Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

TUTAENDELEA KUMUENZI MAREHEMU SOKOINE-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali na Watanzania wote wataendelea kumuenzi shujaa wao, Marehemu Edward Moringe Sokoine. Amesema Marehemu Sokoine wakati wa uhai wake alijitoa kuchapa kazi kwa bidii na amelitumikia Taifa kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Aprili 6, 2019) katika mbio za marathon kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Sokoine. Mbio hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Waziri Mkuu amesema Serikali iliamua kwa makusudi kukiita Chuo Kikuu cha Kilimo jina la Sokoine  ili kumuenzi  shujaa huyo.

Amesema Taifana Watanzania kwa ujumla wataendelea kufuata nyayo za Marehemu Sokoine katika mema mengi aliyolitendea Taifa la Tanzania na siku zote watandelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu.

Waziri Mkuu amesema kufanyika mbio hizo za Marathon ni ushahidi kwamba Marehemu Sokoine bado anakumbukwa na kuheshimiwa  na Watanzania kutokana na mchango mkubwa alioutoa katika ustawi wa Taifa. 

Alisema katika uhai wake, Marehemu Sokoine alikuwa ni mfano bora wa kiongozi wa juu  wa nchi  aliyedhamiria kwa dhati  kupambana na vitendo vya rushwa, uonevu, ubadhirifu na ufisadi.

“Leo hii tunaadhimisha kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Sokoine sambamba na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Magufuli inayoendeleza kwa vitendo  utendaji, uandilifu na mtazamo aliokuwa nao marehemu Sokoine.” 

Akizungumza kwa niaba ya familia ya Marehemu Sokoine, mtoto wa Marehemu, Namelok Sokoine alimshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kuwaenzi kwa vitendo waasisi wa Taifa la Tanzania.

Alisema anafarijika kuona kwamba yale yote aliyoyaamini na kuyasimamia Marehemu Sokoine hivi sasa yanatekelezwa kwa kasi zaidi na ufanisi wa hali ya juu na Serikali inayoongozwa Rais Dkt. Magufuli. 

Amesisitiza kwamba   familia ya Marehemu Sokoine  inaunga mkono kwa dhati  juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano na inaamini kwamba Tanzania yenye neema inakuja.

Katika Marathon hiyo, washindi kwa uapnde wa wanaume waliokimbia kilomita 21 ni Joseph Panga, mshindi wa kwanza, na wa pili alikuwa ni Aliphonce Felix Simbu na mshindi wa tatu alikuwa Lazaro Damasi.

Upande wa wanawake kilomita 21, mshindi wa kwanza alikuwa ni Faulina Abdi Matanga, mshindi wa pili alikuwa ni Magdalena Shauri na mshindi wa tatu alikuwa ni Nathalia Elisante.


Waliohudhuria katika mashindano hayo ni pamoja na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, Wabunge na viongizi pamoja na wengine wa Serikali.


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Moringe Sokoine   kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya viongozi na wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Moringe Sokoine kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Mtoto wa Marehemu Edward Sokoine, Mamelok Sokoine akitoa salamu za familia katika Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha  Marehemu Edward Moringe Sokoine kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Wasanii wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakti alipoozungumza katika Marathoni ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha  Marehemu Edward Moringe Sokoine kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Joseph Panga zawadi ya shilingi milioni moja ambaye aliibukuka kuwa Mshindi wa kwanza wa Marathoni ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Edward Moringe Sokoine, Kilomita 21 wanaume kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. Wa tatu kulia ni mshindi wa pili Alphonce Felix Simbu na Kulia ni mshindi wa tatuLazaro Damas. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Rais wa Shirikisho la Riadha nchini, Anthony Mtaka, Mjane wa Marehemu Edwad Moringe Sokoine, Napono Sokoine na wa tatu kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuzungumza katika Marathon ya Kumbukumbi ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Moringe Sokoine iliyofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid  jijini Arusha Aprili 6, 2019.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Napono Sokoine, Mjane wa Waziri wa Mkuu wa zamani, Marehemu, Edward Moringe Sokoine kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ambapo zilifanyika mbio za Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Moringe Sokoine, Aprili 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



WAHANDISI WATEMBELEA SHULE ZA MANYARA KUHAMASISHA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI

$
0
0
 Mhandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, Joyce Mbunju, akielekeza jambo kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kiteto, mkoani Manyara, kuhusu umuhimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati. 
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dirma, mkoani Manyara, wakimsikiliza Mhandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, Judith Aron (hayupo pichani), alipofika shuleni hapo kuhamasisha umuhimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
 Wahandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, wakigawa zawadi za madaftari na kalamu kwa mwanafunzi Esther Paschal wa Shule ya Sekondari Dirma, mkoani Manyara, aliyefanya vizuri katika masomo ya Sayansi. 
Wahandisi wanawake kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya kutwa ya Babati, mkoani Manyara, mara baada ya kutoa elimu ya umuhimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati kwa wanafunzi hao.
Picha na WUUM


SIMAMIENI VIAPO VYENU: JAJI MSTAAFU SHANGALI

$
0
0

Na Mary Gwera, Mahakama Kuu-Iringa
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Jaji Mary Simbo Shangali ametoa wito kwa Majaji na Mahakimu waliopo katika Utumishi kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kusimamia viapo vyao. 
Akizungumza na Waandishi wa Habari Aprili 05, 2019 mara baada ya hafla ya kuagwa rasmi kitaaluma, iliyofanyika Mahakama Kuu Iringa, Jaji Mstaafu Shangali alisema kuwa ni vyema kutekeleza majukumu kwa kumshirikisha Mwenyezi Mungu.
“Katika usikilizaji wa kesi ni vyema kumshirikisha Mungu na kusimamia viapo, hivyo tusicheze na mambo ambayo tumeapa mbele za Mungu tunapotekeleza majukumu yetu,” alieleza Jaji Mstaafu Shangali.
Aidha; Jaji Shangali aliwatia moyo Majaji na Mahakimu Wanawake  nchini kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi na sheria zilizopo bila kuteteleka.
“Kuwa Jaji mwanamke kwa nchi zetu za Afrika si kazi rahisi kutokana na baadhi ya mila desturi zilizopo, kwa hiyo ni vyema wanawake kutekeleza na kusimamia haki bila kuteteleka,” alisema Jaji Shangali.
Kwa upande mwingine, Jaji Shangali alitoa wito kwa jamii kuelewa kuwa pindi unapokuwa na kesi Mahakamani kuna kushinda au kushindwa, hivyo ni vyema kukubaliana na matokeo.
“Haki sio kushinda bali ni kupata kile unachostahili, kudai kwamba umenyimwa haki sio lugha sahihi, lazima upande mmoja utashinda na mwingine utashindwa,” alisema Jaji Shangali.
Kwa upande wake Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania,  Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi aliyeongoza hafla hiyo alimuelezea Jaji Mstaafu Shangali kuwa alikuwa mchapa kazi na mara zote alisimamia haki.
“Jaji Mstaafu Shangali ni mfano mzuri wa wachapakazi, amefanya kazi vizuri na hadi kufikia mwisho hakuna jalada lolote la kesi aliloacha bila kukamilisha na huu ni mfano mzuri,” alisisitiza Jaji Kiongozi.
Jaji Mstaafu Shangali, alianza kazi Mahakama ya Tanzania mwaka 1983, ambapo katika utumishi wake alishika nafasi mbalimbali na hadi anastaafu Jaji Shangali alikuwa Jaji namba. 1 wa Mahakama Kuu ya Tanzania na vilevile Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, na kufanya jumla ya miaka 35 ya Utumishi wake ndani ya Mahakama.
Jaji Shangali ameishukuru Viongozi na Watumishi wa Mahakama kwa ujumla kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote cha utumishi wake.
 Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania,  Jaji. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (wa tatu kulia) pamoja na Majaji wenzake wa Mahakama Kuu wakijumuika kumuaga kitaaluma Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Jaji Mary Simbo Shangali (wa tatu kushoto).
 Naibu Msajili Mwandamizi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Messeka Chaba (kushoto) pamoja na Naibu Msajili, Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Agatha Chugulu wakiwa katika hafla hiyo.
 Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali wa Mkoa wa Iringa, Bw. Adolf Maganda (kushoto) pamoja na Wakili wa Kujitegemea, Mwakilishi kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Bw. Rwezaula Kaijage (kulia) wakiwa katika hafla fupi ya Kumuaga Kitaaluma Jaji Mstaafu Mary Shangali.
 Mtendaji anayeshughulikia Mahakama za Mwanzo nchini, Bw. Humphrey Paya (katikati) pamoja na Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa, Bw. Elvin Mwakajinga (kulia) na sehemu ya Watumishi wa Mahakama Kanda ya Njombe na wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya kumuaga kitaaluma Jaji Mstaafu Shangali.
 Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi pamoja Wahe. Majaji wenzake akiwa katika picha ya pamoja Wanasheria wa Serikali mkoani Njombe waliohudhuria katika hafla hiyo,wa tatu kushoto ni Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Jaji Mary Shangali, wa tatu kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa, Panterine Kente, wa pili kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Jaji Dkt. Paul Kihwelo, wa pili kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Immaculata Kajetan Banzi, wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Dunstan Ndunguru na wa kwanza kulia ni Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali, Bw. Adolf  Maganda.
 Wahe. Majaji pamoja na Jaji Mstaafu Shangali wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Msajili, Mahakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi na Wilaya-Iringa.
 Picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama Kuu-Iringa na Njombe.
Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa aliyepo uhamishoni kuelekea Mahakama Kuu-Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Immaculata Kajetan Banzi (kushoto) akimkabishi ua kama ishara ya pongezi kwa Jaji Mstaafu Shangali (kushoto), anayeshuhudia katikati ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi.

(Habari na Picha na Mary Gwera, Mahakama Kuu-Iringa)

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA KAMBI YA TIMU YA TWIGA STARS

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mapema leo ameitembelea  Timu ya Soka ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania almaarufu Twiga Stars katika kambi yao iliyopo kwenye hoteli ya Ledger Plaza, Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe mapema leo alipoitembelea  Timu ya Soka ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania almaarufu Twiga Stars katika kambi yao iliyopo kwenye hoteli ya Ledger Plaza, Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia leo alipoitembelea  Timu ya Soka ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania almaarufu Twiga Stars katika kambi yao iliyopo kwenye hoteli ya Ledger Plaza, Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wachezaji wa  Timu ya Soka ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania almaarufu Twiga Stars alipoitembelea timu hiyo leo katika kambi yao iliyopo kwenye hoteli ya Ledger Plaza, Bahari Beach jijini Dar es Salaam.

SIMBA SC, TP MAZEMBE HAKUNA MBABE, KURUDIANA LUBUMBASHI APRIL 13, 2019

$
0
0
 Beki wa Kimataifa wa Uganda na Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, Joseph Ochaya akifurahia jambo na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Rwanda anayecheza Simba SC ya Tanzania, Meddie Kagere, wakati wa mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Mazembe na Simba, mchezo umemalizika kwa sare ya 0-0 kwenye dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Mohammed Ibrahim).
 Kikosi cha Simba SC kilichoanza leo dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo.
 Mashabiki wa Simba SC walifika kushuhudia mchezo huo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Kikosi cha TP Mazembe ya DR Congo kilichoanza leo mchezo dhidi ya Simba SC ya Tanzania.
Beki wa TP Mazembe, Joseph Ochaya akijaribu kumtoka Beki wa Simba SC, Zana Coulibaly katika mchezo ulimalizi uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa sare ya 0-0. Timu hizo zitarudiana tena wiki ijayo, April 13, 2019 mjini Lubumbashi nchini Congo.
 Dua zikiendelea.
 Kiungo wa Simba SC, Haruna Niyonzima akimtoka Mchezaji wa TP Mazembe ya DR Congo kwenye mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mchezo ulimalizika jioni ya leo kwa sare ya 0-0.

 Mashabiki wa TP Mazembe ya DR Congo wakifuatilia mchezo huo.
Nyota wa TP Mazembe, Rianford Kalaba akiondoka na mpira wakati wa mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Mazembe na Simba SC, timu hizo zimetoka sare ya 0-0 kwenye dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

CRDB Insurance Broker Ltd yashiriki Kambi ya Afya ya Mwananchi, jijini Dar

$
0
0
Kampuni ya CRDB Insurance Broker Ltd ikiwa ni mdau mkubwa wa Maendeleo ya sekta ya afya nchini kupitia huduma zake za bima ya afya, imeungana pamoja na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited kufanikisha Kambi ya utoaji wa huduma za afya bure (Mwananchi Afya Camp) iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.

Ushiriki wa CRDB Insurance Broker Ltd katika Kambi ya Afya ya Mwananchi ni sehemu ya kutoa fursa ya upatikanaji wa bima za afya kwa Watanzania wengi hasa ukizingatia watu wengi wamekuwa wakishindwa kumudu gharama za matibabu.
Akizungumza mapema leo, Meneja Mkuu wa CRDB Insurance Broker Ltd, Arthur Mosha amesema  kuwa afya ya binadamu ni muhimu kuliko vitu vyote na ili taifa liendelee tunahitaji watu wenye afya njema. Tumeshuhudia taifa likipoteza nguvu kazi kutokana na kukosa huduma bora za matibabu.

Ni matamanio yetu kuwa wananchi wote wawe na afya bora ili tuendelee kufanya kazi na kuzalisha kwa ajili ya taifa na hii ndiyo sababu tumeamua kuwa sehemu ya washiriki wa Kambi ya Afya ya Mwananchi ili kuhamasisha wananchi wengi kufahamu umuhimu wa afya.
 Afisa wa CRDB Insurance Broker Ltd, Clinton Minja akiwapatia maelezo ya huduma za bima wananchi waliotembelea Banda lao wakati wa Kambi ya Afya ya Mwananchi, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.
Afisa wa CRDB Insurance Broker Ltd, Witness Misese akiwapatia maelezo ya huduma za bima wananchi waliotembelea Banda lao wakati wa Kambi ya Afya ya Mwananchi, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.









SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUENZI MAZURI YOTE YALIOFANYWA NA HAYATI EDWARD SOKOINE

$
0
0
Na Woinde Shizza Globu ya jamii

Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa amesema kuwa serikali itaendelea kutambua mchango wa Hayati Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine, kwani alikuwa mfano katika kupambana na vitendo vya rushwa pamoja na kukemea ufisadi.

Majaliwa ameyasema hayo  leo katika Uwanja wa Shekhe Amri Abeid wakati wa mbio za madhimisho za kumbukumbu ya kifo cha hayati Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine.

Alisema serikali itaendelea kumuenzi hayati Sokoine kwa kuchapa kazi kuwa
bidii kwani mbio hizo ni sehemu ya uimarishaji wa afya ikiwemo kudumisha
amani na upendo.Alipongeza mafanikio makubwa ya kimichezo nchini pamoja na kuipongeza timu ya vijana wenye umri wa miaka 17 na kusisitiza kuwa hii ni historia kwa nchi ya Tanzania.

"Hii ni historia na Tanzania inawezekana kwani ushindi Tanzania unawezakanavna ni zamu yetu "Pia alipongeza Bondia Hassan Mwakinyo kwa kazi nzuri anayofanya ikiwemo kuitikia heri timu ya Simba.Naye Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza alisema serikali itaendelea kushirikiana na Chama cha Riadha Tanzania katika kuhakikisha vipaji vingi vinaibuliwa ikiwemo Tanzania kung'aa zaidi katika michezo mbalimbali.

Awali mtoto wa hayati Sokoine, Namelock Sokoine alishukuru serikali kwa
kuleta maendeleo ikiwemo katika sekta ya afya, miundombinu na nk na
kusisitiza kuwa hayati baba yake, Edward Moringe Sokoine alipokuwa hai
aliweza kutoa asilimia 50 ya mshahara wake kwaajili ya watu maskini.

Hivyo washiriki wa mbio hizo wamelipia fedha zao na wamechangia maskini
ambao hawana uwezo.Awali Rais wa Chama Cha Riadha Tanzania, Anthony Mtaka alisema michezo hiyo ni hamasa na ni kumbukumbu ya kifo cha hayati Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine

Alisema mwaka huu timu ya riadha itakwenda kushiriki mashindano ya riadha Nchini Qatar na nchini Tokyo Japani na kusisitiza wadhamini mbalimbali kujitokeza kwaajili ya kudhamini mchezo huo wa riadha na aliwashukuru wadhamini wa Dstv pamoja na Mamlaka ya Hifadhi(NCAA) kwakuwezesha kudhamini mashindano hayo.

"Tunapata hamasa tunapoona vipaji vipya vinaibuliwa kwani michezo ni ajira hivyo ninaomba wadhamini wengi zaidi kujitokeza " Pia alitoa rai kwa watu wanaoanzisha mashindano hayo ya riadha kila Mkoa na Wilaya wahakikishe wanafuata taratibu na sheria za ikiwemo kusajili mbio hizo, zawadi pamoja na kupewa masharti ya mbio za riadha.

Washindi wa mbio hizo walipewa medali fedha katika mashindano hayo ya
kilomita 21 ni Felix Simbu aliyeshika nafasi ya pili, mshindi wa kwanza ambapo amepokia kitita cha shilingi milioni moja Joseph Panga na Faraja Lazaro kwa upande wa wanaume akiondoka na shilingi laki nane.

Huku upande wa wanawake kilomita 21 wakiwa ni Failuna Matanga, mshindi wa pili Magdalena Shani na mshindi wa tatu Natalia Sule huku watoto wanawake kilomita tano Glory Patrick, Sharon Boniface na wanaume ni Said Barae, Omary Ramadhani na Msabaha Idd.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa akiwapa zawadi washindi wa kwanza wa kilometa 21katika mashindano ya mbio za moringe marathon 

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZUNGUMZA KATIKA MARATHON YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 35 YA KIFO CHA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali na Watanzania wote wataendelea kumuenzi shujaa wao, Marehemu Edward Moringe Sokoine.

Amesema Marehemu Sokoine wakati wa uhai wake alijitoa kuchapa kazi kwa bidii na amelitumikia Taifa kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Aprili 6, 2019) katika mbio za marathon kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Sokoine. Mbio hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Waziri Mkuu amesema Serikali iliamua kwa makusudi kukiita Chuo Kikuu cha Kilimo jina la Sokoine ili kumuenzi shujaa huyo.Amesema Taifana Watanzania kwa ujumla wataendelea kufuata nyayo za Marehemu Sokoine katika mema mengi aliyolitendea Taifa la Tanzania na siku zote watandelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu.

Waziri Mkuu amesema kufanyika mbio hizo za Marathon ni ushahidi kwamba Marehemu Sokoine bado anakumbukwa na kuheshimiwa na Watanzania kutokana na mchango mkubwa alioutoa katika ustawi wa Taifa.

Alisema katika uhai wake, Marehemu Sokoine alikuwa ni mfano bora wa kiongozi wa juu wa nchi aliyedhamiria kwa dhati kupambana na vitendo vya rushwa, uonevu, ubadhirifu na ufisadi.

“Leo hii tunaadhimisha kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Sokoine sambamba na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Magufuli inayoendeleza kwa vitendo utendaji, uandilifu na mtazamo aliokuwa nao marehemu Sokoine.”

Akizungumza kwa niaba ya familia ya Marehemu Sokoine, mtoto wa Marehemu, Namelok Sokoine alimshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kuwaenzi kwa vitendo waasisi wa Taifa la Tanzania.Alisema anafarijika kuona kwamba yale yote aliyoyaamini na kuyasimamia Marehemu Sokoine hivi sasa yanatekelezwa kwa kasi zaidi na ufanisi wa hali ya juu na Serikali inayoongozwa Rais Dkt. Magufuli.

Amesisitiza kwamba familia ya Marehemu Sokoine inaunga mkono kwa dhati juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano na inaamini kwamba Tanzania yenye neema inakuja.Katika Marathon hiyo, washindi kwa uapnde wa wanaume waliokimbia kilomita 21 ni Joseph Panga, mshindi wa kwanza, na wa pili alikuwa ni Aliphonce Felix Simbu na mshindi wa tatu alikuwa Lazaro Damasi.

Upande wa wanawake kilomita 21, mshindi wa kwanza alikuwa ni Faulina Abdi Matanga, mshindi wa pili alikuwa ni Magdalena Shauri na mshindi wa tatu alikuwa ni Nathalia Elisante.Waliohudhuria katika mashindano hayo ni pamoja na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, Wabunge na viongizi pamoja na wengine wa Serikali.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,JUMAMOSI, APRILI 6, 2019
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuzungumza katika Marathon ya Kumbukumbi ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Moringe Sokoine iliyofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid  jijini Arusha Aprili 6, 2019.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Mtoto wa Marehemu Edward Sokoine, Namelok Sokoine akitoa salamu za familia katika Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha  Marehemu Edward Moringe Sokoine kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Moringe Sokoine   kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Baadhi ya viongozi na wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Moringe Sokoine kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Wasanii wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakti alipoozungumza katika Marathoni ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha  Marehemu Edward Moringe Sokoine kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Joseph Panga zawadi ya shilingi milioni moja ambaye aliibukuka kuwa Mshindi wa kwanza wa Marathoni ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Edward Moringe Sokoine, Kilomita 21 wanaume kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. Wa tatu kulia ni mshindi wa pili Alphonce Felix Simbu na Kulia ni mshindi wa tatuLazaro Damas. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Rais wa Shirikisho la Riadha nchini, Anthony Mtaka, Mjane wa Marehemu Edwad Moringe Sokoine, Napono Sokoine na wa tatu kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

VIJANA WAPONGEZA SERIKALI KUWAJENGEA UWEZO KUHUSU KILIMO CHA KITALU NYUMBA

$
0
0
Muonekano nyanya katika moja ya vitalu nyumba vilivyotembelewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika Wilaya ya Dodoma mjini.
Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Ally Msaki akiwa kwenye moja ya kitalu nyumba wakati wa ziara ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika Wilaya ya Dodoma mjini na Chamwino.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU & MAELEZO)]
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Antony Mavunde akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati wa ziara ya kamati hiyo kutembelea mradi wa ujenzi wa vitalu nyumba katika Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma Aprili 06, 2019.
Moja ya Kitalu Nyumba cha mafano katika Wilaya ya Chamwino kama Kinavyoonekana ikiwa ni moja ya mikakati ya kuwainua vijana kupitia programu ya uwezeshaji inayotekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Sehemu ya Vijana zaidi ya 100 wa Wilaya ya Chamwino walionufaika na Programu ya ujenzi wa vitalu nyumba katika kila halmashauri hapa nchini wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Nagma Giga akizungumza wakati wa ziara ya wabunge wa kamati hiyo Wilayani Chamwino Jijini Dodoma, kujionea utekelezaji wa Programu ya ujenzi wa vitalu nyumba katika kila halmashauri hapa nchini.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Holly Green Agric Mhandisi Octavian Lasway akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu namna walivyoweza kutekeleza Programu ya ujenzi wa vitalu nyumba katika halmashauri ya Wilaya ya Chamwino pamoja na kuwajengea uwezo vijana ili kufanya mpango huo unaotekelezwa na Ofisi ya Waziri mkuu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Antony Mavunde akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Nagma Giga wakiwa ndani ya moja ya vitalu nyumba hivyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella IKupa akifurahia jambo na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Nagma Giga akizungumza wakati wa ziara ya wabunge wa kamati hiyo Wilayani Chamwino Dodoma kujionea utekelezaji wa Programu ya ujenzi wa vitalu nyumba.
Mmoja wa wanufaika wa programu ya ujenzi wa vitalu nyumba na mafunzo ya kuwawezesha vijana kutumia ujuzi huo kujikwamua kiuchumi akipongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuiwawezesha vijana.
Sehemu ya miche ya nyanya katika kitalu nyumba kama inavyoonekana katika picha ikiwa tayari kumika katika kitalu nyumba.

Wanufaika wa programu ya kukuza ujuzi eneo la kilimo cha kisasa kupitia teknolojia ya kitalu nyumba “green house” wameipongeza Serikali kwa kuendelea kuwawezesha katika masuala ya kilimo hicho na kujikwamua 
kiuchumi.

Pongezi hizo wamezitoa hii leo Aprili 06, 2019 wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ilipotembelea kukagua utekelezaji wa Programu ya ukuzaji ujuzi kwa vijana katika Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma.

Katika kupongeza jitihada hizo wanufaika wa programu ya kilimo hicho walibainisha mafanikio ikiwemo, kupata ujuzi wa kilimo cha mazao mbalimbali, kujikwamua kiuchumi ikiwa ni sehemu ya kujipatia vipato halali pamoja na kusaidia upatikanaji wa ajira kwa vijana wanaowezeshwa elimu hiyo.

Mtaalam kutoka kampuni ya Holly green Bw. Octovian Lasway alieleza kuwa, zaidi ya vijana 100 wamenufaika na elimu ya kilimo cha kitalu nyumba katika Wilaya hiyo na kusaidia kuondokana na changamoto za ukosefu wa ajira nchini.

“Programu hii imekuja wakati sahihi na imesaidia kundi kubwa la vijana kwa kuzingatia mafanikio yatokanayo na kilimo hiki cha kisasa kinacholeta tija kwa kuwa na mazao bora na kuongeza kipato kwa wananchi,”alisisitiza Octovian.

Akitoa maelezo kwa wanufaika hao, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde alieleza jitihada za Serikali katika kufikia kundi kubwa la vijana katika kuwawezesha na kuwajengea uwezo wa masuala ya ukuzaji ujuzi ili kuendelea kuongeza tija na kujikwamua kiuchumi kwa kuzingatia falsafa ya uchumi wa viwanda.

“Mradi umekusudiwa kutekelezwa kwenye Halmashauri zote 185 Tanzania Bara ambapo awamu ya kwanza itafikiwa mikoa 12 na Halmashauri 83 kwa lengo la kuwezesha vijana kuwa na ujuzi pamoja na stadi za maisha ili kufikia malengo tuliyojiwekea kama Serikali,”alieleza Mavunde

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ajira wa ofisi hiyo Bw.Ally Msaki alieleza kuwa, mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati ya Serikali katika kutatua changamoto ya ajira kwa vijana na kuboresha kipato kwa watanzania.

“Mpango huu unalenga kufikia vijana 18800 nchi nzima ambapo kila Halmashauri itafikia vijana 100 na hadi sasa tumefikia halmashauri za mkoa 10, ikiwemo;Dodoma, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Lindi, Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga na Kagera,”alieleza Msaki

Naye Makamu mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Nagma Giga alifurahishwa na utendaji na bidii ya vijana hao na kuwaasa kuendelea kutumia ujuzi huo kwa vijana wengine nchini.

Naye Naibu Waziri wa Ofisi hiyo anayeshughulikia Watu Wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa aliwataka vijana kutodharau kilimo kwa kuzingatia mchango wake katika kujikwamua kimaisha.

“Maisha hayapo kwenye karamu peke yake bali jembe linauwezo wa kuwatoa na kuwakwamua kiuchumi endapo kutakuwa na umakini na kujitoa kwa bidii,”alisisitiza Ikupa.

Kwa upande wake mwanagenzi Bw.Festo Ezikiel aliendelea kuipongeza serikali kuendelea kuwaamii na kuwajengea uwezo wa kilio cha kisasa cha kutumia kitalu nyumba.

“Tunaipongeza Serikali kutuamii na kutupa ujuzi kuhusu kilimo hiki nasi tunaahidi kushirikisha vijana wengine waliopo katika maeneo yetu ili kujikwamua kiuchumi,”alisema Ezekiel

=MWISHO=

Ugatuaji wa Madaraka sasa kuwa na nguvu ya kisheria na kisera

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe.Selemani Mzee akifungua kikao kazi cha kupokea rasimu ya sera ya Taifa ya ugatuaji wa madaraka jana mjini Masasi
 Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Edwin Mgendera akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu rasimu ya sera mpya ya madaraka kwa umma jana mjini Masasi.
 Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha kupokea maoni ya rasimu ya taifa ya Ugatuaji wa Madaraka ambao ni Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Weenyeviti wa Halmashauri, wabunge, na viongozi wa asasi za kiraia kutoka mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma wakishiriki kikao hicho mjini Masasi jana.


Na Mathew Kwembe, Masasi 

Serikali imesema Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka ya mwaka 2019 ambayo hivi sasa ipo katika hatua ya rasimu itakapokamilika itakuwa na nguvu ya kisheria na kisera tofauti na ile ya mwaka 1998 ambayo ilikuwa ni sera ambayo haikuwa na nguvu ya kisheria. 

Hayo yameelezwa jana mjini Masasi, mkoani Mtwara na Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Kisheria kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Edwin Mgendera mara baada ya kufunguliwa kwa kikao kazi cha kupokea maoni ya wadau juu ya rasimu ya sera ya Taifa ya ugatuaji wa madaraka ya mwaka 2019 kwa wananchi wa mikoa ya kusini ya Mtwara, Lindi na Ruvuma. 

Bwana Mgendera amesema mafanikio na changamoto zilizotokana na utekelezaji wa Sera ya Ugatuaji ya mwaka 1998 imeiwezesha serikali kuja na Sera ya jumla ya ugatuaji kitaifa ambayo itakuwa na nguvu za kisheria na namna bora ya kutekeleza na kutoa huduma kwa ufanisi kwa wananchi toka juu serikalini hadi ngazi za chini za Kitongoji na Mtaa kule kwenye Halmashauri. 

Amesema mwelekeo wa serikali kwa sasa ni huo wa kuwahudumia wananchi kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka ambayo itawekewa nguvu za kisheria na kisera ili kurahisisha suala la utoaji huduma kwa wananchi moja kwa moja kutoka serikali kuu hadi ngazi za kitongoji na mtaa. 

Mkurugenzi huyo wa huduma za Sheria amefafanua kuwa Msingi wa Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka, 1977 Ibara ya 145 na 146 ambazo zimetoa uhalali wa kuanzishwa kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na kubainisha madhumuni ya kuanzishwa kwa Mamlaka hizo yakiwemo kuzipa Mamlaka za Serikali za Mitaa madaraka ya kujiamulia mambo yao ya Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi katika maeneo yao kwa uhuru. 

“Aidha Sheria Na. 7 ya Halmashauri za Wilaya ya mwaka 1982 (sura 287) na Sheria Na. 8 ya Halmashauri za Miji ya mwaka 1982 (sura 288) zinazipa mamlaka hizo majukumu ya kutoa huduma kwa jamii katika maeneo husika,” amefafanua bwana Mgendera. 

Pia Mkurugenzi huyo ameitaja sheria ya Tawala za Mikoa ya Mwaka 1997 ambayo inazipa Tawala za Mikoa jukumu la kuratibu maendeleo katika Mikoa yao ikiwemo kuzisimamia na kuzisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutoa huduma bora kwa usawa kwa jamii. 

Ni kutokana na msingi huo wa sheria bwana Mgendera amesema kuwa masuala ya Ugatuaji wa Madaraka yanafanyika na yataeendelea kufanyika katika hatua mbili muhimu ambazo ni kugatua Madaraka kutoka Serikali Kuu kwenda Ngazi za Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji) na pili kugatua Madaraka kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenda ngazi za Msingi yaani Kata, Vijiji, Mitaa na Vitongoji. 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Kisekta kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Juma Idd ambaye pia ndiye Mratibu wa kikao kazi cha kupokea maoni ya wadau juu ya rasimu ya sera ya Taifa ya ugatuaji wa madaraka ya mwaka 2019 ameeleza kuwa hivi sasa timu yake ipo katika mikoa hiyo ya kusini baada ya zoezi hilo kukamilika katika mikoa ya nyanda za juu kusini ya Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe na Rukwa. 

Ameongeza kuwa baada ya kukamilika katika mikoa hiyo, timu ya kupokea maoni itaelekea katika kanda ya mashariki ambapo Mikoa ya Morogoro, Dar es salaam, Pwani na Dodoma itashirikishwa, na baadaye zoezi hilo kuhamia mikoa ya kaskazini, magharibi na kanda ya ziwa. 

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa wadau wetu muhimu wanapata fursa ya kutoa maoni yao juu ya nini wangependa kiwemo katika sera yetu hii mpya ya Ugatuaji wa Madaraka,” amesema bwana Idd. 

Awali akifungua kikao kazi cha kupokea maoni Mkuu wa Wilaya ya Masasi bwana Selemani Mzee ameeleza umuhimu kikao hicho ambapo amesema kuwa toka mwaka 1998 Serikali kupitia Rasimu ya maboresho ya Serikali za Mitaa (LGRP) imekuwa ikitekeleza dhana ya ugatuaji wa Madaraka ili kufikisha na kuharakisha utoaji wa huduma za Kijami,Kiutawala na Kiuchumi kwa wananchi kwa haraka na kwa usawa. 

Amesema kuwa kupitia dhana ya ugatuaji wa madaraka, wananchi wanapata fursa ya kutosha ya kushiriki na kushirikishwa katika shughuli na masuala yote yanayohusu maendeleo yao na ustawi wa maisha yao. 

Miongoni mwa wanaoshiriki kikao hicho ni pamoja na waheshimiwa Wabunge wanaotoka Mikoa ya kusini ambapo Mbunge wa jimbo la Nachingwea Mheshimiwa Hassan Elias Masala amesema kuwa kikao hicho ni muhimu kwao kama wawakilishi wa wananchi kwani utekelezaji wa ahadi nyingi za serikali kupitia chama kilichopo madarakani hivi sasa unategemea sana utekelezaji wa sera hii ya ugatuaji wa madaraka. 

Naye Bi Miriam Mwaibula mshiriki kutoka asasi isiyo ya kiserikali ya TWAWEZA amesema kuwa maoni yao ni muhimu kwani yatawezesha serikali kupata sera madhubuti na ambayo itakubalika na jamii yote na hivyo kurahisisha utekelezaji wake. 

Kikao hicho cha siku mbili kimewahusisha Wakuu wa Wilaya, Wabunge, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi kutoka katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, Makatibu Tawala wa Wilaya, Viongozi wa dini na Washiriki kutoka Asasi za Kiraia kutoka mikoa ya Mtwara, Lindi, na Ruvuma. 

RAIS MAGUFULI: SERIKALI IMEJIPANGA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UNUNUZI WA UMEME KWA WANANCHI

$
0
0
MAELEZO,DAR ES SALAAM


RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali itaendelea kutekeleza kwa kasi kubwa ujenzi wa miradi ya nishati nchini ikiwemo Mradi wa kufua umeme wa maji katika Mto Rufiji (Stiegler’s Gorges) hatua inayolenga kuwawezesha wananchi wengi kununua umeme kwa gharama nafuu na hivyo kuwawezesha kushiriki katika shughuli za kiuchumi.

Akizungumza leo Jumamosi (April 6, 2019) Mkoani Ruvuma wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa njia ya usafirishaji wa umeme ya kilovolti 220 Makambako- Songea, Rais Magufuli alisema Tanzania ina vyanzo vya kutosha vya kuzalisha umeme hivyo malengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa inashusha bei ya kununua umeme kwa Watanzania.

Aliongeza kuwa kwa sasa bei ya umeme kwa uniti moja hapa nchini ni Dola za Marekani senti 11 hadi 12, hali ambayo inawaumiza wananchi wa kipato cha chini kwani hali hiyo ni tofauti katika mataifa yanayoendelea ambayo yenyewe hayana vyanzo vingi vya umeme ukilinganisha na Tanzania ambayo ina vyanzo vingi vya uhakika vya uzalishaji wa nishati ya umeme.

Aidha Rais Magufuli alisema kutokana na malengo iliyojiwekea Serikali katika kufikia nchi ya kipato cha kati kupitia uchumi wa viwanda, Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kuhakikisha kuwa inakamilisha ujenzi wa miradi mikubwa ya uzalishaji wa umeme ili kuhakikisha kuwa kunawepo na malighafi za kutosha katika viwanda vya ndani na hivyo kulinda masoko ya  bidhaa zinazozalishwa nchini.
“Nchi yoyote inayotaka kujikwamua kiuchumi ni lazima iwe na uwezo wa kuzalisha nishati ya kutosha ya umeme, hatua hiyo itawezesha kulinda masoko yake ya ndani na kuepuka kununua malighafi kutoka nje ya nchi ambazo huuzwa kwa bei kubwa, hivyo Serikali tumejipanga kufanikisha adhma hii” alisema Rais Magufuli.

Aliongeza kuwa Serikali imeendelea kupata ushirikiano kutoka katika wadau mbalimbali wa maendeleo katika kufanikisha ujenzi wa miradi mikubwa ya sekta ya nishati ya umeme, ikiwemo mradi wa kufua umeme wa maji katika Mto Rufiji (Stiegler’s Gorges), ambao unatarajia kuzalisha Megawati 2100 na hivyo kuongeza nguvu katika Megawati 1560 zilizopo kwa sasa katika gridi ya Taifa.

Akifafanua zaidi Rais Magufuli alisema malengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa katika miaka michache ijayo, Tanzania inakuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 5000 katika gridi ya taifa hatua inayolenga kuvifanya viwanda vingi vilivyopo nchini viweze kuzalisha malighafi kwa ajili ya matumizi ya ndani pamoja na kusafirisha nje ya nchi.

Akizungumzia kuhusu mradi wa umeme wa ujenzi wa njia ya usafirishaji wa umeme ya kilovolti 220 Makambako- Songea, Rais Magufuli alisema kupitia mradi huo Serikali imeweza kuokoa kiasi cha Tsh Bilioni 9.8 zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kuzalisha umeme wa mafuta mazito na kuwataka watendaji wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) kusimamia kwa ukamilifu mradi huo ili uweze kuleta manufaa yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard  Kalemani alisema mradi wa umeme ya kilovolti 220 Makambako- Songea unatarajia kuvinufaisha jumla ya vijiji 122 vyenye jumla ya wakazi 22,000 waliopo katika Wilaya saba za Mikoa ya Njombe na Ruvuma, ambapo kipaumbele kimetolewa katika maeneo yaliyopo jirani na mradi huo.

Alisema hatua za awali za ujenzi wa mradi huo ikiwemo usanifu ulianza mwaka 2000-2008, lakini nguvu kubwa ya utekelezaji wa mradi huo zilianza Desemba 2015 ambapo jumla ya transfoma 300 zimewekwa katika maeneo mbalimbali yaliyopitiwa na mradi huo.

“Ulipoingia madarakani mwaka 2015, Mhe Rais umeweza kupunguza gharama kubwa katika matumizi ya umeme wa kutumia mafuta mazito ikiwemo mradi wa Aggreko, APTL na Symbion ambapo takribani Tsh Bilioni 712 zilikuwa zikitumika kwa ajili ya uzalishaji wa mafuta hayo” alisema Dkt. Kalemani.

Kwa upande wake, Balozi wa Usiswi nchini Anders Sjoberg alisema Serikali ya Uswisi itaendelea kuiunga mkono Tanzania katika kutekeleza miradi yote ya maendeleo ambayo imekuwa ikigusa maisha ya wananchi wa kipato cha chini.

Alisema Serikali ya Uswisi tangu miaka ya 1970 imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya nishati kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na Wakala wa Umeme Vjijini (REA) ambapo wamekuwa wakipeleka umeme kwa wananchi wa maeneo ya vijijini ili kuweza kuwaletea maendeleo yao.

CHAMA CHA WANASHERIA NCHINI (TLS) CHAPATA VIONGOZI WAKE WAPYA JIJINI ARUSHA.

$
0
0

Rais mpya wa chama cha wanasheria nchini TLS Dkt. Rugemeleza Nshala
Rais TLS aliyemaliza muda wake Fatma Karume akitoa neno la shukrani leo Jjini Arusha
Dkt. Rugemeleza Nshala kabla ya matokeo ya uchaguzi wa kuwa Rais wa TLS
Dkt.Rugememelela Nshala mara baada ya kutangazwa mshindi wa kiti cha urais wa TLS leo Jijini Arusha katika ukumbi wa AICC.




NA:Vero Ignatus , Arusha

Wanachama wa chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamewataka viongozi wapya watakao kiongoza chama hicho kutoa fursa sawa kwa mawakili walemavu ili kuweza kuhudumia vyema jamii Katika masuala ya kisheria na kuondokana na fikra potofu dhidi ya Watu walemavu.

Wakizungumza Mara baada ya kupiga kura baadhi ya mawakili ambao ni wanachama wa chama hicho wamesema ni vyema kwa viongozi kushirikiana na mawakili walemavu ili kutoa hamasa Katika jamii.

Elibariki Maeda ni Mwenyekiti wa chama chama mawakili wa kujitegemea Kanda ya Arusha amesema Ulemavu sio Sababu ya kushindwa kutekeleza majukumu yao Huku Rais wa chama hicho anaemaliza muda wake Fatma Karume akatoa neno kwa viongozi wajao.

Kwa upande wake Rais aliemaliza muda wake Fatma Karume amesema kuchaguliwa kwa Dkt Rugemeleza Nshala kuongoza chama hicho anaamini chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) iko Katika mikono salama.

Katika hatua nyengine bi Fatma Karume ametumia fursa hiyo kuwashukuru wanachama waliompa dhamana ya kuongoza kwa kipindi alicho kuwa madarakani hivyo ni wakati muafaka kwa wanasheria kumpa ushirikiano chanya Rais Mpya wa TLS.

Matokeo ya uchaguzi huo yametoka kutangazwa jioni ambao Katika Nafasi ya wagombea urais ilikuwa ikigombewa na Godfrey wasong, Gaspar Nicodemas,Godwin Simba,Rugemeleza Nshala na John seka ambapo Dkt Rugemeleza Nshala ameobuka kidedea.


MATOKEO YA RAIS 2019/2020 (TLS)

Jumala ya Kura zilizo poigwa na wanachama wa TLS Ni 1217.

1-Dkt Rugemeleza Nshala kura 647.
2-Godwin Simba kura 354
3-Godfrey Wasonga kura 123
4-58 Gaspar Nicodemas kura 58
5-John Seka kura 29

RAIS DKT. MAGUFULI NA MKEWE MAMA JANETH MAGUFULI WASALI IBADA YA JUMAPILI MKOANI RUVUMA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika ibada ya dominika ya 5 ya Kwaresma katika Parokia ya Mt. Mathias Mulumba Jimbo Kuu Katoliki la Songea mkoani Ruvuma.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika ibada ya dominika ya 5 ya Kwaresma katika Parokia ya Mt. Mathias Mulumba Jimbo Kuu Katoliki la Songea mkoani Ruvuma.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Mathias Mulumba Jimbo Kuu Katoliki la Songea mkoani Ruvuma mara baada ya kuwachangia shilingi milioni tano  kwa ajili ya ukarabati wa Kanisa hilo. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli wakisalimiana na Masista wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Mathias Mulumba Jimbo Kuu Katoliki la Songea mkoani Ruvuma mara baada ya Ibada ya dominika ya 5 ya Kwaresma. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono waumini wa wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Mathias Mulumba Kalemba Jimbo Kuu Katoliki la Songea mkoani Ruvuma mara baada ya ibada.PICHA NA IKULU



MAPUNDA AHAMASISHA WENYE BAA KUUNDA TIMU BORA ZITAKAZOWAKILISHA KWENYE FAINALI YA BONANZA KUBWA LA CASTLE LAGER AFRICA 5s 2019

$
0
0
BALOZI wa Castle Lager Africa 5s nchini Tanzania, Ivo Mapunda amewaomba wamiliki wa Baa kuunda timu bora za kiushindani zitakazowakilisha Baa zao kwenye fainali ya Bonanza kubwa litakayoshirikisha timu 32 kutoka Baa tofauti za jijini Dar es Salaam na kupata timu moja itakayowakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania mwaka huu wa 2019.
 Mapunda aliyasema hayo jana kwa Waandishi wa habari wakati akijiandaa rasmi na ziara ya kutembelea Baa 60 za jijini Dar es Salaam zilizoingia kwenye mchakato wa kiushindani kupitia promosheni zinazoendelea kwenye Baa hizo na kuwaomba wamiliki hao wajitahidi sana kuunda timu bora kwani tunatarajia kuwa na ushindani mkubwa ambao mwisho wa siku utatupatia timu moja kutoka Baa moja itakayotuwakilisha Watanzani kwenye mashindano ya Africa.
Mashindano haya yanafanyika hapa nchini kwa mara ya kwanza lakini ikiwa ni mara ya pili kwa Tanzania kushiriki chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia nhini(TBL) kupitia bia yake ya Castle Lager. Hata hivyo yamekuwa yakifanyika katika nchi nyingine za Afrika hivyo kwa fursa tuliyopewa Watanzania ya fainali za Africa kufanyika Tanzania nawasihi wamiliki wa Baa shiriki tutambue Bingwa wa fainali ya Bonanza atatuwakilisha Watanzania wote na kwa maana hiyo uundaji wa timu zetu na maandalizi kwa ujumla yanapaswa kuwa mazuri, ‘alisema Balozi wa Castle Lager Tanzania,Mapunda’.
“Mwaka jana tulishiriki mashindano haya kwa mara ya kwanza na kupata mwakilishi aliyeshiriki katika michuano ya Kimataifa ya Afrika, yaliyofanyika nchini Zambia kwa kuzikutanisha timu za Afrika Kusini, Zimbabwe, Swaziland Lesotho na wenyeji Zambia”.  
Binafsi niwapongeza sana Wadhamini wa mashindano haya Castle Lager kwa kudhamini mashindano haya ambayo yanawapa fursa wanywaji wao kushiriki michezo ambayo mwisho wa siku unatupa nafasi ya kuitangaza nchi yetu ya Tanzania lakini pia niwashukuru sana kwa kuniona mimi kama nastahili kuwa Balozi wa Castle Lager Africa 5s nchini Tanzania. 
 “Nafahamu Mchakato wa kupata timu zitakazoshiriki katika bonanza hilo umeboreshwa zaidi mwaka huu, ambapo washiriki watapatikana kupitia katika promosheni zinazoendelea katika baa mbalimbali jijini Dar es Salaam”.
Ili kuingia 32 bora, moja ya kigezo muhimu ni kufanya mauzo mengi ambapo kutakuwa na makasha maalumu katika baa husika kwa ajili ya kukusanyia vizibo baada ya mteja kununua bia ya Castle Lager. 
Niwaombe watanzania kutumia nafasi hii, ambayo itawapa wakati mzuri wa kutimiza ndoto zao. Wakati mwingine fursa kama hizi ni nadra sana.
 Baadhi ya Wachezaji wa Baa ya Toroka Uje yenye makazi yake Kinondoni jijini Dar es Salaam wakishangilia mara maada ya kumaliza mchakato wa kuhesabiwa kura zao kupitia vizibo vya Bia ya Castle Lager ili kushiriki Bonanza kubwa la Castle Lager Africa 5s linalotarajiwa kufanyika Leaders hivi karibuni.
Baadhi ya Wahudumu wa Baa ya Toroka Uje wakihesabu yenye makazi yake Kinondoni jijini Dar es Salaam wakihesabu kura kupitia visibo vya Bia ya Castle Lager ili kushiriki Bonanza kubwa la Castle Lager Africa 5s linalotarajiwa kufanyika Leaders hivi karibuni.
 Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli akimkabidhi Balozi wa Castle Lager Africa 5s, Ivo Mapunda mpira wa miguu kuashiria uzinduzi wa mashindayo Castle Lager Africa 5s(ya wachezaji watano watano) yanayotarajiwa kufanyika Nchini mwaka huu wa 2019.
 Balozi wa Castle Lager Africa 5s, Ivo Mapunda

Klabu 10 kuwania ubingwa wa taifa wa kuogelea

$
0
0
Dar es Salaam. Jumla ya klabu 10 zimethibitisha kushindana katika mashindano ya klabu bingwa ya mchezo wa kuogelea yaliyopangwa kufanyika kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), Upanga jijini Dar es Salaam.

Mashindano hayo yamepangwa kufanyika Aprili 13 na 14 na yamedhaminiwa na kampuni za Asas, Samsung, DTB Bank, Snow Cream, Knight Support na kituo cha utangazaji cha Clouds FM.

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Hadija Shebe amezitaja klabu hiyo kuwa ni Bluefins, Champion Rise, Mis Piranhas, klabu ya kuogelea ya Mwanza (MSC), FK Blue na Wahoo ya Zanzibar.

Hadija amezitaja klabu nyingine kuwa ni ISM-Moshi, ISM-Arusha,FK Blue Marlins, Talis-IST na mabingwa watetezi, Dar es Salaam Swim Club (DSC).

Alisema kuwa mashindano hayo yamepangwa kuanza saa 2.00 asubuhi siku ya Jumamosi na waogeleaji watashindana katika staili tano ambazo ni Freestyle, Breaststroke, Butterfly, Backstroke na Individual Medley.

Kwa mujibu wa Hadija, waogeleaji hao pia watashindana katika relay katika mashindano ambayo yamepitishwa na Shirikisho la Mchezo wa kuogelea Duniani (Fina) kuwa ya kutafuta alama za kufuzu mashindano ya Dunia yaliyopangwa kufanyika nchini Korea mwezi Julai.

“Tunatarajia kuona ushindania mkali kwa waogeleaji wetu ili kutafuta nafasi ya kufuzu mashindano ya dunia. Waogeleaji wengi wapo katika maandalizi ya mwisho mwisho kwa ajili ya mashindano hayo, bado tunahitaji wadhamini wa mashindano haya,” alisema Hadija.

Kwa mujibu wa Hadija, kutakuwa na jumla ya vipengele vya mashindano 108 na kila klabu imetakiwa kuwakilishwa na waogeleaji wawili katika kila kipengele cha mashindano ambavyo pia vimepangwa kutokana na umri. “Zaidi ya waogeleaji 200 watashiriki katika mashindano haya makubwa ya Tanzania. Tunaomba wadau wajitokeze kusaidia na kuwapa hamasa waogeleaji wetu ambao kwa sasa wamepata mafanikio makubwa katika mashindano mbalimbali ya kimataifa,” alisema.
 waogealeaji waki-dive katika mashindano ya kuogelea
 waogeleaji wakichuana
  Natalia Ladha akipiga mbizi

MWANAHABARI SHABANI NDYAMUKAMA ALIVYOPUMZISHWA KWAO KAGOMA,MKOANI KAGERA

$
0
0
Hatimaye Safari ya Mwisho ya Mwanahabari wa Vyombo mbalimbali, na Mwalimu Shabani Ndyamukama wa Shule ya Msingi Buhororo ikaishia hapa, ambapo mwili wake umepumzishwa Mnamo Tarehe 6 April 2019 majira ya saa mbili usiku.
 Mtoto wa kwanza wa  marehemu Shaabani, anaitwa Hussein Shaabani Ndyamukama, ambae amepatwa na tatizo la kiafya, jambo ambalo inasemekana kwa kiasi kikubwa limepelekea kifo cha Baba yake kutokana na msongo wa mawazo alokuwa nao.
 Nyumbani kwao na Marehemu Shabani Ndyamukama kijiji Kagoma Wilayani Muleba kusini alipozikwa.
 Mapema Jamaa na marafiki wanaonekana wakifaya maandalizi ya mwisho ya Kaburi kabla ya Kumsitiri marehemu Shabani Ndyamukama.
 Pichani ni mke wa marehemu Shabani, Bi. Hadija S. Ruzamba (aliyebeba mtoto) akifarijiwa na mmoja kati ya waombolezaji
 Sehemu ya Waombolezaji wakimlilia marehemu, Mara baada ya Mwili wake kuwasili kijijini Kagoma - Muleba, nyumbani kwao alipozikwa marehemu.
 Gari lililobeba mwili wa marehemu Shabani kutoka Mwanza alipokwenda kuhudhuria semina na mafunzo kwa Wanahabari, ambapo mauti yalimkuta huko.
 Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini, Bi. Anna Tibaijuka akiwasilisha ubani kwa mjane wa marehemu kwa niaba yake.
 Mwakilishi wa Chama cha Walimu wilaya ya Ngara ambapo marehemu Kituo chake cha kazi kilikuwa huko, akiwasilisha Ubani wao.
 Pichani Jeneza lenye mwili wa Marehemu Shabani Ndyamukama  likiwa limebebwa  kuelekea makaburini.
 Swala ya Jeneza ikiendelea kabla ya kumpuzisha marehemu Shabani Ndyamukama

BURIANI MWANAHABARI SHABANI NASSIB NDYAMUKAMA

$
0
0
Aliyekuwa Mwalimu Wa Shule ya Msingi Buhororo iliyopo Wilayani Ngara, Mkoani Kagera na Mwanahabari Marehemu Shabani Ndyamukama, amezikwa kwao Kijiji Kagoma Wilayani Muleba Jana Aprili 6, 2019. 

Marehemu Shabani (49) ambaye mpaka umauti unamkuta mbali na Taaluma yake ya Ualimu, alitambulika zaidi kama mwanahabari huku akiripotia Vyombo mbali mbali vikiwemo Redio, Magazeti na Globu za kijamii kazi aliyoifanya kwa umakini na ustadi Mkubwa. Mwanahabari huyu mbali na kile kinachosemwa kuwa kifo chake kimesababishwa na Shinikizo la damu, siku za hivi karibuni alikaririwa akiwa ameandika katika moja ya mitandao ya kijamii kuhusu maradhi yake yaliyokuwa yakimsumbua kubwa akitaja Msongo Wa mawazo uliosababishwa na kuugua kwa baadhi ya jamaa Wa karibu yake. 

 Hadi mauti yanamkuta Marehemu Shabani alizidiwa ghafla akiwa Jijini Mwanza katika Semina na Mafunzo kwa wanahabari ambapo Juhudi za kumpeleka hospitali zilifanyika na bahati mbaya akaaga Dunia. Marehemu ameacha mjane na watoto wanne wote Wa kiume.
 Shabani Ndyamukama, enzi za uhai wake

TRC KUENDELEA KUTOA ELIMU YA USALAMA UENDESHAJI WA SHUGULI ZA RELI KWA WAFANYAKAZI WA RELI.

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania TRC  afungua mkutano wa mafunzo ya usalama katika uendeshaji wa shughuli za reli Kwa wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania katika ukumbi wa mikutano wa bandari jijini Dar es Salaam.

 Lengo la mafunzo hayo ni kuwakumbusha wafanyakazi wa reli kuimalisha ulinzi Na usalama wa binadamu Na miundombinu ya reli Kwa kutoa elimu ya usalama katika shughuli za uendeshaji wa reli Kwa madereva, wakaguzi wa reli, wahandisi mawasiliano, wahandisi mitambo, walinzi Na wabadilisha njia za reli.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu Ndugu Kadogosa amesisitiza usalama wa reli unagusa maisha ya watu na kila mmoja ndani ya shirika Anawajibu wa kusimamia sheria Na kanuni zilizowekwa katika uendeshaji wa treni ili kuokoa maisha ya watanzania Na kutunza miundombinu ya reli,Aliendelea kusisitiza Mkurugenzi.

" tunaendelea Na ukarabati wa reli ya zamani kutoka Dar es Salaam Mpaka Isaka, tunategemea ndani ya mwaka mmoja ujao tutakuwa Na reli nzuri sana maana yake tusipokuwa Na umakini wa usalama tunaweza kusababisha ajari zikaongezeka Na Uharibifu kuwa mkubwa,"


Kwa upande wake kaimu mkuu wa kitengo cha usalama wa reli TRC Mhandisi Adolphina Ndyetabula amefafanua kuwepo Kwa elimu ya usalama ambayo hutolewa wa Shirika na wakazi wanaoishi maeneo ya reli ili kuzingatia swala Zima la usalama wao na miundombinu ya reli.
Mkurugenzi Mkuu shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kungu Kadogosa akitoa maelezo kwa wafanyakazi wa TRC kipindi cha ufunguzi wa mafunzo ya usalama katika uendeshaji wa shuguli za Reli katika ukumbi wa bandari hivi karibuni Aprili.

SHONZA AMVALISHA MEDALI YA DHAHABU MSHINDI WA RIADHA YA SOKOINE MEMORIAL MARATHON JIJINI ARUSHA

$
0
0
Naibu Waziri Wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akimvalisha Medali ya dhahabu mshindi namba  Moja Wa mbio za kilometa tano kwa upande Wa wanawake katika mashindano ya riadha ya Sokoine Memorial  Marathon yaliyofanyika Aprili  06,2019 Jijini Arusha

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA MBINGA-MBAMBA BAY KM 67 WILAYANI MBINGA MKOANI RUVUMA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Mbinga mjini mpaka Mbamba Bay km 67, sherehe zilizofanyika Mbinga mkoani Ruvuma. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Alex Mubiru akishuhudia
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akikata utepe pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Alex Mubiru wa pili kutoka kushoto , Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Godfrey Zambi watatu kutoka kulia, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Arch. Elius Mwakalinga wapili kutoka kulia, Mwalikishi wa Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Chrisianus Ako wa kwanza kulia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Alex Mubiru wa kwanza kulia aliyekaa wakiwa katika picha ya pamoja na wakandarasi wa ujenzi wa barabara ya Mbinga mjini mpaka Mbamba Bay km 67, wafanyakazi, wasimamizi pamoja na viongozi wengine.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa kwa wafuraha na wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Mbinga mjini kabla ya kuwahutubia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi(Albinism ) wanaosoma Shule ya St. William iliyopo Mbinga mkoani Ruvuma. Rais Dkt. Magufuli amewachangia watoto hao kiasi cha Shilingi milioni tatu.
 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi pamoja na Wanafunzi wa Shule mbalimbali za eneo la Kigonsera (hawaonekani pichani) Mbinga mkoani Ruvuma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi wa Liganga wakati akiwa njiani kuelekea Mbinga mkoani Ruvuma. PICHA NA IKULU

Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images