Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

BINGWA WA HIP HOP TUPAC SHAKUR ALIVYOUAWA

$
0
0
Na Moshy Kiyungi,Dar es Salaam.

Tupac Shakur alikuwa mwanamuziki maarufu wa muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani.

Alifahamika zaidi kwa jina lake la kisanii la 2Pac.

Shakur aliuawa kwa kupigwa risasi Septemba 13,1996 wakati akiwa anaendesha gari mjini Las Vegas, Nevada nchini Marekani.

Alikuwa mmoja kati ya wasanii wa muziki wa Hip hop, waliouza rekodi nyingi za muziki duniani.2Pac alikuwa mtoto wa Afeni Shakur, ambaye alikuwa mwanachama wa Black Panther Party. Mama yake alitolewa jela mwezi mmoja kabla ya kujifungua mtoto wake Tupac.

Shakur alikuwa na vipaji vingi vilivyo vilivyomuongezea umaarufu akiwa na umri mdogo.Vipaji hivyo vya Shakur ni kwamba alikuwa rappa, mwigizaji, mtayarishaji wa rekodi, mshairi, mwanaharakati na mtunzi wa nyimbo. 

Majina yake halisi alikuwa akiitwa ‘Tupac Amaru Shakur’. Maana halisi ya jina Tupac ni Nyoka inayong’ara. Majina ya ‘TuPac Amaru Shakur’ ni makubwa yaliyoweka historia kubwa katika dunia hasa kwenye suala zima la mziki wa Hip-Hop.

Alizaliwa mnamo mwaka Juni 16, 1971 katika jiji la New York, nchini Marekani.Mara nyingi aliitwa 2Pac, Pac, Makaveli na pia mwenyewe akajiita The Don Kiluminati.Tupac, pia alishawahi kushikilia rekodi ya Guinness ya ulimwengu (Guinnes World Record), kwa kuwa na mauzo ya juu sana kwa msanii wa muziki wa rap ya hip hop.

Shakur aliwahi kupata mauzo takriban milioni 74 kwa hesabu ya dunia nzima na milioni 44 kwa mauzo ya Marekani pekee.Alishirikiana na baadhi ya vikundi na wanamuziki wakubwa nchini mwake kama Outlawz, Thug Life, Danny Boy, Digital Underground, Dr. Dre, Johnny "J",Ice Cube, Nate Dogg, The Notorious B.I.G. na Snoop Dogg.

Chanzo cha kifo chake kilielezwa kwamba mnamo Septemba 07, 1996 Tupac alikwenda katika jiji la Las Vegas, kwa ajili ya kuhudhuria pambano la ngumi kati ya bondia Mike Tyson alipokuwa akinyukana na mpinzani wake Bruce Seldon.

Kwa mujibu wa taarifa zilieleza kwamba 2pac alifikia katika hoteli moja ya kifahari jijini Las Vegas iliyokuwa inaitwa Luxor Hotel - Casino.Mpambano huo wa ngumi ulikuwa unafanyiika katika ukumbi maarufu ujulikanao kama MGM Grand Hotel.

Ilielezwa kwamba siku ya mpambano huo, Tupac alihudhuria sambamba na Goons (kampani) yake akiongozwa na Marion ‘Suge’ Knight, ambaye alikuwa mwanzilishi na mmiliki wa record label ya Death Row.Kampuni hiyo ilikuwa ikisimamia kazi za muziki za Tupac ikiwemo kurekodi nyimbo na kadhalika.

Katika mpambano huo, Tupac aliketi kiti kimoja na mlinzi wake aliyekuwa akiitwa Frank Alexander na rafiki wa Suge knight, sambamba na mcheza filamu maarufu wa Hollywood Louis Gossett Jnr.

Wengine waliokuwa karibu naye walikuwa Mchungaji Jesse Jackson, Charlie Sheen pamoja na mchezaji wa baseball aliyevuma wakati huo Reggie Jackson katika eneo la wageni maalumu (V.I.P).

Kwenye pambano hilo kiti kimoja cha V.I.P, kilitozwa kiasi cha dola za kimarekani 1,000, hiyo ilitokana na ukubwa wa pambano hilo.Hivyo watu walioweza kuketi viti vya V.I.P.walikuwa ni mashuhuri na wenye ‘mkwanja’ wa nguvu.

Wimbo alioingia nao Mike Tyson kabla ya pambano lake kuanza, uliandikwa na Tupac Shakur uliokuwa unaitwa ‘Wrote The Glory’.Katika pambano hilo Mike Tyson aliweza kuibuka kidedea baada ya kumchakaza mpinzani wake Bruce Seldon katika raundi ya pili ya pambano hilo.

Baada ya Pambano hilo kuisha, kundi ambalo lilikuwa linaongozwa na Tupac Shakur, liliingia katika mzozo katika sebure ya ukumbi wa MMG baada ya kurushiana maneno dhidi kundi lingine.Chanzo ugomvi huo hakikuweza kujulikana mara moja licha ya kwamba askari wa usalama ukumbini hapo waliweza kuingilia kati ili kuweka hali ya amani.

Ilielezwa kwamba Tupac na kundi lake waliondoka katika eneo hilo la tukio na kuelekea katika Hotel waliyofikia.Kifo hicho kiliacha maswali mengi na simanzi miongoni mwa wapenzi na mashabiki wa muziki kutoka katika kila pembe za dunia.

2Pac Shakur wakati wa uhai wake alikuwa mmoja kati ya marapa waliojizolea umaarufu mkubwa na mafanikio kupitia kazi ya muziki kwenye miaka ya 1990.

Hata hivyo alikuwa na kipaji kingine cha uigizaji.

Septemba 13, 2019, ‘TuPac Amaru Shakur’ atatimiza miaka 23 tangu kutokea kifo chake baada ya kupigwa risasi mnamo Septemba 13,1996 wakati akiwa anaendesha gari mjini Las Vegas, Nevada.

DAWA MUHIMU ZAIDI YA 300 ZINAPATIKA KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA

$
0
0
Serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kuvuka kiwango cha upatikanaji wa dawa muhimu kwa binadamu kilichowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika ngazi ya Hospitali ya Wilaya kwa kuwa na idadi kubwa ya dawa muhimu zinazopatikana kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alipotembelea Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe kujioinea hali ya utoaji wa huduma.
Waziri Ummy Mwalimu aliyeongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula pamoja na watendaji walio chini ya Wizara yake, amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano imeendelea kuboresha upatikanaji wa dawa kwa wananchi huku ikipitiliza kiwango kilichowekwa na WHO kwa kuwa na dawa muhimu 312 huku kigezo kilichowekwa na Shirika la Afya Duniani kikiwa ni dawa 30.
“Tuna mfumo wa ukusanyaji wa taarifa kuanzia ngazi ya zahanati, kituo cha afya mpaka hospitali unaotuwezesha Serikali kutambua mahitaji na matumizi ya dawa katika vituo vya kutolea huduma” amesema Waziri Ummy wakati akifafanua namna ya Serikali ilivyojipanga kupata takwimu sahihi za dawa.
Waziri Ummy amesema kuwa zipo propaganda zinazoendeshwa na watu wenye ushawishi ambao wamekuwa wakiwahadaa wananchi kwa kusema kuwa dawa hakuna ili hali dawa zipo na zinapatikana katika vituo vya kutolea huduma.
“Ni lazima tumtendee haki Rais wetu DKt. John Pombe Magufuli, amefanya makubwa kwenye Sekta ya Afya kwa kuboresha upatikanaji wa Dawa, tunaposema tumeongeza upatikanaji wa dawa maana yake dawa zinapatikana kwa urahisi hata kwenye vituo binafsi” amesema Waziri Ummy,
Waziri Ummy amezitaja dawa zenye kipaumbele kikubwa zikiwemo Dawa za kudhibiti maambukizi ya bakteria (Antibiotics), Dawa za kudhibiti Malaria, Dawa za magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Dawa za uzazi salama pamoja na Dawa za maumivu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa Ofisi yake kupitia Waziri wa Afya wako mbioni kuwasilisha muswada wa Bima ya Afya ambao utawawezesha wananchi wote sasa kuwa na bima ya afya.
Aidha, Dkt. Chaula amewataka watumishi katika Hospitali hiyo kuwahamasisha zaidi wagonjwa kujiunga na huduma za bima ya afya ili kuwa na uhakika wa matibabu pindi wanapougua.
“Niwaombe watendaji wote hapa kuwasisiza wagonjwa wanaofika hapa kupata matibabu kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya” Alisema Dkt. Chaula.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Winfred Kyambile amesema kuwa hali ya upatikanaji wa huduma imeimarika kutokana na mapato kuongezeka hivyo kuiwezesha Hospitali kutoa huduma bora kwa wananchi.
Dkt. Kyambile amesema kuwa kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa  imesaidia kuongezeka kwa mapato hospitalini hapo, amesema kuwa hapo awali mapato ya hospitali hiyo kwa mwezi yalikuwa Shilingi Milioni 12 huku sasa mapato hufikia Shilingi milioni 90 mpaka 100, fedha ambazo amesema wanazitumia kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikagua dawa zilizopo katika Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula mapema jana walipotembelea Hospitali Teule ya Mkoa wa Njombe kujionea hali ya utoaji wa huduma. 
 Ukaguzi wa hali ya utoaji huduma ukiendelea katika Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe, Kutoka upande wa kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Zainab Chaula na mwisho ni Mganga Mfawidhi Hospitali hiyo Dkt Winfred Kyambile.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa amemebeba mtoto mchanga kwa furaha kwenye wodi ya mama na mtoto katika Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe.

Rais Magufuli atengua uteuzi wa DED Nyasa na amteua Jimson Mhagama kuwa DED Nyasa

MWANAMUZIKI FRED MAYAULA MAYONI ALIICHEZEA YANGA

$
0
0
Na Moshy Kiyungi

Katika orodha ya wachezaji waliowahi kuicheza klabu ya Dar Young Africans ya Tanzania, Fredy Mayaula Mayoni ni miongoni mwao. Historia inaeleza kuwa baba yake alikuwa mwanadiplomasia katika ubalozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Zaire) nchini Tanzania, Mayaula alimfuata baba yake na ndipo alipojiunga klabu hiyo.

 Mayoni alikuwa mwanamuziki mkongwe mwenye kipaji cha utunzi na kuimba muziki wa dansi toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Alikulia na kusomea katika jiji la Dar es Salaam, mnamo  miaka ya 1960. Alimaliza shule za awali bila matatizo na kumaliza elimu yake mwaka 1962, katika chuo cha Kisantu nchini humo.

Fredy alipenda sana kusakata mpira wa miguu. Kati ya mwaka 1968 na 1971,  akicheza nafasi ya winga wa kushoto katika klabu ya ‘AS Vita  ya Kinshasa. Aidha katika juhudi zake za kujituma katika uchezaji wa mpira huo wa miguu, aliweza kuchaguliwa hadi  timu ya taifa ya nchi yake.

Akiwa Tanzainia, Mayaula alianza kuonesha cheche za kusakata kabumbu mara alipojiunga na klabu Dar Young Africans ya jijini Dar es Salaam. Baadae aliondoka akaelekea jiji la Charleroi, nchini Ubelgiji alikokwenda kujiendeleza kimasomo katika maomo ya Data Processing. Akiwa huko alijiunga na timu ya mpira ya ‘Racing Club de Charleroi’ baadae akajiunga na ‘Racing Club de Jette’ ya Brussels.

Mayaula kwa muda mfupi alichezea timu ya FC Fribourg ya Switzerland, na katika kipindi hicho alipoanza kujifunza kupiga gitaa. Muda si mrefu akajiunga na bendi ya wanafunzi wa Kikongo, iliyokuwa ikiitwa Orchestra Africana, akiwa kama mpiga gitaa la rhythm.

Fred aliporudi Kinshasa, akabadili kazi kutoka kwenye mpira wa miguu na kuwa mwanamuziki mtunzi. Haikuchukua kipindi kirefu kugundulika kipaji chake na kiongozi wa bendi ya T.P.OK. Jazz, Franco Luambo Makiadi, aliyemtaka kujiunga katika bendi yake.

Mayoni ndiye aliyetunga wimbo wa Ndaya mwaka 1977, ukaimbwa na mwanamuziki Mpongo Love. Wimbo huo ulikuwa unaongelea kuhusu mwanamke aliye na furaha kutokana na kuwa na mume bora na kuweza kumbana mumewe kutoka kwa wanawake wengine.

Mayaula alitunga wimbo mwingine ‘matata’ uliokuja kuwa maarufu wa Cherie Bondowe’ au ‘Sherry Bondowe. Kibao cha Cherie Bondowe, kilipokewa vizuri sana na wapenzi wa muziki. Kwa bahati mbaya National Censorship Commission ya Zaire wakati huo, iliupiga marufuku wimbo huo kwa kuwa hadithi yake ilikuwa ikimuelezea ‘changudoa’ mmoja aliyekuwa akibainisha shughuli zake zilivyo.

Wasifu wa Fredy Mayaula Mayoni unaonesha kuwa alizaliwa Novemba 06, 1946,  katika jiji la Léopoldville, ambalo sasa linaitwa Kinshasa. Yasemekana kuwa japo Franco alimkaribisha Mayaula kujiunga na bendi hiyo, hakuwahi kuwa mwanachama halisi wa kundi hilo kwani alipendelea kuwa huru kutunga nyimbo zake.

Tungo zake kadhaa zilifanyiwa kazi na T.P. OK. Jazz kama vile Nabali Misere na Moni. Mayaula aliondoka  Zaire mwaka 1981 akiwa na wanamuziki kutoka bendi ya Abeti Masikini na kuhamia Afrika Magharibi. Hadi kufikia mwaka 1984, tayari likuwa merekodi album kadhaa chini ya label ya Disc-orient ya mjini Lome nchini Togo.

Mwaka 1984 alirudi Zaire, ilipotimu  mwaka 1986 alitoka na album iliyoitwa ‘Fiona Fiona’. Mwaka huohuo Tshala Muana alipata umaarufu kutokana na wimbo Nasi Nabali’, uliotungwa na Mayaula Mayoni. Baada ya hapo akarekodi album yake Mizele akiwa na T.P. OK Jazz, wakisindikizwa na waimbaji Carlito Lassa na Malage de Lugendo.

Album ya ‘L’amour au Kilo, ilifyatuliwa mwaka 1993 na miaka saba baadae akatoa album nyingine ya Bikini. Baada ya album hiyo Mayaula alihamia Dar es Salaam na kuanza kufanya kazi ubalozi wa Kongo. Wakazi wengi wa Magomeni jijini Dar es Salaam watamkumbuka Mayaula, ambaye  katika kipindi hicho akifanya kazi ubalozini, alikuwa akiishi maeneo hayo.

Baadaye Mayaula Mayoni akaanza kuugua na kuamua kurudi kwao alikozaliwa katika kijiji cha Makadi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hali ya afya yake ilizidi kuwa mbaya mwaka 2005  alipelekwa nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo juhudi hizo hazikuzaa matunda kwa Mayaula akafariki dunia katika jiji hilo la Brussels nchini Ubelgiji  Mei 26, 2010 akiwa na umri wa miaka 64. Katika maisha yake ya muziki, Mayaula aliwahi kuchaguliwa kama mtunzi bora nchini mwake Zaire 1978, kwa wimbo  Bondowe 2, mwaka 1979 kwa wimbo Nabali Misere na mwaka 1993 Ousmane Bakayoko’

DAWA ZA KULEVYA ZILIVYOMCHOMOA AISHA MADINDA.

$
0
0
Na Moshy Kiyungi,Dar es Salaam

Tatizo la madawa ya kulevya ni janga kubwa duniani kote, ambapo idadi kubwa ya watu wameathirika.

Janga hili halichagui tajiri, masikini, jinsia, rika, vijana kwa wazee pia wamo.Madawa ya kulevya hutumiwa kwa njia ya kunywa, kunusa, kula au hata kujidunga.

Matokeo yake hubadili akili au fikra za mtumiaji kuwa tofauti na akili zake za kawaida.Yasemekana kuwa wapo watu wengi wanaotumia madawa hayo wakiwemo baadhi ya Wasanii, Wanamuziki na baadhi ya vijana, waliojiingiza katika matumizi hayo ya madawa ya kulevya.

Katika makala haya yanamzungumzia aliyekuwa mnenguaji mahiri humu nchini, aliyejiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya, yakapelekea kupoteza maisha yake. Msanii huyo ni Aisha Mohammed Mbegu ‘Aisha Mandinda’, aliyekuwa mnenguaji maarufu humu nchini.

Mara baada ya kujiingiza katika matumzi ya madawa ya hayo, tabia na maisha yake kwa ujumla yalikuja kubadilika kabisa.

Aisha Madinda alifikia hatua ya kucheza picha ya utupu ikarushwa kwenye mitandao ya kijamii, akionesha sehemu zake zote nyeti, akisindikizwa sauti ya kibwagizo cha ‘Alamba Alamba’ kilichochoachiwa na aliyekuwa Mfalme wa taarabu nchini, Mzee Yussuf.

Msemo wa Kiswahili usemao “Majuto mjukuu” ulijionesha dhahiri kwa mwanamama huyo baada ya kujikuta amepoteza mwelekeo wa maisha.

Aliwahi kutamka kuwa anajuta kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya, kwamba yamechangia kuharibu maisha yake aliyoyatengeneza akiwa na nguvu zake.Aisha alisema kwa uchungu kwamba alighiribika na kujikuta akiuza nyumba zake tatu kwa bei ya kama katoa bure, ili kupata fedha za kununua madawa hayo.

Majina yake kamili alikuwa alikuwa akiitwa Aisha Mohammed Mbegu, aliyezaliwa katika Hospitali ya Ocean Road, jijini Dar es Salaam mwaka 1980.Kutokana na wazazi wake kuhamishiwa Mkoani Mbeya kikazi, Aisha alilazimika kuanza masomo yake katika shule ya Msingi Kiganamo iliyopo wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, hadi alipohitimu darasa la saba mwaka 1992.

Mwaka 1993 alihamishia makazi yake mjini Kigoma akajiunga na shule ya Sekondari ya Katubuka.Kwa bahati mbaya hakufanikiwa kuhitimu masomo yake ya sekondari, baada ya wazazi wake kushindwa kumlipia karo hivyo aliishia kidato cha pili tu.

Baada ya kukatisha masomo yake, mwaka 1994, alihamia jijini Dar es Salaam na kuanza kazi ya usafi katika Kampuni iliyojulikana kama Dar Cleaner, ambako alifanya kazi ya usafi katika majengo mbalimbali.

Aisha alijiingiza rasmi kwenye unenguaji mwaka 1996, baada ya Prodyuza wa muziki aliyefahamika kwa jina moja la Maloni, kumtonya kuwa Club Billicanas ilikuwa ikihitaji wanenguaji.

Club ya Billicanas ilianzisha kundi la wanenguaji la Bill Bambums, yeye akawa miongoni mwao.Kundi hilo lilikuwa likiundwa na yeye pamoja na Mussa Hassan ‘Super Nyamwela’, ambao kwa pamoja walikuwa wakitoa burudani maridadi katika ukumbi huo wa Club Bilicanas.

Katika enzi za uhai wake alikiri kwamba alichagua kazi ya unenguaji, akafanikiwa na kudumu ndani ya kazi hiyo kwa takriban miaka kumi na sita.Mwaka 1999, mkali huyo wa nyonga ambaye tayari alishakuwa tishio kokote apandapo jukwaani, alipata ‘mchongo’ wa kwenda kupiga ‘kazi’ Uarabuni katika mji wa Muscat.

Aliambatana na mnenguaji mwenzake aliyekuwa swahiba wake Halima White ambaye naye ni marehemu pia. Walipiga kazi kwa takriban mwaka mmoja na mwaka 2000 walirejea nchini.Aisha mara baada ya kurejea, alichukuliwa na bendi ya Borabora Sound, ambako aliitumikia kwa miezi sita kabla hajaachana nayo.

Aliondoka tena kwenda Bahrain, Uarabuni ambako alipiga kazi katika kumbi mbalimbali nchini humo kwa miezi mitatu.Aisha aliporejea Dar es Salaam kwa mara nyingine, alijiunga na bendi ya The Kilimanjaro Connection ambapo pia hakukaa sana.

Mwaka huohuo wa 2000 mwishoni, akaachana na bendi hiyo, akaamua kufanya biashara zake ndogondogo.Mwaka 2001, Aisha Madinda ndipo aliamua kujiunga rasmi na bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’.

Aisha baada ya kujiunga na bendi hiyo, akawa kivutio kikubwa kwa wapenzi na mashabiki wa bendi hiyo kufuatia urembo wake, shepu nzuri na tabasamu usoni mwake wakati wote.Wapenzi wa bendi hiyo ya Twanga walikuwa wakipaza sauti wakimhitaji pindi Aisha Mdinda ikitokezea siku amekosekana katika onesho la bendi hiyo, kwa kuwa pengo lake lilionekana mapema.

Mnenguaji huyo kwa tabia hakuwa na makuu wala majivuno yeyote, licha ya kujaaliwa kuwa na maisha mazuri.Alifanikiwa kujenga nyumba tatu, alimiliki usafiri wake pia watoto wake aliwapa chakula na malazi bora, pia aliweza kuwapeleka shule nzuri.Aisha Madinda alipiga kazi ya unenguaji hadi mwaka 2011, mwishoni, akaenda kujiunga katika bendi ya Extra Bongo iliyokuwa ikiongozwa na Ally Choki.

Wakati huo tayari alikuwa ameshakuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya.
Ilifikia hatua ya kushindwa kunengua jukwaani, shoga zake walikuwa wakimfariji kwa amaneno matamu kuwa asikate tamaa bado ana nguvu bora alilie uzima wake.

Mkurugenzi wa kampuni African Stars Entertainment Tanzania, Asha Baraka na yeye alionesha dhamira ya kumsaidia Aisha, ili aweze kurudi katika hali yake ya zamani.Hivyo akawa anakwenda kuchukua fedha mara kwa mara kwa ajili ya manunuzi ya mahitaji yake kama mwanamke wa mjini.

Baadae afya yake ilianza kuimarika akaweza kuhudhuria onesho la usiku wa Mwafrika katika ukumbi wa Club Bilicanas.Hakika usiku huo baadhi ya watu walimsahau kwani alikuwa amependeza na amerudi katika hali yake ya zamani.Wakamsisitiza aendelee na tiba ya dawa za Methodine ambazo alikua anatumia.

Wadau wa Twanga Pepeta walipania kumrudisha katika hali yake ya kawaida, wakitamka kuwa kupotea kwa kipaji cha Aisha kuliwauma mno.
Wakajitolea kwa hali na mali ili kuyanusuru maisha yake.Aisha Madinda alikuwa ni mama wa watoto wawili na mjukuu mmoja.

Wakati akihangaika ujinasua na janga hilo ili alikuwa akipita huku na kule ili aweze kupata tiba ya ugonjwa unaomsumbua.Hivyo Aisha aliwahi kuokoka na alithibitisha hilo. Yaelezwa kuwa alifanya hivyo kwa kuamini kwamba matatizo yake yangemalizika kwa kuombewa.

Aisha Mohamed Mbegu maarufu kama ‘Aisha Madinda’ alikutwa na rafiki yake Samira Saleh akiwa amelala usingizi mzito kibarazani nyumbani kwake Mabibo (Nyumbani kwa Samira).Samira alibainisha kwamba Aisha Madinda hakuwa kwake, lakini alimkuta barazani kwake asubuhi ya akiwa hajitambui.

Alisema kuwa alijitahidi kumtingisha lakini Aisha alikuwa kimya na hivyo akaamua kuchukua Bajaji na kumkimbiza hospitali ya Mwananyala, jijini Dar es Salaam.Walipofika katika hospitali ya Mwananyamala majira ya saa 2 asubuhi, Daktari aliyempokea akamwambia tayari mgonjwa wake alishafariki dunia Desemba 17, 2014.

Kamanda wa kanda ya Polisi mkoa wa Kinondoni wakati huo Camillus Wambura, alithibitisha kutokea kwa kifo chake.

Samira alieleza ukweli kwamba yeye kama alivyo Aisha Madinda, ni muathirika wa madawa ya kulevya ambapo anaitaja hospitali ya Mwananyamala ndio Kliniki yao ya kupata tiba saidizi (MAT) ya madawa ya kulevya na ndio sababu hakumpelekea hospitali nyingine yoyote zaidi ya Mwananyamala.

Marafiki wa Aisha Madinda ambao nao ni waathirika wa madawa ya kulevya, walisema Aisha Madinda alikwa amerudia utumiaji wa madawa hayo, wanamashaka kuwa alitumia kiasi kikubwa kuliko inavyohitajika na pengine ndio sababu ya kifo chake.

Maziko ya Aisha Madinda yalicheleweshwa kutokana na zuio la Jeshi la Polisi, kupisha uchunguzi wa sababu za kifo cha ghafla cha mnenguaji huyo.

Hatimae mwili wa Aisha Madinda ukashushwa kwenye nyumba yake ya milele Desemba 19, 2014, kwenye Makaburi ya Kijiji cha Mikwambe, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Hadi mauti yanamkuta alikuwa katika dozi ya kujinasua na matumizi ya mihadarati na alikuwa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Baada kifo hicho Asha Baraka alimwelezea Aisha Madinda kuwa alikuwa ndio kwanza amerejea kutoka Dubai alikokuwa amekwenda kwa shughuli za kimuziki na kwamba alikuwa hajajiunga na bendi yoyote hadi mauti yanamkuta.

Kwa upande wake Katibu wa bendi ya Twanga Pepeta, Luiza Mbutu alisema kuwa Aisha alitazamiwa kuanza mazoezi na bendi ya Twanga Pepeta kwa ajili ya maandalizi ya miaka 16 Luiza Mbutu ndani ya Twanga Pepeta.

Hii ni picha kamili ya ubaya wa kutumia madawa ya kulezya.

Makala hii inakuasa wewe achana na fikra potofu za kutaka kutumia madawa ya kulevya.

Mungu aipumzishe roho yake pahala pema peponi, Amina.

NHIF YAWAFIKIA WANANCHI WA MAFIA NA HUDUMA ZA MKOBA ZA MADAKTARI BINGWA

$
0
0
 Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umezindua rasmi huduma za Mkoba za Madaktari Bingwa wilayani Mafia mkoani Pwani ambazo zitaendelea kwa wiki nzima katika hospitali ya Wilaya ya Mafia.

Akizungunza leo katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  Bernard Konga amesema mpango huu ni mwendelezo wa mkakati wa Mfuko huu kufikia wananchi  na huduma za madaktari bingwa katika maeneo ambayo yana uhaba wa madaktari hao.

Amesema Mfuko kwa nyakati tofauti umeshafikia mikoa 17 na huduma hizo za mkoba za madaktari bingwa ambayo ni Rukwa, Lindi, Kigoma, Pwani, Mara, Tabora, Manyara, Mtwara, Shinyanga, Simiyu, Kagera, Singida, Ruvuma, Iringa, Njombe, Geita na Katavi. Kati ya hiyo mikoa 6 imeshafikiwa na mara mbili.

"Tumeona hitaji la huduma hizi huku Mafia na kwa kushirikiana na Hospitali ya Wilaya hapa Mafia zoezi hili litaendelea kwa wiki nzima kwa kila mwananchi mwenye hitaji la huduma za madaktari hawa ambao wametoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili" alisema Konga

Akifungua huduma hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mafia  Shaibu Nunduma ameipongeza NHIF kwa kuleta huduma hii Mafia.

"Asilimia kubwa ya wagonjwa wetu hawana uwezo wa kuzifuata huduma za madaktari bingwa huko walipo na kwa idadi ya wataalam waliopo hapa Mafia tusingeweza kuhudumia wananchi wa mafia ambao wako 53,083 hivyo naishukuru sana NHIF kwa kutuletea huduma hizi," amesema Shaibu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Anne Makinda amesema
Serikali yetu imeweka mkazo mkubwa katika afya na bajeti ya dawa kwa sasa imeongezeka hadi kufikia takriban bilion 300. Amesema lengo la Serikali yetu ni kila mtu kuwa na bima ya afya na katika kutimiza azma hii, Mfuko huu unalengo la kufikia asilimia 50 ya wananchi mwakani 2020.

"Lengo letu ni kuwa na watu wenye bima ya afya wakiwa wazima maana itakuja siku ambayo ugonjwa unakujia ghafla na huna fedha. Mfuko huu unamwezesha hata mtoto wako kuwa na uhakika wa matibabu kwa mwaka kwa Sh. 50,400 wakati kwa wakulima Sh. 76,800 kwa  kwa mwaka" amesema Makinda

Wakati huo huo wananchi wa Mafia ambao walifika kwa wingi kupata huduma za Madaktari Bingwa hao kutoka Hospitali ya Muhimbili wameushukuru  Mfuko kwa huduma hizo na wameonesha kuhamasika kuitumia fursa hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga akitoa maelezo ya awali wakati wa uzinduzi wa mpango huo katika Hospitali ya Wilaya vs Mafia
 Wananchi Wilayani Mafia wakifuatilia uzinduzi wa huduma za Madaktari Bingwa ambazo zimewezeshwa na Mfuko wa  Taifa wa Bima ya Afya..
Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Mama Anne Makinda akitoa salaam za Bodi wakati wa uzinduzi wa huduma hizo.


 Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Shaibu Nundulu akifungua rasmi huduma za Madaktari Bingwa Mafia  kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa

Easter Holiday Packages from Tanga Beach Resort

Jumia Mobile Week: Gulio la mauzo ya simu mtandaoni kwa punguzo la bei mpaka 60%!!!

$
0
0


Simu ya Tshs. 820,000 kuuzwa kwa Tshs. 8,000 tu!!!!!

Wateja kupelekewa bidhaa bure wakifanya manunuzi yatayaozidi Tshs. 50,000!!!
Dar es Salaam: April 9, 2019. Ulikuwa unajiuliza ni wapi na lini unaweza kununua simu mpya, za kisasa na kwa bei nafuu ambayo haukuitegemea?




Katika jitihada za kuhakikisha kuwa inarahisisha upatikanaji na matumizi ya simu za kisasa kwenye maisha ya kila siku ya Watanzania, Jumia imezindua gulio kubwa la mauzo ya simu za mkononi mtandaoni likijulikana kama ‘Mobile Week.’ Hili ni tukio kubwa la mauzo ya bidhaa zinazohusiana na simu ambapo limeanza leo Aprili 8 na kufikia kikomo mnamo Aprili 14. Lengo kuu la kampeni hii ni kuwapatia wateja muda wa kutosha na fursa ya kununua aina tofauti za simu za kisasa wazipendazo kwa bei nafuu, punguzo kubwa la bei, kujipatia vocha za kurahisisha manunuzi pamoja na zawadi kemekem ndani ya kipindi chote cha kampeni.


Akizungumzia sababu zilizopelekea kuwa na kampeni kubwa ya ‘Mobile Week’ kila mwaka, Meneja Masoko wa Jumia Tanzania, Bw. Albany James ameelezea kuwa, “Simu ni miongoni mwa bidhaa ambazo zinanunuliwa zaidi kwenye mtandao wetu wa Jumia. Lakini pia hata kwa takwimu zinazotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonyesha kwamba watumiaji wa simu za mkononi wanaendelea kuongezeka kila mwaka. 
Mwaka 2018 idadi ya watumiaji wa simu walikuwa takribani milioni 43.6 ukilinganisha na milioni 40 mwaka 2017. Hivyo basi sisi kama wadau katika urahisishaji wa mauzo ya bidhaa mbalimbali tumeona ni vema kuwa na kampeni kubwa ya mauzo ya ‘simu pekee’ kila mwaka ambayo itawawezesha Watanzania kufanya manunuzi kwa urahisi na bei nafuu ukilinganisha na sehemu yoyote ile.”


“Mobile Week’ kwetu sisi ni kampeni muhimu zaidi kutokana na manufaa makubwa iliyonayo si tu kwa wateja wetu bali na Watanzania kwa ujumla. Na ndiyo sababu iliyopelekea kila mwaka kujitahidi kuwa wabunifu na kuiboresha kwa kuja na simu za aina tofuati zaidi kutoka kwa washirika wetu, ofa kabambe, punguzo kubwa la bei, vocha za kurahisisha manunuzi pamoja na zawadi kemkem kupitia ‘Treasure Hunt’ siku ya Jumatano ya Aprili 10 kuanzia saa nane mchana. Ambapo simu aina ya Infinix inayouzwa Tshs. 820,000 itauzwa Tshs. 8,000 tu kwa mteja atakayebahatika kuisaka na kuipata kwenye mtandao wetu. Pia kutakuwa na vocha za manunuzi za kila siku ambapo mteja atakuwa anarahisishiwa manunuzi yake pindi atakapozitumia,” aliongezea Bw. James

“Ningependa kutoa wito kwa Watanzania wote kuitumia fursa hii ya ‘Mobile Week’ kununua simu ambazo walikuwa wanatamani kuwa nazo kwani aina ni nyingi na punguzo la bei ni kubwa tofauti na siku za kawaida. Kampeni ya mwaka huu imekuja kitofauti kwasababu kwa manunuzi yoyote ambayo yatazidi Tshs. 50,000 yatakayofanyika kwenye mtandao wa Jumia, mteja atapelekewa bure kabisa bila ya gharama yoyote ya usafirishaji mpaka pale alipo!” Ikipita fursa hii ni mpaka mwakani tena ambapo sidhani kama kuna mtu anaweza kuvumilia kuishi kpindi chote hiko bila ya simu au kuwa tayari kuingia gharama kubwa kufanya manunuzi mara baada ya kampeni hii kupita,” alihitimisha Meneja Masoko wa Jumia Tanzania.


Miongoni mwa sababu zinazopelekea kuendelea kuenea kwa upatikanaji na matumizi ya simu za mkononi na: kuendelea kuongezeka kwa makampuni ya mawasiliano ya simu, kuongezeka kwa makampuni yanayouza simu hivyo kupelekea upatikanaji kuwa rahisi na kwa bei nafuu, pamoja na uwepo wadau wanaorahisisha upatikanaji wa haraka wa bidhaa kama vile Jumia, soko kubwa la uuzaji na manunuzi ya bidhaa mtandaoni.

Tembelea tovuti ya Jumia sasa, https://www.jumia.co.tz/, kujionea bidhaa tofuati zinazopatikana katika kipindi hiki cha kampeni ya ‘Mobile Week’ kabla haijafikia ukomo. Jumia imejizatiti kuhakikisha manunuzi ya uhakika na usalama, urahisi kwa kukutanisha wanunuzi na wauzaji tofauti kutoka sehemu tofauti kwa wakati mmoja, bidhaa ni halisi na za kisasa, bei ni nafuu ukilinganisha na sehemu zingine, na kikubwa zaidi ni kwamba malipo ya bidhaa ni mpaka pale mteja atakapofikiwa na kujiridhisha nazo, na amepewa uwezo wa kuzirudisha na kuomba kubadilishiwa bila ya gharama yoyote ile!



Balozi Seif atembelea shule ya Sekondari Kinyasini

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amekabidhi msaada wa Laptop Mbili kwa ajili ya matumizi ya kimasomo Kwa Walimu na Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kinyasini iliyopo Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Huo ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati alipofanya ziara kipindi cha nyuma ya kukagua na kuangalia maendeleo na changamoto zinazoikabili skuli hiyo na kuzungumza na Uongozi wa Kamati ya Skuli, walimu, Wazazi na Wanafunzi wa Skuli hiyo.

Akipokea Msaada huo uliowasilishwa na Msaidizi wa Makamu wa Pili wa Rais anayesimamia masuala ya Ustawi Bibi Siti Abass, Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari Kinyasini Mwalimu Kombo Ali Machano alisema msaada huo umeleta ukombozi kubwa kwao na watalazimika kuutunza ili uweze kuendelea kutoa huduma kwa muda mrefu.

Hata hivyo Mwalimu kombo aliomba iwapo utakuwepo uwezekano wa kupatiwa Printa itakuwa ni jambo la faraja litakalowawezesha kuweputa matatizo yanayojitokeza wakati wanapoamua kwenda ku\ichapisha kumbukumbu zao kwenye Kompyuta za nje.

Akielezea furaha yake Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Skuli ya Kinyasini Bwana Is-haka Vuai Kidawa alisema Uongozi wa Skuli hiyo, Wazazi na Wanafunzi bado wanaamini kwamba Kiongozi huyo kamwe hatosita kuendelea kusaidia nguvu za kuimarisha Elimu Skulini hapo.

Bwana Is-haka alisema Wananchi wa Kijiji hicho na vitongoji vyake wanaelewa kwamba Kiongozi huyo wa Juu Serikalini akiwa ndie Mtendaji Mkuu wa Serikali amekuwa akikabiliwa na ahadi nyingi na ukweli usiopingika kwamba inakuwa vigumu kuzitekeleza kwa wakati jambo ambalo wao walilazimika kufanya subra kutokana na ahadi yao hiyo.

Wakati wa ziara yake Skulini hapo Miaka michache iliyopita Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Wazazi wana wajibu na ulazima wa kuhakikisha kwamba watoto wao wanawasimamia vyema katika kupata elimu bora itakayotoa mwanga wa kimaisha katika hatma yao ya baadaye.

Balozi Seif alisema elimu ndio ufunguo pekee pekee utakaowapa njia watoto hao kukabiliana na mazingira ya kimaisha yanayokwenda kwa kasi na haraka ndani ya mfumo wa sasa wa sayansi na Teknolojia.

Katika kuipa sifa Skuli hiyo kongwe ndani ya Mkoa wa Kaskazini Unguja Balozi Seif aliwahimiza Wafaunzi wa Skuli hiyo kuwa na dhamira ya kutafuta elimu kwa gharama yoyote ile.

Alisema wanafunzi lazima wawe na nia ya kutafuta elimu hasa ile ya sayansi ambayo bado ina mapungufu katika taasisi za kijamii kwani kuamua kusoma ni wajibu kwao ili kufanikiwa kimaisha.

Alifahamisha kwamba masomo ya sayansi yanayoonekana kupigwa chenga na wanafunzi walio wengi maskulini ndio yanayotoa fursa kubwa ya ajira katika ulimwengu huu wa sasa wa Sayansi na Teknolojia Ulimwenguni.

Skuli ya Kinyasini ikiwa ni miongoni mwa skuli kongwe ndani ya Mkoa wa Kaskazini Unguja iliasisiwa mnamo mwaka 1946 kwa Darasa la Quran na kuanza kwa darasa la kwanza mwaka 1947 lililoendelea hadi darasa la kumi na moja Mwaka 1973 na sasa limefikia darasa na Kumi na Mbili.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na Walimu pamoja na Uongozi wa Kamati ya Skuli ya Sekondari Kinyasini alipofanya ziara fupi skulini hapo Miaka michache iliyopita na kuahidi kusaidia Kompyuta.
 Balozi Seif akiangalia mabadiliko makubwa ya majengo ndani ya Skuli ya Sekondari ya Kinyasini ambapo ndipo alipoanzia kupata elimu ya msingi katika miaka ya 46.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizunguma na wazazi, kamati ya skuli, walimu na wanafunzi wa skuli ya Sekondari ya Kinyasini kipindi alipofika kuona maendeleo na changamoto zinazoikabili Skuli hiyo. Picha na – OMPR – ZNZ.

Serikali Yanunua Mtambo wa Madini

$
0
0
Na Immaculate Makilika- MAELEZO 

Serikali imenunua mtambo mkubwa wa madini ambao utasaidia kufanya utafiti wa madini, sambamba na kuwasaidia wachimbaji wadogo katika shughuli za madini nchini 

Akizungumza Bungeni leo jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alisema kuwa Serikali imefikia uamuzi huo kwa lengo kuunga mkono wachimbaji wadogo nchini kote wakiwemo wachimbaji wa kijiji cha Busiri wilaya ya Biharamulo. 

Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa ili kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini, Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imenunua mtambo mkubwa wa kumsaidia kufanya utafiti wa kina kwa kuchoronga miamba kwa bei nafuu ili kubaini mashapo zaidi na kuongeza uzalishaji. 

Naibu Waziri, Nyongo aliongeza kuwa Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara kwa wachimbaji wadogo ili wanufaike zaidi na kazi ya uchimbaji. 

Wizara kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini inakamilisha uandaaji wa kitabu cha madini yapatikanayo Tanzania toleo la nne ambacho kitaonesha uwepo wa madini katika mikoa, wilaya na vijiji, ambapo kitasaidia wachimbaji wadogo kutambua madini yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na matumizi ya madini hayo. 

Aidha, Wizara kupitia Mradi wa Usimamizi endelevu wa Raslimali Madini (SMMRP), inakamilisha kujenga vituo vya umahiri katika wilaya ya Bukoba, Bariadi, Songea, Handeni, Musoma, Mpanda na Chunya ili kuwezesha wachimbaji wadogo kujifunza kwa vitendo. 

MAKABIDHIANO YA TUZO BIKOSPORTS

$
0
0
 Msemaji wa Bikosports, Geoffrey Lea, kushoto akimpongeza Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems, kulia baada ya kumkabidhi zawadi yake ya kuwa Kocha Bora wa mwezi Machi, ambapo tuzo hizo ambazo wadhamini Wakuu ni Kampuni ya kubashiri michezo mbalimbali ya Biko Sports.
 Msemaji wa Bikosports Geoffrey Lea kushoto akimpongeza mshambuliaji mahiri wa Simba SC, John Bocco, baada ya kuibuka mchezaji bora wa mwezi Machi, ambapo tuzo hizo zinadhaminiwa na Kampuni ya kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali ya Bikosports.
 Kocha Mkuu wa Simba SC, Mbelgiji Patrick Aussems kulia akiwa na mshambuliaji wake John Bocco, ambaye yeye amepewa zawadi yake ya kuwa Kocha bora wa mwezi Machi, huku Bocco akitangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Machi.

WATANO KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUCHAPISHA PICHA ZA NGONO KUPITIA WHASAPP

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
WATU watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka ya kuchapisha picha za ngono kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao leo Aprili 9, na wakili wa serikali Jenipher Masue ambaye amesema washitakiwa ni Willium Kimaro (35), Oscar Mariselian maarufu Wizkid (30), mkazi wa Nkuungu Dodoma, Doa Godfrey (36), mfanyabiashara, Feisal Mohammed (27) mkazi wa Ilala, Adulrahman Muhidin (34) mkazi wa Temeke Dar es Salaam ambaye ni Ofisa Usafirishaji.

 Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Augustina Mmbando imedaiwa kila mshitakiwa anakabiliwa na shitaka moja kinyume na Sheria ya Makosa ya Mtandao kifungu namba 14 (1) (a) na kifungu cha (2) (a) namba 14 ya mwaka 2015 ambapo wanadaiwa kutenda makosa hayo Aprili 4 na 5, 2016 maeneo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Imedaiwa, Aprili 4, 2016 Mariselian alichapisha picha za ngono kupitia mtandao wa WhatsApp huku akijua kuwa ni kinyume na sheria huku  Kimaro, Godfrey, Mohammed na Muhidin walichapisha picha chafu  kupitia mtandao huo ambazo ni kinyume na sheria hiyopia.

Hata hivyo, wshitakiwa hao wamekana kutenda makosa hayo na wameachiwa huru kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa na mahakama ambayo yaliwataka kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja kutoka taasisi inayotambulika mwenye kitambulisho ambaye atasaini bondi ya Shilingi milioni tano. 

Aidha, mahakama imewataka wadhamini kuhakikisha wanatimiza wajibu wao wa kuhakikisha washitakiwa wanafika mahakamani hapo kila tarehe kesi hiyo itakapotajwa

Pia alisema kwa mshitakiwa ambaye ni mkazi wa Dodoma, kuhakikisha kuwa anafika mahakamani kwa sababu mahakama haikutaka kuzuia washitakiwa kutoka nje ya Dar es Salaam kwa sababu hiyo.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na Hakimu Mmbando ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 9, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

WAKULIMA KASULU WALIA BEI ZA PEMBEJEO

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kasulu

BAADHI ya wakulima wa Wilayani Kasulu wameiomba serikali kupunguza bei za pembejeo za kilimo hususani mbolea za kupandia na kukuzia ili waweze kulima kilimo chenye tija.

Wakulima hao wameiomba serikali kupunguza bei ya mbolea ya kupandia kutoka shilingi elf sabini bei ya sasa kwa mfuko wa kilo hamsini hadi elf arobaini pia kwa upande wa mbolea ya kukuzia ambayo kwa sasa bei yake ni shilingi elf arobaini kwa mfuko wa kilo hamsini wameomba ipungue hadi elf ishirini.

Hayo wameyasema jana kwenye mafunzo ya siku moja juu ya matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima wa Wilaya hiyo na mawakala wanaouza pembejeo ambapo mafunzo hayo yalitolewa kwa udhamini wa kampuni ya GSM sambamba na  uzinduzi wa mbolea yao ya GS Agro.

Said Shaaban ni mmoja wa wakulima waliohudhuria mafunzo hayo alisema kuwa kwasasa bei za pembejeo nyingi zipo juu ambapo wakulima wenye kipato cha chini wanashindwa kumudu gharama hizo za bei na kushindwa kulima kilimo cha kisasa chenye tija.

"Unajua sisi tumezowea kulima kwa mazowea tumekuwa tukitumia mbolea kwenye mazao ya chakula tunayolima ambayo ni mahindi na maharage ambapo hatuwezi kupata mavuno mengi sababu ya kutolima kisasa,Serikali naomba ituangalie sisi wakulima wa chini kwa kupunguza bei za pembejeo za kilimo"alisema

Naye Mwezeshaji wa wakulima Fatuma Bahi kutoka kijiji cha Msambala alisema kuwa changamoto wanayokutana ni upungufu wa maofisa ugani katika vijiji hali inayopelekea kata zaidi hata ya tatu kuhudumiwa na ofisa ugani mmoja.

"Tuletewe maofisa ugani vijijini ili waweze kutupa elimu ya kulima kilimo cha kisasa na chenye tija ili tuweze kufikia malengo yetu na ya Taifa,maana sasa wengi unakuta wanalima kilimo cha mazowea bila ya kuwa na elimu yoyote"alisema

Mhandisi kilimo na umwagiliaji wa Mkoa wa Kigoma Yohana Zephania wakulima wengi hawatumii pembejeo badala yake wanalima kilimo cha mazowea na kujikuta wakipata mavuno machache,lakini wakitumia pembejeo watapata uzalishaji mkubwa.

Mkuu wa kitengo cha mauzo kutoka kampuni ya tanzu ya GS Agro Remi Nindi alisema mbali na kampuni yao kuuza mbolea wamekuwa wakiwatembelea wakulima wao mara kwa mara na kujua changamoto zao.

"Huu ni msimu wa pili tunaenda mbolea yetu ya GS Agro imekuwa ikifanya vizuri kwa shuhuda mbalimbali za wakulima,msimu ujao tutabadilisho muonekano wa rangi ya mfuko tunaoweka mbolea pia tukuwa na mbolea kuanzia kilo tano ili wakulima wote waweze kumudu kuinunua na kulima kilimo chenye tija"alisema.

 Mkuu wa Kitengo cha mauzo kutoka kampuni tanzu.ya GS Agro Remi Nindi akiongea na wakulima na mawakala wa pembejeo Wilayani Kasulu baada ya uzinduzi wa mbolea yao ya GS Agro.

 Mbolea za kupandia na kukuzia GS Agro.kutoka kampuni ya GSM zikiwa kwenye mfuko wa kilo 50 zilizozinduliwa Wilayani Kasulu .

Washiriki wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo ya matumizi sahihi ya pembejeo 

KAMATI YA UCHAGUZI YANGA SC NA TFF ZAKUTANA KUAMUA WAGOMBEA WA NAFASI ZA UONGOZI KLABU YA YANGA

Serikali kuanzisha Makumbusho ya wanamichezo

$
0
0
Na Shamim Nyaki – WHUSM
Serikali imejipanga kuanzisha Makumbusho Maalum katika Uwanja wa Taifa ya kuhifadhi taarifa na picha za wanamichezo walioliletea Taifa heshima katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa.
Hayo yamesemwa leo Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza alipokuwa akijibu swali la msingi la Mhe.Ester Mahawe (Viti Maalum) kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyeuliza ni lini serikali itaandaa utaratibu wa kuwaenzi wanariadha nchini. 

Mhe.Shonza alieleza kuwa Serikali inawatambua na kuwaenzi wanamichezo wote ambao wameletea nchi sifa kubwa wakiwemo Mwanariadha Filbert Bayi aliyevunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 1500 mwaka 1974 ambaye ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, Jumaa Ikanga mshindi wa Medali ya Shaba Mashindano ya All- Africa Games mwaka 1978 na Medali ya Fedha Michezo ya Olimpiki 1980 kwa mbio za mita 5000 hivi sasa ni Kocha wa Riadha wa Taifa Brunei.

“Kanuni ya mafanikio katika michezo popote duniani yanatokana na mwanamichezo mwenyewe kuonyesha juhudi binafsi za kujituma na kujipambanua kuwa bora miongoni mwa wanamichezo wengine,hivyo wanamichezo lazima waendelee na jitihada za kujituma.”alisema Mhe.Shonza.
Aidha, Mhe.Shonza alipojibu swali la nyongeza la Mhe.Anna Gidarya Mbunge Viti Maalum (CHADEMA) Mkoa wa Manyara aliyeuliza ni lini Serikali itaboresha miundombinu ya viwanja katika vyuo vya elimu ya juu, ameeleza kuwa suala la kuboresha miundombinu linahitaji ushirikiano kati ya Serikali na wadau hivyo amewataka waheshimiwa wabunge kuona changamoto hiyo na kuifanyia kazi.
PIX 1.Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akijibu swali leo April 09, 2019 Bungeni Jijini Dodoma.

RAIS DKT. MAGUFULI AMEZINDUA KITUO CHA AFYA MADABA NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI WA MADABA MKOANI RUVUMA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi wa Kijiji cha Mageuzi Wilaya ya Namtumbo wakati akiwa njiani kuelekea Madaba mkoani Ruvuma.Ambapo Rais amechangia Shilingi Milioni nane kwa Shule ya Msingi na Sekondari Mageuzi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakazi wa kijiji cha Ndelenyuma ambapo awali kilikuwa ni kitongoji na sasa ametangaza rasmi kuwa kijiji alipokuwa akielekea Madaba mkoani Ruvuma kwenye uzinduzi wa kituo cha Afya Madaba. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu pamoja na Balozi wa Denmark nchini .Heinar Jensen pamoja na wadau wa Maendeleo wakifunua kitambaa kuashiria Uzinduzi rasmi wa Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma. 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Balozi wa Denmark nchini Heinar Jensen pamoja na wadau wa Maendeleo wakipiga makofi mara baada ya kufunua kitambaa kuashiria Uzinduzi rasmi wa Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu pamoja na Balozi wa Denmark nchini Heinar Jensen,Balozi wa Canada Nchini Pamela O’donnel, Balozi wa Uswisi Nchini Frolence Mattli pamoja na wadau wa Maendeleo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua wa Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu , Mama Janeth Magufuli pamoja na Balozi wa Denmark nchini Heinar Jensen,Balozi wa Canada Nchini Pamela O’donnel, Balozi wa Uswisi Nchini Frolence Mattli pamoja na wadau wa Maendeleo wakifurahi mara baada ya kuzindua wa Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu pamoja na Balozi wa Denmark nchini Heinar Jensen,Balozi wa Canada Nchini Pamela O’donnel, Balozi wa Uswisi Nchini Frolence Mattli pamoja na wadau wa Maendeleo kuashiria uzinduzi wa Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono pamoja na Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Balozi wa Denmark nchini Heinar Jensen,Balozi wa Canada Nchini Pamela O’donnel, Balozi wa Uswisi Nchini Frolence Mattli,Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja pamoja na wadau wa Maendeleo alipokuwa akikagua Wodi ya Wazazi ya  Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagua kitanda cha kujifungulia katika Wodi ya Wazazi katika Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma mara baada ya kuzindua kituo hicho.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagua Vitanda katika Wodi ya Wazazi katika Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma mara baada ya kuzindua kituo hicho.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagua Vifaa katika Wodi ya Wazazi katika Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma mara baada ya kuzindua kituo hicho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Balozi wa Denmark nchini Heinar Jensen,Balozi wa Canada Nchini Pamela O’donnel, Balozi wa Uswisi Nchini Frolence Mattli,Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja pamoja na wadau wa Maendeleo wakiimba wimbo wa taifa wakati wa sherehe za uzinduzi wa  Kituo cha Afya Madaba mkoani Ruvuma. 

 PICHA NA IKULU

MATUKIO MBALIMBALI YA OFISI YA WAZIRI MKUU BUNGENI LEO JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akiteta jambo na Mbunge wa Mikumi Joseph Haule mara baada ya kuhairishwa kwa mkutano wa Bunge unaoendelea Jijini Dodoma Aprili 9, 2019.
 Sehemu ya Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia michango wa Wabunge wakati wa kujadili Hoja ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (Mb) kuhusu mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/ 2020 Bungeni Dodoma Aprili 09, 2019.
 Sehemu ya Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia michango wa Wabunge wakati wa kujadili Hoja ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (Mb) kuhusu mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/ 2020 Bungeni Dodoma Aprili 09, 2019.
 Sehemu ya Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia michango wa Wabunge mapema hii leo Bungeni Dodoma, katikati ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Maimuna Tarishi, na mwenye tai nyekundu ni Katibu Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Andrew Massawe wakati wa Bunge Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Anthony Mavunde (wa kwanza kushoto) pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile (mwenye tai ya blue) wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Andrew Massawe (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) mwenye tai nyekundu na Maimuna Tarishi (Bunge na Waziri Mkuu) nje ya Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
 Makatibu Wakuu Ofisi ya Waziri Mkuu wakiteta jambo mara baada ya kuhairishwa kwa vikao vya bunge vinavyoendelea Jijini Dodoma Aprili 09, 2019, kulia ni Andrew Massawe anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na kushoto ni BMaimuna Tarishi (Bunge na Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama  (mwenye blauzi nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mawaziri na wabunge nje ya Ukumbi wa Bunge Dodoma, wa kwanza kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

UCHAGUZI WA KIHISTORIA KUSHUHUDIWA NCHINI INDIA, WATU MILIONI 900 KUPIGA KURA

$
0
0
* Watu milioni 900 wakiwemo vijana wajiandikisha kupiga kura, siku 38 zatengwa kwa kupiga kura

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

INDIA ina wapiga kura takribani Milioni 900(Ni Mara 18 zaidi ya Idadi ya watanzania wote) waliojiandikisha kwenye Time ya Uchaguzi.

Zoezi la kupiga kura litaanza tarehe 11 April hadi tarehe 19 Mei 2019, yaani takribani siku 38 kwa mizunguko 7 na kisha kura zitaanza kuhesabiwa tarehe 23 Mei 2019.

Waziri Mkuu wa sasa, Narendra Modi na chama chake cha BJP amerudi tena na kuomba kutetea tena kiti hicho.

Akizungumza na vyombo vya habari msemaji wa tume ya uchaguzi nchini humo, Sunil Arora, amesema kuwa uchaguzi utafanyika Aprili 11, mwaka huu na utawahusisha wapigakura milioni 900 na  kati yao wapiga kura milioni 15 ni vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 19.

Katika kipindi cha wiki chache zilizopita, tatizo la uhaba wa ajira na kushuka kwa bei ya bidhaa za kilimo, vilishusha umaarufu wa Waziri Mkuu Modi, lakini wapigakura wanasema Chama Tawala cha  Bharatiya Janata Party (BJP), kitawapiku wapinzani wake baada ya mwezi uliopita jeshi la polisi la nchi hiyo kuingia vitani na wapinzani wa Pakistan hali inayoelezwa imewapa umaarufu zaidi na kuweza kupelekea  kujizolea mamilioni ya kura kutoka maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE APRILI 9, 2019

TASWIRA KUTOKA KONGAMANO LA DIASPORA LA UWEKEZAJI CHINI YA TDC GLOBAL SWEDEN.

$
0
0
Wageni waalikwa wakiwa na mwenyeji wao Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dr. Wilbroad Slaa meza kuu kwenye kongamano la Diaspora linalofanyika ndani ya meli ya abiria, kongamano hilo la siku tatu linalorushwa moja kwa moja na TBC1 ni kongamano la siku 3 ambalo linatarajiwa kumalizika April 11, 2019. Wageni waliotoka Tanzania ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai. katibu katika ofisi ya Rais Zanzibar, Mhe.Salum Maulid Salum, Mkurugenzi kitengo cha Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki Balozi Amisa Mbaga. Wageni wengine waalikwa walikuwepo kwenye mkutano huo ni Ms Asa Jarskog (President-Sweden Subsaharan Africa Chember of Commerce, Mr. Rukwaro Senkoro (Azania Bank), Mr. Octavian Mshiu ( Ag. President-Tanzania Chember of Commerce, Industry and Trade), Mrs Genevieve Kasanga (Head of Communications, Equinor, Tanzania AS), Ms Lucy K. Naivasha (Manager Diaspora Banking- CRDB) na Christine Chambay ( Chairpesrson Tanzania Diaspora Chember of Commerce and Industry) Picha na NY Ebra Vijimambo Blog

Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dr. Wilbroad Slaa akijiandaa kukabidhi zawadi ya kitabu kinachoitwa Dreamers & Doers kwa wageni katika meza kuu kwenye kongamano la uwekezaji chini ya TDC Global kati ni Mwenyekiti wa TDC Global Bwn. Norman Jason na mwingine katika picha ni mmoja ya viongozi TDC Global Bwn. Jeff Msangi ni ndiye mshereheshaji kwenye kongamano hilo.
Wadau mbalimbali Diaspora kutoka kila pembe ya Dunia wakifuatilia kongamano.
Mmoja ya wawekezaji Slim akiongea jambo kwenye kongamano hilo.
Wadau waliojitokeza kwenye kongamano hilola uwekezaji nchini Sweden.

Wadau mbalimbali Diaspora wakifuatilia kongamano.
Kongamano likiendelea.

Kongamano la siku tatu likiendelea ndani ya meli ya abiria.
PICHA CHINI NI WAKATI WA KUTOA ZAWADI YA KITABU CHA DREAMERS & DOERS KWA WAGENI.


Mwenyekiti wa TDC Global akiwatambulisha familia yake (mke na watoto)
Familia ya mwenyekiti wa TDC Global ikipata picha ya kumbukumbu na wageni
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images