Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

The 5th UDSM Research Week Exhibitions. 6th to 8th May 2019.


KUMBUKUMBU

$
0
0

Ni miaka 13 tangu utuache mama, na hatujapata mbadala! Hakika Mama Hana mbadala! 

We miss you so much ucheshi, Upendo, hekima, busara zako Bado zinazunguka fikara zetu. 

Mama hatuishi kukutaja Kila iitwayo Leo. Hata nieleze kwa maneno yote haitoshi kukuelezea Mama, Mungu akupumzishe mahali pema peponi!!

Daima uko mioyoni mwetu tulikupenda na hata Sasa tunakupenda Mama.

Peter, Petty na Angela Msechu

DK.MABODI AZUNGUMZIA MAFANKIO YALIYOTOKANA NA AMANI NCHINI.

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’amesema Maendeleo yanayopatikana Nchini katika Nyanja za Kiuchumi,Kisiasa na Kijamii yanatokana na uwepo wa Amani na Utulivu inayosimamiwa kwa ufanisi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

Hayo aliyasema leo wakati akimwakilisha Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein katika Hafla ya Karamu  huko Tawi la CCM la Fuoni Michenzani Unguja.

Dk.Mabodi amesema kuimarika kwa Sekta mbali mbali zikiwemo za Elimu, Afya, Kilimo, Utawala, Haki za Binadamu, Ustawi wa Jamii, Miundombinu ya Anga, Nchi kavu na Baharini yote hayo ni vielelezo tosha vya utendaji bora na uliotukuka unaoacha Alama nzuri  kwa Vizazi vya sasa na vijavyo uliotekelezwa na Dk.Shein katika Utawala wake wa Awamu ya Saba.

Katika maelezo yake Dk.Mabodi amesema Dk.Shein ametekeleza mambo mengi yaliyoandika Historia ya kipekee Duniani ikiwemo Penchini ya Shilingi 20,000 kwa Wazee wenye Umri wa Miaka 70,Afya bure na Elimu bure mambo ambayo Mataifa mengi Duniani wameshindwa kuyatekeleza kwa Wananchi wao.

Ameeleza kuwa Dk.Shein amesimamia na kulinda Amani ya Nchi isitoweke na kuhakikisha Wananchi wanaishi kwa upendo, huku wakiwa na Uhuru wa kweli wa kufanya kazi halali za kuingia kipato sehemu yoyote ndani na nje ya Zanzibar bila vikwazo.

Amesema Mafanikio hayo hayakuja kama ndoto potofu  bali yametoka na Sera imara za CCM chini ya Ilani yake ya mwaka 2015/2020 inayotekelewa kwa kasi kubwa kwa lengo la kumaliza changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi katika maeneo yao kabla ya mwaka 2020.

Amewasihi Wananchi Visiwani humo bila ya kujali tofauti zao za Kidini,Kisisasa na Kikabila waunge mkonge mkono na kuthamini kwa vitendo juhudi za Dk.Shein za kulinda Amani,Utulivu pamoja na Rasilimali za Nchi.

Amesema ni lazima Wananchi wafikie wakati waishi kwa misimamo imara ya kulinda Amani pamoja na Tunu za Taifa zikiwemo Mapinduzi ya mwaka 1964,Muungano na Uhuru.

“Maendeleo ya Zanzibar yapo mikononi mwa Wananchi wenyewe kwani ndio walinzi wakubwa wa Amani na Utulivu wa Nchi, tusikubali kugawanywa misingi ya kuichafua Nchi yetu sote hili ni Taifa letu lazima tuwe Wamoja.”amesema Dk.Mabodi.

Pamoja na hayo Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM Zanzibar,amesema kuwa Dk.Shein amekuwa akiisimamia kwa Vitendo  Falsafa yake ya  kuwataka Viongozi na Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali kwa ujumla washuke kwa Wananchi wa ngazi zote kwa kuratibu Changamoto zao kasha kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Dk.Mabodi amesema CCM imeendeleza utaratibu wake wa Viongozi kupitia Kamati za Siasa za ngazi mbali mbali kukagua,kutathimini na kutoa maelekezo katika miradi mbali mbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali Kuu,Serikali za Mitaa pamoja na Chama kuhakikisha inawafikia kwa wakati na kuwanufaisha Wananchi wote bila ya ubaguzi.

Amesema kwamba kasi hiyo haitokuwa na kizuizi mpaka mwaka 2020,ambapo Mamilioni ya Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla kwa hiari zao waitapa ridhaa CCM Kidemokrasia ishinde na kuendelea kuongoza Dola.

Akizungumzia hafla hiyo Dk.Mabodi amemshukru Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein kwa Busara,Upendo na Hekima zake kwa kuwaahidi kuliwa Karamu katika Tawi hilo ikiwa ni Sadaka kwa Wana CCM na Wananchi wa eneo hilo.

Katika Risala ya Wanachama wa Tawi hilo la CCM, wameshukru na kupongeza Utekelezaji wa ahadi hiyo kwa vitendo iliyotolewa na Dk.Shein siku za hivi karibuni katika ufunguzi wa Tawi hilo.

Wamesema wanaridhishwa na Utendaji wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Shein katika kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM, na waliahidi kuendelea kukitumikia Chama ili kishinde kwa kila Uchaguzi wa Kidemokrasia.
  WANACHAMA na Viongozi mbali mbali wa Tawi la CCM Fuoni Michenzani wakila Karamu iliyoandaliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla akizungumza na Wana CCM wa Tawi la CCM Fuoni Michenzani akimwakilisha  Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein   katika hafla ya Karamu ambayo ni ahadi iliyotekelewa na Dk.Shein. 
 WANACHAMA wa CCM Fuoni Michenzani wakisikiliza nasaha za Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi.

Ohoooo...Prado v/s Bajaji.!

$
0
0

IKiwa siku chache zimepita tangu kuzinduliwa wiki ya Usalama Barabarani jijini Dar,  hali ya bado si salama sana kwa vyombo vya moto.Pichani ni ajali iliyotokea maeneo ya Kawe-JKT  jana jioni kama uonavyo pichani,na kusababisha foleni  kubwa wakati Askari usalama wa Barabarani akisubiriwa kuja kuchukua hatua za kisheria.Madereva tunaoendesha vyombo vya moto tunapaswa kuwa makini muda wote tuendeshapo,kuepuka madhara ya ajali kama tukio hilo.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 03.05.2019

Waziri Doto Biteko: Zaidi ya kilo 30 za madini zapatikana kutokana na kuanzishwa masoko ya madini

Goodluck Gozbert -Tutaonana Tena (Tribute Song)

Ubalozi wa Tanzania, Jamhuri ya Korea wafanikisha kwa kishindo maadhimisho ya miaka 55 ya Muungano

$
0
0

Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Korea , Mhe. Matilda Masuka akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Tanzania katika kusherehekea miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na miaka 27 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea. Ubalozi wa Tanzania mjini Seoul uliandaa shughuli mbalimbali za kuitangaza nchi kama vile maonesho ya Tingatinga, maonesho ya Kahawa, semina za biashara, utalii na uwekezaji na kubadilishana utamaduni kupitia mapishi ya vyakula mbalimbali. Pia msaanii maarufu wa Tanzania Abdul Nasib maarufu kwa jina la Diamond alifanya onesho la muziki. Katika hotuba yake Balozi Masuka aliwapongeza watanzania na viongozi wa Tanzania kwa kuulinda Muungano na pia alisifu ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea.

Sehemu ya wageni waalikwa wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar 

Mhe. Balozi Masuka akimkabidhi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Korea Mhe. Lee Juyoung baadhi ya mazao yanayolimwa Tanzania ikiwemo korosho wakati wa wiki ya Tanzania kuelekea maadhimishoya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Mhe. Balozi Masuka akimkabidhi Spika huyo majarida na vipeperushi mbalimbali vinavyotangaza vivuytioa vya utalii nchini

Watanzania waishio Korea (TANROK) wakionesha tamaduni za kitanzania kupitia sanaa ya ngoma

Mtaalam wa michoro maarufu ya Tanzania "Tingatinga" akiwafundisha wananchi wa Jamhuri ya Korea kuchora michoro hiyo

Wanafunzi wakiwa wamefuzu na kuonesha michoro yao ya "Tingatinga" inayovutuia

Balozi Masuka akifurahia jambo na wageni waalikwa wakati wa maadhimisho hayo

Balozi Masuka akimkaribisha Seoul msanii wa muziki Diamond alipokwenda kutumbuiza wakati wa maadhimisho ya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Wageni waalikwa wakifurahia muziki kutoka kwa msanii Diamond hayupo pichani

Ratiba ya matukio ya Wiki ya Tanzania jijini Seoul kama inavyoonekana

WAZIRI WA MAMBO YA NJE ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA VIETNAM kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Rais wa Taifa hilo Jenerali Le Duc Anh

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiweka saini katika kitabu cha maombolezo cha ubalozi wa Vietnam hapa nchini kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Rais wa Taifa hilo Jenerali Le Duc Anh aliyefariki April 22,2019, wa pili kutoka kushoto ni Balozi wa Vietnam hapa nchini Mhe. Nguyen Doanh na watatu kutoka kulia ni Mke wa Balozi Doanh pamoja na maafasia ubalozi huo wakishuhudia tukio hilo. 

Mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo Prof. Palamagamba John Kabudi ametoa pole kwa wananchi kupitia kwa Balozi wa Vietnam hapa nchini  nakuelezea kuwa Jamhuri ya Kisoshalisti ya watu wa Vietnam na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zina uhusiano wa muda mrefu na wa miaka mingi tangu enzi za Jamhuri ya watu wa Vietnam wakipigania Uhuru wao kutoka kwa Mareakani na Ufaransa.
Tukio hilo limefanyika katika Ubalozi wa Vietnam uliopo jijini Dar es Salaam leo tarehe 4, Mei 2019



Prof. Palamagamba John Kabudi akielezea jambo mara baada ya kuweka saini kwenye kitabu cha maombolezo
Profesa Palamagamba John Kabudi akizungumza na Balozi Doanh
Mama Doanh pamoja na Maafisa ubalozi wa Vietnam wakimsikiliza kwa makini Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani).

Mazungumzo yakiendelea.
Prof. Palamagamba John Kabudi akiagana na Balozi Doanh mara baada ya kumaliza tukio hilo.

WAZIRI JAFFO: SGR YAANZA KUONESHA MATUNDA KABLA YA KUANZA KUTUMIKA,TRC NA YAP WATIMIZA AHADI KWA DC JOKATE

Uwekezaji kwenye miradi ya umeme vijijini uchagize ukuaji wa uchumi- Simbachawene

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, George Simbachawene ametoa wito kwa Serikali kuhakikisha kuwa uwekezaji mkubwa unaofanywa katika miradi ya umeme vijijini unachagiza ukuaji wa uchumi kwa kupeleka umeme unaotosholeza mahitaji ya wananchi na kusambaza umeme katika Taasisi za Serikali na kijamii.
Simbachawene ameyasema hayo jijini Dodoma, tarehe 4 Mei, 2019 wakati wa kikao kilicholenga kupata taarifa kuhusu mwenendo wa ukusanyaji na utolewaji wa tozo ya mafuta ya petroli kwa ajili ya kugharamia miradi ya umeme vijijini  kwa mwaka 2018/2019.
Akizungumza katika kikao hicho kilichohudhuriwa na  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, Simbachawene alisema, “ Serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hii ya umeme vijijini, hivyo lazima mhakikishe kuwa umeme unaosambazwa unatosheleza mahitaji na si utumike tu kuwasha taa, mtu anapotaka kuanzisha kiwanda au kazi yoyote inayohitaji umeme asikwame, hii itapelekea miradi hii kuleta tija.”
Simbachawene pia aliishauri Wizara ya Nishati kuhakikisha kuwa, wanaendelea kuwashirikisha wawakilishi wa wananchi katika kazi za usambazaji umeme vijijini ili kazi hizo zifanyike kwa ufanisi.
Awali, akitoa taarifa kwa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga, alisema kuwa, katika kipindi cha kuanzia Julai 2018 hadi  mwishoni mwa Aprili, 2019, Wakala umepokea fedha za ndani kiasi cha shilingi bilioni 305.56 ambayo ni sawa na asilimia 97.7 ya fedha zilizopangwa kutolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.
Aliongeza kuwa, kwa upande wa fedha za nje, Wakala huo umepokea kiasi cha shilingi bilioni 87.75 na hivyo kufanya jumla ya fedha zilizopokelewa na Wakala kwa miradi ya umeme vijijini kuwa ni shilingi bilioni 393.31.
Akieleza kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, Mhandisi Maganga alisema kuwa, jumla ya vijiji vilivyofikiwa na umeme Tanzania Bara hadi kufikia tarehe 30 Aprili, 2019 ni 6,590 ambayo ni sawa na asilimia 53.7 ya vijiji vyote vya Tanzania Bara.
Aidha, alisema kuwa, jumla ya Taasisi za umma 8,986 zimepatiwa umeme kupitia miradi hiyo ya umeme vijijini  na matarajio ni kuwa hadi kufikia mwezi Julai, 2020, Vijiji 9,299 ambavyo ni sawa na asilimia 75.7 ya Vijiji vyote vya Tanzania Bara vitakuwa vimefikiwa na umeme.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amesema kuwa, wadau wa maendeleo ikiwemo Umoja wa Ulaya (AU), Serikali ya Sweden na Serikali ya Norway wana imani na Serikali ya Awamu ya Tano hasa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ndiyo maana wanaendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.
Kuhusu upatikanaji wa vifaa vya umeme vinavyozalishwa ndani ya nchi kama vile nguzo, Mgalu alisema kuwa vifaa hivyo vinaendelea kutolewa kwa wakandarasi na kwamba Serikali inaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini ili itekelezwe kwa muda uliopangwa.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka wakiwa katika kikao kilichohusu mwenendo wa ukusanyaji na utolewaji wa tozo ya mafuta ya petroli kwa ajili ya kugharamia miradi ya umeme vijijini  kwa mwaka 2018/2019 kilichofanyika jijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, George Simbachawene (kulia) na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu wakiwa kwenye kikao kilichohusu mwenendo wa ukusanyaji na utolewaji wa tozo ya mafuta ya petroli kwa ajili ya kugharamia miradi ya umeme vijijini  kwa mwaka 2018/2019 kilichofanyika jijini Dodoma.
 Wataalam kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wizara ya Nishati wakifuatilia kikao kilichohusu kilichohusu mwenendo wa ukusanyaji na utolewaji wa tozo ya mafuta ya petroli kwa ajili ya kugharamia miradi ya umeme vijijini  kwa mwaka 2018/2019 kilichofanyika jijini Dodoma.
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti,  Wataalam kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wizara ya Nishati wakifuatilia kikao kilichohusu kilichohusu mwenendo wa ukusanyaji na utolewaji wa tozo ya mafuta ya petroli kwa ajili ya kugharamia miradi ya umeme vijijini  kwa mwaka 2018/2019 kilichofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua wakiwa katika kikao kilichohusu mwenendo wa ukusanyaji na utolewaji wa tozo ya mafuta ya petroli kwa ajili ya kugharamia miradi ya umeme vijijini  kwa mwaka 2018/2019 kilichofanyika jijini Dodoma.

WIZARA YA MADINI YAOMBOLEZA KIFO CHA DKT REGINALD MENGI

Vodacom Tanzania Plc yashiriki maadhimisho ya Miaka 10 ya UCSAF

$
0
0
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti cha ushiriki Mkuu wa mauzo wa Kanda ya Kati wa kampuni ya Vodacom Tanzania Plc, Bi Grace Chambua wakati wa maadhimisho ya miaka 10 ya UCSAF jijini Dodoma mapema wiki hii. Maadhimisho ya mfuko huo wa mawasiliano kwa wote yameadhimishwa na kauli mbiu ikiwa ni “Mawasiliano kwa wote ni kichocheo cha kuufikia uchumi wa kati.

MALECELA NA MKEWE WAMJULIA HALI MTOTO WAO WILLIAM MALECELA

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela na mkewe Mhe Anna Kilango-Malecela wakiwa wamemtembelea kumjulia hali mwana wao William Malecela maarufu kama Le Mutuzu Super Brand aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam kwa matibabu leo Jumapili Mei 5, 2019

WAFANYABIASHARA SOKO LA TENGERU WAPATIWA VITAMBULISHO 1000

$
0
0

Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha

Mkuu Wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakishirikiana na mkuu wilaya ya Arumeru jana wamegawa vitambulisho vya kufanya biashara kwa wafanya biashara wadogo wadogo (machinga) hii ikiwa ni awamu ya pili yaugawaji.

Mkuu wa mkoa huyo pia alikabidhi wilaya ya Arumeru vitambulisho vya machinga Elfu kumi ambavyo vitagawiwa kwa halmashauri mbili zilizopo ndani ya wilaya ya Arumeru ambapo kila halmashauri imekabidhiwa vitambulisho 5000.

Akizungumza kuhusiana na ugawaji huo, Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro alisema kuwa hii ni awamu ya pili ya ugawaji wa vitambulisho ,
awamu ya kwanza waligawa nahii ni awamu yapili wamepokea vitambulisho elfu 10 kutoka kwa mkuu wa mkoa kwaajili ya kuwapatia wafanyabiashara wadogo wadogo.

Alisema kwa jana tu katika soko la Tengeru wamegawa vitambulisho 1000 kwa wafanyabiashara na wataendelea kuvigawa Hadi wafanyabiashara wote wavipate

"kama mnavyoona mimi na timu yangu yote tumeingia sokoni na tumefanyakazi mmeona watendaji wangu wa kata wafanyakazi wa halmashauri wote bila kujali cheo tumeingia kugawa vitambulisho vya machinga na tumegawa vitambulisho 1000 natunaendelea kugawa katika masoko yote"alisema Muro

Alimshukiru mkuu wa mkoa wa Arusha kwenda kuwapa ushirikiano katika zoezi hilo kwani amewapa motisha ya kutosha.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Ariana Mrisho Gambo alisema ameamua kuwapamotisha ya ugawaji wa vitambulisho wafanyakazi wa wawilaya hiyo.
Picha ikionesha Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro wa kwanza kulia akimkabidhi mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha Dr. Wilson  Mahera vitambulisho 2500 Kwa ajili ya kuwagawia wafanyabiashara wadogo wa halmashauri yake


TUSHIKAMANE FOUNDATION YAFANIKIWA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA KUTUNZA WAZEE

$
0
0
 Mwenyekiti wa Tasisi ya Tushikamane Foundation, Rosemary Mwapachu, akizungumza na wadau na Marafiki wa Taasisi hiyo waliofika katika hafla fupi ya kuchangia gharama za Wazee wanaohudumiwa na taasisi hiyo
 Jaji Mstaafu Mark Bomani akieleza na kutoa ushuhuda juu ya taasisi hiyo ilivyokuwa msaada kwa wazee na kutaja kuwa kitu wanachokifanya ni kikubwa zaidi kuliko watu wengine
 Balozi Juma Mwapachu akimpongeza Mkewe Bi Rose Mwapachu kwa kufanya vizuri katika ujenzi wa nyumba ya Wazee na kufanikisha Harambee kwa ajili ya mahitaji ya wazee hao kwa mwezi
 Sehemu ya Washiriki wa Harambee hiyo wakifuatilia kwa makini namna mambo yanavyoenedelea

SHEIKH MTUPA AWATAKA WANAOJIWEZA KIMAISHA KUSAIDIA WASIOJIWEZA NA WENYE MATATIZO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA

SHEIKH wa Mkoa wa Pwani,Khamis Mtupa ametoa rai kwa jamii inayojiweza kimapato,  kujitolea kuwasaidia watu wenye matatizo na wasiojiweza kwani ni njia mojawapo ya kujitengenezea na kujihifadhia twawabu ya kuingia peponi.

Aliyasema hayo wakati akifungua umoja wa Twariqa ,wilayani Kibaha ambazo ofisi yake ipo kata ya Kongowe Mtaa wa Mwambisi.

 Sheikh Mtupa aliwaeleza waumini wa dini ya kiislamu na wananchi kuwa mwanadamu akijihusisha na wenzake katika Twariqa ya kujitolea kusaidia wasiojiweza hujiandalia pepo. 

"Umoja huu wa twariqa ulioanzishwa mtaa wa Mwambisi kila anayeingia basi afahamu Twariqa inachukua dhamana ya yeye kufika peponi In jehanam firdaus Pepo ambayo kama tunazungumzia matokeo ya mtihani basi huyo mwanafunzi anakuwa amepata daraja la kwanza, 

"Hivyo ndugu zangu waislamu na wananchi kwa ujumla tujumuike na wenzetu katika umoja huu wa Twariqa ambao upo mahususi kwa ajili ya kusaidiana" alisema sheikh Mtupa.

Nae sheikh wa wilaya ya Kibaha,Said Mtonda alieleza, lengo la kuanzishwa kwa umoja huo wa Twariqa kwa wilaya ya Kibaha ni umoja wa kushirikiana kwa waumini wa dini ya kiislamu na wananchi katika kutoa msaada kwa waislamu wenzao na jamii pindi wanapopatwa na matatizo jambo la furaha.

Kigogo CUF Kata ya Makurumla atimkia CCM

$
0
0

Na Ripota Wetu,Michuzi TV.

ALIYEKUWA Katibu Kata wa Chama cha Wananchi (CUF) kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Chahasi Shomari amekihama chama hicho na kuhamia Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Chahasi amerudisha kadi ya CUF na kukabidhiwa ya CCM leo na Katibu wa Siasa na Oganaizesheni wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Cholaje Mohamed katika mafunzo ya viongozi wa jumuiya hiyo ngazi ya kata.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi hiyo, Chahasi amesema amefanya uamuzi wa kuhamia CCM kutokana na haki walizokuwa wakizipigania akiwa CUF kuanza kutekelezwa na Rais Dk. John Magufuli pamoja na mshikamano uliopo ndani ya chama hicho tawala.

Amesema Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba amekuwa akipigania haki za kiuchumi hasa kwa wafanya biashara wadogo ambapo sasa wametambulika na serikali.

“Kwa sasa machinga tumeanza kupata neema ya kutekeleza shughuli zetu bila kubughudhiwa na sasa tumepatiwa vitambulisho vya kutambua shughuli zetu,” amesema Chahasi. Ameongeza kuwa Mungu amemteua Rais Magufuli kuwakomboa wanyonge hivyo Watanzania hawana budi kumuunga mkono.

Aidha aliwataka kundi alilokuwa anafanya nalo kazi maarufu kama Mungiki kumuunga mkono uamuzi wake kwa kuwa siasa zinabadilika na kila mmoja anahitaji maisha bora, uchumi na maendeleo kwa Taifa.

Kwa upande wake Cholaje amesema wanaamini Chahasi atakuwa na msaada mkubwa katika CCM kwa kuwa ataonesha mapungufu waliyonayo vyama vya upinzani kwa kusaidia kuyaeleza kwa wananchi.

“Ni siku ya neema kwa ngazi zote za chama kuanzia tawi hadi taifa kwa kuwa tumemchukua mpiganaji wa CUF ambaye alikuwa msaada mkubwa kwa Lipumba,” amesema Cholaje.

Aliongeza kuwa wanatarajia Chahasi atakuwa sehemu ya Kampeni kuanzia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Chahasi amekuwa mwanachama wa CUF tangu mwaka 1999 na anatajwa kuwa alikuwa ni sehemu ya wanamkakati wa waliofanikisha ushindi wa udiwani wa sasa kupitia CUF katika Kata ya Makurumla, Omari Kombo ‘Kijiko’.

Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Chahasi Shomari, akikabidhi kadi ya chama hicho kwa Katibu wa Siasa na Oganaizesheni wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Cholaje Mohamed.
Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Chahasi Shomari, akipa kiapo cha uaminifu kwa chama pamoja na viongozi wa CCM.
Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Chahasi Shomari, akisindikizwa kuingia ukumbini na mmoja wa viongozi wa CCM.
Katibu wa Siasa na Oganaizesheni wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Cholaje Mohamed, akizungumza na wana CCM baada ya kukabidhi kadi kwa aliyekuwa Katibu wa CUF Makurumla, Shomari Chahasi. 

BREAKING NEWZZZZZZ:BASI LA KILIMANJARO EXPRESS LAPINDUKA MKATA,LILIKUWA LIKITOKA ARUSHA KWENDA DAR

$
0
0
 Basi la Kilimanjaro lenye namba za usajili  T 983 AWY limepinduka jioni ya leo mbele ya eneo la MKATA, Tanga. Basi hilo lilikuwa likitokea  jijini Arusha kuelekea jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo wameeleza kuwa katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha eneo la tukio zaidi ya majeruhi kadhaa,Wakielezea zaidi mbele ye Michuzi TV kuhusu chanzo cha ajali hiyo,wakabainisha kuwa chanzo ni mwendo kasi wa basi hilo.

Tutawaletea zaidi  taarifa kamili kutoka Mamlaka husika.
Baadhi ya Abiria waakiangalia baadhi ya majeruhi na ukaguzi wa mizigo yao kufuatia basi hilo kupinduka maeneo ya Mkata,likiwa linatoka  Mkoani Arusha kuelekea jijini Arusha.
Baadhi ya abiria walionusurika katika ajali hiyo wakitoa msaada kwa majeruhi
Baadhi ya Abiria waakiangalia baadhi ya majeruhi na ukaguzi wa mizigo yao kufuatia basi hilo kupinduka maeneo ya Mkata,likiwa linatoka  Mkoani Arusha kuelekea jijini Arusha.
Basi la Kilimanjaro lenye namba za usajili T 983 AWY likiwa limepinduka mbele ya eneo la MKATA, Tanga,hakuna aliyepoteza Maisha.

Wananchi wanapaswa kujua Historia yao- Balozi Seif

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Wananchi wanapaswa kujua Historia yao katika dhana nzima ya kuendelea kulinda Uhuru wao, Heshima, Utamaduni na hata mazingira yao yanayowazunguuka ya kila siku.

Alisema Binaadamu asiyejua Historia yake kamwe anakuwa Mtumwa wakati wote akiendelea kutawaliwa kifikra jambo ambalo ni hatari katika maisha yake yanayomuhusu.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo alipofanya ziara fupi ya kuyakagua Mahandaki Mawili ya Mangapwani yaliyokuwa yakitumika kuhifadhia Watumwa ambayo kwa sasa yamekuwa sehemu muhimu ya kujifunza Historia ya Biashara hiyo iliyopigwa marufuku tokea Karne ya 18.

Alisema Zanzibar ilikuwa kituo muhimu cha Historia iliyounganisha sehemu nyingi Duniani historia ambayo Taasisi inayosimamia masuala hayo ambayo ni Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale ina jukumu la kusimamia vyema maeneo yote muhimu ili Wageni pamoja na Wananchi wapate fursa ya kujifunza zaidi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia aliwakumbusha Vijana wanaosimamia maeneo hayo kufanya jitihada ya kujifunza Historia kamili ili kuepuka tabia ya kutoa Taarifa zisizo na uhakika wa Historia ya maeneo wanayofanyia kazi.

Akitoa ufafanuzi Msimamizi wa Mahandaki ya Mangapwani Makame Omar Said alisema maumbile ya eneo hilo muda wote yamekuwa ya kujificha kutokana na hali halisi ya biashara yenyewe ya Utumwa ilivyokuwa ikifanywa kwa kujificha.

Makame alisema utafiti unaonyesha wazi kwamba bado idadi ya Wazawa kufika eneo hilo kwa ajili ya kujifunza Historia yake ni ndogo ikilinganishwa na Wageni pamoja na Wasomi wa fani za Kihistoria.

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale anayesimamia Utalii na Mambo ya Kale Dr. Amina Ameir Issa alimueleza Balozi Seif kwamba Idara ya Mambo ya Kale ilianzishwa Mnamo Mwaka1920.

Dr. Amina alisema hatua hiyo ilifuatiwa na kutungwa kwa Sheria ya Mambo ya Kale Mnamo Mwaka 1941 ikiwa chini ya uangalizi wa Idara ya Mambo ya Kale ikiwa na lengo la kusimamia maeneo Saba ya Kihistoria hapa Zanzibar.

Aliyataja baadhi ya Maeneo hayo kuwa ni pamoja na Mahandaki ya Mangapwani,Msikiti Mkongwe wa Kizimkazi, Mji wa Makutani uliopo katika Kisiwa cha Tumbatu pamoja na Mji wa Mwinyimkuu uliopo Dunga.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale anayesimamia Utalii na Mambo ya Kale alifahamisha kwamba Mahandaki ya Mangapwani yana bahati kubwa ya kutembelewa na Wageni wengi, Watalii, Wanafunzo pamoja na Watafiti ikilinganishwa na sehemu nyengine za Kihistoria zilizopo Zanzibar.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale Bibi Khadija Bakari Juma alisema Wizara hiyo kwa sasa tayari imeshaandaa mpango maalum wa kushajiisha Utalii wa ndani ili kuimarisha zaidi mapato ya Taifa.

Bibi Khadija alisema mpango huo umeaanza kufanya kazi kwa kuwahusisha watendaji wa Wizara hiyo kama muelekeo wa ushajiishaji ili kuungwa mkono ya Wizara nyengine na baadae Wananchi hapa Nchini.

Katibu Mkuu Habari ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa uamuzi wake wa kutenga Bajeti Maalum kila Mwaka inayolenga kuhudumia Uhifadhi wa Maeneo ya Kihistoria hapa Nchini jambo ambalo limeleta matokeo mazuri katika usimamizi wa maeneo hayo muhimu.

Akielezea changamoto zinayoyakabili maeneo mengi ya Kihistoria Nchini Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” Nd. Rajab Ali Rajab alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba uhaba wa wafanyakazi ni tatizo kubwa linalofaa kuangaliwa na Serikali pamoja na Taasisi inayosimamia maeneo hayo.

Nd. Rajab alisema ufinyu huo wakati mwengine hutoa mwanya kwa wahalifu kufanya hujuma katika maeneo hayo ambayo kwa namna yoyote ile yanapaswa kuheshimiwa na kuenziwa kwa vizazi vya sasa na vile vijavyo.

“ Yapo matendo mabaya wakati mwengine hufanyika ya uharibifu a maeneo ya Hifadhi kama uchafuzi wa mazingira kutokana na kukosa usimamizi imara wa Watendaji”. Alisisitiza Mkuu huyo wa Wilaya ya Kaskazini “B”.

Zanzibar iliyokuwa Kituo cha Biashara ya Utumwa katika Mwambao wa Afrika Mashariki ilisimamisha Biashara hiyo chini ya Utawala wa Uingereza Mnamo Mwaka 1873 licha ya baadhi ya Wafanyabiashara kuendelea kufanya biashara hiyo kwa siri. 
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifanya ziara ya kukagua Mahandaki Mawili ya Mangapwani yaliyokuwa yakitumika kuhifadhia Watumwa ambayo kwa sasa yamekuwa sehemu muhimu ya kujifunza Historia ya Biashara hiyo iliyopigwa marufuku tokea Karne ya 18.
 Balozi Seif Ali Iddi akipewa maelezo ya Biashara ya Utumwa ilivyokuwa ikufanyika katika Mahandaki ya Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale anayesimamia Utalii na Mambo ya Kale Dr. Amina Ameir Issa akielezea jitihada zinazochukuliwa na Wizara kuyasimaia vyema Mahandaki ya Mangapwani.
 Balozi Seif akiuagiza uongozi wa Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale pamoja na ule wa Wilaya kuendelea kuyahifadhi Mahandaki ya Mangapwani ili yaendelee kutoa huduma za Kihistoria. Picha na – OMPR – ZNZ.
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images