Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

MARUFUKU YA MIFUKO YA "RAMBO" KUANZA JUNI 1 MWAKA HUU


MKUTANO WA SABA WA TAPSEA WAFUNGWA LEO JIJINI ARUSHA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utumishi na Utawala bora wa Zanzibar, Seif Shaban Mwinyi akizungumza wakati akitoa hotuba yake ya kufunga Mkutano Mkuu wa Saba wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), uliomalizika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Maganga akizungumza muda mfupi kabla ya kufungwa kwa Mkutano wao Mkuu wa Mwaka, uliomalizika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha.
Mkufunzi na Mkurugenzi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC), Charles Magaya akizungumza muda mfupi kabla ya kufungwa kwa Mkutano wao Mkuu wa Mwaka, uliomalizika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha.





















































KAMATI YA UONGOZI BUNGE LA AFRIKA YAKUTANA NA MABALOZI WA AFRIKA, MASELE AFUNGUKA KUHUSU UBAGUZI NA UNYANYASAJI WA WAGENI

$
0
0
Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika ‘The Pan African Parliament Bureau’ imekutana na Mabalozi ‘Ambassadors’ wanaowakilisha mataifa mbalimbali barani Afrika katika nchi ya Afrika Kusini kujadili masuala kadha wa kadha kuhusu bara la Afrika. 
Mkutano huo ukiongozwa na Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Roger Nkodo Dang kutoka Cameroon, umefanyika leo Ijumaa Mei 3,2019 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Bunge la Afrika kama sehemu ya mkutano wa maandalizi ya Mkutano wa Pili wa Bunge la Tano la Bunge la Afrika jijini Johannesburg Afrika Kusini.
Akizungumza wakati wa mkutano huo wa Mabalozi wa Afrika walioidhinishwa na Jamhuri ya Afrika Kusini, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele ambaye ni mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini na Naibu Waziri wa zamani nchini Tanzania alisema Bunge la Afrika litajadiliana na kutoa Azimio juu ya tabia ya Xenophobic nchini Afrika Kusini.
“Suala hili linapaswa kuchukuliwa kwa umakini, kuna vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na vikundi tofauti kutoka nje inaonekana kama Afrika Kusini haitaki wageni katika nchi yao… La hasha lakini kwa undani kuna matendo ya uharifu kwa kivuli cha Xenophobia”,alisema Mhe. Masele. 
“Ninafurahi na kuhamasishwa na hatua zilizochukuliwa na serikali ya Afrika Kusini ili kukabiliana na mambo yote ya uhalifu.Tutakuwa makini sana wakati tunajadiliana jambo hili kwa sababu hatutaki kuingilia kati mambo ya ndani ya Afrika Kusini au kuingilia kati vyombo vya usalama kutekeleza majukumu yao”,aliongeza.
Masele aliomba mamlaka ya Afrika Kusini kushughulikia suala la tabia ya Xenophobic katika Afrika kwani haikubaliki.
“Sisi kama Wabunge wa Afrika tunatarajia kuona hatua kali zikichukuliwa dhidi ya waharifu wote, wanaharibu sifa nzuri ya Afrika Kusini na Afrika. Bunge la Afrika litapaza sauti na kukemea suala hili..Vikwazo vya hali yoyote dhidi ya watu binafsi au nchi huumiza watu wasiokuwa na hatia hususani wanawake na watoto na huzuia jitihada za maendeleo za watu wetu na nchi ambazo zina vikwazo”,aliongeza.
Kikao cha Pili cha kawaida cha Bunge la Tano la Afrika kinatarajiwa kuanza mnamo Mei 6, 2019 huko Midrand - jijini Johannesburg Afrika Kusini.
Pamoja na mambo mengine , watajadiliana juu ya Kauli mbiu ya Umoja wa Afrika ya mwaka huu "Mwaka wa Wakimbizi na Watu Waliopotea",ambapo pia Bunge la Afrika litajadili Suluhisho la Kudumu juu ya tatizo la wakimbizi barani Afrika.
Hali kadhalika Bunge hilo, litajadili taarifa juu ya amani na usalama katika bara la Afrika ikiwa ni pamoja na maendeleo ya hivi karibuni na hali ya kisiasa Libya, Sudan, Algeria na mchakato wa amani nchini Sudan Kusini. 
Masele anahimiza pande zote zinazohusika katika majadiliano ya amani zisiwe na upendeleo kwa lengo la kutimiza ahadi zilizotolewa kwa watu wa Afrika.Angalia picha za matukio wakati wa mkutanoWajumbe wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wanaowakilisha mataifa mbalimbali barani Afrika katika nchi ya Afrika Kusini wakiwa kwenye mkutano leo Ijumaa Mei 3,2019 jijini Johanesburg Afrika Kusini. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Makao Makuu ya Bunge la Afrika,Midrand,Johanesburg,Afrika Kusini.Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Roger Nkodo Dang kutoka nchi ya Cameroon akizungumza wakati wa mkutano wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wa nchi za Afrika nchini Afrika Kusini.Kulia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akiandika dondoo muhimu wakati wa mkutano wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wa nchi za Afrika nchini Afrika Kusini.Wajumbe wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wanaowakilisha mataifa mbalimbali barani Afrika katika nchi ya Afrika Kusini wakiendelea na mkutano.Wajumbe wa Kamati ya uongozi ya Bunge la Afrika na Mabalozi wanaowakilisha mataifa mbalimbali barani Afrika katika nchi ya Afrika Kusini wakiwa wamesimama kuwakumbuka watu waliofariki dunia kutokana na majanga yaliyotokea katika baadhi ya nchi za Afrika yakiwemo mafuriko na Kimbunga Keneth.Mkutano ukiendelea.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

MBEYA YETU TV: MASHINDANO YA MBEYA TULIA MARATHON 2019

Shule za Serikali Zaongoza Uandishi wa Insha, EAC na SADC

$
0
0
Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma
Wanafunzi Innocent Shirima na Sada Kimangale kutoka shule za Sekondari Moshi (Kilimanjaro) na shule ya Sekondari Kwemnabara (Tanga) wameshinda nafasi ya kwanza ya uandishi wa insha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2018.
Wanafunzi hao wamepewa vyeti na zawadi kwa ngazi ya kitaifa, leo Jijini Dodoma na Kaimu Katibu Mkuu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu.
Akitoa hotuba wakati wa utoaji wa vyeti kwa wanafunzi hao, Dkt. Semakafu amesema Watanzania waache kujizalilisha kwa kusema shule za Serikali sio bora, kwani watoto hao wanaozalilishwa wakienda kwenye ngazi ya Kimataifa wanafanya vizuri.
"Tukio la leo linatuma ujumbe kwa wale wote wanaoiponda elimu ya Tanzania, kwani washidi wa kwanza wa insha za EAC na SADC wote wanatoka katika shule za Serikali  ambazo zinapondwa kila siku," amesema Dkt. Semakafu.
Ameeleza kuwa, walioifikisha Tanzania hapa ilipo ni Watanzania waliosoma hapahapa Tanzania na wala sio watu waliosoma nje ya Tanzania.
Aidha amempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufungua na kupaanua wigo wa elimu kwa Serikali kulipa gharama za wanafunzi hivyo kuwezesha watoto wote wa Tanzania kupata fursa kupata elimu.
Kwa upande wake, Mratibu wa mashindano hayo kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Sylivia Chinguwile amesema mashindano ya uandishi wa insha yamekuwa chachu kwa vijana kufanya utafiti, kujifunza na kufahamu vizuri mchakato na hatua mbalimbali za uimarishaji mahusiano kwa nchi wanachama.
"Mada zinazoshindaniwa huzingatia makubaliano ya wakuu wa nchi, baada ya hapo kila nchi wanachama huwajibika kutangaza na kubainisha vigezo vya ushiriki kama inavyoelekezwa na sekretarieti za jumuiya husika," ameeleza Sylivia.
Amesema, insha hizo huwasilishwa wizarani baada ya kuteuliwa insha bora katika ngazi ya shule na kusahihishwa na jopo la wataalam, ambapo insha bora za SADC hupelekwa Botswana, makao makuu ya SADC ili kushindanishwa na mataifa wanachama wa Jumuiya hiyo.
Kwa upande wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, insha tano bora hupelekwa Arusha makao makuu ya Jumuiya kwa ajili ya kushindanishwa na mataifa wanachama wa Jumuiya hiyo.
Naye, Mshindi wa insha za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Innocent Shirima ambaye pia ni mlemavu wa macho, amesema mashindano yamewapa fursa ya kujifunza masuala ya jumuiya hiyo.
Hata hivyo, ameomba waratibu wa mashindano hayo kuweka kipaumbele  matumizi ya lugha ya kiswahili katika uandishi wa insha ili kuangaza zaidi lugha ya Kiswahili nje ya mipaka ya Tanzania.
Washindi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kitaifa ni Paschal Thomas kutoka Shule ya Sekondari Kibaha (Pwani), Lazarius Yamawasa kutoka Shule ya Sekondari Mzumbe (Morogoro),  Innocent Shirima kutoka Shule ya Sekondari Moshi (Kilimanjaro), Nasra Kondo kutoka Shule ya Sekondari Kifungilo (Tanga), Hanifa Gunter Harms kutoka Shule ya Sekondari Heritage (Pwani), Mwanaisha Mwalimba kutoka Shule ya Sekondari Kwemkabala (Tanga), Asha Pazi kutoka Shule ya Sekondari Kilangalanga Sekondari (Pwani), Jacquiline Kassian kutoka Shule ya Sekondari Harrison UWATA (Mbeya), Samweli Chale kutoka Mbagala Sekondari (Dar es Salaam) na Coloniel Jishosha kutoka Shule ya Sekondari Shinyanga (Shinyanga).
Washindi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ni Sada Kimangale kutoka Shule ya Sekondari Kwemnabara  (Tanga), David Mkinga kutoka Shule ya Sekondari St. Augustine Tagaste (Dar es Salaam) na Alex Paul kutoka Shule ya Sekondari Longido (Arusha).
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma.
 Mratibu wa Mashindano ya Insha kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari toka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi.Sylivia Chinguwile akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu na kushoto ni Kaimu Kamishna wa Elimu Tanzania.

 Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu na Huduma za Jamii toka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Eliabi Chodata akielezea namna ushiriki wa mashindano hayo kwa upande wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma.
 Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Moshi ya Watu wenye mahitaji maalum, Innocent Shirima  Akitoa neon la shukrani kwa niaba ya wenzake wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu akimkabidhi Cheti cha Pongezi Mshindi wa Mashindano ya Insha kwa Wanafunzi wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Sada  Kimangale kutoka Shule ya Sekondari Kwemkabara ya wilayani Muheza mkoani Tanga leo wakati wa hafla ya kuwapa zawadi washindi wa mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma.Kulia ni Mzazi wa mwanafunzi huyo.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu akimkabidhi Cheti cha Pongezi na fedha taslimu shilingi Laki Tano Mshindi wa Mashindano ya Insha kwa Wanafunzi wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Innocent Shirima kutoka Shule ya Sekondari Moshi ya Watu wenye mahitaji Maalum. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo hiyo  leo wakati wa hafla ya kuwapa zawadi washindi wa mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu akimkabidhi zawadi ya fedha Dola za Kimarekani 500 Mshindi wa Mashindano ya Insha kwa Wanafunzi wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Sada  Kimangale kutoka Shule ya Sekondari Kwemkabara ya wilayani Muheza mkoani Tanga leo wakati wa hafla ya kuwapa zawadi washindi wa mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma.Kulia ni Mzazi wa mwanafunzi huyo.Kushoto ni Bibi. Agnesi Kayola Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda toka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu akimkabidhi Cheti cha Pongezi Mshiriki wa Mashindano ya Insha kwa Wanafunzi wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Hanifa Harms kutoka Shule ya Sekondari Heritage ya Kibaha Pwani wakati wa hafla ya kuwapa zawadi washindi wa mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma.Kulia ni Mzazi wa mwanafunzi huyo. Bi. Shamim Yunga.
 Baadhi ya wanafunzi walioshinda Mashindano ya Insha kwa Wanafunzi wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia zoezi la utoaji zawadi wakati wa hafla fupi ya kuwapa zawadi washindi wa mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu akiwa katika picha ya pamoja na Washindi wa Mashindano ya Insha kwa Wanafunzi wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na wazazi wao mara baada ya kumaliza hafla fupi ya kuwapa zawadi washindi wa mashindano hayo kwa mwaka 2018 leo jijini Dodoma. (Picha na Idara ya Habari –MAELEZO).

Mhe. Kikwete asisitiza kuongeza juhudi katika vita dhidi ya malaria barani Afrika

$
0
0
Rais Mstaafu, Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, katika nafasi yake kama mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End malaria Council) alialikwa kuwa mgeni rasmi katika kikao cha 20 cha mawaziri wa afya wa shirikisho la kiuchumi la nchi za Afrika magharibi - ECOWAS - mjini  Cotonou, Benin. 
Kikao hicho kiliendeshwa chini ya chombo maalum cha afya cha  ECOWAS kinachojulikana kama WAHO – (West African Health organization).  Mkutano huu ni mwendelezo wa kikao cha kikazi ambacho Mhe. Kikwete aliendesha Addis Ababa mwezi wa pili mwaka huu alipokutana na wakuu wa taasisi za kikanda za kiuchumi na sasa anaendelea kuongea na  mawaziri wa afya katika kanda hizo.

Akimkaribisha kuongea katika kikao hicho Prof. Stanley Okolo, Mkurugenzi mkuu wa WAHO, alimtambulisha Mhe. Kikwete kuwa ni mkereketwa wa masuala ya afya na mpiganaji katika azma ya kutokomeza malaria. Kwani akiwa kama Rais wa Tanzania aliweza kuanzisha chombo cha  viongozi wakuu wa Afrika wanaopambana na malaria ijulikanayo kama African Leaders Malaria Alliance (ALMA)  ambacho kinaendelea kufanya kazi vizuri barani Afrika.  Kwamba hata baada ya kustaafu Urais bado anayaendeleza mapambano hayo kwa kupitia taasisi ya kutokomeza malaria ambapo yeye ni mjumbe. Taasisi ya kutokomeza malaria imeanzishwa na Bill gates na Ray Chambers na ina jumla ya wajumbe kumi na moja.  Mhe. Kikwete alikutana na mawaziri hao kwa nia ya kwanza kuwaelezea waheshimiwa uwepo wa taasisi ya kutokomeza malaria, pia kuwasisitizia kuhusu umuhimu wa kuongeza nguvu katika vita dhidi ya malaria.  
Katika Hotuba yake Mhe. Kikwete alielezea kuhusu tatizo la malaria duniani na azma ya Taasisi ya Kutokoeza Malaria kuhakikisha kuwa malaria inatoweka duniani kote.  Mhe. Kikwete alisema kuwa pamoja na mafanikio mazuri yaliyopatikana wakati ya mwaka 2000 hadi 2015 ambapo malengo ya millenia ya kupunguza wagonjwa navifo vya malaria yalitimia, report ya malaria ya mwaka 2018 inaonesha kuwa mafanikio hayo yamesimama na kwamba katika mwaka 2017, Asilimia 90 ya wagonjwa na vifo vya malaria vya dunia nzima vilitokea Afrika.  Report hiyo pia imebainisha kuwa nchi 11 zinabeba asilimia 80 ya wagonjwa na vifo vya malaria.  Ukiachia India nchi nyingine kumi zipo Africa ambazo ni Nigeria, Burkina Faso, Ghana, Niger, Mali, Cameroon, DRC, Mozambique, Uganda na Tanzania;  na tano kati ya hizi zipo Afrika Magharibi. Nchi za ECOWAS bado zilibeba karibia nusu ya wagonjwa na vifo vya malaria vya dunia. Pamoja na kuwa hizi nchi kumi zinabeba asilimia kubwa ya malaria katika Afrika, hali ya malaria pia si nzuri katika nchi nyinginezo.
Malaria ni ugonjwa ambao unaweza kutokomezwa kabisa hapa duniani, alielezea Mhe. Kikwete. Marekani ilitokomeza malaria mwaka 1956, China ambayo nayo ilikuwa na tatizo kubwa la malaria,  katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo haijakuwa na mgonjwa hata mmoja wa malaria na hapo Africa magharibi nchi ya Cabo Verde ipo katika mwelekeo wa kuondokana na malaria wakati Gambia na kaskazini mwa Senegal nao wapo kwenye hatua nzuri.  Hivyo ni vyema tukajifunza pia kutoka kwao.  Mheshimiwa Kikwete alisisitiza kuwa ni lazima juhudi za dhati ziwekwe ikiwa ni pamoja na uongozi wa juu wa serikali na wakuu wa Nchi kuwa mstari wa mbele katika mapambano. Uongozi thabiti wa program za malaria, ushirikiano katika kanda zetu, ili kuondokana na ugonjwa huu ambao sio tu ni tatizo la kiafya bali ni tatizo la kimaendeleo na ni lazima kila sekta nayo ijue kuwa inayojukumu katika vita hivi dhidi ya malaria.
 Rais Mstaafu Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, katika nafasi yake kama mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End malaria Council) akiwa mgeni rasmi katika kikao cha 20 cha mawaziri wa afya wa shirikisho la kiuchumi la nchi za Afrika magharibi - ECOWAS- Cotonou, Benin. 3rd May 2018
  Rais Mstaafu Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, katika nafasi yake kama mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End malaria Council) akihutubia katika kikao cha 20 cha mawaziri wa afya wa shirikisho la kiuchumi la nchi za Afrika magharibi - ECOWAS - Cotonou, Benin. 3rd May 2018
 Wajumbe wakimsikiliza  Rais Mstaafu Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, katika nafasi yake kama mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End malaria Council) katika kikao cha 20 cha mawaziri wa afya wa shirikisho la kiuchumi la nchi za Afrika magharibi - ECOWAS - Cotonou, Benin. 3rd May 2018
 Rais Mstaafu Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, katika nafasi yake kama mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End malaria Council) akhutubia katika kikao cha 20 cha mawaziri wa afya wa shirikisho la kiuchumi la nchi za Afrika magharibi - ECOWAS - Cotonou, Benin. 3rd May 2018

MBEYA YETU TV: MASHINDANO YA MBEYA TULIA MARATHON 2019 YAFANA

WATANZANIA WAISHIO UK WAKUBALI KUUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI

$
0
0
 Mbunge wa Busega Dkt Raphael Chegeni akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dk.AshaRose Migiro mara baada ya kufanya mazungumzo na watanzania wanaokaa na kufanya kazi Uingereza katika fani mbalimbali za afya na biashara. 

Watanzania hao wamekubali kupitia umoja wao kuunga jitihada za  Rais Dk.John Magufuli katika kusaidia upatikanaji wa vifaa muhimu vya kisasa, kuchangia fedha na watalaam wa afya ili kuboresha huduma za afya nchini. 

Watanzania hao wamepongeza jitihada za serikali ya awamu ya tano katika ujenzi na uboreshaji wa huduma za afya mijini na vijijini ambapo serikali imekuwa ikijenga Hospitali, vituo vya afya na Zahanati katika kila Kata.
 Mbunge wa Busega, Dk. Raphael Chegeni akizungumza na Baadhi ya maofisa wa Ubolozi wa Tanzania nchini Uingereza. Kulia kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dk.AshaRose Migiro.
Picha ya pamoja 


Mtanzania Isack Ibrahim Emmanuel atamba katika Kick Boxing nchi China

$
0
0
Mtanzania  Isack Ibrahim Emmanuel ambaye ni Mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha  Liaoning jijini Shenyang nchini China ameendeleza ubabe wake katika mchezo wa Kick Boxing baada ya kushinda katika pambano lake lingine la la uzito wa kilo 60kg kwenye mashindano ya “Vita ya Mfalme” katka mji wa Jiling,Jiji la Changchun, kwa kumtwanga kwa TKO mpinzani wake Li Haoran (李浩然).

Wiki iliyopita Mtanzania huyu hodari alimtoa kwa KO mwishoni mwa raundi ya kwanza mpinzani wake aitwaye  Hubulan (胡布).
  Isack Ibrahim Emmanuel baada ya refa kusimamisha pambano baada ya kumchakaza kwa TKO raundi ya kwanza  mpinzani wake  Li Haoran (李浩然).
 Isack Ibrahim Emmanuel baada ya refa kusimamisha pambano baada ya kumchakaza kwa TKO raundi ya kwanza  mpinzani wake  Li Haoran (李浩然).

DRMUMBI SHOW: Wow! Did Tanzania “REJECT” IMF’s biased Report!

Serikali yasisitiza majadiliano kuboresha sekta ya habari

$
0
0
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Serikali imesema haina mpango wa kuendelea kuvifungia vyombo vya habari vinavyokiuka kisheria kwenye utekelezaji wa majukumu na badala yake itaendelea kutumia njia ya majadiliano pale inapotokea changamoto ya kiutendaji.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas aliyasema hayo jana jijini Dodoma wakati akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2019.


Dkt. Abbas alisema ni vyema wadau wa habari wakaunda kamati maalum itakayoketi na kujadiliana na Serikali kuhusiana na changamoto mbalimbali wanazodhani ni vikwazo kwenye utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo vifungu na sheria za habari.


Aidha Dkt. Abbas aliwahimiza wadau wa habari kuzisoma na kuzielewa vyema sheria hususani Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 ili wanapokutana na Serikali kwenye majadiliano wawe na uelewa wa kutosha kuelezea vifungu vyenye changamoto tofauti na hivi sasa ambapo baadhi wanalalamika bila kuweka wazi vifungu gani vina mapungufu.


Katika maadhimisho hayo, washiriki walipendekeza maazimio 16 ikiwemo kuunda kamati itakayoketi na Serikali kujadiliana baadhi ya changamoto zinazokwamisha uhuru wa habari kama vile kufungia vyombo vya habari pamoja na kanuni zenye vikwazo kwenye Sheria ya Huduma za Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016.


Taasisi mbalimbali zilishiriki kufanikisha maadhimisho hayo ikiwemo MISA Tanzania, Ubalozi wa Marekani, Internews, FES, IMS, Umoja wa Mataifa, UTPC, TMF, TEF, UK Aid, TAMWA, MCT, Unesco na Serikali ya Tanzania huku kauli mbiu ikiwa ni “wajibu wa vyombo vya habari kwa demokrasia, tasnia ya habari na uchaguzi nyakati za upotoshaji wa taarifa”.

Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Inmi Patterson akizungumza kwenye maadhimisho hayo ambapo alisisitiza juu ya uhuru wa vyombo vya habari katika kutimiza majukumu yake bila kuingiliwa.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke akitoa salamu zake kwenye maadhmisho hayo.
Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakary Karsan akichangia mada kwenye maadhimisho hayo.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa ofisi ya Tanzania, Stella Vuzo akitoa salamu za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kwenye maadhimisho hayo.
Washiriki wa maadhimisho hayo wakifuatilia ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kwa njia ya vidio.
Fuatilia matukio katika picha kwenye maadhimisho hayo.
Washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2019 kitaifa jijini Dodoma wamesimama kwa muda kama ishara ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) na pia mmiliki wa makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi aliyefariki usiku wa kuamkia jana nchini Dubai akiwa na miaka 77.
Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Washiriki wakifuatia mada kwenye maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Misa Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbas (kushoto) baada ya kuwasili kwenye maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbas akiwa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Inmi Patterson pamoja na viongozi kutoka taasisi mbalimbali kutembelea mabanda ya maonyesho ya kitaaluma kwenye maadhimisho hayo.
Wachezaji wa ngoma za asili kutoka kabila la Wagogo walinogesha mapokezi ya washiriki na viongozi mbalimbali.
Picha na KD Mula

Soko la Pili la madini lafunguliwa Mkoani Shinyanga huku Gramu elfu 30 za dhahabu zikiwa zimeshauzwa

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amefungua soko la madini Ijumaa tarehe 03 Mei, 2019 katika Wilaya ya Shinyanga likiwa ni soko la pili baada ya soko jingine kufunguliwa Wilayani Kahama mwezi mmoja uliopita.
Akitoa hotuba ya ufunguzi wa soko hilo katika eneo la Ofisi ya CCM Mkoa ambapo wafanyabiashara tisa (9) wa Dhahabu na Almasi wamefungua masoko yao hapo, Mhe. Telack amesema tangu agizo la Mhe. Dkt. John Magufuli la kufungua masoko ya madini, tayari madini ya dhahabu yenye gramu 30,924.44 yameshauzwa katika soko la Kahama yakiwa na thamani ya sh. Bilioni 2.9.
Telack amewashukuru wafanyabiashara hao kwa kuitika wito wa Serikali na kufungua soko katika Mkoa wa Shinyanga.
Aidha, ametoa wito kwa wachimbaji wadogo, wauzaji na wanunuzi kutumia soko hilo la madini na waache kuuziana madini sehemu zisizo rasmi na atakayekamatwa anafanya hivyo madini yatataifishwa na wahusika watashtakiwa kwa mujibu wa sheria.
Kaimu Afisa Madini Mkazi Mhandisi Giliard Luyoka, akisoma taarifa ya madini Mkoa, amesema hadi sasa Mkoa una wafanyabiashara wakubwa 9 na wadogo 22 na kuwa licha ya Mkoa kuwa na utajiri wa madini yenye thamani ambapo wachimbaji wadogo wanazalisha wastani wa kilo 600 za dhahabu na karati 1300 za almasi kwa mwaka, hakukuwa na masoko rasmi ya uuzaji wa madini hivyo kupelekea utoroshwaji wa madini hatimaye Taifa kutonufaika na madini hayo.
Naye mwenyekiti wa Chama cha Wachimba madini Mkoa wa Shinyanga Bw.Hamza Tandiko amesema kuwa, wanaunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha madini yote yanayopatikana Mkoani Shinyanga yanawasaidia wananchi wa Mkoa huu kwa kuchangia pato la Taifa.
“Tuendelee kumuunga mkono Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, kufikia mwaka 2025 angalau sisi tuliopo kwenye sekta ya madini tuweze kuchangia angalau asilimia 10 ya pato la Taifa kwani Serikali imeonesha uzalendo kwa kufuta kodi hivyo deni limebaki kwetu” amesema Hamza.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akiwasili katika eneo la soko la madini na kupokelewa na viongozi wa Chama cha wachimba madini Mkoa wa Shinyanga 
 Katibu wa Chama cha Wachimbaji madini Mkoa wa Shinyanga Bw. Gregory Kibusi akitoa neno katika ufunguzi wa soko la madini lililopo Wilaya ya Shinyanga
 Baadhi ya wananchi na wadau wa madini waliohudhuria ufunguzi huo wakimsikiliza mgeni rasmi Mhe. Mkuu wa Mkoa (hayupo pichani) 
  Mwenyekiti wa Chama cha Wachimba madini Mkoa wa Shinyanga Bw. Hamza Tandiko akizungumza katika tukio hilo
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi waliohudhuria ufunguzi wa soko la pili la madini katika Mkoa wa Shinyanga 
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akikata utepe kuashiria ufunguzi wa soko hilo
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wanunuzi wa madini aliyefungua soko leo

MBEYA YETU TV: HAJI MANARA ANOGESHA MBEYA TULIA MARATHON 2019

MBEYA YETU TV: HAJI MANARA ANG'AKA MBEYA, AWASHUKIA KOCHA MWINYI ZAHERA NA KOCHA WA MBEYA CITY

Halmashauri Manispaa ya Tabora yakabiliwa na Uhaba wa vyumba vya Madarasa 132.

$
0
0


Na, Editha Edward-Tabora.

Uhaba wa Miundombinu ya madarasa,viti,meza katika shule za msingi, Halmashauri ya  manispaa ya Wilaya ya Tabora, unatajwa kurudisha nyuma jitahada za  ufaulu wa wanafunzi wilayani humo.

Hayo yamebainishwa mapema hii leo na mkuu wa Wilaya ya  Tabora Manispaa,Erick Komanya wakati akipokea mifuko 200 ya Saruji kutoka shirika la Reli Tanzania Mkoa wa Tabora (TRC).

Komanya amesema tatizo hili la uhaba wa madarasa linayumbisha jitihada za ufaulu kwa vijana walioko mashuleni huku akiwahakikishia  wadau wote wanaotoa michango yao ili kuinua Elimu  katika Halimashauri ya Wilaya ya  Tabora Manispaa kuwa michango hiyo itafanya kazi iliyokusudiwa.

"Madarasa 128 ambayo tumekusudia kuyajenga kwa mwaka huu, kila kata katika Halimashauri ya Manispaa ya Tabora inatakiwa kuhakikisha inajenga vyumba vinne (4)vya Madarasa" amesema Komanya.

Akizungumza na Michuzi Blog  Kwaniaba ya Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini Bwn Kadogosa Masanja,mkuu wa chuo cha Reli mkoani Tabora ndugu John Kaberege,huku akikabidhi mifuko 200 ya saruji amesema shirika limeamua kufanya hivi ikiwa ni moja ya kufanya kazi ya jamii  Coorparate Social Responsibility(CSR).

"Shirika la Reli mkoani Tabora tumeamua kuchangia mifuko hii ya saruji ili kutengeneza mazingira mazuri ya Elimu kwa watoto wetu ambao ni viongozi wa kesho" amesema Kaberege.

Hatahivyo Halimashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Tabora bado inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya Madarasa zaidi ya 230 ikiwa mahitaji ni vyumba 360 na tayari vyumba 128 vimeshaingizwa kwenye mpango wa Ujenzi, hali hii inapelekea baadhi ya wanafunzi kukaa kwa kubanana na  kushusha kiwango cha Ufaulu wao.


MAKAMU WA RAIS WA BUNGE LA AFRIKA AKUTANA NA WABUNGE WAPYA WA BUNGE LA AFRIKA

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele amekutana na Wabunge wapya wa Bunge la Afrika wataoapishwa siku ya Jumatatu Mei 6,2019 wakati wa Mkutano wa Pili wa Bunge la Tano la Bunge la Afrika jijini Johannesburg Afrika kusini.
Mkutano huo wa kuwajengea uwezo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Bunge la Afrika ikiwemo kuwaeleza historia na jinsi bunge hilo linavyofanya kazi umefanyika katika ukumbi mdogo wa makao makuu ya Bunge la Afrika uliopo Midrand,jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Mheshimiwa Masele ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini nchini Tanzania,amewapongeza hao wabunge 26, kutoka nchi tano zikiwemo Eswatini, Msumbiji, Uganda, Zambia na Algeria kwa kuchaguliwa kuwakilisha katika Bunge la Afrika.
Kikao cha Pili cha kawaida cha Bunge la Tano la Afrika kinatarajiwa kuanza siku ya Jumatatu Mei 6,2019 ambapo wabunge zaidi ya 250 watajadiliana juu ya kauli mbiu ya Umoja wa Afrika ya mwaka huu “Mwaka wa Wakimbizi na Watu Waliopotea” na suluhisho la kudumu juu ya tatizo la wakimbizi barani Afrika.
Mijadala mingine itahusu  taarifa juu ya amani na usalama katika bara ikiwa ni pamoja na maendeleo ya hivi karibuni na hali ya kisiasa Libya, Sudan, Algeria na mchakato wa amani nchini Sudan Kusini. 
Na Kadama Malunde – Johannesburg,Afrika Kusini.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza wakati wa mkutano na wabunge wapya wa Bunge la Afrika leo,katika ukumbi mdogo wa Bunge la Afrika,Johannesburg nchini Afrika Kusini 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akiwakaribisha wabunge wapya wa Bunge la Afrika.
Sehemu ya wabunge hao wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akielezea jinsi Bunge la Afrika linavyofanya kazi.
Sehemu ya wabunge hao wakiwa ukumbini.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza ukumbini.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akiwaelezea jambo wabunge hao wakati akiwatembeza katika jengo la ofisi za utawala za Bunge la Afrika.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele akielezea jambo wakati wabunge wapya wa Bunge la Afrika wakitembelea ofisi za Bunge la Afrika nchini Afrika Kusini.
Mheshimiwa Masele akiwaeleza jambo wabunge hao.
Mheshimiwa Masele akizungumza na wabunge hao.
Mheshimiwa Masele akiwaeleza jambo wabunge hao.
Picha ya pamoja,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele na wabunge wapya wa Bunge la Afrika.
Picha ya pamoja,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele na wabunge wapya wa Bunge la Afrika. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

WAZIRI MKUCHIKA AWATEMBELEA WAJANE WA HAYATI SOKOINE NYUMBANI KWAO MONDULI

$
0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akiongozana na wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, mama Napono Sokoine na Nakiteto Sokoine na baadhi ya wanafamilia kuelekea kwenye kaburi la Hayati Sokoine alipoitembelea familia hiyo nyumbani kwao Monduli, jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akisali na wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, mama Napono Sokoine na Nakiteto Sokoine na baadhi ya wanafamilia kwenye kaburi la Hayati Sokoine alipoitembelea familia hiyo nyumbani kwao Monduli, jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akisoma maandishi kwenye kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine alipoitembelea familia ya Hayati Sokoine nyumbani kwao Monduli, jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Kushoto kwake ni msemaji wa familia, Bw. Lemburisi Kivuyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akipokea vazi la kimila kutoka kwa wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, mama Napono Sokoine na Nakiteto Sokoine alipowatembelea wajane hao nyumbani kwao Monduli, jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, mama Napono Sokoine na Nakiteto Sokoine alipowatembelea wajane hao nyumbani kwao Monduli, jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akizungumza na wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, mama Napono Sokoine na Nakiteto Sokoine alipowatembelea wajane hao nyumbani kwao Monduli, jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akimkabidhi kadi ya bima ya afya mjane wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, mama Napono Sokoine alipowatembelea wajane wa Hayati Sokoine nyumbani kwao Monduli, jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akimkabidhi kadi ya bima ya afya mjane wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, mama Nakiteto Sokoine alipowatembelea wajane wa Hayati Sokoine nyumbani kwao Monduli, jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, mama Napono Sokoine na Nakiteto Sokoine na baadhi ya wanafamilia alipowatembelea wajane hao nyumbani kwao Monduli, jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akiagana na wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, mama Napono Sokoine na Nakiteto Sokoine alipowatembelea wajane hao nyumbani kwao Monduli, jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.


MARY MWAKAPENDA

OFISI YA RAIS-UTUMISHI

KIWANDA CHA RUAHA MILLING COMPANY MKOMBOZI KWA WAKULIMA WA ZAO LA MPUNGA NYANDA ZA JUU KUSINI

$
0
0
Naibu meya manispaa ya Iringa kupitia chama chama mapinduzi (CCM),Joseph Ryata akiwa na mkurugenzi wa kiwanda cha Ruaha milling company Atanas Kipeto wakiwa katika kiwanda hicho cha kuchakata mpunga kuwa mchele
Naibu meya manispaa ya Iringa kupitia chama chama mapinduzi (CCM),Joseph Ryata akiwa na mkurugenzi wa kiwanda cha Ruaha milling company Atanas Kipeto akiwa na wadau wengine waliofika katika kiwanda hicho
Mkurugenzi wa kiwanda cha Ruaha milling company Atanas Kipeto akiwa katika kiwanda hicho

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Kiwanda cha Ruaha milling company kuchakata mpunga kilichopo mkoani iringa kimetajwa kuwa mkombozi kwa wakulima wa zao la mpunga ambalo limekuwa likilimwa kwa wingi katika wilaya ya Iringa na mkoa wa mbeya.

Akiwa ametembelea kiwanda hicho naibu meya manispaa ya Iringa,Joseph Ryata alisema kuwa kiwanda hicho kimejengwa kwa kiwango cha kimataifa ambacho kitasaidia kukuza kipato cha wakulima wa zao hilo.

“Kwa kweli jamani niseme ukweli kiwanda hiki ni moja ya viwanda bora sana hapa nchini ambavyo vinachakata mpunga kuwa mchele ukiangalia uwekezaji wake utagundua kuwa Ruaha milling company kinakuja kuwa mkombozi kwa wakulima wetu” alisema Ryata

Ryata aliwataka wakulima wa zao la mpunga kulima kwa wingi zao hilo kwa kuwa kiwanda cha Ruaha milling company kinahitaji kiwango kikubwa cha zao hilo ili kufanya kazi kwa uhakika hivyo wakulima jukumu lenu ni kulima kwa wingi na kwa ubora unaotakiwa.

“Naombeni nitoe rai kwa wakulima kulima kwa wingi zao hili kwa kuwa kiwanda hichi kinahitaji kuwa na tani nyingi za zao hilo la mpunga ili kuhakikisha kiwanda hicho kinafanya kazi kwa ufanisi unaotakiwa” alisema Ryata

Ryata alisema kuwa kiwanda hicho kimekuwa mkombozi kwa kuwa kinaongeza thamani ya zao hilo na kuongeza kipato kwa wakulima wa nyanda za juu kusini kwa kuanzisha kuwa na vifungashio ambavyo vinatoka katika kiwanda hicho.

“Kiwanda hichi kinafanya kila kitu na kinatenga chenyewe kulinga na ubora wa mchele wenyewe hivyo wakulima mnatakiwa kuwa na amani huku mkilima kilimo hicho kwa ubora unaotakiwa” alisema Ryata

Aidha Ryata alisema kuwa serikali inatakiwa kuendelea kuwaunga mkono wawekezaji wazawa kwa kuwa ndio wanafanya kazi ipasavyo kwa kutoa faida inayotakiwa kwa taifa.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kiwanda cha Ruaha milling company,Atanas Kipeto alisema kuwa lengo la kujenga kiwanda hicho ni kuhakikisha anakuza thamani ya zao la mpunga na kukuza maisha ya wakulima ambao wamekuwa wakinyonywa na madalali.

“Mimi nimejenga kiwanda hiki kwa lengo tu la kuwapa thamini yao wakulima wa zao la mpunga ambao wamekuwa wakilima kwa taabu lakini hawapati ile faida au matunda yanayotakiwa kwa kununua bei nzuri ambayo inafaida kwa wakulima” alisema Kipeto

Kipeto aliongeza kuwa amekuwa akinunua zao la mpunga kwa kilo tofauti na wafanyabiashara wengine wanaonunua kwa gunia ambao kwa asilimia kubwa wamekuwa wakiwanyonya wakulima kwa kununua kwa kujaza lumbesa.

“Kununua kwa zao kwa kilo ni kuongeza thamani ya mazao kwa wakulima na ndio njia pekee ya kuacha kuwanyonya wakulima ambao ndio mara nyingi wamekuwa ngazi ya wafanyabiashara kutajirika” alisema kipeto

TUMIENI HATI ZA HAKI MILIKI ZA KIMILA KUTAFUTA MIKOPO YA UWEKEZAJI - DC UYUI

$
0
0

 Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora Gift Msuya akisisitiza umuhimu wa wananchi kutumia hati milki za kimila za kumiliki ardhi kujiletea maendeleo jana katika Kijiji cha Miyenze.
 Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanynge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu akieleza faida za mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100 wa Kijiji cha Miyenze Wilayani Uyui Mkoani Tabora wakati wa hafla ya kufungua mafunzo hayo jana katika Kijiji cha Miyenze.
 Kikundi cha Ngoma kutoka Kijiji cha Miyenze Wilayani Uyui mkoani Tabora kikitoa burudani wakati wa hafla ya kufungua mafunzo kwa wakulima wa Kijiji ya Miyenze yaliyoandaliwa na Kuratibiwa na Ofisi ya Rais MKURABITA ili kuwawezesha wakulima hao kuwa na kilimo chenye tija.
 Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya wazee maarufu wa kijiji cha Miyenze Wilayani humo jana baada ya kukabidhi hati 100 kwa wakazi wa eneo hilo.
 Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mhe Gift Msuya akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya wakulima waliopata hati miliki za kimila za kumiliki ardhi wa kijiji cha Miyenze Wilayani humo.
  Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Miyenze wakimsikiliza jana Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya wakati wa hafla ya ugawaji wa hati za hakimiliki za kimila za ardhi kwa wakazi 100. PIX7. Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya akitoa hati ya hatimiliki ya kimila jana kwa Mkazi wa Kijiji cha Miyenzi Masele Makonda.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya akitoa hati ya hatimiliki ya kimila jana kwa Mkazi wa Kijiji cha Miyenzi Rufunga Maguki. Picha na WHUSM
NA TIGANYA VINCENT
WAKAZI wa Kijiji cha Miyenze wilayani Uyui wametakiwa kutumia hati za hakimiliki za kimila walizopewa kuomba mikopo kwa ajili ya uwekezaji katika kilimo na shughuli nyingine za kiuchumi ili kujiletea maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya wakati wa kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima wa Kijiji cha Miyenze na kukabidhi hati za hakimiliki ya ardhi za kimila kwa wakazi 100.

Alisema wakazi walipata hati za haki miliki hizo za kimila wanao usalama wa zao za ardhi na wameiongezea thamani ambayo inawafanya kuwa na fursa za kupata pesa.

Msuya aliongeza kuwa hati hizo zitawasaidia kupata dhamana hata kwenye vyombo vya kisheria kama vile Mahakama pindi wanatakiwa kuweka mali isiyo hamishika.

Alisema hati walizopata ni fursa pia ya kuwawezesha kuingia ubia na wawekezaji mbalimbali ambao wanatafuta ardhi inayotambulika kisheria kwa ajili ya kuwekeza katika sekta za viwanda, hoteli, maduka na shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wakazi wa Kijiji hicho na maeneo mengine katika wilaya hiyo ambao mashamba yao hayajapimwa kuhakikisha wanaypima ili kuyaongezea thamani na kuwaondoa katika umaskini na kupunguza migogoro.

Alisema hakuna haja ya wananchi kukumbatia maeneo makubwa ambayo hayajapimwa kwa kuwa hayawezi kuwasaidia kupata maendeleo yao na nchi kwa ujumla kwa kuwa ni sawa na mali mfu.

Kwa upande wa Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanynge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu alisema kuwa pamoja na kutoa hati hizo watawajengea uwezo wakulima 100 na viongozi 10 jinsi ya kuendesha kilimo bora na utunzaji wa kumbukumbu za hesabu za kilimo na biashara.

Alisema maeneo mengine ni jinsi ya kutafuta fursa na kuzitumia na ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara na uandishiwa mpango wa biashara na uundaji wa vikundi vya uchumi.

Naye mmoja wa wakulima wa Kijiji cha Miyenze William Mauye aliishukuru Serikali kwa kuwawezesha kupima mashamba yao na hatimaye kuwapatia hati za haki miliki za kimila kwa kuwa zitawasaidia kuinua kipato chao kwa kuwa watakuwa na fursa ya kupata mikopo ya benki.

Alisema mkopo atakaochukua utamwezesha kununuza zana za kilimo za kisasa kwa ajili ya kuboresha kilicho chake cha mpunga na mahindi na hivyo kuongeza uzalishaji.

Mauye aliiomba Serikali kupitia MKURABITA kuendelea kuwasaidia wananchi wa vijiji ili wapimie ardhi yao na kuepuka baadhi ya watu ambao wakuwa wakichukua fedha zao bila hata kuwapimia maeneo yao.

Mhini kuongoza timu ya kuogelea ya Tanzania katika mashindano ya vijana Budapest, Hungary

$
0
0
Muogeleaji nyota nchini, Dennis Mhini ni miongoni mwa waogeleaji saba waliochaguliwa na chama cha mchezo wa kuogelea Tanzania (TSA) kuunda timu ya Taifa itakayo wania taji la michuano ya Dunia iliyopangwa kufanyika nchini, Hungary.
Mhini ambaye kwa sasa anasoma na kuogelea katika shule ya St Felix ya Uingereza, ataungana na waogeleaji wenzake, Delvin Barick wa klabu ya Mwanza na muogeleaji wa kike, Kayla Temba ambaye anatokea klabu ya DSC. 
 Waogeleaji wengine ni Laila Rashid kutoka klabu ya Taliss-IST, Christopher Fitzpatrick (Mwanza), Christian Shirima (DSC) na Khaleed Ladha wa Taliss-IST. 
 Gharama za usafiri, maradhi na mahitaji mengine kwa waogeleaji watatu, Mhini, Delvin na Kayla zitatolewa na Shirikisho la mchezo wa kuogelea duniani (Fina) wakati waogeleaji wanne, Laila, Fitzpatrick , Christian Shirima na Khaleed wanatakiwa kusafirishwa na TSA kwa kushirikiana na wadau. 
 Katibu Mkuu wa TSA, Inviolata Itatiro alisema kuwa Fina imewapa fursa ya kuwakilishwa na waogeleaji wengine kutokana na kuridhishwa na maendeleo ya mchezo wa kuogelea nchini. Inviolata alisema kuwa ni vigumu kuamini hivyo kutokana na changamoto zinazoukabili mchezo, ikiwemo ukosefu wa bwawa la kuogelea la kisasa, lakini bado waogeleaji wa Tanzania wamefanikiwa kufanya vyema katika mashindano ya kimataifa. 
 “Tunahitaji sapoti kutoka kwa wadau, kwani Fina ipotayari kuwasafirisha waogeleaji watatu na kocha wao tu. Hawa waliobaki ni kazi ya TSA na wadau, hata hivyo TSA haina fedha kutokana na kuingia madarakani miezi kadhaa iliyopita,” alisema Inviolata.
 Dennis Mhini akichapa maji
Dennis Mhini akichupa hewani
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images