Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

Wanawake Nchini Wametakiwa Kujitambua Kujiepusha na Vitendo vya Ngono Maofisini.

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hosiptali ya CCBRT, Brenda Msangi akitoa mada yake wakati wa kongamano la mwanamke kwenye ushawishi kufikia ndoto ya  mafanikio kimaendeleo jijini Dar es Salaam.HABARI PICHA/NA PHILEMON SOLOMON
............................................................
WANAWAKE nchini wametakiwa kujitambua jambo litakalo wasaidia kujiepusha na vitendo vya ngono maofisini.


Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi wakati akitoa mada katika kongamano la mwanamke kwenye ushawishi kufikia ndoto ya  mafanikio kimaendeleo lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


Alisema masuala ya unyanyasi wa kingono maofisi yapo lakini yanashindwa kuweka hadharani kwa kuwa yanafanyika kisiri na walengwa wakubwa wakiwa ni wanawake.


"Wanawake tunatakiwa kujitambua kuanzia uvaaji wetu, jinsi tunavyozungumza hali hiyo itaondoa dhana ya kuwa sisi wenyewe tunapenda kufanyiwa vitendo hivyo.


Alisema kumekuwa na vitendo vya unyanyasaji wa kingono maofisini lakini kupitia kongamano ili tunaweza kupiga hatua ya kukabiliana na changamoto hiyo na ndio maana baadhi ya washiriki, wakurugenzi kutoka katika makampuni.


Msangi alisema kukiwepo na mifumo mizuri maofisini itasaidia kujua namna ya kumsaidia muathirika wa vitendo hivyo na hatua za kuchukua.


"Mwanamke akijengwa kifikra na kuwa na uthubutu anaweza kuwa na maendeleo makubwa kiuchumi kuanzia ngazi ya familia na Taifa kwa ujumla.


Mmoja wa wakurugenzi wa shirika hilo, Emelda Mwamanga alisema kwa zaidi ya miaka 10 tangu waanzishe shirika hilo mwaka 2008 wamekuwa wakitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake wa kibiashara na kufanya matamasha mbalimbali kwa ajili ya kuibua vipaji ili  kuwainua kiuchumi.


Kongamano hilo liliandaliwa na Shirika la Woman of Influence la jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mipango na Usimamizi wa Utendaji Afrika Mashariki kutoka Kampuni TBL,Nancey Riwa  (kushoto) akichangia mada wakati wa kongamano hilo (katika) Mkurugenzi wa Uhusiano kutoka VodaCom, Rosalynn Mworsia, na kulia Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hosiptali ya CCBRT, Brenda Msangi.
 Program Meneja Mwandamizi kutoka Kampuni ya Trade Mark, Monica Hangi (aliyesimama kushoto) akifurahia jambo wakati akichangia mada.
 Kongamano likiendelea.

MKURABITA YAHIMIZA KILIMO BIASHA KWA WAKULIMA WA UYUI

0
0
NA TIGANYA VINCENT
WAKULIMA wilayani Uyui wamehimizwa kujiunga na kilimo cha kisasa na kibiashara ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kujiongeze kipato kwa ajili ya maendeleo ya familia zao na Taifa kwa ujumla.

Pia wametakiwa kujiunga na Taasisi za fedha ili waweze kupata mikopo itakayowawezesha kulima kilimo cha kibiashara.

Kauli hiyo imetolewa jana na Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu wakati wa kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima 100 na viongozi 10 wa Kata ya Miyenze wilayani Uyui.

Alisema kilimo biashara ndio kitaweza kuwakwamu kiuchumi wananchi na kuondokana na umaskini na kuwataka wakulima ambao wamesharasimisha ardhi zao kuwa na mashamba darasa ya kilimo biashara ili wawe chachu ya mabadiliko kwa wengine.

Meneja huyo alisema kwa wakulima ambao tayari aridhi zao zimerasimishwa ni rahisi kukopesheka kwa kuwa wanazo hati na baadhi yao wameshaunganishwa na Benki mbalimbali.

Temu alisema ni vema wakulima hao wakatumia hati zao kutafuata mikopo ambao itawaondoa katika kilimo duni na kugeuza kuwa kilimo ambacho kitaleta mapinduzi katika maisha yao.

Aliwataka wakulima walijengewewa uwezo kuwa na mashamba darasa ya kilimo biashara ili wakulima ambao hawakupata fursa hiyo waende kujifunza kwao.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya alisema kuwa mpango wa wilaya hiyo ni kuhakikisha kila kaya inalima ekari tatu za mazao ya biashara pamoja na mazao mengine ili kuwawezesha wananchi kujiongezea kipato. Alisema mazao hayo ni pamoja na tumbaku, pamba, korosho na alizeti.
 Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu akisoma maazimo ya mafunzo wakati wa kufunga jana mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima 100 na viongozi 10 wa Kata ya Miyenze wilayani Uyui.
Afisa Tafiti na Ufuatiliaji kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) Francis Mjuni akitoa elimu jana kwa wanakijiji wa Miyenze wilayani Uyui waliopata hati miliki za kimila juu ya umuhimu wa utunzaji wa kumbukumbu katika shughuli mbalimbali. 
 Baadhi ya wakulima wa Kata ya Miyenze wilayani Uyui wakipata maelezo juu ya umuhimu wa kilimo biashara kutoka kwa Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini wa Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu (hayupo katika picha) wakati wa kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima 100 na viongozi 10 wa Kata hiyo.
 Baadhi ya wakulima wa Kata ya Miyenze wilayani Uyui wakinyosha mikono juu kuunga mkono maelezo ya kuwahimiza juu ya kilimo biashara yalikuwa yakitolewa na Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini wa Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu(aliyesimama kati kati yao) wakati wa kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima 100 na viongozi 10 wa Kata hiyo. Picha na Tiganya Vincent RS Tabora   

HOFU YATANDA MAAMUZI YA HAKIMU BAADA YA KUPOTEA HUKUMU

0
0
Na Ahmed Mahmoud,Arusha

Hakimu wa mahakama ya Mwanzo, Maromboso iliyopo jijini Arusha,Therezia Sidoyeka amejikuta katika wakati mgumu Mara baada ya karatasi za hukumu aliyokuwa alisome mahakamani kutoweka katika mazingira ya utata na kusababisha  ashindwe kutoa maamuzi ya mahakama katika shauri la mirathi ,lililopo mbele yake.

"Jamani hukumu yenu niliyokuwa nimeiandaa kwa kuichapa imetoweka hata sijui ilipo inaonekana baadhi yenu mnaomba sana ,naombeni niandae upya ili niisome jumatatu itakuwa tayari" Alisema hakimu Sidoyeka.

Tukio hilo lisilo la kawaida limetokea mwishoni mwa wiki katika mahakama hiyo na kufanya baadhi yabwasikilizaji kupigwa na butwaa.

Shauri la kesi hiyo Namba 109 la mwaka 1992 lililetwa mahakamani hapo na mlalamikaji , Stephano Balthazar akimpinga Frida Swai ambaye ni mama yake mdogo kuwa msimamizi wa Mirathi ya Marehemu bibi yake aitwaye Monica Mbowe, aliyefariki mwaka 1992 kwa madai ya kushindwa kukusanya,kugawa na kufunga Mirathi katika kipindi cha miaka 28.

Kupotea kwa karatasi za hukumu hiyo kumeibua sintofahamu  katika maamuzi ya mahakama hiyo huku upande wa waleta maombi wakijawa na hofu zaidi ,ukizingatia kuwa nyumba moja ya marehemu iliuzwa kwa Jaji Mstaafu Aishiel Sumari.

Shauri hilo limeahirishwa kwa Mara ya pili mfululizo bila kuwepo na sababu za msingi,ambapo aprili 30,mwaka huu shauri hilo lilikuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutolewa uamuzi hata hivyo hakimu Sidoyeka hakuwepo mahakamani hapo na kuelezwa kuwa shauri hilo limepangiwa tarehe ya Leo,Mei 3 mwaka huu.

Leo wasikilizaji wa pande zote mbili katika shauri hilo walifurika katika chumba cha mahakama huku kila upande ukiwa na shauku ya kutaka kujua maamuzi yatakayotolewa mahakama hapo.

Awali shauri hilo lilianza kuunguruma mahakamani hapo, April 11 mwaka huu,ambapo upande wa mleta maombi ,Stephano Balthazari akiwa na mashahidi sita, alimpinga  msimamizi wa Mirathi Frida Swai kwa madai si mwaminifu,ameshindwa kukusanya Mali za Marehemu na kugawa katika kipindi cha miaka 28 tangu kifo cha marehemu.

Pia alidai kuwa anaoushahidi kuwa Frida Swai amefuja Mali za marehemu bibi yake kwa kuuza baadhi ya nyumba zilizoashwa ikiwemo nyumba ya Kaloleni (Mviringo bar)ambayo ameiuza kwa Jaji Mstaafu Aishiel Sumari bila kufuata taratibu.

Upande wa mjibu Maombi ,Frida Swai aliyekuwa na mashahidi wanne aliiambia mahakama hiyo kwamba Aligawa Mirathi ya marehemu Monica Mbowe mwaka 1995 kwa kufuata wosia wa marehemu ulivyoelekeza.

Alisema kuwa marehemu aliacha Nyumba sita zikiwemo NNE  zilizopo Ungalimited na Mbili zipo kaloleni jijini hapa ambapo Nyumba tatu aligawa moja kwa mjukuu mmoja ,moja kwa Mtoto pekee wa marehemu na nyingine kwa rafiki wa marehemu huku yeye akijigawia Nyumba tatu.

Shauri hilo limepangwa kutolewa uamuzi Mei 6 mwaka huu siku ya jumatatu.

MALI ZA WAKILI MIKONONI MWA SERIKALI,HAKIMU WAKILI KUPANDISWA MAHAKAMANI

0
0
Na Ahmed Mahmoud,Arusha

Serikali imetaifisha rasmi Mali za Wakili maarufu Nchini Median Mwale zenye thamani ya sh,bilioni 1.2 zilizotokana na zao la utakatishaji mara baada ya mahakama kuu kumtia hatiani na kuamuru Mali hizo zitaifishwe.

Akiongea na wandishi wa habari jijini Arusha,katika zoezi la makabidhiano ya mali hizo kati ya ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka DPP na Hazina,Mkurugenzi wa Mashtaka ya jinai Nchini , (ASP )Biswalo Mganga alizitaja Mali hizo kuwa ni pamoja na Magari sita ya kifahari yanayoshikiliwa kituo kikuu cha polisi,jijini hapa.

Mali zingine zilizotaifishwa ni pamoja na Nyumba mbili ikiwemo iliyopo ploti Namba 261 block c Njiro na nyumba nyingine iliyopo ploti namba 22 iliyopo eneo la Ilikyurei ambayo ilikuwa mali ya Wakili Loomo Ojale na shamba moja la ekari 10 lililopo eneo la Ngaramtoni.

Alisema hatua hiyo imekuja kufuatia mahakama kuu kanda ya Arusha,kutaifisha Mali hizo na kwamba April 14,2019 mahakama hiyo ilitoa kibali cha kuzitaifisha rasimi na kuwa Mali ya serikali.

"Kwa mujibu wa sheria Mali zinapotaifishwa kuwa Mali ya serikali zinakuwa chini ya katibu mkuu Hazina" Alisema.

Naye kaimu mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa Mali za serikali Hazina,Benezeth Rutta Alisema kuwa Mali hizo baada ya kukabidhiwa kutoka kwa DPP zinakuwa chini ya uangalizi wa wizara ya fedha zinapangwa kadri serikali itakavyoona inafaa.

"Mali hizi Mara baada ya kukabidhiwa serikalini zitapangiwa matumizi kadri serikali itakavyoona inafaa na kama itaonekana Mali hizo hazifai kwa matumizi ya serikali zitauzwa kwa mnada" Alisema Rutha.

Kwa upande wake kamishina msaidizi wa jeshi la Polisi ,Selemani Nyakulinga Alisema Alisema kuwa mwaka 2011 alipata taarifa kutoka kitengo cha udhibiti wa fedha haramu kuwa kuna watu waligushi na kutaka kuiba fedha dolla la marekani milioni 17.2 kutoka mfuko wa global fund kwa ajili ya kusaidia kutibu malaria na HIV Nchini Tanzania zikitoka kwenye Hazina ya nchi ya Marekani.

Alisema walibaini kuwa waliohusika na wizi huo ni RAIA wa Kenya wakishirikiana na watanzania akiwemo Wakili Median Mwale .

Alisema baada ya kufuatilia walifanikiwa kuwatia mbaroni wahusika wote na baadae mahakama ilibaini kuwa wahusika walishanunua Mali mbalimbali zilizotokana na zao la utakatishaji wa fedha hizo na mahakama kuridhia na kutaifisha Mali hizo kuwa za serikali.

"Leo tulikuwa tumekuwa kuwaonyesha na kuwakabidhi rasimu kuwa wamiliki wapya wa Mali hizo"Alisema Nyakulinga.

Wakati huo huo DPP Biswalo Mganga amesema Wakili Maneno Mbunda na watuhumiwa wengine tisa wanashikiliwa kwa mahojiano kwa makosa mbalimbali .

Biswalo amesema Mtuhumiwa huyo ambaye pia ni Mtumishi wa Serikali katika Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Hakimu ambaye hakutajwa Jina lake, walishirikiana kufanya Kosa la kuhujumu Uchumi kwa kutamka Bei ya chini ya Meno ya Tembo na kumuachia huru Mtuhumiwa.

Tuendelee kushikamana na kupaza Sauti pale wenzetu wanapokumbwa na masahibu ya aina hii maana Nchi hii sasa ilipofikia sio sawa kabisa. Ukitekwa na watekaji wasisikie kelele huku nyuma yao ni rahisi sana kufanya yao.

Tuondoe hofu na uoga ili tuwe na udhubutu kama sio utayari wa kuwatetea na kuwapigania wenzetu. Ukiwa na hofu huwezi kusema, na usipoanza kusema wewe, Siku nawe yakikusibu, hutopata Watu wa kukusemea.

Awali Wakili Mbuda ilidaiwa alitekwa na watu wasiojulikana na taarifa za kutoweka kwake ziliendelea kuenea kwa kasi jijini hapa na hakuna chombo chochote cha doka kilichokuwa tayari kulizungumzia suala hilo

MBUNGE AMTAKA MWENYEKITI KUREJESHA PESA MILION 69 ANAZODAIWA KUZIPOKEA KINYUME CHA SHERIA

0
0
Na Ahmed Mahmoue,Longido

Mbunge wa Longido Stevin Kiruswa,amemtaka Mwenyekiti wa Kijiji cha Eworndeke katika kata ya Kimokokuwa,Mosses Leng'ese kurejesha haraka kiasi cha sh,milion 69 kati ya Mil.135 alizopokea kinyume cha sheria kupitia mradi wa umeme wa grid ya Taifa ili zitumike kuwasaidia akina mama wa kifugaji kama ilivyoamriwa na wananchi wa Kijiji hicho.

Kiruswa ametoa kauli hiyo jana kijijini hapo wakati akiongea na wananchi katika mkutano wa hadhara uliolenga kupata ufumbuzi juu ya fedha za Kijiji zinazodaiwa kutafunwa na mwenyekiti wa Kijiji hicho Mosses Leng'ese na wenzake sita.

Awali mwenyekiti wa Kijiji hicho,Leng'ese na wenzake walidaiwa kujimilikisha maeneo ya wazi ambayo ni Mali ya Kijiji na kujipatia kiasi cha sh,milioni 135 jambo lililoibua mgogoro mkubwa ambao ulimlazimu mkuu wa wilaya Frank Mwaisumbe kuingilia kati na kumtaka mwenyekiti huyo kurejesha sh,milioni 69 kwa wananchi.

Aidha mbunge huyo aliwataka wananchi kuachana na migogoro isiyo na tija badala yake wajielekeze katika utatuzi wa changamoto ikiwemo kuwekeza kwenye ujenzi wa madarasa kwa kuwa suala la ufugaji limekuwa na changamoto ya mifugo kufa kutokana na hali ya ukame.

Naye wakili wa kujitegemea ambaye ni Mzaliwa wa kijiji hicho na mkazi wa Kijiji Arusha,Nicolaus Senteu,alisema mkutano huo umeafikiana kumsamehe mwenyekiti huyo na wenzake kwa sharti la kurejesha fedha hizo na kwamba hatua hiyo imeleta afya kwa Kijiji hicho kuepusha mfarakano.

Aliipongeza jamii hiyo kwa kuonyesha msimamo wa kupigania rasilimali yao iliyotaka kutumika vibaya na wajanja wachache ili itumike kwa manufaa ya wananchi wote.

"Nawashukuru wananchi wa Eworndeke kwa kuonyesha msimamo hasa pale wanapoona rasilimali yao inataka kuporwa na watu wachache kuweza kuirejesha" Alisema Senteu

Aliwashauri viongozi wa Kijiji hicho kuwa na utaratibu wa kuwashirikisha wananchi kwa uwazi zaidi suala litakalosaidia kuondoa migongano ya kimaslahi na kuleta umoja na mshikamano.

Katika hatua nyingine wananchi hao wametaka kiasi cha sh,million 700 zinazotarajia kulipwa kama fidia ya maeneo ya wazi ya kijiji ili kupisha mradi wa umeme wa Grid ya Taifa KV 400 ,zilipwe kupitia akaunti ya kijiji na zitumike ipasavyo kuwaletea maendeleo wananchi.

Wananchi hao walikubaliana kwamba kati ya fedha hizo,sh, milioni 400 zigawanywe kwa vitongoji vinne vya Kijiji hicho na kiasi cha shilingi milioni 300 zitumike kuibua maendeleo Kijiji hapo ikiwemo ujenzi wa madarasa na zahanati.

TUSHIKAMANE FOUNDATION YAFANIKIWA KUCHANGISHA FEDHA ZA KUENDELEA KUTUNZA WAZEE

0
0
 Mwenyekiti wa Tasisi ya Tushikamane Foundation, Rosemary Mwapachu, akizungumza na wadau na Marafiki wa Taasisi hiyo waliofika katika hafla fupi ya kushukuru wafadhili walioiwezesha taasisi hiyo kujenga jengo la kulala wazee wasiojiweza huko Kwembe jijini Dar es salaam wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mwishoni mwa juma hoteli ya New Africa jijini. Nyuma yake kushoto ni wanachama wa Tushikamane Foundation Bi. Anna Kahama na Mwami Mlangwa.
 Jaji Mstaafu Mark Bomani akieleza na kutoa ushuhuda juu ya taasisi hiyo ilivyokuwa msaada kwa wazee na kutaja kuwa kitu wanachokifanya ni kikubwa zaidi kuliko watu wengine
 Balozi Juma Mwapachu akimpongeza Mkewe Bi Rose Mwapachu kwa kufanya vizuri katika ujenzi wa nyumba ya Wazee na kufanikisha Harambee kwa ajili ya mahitaji ya wazee hao kwa mwezi
 Sehemu ya Washiriki wa Harambee hiyo wakifuatilia kwa makini namna mambo yanavyoenedelea

DKT. NDUGULILE ATOA RAI KWA VIONGOZI WA KISIASA KUTOINGILIA KAZI ZA TAALUMA YA AFYA

0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile ametoa rai kwa viongozi wa Kisiasa hapa nchini kuacha kuingilia kazi za Kitaaluma katika sekta ya Afya na kuwaomba wawaache wataalam wafanye kazi zao kwa misingi na miiko ya Kitaaluma inayowaongoza.

Dkt. Ndugulile ameyasema hayo katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, chini ya Kauli Mbiu “Wakunga Watetezi wa Haki za Wanawake”, ambapo alikuwa akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Amesema hivi karibuni kumekuwa na matamko yanayotolewa na baadhi ya viongozi wa kisiasa yanayowakatisha tamaa watumishi wa sekta ya afya na baadhi ya viongozi wameanza kuingilia masuala ya kitaalum, hivyo akawaomba ikiwa viongozi hao watakutana na changamoto za watendaji wa afya waishirikishe wizara ya afya ili wachukuliwe hatua kwa mujibu wa taaluma zao.

“Niwaombe sana viongozi wa Serikali na Viongozi wa vyama, masuala ya kitaaluma yanashughulikiwa kitaaluma kama kuna changamoto na wanataaluma ndiyo maana tuna mabaraza ya taaluma na ndiyo maana sisi wizara tupo mtushirikishe, nimelisema hili kwa sababu nimeona sekta imeanza kuingiliwa” alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt. Faustine Ndugulile amewataka wakunga hapa nchini kuendelea kuzingatia miiko na misingi ya taaluma yao katika huduma wanazotoa kwa jamii na kuahidi kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua wale wote watakaokiuka misingi hiyo kwa kuwa jamii inahitaji heshimu, utu, upendo na kutiwa moyo

Katika hatua nyingine Dkt. Ndugulile ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa maendeleo na jamii kwa ujumla kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha huduma za afya ili changamoto ya vifo vitokanavyo na uzazi vibaki kuwa historia ambapo amesema kwa sasa wanawake 11,000 wanakufa kila mwaka kutokana na uzazi.

Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania, Bibi. Feddy Mwanga ameiomba Serikali kuongeza idadi ya wakunga ili mkunga aweze kutoa huduma kwa kiwango kinachokubalika Kitaifa na kimataifa huku akisisitiza Serikali kuona haja ya kujenga nyumba za wakunga katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya vinavyoboreshwa na vinavyojengwa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthoy Mtaka amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa shilingi bilioni saba fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali tatu za Wilaya Bariadi, Busega na Itilima ambazo ujenzi wake unaendelea vizuri.

Aidha, Kiswaga ameshukuru Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNPFA) kwa namna linavyoshirikiana na Serikali mkoani Smiyu kwa kukarabati baadhi ya vituo, kununuaa vifaa mbalimmbali, kutoa mafunzo kwa wakunga jitihada ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Akitoa taarifa ya Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema Idadi ya wakunga katika vituo vya kutolea huduma za afya Simiyu imeongezeka hali iliyofanya wajawazito wengi kujifungulia katika vituo vya afya kutoka asilimia 62 mpaka asilimia 68, hivyo vifo vya mama wajawazito vimepungua kutoka vifo 48 mwaka 2017 mpaka vifo 40 mwaka 2018.

Naye Makamu Mwakilishi Mkaazi wa UNFPA hapa nchini, Dkt.Hashina Begum amesema kwa kushirikiana na Chama cha Wakunga nchini (TAMA) limetoa mafunzo kwa wakunga 90 kutoka katika vituo vilivyoboreshwa ili kuwasaidia wakina mama wajawazito na watoto kupata huduma za dharura na kupunguza vifo kwa mama na mtoto vitokanavyo na uzazi.

Grace Magengeni Mkunga kutoka Jijini Dodoma amesema” siku yetu imefana tunashukuru hotuba ya Naibu Waziri imetutia moyo katika kuwahudumia wanawake na watoto, nawashauri wenzangu tusimamie taaluma zetu tufanye kazi kwa bidii naamini hao wanaotuingilia majukumu yetu wataachaa maana ni kweli, tunashukuru Naibu Waziri kulisemea hili suala”
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kulia ) akipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa wakunga ya namna wanavyowahudumia wakina mama wajawazito na watoto wakati alipotembelea Banda la Chama cha Wakunga Tanzania(TAMA), katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa katika Uwanja wa Bariadi Mkoani Simiyu.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kulia ) akiangalia baadhi ya vitabu vinvyotuika kutoa elimu kwa wananchi wakati alipotembelea banda la maonesho la Shirika lisio la kiserikali la AGPAHI, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
 Baadhi ya wakunga wakiwa katika maandamano wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akimkabidhi mmoja wa kunga wa moa wa Simiyu cheti kama zawadi ya kufanyakazi nzuri, katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Ulinzi Waimarishwa Soko la Madini Mkoani Tabora

0
0
Na Editha Edward- Michuzi TV,Tabora

Kamati ya Ulinzi na usalama kupitia jeshi la polisi mkoa wa Tabora limeahidi Kuongeza nguvu ya Ulinzi na usalama katika Soko kuu la Madini mkoa wa Tabora kwa kutumia mbinu za kiteknolojia na kuimarisha Ushirikiano dhidi ya Wachimbaji wadogo na Serikali lengo ikiwa ni kuhakikisha wauzaji na wanunuzi wa Madini wote wanakuwa na Ulinzi na usalama dhidi ya biashara hiyo

Yamesemwa hayo hii leo mjini Nzega Mkoani Tabora katika Ufunguzi wa soko la Madini ambalo limejengwa kisasa huku likizingatia Weledi wa juu pamoja na kutekeleza agizo la Serikali ya Awamu ya Tano

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Kamishina Msaidizi Mwandamizi Emmanuel Nley amesema biashara hiyo itakuwa safi na salama Kamati ya Ulinzi imejipanga kuimarisha suala hilo kwa vitendo zaidi

"Soko kuu la kununua na kuuza dhahabu litaimarishwa sana kutakuwa na Askari wa aina mbili Askari wanaovaa Uniform watakuwa hapa na Askari wanaovaa kiraia watakuwa hapa katika jengo hili na zitafungwa teknolojia zilizoimatishwa kutakuwa na CCTV Camera na vyombo vya moto kwa hiyo katika jengo hili kutakuwa na Usalama "Amesema Nley

Kwa upande wake katibu Tawala mkoa wa Tabora Robert Makungu amesema soko hilo limezingatia vigezo vya kibiashara kwani huduma za kifedha zinapatika bila usumbufu wowote

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amesema hatarajii kusikia watu wanatorosha Madini ."Sitaki kusikia mtu anakamatwa kwa kosa la kutorosha Madini atakayekamatwa atachukuliwa hatua za sheria na mtu huyo atakayefanya hivyo ujue hataki maendeleo ya nchi "Amesema Mwanri

Aidha Serikali ya mkoa wa Tabora imeendelea kuwatoa hofu wauzaji na Wafanyabiashara wa kuwauzia Madini katika soko hilo ambapo imesema bei itakuwa ni rafiki na hakutakuwa na ubabaishaji na soko hilo litawasaidia Wafanyabiashara wa Madini kutokwenda nje ya mkoa kuuza madini yao kwani soko hilo limekidhi kila kitu.
Pichani ni Soko kuu la madini la  Mkoani Tabora lililopo Mjini Nzega  Tabor.

Ifikapo Juni 30, mitaa yote ya majiji iwe imesambaziwa umeme- Dkt Kalemani

0
0
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amewaagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha kuwa ifikapo tarehe 30 Juni, 2019, mitaa yote isiyo na umeme katika Majiji yote nchini iwe imesambaziwa umeme.

Dkt Kalemani aliyasema hayo tarehe 5 Mei, 2019, mara baada ya kufanya ziara katika maeneo mbalimbali jijini Dodoma ambayo bado yana nyumba nyingi ambazo hazijaunganishwa na umeme.

Katika ziara hiyo aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt.Tito Mwinuka, Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu, Edward Ishengoma na watendaji wengine kutoka Wizara ya Nishati na TANESCO.

" Mwisho wa kuunganisha umeme kwenye maeneo haya ya Majiji ni Juni 30 mwaka huu, iwe Ntyuka, Mkonze, jijini Dodoma, au Murieti jijini Arusha, haya maeneo yana kero ya umeme lazima yapatiwe nishati hii haraka ili yafanane na hadhi ya Majiji hivyo jukumu la mwananchi ni kufanya wiring na kulipia huduma ya umeme." alisema Dkt Kalemani.

Dkt. Kalemani alisema kuwa kazi ya uuganishaji umeme katika mitaa isiyo na umeme katika mikoa mingine ambayo si majiji itaendelea hadi mwezi Desemba mwaka huu.

Aidha, Waziri wa Nishati aliwataka Wataalam kutoka TANESCO kutokataa malipo ya wananchi wanaotaka kuunganishiwa umeme bali wanapaswa kupokea malipo hayo na kuwasambazia umeme wateja.

Kabla ya kufanya ziara hiyo, Waziri wa Nishati, alifanya kikao na watendaji wa TANESCO ambapo pamoja na kuwapongeza kwa jitihada mbalimbali wanazofanya katika kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na umeme wa kutosha na uhakika, aliwata kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali za umeme zinazoendelea kujitokeza.

Dkt. Kalemani alisema kuwa moja ya changamoto wanayopaswa kushughulikia ni kuunganishia umeme wateja waliolipia huduma ya umeme na hawajaunganishwa kwa muda mrefu ambapo aliagiza kuwa mwisho wa kuwaunganishia umeme wateja hao ni mwezi wa Tano mwaka huu.

Aidha aliiagiza TANESCO kuhakikisha kuwa, ifikapo mwisho wa mwezi wa Tano mwaka huu, maeneo yaliyounganishwa na umeme wa gridi yanapata umeme wa kutosha na wa uhakika ili kuwawezesha wananchi kufanya shughuli mbalimbali bila kikwazo cha uwepo wa nishati ya kutosha.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akionyesha nyumba bado hazijaunganishiwa umeme katika eneo la Ntyuka jijini Dodoma wakati alipofanya ziara ya kukagua maeneo ya mijini ambayo hayana umeme. Wengine katika picha ni watendaji wa TANESCO na Wizara ya Nishati.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akikagua maeneo ambayo hayajaunganishwa na umeme katika eneo la Mkonze jijini Dodoma.Wengine katika picha ni watendaji wa TANESCO na Wizara ya Nishati.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akikagua maeneo ambayo hayajaunganishwa na umeme katika eneo la Mkonze jijini Dodoma.Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka  (kulia) na Mhandisi Ahmed Chinemba kutoka Wizara ya Nishati (kushoto).
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kukagua maeneo ya mijini ambayo hayana umeme. Wengine katika picha ni watendaji wa TANESCO na Wizara ya Nishati.

MKUU WA TAKWIMU ZA BEI ZANZIBAR ATOA TAKWIMU ZA BEI

0
0
 Meneja Uchumi wa Benki kuu ya Tanzania tawi la Zanzibar Moto Ng'winganele Lugobi(kulia)akijibu baadhi ya maswali yalioulizwa katika Mkutano wa Waandishi wa Habari kuhusiana na Takwimu za Bei ambapo imeonekana kupanda kutoka Asilimia 2.8 kwa Mwaka uliomalizia March 2019 hadi asilimia 2.9 kwa mwaka uliomalizia April 2019 hafla iliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini mjini Zanzibar.
 Mkuu wa Takwimu za Bei katika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar Khamis Abdul-rahman Msham akitoa takwimu za bei kwa waandishi wa Habari mbapo imeonekana kupanda kutoka Asilimia 2.8 kwa Mwaka uliomalizia March 2019 hadi asilimia 2.9 kwa mwaka uliomalizia April 2019 hafla iliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini mjini Zanzibar.
-Meneja Msaidizi Idara ya Uchumi Benki ya Tanzania (BOT)Deogratias Macha akifafanua baadhi ya maswali yalioulizwa katika Mkutano wa Waandishi wa Habari kuhusiana na Takwimu za Bei ambapo imeonekana kupanda kutoka Asilimia 2.8 kwa Mwaka uliomalizia March 2019 hadi asilimia 2.9 kwa mwaka uliomalizia April 2019 hafla iliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini mjini Zanzibar.
 Mwandishi wa Habari wa ZCTV Malik Shahran akiuliza maswali katika Mkutano wa Waandishi wa Habari kuhusiana na Takwimu za Bei ambapo imeonekana kupanda kutoka Asilimia 2.8 kwa Mwaka uliomalizia March 2019 hadi asilimia 2.9 kwa mwaka uliomalizia April 2019 hafla iliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini mjini Zanzibar.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Waandishi wa Habari kuhusiana na Takwimu za Bei ambapo imeonekana kupanda kutoka Asilimia 2.8 kwa Mwaka uliomalizia March 2019 hadi asilimia 2.9 kwa mwaka uliomalizia April 2019 hafla iliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini mjini Zanzibar.
 Mwandishi wa Habari wa TBC Swaumu Mwavura akiuliza maswali katika Mkutano wa Waandishi wa Habari kuhusiana na Takwimu za Bei ambapo imeonekana kupanda kutoka Asilimia 2.8 kwa Mwaka uliomalizia March 2019 hadi asilimia 2.9 kwa mwaka uliomalizia April 2019 hafla iliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini mjini Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

RAMADHAN KAREEM TOKA TZUK DIASPORA

0
0

Ndugu Wanafamilia na Watanzania Waishio UK

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania nchini Uingereza - TZUK DIASPORA Ndugu Abraham SANGIWA, pamoja na Uongozi mzima wa TZUK wanawatakia waislam wote duniani mwezi mtukufu mwema wa Ramadan- 2019.

Uvumilivu na huruma ambavyo ni maadili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ni muhimu zaidi hivi sasa kuliko wakati wowote ule.”

Kwa mantiki hiyo Mwenyekiti Ndugu Sangiwa amesema, *“naomba tutumie mwezi huu wa kujitafakari kwa kukumbuka watu waliopoteza maisha wakati wakisaka usalama na hifadhi na tuonyeshe uungwaji mkono kwa mamilioni ambao wamefurushwa makwao au kupoteza maisha kwa sababu ya vita, ugaidi au mateso na wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na familia zao hasa watoto wadogo wasio na hatia .”*

Pia nawaomba Watanzania tunaoishi hapa UK na maeneo mengine ulimwenguni tuonyeshe mshikamano na upendo kati yetu na kwamba mwezi huu mtukufu wa Ramadhani unatuma ujumbe muhimu zaidi hii leo ya kwamba, “kile kinachotuunganisha kiimarike kuliko kile kinachotugawa.”

TZUK tupo pamoja kwa Upendo na Amani

Abraham SANGIWA
Mwenyekiti
Jumuiya ya Watanzania UNITED KINGDOM

Introducing "Usiniache" (Official Video) ♪ BY MONEY

SPIKA NDUGAI AONGOZA HARAMBEE UJENZI WA VYOO SHULE YA MSINGI KARUME MKOANI DODOMA

0
0

 Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai akizungumza na wananchi wa Kibaigwa wakati wa harambee kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi wa Shule ya Msingi Karume iliyopo Kibaigwa Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. Katika harambee hiyo mifuko 763 ya Saruji ilipatikana, fedha kiasi cha Sh. 2, 645, 900 viliziweza kuchangwa ambapo taslimu ilikuwa ni 1,225, 900 na Ahadi 1, 420, 000/=
 Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa,. Job Ndugai (wa pili kushoto) akiongozana  na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa wakati alipowasili na kwenda kukagua ujenzi wa vyoo vya wanafunzi wa Shule ya Msingi Karume iliyopo Kibaigwa Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
 Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (wa tatu kulia) akimsikiliza Afisa elimu Kata ya Kibaigwa, Ndg. Adilla Muna wakati akikagua ujenzi wa vyoo vyaF wanafunzi wa Shule ya Msingi Karume iliyopo Kibaigwa Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
 Wananchi Mbali mbali wa Kibaigwa wakimsikiliza Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (hayupo kwenye picha) wakati wa harambee kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi wa Shule ya Msingi Karume iliyopo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. Katika harambee hiyo mifuko 763 ya Saruji ilipatikana, fedha kiasi cha Sh. 2, 645, 900 viliziweza kuchangwa ambapo taslimu ilikuwa ni 1,225, 900 na Ahadi 1, 420, 000/=

Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (wa pili kulia)akipokea zawadi ya mfuko wa saruji kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa, Ndg. Elisante Maleko (wa pili kushoto) tukio lililofanyika leo katika Shule ya Msingi Karume iliyopo Kibaigwa Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. Shirika la Bima la Taifa lilitoa mifuko 530 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi wa Shule ya Msingi Karume.

Wananchi wanapaswa kujua Historia yao - Balozi Seif Ali Iddi

0
0

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifanya ziara ya kukagua Mahandaki Mawili ya Mangapwani yaliyokuwa yakitumika kuhifadhia Watumwa ambayo kwa sasa yamekuwa sehemu muhimu ya kujifunza Historia ya Biashara hiyo iliyopigwa marufuku tokea Karne ya 18.
 Balozi Seif Ali Iddi akipewa maelezo ya Biashara ya Utumwa ilivyokuwa ikufanyika katika Mahandaki ya Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale anayesimamia Utalii na Mambo ya Kale Dr. Amina Ameir Issa akielezea jitihada zinazochukuliwa na Wizara kuyasimaia vyema Mahandaki ya Mangapwani.
 Balozi Seif akiuagiza uongozi wa Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale pamoja na ule wa Wilaya kuendelea kuyahifadhi Mahandaki ya Mangapwani ili yaendelee kutoa huduma za Kihistoria. Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Wananchi wanapaswa kujua Historia yao katika dhana nzima ya kuendelea kulinda Uhuru wao, Heshima, Utamaduni na hata mazingira yao yanayowazunguuka ya kila siku.

Alisema Binaadamu asiyejua Historia yake kamwe anakuwa Mtumwa wakati wote akiendelea kutawaliwa kifikra jambo ambalo ni hatari katika maisha yake yanayomuhusu.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo alipofanya ziara fupi ya kuyakagua Mahandaki Mawili ya Mangapwani yaliyokuwa yakitumika kuhifadhia Watumwa ambayo kwa sasa yamekuwa sehemu muhimu ya kujifunza Historia ya Biashara hiyo iliyopigwa marufuku tokea Karne ya 18.

Alisema Zanzibar ilikuwa kituo muhimu cha Historia iliyounganisha sehemu nyingi Duniani historia ambayo Taasisi inayosimamia masuala hayo ambayo ni Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale ina jukumu la kusimamia vyema maeneo yote muhimu ili Wageni pamoja na Wananchi wapate fursa ya kujifunza zaidi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia aliwakumbusha Vijana wanaosimamia maeneo hayo kufanya jitihada ya kujifunza Historia kamili ili kuepuka tabia ya kutoa Taarifa zisizo na uhakika wa Historia ya maeneo wanayofanyia kazi.

Akitoa ufafanuzi Msimamizi wa Mahandaki ya Mangapwani Makame Omar Said alisema maumbile ya eneo hilo muda wote yamekuwa ya kujificha kutokana na hali halisi ya biashara yenyewe ya Utumwa ilivyokuwa ikifanywa kwa kujificha.

Makame alisema utafiti unaonyesha wazi kwamba bado idadi ya Wazawa kufika eneo hilo kwa ajili ya kujifunza Historia yake ni ndogo ikilinganishwa na Wageni pamoja na Wasomi wa fani za Kihistoria.

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale anayesimamia Utalii na Mambo ya Kale Dr. Amina Ameir Issa alimueleza Balozi Seif kwamba Idara ya Mambo ya Kale ilianzishwa Mnamo Mwaka1920.

Dr. Amina alisema hatua hiyo ilifuatiwa na kutungwa kwa Sheria ya Mambo ya Kale Mnamo Mwaka 1941 ikiwa chini ya uangalizi wa Idara ya Mambo ya Kale ikiwa na lengo la kusimamia maeneo Saba ya Kihistoria hapa Zanzibar.

Aliyataja baadhi ya Maeneo hayo kuwa ni pamoja na Mahandaki ya Mangapwani,Msikiti Mkongwe wa Kizimkazi, Mji wa Makutani uliopo katika Kisiwa cha Tumbatu pamoja na Mji wa Mwinyimkuu uliopo Dunga.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale anayesimamia Utalii na Mambo ya Kale alifahamisha kwamba Mahandaki ya Mangapwani yana bahati kubwa ya kutembelewa na Wageni wengi, Watalii, Wanafunzo pamoja na Watafiti ikilinganishwa na sehemu nyengine za Kihistoria zilizopo Zanzibar.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale Bibi Khadija Bakari Juma alisema Wizara hiyo kwa sasa tayari imeshaandaa mpango maalum wa kushajiisha Utalii wa ndani ili kuimarisha zaidi mapato ya Taifa.

Bibi Khadija alisema mpango huo umeaanza kufanya kazi kwa kuwahusisha watendaji wa Wizara hiyo kama muelekeo wa ushajiishaji ili kuungwa mkono ya Wizara nyengine na baadae Wananchi hapa Nchini.

Katibu Mkuu Habari ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa uamuzi wake wa kutenga Bajeti Maalum kila Mwaka inayolenga kuhudumia Uhifadhi wa Maeneo ya Kihistoria hapa Nchini jambo ambalo limeleta matokeo mazuri katika usimamizi wa maeneo hayo muhimu.

Akielezea changamoto zinayoyakabili maeneo mengi ya Kihistoria Nchini Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” Nd. Rajab Ali Rajab alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba uhaba wa wafanyakazi ni tatizo kubwa linalofaa kuangaliwa na Serikali pamoja na Taasisi inayosimamia maeneo hayo.

Nd. Rajab alisema ufinyu huo wakati mwengine hutoa mwanya kwa wahalifu kufanya hujuma katika maeneo hayo ambayo kwa namna yoyote ile yanapaswa kuheshimiwa na kuenziwa kwa vizazi vya sasa na vile vijavyo.

“ Yapo matendo mabaya wakati mwengine hufanyika ya uharibifu a maeneo ya Hifadhi kama uchafuzi wa mazingira kutokana na kukosa usimamizi imara wa Watendaji”. Alisisitiza Mkuu huyo wa Wilaya ya Kaskazini “B”.

Zanzibar iliyokuwa Kituo cha Biashara ya Utumwa katika Mwambao wa Afrika Mashariki ilisimamisha Biashara hiyo chini ya Utawala wa Uingereza Mnamo Mwaka 1873 licha ya baadhi ya Wafanyabiashara kuendelea kufanya biashara hiyo kwa siri.

UZALENDO KWANZA NA DHANA YA MABADILIKO KWA JAMII

0
0


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

   

Ukisikia na ukifatilia unaweza ukaona kama jambo la kawaida tu katika kampeni hii ya Uzalendo kwanza inayongozwa na Steve Mangele Nyerere ambaye kwa kipawa ameweza kukusanya wasanii Zaidi ya 400 kutoka tasnia mbalimbali.


Nikiwa mkoani Tanga Wilaya ya Pangani wakati wa uzinduzi wa AWESO CUP, nilipata kusikia ushuhuda na matokeo ya ziara ya kundi hilo kwa mwaka jana katika Wilaya ya Pangani.


Ambapo moja ya jambo linalotajwa sana ni baada ya  kutoa msukumo wa kupatikana ujenzi wa barabara ya lami ya Tanga mpaka pangani.


Unaweza kujiuliza je wasanii wanaweza kujenga barabara mpaka useme ziara yao kuwa ilizaa matunda la hasha , lakini kutokana na umaharufu wao na wingi wa wafuasi katika mitandao ya kijamii waliweza kupaza sauti na kumshawishi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli ambapo aliagiza itangazwe tenda mara moja hili barabara hiyo ijengwe.


Juma Aweso ni Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa jimbo la pangani anathibitisha nguvu ya kundi hili mbele ya wakazi wa Wilaya ya Pangani.


Aweso anasema anawashukuru wakazi wa pangani kwa kumchangua yeye na kuwa mbunge wao na yeye amepata marafiki kutoka uzalendo kwanza ambao kwa sasa wanaisemea vyema wilaya ya pangani hatimaye kwa sasa Rais ameagiza barabara ya lami ijengwe kuanzia Tanga mpaka pangani.


“tulijaribu kwa nguvu zetu ikishindikana lakini kundi la uzalendo kwanza linaloongozwa na Steve Nyerere lilifika hapa Panagani mwaka jana kisha kuamua kuondoka na ajenda moja tu ya barabara ya Tanga pangani na hatimaye Rais wetu Msikivu Dr Magufuli amekubali kujenga bara bara hii kwa kiwango cha lami na mkandarasi ameagizwa aanze mara moja ifikapo mwezi wa tano”anasema Aweso.


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigella ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi katika Tamasha hilo anakiri kupokea maelekezo kutoka ofisi ya Rais na kwa sasa barabara hiyo kuanza kujengwa mapema.


“taratibu za kutangaza tenda zilishaanza na tupo katika hatua za mwisho za kumpata mkandarasi atakayejenga barabara hii hivyo niwatoe shaka wakazi wa pangani kuwa ujenzi wa barabara hii utaanza mapema mwanzoni mwa mwezi May mwaka huu” amesema RC.Shigella  


RC. Shigella anasema katika ujenzi wa barabara hiyo watamuelekeza mkandarsi ujenzi uanzie pangani kwenda Tanga mjini kama mbunge wa jimbo hilo alivyoomba.

Akizingumza kwa niaba ya wananchi wa Pangani Mkuu wa Wilaya ya  Pangani, Zainab Abdalah anamshukuru kiongozi wa kundi la uzalendo kwanza na wasanii wote pamoja na wadau wengine waliofika pangani na kuendelea kuitangaza vyema wilaya hiyo.


Dc.Zainab anasema kuwa wapo wasanii lakini Steve Nyerere amekuwa na moyo wa kipekee na mzalendo kwa nchi yake kuliko vile wwatu wanavyofikiri.

Anasema kuwa sio jambo dogo kwa mtu kuweza kuwashawishi wasanii wenzio waweze kusafiri na kuja kujitolea kufanya hamasa katika wilaya ya pangani na kuacha raha na starehe zilizopo Dar es Salaam.

Anataja kuwa nchi ya marekani imekuwa ikipata umaharufu kutokana na wasaniii wan chi hiyo wanavyoweza kujivunia mambo yaliyopo nchini kwao hivyo Steve kupitia uzalen do kwanza amechagua njia iliyobora ya kuzungumzia kazi zinazofanya na rais wetu na kutoa hamasa kwa maeneo yaliyopo pembezoni kama pangani.

Akziungumza kwa niaba ya Wasanii wenzie Steve Nyerere ametaja kuwa upendo wa Wasanii kwa nchi yao ndio kitu pekee ambacho kinawafanya watoke kwenda sehemu kama hizo kutoa hamasa.


Anasema Wasanii wa kundi la uzalendo kwanza wametambua kuwa umaharufu wao umetokana na watu hivyo ni wakati wa wao kurudi kwa jamii kusema asante na kuwa daraj akw aajili ya kutatua matatizo yao.


“sio muda wote waytanzania wanatakiwa kuelezwa juu ya nchi yao kwa lugha ngumu kuna muda wanahitaji waambiwe kwa lugha nyepesi kupitia uwasilisho wa Sanaa na wanaelewa haraka na kuendelea kumuunga mkono Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli” anasema Nyerere.


Anataja kuwa Rais Magufuli anamuda wa kuzunguka katika maeneo yote haya kuzungumza yaliyyotendeka lakini sisi kama wasanii wazelendo tunaweza kufika na kuwa sauti yake na ujumbe ukafika haraka sana.
 Mwenyekiti wa Kundi la Uzalendo Kwanza Steve Nyerere akizungumz ana wakzi wa Pangani
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shegella akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Uzalendo kwanza Steve Nyerere

RC MOROGORO, DKT. KEBWE STEVEN KEBWE AWAASA MADAKTARI KUFANYA TAHMINI YA MAGONJWA NA AJALI ZITOKANAZO NA KAZI KWA KUZINGATIA MAADILI

0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, MOROGORO

MKUU wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe, amewaasa madaktari kufanya tathmini ya magonjwa na ajali zitokanazo na kazi kwa kuzingatia miongozo iliyopo.

Dkt. Kebwe alitoa wito huo leo Mei 6, 2019 wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa madaktari na watoa huduma za afya kuhusu namna ya kufanya tathmini ya magonjwa na ajali zitokanazo na kazi mjini Morogoro.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na zaidi ya madaktari 100 kutoka mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam na Morogoro wanashiriki mafunzo hayo.

“Mnapofanya tathmini vizuri mnausaidia Mfuko kulipa fidia stahiki, mfanye tathmini kwa haki, msije mkaingia kwenye mtego msikubali kurubuniwa na huu ndio wito wangu kwenu.” Alisema

Dkt. Kebwe aliupongeza Mfuko kwa hatua iliyofikia hususan katika eneo la kutoa elimu kwa wadau kama madaktari ambao ndio huuwezesha Mfuko kutekeleza wajibu wake wa ulipaji Fidia kwa usahihi.“Kwa sasa tayari mmetoa mafunzo kwa madaktari 764 kote nchini na leo hii idadi nyingine inaongezeka hili ni jambo ambalo mnastahili pongezi kwa kufikia hatua hii katika muda mfupi wa uhai wa Mfuko.” Alisema Dkt. Kebwe.

Alisema Mfuko huu ni muhimu katika nchi yetu katika kipindi hiki ambacho taifa linajenga uchumi wa viwanda.Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba alisema licha ya kutoa mafunzo hayo, lakini pia Mfuko hutumia fursa hiyo kuwaelimisha kuhusu shughuli za Mfuko.

Alisema mafunzo hayo yatatolewa na wataalamu kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa kushirikiana na watalamu kutoka Taasisi ya Mifupa MOI na MUHAS.

Aidha Bw. Mshomba alimpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuona umuhimu wa kipekee katika kujenga uchumi wa viwanda kwa kuweka kipaumbele kwa nchi yetu kama namna ya kutufikisha kwenye uchumi wa kati ifikapo 2020-2025 kwani ni ukweli ulio wazi kwamba hakuna nchi iliyoendelea Duniani bila ya kuwa na uchumi wa viwanda na nilazima wote kama watanzania tusimame pamoja kumsaidia Mhe. Rais.

“Sisi kama Mfuko tutamsaidia Mhe. Rais katika azama yake kwa kuahkikisha kwamba, tunafanya kazi kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha na kuwakinga wafanyakazi kwa kutoa elimu ili kuhakikisha kwamba tunalinda nguvu kazi ya taifa kwa kuzuia ajali makazini au kuzipunguza na hata zinapotokea basi malipo ya Fidia yanafanyika kwa haraka”. Alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven Kebwe, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktarina watoa huduma za afya kuhusu namna ya kufanya tathmini ya magonjwa na ajali zitokanazo na kazi mjini Morogoro leo Mei 6, 2019. Mafunzo hayo ambayo yamewaleta pamoja madaktari kutoka hospitali na umma na binafsi kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara yameandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akitoa neon la utangulizi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe (wapili kulia), akipeana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba, mara baada ya kufungua mafunzo ya siku tano kwa madaktari n a watoa huduma za afya kuhusu namna ya kufanya tathmini ya magonjwa na ajali zitokanazo na kazi. Mafunzo hayo yaliypowaleta pamoja Zaidi ya madaktari 100 kutoka mikoa mitano imeanza leo Mei 6, 2019 mjini Morogoro. Wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Ttahmjni wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary.Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, akitoa mada kuhusu kazi za Mfuko
Mkuu wa Kitengo cha Sheria, WCF, Bw.Abraham Siyovelwa, akitoa mada kuhusu masuala ya kisheria katika kutekeleza majukumu ya Mfuko.
Mkurugenzi Mkuu, Bw. Mshomba (wapili kushoto), akibadilishana mawazo na wataalamu (wawezeshaji), Daktari bingwa mbobezi wa mifupa na viungo nchini, Dkt. Robert Mhina(watatu kushoto), Dkt. Hussein Mwanga na Bw. Yahya Kishashu.

Bolt yaanzisha kitufe cha dharura kwa usalama wa madereva

0
0
Kampuni inayotoa huduma za usafiri kwa njia ya mtandaoni nchini - Bolt imezindua kitufe cha dharura (SOS)  kwa lengo la kuimarisha usalama wa madereva kipindi wanapokutana na hatari yoyote.

Akizungunza na waandishi wa  habari jana jijini Dar es Salamaam Meneja wa Bolt Tanzania Remmy Eseka alisema madereva wanaotumia programu hiyo ya Bolt sasa wanaweza kutumia huduma hiyo mpya ya usalama muda wowote watakapo hisi kuwa wapo hatarini au eneo ambalo si salama. 

Alisema matumizi hayo ya kitufe cha dharura dharura (SOS) yamekuwa kama muendelezo wa Bolt kutumia teknolojia kuimarisha usalama wa madereva wanapokuwa barabarani.

"Usalama wa dereva na abiria ni swala la muhimu sana kwetu. Tunaongeza safu ya usalama wa dereva zaidi ya ule uliopo tayari wa kufutalia mubashara safari kwa kutumia GPS na mfumo wa thathmini.

"Kitufe cha dharura (SOS) kilichopo kwenye programu ya Bolt ya dereva, huwezesha taarifa kuwafikia kampuni ya ulinzi ya SGA Tanzania Limited, kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma hizi Afrika Mashariki" alisema meneja kampuni hiyo ambayo zamani ilifahamika kwa jina la Taxify

Aidha, Meneja wa mauzo na masoko kutoka SGA, Faustina Shoo akisem kitufe cha dharura (SOS) kilichowekwa kwenye programu ya madereva kinapotumika, simu hupelekwa kwenye kituo cha dharura cha SGA, ambao baada ya kuhakiki uhalali wa dereva, wanapeleka gari la wagonjwa au timu ya askari kuelekea alipo dereva kuweza kumsaidia kama watoa huduma wa kwanza. 

"Bolt italipia gharama hizi pamoja na gharama zitakazo pitishwa kwa kila  tukio.
Tunaendeleza nia yetu ya kujibu mahitaji ya wateja/wabia kwa kutoa huduma ya uokoaji wa dharura kwa madereva wa Bolt kutokana na ubia huu. "Madereva wa Bolt wanahakikishiwa kupata huduma ya masaa 24 kupitia kitengo chetu cha dharura iwapo watapata tatizo wakiwa safarini.” alisema.
Mmoja wa abiria wanaotumia programu ya Bolt, akipata huduma kutoka kwa dereva bodaboda baada ya Bolt zamani Taxify inayotoa huduma za usafiri kwa njia ya mtandaoni nchini kuzindua kitufe cha dharura (SOS) jijini Dar es salaam jana  kwa lengo la kuimarisha usalama wa madereva kipindi wanapokutana na hatari yoyote.
 

KATIBU WA BUNGE ATEMBELEWA NA MUWAKILISHI UNDP

0
0
  Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai akimsikiliza Kaimu Muwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Natalie Bovely alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma.
  Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai akimsikiliza Kaimu Muwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Natalie Bovely alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma. Mgeni huyo aliambatana na Mshauri Mkuu wa Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo (LSP), Ndugu Takawira Musavengana na Mratibu wa mradi huo Ndugu Mary Lasway.
Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai akipokea zawadi kutoka kwa Kaimu Muwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Natalie Bovely alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Mstaafu Pinda kuzindua kinywaji cha Kweichow Moutai

0
0
 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda anatarajia kuwa mgeni rasmi katika kongamano utamaduni katika ya China Tanzania pamoja na uzinduzi wa kinywaji cha Pombe Kweichow Moutai litakalofanyika Mei 9 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam Mwakilishi wa Kampuni ya China Moutai Group Charles Wang amesema kuwa ujio wa kinjwaji hicho ni kufungua fursa kati  ya nchi ya Tanzania na China ambapo biashara  ya kiywaji hicho kuingia Tanzania inakuwa nchi ya pili kwa Afrika.

Amesema kuwa kinywaji hicho ni maarufu kwa nchini China hivyo soko la Tanzania ni kudumisha mikakati ya kukuza ushirikiano wa kibiashara  baina ya mataifa nje  ujulikanao Belt Road Initiative.

Wang amesema katika uzinduzi huo viongozi mbalimbali watahudhuria wa serikali na wanadiplomasia ,wafanyabiashara kutoka China pia na ujumbe wa maofisa wa kampuni hiyo wataongozwa na Makamu Katibu Mkuu wa Chama ambaye ni Mkurugenzi wa Bodi ya Kampuni.

Amesema kuwa mara ya kwanza kinywaji hicho kiliingia Afrika Kusini mwaka jana  hivyo imeendelea kupanua soko latika nchi za Afrika na kuwa wazalishaji wa bidhaa zenye ubora ambazo zinatamba katika masoko mbalimbali ya Kimataifa Duniani.
Mwakilishi wa China Moutai Group Charles Wang akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ujio wa kinywaji cha Pombe cha  Kweichow Moutai nchini katika uzinduzi utaofanyika Mei 9 jijini Dar es Salaam.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MKURUGENZI WA IDARA YA AFRIKA YA IMF JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0

 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie alipokutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 6, 2019
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 6, 2019

 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha  Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi alipokutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 6, 2019


Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie na ujumbe wake pamoja na  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpang, Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa palamagamba Kabudi na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto james na maofisa wa Wizara alipokutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 6, 2019


 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana  na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie baada ya kukutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 6, 2019

 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Abebe Aemro Selassie akiongea na wanahabari akiwa na  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpang, Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James na maofisa wa Wizara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 6, 2019
PICHA NA IKULU



Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images