Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

WANAHISA WASHAURIWA KUENDANA NA SERA YA SERIKALI.

$
0
0

Benki ya CRDB mkoa wa Morogoro imeamua kushirikiana na serikali katika kuhamasisha wananchi kuchangamkia fursa mbali mbali  kujitokeza  kwenye uwekezaji wa viwanda ili kuendana na matakwa ya sera ya nchi katika mpango uliopo wa miaka mitano .

Akizungumza mara baada ya semina ya wanahisa wa bank ya CRDB mkoa wa Morogoro iliyolenga kuwa elimisha wanahisa na wananchi wengine fursa mbalimbali za kiuchumi na mambo yanayohusu Benki hiyo .
 
Mkurugenzi wa wateja wakubwa Bank ya CRDB Goodluck Nkim amesema wametoa nafasi kwa wanahisa kuelewa Zaidi uwekezaji wa viwanda na kuwaeleza kitu gani wanaweza kufanya ili kufaidika na myororo wa uchumi hii ikiwa ni njia Mojawapo ya CRDB kuonesha mchango wake katika ujenzi wa viwanda huku Mkurugenzi wa benki ya CRDB mkoa wa Morogoro Lusingi Sitta amewataka wananchi kujisajili katika ununuzi wa hisa kwenye bank hiyo kwani umilikiwa hisa unafaida mbali mbali ikiwemo kukuza kipato cha mtu binafsi na makampuni.

Aidha washiriki wamepongeza utoaji wa mafunzo hayo yaliyoweza kuongeza uwelewa wa wanahisa na kuiomba bank iweze kujitanua Zaidi katika kukopesha wanahisa walioko katika vyama mbalimbali vya wakulima ,kuelimisha Zaidi maana ya viwanda na kutengeneza jambo endelevu kwa ajili ya wastafu ambao sasa hivi ni wanahisa wa bank ya CRDB baadala ya kufikilia kuwakopesha . 
 Mkurugenzi wa mikopo kwa wateja wakubwa Goodluck Nkim akiwaelezea wanahisa faida za  kununua hisa katika benki ya CRDB na namna ambavyo wametoa nafasi kwa wanahisa kuelewa Zaidi uwekezaji wa viwanda  na kuwaeleza kitu gani wanaweza kufanya ili kufaidika na myororo wa uchumi.
 Wanahisa wakijisomea  kilichoandikwa  kwenye makablasha waliopewa mara baada ya kujisajili kushiriki mafunzo ya wanahisa na Benki ya CRDB mkoa wa Morogoro .
 Wafanyakazi wa benki ya CRDB mkoa wa Morogoro wakifatilia kwa makini  mada zinazotolewa na wawezeshaji katika mafunzo ya wanahisa mkoani Morogoro.
 Meneje wa bank ya CRDB tawi la Mzumbe mkoani Morogoro Jane Maganga akiteta jambo na Meneja wa mikopo CRDB Denis Kayanda  nje ya mkutano .


 Wanahisa wa benki ya CRDB mkoa wa Morogoro wakisajiliwa na wafanyakazi wa bank hiyo  ili kupokea makablasha ya mkutano kabla ya kuanza mafunzo yaliyolenga kuwa elimisha namna ya  kuchangamukia fursa mbali mbali zinazo wezakujitokeza kwenye uwekezaji wa viwanda.
 Mkurugenzi wa benki ya CRDB mkoa wa Morogoro Lusing Sitta akiteta jambo na Meneja wa CRDB tawi la Mandela mkoa wa Morogoro Stephen Mapunda wakati wa mkutano baina ya benki na wanahisa wa benki hiyo.
 Wafanayakazi wa CRDB wakiwasikiliza  kwa makini wanahisa waliohitaji kujisajili na kupewa kablasha zao zinazoonesha vipengele vya mafunzo ya wanahisa na vyeti vya kuthibibisha kuwa ni wanahisa.

WARSHA YA WATAFITI KUFANYIKA SIKU MBILI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Humphrey Shao , Globu ya Jamii

Tasisi ya Utafaiti na sera nchini (REPOA) Itafanya Warsha ya Mwaka kwa watafiti kote nchini na kutoika mataifa mbalimbali Duniani kwa muda wa siku mbili kuanzia April 10 Mpaka 11 katika ukumbi wa Ledger Plaza Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mtendaji wa REPOA, Dk. Donald Mmary amesema kuwa katika washa hiyo ambayo itahusisha mada kuu isemayo 'MAENDELEO YA UCHUMI WA NDANI KATIKA NGAZI YA CHINI' kama njia kuharakisha mapinduzi ya kimaendeleo nchini Tanzania ambapo katika mapinduzi hayo watazungumzia mapinduzi ya kilimo na viwanda.

“Nchi yetu imepiga hatua kubwa kulingana na uchumi kukua lakini bado kuna maeneo yanayogusa wananchi kuonekana hayajabadilika kwa kasi kwahiyo wameamua kuliangalia hilo jambo hasa ukuaji wa uchumi katika ngazi ya chini kuanzia ngazi ya almashauri, vijiji, mitaa na jamii kiujumla”. Amesema Dk.Mmary.

“Tunatambua kwamba tunapozungumzia maendeleo ya maendeleo ya ndani kwa ngazi ya chini tunazungumzia uwezo wa kutambua fursa zilizopo ambazo zinatokana narasilimali zilizopo hapa nchini”. Amesema Mmary.

amesema kuwa, ukiachana na suala la kutambua fursa vilevile kunakutafuta mbinu na mikakati ya kuzigeuza hizo fursa baada ya kuzitambua na kuwa katika shughuli za kiuchumi.

Pamoja na hayo kiongozi huyo ameongeza kuwa katika washa hiyo wanaweza kujifunza kutokana na uzoefu ambao viongozi mbalimbali wamepata ndani ya nchi kuona changamoto ziko wapi, tunaelekea wapi na tunakosea wapi.

“Tunatambua kwamba nchi yetu ni kubwa na inavigezo vyote vya saizi na ukubwa wa idadi ya watu kulingana na nchi nyingine za Afrika”. Mmary ameongeza.Kwa upande wake mkurugenzi wa tafiti za kimkakati, Jamal Msami amesema kuwa watakuwa na wawasilishaji wa mada kumi na pia kutakuwa na majukwaa ya kujadili muunganiko wa uhusiano katika mada na sera za maendeleo ambapo huko kutakuwa na wataalamu mbalimbali ambao wanaweza wakawa wajasiliamali, viongozi, wabobezi wa mambo ya taaluma za elimu, ujasiliamali na masuala ya uwekezaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Dkt. Donald Mmary akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi zao zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Kongamano hilo kutoka REPOA Dkt. Jamal Msami akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi zao zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Waandishi wa Habari walioshiriki Mkutano huo wa REPOA wakimsikiliza Dkt. Donald Mmary

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU APRILI 8, 2019

TANZIA

$
0
0
Familia ya Msuya na Mtengeti wanasikitika kutangaza kifo cha mpendwa wao Kanali (mstaafu) Ahmed Aboubakar Msuya kilicho tokea jana alfajiri tarehe 7/4/19. 

Marehemu Kanali Msuya ni miongoni mwa kizazi cha vijana  wa Taifa huru la Tanzania waliojiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakati wa harakati za ukombozi wa kusini mwa Afrika. 

Alilijunga na Jeshi la Wananchi kutokana na ushawishi na hamasa alizozipata kutoka kwa Meja Jenerali Sarakikya alipotembelea shule ni kwao. 

Kama vijana wengi wazalendo wa rika lake miaka hiyo, kijana Ahmed alishikwa na hamasa ya kulitumikia Taifa lake na kulikomboa bara la Afrika kutoka kwa wakoloni na ma beberu.  

Baada ya kujiandikisha na kujiunga na JWTZ. Ahmed Msuya alipata mafunzo ya awali ya kijeshi katika chuo cha maofisa wa jeshi Monduli. kati ya vijana walio kuwepo Monduli wakati huo ni pamoja na Rais mstaafu Mh Kikwete.
 Baadae alipelekwa Canada aliposomea Uhandisi. 

Msuya alipigana Namibia na Kagera. Mnamo mwaka 1981 alialikwa Ikulu DSM  na amiri jeshi mkuu wa wakati huo Hayati Mwalimu Nyerere kwa chakula cha mchana. Baada ya maongezi na chakula, Mwalimu alimtishwa askari kijana na mahiri Ahmed Msuya jukumu la kutafuta eneo sahihi na muafaka kwa ujenzi wa kambi ya uchunguzi na Maendeleo ya Uhandisi wakijeshi iliyokuja ikijulikana kama NYUMBU.  

Wakati huo alikuwa na cheo cha Kapteni. Kapteni Msuya alikabidhiwa helicopter na kuzunguka maeneo ya Pwani. Alivutiwa na eneo aliloliona Kibaha ambalo aliliona ni bora kimkakati, kimsingi na kiusalama. Haraka sana aliwataarifu makanda wake wakuu, ambao nao walikubaliana na chaguo lake bila ubishi na ujenzi wa kambi ya Nyumbu ukaanza. 

 Kapteni Msuya alikutana na Balozi Msuya,  mkewe wa miaka 35 mwaka 1982/83 London England na walioana mwaka 1983. Kanali Msuya alitumikia jeshi la Wananchi katika kambi ya Nyumbu na alishiriki katika kubuni na kuzalisha  mfano (prototypes) mbali mbali za magari ya kijeshi na kiraia. 

Alifanya kazi na warika lake pale nyumbu kama kina Kanali Ngingite na Brigadier Simbakalia.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE,APRIL 2019

MWENYEKITI WA TUME ASIKITISHWA NA UKOSEFU WA UADILIFU KWA WATUMISHI WA TUME YA MADINI

$
0
0



Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula akiongea na wafanyakazi wa Tume ya Madini kwenye ukumbi wa mikutano katika ofisi za Tume hiyo mkoani Morogoro. Kulia kwake ni Kamishna wa Tume hiyo Dkt. Athanas Macheyeki. Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula akitolea ufafanuzi masuala mbalimbali yaliyo wasilishwa na Kaimu Afisa Madini Mkazi Morogoro wakati wa kikao chake na wafanyakazi wa Tume ya Madini alipotembelea kwa ziara ya kikazi. Kulia kwake ni Kamishna wa Tume hiyo Dkt. Athanas Macheyeki na kushoto ni Mhandisi Emmanuel Shija Kaimu Afisa Madini Mkazi Morogoro.


Athanas Macheyeki Kamishna wa Tume ya Madini mwenye vitabu mkononi akimsikiliza jambo Mwenyekiti wa Tume Prof. Kikula wakati wakikagua maeneo mbalimbali yanayo zunguka ofisi za Tume ya Madini Mkoa wa Morogoro
…………….

Na Issa Mtuwa- Morogoro

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula amekerwa na kukasirishwa na ukosefu wa uadilifu kwa wafanyakazi wa Tume ya Madini katika baadhi ya Ofisi na kueleza kuwa, suala hilo halitavumilika kwa wanaokwenda kinyume na maadili ya kazi.

Akizungumza na wafanyakazi wa Tume ya Madini Mkoa wa Morogoro katika siku ya kwanza ya ziara yake aliyoianza Aprili 8, 2019, Prof. Kikula amewaeleza wafanyakazi wa ofisi hiyo kuwa, yeye na viongozi wenzake wa tume wamekerwa na kusononeshwa na vitendo vya ukosefu wa uadilifu vinavyofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa Tume ya Madini.

Ametolea mfano wa kitendo kilichofanywa na wanafanyakazi wa Tume hiyo wilayani Chunya ambapo watumishi wote wa kituo hicho wamesimamishwa kazi na Waziri wa Madini Doto Biteko kutokana na kukosa uadilifu na kutoa taarifa isiyo sahihi kwenye takwimu za madini.

“Kuna udanganyifu mkubwa unaofanywa na wachenjuaji madini, na udanganyifu huo unachochewa na watumishi wa Tume. Angalia mfano pale Chunya, wale wachenjuaji wamedanganya lakini ukifuatilia utagundua wafanyakazi wa tume wanahusika na huo udanganyifu, na ndio maana hata Waziri wa Madini aliamua kuchukua hatua ya kuwasimamisha kazi wafanyakazi wote wa kituo kile,” amesema Prof. Kikula.

Kufuatia hali hiyo, Prof. amekemea vitendo hivyo na kueleza kuwa, suala la uadilifu ni muhimu katika kazi za watumishi wa tume na kueleza kuwa, pamoja na kuwepo vishawishi vingi katika sekta ya madini, lakini wanapaswa kukumbuka kuwa kazi ni muhimu kwao na familia zao.

“Mimi na wenzangu tunaumizwa moyoni tunapoona wafanyakazi wa Tume wanakutwa na hatia ya ukosefu wa uadilifu inatusikitisha sana, sana”, amesisitiza Prof. Kikula.

Akitolea ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali yaliyowasilishwa na Kaimu Afisa Madini Mkazi, Prof. Kikula amewapongeza watumishi wote wa kituo cha madini Morogoro kwa kazi nzuri ya kusimamia ukusanyaji wa maduhuli na kuwaomba kuongeza bidii ili wafikie malengo waliyojiwekea.

Kuhusu masuala ya leseni, Prof. Kikula amemuagiza Kaimu Afisa Madini Mkazi kufuatilia leseni zote zilizopo na kubainisha leseni ambazo sio hai na kuzifuta kwa mujibu wa sheria. Aidha, amekumbusha kuhusu kufuata utaratibu halali uliowekwa kwa mujibu wa sheria katika hatua za ufutaji wa leseni hizo na kusema “asimuogope mtu lakini pia asimuonee mtu katika hatua hiyo ya ufutaji wa lesini zisizo hai”.

Aidha, Prof. Kikula amekiri kuwepo kwa changamoto na kuwataka watumishi hao kuwa na subira na kuongeza kuwa, Tume imepanga kununua magari 34 ambayo yatasambazwa katika mikoa yote ili kuongeza tija. Prof. Kikula amezungumza hayo baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya ofisi hiyo ambayo ilieleza kuwepo kwa changamoto kadhaa.

Kwa upande wake, Kaimu Afisa Madini Mkazi Morogoro Mhandisi Emmanuel Shija akisoma taarifa ya ofisi hiyo, pamoja na mambo mengine, amemweleza Mwenyekiti wa Tume masuala kadhaa yanayosimamiwa na ofisi hiyo ikiwemo uanzishwaji wa soko la Madini, ufutaji wa lesseni za uchimbaji kwa wamiliki wanaoshindwa kutimiza vigezo vya leseni zao, ukusanyaji wa maduhuli na changa moto zinazo wakabili katika kutekeleza majukumu yao.

Mhandisi Shija amesema, pamoja na changamoto zilipo, ofisi hiyo inafanya jitihada za kusimamia ukusanyaji wa maduhuli ambapo mpaka sasa imefikia asilimia 53 ya lengo na kwamba, inategemea kufikia malengo ya ukusanyaji waliyojiwekea.

Naye, Kamishna wa Tume ya Madini Dkt. Athanas Macheyeki ambaye amembatana na Mwenyekiti wa Tume, amewapongeza kwa ukusanyaji mzuri wa maduhuli na kuwataka kujiwekea muda wa utekelezaji wa malengo ili waweze kujipima vizuri.

“Unapojiwekea muda wa utekelezaji unakufanya uongeze bidii pindi unapoona uko nyuma ya muda ya utekelezaji wa lengo hivyo ni muhimu wa kulizingatia hilo,”amesema Dkt. Macheyeki.

Prof. Kikula na Dkt. Macheyeki wako mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa shuguli za Tume katika Wilaya mbalimbali zinazofanya shuguli za madini sambamba na kutatua kero za wachimbaji na wadau wa madini, mkoani humo.

SHUHUDIA MSAFARA WA RAIS DKT MAGUFULI MBINGA -SONGEA

MFUMUKO WA BEI WAONGEZEKA

$
0
0

Mkurugenzi wa Sensa ya Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei wa kipindi cha Mwezi Machi mwaka huu.
…………………….
 
Na.Alex Sonna,Dodoma 


Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) imesema kuwa mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia Machi mwaka huu umeongezeka kidogo hadi asilimia 3.1 kutoka 3.0 sawa na ongezeko la asilimia 0.1.

Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Mkurugenzi wa Sensa ya Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo, wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei wa kipindi hicho.

Bw.Kwesigabo ameeleza kuwa kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioshia Machi mwaka huu kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula zikilinganishwa na bei za mwaka ulioishia Machi mwaka jana.

“Hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Machi mwaka huu imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Februari,” amesema Kwesigabo

Aidha amefafanua kuwa kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioshia Machi mwaka huu kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula zikilinganishwa na bei za mwaka ulioishia Machi mwaka jana.

Kwisegabo alitaja baadhi ya bidhaa hizo kuwa ni pamoja na mavazi na viatu(4.4%), kodi ya pango(4.7%), mafuta ya taa(1.8%), dizeli(8.3%), chakula na vinywaji kwenye migahawa(4.6%) na malazi kwenye mahoteli(5.7).

Hata hivyo amefafanua kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa machi mwaka huu umepungua hadi asilimia 0.1 kutoka asilimia 0.5 kwa mwaka ulioishia Februari mwaka huu. Kuhusu hali ya mfumko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki alisema nchini Uganda kwa mwezi ulioishia Februari mwaka huu umebaki asilimia 3.0 kama ilivyokuwa ulioishia Februari.

Pia Kwesigabo ameongeza kuwa kwa upande wa Kenya mfumuko kwa mwaka ulioishia Machi mwaka huu umeongezeka hadi asilimia 4.35 kutoka 4.14 kwa mwaka ulioishia Februari mwaka huu.

NCHI za kusini mashariki mwa Afrika zatakiwa kubuni mbinu mbadala kukabiliana na fedha haramu

$
0
0
Na Woinde Shizza, Globu ya jamii

NCHI za kusini na mashariki mwa Afrika zimetakiwa kuhakikisha kuwa zinabuni mbinu mbadala kuhakikisha kuwa zinakabiliana na tatizo la fedha haramu ambalo limekuwa likizidi kushika kasi katika nchi hizo.

Kamishna Mkuu wa kudhibiti fedha haramu hapa nchini Onesmo Makombe ameyasema hayo jijini Arusha jana alipokuwa akifungua mkutano wa maofisa wa kupambana na fedha haramu kutoka nchi za kusini na mashariki mwa Afrika.

Amesema kuwa suala la fedha haramu limekuwa ni changamoto kubwa katika nchi hizo na kueleza kuwa endapo juhudi makini hazitachukuliwa kukabiliana na tatizo hilo,itasababisha uchumi wan chi hizo kuzidi kushuka.

‘’Serikali za nchi wanachama zitatakiwa kukabiliana na biashara haramu za binadamu,madawa ya kulevya,rushwa na mengineyo yanayofanana nahayo kwani mambo hayo ndiyo yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa fedha haramu”alisema Makombe.

Ameshauri kila nchi mwanachama wa umoja wa kupambana na fedha haramu kwa nchi za kusini na mashariki mwa Afrika kuhakikisha kuwa itatunga sheria kali za kuhakikisha kuwa zinawabana wale wote wanaojihusisha na fedha haramu.

Awali,Mtendaji Mkuu wa kitengo cha kudhibiti fedha haramu hapa nchini,Eliamani Kisanga alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kutengeneza sera na sheria za zitakazojikita zaidi kuhakikisha kuwa
nchi hizo zinakabiliana kikamilifu na tatizo hilo.

Amesema kuwa pia katika mkutano huo watajadili kwa kina ili kuhakikisha kuwa sheria zinazotumika kukabiliana na fedha haramu katika nchi wanachama zinafanana ikiwa ni pamoja na wahusika wanaopatika na makosa hayo kupewa adhabu zinazolingana katika nchi hizo.

Amesema kuwa mkutano huo utakaofanyika kwa juma moja unashirikisha nchi wanachama kumi na nane ambao unahudhuriwa na wajumbe zaidi ya mia mbili kutoka katika nchi hizo na kwamba mada mbalimbali zitawasilishwa na wajumbe watapata fursa ya kubadilishana uzoefu.

Alizitaja baadhi ya taasisi zinazoshiriki katika mkutano huo kuwa ni maofisa wa taasisi za kupambana na fedha haramu kutoka nchi wanachama,idara za mahakama,polisi,waendesha mashitaka,mamlaka za usimamizi wa bima,mabenki na malaka za kupambana na rushwa kutoka nchi
husika.
 Kamishna Mkuu wa kudhibiti fedha haramu hapa nchini Onesmo Makombe akiongea na waandishi wa habari

WABUNGE WARIDHISHWA NA HATUA ZA UWEZESHAJI VIJANA

$
0
0

Makamu Mkuu wa Chuo Cha Ufundi stadi DONBOSCO Auson Ntoga akizungumza wakati wa ziara ya ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ilipotembelea na kujionea wanufaika wa programu hiyo katika Wilaya za Dodoma Mjini na Chamwino mwishoni mwa wiki. 
Sehemu ya wanafunzi wa Chuo cha Ufundi cha DON BOSCO wanaonufaika na mpango wa Serikali kuwaongezea ujuzi vijana kupitia programu maalum inayotekelezwa kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu. 



Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Yaridhishwa na hatua iliyofikiwa katika kuwawezesha vijana takribani 3440 kukuza ujuzi wao kupitia programu ya Ukuzaji ujuzi inayotekelezwa na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu . 

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Nagma Giga amesema kuwa mradi huo ni muhimu katika kuiwezesha nguvu kazi ya Taifa hasa vijana kuwa na ujuzi stahiki. 

“Tunaipongeza Serikali kwa mkakati huu utakaowezesha kupanua wigo wa ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi katika nchi yetu”alisema Giga. 

Mradi wa mafunzo ya ufundi stadi kwa Vijana unatekelezwa kupitia chuo cha ufundi stadi DONBOSCO kwa ufadhili wa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo katika mwaka wa fedha 2019/2020 vijana elfu 10,000 wanatarajiwa kunufaika na mpango huo. 

Akizungumza wakati wa ziara ya Wabunge hao mwishoni mwa wiki Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi,Vijana na Ajira Mhe. Antony Mavunde amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa nguvu kazi ya Taifa inakuwa na ujuzi unaoendana na mahitaji ya ujenzi wa uchumi wa Viwanda. 

Aliongeza kuwa kuwajengea uwezo Vijana kwa kuwapa ujuzi stahiki kunawawezesha kujiajiri na kuzalisha ajira hali inayowawezesha kuchangia katika kukuza uchumi na kuchangia maendeleo ya Taifa. 

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa amesema kuwa Vijana wanayo nafasi kubwa ya kuchangia katika kuleta mageuzi ya kiuchumi kupitia ujuzi wanaopata kupitia programu hiyo. 

“Pamoja na changamoto ya ajira kwa vijana, Serikali yetu sikivu imeendelea kuwapa kipaumbele vijana katika kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo suala la ukosefu wa ajira kupitia utekelezaji wa programu hii itawezesha vijana wengi kujiajiri na kuchangia kukuza uchumi” 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Ally Msaki amesema kuwa uwezeshaji Vijana umepewa kipaumbele kupitia programu hiyo na utaratibu huo ni endelevu kwa dhamira yakuwafanya vijana wachangie katika kukuza uzalishaji na tija. 

Wakizungumza wakati wa ziara ya Kamati hiyo Katika Chuo cha Ufundi Stadi DONBOSCO cha Jijini Dodoma baadhi ya wanufaika akiwemo Bi. Esther Ngallya amepongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuwawezesha Vijana kujikwamua kiuchumi kupitia programu ya kukuza ujuzi inayotekelezwa kupitia chuo hicho. 

Akiafafanua amesema kuwa Serikali imebadili mwelekeo wa maisha ya Vijana walionufaika na Programu hiyo ambao wanauwezo mkubwa kwa sasa nyanja za umeme, ujenzi, tarazo,useremala, umeme, ufundi bomba na nyingine nyingi. 

Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuwawezesha Vijana kupitia programu mbalimbali ikiwemo ya kukuza ujuzi na ile ya ujenzi wa vitalu nyumba katika kila Halmashauri ambapo vijana 100 katika kila halmashauri wanajengewa uwezo ili waweze kutekeleza azma ya kuchangia katika kukuza uchumi na ujenzi wa viwanda.

Teknolojia mpya yatumika kumnasa chatu mkubwa mwenye mimba

$
0
0
Hifadhi moja ya taifa Florida, Marekani imemnasa chatu mkubwa mwenye urefu wa futi 17 (mita 5.2) kwa kutumia teknolojia mpya ya kuwanasa viumbe wavamizi.

Nyoka jike huyo, ambaye ndiye mkubwa zaidi kuwahi kunaswa kwenye hifadhi ya Big Cypress alikuwa na uzito wa kilo 63.5 na alikuwa na 'mimba' ya mayai 73.

Chatu ambao ni wavamizi kwenye eneo hilo wanatishia pakubwa maisha ya viumbe wa asili wa jimbo la Florida.

Watafiti katika hifadhi hiyo waliwategeshea vifaa maalum madume ya chatu ili kuwatafuta majike yanayopandwa na kukaribia kutaga.

"Timu ya watafiti ilimfuatilia dume moja lililofungwa kifaa hicho na kumnasa jike huyo karibu yake," imeeleza taarifa ya hifadhi hiyo kupitia mtandao wa Facebook.

Pamoja na kuondosha nyoka wavamizi, hifadhi hiyo inatumia matokeo ya tafiti zake ili kustadi tabia za nyoka na kutengeneza njia mpya za kukabiliana nao.

Chatu wanachukuliwa kama viumbe wavamizi jimboni Florida toka walipoonekana kwa mara ya kwanza katika viunga vya Everglades miaka ya 1980.

Aina hiyo ya nyoka ina asili ya bara Asia lakini baadhi ya chatu katika jimbo hilo wanaaminika kuachiwa kutoka kwenye umiliki wa watu waliokuwa wanawafuga.

Lakini chatu wengi katika jimbo hilo walitoroka kwenye vituo vya utafiti na uzalishaji baada ya Kimbunga Andrew cha mwaka 1992.

Nyoka hawana wanyama wa asili wa mwituni wa kuwawinda katika jimbo la Florida, hivyo hakuna namna ya asili ya kupunguza namba yao.

Maelfu ya chatu yanakadiriwa kuwa wanaishi meituni katika jimbo la Florida na wamekuwa wakilaumiwa kwa kupotea kwa wanyama wengi.

JE.! UMEYASIKIA MAKUBWA YA MANCHESTER UNITED.?

$
0
0
Manchester United kutangaza dau la usajili la pauni milioni 50 ili kumnasa kiungo kinda wa West Ham Declan Rice,20. (Irish Independent)

Rice, amesema kujiunga na West Ham ulikuwa uamuzi bora kabisa aliowahi kuufanya baada ya Chelsea kumtema akiwa na miaka 14. (Standard)

Beki wa kushoto wa Ajax Nicolas Tagliafico, 26, amesema kuwa mwisho wa msimu huu utakuwa ni muda muafaka wa kuhamia kwenye Ligi ya Premia. Beki huyo raia wa Argentina anawindwa na Arsenal. (Mirror)

Kocha msaidizi wa Manchester United Mike Phelan amesema kiungo wa klabu hiyo Paul Pogba, 26, "bado hajamaliza kazi yake" na anamtaka mchezaji huyo kusalia Old Trafford. (Telegraph).

DAWA MUHIMU ZAIDI YA 300 ZINAPATIKANA KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA.

$
0
0
Na WAMJW - NJOMBE

Serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kuvuka kiwango cha upatikanaji wa dawa muhimu kwa binadamu kilichowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika ngazi ya Hospitali ya Wilaya kwa kuwa na idadi kubwa ya dawa muhimu zinazopatikana kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alipotembelea Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe kujioinea hali ya utoaji wa huduma.

Waziri Ummy Mwalimu aliyeongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula pamoja na watendaji walio chini ya Wizara yake, amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano imeendelea kuboresha upatikanaji wa dawa kwa wananchi huku ikipitiliza kiwango kilichowekwa na WHO kwa kuwa na dawa muhimu 312 huku kigezo kilichowekwa na Shirika la Afya Duniani kikiwa ni dawa 30.

“Tuna mfumo wa ukusanyaji wa taarifa kuanzia ngazi ya zahanati, kituo cha afya mpaka hospitali unaotuwezesha Serikali kutambua mahitaji na matumizi ya dawa katika vituo vya kutolea huduma” amesema Waziri Ummy wakati akifafanua namna ya Serikali ilivyojipanga kupata takwimu sahihi za dawa.

Waziri Ummy amesema kuwa zipo propaganda zinazoendeshwa na watu wenye ushawishi ambao wamekuwa wakiwahadaa wananchi kwa kusema kuwa dawa hakuna ili hali dawa zipo na zinapatikana katika vituo vya kutolea huduma.

“Ni lazima tumtendee haki Rais wetu DKt. John Pombe Magufuli, amefanya makubwa kwenye Sekta ya Afya kwa kuboresha upatikanaji wa Dawa, tunaposema tumeongeza upatikanaji wa dawa maana yake dawa zinapatikana kwa urahisi hata kwenye vituo binafsi” amesema Waziri Ummy,

Waziri Ummy amezitaja dawa zenye kipaumbele kikubwa zikiwemo Dawa za kudhibiti maambukizi ya bakteria (Antibiotics), Dawa za kudhibiti Malaria, Dawa za magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Dawa za uzazi salama pamoja na Dawa za maumivu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa Ofisi yake kupitia Waziri wa Afya wako mbioni kuwasilisha muswada wa Bima ya Afya ambao utawawezesha wananchi wote sasa kuwa na bima ya afya.

Aidha, Dkt. Chaula amewataka watumishi katika Hospitali hiyo kuwahamasisha zaidi wagonjwa kujiunga na huduma za bima ya afya ili kuwa na uhakika wa matibabu pindi wanapougua.

“Niwaombe watendaji wote hapa kuwasisiza wagonjwa wanaofika hapa kupata matibabu kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya” Alisema Dkt. Chaula.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Winfred Kyambile amesema kuwa hali ya upatikanaji wa huduma imeimarika kutokana na mapato kuongezeka hivyo kuiwezesha Hospitali kutoa huduma bora kwa wananchi.

Dkt. Kyambile amesema kuwa kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa  imesaidia kuongezeka kwa mapato hospitalini hapo, amesema kuwa hapo awali mapato ya hospitali hiyo kwa mwezi yalikuwa Shilingi Milioni 12 huku sasa mapato hufikia Shilingi milioni 90 mpaka 100, fedha ambazo amesema wanazitumia kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo.

IGP SIRRO APIGILIA MSUMARI MAANDAMANO YA ACT-WAZALENDO,AONYA.

JAJI KIONGOZI AKAGUA MRADI WA UJENZI WANGING’OMBE NJOMBE NA KUZUNGUMZA NA WATUMISHI

$
0
0
Na Mary Gwera, Mahakama-Njombe
Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi amewataka Viongozi wa Mahakama Mkoani Njombe kuwa na desturi ya kutembelea Magereza mara kwa mara ili kubaini changamoto mbalimbali na kuchukua hatua.
Akizungumza na Watumishi wa Mahakama Mkoani humo katika Ukumbi wa Mahakama ya Mwanzo Makambako Aprili 08, 2019,  Jaji Kiongozi alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa kufanya ukaguzi kwani huwezesha kuangalia mfanano wa hali halisi katika kuendesha mashauri.
“Kuna umuhimu mkubwa katika kukagua Magereza hii husaidia kubaini dosari pamoja na kutambua maeneo yenye udhaifu na kuyafanyia kazi,” alisema Jaji Dkt. Feleshi.
Sambamba na ukaguzi wa Magereza Jaji Kiongozi aliwataka pia kuendelea na kaguzi za Mahakama mbalimbali katika Mkoa wao ikiwa ni pamoja na kukagua rejesta za mashauri kama kumbukumbu za Mashauri na nyinginezo zinawekwa sawa.
Kwa upande mwingine, Jaji Kiongozi aliwasisitiza Watumishi wa Mkoa huo kuendelea kutimiza majukumu yao kwa maadili ili kuilinda sura ya Mahakama kwa wananchi.
“Majaji na Mahakimu wamekasimishwa madaraka ya kutoa haki duniani hivyo si vyema madaraka haya kuyatumia kwa kujihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili, suala la ukiukwaji wa maadili halina mbadala,” alisisitiza Jaji Kiongozi.
 Jaji Kiongozi alizungumzia pia suala ya usikilizwaji wa Mashauri ambapo alisema kuwa mbali na muda Mahakama iliyojipangia katika umalizaji wa mashauri katika ngazi mbalimbali haizuii Hakimu kumaliza kesi chini ya muda uliowekwa mfano kwa Mahakama za Mwanzo miezi sita badala yake kesi inaweza kumalizwa chini ya muda huo.
Awali, akiwasilisha taarifa ya hali ya Mahakama mkoani Njombe, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa huo, Magdalena Nason Ntandu alisema kuwa hadi kufikia Desemba, 2018 Mahakama kwa Mkoa mzima ulibakiwa na jumla ya mashauri 492 na kuanzia Mwezi Januari hadi Machi mwaka huu jumla ya mashauri 825 yamefunguliwa katika mkoa huo na mpaka kufikia mwezi Machi, 2019 jumla ya mashauri 891 yalisikizwa na kubaki mashauri 426 ambayo yanaendelea kusikilizwa.
 Ntandu alieleza kuwa Mahakama yake imefanikiwa katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na kutembelea Mahakama zote ndani ya mkoa huo, kuimarisha mfumo wa usajili wa mashauri (JSDS) kwa kusafisha taarifa zilizokuwa kwenye JSDS 1  kwenda JSDS II, kufanya ukarabati mdogo katika jengo la Mahakama ya Mwanzo Bulongwa na kadhalika.
Mbali ya Mafanikio, Mahakama katika Mkoa huo inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa Watumishi, uhaba wa vyombo vya usafiri pamoja na uhaba wa majengo kwa kuwa baadhi ya maeneo hayana Mahakama.
Aidha katika ziara yake mkoani Njombe iliyopo Kanda ya Iringa, Jaji Kiongozi amekagua mradi wa ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya Wanging’ombe ambapo kwa sasa lipo katika hatua ya msingi na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mbunifu majengo kutoka TBA, Bw. Mustafa Ndambachia jengo hilo linatarajiwa kukamilika tarehe Juni 30, 2019.   
Vilevile Jaji Kiongozi alitembelea Mahakama ya Mwanzo Mdandu na kupata fursa ya kuzungumza na Wananchi wa Tarafa ya Mdandu waliofika kumlaki alipotembelea Mahakamani hapo akiwataka kusuluhisha masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na migogoro ya ndoa kwa ngazi ya uongozi wa kijiji na endapo ikishindikana kupata suluhu ndio yaletwe Mahakamani. 
Wananchi hao walieleza kuridhishwa na huduma inayotolewa Mahakamani ikiwa ni pamoja na mchakato mzima wa utoaji haki na umalizaji wa mashauri kwa wakati.  
 Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (mwenye suti ya kijivu kulia) akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya Wanging’ombe. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Ally Kasinge.
 Jaji Kiongozi akionyeshwa mchoro wa jengo la mradi wa Mahakama ya Wilaya Wanging’ombe.
 Jaji Dkt. Feleshi akizungumza na sehemu ya Wananchi wa Tarafa ya Mdandu waliofika kumlaki alipotembelea Mahakama ya Mwanzo Mdandu. Kushoto kwake ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo.
 Wananchi wakimsikiliza Jaji Kiongozi 
 Jaji Kiongozi akizungumza na Watumishi wa Mahakama mkoani Njombe (hawapo pichani), kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa, Jaji Panterine Kente.
 Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe, Magdalena Nason Ntandu akiwasilisha taarifa ya hali ya Mahakama mkoani Njombe.

 Watumishi wa Mahakama mkoani Njombe wakimsikiliza Jaji Kiongozi alipokuwa akizungumza nao.
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Mwanzo Makambako (mwenye tai nyekundu) akimuonesha Jaji Kiongozi eneo la Mahakama hiyo.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Angela Kairuki, akiongea Bungeni jijini Dodoma, Aprili 9, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu (kushoto), Bungeni jijini Dodoma, Aprili 9, 2019 katikati ni Mbunge wa Viti Maalum Salma Kikwete. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo, akiongea Bungeni jijini Dodoma, Aprili 9, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 9, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Aprili 9, 2019.

MHANDISI LUHEMEJA AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA MIRADI 41 YA DAWASA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja  ameanza ziara ya wiki moja ya kutembelea miradi 41 ya mamlaka hiyo inayoendeshwa kwa fedha za ndani.

Ziara hiyo itakayokuwa ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani itaangalia tathmini ya miezi sita toka kuanza kwa Dawasa mpya.

Akizungumza kabla ya ziara hiyo, Luhemeja amesema kuna miradi 41 inayotekelezwa kwa fedha za ndani ambapo wametenga asilimia 35 ya mapato yao ya kila mwezi kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali.

“Katika kipindi cha miezi tumetumia bilioni 15 kwa ajili ha miradi 41 iiliyopo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji na mingine ikiwa ni mipya itakayotatua changamoto ya maji kwenye maeneo yaliyokosa mtandao kwa muda mrefu,”amesema Luhemeja.

Amesema lengo kuu la Dawasa ni kuwekeza kwenye mtandao kwa kutumia fedha za ndani na kila mwezi wamekuwa wanatumia bilion 3  kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo Gezaulole, Chalinze Mboga, Kisarawe, Kibamba, Kiwalani Pahse 3 na miradi mingine.

Luhemeja ameeleza kuwa kwa sasa Mkoa wa Dar es Salaam upatikanaji wake wa maji ni asilimia 85 ambapo kwa siku yanazalishwa maji Lita milioni 502 kutoka kwenye mtambo wa Ruvu Juu, Ruvu Chini, Mto Kizinga na Visima vilivyojengwa na jamii au watu binafsi.

Ziara ya Afisa Mtendajj Mkuu itamalizika mwishoni mwa wiki hii na inatarajia kuleta faraja kwa wananchi wa maeneo mbalimbali ikiwemo Mabwepande, Bunju na Kitunda ambapo mradi wao unatarajiwa kukamilika Ijumaa hii na wananchi watapata maji kuanzia Jumamosi.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA)Mhandisi Cyprian Luhemeja akiangalia uchimbaji wa mitaro kwa ajili ya ulazaji wa mabomba ya inchi 8 yeye urefu wa Kilomita 2.5 kutoka kwenye tenki la Mabwepande kwa ajili ya kuanza kuwahudumia wananchi wa maeneo ya Bunju, Kitunda na Mabwepande.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) akikagua toleo linalopokea maji kutoka Tanki la maji la Mabwepande litakalohudumia wananchi wa Bunju, Kitunda na Mabwepande.

MAHAKAMA YAAMURU ALIYEKUWA MSAIDIZI WA DC AJENGEWE NYUMBA

$
0
0
Mahakama kuu kanda ya Arusha imemwamuru Janeth Fosbrooke ambaye ni binti wa aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Kondoa marehemu Henry Fosbrooke kumjengea nyumba yenye vyumba kwenye eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 87583,891 mkazi wa eneo la Duluti ,Mzee Juma Isangu .

Mbali na uamuzi huo mahakama hiyo imemwamuru binti huyo amlipe fidia ya kiasi cha sh,5 milioni mkazi huyo ambaye alikuwa msaidizi wa karibu na baba yake ambaye kwa sasa anakabiliwa na matatizo ya kiafya.

Uamuzi huo ulitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Jaji Moses Mzuna katika shauri la ardhi nambari 94 ya mwaka 2016 lililofunguliwa na Fosbrook dhidi ya Isangu huku akisimamiwa na wakili John Lundu.

Katika shauri hilo Fosbrooke aliiomba mahakama hiyo imkabidhi nyumba anayoishi Isangu iliyopo mkabala na hoteli ya Duluti kwa madai ni mali halali ya baba yake mzazi ambaye ni marehemu kwa sasa na kwamba yeye ndiye msimamizi wa mirathi ya baba yake.

Akitangaza hukumu ya kesi hiyo mbele ya pande zote Jaji Mzuna alisema kwamba mahakama imejiridhisha pasi na shaka kwamba nyumba hiyo ni mali halali ya marehemu Fosbrooke na hivyo Isangu anapaswa kuondoka pindi akishajengewa makazi mapya.

Hatahivyo,Jaji Mzuna aliieleza mahakama hiyo kwamba Isangu anapaswa kukabidhi ardhi,nyumba na samani zilizopo ndani ya nyumba hiyo na kushindwa kutii agizo hilo atastahili kulipa kiasi cha sh,500,00 kwa mwezi hadi pale atakapoondoka katika nyumba hiyo.

Katika hukumu hiyo Jaji Mzuna alisema kwamba upande wa mdaiwa utalazimika kulipa gharama zote za uendeshaji wa kesi huku akisisitiza kwamba wadaiwa wana haki ya kukata rufaa endapo hawajaridhika na hukumu hiyo.

Akizungumza mara baada ya hukumu hiyo wakili wa mdaiwa,Neema Osca alisema kwamba mteja wake hajaridhika na hukumu ya kesi hiyo na hivyo wanajipanga kukata rufaa kama mahakama ilivyoagiza.

Hatahivyo,Hemed Isangu ambaye ni mtoto wa Juma Isangu alisema kwamba wao hawajaridhika kabisa na hukumu ya kesi hiyo kwa kuwa wosia wa marehemu Fosbrooke ulieleza bayana kwamba endapo baba yake akitaka kuondoka katika nyumba hiyo basi awasilishe gharama kwa familia na wainunue kwa gharama inayostahiki.

“Hatujaridhika kabisa na hukumu ya hii kesi kwa kuwa hii nyumba baba yangu alipewa na marehemu Fosbrooke kama fidia ya kiinua mgongo baada ya kufanya kazi kama msaidizi wake kwa muda mrefu”alisema Isangu

BURIANI GWIJI WA MUZIKI WA JAZZ HUGH MASEKELA

$
0
0
Na Moshy Kiyungi
Hugh Masekela ni majina ya mwanamuziki mashuhuri wa Afrika Kusini, aliyefariki dunia Januari 24, 2018 jijini Johannesburg, nchini Afrika ya Kusini akiwa na umri wa miaka 78. Chanzo cha kifo chake ni ugonjwa wa tezi dume ulimpata kwa miaka kadhaa ilyopita. Bendi yake ilitoa taarifa ikisema kwamba marehemu Masekela amekuwa akipambana na ugonjwa huo tangia mwaka 2008.

Mwezi Machi 2016 alifanyiwa upasuaji wa jicho baada ya saratani kusambaa, ikabidi akafanyiwa upasuaji mwingine mwezi Septemba mwaka huo huo. Hugh Masekela alisifika kwa nyimbo zake zilizotoa mchango mkubwa katika harakati za kupinga ubaguzi wa rangi. Wasifu wa Masekela, unaonesha kuwa alizaliwa Aprili 04, 1939 katika mji wa KwaGuga huko Witbank, nchini Afrika ya Kusini.

Alikuwa mpulizaji mashuhuri wa tarumbeta wa muziki ya Jazz. Hugh alianza kuimba na kucheza Piano tangia akiwa mtoto, baada ya kuona filamu ya ‘Young Man with a Horn’. Masekela alifahamika ulimwenguni kote kwa aina ya kupiga muziki wa Jazz la mtindo wa Afri Jazz. Alikuwa na talanta ya upulizaji wa tarumbeta, uongozi wa bendi ya muziki, utunzi na mwandishi mahiri wa mashairi ya muziki.

Masekela alijifunza kupuliza tarumbeta akiwa shuleni, kupitia kwa mwalimu wake ni Padri Trevor Huddleston ambaye alikuwa ni mkuu wa shule yao ya Huddleston. Hakuchukua muda Hugh Masekela kuweza kuitawala ala hiyo ya tarumbeta. Mwaka 1956 akajiunga na kundi la Jazz la Herbert’s African Jazz Revue.

Akiwa na umri wa miaka 20, Masekela alikuwa akitumbuiza muziki ya aina tofauti, hasa ya Jazz, Bebop, Funk na Afro beat wakati huo alikuwa na kundi la Jazz Epistles. Kundi hilo lilikuwa na wasanii maarufu kama mpiga kinanda mahiri Abdillah Ibrahim.

Mwaka 1960 Masekela alikwenda London, Uingereza ambako alijiunga na shule ya muziki ya Guildhall School of Music na baadae alikwenda New York, Marekani ambako alisoma katika mji wa Manhattan. Mwaka 1962 alitoa albamu yake ya kwanza iitwayo Trumpet Africa. Miaka miwili baadaye Hugh alitoa nyingine iitwayo The Americanization of Ooga Booga, ambayo ilitamba mpaka kushika chati, hasa baada ya kuchezwa sana na kituo kimoja cha radio cha mjini California.

Mpaka kufikia Agosti 2000, Masekela alikuwa ameuza nakala milioni 50 na kumfanya apate tuzo ya Platinum. Hugh alishirikiana na wasanii kama Miriam Makeba wa Afrika Kusini na Paul Simon wa Marekani kwenye albamu ya Graceland. Tarumbeta lake limesikika zaidi kwenye nyimbo za Gumboots na Diamonds on the soles of her shoes.

Enzi za uhai wake Masekekla aliwahi kusema kwamba alitumia muziki kama silaha ya kusambaza mageuzi ya kisiasa enzi hizo za ubaguzi wa rangi, na alifanikiwa sana. Ilielezwa kwamba Masekela alikuwa ni baba wa muziki wa Jazz nchini Afrika Kusini. Mchango wake mkubwa kimziki ulimebakia ndani kumbukumbu kwenye mamilioni mioyo ya watu.

Aidha kwa upande wake rais wa Afrika Kusini wakati huo, Jacob Zuma alimsifia Masekela kama msanii wa muziki wa  Jazz, mpiga tarumbeta maarufu, mwanaharakati wa utamaduni na mtu aliyekuwa katika harakati za ukombozi.

"Aliuweka hai mwanga wa uhuru duniani kote katika harakati zake za kupinga ubaguzi wa rangi kupitia muziki wake na kushinikiza uungwaji mkono wa Kimataifa, fani ya muziki na nchi kwa Ujumla tumempoteza mtu muhimu sana…" alisema rais Jacob Zuma.

Mwimbaji mmoja wa Afrika Kusini Johnny Clegg alimuelezea Hugh Masekela kama mwanamuziki bora na siku zote akiishi kwa mitazamo ya asili yake ya Afrika Kusini. Nguli huyo aliondoka nchini Afrika Kusini wakati ilipoongozwa na watu weupe mwaka wa 1960, hakurejea hadi pale Nelson Mandela alipoachiwa huru mwaka wa 1990.

Muda wote alikuwa uhamishoni mjini London nchini Uingereza. Baadaye alihamia mjini New York Marekani, ambako alikutana na msanii mwenzake wa Afrika Kusini Miriam Makeba, Dizzy Gillespie na Harry Belafonte. Hugh Masekela na Makeba waliishi maisha ya ndoa ya muda mfupi na Miriam Makeba.

Miongoni mwa nyimbo zake zilizovuma na zilizopendwa ni ule wa "Bring Him Back Home", akishinikiza Nelson Mandela achiwe huru. Hugh Masekela alitumbuiza katika hafla ya ufunguzi wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2010 zilizofanyika nchini Afrika Kusini ikiwa ni mara ya kwanza fainali hizo kufanyika barani Afrika.

Kwa upande wake Waziri wa Sanaa nchini Afrika Kusini Nathi Mthethwa alisema kwamba taifa hilo limempoteza mwanamuziki wa haiba ya kipekee aliburudisha nyoyo za watu wa taifa hilo kupitia miziki yake. Wakati wa enzi wa nguli huyo alikuwa mwanaharakati akipigania haki na kupambana dhidi ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.

Moja ya kazi zake ni “Soweto Blues" muziki ambao ulitumiwa  na makundi ya kupambana na ubaguzi wa rangi Afrika Kusini. Zingine ni pamoja na Tagi, Mandela , Apartheid, Afrika Kusini, Hugh Masekela. Mungu aipumzishe roho yake pahala pema peponi, Amina.

UCHAGUZI MDOGO WA KATA SITA KUFANYIKA MEI 19 MWAKA HUU

$
0
0
Na. Idara ya Habari-NEC

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo wa madiwani kwenye kata sita (6) zilizopo kwenye halmashauri sita (6) katika mikoa sita (6) ya Tanzania Bara.

Mwenyekiti wa Tume Jaji (Rufaa) Semistocles Kaijage amesema Jijini Dar es Salaam leo (Jumanne 09.04.2019) kwamba uchaguzi huo utafanyika tarehe 19 Mei mwaka huu.

Akisoma taarifa kwa umma iliyotolewa na Tume, Jaji Kaijage amesema kwamba fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kati ya tarehe 15 hadi tarehe 19, Aprili mwaka huu.

Aidha Mwenyekiti huyo wa Tume amesema kwamba uteuzi wa wagombea pia utafanyika tarehe 19, Aprili mwaka huu na kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia tarehe 20, Aprili hadi tarehe 18 Mei mwaka huu.

Alifafanua kwamba uchaguzi katika kata hizo, utafanyika sambamba na Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki

“Tume inapenda kuvikumbusha Vyama vya Siasa na wadau wote wa Uchaguzi kuzingatia Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Taratibu, Miongozo na Maelekezo yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa kipindi chote cha Uchaguzi huu mdogo,” alisema Jaji Kaijage.

Awali Jaji Kaijage alisema kwamba maamuzi ya kutangaza uchaguzi kwenye kata hizo yamefanyika baada ya Tume kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa ambaye kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 aliitaarifu Tume juu ya uwepo wazi wa nafasi hizo.

Alisema kwamba nafasi hizo wazi zimetokana na vifo vya Madiwani watano (5) na mmoja (1) kujiuzulu.

Kata hizo ni pamoja na Uwanja wa Ndege iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi, Kitobo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera, Kyela iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya, Mikocheni iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam, Mvuleni iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi na Manda iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume Jaji (Rufaa) Semistocles Kaijage 
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images