Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110150 articles
Browse latest View live

Chamwino warejesha Tabasamu la Jafo

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, Mlowa Chamwino
Ni wiki moja sasa tangu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  Selemani Jafo (Mb) kutembelea eneo la ujenzi wa hospital ya Wilaya ya Chamwino inayojengwa katika Kata ya Mlowo ambapo alikuta kusuasua kwa ujenzi wa hospital hiyo ilihali fedha zilishapokelewa zaidi ya miezi mitano iliyopita: Hali hiyo ilimpelekea kutoa agizo la kuendelea kwa ujenzi huo haraka

Hivi leo Waziri Jafp amerejea tena katika eneo la ujenzi wa hospital hiyo na kiushuhudia ujenzi ukiwa unaendelea kwa kasi na majengo zaidi ya matatu yakiwa yameshaanza kupanda na mengine yakiwa yanakamilishwa kwenye hatua ya jamvi.

Mafundi wa kutosha wakiwa wanaendelea na shughuli za ujenzi katika eneo la Mlowo huku Menejiment ya Chamwino nayo ikitoa muongozo wa nini cha kufanya sambamba na Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiwa inahakiki kuwa kitu kitu kinaenda kama kilivyopangwa ni miongoni mwa vitu vilivyomfanya Waziri Jafo kurejesha Imani na Halmashauri hii kuwa wamejipanga kukamilisha jengo leo ndani ya muda kama alivyoagiza.

Akizungumza katika ziara hiyo Jafo amesema amefurahi kuona ujenzi wa Hospital ya Wilaya umefikia katika hatua nzuri na kuwataka watendaji wa Chamiwno kuendelea na kasi hiyo  ili Hospital hiyo iweze kumailika mapema na iwe yenye ubora wa hali ya juu.
“Leo naweza kuwapongeza mmefanya kazi kubwa ndani ya wiki moja niliyowapa sasa nataka ikifika tarehe 12 Mei majengo ya Hospital hii yawe yamefikia hatua siyo chini ya Lenta kwa majengo yote saba tayari kwa kuezeka na kuanzia tarehe 25 Mei majengo yote yawe yamepauliwa kwa Hospitali” alisisitiza Jafo.

Wakati huo huo Jafo ameugiza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kuanza kupanga Wilaya hiyo kwa mujibu wa sheria za mipango miji ili uweze kuendana na hadhi ya Makao Makuu ya Nchi.
“Chamwino iko karibu sana na Jiji la Dodoma na Jiji hivi sasa wanaenda kwa kasi sana katika upangaji wa maeneo, wanapima viwanja wanauza na wanaongeza mapato yao lakini sioni izo jitihada katika Wilayah ii na nyie ndipo sehemu ambapo Ikulu imejengwa mnatakiwa mjiongeze muanze kupima maeneo na kuuza ili muongeze na mapato ya Halmashauri yenu” alisema Jafo.

Aliongeza kuwa katika eneo hili la Mlowo ambapo hospital inajengwa mngenza kufanya mikutano na wananchi ili mkubalien utaratibu sahihi utakaotumika katika kupima maeneo ya wakazi lakini pia kutafuta maeneo ambayo Halmashauri inaweza kuyanunua, kuyapima na kuyauza kwa wahitaji; Mhakikishe mmetnga maeneo ya huduma za kijamii, makazi, biashara na uwekezaji hii itawasisia sana katika kuongeza mapato.

Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ilipata shilingi Bil 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospital ya Wilaya mapema mwezi Oktoba – Novemba, 2018 na mpaka sasa ujenzi huo unaendelea vizuri.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  Selemani Jafo akiwasili katika eneo la Mlowo inapojengwa Hospital ya Wilaya ya Chamwino kwa ajili ya ukaguzi wa majengo hayo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akikagua ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Chamwino wakati wa ziara yake Wilayani humo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo kitoa amelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Vumilia Boga pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndg. Athumani Masasi wakati wa ziara yake kukagua ujenzi wa Hospital ya Wilaya katika eneo la Mlowo.
Muonekano wa jengo mojawapo katika ya majengo saba yanayojengwa kwa ajili ya Hospital ya Wilaya ya Chamwino.

Elimu ya fedha, taarifa za mikopo ni muhimu-Gavana Luoga

$
0
0
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga, amesema elimu kuhusu masuala ya fedha ni muhimu katika mfumo mzima wa taarifa za mikopo ili kuwawezesha Watanzania kupanga matumizi bora ya mikopo.

Prof Luoga alitoa kauli hiyo katika uzinduzi wa kampeni ya uelimishaji umma kuhusu taarifa za mikopo na fedha iliyoratibiwa na BOT kwa kushirikiana na taasisi ya International Finance Corporation ambayo ni mwanachama wa Kundi la Benki ya Dunia.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mpango, Dk. Philip Mpango, Prof Luoga alisema taarifa za mikopo na elimu ya fedha ni muhimu ili kuhakikisha Watanzania wanaondokana na matumizi ya anasa ya mikopo.

“Kampeni hii ya elimu kwa umma inalenga kuwaelimisha watumiaji wa huduma za fedha na wadau wengine kukuza uelewa wao kuhusu taarifa za mikopo ili kuongeza ushiriki katika matumizi ya taarifa za mikopo hapa nchini,” alisema.

Aidha, Meneja Msaidizi, Mfumo wa Kumbukumbu za Wakopaji kutoka BoT, Nkanwa Magina alisema kampeni hiyo ya miezi mitatu inalenga kuongeza uelewa, mwamko kuhusu taarifa za mikopo na kukuza upatikanaji wa mikopo.

”Kauli mbiu katika kampeni hiyo ni: “Pata Taarifa Yako ya Mikopo Leo. Angalia hali yako ya kifedha ili kupanga mustakabali wako bora wa kesho” inaungwa mkono na wadau mbalimbali katika sekta ya huduma za fedha.

“Wadau hao wameahidi kusaidia kusambaza ujumbe kuhusu umuhimu wa upatikanaji wa mikopo na jinsi Watanzania wanavyoweza kuishi maisha bora kwa kuweza kupata taarifa za mikopo yao na kujua historia ya mikopo yao,” alisema.

Alisema usimamizi mzuri wa mikopo na historia nzuri ya mikopo ni muhimu katika kuwezesha kupata mkopo nafuu."Kuhakiki taarifa yako ya mikopo mara moja kwa mwaka ni huduma inayopatikana bila malipo, tena itakuletea mafanikio kwa kukuandaa vema utakapoenda kuomba mkopo. 

"Historia nzuri ya mikopo inaweza kusaidia kustahili viwango vya chini vya riba na ada, hivyo kuondokana na kutenga fedha kwa ajili ya dharura na gharama zisizotarajiwa," alisema. 

Alisema mikopo inasaidia kupata mahitaji ya sasa, kama vile nyumba au ada ya shule ya mtoto wako, kwa kuzingatia ahadi yako ya kulipa kwa awamu na kwa muda uliopangwa.Aidha, Meneja wa IFC - Tanzania, Manuel Moses alisema taarifa ya mikopo inaonesha taarifa binafsi; utambulisho na taarifa ya mawasiliano na ikiwezekana historia ya ajira; idadi na aina za akaunti za mikopo.

Naye Meneja Maendeleo ya Biashara kutoka Dun & Bradstreet, Josephine Temu alisema kwa sasa, kuna taasisi mbili zilizopatiwa leseni na Benki Kuu ya Tanzania kuandaa na kutoa taarifa za mikopo hapa Tanzania ambazo ni Creditinfo Tanzania Limited na Dun & Bradstreet.Alisema taasisi hizo zinakusanya na kutunza taarifa za mikopo na kutoa taarifa za mikopo kwa kampuni au watu wanaozihitaji kama vile benki. 

Alisema ripoti hiyo ya mikopo inaweza kutolewa na taasisi hizo (Creditinfo na Dun & Bradstreet) mara moja kwa mwaka bila malipo.“Ili kupata taarifa ya mikopo unatakiwa kuwasilisha nakala ya kitambulisho chako cha taifa au kingine kama leseni ya udereva, hati ya kusafiria. Jaza na wasilisha fomu ya maombi ya taarifa yako ya mikopo katika taasisi zinazoandaa taarifa za mikopo ambazo kwa sasa ni Creditinfo au Dun & Bradstreet," alisema.

Akifafanua kuhusu mambo muhimu ya kuangalia kwenye taarifa ya mikopo, Meneja Maendeleo ya Biashara kutoka Creditinfo, Tonny Missokia alisema muhimu ni taarifa binafsi kama vile jina, hadhi ya ndoa, anwani, taarifa za ajira na namba za mawasiliano ni sahihi.
 Meneja Msaidizi, Mfumo wa Kumbukumbu za Wakopaji kutoka BoT, Nkanwa Magina akizungumza katika warsha ya kuhusu elimu ya taarifa za fedha na ripoti za mikopo kwa wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma.
 Meneja Msaidizi, Mfumo wa Kumbukumbu za Wakopaji kutoka BoT, Nkanwa Magina akizungumza katika warsha ya kuhusu elimu ya taarifa za fedha na ripoti za mikopo kwa wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma.
 Wataalam wa Benki Kuu ya Tanzania, Creditinfo na Dun & Bradsheet wakitoa elimu kuhusu umuhimu wa taarifa za mikopo kwa mwananchi eneo la Nyerere Square mchana huu. Kampeni hiyo inaendeshwa kwa pamoja na Benki Kuu ikishirikiana na International Finance Corporation ambayo ni sehemu ya kundi la Benki ya Dunia

MENEJA TRA TEMEKE AIHIMIZA UTOLEWAJI WA RISITI KWA WAFANYABIASHARA, WANUNUZI

$
0
0
MENEJA wa Mamlaka ya Mapato  Tanzania (TRA) Wilaya ya Temeke Gamaliel Mafie anawakumbusha wafanyabiashara na wanunuzi kuendelea kujenga nidhamu ya kutoa risti na kudai risti pindi wanalifanya manunuzi. 

Amesema kuna adhabu kwa mtu ambaye hatoi na kudai risti na kimsingi adhabu yake ikibainika inafikia hadi shilingi milioni nne. na zaidi hivyo lazima mteja au mfanyabiashara atoe na kudai risti.

Mafie aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Temeke Dar es Salaam ambapo alisema imekuwepo na changamoto hiyo ya watu kushindwa kudai risti pindi wanapofanya manunuzi.

Amefafua kuwa Mara nyingi wafanyabiashara na hata wateja hawana tabia ya kudai risti na kutoa hivyo basi TRA inawakumbusha kutekeleza sheria na kushindwa kufanya hivyo nikosa kama alivyotangulia kusema .

Amesema pindi mteja anapopewa risti au kutoa risti hiyo imeunganishwa kwenye mfumo wa ndani wa TRA ambayo inawezssha kujua kwamba ameuza au hajauza.

Akizungumzia Utoaji wa elimu alisema wao kama TRA wanajitahidi kutoa elimu kwa wafanyabiashara na hivi sasa wanajipanga kutoa elimu kwa kina kutokana na mabadiliko ambayo yamefanyika kupitia Bunge.

Amesema kwa asilimia 77 wanatoa elimu na wanaendelea kutoa elimu hiyo na kusisitiza kuwa ulipaji wa kodi ni lazima kwa kila mtanzania kulipa kodi ili mambo mengine katika nchi yaende.

Meneja Mafie alisema wanakuwa na mahusiano mazuri na walipa kodi japo wakati mwingine kunakuwa na hali ya kukimbizana nakwamba hiyo inatokana na baadhi ya wafanyabiashara kukwepa kulipa kodi.

" katika jambo hili ndugu waandishi hapa nishauri Serikali kuona namna ya kuazisha elimu kupitia elimu ya msingi ili.mwanafunzi anapoendelea kupata elimu basi ajuwe ipasavyo kuhusu kodi." Alisema Meneja

Mmoja wa maofisa wanaotoa elimu ya huduma kwa mlipa kodi Paul Magembe alisema wanafanya kazi hiyo kwa kuwatembelea vikundi mbalimbali ili kuwapa elimu ili kuona umuhimu wa kulipa kodi katika jambo ambalo wanalifanya.

Meneja wa TRA Temeke Gamaliel  Mafie

WASANII WA MUZIKI WA DANSI,FILAMU WAWAOMBA WATANZANIA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII VILIVYOPO MAENEO MBALIMBALI NCHINI

$
0
0
Kiongozi wa wasanii wa kundi la uzalendo kwanza Steven Nyerere akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani leo jijini Dar es Salaam kuhusu  Wizara ya Utalii na bodi ya Utali kuendelea kuona mchango wa wasanii katika kuutangaza utalii. (Picha na Emmanuel Massaka,MMG).


*Lengo ni kujifunza,kuongeza pato la Taifa...Stive Nyerere asema Tanzania imebarikiwa

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

BAADA ya Tanzania kuwa ndio nchi ya kwanza duniani kuwa na vivutio vingi vya utalii, wasanii wa filamu na muziki wa dansi nchini, wanaounda kundi la wazalendo kwanza   wamewaomba wananchi  kutembelea vivutio hivyo kwa lengo la kujifunza na kukuza pato la Taifa

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutangaza hifadhi mpya tatu za utalii nchini, uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Wazalendo Kwanza, Steven Nyerere amesema ni muhimu kwa watanzania kutembelea vivutio hivyo vya utalii kwani watapata fursa kujifunza, kuona mambo ya kale pamoja na wanyama mbalimbali. 

Ameongeza kwani hifadhi mbalimbali za taifa zinapoingiza watatilii kutoka ndani na nje ya nchi, fedha zinazopatikana zinatumika katika maendeleo mbali mbali ikiwamo ujenzi wa hospitali, shule, viwanja vya michezo pamoja na  miundombinu ya barabara.

Amesema Tanzania ni nchi ambayo imebarikiwa katika masuala ya utalii kitu ambacho kinasababisha kuwepo kwa watalii wengi wakiwemo Wazungu ambao wengi wao wamekuwa wakipishana angani kuja nchini.

" Mbuga hizi za wanyama na vivutio vingine vya utalii vinapoingiza watalii tunapata fedha ambazo zinatumika katika maendeleo mbalimbali kama ujenzi wa hospitali na viwanja vya michezo," amesema.

Amefafanua hifadhi hizo mpya tatu ambazo ni Biharamulo ,Burugi na Kimisi ni moja kati ya vivutio vipya vya utalii nchini ambavyo vitakuwa vikitangazwa na kundi hilo la Wazalendo kwanza kwa lengo la kuhamasisha jamii na watalii kutoka nje ya nchi kuja kutembelea.

"Kampeni hii ya kutangaza vivutio hivi vipya itakuwa na mabalozi wanne ambazo ndio watatumika kutangaza, Sisi wazalendo kwanza ambapo pamoja na mabalozi hao wapya tutafanya ziara kwenda kuvitembekea  vivutio hivyo na na tutafika mpaka Chato pia na kwa mara ya kwanza jambo hili litakuwa na mvuto wa pekee," amesema.

Kwa upande wake Balozi wa Utalii nchini Nangasu Warema amesema vivutio hivyo vipya vitatangazwa ili kila mtanzania aweze kuvifahamu na kupata fursa ya kuvitembelea.

"Tumezindua rasmi kampeni ya kutangaza hifadhi hizi mpya ya Biharamulo, Burugi na Kibisi, tunawaomba wawekezaji waje kuwekeza kwa wingi katika hifadhi hizi kwani jambo hili lazima litawalipa tu," amesema.

KONGAMANO LA KARATE-JUNDOKAN ULAYA TANZANIA NDANI

$
0
0
Chama cha Karate mtindo wa “Okinawa Goju Ryu” shina la Jundokan lenye makao yake makuu Asato, mji wa Naha, kisiwa cha Okinawa, Japan, kwa mara nyingine tena, kimetoa mwaliko kwa mwakilishi wa tawi la chama hicho nchini Tanzania “Shibu-Cho Tanzania”, sensei Fundi Rumadha anaye shikilia ngazi ya Dan 4 kushiriki kongamano litalofanyika mjini Vienna, Austria julai 18 hadi 21, 2019. Tokea uteuzi wake kama mkuu wa chama hicho Tanzania, sensei Fundi ameweza kuwa pandisha ngazi wanafunzi wapatao 12 ngazi za Shodan na Nidan hapa Tanzania.

Kutokana na maelezo ya wenyeji wa kongamano hilo mkuu wa chama cha Jundokan Austria Dr. Friedrich Gsodam sensei mwenye kushikilia ngazi ya “Hanshi”, Dan 9, ambaye alijifunza Karate chini ya mwanzilishi wa chama hicho master Eiichi Miyazato tangu mwaka 1966, ameweza kukiri na kupendezwa na juhudi za sensei Fundi kuwasaidia wana Jundokan wa Tanzania kufikia ngazi za juu katika Sanaa hii ya Karate.

Viongozi wakuu wa chama hicho cha Jundokan na ujumbe wa Japan utaongozwa na mwenyekiti wake Kancho Yoshihiro Miyazato na ujumbe wa masters au magwiji wa Sanaa hiyo wakiwemo master Tetsu Gima Dan 9, na Sensei Yutaka Oshiro toka Okinawa, Japan. 
Tanzania, chini ya mkufunzi wake sensei Rumadha na Angola chini ya mkufunzi sensei Filomeno ni wataungana na masensei toka Afrika ya kusini, Madagascar, Israel, Argentina, Chile, na mataifa ya ulaya kama Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Poland, Ureno, Corscica, Italy, Urusi, Lithuania, Sweden, Azerbaijan, Scotland, Ireland na Hispania.

Waalikwa watawasili siku ya Alhamisi Julai 18, 2019 katika sehemu maalum ya kijitongoji cha Hollabrunn Vocationa College pembezoni mwa jiji la Vienna, Austria. Kongamano hilo la pekee bala la Ulaya, litafunguliwa kwa semina ya masensei wa matawi yote kwa marekebisho na usahihi wa mbinu tofauti na utumiaji mbinu za kujilinda ikiwemo kata za Sepai, Kururunfa, Sesan na Suparinpei.

Siku ya pili itafuatiwa na mafunzo yatayogawanywa kwa ngazi za mkanda mweupe hadi kahawia, kata za Gekisai dai ichi, Gekisai dai Ni, Saifa, Seiyunchin na Shisochin, na Sanseiru mikanda mieusi Shodan ha Sandan ngazi ya tatu, na hali kadharika nngazi ya nne hadi ya nane, Sanchin na Tensho kata. Nk.
Sensei Fundi anapenda kutoa shukrani zake kwa faraja ya kuwa mmoja ya walimu hao mahili kuhudhuria hayo makongamano muhimu katika ulimwengu wa Karate. Tayari sensei Fundi amesha pata fursa kubwa za kufanya mafunzi kama hayo na masensei au masters wakuu wa Jundokan Karate huko Leeds, UK, Lisbon, Ureno, Warsaw, Poland na hivi karibuni huko Okinawa, Japan. Pia vilevile, sensei Fundi ataelekea Warsaw, Poland akifuatana na mkewe kwa mwaliko maalum toka mkuu wa Jundokan Poland, sensei Monia Wysocka mwenye Dan 6.

“Lengo na tumaini la Jundokan Tanzania, ni kuwa na walimu wa ngazi za juu wa Karate walio mahili katika sanaa na wanaotambulika chini ya baraza la chama hicho huko Okinawa, Japan”, alisema sensei Fundi.

kesi ya uchochezi inayowakibili viongozi tisa wa Chadema yapigwa kalenda kwa mara nyingine

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa Mara nyingine tena imeshindwa kuanza kusikiliza kesi ya uchochezi inayowakibili viongozi tisa wa Chadema,  akiwemo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe kutokana na kutokuwepo mshtakiwa Dk Vicent Mashinji  ambaye yuko Mkoani Ruvuma anahudhuria kesi ya uchochezi inayomkabili  mahakamani huko.

Mapema, wakili wa utetezi, Profesa Abdallah Safari aliwasilisha barua ya udhuru ya Dk Mashinji mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa ambapo katika barua hivyo, mshtakiwa ameomba ruhusa kuwa yuko Songea anakabiliwa kesi ya uchochezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Songea.

Profesa Safari akisoma sehemu ya barua hiyo ameeleza kuwa kesi hiyo namba 9 ya mwaka 2017 imefika katika hatua ya utetezi na kwamba mshtakiwa Mashinji ameridhia kuendelea kwa usikilizwaji wa kesi inayomkabili katika Mahakama ya Kisutu.

Hata hivyo,  Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi amedai,  taarifa ya mshitakiwa haina vidhibitisho vya kutufanya sisi tukubaliane na hoja yao ya  kuendelea na kesi bila ya yeye kiwepo kwa sababu tangu tarehe ya mwisho ya kutajwa kesi hiyo ambayo inafika wiki mbili sasa mshtakiwa alikuwepo mahakamani . Tulitegemea mshtakiwa angeijuza Mahakama kuwa anakesi mahakama ya Songea.

Amedai ni vema mshtakiwa akatuambia kigezo gani ametumia asije kwenye mahakama hii na kwenda Songea

Aidha Wakili Nchimbi ameieleza  Mahakama kuwa, utaratibu wa kisheria  umeleelekeza kwenye sheria ya  mwenendo wa makosa ya jinai (CPA)  shauri lolote la jinai ikifika sehemu ya kuchukua ushahidi ni lazima ushahidi unapochukuliwa mahakami  uchukuliwe mbele mshtakiwa au washtakwa 

Amedai Licha ya  fungu la 197 (1b) sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai linatoa  mwanya kwa kutoa ushahidi isipokuwa mshitakiwa anapokuwa anamatatizo ya kiafya na awe anawakili pia awe ameridhia .

Amedai  suluhu pekee ni kuahirisha llshauri hilo na tarehe nyingine itakayopangwa mshtakiwa aje ajieleze kwa kina sababu za yeye kutofika mahakamani siku ya leo.

Kesi hiyo imeahirishwa  Mpaka kesho, Aprili 17.

Mbali ya Mbowe na Mashinji, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni,  Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu,  Mbunge wa Kibamba, John Mnyika,  Katibu Mkuu Taifa, Vicent Mashinji,  Mbunge wa Kawe,  Halima Mdee,  John Heche na Mbunge wa Bunda,  Ester Bulaya.

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, February 1 na 16, 2018, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.

SERIKALI ZA VIJIJI ZAKEMEWA KUUZA MAENEO YENYE MISITU -NDIKILO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA 

MKOA wa Pwani, umekemea serikali za vijiji zisiingilie kuuza maeneo yenye misitu hata kama hayajahifadhiwa kisheria na badala yake waisimamie na kuilinda. Aidha kila halmashauri imeelekezwa kuimarisha ulinzi wa raslimali za misitu ,ili kuhakikisha kunakuwa na usalama wa misitu na raslimali zake. 

Hayo yalibainishwa na mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga,kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo,   katika siku ya upandaji miti kimkoa iliyofanyika msitu wa Vikindu Mkuranga,wakati akisoma taarifa ya mkuu wa mkoa huyo .

Alisema, endapo maeneo ya msitu ama misitu ya hifadhi utavamiwa katika eneo la mwenyekiti ama mtendaji wa kijiji atawajibishwa kutokana na kutosimamia kikamilifu ulinzi na usalama wa misitu hiyo. 

Sanga alieleza misitu iliyopo kwenye ardhi huria (general land) inakatwa hovyo kutokana na maeneo hayo kutomilikiwa kisheria. Alieleza kwamba, serikali ya vijiji hutumia uwepo wa maeneo hayo kama fursa kwa kuuza maeneo na ardhi kwa wageni. 

Katika hatua nyingine alibainisha, wavamizi 4,500 waliovamia misitu ya hifadhi ya Kazimzumbwi, Ruvu Kusini, Uzigua, Masanganya, Namuete, Utete, Tamburu ,Mhoro mkoani Pwani wameondolewa.

"Kumekuwa na juhudi mbalimbali zilizofanyika hadi sasa, ambapo 2017 /2018 serikali kupitia wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) iliamua kuweka mipaka ya kudumu kuzunguuka maeneo ya misitu ya Kazimzumbwi, Mtanza Sona, Kipo, Namakutwa /Namuete na Uzigua kwa ajili ya kudhibiti uvamizi wa misitu hiyo jambo ambalo lilikuwa halijafanyika kipindi cha nyuma"alifafanua Sanga.

Hata hivyo alisema ,kila mwananchi anapaswa kuelewa umuhimu wa misitu, madhara ya ukataji miti kwa jamii na kwa vizazi vijavyo. 

Awali ofisa misitu Mkoani Pwani, Pierre Ntiyamagwa alisema, ongezeko kubwa la watu na ukosefu wa nishati mbadala kumetoa msukumo wa mahitaji makubwa zaidi ya mazao ya misitu hususan kuni, mkaa, mbao na maeneo ya makazi.

Akielezea kuhusu siku hiyo ya upandaji miti alieleza jumla ya miche 5,680 imepandwa .

Pierre alisema, mkoa huo una jumla ya misitu 87 yenye hekta 335,712 zilizohifadhiwa kisheria na hekta milioni 2.2 za misitu kwenye ardhi huria kati ya hiyo misitu 27 inasimamiwa na serikali kuu chini ya wakala wa huduma za misitu na misitu 57 iko kwenye hifadhi za vijiji. 

Jumia rasmi yaorodheshwa kwenye Soko la Hisa la New York, Marekani

$
0
0
  Pichani kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadock Prescott aakifafanua jambo leo mbele ya Waandishi wa Habari namna walivyojiunga na Soko la Hisa la New York na kuwa kampuni ya kwanza kabisa ya kiteknolojia kuanzishwa Afrika kufanya hivyo, akaongeza na kubainisha kuwa wanataka kuonyesha Dunia ubunifu wa kidigitali unaotokea Afrika na fursa kutoka Afrika kwa upande wa teknolojia na biashara ya mtandaoni,pichani kushoto ni  Meneja Uhusiano wa Umma na Masoko, Jumia Travel Tanzania, Geofrey Kijanga
kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za uuzaji na manunuzi kwa njia ya mtandao, imetangaza rasmi kuwa imeorodheshwa katika Soko la Hisa la New York nchini Marekani. Kuorodheshwa huku ni matokeo ya mafanikio ya timu nzima, wafanyakazi wote wa Jumia Afrika nzima. Tukio hili lilisherehekewa kwa ishara ya kupiga kengele kwenye kila nchi ambapo Jumia inafanya shughuli zake muda sawa sawa na jijini New York.

Ikiwa imeanzishwa mwaka 2012, Jumia ilianza mkakati wa kuboresha maisha ya kila siku barani Afrika, kwa kutumia teknolojia kuleta ubunifu, urahisi na unafuu wa upatikanaji wa huduma kwa wateja. Jumia pia inaziwezesha biashara kukua, kwa kutumia jukwaa ililonalo kuwafikia na kuwahudumia wateja barani kote Afrika. 

Kwa sasa, Jumia inafanya shughuli zake katika nchi 14 ikiwa na wauzaji takribani 81,000 wakiwa wanafanya biashara na mamilioni ya wateja. Jukwaa la biashara kwa mfumo wa mtandaoni limetoa ajira za moja kwa moja kwa wafanyakazi takribani 5,000 Afrika.

“Mafanikio haya kwa kiasi kikubwa yamefanikishwa na bidii ya timu yetu, imani ya wateja wetu, pamoja na kujitolea kwa wauzaji na washirika wetu. Wadau wetu wote wanastahili pongezi kwa hatua hii muhimu, na ndiyo kwanza tuko mwanzoni mwa safari ndefu na kubwa. 

Tutaendelea kujikita zaidi kwenye azma yetu na kufanya kazi kwa bidii zaidi kuwasaidia wanunuzi, wauzaji, washirika na wadau wote wanaofaidika na mapinduzi ya kiteknolojia,” walisema Sacha Poignonnec na Jeremy Hodara ambao ni waanzilishi na Wakurugenzi Wakuu ambao walikuwepo jijini New York, nchini Marekani wakati wa kufanyika kwa tukio hilo.
Akielezea sababu zilizopelekea mpaka Jumia kujiunga na Soko la Hisa kubwa zaidi duniani, Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadock Prescott amebainisha kuwa, “kwa kujiunga na Soko la Hisa la New York na kuwa kampuni ya kwanza kabisa ya kiteknolojia kuanzishwa Afrika kufanya hivyo, tunataka kuonyesha dunia ubunifu wa kidigitali unaotokea Afrika na fursa kutoka Afrika kwa upande wa teknolojia na biashara ya mtandaoni.”

“Jumia kuorodheshwa rasmi kwenye Soko la Hisa la New York ni ishara kwamba kuna ubunifu unatokea barani Afrika - inaionyesha Afrika kuwa ni bunifu, inabadilika na kuwa ya kisasa zaidi. Hatua hii muhimu itatusaidia kuwavutia wauzaji wengi zaidi kwenye mtandao wa Jumia. 

Kwa sababu wauzaji na washirika wengi bado hawajatufahamu vizuri, na pindi wakitujua, tunaamini kuwa watatamani kufanya kazi na sisi,” alisema Bw. Prescott na kuhitimisha kuwa, “Tunaamini pia hii itatusaidia kujenga uaminifu zaini na wauzaji wetu, hususani kwa wale ambao bado hawajaanza kuzoea mfumo wa mtandaoni, wengi sasa watatuona kama kampuni imara na, tunaamini itatusaidia kwenye ukuaji na wateja kukubali huduma zetu. Hivyo basi, ningependa kuchukua fursa hii kuishukuru timu nzima kwa kufanya kazi kwa bidii, kujitolea kwa wauzaji na washirika pamoja na imani kutoka kwa wateja wetu.” 


JAPAN KUIPIGA JEKI TANZANIASHILINGI BILIONI 794 KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) kushoto, akiwa pamoja na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japani-JICA, Bw. Hiroshi Kato, walipokutana na kufanya mazungumzo kwenye Ofisi za ubalozi wa Tanzania mjini Washington DC-Marekani, kando ya Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la KImataifa-IMF
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) kushoto, akiwa pamoja na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japani-JICA, Bw. Hiroshi Kato, walipokutana na kufanya mazungumzo kwenye Ofisi za ubalozi wa Tanzania mjini Washington DC-Marekani, kando ya Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, ambapo JICA imeahidi kutoa ruzuku na mikopo yenye masharti nafuu ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania.

Na Benny Mwaipaja, WFM, Washington D.C

 Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa-JICA inakusudia kuipatia Tanzania mkopo nafuu pamoja na ruzuku wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 345 za Marekani, sawa na takriban shilingi bilioni 794, kwa ajili ya kutekeleza miradi mitatu ya maendeleo ikiwemo ukarabati wa barabara ya Arusha hadi Holili, ukarabati wa Bandari ya Kigoma na Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Visiwani Zanzibar.

Ahadi hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la JICA anayesimamia Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara Bw. Hiroshi Kato, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Mjini Washington D.C nchini Marekani.

Ameitaja miradi hiyo iliyoko mezani kwao inayosubiri kupatiwa fedha wakati wowote kuanzia sasa kuwa ni mradi wa ukarabati wa barabara ya Arusha-Holili utakaopatiwa mkopo wa dola milioni 221, Mradi wa maji safi na usafi wa mazingira Zanzibar utakaopatiwa fedha kupitia mkopo wa dola milioni 99 na mradi wa upanuzi wa Bandari ya Kigoma ambao Japan itatoa ruzuku ya dola za Marekani milioni 25.

Bw. Kato amesema kuwa Japan inajivunia ushrikiano wa muda mrefu kati yake na Tanzania na kwamba iko tayari kusaidia juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kuwaletea wananchi wake maendeleo na kuitaka Serikali kuwasilisha miradi yake ya kimkakati ambayo Japan itafadhili kupitia mikopo yenye riba nafuu pamoja na ruzuku.

Akizungumza na Mwakilishi huyo wa Japan katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameishukuru Japan kwa uhusiano wake mzuri na Tanzania na namna inavyo isaidia nchi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo akitaja mmoja wa miradi hiyo kuwa ni barabara ya juu ya kwanza nchini Tanzania  katika makutano ya Tazara Jijini Dar es Salaam, maarufu kama Daraja la Mfugale.

Dkt. Mpango ameiomba Japan kupitia Shirika lake la JICA kutoa ruzuku na mikopo nafuu ili kutekeleza miradi ya kimkakati ya ujenzi wa reli ya kisasa kwa kiwango cha kimataifa - SGR, Mradi wa kufua umeme wa Rufiji, Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato mkoani Dodoma, ujenzi wa barabara za mzunguko jijini Dodoma, ujenzi wa mtandao wa barabara, upanuzi wa bandari na miradi mingine ya kijamii.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mikutano ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, inayofanyika mjini Washington DC nchini Marekani, ambapo ametumia fursa hiyo kukutana na wadau wa maendeleo kupenyeza ajenda za maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania.

TRA YAKUSANYA BILIONI 42.8 KWA MWEZI MACHI 2019 KUFUATIA UTEKELEZAJI WA STEMPU ZA KODI ZA KIELETRONIKI

$
0
0
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TRA jijini Dar es Salaam kuhusu mamlaka hiyo kukusanya ushuru wa bidhaa Shilingi billioni 42.8 kwa mwezi machi 2019 ukilinganisha na shilingi bilioni 39.3 zilizokusanywa kipindi kama hicho mwaka 2018 ambapo ongezeko hilo limetokana na utekelezaji wa Mfumo wa Stempu za Kodi za Kielektroniki uliotozwa kwenye Sigara, Mvinyo, Pombe Kali, Bia na aina zote za vileo ambao ulianza rasmi tarehe 15 Januari, 2019. Wengine katika picha ni Bw. Abdul Mapembe Kamishna wa Kodi za Ndani (kushoto) na Bw. Richard Kayombo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi (kulia).

Na Veronica Kazimoto, Dar es Salaam

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya ushuru wa bidhaa shilingi bilioni 42.8 kwa mwezi Machi, 2019 ukilinganisha na shilingi bilioni 39.3 zilizokusanywa kipindi kama hicho mwaka 2018 ambacho ni sawa na ongezeko la shilingi bilioni 3.5 au ukuaji wa asilimia 9.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo Charles Kichere amesema kuwa, ongezeko hilo limetokana na utekelezaji wa Mfumo wa Stempu za Kodi za Kielektroniki uliotozwa kwenye Sigara, Mvinyo, Pombe Kali, Bia na aina zote za vileo ambao ulianza rasmi tarehe 15 Januari, 2019.

“Mfumo huu mpya wa stempu za kielektroniki umeonyesha mafanikio makubwa sana. Mwezi Machi mwaka huu tumekusanya ushuru wa bidhaa jumla ya shilingi bilioni 42.8 kutoka kwenye sigara, mvinyo, pombe kali, bia na aina zote za vileo wakati mwaka jana kipindi kama hicho tulikusanya shilingi bilioni 39.3. Kiwango hiki kinatarajiwa kuongezeka maradufu kwani idadi ya viwanda vinavyoendelea kufungiwa mfumo huu mpya vinazidi kuongezeka”, alisema Kichere.

Kichere ametolea mfano wa mzalishaji wa pombe kali aliyekuwa akilipa ushuru wa bidhaa kati ya shilingi milioni 140 hadi 160 kwa mwezi lakini baada ya kufunga mfumo wa stepu za kielektroniki amelipa shilingi milioni 274.

“Pia wapo waliokuwa wanalipa kati ya shilingi milioni 20 hadi 30 lakini kwa sasa wanalipa shilingi milioni 85 hadi 172 kwa mwezi,” aliongeza Kichere.

Alibainisha kuwa, mfumo wa stempu za kodi wa kiektroniki unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza inahusisha bidhaa za sigara, mvinyo, pombe kali, bia na aina zote za vileo wakati awamu ya pili ikihusisha bidhaa za vinywaji baridi, maji, juisi na CD/DVDs ambapo kwa sasa TRA inatekeleza awamu ya kwanza ambayo ilianza rasmi tarehe 15 Januari, 2019 na awamu ya pili itaanza rasmi tarehe 01 Mei, 2019.

“Kama nilivyotangulia kusema kuwa, sasa hivi tuko kwenye utekelezaji wa awamu ya kwanza, hivyo basi bidhaa zote za awamu hii ambazo ziko sokoni na zimebandikwa stempu za zamani na zile ambazo hazijabandikwa stempu za ushuru wa bidhaa kabla ya kuanza kwa mfumo huu wa stempu za kielektroniki, zinaruhusiwa kuendelea kuwepo sokoni hadi tarehe 30 Aprili, 2019, na baada ya hapo zitatakiwa kubandikwa stempu za kodi za kielektroniki kabla ya kuuzwa”, alisema Kichere.

Awali, Kamishna mkuu huyo alizitaja changamoto za stempu za kodi za karatasi zilizopelekea kuanzishwa kwa stempu za kodi za kielektroniki. Alisema changamototo hizo ni pamoja na upotevu wa mapato ya Serikali kutokana na udanganyifu katika taarifa za uzalishaji zinazotolewa na wazalishaji pamoja na kuibuka kwa wimbi la wadanganyifu waliotumia madhaifu ya mfumo wa stempu za karatasi na kuiibia Serikali kwa kutengeneza stempu za kughushi.

Changamoto nyingine ni uwezekano mdogo wa kutambua stempu za kughushi unaochangia uwepo wa bidhaa zisizokidhi viwango vya ubora na zinazoweza kuathiri afya za binadamu pamoja na kutokuwa rahisi kutambua uhalali wa bidhaa iliyoko sokoni kuwa imetengenezwa na mzalishaji halali wa bidhaa hiyo.

Kwa upande wa faida za mfumo wa stempu za kodi za kielektroniki, Kamishna Mkuu Kichere amesema kuwa ni pamoja na kuongeza mapato yanayotokana na ushuru wa bidhaa, kuondoa malalamiko ya kutokutendewa haki ya makadirio ya kodi zinazosimamiwa na TRA, kuwezesha ufuatiliaji wa bidhaa kutoka viwandani, mipakani, bohari zilizoruhusiwa, majengo ya kutunzia bidhaa, sokoni hadi kwa mlaji na kuiwezesha Serikali kutambua mapema kiasi cha ushuru wa bidhaa kitakacholipwa.

Faida nyingine ni kuziba mianya ya uingizaji bidhaa kiholela nchini ambazo hazijalipiwa ushuru stahiki, kuongeza uhiari wa ulipaji kodi kwa kutengeneza wigo sawa wa ushindani baina ya wazalishaji na waingizaji wa bidhaa hususan kwa zile zilizopo sokoni na zinazopaswa kubandikwa stempu za kodi za kielektroniki na kulinda afya ya mlaji kwa kumuwezesha mtumiaji au msambazaji kutambua bidhaa yenye stempu halali na isiyokuwa halali.

Ushuru wa bidhaa unatozwa kwa mujibu wa kifungu cha 124 cha Sheria ya Ushuru wa Bidhaa Sura ya 147 inayoainisha aina za bidhaa zinazotozwa ushuru huu kwa mujibu wa Jedwali la nne (4) la sheria hii sambamba na marekebisho yanayofanyika kupitia Sheria ya Fedha.

Kufuatia sheria hiyo, Kanuni za Stempu za Kodi zilitungwa ili kuhakikisha kuwa, utaratibu wa kutambua kiwango cha uzalishaji na uingizaji wa bidhaa nchini unakuwa ni wa uwazi na unafuatwa kwa lengo la kutoza kodi stahiki.

NGOs ZATAKIWA KUJIKITA KATIKA MIRADI YENYE TIJA NA MASHIKO

$
0
0
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini  bado hayajaonesha uwiano wa fedha zinazotumia na matokeo tarajiwa ya miradi mbalimbali zinazotekeleza kwani zimejielekeza zaidi katika kujenga uwezo na kutumia muda mwingi katika vikao badala ya miradi yenye tija.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema hayo katika hotuba yake wakati akifungua Bodi ya Uratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali leo Jijini Dodoma na kuyataka Mashirika hayo kuangalia miradi inayoleta matkeo chanya badala ya kutumia fedha nyingi katika kujengeana uwezo.

‘’Unakuta Mashirika mengine yanatoa matangazo ya kila dakika katika vyombo vya habari mfano kuhusu Afya ya Mama na Mtoto wakati unbakuta maeneo fulani ya Nchi wakina mama hawana vituo vya Afya, tumieni fedha izo kujenga vituo vya Afya badala ya kufanya vikao na miradi ya kujengeana uwezo’’ Alisema Waziri Mwalimu.

Aidha Waziri Mwalimu amezitaka NGOs kuzingatia misingi ya uwajibikaji na uwazi kama ilivyoanishwa katika Sheria ya NGOs pamoja na Kanuni zake lakini pia ameyataka Mashirika hayo kuhakikisha yanazi ngatia vipaumbele vya Serikali ili kutoa huduma muhimu katika  Maeneo yenye mahitaji.

Aidha Waziri Mwalimu ameitaka Bodi mpya ya Uratibu wa  NGOs itambue kuwa maamuzi watakayoyafanya kuwa ni  maamuzi ya Serikali na kuhakikisha pia wanatenda haki na kuzishughulikia NGOs zinazofanya kazi kinyume na Sheria ya NGOs na Kanuni zake lakini pia kukutana na wawakilishi wa NGOs na kujadiliana nao kuhusu masuala yao.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu ameitaka Bodi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutambua kuwa wanakazi kubwa ya kufanya kwa kuwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanatofautiana kiutendaji na mengine yanajihusisha katika mambo yasiyofaa kwa mujibu wa Sheria.

‘’NGOs nyingine zina fedha nyingi, nyingine zinajihusisha na utafiti, utoaji fedha lakini pia zipo ambazo zinajihusisha na vitendo vya ovyo kwahiyo mnakazi kubwa ya kufanya kwa kuwa mmeaminiwa na Taifa kupewa dhamana ya kusimamia NGOs hapa Nchini.’’Aliongeza Dkt. Jingu.

Dkt Jingu ameongeza kuwa Sekta ya NGOs ni Sekta kubwa na pana na muhimu kwa Taifa kwa kuwa inahusisha Mashirika ya Kitaifa na Kimataifa na Mashirika haya ni takribani 8,310 na yanafanya kazi mbalimbali ikiwemo kufanya kampeni za kuleta mabadiliko.

Wakati huohuo  Mwakilishi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya Kitaifa Bw. Ngunga Tepani amesema kwa sasa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanapatia changamoto nyingi sana zikiwemo za kisera na kiutekelezaji na hivyo kuiomba Bodi mpya kutoa huduma kwa mashirika hayo kwa kuyasimamia vema ili yaweza kuwa Sekta inayokua badala Sekta inayoanguka.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amezindua Bodi ya Nne ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kufuatia hatua ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumteua Dkt. Richard Faustine Sambaiga kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo na kuteuliwa kwa wajumbe wa Bodi.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akijadiliana jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Uratibu wa NGOs.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Watoto akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Uratibu wa NGOs.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Uratibu wa NGOs.
  Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Neema Mwanga akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Uratibu wa NGOs.
 Baadhi ya Wajumbe wa Bodi mpya ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na wadau wa NGOs wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Uratibu wa NGOs.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapya wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali mara baada ya uzinduzi wa Bodi hiyo. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

PSSSF Yawalipa Wastaafu 9900

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Mfuko mpya wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF umekamilisha kulipa malimbikizo ya deni la wastaafu wapatao 9971 lililorithiwa kutoka katika mfuko wa PSPF.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Mussa Sima alipokuwa akimuwakilisha Waziri mwenye dhamana ya Mifuko ya Jamii kujibu swali la Mbunge wa Mbozi, Mhe. Paschal Haonga lililohoji juu ya muda gani wastaafu katika Halmashauri za Wilaya nchini watalipwa fedha zao.

Sima amesema kuwa mfuko huo umekamilisha mfumo wa ulipaji mafao utakaowezesha kufanya malipo katika ngazi ya Mkoa na hivyo kuwezesha mfuko kulipa mafao ndani ya muda uliowekwa kisheria wa siku 60 tangu mwanachama anapowasilisha madai.

"Hadi kufikia Februari 2019, mfuko wetu umetoa kiasi cha shilingi Bilioni 888.39  kwa ajili ya kuwalipa wastaafu waliotoka katika mfuko wa PSPF", alisema Sima.

Akizungumzia kuhusu tetesi za Serikali kutumia vibaya fedha za PSPF, Sima amesema kuwa mifuko hiyo inaendeshwa kwa mujibu wa Sheria ambayo inasimamia muundo wa utawala na mfumo wa maamuzi na usimamizi wa uwekezaji wa fedha za mfuko, hivyo, si kweli kwamba Serikali inaweza kuingilia uendeshaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii au kufanya maamuzi ya uwekezaji.

Aidha, Sima amefafanua kuwa sheria za mifuko hiyo  chini ya Kanuni Namba 24 na 25 ya Kanuni mpya za Mafao ya Hifadhi ya Jamii za Mwaka 2018 zimetoa wigo mpana zaidi kwa wanachama waliochangia kwa miaka isiyopungua 10 kuweza kupata huduma hiyo tofauti na awali.

Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa mifuko hiyo inaendelea kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wanachama wake kupitia vikundi vya kuweka na kukopa katika maeneo ya kazi, mifuko hiyo inaweza kutoa mikopo kwa SACCOs hadi asilimia 10 ya rasilimali za mfuko.

MHITIMU AVAMIA MTANDAO WA SERIKALI NA KUJIAJIRI KWA DONGE NONO

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
BRIGHT CHABOTA mhitimu wa chuo aliyesomea masuala ya TEHAMA kutoka nchini Afrika Kusini anasakwa na polisi nchini humo kwa tuhuma za kudukua tovuti ya serikali na kujiajiri huku akijilipa mshahara wa donge nono.

Chabota alidukua data za serikali na kujiajiri katika sekta ya afya huku akipokea mshahara bila kufanya kazi kwa miezi 9 kuanzia mwezi Juni mwaka uliopita.

Kijana huyo aligundulika baada ya serikali kukosa rekodi ya malipo kutoka kwake zikiwemo ada ya bima za matibabu hata wazazi wake walipohojiwa walieleza kuwa mtoto wao ameajiriwa na serikali na amekuwa akiwatumia fedha za matumizi. 

Imeelezwa kuwa Chabota alikuwa akijilipa randi 7000 kwa mwezi ambazo ni sawa na shilingi milioni 1.2 kwa mwezi bila kufanya kazi.

Je, udukuzi huu wa Chabota ambaye baba yake ni raia wa Zambia na mama yake akitokea Afrika kusini ni suluhisho kwa vijana waliokosa ajira? nini kifanyike kuhusiana na utaalamu alioufanya kijana huyu?

TAARIFA KWA UMMA

MATAJIRI WAJITOKEZA KUKARABATI KANISA KONGWE LENYE MIAKA 850 LILILOTEKETEA KWA MOTO NCHINI UFARANSA

$
0
0
 Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MAMLAKA ya Zimamoto ya Jiji la Paris imetangaza kuwa wamefanikiwa kudhibiti moto uliokuwa ukiwaka katika jengo la kanisa la kale la Notre Dame. Ingawa bado kuna moto unaendelea kuwaka katika paa moja wapo la jengo hilo maarufu la utamaduni.
Moto uliolipuka na kushika paa lililoezekwa kwa mbao ulienea kwa masaa manne huku ukiharibu kabisa upande wa juu wa ghorofa wenye urefu wa mita 93.
Wazima moto takribani 400 wamehusika katika kuzima moto huo, huku maji ya kuzima moto yakimwagwa kwa njia ya anga ili kuokoa jengo hilo lenye miaka 850 tangu kujengwa.
 Shirika la utangazaji la Al Jazeera limeripoti kuwa, Mkuu wa kitengo cha zimamoto Jean-Claude Gallet ameeleza kuwa eneo kubwa la kanisa limeweza kuokolewa na kwamba hata mnara wa kengele ambao ndio ulikuwa hatarini kufikiwa na moto upo salama.

Vyombo vya habari vya Ufaransa vimeeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa moto umetokana na shughuli za ukarabati zilizokuwa zinaendelea kwenye jengo hilo la kihistoria. Ofisi ya Upelelezi ya Paris imeeleza inaendesha uchunguzi juu ya sababu ya kutokea kwa moto huo.

Msinyori Patrick Chauvet ameeleza sehemu kubwa ya kuvutia ya jengo imeweza kubaki salama.

 Rais wa Ufaransa Macron Emmanuel ameeleza kuwa, ‘Kwa kiwango kikubwa uharibifu haujatokea, ingawa vita vya moto hivi havikushindwa kwa ukamilifu wake’. Ameitaja Notre Dame kama kiini cha maisha ya wafaransa. Hivyo ametoa wito kulijenga upya jengo hilo.
‘Ni jambo ambalo lilitegemewa na wafaransa, hii ilistahili kuhifadhi historia yetu! Ni sehemu ya mwisho kujivunia’ alieleza waandishi wa habari.

Wakazi wa Paris na watalii walijikusanya kutazama tukio hilo la kuogofya likiendelea karibu na kingo za mto Seine huku wahudumu wa dharura wakizima moto. Jengo hilo lilikuwa kwenye ukarabati wa gharama ya dola milion 6.8.
Msemaji wa kanisa amesema kuwa eneo lote lililokuwa na mbao zilizoezekwa karne ya 12 limeungua.

Wakazi wa karibu na jengo hilo waliondolewa kama tahadhari ikitokea jengo hilo likiangushwa na moto uliokuwa unawaka katika jengo la kanisa ameeleza Meya wa paris,  Anne Hidalgo.

Mashuhuda walikuwa wakilia kuona jengo hilo linaungua. Na tahadhari imetolewa kwa wote wanaopita karibu na jengo la kanisa.

Inasikitisha kuona jengo hili likiwaka moto, Kanisa hili ni alama ya jiji la Paris duniani kote! Mtoto Claire, ameeleza "Notre Dame ni moyo wa Paris na niliposikia tu jengo linawaka moto nikajiuliza tutabaki na nini?" Alieleza

Jengo hilo limekuwepo tangu wakati wa vita vya kidini, miaka zaidi ya 850 iliyopita lilianza kutumika na tayari matajiri wawili nchi Ufaransa  wanatoa euro milioni 300 kulitengeneza kanisa hilo. Bilionea Francois-Henri Pinault anatoa euro milioni 100, huku bilionea Benard Arnault akitoa euro milioni 200.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRIL 17,2019

SERIKALI YAANDAA MPANGO MAALUM KUIMARISHA WAWEKEZAJI

$
0
0

Na Grace Semfuko-MELEZO


Serikali inaandaa Mpango Maalum wa kuimarisha na kuongeza wawekezaji katika sekta mbalimbali ikiwepo ya mifugo na Kilimo ili kuongeza upatikanaji wa nyama,siagi na Maziwa pamoja na Chakula nchini.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Uwekezaji Angela Kairuki amesema Mpango huo unaanza na kuzungumza na wawekezaji katika nchi mbali mbali duniani ambao wana uwakilishi wa kibalozi nchini Tanzania.


Kairuki aliyasema hayo ofisini kwake jijini Dar Es Salaam mara baada ya kufanya mazungumzo na mabalozi watatu wanaoziwakilisha nchi zao akiwepo Balozi wa Afrika Kusini Bw.Thamsanqa Dennis Mseleku, Balozi wa Ilerand Be.Paul Sharlock na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bi Imni Paterson ambao kwa nyakati tofauti wamemweleza Waziri kuwa wamekuwa na Mpango madhubuti wa kuongeza wawekezaji Binafsi ili kuinua uchumi na kuongeza ufanisi wa bidhaa za viwanda.


Kairuki alisema Serikali inaandaa mikutano mikubwa na wawekezaji wa nchi hizo Jijini Dar Es Salaam ambapo ataanza na wawekezaji wa China utakaofanyika April 17 mwaka huu ukihusisha pia taasisi mbali mbali za Serikali zinazosaidia uwekezaji ili kuangalia fursa,kushauriana na kusikiliza changamoto za Uwekezaji nchini.


Kwa upande wake Balozi wa Ireland nchini Tanzania Bw. Paul Sharlok alisema nchi yake inaendelea kuhamasisha wawekezaji na kutangaza vivutio vyilivyopo Tanzania ambapo katika mkutano Mkubwa wa Kiuchumi wa Ireland na Afrika  unaofanyika mara moja kwa miaka miwili kwa mwaka jana walipendekeza kuwekeza kwenye sekta ya kilimo Biashara na kuwaunganisha wawekezaji wa Ireland na Tanzania katika kufanya kazi pamoja.


"Sisi Ireland tuna Mpango maalum kuhusu uchumi wa Afrika, kila baada ya miaka miwili tunakuwa na mkutano Mkubwa wa kiuchumi wa Ireland na Afrika, mwaka Jana tulizungumzia Kilimo Biashara na tuliweza kuwaunganisha wafanyabiashara wengi wa Tanzania, mwakani tutafanya mkutano huo natumaini sekta Binafsi na Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC watashiriki" alisema Balozi sharlock.


Nae Balozi wa Marekani nchini Tanzania Imni Paterson alisema kwa muda mrefu Marekani imekuwa na mikakati mingi ya kiuchumi kuhusu Tanzania, wataiendeleza mikakati hiyo na pia wataanzaa mkutano wa pamoja baina ya Wizara ya Uwekezaji na wawekezaji wa kimarekani ili kupata majadiliano ambayo yatasaidia pande zote.
Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angellah Kairuki akifafanua jambo kuhusu sekta ya uwekezaji nchini kwa Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania, Frederic Clavier alipomtembelea leo Ofisini Kwakwe Jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu, Angellah Kairuki akifafanua jambo kuhusu sekta ya uwekezaji nchini kwa Balozi wa Norway nchini, Elisabath Jacobsen walipokuatana leo Ofisini Kwakwe Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu, Angellah Kairuki akifafanua jambo kuhusu sekta ya uwekezaji nchini kwa Balozi wa Norway nchini, Elisabath Jacobsen walipokuatana leo Ofisini Kwakwe Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angellah Kairuki, akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo kutoka Marekani USAID, Andy Karas katika mazungumzo mafupi yalifanyika Ofisini Kwakwe Jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angellah Kairuki akizungumza na Balozi wa Uholanzi nchini, Jeroen Verheul, alipomtembelea Ofisini Kwakwe Jijini Dar es Salaam. (Picha na Paschal Dotto-MAELEZO)


Waziri Kairuki Akutana na Mabalozi wa Nchi Tatu Kuzungumzia Uwekezaji.

$
0
0

Na.Paschal Dotto-MAELEZO.

Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angellah Kairuki ameanza kukutana na wawekezaji kutoka balozi za Ufaransa, Uholonzi, Norway na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Marekani, USAID, mazungumzo mafupi baina wao yamefanyika leo kwa wakati tafaouti, huku Waziri Kairuki akisema kuwa mazungumzo hayo yalilenga kuongeza ushirikiano katika sekta ya uwekezaji nchini.

Katika mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini, Frederic Clavier, Waziri Kairuki alisema kuwa nchi ya ufaransa na Tanzania zina ushirikiano wa muda mrefu katika sekta mbalimbali ikiwemo ya uwekezaji pamoja na biashara.

“tulikuwa na mazungumzo na Balozi wa Ufaransa ambaye tumejadili mambo mbalimbali katika ushirikiano wetu, ili kuwaita wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Ufaransa waje nchini kama ilivyokuwa mwaka jana,” alisema Waziri

Akitoa mfano Waziri Kairuki alisema kulikuwa na ugeni wa wawekezaji na wafanyabiashara kutoka huko Ufaransa na walifanya majadiliano na Tasisi ya uwekezaji nchini, TPSF, akasema, “kwa hiyo na mwaka huu tumekubaliana watawaalika tena TPSF na TIC (Kituo cha uwekezaji) ili kuweza kujadili mambo ya uwekezaji”.

Kukutana na wawekezaji hao kutoka nchi mbalimbali Waziri Kairuki amesema kutabainisha fursa kadhaa na kufuatilia changamoto ili uwekezaji mkubwa uweze kufanyika nchini, pia Waziri Kairuki alieleza kuwa wamekubaliana na Balozi wa Ufaransa kuwa na ugeni mkubwa wa wawekezaji kati ya mwezi Mei na Septemba ambao watakuja kuwekeza katika sekta ya kilimo.

Aidha, Waziri Kairuki alimhakikishia Balozi wa Ufaransa kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji kwa kuendelea kuwajengea mazingira na hivyo kuhimiza wawekezaji kutoka Ufaransa kuongezaka nchini kutoka 40 waliowekeza kwa sasa.

“Uwekezaji unaongeza pato letu, unaongeza fedha za kigeni, ajira pamoja na masuala mengine katika uchumi, katika hili Ufaransa wamesema wako tayari kuanzisha jukwaa la biashara kwa wafanyabiashara kutoka Tanzania na Ufaransa ili kuweza kuvutia zaidi wawekezaji”, Waziri Kairuki.

Aidha, Balozi Clavier aliongeza kuwa Serikali ya Ufaransa inaridhishwa na jitihada za Rais Magufuli na kuwa nchi yake ilikuwa inachangia maendeleo ya nchi Euro milioni 50 kwa mwaka na imeongeza mpaka kufika Euro milioni 100, ambazo zitatumika katika uwekezaji mbalimbali hapa nchini ikiwemo Sekta ya mafuta, Viwanda vya Dawa na kilimo.

Katika mazungumzo mengine na Mabalozi wa Uholanzi, Jeroen Verheul, Norway, Elisabeth Jacobsen pamoja na Mkurugenzi Mkazi USAID, Andy Karas, Waziri Kairuki amewahakikishia kuwa atakutana na wawekezaji kutoka nchi hizo, kuwasikiliza changamoto zao na kuzitatua ili kuimarisha sekta ya uwekezaji nchini.
Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu, Angellah Kairuki akifafanua jambo kuhusu sekta ya uwekezaji nchini kwa Balozi wa Norway nchini, Elisabath Jacobsen walipokuatana leo Ofisini Kwakwe Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Ndumbaro afanya mazungumzo na balozi wa Italia nchini

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Damas Daniel Ndumbaro(Mb.), amefanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini, Mheshimiwa Roberto Mengoni katika ofisi za wizara Dodoma. Katika mazungumzo hayo, miongoni mwa mambo mengine, Tanzania na Italia zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika sekta za uwekezaji, utalii pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia. 
Mazungumzo yakiendelea. 
Msaidizi wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Charles Faini (wa kwanza na kulia) na Afisa wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Kisa Mwaseba (wa mwisho kushoto), wakifuatilia mazungumzo baina ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro(Mb.) na Balozi wa Italia nchini, Mhe Roberto Mengoni. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (Mb.) na Balozi wa Italia nchini, Mhe Roberto Mengoni, wakiagana mara baada ya mazugumzo. 

WAZIRI KALEMANI ASISITIZA TAASISI ZA UMMA VIJIJINI ZIWEKEWE UMEME

$
0
0
Na Veronica Simba – Dodoma

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewaagiza wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuwasimamia wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini nchi nzima, kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha kuunganisha umeme kwa taasisi zote za umma zilizo katika maeneo yao.

Alitoa maagizo hayo kwa nyakati tofauti jana, Aprili 16, 2019 akiwa katika ziara ya kazi wilayani Chamwino, Mkoa wa Dodoma, ambapo aliviwashia umeme vijiji vya Buigiri na Mwigamwile.

Akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Buigiri pamoja na wananchi, Waziri alisisitiza kwamba, kitendo cha kuwasha umeme katika shule hiyo kinalenga kutoa hamasa katika utekelezaji wa maagizo ya serikali kuwa taasisi zote za umma ni lazima zipelekewe umeme.

“Niwaombe viongozi wa Halmashauri za Vijiji na Wilaya nchini kote, kuhakikisha taasisi za umma katika maeneo yenu zinalipia gharama ya kuunganishiwa umeme ambayo ni shilingi 27,000 tu kwa ninyi mlioko vijijini, ili taasisi hizo zote ziunganishiwe umeme,” alisisitiza.

Aidha, kuhusu suala hilo la kulipia gharama za kuunganishiwa umeme, Waziri alilazimika kutoa msisitizo kwa viongozi na wananchi kwani alisema kumekuwepo na tabia ya baadhi ya watu kulalamika kuwa hawajaunganishiwa umeme lakini baada ya kufuatilia sababu iliyobainika ni kuwa wanakuwa hawajalipia huduma hiyo.

“Lipieni umeme. Msibaki kulalamika tu. Mlalamike mkiwa mmelipia.”

Katika hatua nyingine, Waziri Kalemani aliwataka wanafunzi wa Shule hiyo ya Buigiri kuongeza jitihada katika masomo kwani tayari wamepelekewa umeme ili kuongeza kiwango cha ufaulu shuleni hapo.

Awali, akizungumza wakati wa tukio hilo la uwashaji umeme, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga alimweleza Waziri kuwa, Shule husika imekuwa na kiwango duni cha ufaulu kutokana na sababu mbalimbali, mojawapo ikiwa ni ukosefu wa umeme tangu ilipoanzishwa mwaka 2007.

Akiwa katika kijiji cha Mwigamwile, Waziri Kalemani aliwasha umeme katika Ofisi mpya ya Serikali ya Kijiji, ili kuendelea kutoa msisitizo wa azma ya serikali kuhakikisha taasisi za umma zinaunganishiwa umeme.

Aidha, ili kuonesha msisitizo zaidi, Waziri Kalemani, alilazimika kulipa yeyé mwenyewe shilingi 27,000 ikiwa ni gharama za kuunganisha umeme katika kisima cha maji kilichoko kijijini Ikoa, Kata ya Ikoa ambacho pamoja na kuwa kimekamilika kwa muda mrefu hakijaanza kufanya kazi kutokana na kutokuwa na umeme.

Waziri aliwaagiza wataalamu wa TANESCO kuunganishia kisima hicho umeme kabla ya Jumanne ijayo, Aprili 23 mwaka huu.

Katika maeneo yote ya Wilaya hiyo ambayo Waziri alipita kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, alimsisitiza Mkandarasi kuongeza kasi ya kuunganisha umeme ambapo alimtaka kufikia Desemba mwaka huu, awe amekamilisha kazi ya kuviunganishia umeme vijiji na vitongoji vyote vya Jimbo la Chilonwa.

Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye alifuatana na Waziri katika ziara hiyo, Joel Mwaka, alimwambia kuwa vijiji 20 vya jimbo hilo kati ya 47 vilivyopo, havijafikiwa na umeme.

“Pamoja na kuwa mkataba unaonesha kazi hii ya kuunganisha umeme kupitia mradi wa Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza (REA III, Phase I) inatakiwa ifikie tamati Juni mwakani, lakini nakuagiza wewe mkandarasi ukamilishe kazi hii ifikapo Desemba,” alisisitiza Waziri.

Mbali na kuwasha umeme katika vijiji vya Buigiri na Mwegamile, Waziri pia alikagua utekelezaji wa miradi ya umeme katika vijiji vya Ikoa (Kata ya Ikoa), Nguga (Kata ya Msamalo) na Mlebe (Kata ya Msamalo).

Viongozi wengine walioshiriki ziara hiyo ni pamoja na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala, Mhandisi Innocent Luoga, Kaimu Meneja wa TANESCO, Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Tumaini Nyari, pamoja na wahandisi wasimamizi wa miradi ya umeme vijijini kutoka wizarani na REA.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwasha umeme katika ofisi mpya ya Serikali ya Kijiji cha Mwigamwile, wilayani Chamwino, Mkoa wa Dodoma, alipokuwa katika ziara ya kazi, Aprili 16, 2019.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (mwenye shati la bluu), akilipia shilingi 27,000 ikiwa ni gharama ya kuunganisha umeme katika kisima cha maji kijijini Ikoa, Kata ya Ikoa, wilayani Chamwino, Mkoa wa Dodoma, akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, Aprili 16, 2019.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (mwenye shati ya bluu-katikati), akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mlebe, Kata ya Msamalo, wilayani Chamwino, Mkoa wa Dodoma, akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, Aprili 16, 2019.
Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala, Mhandisi Innocent Luoga (kushoto) na viongozi wengine kutoka wizarani, TANESCO, REA na wilayani, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Buigiri pamoja na wananchi wa maeneo jirani, katika tukio la kuwawashia rasmi umeme, Aprili 16, 2019.
Sehemu ya umati wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Buigiri iliyopo Chamwino, Dodoma, wakionesha furaha yao mbele ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani), alipofika kuwawashia rasmi umeme akiwa katika ziara ya kazi, Aprili 16, 2019.
Taswira ya jengo jipya la ofisi ya serikali ya kijiji cha Mwigamwile, wilayani Chunya, Mkoa wa Dodoma, kama ilivyonaswa wakati Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) alipofika kuwasha rasmi umeme akiwa katika ziara ya kazi, Aprili 16, 2019. Waziri alisisitiza dhamira ya serikali kuunganisha umeme katika taasisi zote za umma.
Sehemu ya umati wa wanawake na watoto wa Kijiji cha Mwigamwile kilichopo Chamwino, Dodoma, wakionesha furaha yao mbele ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani), alipofika kuwawashia rasmi umeme akiwa katika ziara ya kazi, Aprili 16, 2019.
Viewing all 110150 articles
Browse latest View live




Latest Images