Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

Rc mbeya awashukuru wananchi na viongozi mbali mbali ziara ya Rais Dkt. magufuli

$
0
0
Ndugu zangu wana Mbeya Tunawashukuru sana wote Kwa umoja wenu na upendo wenu mliouonesha Kwa Mh Rais wetu Dkt John P. Magufuli. Mlikuwa wengi na mmefunika. Najua zipo changamoto nyingi ambazo watu wetu waliamua kuandika mabango ili Mh Rais atatue. Nitumie nafasi hii kuwajulisha wote kujenga utamaduni wa kufika ofsn kwangu au kwa wasaidizi wangu maana tumepewa kazi ya kusikiliza na kutatua kero.

Nawashukuru sana CCM Mbeya, Chini ya Uongozi wa Mzee Mwakasole Mwenyekiti, hakika mmetenda haki katika ziara hii. Chama n mshauri na Mwajiri wa Serikali, umoja na mshikamano ndio msingi wa kufika mbele. Nashukuru sana viongozi wa Dini zote Kwa umoja wenu. Mmeshikamana na hakika mmetusaidia sana kumsimika Mungu baba katika kila kona ya ziara yetu. Asante sana. Pia nawashukuru sana snaa wafanyabiashara na wadau wengine wote kwa namna mlivyonibeba na kuwa pamoja na mimi katika sherehe za MEI MOSI mmeonesha umoja sana. Assnte sana.

Umefika wakati wa kuijenga Mbeya Kwa kasi na umoja. Sote tuwe na dhamira ya kuifanya Mbeya big city... asante sana sana sana Wana Mbeya, Mbarali, Chunya, Busokelo, Kyela, na kata zake zote.

Mawaziri na Wabunge wote nawashukuru sana. Mh Lukuvi, Mh. Jafo, Mh. Hasunga, Mh. Naibu Speaker, Mh. Biteko, Mh. Kakunda, Mh. Mwanjelwa, Dkt Mwakyembe na Mh Naibu waziri wa ujenzi Pamoja na Mawaziri wengine wote. Wabunge wote wa mkoa huu mmenipa heshima kubwa. Assnte sana Jeshi la Police Kwa kazi nzuri ya kulinda amani chini ya mzee Wangu Kamanda wa Police Mkoa Matei Asante sana

Wakuuu wa Wilaya, Ma DAS na Wakurugenzi wote Ndio mmekuwa kiungo namba Sita katika ziara hii yote. Yote tuliyoagizwa tutatekeleza kama yalivyo. Mmechapa kazi vzr thanks sana.

Asanteni sana snaa. Mimi na wenzangu wote katika ofisi yangu nawashukuru sana
Albert Chalamila
RC Mbeya
03/05/2019

TANZIA

WAZIRI MKUCHIKA AWATAKA WAAJIRI KUWAPA RUHUSA MAKATIBU MAHSUSI KUHUDHURIA SEMINA NA VIKAO

$
0
0
WAZIRI wa Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala bora, George Mkuchika amewataka waajili kuwapa ruhusa makatibu mahsusi kuhudhuria semina na vikao, kwani kutokufanya hivyo wanarudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Mkuchika ameyasema hayo leo wakati akifungua mkutano mkuu wa saba wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) unaofanyika jijini Arusha na kuwaambia kuwa wao kama Serikali wanaadaa waraka kwa waajili hao kuona umuhimu wa kuwapa ruhusa makatibu hao mahtasi.

Amesema kuwa mwajili hatakiwi kumnyima ruhusa Katibu Mahsusi, kwani viongozi wakuu wa nchi wanatambua umuhimu wa makatibu hao katika kujenga maendeleo ya nchi kwani hakuna viongizi waliofanikiwa bila wao.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utumishi na Utawala bora wa Zanzibar, Seif Shaban Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatoa ushirikiano wa dhati kujenga na kuongeza ushiriki wa Makatibu Mahsusi kwa maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi nchini (TAPSEA), Zuhura Maganga amesema changamoto ya mtaala inarudisha nyuma taaluma yao ikiwa pamoja na kutokupandishwa madaraja kwa Makatibu Mahsusi jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya kada hiyo.
Waziri wa Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala bora, George Mkuchika akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano wa Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utumishi na Utawala bora wa Zanzibar, Seif Shaban Mwinyi akizungumza wakati akitoa salamu zake kwa wanachama wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) wakati wa Mkutano wao Mkuu wa Mwaka, uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro akizungumza wakati akitoa salamu zake kwa naiba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, katika Mkutano wa Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Maganga akizungumza katika Mkutano wao Mkuu wa Mwaka, uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha.
Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC), Seleman Shindika akizungumza katika Mkutano wao Mkuu wa Mwaka, uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha.
Waziri wa Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala bora, George Mkuchika akipokea zawadi tuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Maganga.
Waziri wa Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala bora, George Mkuchika akimkabidhi tuzo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utumishi na Utawala bora wa Zanzibar, Seif Shaban Mwinyi.











































































































UJERUMANI YATOA MSAADA WA SH. BILIONI 330 KWA AJILI YA MRADI WA MAJI MKOA WA SIMIYU

$
0
0
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
SERIKALI ya Ujerumani kupitia Benki yake ya  Maendeleo (KfW), imeipatia Tanzania msaada wa  Euro milioni 127.7, sawa na sh. bilioni 330, kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria katika mkoa wa Simiyu.
Makubaliano ya msaada huo kupitia mikataba miwili yamesainiwa Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James kwa niaba ya Serikali na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani, (KfW) anayeshughulikia nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya, Dkt. Klaus Mueller.
Katika mkataba wa kwanza, kiasi cha Euro 102.7, sawa na shilingi bilioni 265 kimetolewa na Mfuko wa Kimataifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi (Green Climate Fund) na mkataba wa pili unahusisha Euro milioni 25, sawa na sh. bilioni 65 ambazo zimetokelewa na Benki ya Maendeleo ya UJerumani (KfW).
Mbali na mradi wa maji  wa Simiyu ambao chanzo chake cha maji ni kutoka Ziwa Victoria, miradi mingine itakayonufaika na msaada huo ni kilimo endelevu cha umwagiliaji, usafi wa mazingira, maji na malisho ya mifugo na kuzijengea uwezo taasisi zitakazotekeleza mradi huo hasa mamlaka za maji katika Wilaya tano za Bariadi, Itilima, Meatu, Busega na Maswa zitakazonufaika na mradi huo.
"Kutokana na umuhimu wa mradi huo wa maji, Serikali kwa upande wake itachangia Euro milioni 40.7 sawa na sh. bilioni 104 na wananchi watakao nufaika na mradi huo watachangia Euro milioni 1.5 sawa na sh. bilioni 3.8 na kufanya gharama za mradi mzima kufikia zaidi ya Euro milioni 171 sawa na zaidi ya sh. bilioni 446" alisema Bw. Doto James
Aliishukuru Serikali ya Ujerumani kupitia Mfuko wake wa Kimataifa wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi (GCF) na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) kwa kutoa kiasi hicho kikubwa cha fedha kitakachotumika kutekeleza mradi huo utakachukua miaka mitano hadi kukamilika kwake.
"Katika kipindi cha miaka  mitatu Serikali ya Ujerumani imeipatia Tanzania zaidi ya Euro 202.8 sawa na shilingi bilioni 518.5 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za afya, nishati, uhifadhi wa maliasili, udhibiti wa fedha za umma na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi" alisisitiza Bw. James
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki ya KfW amesema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa Mfuko wa Kimataifa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kutoa kiasi kikubwa cha fedha cha Euro milioni 102.7 kwa mkupuo katika nchi za kiafrika tangu mfuko huo uanzishwe.
"Tunaamini kuwa zaidi ya watu 500,000 watanufaika na mradi huu wa maji kutoka Ziwa Victoria unaohusiana na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa kutuhifadhi vyanzo vya maji, usafi wa mazingira, kuendesha kilimo bora chenye kuhifadhi mazingira" aliongeza Dkt. Mueller.
Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo, amempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli na uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango kwa kuipatia Wizara yake zaidi ya shilingi trilioni 3 katika kipindi kifupi cha miaka mili kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maji inayoendelea kujengwa nchini kote.
Alitaja sababu za mkoa wa Simiyu kunufaika na msaada huo kuwa ni mkoa unaokabiliwa na hali mbaya ya hewa ukiwemo ukame na kwamba mradi huo utawawezesha wananchi kuhimili mabadiliko ya tabianchi na kwamba katika ukanda huo wa Ziwa kutakuwa na miradi ya maji yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 1.2 itakayokuwa inatekelezwa.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Mahamoud Mgimwa amesema Bunge litahakikisha linausimamia mradi huo utekelezwe kwa wakati kwa sababu Serikali imedhamiria kwa dhati kuona kwamba wananchi wanapata maji safi na salama kwa asilimia 95 ifikapo mwaka 2025.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW)  katika nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya Dkt. Klaus Mueller, wakisaini Mkataba wa msaada wa  Euro milioni 127.7 sawa na Sh. bilioni 330 kwa ajili ya kugharamia mradi  wa maji kutoa Ziwa Victoria kupitia mradi wa kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Tabia nchi katika Mkoa wa Simiyu, hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia)  na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW)  katika nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya Dkt. Klaus Mueller, wakibadilishana mkataba wa msaada wa  Euro milioni 127.7 sawa na Sh. bilioni 330 kwa ajili ya kugharamia mradi wa maji katika Mkoa wa Simiyu, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia)  na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW)  katika nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya Dkt. Klaus Mueller, wakionesha mkataba wa msaada wa  Euro milioni 127.7 sawa na Sh. bilioni 330 kwa ajili ya kugharamia mradi wa maji katika Mkoa wa Simiyu baada ya kusainiwa, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia), akieleza kuwa licha ya msaada wa Sh. bilioni 330 kutoka Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW), kwa ajili ya  mradi wa maji ya Ziwa Victoria katika Mkoa wa Simiyu, Serikali ya Tanzania itachangia kiasi cha Euro milioni 40.7 ambayo ni sawa na Sh. 104.1 kutokana na umuhimu wa mradi huo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo (kushoto), Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe. Mahamouud Mgimwa (Mb)(wapili kushoto), Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedhja na Mipango Bw. John Rubuga (wa pili kuli) na Kamishna wa Sera wa Wizara hiyo Bw. Mgonya Benedicto wakiwa katika  hafla ya utiwaji saini mikataba miwili yenye jumla ya kiasi cha Euro milioni 127.7 sawa na Sh. bilioni 330 kwa ajili ya kugharamia mradi wa maji katika Mkoa wa Simiyu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo, akieleza kuwa Euro milioni 127.7 sawa na Sh. bilioni 330 zilizotolewa na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW)  zitawanufaisha wananchi wa Mkoa wa Simiyu kupitia miradi ya maji, kilimo cha umwagiliaji na usafi wa mazingira, wakati wa hafla ya kusaiiniwa kwa msaada wa fedha hizo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti  wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Mahamoud Mgimwa (Mb), akieleza kuwa msaada wa Sh. bilioni 330 zilizotolewa kwa ajili ya miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi utasaidia kuondoa malalamiko ya mda mrefu ya wabunge wa wilaya zitakazonufaika na mradi huo kuhusu ukosefu wa maji Mkoa wa Simiyu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (katikati)  na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW)  katika nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya Dkt. Klaus Mueller (wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Tanzania na Benki ya KfW ya Ujerumani baada ya kukamilika kwa hafla ya kusainiwa mkataba wa msaada wa  Euro milioni 127.7 sawa na Sh. bilioni 330 kwa ajili ya kugharamia mradi wa maji kutoa Ziwa Victoria kwenda Mkoa wa Simiyu. (Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango)

JK Mgeni Rasmi kwenye kikao cha mawaziri wa Afya wa ECOWAS mjini Cotonou, Benin

$
0
0
Rais Mstaafu, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, katika nafasi yake kama mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End malaria Council) alialikwa kuwa mgeni rasmi katika kikao cha 20 cha mawaziri wa afya wa shirikisho la kiuchumi la nchi za Afrika magharibi - ECOWAS.  

Kikao hicho kiliendeshwa chini ya chombo maalum cha afya cha  ECOWAS kinachojulikana kama WAHO – (West African Health organization). Mkutano huu ni mwendelezo wa kikao cha kikazi ambacho Mhe. Kikwete aliendesha Addis Ababa mwezi wa pili mwaka huu alipokutana na wakuu wa taasisi za kikanda za kiuchumi na sasa anaendelea kuongea na  mawaziri wa afya katika kanda hizo.

Akimkaribisha kuongea katika kikao hicho Prof. Stanley Okolo, Mkurugenzi mkuu wa WAHO, alimtambulisha Mhe. Kikwete kuwa ni mkereketwa wa masuala ya afya na mpiganaji katika azma ya kutokomeza malaria. Kwani akiwa kama Rais wa Tanzania aliweza kuanzisha chombo cha viongozi wakuu wa Afrika wanaopambana na malaria ijulikanayo kama African Leaders Malaria Alliance (ALMA)  ambacho kinaendelea kufanya kazi vizuri barani Afrika.  
Kwamba hata baada ya kustaafu Urais bado anayaendeleza mapambano hayo kwa kupitia taasisi ya kutokomeza malaria ambapo yeye ni mjumbe. Taasisi ya kutokomeza malaria imeanzishwa na Bill gates na Ray Chambers na ina jumla ya wajumbe kumi na moja.  

Mhe. Kikwete alikutana na mawaziri hao kwa nia ya kwanza kuwaelezea waheshimiwa uwepo wa taasisi ya kutokomeza malaria, pia kuwasisitizia kuhusu umuhimu wa kuongeza nguvu katika vita dhidi ya malaria.  

Katika Hotuba yake Mhe. Kikwete alielezea kuhusu tatizo la malaria duniani na azma ya Taasisi ya Kutokoeza Malaria kuhakikisha kuwa malaria inatoweka duniani kote.  

Mhe. Kikwete alisema kuwa pamoja na mafanikio mazuri yaliyopatikana wakati ya mwaka 2000 hadi 2015 ambapo malengo ya millenia ya kupunguza wagonjwa navifo vya malaria yalitimia, report ya malaria ya mwaka 2018 inaonesha kuwa mafanikio hayo yamesimama na kwamba katika mwaka 2017, Asilimia 90 ya wagonjwa na vifo vya malaria vya dunia nzima vilitokea Afrika.  
Ripoti hiyo pia imebainisha kuwa nchi 11 zinabeba asilimia 80 ya wagonjwa na vifo vya malaria.  Ukiachia India nchi nyingine kumi zipo Africa ambazo ni Nigeria, Burkina Faso, Ghana, Niger, Mali, Cameroon, DRC, Mozambique, Uganda na Tanzania;  na tano kati ya hizi zipo Afrika Magharibi. 

Nchi za ECOWAS bado zilibeba karibia nusu ya wagonjwa na vifo vya malaria vya dunia. Pamoja na kuwa hizi nchi kumi zinabeba asilimia kubwa ya malaria katika Afrika, hali ya malaria pia si nzuri katika nchi nyinginezo.

Malaria ni ugonjwa ambao unaweza kutokomezwa kabisa hapa duniani, alielezea Mhe. Kikwete. Marekani ilitokomeza malaria mwaka 1956, China ambayo nayo ilikuwa na tatizo kubwa la malaria,  katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo haijakuwa na mgonjwa hata mmoja wa malaria na hapo Africa magharibi nchi ya Cabo Verde ipo katika mwelekeo wa kuondokana na malaria wakati Gambia na kaskazini mwa Senegal nao wapo kwenye hatua nzuri.  
Hivyo ni vyema tukajifunza pia kutoka kwao.  Mheshimiwa Kikwete alisisitiza kuwa ni lazima juhudi za dhati ziwekwe ikiwa ni pamoja na uongozi wa juu wa serikali na wakuu wa Nchi kuwa mstari wa mbele katika mapambano. 

Uongozi thabiti wa program za malaria, ushirikiano katika kanda zetu, ili kuondokana na ugonjwa huu ambao sio tu ni tatizo la kiafya bali ni tatizo la kimaendeleo na ni lazima kila sekta nayo ijue kuwa inayojukumu katika vita hivi dhidi ya malaria.

Baadhi ya wakinamama wajawazito hupoteza maisha kwa kuchelewa kufika vituo vya Afya.

$
0
0


Mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka akizungumza Wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe salama ilyofanyika mkoni hapo.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi wa Jiongeze tuwavushe salama iliyofanyika mkoani Simiyu.
Wadau wakiwa katika uzinduzi wa Kampeni ya Jiongeze tuwavushe salama Mkoani Simiyu.

Na.Vero Ignatus.

Baadhi ya akina  mama katika Halmashauri ya mji Bariadi hawana maamuzi ya kwenda hospitali kupata huduma za afya, wakisubiri ruhusa kutoka Kwa waume wao au wakwe zao.

Hayo yamesemwa na  Mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto katika halmashauri ya Mji wa Bariadi, Frida Buyoga katika uzinduzi Wa kampeni ya ' Jiongeze Tuwavushe Salama katika mkoa wa Simiyu, amesema ukosefu huo wa kutoa maamuzi umepelekea wengi wao kupoteza Maisha Kwa sababu ya kuchelewa kufika vituo vya Afya.

Ukosefu wa maamuzi pia unapelekea baadhi ya akina mama hao  kushindwa kupanga uzazi wa mpango mpaka wawaulize waume zao.

 Buyoga,  amesema hali hii imepelekea vifo vya vya akina mama 14 , kati ya 120 waliochelewa kufika vituo vya afya kwa sababu mbalimbali mwaka jana.

Licha ya akina mama hao kufariki, watoto wao waliokuwa bado hawajazaliwa (tumboni)  walikutwa hawachezi (wamefariki) baada ya kuchelewa kufika vituo vya Afya.

Amesema miongoni mwa sababu nyingine zinazopelekea baadhi ya akina mama  kuchelewa kufika vituo vya Afya ni pamoja na umbali Wa baadhi ya  vituo vya Afya, ambapo baadhi yao hulazimika kusafiri hadi kilometa 30 kwenda katika vituo vya Afya.

" Jitihada Kubwa zimefanyika kusaidia wajifungue Salama, ikiwemo ujenzi Wa zahanati na vituo vya Afya unaofanywa na serikali na wadau wa maendeleo.

Amesema katika halmashauri ya mji wa Bariadi, akina mama wastani 15-22 wanajifungua kila wiki , ikiwa ni ongezeko Kwa wanaokwenda kujifungua katika vituo vya Afya.

" Baadhi ya akina mama wamekuwa wakijifungua Nyumbani, lakini baada ya kuwapa elimu, wengi wao sasa hivi wanakwenda vituo vya Afya kujifungua na kupata huduma Kwa ajili yao na watoto wao, anasema Buyoga.

Amesema uzinduzi Wa kampeni ya 'Jiongeze Tuwavushe Salama' utasaidia sana kuelimisha akina mama kwenda katika vituo vya Afya, kujua Afya zao na kufuatilia chanjo zote muhimu, ili kujilinda wao na watoto wao.

BALOZI DKT. ULISUBISYA MPOKI AFUNGA MKUTANO WA WATAALAMU WA DAWA ZA USINGIZI NA GANZI

$
0
0
      Balozi Dkt.Ulisubisya Mpoki akimkabidhi Dkt.Albert Ulimali cheti cha  mafuzo ya  kutoa  huduma za dawa ya usingizi na ganzi  yaliyofanyika kwenye hoteli ya Peacock jijini Dar es salaam.
 Balozi Dkt.Ulisubisya Mpoki  akifunga Mkutano wa  wataalamu wa kutoa  huduma za dawa ya usingizi na ganzi  iliyofanyika kwenye hoteli ya Peacock jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wataalamu wa kutoa  huduma za dawa ya usingizi na ganzi wakiwa kwenye mkutano uliofanyika katika  hoteli ya Peacock jijini Dar es salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

MAUA SAMMA ALIVYOKONGA NYOYO ZA MASHABIKI WAKE KING SOLOMONI

$
0
0
Mwanamziki wa nyimbo za kizazi kipya, Maua Sama akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa nywele za zambarau kutoka Kampuni ya Darling uliofanyika katika Ukumbiwa King Solomoni Kinondoni usiku wa kumkaia leo jijini Dar es Salaam.
Wanamitindo kutoka Kampuni ya Shahbaaz wakionyesha mitindo mbalimbali ya matumizi ya nywele wakati wa uzinduzi wa nywele za zambarau(purple) kutoka Kampuniya Darling uliofanyika katika Ukumbiwa King Solomoni Kinondoni usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA NNE KWA WATU WANAOAMINI UMILIKI WA ARDHI NA MAKAZI UKO SALAMA

$
0
0
Na Munir Shemweta, DODOMA

Tanzania imeshika nafasi ya nne kati ya nchi tisa za Kusini na Mashariki mwa Afrika zilizofanyiwa utafiti kwa kuwa na asilimia 64 ya watu wanaoamini kuwa hali ya umiliki wa ardhi na makazi ni salama.

Hayo yalibainika leo tarehe 3 Mei 2019 wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Msingi kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, uzinduzi ulifanyika jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa kuzindua Ripoti hiyo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema kiwango hicho ni kikubwa zaidi ya wastani wa asilimia 61 kwa nchi tisa zilizofanyiwa utafiti katika Afrika ya Magharibi.

Aidha, Utafiti wa Ripoti hiyo unaonesha Tanzania imeshika nafasi ya kumi kati ya nchi 33 zilizoshiriki katika Utafiti huo kwa kuwa na asilimia zaidi ya hamsini ya watu wanaomiliki makazi yao wenyewe.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, matokeo ya utafiti huo yametokana na hatua mbalimbali ambazo serikali imeendelea kuzichukua ili kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na usalama wa umiliki wa ardhi na makazi.

Kawa mujibu wa Dkt Mabula, kama ungefanyika utafiti mwingine leo basi huenda matokeo yake yangekuwa tofauti kutokana na Serikali kudhamiria kupanga , kupima na kumilikisha kila kipande cha ardhi na kutolea mfano katika mwaka wa fedha 2018/2019 Serikali ilipanga kupima na kumilikisha vipande vya ardhi.

Dkt Mabula alibainisha kuwa, takwimu zinaonesha kati ya mwezi Agosti 2018 na Machi 2019 Hatimiliki 36,428 zimeandaliwa kwa wamiliki wa viwanja na mashamba na Hatimili za kimila 286472 ziliandaliwa kwa ajili ya wamiliki wa ardhi walioko vijijini.

Dkt Mabula alisema, hatua nyingine ambazo serikali imechukua ni pamoja na kuanza kutumia mifumo ya kielektroniki katika utoaji huduma za ardhi ambapo Mfumo Unganishi wa Kumbukumbu za Sekta ya Ardhi (ILMIS) umeendelea kufanyiwa majaribio katika wilaya za Ubungo na Kinondoni na kusisistizia kuwa mfumo huo utasaidia kuongeza kasi ya umilikishaji ardhi na kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa..

Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt Albina Chuwa alisema utafiti uliofanyika ulishirikisha sekta zote muhimu na kuzitaja baadhi yake kuwa ni pamoja na Wizara ya Ardhi, Global Land Allience, DFID sambamba na wananchi wote wakiwemo wakuu wa kaya za Tanzania Bara na Zanzibar.

Alisema, Tanzania ni nchi ya kwanza kutoa ripoti yake mwenyewe kati ya nchi 33 na ripoti hiyo itatumiwa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika kupanga mipango yake na kuzitaka taasisi za vyuo kutumia ripoti hiyo kufanyia utafiti ili kuisaidia sekta ya ardhi.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizindua Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Msingi kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 3 Mei 2019. Kushoto ni Mwakilishi wa kutoka Taasisi ya Prindex David Ameyaw na wa pili kulia ni Mtakwimu Mkuu Serikali Dkt Albina Chuwa.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akionesha Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Msingi kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania baada ya kuizindua jijini Dodoma leo tarehe 3 Mei 2019. Kushoto ni Mwakilishi wa kutoka Taasisi ya Prindex David Ameyaw na wa pili kulia ni Mtakwimu Mkuu Serikali Dkt Albina Chuwa.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi wa taasisi wakati wa uzindua Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Msingi kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 3 Mei 2019. Wa pili kushoto waliokaa ni Mwakilishi wa kutoka Taasisi ya Prindex David Ameyaw na wa pili kulia waliokaa ni Mtakwimu Mkuu Serikali Dkt Albina Chuwa.(PICHA NA WIZARA YA ARDHI)


WAZALISHAJI WA MAZAO YA NAFAKA NCHINI WAHIMIZWA KUONGEZA THAMANI BIDHAA ZAO

$
0
0
Wazalishaji wa mazao ya nafaka nchini wahimizwa kuongeza thamani bidhaa wanazozalisha nchini na sio kuuza mazao ghafi ili soko liweze kuongezeka na kuleta faida katika sekta ya kilimo inayochangia katika ukuaji wa uchumi nchini. 

Hayo yamesemwa na Mheshimiwa Richard Kasesela, Mkuu wa Wilaya wa Iringa alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa wazalishaji wa mazao ya nafaka nchini uliofanyika tarehe 3 Mei, 2019 mkoani Iringa uliondaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade). 

Akiongea na washiriki zaidi ya 150 amesema sekta ya kilimo inaajiri watanzania zaidi ya asilimia 67 na kuchangia katika pato la Taifa kwa asilimia 30 na kuingiza dola bilioni 1.2 ambazo ni chache ukilinganisha na ardhi tuliyonayo na inalisha asilimia 65 ya malighafi katika sekta ya viwanda na zaidi ya asilimia100 katika chakula. 

“Kuna bidhaa hatujaziendeleza hadi sasa na zina fursa nzuri sana kwenye masoko nje ya nchi kama vile cornflakes na zinaliwa nchi nzima na hadi sasa Watanzania hawajaamua kuwekeza kwenye viwanda vinavyozalisha bidhaa hizi” alisema Mhe Kasesela 

Aliongeza kwa kusema kuwa msingi wa ustawi wa kilimo ni upatikanaji wa soko la uhakika, katika kutekeleza hilo serikali ya awamu ya tano imetengeneza mazingira rafiki kupitia uwekezaji wa viwanda kwa kutumia malighafi zake nchini 

Ameiomba TanTrade isaidie wafanyabiashara nchini katika kufundisha mikakati mbalimbali ya biashara hasa kwa kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia ili kuweza kufanya biashara kupitia simu za viganjani kupitia mifumo mbalimbali ya tehama. 

Alihitimisha kwa kutoa wito kuwa katika mkutano huo maazimio yajikite kwenye kutoa majibu ya ubora wa mbegu, namna ya uhifadhi bora wa mazao, kuondokana na kilimo cha kutegemea mvua hasa katika maeneo yanayopitiwa na mito kwa kutumia maji machache, kuboresha mifumo mizuri ya kupata takwimu sahihi, masoko na pia kufanya mkutano huu uwe endelevu kila mwaka na katika kila maazimio yanayotolewa kwenye mkutano maafisa biashara, kilimo na ushirika wa serikali lazima washiriki ili kuweza kusaidia katika kusimamia na kutekeleza maazimio ya kila mkutano 

Bw Edwin Rutageruka, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade aliongeza kwa kusema kuwa mkutano huu utakuwa chachu kwa wazalishaji ili kuleta matokeo ya kuongeza uzalishaji, kuweza kutosheleza soko la ndani na kuangalia masoko katika nchi zinazotuzunguka katika ukanda wa Afrika Mashariki na nchi katika nchi wanachama wa jumuiya ya SADC 

Na amewasisitiza wazalishaji wa mazao ya nafaka nchini kushiriki katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ambapo kutakuwa na mikutano ya wafanyabiashara (B2B) ili kuweza kupata masoko endelevu. 

Bw Ledis Kigala, Afisa Programu kutoka Baraza la Nafaka la Afrika Mashariki aliongeza kwa kusema kuwa, Tanzania inauza mazao ya nafaka kama vile mchele, mahindi na maharage katika nchi jirani. Wakulima wameweka nguvu zaidi kwenye uzalishaji wa mahindi meupe wakati asilimia 90 ya mahindi yanayozalishwa duniani ni ya Njano. 

Pia alisema kuwa kuna fursa kubwa ya masoko kwa mazao ya nafaka hasa mahindi na mtama kwaajili ya matumizi ya viwanda vya bia ingawa hadi sasa changamoto kubwa katika sekta ya mazao haya ni uwepo wa sumu kuvu na uhifadhi bora wa mazao. 

Nae Bi Karungi Gotifrid, Afisa Ubora kutoka Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko amewahimiza wakulima wa mazao ya nafaka kujiunga katika vikundi ili waweze kupewa elimu na alitoa vigezo vya mahindi yanayonunuliwa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kama ifuatavyo unyevunyevu chini ya asilimia 13, mahindi yasiyokomaa chini asilimia 1, uchafu chini ya asilimia 1, mahindi yaliyooza na yenye ugonjwa hayatakiwi kuwepo ili kuepusha sumu kuvu, mahindi yaliyoliwa na wadudu hayatakiwi kuwepo kwasababu yanaondoa kiini ambacho kinahitajika kwa bianadamu vilevile mdudu hai haitajiki ndani ya magunia ya mahindi na pia mahindi yaliyovunjika yawe chini ya asilimia 1 

WAANDISHI WA HABARI,WADAU WA HABARI SHINYANGA WAADHIMISHA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

$
0
0


Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga 'Shinyanga Press Club - SPC) imeadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani na kutaka usalama wao uzingatiwe kwenye kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu pamoja na uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo, Mei 3, 2019 kwenye ukumbi wa mikutano wa Liga Hoteli Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimwakilisha mkuu wa mkoa huo Zainab Telack na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Shinyanga wakiwemo viongozi wa kidini, siasa, makampuni,serikali na taasisi zisizo za kiserikali. 

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Mkuu huyo wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko amewataka wanahabari mkoani Shinyanga kutumia kalamu zao vizuri kuhamasisha amani na utulivu vitawale kwenye kipindi cha uchaguzi wa Serikai za mitaa na uchaguzi mkuu ujao, ili wananchi waweze kuchagua viongozi wanaowataka kuwaletea maendeleo bila ya kubughuziwa. “Kauli mbiu yenu ya maadhimisho ya uhuru wa habari mwaka huu 2019 'ya “Jukumu la UTPC na Klabu za Waandishi wa habari kuchangia uchaguzi huru na haki”, 

imekuja kwa muda muafaka, ikiwa tunaelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa ambapo waandishi wa habari ni kiungo muhimu kwenye uchaguzi huu ikiwamo kutoa taarifa kwa wananchi pamoja na kudumisha amani,”amesema Mboneko. “Hivyo nawaomba waandishi wa habari muitumie kalamu yenu vizuri sana kwenye kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ili kutoa taarifa kwa wananchi juu ya umuhimu wa kupiga kura, pamoja na kulinda amani kwenye uchaguzi,”ameongeza Mboneko. 

Pia amewataka waandishi wa habari kujikita kuandika habari kwa wingi zenye kuhamasisha wawekezaji wa viwanda kwenda kuwekeza mkoani Shinyanga ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa wa Shinyanga. Kwa upande wake Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Lutusyo Mwakyusa, amewatoa wasiwasi waandishi wa habari na kuhusu usalama wa waandishi wa habari wakati wa uchaguzi akibainisha kuwa usalama utakuwepo juu yao kwenye kipindi hicho cha uchaguzi wa Serikali za mitaa na kutoa wito kwao huku akiwakumbusha kuwa kutokiuka miiko na maadili na taaluma zao. 

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga Shabani Alley, akisoma hotuba ya Klabu hiyo, amewaomba viongozi wa Serikali kufanya kazi kwa ukaribu na waandishi wa habari, ili kuutangaza mkoa huo pamoja na kudumisha amani na utulivu ili upate kukua kimaendeleo. 

"Waandishi wa habari mkoani Shinyanga tumejipanga vyema kushirikiana na serikali, wanasiasa na wadau mbalimbali katika kuhakikisha kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao unakuwa wa haki,tunaomba tuendelee kushirikiana ili kuhakikisha mkoa wetu unakuwa salama na kukua kimaendeleo",aliongeza Alley.


Maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mwaka huu 2019 yana kauli mbiu isemayo “Jukumu la UTPC na Klabu za waandishi wa habari kuchagia uchaguzi huru na haki” ambapo wadau wa habari na waandishi wa habari mkoani Shinyanga pia wamejadili pia kuhusu usalama wa mwandishi wa habari katika kipindi cha uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu na umuhimu wa vyombo vya habari katika uchumi wa viwanda. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Shinyanga Press Club. Mboneko aliwataka waandishi wa habari mkoani humo kutumia kalamu zao kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kupiga kura ili kuchagua viongozi sahihi pamoja na kudumisha amani. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ,Shaban Alley,kulia ni Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Lutusyo Mwakyusa. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwataka waandishi wa habari mkuano Shinyanga kujikita pia kuandika habari za kuchochea uwekezaji wa viwanda ili kukuza uchumi wa mkoa. Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoani Shinyanga Shabani Alley akisoma hotuba ya Klabu hiyo siku ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani mwaka 2019. Awali kabla ya kuanza kwa maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga, mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiongoza Sala ya kumuombea Mmiliki na Mwanzilishi wa Makampuni ya IPP MEDIA Dkt. Reginald Mengi ambaye amefariki dunia jana akiwa Dubai kwa matibabu.Dkt. Mengi ni miongoni mwa watu ambao wana mchango mkubwa sana kwenye Tasnia ya Habari. Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Lutusyo Mwakyusa akiwahakikishia usalama wao waandishi wa habari kwenye kipindi cha uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao 2020. Mkurugenzi msaidizi wa Radio Faraja FM Stereo Mjini Shinyanga Anikazi Kumbemba ambaye pia ni Mwandishi Mwandamizi akielezea dhumuni la maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani. Waandishi wa habari Mkoani Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari. Waandishi wa habari mkoani Shinyanga pamoja na wadau wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari. Wadau wa habari Mkoani Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani. Maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Shinyanga yakiendelea. Waandishi wa habari na wadau wakiwa kwenye maadhimisho siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani. Shabani Katambi ambaye ni mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini akichangia mada kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani mkoani Shinyanga. Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akichangia mada kwenye maadhimisho siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani na kuwataka waandishi mkoani Sinyanga wakijikite pia kuandika habari za kuhamasisha utalii ili Serikali iweze kupata mapato. Diwani wa Kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi (CHADEMA)akichangia mada kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani mkoani Shinyanga na kuwataka waandishi wa habari mkoani humo, waandike pia habari ya kufufua kiwanda cha Nyama ambacho hakifanyi kazi katika manispaa hiyo. Waandishi wa habari na wadau wa habari wakiendelea kusikiliza uchangiaji wa mada kwenye maadhimisho hayo ya uhuru wa vyombo vya habari. Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Maguja akichangia mada kwenye maadhimisho ya uhuru wa habari na kuwataka wanahabari wajikite pia kwenye maadili pale wanapokuwa wakiandika habari zao ili kuepuka kujiingiza kwenye matatizo. Mdau wa habari Chief Abdala Sube naye akichangia mada kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari na kuvipongeza vyombo hivyo namna vinavyofanya kazi ya kutetea maslahi ya wananchi kwa kutatua kero zao. Mwenyekiti wa mtaa wa Dome manispaa ya Shinyanga Solomoni Najulwa 'Cheupe', akivipongeza vyombo vya habari namna vilivyosaidia kuunyosha mtaa huo ambapo ulikuwa ukikabiliwa na changamoto nyingi. Waandishi wa habari wakiwa na wadau wa habari kwenye maadhimisho ya uhuru wa habari wakisikiliza uchagiaji wa mada mbalimbali. Mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru Chibura Makorongo akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya uhuru wa vyombo vya habari, na kuwataka viongozi wa Serikali waboreshe mahusiano mazuri na wana habari ili kutangaza fursa za mkoa. Wadau wa habari Mkoani Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani. Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakipiga picha ya pamoja na wadau wa habari mara baada ya kumaliza kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

TEN/MET, YAWASIMAMISHA WANAHABARI KUMKUMBUKA DK MENGI

$
0
0

Na Joachim Mushi


MTANDAO wa Elimu Tanzania (TEN/MET) jana uliwasimamisha waandishi wa habari mbalimbali kwa dakika moja kabla ya kuanza mkutano nao, ikiwa ni ishara ya kumkumbuka Marehemu Dk. Reginald Mengi Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP ambaye amefariki dunia.


Akizungumza kabla ya tukio hilo, Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga alisema Marehemu Mengi alikuwa mmoja wa wadau wa elimu na amefanya mambo mengi kuchangia mafanikio ya sekta hiyo hivyo wanakila sababu ya kumkumbuka.

"...TEN/MET imeguswa na msiba wa Marehemu Dk. Mengi kwa kuwa alikuwa mdau mzuri katika kuchangia elimu, amefanya mambo mengi kuchangia na kusaidia wahitaji katika elimu...naomba tusimame kwa dakika moja kumkumbuka," aliwaambia wanahabari.

Jana  TEN/MET ilikutana na waandishi wa habari mbalimbali jijini Dar es Salam kuzungumzia shughuli za maadhimisho ya Juma la ELimu (GAWE) linalo tarajia kufanyika mkoani Tanga katika Wilaya ya Handeni.

Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Wayoga akizungumzia maadhimisho hayo alisema mwaka huu yataanza Mei 6 hadi 10, 2019 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chanika, huku yakiambatana na mikutano vijiji mbalimbali kwa madhumuni ya kuhamasisha wanajamii kuhusu ushiriki wa pamoja na serikali katika kuboresha elimu iliyojumishi na endelevu.

"...Tarehe 10 Mei itakuwa ni kilele cha wiki ya uhamasishaji wa Elimu. Mgeni na mgeni wa Heshima atakuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa. Kamati ya Maandalizi ya TEN/MET imeamua Kauli mbiu kwa Tanzania iwe ni: “ELimu Bora, Haki Yangu”.

Aidha alisema maadhimisho ya juma la elimu yatazinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Suleman Jafo mkoani Tanga yatakayofanyika  Wilayani Handeni.

"...Tarehe 10 Mei itakuwa ni kilele cha wiki ya uhamasishaji wa Elimu. Mgeni na mgeni wa Heshima atakuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa. Kamati ya Maandalizi ya TEN/MET imeamua Kauli mbiu kwa Tanzania iwe ni: “ELimu Bora, Haki Yangu”. Alisema Mratibu huyo.
Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumzia maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) linalotarajia kufanyika katika Wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga. Kulia ni Mwenyekiti wa GAWE, James Ogondick na Ofisa Utetezi TEN/MET, Bw. David Sizya (kushoto). 
Sehemu ya waandishi wa hahabari kulia wakiwa wamesimama kwa dakika moja kabla ya kuanza mkutano wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) na wanahabari kuzungumzia shughuli za maadhimisho ya Juma la ELimu (GAWE) linalo tarajia kufanyika mkoani Tanga katika Wilaya ya Handeni. 

Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga pamoja na meza kuu wakiwa wamesimama kwa dakika moja kabla ya kuanza mkutano wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) na wanahabari kuzungumzia shughuli za maadhimisho ya Juma la ELimu (GAWE) linalo tarajia kufanyika mkoani Tanga katika Wilaya ya Handeni. 

WAANDISHI WALIA KUFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU,BILA MIKATABA,BILA MISHAHARA/IKIWEPO NI FINYU

$
0
0

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana akizungumza na waadhishi wa habari mkoani Arusha katika siku ya Maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani yanayofanyika kila mwaka 3 .Mei
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Mkoani Arusha Cloud Gwandu katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Golden Rose Hotel
Victor Maleko Meneja programu kutoka Umoja wa Vilabu vilabu vya waandishi wa habari Tanzania UTPC.amesema bado hawatanyamaza hadi tujue hatma ya waandishi wa habari,bora tuendelee kupiga kelele tu.
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa(Utawala)wa Arusha David Lyamongi akizungumza na waandishi akimuwakilisha RAC Richard Kwitega.

Baadhi ya waandishi kushoto Lilian Joel wa gazeti la uhuru na Cythia Mwilolezi kutoka gazeti la Nipashe ,wakifuatilia mambo kwa makini
Waandishi wa vyombo mbalimbali Jijini Arusha.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano ,wa kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.
Waandishi wakifuatilia mada kwa makini
Waandishi wakifuatilia kinachoende
Waandishi wakiwa katika ukumbi wa mkutano tayari kwa kuanza kongamano la maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo ya habari duniani.
Mwandishi Abraham Gwandu akifuatilia jambo kwa makini katika kongamano la siku moja la maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari Jijini Arusha,akiwa na Seif Mangwangwi
Grace Macha mwandishi wa Tanzania Daima akiwa katika kongamano la siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani Jiji Arusha.
Kutoka kushoto ni Shaban Mdoe Katibu mwenezi wilaya ya Arumeru,Katikati Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Jijini Arusha Cloud Gwandu na Afisa programu Victor Maleko kutoka UTPC.


Na.Vero Ignatus ,Arusha.

Katika kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani,waandishi wa habari mkoani arusha wamekutana kwa pamoja ili kujadili na kuangalia changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika utekelezaji wao wa ukusanyaji wa habari wa kila siku na namna yavkupata ufumbuzi.

Akizungumza mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoani hapo Claud Gwandu amesema kwa sasa kilio kikubwa cha waandishi ni kufanya kazi katika vyombo vya habari bila malipo,kukosa mikataba sambamba na kutopewa ushirikiano wakati wa utafutaji wa habari.

Gwandu amesema wanahabari wengi wanafanya kazi bila mikataba,malipo yanakuwa duni sana au hakuna kabisa, amesema, kinakosekana chama cha wafanyakazi waandishi wa habari,jambo ambalo inapelekea kutoonekana dalili za matatizo ya waandishi hayatatuliwi kwa haraka.

"Tunakosa chama cha wafanyakazi waandishi wa habari ,jambo ambalo linatupa wasiwasi kutoona wapi matatizo yetu yanashughulikuwa kwa haraka ukizingatia sisi ndiyo tunahabarisha umma,tunaelimisha,na tunaonya pia.alisema Gwandu"

Amesema waandishi wanafanya kazi katika mazingira magumu bila kuwa na mikataba,bila mishahara,ameviomba vyama vya utetezi wa haki za binadamu kuangalia upya swala hili dhidi ya wanahabari kufanya kazi bila kulipwa maana huo ni sawa na utumwa wa aina fulani.

Kwa upande wake Meneja Programu kutoka Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC) Victor Maleko amesema kuwa hawajachoka kufanya kazi ambayo zitahakikisha kila mwandishi atakuwa sawa na kupata stahiki zake.

Ni kweli waandishi wanafanya kazi katika mazingira magumu,ya vitisho,kupotea katika mazingira ya kutatanisha,kupoteza maisha , ila hatutakaa kimya tunaendelea kupiga kelele hadi tutakapojua hatma ya waandishinwa habari alisema."UTPC kuna utaratibu tunmalizia kuuweka wa kuhakikisha kila mwanahabari anapata stahiki zake kulingana na kazi zake"

Kwa upande wake mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana amewataka waandishi amewataka kuzingatia utanaduni,uzalendo,

kutumia kalamu zao vizuri,kutetea uhuru wa watu binafsi na ziwalinde wao wenyewe,na kuzilinda habari walizoziandika."Kalamu za waandishi wa habari ni silaha, zinaweza kuua, kujeruhi na kuokoa,zitumieni vizuri kwa kuilinda Amani ya nchi,uzalendo na utamaduni wa nchi yenu'' akisema Shana.

Kamanda Shana amezungumzia pia kuhusiana na haki za watoto haswa katika mkoa wa Arusha kumekuwa na wimbi la kulawitiwa na kubakwa kwa watoto ambapo kesi zake wazazi wanamalizana na wanaukoo,amesema swala hilo halitafumbiwa macho akibainika mazazi au mlezi amepewa hongo Jeshi la polisi litashughulika nae ipasavyo.

Pia amewataka waandishi kuwa mstari wa mbele kwa kutumia kalamu zao vizuri kupinga ndoa za jinsia moja ambayo ni kinyume na maadili na utamaduni wa Taifa la Tanzania kwani hata vitabu vya dini vinapinga swala hilo.

Pia amewahakikishia waandishi ulinzi na usalama wakati wa Uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na ule wa 2020. Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa(Utawala)wa,Arusha David Lyamongi ambae alimuwakilisha Katibu Tawala mkoa Richard Kwitega amesema wanatambua umuhimu na thamani ya waandishi wa habari na utendaji kazi wao.

Akijibu swali lililoulizwa na mmoja wa waandishi kuhusiana na vitisho kutoka kwa baadhi ya viongozi amesema kuwa mkoa wa Arusha hawapo katika muundo huo bali wameendelea kushirikiana na vyombo vya habari kwa hali mzuri

Amesema swala hilo la kamatakamata la waaandishi wa habari halijawekwa wazi linafanywa na uongozi wa mkoa,wilaya ,kata,amesema wataendelea kulinda haki za waandishi,amesema atapeleka taarifa hizo kwa uongozi wa mkoa kama kuna chombo chochote kile kinachoonea waandishi wa habari atoe maelekezo yake kudhibiti hali.

Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo jukumu la UTPC na klabu za waandishi wa habari kuchangia uchaguzi huru na wa haki.

Mhini kuongoza timuya kuogelea Tanzania mashindani ya vijana Budapest

$
0
0
Na Mwandishi wetu

Muogeleaji nyota nchini, Dennis Mhini ni miongoni mwa waogeleaji saba waliochaguliwa na chama cha mchezo wa kuogelea Tanzania (TSA) kuunda timu ya Taifa itakayo wania taji la michuano ya Dunia iliyopangwa kufanyika nchini, Hungary.

Mhini ambaye kwa sasa anasoma na kuogelea katika shule ya St Felix ya Uingereza, ataungana na waogeleaji wenzake, Delvin Barick wa klabu ya Mwanza na muogeleaji wa kike, Kayla Temba ambaye anatokea klabu ya DSC.

Waogeleaji wengine ni Laila Rashid kutoka klabu ya Taliss-IST, Christopher Fitzpatrick (Mwanza), Christian Shirima (DSC) na Khaleed Ladha wa Taliss-IST.

Gharama za usafiri, maradhi na mahitaji mengine kwa waogeleaji watatu, Mhini, Delvin na Kayla zitatolewa na Shirikisho la mchezo wa kuogelea duniani (Fina) wakati waogeleaji wanne, Laila, Fitzpatrick , Christian Shirima na Khaleed wanatakiwa kusafirishwa na TSA kwa kushirikiana na wadau.
Katibu Mkuu wa TSA, Inviolata Itatiro alisema kuwa Fina imewapa fursa ya kuwakilishwa na waogeleaji wengine kutokana na kuridhishwa na maendeleo ya mchezo wa kuogelea nchini.

Inviolata alisema kuwa ni vigumu kuamini hivyo kutokana na changamoto zinazoukabili mchezo, ikiwemo ukosefu wa bwawa la kuogelea la kisasa, lakini bado waogeleaji wa Tanzania wamefanikiwa kufanya vyema katika mashindano ya kimataifa.

“Tunahitaji sapoti kutoka kwa wadau, kwani Fina ipotayari kuwasafirisha waogeleaji watatu na kocha wao tu. Hawa waliobaki ni kazi ya TSA na wadau, hata hivyo TSA haina fedha kutokana na kuingia madarakani miezi kadhaa iliyopita,” alisema Inviolata.

Wazalishaji wa mazao ya nafaka nchini wahimizwa kuongeza thamani bidhaa zao

$
0
0
Na Theresa Chilambo, TanTrade.

Wazalishaji wa mazao ya nafaka nchini wahimizwa kuongeza thamani bidhaa wanazozalisha nchini na sio kuuza mazao ghafi ili soko liweze kuongezeka na kuleta faida katika sekta ya kilimo inayochangia katika ukuaji wa uchumi nchini.

Hayo yamesemwa na Richard Kasesela, Mkuu wa Wilaya wa Iringa alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa wazalishaji wa mazao ya nafaka nchini uliofanyika tarehe 3 Mei, 2019 mkoani Iringa uliondaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade). 

Akiongea na washiriki zaidi ya150  amesema sekta ya kilimo inaajiri watanzania zaidi ya asilimia 67 na kuchangia katika pato la Taifa kwa asilimia 30 na kuingiza  dola bilioni 1.2 ambazo ni chache ukilinganisha na ardhi tuliyonayo na inalisha asilimia 65 ya malighafi katika sekta ya viwanda na zaidi ya asilimia100 katika chakula.    

“Kuna bidhaa hatujaziendeleza hadi sasa na zina fursa nzuri sana kwenye masoko nje ya nchi kama vile cornflakes na zinaliwa nchi nzima na hadi sasa Watanzania hawajaamua kuwekeza kwenye viwanda vinavyozalisha bidhaa hizi” alisema Mhe Kasesela
Aliongeza kwa kusema kuwa msingi wa ustawi wa kilimo ni upatikanaji wa soko la uhakika, katika kutekeleza hilo serikali ya awamu ya tano imetengeneza mazingira rafiki kupitia uwekezaji wa viwanda kwa kutumia malighafi zake nchini.

Ameiomba TanTrade isaidie wafanyabiashara nchini katika kufundisha mikakati mbalimbali ya biashara hasa kwa kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia ili kuweza kufanya biashara kupitia simu za viganjani kupitia mifumo mbalimbali ya tehama.   

Alihitimisha kwa kutoa wito kuwa katika mkutano huo maazimio yajikite kwenye kutoa majibu ya ubora wa mbegu, namna ya uhifadhi bora wa mazao, kuondokana na kilimo cha kutegemea mvua hasa katika maeneo yanayopitiwa na mito kwa kutumia maji machache, kuboresha mifumo mizuri ya kupata takwimu sahihi, masoko na pia kufanya mkutano huu uwe endelevu kila mwaka na katika kila maazimio yanayotolewa kwenye mkutano maafisa biashara, kilimo na ushirika wa serikali lazima washiriki ili kuweza kusaidia katika kusimamia na kutekeleza maazimio ya kila mkutano.

Edwin Rutageruka, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade aliongeza kwa kusema kuwa mkutano huu utakuwa chachu kwa wazalishaji ili kuleta matokeo ya kuongeza uzalishaji, kuweza kutosheleza soko la ndani na kuangalia masoko katika nchi zinazotuzunguka katika ukanda wa Afrika Mashariki na nchi katika nchi wanachama wa jumuiya ya SADC.

Na amewasisitiza wazalishaji wa mazao ya nafaka nchini kushiriki katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ambapo kutakuwa na mikutano ya wafanyabiashara (B2B) ili kuweza kupata masoko endelevu.

Ledis Kigala, Afisa Programu kutoka Baraza la Nafaka la Afrika Mashariki aliongeza kwa kusema kuwa, Tanzania inauza mazao ya nafaka kama vile mchele, mahindi na maharage katika nchi jirani. Wakulima wameweka nguvu zaidi kwenye uzalishaji wa mahindi meupe wakati asilimia 90 ya mahindi yanayozalishwa duniani ni ya Njano.

Pia alisema kuwa kuna fursa kubwa ya masoko kwa mazao ya nafaka hasa mahindi na mtama kwaajili ya matumizi ya viwanda vya bia ingawa hadi sasa changamoto kubwa katika sekta ya mazao haya ni uwepo wa sumu kuvu na uhifadhi bora wa mazao.

Nae Karungi Gotifrid, Afisa Ubora kutoka Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko amewahimiza wakulima wa mazao ya nafaka kujiunga katika vikundi ili waweze kupewa elimu na alitoa vigezo vya mahindi yanayonunuliwa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kama ifuatavyo unyevunyevu chini ya asilimia 13, mahindi yasiyokomaa chini asilimia 1, uchafu chini ya asilimia 1, mahindi yaliyooza na yenye ugonjwa hayatakiwi kuwepo ili kuepusha sumu kuvu, mahindi yaliyoliwa na wadudu hayatakiwi kuwepo kwasababu yanaondoa kiini ambacho kinahitajika kwa bianadamu vilevile mdudu hai haitajiki ndani ya magunia ya mahindi na pia mahindi yaliyovunjika yawe chini ya asilimia 1. 

MKUCHIKA AWATEMBELEA WAJANE WA SOKOINE MONDULI

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, mama Napono Sokoine na Nakiteto Sokoine na baadhi ya wanafamilia alipowatembelea wajane hao nyumbani kwao Monduli, jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akiagana na wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, mama Napono Sokoine na Nakiteto Sokoine alipowatembelea wajane hao nyumbani kwao Monduli, jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUACHA KUSHABIKIA NDOA ZA JINSIA MOJA

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha

JESHI la polisi mkoa wa Arusha,limewataka wanahabari nchini kutokushabikia au kuunga mkono ndoa za Jinsia moja ambayo ni vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu havikubaliki na ni kinyume cha maadili .

Rai hiyo imetolewa May 3 na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana, alipokuwa akifungua kongamano la maadhimisho ya siku ya vyombo vya habari Duniani lililoandaliwa na Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha APC kwenye ukumbi wa hotel ya Golden rose ya jijini Arusha.

Amesema kuna harakati zinazoendelea Ulimwenguni za kutaka kuungwa mkono ndoa za jinsia moja ,wanahabari wasiunge mkono vitendo hivyo na badala yake waungane pamoja kupiga vita hata kama tutatengwa na Jumuia za kimataifa vitendo hivyo ni kinyume cha maadili.

Amewataka wanahabari kutambua kuwa hakuna uhuru usio kuwa na mipaka hivyo akawataka wazingatia uzalendo katika kazi zao ili kuhakikisha habari zinazoandikwa zisiwe zinachafua nchi au mkoa na Uhuru uliopo utumike kuwalinda wanahabari wenyewe na watu wengine.

Amesema lipo tatizo la watoto kubakwa na kulawitiwa mkoani Arusha na wazazi huwa wanayamaliza kienyeji kwa kupitia vikao amesema anaomba wanahabari na wananchi kuwafichua watu wa aina hiyo na jeshi la polisi limewasha moto wa kupambana na vitendo vyote vya ukatili huo..

Amewahakikishia ulinzi wa wanahabari wanaokumbana na madhira wakati wa kutekeleza majukumu yao na kuwalinda dhidi ya vitendo vyote vya uvunjifu wa amani na ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo wakati wa chaguzi za serikali za mitaa zitakazofanyika nchini kote mwaka huu.

Amewataka wanahabari kutokukubaliwa kutumiwa na watu wenye nia mbaya kuvuruga amani ya nchi na kusisitiza kuwa Arusha ni Geneva ya Afrika na anataka ibakie kuwa Geneva ya kweli kwa kutanguliza maslahi ya taifa mbele katika kutimiza majukumu yao ya kila siku .

Awali mwenyekiti wa APC,Claud Gwandu, amesema kwa siku za karibuni kumekuwepo na migogoro kati ya wanahabari na serikali na vyombo vyake hali ambayo inaondoa uhusiano uliokuwepo na badala yake kujenga chuki .

Amesema haoni sababu ya kugombana kati ya wanahabari na serikali na vyombo vyake,na matokeo yake ni wanahabari kukamatwa na vyombo vya dola na hivyo kuibua migogoro ambayo haina ulazima.

Kauli mbiu ya mwaka huu inasema Jukumu la UTPC na Klabu za waandishi wa habari kuchangia uchaguzi huru na haki .

WAZIRI WA MAMBO YA NJE ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA VIETNAM

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi amesaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Vietnam hapa nchini kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Rais wa Taifa hilo Jenerali Le Duc Anh aliyefariki April 22,2019.

Akizungumza mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi huo wa Vietnam Profesa Palamagamba John Kabudi ametoa pole kwa wananchi wa Vietnam na kuongeza kuwa Jamhuri ya Kisoshalisti ya watu wa Vietnam na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zina uhusiano wa muda mrefu na wa miaka mingi tangu enzi za Jamhuri ya watu wa Vietnam wakipigania Uhuru wao kutoka kwa Mareakani na Ufaransa.

Ameongeza kuwa Uhusiano baina ya Jamhuri ya watu wa Vietnam na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sasa umekuwa katika nyanja ya kiuchumi hususani katika eneo la mawasiliano ambapo ameitaja kampuni Halo tell kama mojawapo ya kampuni iliyowekeza katika sekta ya mawasiliano.

Ameyataja mahusiano mengine yapo katika sekta ya kilimo hususani katika kilimo cha korosho na kahawa na kwasababu hizo kama mataifa Rafiki ya muda mrefu amefika katika ubalozi huo kwa ajili ya kuhani msiba wa aliyewahi kuwa Rais wa Taifa hilo Jenerali Le Duc Anh ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 98.

Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya watu wa Vietnam hapa nchini Balozi Nguyen Kim Doanh,amshukuru Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi kwa kufika kwake kuhani msiba huo na kuongeza kuwa hali hiyo inaendelea kukuza na kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya mataifa hayo mawili.

Amemtaja Jenerali Le Duc Anh kama mmoja wa viongozi waliokuza kwa kiasi kikubwa mahusiano baina ya Tanzania na Vietnam na kwamba ana matumaini makubwa kwa siku za usoni mahusiano baina ya nchi hizi mbili yataendelea kukuzwa na kuimarishwa.

UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM) WAPEWA MAELEKEZO YA KUJIZATITI KATIKA MAPAMBANO YA KUJIKOMBOA KIUCHUMI

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeweka bayana msimamo na mwelekeo wake katika masuala ya Kilimo na Viwanda, Ulinzi na Usalama na Sayansi na Teknolojia katika muktadha wa mapambano ya kujikomboa kiuchumi na mwelekeo wa siasa za kidunia.

Akizungumza katika Mkutano Maalum wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM amesema katika mazingira ya sasa ya kidunia mapambano ya kiuchumi yamejikita katika namna ambavyo nchi masikini zinasimamia ipasavyo sekta ya kilimo, uzalishaji wa kilimo wenye tija sambamba na viwanda vitakavyochakata bidhaa za kilimo na kujenga uwezo wa kuzalisha chakula, kujitosheleza ndani na ziada.

Ndg. Bashiru Ally amefafanua unyeti wa suala la ulinzi na usalama na kwamba vijana ndio walinzi wa mwanzo na wananchi kwa ujumla, hivyo uzalendo, nidhamu, kufanya kazi, utii na kujitoa ni misingi muhimu kwa vijana wa CCM. Aidha, ameeleza jitihada zetu za kujikomboa kiuchumi hazitapokelewa vizuri na wasiotutakia mema na maadui zetu ambao wako ndani na nje ya nchi, na kwa mantiki hii vijana wa kitanzania wana jukumu ya kuilinda nchi yetu, kutetea msimamo wetu, kuyasemea mazuri yanayofanywa na Serikali yetu.

Akizungumzia kuhusu Sayansi na Teknolojia Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM ameeleza wigo wa Sayansi na Teknolojia ndio ulipo uwanja wa mapambano na ni muhimu kujihami mapema na kuwa tayari kukabiliana mashambulizi ya kimtandao, wanaotumia mitandao kupotosha kazi nzuri inayofanyika katika nchi yetu lazima wajibiwe kwa hoja na kwa ushahidi wakati wote.

Ndugu Bashiru Ally amewataka wajumbe wa Mkutano Maalum wa Baraza Kuu la UVCCM kutupatia aina ya Kiongozi (Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kutoka vijana) ambaye anaelewa mazingira tuliyomo na awe tayari kusimama imara kuulinda Muungano wetu, kujenga umoja, kulinda uhuru wetu, mtu mwenye msimamo usioyumba, atakayelinda heshima ya viongozi wetu na anayeakisi maono na mwelekeo wa Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vitendo vya ukabila, udini, ubaguzi wa rangi, vitendo vya rushwa, kila jambo linalokwenda kinyume na Katiba, Kanuni na desturi nzuri za Chama Cha Mapinduzi (CCM) havina nafasi katika Umoja wa Vijana wa CCM amesema Ndg. Bashiru Ally akihitimisha hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano Maalum wa Baraza Kuu ya UVCCM.

Mkutano Maalum wa Baraza Kuu la UVCCM unaketi kuchagua Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa anayewakilisha Umoja wa Vijana baada ya nafasi hiyo kuwa wazi, umehudhuriwa na Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi na Mzee Kombo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM pamoja na Viongozi wa UVCCM wakiongozwa na Ndg. Kheri James Mwenyekiti wa UVCCM.

Imetolewa na,

*IDARA YA ITIKADI NA UENEZI*
*CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)*

Wizara ya Mambo ya Nje kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.)  amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini, Bw. Japhet Justine (kushoto). 

Mazungumzo kati yao yalijikita katika kuangalia namna ya kushirikana ambapo Bw. Justine amemweleza Prof. Palamagamba John Kabudi kuwa, Benki ya Maendeleo ya Kilimo itaendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki hususan katika kuangalia fursa za masoko nje ya nchi kupitia Balozi za Tanzania. Masoko hayo  yatakuza biashara ya bidhaa ghafi za Tanzania nje pamoja na kuongeza thamani ya mazao yanayolimwa nchini.

Kwa upande wake,  Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi alimhakikishia ushirikiano Mkurugenzi huyo ili kuhakikisha mazao kutoka Tanzania yanapata soko nje ya nchi. Pia alimweleza kuwa, Wizara itaendelea kushirikiana na Benki hiyo katika kuweka mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji kutoka nje kwa ajili ya kuja nchini kuwekeza kwenye sekta ya kilimo kwani kuimarika kwa sekta hiyo  kutatoa fursa ya kuanzishwa kwa viwanda vya usindikaji mazao ndani ya nchi na kuzalisha ajira kwa vijana.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 03 Mei 2019
Mhe. Prof. Kabudi akisisitizia jambo wakati wa mazungumzo  na Bw. Justine.
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>