Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA ELIMU AFANYA UKAGUZI WA HATUA ZA MAANDALIZI YA UWEKAJI JIWE LA MSINGI JENGO LA CHUO KIKUU MZUMBE KAMPASI YA MBEYA

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhe. Prof. Joyce Ndalichako leo ametembelea na kukagua hatua za maandalizi ya ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya, ambapo amepongeza Uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa hatua za ujenzi ulipofikia.

Akiwa ameambatana na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Pro. Lughano Kusiluka, Prof Ndalichako amemwelekeza Mkandarasi wa Ujenzi kuhakikisha kufikia Juni 2019 ujenzi wa Jengo hilo kuwa umekamilika kama ilivyopangwa.

Kukamilika kwa ujenzi kutawezesha jumla ya wanafunzi 900 kupata vyumba vya madarasa mbali na kumbi za mikutano na ofisi za uendeshaji. Jengo hilo linatarajiwa kuwekwa jiwe la Msingi na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Joseph Magufuli Mei 1, 2019.
 
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akiongozwa na Mkandarasi wa mradi akikagua vyuma vya madarasa mara alipowasili kukagua ujenzi wa jengo la ghorofa tano la Taaluma na Utawala linalotazamiwa kumalizika mwezi Juni,2019. Pamoja naye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka, Naibu Mawakamu Mkuu wa Chuo Utawala na fedha Prof. Ernest Kihanga na wasimamizi wa ujenziWaziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiweka saini kwenye kitabu cha wageni kwenye eneo la ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya mbeya mara tu baada ya kuwasili. Aliyeshika kitabu ni Injiani Thadeus Koyanga na kushoto anayeshuhudia tukio hilo ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka ( Mwenye Kaunda suti kushoto) Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako (kushoto) akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka ( Mwenye Kaunda suti kushoto) pamoja na Mkandararasi na wajenzi; wakikagua ramani ya jengo la Taaluma na Utawala la Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya. Profesa Ndalichako (katIkati) akikagua mahali litakapojengwa jiwe la msingi ambalo litawekwa rasmi na Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muuungano wa Tanzania Dr.John Pombe Joseph Magufuli Mei 1, 2019. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka na kulia ni Mkadarasi wa Ujenzi Injinia Thedeus Koyanga (mwenye shati la mikono mirefu) akifuatiwa na Profesa Ernest Kihanga Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha.Mhe. Profesa Joyce Ndalichako alikagua muonekano wa nje wa jengo la Taaluma na Utawala la chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya pamoja na kukagua usafi wa mazingira, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi kabla Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli hajafika kuweka jiwe la msingi.

ELIMU YA AFYA YA UZAZI BADO NI CHANGAMOTO KWA WASICHANA NA VIJANA

$
0
0
Pamella Chogo kutoka Taasisi ya Kimataifa ya "Chanya Change"akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)
Anna Mahenge Mtaalamu wa Masuala ya Afya ya uzazi anasema familia nyingi zimekuwa zikishindwa kukaa na mabinti zao na kuwaeleza ukweli kuhusu afya uzazi 

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Kutokana na asilimia kubwa ya wasichana na vijana kutokuwa na uelewa juu ya Afya ya uzazi jamii kuanzia ngazi ya familia zimetakiwa kuwajengea uwezo ikiwa ni sehemu ya kuwaelimisha kuhusiana na afya ya uzazi katika maisha ya kila siku,

Taasisi ya Kimataifa ya "Chanya Change"imeendelea kutoa elimu ya kujitambua na kuchukua tahadhari kutokana na vihatarishi katika mazingira wanayo ishi wasichana zaidi ya 100 katika shule mbalimbali katika jiji la Arusha wakiwa na lengo la kuwasaidia kujitambua ,kutoa hamasa katika masomo ya sayansi pamoja na mafunzo ya Tehama kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo 

Akizungumza na Michuzi Blog Pamela Chogo ambae ni muandaaji wa warsha hiyo iliyo andaliwa na taasisi ya Kimataifa ya "+Chanya Change" kwa ajili ya wasichana amesema Msichana ana nafasi kubwa katika kuchochea shughuli za kimaendeleo ya taifa hususani katika Masuala ya Sayansi na teknolojia (TEHAMA) 

Amesema jamii inatakiwa kuondokana na mtazamo hasi kuhusu watoto wa kike kwamba hawawezi kufanikisha mambo,badala yake watambue wanawake wengi wamekuwa wakutumia changamoto hiyo Kuwa fursa katika jamii wanazo ishi hatimae wameleta chachu ya Maendeleo kuelekea Tanzania ya Viwanda.

"Ni wakati muafaka kwa jamii kuondokana na mtazamo Hasi kuhusu mtoto wa kike Kuwa hawezi kufanikisha Mambo muhimu katika jamii,mwanamke ndio msingi wa maendeleo"alisema Pamela.

Amesema bado kumekuwa na wimbi kubwa kwa baadhi ya wasichana kuto jitambua kutokana na kukosa elimu ya Afya ya uzazi kwa Vijana ngazi ya familia hivyo wazazi wanajukumu kubwa la kuelimisha Watoto wao wa kike wakaribiapo Rika la balehe ili kuepukana na ongozeko la ndoa,mimba za utotoni.

"Wazazi wengi bado wanatamaduni za kizamani ambazo zimekuwa chanzo Cha wasichana wengi kujiingiza Kwenye makundi Hasi yanayo pelekea kupata magonjwa na Matumizi ya madawa ya kulevya kwa kukosa elimu ya jinsi"

Anna Mahenge ni mtaalamu wa Masuala ya Afya ya uzazi anasema familia nyingi zimekuwa zikishindwa kukaa na mabinti zao na kuwaeleza ukweli kuhusu afya uzazi jambo ambalo limekuwa likichangia ongezelo la vihatarishi na maambukiIi ya magonjwa ya zinaa pamoja na mimba za utotoni.

"Kuficha ficha mambo kwa wazazi juu ya wasichana kuhusu maumbile na maungo ya uzazi bado ni Changamoto kwa jamii, hivyo jamii ibadilike"alisema muuguzi huyo.

Nao baadhi ya wasichana waliowashiriki katika warsha hiyo wamesema Asasi za Kiraia zinazo hudumia jamii waige mfano wa kinacho fanywa na taasisi ya Chanya Change ili kufika katika maeneo husika na kutoa elimu ili kukiandaa kizazi chanya kwa siku zijazo.

UNAIKUMBUKA BEMBEYA JAZZ YA GUINEA?

$
0
0
Na Moshy Kiyungi
Miaka ya nyuma palikuwa na wimbo wa Whsky Soda,  uliojizolea umaarufu mkubwa miongoni mwa wapenda muziki katika nchi za Afrika ya Mashariki na Kati. Wimbo huo ulipokuwa ukipigwa katika radio yeyote, watu walikuwa wakiufurahia kusikia sauti ya maneno yasiyo eleweka ya ‘Chapombe’, neno la “ila Whsky Soda”.

Wimbo huo uliopigwa katika mtindo wa aina yake, ni kazi nzuri ya bendi Bembeya Jazz toka nchini Guinea, ambayo hutajwa kama ni nguzo ya historia ya muziki wa kisasa wa Afrika Magharibi. Mwaka 1958 kulikuweko na kura ya maoni katika nchi zilizotawaliwa na Wafaransa  huko Afrika Magharibi, ambapo wananchi waliulizwa kama wanataka kuendelea kuwa chini ya Ufaransa. Nchi ya Guinea ndio  pekee iliyokataa.

Ahmed Sekou Toure akachaguliwa kuwa rais  wa nchi hiyo, na kati ya vitu alivyoanzisha mara  moja ilikuwa ni Bendi ya Taifa iliyoitwa Syli National Orchestra. Bendi hiyo ilikuwa na maskani katika jiji la Conakry, iliendelea kukua hatimae  mwaka 1961, ikagawanyika katika makundi mawili ya Bala et ses Balladins na Keletigui et Ses Tambourinis.

Kutokana na upenzi wake wa sanaa, rais Sekou Toure alitengeneza bendi za mikoani, ambazo alizifadhili kwa vyombo na fedha. Katika jiji la Beyla Kusini Mashariki mwa Guinea kwenye mwaka 1961, Gavana wa mkoa huo Emile Conde alianzisha kakundi kake kadogo kakiwa na gitaa moja tu kavu. Pasipo uzoefu mwingi lakini taratibu kakanza kujitokeza mbele ya jamii.

Kabendi hako toka mikoani, kalishinda mashindano mengi na kujulikana sana mjini Conakry. Hatimae Chama tawala kiliitaka bendi ya Bembeya ihamie Conakry mwaka 1965. Kabendi hako kakataifishwa na kufanywa bendi ya Taifa kama zile nyingine mbili.

Bendi hii ilianza kwa kuitwa Beyla Jazz, lakini siku moja April 1961, katika mkutano wa bendi wakaamua kujiita Bembeya Jazz. Wakati huo Guinea kulikuwa na aina mbili za wanamuziki wale waliopiga muziki wao wa  asili na wale waliotoka kwenye shule za Kifaranza amabo walipiga muziki wa asili ya Cuba.

Amri ilitolewa na serikali kuelekeza wanamuziki wapige muziki kutokana na vionjo vya kwao katikati ya miaka ya 1960. Hivyo ukisikia nyimbo za Bembeya Jazz kabla ya hapo unasikia vionjo vya Cuba kama zile za Whisky Soda na Mamiwata,  ni mfano wa upigaji huo. Baada ya hapo mpaka ilipokuja kurekodi mara ya mwisho bendi hiyo imekuwa na vionjo vya muziki wa asili wa Guinea.

Wakati wa uhai wa Sekou Toure, nchi hiyo ilianzisha nembo ya kurekodia iliyoitwa Syliphone. Ilikuwa  ni nembo  ya Taifa, jambo hilo halikuwahi kufanyika popote Afrika. Tanzania ilijaribu kuiga mfumo huo na iliweza kutoa kazi chache kwa kutumia Kampuni ya Filamu Tanzania na kuwa na nembo za TFC na Sindimba.

Uchumi wa nchi ya Guinea iliporomoka mnamo miaka ya 1970. Nembo hiyo iliweza kutoa album 80 na ikawa ndiyo mwisho wa bendi hiyo. Kufuatia hali ya Uchumi kuwa mbaya, baadhi ya wanamuziki wa nchi hiyo wakaanza kuelekea nchini ya Ufaransa na nyingine kujitafutia maisha. Yaelezwa kwamba rais  Sekou Toure alifanya kazi kubwa kwa nchi yake kwa upande wa sanaa na kuweza kuifanya Guinea kuwa kati ya nchi zilizoongoza Afrika katika utamaduni wa muziki.

Kila kizuri hakikosi kasoro. Rais huyo taratibu akaanza kufanya udikteta mkubwa kwa watu  waliompinga. Kila  aliyefanya hivyo alipotea au kuuawa.
Kama ilivyotokea kwa Fodeba Keita msanii aliyeanzisha kundi la kwanza la Ballet nchini Guinea, rais Sekou Toure akamfanya Waziri wa Mambo ya Ndani, lakini kufikia mwishoni mwa miaka ya 1960, rais huyo akawa na wasiwasi wa kupinduliwa na Fodeba.

Kwa mamlaka aliyokuwa nayo, alimfunga na hatimae Fodeba akapotea wala haikujulikana alikufa vipi au lini. Pamoja na udikteta huo alikuwa tofauti na ule wa aliyekuwa rais wa Zaire sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mobutu Seseseko. Rais Toure alikuwa mzalendo hakuwa fisadi wa kuiba mabilioni na kuyatorosha nje, ila aligeuka akawa katili kwa kulinda himaya ya utawala wake.

Pamoja na maelfu ya Waguinea kuikimbia nchi yao kutokana na utawala huo, Wanamuziki wachache walimlaani, wengine walifaidika na fadhila zake katika tasnia ya muziki. Kufikia mwaka 1980 Bembeya Jazz ilikuwa haipigi tena maonyesho ya kawaida  labda kwa kukodishwa.

Kati ya mambo makubwa ya kusikitisha yaliyo kikumba kikundi hicho ni kifo cha muimbaji wao Demba Camara, aliyefariki katika ajali ya gari lao lililokuwa likiendeshwa na dereva wa bendi yao ilipopinduka wakiwa safarini. Katika gari hilo pia alikuweko Sekou 'Bembeya' Diabate (Diamond Finger).

Demba alikutwa ametupwa nje ya gari, walipowasili wanamuziki wengine waliokuwa katika gari jingine. Mwanamuziki Sekou 'Bembeya' Diabate, bado anafanya maonesho lakini hasa nje ya Guinea. Hakuna ubishi kuwa historia ya sanaa ya Tanzania, iliiga baadhi ya taratibu za sanaa za rais Sekou Toure wa Guinea, kwa kuanzishwa kwa kundi la Sanaa la Taifa.

Si hivyo tu kwani kulianzishwa bendi ya Wanawake,  iliyotokana na ziara za rais huyo hapa kwetu. Yeye alikuja kasindikizana na kundi kubwa la wasanii wa kundi la Taifa.

Dar ya kijani ya UVCCM yavuna wanachama 500

$
0
0
Na Ripota Wetu,Michuzi TV

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Rodrick Mpogolo, amewapokea wanachama wapya wa chama hicho kupitia kampeni ya Dar ya kijani inayoratibiwa na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam.

Kampeni hiyo ya Dar ya Kijani ina lengo la kurudisha mitaa, kata na majimbo yote katika himaya ya chama, inawataka vijana na wanachama wote kuimarisha ushirikiano na kupata ushindi wa pamoja wenye heshima kwa chama hicho tawala.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwa Wilaya ya Kinondoni, Mpogolo, amewataka vijana kuwa makini na waadilifu kwani wao ndio wataokaojenga hehima ya chama na Taifa kwa ujumla.

“Vijana ndio tunao wategemea katika uchaguzi ujao tunahitaji vijana makini na waadilifu ambao watakitumikia chama chetu cha Mapinduzi na Serikali yetu. jiepushieni mbali na tabia ambazo zitawaondelea maadili yenu. Ili mkawe viongozi makini kwani taifa letu linaitaji viongozi makini na wachapakazi .

Amesema yeye hatoita Dar ya Kijani ila anaitambua Tanzania ya Kijani kutokana na kaz kubwa inayofanywa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi ya kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli.

“Mimi sitaita Dar es Salaam ya Kijani bali nitaita Tanzania ya Kijani kwa sababu Rais wetu mpendwa Dk. John Magufuli anafanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo nchini, tunaona ujenzi wa barabara za juu pale Ubungo na tunashuhudia maendeleo makubwa yanayofanywa katika sekta ya elimu vituo vya afya, kuwasaidia wamachinga kwa kuwapa vitambulisho vya ujasiriamali, bodaboda.

“Pia ameleta usawa kwa Watanzania wote kuwa sawa. Kwahiyo kwa namna hii lazima chama chetu kiendelee kushika hatamu kwa sababu tunawatumikia wananchi ipasavyo kwa namna hii nina uhakika Tanzania inaenda kuwa ya kijani,” amesema Mpogolo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, amesema kuwa lengo la kampeni hiyo ya Dar es Salaam ya Kijani ni kuwaandaa vijana na chaguzi zijazo ikiwamo wa Serikali za Mitaa mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 ili chama hicho kipate ushindi wa kishindo.

“Lengo la Dar es salaam ya Kijani ni kuwaanda vijana wa Mkoa wa Dar es salaam katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa lakini kuwataka vijana kuhakikisha wanajitokeza katika kugombea nafasi lakini pia kuhakikksha CCM kinapata ushindi wa kishindo kwa mkoa wote,” amesema Kilakala

Amesema tangu kampeni hiyo ilipozinduliwa Machi 17, mwaka huu jijini Dar es Salaam imefanikiwa kuvuna zaidi ya wanachama 500 ambao wamejiunga na chama hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizunguka kwenye uzinduzi wa Dar ya Kijani ambayo sasa imetua Wilayani Kinondoni
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, akizungumza katika uzinduzi huo 
 Vijana wa CCM wakiwe kwenye uzinduzi huo Wilayani Kinondoni 

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIWIRA PAMOJA NA KUFUNGUA KIWANDA CHA MAPARACHICHI KILICHOPO RUNGWE MKOANI MBEYA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Uyole nje kidogo ya jiji la Mbeya wakati akiwa njiani kuelekea Wilayani Rungwe.
 Wananchi wa Kiwira wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo hilo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kiwira Wilayani Rungwe wakati aliposimama kuwasalimia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine wa Mkoa wa Mbeya, Mawaziri, Wabunge akikata utepe kufungua kiwanda cha Maparachichi cha Rungwe Avocado Campany mkoani Mbeya.
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maparachichi yanayohifadhiwa kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi katika kiwanda cha Rungwe Avocado Campany mkoani Mbeya. 
 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mashine maalumu ya kuangalia ubora wa maparachichi katika kiwanda cha Rungwe Avocado Campany mkoani Mbeya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyakazi pamoja na wananchi katika eneo la kiwanda cha cha Rungwe Avocado Campany mkoani Mbeya. PICHA NA IKULU

MAHABUSU 201 WANUFAIKA NA ZIARA YA NAIBU KATIBU MKUU NA DPP KATIKA MAGEREZA MKOANI MARA

$
0
0
Mahabusu 201 waliokuwa katika magereza ya Wilaya za Musoma, Tarime na Mugumu Serengeti wamefutiwa kesi zao mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili kufuatia ziara ya ukaguzi ndani ya magereza hayo ya mkoa wa Mara iliyofanywa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Bw. Biswalo Maganga mwishoni mwa wiki iliyopita.

Viongozi hao walioambatana na wataalamu wao walifanya ukaguzi ndani ya magereza na kuzungumza na wafungwa na mahabusu walioko ndani ya magereza hayo nao ili kujua changamoto za kisheria zinazowakabili na kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha kuwa changamoto hizo zinatatuliwa.

Baada ya kuzungumza na mahabusu hao na kupitia majalada yao Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Biswalo Mganga aliwaagiza waendesha mashtaka mkoa wa Mara kwenda Mahakamani na kuzifuta kesi zilizokuwa zikiwabili mahabusu hao ambao wataachiwa huru baada ya Mahakama kupokea nia ya DPP ya kufuta kesi hizo kwa mujibu wa sheria.

Mahabusu hao 29 wanatoka katika Gereza la Wilaya ya Musoma, 106 wanatoka katika Gereza Tarime na wengine 66 wanatoka katika Gereza Mugumu-Serengeti.

Katika Mahabusu hao wanawake ni 11, Watoto 39, wazee 9 na wanaobakia ni vijana ambao walikuwa wakikabiliwa na kesi mbalimbali ambazo zilionekana zinaweza kumalizwa nje ya Mahakama, zile ambazo ushahidi wake ulionekana kuwa hafifu, kesi ndogo ndogo kama kupigana, kutukanana, wizi wa simu na vitu vingine vidogo vidogo, kutishiana kwa maneno, waliokiri kunywa gongo na kuvuta bangi, wengine walionekana kuwa mashahidi wa mashtaka.

Akizungumza na wafungwa na mahabusu katika nyakati tofauti ndani ya magereza hayo Naibu Katibu Mkuu Bw. Mpanju aliwataka mahabusu watakaofutiwa Mashtaka yao kubadili mienendo yao na kuwa raia wema na kuacha kuishi kimazoea kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria na Serikali haitoacha kuwachukulia hatua za kisheria.

“Ndugu zanguni mmeona kazi kubwa tulioifanya leo hii humu ndani, ni wajibu wenu kuwa raia wema na kubadili mienendo ya maisha yenu, muache kuishi kwa mazoea, muangalie mnavyoishi na mkiachiliwa mkaambie na wenzenu kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria na Serikali haitawaacha lazima hatua za kisheria zichukuliwe”, alisema Bw, Mpanju.

Naye Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ambaye ni mratibu wa upelelezi wa kesi za jinai nchini Bw. Biswalo Mganga aliwataka wote wanaohusika na kazi ya upelelezi wa kesi mbalimbali zinazowakabili mahabusu hao kuhakikisha wanakamilisha upepelezi wa kesi mbalimbali kwa wakati ili kuondoa hali ya upelelezi kuchelewa.

Amesema kitendo cha kuchelewesha upelelezi kinawafanya watuhumiwa wa makossa ya jinai nchini kukaa magerezani kwa muda mrefu bila ya kujua hatma zao na hivyo kufanya magereza kuwa na msongamano ambao unaweza kuzuiliwa.

“Wapelelezi mlioko hapa, nadhani mnaelewa ninacho kisema hapa, fanyieni kazi haraka kesi za watuhumiwa hawa ili ziweze kumalizwa na  wajue moja kama wanafungwa au wanaachiwa huru maana kwa kuendelea kuwa mahabusu hakuna tija kwa taifa, hawa watu humu ndani wanatakiwa wafanye kazi za uzalishaji na hiyo inakuwa sehemu ya urekebishwaji na sio kukaa bure na kujazana”, alisema Bw. Mganga

Mahabusu hao walikabidhiwa kwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Mara ili kuhakikisha wanarudisha vitu walivyoiba, wanaombana misamaha na kuwa raia wema ndani ya jamii zao na kuambiwa kuwa Serikali itawachukulia hatua za kisheria tena iwapo wataenda uraiani na kujihusisha na vitendo vya kihalifu.
Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu Mpanju aliongozana na wataalamu wa Sheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) Taifa akiwemo Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Dkt. Edson Makallo na Mkoa wa Mara, Maafisa kutoka Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Waendesha Mashtaka kutoka TANAPA.

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju ( katikati) akitoa maagizo nje ya gereza la Wanawake la WIlaya ya Musoma baada ya kutembelea gereza hilo kwa ajili ya kufanya ukaguzi na kuzungumza na wafungwa na mahabusu
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju ( alieshika fimbo nyeupe) ikiwa katika picha ya pamoja na timu ya wataalamu nje ya gereza la Wilaya ya Musoma mkoani Mara baada ya kufanya ukaguzi ndani ya gereza hilo na kuzungumza na wafungwa na mahabusu walioko ndani ya gereza hilo.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju ( alieshika fimbo nyeupe) ikiwa katika picha ya pamoja na timu ya wataalamu nje ya gereza la Wilaya ya Tarime mkoani Mara baada ya kufanya ukaguzi ndani ya gereza hilo na kuzungumza na wafungwa na mahabusu walioko ndani ya gereza hilo.
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Bw. Biswalo Mganga (katikati ya Maaskari Magereza) katika picha ya pamoja na timu ya wataalamu nje ya gereza la Wilaya ya Mugumu- Serengeti mkoani Mara baada ya kufanya ukaguzi ndani ya gereza hilo na kuzungumza na wafungwa na mahabusu walioko ndani ya gereza hilo na kuwaachia huru mahabusu 66.

MBULU WAMFAGILIA RAIS MAGUFULI

$
0
0
MKUU wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Chelestino Simbalimile Mofuga amempongeza Rais John Magufuli kwa kufanya maendeleo makubwa kwenye uongozi wake wa awamu ya tano mithili ya Rais aliyekaa madarakani kwa muda wa miaka 40.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa ujenzi wa jengo jipya la makao makuu ya halmashauri hiyo linalojengwa na Kampuni ya Mzinga Holding Ltd, katika kata ya Dongobesh litakalogharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.7 Mofuga alisema Rais Magufuli amewatendea mengi watanzania.

Alisema pamoja na miradi mikubwa ya kimkakati aliyoitekeleza ikiwemo ya ujenzi wa barabara za juu, kununua ndege, elimu bila malipo na mradi mkubwa wa umeme pia amefanikisha miradi ya maendeleo kwenye elimu, afya na maji.

Alisema kwa muda wa miaka minne ya utawala wa awamu ya tano serikali ya awamu ya tano imefanyika maendeleo mengi kwenye kila sehemu hapa nchini huku wilaya ya Mbulu ikiwa na miradi mingi ya maendeleo.

"Tunawashukuru sana viongozi wa dini kwa kumuombea Rais Magufuli kwani maendeleo aliyoyafanya Tanzania utadhani amekaa madarakani kwa muda mrefu wa zaidi ya miaka 40," alisema Mofuga.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Hudson Kamoga alimshukuru Rais John Magufuli kwa kuwapatia fedha za ujenzi wa jengo hilo litakalokuwa mfano wa majengo bora mapya ya halmashauri nchini. Kamoga alisema Rais John Magufuli ameipendelea halmashauri ya wilaya ya Mbulu kwani ameiwezesha kufanikisha miradi mingi ya maendeleo.

"Pamoja na jengo jipya la halmashauri ya wilaya litakalogharimu shilingi bilioni 4.7 pia amewezesha ujenzi wa bwawa la umwagiliaji Dongobesh na fedha kwenye idara za afya, elimu na miundombinu," alisema Kamoga.

Mbunge wa jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Maasay alimshukuru Rais Magufuli kwa kufanikisha mradi huo na ujenzi wa hospitali ya Wilaya, kituo cha afya Dongobesh, kwani ndiyo faida ya kuchagua kiongozi anayetekeleza ilani ya uchaguzi.

Massay alisema wanamshukuru Rais Magufuli kwa utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo ya elimu, afya, maji, miundombinu ikiwemo na ujenzi huo ambao utasogeza huduma ya jamii karibu zaidi na wananchi wa jimbo hilo.

Alisema ili mwananchi wa Haydom afike Mbulu mjini makao makuu ya halmashauri hiyo atakwenda kilomita 86 na Dongobesh kilomita 52 hivyo hapo patakuwa karibu zaidi.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Joseph Mandoo alisema madiwani wa halmashauri hiyo ndiyo waliamua makao makuu yawe Dongobesh baada ya wataalamu kupendekeza eneo hilo.

Mandoo alisema wataalamu hao waliagizwa na madiwani wafanye utafiti wa kata inayofaa kuwa makao makuu ya halmashauri hiyo nao wakapendekeza kata ya Dongobesh.
 Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Chelestino Simbalimile Mofuga akizungumza na wananchi wa kata ya Dongobesh wakati akizindua ujenzi wa jengo la makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya hiyo lenye thamani ya shilingi bilioni 4.7.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Stanley Kamoga (kushoto) akimuangalia mzee wa Kata ya Dongobesh aliandika historia ya eneo la ujenzi wa jengo jipya la makao makuu ya Halmashauri hiyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Chelestino Simbalimile Mofuga (watatu kushoto) akichimba kwa sururu wakati azindua ujenzi wa jengo jipya la makao makuu ya halmashauri ya wilaya hiyo lenye thamani ya shilingi bilioni 4.7 kwenye kata ya Dongobesh litakalojengwa na kampuni ya Mzinga Holding Ltd.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Chelestino Simbalimwile Mofuga (katikati) akizungumza wakati akikagua ramani ya jengo jipya la Halmashauri ya Wilaya hiyo linalojengwa na Kampuni ya Mzinga Holding Ltd kwa gharama ya shilingi bilioni 4.7 katika kata ya Dongobesh, kushoto ni mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Flatei Maasay na kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Joseph Mandoo.

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI AFANYA MABADILIKO YA BAADHI YA MAKAMANDA WA MIKOA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, (CGF) Thobias Andengenye, amefanya mabadiliko ya baadhi ya Makamanda wa Mikoa hapa nchini.

Makamanda walioguswa na mabadiliko hayo ni Kamishna Msaidizi wa Zimamoto (ACF) Mohamed Kondo, aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kinondoni, anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya.

Kamishna Msaidizi (ACF) Juma Yange, aliyekuwa Kitengo cha Utawala Mkoa wa Kinondoni, anakuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kizimamoto Kinondoni.

Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto (ASF) John Francis, aliyekuwa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Handeni Mkoani Tanga, anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Rukwa.

Vilevile, aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kigoma, Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto (ASF) Athumani Basuka, anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Hai – Siha, nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi (ASF) Jumbe Juma.

Pia aliyekuwa Kamanda wa Kiwanja cha Ndege Mkoa wa Iringa, Mkaguzi wa Zimamoto (INSP) Hamisi Dawa, anaenda kuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kagera. 

Mabadiliko haya ni ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaendelea kutoa wito kwa Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Makamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mikoa na Wilaya katika suala la Kinga na Tahadhari Dhidi ya majanga.

Imetolewa na;
Joseph Mwasabeja – (INSP)
Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Makao Makuu.


IGP SIRRO AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI IRINGA

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (kulia)  akizugumza jambo na kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Wilbrod Mutafungwa aliyekutananae mkoani humo wakati akiwa njiani kuelekea mikoa ya Iringa na Njombe kwa ziara ya kikazi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (kushoto) akipokea salamu ya heshima ya kijeshi wakati alipowasili Leo katika mkoa wa Iringa kwa ziara ya kikazi  ya siku moja yenye lengo la kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makazi ya askari pamoja na utendaji wao wa kazi za Polisi. . 
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (kulia)  akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi (kushoto) wakati alipomtembelea ofisini kwake leo mkoani humo akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makazi ya askari pamoja na utendaji wao wa kazi za Polisi, aliyepo katikati ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Juma Bwire. Picha na Jeshi la Polisi. 

Whatsapp kutumika kuhudumia wateja wa Tigo

$
0
0

. Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Tigo Mwangaza Matotola, akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) namna ambavyo huduma ya WhatsApp inavyoweza kutumiwa na mteja kuuliza au kupata ufafanuzi kutoka kwa watoa huduma wa Tigo. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Tigo Woinde Shisael

. Meneja Mawasiliano wa Tigo Woinde Shisael (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya WhatsApp ambayo inaweza kutumiwa na wateja wa kampuni hiyo kuuuliza au kupata ufafanuzi wa bidhaa na huduma mbali mbali za kampuni hiyo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha Tigo Mwangaza Matotola

 Baadhi ya waandishi wa habari wakiuliza maswali wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya WhatsApp ambayo inaweza kutumiwa na wateja wa Tigo kupata ufafanuzi au kutatuliwa changamoto mbali mbali wanazokumbana nazo wakati wakitumia mtandao wa Tigo.


 

Kampuni ya Tigo Tanzania, leo imezindua huduma ya whatsApp kwa ajili ya kuwahudumia wateja wake.

Huduma hii ya kidijitali, itawawezesha wateja wa Tigo kutuma dukuduku zao na kupokea majibu ya papo kwa papo watakapotumia namba ya WhatsApp ambayo ni 0675100100.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo mpya jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Tigo Mwangaza Matotola alisema, Tigo imekuwa kampuni ya kwanza nchini kutumia mtandao wa kijamii wa WhatsApp kuwahudumia wateja wake.

“Kupitia huduma hii mpya, wateja wa Tigo watapata uzoefu binafsi pamoja na kupata majibu ya papo kwa papo watapotaka kupata ufafanuzi wa jambo au utatuzi wa changamoto zozote katika kutuia mtandao wetu,” alisema WhatsApp ni moja kati ya mitandao ya kijamii yenye nguvu sana duniani kwa sasa.

“Kwa kuzingatia ukweli huu, huduma hii itawawezesha wateja wa Tigo kupata huduma binafsi na zenye usalama. Uzinduzi wa huduma hii ni moja kati ya mikakati yetu ya kuhamasisha maisha ya kidijitali, vile vile tunapanua wigo wa namna wateja wetu wanavyoweza kuhudumiwa tunavyoongeza WhatsApp kwenye huduma zetu za mitandaoa ya kijamii kama Facebook, Instagram na Twitter. Huduma ya WhatsApp inapitakana kwa wateja wote wa Tigo,” alifafanua Mwangaza.

Mwangaza aliongeza kuwa, huduma hiyo imetengenezwa maalum kwa ajili ya kumhudumia mtu mmoja mmoja na siyo kuwahudumai watu kwa pamoja kama kundi (group la WhatsApp). “Mteja siyo tu ataweza kujielezea kupitia huduma hii lakini pia anaweza kutuma picha kwenye mfumo wa ‘screenshot’ kwenda namba 0675100100 na atapata majibu ya papo kwa papo kwa kile atachoakiuliza au kutaka ufafanunuzi/utatuzi,” alisema.

“Tigo Tanzania inajivunia kuwa kampuni ya simu namba moja kwenye mageuzi ya kidijitali pamoja na uvumbuzi. Tigo imeweza kuwa ya kwanza kuzindua bidhaa nyingi kwenye soko la Tanzania ambazo zinathibitisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora kwa wateja wetu pamoja na uzoefu wa aina yake. huduma hii ya WhatsApp ni sehemu ya safari yetu hii ya mageuzi ya kidijitali,” aliongeza

Wateja wanaotumia WhatsApp wanaweza kuwasiliana na kitengo cha huduma kwa wateja cha Tigo muda wowote wanaopenda na kama itatokea kukawa na kuchelewa kupata mrejesho atapokea ujumbe mfupi.Huduma hii mpya ya WhatsApp kwa ajili ya kuwahuduma wateja, ni sehemu ya mkakati wa kampuni ya Tigo kuwapatia wateja wake uzoefu wa aina yake. 

KAMATI NDOGO YA ARDHI YAKUTANA JIJINI DODOMA KUJADILI MUSTAKABALI WA WANAWAKE KUMILIKI ARDHI NCHINI

$
0
0
Na Anthony Ishengoma
Kamati ya Uwezeshaji Wanawake katika Umiliki na Matumizi ya Ardhi inakaa leo Jijini  Dodoma  kujadili na kuhainisha fursa na vikwazo  vya kuwezesha umiliki wa ardhi kwa wanawake na kupanga mikakati ya kufikia lengo la wanawake kumiliki na kutumia ardhi kwa maendeleo yao.

Akifungua Kikao cha Kamati hiyo mapema leo Jijini Diodoma Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Patrick Golwike amewaambia wajumbe wa kamati hiyo kuwa kikao hicho ni muhimu kwa kuwa kinajaadili namna bora ya kuwawezesha wanawake kumiliki na kutumia  ardhi katika kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Aidha Golwike ameongeza kuwa pamoja na kuwepo kwa sheria na jitihada mbalimbali kutoka kwa wadau wa kusaidia wanawake kunufaika na ardhi bado kuna vikwazo vinavyoathiri wanawake kumiliki ardhi kwa sababu mbalimbali zikiwemo mila na desturi, ufahamu mdogo wa umiliki ardhi ikiwemo ukosefu wa dhamana za kiuchumi.

Golwike amewataka wajumbe wa kamati hiyo kupitia kwa Taasisi wanazotoka kuwa wabunifu wakwenda na ubunifu wa sayansi na teknolojia katika kuwawezesha wanawake kumiliki na kutumia ardhi kama njia ya kujikwamua kiuchumi.

Akitoa ufafanuzi kwa vyombo vya habari vilivyotaka kujua hasa lengo la Kamati hiyo ndogo ya Ardhi Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maeandeleo ya Jamii Julius Mbilinyi amesema kuwa Kamati hii iliundwa ili kufikia Malengo Endelevu na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano kwa kuhakikisha wanawake wanapata fursa ya kumiliki ardhi na kuitumia kujiletea maendeleo.

Aidha Mbilinyi ameongeza kuwa kamati ndogo ya ardhi imejiwekea mikakati ya kuhakikisha wanawake wanaondokana  na  vikwazo vya muda mrefu kama vile mila na desturi ili waweze kutumia fursa ya kumiliki ardhi na kuitumia kujiendeleza kiuchumi na kuwa Sehemu ya uchumi mpana wa Nchi yetu.

‘’Suala kubwa sio umiliki wa ardhi kwa wanawake lakini pia ni kuangalia namna bora wanawake hawa wanaitumia fursa ya mali hisa ya ardhi kujiletea maendeleo ili wawe sehemu ya uchumi mpana wa Taifa letu”. Aliongeza Mbilinyi.

Wakati huohuo Marry Ndalo kutoka Shirika la Kimataifa la Care ameongeza kuwa Kamati hiyo kimsingi inawakutanisha wadau kutoka Mashirika yasiyo ya Kiserikali na kuwaweka pamoja kujadiliana masuala ya ardhi lakini pia kupata taarifa kuhusu idadi ya Wanawake wanaomiliki ardhi na wasio miliki ardhi ili kuweka wanawake katika mjadala wa ardhi ambao inaajiri wanawake wengi.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Patrick Golwike kulia pamoja na Mwakilishi kutoka Shirika la Kimataifa la Care Marry Ndalo wakiwa tayari kwa ufunguzi wa kikao cha Kamati Ndogo ya Ardhi kujadili suala la umiliki wa ardhi kwa wanawake mapema leo Jijini Dodoma.
  Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Julius Mbilinyi kushoto pamoja na Mwakilishi kutoka Shirika la Kimataifa la Care Marry Ndalo wakiwa tayari kwa ufunguzi wa kikao cha Kamati Ndogo ya Ardhi kujadili suala la umiliki wa ardhi kwa wanawake mapema leo Jijini Dodoma.
 Picha ya pamoja ya Kamati ndogo ya Ardhi mara baada  ufunguzi wa kikao cha Kamati Ndogo ya Ardhi kujadili suala la umiliki wa ardhi kwa wanawake kilichofanyika katika ofisi mpya za Wizara ya Afya zilizoko Mtumba Jijini Dodoma.
Baadhi ya Washiriki wa Kamati ndogo ya Ardhi inayokutana leo Jijini Dodoma kujadili suala la umiliki wa ardhi kwa wanawake katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mtumba Jijini Dodoma.

WAKALA WA SERIKALI MTANDAO WAJA NA MFUMO WA KUONGEZA UFANISI SERIKALINI

$
0
0
Na Alex Sonna, Dodoma
WAKALA wa Serikali Mtandao umetengeneza Mfumo Shirikishi wa Kusimamia Shughuli na Rasilimali za Taasisi (ERMS) utakaowezesha kusimamia, kufuatilia, kukagua na tathmini ya utekelezaji wa shughuli zote za umma kwa ufanisi.

Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Tanzania, Dkt Jabiri Bakari wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dodoma amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa matumizi ya tehama katika kuboresha utendajikazi serikalini.

Dkt.Bakari amesema kuwa wameamua kutumia utaalamu wetu wa kidigitali kutengeneza mfumo wa ERMS ambao ni dirisha moja linalounganisha shughuli zote za ndani ya taasisi kuongeza ufanisi katika utendajikazi na utoaji huduma bora kwa umma. Aidha amesema kuwa kuwa mfumo huo utakuwa na moduli 18 zinazounganisha shughuli mbalimbali za utendajikazi zinazotegemeana kuwezesha kubadilisha taarifa miongoni mwa idara na kusimamia rasilimali watu, fedha na vitendea kazi.

Dkt. Bakari amesisitiza kuwa mfumo huo unawezesha ushughulikiaji wa miamala kutoka idara moja hadi nyingine zikiwemo ankara za bidhaa na huduma, mapato na matumizi, ufuatiliaji na utekelezaji wa shughuli kulingana na mipango na bajeti. "Pia utawezesha usimamizi wa majukumu ya watumishi, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi, utekelezaji wa shughuli za manunuzi na utayarishaji wa taarifa mbalimbali za utendaji''amesema Dk.Bakari
Hata hivyo amesema kuwa mfumo huu utawawezesha maofisa masuuli na watumiaji wengine wa mfumo kupata taarifa mbalimbali kulingana na mahitaji yao.

Dkt. Bakari amesema kuwa mfumo huo wa ERMS unaweza kuunganishwa na kubadilishana taarifa na mifumo mingine mikuu ya serikali ikiwemo Mfumo Mkuu wa Uhasibu, Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Rasilimaliwatu (HCMIS), Mfumo wa Malipo ya Serikali Kieletroniki (GePG), Mfumo wa Barua pepe Serikalini (GMS) na Mfumo wa Ofisi Mtandao. Pia amesisitiza kuwa moduli za mfumo huo zinaweza kuongezwa au kupunguzwa bila kuathiri utendaji kazi wa moduli nyingine au mfumo kwa ujumla.

Amezitaja baadhi ya mifumo mingine ambayo wakala umeitengeneza katika utekelezaji wa jitihada za serikali mtandao ambao ni tovuti kuu ya serikali, tovuti kuu ya ajira, mfumo wa barua pepe serikalini ambao unatumiwa na taasisi za umma 402 zikiwemo ofisi za ubalozi nje ya nchi kwa ajili ya kubadilishana taarifa serikalini. Aidha Dkt. Bakari amezitaka taasisi za umma kuendelea kutumia tehama katika kuboresha utendaji kazi serikani na utoaji huduma kwa umma kwa kuzingatia miongozo na viwango vya serikani mtandao.

 Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Tanzania, Dkt. Jabiri Bakari akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuwa Wakala wa Serikali Mtandao iliyotengeneza mfumo wa matumizi ya Tehama katika kuboresha utendaji kazi Serikalini.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia kwa usikivu Taarifa ya Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Tanzania, Dkt. Jabiri Bakari leo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuwa Wakala wa Serikali Mtandao iliiyotengeneza mfumo wa matumizi ya Tehama katika kuboresha utendaji kazi Serikalini.
Sehemu ya wafanyakazi wa Wakala wa Serikali Mtandao wakifuatilia taarifa ambayo ilikuwa inatolewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Tanzania, Dkt. Jabiri Bakari, leo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Mjasiliamali mkazi wa Mbezi mwisho jijini Dar akabidhiwa kitita chake cha milioni kumi kutoka Biko.

MAHAKAMA YAUTAKA UPANDE WA MASHTAKA KUANDAA MASHAHIDI WOTE KWENYE KESI DHIDI YA VIGOGO WA SIMBA

$
0
0
 
 Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka kuhakikisha inaandaa wote wanaotarajiwa kutoa ushahidi wao dhidi ya kesi ya vigogo wa Simba ambayo itasikilizwa kwa siku tatu mfululizo, mwezi ujao.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, Makamu wake, Geofrey Nyange maarufu kwa jina la Kaburu na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Takukuru,Leonard Swai kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini mshtakiww Aveva hayupo.

Hakimu Simba amesema shauri hilo litakapokuja tena mahakamani hapo tunawahitaji mashahidi wote waliobaki kufika kwa ajili ya kutoa ushahid. " Upande wa mashtaka tunategemea mtatuletea mashahidi wote waliobaki ambao nataka watoe ushahidi kwa siku tatu mfululizo,"amesema Simba.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 13 kwa ajili ya kutajwa na itasikilizwa Mei, 15, 16 na 17 mwaka huu.

Katika kesi hiyo Hans Poppe anakabiliwa na mashtaka mawili ya kughushi nyaraka na kuwasilisha nyaraka za uwongo yeye pamoja na wenzake.

Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashtaka mengine zaidi ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kuhamisha fedha hizo bila mamlaka ya Kamati ya Utendaji ya Simba, kujipatia pesa isivyo halali (Aveva) na utakayishaji fedha yanayowakabili wote, Aveva na Kaburu.

Katika maelezo ya awali, washtakiwa hao wanadaiwa kuwa Machi 12, 2016, Klabu ya Simba ililipwa jumla ya Dola za kimarekani 319, 212 na Klabu ya Etoile Sportive Du Sahel ya nchini Tunisia.

Kiasi hicho cha fedha kilikuwa ni ada ya uhamisho wa mchezaji Emmanuel Okwi kwenda Klabu ya Etoile Sportive Du Sahel ya nchini Tunisia.

RAIS DKT. MAGUFULI AENDELEA NA ZIARA YAKE RUNGWE NA KYELA MKOANI MBEYA

$
0
0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia wananchi wa Busokelo wilayani Rungwe katika mkoa  wa Mbeya wakati sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi wa barabara ya

lami ya Katumba-Busokelo-Tukuyu yenye urefu wa Kilometa 81.3 ambapo kilometa 10 kati yake ujenzi umeshakamilika. Pamoja naye ni Mbunge na Waziri Mstaafu Profesa Mark Mwandosya na mkewe Mama Lucy Mwandosya.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Busokelo wilayani Rungwe katika mkoa wa Mbeya wakati sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi wa barabara ya

lami ya Katumba-Busokelo-Tukuyu yenye urefu wa Kilometa 81.3 ambapo kilometa 10 kati yake ujenzi umeshakamilika. Pamoja naye ni Mbunge na Waziri Mstaafu Profesa Mark Mwandosya na mkewe Mama Lucy Mwandosya na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila (kulia).

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisindikizwa na Mbunge na Waziri Mstaafu Profesa Mark Mwandosya na mkewe Mama Lucy Mwandosy baada ya sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi wa barabara ya lami ya Katumba-Busokelo-Tukuyu yenye urefu wa Kilometa 81.3 ambapo kilometa 10 kati yake ujenzi umeshakamilika.
.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi wa barabara ya lami ya Katumba-Busokelo-Tukuyu yenye urefu wa Kilometa
81.3 ambapo kilometa 10 kati yake ujenzi umeshakamilika.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga wananchi  baada ya sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi wa barabara ya lami ya Katumba-Busokelo-Tukuyu yenye urefu wa Kilometa
81.3 ambapo kilometa 10 kati yake ujenzi umeshakamilika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi  eneo la Suma wakati akielekea kuuweka jiwe la msingi wa barabara ya lami ya Katumba-Busokelo-Tukuyu yenye urefu wa

Kilometa 81.3 ambapo kilometa 10 kati yake ujenzi umeshakamilika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifunua pazia akisaidiana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila  kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi wa barabara ya lami ya
Kikusya-Ipinda-Matema yenye urefu wa Kilometa 39.1 ambayo itagharimu shilingi Bilioni 65
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila  baada ya kuweka jiwe la msingi wa barabara ya lami ya Kikusya-Ipinda-Matema
yenye urefu wa Kilometa 39.1 ambayo itagharimu shilingi Bilioni 65
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi wa barabara ya lami ya Kikusya-Ipinda-Matema yenye urefu wa Kilometa 39.1 ambayo itagharimu shilingi Bilioni 65.
.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na  wananchi na kusikiliza kero zao eneo la Tenende, Kyela, baada ya kuweka jiwe la msingi wa barabara ya lami ya Kikusya-Ipinda-Matema yenye urefu wa Kilometa 39.1 ambayo itagharimu shilingi Bilioni 65.



ATE yazindua rasmi tuzo ya Mwajiri Bora kwa mwaka 2019

$
0
0
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) wamezindua rasmi mchakato wa kumtafuta mwajiri bora kwa mwaka 2019 lengo likiwa ni kutambua na kutoa tuzo kwa Waajiri wenye misingi bora ya usimamizi wa nguvu kazi na rasilimali watu ili kuwawezesha kutimiza wajibu wao kwa ajili ya kuongeza uzalishaji kibiashara.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa ATE Dkt. Aggrey Mlimuka alisema kwamba Tuzo ya mwajiri bora wa mwaka (EYA) ni zoezi lililoanzishwa na kuendeshwa kila mwaka na Chama cha Waajiri Tanzania tangu mwaka 2005 ambapo Tuzo za mwaka huu pia zimepanuka sio tu kujali rasilimali watu bali pia kutambua Waajiri wanaofuta taratibu za kitaifa na kimataifa katika uendeshaji wa biashara zao.

“Ushiriki wa Tuzo ya Mwajiri Bora umeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na ukweli kuwa waajiri wengi wamehamasishwa kuthamini watu katika kufanikisha shughuli za biashara kama nyanja muhimu ya usimamizi wa rasilimali watu mahali pa kazi” Alisema Dkt. Mlimuka. 

Akielezea zaidi kuhusu tuzo ya mwaka huu 2019, Dkt. Mlimuka alisema kuwa Kutokana na maoni waliyopokea kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, wadau na wataalamu wetu mbalimbali, tuzo ya mwajiri bora kwa mwaka huu 2019 imekuja na vipengele vipya vitatu (3) na kufanya kuwa na Jumla ya vipele 38 kutoka vipengele 35 vilivyokuwepo awali na.

Dkt Mlimuka amevitaja vipengele vilivyoongezeka kuwa ni Mwajiri Bora anaeendaleza Mafunzo ya Ujuzi wa Kazi kwa wahitimu (Internship),Mwajiri Bora anayetoa mafunzo ya Uanagenzi (Apprentiship) na Mwajiri Bora anayezingatia Haki Rasilimali (Local Content)

“Lengo la kuongeza vipengele hivi ni kuendelea kuziboresha tuzo hii na kuongeza ushindani miongoni mwa washiriki na pia kujaribu kugusa kila eneo ambalo litaleta tija katika ukuzaji na uendelezaji wa rasilimali watu katika maeneo ya kazi.” Alisema Dkt. Mlimuka.

Dkt. Mlimuka aliendelea kwa kusema kuwa Tuzo hizo mpya zitakuwa ni nyongeza ya zile ambazo zimekuwa zikitolewa katika masuala ya utawala na uongozi, ubora katika usimamizi wa rasilimali watu, bidhaa au huduma, uzalishaji na ubunifu, uwajibikaji katika mwenendo wa biashara, utendaji unaokidhi, ushirikishwaji wa mwajiriwa, ukuzaji wa vipaji, mafunzo na maendeleo pamoja na usalama wa mwajiriwa katika mazingira ya kazi. 

Tuzo nyingine ni ile  ya uwiano wa kazi na maisha,  mwajiri bora ni yule anayesimamia vema nguvu kazi inayoonekana kupotea/kupuuzwa, Waajiri bora wenye mikakati inayojali afya za waajiriwa, tuzo ya utofautishwaji na ushirikishwaji yaani (diversity and inclusion), Waajiri bora waonaowachochea na kuwajali waajiriwa wenye ujuzi, Waajiri bora wenye mahusiano mazuri baina ya waajiri na waajiriwa, Waajiri bora wenye majina makubwa na imara huvutia wateja, waajiriwa, wadau na mwajiri bora aliyewekeza kwenye teknolojia.

“Pia tutaendelea kuwa na Tuzo ya Mshindi wa Jumla (Overall) na tuzo kulingana na ukubwa, nazo ni zile zinazohusu tuzo ya waajiri bora katika sekta binafsi, sekta za umma pamoja na mashirika ya ndani ya nchi.” Alielezea Dkt. Mlimuka.

Dkt. Mlimuka pia alitumia siku hiyo kuwaarifu waajiri kuwa kitabu cha Mwongozo wa Misingi Muhimu ya Kusimamia Rasilimali Watu ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka kipo tayari hivyo kuwaomba waajiri wote waweze kujipatia mwongozo huu utakaoelekeza makampuni mambo ya kuzingatia katika usimamizi wa rasilimali watu ili kuongeza tija na kuongeza ushindani.

 Mchakato wa kumpata Mwajiri Bora wa Mwaka huwa na sehemu mbili; sehemu ya kwanza ni ya utafiti itakayopelekea kupata washindi na kwa sasa sehemu hiyo ipo chini ya kampuni binafsi, TanzConsult inayoongozwa na Prof. BAT Kundi na sehemu ya pili ni usimamizi wa matukio mpaka kilele cha sherehe ambacho kimepangwa kufanyika mapema mwezi Desemba 2019.  

Hivi wanachama waajiri watatarifiwa kutembelea tovuti maalumu kwa tuzo hizi www.eya.co.tz kwa ajili ya kujua Zaidi jinsi ya kushiki. Mwaka huu pia tumeamua kuanza mchakato huu mapema Zaidi ili kuwapa Waajiri wengi muda wa kujiandaa.
Mkurugenzi Mtendaji wa ATE Dkt. Aggrey Mlimuka akizungumzia uzinduzi wa mchakato wa kumtafuta mwajiri bora kwa mwaka 2019 lengo likiwa ni kutambua na kutoa tuzo kwa Waajiri wenye misingi bora ya usimamizi wa nguvu kazi na rasilimali watu ili kuwawezesha kutimiza wajibu wao kwa ajili ya kuongeza uzalishaji kibiashara. Kulia ni Msimamizi wa Mchakato huo kutoka Kampuni binafsi ya TanzConsult Prof. BAT Kundi.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU APRIL 29, .2019

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA WAADHIMISHA MIAKA 55 YA MUUNGANO

$
0
0

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akiwahutubia washiriki wa hafla ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyofanyika katika Hoteli ya Leela Palace jijini New Delhi, India tarehe 26 Aprili 2019. Katika hotuba yake, Balozi Luvanda alieleza kuwa, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni wa kihistoria na wa kupigiwa mfano duniani kote. Pia alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na India ambao umedumu kwa miaka 58. 
Mhe. Balozi Luvanda (wa pili kushoto) kwa pamoja na mgeni rasmi Mhe. Shri Sanjiv Arora ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa India anayeshughulikia Masuala ya Kikonseli, Paspoti, Visa na Diaspora wa (kushoto) na wageni waalikwa wakionesha jarida kuhusu miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini India na kuzinduliwa rasmi katika hafla hiyo. 
Mhe. Balozi Luvanda (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mhe. Shri Sanjiv Arora ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa India anayeshughulikia Masuala ya Kikonseli, Pasipoti, Viza na Diaspora wa India wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano. 
Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa nchi mbalimbali walioudhuria hafla ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano. 
Mhe. Balozi Luvanda (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania, New Delhi wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano.

WAZIRI MKUU AZINDUA MAABARA YA TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe wakati alipozindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiweka jiwe la msingi, wakati alipozindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza, katika mkutano wa Pili wa Pamoja wa Mtandao wa Vyombo vya Udhibiti wa Nyuklia kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Aprili 29, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Meneja Muandamizi wa Kituo cha Kimataifa cha Sayansi na Teknolojia na Mshauri wa Masuala ya Kidiplomasia (ISTC), Dkt. Kamen Velichkov, baada ya kufungua mkutano wa Pili wa Pamoja wa Mtandao wa Vyombo vya Udhibiti wa Nyuklia kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Aprili 29, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akioneshwa kifaa cha kupimia mionzi na Mkurugenzi wa Kinga ya Mionzi, Dkt Firm Banzi, baada ya kuzindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimkabidhi cheti na pesa kwa kutambua uaminifu wao kwa Mtafiti wa Mionzi Daraja la Pili, Machibya Matulanya baada ya kuzindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi wa Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU AZINDUA MAABARA YA NYUKLIA

$
0
0

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akitazama vifaa vya kisasa katika maabara ya nyuklia
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akitazama vifaa vya kisasa katika maabara ya nyuklia
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema Akizungumza
Mbunge wa Viti Maalumu Catherine Magige akizungumza

Wananchi wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa maabara
Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi na kamati ya maandalizi
picha ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa pamoja na Wafanyakazi wa Tume ya mionzi.
picha ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa pamoja naViongozi wa Mkoa wa Arusha

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akitazama maabara ya Nyulia iliyozinduliwa katika tume ya Mionzi jijini Arusha.



Na Vero Ignatus, Arusha.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amezindua maabara ya kisasa ya nyuklia iliko katika Time ya Mionzi Tanzania jijini Arusha ambapo maabara hiyo itasaidia kutumia nyuklia kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya taifa.

Majaliwa amesema kuwa maabara hiyo ni muhimu katika kuhakikisha kuwa hakuna madhara yanayotokana na matumizi ya mionzi kwa kuwa na vifaa na wataalamu waliobobea katika mionzi.

Aidha amesema kuwa Tanzania ina hazina ya tank 58.2 za nyuklia katika maeneo mbalimbali ikiwemo Namtumbo,Nachingwea,Minjingu na Songea Vijijini."Maabara hii ya kisasa itasaidia kuongeza mchango wa nyuklia kwenye ustawi wa jamii na maendeleo ya taifa" Alisema Majaliwa

Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Dr.Faustine Ndugulile ambaye alimuwakilisha Waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia amesema kuwa maabara hiyo ya kisasa barani Afrika imejengwa kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Umoja wa nchi za Ulaya na serikali ya Tanzania .

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema maabara hiyo itawawezesha Wataalu kudhibiti mionzi katika maeneo mbalimbali hususan viwanja vya ndege.

Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Atomiki Najat Mohammed ametaja majina ya Wafanyakazi bora ambao wamedhibiti vyanzo vya mionzi katika bidhaa na maeneo ya mipakani licha ya kushawishiwa na rushwa
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live


Latest Images