Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

RC MAKONDA AAGIZA KASI NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KIMAENDELEO KWA WAKATI KINONDONI

$
0
0
* Awalipua wanaotekeleza miradi chini ya viwango na kwa kusuasua

*Amwagiza DC Kinondoni kuhakikisha vibarua wanalipwa stahiki yao bila makato

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo Aprili 15 amefanya ziara yake katika Manispaa ya Kinondoni na kukagua miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa huku akiwataka watendaji kukamilisha miradi hiyo kwa muda muafaka kama ilivyopangwa ili wananchi waweze kunufaika na miradi hiyo.

Akizungumza mara baada ya kutembelea takribani  miradi  tisa Makonda amesema kuwa kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo inaridhisha huku akiwataka wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa soko la kisasa la Magomeni kutokubaliana na mshauri ambaye amekuwa akibadilisha michoro na vipimo hasa kwa kupunguza wakati ujenzi ukiendelea hali inayopelekea majengo kutofaa kwa matumizi ya baadaye.

Ameeleza kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha huduma za muhimu zinapatikana kwa wananchi huku akieleza kuwa ujenzi wa kituo cha afya cha Kigogo kati kitakachokamilika Mei 30 kitapunguza adha kwa wananchi kwa kuwa hadi kukamilika kwake huduma zote zikiwemo za upasuaji zitakuwa zinapatikana na zitahudumia eneo hilo lenye wakazi zaidi ya elfu sabini.

Akiwa katika shule ya sekondari Mzimuni Makonda amekagua mradi wa ujenzi wa madarasa 6 na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo ambapo amewataka kuwa nidhamu, malengo na kusikiliza wanachofundishwa na walimu wao.

Aidha RC Makonda ametembelea ujenzi wa barabara ya barafu Mburahati ambapo ameeleza kutoridhishwa na ujenzi huo ambao upo chini ya kiwango na kuagiza kandarasi inayosimamia ujenzi wa barabara hiyo kufanya kazi usiku na mchana kwa viwango vinavyostahili kabla hajarudi tena kwa ajili ya ukaguzi. Pia amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo kuhakikisha kuwa vibarua wanaofanya kazi katika eneo hilo wanalipwa gharama za shilingi 12,500 kwa siku kama wanavyostahili na hiyo ni baada ya vibarua hao kutoa malalamiko kuhusu malipo yao kwa Rc Makonda.

Katika mradi wa barabara ya Ubungo (Simu 2000) Makonda amesema kuwa ujenzi huo ukamilike kwa wakati huku akieleza fedha za ujenzi wa mita 200 ambazo zimechukuliwa na zitajengwa na Manispaa inayosimamia ujenzi wa Flyover (Ubungo) zikatengeneze barabara ya Shekilango hadi Ubungo Maziwa ili kupunguza adha kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Aidha Makonda ameeleza kufurahishwa na ujenzi wa soko la Sinza, kituo cha afya Msasani, na ujenzi wa kituo cha afya cha Kigogo kati ambacho Manispaa ilijiongeza kwa kununua majengo na kuyakarabati ili waweze kuhudumia afya za wananchi hao.

Katika ziara hiyo Makonda ametembelea na kukagua; ujenzi wa soko la kisasa la Magomeni, ujenzi wa vyumba vya madarasa 6 katika shule ya Sekondari Mzimuni, ujenzi wa kituo cha afya cha Kigogo kati, ujenzi wa barabara ya Barafu Mburahati, ujenzi wa mitaro Tandale, ujenzi wa barabara simu 2000 Ubungo, ujenzi wa soko Sinza, ujenzi wa barabara ya Mabatini pamoja na ujenzi wa kituo cha afya Msasani.

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam iliyoanza Aprili 13 kwa kutembelea Manispaa ya Kigamboni imelenga kukagua miradi yote ambayo inasimamiwa na Serikali na hiyo ni sambamba na kulinganisha taarifa zinazopelekwa ofisini kwake na kile kinachotendeka katika maeneo husika.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikatisha katika barabara ya Barafu Mburahati jijini Dar es salaam wakati akikakugua ujenzi wa barabara hiyo, leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (katikati) akikagua ujenzi wa mtaro katika eneo la Tandale jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake aliyoifanya leo katika Manispaa ya Kinondoni, kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Daniel Chongolo, leo jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikagua ujenzi wa barabara ya Barafu Mburahati ambako ameagiza kasi na viwango vitumike katika ujenzi huo na amemwagiza Mkuu wa Wilaya hiyo Daniel Chongolo kuhakikisha vibarua wanalipwa stahiki yao bila makato yasiyo na msingi, leo jijini Dar es Salaam. 
Muonekano wa jengo la kituo cha afya Msasani, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

UTUMISHI YAANZA KUTOA HUDUMA KATIKA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA

$
0
0
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeanza kutoa huduma katika ofisi zake kwenye Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli kuzindua ofisi za Wizara zilizojengwa katika mji huo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi. 

Akizungumzia kuhusu utoaji wa huduma katika Mji wa Serikali, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amesema, ofisi yake iko tayari na imejipanga kikamilifu kutoa huduma kwa wananchi na wadau wote wa masuala ya kiutumishi na utawala bora.

Dkt. Ndumbaro ametoa wito kwa wananchi, watumishi wa umma na wadau wengine kufuata huduma katika ofisi yake iliyopo Mtumba kwenye Mji wa Serikali na kuongeza kuwa, kwa sasa Idara zilizohamia ni ya Utawala na Utumishi wa Umma na ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu ambazo zina wateja wengi, hivyo watumishi wa umma na wananchi wajitokeze kupata huduma. 

Aidha, Dkt. Ndumbaro amesisitiza kuwa, mwananchi au mtumishi yeyote mwenye uhitaji wa kupata huduma kutoka kwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wafike katika ofisi za Mtumba ili waweze kuhudumiwa ipasavyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 13 Aprili, 2019, alizindua rasmi ofisi za wizara zilizojengwa katika Mji wa Serikali na kuelekeza Watumishi waanze kutoa huduma kwa wananchi mapema iwezekanavyo.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro, akizungumza kuhusu ofisi yake kuanza kutoa huduma kwenye Mji wa Serikali ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wakati akizindua ofisi za Wizara zilizojengwa katika mji huo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro, akifurahia jambo na wasaidizi wake baada ya ofisi yake kuanza kutoa huduma kwenye Mji wa Serikali ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wakati akizindua ofisi za Wizara zilizojengwa katika mji huo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.

TACAIDS kukutana na wadau kujadili maambukizo ya ukimwi kwa vijana wadogo jijini Dar es Salaam.

$
0
0
Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii

KATIKA kuhakikisha nchi inaondokana na Maambukizo mapya ya ukimwi kwa vijana wadogo,Tume ya kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) Imepanga kuwakutanisha wadau mbali mbali nchini kwa lengo kuwasaidia wasichana Balehe ili waweze kujitambua na kujiepusha makundi hatarishi.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uhamishaji na Habari kutoka (TACAIDS) Jummanne Isango wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelezea kongamano la mwaka la wadau wanaotekeleza Afua za kusaidia mabinti wenye Rika Balehe na wanawake vijana.

Isango amesea amesema lengo la mkutano huo imetokana wasichana balehe na wanawake vijana wamekuwa wahanga wakubwa wa athari zinatokana na mdororo wa kijamii na kiuchumi ambazo husababisha kujiingiza katika vitendo vinavyoweza kuhatarisha masuala ya afya.

Hata hivyo.Isango amesema Mkutano huo unaopangwa kufanyika Tarehe 16 April hadi aprili tarehe 17 mwaka huu utafanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mwalimu nyerere (JNICC) jijini Dar es Saalam utajikita kutoa elimu kwa makundi hayo kuwapa utayari wa kupambana na changamoto husika,

Amesema mkutano nl huo ni wa mara ya kwanza kufanyika nchini unatajwa kuwakutanisha wadau mbali mbali wa maendeleo pamoja na asasi za kiraia wanaotekeleza afua mbali mbali za kuwasaidia wasichana hao.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa Tacaids Jumanne Isango akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano wa wadau wa kujadili masuala ya Ukimwi kwa Vijana utaofanyika kesho jijini Dar es Salaam.

WANAWAKE WATAKIWA KUTUMIA FURSA KUJIONGEZEA MASOKO

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Wito umetolewa kwa Wanawake wanaofanya shughuli za uvuvi na kuchakata mazao ya uvuvi kutumia chama chao kuweza kupanua fursa ya masoko baina ya wao kwa wao kutokana na sehemu wanazotoka.

Hayo yamesemwa leo April 15 jijini Dar es Salaam 2019 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Dk .Rashid Tamatama alipokuwa akifungua kikao cha kwanza cha TAWFA Kilichofanyika katika Hotel ya Mbezi Garden Jijini Dar es Salaam.

“TAWFA ni mtandao au chombo kitakachotumika kuwaunganisha kwa pamoja Wanawake wote wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi hapa nchini ,pia kupitia TAWFA,nataraji kwamba wanawake watatoa changamoto na uzoefu wao kwa sauti moja katika shughuli za uvuvi na kuuza mazao ya uvuvi”amesema Dk . Rashid.

Amesema kuwa TAWFA Ndio chombo pekee kutoka Tanzania kitakachokuwa mwanachama katika mtandao wa Africa (Africa Women fish processors and Traders Association-AWFISHNET) Ambao umeunganisha wanawake wote Africa wanaojishughulisha na uchakataji na biashara ya samaki na mazao yake ili wawe na sauti moja katika kushiriki kwenye masuala mbalimbali.

Pia alitoa wito kwa wanawake wote wanaohusika katika mtandao wa TAWFA waweze kushirikiana,kupendana na kusaidiana katika shughuli zenu ili kuwa na uelewano wa kibiashara na kukuza kipato na uchumi kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Dk .Rashid Tamatama akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Chama cha Wanawake wanaojishughulisha na kuchakata mazo ya uvuvi nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Dk .Rashid Tamatama akizungumza na Wanachama wa Chama cha Wanawake wanaojishughulisha kuchakata mazo ya Uvuvi nchini(TAWFA) Wakati wa hafala ya ufunguzi wa Chama hicho Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Emedo akizungumza mbele ya mgeni rasmi kumeuleza mchakato wa kuanzishwa kwa TAWFA
Sehemu ya Wanachama wa TAWFA Walioshiriki uzinduzi wa chama chao jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Dk .Rashid Tamatama akikagua baadhi ya mazo ya uvuvi yalionyeshwa na Wanawake hao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Dk .Rashid Tamatama akikagua baadhi ya mazo ya uvuvi yalionyeshwa na Wanawake hao.
Sehemu ya Wanachama wa TAWFA Walioshiriki uzinduzi wa chama chao jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Dk .Rashid Tamatama akiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa TAWFA.

SERIKALI KUANDAA SHERIA,KANUNI KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI

$
0
0
Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii

WAZIRI wa  Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),Januari Makamba amesema kwamba katazo la kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki nchini litakuwa la kisheria na kanuni zake zitakazokuwa na adhabu kwa wale watakaokiuka.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Makamba pia amesema katika kipindi hichi cha mpito,wizara yake itaweka utaratibu wa mahali pa kuiweka,sehemu ya kuisalimisha na kuiteketeza kwa walio na mifuko hiyo katika magodauni yao kabla haijawa kosa kisheria kwa muda uliowekwa na Serikali.

Kwa kukumbusha tu,mapema wiki iliyopita Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa bungeni Mjini Dododma,alisema kuanzia Juni Mosi mwaka huu, itakuwa ni marufuku kutengeneza, kuuza, kuingiza na kutumia mifuko ya plastiki kwa ajili ya kubebea bidhaa za aina yoyote.

Hivyo Waziri Makamba wakati anazungumza na wadau wa mifuko ya plasiki, kuhusu fursa za uwekezaji katika uzalishaji wa mifuko mbadala ya plastiki amefafanua katazo hilo litakuwa la kisheria na sio tamko.

Ameongeza kuwa katazo hilo  ni kuanzia uzalishaji, kuuza, kuingiza, kumiliki, kuhifadhi kutumia,yote hayo ni makosa.Kanuni hizo watakazoweka zitakuwa na adhabu kwa watakaokiuka hata atakayekutwa naye na kutakuwa na faini au vifungo kwa mujibu wa sheria,kanuni zitakapokamilika zitatangazwa"alisema Makamba

Pia amesema katazo hilo halitausisha vifungashio vya plastiki kwa bidhaa kama Korosho,maziwa, na nyinginezo bali litaanza kwa mifuko ya plastiki inayotumika kubebea bidhaa.

Wakati huo huo Makamba amesema uwamuzi wa katazo hilo si wa gafla kama inavyosemwa na baadhi ya wamiliki wa viwanda vya kutengeneza mifuko ya plastiki kwani inafahamika tangu Agosti mwaka 2016 kwa wadau kuandikiwa barua kujadili  kupiga marufuku mifuko hiyo.

Makamba amesema katazo hilo lina manufaa kwa taifa kàtika kutunza mazingira na kwamba kwa mwaka mifuko bilioni 3 inaishia katika fukwe za mito,bahari na kukaa muda mrefu ikichafua mazingira.
  
Kwaupande wake ,Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda amewataka watakaopewa mamlaka ya kusimakia katazo hilo kutolichukulia kama fursa ya kuomba na kupokea rushwa.

Kwa baadhi ya mawakala na wafanyabiashara wa mifuko ya plastiki kutoka Sokoni Kariakoo wameiomba serikali iwaongezee muda wa kuiuza hadi Januari mwakani, kwani bado ipo mingi na wanadaiwa na wafanyabiashara raia wa china waliowapa.

Hat hivyo,Waziri Mahakama akijibu hoja hiyo,alisisistiza kuwa katazo hilo ni msimamo  wa Serikali na halitarudi nyuma hivyo wakae na waliowauzia kuona kama watawalipa fidia ama la.

WIZARA ZAANZA KUHAMIA MJI WA SERIKALI, IHUMWA

BWAWA LA MINDU: MTIRIRIKO WA MAJI WA UHAKIKA NI MUHIMU

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Tatu ya Maji ya Taifa Prof.Hudson Hamis Ngotagu (mwenye miwani) pamoja na wajumbe wa bodi, na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Maji wakikagua mtiririko wa maji katika kituo cha upimaji cha Mzinga Konga, mkoani Morogoro. Mtiririko wa maji kuelekea katika bwawa la Mindu linalotegemewa kama chanzo cha maji mjini Morogoro umebainika kupungua kwa sababu ya matumizi yasiyofaa ya maji na shughuli nyingine za kibinadamu. 
Hali halisi ya mtiririko wa maji katika kituo cha Mzinga-Konga, vipimo vikionyesha kiwango cha maji yalivyopungua. 
1 Taswira ya hali ya maji katika bwawa la Mindu ambalo ni chanzo cha maji katika mji wa Morogoro. Kiwango cha maji kinachoonekana kinatakiwa kuongezeka kwa mujibu wa wataalam kwa kulinda mtiririko wa maji. Mito inayotiririsha maji katika bwawa la Mindu maji yake yamechepushwa au kubadilishwa mwelekeo kutokana na shughuli za kilimo ikiwamo mto Mlali na mto Mgera. 

VIONGOZI WA DINI NA WAGANGA WA TIBA ASILI NI NGUZO MUHIMU KATIKA KUTOKOMEZA TB NCHINI

$
0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na Wadau wa kupambana dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu katika ufunguzi wa Mkutano wakwanza wa wadau wenye lengo la ushirikiano katika kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu nchini leo kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.(Picha na Emmanuel Masska,MMG)
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi akieleza jambo kuhusu mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu nchini baada ya kupewa fursa ya Kumkaribisha mgeni rasmi, Mhe. Ummy Mwalimu katika ufunguzi wa Mkutano wa kwanza wa wadau wenye lengo la ushirikiano katika kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu nchini ulio fanyika leo kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim (katikati) akiwa na baadhi ya wadau wa masuala ya Kifua Kikuu wakijadi mambo mbalimbali katika ufunguzi wa Mkutano wakwanza wa Wadau wenye lengo la kuimarisha ushirikiano katika kutokomeza ugonjwa huo nchini leo kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wadau wa masuala ya Kifua Kikuu wakifuatilia neno kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Hayupo kwenye picha) katika ufunguzi wa Mkutano wakwanza wa Wadau wenye lengo la kuimarisha ushirikiano katika kutokomeza ugonjwa huo nchini leo kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
Moja ya kikundi ambacho kimekuwa kikishiriki katika kampeni ya kupiga vita ugonjwa wa kifua kikuu kikitumbuiza katika mkutano huo.


Na WAMJW – DSM 

Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa viongozi wa madhehebu ya dini na Waganga wa tiba asili ni nguzo muhimu sana katika kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu(TB) nchini. 

Ameyasema hayo leo katika ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa wadau wenye lengo la ushirikiano katika kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) nchini uliofanyika Jijini Dar es salaam 

Waziri Ummy amesema kuwa Waganga wa Jadi na Viongozi wa Dini ni Wadau muhimu sana katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa TB, huku akidai kutokana na utafiti uliofanywa 2018 na Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua kikuu na Ukoma unaonesha kuwa waganga wa jadi wamekuwa wahanga wakubwa wa ugonjwa wa kifua kikuu. 

Aliendelea kusema kuwa, viongozi wa dini ni kundi lingine muhimu katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuu nchini, hii ni kutokana na idadi kubwa ya waumini wanaowaamini katika kufikisha ujumbe. 

“Waganga wa jadi, ni wadau muhimu sana katika mapambano ya kifua kikuu, utafiti wa 2018 uliofanywa na mpango wa taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma unaonesha kuwa Waganga wa jadi na wenyewe wamekuwa wahanga wa ugonjwa wa kifua kikuu, na viongozi wa dini tunawahitaji wanaposimama katika makanisa na katika misikiti yetu ili wawe wanawakumbusha waumini juu ya ugonjwa wa Kifua Kikuu” alisema Waziri Ummy 

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa 2017, Tanzania iligundua na kuwapatia matibabu takribani wagonjwa 75,000 ikiwa ni sawa na 44% tu ya wagonjwa wanaokadiriwa kuugua TB, hii ina maana ya kuwa wagojwa 85,000 (56%) hawagunduliwi na hivyo kukosa matibabu kila mwaka nchini. 

Pia, Waziri Ummy amesema kuwa TB huathiri takriban watu milioni 10.4 duniani kila mwaka na 25% ya wagonjwa wanatoka barani Afrika. Tanzania ni miongoni mwa nchi 13 barani Afrika zenye kiwango kikubwa cha wagonjwa wa TB na inakadiriwa kuwa na wagonjwa wapya wa TB 154,000 kila mwaka. 

Mbali na hayo, Waziri Ummy amesema kuwa, Wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, imeendelea kutoa huduma za uchunguzi na matibabu bila malipo katika vituo vya kutolea huduma vya serikali na binafsi, hali iliyoleta mafanikio ikiwamo kuvuka malengo ya mwaka 2018 ambapo tuliwafikia wagonjwa 75,845 ikiwa ni sawa ongezeko la asilimia 22 kutoka mwaka 2015. 

Naye, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammad Bakari Kambi amesema kuwa Tanzania ina wastani wa jumla ya Wagonjwa 154,000 ambao wanatakiwa kuibuliwa na kuanzishiwa matibabu, licha ya changamoto ya kutowafikia wote ametoa wito juu ya umuhimu wa ushirikishwaji wa watu na taasisi mbali mbali ili kurahisisha mapambano haya dhidi ya ugonjwa wa TB. 

Kwa upande wake Meneja wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Dkt.Beatrice Mutayoba amesema kuwa kila mwaka watoto 1,000,000 wanaugua kifua kikuu Duniani, huku watoto 250,000 wanafariki. 

“Kwa bahati mbaya Kifua kikuu hakijaacha watoto, kila mwaka watoto 1,000,000 wanaugua kifua kikuu Duniani, huku watoto 250,000 wanafariki, huku nchini Tanzania 10% ya watu 68,000 wanaogundukila kuwa na Kifua kikuu huwa ni watoto” alisema Beatrice Mutayoba 

KANISA MAARUFU DUNIANI LATEKETEA KWA MOTO UFARANSA

$
0
0


Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

KANISA la Notre Dame lililopo Paris nchini Ufaransa likiwa ni  kanisa kubwa na mashuhuri duniani limeteketea kwa moto huku chanzo chako kikiwa hakijafahamika.

Polisi wamewataka raia kutokupita kwenye maeneo ya karibu ili kurahisisha uokoaji unaofanywa na vyombo vya usalama.

Meya wa Parid Anne Hidalgo ameeleza kuwa moto huo ni mkubwa na kuhakikisha kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vipo kazini katika kuzima moto huo.

Rais wa nchi hiyo Macron Emmanuel kupitia mtandao wa twitter ameeleza pia kusikitishwa na ajali hiyo huku akikanusha kuwa tukio hilo lilipangwa.

Kanisa hilo lililojengwa  kuanzia karne ya 13 na kukamilika karne ya 15 na huchukua watu zaidi ya million 13 kwa mwaka na hutembelewa na zaidi ya watu 30000 kwa siku.

VANILA NI DHAHABU YA KIJANI, MKAKATI WA KUKOMESHA WIZI MASHAMBANI WASUKWA WEZI NA WALANGUZI KUKIONA– RC GAGUTI

$
0
0

Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti


Na: Sylvester Raphael

Dhahabu ya kijani (vanilla) Mkoani kagera sasa yawekewa mikakati imara ya kuwanufaisha wakulima na kuinua uchumi wa mkoa badala ya wananchi kutegemea mazao kama ndizi na kahawa tu ambayo yamekuwa yakilimwa kwa mazoea lakini bila kumnufaisha mkulima kulingana na anavyokuwa amewekeza hadi kuuza sokoni.

Mikakati hiyo imefikiwa baada ya Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti kuitikia wito wa wakulima wa mazao ya vanilla, kakao, na chia na kufanya kikao nao katika Shule ya Sekondari KADEA Kanyigo Wilayani Missenyi na kusikia kilio chao cha wizi wa vanilla changa pamoja na marando yake.

Mara baada ya kutembelea na kukagua shamba la vanilla la Mwalimu Jovin Mbanga Mkuu wa Mkoa Gaguti alikutana na wakulima na kusikiliza kilio chao cha wizi wa vanilla changa na marando katika mashamba yao ambapo wizi huo mara baada ya kufanyika vanilla hizo huuzwa nchi jirani ya Uganda.

Wakimweleza Mkuu wa Mkoa wakulima wa vanilla walisema kuwa changamoto kubwa ni wizi wa vanilla ambapo wanalazimika kulala mashambani wakilinda kila siku zisiibiwe. Wizi huo hufanywa na baadhi ya Watanzania wasiokuwa wazalendo wakishirikiana na wafanyabiashara kutoka nje nchi kwa kupewa mitaji ya kununulia vanilla za wizi.

Pia wakulima hao mbale ya Mkuu wa Mkoa walitoa changamoto zao kuwa ni kutokuwa na masoko rasmi ya kuuza vanilla zao mara baada ya kukomaa aidha, wanunuzi wanaojishughulisha na ununuzi wa vanilla kutosajiliwa na kutambulika Kiserikali ili mwananchi akiwa na vanilla zake aweze kuziuza katika soko na kwa mnunuzi maalum.

Baada ya Mkuu wa Mkoa Gaguti kusikiliza kwa makini malalamiko ya wakulima hao alitoa maelekeza mahususi kuhusu zao la vanilla katika Mkoa wa Kagera Kwanza; Aliagiza kuanzia tarehe ya kikao Aprili 15,2019 vanila itakuwa na muda maalum wa kuvunwa mashambani na kutakuwa na vituo maalum kama masoko ya kununulia vanilla hizo ambapo wafanyabiashara ni marufuku kwenda moja kwa moja kwa wakulima.

Akitoa ufafanuzi zaidi Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kwa mwananchi yeyoyote atakayekamatwa na vanilla kabla ya tarehe ya kuvunwa kutangazwa atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi.

Pili; Wakulima wa Vanila wajiunge katika ushirika wa vyama vya msingi ambapo itakuwa rahisi katika kubainisha wezi, kuwa na soko la uhakika lakini pia kuuza vanilla ambazo tayari zimeongezwa thamani ili kupat bei nzuri zaidi na kuweka urahisi zaidi wa Serikali kuwasimamia kama ushirika kuliko mwananchi mmoja mmoja.

Tatu; Wafanyabiashara wote au makampuni yote yanayojihusisha na ununuaji wa vanilla wanatakiwa kujisajili na kupewa leseni ya kununua vanilla kuliko ilivyo sasa. Pia kwa Taasisi au Makampuni ambayo yanatoa ruzuku kwa wakulima wanunue vanilla kwa wakulima kulingana na bei ya soko na si kuwanyonya wakulima.

Aidha, Mkuu wa Mkoa alitoa rai kwa Watendaji wa Vijiji na Kata kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kikamilifu kama wanataka kuendelea kubaki kazini hasa jukumu la ulinzi na usalama kwa mfumo wa Nyumba Kumi Bora za Usalama ambapo wezi wa vanilla watabainika kirahisi kila eneo.

Mkuu wa Mkoa Gaguti pamoja na kufanya kikao na wakulima wa vanilla pia alichoma zana haramu katika mwalo wa Kabindi Kashenye Kanyigo Wilayani Missenyi na kutangaza rasmi kuwa mwaka huu wa 2019 atakikisha anatokomeza magendo yote iwe ya uvuvi, kahawa au vanilla na kuwataka wananchi wanaojishughulisha na biashara hiyo haramu kuacha mara moja.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Denice Mwila aliwataka wananchi wa Missenyi hasa Wakulima wa Vanila Kanyigio kubadilika kwani alisema kuwa wizi mwingine wa vanilla unatokea ndani ya familia na alitoa mfano kwa kusema kuwa unakuta shamba ni la baba na akitoka kwenda pengine Bukoba Mjini kufanya shughuli zake mama au mtoto anavuna vanilla haraha haraka na kuziuza lakini baba akirudi anaambiwa vanilla zimeibwa.

Katika kuchukua hatua kwa baadhi ya watuhumiwa ambao waliwahi kutajwa katika mikutano ya hadhara au kupigiwa kura Mkuu wa Mkoa alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Denice Mwila kuwa watu hao walipoti mara moja ofisini kwake na hatua zianze kuchuuliwa ambapo Mkuu huyo wa Wilaya alitekeleza agizo hilo mara moja kwa kuondoka na Mzee George Lubale aliwahi kutuhumiwa kujihusisha na wizi wa vanilla.

Vanila ni zao ambalo linaonekana kutaka kuukomboa mkoa wa Kagera, zao hili linalimwa katika sehemu yenye kivuli hasa kwenye migomba au kwenye miti na linahitaji mwanga sawa na kivuli asilimia 50% kwa 50%. Vanila inapandwa marando ambapo yanapandwa na kuwekewa mti aina ya jatrofa ili kukua kwa kupanda mti huo na mazao yake ni kama maharage. Bei kwa sasa sokoni tena kwa vanila changa ni kati ya shilingi 20,000/= hadi 30,000/= kwa kilo moja.

Mwaka 2017/18 bei ya vanilla mkoani kagera ilifikia kati ya shilingi 100,000/= hadi 150,000/= na siku za nyuma vanilla iliwahi kuzalishwa Mkoani Kagera hadi kufikia tani 103 lakini kwa sasa zinazalishwa tani 10 hadi 12 ambapo zao hili limekuwa likingiiza zaidi ya shilingi milioni 800,000/= Vanila inastawi au inalimwa na kukomaa kwa miezi tisa tu tayari unavuna na kuuaga umasikini milele badala ya kutegemea zao moja la kahawa.






 

GOLIKIPA ALIYEVUNJIKA MGUU HOROYA APEWA MKATABA MPYA...

$
0
0

Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii 

Golikipa wa Klabu ya Horoya Athlètic Club ya Guinea, Khadim Ndiaye ameongezwa mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo baada kuvunjika vibaya mguu wake katika mtanange wa Robo Fainali ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco. 

Kipa huyo wa Kimataifa wa Senegal aliyecheza michezo yote ya Michuano ya Kombe la Dunia 2018 nchini Russia ameongezwa mkataba huo kutokana na mkataba wake wa awali kumalizika mwaka huu, Horoya imetaka kuwa na Kipa huyo kwa kumpa mkataba leo April 14.

Mmiliki wa timu hiyo, Antonio Souare amehakikisha Ndiaye anakuwa sehemu ya timu hiyo endapo atastaafu kusakata kabumbu na atapata mafunzo ya Ukocha barani Ulaya. 

Kipa huyo alikutwa na mkasa huo baada yakugongana na mwenzake, Boubacar Samassekou kabla hajatolewa nje na machela katika mchezo waliokubali kichapo cha bao 5-0.

Horoya kupitia Mitandao ya Kijamii imethibitisha kuwa Ndiaye anaendelea kupatiwa matibabu katika Hosptitali ya Cheick Zaidi University mjini Rabat nchini Morocco.Imeelezwa kuwa Kipa huyo alikuwa anaipenda timu hiyo ya Horoya kiasi kwamba hata akipewa mkataba na Barcelona angekataa licha 

yakuachwa kwenye Kikosi cha timu ya taifa cha Kocha Aliou Cisse tangu kumalizika kwa Michuano ya Kombe la Dunia 2018.

Ndiaye alianza kucheza Soka katika timu ya Senegal kabla hajaenda kucheza kwa mkopo katika Klabu ya ASC Linguère kabla hajaenda kucheza kwa mkopo nchini Sweden katika Klabu ya Kalmar FF mwaka 2012.

Alirejea nyumbani nakujiunga na timu ya ASC Diaraf yenye Makao Makuu mjini Dakar ambapo alicheza msimu mmoja nakutimkia Horoya AC n November 2013.

Ndiaye amecheza michezo 28 katika Kikosi cha timu ya taifa, amefanikiwa kuiwakilisha nchi hiyo katika Mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2012 na 2017.


CHANZO: BBC



MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRIL 16,2019

SPIKA NDUGAI AFUNGUA KIKAO CHA USALAMA WA CHAKULA NA LISHE JIJINI ARUSHA

$
0
0
 Spika wa Bunge,  Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mwakilishi wa Umoja wa Afrika kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, David Phiri wakati alipowasili kufungua Kikao cha Umoja wa Wabunge wa Afrika ya Mashariki wakuangalia Usalama wa Chakula na Lishe tukio lililofanyika leo katika hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha. Katikati ni Mwakilishi kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Ndg. Fred Kafeero
 Spika wa Bunge, Job Ndugai akiongozana na Mwakilishi kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Fred Kafeero (kulia) wakielekea kwenye Ukumbi wa Mkutano kwa ajili ya mazungumzo kabla ya Spika Ndugai kufungua Kikao cha Umoja wa Wabunge wa Afrika ya Mashariki wakuaangalia Usalama wa Chakula na Lishe tukio lililofanyika leo katika hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (wa pili kulia) akimsikiliza Mwakilishi Umoja wa Afrika kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, Ndg. David Phiri (kulia) wakati akiwa katika chumba cha mapumziko kabla ya kufungua kikao cha Umoja wa Wabunge wa Afrika ya Mashariki wakuangalia Usalama wa Chakula na Lishe kilichofanyika leo katika hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha. Kuanzia kushoto ni Mwakilishi kutoka Umoja wa Afrika Masuala ya Kijamii, Dkt. Margaret Anyetei, Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge wa Afrika ya Mashariki wakuaangalia Usalama wa Chakula na Lishe, Dkt. Abdi Hassan na Mwakilishi kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Fred Kafeero.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza na Wajumbe Umoja wa Wabunge wa Afrika ya Mashariki wakuangalia Usalama wa Chakula na Lishe wakati wa kikao kilichofanyika leo katika hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha.
Wajumbe Umoja wa Wabunge wa Afrika ya Mashariki wakuangalia Usalama wa Chakula na Lishe wakiwa katika kikao kilichofanyika leo katika hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati) katika picha ya pamoja na Wajumbe Umoja wa Wabunge wa Afrika ya Mashariki wakuangalia Usalama wa Chakula na Lishe tukio lililofanyika leo katika hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha. (PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Bungeni jijini Dodoma Aprili 16, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Mikumi Joseph Haule, Bungeni jijini Dodoma Aprili 16, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DC MURO NA KKKT MERU WATOA NG’OMBE 20 KWA WANANCHI

$
0
0
Na Woinde Shizza Globu ya jamii

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro kwa kushirikiana na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Meru Wametoa ng'ombe 20 kwa watu waishio katika mazingira magumu.

Wakikabidhi ng'ombe hizo Askofu wa dayosisi hiyo Elias Kitoipamoja na mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro wamesema Kanisa pamoja na Serikali wanashirikianapamoja na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha wanasaidia wananchi kiroho na kimwili katika kuleta maendeleo yanayolenga kuwaondolea umasikini wananchi.
"Fedha za kununua Ng'ombe hizi zilipatakana kwa shida sana kutoka kwa wadau walioko Marekani , kufuatia mahusiano mazuri kati ya kanisa , serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ya utoaji wa ng'ombe 20 wenye thamani ya zaidi ya milioni 20 alisema

Askofu Kitoi Alisema kama dayosisi ya Meru hawakuliangalia jambo hilo kibinadamu zaidi walimuomba Mungu ili waweze kufikisha mradi huo sehemu husika ambapo walishirikiana na wakuu wa majimbo, wachungaji pamoja na wainjilisti ili kuwapata wale wahitaji katika sharika zao jambo alilosema limefanyika kwa uaminifu.

Aliongeza kwa kuwataka waliopewa ng'ombe hizo kuwa mawakili wema ili kuwasaidia na wahitaji wengine pindi zinapozaliana huku akisema kuwa wamepatiwa bure bila malipo yoyote isipokuwa katika kila uzao wa kwanza kwa kila ng'ombe atapelekwa Kanisani.

"Tunatamani muendeleze mradi huu ili wengine wanufaike tumeweka utaratibu kuwa kila Mzaliwa wa kwanza wa ndama jike atapelekwa Kanisani ili apatiwe muhitaji mwingine lakini mzaliwa wa kwanza dume ataletwa kanisani kama Limbuko na hii itakuwa manufaa kwa usharika husika"alisema Askofu.

katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Cornel Muro alisema anatambua mchango mkubwa wa Kanisa katika wananchi wa Arumeru ambapo hapo awali walishakabidhi mbuzi kwa wananchi hao

Aidha Muro aliwataka wanufaika wa mradi huo kutumia fursa hiyo kikamilifu lengo likiwa ni kutokomeza umaskini katika Jamii ambapo alisema yeyote atakayeshindwa kutunza ng'ombe hao ni vema akarudisha Katika Usharika wake ili apatiwe mtu mwingine ambaye ni muhitaji .

"Nitoe rai kwa wote mliopatiwa zawadi hii kama mkishindwa kuwatunza ng'ombe hawa warudisheni Kanisani ili wapatiwe wengine wenye uhitaji zaidi na watakaothamini hili"Alisema Muro

Mkuu huyo wa Wilaya aliahidi kutoa ufadhili wa kuchanja ng'ombe wote kama mchango wake na kuunga mkono juhudi za Dayosisi hiyo ambapo alisema pia atawaunganisha na Afisa mifugo wa Halmashauri ya Meruili ng'ombe hao wapatiwe huduma stahiki.

Picha ikionyesha Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akishirikiana na mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Meru Elias katoi wakitoa ng'ombe 20 kwa familia zisizojiweza. 


Ajiuwa kwa kujichinja chinja

$
0
0
Na Woinde Shizza globu ya jamii

MTU mmoja alietambulika kwa jina la Lazaro Keorori (53) mkazi mtaa Wa Simanjiro Kata ya Sombetini amefariki dunia Mara baada ya kujichinja chinja na kisu kikali.

Akizungumza na waandishi Wa habari kamanda Wa polisi mkoa Wa Arusha Jonathan Shana alisema kuwa tukio hilo limetokea aprili 15 majira Saa moja asubui . 

Alibanisha kuwa uchunguzi ulifanywa na jeshi la polisi umebaini kuwa marehemu amechukuwa uwamuzi huo kutokana na mgogoro Wa kifamilia uliokuwepo kati yake nawake zake wawili .

"Marehemu alikuwa na msongo Wa mawazo uliompelekea yeye kuamua kuchukuwa uamuzi Wa kujiuwa ,na kwamaelezo ya watu waliohojiwa walisema aliingia ndani usiku akachukuwa kisu kidogo chenye makali akaanza kujichinja sasa ,pamoja alikuwa chumbani watu waligundua Saa ile ambapo roho ilikuwa inataka kutoka akawa anapiga kelele ndio watu wakamjua ila haikuwezekana kumuokoa roho take" alisema kamanda

Aidha aliwaasa wananchi haswa wanafamilia wakiwemo wanaume kutochukuwa maamuzi ya haraka haraka na kuwasihi iwapo wakipata msongo Wa mawazo ni vizuri wakaenda kupewa ushauri katika nyumba za ibada au katika familia na sio kujichukulia sheria mkononi.

Wakati huo huo jeshi la polisi linawashikilia watu Tisa kwa makosa ya kuwatapeli watu Aridhi.Kamanda Wa polisi amesema kuwa sasa ivi mkoa Wa Arusha umegubikwa na wimbi la matapeli ambapo wanajidai wao ni maafisa ardhi ,huku wengine wakijifanya ni matajiri wanunuaji huku wengine wakijidai ni wenye mashamba .

Aisha alibainisha kuwa jeshi la polisi limefanya operation na kuwakamata watu Tisa ambapo kati yao wawili ni wafanyakazi Wa halmashauri ya jiji la Arusha ,huku wawili wakiwa ni wafanyakazi Wa ofisi ya Aridhi Kanda ya kaskazini na wengine sita waliobaki ni wananchi Wa kawaida.

Kamanda alisema kuwa watu hao watafikishwa mahakamani pindi tu upelelezi utakapo kamilika ,pia alitoa wito kwa wananchi kufuata sheria na kufanya uchunguzi kabla ya kununua au kuuza nyumba au kiwanja.

Picha kamanda Wa polisi mkoa Wa Arusha Jonathan Shana akionyesha waandishi Wa habari kisu ambacho marehemu Lazaro Keurori alitumia kuji chinjia chinjia .

OFISI YA WAZIRI MKUU YAHAMIA RASMI MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Maimuna Tarishi akiwa anatekeleza majukumu yake katika Ofisi yake Mpya iliyopo katika Mji wa Serikali Kata ya Mtumba, Jijini Dodoma ikiwa ni kutekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alilotoa tarehe 13 Aprili, 2019.
 Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge)  Maimuna Tarishi akizungumza na baadhi Wakuu wa Idara na Vitengo wakati alipofanya kikao cha kuwakaribisha katika ofisi zao mpya zilizopo katika Mji wa Serikali Aprili 15, 2019.
 Mkurugenzi wa Uwekezaji, Bw. Joseph Mramba (katikati) akieleza jambo kwa Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Maimuna (hayupo pichani) juu ya utayari wa kutekeleza majukumu yao wakati wa kikao hicho kilichofanyika Aprili 15, 2019 katika Mji wa Serikali, Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Maimuna Tarishi akiwaonesha baadhi ya Watumishi wa Ofisi yake (hawapo pichani) namna Mji wa Serikali ulivyo walipofanya ziara ya kuzunguka kujua maeneo mbalimbali ya Wizara na huduma zilizopo katika Mji huo.
 Afisa Mipango Miji wa Jiji la Dodoma, Bw. William Alfayo (wa tatu kutoka kulia) akiwaonesha baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waliombatana na Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Maimuna Tarishi (wa pili kutoka kushoto) maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Balozi katika Mji huo.
 Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Maimuna Tarishi akiwaeleza jambo Watumishi wa Ofisi yake kuhusu Miundombinu, huduma na mahitaji mbalimbali yatakayokuwa yanapatikana katika Mji huo wa Serikali uliopo Kata ya Mtumba, Jijini Dodoma. (Kushoto) ni Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe. 
 Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Madini, Bw. Msajigwa Kabigi (wa pili kutoka kulia) akimpa taarifa Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Maimuna Tarishi (katikati) juu ya zoezi la kuamishia ofisi zao rasmi katika Mji huo wa Serikali uliopo Kata ya Mtumba, Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Maimuna Tarishi akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Naibu waziri wa Madini iliyopo katika Mji wa Serikali alipotembelea Wizara hiyo ambayo tayari imekwisha hamia Mji wa Serikali.
 Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Maimuna Tarishi akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Ofisi yake baada ya kumaliza majukumu yao kwa siku ya kwanza katika Ofisi zao mpya zilizopo katika Mji wa Serikali.
Muonekano wa jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) iliyopo katika Mji wa Serikali uliopo Kata ya Mtumba, Jijini Dodoma.

Elimu ya fedha, taarifa za mikopo ni muhimu-Gavana Luoga

$
0
0
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga, amesema elimu kuhusu masuala ya fedha ni muhimu katika mfumo mzima wa taarifa za mikopo ili kuwawezesha Watanzania kupanga matumizi bora ya mikopo.

Prof Luoga alitoa kauli hiyo katika uzinduzi wa kampeni ya uelimishaji umma kuhusu taarifa za mikopo na fedha iliyoratibiwa na BOT kwa kushirikiana na taasisi ya International Finance Corporation ambayo ni mwanachama wa Kundi la Benki ya Dunia.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mpango, Dk. Philip Mpango, Prof Luoga alisema taarifa za mikopo na elimu ya fedha ni muhimu ili kuhakikisha Watanzania wanaondokana na matumizi ya anasa ya mikopo.

“Kampeni hii ya elimu kwa umma inalenga kuwaelimisha watumiaji wa huduma za fedha na wadau wengine kukuza uelewa wao kuhusu taarifa za mikopo ili kuongeza ushiriki katika matumizi ya taarifa za mikopo hapa nchini,” alisema.

Aidha, Meneja Msaidizi, Mfumo wa Kumbukumbu za Wakopaji kutoka BoT, Nkanwa Magina alisema kampeni hiyo ya miezi mitatu inalenga kuongeza uelewa, mwamko kuhusu taarifa za mikopo na kukuza upatikanaji wa mikopo.

”Kauli mbiu katika kampeni hiyo ni: “Pata Taarifa Yako ya Mikopo Leo. Angalia hali yako ya kifedha ili kupanga mustakabali wako bora wa kesho” inaungwa mkono na wadau mbalimbali katika sekta ya huduma za fedha.

“Wadau hao wameahidi kusaidia kusambaza ujumbe kuhusu umuhimu wa upatikanaji wa mikopo na jinsi Watanzania wanavyoweza kuishi maisha bora kwa kuweza kupata taarifa za mikopo yao na kujua historia ya mikopo yao,” alisema.

Alisema usimamizi mzuri wa mikopo na historia nzuri ya mikopo ni muhimu katika kuwezesha kupata mkopo nafuu."Kuhakiki taarifa yako ya mikopo mara moja kwa mwaka ni huduma inayopatikana bila malipo, tena itakuletea mafanikio kwa kukuandaa vema utakapoenda kuomba mkopo. 

"Historia nzuri ya mikopo inaweza kusaidia kustahili viwango vya chini vya riba na ada, hivyo kuondokana na kutenga fedha kwa ajili ya dharura na gharama zisizotarajiwa," alisema. 

Alisema mikopo inasaidia kupata mahitaji ya sasa, kama vile nyumba au ada ya shule ya mtoto wako, kwa kuzingatia ahadi yako ya kulipa kwa awamu na kwa muda uliopangwa.Aidha, Meneja wa IFC - Tanzania, Manuel Moses alisema taarifa ya mikopo inaonesha taarifa binafsi; utambulisho na taarifa ya mawasiliano na ikiwezekana historia ya ajira; idadi na aina za akaunti za mikopo.

Naye Meneja Maendeleo ya Biashara kutoka Dun & Bradstreet, Josephine Temu alisema kwa sasa, kuna taasisi mbili zilizopatiwa leseni na Benki Kuu ya Tanzania kuandaa na kutoa taarifa za mikopo hapa Tanzania ambazo ni Creditinfo Tanzania Limited na Dun & Bradstreet.Alisema taasisi hizo zinakusanya na kutunza taarifa za mikopo na kutoa taarifa za mikopo kwa kampuni au watu wanaozihitaji kama vile benki. 

Alisema ripoti hiyo ya mikopo inaweza kutolewa na taasisi hizo (Creditinfo na Dun & Bradstreet) mara moja kwa mwaka bila malipo.“Ili kupata taarifa ya mikopo unatakiwa kuwasilisha nakala ya kitambulisho chako cha taifa au kingine kama leseni ya udereva, hati ya kusafiria. Jaza na wasilisha fomu ya maombi ya taarifa yako ya mikopo katika taasisi zinazoandaa taarifa za mikopo ambazo kwa sasa ni Creditinfo au Dun & Bradstreet," alisema.

Akifafanua kuhusu mambo muhimu ya kuangalia kwenye taarifa ya mikopo, Meneja Maendeleo ya Biashara kutoka Creditinfo, Tonny Missokia alisema muhimu ni taarifa binafsi kama vile jina, hadhi ya ndoa, anwani, taarifa za ajira na namba za mawasiliano ni sahihi.

VODACOM YAZINDUA DUKA LAKE MASAKI JIJINI DAR

$
0
0
 Mkuu wa Bidhaa wa Vodacom, Linda Riwa  (wapili kulia) na Devota Kijogoo (kulia) wakifurahia katika hafla ya uzinduzi wa duka la Vodacom Masaki, mapema leo. Kampuni hiyo inaendelea kutanua apatikananji wa huduma zake ili kuhakikisha kwamba wateja wake wanapata huduma bora.
 Mkuu wa Bidhaa wa Vodacom, Linda Riwa  (wapili kulia) na Devota Kijogoo (kulia) wakikata utepe kuzindua duka la Vodacom Masaki mapema leo. Kampuni hiyo inaendelea kutanua apatikananji wa huduma zake ili kuhakikisha kwamba wateja wake wanapata huduma bora. 
Mkuu wa Bidhaa wa Vodacom, Linda Riwa  (watatu kulia) na Devota Kijogoo ( wapili kulia) wakikata keki katika hafla ya uzinduzi wa duka la Vodacom Masaki. Kampuni hiyo inaendelea kutanua apatikananji wa huduma zake ili kuhakikisha kwamba wateja wake wanapata huduma bora.  

WATEJA WA TIGO MIKOA YA MBEYA NA IRINGA KUFANYA MALIPO KWA KUTUMIA MFUMO WA KIELETRONIKI WA MALIPO SERIKALINI (GePG)

$
0
0
Mkuu wa Mauzo wa Tigo kwa mikoa ya Mbeya na Rukwa Ladislaus Karlo (wa kwanza kushoto) akiwaonyesha waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi wa Mfumo wa Kielekroniki wa Malipo Serikalini (GePG) kwa mkoa wa Mbeya namna mteja anavyoweza kutumia simu yake kufanya malipo. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Malipo ya Biashara kwa Tigo Pesa wa Tigo Dennis Sakia na anayefuatia ni Afisa Uhusiano Msaidizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa mazingira Mbeya, Kadri Makongwa.
Afisa Uhusiano Msaidizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa mazingira Mbeya, Kadri Makongwa (kati kati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kielekroniki wa Malipo Serikalini (GePG) kwa mkoa wa Mbeya. Kulia ni Meneja wa Malipo ya Biashara kwa Tigo Pesa wa Tigo Dennis Sakia na kushoto ni . Mkuu wa Mauzo wa Tigo kwa mikoa ya Mbeya na Rukwa Ladislaus Karlo.
Waandishi wa habari wakimskiliza Mkuu wa Mauzo wa Tigo kwa mikoa ya Mbeya na Rukwa Ladislaus Karlo (wa kwanza kushoto) wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kielekroniki wa Malipo Serikalini (GePG) jijini Mbeya. Wa kwanza kulia ni . Meneja wa Malipo ya Biashara kwa Tigo Pesa wa Tigo Dennis Sakia na anayefuatia ni Afisa Uhusiano Msaidizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya, Kadri Makongwa,



Fanya malipo ya haraka, urahisi na kwa usalama kwa zaidi ya idara 300 za Serikali, mawakala na mamlaka mbali mbali kupitia Tigo Pesa

Wateja wa Kampuni ya Tigo wa mikoa ya Mbeya na Iringa sasa wanaweza kufanya malipo kutumia mfumo wa Kielektroniki wa Malipo Serikalini (GePG) baada ya kampuni hiyo kuongeza malipo ya Serikalini kwenye App yake ya Tigo Pesa.

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya (WSSA) Afisa Uhusiano Msaidizi wa WSSA Mbeya Kadri Makongwa, alisema mfumo wa GePG umerahisisha upatikanaji wa ankara na kufanya malipo kwa wananchi na kuongeza kuwa umeleta faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuboresha uwekaji wa kumbukumbu, utoaji wa taarifa, kupunguza ubadhirifu na kuongeza mapato kwa idara mbali mbali na taasisi za Serikali 

“Mfumo wa GePG, pia imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza fursa za biashara kwa kampuni zinazotoa huduma za malipo kama Tigo. Wananchi wanaweza kupokea ankara zao moja kwa moja kutoka ofisi na mashirika ya Serikali ikiwa ni pamoja na za kutoka (WSSA) 

Malipo pia yanaweza kufanyika kwa njia mbali mbali za kimtandao, na kufurahisi na mahali popote kwa njia ya simu za kiganjani, benki au kwa njia ya mtandao.,” alisema 

“Kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi wengi ni moja kati ya malengo mkakati yetu,” alisema Makongwa 

Kwa upande wake Mkuu wa Mauzo wa Tigo kwa Mbeya na Rukwa Ladislaus Karlo alisema “Zaidi ya wateja milioni 7 wanaotumia huduma yetu ya Tigo Pesa sasa wana uwezo zaidi wa kufanya malipo kwa haraka kwenda kwa taasisi, Wizara na wakala wa Serikali zaidi ya 300 kupitia Tigo Pesa USSD, Tigo Pesa App na QR Code,” 

Baadhi ya taasisi za Serikali ambazo malipo yanaweza kufanywa kwa Tigo Pesa ni pamoja na Wizara ya Ardhi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka za Miji, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mamlaka ya Misitu (TFS), Wizara ya Utalii, Bodi ya Utalii, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka za Maji katika miji ya Mwanza (MWAUWASA), Tanga (Tanga UWASA), Dar es Salaam (DAWASA), Dodoma (DUWASA), Hospitali mbali mbali kama vile Muhimbili, Mwananyamala na idara nyingine zaidi ya 300. 

Ili kufanya malipo kwa kutumia Tigo Pesa App na QR Code, wateja wa Tigo wanahitaji kupakua App ya Tigo Pesa na kuscan QR code kisha kuingiza namba ya siri ili kufanikisha muamala.

Ili kufanya malipo kwa kutumia menu ya Tigo Pesa, mteja anatakiwa kufuata hatua zifuatazo;. 

1) Kupiga *150*01# kisha kuchagua Lipa Bili
2) Kuchagua namba 5 (Malipo ya Serikali)
3) Kuingiza tarakimu 12 za mamlaka au taasisi anayotaka ipokee malipo 
4) Kuingiza kiasi cha fedha anachotaka kulipa
5) Kuingiza namba ya siri kwa ajili ya kuruhusu malipo

Kwa upande mwingine, wateja wanaweza kutumia App ya Tigo Pesa ambayo inarahisisha ufanyaji wa malipo kwa kiasi kikubwa.

Baada ya kukamilisha malipo, wateja wa Tigo watapokea risiti ya kielektoniki kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi unaothibitisha kuwa muamala umefanyika kikamilifu. Risiti hiyo ya kielektroniki inakubalika kama uthibitisho tosha wa malipo na inaweza kusaidia kurahisisha kufuatilia malipo kwa kuwa ni rahisi kuhifadhi na kuipata pale inapohitajika ukilinganisha na risiti za karatasi ambazo ni rahisi kupotea au kuharibika.

Tigo inawakaribisha wateja wake kuanza kutumia huduma hii ya Malipo ya Kieletroniki Serikalini (GepG) sasa. 
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images