Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

TIMUN 2019 YAANZA RASMI MORO

$
0
0
MKUTANO kivuli wa Baraza la Umoja wa mataifa (TIMUN2019) umeanza Jana tarehe 29/4/2019 katika mji wa Morogoro, kiasi cha kilometa 192 kutoka mji wa kibiashara wa Dar es salaam.

Mkutano huo ambao unahudhuriwa na vijana 200 kutoka duniani kote unafanyika chini ya kaulimbiu "Sauti za Vijana kwenye Malengo ya Maendeleo Endelevu: Uwezeshwaji Ujumuishwaji na Usawa."

Afisa wa Habari katika kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC)  Bi. Nafisa Didi akizindua rasmi mwanzo wa mkutano kwa niaba ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa alihimiza vijana kutumia vizuri muda wao katika mkutano huu wa siku tano na kuonyesha vipaumbele vinne muhimu vya kujadiliwa kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu ya dunia (SDGs).

Mkutano huo mkubwa unaendeshwa kwa mfano wa mfumo wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kisheria na kikanuni. Mkutano huo unatambuliwa kimataifa kama Tanzania International Model United Nations (TIMUN) 2019 unajumuisha vijana kuanzia miaka 15-30.

Kwa mujibu wa taarifa majadiliano katika mkutano huo yatalenga zaidi ushiriki wa vijana katika kipengele cha tatu cha SDG kinachogusa Afya na ustawi; Kipengele cha nane kazi zenye staha na ukuaji wa uchumi; kipengele cha 13 mabadiliko ya tabia nchi na kipengele cha 16 cha amani, haki na kuwa taasisi zenye uwezo .

TIMUN  inaendeshwa na Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA), na hufanyika kila mwaka kwa vijana kuletwa pamoja kutoka mataifa mbalimbali duniani .

Tukio la mwaka huu limedhaminiwa na Umoja wa Mataifa Dar es salaam, ofisi ya Waziri Mkuu, UNICEF, UNFPA, UNIC, Ubalozi wa Marekani, Pathfinder, Plan International na International Youth Foundation.
Mratibu wa TIMUN 2019, Kevin Edward akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki (hawapo pichani) wakati wa mkutano kivuli wa Baraza la Umoja wa Mataifa (TIMUN2019) ulioanza kuunguruma jana mjini Morogoro.
Afisa wa Habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Nafisa Didi akifungua rasmi mkutano wa kivuli WA Baraza la Umoja wa Mataifa kwa niaba ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa ulioanza kuunguruma jana mjini Morogoro.
Baadhi ya vijana wanaoshiriki mkutano kivuli wa Baraza la Umoja wa Mataifa (TIMUN 2019) kutoka nchini mbalimbali unaoendelea kuunguruma mjini Morogoro.
Picha ya pamoja ya makundi ya vijana wanaoshiriki mkutano kivuli wa Baraza la Umoja wa Mataifa unaoendelea kuunguruma mjini Morogoro.

Vodacom Tanzania yazindua duka jipya kwa wateja wake ndani ya Aura mall jijini Dar

$
0
0
 Mkuu wa Mauzo Kanda ya Dar na Pwani, George Lugata  (kushoto) na bwana  Mirza Ngoshani (mwenye Tshirt ya blue)   wakikata utepe kuzindua duka jipya la Vodacom katika jengo la Aura mall hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa, kampuni ya Vodacom ina maduka 100 na inaendelea kupanua upatikanaji wa huduma ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma kirahisi zaidi. Wengine pichani ni watoa huduma wa duka hilo duka hilo jipya litakalotoa huduma kila siku kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa tatu usiku. 
Mkuu wa Mauzo wa Vodacom Kanda ya Dar na Pwani, George Lugata (wa pili kulia) akizungumza na wageni na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania baada ya uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo lililopo katika jengo la Aura mall jijini Dar es Salaam. Kampuni ya Vodacom ina maduka 100 na inaendelea kupanua upatikanaji wa huduma ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma kirahisi zaidi. Wengine pichani ni watoa huduma wa duka hilo duka hilo jipya litakalotoa huduma kila siku kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa tatu usiku.     

WCF YASHINDA TUZO KATIKA MASWALA YA AFYA NA USALAMA MAHALA PA KAZI JIJINI MBEYA

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi Tuzo na Cheti Bw. Masha Mshomba Mkurugenzi Mkuu wa WCF. Mfuko umekuwa Mshindi katika masuala ya afya na usalama kazini baina ya Taasisi za Bima na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Tuzo hiyo imetolewa katika Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani, 2019.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi Cheti cha ushiriki wa Siku ya Afya na Usalama Duniani Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini Dkt. Abdulssalaam Omary jijini Mbeya.
  Tuzo na Cheti katika masuala ya afya na usalama kazini baina ya Taasisi za Bima na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Tuzo hiyo imetolewa katika Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama(wa kwanza kushoto) akipata maelezo ya Mfuko kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulssalaam Omary (wa pili kulia) alipo tembelea banda hilo. Wa tatu kushoto ni Mwakilishi wa ILO Afrika  Bw. Jealous G. Chirove na Naibu  waziri  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Anthony Mavunde (katikati kulia)

Mkurugenzi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha Mshomba (katikati) akifurahia pamoja na wafanyakazi wa Mfuko baada ya Mfuko kuwa Mshindi katika masuala ya afya na usalama kazini baina ya Taasisi za Bima na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
Mkurugenzi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha Mshomba (wa pili kushoto) pamoja na wafanyakazi wengine wa WCF mara baada ya kupata Tuzo na Cheti cha ushindi wa huduma bora za Bima.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wakifurahia baada ya kupata wakifurahia pamoja na wafanyakazi wa Mfuko baada ya Mfuko kuwa Mshindi katika masuala ya afya na usalama kazini baina ya Taasisi za Bima na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu Wenye Ulemavu), Stella Ikupa (aliyeketi) akipata maelezo ya mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kutoka kwa Mkurugenzi wa huduma za Tiba na Tathmini Dkt. Abdulssalaam Omary (wa pili kulia) walipo tembelea banda hilo
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini Dkt. Abdulssalaam Omary akimpa maelekezo Dkt. Kiva Mvungi kutoka Geita Gold Mine kuhusiana na viwango vya ulemavu kwa mujibu wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi
Afisa Matekelezo Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Amina Likungwala akitoa zawadi kwa wadau mbali mbali waliotembelea banda la WCF wakati wa maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Duniani, 2019 yaliyofanyika kitaifa jijini Mbeya
Wadau mbalimbali waliotembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wakipata maelezo juu ya mafao na shughuli za Mfuko wakati wa maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Duniani, 2019 yaliyofanyika kitaifa jijini Mbeya
Afisa afya na usalama mahali pa kazi  kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Robert  Duguza akitoa maelezo juu ya huduma na mafao yatolewayo na WCF kwa mdau aliyetembelea banda la Mfuko huo
Watu mbalimbali wakiendelea kutembela katika Banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)  wakati wa maadhimisho ya siku ya usalama na afya Duniani ambapo kitaifa imefanyia mkoani Mbeya.
Afisa Mwandamizi, Afya na Usalama Mahali pa Kazi  kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Bi. Tumaini Kyando akitoa maelezo ya Mafao yanayotolewa na WCF kwa wageni na wadau waliotembelea banda la Mfuko huo
Meneja Tathmini, Vihatarishi  wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bi. Naanjela Msangi akifafanua umuhimu wa kufanya tathimini ya vihatarishi  katika maeneo ya kazi kwa wadau waliotembelea banda la Mfuko wakati wa maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Duniani, 2019 yaliyofanyika kitaifa jijini Mbeya
Afisa Mwandamizi wa Mahusiano kwa Umma kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Sebera Fulgence akimkabidhi Kava la Gurudumu  mdau aliyetembelea Banda la WCF
 Afisa Matekelezo Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Amina Likungwala akitoa zawadi kwa wadau mbali mbali waliotembelea banda la WCF
Baadhi  wa WCF wakiwa katika banda lao 
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza mbele ya Banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Duniani, 2019 yaliyofanyika kitaifa jijini Mbeya



Mhe. Schreiber asisitiza Tanzania kutosaini mkataba wa EPA

$
0
0
Mbunge na Mwenyekiti wa Kamati inayohusika na Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani Mhe. Eva-Maria Schreiber amefanya ziara ya siku saba hapa nchini. Mhe. Schreiber amepata fursa ya kutembelea mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma, ambapo pia amekutana na wenyeviti wa Kamati mbalimbali za Bunge.

Akiwa nchini Mbunge huyo ametembelea mradi wa maji ujulikanao kama “Seven Towns Urban Upgrading Programme/ Kigoma Urban Water Supply and Sanitation”. Mradi unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya na Serikali ya Ujerumani kupitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW). 

Aidha, mradi huo unahusisha mikoa ya Kigoma, Shinyanga na Lindi. Kwa upande wa Kigoma, utekelezaji wa mradi huu ulianza mwezi Machi 2013 na utakamilika mwezi Oktoba, 2019.Mhe. Schreiber amekutana na kufanya mazungumzo na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo na waandishi wa habari Mhe. Schreiber amesisitiza umuhimu wa Tanzania kutokusaini Mkataba wa Makubaliano ya Kuichumi (EPA) kati ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya na nchi za Afrika.

Pia alieleza kuwa endapo Tanzania na nchi nyingine za Afrika hazitofaidika na Mkataba huo kwakuwa zitapoteza mapato. 
Sehemu ya waandishi wakimsikiliza kwa makini Mhe. Schreiber.
Mhe. Schreiber akiendelea kuzungumza na waandishi wa Habari. 

MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MEI MOSI YAPAMBA MOTO SOKOINE MBEYA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu  Jenista Mhagama amekagua maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi na kusema ameridhishwa na hatua zilizofikiwa.

Ametoa kauli hiyo Aprili 29, 2019 baada ya kupokea taarifa ya mbalimbali za Kamati ya Maandalizi walipokutana kujadili na kupanga mipango katika kuelekea kilele cha sherehe hizo zinazotarajiwa kuadhimishwa katika Viwanja vya Sokoine Jijini Mbeya.

Waziri amesema Kamati ya Mkoa kwa kushirikiana na Ofizi yake imeendelea na maandalizi hayo na kuendelea kutoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kufika kwa wingi katika viwanja hivyo siku ya tarehe 1 Mei, 2019.

“Hadi sasa maandalzi yamefikia hatua nzuri na watu wanafanya kazi kwa umoja ili kuhakikisha shughuli hii inafana, wito wangu wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kuunga mkono wafanyakazi wa Tanzania katika siku yao hii muhimu.”Alisema waziri Mhagama.

Waziri aliwataka wanakamati hao wahakikishe wanasimamia vizuri wageni, pamoja na shughuli zote zitakazofanyika uwanjani hapo ili kuhakikisha wanaifikia siku hiyo kwa ushindi mkubwa.

Aidha Waziri aliongezea kuwa, uwepo wa maadhimisho hayo Jijini Mbeya wanachi wayatumie kama fursa ya kimaendeleo kwa kuwa mkoa utapokea wageni wengi hivyo waendelee kuwahudumia vyema.

Aidha kwa Upande wake rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya aliendelea kuhamasisha wananchi hususan wafanyakazi wote kujitokeza kwa wingi kuja kuiadhimisha siku hiyo.

 “Ni wakati sahihi kwa wafanyakazi wote nchini kuitumia siku hii maalum katika kuiadhimisha na kuienzi ikiwa ni sherehe ya upekee sana hivyo mjitokeze kwa wingi pamoja na wananchi wote kwa ujumla.”Alisisitiza Nyamhokya.

Maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi yatahadhimishwa Kitaifa katika Mkoa wa Mbeya ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, aidha maonesho hayo yatapambwa na shughuli mbalimbali ikiwemo; Maandamano ya wafanyakazi na magari, Kwaya maalum, Nyimbo maalum kutoka kwa Vyama vya Wafanyakazi, wimbo maalum kutoka kwa wasanii wa kizazi kipya, vikundi vya ngoma kutoka mikoa mbalimbali, Nyimbo maalum kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Kauli mbiu ya maonesha ya mwaka huu inasema; “Tanzania ya Uchumi wa Kati Inawezekana, Wakati wa Mishahara na Masilahi Bora kwa Wafanyakazi ni SASA”
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akizungumza jambo kwa kamati ya maaandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe ya Wafanyakazi za Mei Mosi walipokutana nao kukagua maandalizi hayo katika Viwanja vya  Sokoine Jijini Mbeya Aprili 29, 2019.
 Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya akichangiua jambo wakati wa kikao hicho.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
 Mjumbe Kamati ya Utendaji CWT Mwalimu Joyce Julius akichangia jambo katika kikao cha maandalizi ya sherehe za Mei Mosi kilichofanyika katika Viwanja vya Sokoine Jijini Mbeya aprili 29, 2019.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akiangalia mazingira ya uwanja wa Sokoine utakaotumika kwa ajili ya Maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi kitaifa Jijini Mbeya alipokutana na kamati ya maandalizi ya sherehe hizo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama pamoja na wajumbe wa kamati wakiwa katika ukaguzi wa maadalizi ya sherehe za Mei Mosi katika viwanja vya Sokoine Mkoani Mbeya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama pamoja na kamati hiyo wakiangalia mtaro unaopitisha maji katika viwanja vya Sokoine ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kufikia Kilele cha Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) Jijini Mbeya.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

MAKATIBU WAKUU TANZANIA NA UGANDA WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO

$
0
0
Katibu Tawala Mkoa wa kagera Profesa Faustin Kamuzora akizungumza wakati wa mkutano wa mahusiano kujadili changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda unaofanyika Bukoba mkoani Kagera, wa pili kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe, kushoto ni Balozi Paul Mkumbya kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda na kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Paul Makelele.
Ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa Mahusiano kujadili changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda unaofanyika Bukoba mkoani Kagera wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa siku mbili.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa mahusiano kujadili changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda unaofanyika Bukoba mkoani Kagera.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika (kulia) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Tanzania wanaoshiriki mkutano wa mahusiano kujadili changamoto zinazoikabili nchi za Tanzania na Uganda unaofanyika Bukoba mkoani Kagera. Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo Elisante Ole Gabriel na anayemfuatia ni Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe.
Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt Aziz Mlima (Kushoto) akimsikiliza Mpima Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Julius Msofe (wa pili kulia) wakati wa mkutano wa mahusiano kujadili changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda unaofanyika Bukoba mkoa wa Kagera. Kulia ni Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha.
Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt Aziz Mlima (wa tatu Kulia) akizungumza wakati wa kujadiliana na ujumbe wa Uganda katika mkutano wa mahusiano kujadili changamoto zinazozikabili nchi za Tanzania na Uganda unaofanyika Bukoba mkoani Kagera. Kulia ni Mthamni Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI).

Na Munir Shemweta, WANMM BUKOBA

Makatibu Wakuu wa Tanzania na Uganda wanakutana mjini Bukoba mkoani Kagera katika mkutano wa mahusiano kujadili changamoto zinazozikabili nchi hizo ikiwemo Uimarishaji Mpaka wa Kimataifa pamoja na Matumizi endelevu ya rasilimali za Bonde la mto Kagera..

Mkutano huo wa siku mbili umeanza tarehe 29 April 2019 mjini Bukoba na kuwakutanisha Makatibu Wakuu wa nchi hizo mbili kutoka Wizara za Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mifugo, Wizara ya Maji pamoja na Wizara ya Nishati.

Kabla ya mkutano huo, Wataalamu wa sekta shiriki kutoka Tanzania na Uganda walikutana na kujadiliana kuhusiana na changamoto zinazozikabili nchi hizo mbili kwa nia ya kuwasilisha mapendekezo yaliyofikiwa kwa Makatibu Wakuu wa nchi hizo.

Baadhi ya Changamoto zinazojadiliwa  kwenye mkutano huo, ni pamoja na Uimarishaji na Uthamini wa Mpaka wa Kimataifa wa Tanzania na Uganda, Mpango kabambe wa utunzaji mto Kagera na Matumizi endelevu ya rasilimali kati ya Tanzania na Uganda katika Bonde la Mto Kagera.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe alisema mkutano huo ni mfululizo wa mikutano kati ya nchi hizo mbili wenye lengo la kutatua changamoto zinazozikabili nchi hizo kwa nia ya kuleta maendeleo.

Alisema, pamoja na kuwepo changamoto kadhaa lakini Tanzania na Uganda zinaendelea kufurahia mahusiano mazuri yaliyopo kwa kukutana na kujadiliana masuala mbalimbali yenye lengo la kuleta manufaa kwa nchi na watu wake.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Profesa Faustin Kamuzora aliuzungumzia mkutano huo kama njia ya kuzifanya nchi husika kufanya kazi pamoja na kuzidisha ushirikiano wenye nia ya kuleta maendeleo na kusisitiza kuwa, utekelezaji wa makubaliano yatakayofikiwa unapaswa kufanywa kwa wakati.

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI TEMEKE LAZINDUA KAMPENI YA NINACHO, NAJUA KUKITUMIA

$
0
0
Kamanda wa Viwanja vya Ndege wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini (ACF) Maria Kulaya, akisalimiana na Katibu Tawala Wilaya ya Temeke Bi. Bupe Mwakibete (kulia), alipowasili katika viwanja vya Mwembe Yanga, kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Ninancho, Najua kukitumia, iliyofanyika katika viwanja hivyo Temeke Dar es salaam mapema leo asubuhi tarehe 30/04/2019
Katibu Tawala Wilaya ya Temeke Bi. Bupe Mwakibete akitoa hotuba kwa wananchi na wakazi wa Wilaya ya Temeke, kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Ninancho, Najua kukitumia iliyofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es salaam, mapema leo asubuhi.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kizimamoto Temeke (ASF) Puyo Nzalayaimisi, akihutubia wananchi na wakazi wa Wilaya ya Temeke, kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Ninancho, Najua kukitumia iliyofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es salaam mapema leo asubuhi.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya akitoa salamu kwa niamba ya Makamanda wa Mikoa na Kumkaribisha Mgenia Rasmi Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Ninancho, Najua kukitumia iliyofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es salaam mapema leo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke Bi. Bupe Mwakibete (kulia) akimsikiliza Sajini wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Lugendo Rashidi (kushoto), alipotembelea Banda la kutolea elimu, kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Ninancho, Najua kukitumia iliyofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es salaam, mapema leo. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji Makao Makuu)

MKURABITA YATOA MAFUNZO KWA WAJASILIAMALI-MTWARA

$
0
0
JOSEPH MPANGALA
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za wanyonge Tanzania MKURABITA kwa kushirikiana na Manispaa ya Mtwara Mikindani,Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA pamoja na taasisi mbalimbali za Kifedha zimetoa mafunzo kwa wajasilimali zaidi ya Elf Moja  ili kuweza kujenga uwezo katika kuweka Kumbukumbu za Biashara na kuongeza kipato.

Akiongea katika Ufunguzi wa Mafunzo hayo ya Siku mbili Mtaala wa Sheria Kutoka MKURABITA Jane Lyimo anasema Walianza kwa kufanya tathmini ili kuweza kugundua changamoto za  wafanyabiashara wa Mkoa wa Mtwara na kwa kiasi gani wamerasimishwa na kutambulika na serikali.

“Kazi kubwa iliyofanyika ni pamoja na kufanya Tathmini kwa wafanya biashara elf moja nia na madhumuni ni kutaka kujua wafanyabiashara wa manispaa wako katika hali gani,biashara zao zinaendeshwa katika mfumo gani,wako rasmi au hawako rasmi,ni Changamoto gani wanakutana nazo na baada ya kumaliza tathmini ni kuwapeleka katika mafunzo”Amesema Jane Lyimo.

Ameongeza kuwa Tathmini imeonesha kuwa Biashara nyingi Mkoani Mtwara Zinashindwa kukua kutokana na sababau mbali mbali ikiwemo kutunza kumbukumbu za Mauzo pamoja na kujiunga na mifuko ya jamii.

‘’Wafanyabiashara elf moja waliofanyiwa Tathmini ni wafanyabiashara 153 tu ndio ambao wanatunza Kumbukumbu lakini pia Wafanyabiasha Tisa kati ya elf Moja ndio wamejiunga na mifuko ya jamii idadi ambayo ni ndogo na wengi wa wafanyabiashara hawatunzi fedha zao katika Taasisi za Kifedha hii inapelekea mitaji yao kushindwa kukua kutokana na Kutokuwa na Uhusiano katika Taasisi za Kifedha”

Zaidi ya wajasiliamali 1000 wameshiriki katika Mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya Kurasimisha biashara zao pamoja Elim ya ulipaji wa Kodi. 
 Mtaalam wa Sheria Kutoka MKURABITA Jane Lyimo akiongea na waandishi wa Habari Juu ya Mafunzo ya siku Mbili kwa wajasiliamali wa Manispaa ya Mtwara Mikindani kwa lengo la kujiongezea Kipato katika Biashara zao.
Afisa Biashara Manispaa ya Mtwara Mikindani Edward Matulanya akitoa mafunzo juu ya umuhimu wa kurasimisha bishara ili kuweza kutambulika na serikali na umuhimu wa ulipaji wa kodi.

Baadhi ya wajasiliamali kutoka manispaa ya Mtwara Mikindani wakisikiliza kwa Makini Mfunzo yaliyoandaliwa na MKURABITA kwa lengo la kuwajengea uwezo juu kukuza mitaji na kutunza kumbukumbu.

MKURABITA YATOA MAFUNZO KWA WAJASILIAMALI - MTWARA

$
0
0
Mtaalam wa Sheria kutoka MKURABITA, Jane Lyimo akiongea na waandishi wa Habari Juu ya Mafunzo ya siku Mbili kwa wajasiliamali wa Manispaa ya Mtwara Mikindani kwa lengo la kujiongezea Kipato katika Biashara zao.
Baadhi ya wajasiliamali kutoka manispaa ya Mtwara Mikindani wakisikiliza kwa Makini Mfunzo yaliyoandaliwa na MKURABITA kwa lengo la kuwajengea uwezo juu kukuza mitaji na kutunza kumbukumbu.
Afisa Biashara Manispaa ya Mtwara Mikindani Edward Matulanya akitoa mafunzo juu ya umuhimu wa kurasimisha bishara ili kuweza kutambulika na serikali na umuhimu wa ulipaji wa kodi.

NA JOSEPH MPANGALA.

Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za wanyonge Tanzania MKURABITA kwa kushirikiana na Manispaa ya Mtwara Mikindani,Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA pamoja na taasisi mbalimbali za Kifedha zimetoa mafunzo kwa wajasilimali zaidi ya Elf Moja  ili kuweza kujenga uwezo katika kuweka Kumbukumbu za Biashara na kuongeza kipato.

Akiongea katika Ufunguzi wa Mafunzo hayo ya Siku mbili Mtaala wa Sheria Kutoka MKURABITA Jane Lyimo anasema Walianza kwa kufanya tathmini ili kuweza kugundua changamoto za  wafanyabiashara wa Mkoa wa Mtwara na kwa kiasi gani wamerasimishwa na kutambulika na serikali.

“Kazi kubwa iliyofanyika ni pamoja na kufanya Tathmini kwa wafanya biashara elf moja nia na madhumuni ni kutaka kujua wafanyabiashara wa manispaa wako katika hali gani,biashara zao zinaendeshwa katika mfumo gani,wako rasmi au hawako rasmi,ni Changamoto gani wanakutana nazo na baada ya kumaliza tathmini ni kuwapeleka katika mafunzo”Amesema Jane Lyimo.

Ameongeza kuwa Tathmini imeonesha kuwa Biashara nyingi Mkoani Mtwara Zinashindwa kukua kutokana na sababau mbali mbali ikiwemo kutunza kumbukumbu za Mauzo pamoja na kujiunga na mifuko ya jamii.

‘’Wafanyabiashara elf moja waliofanyiwa Tathmini ni wafanyabiashara 153 tu ndio ambao wanatunza Kumbukumbu lakini pia Wafanyabiasha Tisa kati ya elf Moja ndio wamejiunga na mifuko ya jamii idadi ambayo ni ndogo na wengi wa wafanyabiashara hawatunzi fedha zao katika Taasisi za Kifedha hii inapelekea mitaji yao kushindwa kukua kutokana na Kutokuwa na Uhusiano katika Taasisi za Kifedha”


Zaidi ya wajasiliamali 1000 wameshiriki katika Mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya Kurasimisha biashara zao pamoja Elim ya ulipaji wa Kodi.

Waziri mkuu ahitimisha kilele cha maadhimisho ya miaka (10) ya mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF)

$
0
0
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, katika kilele cha maadhimisho ya miaka (10) ya mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) , kwenye viwanja vya Nyerere Square, jijini Dodoma Aprili 30, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, Meneja wa Kanda wa TCRA, Anthonio Manyanda, wakati akikagua mabanda, kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka (10) ya mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) , yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square, jijini Dodoma Aprili 30, 2019.
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akiteta jambo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, katika kilele cha maadhimisho ya miaka (10) ya mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) , yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square, jijini Dodoma Aprili 30, 2019.

 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akihutubia, katika kilele cha maadhimisho ya miaka (10) ya mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) ,kwenye viwanja vya Nyerere Square, jijini Dodoma Aprili 30, 2019.
Wajasiriamali wadogo wadogo (Wamachinga) wakimsikiliza Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akihutubia, katika kilele cha maadhimisho ya miaka (10) ya mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) , yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square, jijini Dodoma Aprili 30, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

KAMPENI ZA UCHAGUZI WA YANGA ZAZINDULIWA RASMI LEO

$
0
0
KAMPENI za Uchaguzi Mkuu wa Yanga zimezinduliwa rasmi leo kwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa klabu hiyo Dkt. Mshindo Msolla amesema kuwa uzoefu wake katika sekta ya michezo utamsaidia kuibadilisha Yanga na kuleta mabadiliko.

Dkt. Msolla amezindua kampeni hizo katika makao makuu ya Klabu ya Yanga na kunadi sera zake mbele ya wanachama wa klabu hiyo na kueleza kuwa uzoefu wake katika sekta ya  michezo kwa muda wa miaka 40 utamsaidia kuweza kutekeleza mipango ya klabu kwa wakati na lengo kuu ni kuirudisha timu kwa Wananchi.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo, Msolla amesema kuwa amedhamiria kuleta mabadiliko ndani ya Yanga ili kutatua changamoto zilizopo kwenye taasisi hiyo ikiwemo ya uongozi ambalo lilikuwa linaathiri ufanisi wa klabu.

"Kwa kipindi kirefu kumekuwa na changamoto ya kiuongozi na matokeo yake changamoto hiyo imefanya kuwe na ombwe la uongozi, nimeamua kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa klabu kwa sababu nina uzoefu wa kutosha hasa baada ya kuwa kwenye tasnia ya mpira kwa muda wa miaka 40 katika nyanja mbalimbali,"

"Nitahakikisha ninajenga umoja ndani ya klabu kwa wanachama na wapenzi wa Yanga na kuirudisha timu kwa wananchi kwa kuimarisha matawi yaliyopo, kuanzisha matawi mapya, matawi kupelekewa katiba ili wawe na uelewa wa katiba ya klabu yao na kuendeleza mchakato wa maboresho ya mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu.

"Nitahakikisha Yanga inatengeneza Historia yake kwa kuboresha eneo la klabu na kufanya iwe sehemu ya utalii kama ulaya bila kusahau maboresho ya uwanja wa Kaunda pamoja na ukarabati wa jengo la klabu pamoja na kuweka misingi bora ya uwajibikaji," amesema Msolla na kuomba wanachama wamchague.

Yanga inatarajia kufanya uchaguzi wake Mei 5 mwaka huu na leo kampeni zimezinduliwa rasmi kwa wagombea ili kupata viongozi wapya kwa ngazi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ndani ya Yanga.

RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA KUFANYA VIBAYA KWA SERENGETI

$
0
0
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amesema kitendo cha timu za Taifa kufungwa anatamani siku moja awe Waziri wa Michezo ili apange timu mwenyewe.

Magufuli amesema huwa anaumia sana na  ameboreka kwa kitendo cha timu ya Taifa ya Vijana, Serengeti Boys kufungwa mabao mengi katika ardhi ya nyumbani.

Akizungumza leo wakati wa hotuba mbele ya wananchi wa mkoa wa Mbeya wilayani Kyela, Magufuli amesema hajafurahishwa na timu ya vijana kufungwa mabao mengi tena wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani na mashindano wakiwa wameandaa wenyewe.

"Hii ni aibu kwa Taifa, tupo milioni 55 tukifungwa tunaaibika wote haiwezekani Waziri unaangalia tu labda kufungwa ni mchezo mzuri, mashindano tumeaandaa wenyewe, uwanja wa kwetu wenyewe, tumefungwa mabao mengi kwelikweli, hili ni jambo la ajabu ungechukua hata timu ya Kyela tusingefungwa hivi, " amesema Magufuli.

"Sasa hili linapaswa liangaliwe kwa usawa, ninatamani siku moja niwe Waziri wa Michezo na nikiwa Waziri wa Michezo timu nitaipanga mwenyewe, na timu nyingine hiyo nayo inajiandaa sijui na wao watapigwa kama hawa,"

Michuano ya Afcon ambayo imemalizika wikiendi hii, Cameroon imebebwa ubingwa kwa vijana, huku Tanzania ikitolewa na zigo la mabao 12 ya kufungwa na imefunga mabao sita pekee kwenye michezo mitatu.

RC AWAKUTANISHA VIONGOZI NA WATAALAMU KATIKA KIKAO CHA MAJUMUISHO YA ZIARA DAR

$
0
0
*Awapongeza watendaji kwa kuufanya Mkoa huo kuwa kinara ukusanyaji mapato

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amefanya kikao cha majumuisho kilichowakutanisha wakuu wa Wilaya, wakurugenzi, wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala, washauri wa miradi na wakandarasi na hiyo ni kufuatia ziara iliyofanywa na RC huyo katika kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo jijini humo.

Akizungumza na watendaji hao Makonda amewapongeza watendaji kwa juhudi wanazozifanya katika kuleta maendeleo na kuwataka watimize ahadi zao kama walivyohaidi na hiyo hasa ni katika ujenzi wa vituo vya afya Buguruni na Kigogo kwa kuikamilisha kwa wakati huku akifurahishwa na kasi ya ujenzi wa hospitali za Wilaya za Ilala na Kigamboni ambazo zinajengwa kwa jumla ya shilingi bilioni 1.5 fedha ambazo zilizotolewa na Rais John Joseph Magufuli katika kuboresha sekta ya afya.

Aidha ameitaka Halmashauri ya Ubungo kuongeza kasi zaidi katika utatuzi wa kero za wananchi na kuwataka viongozi kuacha siasa na kuchapa kazi huku akielekeza nguvu zaidi iwekwe katika  shughuli za kimaendeleo.

Vilevile amewasisistiza wataalamu wa kusimamia miradi jijini humo kushirikisha wazawa katika miradi mikubwa ya kimaendeleo pindi tenda zinapotangazwa ili kuweza kuwainua na kuwapa fursa zaidi.

Wakati huo huo Makonda ametumia nafasi hiyo kuzipongeza halmashauri zote na watendaji wao kwa kuufanya Mkoa huo kuwa kinara katika ukusanyaji wa mapato kwa kipindi cha robo mwaka kwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 118.4 ikifuatiwa na Jiji la Dodoma lililokusanya  bilioni 57.3 na Jiji la Mwanza shilingi bilioni 22.9 huku Wilaya za Ilala na Kinondoni zikifanya vizuri zaidi nchini.

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ilimulika miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika Wilaya zote jijini humo na katika ufanyaji wa tathimini hiyo viongozi na wasimamizi wa miradi hiyo wametakiwa kutimiza ahadi zao kwa kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.

YATUNZE MAZINGIRA YAKO YAKUTUNZE

$
0
0
 Mfanyabiashara wa Matunda akiendelea na biashara yake huku pembeni kukiwa na mtaro wa maji machafu katika eneo  Kinondini  jijini Dar as Salaam, jambo ambalo ni hatari kwa afya ya walaji.
Wananchi wanaaswa kutunza mazingira yao na kuwa safi kuepukana na magonjwa mbalimbali yanayoweza kusababishwa na uchafu.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mfanyabiashara wa Matunda akiendelea na biashara yake huku pembeni kukiwa na mtaro wa maji machafu kama inavyo onekana pichani katika eneo  Kinondini  jijini Dar as Salaam.
Mfanyabiashara wa mahindi akiendelea na kazi katika  eneo  Kinondini  jijini Dar as Salaam. akiendelea na kazi

Mhasibu UDART afikishwa kizimbani kwa tuhuma za kughushi Tiketi

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
MHASIBU  wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART), Alphonce Kika (29), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa akikabiliwa na mashtaka 36 ya  kughushi tiketi zenye namba tofauti tofauti za mabasi ya mwendo kasi.

Mshtakiwa Kika anayeishi Mabibo, Loyola amesomewa shtaka lake leo Aprili 30, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde wa Mahakama hiyo na kusomewa mashtaka 36 ya kughushi.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Janeth Mugho akisaidiana Jenifa Masue amedai, mshtakiwa ametenda makosa hayo Aprili 4, 2019 katika Kituo cha mabasi ya mwendo kasi kilichopo Mbezi ndani ya Wilaya ya Ubungo na jijini Dar es Salaam.

Imedaiwa siku ya tukio mshtakiwa Kika  kwa nia ya kudanganya au kutapeli alighushi tiketi 36 za basi zenye namba tofauti tofauti za Aprili 18, 2019 akidanganya kuwa zimetolewa na UDART kitu ambacho si kweli.

Hata hivyo, mshtakiwa amekana mshtaka yote na amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana amhapo mahakama imemtaka kuwa na  mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh milioni 20.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 13,2019, kwa mujibu wa upande wa mashtaka  upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.
MHASIBU wa Kampuni ya Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART) ,Alphonce Kika ,akisindikizwa na polisi kuelekea katika  kizimba cha  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwa ajili ya kusomewa mashtaka 36  ya kugushi yanayomkabili .


RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA MAJENGO MAPYA YA CHUO CHA UALIMU MPUGUSO WILAYANI RUNGWE PIA AZUNGUMZA NA WANANCHI WA TUKUYU MKOANI MBEYA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na viongozi wengine kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Majengo mapya ya Chuo cha Ualimu Mpuguso Rungwe mkoani Mbeya.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kyela mkoani Mbeya.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Rungwe hawaonekani pichani wakati akielekea Chuo cha Ualimu Mpuguso kilichopo Rungwe mkoani Mbeya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Mpuguso Rungwe mkoani Mbeya mara baada ya kuweka jiwe la msingi msingi ujenzi wa Majengo mapya ya Chuo cha Ualimu Mpuguso.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiimba pamoja na wananchi waliokusanyika katika viwanja vya chuo cha Ualimu Mpuguso mara baada ya kuwasili chuoni hapo.
Wananchi wa Rungwe mkoani Mbeya wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati aliposimama kuwasalimia kabla ya kwenda Chuo cha Ualimu Mpuguso. 


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Tukuyu Wilayani Rungwe wakati akielekea Mbeya mjini. PICHA NA IKULU

WAZIRI MHAGAMA AWAASA WAFANYAKAZI KUTIMIZA WAJIBU WAO

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista mhagama amewaasa wafanyakazi nchini kufanya kazi kwa bidii na uzalendo ili kuendelea kutimiza wajibu wao na kujiletea maendeleo nchini.

Ametoa kauli hiyo mapema hii leo Aprili 29, 2019 alipokuwa akihutubia wafanyakazi walioshiriki katika semina maaalum ya wafanyakazi iliyowakutanisha wajumbe kutoka vyama mbali mbali vya wafanyakazi ili kujadili chimbuko la sherehe za wafanyakazi (Mei Mosi) na kujadili masuala ya sheria za kazi katika ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya.

Akizungumza na wajumbe wa semina hiyo, waziri Mhagama aliwaasa wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa weledi na tija ili kuendelea kuwa na taifa lenye maendeleo kwa kuzingatia mchango wa wafanyakazi nchini.

“Wafanyakazi endeleeni kufanya kazi kwa umoja, weledi huku mkizingatia kanuni, taratibu na sheria zinazowaongoza katika kutekeleza majukumu yenu pasipo kukiuka masuala ya msingi yanayowahusu,”alisema Waziri Mhagama.

Aliongezea kuwa, katika kuhakikisha Taifa linakuwa na maendeleo endelevu ni vyema wafanyakazi wakaendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa kuzingatia mchango mkubwa wa wafanyakazi nchini katika kujiletea maendeleo kwa kuzingatia tija walioyonayo nchini.

“Niwakumbushe kuwa nyie ni wadau muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu na Serikali inawategemea katika kuchangia maendeleo ya nchi hivyo mnapaswa kujali maeneo yenu ya kazi na kuendelea kuvitumia vyama vya wafanyakazi katika kueleza masuala yenu na kutumia vyama vyenu kutatua changamoto zinazowakabili,”alisisitiza Waziri Mhagama



Sambamba na hilo Waziri aliwataka wafanyazkai kuendelea kuzingatia uwajibikaji wenye misingi ya haki na usawa ili kuwa na mazingira salama ya kiutendaji pasipo kuvunja sheria za wafanyakazi ili kuwa na matokeo chanya kama inavyotarajiwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TUICO Taifa Bw. Paulo Sangeze alieleza shukrani zake kwa namna serikali inavyoendelea kuunga mkono uwepo wa Vyama vya wafanyakazi na kuahidi kutoa ushiorikiano kila itakapohitajika.

“Kwa dhati ya moyo wangu na kwa niaba ya TUCTA ninatoa shukrani kwa Serikali kwa namna inavyounga mkono shughuli za vyama vya wafanyakazi na hakika kumekuwa na mabadiliko makbwa tofauti na ilivyokuwa awali,”alisisitiza bw. Sangeze
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiimba wimbo wa umoja na mshikamano pamoja na baadhi ya viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi walipokutana wakati wa Semina kwa wafanyakazi kuhusu masuala ya Sheria za wafanyakazi na chimbuko la Siku ya Wafanyakazi Duniani iliyoandaliwa na TUICO Taifa na kufanyika Aprili 29, 2019 ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya.

 Sehemu ya wajumbe walioshiriki semina hiyo wakiimba wimbo wa umoja na mshikamano.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akihutubia wakati wa semina ya kueleza masuala ya Sherehe za Mei Mosi pamoja na Sheria za wafanyakazi iliyoandaliwa na TUICO Taifa Jijini Mbeya.
 Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya akichangiua jambo wakati wa semina hiyo.
 Sehemu ya wajumbe wa semina hiyo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa semina hiyo.
 Mwenyekiti wa TUICO Taifa Bw. Paulo Sangeze akitoa neno la shukran kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa semina.
 Mwenyekiti Kamati ya Wanawake Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Bi. Rehema Ludanga akichangia jambo wakati wa semina hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa semina hiyo mara baada ya kutoa hotuba yake Jijini Mbeya, kushoto kwake ni Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya na kulia kwake ni Mwenyekiti wa TUICO Taifa Bw. Paulo Sangeze.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

HOTUBA YA WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA, AWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA 2019/20

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako. 

WAZIRI MHAGAMA AWAONYA WAAJIRI WOTE KUTONYANYASA WANAWAKE

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista mhagama amewataka waajiri wote nchini kutonyanyasa wanawake katika masuala ya kazi ili kuwa na usawa maeneo ya kazi.

Ameitoa kauli hiyo tarehe 30 Aprili, 2019 alipokuwa akifungua semina ya siku moja ya viongozi wanawake kutoka vyama mbalimbali vya wafanyakazi nchini walipokutana kujadili masuala yanayowahusu wawapo kazini ikiwemo; haki na wajibu wao wawapo kazini iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Paradise Inn Jijini Mbeya.

Waziri alieleza kuwa waajiri hawana budi kubadili mitazamo hasi iliyopo katika jamii ya kuona wanawake ni viumbe dhaifu na wenye majukumu mengi yanayoweza kukwamishi jitihada zao wawapo kazini badala yake wawaone kuwa ni viungo muhimu katika kuchangia uzalishaji na maendeleo nchini.

“Mchango wa wanawake ni mkubwa endapo utatambuliwa na kuthamini katika nyanja zote za ukuaji wa uchumi, hivyo ni vyema maeneo ya kazi waajiri watimize wajibu wao kwa kundi hili kwa kuzinigatia sheria zilizopo na wasinyanyaswe na waendelee kuheshimiwa na kupewa haki na stahiki zao kama wafanyakazi wengine.”alisisitiza Waziri Mhagama.

Waziri alieleza jitihada za serikali ni kuhakikisha inasimamia vyema sheria na taratibu za kazi nchini kwa kuliangalia kundi hili ili kuwa na waajiriwa wenye kuzingatia usawa wa kijinsia.

“Ninakemea vitendo vya unyanyasaji wa haki za wanawake kazini ikiwemo kukoseshwa haki zao na vyama hivi vya wafanyakazi viendelee kuleta tija katika kukemea matendo hayo,”alisistiza Waziri Mhagama.

Aidha Waziri aliwataka wanawake kuendelea kuvitumia vyama vya wafanyakazi kama jukwaa maalum la kueleza na kutatua changamoto zao.

Aliongezea kuwa, pamoja na changamoto wanazokutana nazo wanawake hawana budi kujiendeleza kielimu ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yaliyopo katika masuala ya kazi.

“Wanawake umefika wakati kuendelea kujiendeleza katika eneo la elimu ili kuwa na vigezo mahususi vitakavyo wapa nafasi nzuri katika maeneo yenu ya kazi.”alisisema Waziri Mhagma.

Naye rais wa Shirikizo la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya alimpongeza waziri pamoja na changamoto zilizopo katika kufikia haki sawa kwa wote , alieelza umuhimu wa kuendelea kuliinua kundi hili ili kuwasaidia wanawake wa Kitanzania katika kupata haki na usawa kwenye maeneo yao ya kazi.

“Wanawake wana uwezo mkubwa hivyo tuendelee kujali na kutunza nafasi zao wawapo kazini ili kuwezesha Taifa kuendelea kuwa na maendeleleo,” alisisitiza Nyamhokya.

Kwa upande wake Mwenyekiti Kamati ya Wanawake Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Bi. Rehema Ludanga alieleza kuwa, ni wakati sahihi kuendelea kuchangamkia fursa za maendeleo ikiwemo uanzishwaji wa viwanda vya wanawake vitakavyosaidia kuondokana na hali ya utegemezi na kuchangia katika ongezeko la uzalishaji nchini.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista mhagama akihutubia washiriki waliohudhuria semina ya wanawakekutoka katika vyama mbalimbali vya wafanyakazi iliyoandaliwa lengo la kujadili maeneo yanayowahusu wawapo kazini na mazingira ya uongozi kwa ujumla.Semina imefanyika hii leo tarehe 30 Aprili, 2019 Ukumbi wa Paradise Jijini Mbeya.
 Washiriki wa semina hiyo wakifuatilia hotuba mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista mhagama (hayupo pichani) wakati wa semina hiyo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista mhagama pamoja na baadhi ya viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi wakipokea dua maalumu ya kufungua semina hiyo Jijini Mbeya.
 Rais wa Shirikizo la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya akisalimia washiriki wa semina hiyo.
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Dkt. Yahya Msingwa akieleza jambo wakati wa semina hiyo.
 Mwenyekiti Kamati ya Wanawake Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bi. Rehema Ludanga akichangia jambo wakati wa semina hiyo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista mhagama (katikati) pamoja na viongozi wa Vyama vya wafanyakazi nchini, wakifuatilia hoja wakati wa semina maalum kwa wanawake kutoka katika vyama mbalimbali vya wafanyakazi nchini iliyofanyika Aprili 30, 2019 Jijini Mbeya.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista mhagama pamoja na baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiimba wimbo wa umoja na mshikamano wakati wa semina hiyo.
 Washiriki wa semina hiyo wakiimba wimbo wa kumshukuru mgeni rasmi kwa kujumuika nao katika semina hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista mhagama (katikati walio kaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa semina hiyo mara baada ya ufunguzi rasmi Aprili 30, 2019 Mkoani Mbeya.

RAIS DKT MAGUFULI AHUTUBIA TAIFA KWENYE SHEREHE ZA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI (MEI MOSI) JIJINI MBEYA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe Jenista Mhagama na viongozi wa Wafanyakazi wakishuhudia maandamano ya wafanyakazi wakati wa sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani maarufu kama Mei Mosi katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo Jumatano Mei 1. 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe Jenista Mhagama na viongozi wa Wafanyakazi wakishikana mikono na kuimba wimbo wa MSHIKAMANO (Solidarity Forever) wakati wa sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani maarufu kama Mei Mosi katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo Jumatano Mei 1. 2019

 Muonekano wa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia Taifa wakati wa sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani maarufu kama Mei Mosi leo Jumatano Mei 1. 2019
 PICHA NA IKULU
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images