Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Mdau Mwajuma Adam Mpenda Alamba Nondozzz

$
0
0
Mdau Mwajuma Adam Mpenda akiwa kwenye Pozi la picha mara baada ya kulamba Nondozz yake ya kwanza ya Ugavi (Bachelor Of Science in Procurement) katika Chuo Kikuu cha Mt. Augustine,Jijini Mwanza hivi karibuni.
Mdau Mwajuma Adam Mpenda akiwa kwenye picha ya pamoja na shost ake,Najda Kabati wakati wa mahafali yao hayo yaliyofanyika hivi karibuni kwenye Chuo Kikuu cha Mt. Augustine,Jijini Mwanza.

SHORT COURSE ANNOUNCEMENT: PROTOCOL AND PUBLIC RELATIONS

Mwaliko kwenye Kongamano la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 8/12/2013

$
0
0
Kwa niaba ya Uongozi wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, napenda kuwakaribisha watanzania wote wenye mapenzi mema kwenye kongamano  la kujadili mchango wa rasilimali zetu kwa maendeleo ya taifa letu. Kongamano hilo litafanyika tarehe 8 Desemba 2013  ndani ya ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia saa 7.30 mchana hadi saa 12 jioni. Kongamano hilo litarushwa moja kwa moja na ITV na Radio one. 

Mada kuu ya kongamano hilo ni, “Mchango wa Rasilimali zetu katika maendeleo ya Taifa na Nafasi ya Mtanzania Kumiliki Rasilimali hizo”. 

Tunapenda kuchukua fursa hii kwa heshima kubwa kuwaomba wote wenye uchungu na rasilimali zetu na wadau wote wenye uelewa mpana kuhusiana na masuala ya usimamizi wa rasilimali mfike ukumbini siku hiyo ili muwe miongoni mwa watanzania wenye nafasi kubwa ya kutoa mchango wao katika kutoa elimu kwa watanzania juu ya nafasi yao katika kumiliki rasilimali zetu na mchango wake kwa maendeleo ya taifa letu.  

Miongoni mwa wazungumzaji siku hiyo ni pamoja na maprofesa waliobobea katika usimamizi wa rasilimali, wazungumzaji wengine waalikwa ni pamoja na Mheshimiwa John Mnyika (Waziri kivuli wa Nishati na Madini), Dkt Reginald Mengi (Mwenyekiti wa taasisi ya sekta binafsi Tanzania), na wadau katika sekta ya madini. Na Mgeni Rasmi atakayefunga kongamano hilo ni Mheshimiwa Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini. 
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa ushiriki  wenu kwenye kongamano hili. 

Karibuni nyote: 

Mr. Faraja Kristomus
(Katibu – UDASA)
0787525396 / 0717086135
Kwa maoni kuhusu mada husika tuandikie: kongamanoudasa@gmail.com

Article 24

news alert: JK APANDISHA VYEO MAAFISA WA POLISI, AFANYA UTEUZI WA NAFASI ZA MADARAKA

Catholic Relief Services (CRS) Tanzania launches soybean value chain project “Soya ni Pesa (SnP)”

$
0
0
        U.S. Embassy Tanzania                                                                                                                               December 3, 2013
The American People, through the United States Department of Agriculture (USDA) will sponsor a $20 million dollar, four-year projectentitled Soya ni Pesa (SNP) that intends to reach 3,000 smallholder farmers with assistance for the production and marketing of soybeans.  The ultimate goal of the project is to increase coverage to more than 11,000 farmers over the duration of the project.  The project implementer Catholic Relief Services Tanzania (CRS) will host a formal launch of SNP on December 4 at the Julius Nyerere International Conference Centre (JNICC) in Dar es Salaam.  At the launch, CRS will bring together governmental officials, donors, private sector, and national and international NGOs to discuss and share experiences, challenges, and opportunities to improve the soybean value chain development.  The SNP project further demonstrates the American People’s commitment to sustainable agricultural and economic growth, particularly in Tanzania’s domestic poultry industry.

The launch event takes place one year after initial SNP activities started in the field in Njombe and Ruvuma regions.  While soybeans have been grown in Tanzania since the early 1990s, there is a large and untapped potential to increase domestic production and processing, given the right investments.  Soybean crops have the potential to improve soil fertility, provide a source of protein for human consumption and animal feed, and contribute to income for Tanzanian smallholder farmers. The SNP project aims to double current production levels by 2016, while also promoting localized poultry rising for egg and meat production. 


In its first year, the SNP project linked participating farmers to potential buyers which resulted in sales of 850 megatons at two to three times the conventional price.  This demonstrates that it is possible for smallholder farmers to generate profits from soybeans, while buyers can satisfy at least part of their demand for this crop domestically.  The poultry component has reached 1,000 households with training on chicken and egg production.  The SNP project launch event will bring together the many different stakeholders in the soybean value chain, including Government of Tanzania representatives, soybean producer groups, private sector buyers and processors, donor agencies, and other actors interested in soybeans, the Southern Agricultural Corridor (SAGCOT), and value chain development.



CRS is the official relief and development agency of the U.S. Conference of Catholic Bishops, and has been working in Tanzania for over 50 years.  CRS works in partnership with local organizations, including the Catholic Church, secular NGOs, and other organizations, in efforts to support vulnerable communities to meet their basic needs. SNP is implemented in Tanzania through local partners Caritas Songea, Caritas Njombe, and WOPATA in Ruvuma, Njombe, and Morogoro respectively.  Muvek is implementing the poultry production component of the project in Njombe and Songea

DK MIGIRO APONGEZWA KUTEULIWA NA RAIS KUWA MBUNGE WA HESHIMA

$
0
0
 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipongezwa na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mbunge, jioni mjini Mbalizi, jijini Mbeya. Viongozi hao wamo kwenye ziara ya kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Akizungumzia uteuzi huo, mjini Mbalizi jioni hii, Dk. Migiro amemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa uteuzi huo ambao ameupokea kwa furaha, na kueleza kuwa kitendo hicho kinadhihirisha jinsi Rais Kikwete alivyo na imani naye pamoja na imani kwa Wanawake wa Tanzania
 Dk. Migiro (kulia), akipongezwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa uteuzi wake huo.
 Dk. Migiro akizungumza na vyombo vya habari, jinsi alivyopokea kwa furaha uteuzi wake huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akimpongeza Dk. Migiro kwa kuteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mbunge.

SSRA YATOA ELIMU KWA VIONGOZI WA MKOA WA LINDI

$
0
0
Na Abdulaziz Video,Lindi Katika kulinda na kutetea ikiwemo kuendeleza maslahi ya mwanachama wa Mifuko ya hifadhi ya jamii Nchini,Mamlaka ya Usimamizi wa sekta ya Hifadhi za Jamii(SSRA)Imetoa mafuno kwa viongozi na waajiri Mkoani Lindi ili kutekeleza sheria iliyounda mamlaka hiyo na kuhakikisha huduma bora zinamfikia kila Mtanzania 
Akifungua mafunzo hayo,Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila kuwa Serikali inaandaa utaratibu maalumu utakaowawezesha wanachama wa mfuko husika kunufaika nao wakiwa kazini ama baada ya kumaliza utumishi wao. 
 Pia amewasisitizia wafanyakazi nchini kuwa suala hilo limepewa kipaumbele ili kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo. Huku akiwasihi wafanyakazi wenye mawazo ya kuacha kazi ili tu wachukue mafao yao ya kujitoa kuachana na fikra hizo potofu ambazo alisema zitaleta athari kwa familia zao. Pamoja na Rai hiyo Mwananzila aliwataka SSRA kuhamasisha Mifuko ya Hifadhi za Jamii kutembelea mara kwa mara wanachama wao ikiwemo kutoa elimu ya mafao/Mikopo ambapo kufanya hivyo kutasaidia watumishi kujipanga baada ya kustaafu kuliko sasa mtumishi anachukia kustaafu 
“Jamani tunashuhudia wengi wanaona kustaafu ni kukaribia kifo na utumia mbinu nyingi kukwepa hilo kumbe kupitia Mifuko hii sasa ni mkombozi wa maisha ya wastaafu ila ni wazi kuna mifuko mingine ni kandamizi kwa mstaafu na haitoi fursa kwa mtumishi kushawishika kujiunga….”Alimalizia Mwananzila.
 Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa mamlaka hiyo Sarah Kibonde Msika akitoa mada katika mafunzo hayo alieleza kuwa SSRA imetoa miongozo sita (6) kwa lengo la kuhakikisha sekta ya hifadhi ya Jami inakuwa bora na endelevu itakayo boresha wanachama wa sekta ya hifadhi ya jamii kama ilivyoainishwa kwenye sheria na kufafanua kuwa miongozo hiyo pia itasaidia kuhakikisha mwanachama anapata haki yake anayostahili kwa wakati muafaka na kuondoa migongano baina ya mifuko,waajiri na waajiriwa. 
Pia Miongozo hiyo itahakikisha uwekezaji wa mifuko unaleta maendeleo bila kuhatarisha afya ya mifuko na utawala bora unaziongatiwa katika shughuli zote za uwekezaji kwa manufaa ya mifuko,wanachana na Taifa kwa Ujumla. 
‘Mamlaka inategemea kuwa katika kipindi kijacho sekta ya hifadhi ya jamii itakuwa endelevu,yenye mafao bora na mifuko ya hifadhi ya jamii itaongezeka. Kwa kuwa mamlaka inao uwezo wa kuchukua hatua za kinidhamu ikiwa pamoja na kutoa adhabu kwa wasimamizi na wadhamini wa mifuko kwa kutotekeleza matakwa ya sheria”Alieleza Kibonde alipokuwa anamalizia mada yake Mada nyingine katika Mafunzo hayo iliwasilishwa na Mkurugenzi wa Sheria SSRA,Bw Ngabo Patrick ambapo alieleza mafanikio na changamoto pamoja Muelekeo wa SSRA Ikiwa pamoja na kuendelea na mpango wa kuwianisha na kuhuisha mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuhimiza wanajamii wengi zaidi kuingia katika mfumo wa hifadhi za jamii na kutopoteza haki zao pale inapobidi kuondoka katika mifumo hiyo 
Mafunzo ya Siku moja yamefanyika mjini Lindi ambapo pia baadhi ya Changamoto ilibainika ni vema Elimu Hiyo pia ikifikishwa kwa watumishi wa kada ya chini kupitia Mifuko ya Hifadhi pamoja na Mamlaka hiyo
 Mkuu wa Mkoa wa Lindi akifungua Mafunzo kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Abdul Dachi na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Sheria SSRA,Ngabo Patrich
 Baadhi ya Viongozi wakisiliza Mada zilizokuwa Zikiwasilishwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta za Hifadhi za jamii katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi
 Mkuu wa mawasiliano na uhamasishaji,Bi Sarah Kibonde Msika akiwasilisha mada kuhusiana na malaka ya SSRA
 Katibu wa Tughe Mkoa wa Lindi,Bi Frola Urassa akitaka apewe Ufafanuzi kuhusiana na Tofauti ya mafao yanayotolewa na mifuko ya Jamii
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila akiwa katika Picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi yake pamoja na watumishi wa SSRA.

DR ASHAROSE MIGIRO AZUNGUMZIA KUTEULIWA KWAKE KUWA MBUNGE.

wanawake live na Joyce Kiria: HIKI NDIO CHANZO CHA BINTI HUYU KUPATA UJAUZITO

Balozi Chabaka Kilumanga Awasilisha hati za Utambulisho kwa Rais wa VISIWA VYA Comoro

$
0
0
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Visiwani Comoro, Mhe. Chabaka Kilumanga, leo tarehe 3 Desemba 2013 amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Dkt. Ikililou Dhoinine Rais wa Muungano wa Visiwa vya Muungano wa Comoro. 
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ikulu ya Beit Salaam, Mhe. Balozi Kilumanga na Mhe. Rais Dhoinine walipata fursa ya kuzungumza machache katika muktadha wa kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kindugu uliopo kati ya Tanzania na Comoro kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo. Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Comoro pamoja na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania mjini Moroni.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Visiwani Comoro, Mhe. Chabaka Kilumanga, akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Dkt. Ikililou Dhoinine Rais wa Muungano wa Visiwa vya Muungano wa Comoro mjini Moroni leo. 
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Visiwani Comoro, Mhe. Chabaka Kilumanga, leo akiongea na  Mhe. Dkt. Ikililou Dhoinine Rais wa Muungano wa Visiwa vya Muungano wa Comoro baada ya kuwasilisha hati za utambulisho katika Ikulu ya Moroni, leo. 

TASWIRA MWANANA ZA VIKWANGUA ANGA VYA JIJINI DAR USIKU HUU

DR SLAA KUFANYA ZIARA YA SIKU 20 KATIKA MIKOA YA SHINYANGA NA KIGOMA

$
0
0

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa  (pichani) ataanza ziara ya siku 20 katika mikoa ya Shinyanga na Kigoma, kuanzia Desemba 4-23, mwaka huu.  

Lengo la ziara hiyo ambayo imetokana na maombi ya muda mrefu ya viongozi wa chama katika maeneo husika, ni kuimarisha na kukagua uhai wa chama katika majimbo ya mikoa hiyo.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakutana na wananchi katika mikutano ya hadhara ambapo atazungumzia masuala ya kitaifa na eneo husika, kisha atafanya vikao vya ndani na viongozi pamoja na wanachama.

Siku ya Jumatano Desemba 4, mwaka huu Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakuwa Wilaya ya Kahama, siku inayofuata Desemba 5, atakuwa Wilaya ya Kakonko, Jimbo la Buyungu na Desemba 6, atakuwa Jimbo la Muhambwe.

Ratiba ya siku zinazofuata itaendelea kutolewa kwa vyombo vya habari.

Imetolewa leo Jumanne, Desemba 3, 2013, Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA


CHADEMA yazindua rasimu ya mabadiliko ya tabia-nchi

$
0
0
Picture
Kwa kuzindua rasimu ya sera hii ya Mabadiliko ya Tabianchi, CHADEMA kinakuwa chama cha kwanza Tanzania na Afrika nzima kuwa na sera ya namna hii, huku pia kikiwa ni moja ya vyama vichache duniani vyenye sera ya suala hili ,mtambuka. Baadae itafuata sera ya elimu na uchumi na masuala mengine ya kijamii, kama vile afya, maji, ajira, vijana n.k.

Hii ni rasimu ya sera. Hivyo kuanzia jana hadi Desemba 31 mwaka huu, CHADEMA kitakuwa kinapokea maoni ya Watanzania wote, wote kabisa kuboresha rasimu hii kisha kuwa na sera kamili itakayozinduliwa muda si mrefu. Kwa hiyo kila Mtanzania ajitahidi kuwasilisha maoni yake kwa njia yoyote anayoweza ili kusaidia nchi yetu ambayo hadi sasa chini ya utawala wa CCM,haina sera mahsusi ya suala muhimu na mtambuka kama hili.

Mabadiliko ya tabianchi ni jambo bayana linalotokea kwa dhahiri na kuathiri kila sehemu ya dunia tuishiyo kwa kasi ya ajabu. Nchi yetu ya Tanzania ni mhanga mkubwa tayari imeshaathirika sana na mabadiliko ya tabianchi, kama inavyobainika katika  namna mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukame uliokithiri na wa mara kwa mara ambao una athari kubwa sana kwenye kilimo, usafirishaji, nishati, biashara, na sekta ya uchumi-jamii.  Hivi sasa zaidi ya asilimia 70 ya majanga yote ya asili yanayotokea Tanzania yahahusiana na mabadiliko ya tabianchi vikiwemo ukame na mafuriko.

Wakati wa matukio hayo, kilimo katika maeneo husika hudorora au kusimama kabisa, mifugo mingi na wanyama pori hufa kwa kukosa chakula na maji na wakati mwingine husambazwa na mkondo wa maji yaliyofurika.  Kutokana na ukame wa muda mrefu, Tanzania kwa vipindi tofauti, imekuwa ikiathirika na ukosefu mkubwa wa nishati, ambao umekuwa na athari kubwa kijamii na kiuchumi.  Aidha, matukio ya mafuriko ya mara kwa mara yamekuwa na madhara makubwa kwa binadamu, mali na miundominu.

Kilimo na ufugaji, ambavyo ni shughuli kuu za kiuchumi kwa wananchi wengi wa Tanzania, kwa kiasi kikubwa zinategemea mvua za misimu.  Hii inamaanisha kwamba uchumi wa Tanzania, kwa kiasi kikubwa, unategemea tabianchi.  Kwa hiyo, ingependa kutoa mwongozo katika jambo hilo.  Hivyo, waraka huu ni mwongozo wa Sera ya CHADEMA ya mabadiliko ya tabianchi.

Waraka huu wa Sera unafafanua mpango mzima wa CHADEMA wa namna ya kushughulikia mabadiliko ya tabianchi na masuala mengine husianifu. Inatarajiwa kwamba viongozi wetu wa kisiasa katika ngazi za kanda, mikoa.  Wilaya na kata  wataiweka sera hii katika muktadha wa maeneo yao ili iendane na maeneo husika.
Mwisho, ninawashukuru Wajumbe wote wa Kamati Kuu kwa kuona umuhimu wa sera hii na kutoa mawazo ya awali ambayo wataalamu wetu waliyatumia hadi kuwa na mwongozo kamili wa sera.

Ninamshukuru Bwana Finias Magesa kwa kuratibu mawazo yote mpaka kuandikwa kwa rasimu ya awali ya waraka huu.  Pia ninaishukuru Kamati ya Wataalamu ya CHADEMA inayohusika na Sera kwa ajili ya kuuhariri waraka huu na kuuboresha.  Juhudi zao zinapaswa kuthaminiwa sana kwani wamekifanya CHADEMA kuwa chama tofauti chenye mawazo mbadala na bila shaka cha kwanza kuwa na sera inayotoa mwongozo wa mambo yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa namna ya kipekee kabisa, ninapenda kumshukuru kwa dhati, mshirika wetu muhimu na wa muda mrefu, Konrad Adeneur Stiftung (KAS), kwa kugharamia uzalishaji wa waraka huu.
………………………
Freeman Aikael Mbowe
Mwenyekiti wa Taifa,
CHADEMA

MSHINDI WA MBIO ZA MITUMBWI ZA BALIMI KUONDOKA NA ZAWADI NONO

$
0
0
Meneja Mauzo na Usambazaji wa TBL, Kanda ya Ziwa , Malaki Sitaki(kulia) akimkabidhi kikombe Mwenyekiti wa Chama cha mbio za Mitumbwi Taifa, Richard Mgabo ikiwa ni zawadi ya mshindi wa kwanza wanaume katika fainali za mashindano ya mbio za mitumbwi yanayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki katika ufukwe wa Mwaloni jijini Mwanza kwaudhamini wa Bia ya Balimi Extra Lager.Kushoto ni Mratibu wa Mashindano hayo, Peter Zacharia.


MSAADA TUTANI WADAU

$
0
0
Kuna dada anaitwa HAPPYNESS KASIL anautafuta ukoo wa mama yake mzazi kwani haufahamu.

Mama na baba yake wote ni kabila la wasukuma,mama yake amezaliwa NGUNDU wilaya ya NKWIMBA mkoa wa MWANZA.Baba yake amezaliwa NYANGUGE –BARIADI –SHINYANGA.

Mama yake anaitwa MATHAR DANIEL.Baba yake anaitwa KASIL SANAGU MAJAB.Mama yake alifariki mwaka 2001.Baba yake pia alifariki mwaka 2010.Katika familia yao walizaliwa watoto sita 

1.Charle Kasil
2.Happyness Kasil
3.Faustn Kasil
4.Daniel Kasil
5.Mariam Kasil
6.Neema Kasil

Wamefariki watoto 3 na wamebaki 3 .Waliofariki ni Charle Kasil ,Mariam Kasil na Neema kasil.Waliobaki ni Happy kasil. Faustn kasil na Daniel Kasil.Wazazi wake walikuwa wanaishi NYARUGUSU GEITA –MWANZA.

Baba yake alikuwa akinunua dhahabu Nyarugusu na anauza MWANZA.Mama yake alikuwa mama wa nyumbani.Mama yake alisoma shule ya sekondari NGUNDU wilaya ya NKWIMBA mkoa wa MWANZA na kuhitimu form 4.Anamfahamu mama yake mkubwa anaitwa ESTHER DANIEL alikuwa anaishi MWANZA sasa hivi hafaamu alipo .Shangazi zake ni SALOME SANAG na LUSIA SANAG.

Salome alikuwa anaishi MSOMA na Lusia alikuwa anaishi NGULYAT.Bibi na babu mzaa baba walikuwa wanaishi NYANGUGE BARIADI.Jina la ukoo wa baba yake ni SANAGU MAJAB.Kwa sasa Happy na wadogo zake wanaishi SIRARI9mpakani mwa Tanzania na Kenya) .

Anaomba mtu yoyote anae ujua ukoo wa mama yake amjulishe kwa namba zifuatazo (+255 782 781834) 

MDAU WA GLOBU YA JAMII

pilipili kali iliyomtajirisha mjasiriamali wa rwanda

$
0
0
Hii ni chupa ya moja ya pilipili kali kuliko zote duniani. Inatengenezwa nchini Rwanda na mfanyabiashara maarufu nchini humo aitwaye Sina Gerard. Alianza kufanya biashara ya kuoka mikate na kuiuza kwenye kiosk pembeni mwa barabara miaka takriban 25 iliyopita, akiwa na mfanyakazi mmoja tu. Hivi sasa yeye ni milionea mkubwa sana  anayeajiri mamia ya wafanyakazi pamoja na kuwapa biashara maelfu ya wakulima wadogo kwa kuwapa pembejeo na mbegu na kisha kununua mazao yao. 
Kwa hapa kwetu tunaweza kumfananisha na Bakhressa. Tunaileta taarifa hii hapa kufuatia ripoti yetu ya juzi kutoka wilayani Rungwe, ambako wakulima wanalalamika kwa kukosa soko la ndizi zao (BOFYA HAPA). Si vibaya wahusika wakaangalia njia za kuwapeleka watu hao wa Rungwe na kwingineko kwa Bwana Sina Gerard kupata msaada wa mawazo ya nini kifanyike. Kwani pamoja na pilipili yeye pia anasindika na kuuza bidhaa zitokanazo na ndizi pamoja na matunda mbalimbali. 
Kwa taarifa zake zaidi BOFYA HAPA

yale yaleeeeee....

$
0
0
Basi hapo wakisemwa ama hatua zikichukuliwa dhidi ya kuvunja sheria waziwazi namna hiyo wanakuja juu na kudai wanaonewa....

MATENGENEZO YA BARABARA YA KILWA ROAD ILIYOJENGWA CHINI YA KIWANGO YAANZA

$
0
0
Baada ya serikali kukataa kupokea barabara ya Kilwa Road jijini Dar es salaam iliyojengwa chini ya kiwango, ujenzi mpya umeshaanza kwa gharama ya mkandarasi mwenyewe.

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Unakumbuka Western Jazz Band na ngoma yao 'Rosa?'
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images