Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

Mashabiki waliomkosha Ommy Dimpoz wafanyiwa Shopingi GSM Mall

$
0
0
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz akiwafanyia shopingi mashabiki wake wawili wa Muziki katika maduka ya GSM Mall yaliyopo eneoa la Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam jana. Dimpoz aliwazawadia mashabiki wake wawili hao baada ya kuwachagua kupitia Instagram wakiwa wanafuatilia muziki wake mara nyingi



SMZ YAUNGA MKONO JUHUDI ZA BENKI YA NMB KUWAUNGANISHA WAFANYABIASHARA KISIWA CHA PEMBA.

$
0
0
MWENYEKITI wa klabu ya Wafanyabiashara wa NMB Kisiwani Pemba Abdalla Ali Said, akimkabidhi cheti cha shukurani mmoja wa wafanyabiashara na mteja wa benk ya NMB Pemba, Mwanakhamis Khamis, wakati wa hafla ya uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara hafla iliyofanyika mjini Chake Chake.
MWENYEKITI wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB Kisiwani Pemba Abdalla Ali Said, akimkabidhi cheti meneja wa NMB Tawi la Pemba Ahmed Nassor, kwa niaba ya mfanyabiashara Abdalla Nassor Abdalla, wakati wa hafla ya uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara hafla iliyofanyika mjini Chake Chake. 
MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadid Rashid (kushoto), akisalimiana na mwenyekiti wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB Kisiwani Pemba, Abdalla Ali Said (Ngonda) baada ya kuchaguliwa kwake na wafanyabiashara wakati wa uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadid Rashid (kushoto), akisalimiana na mwenyekiti wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB Kisiwani Pemba, Abdalla Ali Said (Ngonda) baada ya kuchaguliwa kwake na wafanyabiashara wakati wa uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MWENYEKITI Mteuliwa wa klabu ya wafanyabiashara ya NMB Kisiwani Pemba Abdalla Ali Said (Ngonda), akizungumza na wafanyabiashara katika mkutano wa uzinduzi wa klabu hiyo, mkutano uliofanyika mjini Chake Chake.
MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadid Rashid, akizungumza na wafanyabiashara wa Pemba, wakati wa uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB Pemba, uzinduzi huo uliofanyika mjini chake chake.
MENEJA wa NMB kanda ya Dar es Salam na Zanzibar, Badru Iddi akizungumzia malengo ya Benk ya NMB kanda yake kwa mwaka 2019, wakati wa uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB Pemba, hafla ya uzinduzi huo uliofanyika mjini Chake Chake.
MWAKILISHI kutoka NMB Loelia Kibasa, akiwasilisha mada kuhusu NMB na Idara ya biashara, wakati wa ufunguzi wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB kisiwani Pemba, halfa iliyofanyika mjini Chake Chake.


MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadid Rashid, amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inaunga mkono juhudi mbali mbali zinazochukuliwa na benki ya NMB, katika kuwaunganisha wafanyabiashara wa Kisiwa cha Pemba, jambo linaloweza kupelekea kuongezeka kwa mapato ya nchi. 

Alisema wafanyabiashara ni watu muhimu katika maendeleo ya uchumi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, katika suala zima la kukusanya mapato. 

Alisema malengo ya Serikali ya awamu ya saba ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuhakikisha, inaboresha mapato ya serikali kupitia kodi na kuziba mianya yote ya ukwepaji wa kodi, ambayo husababisha upotevu wa mapato ya serikali hali inayopelekea kuzoretesha maendeleo ya nchi. 

Mkuu huyo wa Wilaya ya aliyaeleza hayo, mjini chake chake wakati wa uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara wa Pemba, ikiwa ni klabu ya kwanza kisiwani hapa kuanzishwa na NMB. 

“Muunganiko huu pia utaweza kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara, katika suala la kodi na jinsi ya kutunza fedha, jambo hili ni muhimu litaweza kusaidia malengo ya wafanyabiashra, ili kuweza kujengewea uwelewa katika suala zima la ulipaji wa kodi”alisema. 

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya alisema, kuanzishwa kwa klabu hiyo itaweza kutoa mwangaza kwa wafanyabiashara, kupata mafunzo mbali mbali ya biashra, pamoja na kuelimishwa juu ya utunzaji wa kumbukumbu za biashara, masoko, huduma nzuri kwa wateja, upangaji wa bei, sheria za biashara na mahesabu ya fedha. 

Aidha aliwataka wafanyabiashara kufanya utafiti kwa kina wa biashara wanayotaka kuifanya, kabla ya kuomba mkopo ili fedha wanazopatiwa waweze kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa, pamoja na benki kufuatilia wafanyabiashara waliowapatia mikopo na kujuwa biashara zao ipasavyo.

Meneja wa NMB kanda ya Dar es Salam Badru Iddi, alisema NMB imeamua kuwafikia wananchi wote wa kipato cha chini Tanzania nzima, kwani mwaka 2018 walifungua klabu za wafanyabiashara 50 Tanzania na mwaka 2019 mikakati yao ni kufungua klabu 36 Tanzania ikiwemo ya Kisiwani Pemba. 

MNYIKA AJIKOROGA, NAIBU WAZIRI WA MAJI AMPA 'MAKAVU' BUNGENI

$
0
0
Said Mwishehe, Globu ya jamii

MBUNGE wa Kibamba katika Jiji la Dar es Salaam John Mnyika (CHADEMA) ametakiwa kufanya ziara ndani ya jimbo lake ili kuona utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofanywa na Serikali ikiwemo ya miradi ya maji.

Mnyika ameelezwa hayo leo Bungeni Mjini Dodoma baada ya Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso kuelezea hatua ambazo zinachukuliwa na Serikali kutatua changamoto ya uhaba wa maji.

Wakati Aweso anazungumzia miradi ya maji alizungumzia jimbo la Kibamba na miradi ya maji ambayo imefanyika lakini baada ya maelezo hayo Mnyika alisimama bungeni na kumtaka aombe radhi kwa madai Naibu Waziri anasema uongo bungeni.

Mnyika alisema "Nimemsikia Naibu Waziri wa Maji anavyoelezea miradi ya maji na ametaja jimbo la Kibamba lakini ukweli hayo anayoyasema hayana ukweli wowote na ni vema akaomba radhi kwa kusema uongo bungeni."

Baada ya kauli hiyo ya Mnyika, Naibu Waziri wa Maji alitakiwa kutoa ufafanuzi na hapo ndipo alipoamua kumpa makavu mbunge huyo kwa kuelezea hatua ambazo zimefanywa na Serikali katika kutatua changamoto ya maji katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Kibamba jijini Dar es Salaam.

"Naomba nitumie nafasi hii kumshauri ndugu yangu Mnyika, tatizo lake hafanyi ziara katika jimbo lake na hivyo hata miradi ya maendeleo inavyotekelezwa na Serikali haoni.Ukitoka Bungeni nenda kafanye ziara ya kutembelea jimbo.

"Kote ambako nimetaja uwepo wa miradi ya maji iliyokamilika utaikuta.Wizara ya Maji kwa niaba ya Serikali inafanya kazi kubwa ya kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana,"amesema Aweso.

Naibu Waziri huyo pia ametumia nafasi hiyo kueleza wazi Serikali imedhamiria kutatua changamoto ya uhaba wa maji nchini na ndio maana imeanzisha Wakala wa Maji Vijijini ambayo itakwenda kumaliza tatizo lililoko sasa na kwamba Wizara ya Maji iko makini.

"Kupitia Wakala wa Maji Vijijini tunakwenda kumaliza tatizo la uhaba wa maji, na hata wale wakandarasi uchwara katika maji nao wanakwenda kuondoka kwa namna ambavyo Wizara ya Maji tumejipanga,"amesema Aweso.
MBUNGE wa Kibamba katika Jiji la Dar es Salaam John Mnyika (CHADEMA) akifafanua jambo Bungeni leo.Picha hisani ya Edwin Njwahuzi -Mwananchi.

WAZIRI LUKUVI ATOA NENO KWA MABENKI MAONESHO YA NMB NYUMBA DAY JIJINI ARUSHA

$
0
0
WAZIRI wa Ardhi Nyumba Maendeleo na Makazi ,William Lukuvi,amezitaka Taasisi za Kifedha hapa nchini ikiwemo Benki kuwawezesha wananchi wa hali ya chini kupata mikopo ya nyumba kwa riba nafuu.

Aidha amezitaka taasisi hizo za kifedha kushirikiana na kampuni za ujenzi ili kuwasaidia wananchi wanaochukua mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba,kumiliki nyumba kwa gharama nafuu.

Waziri Lukuvi aliyasema hayo jijini Arusha katika maonyesho ya NMB Nyumba Day,yaliyofanyika jijini hapa na kukutanisha wateja na watoa huduma katika ujenzi na uuzaji wa nyumba ambapo Benki ya NMB inatoa huduma ya mikopo kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kumiliki nyumba.

Amesema kuwa taasisi za fedha zinazotoa mikopo ya nyumba zinatakiwa kutafuta namna ya kuwasaidia wananchi ili kuweza kumudu na kupata nyumba kwa gharama nafuu.

"Ili gharama za ujenzi wa nyumba za Tanzania zisiwe za ghali taasisi za kifedha kuweni na mpango mahsusi,endelevu na ulio rahisi wa kumkopesha mtu nyumba,ili wananchi wa hali ya chini kupata mikopo kwa riba nafuu na mshirikiane na kampuni za ujenzi ili kuwasaidia wananchi wanaochukua mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba,kumiliki nyumba kwa gharama nafuu," alisema

Waziri Lukuvi aliipongeza Benki ya NMB kwa kuanzisha mikopo hiyo ambapo ni miongoni mwa Benki zilizopo hapa nchini ambazo zinashirikiana na wadau wengine kuhakikisha wananchi wanapata mikopo kwa riba nafuu na kuwawezesha kumiliki nyumba za makazi.

Awali Kaimu Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati kutoka Benki ya NMB,Salie Mlay,anasema benki hiyo imekuwa baina ya wananchi na serikali katika kuwawezesha wananchi ili wapate makazi bora. 
Waziri wa Ardhi,Nyumba Maendeleo na Makazi William Lukuvi,akizungumza na wananchi jijini Arusha leo,katika hafla ya maonyesho ya nne ya NMB Nyumba Day,yaliyofanyika katika eneo la Baracuda,jijini Arusha,maonyesho yaliyolenga kuwakutanisha wateja na watoa huduma za ujenzi na uuzaji wa nyumba ambapo benki ya NMB inatoa huduma ya mikopo kwa ajili ya kuwawezesha wateja wake kumiliki nyumba 
WAZIRI wa Ardhi Nyumba Maendeleo na Makazi ,William Lukuvi,maonesho ya NMB Nyumba Day,yaliyofanyika jijini Arusha akimsikiliza mmoja wa Wadau wa Maonesho hayo wakati wa maonesho hayi yaliyowakutanisha wateja na watoa huduma katika ujenzi na uuzaji wa nyumba ambapo Benki ya NMB inatoa huduma ya mikopo kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kumiliki nyumba.Pichani kulia ni Kaimu Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati kutoka Benki ya NMB,Salie Mlay.

UHAMASISHAJI WA UTAFITI UTAWEZESHA UHIFADHI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

$
0
0


Na Ismail Ngayonga,MAELEZO

TATHMINI za uwekezaji katika kutunza mazingira katika nchi ni moja ya kazi muhimu za Ofisi ya tathmini ya Baraza la Kituo cha Kimazingira Duniani (GEF) linalotoa taarifa na matokeo ya jumla ya miradi na utendaji katika ngazi ya kitaifa.

Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA) ambao ni mwongozo muhimu katika kuleta maendeleo endelevu, unatambua kuwa mazingira bora ni msingi wa maendeleo endelevu na kupunguza umaskini.

Mkakati huu umeainisha malengo 15 yanayohusu mazingira na utekelezaji wa MKUKUTA unahusisha wadau mbalimbali, ambapo Ofisi ya Makamu wa Rais (OMR) inalo jukumu la kuratibu ujumuishaji wa masuala ya mazingira katika mipango na bajeti za kisekta za kupunguza umaskini.

Katika kutekeleza jukumu hili, OMR imefanikisha na inaendelea kutekeleza mipango na programu kadhaa ikiwemo ile ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Mazingira, Sheria ya Mazingira na Kanuni zake.

Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 imeeleza wazi wajibu na majukumu ya wadau mbalimbali kuanzia serikali za mitaa hadi taifa ikisisitiza mipango na usimamizi wa matumizi endelevu ya mazingira: kudhibiti uchafuzi wa mazingira; utunzaji wa taarifa na takwimu za mazingira; utafiti na ushiriki wa jamii na utekelezaji wa majukumu yatokanayo na mikataba ya kimataifa.

Akiwasilisha Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/19, Waziri wa Nchi Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Januari Makamba anasema Serikali kupitia Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeendelea kutekeleza Ajenda ya Taifa ya Utafiti katika Mazingira (NERA 2017-2022).

Waziri Makamba anasema katika mwaka wa fedha 2017/18, NEMC kwa kushirikiana na wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kamisheni ya Matumizi ya Ardhi, Taasisi ya Huduma za Misitu na Halmashauri ya Wilaya ya Same imefanya tathmini ya hali ya mazingira kwenye maporomoko ya ardhi katika milima ya Mamba Miamba iliyopo Wilayani Same.

Anaongeza kuwa katika tathmini ya utafiti huo ilibaini chanzo cha maporomoko hayo ni aina ya udongo wa mfinyanzi uliopo katika eneo hilo pamoja na shughuli za kibinadamu zinazofanyika huko ikiwa ni pamoja na ukataji holela wa miti na uchomaji moto hovyo katika maeneo hayo.

Aidha anasema NEMC limepeleka mapendekezo ya kuzuia uharibifu wa mazingira katika eneo hili kwa wadau ili hatua thabiti za uhifadhi zichukuliwe, ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kulitangaza eneo hilo kuwa ni eneo tete la mazingira na kulitengenezea mpango wa kudhibiti uharibifu wa mazingira.

“Katika mwaka 2017/18, Baraza limefanya utafiti wa uharibifu wa mazingira wa Bwawa la Mindu lililopo katika Manispaa ya Morogoro na mmonyonyoko wa ardhi katika fukwe za Ziwa Viktoria. Matokeo ya tafiti hizo yalibainisha vyanzo mbalimbali vya uharibifu na kupendekeza hatua za kuchukuliwa” anasema Waziri Makamba.

Kwa mujibu wa Waziri Makamba anasema NEMC imefanya utafiti wa namna ya kuboresha mazingira ya mji wa Dodoma ili uwe ‘mji wa kijani’ kwa kutumia dhana za green city, eco-buildings nasustainable construction.

Akifafanua zaidi anasema katika mwaka 2017/18, Baraza limeendelea kuratibu shughuli za Hifadhi Hai kwa kuwasilisha taarifa za awali katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa ajili ya kuingiza Hifadhi ya Gombe Ugalla -Masito kwenye mtandao wa Hifadhi Hai za Dunia.

Waziri Makamba anasema NEMC pia imeandaa Mpango wa Usimamizi wa Mazingira (Environmental Management Plan-EMP) kwa maeneo mawili ambayo ni Dakio la Bonde la Kihansi na eneo la Ziwa Chala–Jipe. Aidha, Baraza limekamilisha zoezi la uwekaji mipaka katika eneo la Kihansi ambalo linatarajiwa kutangazwa kuwa eneo lindwa la kimazingira.

Anasema katika mwaka 2018/19, Baraza litaendelea kukusanya takwimu na na kuandaa taarifa za hali ya mazingira ya milima nchini, taarifa ya mazingira ya pwani (State of the Coastal Environment Report – SOCR, 2018); utafiti wa mifumo ya ikolojia ya hali ya mabonde ya mito mikubwa, maeneo ya malisho ya mifugo na wanyamapori.

Tanzania ni nchi yenye uwezo mkubwa wa kuweza kutoa manufaa kimazingira duniani, kwa kuzingatia changamoto za kimazingira za kitaifa na kimataifa zinazoikumba nchi ni wajibu wa wadau wa kitaifa na kimataifa kuwekeza rasilimali ili kukuza, kuchangia na kuthibiti maliasili ili kuboresha na kuongeza mchango wa Tanzania katika mazingira Duniani.

TBS Yatoa Elimu kwa Wananchi 22,322

$
0
0
Na Neema Mtemvu - TBS
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limemaliza Kampeni yake ya kutoa Elimu kwa umma katika Wilaya ya Nachingwea, Kilwa, Songea, Bukoba, Kahama,Tarime, Nyamagana, Korogwe, Kilombero na Kisarawe juu ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa na shirika hilo.

Kampeni hiyo ya Elimu kwa umma imefanyika katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya Shule za Msingi na Sekondari, Masoko, Stendi, Minadani na maeneo mengine ya wazi ambapo wananchi walijitokeza kupata elimu na ufahamu wa masuala mbalimbali yahusuyo Ubora wa Bidhaa.

Kwa upande wake Afisa Masoko Mwandamizi, Gladness Kaseka amewakumbusha Wananchi wote kuwa vita ya bidhaa hafifu sio ya TBS pekee bali ni ya Taifa kwa ujumla.

"Kampeni hii imeweza kuwafikia wananchi 22,322 kati yao wajasiriamali 437,wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari 6,653 na wananchi 15,232," Alisema Kaseka.

Aliwasisitiza wananchi kuendelea kutoa taarifa kupitia mawasiliano waliyopewa pale wanapogundua uwepo wa bidhaa hafifu katika soko.

Vilevile Shirika lilipata fursa ya kutoa semina kwa wajasiriamali wanaojihusisha na bidhaa mbalimbali zikiwemo za nafaka, sabuni,mikate, maziwa,pilipili,siagi ya karanga, karanga,korosho,mvinyo,mafuta ya kula,asali,batiki,vikoi na unga lishe juu ya utaratibu wa kupata leseni ya kutumia alama ya ubora ya TBS bure. 

Kampeni hiyo imemalizikia katika Wilaya za Korogwe, Kilombero  na Kisarawe.
 Afisa Uhusiano (TBS) Neema Mtemvu akizungumzia umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS na wanafunzi wa shule ya msingi Malunga wilayani Kahama.
 Wanafunzi wa shule ya sekondari Sirari wilayani Tarime wakisikiliza masuala ya ubora wa bidhaa
 Wajasiriamali wilayani korogwe wakifuatiliwa utaratibu wa kupatiwa leseni ya kutumia alama ya ubora bure.
 Wajasiriamali wilayani Kisarawe wakisikiliza kwa makini utaratibu wa kufuata ili kupata leseni ya kutumia alama ya ubora ya TBS bure.
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari  Kibaoni wilayani Kilombero,wakisikiliza kwa makini masuala yahusuyo ubora wa bidhaa
Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi(TBS) Amina Yasin akizungumza na wananchi wa soko kuu la Ifakara, wilayani Kilombero, juu ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS.

ACT WAZALENDO WAKIANDAMANA TU WATAPIGWA WATACHAKA-MUROTO

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAKATI kesho ya Aprili 9,mwaka huu Chama cha ACT Wazalendo kikitarajia kufanya maandamano makubwa ,tayari Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limesema limejipanga kukabiliana na waandamanaji hao na iwapo watajitokeza watapigwa mkapa watachakaa.

Akizungumza leo Aprili 8,2019, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema kuwa kupitia mitandao ya kijamii kuna taarifa za ACT Wazalendo kutaka kufanya maandamano kwa kushirikiana na baadhi ya vyama vingine kikiwemo Chama cha NCCR-Mageuzi.

"ACT Wazalendo wanakusudia kufanya maandamano kesho yaani Apirili 9,2019. Nataka kuwaambia hao wanaotangaza maandamano kwa njia ya mtandao wakiingia barabarani kama ni kweli watapigwa watachaa.Narudia tena watapigwa watachakaa,"amesema Kamanda Muroto .

Amefafanua Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa sasa linaendelea na mazoezi na lipo tayari kukabiliana na wandamanaji, hivyo wanawasubiri kwa hamu kama wapo huku akifafanua maandamano hayo ni haramu na hayapaswi kufanyika.

"Wananchi wa Mkoa wa Dodoma msiwe na wasiwasi, endeleeni na shughuli zenu kama kawaida na wabunge nao waendelee na vikao vya Bunge.Polisi tumejipanga na tuko tayari,"amesema Kamanda Muroto na kusisitiza watakaondamana hiyo kesho watapigwa watachaa.

Kwa kukumbusha tu, ACT Wazalendo walitangaza kufanyika kwa maandamano hayo ikiwa ni sehemu ya kuonesha hisia zao za kutofurahishwa na uamuzi wa Bunge la kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Profesa Mussa Assad

NEC yaungana na familia ya kumhifadhi marehemu Nanyaro kijijini kwao Arusha

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeungana familia, ndugu, jamaa na marafiki  kuuaga na kuuhifadhi kwenye makazi yake ya milele,  mwili wa mtumishi wake Clarence Nanyaro aliyefariki Aprili 2 mwaka huu na kuzikwa kijijini kwao Nkomaala, wilayani Meru mkoani Arusha.
Tume katika mazinshi hayo iliwakilishwa na Mkurugenzi Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Zanzibar, Felix Wandwe aliyeambatana na baadhi ya watumishi kumhifahdi marehemu Nanyaro aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Habari wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura.
Akizungumza wakati akitoa salamu za rambirambi, Mkurugenzi Wandwe alisema Tume inaungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki kuombeleza msiba wa mtumishi wake kwani marehemu Nanyaro alikuwa mtu wa kuaminiwa kutokana na utendaji kazi wake mzuri.
“Kwa niaba  ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi napenda kuwasilisha salamu za rambirambi kwa masikitiko makubwa.Marehemu alifanya kazi vizuri sana na tulimuamini na kumpenda, lakini kwa mapenzi ya  Mungu amemchukua, tunasema Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidewe” alisema Mkurugenzi Wandwe na kuongeza kuwa.
“Kuhusiana na suala la rambirambi napenda kueleza kwamba Ofisi inafanya utaratibu wa michango mbalimbali ambayo  baada ya hapa tutawasiliana na familia kujua utaratubu wa kuwasilisha.” “Pili kwa kuwa marehemu alikuwa mtumishi wa Serikali, kwa niaba ya Tume niseme kwamba zitafanyika taratibu za kisheria, kanuni na taratibu kuhusiana na stahiki zake na atapewa mtu kama sheria zinavyoelekeza”. 
Akitoa shukrani kwa niaba ya familia, Mkuu wa Boma Mzee Gadiel Nanyaro aliishukuru Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa huduma waliyoitoa kwa marehemu na kumuomba mwakilishi wake kufikisha shukrani hizo ofisini kutokana na ushirikiano mkubwa waliyoutoa kwa familia. Marehemu Nanyaro mbali na kufanya kazi Tume tangu mwaka 2015 hadi umauti unamkuta, pia alifanya kazi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Utangazaji (TBC) kwa nafasi mbalimbali.
Alifariki tarehe 2 Aprili mwaka huu kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na hivi karibuni alipata ‘Mild Stroke’ ambao ulisababisha alazwe kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa takribani siku 19 hadi umauti ulivyomkuta.
Akisoma akitoa salamu za rambirambi wakati watumishi wa Tume wakiaga mwili wa marehemu jijini Dar es Salaam, Mkugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura ya NEC, Giveness Aswile alisema alitoa shukrani za Tume kwa madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali ya Bochi kwa jitihada walizofanya katika kuokoa uhai wa marehemu.
“Tume inatoa shukrani kwa madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali ya Bochi kwa jitihada walizofanya katika kuokoa uhai wa marehemu.Pia inawashukuru viongozi wa dini, watu binafsi na taasisi mbalimbali kwa kumuhudumia marehemu wakati wa uhai wake.” alisema Mkurugenzi Aswile.

Marehemu ameacha mjane na watoto.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.
 Mkurugenzi Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Zanzibar, Felix Wandwe, akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Clarence Nanyaro, aliyezikwa mwishoni mwa juma hili kijijini kwao Nkomaala, wilayani Meru mkoa wa Arusha.
 Mjane wa Marehemu Clarence Nanyaro akiaga mwili wa marehemu
 Baba wa marehemu mzee Sabaya Nanyaro akiaga mwili wa marehemu mwanaye wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa marehemu.
 Mkurugenzi Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Zanzibar, Felix Wandwe akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.
 Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.
 Baba na mama wa marehemu wakiwa an nyuso za huzuni wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa marehemu.
 Baadhi ya waombolezaji waliohudhuria kumuaga marehemu Clarence Nanyaro, kwenye kijiji cha Nkomaala wilayani Meru mkoani Arusha.
 Baadhi ya waombolezaji waliohudhuria kumuaga marehemu Clarence Nanyaro, kwenye kijiji cha Nkomaala wilayani Meru mkoani Arusha.
 Baadhi ya waombolezaji wakishusha mwili wa marehemu kwenye kaburi lake.
 Baadhi ya watoto wa marehemu Clarence Nanyaro (wawili mbele) na mjane wa merehemu (kushoto aliyeshika kichwa) wakiwa kwenye majonzi wakati wa kuuaga mwili wa marehemu mpendwa wao.
 Mkurugenzi Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Zanzibar, Felix Wandwe, akimpa pole mjana wa marehemu Clarence Nanyaro an mtoto wake (kulia) baada ya kuuhifadhi mwili wa marehemu.
 Mkurugenzi Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Zanzibar, Felix Wandwe, akimpa pole baba wa marehemu mzee Sabaya Nanyaro.
 Mkurugenzi Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Zanzibar, Felix Wandwe, akimpa mkono wa pole mama wa marehemu Clarence Nanyaro.
 Mkurugenzi Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Zanzibar, Felix Wandwe, akiagana na Mkuu wa Boma, Mzee Gadiel Nanyaro baada ya kumaliza mazishi ya marehemu.
 Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Giveness Aswile wakati watumishi wa Tume walipouaga mwili wa mtumishi mwenzao Clarence Nanyaro katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi an waombelezaji wengine wakishiriki katika ibada ya kumuaga marehemu Clarence Nanyaro katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Picha na NEC


Airtel, DTBi yatoa mafunzo kwa wajasiriamali wanawake

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) imemaliza kutoa mafunzo ya Tehama kwa wanawake wajasiriamali yenye lengo la kuwapa ujuzi wa kutumia kompyuta ili kurahisha kufanya biashara zao kwa njia ya mtandao.

Mafunzo hayo yalikuwa yakifanyika kwenye maabara ya Tehama iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama Manispaa ya Kinondoni na yamefikia tamati mwishoni mwa wiki chini ya udhamini wa Airtel kwa kushirikiana na DTBi

Akiongea jijini Dar es Salaam mara baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo, Meneja maabara ya Airtel Fursa na ambaye pia alikuwa ni mratibu wa mafunzo hayo Michael Thomas alisema kuwa teknolojia inaweza kuwafanya wajasiriamali kupata na kutumia ujuzi wa mtandao na kupata taarifa au habari ambazo zina umuhimu na tija kubwa kwao. ‘Ni furaha sana kuona wajasiriamali wetu na hasa wanawake wamejitokeza kwa wingi kuja kupata mafunzo ya Tehama ambayo yatawasaidia kuendesha biashara zao kwa njia ya kisasa ya mtandao’, alisema Thomas.

‘Mafunzo haya ya Tehama yamewapa ujuzi wajasiriamali jinsi ya kutumia vitabu vya biashara kwa ajili ya kuhifadhi rekodi zao. Vile vile, yamewapa ujuzi wa kutumia kompyuta na hasa kwenye kufanya mahesabu ya mauzo na manunuzi, alisema Thomas huku akiongeza kuwa hii itakuwa ni fursa ya kipekee ya kukuza biashara zao kwa kutumia njia ya mtandao.

”Natoa rai kwa kwa wale wajasiriamali wanaonza au waliopo kwenye biashara kupata mafunzo ya Tehama kwani itasaidia kuwapunguzia kazi zao na vile vile kukuza biashara kwa njia bora ya kisasa ya mtandao, alisema Thomas.

Thomas alisema kuwa wajasiriamali wanawake wako na hamasa kubwa ya kujifunzi kozi mbali mbali zinazotolewa hapa. Tulikuwa na wajasiriamali wanawake 26 hapa na wote wameonyesha nia ya kweli ya kupata mafunzo, aliongeza Thomas.

Thomas aliongeza kuwa mpaka kufikia mwisho wa mafunzo hayo wajasiriamali hao wameweza kujifunza maana na historia ya kompyuta, kutumia applikesheni na programu tofauti za kompyuta, kutumia teknolojia kutangaza biashara na hasa kwenye face book na instragrams, kutumia kompyuta kuweka rekodi ya biashara zao, kutumia kompyuta kufanya hesabu ili kujua faida na hasara na pia kuweza kuzijua baadhi ya mambo ndani ya kompyuta.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema Airtel pamoja na DTBi zimeweza kuvuta wanafunzi wengi kujifunza Tehama tangu kuzinduliwa kwa maabara hiyo. Tumeweza kutoa mafunzo mengi kwa vikundi mbali mbali ikiwemo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, waalimu na kwa sasa wanawake wajasiriamali. Naomba nitoe rai kwa yeyote ambaye anataka kujifunza Tehama kujitokeza kwani tuna waalimu wanzuri na waliobobea, alisema Singano.

Wakati huo huo, DTBi imetangaza mafunzo ya Tehama kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wakati wa likizo inayokuja na kuwaomba Wazazi na walezi kuwasajili kwa kupitia www.teknohama.or.tz or www.airtelfursa.com au kwa kutembelea maabara ya Airtel Fursa ambayo ipo kwenye shule ya msingi ya Kijitonyama.
 Meneja wa maabara ya Airtel Fursa, Michael Thomas akitoa maelekeo ya mafunzo ya kutumia kompyuta kwa moja ya wajasiriamali wanawake Joyce Mmasi kwenye mafunzo ya Tehama kwa wajasiriamali wanawake yenye lengo la kuwapa ujuzi wa kutumia kompyuta ili kurahisha kufanya biashara zao kwa njia ya mtandao. Mafunzo hayo yaliendesha na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Meneja wa maabara ya Airtel Fursa, Michael Thomas akitoa maelekeo ya mafunzo ya kutumia kompyuta kwa moja ya wajasiriamali wanawake Elizabeth Joshua kwenye mafunzo ya Tehama kwa wajasiriamali wanawake yenye lengo la kuwapa ujuzi wa kutumia kompyuta ili kurahisha kufanya biashara zao kwa njia ya mtandao. Mafunzo hayo yaliendesha na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi wa Fedha kutoka Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) Makange Mramba (kushoto) akimkabidhi cheti moja ya wajasiriamali wanawake Martha Aloyce baada ya kuhitimu mafunzo ya Tehama kwa wajasiriamali wanawake yenye lengo la kuwapa ujuzi wa kutumia kompyuta ili kurahisha kufanya biashara zao kwa njia ya mtandao. Mafunzo hayo yaliendesha na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi wa Fedha kutoka Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) Makange Mramba (kushoto) akimkabidhi cheti moja ya wajasiriamali wanawake Devotha Michael baada ya kuhitimu mafunzo ya Tehama kwa wajasiriamali wanawake yenye lengo la kuwapa ujuzi wa kutumia kompyuta ili kurahisha kufanya biashara zao kwa njia ya mtandao. Mafunzo hayo yaliendesha na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi wa Fedha kutoka Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) Makange Mramba (kushoto) akimkabidhi cheti Ali Mohammed baada ya kuhitimu mafunzo ya Tehama kwa wajasiriamali yenye lengo la kuwapa ujuzi wa kutumia kompyuta ili kurahisha kufanya biashara zao kwa njia ya mtandao. Mafunzo hayo yaliendesha na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Matukio Airtel Tanzania Dangio Kaniki.


TRC yajivunia Ubora wa Miundombninu, Idadi ya Ajali yapungua lengo ni Kuzimaliza kabisa

$
0
0
Na Grace Semfuko-MAELEZO
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania TRC Masanja Kadogosa amesema shirika lake limepunguza ajali kubwa za treni kwa asilimia miamoja katika kipindi cha miaka mitatu na nusu na kwamba wanakusudia kuziondoa kabisa hata ajali ndogo kwa kuimarisha miundombinu ya reli.
Bw. Kadogosa alisema hatua hiyo inatokana na kuimarisha miundombinu ya Reli, Ukarabati wa Mabehewa na usimamizi wa usalama wa reli kazi kazi ambayo imefanywa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kutokana na kutoa zaidi ya shilingi Bilioni 3 za kuimarisha miundombinu ya reli inayosimamiwa na TRC.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungua mafunzo ya usalama katika uendeshaji wa shughuli za Reli kwa Wafanyakazi wa TRC, Mkurugenzi Mkuu huyo wa TRC alisema Serikali imekuwa ikiwawezesha kwenye uboreshaji wa miundombinu na sasa wameweza kudhibiti ajali  kwa kusimamia kwenye maeneo yote kuanzia upakiaji wa Abiria na mizigo, usalama wa njia za Reli pamoja na kuimarisha maeneo yaliyokuwa yakisababisha ajali za mara kwa mara.
“Sisi TRC hatutegemei kuwepo kwa ajali kubwa tena kwenye eneo letu, na hata hizi ndogo zilizopo zinazotokana na uzembe wa baadhi ya wafanyakazi tunaziondoa, tumeondokana na ajali hizi kwa sababu tumeimarisha miundombinu yetu yote na sasa tunatoa mafunzo ya usalama kwa wafanyakazi ili kuhakikisha tunaziondoa changamoto zote, tunamshukuru Mheshimiwa Rais Magufuli kwani fedha alizotoa zimefanikisha mambo haya” alisema Kadogosa.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha usalama wa reli na ulinzi TRC Mhandisi Adolfina Ndyetabula alisema usalama umeimarika na kuwataka wananchi kuitumia reli hiyo kwa ajili ya usafiri wa Abiria na mizigo.
“Huduma za Reli inayosimamiwa na TRC ni salama na tumeimarisha ulinzi, naomba wananchi tumieni huduma hizi” alisema Mhandisi Ndyetabula.
Nae Mkaguzi wa ishara,mawasiliano na umeme Wandema Mtambalike alisema suala la mawasiliano katika usafiri wowote duniani ni muhimu na kuongeza kuwa kwao yameleta manufaa makubwa ya kuondoa ajali za treni.
Mafunzo hayo ya wafanyakazi wa TRC yalihusisha idara za Ukaguzi wa Treni na njia yake, Ulinzi na Usalama, Umeme, ubadilishaji wa njia za treni, mafundi pamoja na watoa huduma kwenye reli hiyo.

KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE APRIL 11,2019.

WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA AWATAKA WALIMU KUWA WAZALENDO NA NCHI YAO

$
0
0
Mwenyekiti wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi,mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na naibu meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Lyata 
Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda akiwa na Mwenyekiti wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi alipokuwa kwenye mkutano na walimu wazalendo mkoani Iringa kujadili maswala ya uzalendo wa wananchi wa Tanzania kwa nchi yao
Baadhi ya walimu wazalendo walihudhulia mkutano huo uliongozwa na Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda







NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

WAZIRI mkuu mstaafu Mizengo Pinda amewataka walimu wazalendo wa mkoa wa Iringa kujifunza uzalendo kuwa na uzalendo wa nchi yao ili kuendeleza umoja na mshikamano na amani iliyopo inayosaidia kuleta maendeleo bila kuwa na chuki na visasi ambavyo mara nyingi vimekuwa vikivuruga amani.

Akizungumza na baadhi ya walimu wa shule za sekondari na shule ya msingi mkoani Iringa waziri mkuu mstaafu mizengo panda aliwataka walimu hao kujifunza nini maana ya kuwa mzalendo na ndio silaha pekee ya kuhakikisha tunakwepa kuanzisha vita kwenye nchi hii.

Kuthamini vitu vilivyopo katika nchi yako ni moja ya kuwa mtanzania mzalendo kwa kuwa utakuwa unalinda mali za nchi na kuhakikisha amani inakuwepo kwa kuna wananchi ambao ni wazalendo na nchi yao bila kujali itikadi ya vyama vilivyopo katika nchi hiyo” alisema Pinda

Pinda alisaema kuwa nchi nyingi ambazo hazijaingia kwenye vita ni nchi zile ambazo zimekuwa zikibadilishana uongozi bila kutumia mabavu,hivyo utaona nchi nyingi zinapigana kwa ajili ya kugombea madaraka lakini hali tofauti kwa nchi ya Tanzania.

“Angalieni nchi kama Somalia tu hapo jirani wanavyopigana kwa ajili ya kugombea kuongoza nchi huo sio uzalendo wa wananchi wa Somalia ndio maana leo hii nawaambieni kuwa lazima mjifunze nini maana ya uzalendo ili kulinda na kuthamini amani ya nchi yenu” alisema Pinda

Pinda aliongeza kwa kusema kuwa uzalendo kwa wananchi wa Tanzania umeanza kupungua kwa kuwa watu wengi hawajui nini maana ya kuwa mazalendo hivyo wanatakiwa kujifunza katika umri huo kuwa wazalendo na nchi yao.

Pinda aliwata walimu kuanza kuwa na uzalendo kuanzia pale ulipozaliwa au ulipokulia ndio utaanza kuijenda nchi hii kwa kuwa umeenza kuthamini toka ulipokuwa mdogo hadi ukubwani kwa kuwa watakuwa na lengo la kulinda amani ya nchi.

“Uzalendo pia huanzia pale unapohuzulia mikutano ya hadhara kwa lengo la kujifunza na kujua muelekeo wa mtaani kwako au kujua mwelekeo wa taifa kwa kuwa kwenye kila mkutano wa hadhara kuna mambo ya msingi utajifunza tu” alisema Pinda

Naye mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi aliwataka walimu kuwa makini na viongozi ambao wanawachagua kwa kuwa ndio chanzo cha kuharibu maendeleo ya nchi kutokana na kiongozi huyo kutokuwa na uzalendo wan chi yao.

“Wananchi wanasababisha umasikini wenyewe kutokana na kuchagua viongozi ambao hawana uwezo ndio hupelekea umaskini katika kwa wananchi waliomchagua kiongozi waliyekuwa na imani naye,hivyo kukosea kuchagua kiongozi bora ni kujitafutia matatizo wenyewe” alisema Ngerera

Hapi aliongeza kwa kuwaambia walimu hao kuwa sehemu ya kumfundisha wananchi uzalendo ni katika umri mdogo hasa wanafunzi kwa kuwa ndio kipindi ambacho wengi wameanza kuwa na uelewa wa maisha ni nini.

“Jamani lazima mjifunze mnapotaka kumlaumu kiongozi mlimchagua wenyewe ni lazima mjipie wenyewe kwanza mlikosea wapi na sasa mnatakiwa mfanye nini ili kuhakikisha mfanya kazi huku mkiwa mmetawaliwa na uzalendo wenu” alisema Hapi

Kwa upande wake Mwenyekiti wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi alimuakikishia waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda kuwa walimu wazalendo wamekuwa wazalendo kweli kweli kwa kuijenga Iringa mpya na kufanya kazi pamoja na serikali pamoja na chama tawala.
“Walimu unaowaona humu ndani wote ni wanachama wa chama cha mapinduzi na wapo tayari kukitumikia chama tawala kwa kuwa kinaongoza vizuri serikali kwa miaka yote” alisema Ngowi

Ngowi alisema kuwa walimu wazalendo wamekuwa wakifanya kazi ya kuutangaza uzalendo kwa wanafunzi na wananchi wote ambao wanatuzunguka kwa lengo la kufanya kazi pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli

“Rais wetu amekuwa akifanya kazi kwa kutunganisha watanzania wote kuwa kitu kimoja hivyo hata sisi walimu wazalendo mkoa wa Iringa tunamuunga mkono kwa kila jambo jema ambalo anaifanyia nchi yetu” alisema Ngowi

Ngowi alimazia kwa kumuomba waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda kuwafikishia salamu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kuwa walimu wazalendo mkoa wa Iringa wapo makini na wapo tayari kufanya kazi pamoja naye kwa kila jambo.

LIPENI KODI KWA WAKATI KWA MANUFA YA TAIFA -DC KIGAMBONI

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri akizungumza na wawekezaji wa vituo vya kuhifadhi mafuta na gesi ambampo ali wasisitiza waendelee kushirikina na wananchi pamoja na kulipa kodi kwa wakati kwa manufaa ya taifa letu katika mkutano uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi,John Makuri akizungumza na wawekezaji wa vituo vya kuhifadhi mafuta na gesi ambapo aliwahakikishi watatekeleza majukumu yao ya kulinda usalama wa raia na mali zao katika mkutano uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wawekezaji wa vituo vyakuhifadhi mafuta na gesi wakimsiliza Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri (hayupo pichani) katika mkutano uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.

YALIYOJIRI BUNGENI LEO APRIL 8,2019

RAIS DKT. MAGUFULI AKAGUA MASHAMBA YA MAHINDI YA GEREZA LA KILIMO NA MIFUGO LA KITAI MBINGA MKOANI RUVUMA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike mara baada ya kuwasili katika eneo la Mashamba ya Mahindi ya Gereza la Kilimo na Mifugo la Kitai lililopo Mbinga mkoani Ruvuma.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Mashamba ya mahindi ya Gereza la Kilimo na Mifugo la Kitai lililopo Mbinga mkoani Ruvuma huku akitoa maelekezo kwa viongozi hao wa Jeshi la Magereza nchini.
 Sehemu ya Mashamba hayo ya Gereza la Kilimo na Mifugo la Kitai lililopo Mbinga mkoani Ruvuma ambayo yamelimwa ekari 650 za mahindi katika mwaka huu.
  Baadhi ya Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Magereza wakisikiliza hotuba ya . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyokuwa akiitoa katika eneo hilo la Kitai Mbinga mkoani Ruvuma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Magereza katika eneo la Gereza la Kitai mara baada ya kukagua mashamba ya mahindi ya Gereza hilo lililopo Mbinga mkoani Ruvuma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza huku akiwa na mwanafunzi wa darasa la saba Cristian Josephat Komba ambaye alizungumza kuhusu uchakavu wa vyoo katika  Shule ya Msingi ya Kitai. Rais Dkt. Magufuli alichangia kiasi cha Shilingi milioni tano kwa ajili ya ujenzi wa vyoo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza huku akiwa na mwanafunzi wa darasa la saba Cristian Josephat Komba ambaye alizungumza kuhusu uchakavu wa vyoo katika  Shule ya Msingi ya Kitai. Wapili kutoka kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Onesmo Luwena 
 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wanafunzi wa katika  Shule ya Msingi ya Kitai mara baada ya kuwachangia kiasi cha Shilingi milioni tano
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike mara baada ya kuwahutubia. PICHA NA IKULU

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA MAHINDI CHA MLALE JKT SONGEA MKOANI RUVUMA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wapili kutoka kulia, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Husein Mwinyi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi CDF Jenerali Venance Mabeyo, watano kutoka  kulia, Mkuu wa JKT Meja Jenerali Martin Busungu watano kutoka kushoto, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Godfrey Zambi wanne kutoka kushoto pamoja na Mawaziri, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kiwanda cha Kuchakata Mahindi cha Mlale JKT kilichopo Songea mkoani Ruvuma. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Husein Mwinyi  wakivuta utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kiwanda cha Kuchakata Mahindi cha Mlale JKT kilichopo Songea mkoani Ruvuma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mashine za Kiwanda cha kuchakata Mahindi cha Mlale JKT kilichopo Songea mkoani Ruvuma huku akipata maelezo

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia unga wa mahindi (Sembe) uliopakiwa tayari kwa ajili ya kuingia sokoni katika kiwanda hicho cha kuchakata Mahindi cha Mlale JKT kilichopo Songea mkoani Ruvuma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anatoka ndani ya Kiwanda hicho cha kuchakata mahindi pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi CDF Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya ukaguzi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua sehemu ya awali ya mashine za kuchakata mahindi katika kiwanda hicho.

 Sehemu ya Mashine za Kiwanda hicho cha Kuchakata mahindi chha JKT Mlale.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Gawio la Shilingi Milioni 700 kutoka kwa Mkuu wa JKT Meja Jenerali Martin Busungu mara baada ya uzinduzi wa Kiwanda hicho.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibonyeza kitufe kuwasha mitambo ya kuchakata mahindi katika kiwanda hicho. PICHA NA IKULU

RAIS MAGUFULI: TUYATUMIE MAJESHI KATIKA KAZI ZA DHARURA KUHARAKISHA MAENDELEO KWA WANANACHI

$
0
0
RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Viongozi na Watendaji wa Wizara, Taasisi, Wakala na Mashirika ya Umma kuvitumia vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)katika kazi za dharura zinazohitaji kasi ya haraka ya utekelezaji ili kuwaletea Maendeleo Watanzania.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha Kuchakata Mahindi katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mlale Mkoani Ruvuma leo Jumatatu (April 8, 2019), Rais Magufuli alisema JTWZ na JKT ni miongoni mwa majeshi ya vyombo vya ulinzi na usalama yanayofanya kazi zake kwa kasi kubwa katika miradi mbalimbali pindi wanapopewa dhamana na Serikali.

Aliongeza kuwa pamoja na majukumu yake ya msingi katika kusimamia masuala ya ulinzi na usalama, vyombo vya ulinzi Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JTWZ) wakati wa hali ya usalama majeshi hayo yamekuwa yakitumika katika kutekeleza kazi za dharura pindi zinapotokea.

“Nawagiza Watendaji na Viongozi wa Wizara, Taasisi za Umma ndani ya Serikali kuvitumia vyema vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ikiwemo majeshi yetu ya JWTZ na JKT katika kutekeleza kazi za dharura zinatokea mara kwa mara, kwa mfano nimwemwagiza CDF sasa aunde magari ya zimamoto na kuyapeleka katika viwanja vyetu vya ndege ambapo ni miaka miwili sasa pamoja na zabuni yake kutangazwa na pesa kuwepo hakuna gari hiyo pale TAA (Mamlaka ya Viwanja vya Ndege)” alisema Rais Magufuli.

Akitolea mfano Rais Magufuli alisema kutokana na imani kubwa ya utendaji kazi wa JWTZ na JKT, Serikali imekuwa ikitoa zabuni za miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa nyumba na Ofisi za Serikali katika Miji ya Dar es Salaam, Dodoma na maeneo mengine ya nchi ambapo majeshi hayo yameweza kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi wa hali ya juu.

Akifafanua zaidi Rais Magufuli alisema Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuyawezesha majeshi yote ya vikosi vya ulinzi na usalama nchini ili yaweze kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda, ambapo alipongeza juhudi kubwa zinazofanywa na JWTZ katika kuunga mkono sera ya Serikali ya ujenzi wa viwanda kwa kuanzisha kiwanda cha kuzalisha maji na kiwanda cha kuchakata mahindi.

Aidha Rais Magufuli alisema kuvitumia vyombo vya ulinzi na usalama katika miradi ya dharura kutasaidia kuharakisha maendeleo kwa Watanzania, kwa kuwa historia inaonyesha kuwa majeshi ya Tanzania ikiwemo JWTZ hayajawahi kushindwa kazi yoyote inayopewa na Serikali huku na mfano ujenzi wa ukuta katika machimbo ya madini ya Tanzanite eneo la Mererani, ambalo lilijengwa kawa kipindi cha miezi 3 tu pamoja na ukubwa na ugumu wa kazi hiyo katika eneo hilo.

Akizungumzia kuhusu Kiwanda cha kuchakata mahindi cha Kambi ya JKT Mlale, Rais Magufuli alisema Kiwanda hicho kilichojengwa kwa gharama ya Tsh Milioni 414.77 na kuwa na uwezo wa kusindika tani 400 za mahindi, hakina budi kuwa msaada mkubwa kwa wakulima wa Mkoa wa Ruvuma ambao sehemu kubwa wanajishughulisha na uzalishaji wa mahindi.

Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi alisema mbali na majukumu ya ulinzi wa mipaka ya nchi na ulinzi wa amani katika nchi zenye migogoro, Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini ikiwemo JWTZ yamekuwa yakishiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali ikiwemo kuunga mkono sera ya Serikali ya Uchumi wa Viwanda.

Alisema kuwa Wizara yake imejipanga kuhakikisha kuwa inapunguza utegemezi wa bajeti kwa kuhakikisha kuwa inashiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali ikiwemo kujihusisha na shughuli za kilimo na uvuvi ili kuwezesha majeshi hayo kuwa na akiba ya kutosha ya chakula.

Aliongeza kuwa katika mwaka 2019, Serikali imechukua jumla ya vijana 32,000 ikiwemo vijana 20,000 wa mafunzo kwa mujibu wa sheria na vijana 12,000 wa mafunzo ya kujitolea ambao wamekuwa chachu ya mabadiliko makubwa ya kiutendaji na uzalishaji mali.

Naye Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo alisema JWTZ inaendelea kuunga mkono sera ya Serikali ya kufikia uchumi wa viwanda ambapo mbali na kuzindua viwanda vya maji na mahindi, Jeshi hilo limejipanga kuongeza wigo wa uanzisha wa viwanda vingine vingi zaidi ikiwemo viwanda vya kuchakata alizeti.

Alisema hadi sasa Jeshi hilo limeweza kupiga hatua kubwa zaidi katika uzalishaji wa malighafi mbalimbali za viwandani, na kuweza kutengeneza sera za jeshi hilo na hivyo kusaidia kuokoa kiasi kikubwa cha fedha zilizokuwa zikitumika hapo awali.

WANARIADHA MASHUHURI KUSHIRIKI NGORONGORO MARATHONI APRIL 20

$
0
0
Na woinde shizza globu ya jamii Arusha

Wanariadha nyota wa Tanzania  Alfonce Simbu na Josephy Panga ni miongoni mwa wakimbiaji mashuhuri ambao watashiriki katika mashindano ya Ngorongoro marathon  yanayotarajiwa kufanyika April 20 mwaka huu.
 
Wakimbiaji wengine nyota waliothibitisha kushiriki mashindano ni pamoja na Failuna Matanga,Anjelina Tsere ,Magdalena Shauri ,Fabian Joseph ,Faraja Damas pamoja na Natalia Elsante.

Akizungumza na Globbu ya Jamii leo muandaaji wa mbio hizo Meta Petro alisema kuwa mbio hizi ambazo zinafanyika kwa miaka 12 mfululizo zitashirikisha wakimbiaji zaidi ya 1000 kutoka ndani na nje ya nchi  wakiwemo wakimbiaji mashuhuri kutoka nchini Kenya.

Alisema mbio hizo zitakuwa za kilometa 21 ,kilometa tano pamoja na kilometa mbili na nusu kwa ajili ya watoto ambapo alitaja zawadi kuwa mshindi wa kwanza  wa kilometa 21 atapata milioni moja ,mshindi wa pili atapata laki tano ,na mshindi wa tatu atapewa laki tatu.

Alitaja malengo ya mbio hizo ni kupiga vita ujangili pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani.

"Unajua wananchi wengi na maanisha wa Tanzania wengi wamekuwa na tabia ya kutotembelea hifadhi zetu za taifa hivyo mbio hizi zitasaidia kuhamasisha wa Tanzania kuwa na tabia ya kutembelea hifadhi zetu" alisema Meta
  
Alisema  kuwa kwa washindi wa mita zote ambao watashika kuanzia Namba tano hadi kumi wao watapata fursa ya kutembelea mbuga ya wanyama  ya Ngorongoro  kwa ajili ya kujionea vivutio vilivyopo katika hifadhi hiyo.

Alitoa wito kwa wa Tanzania kujitokeza kushiriki mbio hizo .
Muandaaji wa Ngorongoro marathon akizungumza na Mwandishi wa habari hizi hii leo 

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KAMBI YA SERENGETI BOYS

$
0
0
*Asema Watanzania wanamatumaini makubwa kwao, waongeze bidii,

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametembelea kambi ya timu ya Taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 na kuwaeleza kuwa Watanzania wanamatumaini makubwa dhidi yao, hivyo waongeze bidii.

Alitembelea kambi hiyo Serengeti Boys iliyoko katika jiji la Kigali nchini Rwanda. Waziri Mkuu alikwenda Rwanda Aprili 7, 2019 kumuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye kumbukumbu za miaka 25 ya mauaji ya Kimbari.

Akizungumza na wachezaji hao jana (Jumapili, Aprili 8, 2019) Waziri Mkuu aliwataka vijana wanaounda timu hiyo ya Serengeti Boys wahakikishe wanafanya mazoezi ya kutosha ili waweze kushinda mechi zinazofuata.

“Watanzania wanamatumaini makubwa dhidi yenu nasi tunazidi kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu muweze kuibuka na ushindi katika michezo yenu iliyobakia itakayowawezesha kushiriki mashindano ya kombe la dunia.”

Kadhalika, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuipongeza timu hiyo ya Serengeti Boys kwa namna wanavyoitangaza nchi kimataifa kupitia kwenye mashindano mbalimbali wanayoshiriki na kuibuka na ushindi.

Waziri Mkuu alisema endapo timu hiyo ya Taifa ya vijana ya Serengeti Boys itaibuka na ushindi katika michezo yake miwili itakuwa imekata tiketi ya kushiriki mashindano ya dunia huko nchini Brazil kwa vijana wa umri wa miaka 17.

Kwa upande wao, wachezaji na uongozi wa timu ya Serengeti Boys walimkabidhi Waziri Mkuu kombe walilolipata baada ya kuichapa timu ya Rwanda katika mashindano maalumu kwa ajili ya kujiandaa na AFCON-U17.

Mashindano hayo maalumu ya Kimataifa yalishirikisha timu za umri wa chini ya miaka 17 kutoka nchi tatu ambazo ni Tanzania, Cameroon na wenyeji Rwanda, ambapo Serengeti Boys ilishinda mabao mawili kwa moja dhidi ya Cameroon na kutoka sare ya mabao matatu kwa matatu na Rwanda.

Pia, wachezaji hao wamemuahidi Waziri Mkuu kwamba watajitahidi kadiri ya uwezo wao kuhakikisha wanaibuka na ushidi katika mechi zilizobakia ili waweze kushiriki kombe la dunia. “Hatutawaangusha Watanzania.”

Awali, Waziri Mkuu alimshukuru Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mheshimiwa Balozi Ernest Mangu pamoja na maofisa wa ubalozi na Watanzania waishio Rwanda kwa kuendelea kuipa moyo Serengeti Boys. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhiwa kombe kutoka Nahodha wa timu ya Serengeti Boys, Morice Michael katika ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda, April 7,2019, kufuatia timu hiyo kuibika bingwa katika mashindano maalum kimataifa yaliyofanyika nchini humo. Mashindano hayo yalishirikisha timu za umri wa chini ya miaka 17 kutoka nchi tatu ambazo ni Tanzania, Cameroon na wenyeji Rwanda. Wanaoshangilia kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Ernest Mangu na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya Serengeti Boys, Khalid Abdallh.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Cherie Blair ambaye ni Mke wa Waziri Mkuu wa Zamani wa Uingereza, Tony Blair walipokutana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali nchini Rwanda April 8, 2019. Majaliwa na Cherie walikuwa wakitoka kuhudhuria hafla ya kumbukumbu ya miaka 25 ya mauaji ya kimbari nchini humo iliyofanyika April 7, 2019. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Ernest Mangu.
 Waziri Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Serengeti Boys .katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania. Kigali Rwanda April 7, 2019. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

KATIBU MKUU WA CCM DKT.BASHIRU AUNGURUMA ZANZIBAR

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Dk.Bashiru Ali Kakurwa amewataka vijana nchini kuwa mstari wa mbele kulinda kwa vitendo urithi wa fikra za kimaendeleo zilizoasisiwa na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Alisema kundi hilo la vijana linatakiwa kujengewa mazingira rafiki ya kuelezwa na kurithishwa maadili,historia na itikadi yakinifu zinazotokana na harakati za miongozo ya ASP na TANU ili kupata viongozi bora na makini wa sasa kama akina hayati Karume,Nyerere na Aboud Jumbe.

Wito huo ameutoa katika Mahojiano Maalum na Kituo cha Radio ya Bahari FM kilichopo Migombani Zanzibar, wakati akizungumzia siku ya Mashujaa ya kumbukizi ya miaka 47 toka kuuawa kwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Karume.

Alisema bila Waasisi wa Mapinduzi ya Januari 12,mwaka 1964 wakiongozwa na Hayati Karume pasingekuwepo na Muungano pamoja na uhuru wa Waafrika wa Zanzibar.

Alieleza kuwa ukweli ni kwamba Mapinduzi hayo ndio chimbuko la uhuru wa kimwili na kifikra,utu,haki za binadamu,ustawi wa kijamii na kimaendeleo pamoja na ukuaji wa Demokrasia.

Alisema miaka 47 ni umri ni mingi lakini ni muhimu kukumbushana kuwa bila jasho na damu za wanamapinduzi bado Zanzibar mpaka leo ingendelea kuwa chini ya Utawala wa Kisultani.

" Lazima tukumbushane japo kwa muda mdogo kwani miaka 47 ni mingi kwa umri lakini kwa nchi ambayo ni tegemezi na ipo katika nchi zinazoendelea ni michache sana kwani Watu waliopinduliwa bado wapo na wanatamani kurudi tena, jambo ambalo haliwezekani.",alisema Dkt.Bashiru.

Pamoja na hayo alisisitiza mambo matatu ya msingi yanayotakiwa kuzingatiwa na Vijana pamoja na makada wa CCM kuwa kwanza kutambua historia halisi ya Taifa lao, pili kusimamia misingi ya waasisi wa Taifa lao na tatu kuwa wabunifu ili waendeleze mapambano katika Mazingira Mapya ya zama za sasa za Sayansi na Teknolojia.

Dkt.Bashiru aliweka wazi kuwa ukombozi haupatikani bila ya mapambano baina ya pande mbili, hivyo CCM katika suala la Mapinduzi na Muungano ni lazima iwe imara katika kulinda upande wa kulinda historia isipotoshwe na waliopinduliwa.

Alisema CCM ambayo imeshinda kwa awamu ya kwanza ya ukombozi wa kisiasa ni lazima Jeshi lake ambalo ni Wanachama, Viongozi na Watendaji wasibweteke bali waendelee kuongeza nguvu za kumiliki umma na kuhakikisha upinzani unakosa sifa za kubaki katika ushindani wa kisiasa.

"Tusipojiimarisha vizuri hata haya Mapinduzi tunayoyazungumzia leo yatatuponyoka kwani mifano ipo mingi Nchi kama Somalia, na Sudan yaliwahi kuwa Mataifa huru yakawa shwari lakini leo hii katika mataifa hayo kunawaka moto.",alifafanua Katibu Mkuu huyo.

Aliongeza kuwa uwepo wa Muungano ni kwa sababu unalindwa hivyo ni muhimu kuambizana ukweli kuwa waliopinduliwa bado wapo na hawautaki muungano na wanaendelea kujenga hoja dhaifu ili muungano huo uvunjike.

Akizungumzia dhana ya Umoja uliossisitizwa na Waasisi wa Mapinduzi Dkt.Bashiru alieleza kuwa dhana hiyo ya umoja inatakiwa kurutubishwa hasa katika kusimamia misingi ya ukweli,haki,usawa na utu.

Katika maelezo yake Dkt.Bashiru alifafanua kuwa pindi wananchi wanapoanza kudharau yale yaliyopatikana kwa jasho na damu basi panavunjwa msingi mkuu wa maendeleo.

Alisema watu wanatakiwa kupewa haki mbali mbali kama haki ya kufikri, haki ya elimu, haki ya Afya pamoja na haki ya elimu pamoja na haki ya kujitawala kama Taifa mambo ambayo toka enzi ya Katiba za ASP na TANU mpaka hivi sasa zimeanishwa vizuri katika Katiba ya CCM ya mwaka 1977 iliyoeleza namna ya haki kuzilinda na kuzisimamia haki hizo.

Alisema CCM na Serikali zake inapambana vikali na vitendo vya rushwa ambayo ndio chimbuko la kuwakosesha haki mbali mbali wananchi.

Dkt.Bashiru akizungumzia mfumo wa Vyama vingi kuwa upo Kikatiba na Kisheria na kueleza kuwa miongoni mwa faida za mfumo huo ni vyama hivyo kuchangia uwepo wa amani na utulivu.

Alisema Chama Cha Mapinduzi hakikukurupuka kukubali mfumo huo bali kiliamini kuwa vyama hivyo vitakuwa na imani ya kisiasa,kushindanisha imani hizo na mikakati ili kupata Taifa bora na imara kwa nyanja zote hatua ambayo bado haijafikiwa.

Pamoja na hayo alipongeza kasi ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa upande wa Zanzibar kwa kueleza kuwa ameridhishwa na kazi hiyo ambayo ndio sehemu muhimu ya Chama Cha Mapinduzi kujijenga kisiasa kwa kuvuna wanachama wengi.

Aidha alitoa wito kwa Wanachama wa CCM kwa Zanzibar na Tanzania bara kuwa wahakikishe CCM inashinda kwa kura nyingi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019 pamoja na uchaguzi Mkuu wa Dola wa mwaka 2020,ili kuendelea kulinda Tunu za Taifa za Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar.

Katika mahojiano yake hayo aliahidi kuwa CCM itaimarisha Vyombo vyake vyoye vya Habari vilivyopo Zanzibar na Tanzania bara ili Watendaji wake wafanye kazi katika mazingira rafiki na kupata maslahi yanayoendana na hadhi ya Taasisi wanayoifanyia kazi.

Pamoja na hayo alizipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na CCM kwa ujumla kwa kuandaa utaratibu mzuri wa kuwaenzi na kuwaombea Dua ya Kitaifaa Waasisi mbali mbali walioshiriki katika harakati za Ukombozi wa Zanzibar wakiongozwa na Hayati Karume.

Mapema Katibu Mkuu huyo aliwatembelea Viongozi wastaafu mbali mbali wa CCM na Serikali zake akiwemo Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Waziri wa Zamani wa Mambo ya Ndani wa Serikali ya awamu ya Tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Ameir Mohamed, Rais mstaafu wa awamu ya Sita Dkt. Amani Abeid Karume na Mke wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume.
 KATIBU Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally Kakurwa akizungumza katika Kipindi Maalum kinachozungumzia Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa Zanzibar huko katika Kituo cha Radio ya Bahari FM Migombani Zanzibar.
RAIS mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya Sita Dkt.Amani Abeid Karume(kushoto), Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally Kakurwa(katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM zanzibar Dk.Abdulla Juma mabodi(kulia).
  KATIBU Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally Kakurwa(kushoto),Mke wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume(katikati),Naibu Katibu Mkuu wa CCM zanzibar Dk.Abdulla Juma mabodi(kulia)wakiwa na Mama Fatma Karume nyumbani kwake Maisara.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM zanzibar Dk.Abdulla Juma mabodi(kushoto) akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally Kakurwa(kulia) wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hayati Abeid Karume Zanzibar mara baada ya Katibu Mkuu kuhitimisha ziara yake fupi iliyoambatana na shughuli ya Hitma ya Siku ya Mashujaa.(PICHA NA IS-HAKA OMAR-AFISI KUU CCM Z'BAR).
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images