainisha kuwa tatizo ni kuwapo kwa upungufu wa wakunga .
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Faustine Ndugulile akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mkunga duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Simiyu na kuwataka wakunga kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na kuacha lugha za matusi kwa wajawazito ili kuhamasisha kujifungulia kwenye huduma za kiafya na ili kumaliza vifo vitokanavyo na uzazi.Picha na Marco Maduhu- Malunde 1 blog Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile (wa pili kulia) akiwa na viongozi wa mkoa wa Simiyu kwenda kukagua mabanda ya wadau wa sekta ya afya likiwemo shirika la AGPAHI ambao wametoa huduma mbalimbali za kiafya kwenye maadhimisho hayo ya siku ya mkunga duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Simiyu. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile akiwa kwenye banda la Shirika la AGPAHI akipewa maelezo na Mratibu wa AGPAHI mkoa Simiyu Dafrosa Chalres namna linavyotoa huduma ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama pamoja na kuwapima maambukizi ya VVU na kuanza kuwapatia huduma wale ambao wanagundulika kuwa na magonjwa hayo. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile , akipokea kijizuu kwenye banda la Shirika la AGPAHI. Muuguzi mkunga Conchesta Alexander kutoka kituo cha afya Muungano Bariadi mkoani Simiyu, akitoa elimu kwa akina mama mkoani humo juu ya kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi ugonjwa ambao unaua akina mama wengi wakati wa kujifungua. Muunguzi mkunga kutoka kituo cha afya muungano Bariadi , Elizabeth Holela akitoa elimu kwa akina mama juu ya saratani ya mlango wa kizazi, madhara yake pamoja na namna ya kujikinga. Muuguzi mkunga kutoka hospitali ya mkoa wa Simiyu Conchesta Alexander akiendelea kutoa elimu kwa akina mama mkoani humo kwenye Banda la AGPAHI namna ya kujiepusha na magonjwa ya saratani ya mlango wa kizazi. Akina mama mkoani Simiyu wakiwa kwenye Banda la Shirika la AAGPAHI kupewa elimu ya saratani ya mlango wa kizazi, ili kutokomeza vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi. Akina mama mkoani Simiyu wakiwa kwenye Banda la Shirika la AGPAHI kupewa elimu ya saratani ya mlango wa kizazi, ili kutokomeza vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi. Mratibu wa Shirika la AGPAHI mkoani Simiyu Dafrosa Charles akitoa elimu kwa mmoja wa wanaume mkoani Simiyu namna ya kumkinga mke wake kutopata saratani ya mlango wa kizazi. Muuguzi mkunga Mwaisha Yoma kutoka kituo cha afya Muungano Bariadi akichukua maelezo kwa mmoja wa akina mama ambaye amejitokeza kufanyiwa uchuguzi wa saratani ya mlango wa kizazi kutoka kwenye Banda la AGPAHI. Pendo Mbonje ambaye ni mmoja wa akina mama mkoani Simiyu ambao wamejitokeza kufanyiwa uchunguzi wa Saratani ya mlango wa kizazi katika banda la AGPAHI, wakati wa maadhimisho ya ukunga duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani humo Simiyu. Seke Ndongo akielezea namna alivyofanyiwa uchuguzi wa Saratani ya mlango wa kizazi na alivyopewa elimu ya kujikinga na saratani hiyo. 




Katibu tawala wa mkoa wa Simiyu Jummane Sagini akiiomba wiraza ya afya impatie wauguzi wakunga ili kukabiliana na tatizo la vifo vya uzazi mkoani humo, ambapo kwa mwaka jana walipoteza maisha akina mama 40. Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania Feddy Mwanga akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mkunga duniani kitaifa mkoani Simiyu, na kuelezea malengo ya maadhimisho hayo kufanyika mkoani Simiyu kuwa ni kuunganisha nguvu za pamoja kupambana kumaliza tatizo la vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi. Wakunga wakiwa kwenye maadhimisho yao kitaifa mkoani Simiyu wakisikiliza nasaha za Naibu waziri wa afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Faustine Ndugulile namna ya kuzingatia maadili ya kazi yao kiufasaha ili kutokomeza vifo vya uzazi. Wananchi mkoani Simiyu wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya mkunga duniani mkoani humo. Awali naibu waziri wa afya maendeleo ya jamiim jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile mwenye kaunda suti akipokea maandamano ya wakunga kwenye maadhimisho hayo kitaifa mkoani Simiyu. Wakunga wakiingia kwa maandamano kwenye uwanja wa michezo wa halmashauri ya mji wa Bariadi wakitokea kwenye kituo cha afya cha Muungano mjini Bariadi. Wauguzi wakunga nao hawakuwa nyuma kutoa burudani kwenye maadhimisho yao ya siku ya mkunga duniani, yaliyofanyika kitaifa mkoani Simiyu. Wakunga wakiendelea kutoa burudani. Picha na Marco Maduhu- Malunde 1 blog
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images