Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

BABA ADAIWA KUMNYONGA MWANAE HADI KUFARIKI DUNIA, AKIDAI SIO MTOTO WAKE

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha 

JESHI la polisi mkoani Pwani linamshikilia Robison Enerst (33) fundi ujenzi kwa tuhuma ya kumnyonga shingo,  mwanae Modesta Robison mwezi umri wa miezi sita, akidai sio mtoto wake. 

Kamanda wa polisi mkoani hapo, ACP Wankyo Nyigesa, alieleza kwamba, tukio hilo limetokea April mosi, mwaka huu  huko mtaa wa Vitendo kata ya Misugusugu ,Kibaha. 

"Kabla ya kuolewa na mtuhumiwa, mama wa mtoto (marehemu)  alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine ambae mtuhumiwa anamtuhumu ndio baba halali wa mtoto ""Hali hiyo ilisababisha migogoro ya mara kwa mara kati ya wazazi hao "alifafanua Wankyo. 

Wankyo alibainisha, wamemkamata mtuhumiwa ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria na mwili wa marehemu umehifadhiwa hospital ya rufaa ya mkoa ya Tumbi, kabla ya kukabidhiwa ndugu kwa mazishi. 

Kamanda huyo alitoa rai kwa wananchi, kuwa wanapokuwa na mashaka na jambo fulani la kihalifu watoe taarifa mapema katika vituo vya polisi ili yaweze kushughulikiwa mara moja kabla ya kuleta madhara yeyote kwa lengo la kudhibiti watuhumiwa. 

Hata hivyo, baada ya kumhoji mama wa marehemu yeye alidai mtuhumiwa alishafanya majaribio ya mtuhumiwa kumuua marehemu mwanae mara mbili.  Anaeleza, mara ya kwanza alitaka kumpa sumu ya vidonge lakini mama huyo aliwahi kumuokoa .

"Mara ya pili mtuhumiwa alinoa panga ili amkate mtoto lakini hakufanikiwa pia kufikia april 1, ambapo alimuua mtoto kwa kumnyonga shingo hadi kufariki dunia "

Serikali kuwashtaki wanaohujumu Miradi

$
0
0
Serikali imetoa  onyo kwa  wafanyabiashara au mtu yoyote  mwenye nia  ya kuhujumu Miradi ya Serikali kwa maslahi binafsi kuacha mara moja na endapo mtu  atathibitika kuhusika na suala hilo sheria kali zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni  leo alipotembelea Kiwanda na  Shamba la Miwa katika Gereza la  Mbigiri  ambalo linakadiriwa kuzalisha tani za sukari Laki Mbili  kwa Mwaka na kuondoa adha ya kuagiza sukari nje ya nchi.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kukuza viwanda mbalimbali ikiwemo kiwanda cha Sukari Mbigiri na kuwezesha mamia ya wananchi kupata ajira pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

“Kuna taarifa za baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wa sukari kupenyeza maslahi yao binafsi katika miradi hii mikubwa ya serikali ikiwemo shamba hili la miwa hapa Mbigiri, nawaasa waache mara moja kwani watakapobainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu yao ikiwemo na kosa la uhujumu uchumi” alisema Masauni

Akitoa taarifa ya shamba hilo Mkuu wa Gereza Mbigiri, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Shija Fungwe alisema shughuli zinaendelea katika shamba hilo kwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa kutoka katika gereza hilo huku wafungwa 280 wakitumika katika shamba hilo.

“Kazi ya kupanda eneo lililo tayari inaendelea huku kazi ya kulima hekta 500 inaendelea na kati ya hizo hekta 200 zimeshalimwa kwa awali na lengo letu ikifika mwezi juni mwaka huu inatakiwa zilimwe hekta 700 tukitumia nguvu kazi ya wafungwa” Alisema ACP Fungwe

Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameelekeza  kubadilishwa  kwa Mjumbe wa Bodi ya Kiwanda hicho, ACP Rocky Mbena  anaewakilisha Jeshi la Magereza.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akiwasili katika eneo la Kiwanda na  Shamba la Miwa Mbigiri linalohudumiwa na Gereza la Mbigiri wakati wa ziara ya kutembelea mradi huo   mkoani Morogoro.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto), akisikiliza maelezo yanayohusu maendeleo ya Shamba la Miwa Mbigiri linalohudumiwa na Gereza la Mbigiri wakati wa ziara ya kutembelea mradi huo  mkoani Morogoro.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

KUONDOLEWA KWA VAT KWENYE TAULO ZA KIKE KWAPONGEZWA

$
0
0

I4ID kwa kushirikiana na Taasisi binafsi ambao ni wabia wake walishiriki kwenye Maonyesho ya ubunifu yaliyofanyika kuanzia tarehe 25 mpaka 29 Mwezi March 2019 COSTECH BUILDING,Sayansi kijitonyama,Dar es salaam.
Wabia wa I4ID wakizungumzia katika maonesho hayo walishukuru serikali kuondoa tozo ya ushuru (VAT) katika soko la bidhaa za taulo za kike,wabiahaowalioshiriki katika maoneshohayo ni kama ANUFLO (Hedhicup),ELEA,GLORYPADS pamoja na BINTI FOUNDATION.
Kwa upandewa mabaloziwa hedhisalama/hedhi salama inatuhusu Wasanii JB na Wastara alishiriki kikamilifu katika kuelimisha umma katika maonesho hayo.


ROMAN MNG'ANDE 'ROMARIO' MWENYE VIMBWANGA

$
0
0
Na Moshy Kiyungi
Kila onyesho la bendi ya Msondo hufikia kipindi mtu akijikuta akicheka kufuatia vimbwanga vya mpulizaji wa tarumbeta Roman Mng’ande ‘Romario’ Hujituma kwa kucheza na tarumbeta huku akilitumia umbo lake fupi lililojaa minofu, kuwapagaisha watu ukumbini, vimemfanya kuwa maarufu miongoni mwa wasanii wa bendi ya Msondo Ngoma.

Majina yake kamili anaitwa Roman Mng'ande ambae ni mwanamuziki mwenye historia kubwa katika muziki hapa nchini. Umaarufu wa Romario haukuja hivi hivi bali ulitokana na mambo mbalimbali yakiwemo ya vituko, mavazi, unyoaji wake wa nywele wa aiana yake na vichekesho vingi anavyofanya akiwa kwenye kazi yake hiyo.


Msanii huyo, amevuma masikioni mwa mashabiki wengi hususan wapenzi wa muziki wa dansi hadi nje ya mipaka yetu hususan katika jiji la Nairobi ambako ni gumzo kutokana na mbwembwe zake. Licha ya kazi yake ya kupuliza tarumbeta, Romario hufanya mbwembwe lukuki zikiwemo za kuvuta kidevu chake chenye ‘mzuzu’ weye ndevu ndefu wakati akicheza jukwaani.

Aidha hufanya ‘rap’ kufokafoka huku akionesha jinsi ‘Msondo’ unavyochezwa akitumia umbo lake kubwa japo mfupi.

Mg’ande alipata elimu katika shule ya sekondari Kingurunyembe, huko Morogoro.

Alianza kuzungumzia historia yake kimuziki ambapo alisema alianza kujiingiza kwenye tasnia hiyo mwaka 1973,  akiwa katika kundi la Father Kanuti, mjini Morogoro aliyekuwa mwalimu mzuri wa ala za upepo.

Alisema akiwa kwenye kundi hilo, alianza kwa kupiga vyombo mbalimbali ikiwemo tarumbeta ambalo kwa sasa ana uzoefu nalo mkubwa.

Romario alisema katika kundi hilo, alidumu kwa miaka sita, mwaka 1979 alijiunga na bendi ya Urafiki Jazz iliyokuwa na masikani yake jijini Dar es Salaam.

Kilichomsukuma  yeye kujiunga na kundi la Urafiki Jazz, alisema kuwa alihitaji kukuza kipaji chake cha muziki na kujipatia ukomavu, chini ya uongozi wa bendi hiyo Juma Mrisho ‘Ngulimba wa Ngulimba.

Mng'ande, ambaye anasifika kwa vituko na tambo za kila aina, alisema katika kundi hilo hakuweza kudumu kwa muda mrefu kutokana na kuhitajika katika kundi la Tanzania Stars Magosi.

Alijinasibu kuwa mara kwa mara viongozi wa bendi hiyo, walikuwa wakimfuata ili aweze kujiunga nalo ili kuiongezea nguvu bendi hiyo.

Msanii huyu alisema mwaka 1981 uongozi wa Tanzania Stars Magosi, ulifanikiwa kumuhamisha kutoka bendi ya Urafiki, baada ya ‘kumpandia’ dau nono.

"Unajua sisi wasanii ni kama vile wachezaji mpira mtu akikupandia dau huwezi kuliacha, lazima umfuate...tunafanya muziki ili tupate hela sasa kama umepewa hela utaweza kuziacha….” Alisema kwa kujiamini Romario.

Aliongeza kwa kusema kuwa alipofuatwa na viongozi wa Tanzania Magosi hakuweza kukataa kwani aliangalia maslahi mbele mambo mengine baadae.

Mng’ande akiwa na bendi hiyo alifanikiwa kujiongezea umaarufu na kuanza kusikika masikioni mwa mashabiki wengi.

Hata hivyo Mng’ande alidumu katika bendi hiyo hadi mwaka 1983.

Sifa zake nzuri zilipelekea kufuatwa na viongozi wa bendi ya Juwata Jazz kipindi hicho sasa Msondo Ngoma, ili aende kujiunga na bendi hiyo.

“Viongozi wa Juwata walinitafuta na kumueleza dhamira yao ni kutaka nijiunge na bendi yao ambayo kipindi hicho ilikuwa tishio kwa bendi zingine hapa nchini” alisema Romario.

Mng’ande alisema baada ya kufuatwa na viongozi wa Juwata na kuonyesha nia ya kutaka kumchukua kwenye kundi hilo, hakufanya kosa na aliwaambia milango iko wazi.

"Lengo langu lilikuwa kuimba kwenye bendi kubwa kama Juwata, hivyo nilipofuatwa sikufanya kosa nikawaambia milango iko wazi waje tuzungumze. “alitamka Mng’ande.

Alisema mwaka 1983, akajiunga rasmi na bendi ya Juwata Jazz, wakati huo ikiwa na waimbaji mahiri akiwemo marehemu TX Moshi William, Joseph Maina, Athumani Momba, Suleiman Mbwembwe na kiongozi wa bendi hivi sasa Said Mabera na wengine wengi.

Mng'ande, alisema tokea kipindi hicho hadi sasa hajatoka kwenye bendi hiyo wala hafikirii kutoka mpaka atakapoamua kuachana na muziki.

"Kama nilirogwa basi viongozi wa Msondo walipata mganga, kwani tokea nilipojiunga na bendi hiyo hadi sasa sijatoka wala sifikirii kutoka hata iweje.

Akielezea juu  ya mafanikio aliyoyapata kupitia muziki, Romario alisema “Nimepata mafanikio makubwa nikiwa katika bendi hii na imenisaidia kufahamiana na watu wengi, viongozi wa serikali, kwa kweli nimepata mafanikio makubwa katika maisha yangu…”.

Alisema kuwa hawezi kusita kukiri kwamba bendi ya Msondo, imemtoa kimaisha, amemfanya kiwango chake cha muzimki kukua siku hadi siku, hatoweza kuisahau katika maisha yake yote.

Mng'ande, alisema hana mpango wa kuanzisha bendi na lengo lake ni kuzidi kujiimarisha katika kazi yake hiyo ili bendi yake ya Msondo Ngoma, iweze kufanya vyema zaidi.

Alisema katika maisha yake ya muziki hawezi kumsahau marehemu TX Moshi kwani alikuwa rafiki yake mkubwa na alikuwa akimshauri mambo mengi.
Romario, alisema wanamuziki wengine ambao hawezi kuwasahau ni pamoja na Said Mabera na Muhidin Maalim Gurumo.

Wimbo ambao hawezi kuusahau ni kibao cha “Isikutonza iyudi Chaum”, uliotungwa na marehemu Suleiman Mwanjiro na yeye alishiriki kwa kiasi kikubwa kupiga vyombo katika wimbo huo.

“Huo wimbo ukipigwa hata niwe wapi lazima nisimame kidogo niusikilize, naupenda sana kuliko wimbo mwingine, nilishirikishwa kuupiga…” Romario alijigamba.

Alisema albamu za Msondo ambazo hawezi kuzisahau ni pamoja na ‘Mwanaume tumeumbwa mateso’ na ‘Kilio cha mtu mzima’.

Romario mbali na kipaji cha kupuliza tarumbeta, amejaaliwa kipaji cha uimbaji ambapo mara nyingi ameonekana akiimba nyimbo mbalimbali.

Romario Mng'ande ni baba wa familia yenye mke na watoto wanne.

WATAALAMU 25 KUTOKA NCHI SITA ZA AFRIKA WAKUTANA KUSHIRIKI MAFUNZO YA ULINZI NA USALAMA WA VYANZO VYA MIONZI

$
0
0

Wataalamu 25 wa Ulinzi na Usalama wa vyanzo vya mionzi kutoka katika nchi sita za Afrika wanaoshiriki katika mafunzo ya wiki mbili ya jinsi ya kuendesha mafunzo ya ulinzi na usalama wa vyanzo vya mionz katika nchi zao wakiwa katika picha ya pamoja katika Makao Makuu ya Ofisi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) Jijini Arusha. Mafunzo hayo yanaendeshwa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania kwa ushirikiano na Jumuia ya Umoja wa Ulaya (EU).

Wataalamu wa Ulinzi na Usalama wa vyanzo vya mionzi kutoka katika nchi sita za Afrika wanashiriki katika mafunzo ya wiki mbili ya utoaji mafunzo ya ulinzi na usalama wa vyanzo vya mionzi yanaoendeshwa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa ushirikiano na Jumuia ya Umoja wa Ulaya (EU) 

Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano cha Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Peter Ngamilo amesema kuwa mafunzo hayo yanafanyika katika ofisi za Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania jijini Arusha na jumla ya washiriki 25 wanashiriki mafunzo hayo kwa kwa lengo la kupata ujuzi wa namna ya kufundisha wataalamu mbali mbali wanaohusika na ulinzi na usalama wa vyanzo vya mionzi katika nchi zao. 

Ngamilo amesema kuwa baada ya wakufunzi hao wa ulinzi na usalama wa vyanzo vya mionzi kumaliza mafunzo yao watakuwa na uwezo wa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wenzao wa idara mbalimbali za kitaifa katika nchi zao katika kuhakikisha kuwa vyanzo vya mionzi vinatumika katika njia zilizo salama na halali. 

“Wakufunzi hawa waliopo kwenye mafunzo wakitoka hapa watakuwa na uwezo wa kuandaa na kufanya mafunzo ya ulinzi na usalama wa vyanzo vya mionzi kwa wadau mbalimbali katika nchi zao, pia watatumika kama wataalamu katika kushughulikia matukio yoyote ya maafa ya vyanzo vya mionzi iwapo yatatokea katika nchi za bara la Afrika”alisema Ngamilo. 

Hata hivyo amesema kuwa vyanzo vya mionzi visipodhibitiwa vinaweza kutumika katika vitendo vya kigaidi na kuleta madhara makubwa kwa jamii na kuathiri shughuli za kimaendeleo na kiuchumi 

Na pia amesema kuwa wakufunzi hao wanajengewa uwezo wa kutoa mafunzo ya kubaini usafirishaji haramu wa vyanzo vya mionzi hasa kwa wataalamu wa mamlaka za ulinzi na usalama ikiwemo Polisi, Walinzi waliopo mipakani na wasimamizi wa Tekinolojia ya Nyuklia, maafisa forodha na wataalamu wa kupambana na majanga ya nyuklia. 

Amezitaja metaja nchi wanazotoka washiriki wa mafunzo hayo ni pamoja na Burundi, Uganda, Congo(DRC), Zambia,Ghana na wenyeji Tanzania. 

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UPANUZI WA UWANJA WA NDEGE WA MKOANI MTWARA

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Mbunge wa Mtwara Vijijini Hawa Ghasia pamoja na Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mtwara wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi la mradi wa Upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mtwara hafla iliyofanyika leo tarehe 2 Aprili 2019 mkoani humo. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakwanza kutoka kulia pamoja na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Ujenzi, Wabunge pamoja na viongozi wa mkoa, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mtwara.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la uwanja wa ndege wa Mtwara kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa upanuzi wa uwanja huo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi waliofika katika uwanja wa ndege wa Mtwara mara baada ya kuweka jiwe la Msingi la mradi wa Upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mtwara hafla iliyofanyika leo tarehe 2 Aprili 2019 mkoani humo. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa kushoto pamoja na  Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe kulia wakati Kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Mtwara na Dar es Salaam ilipoku wa ikitumbuiza uwanjani hapo. PICHA NA IKULU

TAARIFA KWA UMMA: USHIRIKI KATIKA MIKUTANO YA KIBIASHARA KWENYE MAONYESHO YA 43 YA SABASABA

DUA MAALUM YA KUWAOMBEA MASHUJAA YAFANYIKA MIGOMBANI ZANZIBAR

$
0
0
Na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar
Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Saleh Omar Kaabi amewaongoza Viongozi wa Serikali, Ndugu, Jamaa na Marafiki katika Dua maalum ya kuwaombea Viongozi mbali mbali wa Kitaifa waliotangulia mbele ya haki akiwemo Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi.

Dua hiyo ilianza kwa kisomo cha Khitma na kuzuru Kaburi lake huko nyumbani kwa Marehem Migombani nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Akitoa nasaha zake Mufti Kaabi amesema Marehem Aboud Jumbe alikuwa ni Mtu aliyependa mashirikiano katika kuliongoza Taifa kwa umahiri. Ame

sema Marehem pia alikuwa kiongozi muadilifu, aliyependa Wananchi wa Zanzibar washiriki kikamilifu katika kutafuta Elimu ndani na nje ya nchi ili kuendeleza maendeleo ya Zanzibar.

“Katika kupigania haki ya elimu kwa Wananchi Marehem alishajihisha wananchi kutafuta Nafasi za kusoma nje Skolaship na ndani ili kuhakikisha jamii inafaidika na fursa hizo” Alisema Shekh Kaabi

Katibu Mkuu wa Mufti sheikh Fadhil Soraga alisema iko haja kubwa ya kuwaombea dua viongozi kwani wamefanya mengi mazuri na yanaendelezwa hadi leo ikiwemo kushajihisha Wananchi kuishi kwa amani na utuluivu.

Amesema kuna umuhimu wa Viongozi waliopo madarakani kuyaendeleza kwa umakini mkubwa yote mazuri yaliyoasisiwa na viongozi hao kwa faida ya Kizazi cha sasa na baadae.

Awali Shekh Thabit Nooman Jongo kutoka Ofisi ya Mufti alisema lengo la dua hiyo ni kuwakumbuka viongozi wote walioshika nyadhifa mbali mbali za uongozi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambao kwa sasa wametangulia mbele ya haki ili Mwenyezi Mungu awasamehe makosa yao.

Alisema dhamira kubwa ya kuwaombea dua ni kuwakumbuka kwa yale waliyoyafanya katika nchi hii akiwemo Marehemu Rais Mstaafu Alhajj Aboud Jumbe Mwinyi kwa mambo mengi yaliyoyafanyika katika uongozi wake.

Miongoni mwa mambo aliyoyafanya wakati wa uhai wake ni pamoja na kuwaunganisha wananchi wote wa Unguja na Pemba na kuwa kitu kimoja ili kuendelea kuishi kwa amani na utulivu kama alivyotaka Marehemu Mzee Karume.

Ibada hiyo ya kuwaombe Dua Viongozi wa Kitaifa itaendelea katika maeneo tofauti ambapo itaendelea Chukwani kwa kumuombea marehemu Mzee Thabit Kombo, na kesho itasomwa Dua ya Marehemu Idrissa Abdulwakil huko Makunduchi.

Kwa upande wa Pemba Viongozi ndugu na Jamaa wa Marehemu watakusanyika kumuombea Waziri kiongozi mstaafu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt Omar Ali Juma huko kijijini kwao Wawi.

Dua hiyo itakuwa endelevu kila ikifika kumbu kumbu ya Mashujaa ambayo kilele chake hufanyika April saba Kisiwandui mjini Zanzibar
 Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi akiongoza Viongozi wa Serikali ndugu na Jamaa katika Dua maalum ya kuwaombea Mashujaa ambapo imeanza kwa aliekuwa Rais wa Zanzibar awamu ya Pili Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi hadi kufikia kilele chake siku ya 07/04/2019 Kisiwandui Zanzibar.
 Baadhi ya waheshimiwa na wananchi mbalimbali waliohudhuria katika Dua maalum ya kuwaombea Mashujaa ambapo imeanza kwa aliekuwa Rais wa Zanzibar awamu ya Pili Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi hadi kufikia kilele chake siku ya Mashujaa 07/04/2019 Kisiwandui Zanzibar.
Baadhi ya waheshimiwa na wananchi mbalimbali waliohudhuria katika Dua maalum ya kuwaombea Mashujaa ambapo imeanza kwa aliekuwa Rais wa Zanzibar awamu ya Pili Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi hadi kufikia kilele chake siku ya Mashujaa 07/04/2019 Kisiwandui Zanzibar, PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2019 MKOANI SONGWE

$
0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwasha Mwenge kuashiria kuzinduliwa kwa mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Mlowo mkoani Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mwenge kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa kwa mwaka 2019 Ndugu Mzee Mkongea Ali kutoka Mjini Magharibi kuashiria kuanza kwa mbio za Mwenge wa Uhuru 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MAHAKAMA YAWAHUKUMU WAWINDAJI SITA MIAKA 23 JELA KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

MAHAKAMA ya Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida imewahukumu wawindaji haramu sita kutumikia kifungo cha miaka 23 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa ya nyara za serikali ambazo ni vipande vinne vya meno ya tembo na magamba ya Kakakuona

Aidha Mahakama hiyo imeamuru pikipiki aina ya  Sanlg yenye namba za usajiliT 717 CPD  itaifishwe na kuwa Mali ya serikali.

 Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Stella Kiama ambaye amesema upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake sita na vielelezo wameweza kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka kuwa washtakiwa walitenda makosa hayo.

Vielelezo ni meno ya tembo, magamba ya kakakuona, pikipiki moja, nyaraka za kuchukulia mali, nyaraka za kuonyesha mwenendo wa vielelezo.
Washtakiwa waliohukumiwa kifungo hicho ni, Aloyce Abiniel, Jonas Chiata, Anton Magomba, Anderson Wami Matayo Rogan na George Joseph.

Akisoma Hukumu hiyo, Hakimu Kiama amesema katika shtaka la kukutwa na vipande vinne vya meno ya Tembo, washtakiwa wote wanahukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 gerezani  huku katika shtaka la kukutwa na magamba ya Kakakuona, linalomkabili mshtakiwa wa tano peke yake, amehukumiwa kutimikia kifungo cha miaka 20 gerezani.

 Aidha katika shtaka la tatu, washtakiwa wote hao wamehukumiwa kulipa faini ya sh. 135,542,880.00  na kama watashindwa basi watatumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani.

Washtakiwa hao kabla ya kusomewa adhabu walipewa nafasi ya kujitetea ambapo washtakiwa hawakuwa na chochote cha kusema isipokuwa Mshtakiwa wa Chiata kupitia wakili wake alisema yeye ni mkosaji wa kwanza na pia ana familia inayomtegemea mke na watoto na mke wake ni mgonjwa sana.

Katika kesi hiyo upande wa Jamuhuri uliwakilishwa na Wakili wa Serikali, Salimu Msemo, akisaidiana na  Petrida Muta na Tulumanywa Majigo. Na upande wa Utetezi mshtakiwa Chiata alikuwa akitetewa na wakili John Chigongo.

DOROTHY MASUKA, MWANAMAMA ALIYEPAMBANA NA VIKWAZO KATIKA MUZIKI

$
0
0
Na Moshy Kiyungi, Dar es Salaam

Aprili 2, 2019

Ili kufikia lengo tarajiwa, mtu anahitajika kutanguliza nia ya dhati bila kuogopa viwazo vinavyoweza kujitokeza ili kukukwamisha.

Katika makala haya yanamzungumzia mwanamama maarufu Dorothy Masuka ambae kama yu hai, basi ni bibi wa umri wa miaka 84 kwa sasa. Pasi shaka kutajwa kwa jina hilo nitawagusa wengi waliokuwa vijana wa miaka ya nyuma.

Masuka ni mwanamuziki aliyezaliwa katika mji wa Bulawayo, nchini   Zimbabwe (zamani South Rhodesia) mwaka 1935.

Baba yake alikuwa na asili ya Zambia wakati mama yake ni wa kabila la Zulu toka Afrika ya Kusini. Akiwa msichana mdogo wa miaka 12, familia yake ilihamia nchini Afrika ya Kusini, ambako kwa bahati nzuri alifanikiwa kuingizwa katika shule ya bweni ya Wakatoliki katika jiji la Johannesburg.

Kadri alivyokuwa akiendelea kukua, talanta yake ya uimbaji ilikubalika katika kipindi kifupi, akaanza kufanya matamasha ya shuleni kwake. Masuka alikuwa akihusudu sana na muziki wa Jazz ya Wamarekani pia muziki wa Kiafrika hususani wakati ambao mwanamuziki wa Kiafrika Dolly Rathebe, alipopata umaarufu mkubwa.

Kampuni iliyokuwa imeanzishwa ya kurekodi nyimbo ilikuwa na jina la Troubador, ilimwalika Dorothy kurekodi nyimbo ambazo ziliweza kufanikiwa. Hiyo ndiyo ilikuwa kengele ya mwazo ikiashiria kufikia mafanikio aliyokuwa akiyapenda.

Masuka wakati fulani akiwa na umri wa miaka 16, alikataliwa kuingia shule ya bweni hivyo akalazimika kwenda mjini Durban, nchini Afrika ya Kusini ambako alijiunga katika shule iliyojulikana kwa majina ya African Ink Spots, ikimilikiwa na  Philemon Mogotsi.

Licha ya uongozi wa shule na pamoja na familia yake kumtaka kubakia katika shule hiyo, yeye aliamua kurudi tena Bulawayo, nchini Zimbabwe. Alipofika huko wawezeshaji pamoja na Kampuni ya kurekodi walimuwezesha kufikia adhma yake ya uimbaji.

Wakati akiwa safarini akirudi  Johannesburg, Masuka alitunga wimbo ukapewa jina la 'Hamba Notsokolo'.

Alipotimiza umri wa miaka 20, picha zake zilianza kuonekana juu ya majarida mbalimbali. Aidha alipata fursa ya kutalii na kushiriki onesho nchini Afrika ya Kusini, likiwajumuisha wanamuziki wakubwa toka Afrika. Katika onesho hilo aliweza kukutana na wanamuziki wakubwa akiwemo Miriam Makeba, bendi maarufu ya African Jazz na nyingine nyingi.

Makeba alimtaja Dorothy na kumuimba katika wimbo wake wa 'Kulala' wakati wa onesho lake  lililorekodiwa katika album. Hata hivyo mwanamuziki mwingine toka Afrika ya Kusini Aura Msimang, pia aliuimba wimbo huo. Baadhi ya nyimbo zake zilizokuwa na ujumbe mkali, ambazo mamlaka husika ilizilizuia zisichezwe.

Dorothy Masuka alikuwa katika mji wa  Bulawayo mwaka 1961, wakati ambapo alinyang’anywa kwa nguvu moja wa nyimbo zake alizorekodi. Baadae alishauriwa kutorudi mjini humo hadi atakapohakikishiwa usalama wake.

Mnamo mwaka 1965 Dorothy aliwahi kuwa mkimbizi na kufanya kazi katika nchi za Malawi na hapa nchini Tanzania. Mwaka huohuo alirejea tena katika mji wa Bulawayo, nchini Zimbabwe. 

Hakuchukuwa kipindi kirefu akatoroka tena na akurudi nchini humo hadi pale nchi hiyo ya Zimbabwe ilipoundwa mwaka 1980. Dorothy Masuka alirekodi album iliyotikisa ulimwengu ya ‘Pata Pata’ mwaka 1990.

Baadae alirudi tena katika mji aliokuwa akiupenda mno wa Johannesburg, ambako lirekodi album nyingine ya Magumede.

Mwaka 2001 album yake Mzilikazi ilirekodiwa. Mwanamama huyo bado huweza kusafiri na kucheza muziki sehemu mbalimbali duniani.

Aidha alitembelea miji wa London na mwaka 2002, alikuwa katika jiji la New York nchini Marekani ambako aliungana kupiga muziki jukwaa moja na kundi la Mahotella Queens.

Desemba 2002, Dorothy alifanya onesho huko London kwa nia ya kuitangaza CD yake mpya ya ‘The Definitive Collection’

Mwisho.

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa namba 0784331200, 0713331200, 0736331200 na 0767331200.

FUVU LA KICHWA CHA MWANAFUNZI SCOLASTICA ANAYESADIKIWA KUUAWA LILIVUNJIKA-SHAHIDI

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.


SHAHIDI wa kwanza katika shauri la mauaji ya kukusudia namba (CC  48/2018) ,Dkt Alex Mremi ameieleza Mahakama kuu Kanda ya Moshi kuwa  wakati wa uchunguzi wa mwili wa Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Scolastika  Humphrey Makundi walibaini uwepo wa jeraha kubwa katika paji la uso na alivunjika fuvu la kichwa.


Mbele ya  Jaji  mfawidhi  wa mahakama kuu ,Divisheni  ya rushwa  na uhujumu Uchumi Dar es salaam ,Firmin Matogolo ,shahidi huyo ambaye ni Daktari Bingwa na Mkuu wa kitengo cha Patholojia alieleza kuwa  katika uchunguzi  huo pia walibaini jeraha kubwa lililokuwa kwenye paji la uso lilisababishwa na kupigwa na kitu kizito kisicho na ncha.


Akiongozwa na  Wakili Mkuu wa serikali,Joseph Pande  anayewakilisha upande wa Jamhuri  ,Dkt Mremi ambaye ni Daktari Bingwa na mkuu wa kitengo cha Patholojia ,Hoapstali ya Rufaa ya KCMC alieleza kuwa ukubwa wa jeraha lilolkuwa katika Paji la uso lilikuwa na ukubwa wa sentimita 6 kwa 5.


“Katika uchunguzi tulibini mwili wa marehemu ulikuwa na Nguo,T shirt ,Bukta pamoja na sox na lengo la uchunguzi huu lilikuwa ni kubaini chanzo cha kifo cha marehemu na tulibaini ni uwepo wa jeraha kiasi cha kuvunja mfupa,kitaalamu ni jeraha hilo ndio lilisababisha umauti”alieleza Dkt Mremi.


Dkt Mremi ambaye pia ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Tumaini  aliieleza mahakama kuwa mwili waliyofanyia uchunguzi ulikuwa ni wa mtoto mwenye umri kati ya miaka 15 na 17 huku akieleza sababu zilizopelekea kutambua hilo ni kutokana na muonekano wa meno.


“Meno yanaota kulingana na umri ,tulichobaini marehemu meno ya mwisho “Magego” yalikuwa bado yako chini hayajaota na alikuwa na majeraha mengine yalikuwa mabegani,Mgongoni na mapajani haya hayakuwa makubwa ukilinganisha na lile la kwenye paji lauso”alieleza Dkt Mremi.


Alieleza kuwa yapo maswali waliyojiuliza moja wapo ni kuwa marehemu alihusiana na nani,ndipo wakachukua sampuli katika maeneo ya mwili wa marehemu ili kubaini vinasaba (DNA) huku akitaja maeneo hayo kuwa ni mifupa kwenye mapaja,Mbavu na nyama kutoka sehemu za siri na kwenye makalio.


Akieleza sababu za kuchukua sampuli katika maeneo mbalmbali ya mwili ,Dkt Mremi alieleza kuwa kutokana na mwili kuanza kuharibika walilazimika kuchukua maeneo hayo ili kurahisisha usomaji wa vinasaba(DNA).


“Kwenye Jeraha tulichukua kipnde cha mfupa n nyama nyama kwenye maeneo yenye mchubuko ili kupata tissue zitakazo saidia kuangalia kwa ukaribu kitaalamu tunaita Histopathology ,kutizama kwa undani zaidi ya macho ya kawaida”alieleza Dkt Mremi.


Dkt Mremi alieleza kuwa uchunguzi huo husaidia kubaini jeraha lililokuwepo katika mwili wa marehemu huyo kama ni limekuwepo kabla ya kifo ama baada ya kifo na kwamba kilichoonekana majeraha hayo marehemu aliyapata wakati bado akiwa Hai.


“Tulichukua pia Sampuli ya meno na vipimo vya Damu kwa wazazi wa marehemu ,ambapo pia tulichukua sampuli ya ute wa mate na hizi tulichukua kwa mtu aliyetambulishwa kwentu kama baba wa marehemu ,aliyetambulishwa kwa jina la Jackson Makundi na mama Makundi.”alieleza Dkt Mremi.


Alieleza kuwa baada ya kukamilisha taratibu zote za kiuchunguzi walikabidhi mwili wa marehemu kwa ndugu na kisha kuandaa taarifa ambayo ilitiwa saini na madaktari wote walioshiriki katika uchunguzi huo uliofanyika katika chuma cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya KCMC.


Kuhusu kilichoandikwa katika ripoti hiyo Dkt Mremi alieleza kuwa kulikuwa na maelezo ya kile kilichobainika katika uchunguzi wao ikiwemo jeraha kubwa katika paji la uso linalotajwa kuwa sababu kubwa ya kifo pamoja na michubuko na kuiomba Mahakam kuipokea kama kielelezo katika shauri hilo.


Upande wa utetezi katik a shauri hilo linalovuta hisia za watu ,wakili David Shiratu ktika maswali kwa shahidi alitka kujua kwa nini katika uchunguzi huo hawakutumia kifaa maalumu cha Carbon 14 ili kujua umri sahihi wa marehemu .


“Mlikadiria umri wa marehmu ni kati ya miak 15 na 17 ,ni kwa nini hamkutaka kutumia Carbon 14 ili kujua umri wa mwili mliokuwa mnauchunguza”aliuliza Shiratu .


Akijibu swali hilo Dkt Mremi alieleza mahaka kuwa zipo njia nyingi za kubaini umri na njia waliyotumia ilikuwa ni mojawapo  huku akileza kuwa matumizi ya Carbon 14 yangeongeza gharama na kwamba hawakuhitaji njia ngumu kupata Vinasaba.


Shauri la mauaji  ya mwanafunzi  Humphrey Makundi aliyekuwa akisoma kiato cha pili katika  sekondari ya Scolastika imeanza kusikilizwa mfululuzo  likimkabili mmiliki wa shule hiyo ,Edward Shayo,Mwalimu wa nidhamu Labani  Nabiswa  na mlinzi wa shule ,Hamis Chacha.


Wakati wa usikilizwaji wa awali Agosti 27 2018 mbele  ya jaji Haruna Songoro ,upande wa mashtaka  ukiongozwa  wakili wa serikali mkuu Joseph  Pande,ulieleza utaita  mashahidi 34 katika kesi hiyo.


Pia,Pande aliijulisha mahakama kuwa  kuwasilisha vieelelezo vya nyaraka 15 yakiwamo maelezo ya kukiri kosa ya mshtakiwa  Chacha  akiwa polisi na kwa mlinzi wa amani.


Mbali na nyaraka hizo ,watawasilisha taarifa  ya mawasiliano  ya simu kutoka kampuni ya Vodacom inayodaiwa kuonyesha  washtakiwa waliwasiliana muda na siku ya mauaji.


Mbali na vielelezo hivyo ,upande  huo wa mashtaka  ulieleza mahakama   kiuwa utawasilisha vielelezo halisi (physical or real) ambavyo ni simu saba ,panga moja na nguo za marehemu.


Kwa upande wa mawakili wa utetezi,wao waliiambia Mahakama  kuwa orodha ya mashahidi wao  pamoja na vielelezo  watakavyotumia ,wataviwasilisha kabla ya washtakiwa kuanza kujitetea.


Mwanafunzi huyo alitoweka shuleni mnamo Novemba 6,2017 na baadaye kubainika ameuawa  na watu wasiojulikana baada ya maiti ya mtu aliedaiwa ni mtu mzima mwenye  ndevu ,kufukuliwa kwa amri ya mahakama.


Mwili wa mtoto huyo uliokotwqa Novemba 10,2017 katika mto Ghona mita 300 kutoka  shuleni hapo ,polisi waliuchukua  waliupeleka Hospitali ya Mawenzi na kuzikwa kwa madai haukutambuliwa .kwakuwa mwili huo ulishaanza kuoza na ulikuwa haujatambuliwa ,ulizikwa siku iliyofuata  ya Novemba 11 na Manispaa ya Moshi  katika makaburi ya kranga  yaliopo mjini hapa.


 Upande wa Jamhuri katika Shauri hilo unawakilishwa na Wakili wa serikali Mkuu ,Joseph Pande,Wakili wa serikali Mwandamizi ,Abdala Chavula,Wakili wa serikali Mwandamizi ,Omary Kibwana  na Wakili wa serikali Lucy Kiusa.


Upande wa utetezi unawakilishwa na Wakili wa kujitegemea Elikunda Kipoko na Gwakisa Sambo wanaomtetea  mshtakiwa wa pili ,Wakili wa kijitegemea David Shilatu anayemtetea mshitakiwa wa kwanza na Patrick Paul anaye mtetea mshtakiwa wa tatu.
Washtakiwa katika shtaka la Mauaji ya Mwananfunzi wa Shule ya Sekondari ya Scolastica ,Humphrey MAkundi ,aliyebeba chupa ya maji ni Hamisi Chacha ,Laban Nabiswa (mwenye shati nyeupe)  na Edward Shayo wakisindikizwa na askari kuingia katika chumba cha Mahakam kwa ajili ya usikilizwaji wa shauri linalowakabili,
Mshitakiwa wa pili katika shtaka la mauaji ya Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Scolastica ,Edward Shayo akiingia katika chuma cha Mahakama wakati shtaka linalomkabili yeye na wenzake lilipoanza kusikilizwa .

Baadhi ya ndugu wa Washatwakiwa wakiwa katika chumba cha mahakama.
Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi ambako shughuli za mahakama kuu kanda ya Moshi zimefanyika katika usikilizaji wa shauri la Mauaji ya Mwanafunzi wa kidato cha Pili katika shule ya sekondari ya Scolastica mjini Moshi.

WAMFAHAMU MSANII VANESSA MDEE KUWA NI MWANASHERIA?

$
0
0
Na Moshy Kiyungi, Dar es Salaam
Aprili 2, 2019.

Baadhi ya vijana wanaochipukia katika tasnia ya usanii wa muziki, hajali kuwa elimu ni muhimu kwa mafanikio yao. Ili kuthibitisha hili, soma makala hii utafahamu historia ya msanii maarufu humu nchini Vanessa Mdee.

Mdee ni msomi wa Chuo Kikuu mwenye shahada ya Sheria, aliyeweka pembeni shahada yake akaelekeza nguvu kwenye  tasnia ya muziki wa Bongo Flava. Vanessa Mdee maarufu kama ‘Vee Money’ alizaliwa Juni 7,1988 jijini Arusha.

Ni msanii wa muziki  mwenye talanta nyingi zikiwemo za kuandika nyimbo pia ni mjasiriamali. Vanessa amekuwa akifahamu tamaduni mbalimbali baada ya kuwa katika majiji mbalimbali duniani kama vile Arusha, New York, Paris na Nairobi.

Alipata elimu ya sekondari katika shule za kisasa zilizopo jijini Arusha, baadae akaenda kupata elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki, alikochukua Shahada ya Sheria. Baadae Mdee kwa haraka akaanza kujishughulisha na maswala ya ubunifu na sanaa.

Kama walivyofanya wanamuziki wengi duniani kuachana fani walizosomea, Mdee ni miongoni mwao.  
Aliiacha fani yake ya Sheria kamaamua kujikita katika masuala ya muziki iliyomletea mafanikio makubwa.

Ikumbukwe kwamba huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, yupo mwanamuziki ajulikanae kwa majina ya Koffi Olomide, msomi wa Chuo Kikuu mwenye shahada mbili. Aliamua kuziweka kando na kufanya muziki.

Mwanzoni mwa mwaka 2007, Mdee alipata fursa ya ukaguzi kwa MTV VJ Search jijini Dar es Salaam. Baadae, alijiunga na Carol na Kule kuwa mwenyeji wa Coca Cola Chart Express.

Mwaka wa 2008, Mdee aliwahi kufanya maonyesho huko Nigeria, Afrika Kusini, Kenya, Msumbiji, Angola, Uganda, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Pia umaarufu wake unalijulikana nchi za Marekani na Brazil.

Mwaka huo huo wa 2008, Mdee alifanya kazi na Shirika la Staying Alive juu ya mradi wa karibu na moyo wake.

Vanessa alipaswa kutembelea Uwanja wa Fisi jijini Dar es Salaam akiambatana na Balozi maalum wa Alive Foundation Kelly Rowland.

Aidha Mdee ni mtangazaji wa vipindi katika Televisheni na redio mbalimbali.

Anafahamika kama mwanamke wa kwanza kutoka nchini Tanzania kutangaza katika kituo maarufu cha luninga MTV Vj, kuanzia mwaka 2007.

Baadae kutangaza katika shindano la Epic Bongo Star Search na kipindi cha dume katika Channel ya ITV .

Mwaka 2012 Mdee alijiunga na kundi la B’Hits na kushirikishwa na msanii nguli Ay pamoja na msanii Ommy  Dimpoz, katika wimbo.

Akitangazia luninga ya Mtv mwaka 2008, akiwa balozi wa Alive Foundation, aliamua kwenda kutembelea Uwanja wa fisi akiambatana na Balozi Kelly Rowland.

Vanessa Mdee pia alijiunga Malaria No More Kampeni, iliyokuwa na lengo la kutokomeza malaria.

Mwaka 2009 Mdee alitangaza katika maonesho ya Sauti Za Busara International Music Festival, ambayo hufanyika Visiwani Zanzibar.

Aidha  mwaka 2011 alikuwa mtangazaji wa kituo cha radio nchini kijulikanacho kama Choice FM na kufanya iterview na wasanii kibao wakiwemo

K'Naan, Kelly Rowland, Mac Miller, Rick Ross, Ludacris, Miguel, Donald, Naazizi, Xtatic, Stella Mwangi, Camp Mulla, Tay Grin, Teargas, Dr. Sid and many more African and International acts.

Vilevile Vanessa aliwahi kupata tunzo na kushiriki katika kazi na matangazo mbalimbali yakiwemo ya Music Awards, Airtel, Coke Studio, Crown Paints, Music Tours mwaka 2014 na kufanya nyimbo kibao ikiwemo ‘Siri’ ,’Hawajui’ na ‘Closer’.

Baadhi ya nyimbo za msanii Vanessa Mdee ni Wet, Juu, Kisela,Cash Madame, Niroge, Banbino na Nobod but Me. Zingine ni Scratch My Back, Kwangu Njoo, Move, Reekado Banks, Bounce, Pumzi ya Mwisho na Hawajui. Mdee aliachia vibao vingine ‘matata’ vya Come Over Shadee, Unfollow, Don’t  You Know, Never Ever, Tusimame , The Way you Are na Closer.

Wengi yawezekana wasiwe wanafahamu kuwa Vanessa Mdee ana dada yake aitwaye Nancy ‘Namtero’ Mdee aka Tero.

Tero alikuwa mtangazaji maarufu wa kipindi cha Str8 Up cha KTN ya Kenya.

Hata hivyo Tero ameachana na fani hiyo kwa sasa na kuanzisha familia.

Vanessa Mdee kama walivyo binaadamu wengine, yupo kwenye mahusiano na mwanamuziki Mtanzania Juma maarufu kama Jux.

Mwisho.

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa namba 0713331200, 0767331200, 0736331200 na 0784331200.

MKAZI WA MTWARA ALAMBA MAPESA YA VODACOM TUZO POINTS

$
0
0
 Meneja wa Vodacom Tanzania (PLC), mkoani Mtwara, Charles Minungu (kushoto) akiwa na meneja wa vodashop Mtwara, Frank Daud wakimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi 500,000/-mmoja wa washiriki wa kampeni ya Vodacom M-Pesa Tuzo Points, Eladius Lutha mkazi wa Naliendele katika hafla iliyofanyika Mtwara. Kupitia kampeni hii wateja 140 wa Vodacom walizawadiwa shilingi 25,000/-kila mmoja na baada ya kampeni kumalizika wateja 10 wa Vodacom nchi nzima watazawadiwa shilingi 500,000/-kila mmoja.

SIMBA KUIVAA TP MAZEMBE APRILI 6 MWAKA HUU

$
0
0
Na Agness Francis, blogu ya Jamii. 

ZIMEBAKI siku 4 wawakilishi wa Tanzania   klabu bingwa barani Afrika Simba SC kuwavaa TP Mazembe ya nchini Congo katika mchezo wa robo fainali. 

Mchezo huo utakaoanza kutimua vumbi majira ya saa kumi jioni Aprili 6 mwaka huu katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salam kwa viingilio vya 4000 mzunguko, VIP B 10000, VIP A 20000, huku tiketi za platinum zikiuzwa kwa 100,000, na mchezo wa marudiano kati ya timu hizo utafanyika April 12 2019 mjini  Lubumbashi huko nchini Congo.

Msemaji wa   Simba SC Haji Manara akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kuelekea mchezo huo
 kauli mbiu yao ya Yes we can ndio itakayotumika tena  dhidi ya mchezo huo, ambapo pia ilitumika kwenye hatua ya makundi dhidi ya JS Saoura na Allyahal ambapo walifanikiwa kupata matokeo mazuri wakiwa katika uwanja wa nyumbani. 

"Tunakwenda na Slogan ile ile ya Yes We Can, kwa sababu imelipa na inatuweka salama zaidi huku tukicheza bila wasi wasi Tutawakabili Mazembe huku tukiujua ubora wao lakini Simba ishazoea kuishangaza Afrika na Dunia kwa ujumla na tutafanya hivyo Jumamosi na tutaendelea na kauli mbiu hiyo tutakapokwenda Lubumbashi Congo katika mchezo wa marudiano Insha'Allah" Haji S Manara Afisa habari Simba Sc.

Hata  hivyo Msemaji huyo amekanusha uvumi unaozagaa kuhusu mgomo wa Nyota wao  tegemezi Emmanuel Okwi raia wa Uganda pamoja na Cloutous  Chama kutoka nchini. 

"Sio kweli kuhusu taarifa zinazozagaa kuhusu kugoma kwa wachezaji wetu hao, walipata ruhusa ya mwalimu na sasa wamesharejea kambini kuendelea na mazoezi pamoja na wenzao" amesema Manara. 

Manara amemalizia kwa kusema kuwa "hakuna  mchezaji kutoka Afrika Mashariki anayeweza kugoma kuchezea Simba, tumepoke maombi mengi kutoka kwa wachezaji wa ndani na nje ya nchi kwa barua ili tuwasajili na wengine wanaotoka klabu kubwa tu hapa nchini kila mtu anataka kuchezea Simba.

Upasuaji saratani ya matiti sasa kufanyika bila kuliondoa

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na kampuni ya dawa ya Roche ya nchini Kenya imeandaa mkutano wa kisayansi wa kuwajengea uwezo wataalam wa Radiolojia, Pathiolojia, Upasuaji, tiba ya mionzi na dawa kufanya upasuaji wa saratani ya matiti kwa kutoa uvimbe bila kuondoa titi lote kwa wagonjwa wenye dalili za mwanzoni.

Mkutano huo wa kisayansi ambao ni wa kwanza kufanyika katika Hospitali ya Mloganzila umefunguliwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili Prof. Lawrence, umelenga kukumbushana namna bora ya kuwapatia matibabu kwa njia ya kisasa wagonjwa ambao wamethibitika kuwa na saratani ya matiti. Mafunzo hayo yanashirikisha wataalam 30 kutoka Muhimbili pamoja na Hospitali za rufaa nchini ambazo ni Bugando, KCMC, Mbeya na Hospitali binafsi ya Besta.

Kupitia mtaalam mbobezi kutoka Nairobi, Kenya Dkt. Peter Bird, wataalam hao watapatiwa mafunzo ya nadharia na vitendo kwa muda wa siku nne ambapo pia mada mbalimbali zinazohusu utoaji wa matibabu ya saratani ya matiti zitawasilishwa.

“Nichukue fursa hii kuwashukuru kampuni ya dawa ya Roche kwa kushirikiana na hospitali yetu ili kuwajengea uwezo wataalam hapa nchini kwani wataalam watakaofaidika na mafunzo haya wataenda kuwajengea uwezo wataalam wengine”. Amesema Prof. Museru Akifafanua amesema saratani ya matiti inachangia vifo kwa wanawake duniani kwa asilimia 25 hadi 35, pia saratani ya matiti ipo kwa kiwango cha juu katika nchi zilizoendelea kuliko nchi zinazoendelea japokuwa vifo vingi vinavyotokana na saratani hiyo hutokea katika nchi zinazoendelea kutokana na wagonjwa kuchelewa kufika hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Kwa Tanzania saratani ya matiti ni ya pili kwa kusababisha vifo kwa wanawake wenye saratani ikiongozwa na saratani ya shingo ya kizazi, pia katika wanawake 20, mmoja wao yupo kwenye hatari ya kupata saratani hii ya matiti. Vilevile inakadiriwa kuwa asilimia 80 ya wagonjwa wanaothibitika kuwa na saratani ya matiti nchini Tanzania wanafika hospitalini wakiwa katika hatua ya tatu na ya nne ya ugonjwa ambapo matibabu yake yanakuwa hayatoi matokeo mazuri.

Wakati huohuo, Kampuni ya dawa ya Roche imeipatia Hospitali ya Mloganzila msaada wa vifaa tiba (Biopsy gun and needle) vitakavyotumika kuchukua sampuli ya uvimbe kwa mgonjwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili -MNH- Prof Lawrence Museru akifungua mafunzo ya siku nne ya kuwajengea uwezo wataalam wa Radiolojia, Pathiolojia, Upasuaji, tiba ya mionzi na dawa namna bora ya kufanya upasuaji wa saratani ya matiti kwa kutoa uvimbe bila kuondoa titi lote kwa wagonjwa wenye dalili za mwanzoni.
Washiriki wa mafunzo hayo pamoja na baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Mloganzila wakimsikiliza Prof. Museru wakati akizungumza katika mafunzo hayo ambayo yanafanyika katika Hospitali ya Mloganzila.
Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila Dkt. Julieth Magandi akiwasilisha mada kuhusu ugonjwa wa saratani ya matiti nchini katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na MNH kwa kushirikiana na kampuni ya dawa ya Roche.
Dkt. Stephen Maina kutoka Roche (wa kwanza kulia) akimkabidhi msaada wa vifaa tiba Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili Prof. Lawrence Museru (Biopsy gun and needle) vitakavyotumika kuchukua sampuli ya uvimbe kwa mgonjwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru (wa pili kutoka kushoto kwa walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo, anayemfuatia ni Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi, wa kwanza kulia ni Dkt Stephen Maina. (kushoto) ni Mkurugenzi wa Upasuaji Dkt. Deogratius Masatu.

RAIS DKT MAGUFULI AWASILI MKOANI MTWARA KUANZA ZIARA YA KIKAZI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wafanyakazi wa ndege ya Bombadier Q400 ya ATCL aliyotumia kusafiria kutoka Dar es salaam hadi Mtwara alikoanza ziara ya kikazi ya siku tatu leo Aprili 2, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasisius Byakanzwa alipowasili kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Mtwara, leo Aprili 2, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasisius Byakanzwa na viongozi wengine alipowasili kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Mtwara leo Aprili 2, 2019. PICHA NA IKULU

WAZIRI MKUU MGENI RASMI MBIO ZA SOKOINE MARATHON ,WANANCHI WAJIANDIKISHA MCHANA NA USIKU KUSHIRIKI

$
0
0
Na Woinde Shizza Globu ya jamii.


Zoezi la uandikishwaji wa mbio za kumuenzi hayati Edward Sokoine linafanyika usiku na mchana ili kutoa nafasi kwa wale waokuwa kazini wakati wa mchana ili wapate nafasi ya kujiandikisha kushiriki mbio hizo.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Lembrisi Kipuyo aliyasema hayo Leo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mwisho ya mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika April 6 jijini Arusha.

Akizungumzia swala la uandikishwaji usiku na mchana alisema awali walikuwa wanaandikishwa mchana lakini kutokana na maombi ya watu wengi kuchelewa makazini ndio maana wameamua kuandikisha adi usiku wa SAA mbili.

Alisema uandikishwaji umeanza tangu wiki iliopita katika vituo viwili ambavyo ni uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini hapa pamoja na ofisi za utamaduni na michezo wilayani Monduli huku akibainisha kuwa muitikio wawashiriki wa mbio hizo ni mkubwa.

Kwa upande wake Katibu wa chama cha riadha mkoani Arusha Alfred Shahanga alisema kuwa njia zimeshapimwa na kuthibitishwa na njia za mbio hizo zitakuwa katikati ya jiji la Arusha na kwaupande wa swala la usalama ni la uhakika.

"Mbio zote zitaanzia mnara wa saa na zitamalizikia katika uwanja wa sheik Amri Abeid na mgeni rasmi wa mbio hizo atakuwa Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa Kasimu " alisema Shahanga

Alitaja zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa kilometa 21 kuwa mshindi wa kwanza atapatiwa kiasi cha shilingi milioni moja ,mshindi wa pili shilingi laki saba na mshindi wa tatu atapatiwa laki tano.

Shahanga aliwataka wakazi wa Mkoa wa Arusha na Mkoa Jirani kujitokeza kushiriki mbio hizo ili kuenzi kwa pamoja kuanzimisha miaka 38 ya kifo cha aliekuwa Waziri mkuu wa zamani hayati Edward Moringe Sokoine.


Picha Mwenyekiti wa Sokoine Marathon Lebris kipuyo akiongea na waandishi wa habari

TIC YAPANDA MBEGU KWA VIJANA NCHINI KUHUSU KUANZISHA UWEKEZAJI BINAFSI

$
0
0
SUALA la ukuzaji wa kada ya ujasiriamali mdogo na wa kati (SME) siyo tu limesisitizwa na Ilani ya Chama Tawala, bali pia ni utekelezaji wa majukumu ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kama lilivyoanishwa na Mpango Mkakati wa Kituo 2016-2021.

Hivyo katika kutekeleza majukumu hayo Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe, aliyekuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo la uchumi na uwekezaji lililoandaliwa na UVCCM amefafanua mambo mbalimbali kuhusu uwekezaji nchini.

Kongamano hilo limefanyika mkoani Mtwara ambapo kwa sehemu kubwa lilijikita kujadili uwekezaji unavyotatua changamoto za ajira kwa vijana.

Hotuba ya Mwambe kwenye kongamano hilo imewatia hamasa vijana ambapo amewataka kujiamini na kuthubutu katika kuibua na kutekeleza miradi ya uchumi kwenye sekta za kipaumbele ambazo ni kilimo, viwanda, madini, mifugo na uvuvi.

Pia amewaaleza washiriki kutafiti na kutambua fursa zinazowazunguka mahali walipo na kuibua miradi ya uwekezaji inayoweza kutekelezwa kwa lengo la kutengeneza ajira na kuzalisha bidhaa au huduma zinazolenga kuinufaisha jamii na Taifa kwa ujumla.

Amefafanua kuwq kwa muktadha huo vijana amesema kuwamtazamo wao wa kwanza wa kupata ajira iwe ni ile inayotokana na uwekezaji wao wenyewe/ kujiajiri. Hivyo kujiamini na kuthubutu ni hatua kwa vijana katika kutengeneza ajira badala ya kutegemea dhana iliyozoeleka ya kutafuta ama kusubiri kuajiriwa.

"Elimu ya uwekezaji na uchumi iliyotolewa kupitia kongamno hili, inatafsiriwa kuwa ni mbegu bora ya maendeleo iliyopandwa kwa takribani washiriki 600 wengi wao wakiwa vijana ambao ni wawekezaji watarajiwa kwa jamii ya Watanzania na Taifa kiujumla.

"Kinachotakiwa ni vijana kuanza utekelezaji wa kuyaishi yote waliyoelekezwa ikiwa ni pamoja na kuanzisha vikundi vya watu watano sambamba na kusajili kampuni. Baada ya kusajili kampuni wafuate hatua inayofuata ya kubuni/kuibua miradi mbalimbali ya uchumi kwa utekelezaji," amesema.

Pia Mwambe alisema ‘utekelezaji wa uanzishaji wa vikundi ni hatua muhimu kwa vijana kutokana na ukweli kwamba itawasaidia kunufaika na vyanzo vya fedha za uwezeshaji kutoka Serikalini na sekta binafsi inayotolewa kupitia kwenye vikundi kwa ajili ya mitaji ya kutekeleza shughuli/miradi ya kiuchumi na uwekezaji .

Ametumia kongamano hilo kuwatambulisha washiriki Ofisi za Kanda ambapo kuna Kanda ya Kusini zinapatikana Mtwara Jengo la Mkuu wa Mkoa, Ofisi za TIC Kanda ya Mashariki zinapatikana Dar es Salama Jengo la TIC Makao Makuu na Ofisi za TIC Kanda ya Kati zinapatikana Dodoma Jengo la Manispaa.

Pia kuna ofisi za TIC Kanda ya Magharibi zinapatikana Kigoma Jengo la Mkuu wa Mkoa, ofisi za TIC Kanda ya Kaskazini zinapatikana Moshi Jengo la Mkuu wa Mkoa, Ofisi za TIC Kanda ya Ziwa zinapatikana Mwanza Barabara ya Kenyatta na ofisi za TIC Kanda ya Nyanda ya Juu Kusini zinapatikana Mbeya Jengo la Benki ya NBC.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Moses Machali alitumia kongamano hilo kutoa ufafanuzi zaidi ya kwamba vijana waamke kutumia fursa za uwekezaji zilizopo ili kuibua miradi ya uchumi na uwekezaji katika maeneo yanayowazunguka.

"Vijana kuweni na tabia ya kujishughulisha kutekeleza miradi ya kiuchumi ikilenga maeneo ya uzalishaji, usambazaji na ulaji. Kwa msisitizo Mhe.Machali alisema ‘Vijana wakati huu ni wa kupambana na kuthubutu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.

"Ni wajibu wa vijana kuchukua hatua kwa vitendo katika kuanzisha miradi ambayo itachangia kwenye maeneo matatu makuu ya uchumi ambayo ni uzalishaji, usambazaji na ulaji, "amesema.

Serikali kushirikiana na Unesco kuhakikisha usalama wa waandishi wa habari

$
0
0
SERIKALI imesema kwamba iko tayari kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni  (UNESCO) na wadau wengine kuhakikisha usalama wa waandishi wa habari wakati wakitekeleza kazi zao.
Kauli hiyo imetolewa Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo wakati wa kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu usalama wa waandishi wa habari.
Akizungumza kwa niaba ya wizara Msimamizi wa Usalama wa Waandishi wa Habari,  Patrick Kipangula alisema kwamba serikali imeweka mazingira sawa ya kumlinda mwandishi wa habari ili kuiwezesha nchi na wananchi kuwa na taarifa za uhakika zinazogusa maisha na maendeleo yao.
Alisema kwamba katika kongamano hilo ni vyema washiriki wake wote wakatazama rasimu hiyo ambayo itakuja kuwasilishwa katika kikao kikubwa cha kitaifa kuzungumzia usalama wa waandishi.
Akizungumzia masuala ya sasa ambapo kukitokea tatizo kuhusu waandishi kunakuwa na malalamiko mengi, alisema kwamba ni vyema ikatambulika kwamba sehemu nyingi duniani na hapa nchini matatizo mengi dhidi ya waandishi wa habari hayasababishwi na serikali bali na watu binafsi.
Alisema waandishi wanapaswa kuelewa sheria wanazofanyia kazi ili kujua haki zao na pia kujua misngi ya usalama wao.
Alisema ni matumaini yake kwamba taarifa hiyo inayopikwa itasaidia kutambua  mazingira ya waandishi hapa nchini na kuwezesha kuwa na usalama zaidi kama Umoja wa Mataifa unavyotaka katika kuzingatia vipengele vyake vya maendeleo endelevu hasa kipengele cha 16 na 10 hasa kifungu cha kwanza na cha pili kinachogusa usalama waandishi wa habari na wafanyakazi wa habari.
Alisema kwa sasa serikali imepania kuhakikisha kwamba waandishi wa habari wanakuwa salama na kwamba uhuru wa habari hautishiwi kwa kuwanyima uhuru waandishi wa habari.
Alisema sheria ya vyombo vya habari imetengenezwa kumlinda mwandishi wa habari hasa kwa kuzingatia kwamba waandishi pia wanatakiwa kupelekwa mafunzo na kuwekewa bima.
Katika mkutano huo ambao wawakilishi wa UNESCO walikuwepo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Tirso Dos Santos aliwataka washiriki kuchangia ripoti hiyo ili iweze kuwa msingi wa usalama kwa waandishi wa habari.
Alisema taarifa hiyo ambayo pia imetengenezwa kwa taarifa kutoka katika mashirika ya kiraia ni muhimu sana katika utekelezaji wa malengo endelevu ya dunia.
Alisema amefurahishwa sana na juhudi za serikali za kuandika taarifa hiyo, huku akisema mchango wa wadau ni muhimu ili kuwa na ripoti iliyokamilika.
Hii ni mara ya kwanza kwa serikali kuandaa ripoti kwa kusaidiwa na UNESCO kuhusu usalama wa waandishi wa habari ingawa mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa yakifanya.
Ripoti hiyo ya serikali inatarajiwa kuwasilishwa kwa mamlaka za juu na kujadiliwa Juni mwaka huu, huku taarifa hiyo ikitakiwa kukamilika Mei.
Naye Ofisa programu wa Unesco kitengo cha Habari na Mawasiliano, Nancy Kaizilege alisema katika mkutano huo kwamba ripoti hiyo ni mchanganyiko wa ripoti mbalimbali ikiwamo maswali yaliyoulizwa kwa kupitia mitandao.
Alisema kwamba taarifa hiyo inatarajiwa kufikishwa Wizara ya Fedha kabla ya kwenda kwenye mkutano mkubwa wa wadau.
Alisema kimataifa shauri hilo litakuwa wazi Julai mwaka huu wakati kwa Afrika itakuwa ni juni nchini Morocco.
Katika mkutano huo uliofanyika katika ofisi za UNESCO, wadau walikuwa wanaangalia rasimu ya serikali na usahihi wake kabla ya kwenda kwenye majadiliano katika jukwaa kubwa la kisiasa baadae mwaka huu.
Kwa mujibu wa vipengele vya SDG mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa wanatakiwa kutoa taarifa za hiari kuhusu usalama wa waandishi wa habari na wafanyakazi wa vyombo vya habari.
 Msimamizi wa Usalama wa Waandishi wa Habari wa Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Patrick Kipangula akitoa neno la ufunguzi wakati wa kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu usalama wa waandishi wa habari lililofanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Tirso Dos Santos akizungumza wakati wa kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu usalama wa waandishi wa habari lililofanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.
 Ofisa programu wa Unesco kitengo cha Habari na Mawasiliano, Nancy Kaizilege akifafanua jambo wakati wa kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu usalama wa waandishi wa habari lililofanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.
 Wadau wa tasnia ya habari wakitoa maoni wakati wa kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu usalama wa waandishi wa habari lililofanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.
 Ofisa programu wa Unesco kitengo cha Habari na Mawasiliano, Nancy Kaizilege akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wadau wakati wa kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu usalama wa waandishi wa habari lililofanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.
 wadau wa tasnia ya habari walioshiriki kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu usalama wa waandishi wa habari lililofanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.
 Wadau wa tasnia ya habari wakiendelea kujadiliana wakati wa kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu usalama wa waandishi wa habari lililofanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Tirso Dos Santos akifafanua jambo wakati wa kongamano la uandazi wa taarifa ya serikali kuhusu usalama wa waandishi wa habari lililofanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images