Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 283 | 284 | (Page 285) | 286 | 287 | .... | 3286 | newer

  0 0

  PAMOJA NA BAADHI YA VIONGOZI WA MAJIMBO NA HII NI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

   
  1. Kikao kilichofanyika ofisi ya Mkoa Ujiji kilibeba AGENDA ya Kujadili na Kuboresha ujio wa ziara ya Katibu Mkuu (T) Dr. P. Slaa Mkoani Kigoma 5/12/2013
   
  -      Ambapo atatembelea majimbo yote 8 ya mkoa Kigoma kwa mikutano si chini ya miwili kwa kila jimbo na baadae mkutano wa mwisho, jioni Mkutano ufanyike makao Makuu ya Jimbo. Lengo likiwa kuangalia uhai wa chama.
   
  -      Mambo makuu na muhimu yalizingatiwa
   
  -      Usalama kwa Kiongozi huyo kufutia sakata la Maamuzi ya kamati kuu dhidi ya Mhe.Zitto na mapokeo ya wanachama wetu.
   
  -      Kutoa taarifa rasmi kwa majimbo na kupokea hali ilivyo au inavyoonekana katika maeneo yao.
   
  -      Baada ya Tafakuri ya kina na ya Hekima na Busara pevu katika ujio huo iliazimiwa ifuatavyo
   
  i.             Mkoa uliomba Taifa lihairishe na kusogeza mbele tarehe ya ziara hiyo muhimu kwa mkoa wetu, ili Mkoa kama ngazi ya chini ya Kanda na Taifa uwezekwenda katika majimbo hayo na kuwaelimisha wanachama na wapenzi wetu juu ya kuheshimu na kuwa na nidhamu na maamuzi yatolewayo na ngazi ya juu yetu. 

  Hata kama yanamaumivu ….katiba yetu ifuatwe katika kutatua tatizo – Maoni ya Wengi Mkoani na Viongozi wa Chama ni kuudhiwa na maamuzi ya k/kuu ambayo dhahiri yalilenga kumilika Zitto – Kisiasa.
   
  ii.            Mkoa ulitishika na vitisho baada ya kupokea taarifa toka kwa baadhi ya viongozi wa majimbo ya mkoa kwa hali ya usalama si nzuri kwa ujio wa kiongozi wetu Dr. Slaa kufika Kigoma kwa kipindi hiki wakati wanachama na wapenzi wakitafakari na kwa kauli tofauti zisizolenga kuwepo usalama.
   
  iii.           Kwa hekima ya kikao kilijiridhisha kwa kupata maoni toka katika majimbo 6 kuwa hali ni mbaya kabisa wakishauri Katibu mkuu asogeze mbele ziara yake kupisha mtafaruku huu na kwa usalama wa Chadema na viongozi wake Kitaifa.
   
  iv.          Hivyo Mkoa kupitia kikao hicho kuwa ni bora kuzuia kuliko kutibu, tayari sintofahamu zimeonekana, viongozi na hasa wa majimbo kutofautiana mitazamo ni HATARI katika hali hiyo. Mkoa ulijiridhisha usalama hautakuwepo kwa ujumla hata kama baadhi ya majimbo yakisema wao wapo salama tu.
   
  v.            HOFU/TAHADHARI -   Endapo hali haitokuwa salama Mungu apishe mbali.

  Mkoa hautokwepa lawama na Uzembe wa makusudi kwani wajibu wa ngazi ya chini ni kutoa ushauri kwa ngazi ya juu. Hivyo mkoa unatoa ushauri kwa Makao Makuu (T) Chadema kusogeza mbele ziara hiyo hadi hali itulie na mkoa upite majimboni kujiridhisha na usalama kwa viongozi wake na hasa wa Taifa.
     
  LENGO KUU:  NI KUHAKIKISHA CHADEMA TUNAPITA SALAMA KATIKA WAKATI HUU MGUMU KWETU – CHADEMA
   
  Asanteni
    
                                                 
  ALHAJ. JAFARI KASISIKO                                           MSAFIRI WAMALWA
  M/KITI MKOA                        01/DEC.2013                KATIBU MKOA
  0756439200                                                                0786448443
  0714439200                                                               0756448442
   
    
  CHADEMA MKOA KIGOMA
   
   
   

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kulia) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa droo ya kwanza ya ‘Mimi Ni Bingwa’ iliyowapata washindi 23 ambao wawili kati yao walijishindia shilingi milioni tano, washindi 20 walijishindia shilingi milioni moja kila mmoja na mshindi mmoja akashinda tiketi mbili na safari ya kwenda kuangalia mechi ya klabu ya Manchester United moja kwa moja (live) katika ligi kuu ya mpira wa miguu nchini Uingereza kwenye uwanja wa Old Trafford. Kushoto ni Msmamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania Bw Abdallah Hemedy. Droo hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
  Wananchi wakiwa wanafuatilia vyema burudani iliyokuwa ikitolewa na vikundi mbalimbali vya burudani wakati wa kuchezeshwa kwa droo hiyo ya Mimi ni Bingwa jana kwenye viwanja vya Coco Beach jijini Dar es salaam.

  KAMPUNI ya mawasiliano ya Airtel Tanzania imetangaza washindi wa droo ya kwanza ya ‘Mimi Ni Bingwa’ inayolenga kuwazawadia wateja wake waaminifu.

  Katika droo hiyo pia washindi wawili walizawadiwa safari ya kwenda kuangalia mechi ya klabu ya Manchester United moja kwa moja (live) katika ligi kuu ya mpira wa miguu nchini Uingereza kwenye uwanja wa Old Trafford.

  Akizungumza wakati wa droo hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema droo hiyo imefuatia baada ya kampuni yake kuingia katika ushirikiano na klabu ya Manchester United wiki chache zilizopita.

  “Leo hii tunatangaza washindi wa droo yetu ya kwanza ya promosheni ya ‘Mimi Ni Bingwa’. Tunaamini kuwa ushirikiano wetu na klabu ya Manchester United utawapa wateja wetu uzoefu mpya katika uangaliaji wa soka. “Bado kuna zawadi nyingi zitashindaniwa ikiwa ni pamoja na zawadi kubwa ya Shilingi milioni 50. Kadri unavyoshiriki kwa kujibu maswali ndivyo utakapopata nafasi kubwa ya ushindi,” alisema Mmbando.

  Alimtaja mshindi wa tiketi mbili kuwa ni Leonard Dickson Lyatuu, mkazi wa Njiro mkoani Arusha na kuongeza kuwa nafasi nyingine 13 na tiketi bado zitashindaniwa mwishoni mwa droo ya mwezi wa kwanza itakayomalizika katikati ya mwezi Desemba mwaka huu.

  Pia aliwataja Harrison Wilson Mwambogola, mkazi wa Kigogo jijini Dar es Salaam na Stephen Asheri Chapile, mkazi wa Tengeru mkoani Arusha waliojishindia shilingi milioni 5 kila mmoja na wateja wengine 20 ambao wamejishindia shilingi milioni moja (1) kila mmoja.

  Washindi wengine walioibuka na zawadi ya shilingi milioni moja kila mmoja ni Tabu Nasiru, David Geoffrey Mtitu, Fikiri Samuel Ndaki, Godfrey David Msiu, Dickson Victor Mjata, Joseph Dominic Mboya, Benezek Bahati Macha , Stephen Asheri Chapile, Bida Edwin Mwaisoloka, Rashid Jacob Kagombola, Joseph Steven Mambo, Harrison Wilson Mwambogolo,Andronice Constantine Lashayo, Abdi Ibrahim Mohammed.

  Mmbando alisema kuwa bado zawadi nyingi zaidi kushindaniwa na kuongeza kuwa ili kushiriki katika promosheni hiyo mteja anatakiwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) ukiwa na neon “BINGWA’ kwenda namba 15656.

  Aliongeza kuwa Airtel pia imeweka vituo maalum kwa ajili ya wapenzi wa Man U kuangalia mechi za Manchester United bure kupitia luninga kubwa, hususani katika maeneo ya Coco Beach huku wakipata burudani kabla na baada ya mechi. Droo hiyo ilishuhudiwa na mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mwanafunzi Peter Robert Kilave wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari ya Kata Tushikamane ya mjini Morogoro baada kuibuka mshindi wa kwanza katika shindano la Insha kuhusu Ujenzi wa Miundombinu Afrika Mashariki.Mwanafunzi Peter amechukua ushindi wa kwanza kwa wanafunzi wote wa shule za sekondari wan chi tano za jumuiya ya Afrika Mashariki .
  Peter alipokea tuzo hiyo wakati wa Mkutano wa wa kuu wan chi za jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika hoteli ya Speke’s Bay Resort,Munyonyo, Kampala Uganda juzi.Kutokana na ushindi huo Mwanafunzi huyo amepewa tuzo ya dola za Marekani 1500, na cheti na alikabidhiwa zawadi hizo na mwenyekiti mpya wa jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
  Picha na Freddy Maro

  0 0

   Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya LG Electronics wa Afrika Mashariki, Moses Marji (kushoto), Mtafiti katika Idara ya Vijidudu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Muhimbili (MUHAS), Dk Billy Ngasala na Meneja Masoko wa LG, Soyoung Lee, wakifungua pazia kuashiria uzinduzi wa viyoyozi vya kufukuza mbu viitwavyo ‘LG Mosquito Away’ jijini Dar es Salaam leo.  
   
  Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya LG Electronics wa Afrika Mashariki, Moses Marji (katikati), Mtafiti katika Idara ya Vijidudu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Muhimbili (MUHAS), Dk Billy Ngasala (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Alshaaf, Aliraza Rajani wakifanya mahojiano na waandishi wa habari katika uzinduzi wa LG Mosquito Away jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi –Zanzibar

  Wananchi wa Shehia ya Mwanyanya nje kigogo ya mji wa Zanzibar wakiongozwa na Kikundi cha Vijana wa Green Society cha eneo hilo, wameshiriki katika kazi ya ukusanyaji na uzoaji wa taka katika shehia hiyo.

  Wakizungumza mara baada ya kazi hiyo, Mwenyekiti wa Green Society Bw. Ali Abdallah Ali na Ali Bakari Khatibu, wamesema mbali ya kikundi hicho kushiriki katika kazi hiyo ya uzoaji taka, pia kikundi hicho kitaendelea na kazi ya ustawishaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na kupanda miti ya kisasa na kuitunza ile ya uwoto wa aslai iliyopo katika eneo hilo.

  Wamesema Kikundi hicho cha Mwanyanya Green Society kitahakikisha kuwa kila kijana na mwananchi wa eneo hilo la Mwanyanaya anashiriki kwa hali na mali katika kazi za usafi wa mazingira na kulifanya eneo la Mwanyanaya kuwa lenye kijani kibichi na lisilokuwa na taka.

  Awali Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Mazingira Zanzibar Bi. Zuwema Juma Hamadi, ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika shughuli hiyo, alisema kuwa ofisa yake imeanzisha operesheni ya uzuiaji wa uchimbaji wa mchanga kiholela ikiwa ni sehemu ya kuzuia uharibifu wa mazingira.

  Vijana hao wa Green Society, wameitumia siku hiyo kama sehemu ya uzinduzi wa kikundi chao ambacho mbali ya kujihusisha na masuala ya ustawishaji wa mazingira pia kinalenga katika kumkwamua kijana katika matumizi ya dawa za kulevya na kumjengea mazingira ya kujiajiri.

  Aidha Vijana hao wametoa wito kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kujitolea katika masuala ya usafi na usawishaji wa mazingira kwani kwa kufanya hivyo kutaiwezesha nchi yetu kuwa ya kijani kibichi.

  0 0
 • 12/02/13--06:05: mahafali ya sita DUCE
 • kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Balozi Nicholas Kuhanga (wanne kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wa chuo hicho pamoja na viongozi wakuu wa Chuo kikuu kishiriki cha elimu Dar es Salaam (DUCE) katika mahafali ya sita ya DUCE yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
  Wanafunzi waliofanya vizuri zaidi (waliosimama nyuma) wakiwa katika picha ya pamoja na kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Balozi Nicholas Kuhanga (wanne kushoto waliokaa) a pamoja na viongozi wakuu wa chuo hicho pamoja na viongozi wakuu wa Chuo kikuu kishiriki cha elimu Dar es Salaam (DUCE) katika mahafali ya sita ya DUCE yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

  0 0
 • 12/02/13--06:10: Article 16


 • 0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt. Stagomena Tax, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Katibu Mtendaji wa DADC, Dkt. Stagomena Tax, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa mazungumzo leo, Dec 2, 2013.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Katibu Mtendaji wa DADC, Dkt. Stagomena Tax, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa mazungumzo leo, Dec 2, 2013. Kushoto ni Ofisa Mawasiliano, Charles Mubita. Picha na OMR

  0 0

  Minister for Water, Prof. Jumanne Maghembe has opened Nile equatorial lakes subsidiary action program (NELSAP) a dissemination workshop on NELSAP projects’ output in Dar es Salaam today.

  The two day workshop aim at enhancing awareness among the basin policy level stakeholders on the activities of the Nile Basin Initiative (NBI) and the role of the NELSAP in contributing towards poverty reduction, reversal of environmental degradation and stimulation of economic growth in creating awareness on regional planning tools that have been developed by the NELSAP with special focus the Multi-Sector Investment Opportunities Analysis (MSIOA).

  Another objective of the workshop is to promote the added value of NBI/NELSAP Cooperation in bringing to the fore the regional/international profile and niche that NELSAP offers in as far as water resources management and development, fostering information sharing and collaborative interaction between the NBI/NELSAP and its stakeholders including regional agencies and development partners and promoting and strengthening stakeholder involvement and regional cooperation within NEL sub-basins so as discuss with the countries the need to take on board NELSAP prepared investment projects through country programming and to discuss, with the countries, the status of NELSAP Financial Sustainability Strategy and Plan moving forward.
   Minister for Water, Prof. jumanne Maghembe, NBI-NELSAP Reginal Coordinator, Antoine Sendama and Assistant Director Water Resources Ministry for Water Tanzania, Dr. George Lugomela.
   NBI-NELSAP Reginal Coordinator, Antoine Sendama gives his speech to the workshop participants.
  Minister for Water, Prof. Jumanne Maghembe giving his speech to the workshop participants.
   A group photo of the members of the workshop of NELSAP with the Guest of Honor, Prof. Jumanne Maghembe .

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akizungumza wakati alipokuwa akiongoza harambee ya kuchangia maendeleo ya wanawake na watoto iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Anglikana Dayosisi Mtandi Masasi, mkoani Mtwara jana. Jumla y Sh103 milioni zilichangishwa kwenye harambee hiyo. 
  Askofu Msataafu wa Dayosisi ya Mtandi Masasi, Oscar Mnung'u akisalimu waumini.
  Mwimbaji wa nyimbo za injili, Rose Mhando akiimba katika Kanisa Kuu la Anglikana Dayosisi ya Mtandi Masasi wakati wa harambee ya kuchangia maendeleo ya wanawake na watoto iliyofanyika kanisani hapo juzi.
  waumini wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mtandi Masasi wakifatilia kwa umakini harambee hiyo.
  Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwaaga waumini wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mtandi Masasi baada ya kumaliza kuendesha harambee ya kuchangia maendeleo ya wanawake na watoto iliyofanyika katika Kanisa Kuu la dayosisi hiyo, juzi. Jumla ya Sh103 milioni zilichangishwa katika harambee hiyo.

  0 0
 • 12/02/13--07:04: Article 12

 • 0 0

  Rais waZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania Jaji Francis S.K.Mutungi,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kusalimiana na Rais leo.
  Rais waZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania Jaji Francis S.K.Mutungi,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kusalimiana na Rais leo.
  Rais waZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania Jaji Francis S.K.Mutungi,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar,baada ya mazungumzo yao leo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

  0 0

  Picture 019
  Aliyekuwa Miss Tanzania 1999, ambaye pia ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu akipozi mara baada ya kulamba Nondozzz ya shahada ya Uzamili wa Mawasiliano ya Umma katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine jijini Mwanza.
  Picture 018
  Hoyce Temu akipata Ukodak na Mdau wa tasnia ya habari nchini.
  Picture 013
  Hoyce Temu katika pozi na marafiki zake mara baada ya kulamba Nondozz.


  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Kuhudumia Waathirika wa Dawa za kulevya na UKIMWI iitwayo Medicins Du Monde - Harm Reduction Programe alipofika na ujumbe wake Ikulu jijini dar es salaam leo. PICHA NA IKULU

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa mji wa Rujewa,Mbarali na Vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Barafu mapema leo,mkoani Mbeya.Kinana amesema kuwa Serikali inapaswa kutengeneza njia nzuri na ya haraka ya kuwajibisha Ofisi za Umma ili kuweza kuwachukulia hatua Wafanyakazi wanaofuja fedha za umma ambao ndio walipa Kodi,Kinana ameyasema hayo katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika Lujewa Wilaya ya Mbarali ambayo imetuhumiwa kufanya ufujaji wa fedha za  maendeleo shilingi bilioni 2.4  na baadhi ya viongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo kati ya 2010 mpaka 2012.
   Sehemu ya eneo la mto Mbarali,kama lionekanavyo pichani ikiwa ni mradi wa ujenzi  wa skimu ya umwagiliaji Mwandamtitu,unaohusisha kata tatu za Rujewa,Ubaruku na Imalilo,Wilayani Mbarali mkoani Mbeya,ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake walitembelea mradi huo unaofaa kwa kilimo cha umwagiliaji mapema leo jioniMradi huo ambao umechangiwa kiasi cha shilingi milioni 50 na Wananchi ikiwa ni sehemu ya asilimia 20 ya mchango wa jamii kwa ajili ya uchimbaji wa mfereji mkuu.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbarali,Bwa.Adam Mgoyi alieleza kuwa Ujenzi huo haukukamilika kwa wakati kama ilivyokusudiwa kutokana na kukosekana kwa fedha kutoka serikalini kupitia Wizara ya Kilimo,chakula na Ushirika kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi. Mkurugenzi huyo alieleza pia changamoto za Mradi huo wa Mwendamtitu kuwa unakabiliwa na changamoto ya kutopatikana kwa kibali cha matumizi ya maji kinachotolewa na Mamlaka ya Bonde la Mto Rufiji,kutopatikana kwa kibali hicho kunahatarisha umuhimu mkubwa wa uwepo wa mradi huu.
   Mkuu wa Mkoa,Mh.Abbas Kandoro akifafanua jambo kuhusiana na mradi huo wa umwagiliaji kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokwenda kutembelea eneo hilo mapema leo jioni akiwa sambamba na ujumbe wake,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt Asharose Migiro.
   Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt Asharose Migiro akiwahutubia wakazi wa mji Rujewa,Mbarali na Vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Barafu mapema leo,mkoani Mbeya.
  Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo jioni Rujewa,Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.Katika mkutano huo Nape aliwatahadharisha wakazi wa eneo hilo hasa vijana kuwa makini na maneno ya Wanasiasa,ambayo baadhi yao wamekuwa wakiwapotosha na kiasi hata kupelekea vurugu ambazo hazina msingi wowote na zinaweza kuepukika iwapo busara ikitumika.

  0 0

  DSC_0305
  Naibu Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo cha Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkutano wa mabadiliko ya Tabianchi (COP 19) amesema kuna ugumu na umuhimu wa mkutano wa mabadiliko ya Tabianchi, na kuongeza kuwa wamekubaliana wawe na mkataba kwa nchi wanachama jinsi ya kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa kwa kiwango ambacho hakitaongeza Madini Joto duniani.

  Muyungi alisisitiza kwamba kuna umuhimu wa wanachama kukubaliana kwa maandishi na kuandika mkataba vile vile amesema walikubaliana kutokufuta mkataba mama wa 1992, na umuhimu wa kupunguza Gesi Joto na kuangalia uchangiaji wa tatizo la Madini Joto katika duniani.
  DSC_0226
  Afisa Habari kutoka Kitengo cha Habari Umoja wa Mataifa(UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari katika hoteli ya Holiday Inn juu ya changamoto na mafanikio ya mkutano wa mwisho wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 19) na msimamo wa Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla juu ya masuala ya Tabianchi na Mazingira duniani. 

  Kutoka kulia ni Mtaalamu wa mambo ya Nishati na Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Abbas Kitogo, Mwakilishi kutoka Youth of United Nations Association (YUNA) Adam Anthony na mgeni rasmi Naibu Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo cha Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi.


  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Bi. Salama Abuud Talib akimkaribisha Makamu Mwenyekiti UWT Bi. Asha Bakari Makame kuzungumza na wandishi wa Habari kuhusu miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wa Jumuiya hiyo.
  Makamu Mwenyekiti UWT Bi. Asha Bakari Makame akizunguza na wandishi wa Habari kuhusu miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
  Mwandishi wa Habari wa Chuchu Fm Radio Rahama Suleiman akitaka ufafanuzi wa kitu kwenye Mkutano wa UWT ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI YALIYOZUNGUMZA

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani katika kata ya Mbalatse wilaya ya Makete 
   Wakazi wa Mbalatse wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Makete akitoa hotuba yake
   Diwani wa kata ya Mbalatse Sikumu Msigwa akisoma Risala ya wanaoishi na VVU mbele ya mgeni rasmi
   Akimkabidhi mkuu wa wilaya hotuba yao.
  ====
  Na Edwin Moshi, globu ya jamii Makete

  Pamoja na jitihada za kuhakikisha kila pembe ya nchi hii dawa za kupunguza makali ya VVU zinapatikana kwa urahisi, kioja kimejitokeza wilayani Makete mkoani Njombe kwa baadhi ya wanaoishi na virusi vya ukimwi ambao walikuwa wanatumia dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo (ARV) kuacha kutumia dawa hizo kwa makusudi

  Pamoja na hayo wengine wanakataa kuzinywa dawa hizo licha ya kushauriwa na wataalamu wa afya kuanza kutumia kutokana na afya zao kuanza kuzorota

  Hayo yamebainika katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yakliyoadhimishwa kiwilaya katika kata ya Mbalatse wilayani Makete mkoani Njombe

  Akisoma risala ya wanaoishi na virusi vya UKIMWI katika kata ya Mbalatse, diwani wa kata hiyo Mh. Sikumu Msigwa amesema miongoni mwa mambo yanayosababisha kasi ya maambukizi mapya ya VVU katani hapo ni pamoja na mila potofu za kurithi wajane na wagane, wanaume kuoa wake wengi, ngono zembe, wenye vvu kukataa kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi na kujiingiza katika ulevi wa kupindukia na kufanya ngono bila kondomu

  Akihutubia mamia ya wakazi wa Mbalatse waliofika kwenye maadhimisho hayo mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro amekemea vitendo vinavyochangia ongezeko la VVU ikiwemo kuwasihi waviu kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU kama walivyoshauriwa na wataalamu wa afya ili waimarike afya zao na wazidi kujenga nguvu kazi ya Taifa

  Amesema endapo watatumia dawa hizo kwa usahihi upo uwezekano wa kuishi zaidi ya miaka 20 na wakaendelea kufanya shughuli zao kama kawaida, ikiwemo kuitunza familia ambayo inamtegemea kwa kiasi kikubwa

  "Ukitumia arv ndugu zangu lazima maisha yako yatakuwa marefu, na uzuri serikali yetu inawajali wananchi wake na dio maana hizo dawa zinafika mpaka huku, kwa kweli naombeni tubadilike, mkoa wetu ndio unaoongoza kitaifa, lakini bado jitihada tunatakiwa sisi ndio tuongeze, tukikubali kubadilika sisi, hata hizi kampeni za kupamban na VVU zitafanikiwa sana" alisema Matiro

  Maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani huadhimishwa Desemba Mosi ya kila mwaka, ambapo mwaka huu kauli mbiu ilikuwa Tanzania bila maambukizi mapya ya VVU, na vifo vitokanavyo na UKIMWI inawezekana

  0 0
 • 12/02/13--13:00: Article 4

 • 0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Engineer Felchesmi Mramba kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

  Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam leo, Jumatatu, Desemba 2, 2013, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Florens Turuka inasema kuwa uteuzi huo umeanza leo hii.

  Kabla ya uteuzi wake, Eng. Mramba alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo la TANESCO.

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu.
  Dar es Salaam.

  2 Desemba, 2013

older | 1 | .... | 283 | 284 | (Page 285) | 286 | 287 | .... | 3286 | newer