Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

UFAFANUZI WA TAARIFA INAYOSAMBAZWA NA WAFANYABIASHARA KATIKA UHAKIKI WA BIDHAA ZILIZOFUNGASHWA

$
0
0
Kumekuwepo na taarifa ambayo imesambazwa katika mitandao ya kijamii kutoka kwa mfanyabiashara mmoja katika Mkoa wa Morogoro akilalamika kuitwa katika ofisi za Wakala wa Vipimo kwa ajili ya kulipa faini kwa kosa alilolitenda la kuuza bidhaa zake pasipo kutumia mizani.

Napenda kuufahamisha umma kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo Sura 340 Wakala wa Vipimo ina wajibu wa kukagua bidhaa zilizofungashwa Viwandani na katika maduka ya jumla ili kuhakiki usahihi wa vipimo kabla bidhaa hizo hazijamfikia mlaji wa Mwisho.

Kumekuwa na udanganyifu ambao unafanywa na wafanyabiashara wachache wasio waaminifu kwa kupunguza uzito wa bidhaa zilizofungashwa au kufungasha bidhaa pungufu kwenye viroba hususani unga wa mahindi ili kuwapunja wateja wanaoenda kununua bidhaa katika maduka yao.

Katika ukaguzi uliofanyika Mkoani Morogoro tarehe 29 Aprili, 2019 wafanyabiashara 29 wa maduka ya jumla walikaguliwa. Baadhi ya
waliokaguliwa walikutwa na kosa la kuuza bidhaa hususani unga wa mahindi ukiwa na uzito pungufu. Wafanyabiashara walijaziwa fomu maalumu za wito kuwataka wafike ofisi ya Wakala wa Vipimo Morogoro kwa ajili ya hatua zaidi. Zoezi hili lilikuwa maalumu kukidhi malalamiko yaliyoletwa Wakala wa Vipimo na baadhi ya Wananchi wakilalamika kuwa bidhaa nyingi hususani unga wa mahindi haufikii vipimo ambavyo vinaonyeshwa katika vifungashio vya unga huo.

Kama utaratibu wa Wakala wa Vipimo ulivyo wafanyabiashara hao walijaziwa fomu za wito ili wafike ofisini kwa ajili ya kupewa elimu na ushauri ikibidi kutozwa faini au kufikishwa mahakamani. Kwa mfanyabiashara wa jumla kuwa na mizani katika eneo lake la biashara kunamhakikishia kupokea na kuuza bidhaa iliyotimia kulingana na kiasi kilichoandikwa katika mfuko au kifungashio.

Wakala wa Vipimo inatoa wito kwa wafanyabiashara wote kufanya biashara zao pasipo kukiuka taratibu na Sheria ambazo zimewekwa na itaendelea kufanya kaguzi mbalimbali kwa lengo la kuwalinda wananchi ili waweze kununua bidhaa kwa usahihi kulingana na thamani ya fedha wanazotoa.

Imetolewa na;
Afisa Mtendaji Mkuu
WAKALA WA VIPIMO

 Mkurugenzi  wa Huduma za Ufundi Stella Khawa(katikati) akitoa ufafanuzi kwa vyombo vya habari juu ya umuhimu wa kuhakiki bidhaa zilizofungashwa kwa kutumia mizani iliyohakikiwa na Wakala wa Vipimo
Maafisa wa Wakala wa Vipimo wakieleza umuhimu wa kuhakiki bidhaa zilizofungashwa kwa kutumia vipimo sahihi (Mizani).

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MWONGOZO WA UBANDIKAJI STEMPU ZA KODI ZA KIELEKTRONIKI KATIKA BIDHAA ZENYE STEMPU ZA ZAMANI NA ZISIZO NA STEMPU

Tume ya Utumishi wa Walimu yaadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani

$
0
0
 Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) wakiwa wamebeba bango wakati wa Maandandano ya kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi yaliyofanyika Mei 1, 2019 jijini Dodoma.
  Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) wakiwa wamebeba bango wakati wa Maandandano ya kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi yaliyofanyika Mei 1, 2019 jijini Dodoma.
 Wafanyakazi wa TSC wakiwa katika maandamano kuelekea uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
 Wafanyakazi wa TSC wakiwa ndani ya uwanja wa Jamhuri wakati wa maandamano ya kuadhimisha siku ya Wafanyakazi yaliyofanyika Mei 1, 2019 jijini Dodoma.
Wafanyakazi wa TSC wakipita mbele ya mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) yaliyofanyika Mei 1, 2019 katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.

MATUKIO MBALIMBALI YA MKUU WA WILAYA YA TUNDURU WILAYANI HUMO

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera aliyevaa suti akiangalia moja  ya mashine ya kufyatulia tofali alipotembelea chuo cha Ufundi kinachomilikiwa na taasisi ya Kiuma,kulia mwalimu wa Useremala wa chuo hicho Patrick Komba,
 Mwenyekiti wa  Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kiuma Dkt Matomora Matomora kushoto akimueleza jambo jana Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera juu ya vijana wa Tunduru kushindwa kujitokeza kujiunga na chuo cha Ufundi jambo lililochangia vijana wengi  wilayani Tunduru kuwa maskini.
 Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera kushoto akipokea Bendera ya Chama cha Wananchi cuf kutoka kwa aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji cha Fundimbanga kupitia chama hicho ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi,hata hivyo katika mkutano huo Mkuu wa wilaya alilazimika kutimua mbio baada ya kutokea kwa Nyoka watatu kutoka juu ya Mti  hivyo kusababisha taharuki kubwa kwa Wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Picha na Muhidin Amri

Wafanyakazi wa JKCI waadhimisha siku ya wafanyakazi duniani

$
0
0
 Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiandamana kuingia katika Uwanja wa Uhuru wakati wa maandamano ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani iliyoadhimisha kitaifa mkoani Mbeya na kusherehekewa na wafanyakazi wa mkoa wa Dar es Salaam katika Uwanja Uhuru leo Jijini Dar es Salaam
 Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiandamana kuingia katika Uwanja wa Uhuru wakati wa maandamano ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani iliyoadhimisha kitaifa mkoani Mbeya na kusherehekewa na wafanyakazi wa mkoa wa Dar es Salaam katika Uwanja Uhuru leo Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika picha ya pamoja baada ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani iliyofanyika kitaifa mkoani Mbeya na kusherehekewa na wafanyakazi wa mkoa wa Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru leo Jijini Dar es Salaam

Picha na: Genofeva Matemu - JKCI

RAIS DKT SHEIN AJUMUIKA NA WANANCHI KATIKA MAZIKO YA KATIBU MKUU WIZARA YA BIASHARA ZANZIBAR JUMA ALI JUMA

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiifariji Familia ya Marehemu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Ndg. Juma Ali Juma Wajane wa Marehemu alipofika nyumbani kweke Kijichi  Wilaya ya Magharibi A Unguja kutowa mkono wa pole  leo asubuhi.(Picha na Ikulu) 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akishiriki katika kuusalia Mwili wa Marehemu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Ndg, Juma Ali Juma, ikisaliwa katika Masjid ya Kijichi (Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiitikia dua baada ya kumaliza Sala ya Maiti ilioongozwa na Sheikh Said Seif Salam, iliofanyika katika Masjid ya Kijichi Wilaya ya Magharibi A Unguja.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Wananchi katika mazishi ya Marehemu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Ndg, Juma Ali Juma, yaliofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar leo, (Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Juma Ali Juma yaliofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar leo.(Picha Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Wananchi akiitikia dua ikisomwa na Sheikh Dkt. Muhiddin Ahmad Khamis, baada ya kumalizika mazishi ya Marehemu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Ndg. Juma Ali Juma.(Picha na Ikulu)


NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Ndg. Ali Khamis, akisoma wasifu wa Marehemu wakati wa mazishi yaliofanyika katika makaburi ya mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi B Unguja leo,(Picha na Ikulu)

RAIS MAGUFULI:WAFANYAKAZI NYONGEZA MSHARA SUBIRINI KWANZA, BADO SIJAONDOKA MADARAKANI

$
0
0
*Asema ahadi yake anaikumbuka na iko pale pale...ila kwa sasa ni miradi ya maendeleo

*Awaambia kupanga ni kuchagua na bora akawa mkweli

*Asisitiza Serikali inawajali wafanyakazi na inatambua mchango wao


Na Said Mwishehe, Michuzi TV
RAIS Dk.John Magufuli amesema ahadi yake ya kupandisha mishahara kwa watumishi wa umma kabla hajaondoka madarakani anaikumbuka na iko pale pale lakini amewaambia kwa sasa bado yupo madarakani, hivyo wavute subira.

Amefafanua kupanga ni kuchagua, hivyo badala ya kuongeza mishahara ya wafanyakazi wa umma , Serikali imeamua kujenga nchini kupitia miradi mikubwa mbalimbali ya maendeleo kwa kutumia fedha za ndani na kwake la kujenga nchi ni muhimu kwani faida yake itaonekana kwa kizazi cha sasa na kizazi kijacho.

Rais Magufuli amesema hayo leo Mei 1,2019 mkoani Mbeya wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafayakazi Duniani (Mei Mosi) ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza jitihada zinafanywa na Serikali kuhakikisha wafanyakazi wa kada zote wananuifa na miradi ya maendeleo.

"Kauli mbiu ya Siku ya Wafanyakazi ya mwaka huu inasema hivi Tanzania ya uchumi wa kati inawezekana, wakati wa mishahara na maslahi bora kwa wafanyakazi ni sasa.Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) amenikumbusha ahadi yangu ambayo niliitoa kwenye maadhimisho kama haya mwaka jana kuhusu nyongeza ya mshahara.

"Nilitoa ahadi kwamba kabla ya kuondoka madarakani nitaongeza mshahara lakini ni vema wakaelewa bado sijaondoka madarakani,"amesema Rais Magufuli.

Amefafanua kwa namna ambavyo miradi ya maendeleo inafanyika nchini na maelezo ambayo ameyatoa ni kwamba nchi inakwenda vizuri kiuchumi na hivyo wafanyakazi wote wanapaswa kuvuta subira kwani subira huvuta heri.

"Mambo yanayofanyika katika Taifa letu ni makubwa. Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia kuna nchi ziliamua wafanyakazi wasilipwe fedha ili kujenga nchi yao. Kwa Tanzania tumeamua kuanzisha miradi kwa ajili ya maendeleo yetu.

"Wafanyakazi mimi ni mtumishi wenu, Serikali inawapenda na kuwajali.Pia huwa ninasikiliza ya wafanyakazi, wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, wavuvi na makundi mengine, hili ni Taifa letu na lazima tulijenge kwani hakuna wa kutusaidia kulijenga. Hatua ambazo tunachukua ni kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.

"Nawapenda watanzania wote na mimi nimekuwa mwalimu, mke wangu ni mwalimu, hivyo tunafafahamu changamoto za wafanyakazi. Waziri Mkuu Majaliwa naye ni mwalim na mkewe ni mwalimu,Waaziri Mhagama naye ni mwalimu, hivyo tunatambua shida zenu.

"Naomba wafanyakazi muamini kuwa Serikali inawapenda wafanyakazi wote na ndio maana .tuliamua kuchukua jukumu la kubeba kikokotoo cha zamani ambacho ni kigumu na hata nchi za ulaya hawana hicho,"amesema Rais Magufuli.

Ameongeza badala ya kuongeza posho na mishahara kwa wafanyakazi ni vema kwanza fedha ndogo ambayo inapatikana ikatumika kufanya maendeleo na mbali ya miradi ya maendeleo Serikali imeendelea kulipa madeni ya aina mbalimbali ambayo yamegharibi mabilioni ya fedha. Pia Serikali imeendelea kuajiri watumishi wapya wa kada mbalimbali pamoja na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii.

"Serikali imekuwa ikilipa madeni, na hadi jana takwimu zinaonesha kuna ajira mpya zikiwemo za walimu 19,000 wapya , madaktari na watumishi wengine wa sekta ya afya wapya 11,000 wameajiriwa. Na hapo bado hujaweka sekta nyingine.

"Ndugu zangu wafanyakazi kupanga ni kuchagua, tungeweza kuamua tusiajiri ili fedha hizi tuongezeane posho.Nataka kusema ahadi yangu iko palepale, muda wangu haujaisha na kwa maono yangu uchumi bado unakuwa kwa asilimia saba na Tanzania ni miongoni mwa nchi tano barani Afrika ambayo uchumi wake unakuwa kwa kiwango cha hali ya juu,"amesema Rais Magufuli.

Ameongeza kwa uchapakazi unaoendelea kufanyika nchini kupitia watanzania wa makundi mbalimbali anaamini kuna mambo mazuri yanakuja mbeleni na ameona ni bora awe mkweli badala ya kudanganya tu ataongeza mshahara halafu usiwepo.

Wakati huo huo Rais Magufuli ametumia nafasi hiyo kuelezea kuwa ni kweli ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka Sh.bilioni 850 kwa mwezi hadi kufikia Sh.trilioni 1.3.Pia mapato ambayo sio ya kodi nayo yameongezeka na  hasa baada ya mashirika na kampuni kutoa gawio kwa serikali na mwaka jana wamepata gawio la zaidi ya Sh.bilioni 700 na hayo ni mafanikio makubwa.

"Pamoja na ukusanyaji wa mapato kuongeza kuna changamoto  ambazo zipo ikiwemo ya fedha nyingi kutumika kwa ajili ya kulipa mshahara kwani kwa kila mwezi Serikali inalipa Sh. bilioni 580.

"Bahati nzuri siku hizi mishahara inalipwa kwa wakati.Tukishalipa mshahara kiasi ambacho knabaki tunatakiwa kulipa madeni na nyingine kutumika kufanya maendeleo na hivyo kiasi kidogo ambacho kinabaki ndio tunajiuliza kiende wapi.

"Jinsi tunavyojiuliza, ndivyo ambavyo hata wakulima nao wanajiuliza kuhusu mbegu yake ya mavuno ale kwasababu ya njaa au atunze kwa ajili ya mbegu.Ndivyo ambavyo wafanyabiashara nao wanavyojiuliza nini wafanye kuhusu mtaji wao.

"Serikali tumeona ni busara kiasi kidogo ambacho kinabaki kikatumika katika miradi ya maendeleo ili iwe kichocheo.Kwa kutumia utaratibu huo ndio maana ujenzi wa reli ya kisasa unaendelea kwa kutumia fedha za ndani ambazo zimetolewana Watanzania wote,"amesema Rais Magufuli.

Pia amesema kuna ujenzi wa barabara katika meneo mbalimbali nchini, na kwamba kwa taarifa ya jana tu Benki ya Maendeleo Afrika imeidhinisha mkopo wa ujenzi wa barabara wa kilometa 110 ambazo ni nyingi.

Rais Magufuli amesema wameamua kukarabati na kujenga meli mpya katika maziwa mbalimbali,kuna upanuzi wa  bandari ya Dar es Salaam,Tanga na Mtwara. "Tumenunua ndege mpya nane, upanuzi wa viwanja vya ndege 11".

Ameongeza kuna ujenzi wa umeme wa maji katika maporomoko ya mto Rufiji ambako zitapatikana megwati 2100, pia kuna mradi wa umeme Kinyerezi na lengo ni kuwa na megawati 5000."Kero kubwa ni bei kubwa ya umeme na lengo la Serikali ni kuwa na umeme wa kutosha na kisha kupunguza bei.

"Mbali ya miradi ya maendeleo pia Serikali imendeelea kuboresha huduma muhimu kwa ajili ya wananchi ambapo .Katika sekta ya afya tunaendelea na ujenzi wa vituo vya afya 64 nchini ambavyo vinatumia fedha nyingi,tunanunua dawa na vifaa tiba  ambapo bajeti yake ni kubwa.

"Kwa upande wa maji nako kuna miradi mingi inaendelea na zaidi ya Sh.trilioni moja zinatumika kufanikisha miradi hiyo katika miji 21 nchini.Hatua mbalimbali Serikali inafanya ili kuhakikisha nchi inapiga hatua kimaendeleo,"amesema Rais Magufuli.

RAIS DKT.SHEIN AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI ZANZIBAR

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa meza Kuu kushoto Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto, Mhe. Maudline Castico, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Mkuu wa Mkoa wa Kusinu Unguja Mhe. Hassan Khatib na kulia Mwenyekiti wa Shirikisho la la Vyama Vya Wafanyakazi Ndh. Ali Mwalim Katibu Mkuu wa ZATUC Ndg. Khamis Mwinyi na Mwakilishi wa ILO Getrude Sima wakiimba wimbo wa mshikamano wa Wafanyakazi.wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani iliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein.Tunguu.(Picha Ikulu) 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Shein akihutubia Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duni ukumbi wa Chuo Kikuu cha SUZA Tunguu Zanzibar(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wanaofanyika Kazi zao Zanzibar wakihudhuria Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani(Picha na Ikulu)

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI CHUO KIKUU CHA MZUMBE MKOANI MBEYA

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi jengo la Taaluma na Utawala la chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Mbeya.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kukagua majengo ya Chuo Kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya mara baada ya kuweka jiwe la msingi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo ya ujenzi wa majengo ya Utawala na Taaluma katika chuo Kikuu cha Mzumbe tawi la mkoani Mbeya.PICHA NA IKULU

IKULU MABINGWA WA NETBALL KOMBE LA MEI MOSI KWA MARA YA TATU MFULULIZO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Netball Nahodha wa timu ya Ofisi ya Rais Ikulu Sophia Komba wakati wa Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Leo Jumatano Mei 1, 2019. Timu hiyo imetwaa kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo PICHA NA IKULU

KARIBU UJIUNGE NA MAFUNZO YA GOJU RYU JUNDOKAN KARATE-DO JIJINI DAR ES SALAAM

UJENZI HOLELA CHANZO MAFURIKO ARUMERU

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha

Ujenzi holela uliojegwa na baadhi ya wananchi  wilaya ya Arumeru imeelezwa kuwa ndio chanzo kikubwa cha mafuriko  yaliotokana na maji kutwaama sehemu moja .

Hayo yamebainishwa na Mkuu Wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro  wakati  
akizungumza na Wananchi Wa Wilaya hiyo waliokumbwa na mafuriko hayo alipofanya 
ziara ya kuwatembelea na kuwapa pole wananchi waliokubwa na mafuriko  
ambayo yamepelekea kuharibiwa kwa baadhi ya Mali zao.

Alisema kuwa ujenzi holela uliojengwa na baadhi ya wananchi ndio 
umesababisha mafuriko hayo ,kwani wananchi baadhi ya wananchi wamejenga  
nyumba katika njia asili zakupitishia maji  .

Aidha aliwataka wananchi wote waliojenga mabondeni  na kuzuia njia asili za  
maji kubomoa Mara moja ili kuepusha mazara makubwa  ambayo yanaweza kutokea  
hapo baadae kama vifo.

 "Mimi nathani hii Mara ya pili hili tatizo kutokea na mwaka Jana lilitokea tena  
mmekaa tumekubaliana  kuvunja kuta zote ambazo zinazuhia maji kupita kwenye  
mkondo wake hivyo basi najua kunawatu wataathirika lakini inabidi ili  
tuweze kutatua tatizo kubwa linaloweza kutokea apo baadae" alisema Muro 

Aliwataka wananchi kufuata sheria za ujenzii  wa miipango miji nakuacha kujenga kiholela holela ilikuondokana na adha inayoweza kuutokea.   

Kwa upande mmoja ya moja ya mwananchi alieathirika Rose Nassari aliishukuru serikali kwa kuwatembelea na kuwapo pole  pamoja na kuwapa elimu ya hasara ya kujenga kwenye mikondo  ya maji.

Mafuriko hayo yamekumba katika baadhi ya kaya za vijiji vya nduruma pamoja na shangarai. picha ikionyesha mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro  akiongea na wananchi wa wilaya  hiyo wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea wananchi wake waliokubwa na tatizo mafuriko  ,ambapo alisema ujenzi hoela  ndio chanzo cha mafuriko hayo na kuwataka wananchi waachie njia za asili za maji  ili yaweze kupita
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza na Wananchi wa wilaya hiyo wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea wananchi wake waliokubwa na tatizo mafuriko ,ambapo alisema ujenzi hoela ndio chanzo cha mafuriko hayo na kuwataka wananchi waachie njia za asili za maji ili yaweze kupita

Picha ikionesha mwananchi mmoja wa kijiji cha Shangarahi akiwa
amebebwa mgongoni tayari kwa kuvushwa daraja mara baada ya daraja hilo kusombwa na maji.

Schreiber asisitiza Tanzania kutosaini mkataba wa EPA

$
0
0
Mbunge na Mwenyekiti wa Kamati inayohusika na Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani Mhe. Eva-Maria Schreiber amefanya ziara ya siku saba hapa nchini. Mhe. Schreiber amepata fursa ya kutembelea mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma, ambapo pia amekutana na wenyeviti wa Kamati mbalimbali za Bunge.

Akiwa nchini Mbunge huyo ametembelea mradi wa maji ujulikanao kama “Seven Towns Urban Upgrading Programme/ Kigoma Urban Water Supply and Sanitation”. Mradi unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya na Serikali ya Ujerumani kupitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW). 

Aidha, mradi huo unahusisha mikoa ya Kigoma, Shinyanga na Lindi. Kwa upande wa Kigoma, utekelezaji wa mradi huu ulianza mwezi Machi 2013 na utakamilika mwezi Oktoba, 2019.Mhe. Schreiber amekutana na kufanya mazungumzo na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo na waandishi wa habari Mhe. Schreiber amesisitiza umuhimu wa Tanzania kutokusaini Mkataba wa Makubaliano ya Kuichumi (EPA) kati ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya na nchi za Afrika.

Pia alieleza kuwa endapo Tanzania na nchi nyingine za Afrika hazitofaidika na Mkataba huo kwakuwa zitapoteza mapato. 
Sehemu ya waandishi wakimsikiliza kwa makini Mhe. Schreiber 
Mhe. Schreiber akiendelea kuzungumza na waandishi wa Habari. 

Prof. Kabudi ashiriki maadhimisho ya siku ya Taifa la Uholanzi

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akihutubia kwenye kuadhimisha siku ya Taifa la Uholanzi, kulia ni Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jeroen Verheul. 

Prof. Palamagamba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alitumia fursa hiyo kuelezea mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Uholanzi katika sekta mbalimbali zikiwemo Kilimo, Elimu, Biashara na Ujenzi wa Miundombinu. Pia alilipongeza taifa hilo kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania kwenye kuleta maendeleo nchini.

Aidha, Prof. Kabudi alieleza kuwa Tanzania inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuwavutia wawekezaji wa Uholanzi kuja kuwekeza nchini kwa wingi, ambapo alieleza kuwa mpaka sasa Uholanzi ni miongoni mwa nchi 10 zinazoongza kwa uwekezaji nchni, ambapo imewekeza jumla ya miradi 159 Tanzania.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Mabalozi mbalimbali wanao ziwakilisha nchi zao hapa pamoja na wawakilishi wa mashirika ya Kimataifa. 
Prof. Palamagamba John Kabudi akiendelea kuhutubia kwenye maadhimisho hayo. 
Sehemu ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchni zao hapa pamoja na wageni mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) alipokuwa akihutubia. 
Juu na chini ni sehemu nyingine ya wageni waalikwa aliohudhuria maadhimisho hayo wakisikiliza hotuba hiyo ya Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Hayupo pichani). 
Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.) akigonganisha glasi na Mhe. Balozi Jeroen Verheul kwa kuwatakia viongozi wa Tanzania na Uholanzi Nguvu na Afya Njema. 
Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.) akigonganisha glasi na Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal. 
Prof. Palamagamba John Kabudi akizungumza na Mabalozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo. 
Sehemu Nyingine ya wageni waalikwa wakisalimiana na kubadilishana mawazo wakati wa maadhimisho hayo yakiendelea. 
Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo. 

Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje washiriki maadhimisho ya Mei Mosi kwa kishindo jijini Dodoma

$
0
0
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (katikati) na viongozi wengine akiwemo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula (kushoto) wakiwa wamesimama kuwasalimu Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) walipopita mbele ya jukwaa kuu wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma tarehe 1 Mei 2019. Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka 2019 ni "Tanzania ya uchumi wa Kati inawezekana, wakati wa mishahara na maslahi bora ya wafanyakazi ni sasa".
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) kwa shangwe na furaha huku wakiwa wameinua juu bango lao wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi) 
Sehemu ya wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye maadhimisho hayo 
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa na bango la Wizara wakati wa maadhimisho ya mei Mosi jijini Dodoma. 
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye maadhimisho ya Mei Mosi jijini Dodoma 
Ilikuwa ni shangwe na furaha kwa Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuadhimisha siku yao ya wafanyakazi inayoadhimishwa duniani kote tarehe 1 Mei kila mwaka 
Wafanyakazi waWizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa na ari katika kuadhimisha siku yao 
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakijumuika na wenzao duniani kote kuadhimisha Mei Mosi 
Sehemu nyingine ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 
Juu na chini ni umati wa Wafanyakazi kutoka Wizara, Sekta na Taasisi mbalimbali wakiadhimisha siku ya wafanyakazi duniani 
Wafanyakazi wa Wizara ya Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa jukwaani wakati wa maadhimisho ya Mei Mosi 
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani 
Sehemu nyingine ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa uwanjani wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani 
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walishiriki kwa wingi kuadhimisha siku yao 
Sehemu nyingine ya wafanyakazi hao wakiwa kwenye maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma 
Ni nyuso za tabasamu kama zinavyoonekana kwa Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki waliposhiriki kikamilifu maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani 
Watoto hawakuachwa nyuma na wazazi wao ambao ni Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuja kuadhimisha siku ya mfanyakazi duniani kama inavyoonekana pichani 
Juu na chini ni sehemu ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiungana na wafanyakazi wengine kuimba wimbo wa mshikamano "Solidarity Forever" kama wanavyoonekana pichani 
Picha ya pamoja 

WANANCHI WA BUSI, MAUNO AMBAO HAWAJAJENGA MAENEO YAO KUPATA UMEME

$
0
0
Waziri wa Nishati,Merdard Kalemani,akizungumza na baraza la madiwani wa Kondoa kabla ya kuanza ziara ya kuwasha umeme katika kijiji cha Mauno pamoja kituo cha Afya cha Busi mkoani Dodoma
Sehemu ya madiwani wakimsikiliza Waziri wa Nishati,Merdard Kalemani (hayupo pichani) wakati akizungumza nao katika kikao hicho

Waziri wa Nishati,Merdard Kalemani,akizungumza na wananchi wa Kinyasi alipfanya ziara ya kuwasha umeme kijiji cha Mauno pamoja na Kituo cha Afya cha Busi wilayani Kondoa
Waziri wa Nishati,Merdard Kalemani,akiwaonyseha wananchi kifaa cha kuunganishia umeme
Waziri wa Nishati,Merdard Kalemani akiwakabidhi wananchi kifaa cha kuunganishiwa umeme katika kitongoji cha Kinyasi.
Waziri wa Nishati,Merdard Kalemani,akimueleza jambo mbunge wa Kondoa ambaye pia ni Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji kabla ya kuwasha umeme katika kituo cha Afya cha Busi
Waziri wa Nishati,Dk.Merdard Kalemani,akisisitiza jambo kwa wananchi wa kijiji cha Busi kabla ya kuwasha umeme katika kituo cha Afya
Baadhi ya wananchi wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nishati,Dk.Merdard Kalemani alipokuwa anazungumza nao kabla ya kuwawashia umeme katika kituo cha Afya cha Busi.
Waziri wa Nishati,Dk.Merdard Kalemani,akiwasha umeme katika kituo cha Afya cha Busi wilaya ya Kondoa.Picha Zote na Alex Sonna-Fullshangwe blog



Na.Alex Sonna,Kondoa

WAZIRI wa Nishati Dk. Medard Kalemani amewataka wakazi wa vijiji vya Mauno na Busi wilayani Kondoa ambao bado hawajajenga kwenye maeneo yao kuweke miti ili wasogezewe huduma ya umeme kwa haraka.

Pamoja na hayo, amemwagiza Meneja wa shirika la umeme (Tanesco) pamoja na mkandarasi kuhakikisha wanamaliza kusambaza huduma ya umeme katika vijiji vyote vilivyosalia wilayani Kondoa ndani ya wiki moja.

Waziri Kalemani ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kuwasha umeme katika Kijiji cha Mauno pamoja na kituo cha Afya cha Busi huku akiwa ameongozana na Mbunge wa jimbo la Kondoa ambaye ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji. 

Waziri Kalemani amewataka wananchi hao kuwa, kuanzia sasa uunganishwaji wa umeme ni sh. 27,000 tu, uwe wa Tanesco au Rea huku akiahidi kupiga mnada wa kuku wa mkazi ambaye atashindwa kulipia kiasi hicho kwa ajili ya kuunganishiwa huduma hiyo.

Kalemani amefafanua kuwa Tanesco kupitia mkandarasi hawana sababu ya kusuasua kuwasha umeme katika maeneo hayo kwa kuwa nguzo na nyaya wanazo za kutosha,Aidha Waziri Kalemani ameahidi kurejea kwenye kata hiyo mwezi ujao kufuatilia agizo lake.

Mbunge wa Kondoa,Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji,aliwataka wananchi kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za serikali za kuwapelekea huduma ya umeme kwa kutumia fursa hiyo kuingiza umeme katika nyumba zao.

Pia ameishukuru Serikali ya awamu ya Tano kwa jitihada kubwa inazozifanya kupeleka maendeleo kwa wananchi na kujali wananchi wanyonge na wenye hali ya chini.

Mmoja wa wakazi kijijini cha Busi Bw.Nuru Bi Mdanga akizungumza baada ya kuwashiwa umeme ameelezea furaha yake ya kupunguzwa kwa gharama ya uunganishwaji wa huduma hiyo pasipokujali unatokea Rea au Tanesco.

RC SHIGELLA AWAPIGA MARUFUKU TABIA YA WAKUU WA WILAYA ZA MKOA HUO KUWAWEKA NDANI WAFANYAKAZI

$
0
0

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi 
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) happines Sima akizungumza wakati wa maadhimisho hayo leo 
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akikabidhi zawadi ya TV kwa wafanyakazi mbalimbali
Sehemu ya watumishi wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa Martine Shigella 
Sehemu ya wafanyakazi na wananchi wakiwa kwenye maadhimisho hayo leo
Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kushoto ni Meneja wa Mfuko huo mkoa wa Tanga Happines Sima akiweka sawa mwamvuli wakipita mbele ya mgeni rasmi 


MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella amewapiga marufuku wakuu wa wilaya za mkoa huo kukamatwa kwa watumishi na kuwekwa ndani wafanyakazi kwa misingi isiyofuata sheria na taratibu zilizopo nchini. 

Shigella aliyasema hayo leo wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambapo kimkoa iliadhimishwa kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga ambapo alisema kama sio kosa ambalo linaweza kuhatarisha amani, linalohusisha na wizi, mauaji. 

Alisema badala yake watumie taratibu za kisheria wawafikisha kwenye mamlaka za waajiri wao waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu sheria zilizopo ili kuweza kuwarekebisha kitabia. 

“Mfanyakazi anaweza akawa amechelewa lakini anaweza kuwa na sababu za msingi lakini haumsikilizi wala haufanyi hivyo unamuaaguza Mkuu wa wilaya (ODC) amkamate amweke ndani hii sio sawa acheni kutumia madaraka yenu vibaya”Alisema .

Alisema wakifanya hivyo watakuwa wamejenga misingi ya utawala bora, haki za binadamu ikiwemo utamaduni na utaratribu wa kuheshimia jambo ambalo litasaidia kuwawezesha kupiga hatua ya kubwa za kimaendeleo kwao na jamii zinazowazunguka. 

“RPC wafikishie wakuu wa Polisi wilaya za mkoa huu kwamba kuanzia sasa wa wafanyakazi kwenye mkoa wa Tanga kama sio la kuhatarisha amani,wizi ,mauaji ni marufuku kuwekwa ndani wafanyakazi kwa misingi isiyofuata taratibu “Alisema . Hata hivyo aliwataka lazima waweze kuweka mazingira mazuri ya kuwajenga wafanyakazi wao ili waweze kuona kosa walilofanya waweze kujutia na kuweza kujirekebisha badala ya kutumia mamlaka waliyonayo vibaya. 

WAFANYAKAZI SHIRIKA LA POSTA WALIVYOSHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI (MEI MOSI) KITAIFA MBEYA NA DAR ES SALAAM 2019

$
0
0

Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, akiwahutubia wafanyakazi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam leo.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda (wa pili kushoto), akiwa pamoja na Wakuu wa Wilaya (kulia) na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), wakiimba wimbo wa mshikamano, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam leo.
 Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania wakisakata rumba katika gari lao la matangazo kabla ya kuingia katika viwanja vya uhuru kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Shirika la Posta wakiwa nje ya uwanja wa Uhuru tayari kuingia uwanjani kwa maandamano katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
Wafanyakazi wa Shirika la Posta wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi, ndani ya Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Shirika la Posta wakiwa wenye furaha huku wamebeba bango lenye ujumbe maalum wakipita mbele ya mgeni rasmi,Jijini Dar es salaam.
Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakipita mbele ya mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, na bango lao lenye ujumbe maalum.
Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakimpungia mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wakati wakipita na bango lao.
Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakiwa na furaha huku wamebeba miavuli yao, wakipita kwa maandamano mbele ya mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda.
Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakifurahi wakiwa kwenye jukwaa kumsikiliza mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda.
Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania wakipita na Pikipiki zao za kutolea huduma mbalimbali za Shirika mbele ya mgeni Rasmi.
Magari ya kusafirisha vifurushi na kutoa huduma zingine za Shirika la Posta Tanzania yakipita kwa msafara mbele ya mgeni katika viwanja vya Uhuru, jijini Dar es Salaam. 
Meneja Rasilimali watu, Miriam Mbaga kwa niaba ya Postamasta Mkuu, akimkabidhi cheti mfanyakazi hodari kitaifa wa Shirika la Posta, Madaraka Simba (kulia), katika maadhimisho ya Mei Dei, mkoani Mbeya.
Meneja Rasilimali watu, Miriam Mbaga kwa niaba ya Postamasta Mkuu, akimkabidhi cheti mfanyakazi hodari wa Mkoa wa Mbeya, Godwin Davis (kulia), katika maadhimisho ya Mei Dei, mkoani humo.
Mwenyekiti (TEWUTA) Makao Makuu Shirika la Posta, Aneth Mdamu, katika hafla fupi ya kumpongeza mfanyakazi bora kitaifa wa Shirika la Posta, Madaraka Simba.
Meneja wa Shirika la Posta mkoani Mbeya, Abdon Mahimbo (katikati mwenye koti), akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi walioshiriki sherehe za Mei Dei, jijini humo.

RC MAKONDA AMUAGIZA RAS NA WAKURUGENZI WA MANISPAA KUWAPANDISHA MADARAJA WATUMISHI WANAOSTAHILI

$
0
0
* Akumbusha waajiri kuwaajiri walemavu kama sheria inavyosema

*Awapongeza wafanyakazi kwa juhudi wanazozifanya katika ujenzi wa taifa

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda amemuagiza Katibu tawala wa Mkoa na Wakurugenzi  wa Halmashauri zote jijini humo kuhakikisha wanawapandisha madaraja Watumishi wanaostahili ndani ya mwezi mmoja kuanzia leo.

 Makonda ametoa agizo hilo wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) ambayo Mkoani humo yameadhimishwa katika uwanja wa uhuru jijini humo, amesema kinachomshangaza ni kuona wafanyakazi wanaostahili kupandishwa madaraja hawapandishwi licha ya kuwa na sifa na vigezo vinavyostahili.

Aidha  Makonda amewaagiza maafisa kazi kushughulikia kero za wafanyakazi kwa wakati ili watumishi wafanye kazi zao bila vikwazo.

Pamoja na hayo Makonda amewataka waajiri kuhakikisha watumishi wanafanya kazi katika mazingira bora na salama huku akiwakumbusha kuajiri walemavu kama sheria inavyowataka.

Hata hivyo   amehimiza watumishi kujituma katika kazi wanazofanya huku akiwapongeza walimu na watumishi wengine kwa juhudi za kushughulikia kero za wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Paul Makonda akizungumza na wafanyakazi pamoja na wakazi wa Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi duniani Mei Mosi yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Muhimbili yang’ara maadhimisho ya wafanyakazi duniani

$
0
0
Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wameungana na wenzao duniani kushiriki maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo hufanyika Mei Mosi kila mwaka.

Wafanyakazi wa MNH walianza maandamano katika hospitali hii kuelekea Uwanja wa Uhuru ambako wameungana na wenzao kutoka taasisi mbalimbali jijini Dar es Salaam kuadhimisha siku hii muhimu kwa wafanyakazi nchini na duniani kote.

Katika kuadhimisha siku hii wafanyakazi wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kujenga uchumi imara, huku kauli mbiu ikiwa ni, “Utawala bora ni kwa maendeleo ya nchi.” Mgeni rasmi katika maadhimisho haya, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ongezeko la mshahara ni moja ya jambo muhimu kwa wafanyakazi na kwamba linamgusa kila mmoja. Pia, ametaka kuwapo kwa usalama mahala pa kazi ili kuondoa hofu kwa wafanyakazi.

“Naomba suala la usalama na afya katika sehemu ya kazi lizingatiwe, pia nawaomba viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kufuatilia usalama na afya mahala pa kazi, niwaombe viongozi wanipatie taarifa ni kampuni zipi hazipeleki michango ya wafanyakazi katika mifuko ya hifadhi. Hili lifuatiliwe ili kuondoa kero kwa wafanyakazi.”

Pia, amewapongeza wafanyakazi mbalimbali kwa utumishi bora kwani wamekuwa wakifanya kazi nzuri licha ya kuwapo kwa changamoto mbalimbali. Makonda pia amewapongeza walimu kwa kazi nzuri wanayofanya na amewaleza Watanzania kwamba walimu wanaowajenga watu hasa wanafunzi kufikia mafanikio mazuri katika maisha.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwa kwenye maandamano ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani ambayo hufanyika Mei Mosi kila mwaka.
 Maandamano yakiendelea jijini Dar es Salaam ambako wafanyakazi mbalimbali wameshiriki leo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambako wameshiriki maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani pamoja na wenzao kutoka taasisi na kampuni mbalimbali jijini Dar es Salaam.
 Maandamano yakiendelea karibu na Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam katika barabara ya Taifa.
 Wafanyakazi wa Muhimbili wakiwa na wenzao kutoka taasisi mbalimbali wakishiriki kwenye maandamano leo jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images