Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110172 articles
Browse latest View live

CRDB Iringa yawataka wajasiliamali na wafanyabiashara kutafuta fursa za uwekezaji kutekeleza sera ya Taifa ya Tanzania ya Viwanda

$
0
0

Mkurugenzi wa bank ya CRDB tawi la Iringa Kissa Samweli akizungumza na wateja wa CRDB jana wakati wa warsha ya siku moja ya wanahisa juu ya kuchangamkia kutafuta fursa za kufanya kuunga mkono jitihada za serikali juu ya sera ya Tanzania ya viwanda
Mkurugenzi wa bank ya CRDB tawi la Iringa Kissa Samweli (kushoto) akimsikiliza mteja wa CRDB mfanyabiashara George Kaundama ambae ni mmoja kati ya wateja wakongwe ambao wanamiliki hisa katika bank hiyo jana wakati wa warsha ya siku moja ya wanahisa juu ya kuchangamkia kutafuta fursa za kufanya kuunga mkono jitihada za serikali juu ya sera ya Tanzania ya viwanda


washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia mada mbali mbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa mafunzo hayo

…………………………

NA Francis Godwin, Iringa

Benk ya CRDB imetoa rai makundi mbali mbali kama ya wajasiriamali na wafanyabiashara wakubwa kuchangamkia fursa ya mikopo ili kujikita kutafuta fursa ya kuendeleza ama kuboresha viwanda vidogo vidogo na viwanda vikubwa kama utekelezaji wa sera ya taifa ya Tanzania ya viwanda .

Akitoa rai hiyo wakati wa semina ya siku moja kwa umma iliyotolewa kwa wanahisa wa CRDB tawi la Irina jana mkurugenzi wa CRDB tawi la Irina Kissa Samwel alisema kuwa bank hiyo imekuwa mbele kutekeleza sera ya Taifa ya Tanzania ya viwanda kwa kutoa mikopo kwa makundi mbali mbali kwa ajili ya kuyawezesha kuboresha shughuli zao.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa aina ya mikopo ambayo wamekuwa wakiitoa ni ile ya chini kabisa ya vikundi kuanzia kiasi cha shilingi 300,000 na kuendelea pia mikopo ya wafanyabiashara wa kati na wakubwa pamoja na mikopo binafsi .

Alisema mikopo ya uendeshaji wa biashara ni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya uendeshaji biashara ya kila siku kama kununua malighafi katika uzalishaji viwandani ,kununua vipuli vinavyohitajika katika matengenezo ya mara kwa mara ya mitambo ikiwa ni pamoja na kununua vitu vinavyohitajika katika usindikaji kiwandani .

Aidha mikopo hiyo hutolewa kwa ajili ya mahitaji ya gharama za uendeshaji ya kila siku kama kulipa mishahara ,gharama za maji ,umeme ,usambazaji wa bidhaa na gharama za riba ya mikopo ,mahesabu na ukaguzi na kodi na kuwa mkopo huo hutegemea mahitaji ya biashara kwa kuzingatia mtiririko wa mahesabu .

Alisema kuwa aina ya wateja ni watu binafsi ,biashara za ubia,makampuni ,biashara muunganiko ,mashirika ya umma ,vikundi na vyama vya ushirika

Makundi mengine ni azaki ,taasisi zisizo za serikali ,serikali kuu ,wakala wa serikali na wizara kuwa lazima wakopaji wawe wanaishi aum wamesajiliwa nchini Tanzania na si vinginevyo.

Aidha alisema wakopaji wasiokubalika ni watoto chini ya miaka 18 ,wale waliotangazwa kufilisika ,wasio na akili timamu ,kampuni zilizofilisika au ziko katika mchakato wa kutangazwa kufilisika hao pia hawatahusika na mikopo hiyo .

Kwani alisema lengo la CRDB kuona wenye sifa ya kunufaika na mikopo hiyo wananufaika na kuendelea kutekeleza sera ya Tanzania ya viwanda kwa kuwapa mikopo wote wenye sifa stahiki katika kutekeleza sera hiyo na wao kujikwamua kiuchumi.

“Mitaji iko mingi sana CRDB sera nzuri ya serikali ipo hamna sababu ya kusumbuka pia wateja wakubwa tunawakaribisha kuna mikopo mikubwa kwao kwani hakuna sababu ya kundi lolote kulalamikia mitaji kwetu mitaji iko wazi hivyo tunawakaribisha wote ili kuunga mkono juhudi za serikali na sisi wenyewe kuwa na maisha bora “ alisema mkurugenzi huyo

Mwanahisa Georege Kaundama ambae ni mmoja kati ya wafanyabiashara mkoani Iringa alipongeza CRDB kwa kuandaa semina hiyo kwa wanahisa wake na kuwa elimu iliyotolewa imewahamasisha wengi kuona sababu ya kuboresha biashara zao zaidi kwa kupitia bank hiyo .

Alisema kuwa kwa upande wake hajutii kuwa mmoja kati ya wanahisa kwani bank hiyo hataka kama uchumi umeyumba kiasi gani wamekuwa wakitoa gawio kwa wanahisa wake na hivyo silaha pekee ni kuendelea kuwepo badala ya kukimbilia bank mpya zinazoanzishwa kwani tofauti ya CRDB na hizo mpya ni ukongwe wake na mwanga ambao wanauona mbele si mwanga hafifu ni mwanga unaong’aa.

“ Imekuwa ni tabia ya kila mwanadamu anapoona kitu kipya kimekuja ama kuna usemi usemao kipya kinyemi ni lazima aende akaguse kuona ila tofauti ya CRDB toka tulipo gusa wakati huo hadi leo wao wapo imara hawayumbi wanazidi kusonga mbele “ alisema Kaundama.

Meneja Msimamizi usalama wa bank hiyo Theophel Akoro alisema kuwa sera ya viwanda iko bayana na kuwa watanzania waliowengi bado hawajajua kuwa ushiriki wao katika shughuli mbali mbali za uzalishaji iko kwenye sera ya Taifa ya kuendelea Tanzania ya viwanda .

Hata hivyo alisema kwa kuwa wengi wameshindwa kutambua vipaumbele katika sekta hiyo ambavyo wangeweza kuchukua hatua ya kuvifanyia kazi vipaumbwele hivyo ili kunufaika na sera ya Taifa ya viwanda .

Aidha alipongeza serikali ya mkoa wa Iringa kwa kutambua fursa ya uwekezaji katika uboreshaji wa miundo mbinu ya uwanja wa ndege wa Nduli pamoja na utalii kwani maeneo hayo ni sehemu kubwa zaidi yaukuzaji wa sekta ya viwanda nchini na kuwataka wananchi kila mmoja kwa uwezo wake kutafuta fursa anayoweza kunufaika nayo kuelekea Tanzania ya viwanda kama ni mkulima kusindika na kulima kisasa kama maana kilimo biashara ili kuwa mmoja wao katika endelezaji viwanda nchini. 

DC GONDWE ATAKA MBIO ZA TANGA CITY KUTANGAZA UTALII WA MKOA

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Godwin Gondwe akivalishwa medali mara baada ya kumaliza mbio KM 21 za Tanga City Marathon zilizomalizikia Uwanja wa Mkwakwani. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Godwin Gondwe akifurahia baada ya kuvalishwa medali mara alipomaliza mbio za Tanga City Marathon 2019 iliyofanyika na kumalizikia Uwanja wa Mkwakwani. Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Godwin Gondwe akimaliza Mbio za KM 21 katika Uwanja wa Mkwakwani-Tanga. 
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Godwin Gondwe akihojiwa na mwanahabari mara baada ya kumaliza mbio KM 21 za Tanga City Marathon zilizomalizikia Uwanja wa Mkwakwani. 
Wakimbiaji wakionyesha umahili wao.


Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Tanga. 

KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Tanga Godwin Gondwe amesema mkoa huo utaendelea kutumia mashindano ya riadha ya Tanga City Marathon kuweza kutangaza fursa za uwekezaji na utalii zilizopo mkoani Tanga. 

Gondwe ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Handeni ameyasema hayo leo wakati akifunga mashindano ya Tanga City Marathon yaliyofanyika jijini Tanga ambapo msimu huu yameshirikisha washiriki 1,300 kutoka mikoa mbalimbali na nje ya nchi. 

Amesema watafanya hivyo kutokana na kwamba mkoa huo kuwa na maeneo makubwa ya uwekezaji yaliyopo mkoani Tanga ili kuweza kuwa vutia kuwekeza kutokana na fursa kubwa zilizopo. “Ndugu zangu tutaendelea kuitumia Tanga City marathon kuweza kutangaza mkoa wa Tanga... Lakini pia kutangaza utalii hata uwekezaji mkoa wa Tanga kwani tuna fursa nyingi sana ambazo mnaweza kuzichangamkia kwenye kufanya uwekezaji “ Amesema. 

Hata hivyo aliwapongeza washiriki ambao wamefanya vizuri kwenye mashindano hayo na kuwataka kuendelea kujiweka imara kwa kushiriki kwenye mazoezi mara kwa mara ili kuweza kujiandaa na yale yajayo. “Mashindano hayo ya Tanga City Marathon yameufanya mkoa wetu uweze kuendelea kutangazika lakini niwaambie waandaaji wafungue mapema dirisha la usajili msimu ujao “Alisema.

Amesema kwani iwapo watafungua mapema dirisha la usajili wanaweza kupata wadhamini ambao wataweza kuongeza chachu kwenye mashindano hayo msimu ujao. “Pia niwaambie kwamba Mkuu wetu wa Mkoa Martine Shigella anatambua anatambua sana mchango wenu mlijitokeza kushiriki mashindano hayo na sio kwenye michezo pekee anathamini Tanga City Marathon lakini kubwa amenielezea amefurahi kusikia vijana wa shule zetu wameshiriki nao Tanga City Marathon”Amesema.

 Hata hivyo pia aliwaagiza wakuu wa shule za Sekondari, Msingi na Vyuo vikuu kuhakikisha wanajiandaa kikamilifu ili kuweza kujipanga kwa ajili ya mashindano yajayo ili nao waweze kupeleka washiriki ambao watashindano kwenye mbio za kilomita tano.

WAZIRI UMMY AAHIDI NEEMA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA

$
0
0


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipokea hotuba kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Ernest Benzi wakati walipofanya ziara ya kukagua jengo la mama na mtoto (Maternity Block). Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula na nyuma viongozi wengine wa Wizara na Hospitali.
Jengo jipya la Mama na Mtoto (Maternity Block) lililopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (kushoto)akiongea jambo wakati alipofanya ziara ya kukagua jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General). Kulia ni katibu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na mama aliyejifungua katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakati alipofanya ziara ya kutembelea jengo jipya la Mama na Mtoto katika Hospitali hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula wakiangalia kitu katika wodi ya akinamama waliojifungua wakati walipofanya ziara ya ukaguzi wa jengo jipya la mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.


……………………..
Na WAMJW-Dodoma

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameahidi kutoa Tsh. Milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Waziri Ummy ametoa ahadi hiyo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea jengo jipya la mama na mtoto (Maternity Block) katika Hospitali hiyo ili kujionea hali ya utoaji huduma kwa akina mama wajawazito na watoto.

“Ninaahidi kutoa Milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la OPD ya kisasa yenye uwezo wa kupokea wagonjwa wengi zaidi tofauti na OPD iliyopo sasa”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kurekebisha na kufanya maboresho katika baadhi ya maeneo yaliyoonekana kuwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuyapa majina majengo yote ya Hospitali hiyo ili kuepusha usumbufu kwa wagonjwa pindi wanapotaka kupata huduma katika majengo tofauti.

Aidha, Waziri Ummy ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kujenga ghorofa ambayo itakua maalum kwa ajili ya matibabu ya watoto pekee yenye uwezo wa kulaza watoto wengi sambamba na chumba cha uangalizi maalum kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda (Intensive Neonatal Care Unit) na wale wanaohitaji uangalizi maalum (ICU).

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula amesema Wizara itaendelea kushirikiana na uongozi wa Hospitali hiyo katika kutatua changamoto mbalimbali zilizoonekana katika Hospitali hiyo ikiwa ni pamoja kuongeza watumishi wa kada mbalimbali ili kukidhi mahitaji.
a
“Naomba niwaahidi tutaongeza watumishi wa kada mbalimbali ili kuziba mapungufu yanayoonekana, lengo likiwa ni kuboresha huduma katika Hospitali hii inayotegemewa na watu wengi wa Dodoma na kutoka maeneo ya jirani”. Amesema Dkt. Chaula.

Hata hivyo Dkt. Chaula amewataka watumishi wa Hospitali hiyo kushirikiana ili waweze kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa wanaokwenda hospitalini hapo.

Katika ziara hiyo iliyoenda sambamba na siku ya Afya Duniani imejumuisha viongozi mbalimbali wa Wizara akiwemo Mkurugenzi wa Sera na Mipango Edward Mbaga wameondoka na azimio la kufanya maboresho katika Hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na kujengwa kwa jengo maalum la kupokea wageni mbalimbali wanaokuja Dodoma.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AONGOZA WANANCHI HITMA YA MZEE KARUME KISIWANDUI ZANZIBAR LEO

$
0
0


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka Shada la Maua katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, baada ya kumalizika kwa kisomo cha Hitma iliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar
MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua katika kaburi la Mareheme Mzee Abeid Amani Karume, baada ya kumalizika dua ya kumuombea iliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar leo
MWAKILISHI wa Familia ya Marehemun Mzee Abeid Amani Karume, Balozi Ali Karume baada ya kumalizika hafla ya kisomo cha Hitma na Dua kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, iliofanyika Afisi Kuu ya CCM Zanzibaer leo.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed, kuhudhuria hafla ya Hitma ya Dua ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kuhudhuria Hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Viongozi na Wananchi katika Hitma na Dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, kushoto Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi,Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,. Balozi Seif Ali Iddi na Rasi Mstaaf wa Tanzania Mzee Aliu Hassan Mwinyi na kulia Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali,Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ameni Karume na Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Dr. Abdallah Juma Sadala
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuika na Wananchi wa Zanzibar katika Hitma na Dua ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliofanyika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, kushoto Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Mgeni Hassan Juma na kulia Mama Shadya Karume na Mama Fatma Karume, wakiitiikia dua wakati wa hafla hiyo ya Hitma ya Mzee Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, iliofanyika leo Afisi Kuu ya CCM Zanzibar
WANANCHI kutoka sehemu mbalimbali ya Mji wa Zanzibar wakihudhuria Hitma na Dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, iliofanyika leo katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar
WANAINCHI wakishiriki katika Kisoma cha Hitma ba Dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliofanyika leo Afisi Kuu ya CCM Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia dua ya kuhitimisha Hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume ,ikisomwa na Sheikh Jaffar Abdallah Abdald, katika hafla hiyo iliofanyika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.kushoto Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Salif Omar Kabi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seiff Ali Iddi na Rais Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi na kulia Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali nac Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe. Dkt Amani Abeid Karume

RAIS Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Mkuu Brigedi ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo, alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kuhudhguria Hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume 
RAIS Mstaaf wa Zanzibar Mhe.Dkt. Amani Abeid Karume akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja akihudhuria hafla ya Hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, iliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar Leo 
KATIBU Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ali akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe Mohammed Aboud Mohammed alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kuhudhuria hafla ya Hitma ya  Marehemu Mzee Abeid Amani Karume 

WAZIRI LUGOLA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA UPELELEZI WILAYA YA MBOGWE KWA TUHUMA ZA KUPOKEA RUSHWA

$
0
0


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola aakizungumza na wananchi wa Kata ya Ilolangulu Wilayani Mbogwe, Mkoani Geita (hawapo pichani) baada ya kusikiliza malalamiko yao kuhusu polisi kuchukua rushwa. Lugola alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kumsimamisha kazi Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilayani humo (OC CID), pamoja na Mkaguzi wa Jeshi hilo kwa kosa la kutuhumiwa na wananchi hao.
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Ilolangulu Wilayani Mbogwe wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (hayupo pichani) alipokuwa anazungumza nao baada ya kusikiliza malalamiko yao kuhusu polisi kuchukua rushwa. Lugola alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kumsimamisha kazi Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilayani humo (OC CID), pamoja na Mkaguzi wa Jeshi hilo kwa kosa la kutuhumiwa na wananchi hao.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Mbogwe, Mkoani Geita, baada ya kuzungumza na wananchi wa Kata ya Ilolangulu wilayani humo, akiskiliza malalamiko yao kuhusu polisi kuchukua rushwa. Lugola alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kumsimamisha kazi Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilayani humo (OC CID), pamoja na Mkaguzi wa Jeshi hilo kwa kosa la kutuhumiwa na wananchi hao.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani na Nchi


Na Mwandishi Wetu, Geita.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu kumsimamisha kazi Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Mbogwe (OC CID) Mkoani Geita, pamoja na Mkaguzi wa Jeshi hilo kwa kosa la kutuhumiwa kuomba na kupokea rushwa.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata za Ilolangulu na Busabaga wilayani humo, Lugola alisema Polisi hao ambao waliomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni nne kutoka kwa wananchi wa Kata hizo

ambao walikuwa wanataka kuwaombea dhamana ndugu zao, ndipo polisi hao wakaomba fedha kiasi hicho ili watolewe mahabusu ya Polisi katika Kituo cha Polisi Mbogwe.Maafisa hao wa Polisi ambao wanadaiwa kupokea rushwa kutoka kwa wananchi hao ni OC CID wa Wilaya hiyo, Luitiko Kibanda na Mkaguzi wa Polisi aitwaye kwa jina la Kessy ambao wananchi hao pamoja na Mbunge wao
walisema waliwakabidhi fedha kiasi hicho.

”Wananchi walipitisha mchango kila kaya ili kuwanusuru wenzao na viongozi wao haikutosha wakamuomba Mbunge wao akawachangia shilingi laki tano pia wakachukua na hela yao iliyokuwa ni ya kujengea zahanati wakawapelekea polisi, bila hata aibu polisi hawa wakachukua fedha hizo, bila kujali hali za kiuchumi walizonazo wananchi hao”alisema Lugola.

Lugola alisema licha ya Kata hizo kukithiri vitendo vya wizi na ubakaji na Polisi kufanya wajibu wao kuwakamata watuhumiwa mbalimbali, lakini ni kosa kuwaonea wananchi kwa kuwaomba rushwa kupitia kisingizio cha utoaji wa dhamana huku sheria ikieleza kwa makosa yanayodhaminika dhamana itolewe kwa mujibu wa sheria na siyo kuwanyanyasa wananchi.

Aidha, Waziri Lugola alitoa onyo kwa Polisi nchini ambao wanawafanya wananchi mtaji kwa kuwabambikiza kesi kisha kuwaomba pesa, kuacha tabia hiyo mara moja na endapo wakibainika hatawavumilia, hatawaonea huruma
hivyo sheria itafuata mkondo wake.

Kwa Upande wake Diwani wa Kata ya Ikobe, Wilayani humo, Costantine Kwezi, alimuomba Waziri kuwasaidia kukamilisha kituo cha polisi katika Kata yake na pia kuongeza idadi ya askari kituoni hapo, kwasababu kituo hicho kina askari mmoja ambaye anazidiwa na majukumu.

Baadhi ya kina mama katika mkutano huo, nao walimuomba Waziri huyo kuwasaidia waume zao waliokamatwa kwa kosa la kusingiziwa kuwa ni majambazi kuachiwa huru, kutokana na kukosa hela ya kuhudumia familia na wao wameachwa bila kazi na watoto wadogo.

WANYARANDWA WAANDAMANA KUADHIMISHA MAUAJI YA KIMBARI ARUSHA

$
0
0

Na Ahmed Mahmoud,Arusha.

Mamia ya Wanyarandwa wamekusanyika na kuandamana katika viunga vya jiji la Arusha ikiwa ni ishara ya kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 tangu kutokea kwa mapigano na mauaji ya Kikabila Nchini na kusababisha mauaji ya maelfu ya Wanyarandwa.

Maadhimisho hayo yaliyofanyika jijini Arusha yanalenga kuhamasisha umoja na amani miongoni mwa wanyarandwa kuungana kama taifa bila kujali tofauti za kikabila .

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanyarandwa wanaoishi katika Mataifa mbalimbali duniani Murenzi Daniel amesema kuwa maadhimisho hayo yanalenga kuwakumbusha kudumisha amani na umoja kama nguzo muhimu ambayo kwasasa hawako tayari kuipoteza na wanawataka Wanyarandwa duniani kote kuungana

Tedy Shungushu ni Mnyarandwa anayeishi jijini Arusha amesema kuwa kumbukumbu hiyo ni ya muhimu kama taifa kujitafakari na kuona namna ambavyo wanawakumbuka watu waliowapoteza katika mauaji hayo na kuwaenzi kila mwaka.

Kwa upande wao Watanzania walioshiriki katika maadhimisho hayo Maurin Njobi na Omega Urio wamesema kuwa yanawakumbusha kama Watanzania kudumisha amani na upendo na mshikamano kama taifa ili kuondoa uwezekano wa matukio kama hayo kutokea nchini

Zaidi ya watu Laki nane wanatajwa kupoteza maisha kwenye mauaji hayo ya Rwanda nchi ambayo kwa sasa inaongozwa na Rais wake Paul Kagame.

 


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS DKT MAGUFULI KATIKA KUMBU KUMBU YA MIAKA 25 YA MAUAJI YA KIMBARI NCHINI RWANDA

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mwenye Tai nyekundu akiwa na viongozi wa Mataifa mbalimbali Aprili 7/2019 wakitoa heshima katika eneo la kumbukumbu ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akibadilishana Mawazo na Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo walipo kutana leo Aprili 7/2019 katika Mji wa Kigali wakati waziri Mkuu alipokuwa anamuwakilisha Rais Dkt Magufuli katika kumbukumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994 nchni Rwanda.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin Mkapa walipo kutana leo Aprili 7/2019 katika Mji wa Kigali wakati waziri Mkuu alipokuwa anamuwakilisha Rais Dkt John Magufuli katika kumbukumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994 nchini Rwanda.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na mwenyeji wake Waziri wa mambo ya Nje wa Rwanda Balozi Richard Sezibera aliyempokea  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kigali alipo wasili leo Aprili 7/2019 alipo fika kumuwakilisha  Rais Dr John Magufuli katika kumbumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994 Kkulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Rwanda Balozi Ernest Mangu.


PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU. 

MIAKA 47 YA KIFO CHA HAYATI ABEID AMAN KARUME: HATUSAHAU HATUSAMEHE

$
0
0
Na Dkt. Muhammed Seif Khatib
Saa kumi na mbili magharibi. Tarehe kama ya leo. Unyama ulifanyika. Unyama ulifanyika wa kuutorosha uhai. Kutorosha uhai mbichi wa mkombozi wa Waafrika wa Zanzibar, Abeid Amani Karume.Yalikuwa mauaji ya kikatili ya kummiminia darzeni nzima ya risasi ya mtu aliyekuwa hana silaha ya kujilinda.Mwuwaji ni mwaajiriwa wa Serekali.Mwuwaji aliyekula kiapo cha utii cha uaskari cha kuilinda Taifa na viongozi wake. 

Hiki kilikuwa kisasi cha kurithi kwa muuwaji huyu kutoka kwa baba yake?Kama ni hivyo sababu ya mauaji ya kikatili ni ileile ya baba wa muuwaji huyu?Mwaka 1946 serekali ya kikoloni iliitoa nafasi ya ushiriki katika Bunge la Zanzibar kwa wawakilishi wa wananchi ya kuteuliwa kwa misingi ya kikabila ya Waarabu watatu,Wahindi wawili,Mzungu mmoja na Mshirazi(Mwaafrika) mmoja.

Jumuia ya African Association ya Zanzibar ikalalamikia kunyimwa kwa nafasi za kutosha za uwakilishi ya Waafrika ambao ndiyo wengi na wenye asili ya Zanzibar.Wakaloni na Sultani mwaka 1950 wakafanya mabadiliko ya uwakilishi katika Baraza la kutunga sheria ya kuteua Waarabu wanne,Waafrika wanne,Wahindi watatu na Mzungu mmoja.

Usawa huu wajumbe wanne wa Waarabu na Waafrika ukaikera sana Jumuia ya Kiarabu ya Zanzibar na kuamua kuvisusia vikao Baraza.Ikatokea mmoja ya Waarabu aitwaye Ahmed Mugheiry kutokubaliana na Waarabu wenzake waliotaka idadi ya Waafrika ipunguzwe na isiwe sawa na ya Waarabu.

Mughery akasusiwa na Waarabu wenzake.Kundi la Waarabu wakamjeruhi kwa visu.Mughery akaharakishwa hospital ya Mnazi Mmoja kwa matibabu.Wakati anapatiwa matibabu, Mwarabu Mohammed Barwani akiigiza kuwa ndugu wa mgonjwa Mughery akaingia wodini na kuchomoa kisu na kumchoma tumboni na kifuani hadi kufa kwa kosa la kutetea Waafrika.

Huyu muuwaji Mohammed Barwani ndiye aliyemzaa muuwaji wa Abeid Karume aitwaye Homoud Mohammed Barwani kwa bunduki ya kivita miaka 22 baadaye tarehe kama ya leo.Huu ukoo wa mauaji ya kikatili yumkini katika damu yao na nafsi yao wana chuki dhidi ya Waafrika wa Zanzibar.Kwa nini baba na mtoto waue viongozi wanaotetea masilahi ya Waafrika wanyonge, kundi lilokosa fursa na haki za msingi katika ardhi ya nchi yao?

Kosa la Abeid Karume kwa muuwaji Homoud ni kupigania haki ya Waafrika?Waafrika wa Zanzibar kabla kufanikwa kwa Mapinduzi ya Januari mwaka 1964 yaliyoongozwa na Abeid Karume walilazimishwa na utawala wa Kiarabu wa Kisultani wawe watu duni.Ni wao waljofanywa watumwa na kugeuzwa bidhaa ya kuuzwa sokoni.

Mwaka 1859 katika soko la watumwa Zanzibar bei ya mtumwa mtoto ni sh.25 na mtu mzima sh.45. Na kwamba mwaka 1840 kiasi ya watumwa hao millioni moja na laki sita waliuzwa nje ya Zanzibar.Waafrika hawa Zanzibar ndiyo walioimarisha mashambaya minazi na Karafuu iliyokuwa inamilikiwa na mabepari wa Kiarabu.

Majengo makubwa ya kihistoria leo katika Mji Mkongwe na Kasir nyingi za Sultan tofauti zimejengwa kwa nguvu za Waafrika wa Zanzibar.Kwa miaka nenda miaka rudi wachumaji wa karafuu na wakwezi wa minazi katika mashamba walikuwa Waafrika.Marobota kwa marobota ya mazao ya karafuu na mbata kwa miaka kadha ikibwebwa katika migongo iiliyoota masuguru ya wachukuzi na makuli Waafrika.

Mji Mkongwe ulikuwa unakaliwa na Masultani, Waarabu, ,Wazungu na Wahindi matajiri.Hata hivyo, wapishi wao,madobi wao,mayaya wao na matopasi wao walikuwa Waafrika kutoka mitaa ya ng'ambo.Masultani na Waarabu matajiri walistarehesha na matamanio ya miili yao kwa wanawake wa Kiafrika waliowabatiza kwa jina la ‘ masuria’ bila kuwaoa.

Ingawa Waafrika ndio nchi yao Zanzibar walibaguliwa katika kila kitu.Walinyimwa kumiliki ardhi na mashamba.Elimu walikoseshwa huku Waarabu na Wahindi wakijenga na kuendesha skuli zao za makabila.Huduma za elimu za msingi zilikuwa za kulipia ambapo Waafrika walikosa fedha za kulipia.

Wale waliokuwa wanaishi mjini katika mitaa duni isiyokuwa na miundombinu wala fursa walitakiwa walipiye kodi ya viwanja kwa vibanda vya kuishi.Waafrika wengi walikufa kwa kukosa huduma za kiafya na lishe.Kwa matokeo hayo Waafrika wa Zanzibar kuajiriwa katika za serekali na kubaki kuwa matarishi na wafagiaji katika maofisi ya srekali kwa miaka nenda
miaka rudi.

Ni Karume na chama cha Afro – Shirazi waliokuja kuleta Mapinduzi ya kuondoa dhuluma hii na kurejesha utu na heshima ya Mwafrika.Kumbe bado wapo watu wanaotaka Mwaafrika awe mtwana,mjakazi na suria katika Zanzibar.Mohammed Barwani na mwanawe Homoud Mohammed Barwani hawataki mabadiliko hayo.Leo ni siku ya kumbukumbu ya kuuwawa Karume.Wauwaji hatuwasahau na hatuwasamehe.

RAIA WA RWANDA WAISHIO NCHINI WAADHIMISHA MIAKA 25 YA MAUAJI WA KIMBARI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii 

RAIA wa Rwanda waishio nchini Tanzania leo Aprili 7 wameadhimisha miaka 24 ya mauaji ya kimbari yaliyopoteza zaidi ya watu milioni moja kwa siku 100 hasa kabila la Watutsi na kuacha yatima, wajane wengine wengi katika hali ngumu. Raia hao wameeleza kuwa kilichotokea hawatakisahau na hakitatokea tena. 

Akizungumza katika kumbukizi hiyo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameeleza kuwa tukio hilo linakumbukwa pia na watanzania na kuahidi kuzidi kushirikiana nao katika masuala ya kujenga nchi na kusema kuwa hata mwaka 2016 Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli alifanya ziara nchini Rwanda alipotembelea kituo cha mauaji hayo huko Kigali na kueleza kuwa mauaji hayo yalianza kwa kupandikiza chuki katika jamii na kusisitiza kuwa hayo hayatatokea tena Rwanda na kwingineko Afrika. 
Aidha Mwakyembe ameeleza kuwa lazima tusaidiane na kushirikiana ili kuhakikisha janga kubwa kama hilo halitatokea tena. Aidha amesema kuwa mauaji hayo hayakutokea kama radi huku akiwaasa wananchi kuacha kupandikiza maneno ya chuki katika jamii. 

Kwa upande wake Balozi wa Rwanda nchini, Eugine Kayihura ameeleza kusikitishwa na tukio hilo ambalo liliathiri wananchi na taifa kwa ujumla lakini baada ya vita Rwanda iliungana tena na kuwa wamoja na kuleta maendeleo, ameeleza kuwa wanawakumbuka wenzao ambao walilengwa kuuawa na hawatasahaulika kamwe. 

Pia amesema kuwa kwa sasa wananchi wameungana pamoja na wapo sambamba katika kuleta maendeleo nchini humo. Aidha ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kudumisha mahusiano bora pamoja na jumuiya ya umoja wa mataifa kwa kuzidi kuonesha ushirikiano na wao kama taifa watazidi kusimama imara katika kuhakikisha mauaji ya aina hiyo hayatatokea tena watazidi kushirikiana, na kuwa na umoja . 
Mwakilishi wa taasisi ya kimataifa inayoshughulikia masuala yaliyosalia ya mahakama za makosa ya jinai (IRMCT) Samuel Algozin amesema kuwa miaka 25 iliyopita tangu kupotea kwa wajamii hao ambao wengi walikuwa wanawake, watoto na wazee na wengine kuachwa yatima na wajane hawatasahaulika, watakumbukwa kwa yote waliyofanya katika kulitetea taifa. 

Amesema kuwa wataendelea kulinda na kutetea haki za binadamu na kuhakikisha mauaji ya aina hiyo hayatatokea tena kama yalivyotokea mwaka 1994 na wataendelea kusimama pamoja katika kuhakikisha haki za binadamu zinatekelezwa. 

Pia Mwakilishi wa umoja wa mataifa (UN), Alvaro Rodriguez ameeleza kuwa waliouawa katika mauaji hayo nchini Rwanda miaka 25 iliyopita watakumbukwa Rwanda na kwingineko na kueleza kuwa kuokoa maisha ya watu lazima kuwe na matendo hasa kwa kuangalia masuala ya haki na usawa pamoja na kutetea haki za binadamu huku akieleza kuwa ni lazima kila nchi ijizatiti katika kutimiza malengo yake ya kulinda haki za binadamu. 

Maadhimisho hayo yalianza kwa matembezi na kufuatiwa na kwa sala fupi na baadaye mishumaa kuwashwa kama ishara ya kuwakumbuka wenzao waliouwawa kwenye mauaji hayo. Mwisho.
Balozi wa Rwanda nchini, Eugine Kayihura (wa pili kulia) akiongoza matembezi maalum ya wameadhimisha miaka 24 ya mauaji ya kimbari yaliyopoteza zaidi ya watu milioni moja kwa siku 100 hasa kabila la Watutsi na kuacha yatima, wajane wengine wengi katika hali ngumu, yaliyonyika leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiongozwa na Balozi wa Rwanda nchini, Eugine Kayihura pamoja na viongozi wengine, kuwasha mishumaa wakati wa  kuadhimisha miaka 24 ya mauaji ya kimbari yaliyopoteza zaidi ya watu milioni moja kwa siku 100 hasa kabila la Watutsi na kuacha yatima, wajane wengine wengi katika hali ngumu, yaliyonyika leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza katika maadhimisha miaka 24 ya mauaji ya kimbari yaliyopoteza zaidi ya watu milioni moja kwa siku 100 hasa kabila la Watutsi na kuacha yatima, wajane wengine wengi katika hali ngumu, yaliyonyika leo jijini Dar es salaam.
Balozi wa Rwanda nchini, Eugine Kayihura akizungumza katika maadhimisha miaka 24 ya mauaji ya kimbari yaliyopoteza zaidi ya watu milioni moja kwa siku 100 hasa kabila la Watutsi na kuacha yatima, wajane wengine wengi katika hali ngumu, yaliyonyika leo jijini Dar es salaam.





























TBS YAFANYA MSAKO MKALI MIKOA YA KANDA YA ZIWA KUONDOA NGUO ZA MITUMBA, BIDHAA ZISIZO NA UBORA

$
0
0
Na Ripota Wetu, Musoma

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeamua kuendesha ukaguzi wa kushutukiza katika masoko yaliyopo  wilayani Musoma Mjini, mkoani Mara ikiwa ni mwenedelezo wa mkakati wa shirika hilo kuondoa bidhaa ambazo hazina ubora kwenye soko nchini.

Ukaguzi huo umeendeshwa na maofisa wa TBS ambapo ukaguzi huo umekwenda sambamba na kuondoa kwenye soko nguo za ndani za mitumba kutokana na matumizi yake kupigwa marufuku nchini kwa kuwa zina madhara kiafya kwa watumiaji.

Mbali na hatua hiyo, pia sampuli mbalimbali za bidhaa zimechukuliwa katika masoko hayo kwa lengo la kwenda kuzipimwa kwenye maabara za shirika hilo ili kujiridhisha kama zinakidhi  viwango, huku vilainishi vya magari visivyokuwa na ubora vikiondolewa kwenye soko, kwenye baadhi ya maeneo ya kanda ya ziwa ambako operesheni hiyo imefanyika.

Akizungumza wakati wa operesheni hiyo Mkaguzi wa TBS, Baraka Bajije, amesema kuwa katika ukaguzi huo unaendelea Kanda ya Ziwa kabla ya Musoma Mjini umefanyika pia masoko maeneo ya Mwanza Mjini, Sengerema, Magu, Bunda na sasa Musoma  Mjini ambapo wamefanikiwa kukamata shehena ya nguo za ndani za mitumba pamoja na taulo zinazokadiriwa kuwa na thamani ya Sh. milioni 10.

Amesema kuwa Sheria ya Viwango Namba 2 ya mwaka 2009 inazuia matumizi ya nguo za ndani za mitumba pamoja na taulo, lakini bado watu wasiowaaminifu wamekuwa wakiziingiza  kwenye soko la Tanzania kupitia njia za panya.

Pia Bajije amesema bidhaa hizo haziruhusiwi kabisa kuwepo sokoni kutokana na madhara yake kwa watumiaji ikiwemo kusababisha magonjwa sugu ya fangasi, kansa ya ngozi na magonjwa mengine.

Ametoa mwito kwa Watanzania kuacha kabisa kutumia nguo hizo kutokana na madhara yake kuwa makubwa.Wakizungumza wakati wa operesheni hiyo baadhi ya wananchi wameunga mkono hatua zinazochukuliwa na TBS kuondoa sokoni nguo hizo. "Nguo hizi za ndani za mtumba watu

tulikuwa tunazipenda kwa sababu uimara na unafuu wa bei, lakini baada ya  kuelimishwa madhara yake na TBS, lazima na sisi Watanzania tubadilike," amesema Joyce Magesa.

"Leo hii watu wanapenda kuzinunua kwa kuvutiwa na bei ya Sh. 1,000 kwa sidiria, lakini ukipata kansa ya matiti gharama za kujitibia hazilingani kiasi hicho cha fedha.Nikiri wanawake walio wengi ndio watumiaji wa kubwa ikilinganishwa na  wanaume,lakini elimu tunayoendelea kuipata kutoka TBS itatusaidia kuachana na uvaaji wa nguo za ndani ambazo ni za mtumba,"amesema.

Imefafanuliwa nguo za ndani zilizopigwa marufuku ni pamoja na soksi, taiti, sidiria, taulo na nyingine. Wakati huo huo  TBS inaendesha operesheni ya ukaguzi wa bidhaa sokoni ili kubaini bidhaa zisizo na viwango zilizopo humo. Kwa sasa maofisa wa shirika hilo wapo mikoa ya kanda ya ziwa wakiendesha uendesha msako huo wa bidhaa hafifu sokoni.
 Sehemu ya shehena ya nguo za mitumba zikiwa zimekamatwa kwenye masoko mbalimbali ya Musoma Mjini baada ya maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania(TBS) kufanya msako wa kushtukiza
 Taulo ambazo zimeshutumika maarufu taulo za mtumba zikiwa zimeshikiliwa na maofisa wa TBS baada ya kuzikamata katika masoko ya wilayani Musoma Mjini baada ya kufanya msako mkali

 
 Nguo za mitumba zikipakiwa kwenye gari baada ya kukamatwa na maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania(TBS)waliopo mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo wanaendelea na msako wa kushtukiza katika masoko kwa lengo la kuondoa bidjaa zisizokuwa na ubora pamoja na nguo za mitumba

MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRIL 8,2019

TFS YAPELEKA ELIMU YA UTUNZAJI MAZINGIRA KWA WANAFUNZI SEKONDARI YA MINAKI, PUGU

$
0
0
WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umeweka mkakati kuhakikisha inatoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani na Sekondari ya Pugu jijini Dar es Salaam kwani wanaamini iwapo wanafunzi hao watakuwa na uelewa mzuri kuhusu misitu iliyopo watakuwa mabalozi wazuri na walinzi wa misitu nchini.

 Akizungumza na wanafunzi wa shule hizo kwa nyakati tofauti, Meneja Masoko wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Mariam Kobero amesema Serikali imekuwa ikifanya jitihada kubwa za kuhakikisha misitu yetu nchini inalindwa na kudhibiti uharibifu wa mazingira na katika jitihada hizo hizo TFS nayo imekuwa na mikakati ya kufanikisha misitu nchini inatunzwa na kulindwa wakati wote.

Kobero amesema kwa kutambua umuhimu na faida za misitu TFS imeona ni vema ikakutana na wanafunzi wa shule hizo kwa lengo la kutoa elimu ambayo itajikita zaidi kuelezea faida za misitu na umuhimu wa kuilinda kwani ili misitu iwe salama ni jukumu la kila Mtanzania kuwa mlinzi ikiwa pamoja na kutokuwa tayari kuona msitu unaharibiwa halafu anakaa kimya.

"Wakala wa Huduma za Misitu hatujalala, tunatambua pamoja na mambo mengine ni wajibu wetu kukutana na makundi ya watu mbalimbali ili kutoa elimu inayohusu umuhimu wa misitu kuilinda na kutokata miti hovyo.Hivyo leo hii tumeamua kuzungumza na wanafunzi wetu hao ambao tunaamini watakuwa mabalozi wetu waa wazuri kwa wananchi wengine.

"Pia wanafunzi hawa tunawaleza si tu kuhusu misitu tuliyonayo bali tunawaeleza na uwepo wa fursa ya kufanya utalii wa ndani kwa watanzania kwani katika misitu yetu kuna vivutio mbalimbali. Kwa hapa Pugu tu , katika kilele cha Mlima Pugu ukienda unauona mji wote wa Dar es Salaam.Watalii wengi kutoka nje wanakuja , hivyo tunawaambia wanafunzi wafahamu na wao watawafahamisha wengine," amesema Kobero.

 Alipoulizwa iwapo ipo haja ya kuwa na mitaala inayozungumzia kwa kina kuhusu misitu na mazao yatokanayo na misitu pamoja na utalii, Kobero amesema anatambua uwepo wa masomo yanayozungumzia kuhusu faida za misitu na utalii lakini kwake anaona ni vema ukaweka msisitizo zaidi kwa kuweka masomo yaliyojikita katika maeneo hayo ili kuwajengea wanafunzi uelewa mpana zaidi.

Kuhusu iwapo elimu hiyo ambayo imetolewa kwa wanafunzi wa Sekondari ya Pugu na Minaki, Kobero amesema mkakati wa TFS ni kuhakikisha kanda zote kunakuwa na utaratibu huo na kwamba waaamini watawafikia wanafunzi wengi zaidi pamoja na makundi ya watu mbalimbali kwani lengo ni kuunganisha nguvu katika ulinzi wa misitu iliyopo nchini.

Kwa upande wa wanafunzi wa shule hizo wamesema wanaipongeza TFS kwa uamuzi wake wa kuona haja ya kutoa elimu inayohusu utunzaji misitu kwao, kwani kuna mambo wamejifunza na wanaamini yatawasaidia kushiriki kikamilifu kwenye utunzaji misitu nchini.

Wamesema ni kweli wanafahamu faida za misitu lakini elimu ambayo wameipata kutoka TFS wamebaini kuna mambo mengi ambayo hawakuwa wanayajua lakini sasa wamepata mwanga huku wakitumia nafasi hiyo kuomba mafunzo hayo yawe endelevu na sio kwao tu bali na kwa wengine kwani wote wanajenga Tanzania moja na kwamba misitu ni uhai.
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Pugu jijini Dar es Salaam wakiwa ndani ya msitu wa asili wa Pugu ambapo lengo la ziara hiyo ni kujifunza kuhusu uhifadhi wa mazingira lakini msitu huo ndiko unakopatikana mti wa Mpugupugu ambao ndio chimbo la jina la Sekondari ya Pugu
 Moja ya mti mrefu uliopo ndani ya msitu wa asili wa Pugu

 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki wilayani Kisarawe mkoani Pwani na Sekondari ya Pugu jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) kuwapeleka kwenda kushuhudia vivutio vilivyomo kwenye Msitu wa asili wa Pugu
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki wilayani Kisarawe mkoani Pwani wakionesha furaha yao baada ya kufanya utalii wa ndani kwa kwenda Msitu wa Asili wa Pugu .
 Baadhi ya wanafunzi wakishangilia baada ya kufika juu ya kilele cha Mlima wa Pugu ambapo walitembea kwa saa moja na nusu hadi kufika keleleni

OFISA UFUGAJI NYUKI WA TFS ASEMA KUNG'ATWA NA NYUKI KUNA FAIDA KUBWA KATIKA MWILI WA BINADAMU

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

IMEELEZWA kuwa binadamu kukang'atwa na mdudu nyuki kuna faida nyingi sana katika mwili wa binadamu ikiwemo ya kusaidia kuondoa sumu mwilini, hivyo kwa wale ambao watang'atwa hawana sababu ya kumuua nyuki.

Hayo yameelezwa na Ofisa Ugugaji Nyuki kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Rueben Nyambita wakati anazungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minaki wilayani Kisarawe pamoja na Shule ya Sekondari Pugu ya jijini Dar es Salaam ambapo TFS imeamua kuzungumza na wanafunzi hao kwa lengo la kuwapa elimu inayohusu utunzaji wa misitu , faida za uwepo wa misitu na ufugaji nyuki katika misitu mbalimbali chini.

Hivyo TFS imeamua kuja na mkakati wa kuhakikisha inazungumza na wanafunzi mbalimbali kuanzia shule za msingi, sekondari na vyuo ambapo wanaamini wakiipata vema elimu kuhusu utunzaji misitu na rasilimali za misitu watakuwa mabalozi wazuri kwa wengine.Hivyo maofisa wa kada mbalimbali wa TFS walienda katika shule hizo kuzungumzia misitu na faida zake pamoja na utalii unaopatikana ndani ya hifadhi za misitu ikiwemo ya asili na hasa ambayo iko chini ya TFS.

Wakati wanazungumza na wanafunzi hao kwa nyakati tofauti, Nyambita pamoja na kuzungumzia faida nyingi zinazopatikana kutoka kwa mdudu nyuki akatumia nafasi hiyo kueleza iwapo binadamu atang'atwa na nyuki, basi sumu iliyokuwa mwili itaondoka."Kukang'atwa na nyuki kuna faida, hivyo ukiona amekung'ata mahali ujue anakwenda kuondoa sumu na tunatarajia kuwa uvimbe wake hauwezi kuwa mkubwa."

Nyambita ameongeza hata kama binadamu ataumwa na nyuki watatu, wanne, watano au hata 10 bado watasaidia kundoa sumu na iwapo mhusika atavimba sana kuliko kawaida maana yake mwili wake utakuwa na sumu nyingi , hivyo inapokutana na sumu ya nyuki inasababisha aleji.

Hata hivyo amefafanua nyuki anayo sumu lakini haina madhara sana kwa binadamu zaidi ya tiba lakini iwapo binadamu ataumwa na nyuki wengi sana kwa wakati mmoja basi ni rahisi kupata madhara kwani sumu ya nyuki itakuwa nyingi mwilini."Wanafunzi na wananchi kwa ujumla msigope kuumwa na nyuki kwani ni sehemu ya tiba."

Kuhusu asali inavyotengenezwa, Nyambita amewaambia wanafunzi hao kuwa, asali ya nyuki inatengenezwa kutokana na mimea mbalimbali ambayo nyuki hupendelea kwenda kufyonza maji na hasa kwa maua ambayo yanatoa maji yenye ladha ya sukari.

"Asali ya nyuki inatengenezwa na sukari ambayo inaitwa glukosi inayopatikana kwenye mimea mbalimbali.Nyuki anapotua kwenye mmea anavyonza maji na kisha anachuja sukari inayopatikana kwenye ule mmea ambayo ni kati ya asilimia 25 hadi 40 maji ya mimea hiyo inakuwa na sukari.Pia nyuki mwenyewe anavyo vimeng'enya vya kutengeneza asali kwa asilimia 75 hadi asilimia 80,"amesema Nyambita.

Alipoulizwa na wanafunzi hao kwanini asali inaganda, amewajibu inatokana na glukosi ambayo ipo kwenye asali na ndio maana inasababisha kuganda na kuganda haina maana imeharibika.Kuhusu rangi tofauti ya asali , amesema hiyo inatokana na mimea ambayo nyuki ameifikia na kwa kuwa mimea ina rangi tofauti ni jambo la kawaida asali nayo kuwa na rangi tofauti tofauti.

Wanafunzi hao wameelezwa kuwa nyuki anapotengeneza asali, kwa kawaida anatengeneza kwa ajili ya chakula chake kwa kutambua kuna nyakati za ukame na njaa na hivyo anajiandaa kwa kuwa na chakula cha akiba lakini binadamu kwa uroho wao wameamua kula chakula cha nyuki ambayo ndio hiyo asali inayopendwa na watu wa rika mbalimbali.

Pia amesema kuna maziwa ya nyuki na hayo ni maalumu kwa ajili ya kulishwa malkia wa nyuki kutokana na jukumu ambalo analifanya kwa nyuki wengine, huku ikielezwa maziwa ya nyuki yana protini nyingi na kwa mwenye kuitumia anakuwa na akili nyingi sana na kama ni mwanafunzi atakuwa anafanya vizuri kwenye masomo kwa kushika nafasi za juu.

"Wanafunzi na Watanzania wenzangu kwa ujumla niwaambie tu kuna faida nyingi sana za uwepo wa nyuki , hivyo ni vema tukahakikisha tunazalisha kwa wingi mazo ya nyuki ambayo yanaweza kutuingizia kipato kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.Kuna aina mbili za kufuga nyuki ikiwemo ile ya asili na ya kisasa lakini hii ya kisasa ambayo ni kutumia mzinga nyuki wanatoa asali nyingi zaidi,"amesema Nyambita.

Pamoja na hayo yote TFS kupitia maofisa wake ambao walikuwa sehemu ya kwenda kuzungumza na wanafunzi hao wametumia nafasi hiyo kueleza kwa kina kuhusu umuhimu wa kufidhi misitu ya asili na kuhamasisha watanzania kuwa na utamaduni wa kufanya utalii wa ndani wa kutembelea hifadhi hizo.


MFUKO WA BIMA YA TAIFA ULIVYOSHIRIKI KUTOA HUDUMA KWA WANA MICHEZO KUMBUKUMBU YA SOKOINE

$
0
0
Wanamichezo wakipewa huduma ya vipimo katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) wakati mashindano ya kumbukumbu ya Sokoine jijini Arusha. 
Wanamichezo wakipewa huduma ya vipimo katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) wakati mashindano ya kumbukumbu ya Sokoine jijini Arusha. 
Mmoja wa wanamichezo akipimwa urefu na huduma nyingine za huduma ya afya katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) wakati mashindano ya kumbukumbu ya Sokoine jijini Arusha. 
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) ukitoa huduma za vipimo vya afya wakati mashindano ya kumbukumbu ya Sokoine jijini Arusha. 
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) ukitoa huduma za vipimo vya afya wakati mashindano ya kumbukumbu ya Sokoine jijini Arusha.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) ukitoa huduma za vipimo vya afya wakati mashindano ya kumbukumbu ya Sokoine jijini Arusha. 

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF),mkoa wa Arusha,Isaya Shekifu akifurahia baada ya kumalizia mbio za kilometa tano wakati mashindano ya kumbukumbu ya Sokoine jijini Arusha. 

Mwenge wa Uhuru Kung’arisha miradi ya Shilingi Bilioni 45.4 Rukwa.

$
0
0
Mwenge wa Uhuru wa Mwaka 2019 utakaokimbizwa katika wilaya tatu na Halmashauri Nne za Mkoa wa Rukwa unategemewa kuweka Mawe ya Msingi, kukagua na kuzindua miradi 35 ya maendeleo pamoja na vikundi 11 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambapo miradi hiyo ina thamani ya Shilingi Bilioni 45,404,104,489.59.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo baada ya kukabidhiwa mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia. Jenerali. Mstaafu Nicodemus Mwangela mara tu baada ya kuvuka daraja la mto Momba mbao ndio mpaka wa Mkoa wa Rukwa na Songwe katika Kijiji cha Kilyamatundu, Wilayani Sumbawanga.

Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Mwenge wa uhuru ukiwa katika Mkoa wa Rukwa utakimbizwa umbali wa jumla ya Kilomita 832.5 kuanzia tarehe 7 hadi 11, April, 2019 nahatimae kuwakabisdi majirani Mkoa wa Katavi, ambao utakuwa mkoa wa tatu tangu kuwashwa kwake katika mkoa wa Songwe mapema mwezi huu.

Wakati akifafanua michanganuo ya uchangiaji wa miradi hiyo Mh. Wangangabo alisema “Wananchi Shilingi 244,524,500.00 sawa na asilimia 0.5 ya gharama zote.Halmashauri Shilingi 619,611,106.00 sawa na asilimia 1.4, Serikali Kuu Shilingi 16,426,480,402.00 sawa na asilimia 36.2, Wadau wa maendeleo Shilingi 759,489,800 sawa na asilimia 1.7 Aidha, kuna mradi wa uchimbaji makaa ya mawe ambao unathamani ya Shilingi 27,353,998,681.59 mradi huu utakaguliwa, ambao una wastani wa asilimia 60.2 ya gharama zote.”

Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 aliupongeza uongozi wa mkoa wa Rukwa kwa mapokezi mazuri aliyoyapata na kuwaahidi kutowaangusha wananchi katika ukaguzi wake wa miradi ambayo Mwenge wa Uhuru utaipitia.

Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 ni “Maji ni haki ya kila Mtu, tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa”
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akikiri kuupokea Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2019 baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia. Jenerali. Mstaafu Nicodemus Mwangela (kushoto).

Masauni lauds efforts by Meadows Academy

$
0
0

The Deputy Minister for Home affairs Hon Hamaad Masauni addressing participants at Uhuru Walk 5

Speaking at the just-ended Uhuru Walk 5, the Deputy Minister of Home Affairs Hon Hamaad Masauni, lauded the efforts pitched in by Upanga-based Meadows Academy in using the Uhuru Walk event to raise the spirit of community service while engaging in capacity building activities at Tumaini la Maisha (Muhimbili) as well as the House of Blue Hope.

"What particularly strikes me as a unique concept about Uhuru Walk is that it is an effort by a small kindergarten to mobilise community support and invest in human resource at the very beginning of life.  We see several efforts around us in which organisations build structures and buildings, which are of course very necessary, but what we usually forget is that the most important building blocks of growth in any nation, are the people.  And this is something, that you as all know, our Hon President H E Dr John Pombe Magufuli, regularly reminds us that we must not forget those around us who are less privileged, that we must remain fair to the idea of collective development."

He ended his speech as follows: I would like to end by quoting what the Almighty says in the Holy Qur’an "Hal jaza-ul Ihsan Illal Ihsan" Is there any reward for Good other than Good ? - Surah Ar-Rahmaan

Hon Masauni, flanked by Upanga West Ward Councillor Hon Adnan Kondo and Fire Rd Chairperson Bi Jokha, then proceeded to lead 800 odd walkers in the 6.3km walk, which brought several schools including Azania Secondary School
Tambaza Secondary School
Zanaki Secondary School
Aga Khan Mzizima Secondary School
Dar es Salaam International Academy
Academic International Secondary School

 Owners of Meadows Academy Mohamedarif Suleman and Mohamed Suleman pose for a group photograph with the leadership of Upanga West Bi Jokha Lamki - mwenyekiti Fire Rd and Hon Adnan Kondo, Diwani Upanga West
A section of the 800 participants at the start of the event
 Kinders of the Meadows Academy helping the chief guest in cutting the ribbon as Mohamedarif Suleman, Event Team Leader (left) and Hon Adnan Kondo (Right) look on

 Hon Hamaad masauni, Deputy Minister of Home Affairs (extreme left) walking the 6.3km route flanked by Hon Adnan Kitwana Kondo, Diwani Upanga West and Mwenyekiti Fire Rd, Bi Jokha Lamki

NUKUU ZA NDG. POLEPOLE KWENYE MKUTANO MKUU WA JIMBO LA SIKONGE, WILAYA YA SIKONGE- MKOA WA TABORA

$
0
0
1. "Kwa niaba ya Viongozi wakuu wa Chama nitoe shukrani za dhati kwa wananchi kwa kukipatia heshima Chama chetu katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, asanteni sana" Ndg. Polepole

2. "Niwaombe Vikao vya kamati za siasa vinapo keti muwe na agenda za maendeleo na muwaalike watu wa Serikali ya Wilaya ili mpate mrejesho wa maendeleo ya wananchi na muwe na uelewa wa pamoja kuhusu utolewaji wa maendeleo kwa wananchi" Ndg. Polepole

3. "Hizi kazi za uongozi ni dhamana, tumepewa sio kwa sababu sisi ni bora zaidi hapana ila kwa sababu umma umetuamini kwa maslahi ya watanzania wote lazima tufanye kazi kwa bidii sana, kwa kujitoa, unyenyekevu na uaminifu wa hali ya juu" Ndg. Polepole

4. "Mbunge anayefanya kazi nzuri tumuache ajimwage kwa asilimia zote na tunawatangazia wanaCCM wengine wenye ndoto za ubunge katika majimbo hayo waache vurumai na wasubiri mpaka tutakapo watangazia  kwa mujibu wa Katiba" Ndg. Polepole

5. "Mara zote kwetu upinzani haujawahi kuwa tatizo kwenye uchaguzi, tatizo huwa ndani yetu wenyewe nongwa za sisi kwa sisi lazima tujirekebishe" Ndg. Polepole

6. "Unapokuwa na ukombozi wa kisiasa lazima uende sambamba na ukombozi wa kiuchumi, ndio maana sasa Serikali ya awamu ya tano imeamua kupambana kuhakikisha tunakuwa na uchumi wa kujitegemea na jumuifu" Ndg. Polepole

7. "Kuna watu hawataki kuona wala kusikia maendeleo yetu kama Nchi, sisi hatutabishana  nao maana kubishana na mjinga nawe unaonekana mjinga tu ila tutaendelea kufafanua mambo mazuri ambayo Serikali ya CCM chini ya Ndg. Magufuli inayafanya kwa nchi yetu" Ndg. Polepole

8. "Ndg. Magufuli ameleta heshima kubwa mno kwa nchi yetu na Afrika nzima naomba wanaCCM tuendelee kumuunga Mkono" Ndg. Polepole

Pamoja na mambo mengine Ndg.  Polepole ameeneza mambo mazuri yanayofanywa na Serikali ya CCM chini ya Uongozi wa Ndg. John Pombe Joseph Magufuli katika eneo la ujenzi wa reli ya kisasa, ununuzi wa ndege, miradi ya ufuaji wa umeme, ulindaji wa maslahi ya wananchi katika madini, uboreshaji wa huduma za Afya, Elimu na Maji na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya usafiri na usafirishaji. 

Imetolewa na:
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI





Deputy Minister Mwanjelwa to officiate the second Graduation Ceremony for Postgraduate Diploma in Leadership

$
0
0
Dar es Salaam: Graduation Ceremony for the second cohort of the UONGOZI Institute’s Postgraduate Diploma in Leadership Programme is scheduled to take place on 09th April, 2019 at the Mlimani City Conference Centre, where a total of 33 participants will be awarded their diplomas.

The Ceremony will be officiated by the Deputy Minister, President’s Office – Public Service and Good Governance, Hon. Dr. Mary Mwanjelwa (MP).

Launched in 2017, the Programme is jointly delivered by UONGOZI Institute and Aalto University Executive Education of Finland. The one-year Programme aims to develop leadership competencies in three areas; Making Strategic Choices, Leading People and Other Resources and Excelling in Personal Leadership Qualities.

“We are pleased to note that 97% of the participants, who joined the Programme in April, 2018, will graduate. This has been an intensive and challenging Programme, and the discipline and commitment they have shown is a true testament of their leadership capacity” said Prof. Semboja, CEO of UONGOZI Institute.

The second cohort of participants comprises of senior leaders from various ministries and public agencies of the United Republic of Tanzania.

“Understanding leadership is utterly important. In my view, anyone can be a leader but not all can be effective leaders. Effective leaders must exhibit specific skills and attributes to achieve sustainable results. This Programme has challenged our efficiency, particularly in developing innovative and sustainable solutions, and building winning teams,” said Hon. John Mongella, Regional Commissioner of Mwanza and one of the graduates.

The Ceremony will also be attended by 35 participants from the third cohort of the Programme, scheduled to begin in April, 2019. The cohort includes senior leaders from the Public, Private and Civil Society Organisations within the country.

Nelson Mandela Foundation Recognizes 16 Year Old Zuriel Oduwole

$
0
0
For her social entrepreneurial spirit teaching young unemployed women across Africa a basic film making class, and her global advocacy for girls education to prevent early marriages, the Nelson Mandela Foundation has recognized and honored 16 year old Zuriel Oduwole in Johannesburg - South Africa.
A filmmaker since the age of 9, when she made her first short documentary about the Ghana Revolution, she shared a short film about the centenary life of Nelson Mandela with the Foundations leadership, before being treated to a private tour of the foundation, including archives and priceless collections of the former President.

DC Joketi Mwegelo awasihi vijana kutenda matendo mema

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Joketi Mwegelo akizungumza katika maadhimisho ya Siku Kutenda Mema iliyofanyika viwanja vya Don Bosco jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Joketi Mwegelo amesema kuwa ukuta kwa vijana ni kutenda matendo yaliyo mema ikiwemo kusaidia au kutoa msaada pale penye uhitaji, wakati wa Maadhimisho ya Siku Kutenda Mema 'Good Deeds Day' iliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco Jijini Dar es Salaam.

Amesema hata vitabu vya Mungu vinafundisha kutenda mema ikiwemo kutoa pale panapohitajika na mafanikio yake yataonekana kwa kile ambacho mtu anajitoa. Mwegelo amesema hata yeye katika harakati zake vijana wenzake wamekuwa na mchango mkubwa wa kujitoa bila kuangalia maslahi ya kifedha.

Aidha amesema kuwa maadhimidlsho ya siku ya kutenda mema iwe ni njia ya jamii kuangalia vitu vya kufanya katika kusaidia watu wengine.

Naye Mwenyekiti wa Vipco na Mratibu wa Maadhimisho hayo, Emmanuel Makundi amesema kuwa wameandaa maadhimisho kwa kutambua matendo mema ndio nguzo ya amani, na matendo mema ni pamoja kuhakikisha kila mmoja anaishi kwa amani.

Makundi amesema wamefanya mambo mbalimbali ya jamii na watu wamekuwa na mwitikio katika kuwaunga mkono wa kusaidia watu wengine.

Afisa Uhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Mkoa wa Dar es Salaam, Mariam Juma amesema kuwa mahitaji ya damu kwa nchi ni chupa laki tano lakini ukusanyaji umefikia laki tatu hivyo wanahitaji wananchi wajitokeze katika kuchangia damu.
 Mwenyekiti wa VIPCO Emmanuel Makundi akizungumza kuhusiana na maadhimisho ya siku ya kutenda mema na mchango wa wadau mbalimbali yaliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco jijini Dar es Salaam.
 Vijana wakichangia Damu katika maadhimisho ya Siku Kutenda Matendo mema yaliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco jijini Dar es Salaam.
 Afisa Uhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Mkoa wa Dar es Salaam Mariam Juma akizungumza hali ya uchangiaji wa damu katika maadhimisho ya Siku ya Kutenda Mema iliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco Jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja wakitangaza amani katika maadhimisho ya siku ya kutenda matendo Mema iliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110172 articles
Browse latest View live




Latest Images