Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

UIMARISHAJI MPAKA WA TANZANIA NA KENYA WAENDELEA KWA KASI

0
0






Na Munir Shemweta, NGORONGORO

Kazi ya uimarishaji mpaka wa Tanzania na Kenya kuanzia eneo la Ziwa Natroni katika wilaya ya Ngorongoro hadi Namanga wilaya ya Longido mkoani Arusha inaendelea kwa kasi kubwa na sasa ukaguzi kwa ajili ya kuimarisha mpaka huo umekamilika.

Ukaguzi wa mpaka katika eneo hilo unafuatia kukamilika zoezi la uimarishaji mpaka kwa kuweka alama za mipaka ya nchi hizo mbili kuanzia Ziwa Victoria mkoani Mara hadi Natron wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha kwa umbali wa kilomita 238.

Tayari timu za wataalamu kutoka nchi za Tanzania na Kenya zimefanya ukaguzi eneo la mpaka kuanzia eneo la Natroni wilaya ya Ngorongoro hadi Namanga wilaya ya Longido ambapo timu hizo zimeainisha mahitaji ya uimarishaji mpaka huo na kilichobaki ni uwasilishaji ripoti.

Kaimu Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Samuel Katambi mwishoni mwa wiki alitembelea mpaka wa nchi za Tanzania na Kenya kijiji cha Engoserosambu, eneo karibu na Ziwa Natron la cha Nani katika wilaya ya Ngorongoro pamoja na Namanga wilaya ya Longido mkoani Arusha kwa ajili ya kujionea kazi ya ukaguzi iliyofanyika ikiwa ni maandalizi ya uimarishaji mpaka.

Katika ziara hiyo Katambi alijionea jinsi wataalamu wa nchi mbili za Tanzania na Kenya walivyoshiriki katika kazi ya ukaguzi kwa nia ya kuanisha mahitaji ya uimarishaji mpaka kwa kuwekaji alama kwenye maeneo ambayo vigingi vya mipaka vimeharibika ili kupata picha halisi kwa ajili ya kuhuisha mpaka huo.

Kwa mujibu wa Katambi, ukaguzi wa mpaka wa Tanzania na Kenya katika eneo la kuanzia Natroni hadi Namanga ni matokeo ya mkutano wa Narok uliofanyika nchini Kenya ambapo nchi husika zilikubalina kabla ya kuanza kazi ya kuimarisha mpaka zifanye ukaguzi ili kujua mahitaji halisi wakati wa kuimarisha mpaka.

‘’Ukaguzi ni muhimu sana ili kuwa na bajeti halisi ya kazi, kufahamu ni vigingi vingapi vinahitajika kuongezwa na umbali wa kuweka vigingi hivyo sambamba na njia za kupitisha vifaa wakati wa ujenzi wake’’ alisema Katambi

Kaimu Mkurugenzi huyo wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi alisema, zoezi hilo la uimarishaji mpaka wa Tanzania na Kenya litakapokamilika litaendelea maeneo mengine kutoka Namanga kuelekea mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Tarakea mkoani Kilimanjaro, Hororo hadi kijiji cha Jasini kilichopo wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga na hivyo kukamilisha uimarishaji mpaka huo wenye urefu wa kilomita 760 kutoka Ziwa Victoria hadi Jasini.

Mkuu wa Kikosi Kazi cha Ukaguzi Uimarishaji Mpaka wa Tanzania na Kenya kwa upande wa Tanzania Joseph Ikorongo kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, zoezi la ukaguzi kwa ajili ya maandalizi ya uimarishaji mpaka wa nchi hizo mbili eneo la Ziwa Natron hadi Namanga limeenda vizuri na jumla ya kilomita 128 zimeshakaguliwa na lengo la ukaguzi huo ni kuandaa taarifa ya kina itakayowezesha kuwa na mpango kazi halisi.

Kwa mujibu wa Ikorongo, ukaguzi huo umehusisha kipande cha eneo ambalo halijawahi kuwekewa alama tangu enzi za ukoloni la Ziwa Natroni kati ya kijiji cha Nani na Jema lenye urefu wa kilomita 20 na eneo la kilomita 110 lilokuwa na alama kati ya kilomita moja hadi mbili.

Mkuu huyo wa Kikosi kazi cha Ukaguzi wa mpaka kwa upande wa Tanzania alibainisha kuwa, katika ukaguzi huo, kikosi kazi kimebaini jumla ya alama 47 zikiwa imara huku alama 11 zikihitaji kujengwa upya na alama 3 zikihitaji marekebisho. Ikorongo alisema, eneo la mpaka kuanzia Ziwa Victoria mkoani Mara hadi Jasini mkoa wa Tanga lenye urefu wa kilomita 760 ndiyo eneo refu la mpaka ukilinganisha maeneo mengine ya mipaka ya Tanzania na nchi jirani
 Kaimu Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Samuel Katambi akitoa maelekezo kwa timu ya ukaguzi wa Tanzania na Kenya katika eneo la Namanga mkoani Arusha kuhusiana na kigingi cha mpaka kilichoanguka eneo la Namanga baada ya kutembelea kuona ukaguzi kwa ajili ya maandalizi ya kuimarisha mpaka wa nchi hizo kutoka eneo la Ziwa na Natron hadi Namanga. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Ukaguzi kwa upande wa Tanzania kutoka Wizara ya Ardhi Joseph Ikorongo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Samuel Katambi akiangalia moja ya kigingi cha mpaka kilichowekwa katika mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la kijiji cha Engoserosambu wilaya ya Ngorongoro wakati alipotembelea kuona ukaguzi kwa ajili ya maandalizi ya kuimarisha mpaka wa nchi hizo kutoka eneo la Natron hadi Namanga. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Ukaguzi upande wa Tanzania kutoka Wizara ya Ardhi Joseph Ikorongo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Samuel Katambi (Kulia) akielekea kuangalia moja ya alama za mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la kijiji cha Engoserosambu wilayani Ngorongoro wakati alipotembelea kuona ukaguzi kwa ajili ya maandalizi ya uimarishaji mpaka wa nchi hizo kutoka eneo la Ziwa Natron hadi Namanga. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Ukaguzi kwa upande wa Tanzania kutoka Wizara ya Ardhi Joseph Ikorongo.
 Mkuu wa Kikosi cha Ukaguzi wa mpaka wa Tanzania na Kenya kwa upande wa Tanzania kutoka Wizara ya Ardhi Joseph Ikorongo akimuonesha Kaimu Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Samuel Katambi (Wa pili Kulia) muelekeo wa alama ya mpaka kati ya nchi hizo eneo la Namanga mkoani Arusha wakati alipotembelea kuona ukaguzi kwa ajili ya maandalizi ya uimarishaji mpaka wa nchi hizo kutoka eneo la Ziwa na Natron hadi Namanga.
 Mkuu wa Kikosi cha Ukaguzi kwa upande wa Tanzania kutoka Wizara ya Ardhi Joseph Ikorongo (Wa pili Kulia) akimuonesha Kaimu Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Samuel Katambi (Wa pili Kushoto) muelekeo wa alama ya mpaka kati ya Tanzania na Kenya katika kijiji cha Engoserosambu Loliondo wilaya ya Ngorongoro mkoa wa Arusha wakati alipotembelea kuona ukaguzi kwa ajili ya maandalizi ya uimarishaji mpaka wa nchi hizo kutoka eneo la Ziwa na Natron hadi Namanga.
 Kaimu Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Samuel Katambi akioneshwa eneo unapopita mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Namanga mkoani Arusha na Afisa aliyeshiriki ukaguzi wa mpaka huo kutoka Wizara ya Ardhi John Solwa wakati alipotembelea kuona ukaguzi kwa ajili ya maandalizi ya uimarishaji mpaka wa nchi hizo kutoka eneo la Ziwa na Natron hadi Namanga. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Ukaguzi kwa upande wa Tanzania kutoka Wizara ya Ardhi Joseph Ikorongo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Samuel Katambi akiangalia kigingi cha mpaka kati ya Tanzania na Kenya kilichoanguka katika eneo la Namanga mkoani Arusha baada ya kutembelea kuona ukaguzi kwa ajili ya maandalizi ya uimarishaji mpaka wa nchi hizo kutoka eneo la Ziwa na Natron hadi Namanga. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Ukaguzi kwa upande wa Tanzania kutoka Wizara ya Ardhi Joseph Ikorongo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Samuel Katambi (wa sita waliosimama) akiwa katika picha ya pamoja na kikosi kazi kilichoshiriki kazi ya ukaguzi mpaka wa Tanzania na Kenya baada ya kutembelea kuona ukaguzi kwa ajili ya maandalizi ya uimarishaji  mpaka wa nchi hizo kutoka eneo la Ziwa na Natron hadi Namanga. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Ukaguzi kwa upande wa Tanzania kutoka Wizara ya Ardhi Joseph Ikorongo. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA-WIZARA YA ARDHI)


BALOZI WA MISITU NCHINI ATUMA SALAMU KWA VIJANA KUTAMBUA THAMANI YA MISITU...TFS NAO WAGUSIA MAPAFU YA DAR ES SALAAM YANAVYOHARIBIWA

0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BALOZI wa Misitu nchini ambaye pia ni Miss Tanzania namba mbili Nelly Kazikazi amewashauri Watanzania wote nchini na hasa vijana kushiriki kikamilifu katika kutunza misitu iliyopo nchini huku akisisitiza kuna kila sababu ya kuwa na utaratibu kwa kila mmoja wetu kupanda miti.

Wakati Balozi wa Misitu akihamasisha upandaji miti, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umesisitiza kuendelea na mkakati wake wa kuhakikisha inarejesha misitu ya asili katika maeneo ambayo imeharibiwa kwa kupanda miti ya asili kadri inavyowezekana ukiwemo Msitu wa Pugu ambao ndio mapafu ya Jiji la Dar es Salaam.

Hayo yameelezwa jana kwa nyakati tofauti baada ya kupandwa kwa miti zaidi ya 300 ya asili aina ya Mkakangazi katika Msitu wa Pugu mkoani Pwani. Wakati wa upandaji huo wa miti mbali ya kuwepo kwa maofisa wa TFS na Balozi wa Misitu, pia walikuwepo wadau wengine ambao ni wanafunzi wa Shule ya IST ya jijini Dar es Saalam.

Akizungumzia umuhimu wa kupanda miti, Balozi wa Misitu Nelly Kazikazi amesema vijana wanapaswa kutambua thamani ya misitu nchini na kuhakikisha wanashiriki kuilinda na kwamba wasidharau misitu kwani faifa zake nyingi na hivyo ni vema wakahamasika kuingeza badala ya kuipunguza.

"Nawahamasisha vijana wenzangu tuongeze namba ya misitu, tuwe na uaminifu kwa kupanda miti kadri tunavyoweza.Nafahamu wapo wanaokata miti kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya kibadamu lakini ni vema sote kwa umoja wetu tukapanda miti.

"Tunahitaji hewa safi ambayo inatokana na miti.Tunahitaji kivuli na kubwa zaidi misitu ule ukijani wake unaleta faraja kwa maisha ya binadamu,"amesema Nelly na kuongeza kwa kuwa mbali ya kuwa balozi wa misitu ni mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM), hivyo atahamasisha wanafunzi wengine kutambua thamani ya misitu iliyopo nchini. 

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Nanzia Charles amesema katika Msitu wa Pugu wenye hekta zaidi ya 2000 kuna miti iliyoharibiwa sana huko nyuma, kwa hiyo wanaendelea kupanda miti kwa lengo la kuufanya msitu huo kubaki kwenye uasili wake.

"Msitu wa Pugu na ule wa Kazimzumbwi tunasema ndio mapafu ya Dar es Salaam na kwa mazingira hayo TFS tumekuwa makini kuilinda na kila mara tunapanda miti katika maeneo ambayo tunabaini umefanyika uharibifu.Pia tunafahamu msitu wa Pugu ni wa asili na hivyo miti ambayo tunairejesha ni ile ya asili,"amesema Charles.

Kuhusu kuharibiwa kwa msitu wa Pugu amesema ulianza mwaka 2000 na sababu kubwa imetokana na msitu huo kuwa karibu na jiji la Dar es Salam, hivyo baada ya kubaini waliweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha msitu unabki salama ikiwa pamoja na kuweka walinzi na kupanda miti mara kwa mara na kuanzisha Kamati za mazingira kwa kushirikisha wananchi wanaouzunguka misitu.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Kampuni ya Ashton Media inayojihusisha na utenegezaji wa mabango ya matangazo Abbas Hirji amesema kampuni yao imeamua kushirikiana na TFS kutoa elimu kuhusu umuhimu wa utunzaji misitu na kufafanua kuna changamoto kubwa ya uharibifu wa mazingira.

"Ukiwa chini huwezi kuona uharibifu ambao umefanyika katika misitu yetu lakini ukiwa kwenye ndege utaona namna ambavyo moshi unawaka katika misitu kwasababu tu ya baadhi ya watu kuandaa mkaaa.Misitu yetu inaharibiwa sana.Hivyo tukaona tunalojukumu la kushirikiana na TFS ili tutoe elimu ya utunzaji misitu kwa faida yetu na watakaokuja.

"Mabango ambayo tumeyatengeneza yanazungumzia utunzaji wa misitu kupitia jumbe mbalimbali ambazo zipo kwenye mabango, tunaamini kwa kufanya hivyo tutakuwa tumesaidia kutoa elimu ya kutunza misitu yetu.Ni wajibu wetu kuilinda na kuitunza, hivyo tutaendelea kushirikiana na TFS ili kufanikisha dhamira njema ambayo kampuni yetu inayo kwa nchi yetu,"amesema Hirji .

Wakati huo huo Ofisa Misitu Mkuu Ugavi na Uenezi kutoka TFS 

Shaaban Kihulah amesema Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania umejipanga kuendelea kushirikiana na wadauo wote kuhakikisha misitu inatunzwa na ile ambayo imeharibiwa basi inarejeshwa kwenye uasili wake.

Amesema katika kuhakikisha malengo hayo wanafanikiwa wameamua kushirikiana kwa karibu pia na wanafunzi wa shule mbalimbali na vyuo kwa kuamini kwamba kwa kufanya hivyo idadi ya mabalozi wa misitu itaongezeka na kuondoa tatizo la uharibifu.

Katika kushirikiana huko na wanafunzi amesema katika upandaji miti wa Msitu wa Pugu wameshirikiana na wanafunzi wa Shule ya IST na wanaamini utamaduni huo utaendelea siku hadi siku.
 Balozi wa Misitu nchini ambaye pia ni Miss Tanzania namba mbili Nelly Kazikazi akipanda mti katika Msitu wa Pugu ikiwa ni ishara ya kuhamasisha watanzani kujenga utamaduni wa kupanda miti na kulinda misitu nchini
 Mwanafunzi wa Shule ya IST ya jijini Dar es Salaam Sallah Hirji akipanda mti katika Msitu wa Pugu ambapo baada ya kupanda mti amehamasisha watoto wengine nao kujenga utamaduni wa kutunza misitu nchini
 Baadhi ya maofisa wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) wakiwa na wafanyakazi wa Kampuni ya Ashton pamoja na wanafunzi wa shule ya IST katika bango ambalo linazungumzia umuhimu wa kutunza miti
Balozi wa Misitu ambaye pia ni Miss Tanzania namba mbili akiwa katika mlango wa kuingia katika pango la popo lililipo katika Msitu wa Pugu baada ya kupanda miti ndani ya msitu huo.

SERIKALI YADHAMIRIA KUKAMILISHA SKIMU ZOTE ZA UMWAGILIAJI AMBAZO UTEKELEZAJI WAKE HAUJAKAMILIKA - MHE MGUMBA

0
0
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali Bungeni leo tarehe 15 Aprili 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akifuatilia mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma leo tarehe 15 Aprili 2019. Mwingine pichani ni Naibu Waziri ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Juliana Shonza (Mb).



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma


Serikali inayo dhamira ya kukamilisha skimu zote za umwagiliaji ambazo utekelezaji wake haujakamilika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha. 

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 15 Aprili 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe Azza Hillal Hamad aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Bwawa la Umwagiliaji katika Kijiji cha Ishololo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Mhe Mgumba amesema kuwa Skimu hiyo ipo miongoni mwa skimu za umwagiliaji zitakazopewa kipaumbele katika kutekeleza Mpango Kabambe wa Taifa wa Umwagiliaji (Irrigation Master Plan 2018 - 2025) ambao kwa sasa umeanza kutekelezwa. 

Alisema kwa kuzingatia umuhimu wa miradi hiyo ukiwemo mradi wa umwagiliaji Ishololo, tayari Serikali imekwishaanza mazungumzo na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la JICA kwa lengo la kuboresha miradi yote ambayo haijakamilika na ile inayofanya kazi chini ya ufanisi uliokusudiwa. 

Naibu Waziri huyo wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) alisema kuwa mradi wa ujenzi wa bwawa wa Ishololo uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini ni moja kati ya miradi iliyokuwa ikitekelezwa kupitia Mradi wa Uwekezaji katika Kilimo katika Wilaya (DASIP) chini ya iliyokuwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika. 

Alisema Utekelezaji wa Mradi huo ulifikia ukomo wake mwezi Desemba 2013 ambapo Benki Maendeleo ya Afrika ilisitisha kutoa fedha za utekelezaji wa miradi wakati utekelezaji wake ukiwa haujakamilika.

RC MAKONDA AWAONYA TBA, ATAKA PESA ZILIZOTOLEWA NA RAIS MAGUFULI KUTUMIKA KUKAMILISHA MIRADI KWA WAKATI

0
0
*Aeleza kutofurahishwa na kasi na utekelezaji wa miradi katika Manispaa ya Ilala

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo Aprili 13 amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika  Wilaya ya Kigamboni na kuwaagiza Wakala wa Majengo ya serikali nchini (TBA) kuhakikisha wanakamilisha kwa haraka ujenzi wa majengo ya Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni, Ofisi ya Mkuu wa wilaya pamoja  na nyumba za viongozi kabla ya Juni 30 mwaka huu.

 Makonda amesema kuwa wakala hiyo ikishindwa kutekeleza agizo hilo watachukuliwa hatua ikiwemo kunyang'anywa mradi, kurudisha fedha na vifaa viliyobaki vilevile watalazimika kulipa kodi ya jengo la mtu binafsi linalotumiwa kama Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyi.

Hayo yamekuja baada ya  wa  Mkuu wa Mkoa kuchukizwa na hali ya kusuasua katika utekelezaji wa miradi hiyo licha ya kuongezewa muda zaidi ya mara mbili na fedha zote za ujenzi walishapatiwa lakini utekelezaji umekuwa duni hali inayopelekea  serikali kuzidi kutumia mamilioni ya pesa kulipa kodi ya pango kwenye jengo la mtu binafsi linalotumika kama ofisi ya mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Kigamboni.

Akiwa katika mradi wa ujenzi wa jengo la hospitali ya Wilaya ya Kigamboni  Makonda ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo uliogharimu takribani bilioni 1.5 kutoka Serikalini na amemuagiza mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha jengo linakabidhiwa kabla ya Juni 30 mwaka huu.

Kwa upande wake Mratibu mkuu wa Wakala wa Majengo ya serikali (TBA) Mkoa wa Dar es salaam Mhandisi Wilson Tesha amemuahidi RC Makonda kuwa wakala hiyo itahakikisha wanakamilisha ujenzi kabla ya Juni 30 kama walivyoagizwa.

Vilevile Mkuu wa Mkoa huyo ameitaka halmashauri ya Manispaa ya Ilala kujitathimini kuhusiana na miradi inayotekelezwa kwa kuwa hafurahishwi na utendaji kazi wao ambapo amesema kuwa shilingi bilioni 14 za ujenzi wa mtaro katika mto Msimbazi zimetengwa ila hakuna kinachoendelea na amemwagiza Mkurugenzi kuita kikao cha madiwani mapema jumanne ili wampe maelezo ya kina kuhusu kinachokwamisha utendaji kazi katika miradi husika.

Standard Chartered waelezea mkakati wa kuitangaza Tanzania mbio za Belt and Road

0
0
BENKI ya Standard Chartered imesema kazi yake kubwa nchini ni kuwezesha Tanzania kufanya biashara yenye faida na taifa la China kupititia mkakati wa Belt and Road. Benki hiyo imesema ikiwa na wateja 100 wa China (makampuni yenye nguvu) wao wanawezesha wananchi wa Tanzania na serikali kufaidika na biashara na China.

Kauli hiyo imetolewa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Bw.Sanjay Rughani akizungumza katika mashindano ya Belt and Road yaliyofanyika jana alfajiri. 
Mashindano hayo ni sehemu ya mashindano yanayoendeshwa kwa siku 90 duniani kote. Tanzania ikiwa ni ya 33 kufanya tukio hilo kati ya nchi 44.

Mashindano hayo yaliyofanyika Green Ground, Oysterbay yaliyojulikana kama Belt and Road Relay Race Tanzania washindi walikuwa Henry Li kutoka China aliyeshika nafasi ya kwanza, Herman Kambugu kutoka Uganda aliyeshika nafasi ya pili na Jack Messen aliyeshika nafasi ya tatu akitokea Uingereza. Rughani alisema kwa mwaka jana benki hiyo ilileta biashara ya dola za Marekani milioni 100 nchini Tanzania na kwamba benki hiyo ndiyo inayoongoza kwa kuwezesha biashara kati ya Tanzania na China.

Aidha alisema kwa mwaka jana waliwezesha kujengwa kwa viwanda viwili ambavyo wawekezaji ni kutoka China, viwanda ambavyo vimeajiri watanzania 3,000. Alisema katika mkakati wa ukanda wa hariri, benki hiyo inafanya juhudi kubwa za kuwezesha Tanzania inanufaika kibiashara na China.

"Tunataka watanzania waende katika dunia, wafanyabiashara wa hapa waende China" alisema Rughani na kuongeza kuwa ni lengo lao kuhakikisha kwamba wanaitangaza Tanzania.
Aidha katika mkakati huo alisema kwamba wana dawati maalumu linaloshughulikia Wachina na wafanyabiashara wanaotaka kufanyabiashara na China.

Mbio hizo za jana ni sehemu ya mbio za siku 90 zinazofanyika katika nchi 44 miongoni mwa nchi zilizomo katika mkakati huo wa Belt ulioanzishwa na China mwaka 2013 kwa ajili ya kuboresha biashara na maendeleo ya jamii mbalimbali duniani kwa ushirikiano wa karibu na China.
Nchi hizo zimo za bara la Amerika, Ulaya na Afrika na Asia.

Mbio hizo za kuamsha uelewa miongoni mwa wadau na wateja wa benki hiyo zilizinduliwa Februari 14 mjini Hong Kong kwa mbio za marathon zilizoshirikisha watu elfu 74. Aidha mbio hizo zitamalizikia nchini China Mei 11 wakati wa jukwaa la washiriki wa mkakati huo wa Belt and Road.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani akizungumza  na wafanyakzi wa banki hiyo, wateja, wafanyakazi wa Ubalozi wa China na kumkaribisha Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke  kutoa neno la ufunguzi wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke akingumza wakati wa ufunguzi wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizoandaliwa na benki hiyo zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani.
Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke akinyoosha bendera kuashiria ufunguzi ufunguzi wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay

Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani wakishiriki kwenye  mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered, wafanyakazi wa ubalozi wa China Nchini Tanzania pamoja na wadau mbalimbali wa Benki hiyo wakishiriki kwenye  mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
 Mshindi wa kwanza kutoka China Henry Li akimaliza mashindano ya mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam. 
 Mshindi wa tatu kutoka Uingereza Jack Messen akimaliza mashindano ya mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam. 
 Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke akimvalisha medali mshindi wa kwanza anatoka China Henry Li  wakati wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani akimpa zawadi mshindi wa pili kutoka Uganda Herman Kambugu  wakati wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni  mshindi wa kwanza kutoka China Henry Li na wa kanza kulia ni mshindi wa tatu kutoka Uingereza Jack Messen.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani akimpa zawadi mshindi wa tatu kutoka Uingereza Jack Messen  wakati wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke (kushoto) akipiga makofi  pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani(kulia) mara baada ya kutoa zawadi za medali wa washindi wa wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground jijini Dar es Salaam. katikati ni Mshindi wa kwanza anatoka China Henry Li akionesha tuzo, wa pili kulia ni  Mshindi wa tatu kutoka Uingereza Jack Messen na wa pili kushoto ni  Mshindi wa pili kutoka Uganda Herman Kambug.
Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani wakiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanayakazi wa Ubalozi huo pamoja na wateja wa Benki ya  Standard Chartered wa nchini China leo wakati wa mbio za Standard Chartered Belt & Road Relay zilizofanyika Green Ground, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

MHASHAMU BABA ASKOFU MKUU BEATUS KINYAIYA AWATAKA VIJANA KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA UJENZI WA TAIFA

0
0
Mhashamu Baba Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki Dodoma Beatus Kinyaiya amewataka Vijana kuwa mstari wa mbele kwenye kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii,kiuchumi na kisiasa ili kuijenga na kuistawisha Tanzania kwa kuwa ndio kundi kubwa linalotegemewa kwa kiasi kikubwa kwenye Kusukuma ajenda mbalimbali za kimaendeleo.

Baba Askofu Kinyaiya ameyasema hayo jana wakati wa adhimisho la Ibada ya Jumapili ya Matawi katika Kanisa la Mt. Yohana Mtume Kikuyu,Dodoma ambapo pia siku hii huwa ni maalum kwa ajili ya VIJANA WAKATOLIKI ULIMWENGUNI na kwa jana ilisimamiwa na VIJANA WAKATOLIKI WAFANYAKAZI*(VIWAWA)*

“Vijana wa Kanisa muwe mfano bora,ishini katika haki,upendo na kujituma na msiwe wasaliti wa nafsi zenu.Mfanye kazi kwa bidii na kujituma kwani Taifa linawategemea.Nimefurahi juu ya uanzishwaji wa Kituo cha Vijana ambacho kitatoa pia mafunzo ya Ufundi,jukumu la kukamilika kwake namuachia kijana mwenzenu Anthony Mavunde”-Alisisitiza Baba Askofu Mkuu Kinyaiya

Akizungumza katika Ibada hiyo,Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde ,amewahidi Vijana hao kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha ujenzi wa kituo hicho na akachangia Mifuko 100 ya saruji na fedha Tsh 1,000,000 na kuongoza harambee iliyopelekea kupatikana matofali 7000 ili ujenzi wa ukuta kuzunguka kituo uanze mara moja na pia kutoa ahadi ya kuwapatia vifaranga 500 kwa ajili ya mradi wa Kuku wa Mayai ili waweze kujiendesha kiuchumi.

“Baba Askofu Mkuu,mimi katika maisha yangu muda mrefu nilikuwa mtumishi wa Altareni kanisani na nimekuwa sehemu ya VIWAWA,namuomba Mungu atusaidie yote tuliyopanga leo yatimie ili kituo hichi kiwasaidie Vijana wengi hasa katika kutatua changamoto ya ukosefu wa Ajira”-Alisema Mavunde




RC MAKONDA AMUAGIZA MKURUGENZI ILALA KUITISHA KIKAO CHA DHARURA CHA BARAZA LA MADIWANI

0
0
*Aeleza kutofurahishwa na utekelezaji wa miradi Wilayani humo

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

KULEGALEGA na siasa chafu ya kukwamisha miradi ya maendeleo kwa makusudi kunakofanywa na baadhi ya Madiwani wa Wilaya ya Ilala, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda amemuagiza mkurugenzi wa manispaa hiyo kuitisha   kikao cha dharura cha Baraza la madiwani siku ya jumanne na endapo wajumbe watakaidi atalazimika kumpelekea Rais Magufuli mapendekezo ya kuvunja baraza hilo au kubadilisha mfumo kwa faida ya wananchi.

Makonda amesema kuwa inashangaza kuona serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais John Joseph Magufuli imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya utatuzi wa kero sugu za wananchi lakini baadhi ya wanasiasa wasiowatakia mema wananchi wamekuwa wakipinga miradi hiyo kwa makusudi na kupelekea wananchi kuona serikali yao haiwajali wakati tayari imeshatoa fedha za utatuzi wa kero zao.

Miongoni mwa miradi ambayo serikali imetoa pesa lakini zimeishia kubaki kwenye akaunti bila kutumika ni ujenzi wa machinjio ya kisasa vingunguti, ujenzi wa soko la kisutu na maboresho ya mto msimbazi ambao umekuwa ukisababisha athari za mafuriko kwa wananchi.

Serikali mbioni kuanza Mpango wa Uagizaji wa Gesi ya Mitungi (LPG) Kwa Pamoja

0
0
Serikali imesema iko katika hatua za awali za kuandaa mpango wa uagizaji wa gesi ya mitungi (LPG) kwa pamoja kama ilivyo kwa mafuta ya Petroli hali itakayosaidia kudhibiti masuala mbalimbali ikiwemo bei ya gesi hiyo .

Akizungumza wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanyika jijini Dodoma, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani alisema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa, wananchi katika maeneo yote nchini wanafikiwa na huduma hiyo, hivyo Serikali itaratibu usambazaji wa gesi hiyo badala ya kuwaachia wauzaji wenyewe kuamua maeneo wanayotaka kupeleka gesi.

‘’ Serikali ikitangaza bei elekezi kulingana na soko, itawafanya wauzaji wafuate bei hiyo badala ya wao kujipangia, hii itasaidia wananchi kuuziwa gesi kwa gharama inayofanana katika maeneo mbalimbali ambapo gesi hiyo itauzwa.”alisema Dkt. Kalemani.

Alieleza kuwa, suala la sasa la kila muuzaji kujiamulia sehemu anayotaka kupeleka gesi inafanya maeneo mengine kukosa kabisa nishati hiyo hivyo sasa Serikali itaweza kuwadhibiti wauzaji na kuhakikisha kuwa maeneo yote nchini yanafikishiwa gesi.

Aliongeza kuwa, utaratibu wa kuagiza gesi inayotumika majumbani kwa pamoja utasaidia Taifa kutambua kiwango halisi cha gesi kinachohitajika nchini na kiasi cha gesi kinachoingizwa nchini na hivyo kusaidia pia katika shughuli za ukusanyaji wa mapato.

Awali, akitoa taarifa kwa Wajumbe wa Kamati hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Erasto Simon alisema kuwa, Wakala huo kwa sasa unafanya tathmini ya namna bora ya kuanza uagizaji wa pamoja wa gesi ya mitungi (LPG) kwa kuzingatia maoni kutoka kwa wadau mbalimbali.

Akizungumzia faida mbalimbali zinazotokana na uagizaji wa mafuta wa pamoja, Simon alisema kuwa, ni kuweka mazingira sawa ya kibiashara kwani gharama za uagizaji wa mafuta ziko sawa kwa makampuni yote na kuondoa mianya ya rushwa katika uagizaji wa mafuta kwani ufunguzi wa zabuni hufanyika kwa uwazi na washiriki wote huridhika na matokeo ya zabuni.

Alitaja faida nyingine kuwa ni, Taifa kuwa na uhakika wa usalama wa upatikanaji wa mafuta kwa muda wote na kuwezesha Serikali kuwa na takwimu sahihi za mafuta zinazosaidia katika ukusanyaji wa mapato na kupanga bei elekezi ya mafuta.

Aliongeza kuwa, mfumo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja umewezesha nchi kudhibiti ubora wa mafuta yanayoingia nchini na pia kuongezeka kwa sehemu za kupokelea mafuta kama bandari ya Tanga na Mtwara, tofauti na ilivyokuwa awali kwani Bandari ya Dar es Salaam ndiyo ilikuwa ikitumika kwa shughuli hizo.

Kutokana na hilo, alisema kuwa, nchi mbalimbali barani Afrika kama vile Malawi, Zambia na Msumbiji wamekuja kujifunza kuhusu mfumo huo wa uagizaji mafuta ili waweze kuutumia katika nchi zao.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dunstan Kitandula wakati wa Semina ya Wabunge hao iliyohusu Sekta ya Nishati iliyofanyika jijini Dodoma.
 Watendaji mbalimbali kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Taasisi hizo wakifuatilia taarifa zilizokuwa zikitolewa wakati wa semina ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyohusu Sekta ya Nishati.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa kuhusu Sekta ya Nishati katika Semina ya Wajumbe hao iliyofanyika jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Erasto Simon, akiwasilisha taarifa kuhusu Wakala huo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati wa Semina ya Wabunge hao iliyohusu Sekta ya Nishati.

WASOMI NCHINI WAASWA KUTUMIA ELIMU YAO VIZURI KUIKOMBOA JAMII

0
0
Na Ahmed Mahmoud, Arusha

Wahitimu nchini wameaswa kutumia elimu yao vizuri katika kuwa chachu ya kuwakomboa wengine katika changamoto mbalimbali zinazowakabili ndani ya Jamii.

Hayo yalisemwa Jana na Mwenyekiti wa umoja wa wanawake ccm mkoa wa Arusha, Yasmin Bachu wakati akizungumza katika mahafali ya 20 ya wanafunzi 154 wa kidato cha sita katika shule ya sekondari Enaboishu iliyopo mjini hapa.

Alisema kuwa, wanapaswa kutumia elimu hiyo waliyoipata kuwa watatuzi wa changamoto mbalimbali katika jamii kwani wao Ndio wanaotegemewa kuleta mabadiliko chanya.

Aidha aliwataka wanafunzi hao pia kuhakikisha wanatoa elimu na kupinga vitendo viovu vya madawa ya kulevya kwa vijana sambamba na kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia ambao ndio umeshamiri katika jamii nyingi kutokana na mila na desturi zilizopo.

"nawaombeni jamani mkawe mfano wa kuigwa na muwe mabalozi wazuri wa kabadilisha Jamii Kwa kutoa elimu Kwa vijana wenzenu juu ya vitendo mbalimbali viovu, ili kupitia nyie tuweze kuona mabadiliko makubwa. "alisema Bachu.

Kwa upande wa Mkuu wa shule hiyo, Godwin John alisema kuwa, shule hiyo imekuwa ikiwandaa wanafunzi kufanya vizuri ikiwemo kutoa motisha kwa wanafunzi wanaofanya vizuri pamoja na walimu ili kuongeza kiwango cha ufaulu zaidi shuleni hapo.

Alisema kuwa, shule hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vioo vya vyumba vya madarasa, ukosefu wa madarasa, ulipaji ada wa kusuasa hivyo kuwataka wazazi pamoja na walezi kuhakikisha wanawekeza zaidi kwa watoto wao kwani huo ndio urithi pekee unaotakiwa kutolewa kwa watoto.

Naye Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo, Titi mzava aliwataka wanafunzi hao kutobweteka na elimu hiyo waliyoipata badala yake wakawe mfano bora wa kuigwa katika kuitangaza shule hiyo.

Aidha aliwataka wanafunzi hao pindi wanaporejea mtaani wakawe chachu ya mabadiliko kwa vijana wenzao kupitia elimu hiyo waliyoipata.

WATUMISHI WA TUME WANAOSHIRIKI KATIKA UKAGUZI WA RASILIMALI WATU KWA TAASISI 56 WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI

0
0
Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma wanaoshiriki katika Ukaguzi wa Rasilimali watu  katika Mikoa mitano yenye jumla ya Taasisi 56 zilizopo nje ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la  kuangalia kiwango cha uzingatiaji wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo katika usimamizi na uendeshaji wa Rasilimali watu katika Utumishi wa Umma wametakiwa kuzingatia maadili.

Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma,   Richard Odongo amezungumza na watumishi wa Tume pamoja na maafisa wanaofanya ukaguzi huo jijini Dar es Salaam na amewaasa kuzingatia maadili na wahakikishe wanatekeleza jukumu hili kwa uadilifu na uaminifu  mkubwa.

Odongo amesema kuwa Watumishi wa Tume wanaokwenda kufanya ukaguzi huo wanapaswa watambue kuwa wamebeba dhamana kubwa ya Tume ya Utumishi wa Umma hivyo wakati wote wajiepushe na mienendo isiyofaa, wakatekeleze jukumu hili la kisheria la ukaguzi wa rasilimali watu kwa weledi, wazingatie maadili na wahakikishe wanatoa maamuzi ya haki na taarifa sahihi na kwa wakati.

Mikoa itakayokaguliwa ni Dodoma, Morogoro, Pwani, Mbeya na Mtwara; miongoni mwa Taasisi 56 zitakazokaguliwa ni pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu); Wizara ya Nishati; Wizara ya Madini; Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Tume ya Utumishi wa Walimu; Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Ukaguzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya Tume yaliyopangwa kufanyika katika mwaka huu wa fedha wa 2018/2019 ambapo Tume  tayari imefanya ukaguzi kwa Taasisi 33 zilizopo katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Tume pia inatarajia kufanya ukaguzi mwingine katika Mikoa mingine mitano ambapo jumla ya Taasisi 61 zitakaguliwa, lengo likiwa ni kuangalia ni kwa kiwango gani masuala ya Rasilimali Watu yanasimamiwa na kuendeshwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali katika Utumishi wa Umma; kuimarisha utendaji na uwajibikaji unaozingatia malengo na matokeo yanayopimika.
Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Richard Odongo (aliyesimama) akisisitiza jambo kwa watumishi na Maafisa wa Tume (jijini Dar es Salaam) watakaoshiriki katika Ukaguzi wa Rasilimali watu kwa Mikoa mitano yenye jumla ya Taasisi 56, kuangalia namna masuala ya rasilimali watu yanavyosimamiwa kwa kuzingatia Sheria. (Picha na Ofisi ya Rais – Tume ya Utumishi wa Umma)

KIKAO CHA WADAU KUHUSU UHAKIKI WA TAKWIMU ZA VYAMA VYA USHIRIKA NCHINI CHAFANA

0
0
Kikao cha Wadau wa Vyama vya Ushirika nchini kimefanyika leo Jumatatu, Aprili 15, 2019 Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili taarifa ya uhakiki wa takwimu za Vyama vya Ushirika na kutoa maazimio juu ya majukumu yanayopaswa kutekelezwa na kila mdau kulingana na matokeo na changamoto zilizobainishwa. Taarifa hii itasaidia katika kuboresha utendaji kazi wa Vyama vya Ushirika nchini.  

Akifungua kikao hicho, Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Bw. Tito Haule  amesisitiza  umuhimu wa kuwa na takwimu sahihi za Vyama vya Ushirika na amewataka wadau wa ushirika nchini  kutotoa takwimu za Vyama vya Ushirika bila kuwasiliana na mamlaka husika ambayo ni Tume ya Maendeleo ya Maendeleo ya Ushirika.

Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania ilifanya zoezi la uhakiki wa Takwimu za Vyama vya Ushirika nchini na kupanga SACCOS kwenye madaraja (SACCOS Categorization) mwaka 2018 ili kupata takwimu sahihi za Vyama vya Ushirika. Zoezi hilo lilikamilika mwishoni mwa mwaka 2018 na taarifa ya uhakiki huo iliandaliwa ambayo imesaidia kupata takwimu halisi za vyama hivyo.
 Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Bw. Tito Haule, akifungua Kikao cha Wadau wa Vyama vya Ushirika nchini kujadili taarifa ya uhakiki wa takwimu za Vyama vya Ushirika.
 Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Tathmini wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC),  Buji Bampebuye, akitoa mada kwenye Kikao cha Wadau wa Vyama vya Ushirika nchini kujadili taarifa ya uhakiki wa takwimu za Vyama vya Ushirika.
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC),  Josephat Kisamalala, akitoa mada kwenye Kikao cha Wadau wa Vyama vya Ushirika nchini kujadili taarifa ya uhakiki wa takwimu za Vyama vya Ushirika

Wadau wa Ushirika wakiwa kwenye Kikao cha Wadau wa Vyama vya Ushirika nchini kujadili taarifa ya uhakiki wa takwimu za Vyama vya Ushirika.

KOPAFASTA KUWAPA SHAVU WASANII WA SANAA ZA UFUNDI

0
0
Na Agness Francis blogu ya jamii. 

KAMPUNI ya kutoa mikopo ijulikanayo kama Kopa fasta imeamua kuunga mkono juhudi za wasanii wa sanaa za ufundi kwa kutoa fursa ya kutoa mikopo kwao ili kujiendeleza katika kazi zao za kisanaa zinazowapatia kipato hapa nchini. 

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam Meneja wa Kopa Fasta Patrick Kang'ombe wakati wa uzinduzi wa mradi huo amesema kuwa kampuni hiyo inatoa mikopo kupitia makundi mbalimbali kwa wanachama ambao wamesajiliwa na wa miradi ya TACIP na PSGP inayotekelezwa na kampuni ya DataVision International kwa kushirikiana na taasisi na wizara za serikali. 

Kang'ombe amesema leongo la Kopa fasta ni kusaidia kuboresha sekta zisizo rasmi kama wasanii wa sanaa za ufundi ,ili kuwasaidikundia kuwa mikopo ya fedha na vitendea kazi, pamoja na kujenga uwezo kupitia mafunzo ya usimamizi wa fedha, biashara na uwekezaji. 

"Huduma yetu ni tofauti, kwani tumechagua sekta ambazo zimesahaulika na zimekuwa zikichukuliwa kuwa hazikopesheki, kwa maana ya kutokuwa na uwezo wa kuweka dhamana na kutoaminika kupewa mikopo, zimekuwa changamoto kubwa kwa sekta hizo, na kuzifanya kubaki nje ya mfumo rasmi pamoja na kuwa zimekuwa na mchango mkubwa katika pato la Taifa "amesema Kang'ombe. 

Aidha Meneja wa M-Lipa Maclean Geofrey ametoa ufafanuzi kuwa wanashirikiana na Kopa fasta katika mfumo ambao unawawezesha kupata malipo ambayo hayatumii fedha taslimu kukopa na kurejesha fedha. 

"Tunawawezesha makundi yasio rasmi kupata mkopo na kurejesha kupitia mfumo wa M-Lipa kupitia simu janja ya mkononi (Smartohone) pia msanii huyo wa sanaa za ufundi ili aweze kuomba na kupata mkopo anatakiwa awe mwanachama aliyesajiliwa na miradi inayofanya kazi na kopa fasta"amesema Maclean. 

Hata hivyo Mratibu wa ( TACIP) mradi wa utambuzi wa wasanii wa sanaa za ufundi Saul Mpock, amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuwapa kipaumbele hapa nchini, kuwatengenezea mfumo wasanii hao ili waweze kukopesheka.
Meneja wa Kopafasta Patrick Kang'ombe pamoja na Wadau mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo wakikata keki kwa pamoja wakiashiria uzinduzi rasmi wa kopafasta leo Jijini Dar es Salaam.


Meneja wa Kopafasta Patrick Kang'ombe akifafanua lengo la kuwapa mikopo   wasanii wa sanaa za ufundi leo Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Kopafasta.
Baadhi ya wadau mbalimbali waliojitokeza katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Kopafasta leo Jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi wa TAA wapigwa msasa na KOICA

0
0
Watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kutoka Menejimenti na Vitengo vya Usalama, na uzuiaji wa wanyama pori na ndege hai  leo wameshiriki katika mafunzo  ya kuwajengea uwezo wa utendaji katika Viwanja vya Ndege yaliyoandaliwa na KOICA (Korea International Cooperation Agency)  na kutekelezwa na wataalam kutoka Kiwanja cha Ndege cha Incheon kilichopo Korea Kusini ambacho kinaaminika kuwa na ubora nambari moja katika nyanja ya usalama na uendeshaji duniani.

Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa watu mashuhuri Katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jengo la pili la abiria (TB II), ikiwa ni  mwendelezo wa mpango wa mafunzo ya miaka mitatu kwa watendaji wa TAA na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA).
Akitoa maelezo kuhusu mafunzo hayo Meneja wa Mafunzo kutoka Kiwanja cha Ndege cha Incheon Bi. Ji-Yoon Park ameeleza kwamba mafunzo hayo ni mwendelezo wa mafunzo ya awali ambapo kwa awamu ya kwanza Mafunzo yalitolewa kwa watendaji takribani 15 kutoka TAA na ZAA na mafunzo haya ni sehemu ya mpango wa mafunzo ya miaka mitatu (2018 – 2020).

Mafunzo haya yatafanyika kwa siku mbili kuanzia leo tarehe 15 Aprili na yatamalizika siku ya kesho16 Aprili nakuendelea huko Zanzibar ambapo yatafanyika katika Mamlaka ya Viwanja vya ndege   Zanzibar.
Katika awamu ya kwanza ya mafunzo haya yalifanyika mwezi Septemba mwaka jana na Watendaji kumi na tano (15) walinufaika na mafunzo haya ikiwa ni (10) kutoka TAA na watendaji na  watano (05) kutoka ZAA.

Ikumbukwe kuwa TAA na ZAA mnamo Juni 2018 waliingia katika makubaliano na KOICA  ya kutoa mafunzo kwa Watumishi  kwa muda wa miaka mitatu ambapo kufikia mwaka 2020 Watumishi 45 watakuwa wamenufaika na mafunzo hayo kutoka Utawala, kada za Ulinzi na Usalama, Tehama, na Uendeshaji.
  Msimamizi Mwandamizi na Mkaguzi wa Usalama wa anga Sanghoom (Mark) Lim akitoa mafunzo kwa Watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kutoka Menejimenti na Vitengo vya Usalama, Uendeshaji na uzuiaji wanyamapori kuhusu masuala ya Usalama katika Viwanja vya Ndege ndani ya Ukumbi wa watu Mashuhuri (VIP) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA TB II).
 Watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kutoka Menejimenti na Vitengo vya Usalama, Uendeshaji na uzuiaji wanyamapori  wakiwa katika mafunzo ndani ya Ukumbi wa watu Mashuhuri (VIP) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA TB II).Walioketi mbele kushoto ni Meneja Rasilimali watu na Utawala Bw. Abdi Mkwizu kulia ni Mkurugenzi wa kituo cha Mafunzo ya Anga cha Kiwanja cha Ndege cha Incheon Bw. Chin Hyong, Ryu.
Meneja wa Mafunzo kutoka Kiwanja cha Ndege cha Incheoni Bi. Ji-Yoon Park akitoa mafunzo kwa Watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kutoka Menejimenti na Vitengo vya Usalama, Uendeshaji na uzuiaji wanyamapori kuhusu namna ya kuandaa mpango wa kuwaongezea uwezo watendaji katika Viwanja vya Ndege. Mafunzo hayo yamefanyika ndani ya Ukumbi wa watu Mashuhuri (VIP) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA TB).

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAANDAA KIKAO CHA WAWEKEZAJI NA WADAU WA MIFUKO MBADALA WA PLASTIKI JIJINI DAR ES SALAAM.

0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira January Makamba akiongea wakati wa Kikao kilichokutanisha Wadau na Wazalishaji wa mifuko mbadala wa plastiki kilichofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira January Makamba akiwa pamoja na Waziri waNchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Angellah Kairuki, Waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda wakati wa kikao Wadau wa uzalishaji na uwekezaji wa mifuko mbadala wa plastiki kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wadau wa uzalishaji na uwekezaji katika mifuko mbadala wa plastiki waliohudhuria kikao hiko katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kikao hiko kiliandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira January Makamba akiteta jambo na  Waziri waNchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Angellah Kairuki wakati wa kikao cha Wadau na Wawkezaji wa mifuko mbadala wa plastiki kilichofanyika jijini Dar es Salaam. 

WASANII WASHAURIWA KUHUSISHA MAWAKILI KWENYE MIKATABA YA KAZI ZAO

0
0
Ay,Mwanafa wadaiwa  kudhulumiwa haki zao

WASANII  wote nchini wameombwa kujitathimini upya katika mikataba au makubaliano wanayoingia na makampuni, mashirika, wamiliki wa filamu kwenye kazi zao.

Akizungumza na wasanii wakili wa wasanii Alberto Msando  katika kongamano la waigizaji lililoandaliwa na  bodi ya filamu (TFB)  pamoja na chama cha waigizaji (TDFAA)  lililofanyika ukumbi wa Suma JKT Mwenge jijini Dar es salaam. amesema ni wakati wa Wasanii kujitathimini na kuingia makubaliano ya kikazi kwa njia ya maandishi ili kuepuka unyonywaji na utapeli kwenye malipo baada ya kazi na kabla ya kazi.

"Mikataba inasaidia wasanii kuwa na adabu na nidhamu ya kazi kutokana na kumtaka muda maalum kuwepo kwenye kazi na hata hivyo inamsaidia msanii kudai stahiki zake  haraka huku akiwa na vielelezo husika ," alisema Msando.

Msando amewataja baadi ya wadau wakiwemmo waandaaji wa filamu,watunzi wa filamu pamoja na watengenezaji wa matangazo ambao wanawatumia wasanii kwenye matangazo hayo, kuwa na leseni za kikazi ili kutambulika kisheria.

Halikadhalika amewatolea mfano wasanii kama Ambwene Yesya a.ka AY Khamisi Mwinjuma a.k.a MwanaFA,Wema Sepetu pamoja na Masanja Mkandamizaji ambao wameshapata matatizo kwenye kazi zao kutokana na mikataba wanayoingia na wakifika katika mikono sheria wanafanikiwa kupata haki zao ,Hivyo amewasihi wasanii kufika kwenye vyombo vya sheria au hata kusaini mikataba na kuhusisha Mawakili .

Pia ametoa rai kwa wasanii kujiandikisha kwenye vyama vya sanaa,bodi ya filamu pamoja baraza la sanaa ili kutambulika kama msanii mwenye kutambulika.


Serikali Kufanya Mabadiliko ya Kanuni za Matumizi ya Nyavu Baharini

0
0

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Serikali imepanga kufanya mabadiliko ya kanuni za matumizi ya nyavu upande wa bahari ili wavuvi waweze kutumia nyavu za milimita nane badala ya milimita kumi zilizokuwa zikitumika awali.

Hayo yamesemwa leo, Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi lililohoji kuwa ni lini Serikali itakuwa tayari kufanya utafiti katika eneo la Ziwa Victoria kama inavyofanya upande wa Bahari ili kuweza kuruhusu matumizi ya nyavu za chini ya milimita nane.

Ulega amesema kuwa kwa mujibu wa Sheria, nyavu za kuvulia dagaa zenye ukubwa wa macho chini ya milimita nane zimekatazwa kutumika kwa uvuvi wa dagaa katika maji baridi ikiwemo maeneo ya maziwa kwa sababu tafiti zinaonyesha kuwa aina hiyo ya nyavu ikitumika itavua dagaa wachanga hivyo kuathiri uvuvi wa dagaa.

"Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania itafanya utafiti na endapo itaridhika itaruhusu wavuvi wanaovua ziwani wavue kwa kutumia aina hiyo ya nyavu, kwa upande wa bahari Serikali imeielekeza TAFIRI kufanya utafiti na kujiridhisha kwa ajili ya kufanya mabadiliko ya kanuni kwa haraka ili ikiwezekana tuweze kutumia nyavu za milimita nane zitakazoweza kuwanufaisha wavuvi wa upande wa bahari", alisema Ulega.

Amefafanua kuwa kwa upande wa bahari, nyavu zilizokuwa zikitumika kuvua dagaa ni milimita kumi lakini maoni ya wadau wengi yanaonesha kuwa milimita kumi zimeshindwa kuvua dagaa ndio maana Serikali imeamua kufanya utafiti huo ili kuona kama inawezekana wavuvi wa bahari kutumia nyavu za milimita nane.

Akizungumzia kuhusu uvuvi wa samaki aina ya Gogogo, Ngele na Mingu waliopo katika Ziwa Victoria, Naibu Waziri Ulega amesema kuwa katika mabadiliko ya Kanuni yanayofanyika hivi sasa Serikali imezingatia kufanya makubaliano ya kupitisha kanuni rasmi itakayoruhusu uvuaji na matumizi ya aina hizo za samaki.

Waziri Ulega ametoa rai kwa wavuvi kuendelea kuzingatia sheria na kanuni zilizopo kwani Sheria na kanuni hizo zinalenga uvuvi unaofanyika nchi uwe endelevu na wenye tija.


BENKI YA CRDB, UBA WAUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA MAJI WA RUFIJI

0
0
BENKI ya CRDB kwa kushirikiana na Benki ya UBA (Tanzania) zimedhamini utekelezaji wa mradi wa umeme wa maji wa Rufiji (Rufiji Hydro Power Project) unaotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ikiwa ni mkakati wakusaidia juhudi za Serikali kukamilisha mradi huo.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema kuwa Benki ya CRDB ikiwa benki ya kizalendo imeamua kuungana na jitihada za Serikali kufanikisha miradi mbalimbali, na sasa wametilia mkazo katika mradi huo muhimu unaolenga kuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme nchini.  

Kwa upande wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Mwinyimvua Hamisi alisema, dhamana hizo zilizokabidhiwa ni muhimu sana katika kuhakikisha kwamba utekelzaaji wa mradi wa bwawa la kufua umeme wa maji wa mto Rufiji unaanza bila kuchelewa na kuhakikisha kwamba ratiba iliyokubaliwa baina ya serikali na mkandarasi itatekelezwa kwa mujibu wa mkataba.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaaban alisema “Jambo hili la uwekaji wa dhamana ni muhimu sana kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu kwani ni mradi wenye gharama kubwa kiasi cha shilingi za kitanzania trilioni 6.6 kwa hivyo ni mradi unaogharimu fedha nyingi katika historia ya nchi yetu katika miaka ya hivi karibuni.” Alisema Bi. Amina.

Kwa upande wake Naibu Gavana wa BoT, Dkt. Benard Kibese alisema, kazi kubwa ya BoT katika utekelezaji wa mradi ni kuweka mazingira mazuri ili kuhakikisha ushiriki wa taasisi za fedha za hapa nchini unakuwa mkubwa.

Mwisho kabisa Mkuurgenzi Mtendaji wa TANESCO Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka aliishukuru serikali ya awamu ya tano chini wa uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwezesha hatua hiyo kufikiwa kwani mradi huo bila pesa kulipwa mkandarasi hawezi kufanya kazi yake ipasavyo. Dkt. Mwinuka alisema hatua ya leo inawezesha pesa kulipwa kwa mkandarasi pale zitakapohitajika au pale ambapo mkandarasi anastahili kulipwa kwa hivyo kuanzia sasa utekelezaji wa mradi huu hautakuwa na kikwazo chochote katika ulipaji wa pesa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akiwa na Mkurugenzi Mtedanji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela (wa tatu kushoto) wakimkabidhi hati za dhamana Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,  Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka (wa nne kulia), katika hafla fupi, iliyofanyika leo kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam. walioshuhudia ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Mwinyimvua H. Hamisi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi.Amina Shaaban, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Bernard Kibese, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles E. Kichere na Balozi wa Misri hapa nchini Mhe.Mohammed Gabel Abulwafa. Wakandarasi wanaotekeleza mradi huo wanatoka nchini Misri.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Mwinyimvua Hamisi akizungumzia umuhimu wa utekelezaji wa mradi wa bwawa la kufua umeme wa maji wa mto Rufiji, unaotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), katika hafla hiyo, iliyofanyika leo kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika hafla hiyo, iliyofanyika leo kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
Balozi wa Misri nchini Tanzania, Mohamed Gabel Abulwafa akizungumza katika hafla hiyo, iliyofanyika leo kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shaaban akizungumza katika hafla hiyo, iliyofanyika leo kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Bernard Kibese akizungumza katika hafla hiyo, iliyofanyika leo kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,  Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka akizungumza katika hafla hiyo, iliyofanyika leo kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.











MWENYEKITI WA CCM TAIFA RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM (NEC) IKULU CHAMWINO JIJINI DODOMA

0
0
 Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi Rais Dkt. John Pombe Magufuli na MAkamu Mwenykiti wa CCM (VIsiwani) na Rais wa Zanzibar na Baraa la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein  wakitoka kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya  chama hicho (NEC)  kilichofanyika
Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Jumatatu Aprili 15, 2019.
Wajumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya  Chama Cha Mapinduzi (NEC) wakitoka kwenye kikao chao kilichofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumatatu Aprili 15, 2019
Katibu Mkuu wa  Chama Cha Mapinduzi Dkt. Bashiru Ally akizungumza na Wajumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya  Chama hicho  (NEC) kabla ya kuanza kwa kikao chao kilichofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo  chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt. John Pombe
Magufuli Jumatatu Aprili 15, 2019

Kamati ya Maudhui ya TCRA yatoa onyo kali kwa vituo vya Star TV na Magic FM

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imeotoa onyo kwa Kampuni za vyombo vya habari vya Sahara Media Group na African Media Group kutokana na kutangaza habari za magazeti baadhi ya habari kiundani.

Akizungumza wakati wa kutoa maamuzi ya kamati ya maudhui TCRA Mwenyekiti wa Kamati hiyo Vallerie Msoka amesema kuwa kituo cha Magic FM ilitangaza habari za habari magazeti katika kiundani ambayo ni kinyume na sheria ya zuio la Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harison Mwakyembe.

Amesema kuwa habari iliosomwa na Megic FM katika moja ya magazeti kuhusiana na matumizi ya kondomu ambapo watangazaji walikuwa wanadisi juu ya matumizi hayo.

Msoka amesema kuwa African Media Group katika utetezi wake walidai kuwa wakati linafanyika kosa hilo Megic FM ilikuwa chini ya umiliki mwingine na kuomba msamaha huo katika kamati hiyo.

Aidha amesema kuwa utetezi wa Megic FM haufanyi umiliki wa mtu mwingine kuharalisha utangazaji uliofanyika huku wakijua ni zuio la Waziri Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harison Mwakyembe Kwa upande wa Star Tv walitangaza habari ya Waziri wa Madini Dotto Biteko kiundani zaidi huku wakijua ni kosa kwa zuio la Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dk.Harison Mwakyembe.

Msoka amesema katika utetezi wake kampuni inayomiliki Star Tv ilisema kuwa wakati wanatangaza habari za magazeti aliyefanya hana uzoefu na kudai kuwa wale wazoefu wanaacha kazi.Amesema kuwa utetezi wa star tv haufanyi kuondoka kwa wafanyakazi ndio kutangaza habari za magazeti kiundani.
Amesema kuwa kwa vituo hivyo kama hawajalidhika wanaweza kukata rufaa ndani ya siku 21 pamoja kutaka kufuata sheria za utangazaji.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Vallerie Msoka akitoa maazimio ya ukiukaji maudhui ya Utangazaji kwa Vituo vya Star Tv na Magic FM leo jijini Dar es Salaam.

AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA GARI -RPC WANKYO

0
0
DICKSON Archibold Maro (53) amekutwa amefariki dunia ndani ya gari IT, aina ya noah yenye namba za cheses 603026045 baada ya kuugua ghafla. 

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, ACP Wankyo Nyigesa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, karibu na kituo cha mafuta cha state oil, huko Mdaula, Bwilingu Chalinze mkoani Pwani. 

Alisema gari hiyo ilikuwa ikitokea Dar es salaam kuelekea Tunduma mkoa wa Songwe. "Baada ya kufika kituo cha mafuta cha state oil, marehemu aliugua ghafla akiwa amepaki gari eneo hilo "alifafanua Wankyo. 

Wankyo alielezea, wahudumu wa kituo hicho walitoa taarifa kwa askari polisi ambao walifika mara moja na kukuta marehemu akiwa na hali mbaya. 

Jitihada za kumuwahisha marehemu kituo cha afya Chalinze zilifanyika lakini baada ya kufikishwa kituoni hapo aligundulika amekwishafariki.

Hata hivyo, Kamanda huyo alisema kwamba, marehemu Dickson alipopekuliwa alikutwa na shilingi 285, 000 pamoja ,dola 400, simu mbili aina ya itel , tecno na karibu na gia kulikutwa chupa mbili za maji na chupa ya juice zilizonywewa. 

Wankyo alisema, utaratibu unafanyika kwa kushirikiana na clearance agency wanaohusika na upatikanaji wa bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine ili liweze kuondolewa kituo cha polisi Chalinze ambapo limehifadhiwa. 

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospital ya rufaa ya Tumbi kwa uchunguzi wa daktari na ndugu wa marehemu wamejitokeza ili baada ya uchunguzi wakabidhiwe mwili huo kwaajili ya mazishi. 
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images