Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live

SPIKA NDUGAI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA KANUNI ZA BUNGE JIJINI DODOMA

0
0


Spika wa Bunge, Job Ndugai (Katikati) aongoza Kikao cha Kamati ya Kanuni za Bunge kilicholenga Kupokea na Kujadili Waraka wa Spika kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya nyongeza ya Nane katika Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016 kilichofanyika 01 Aprili, 2019 katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
 Mbunge wa kaliua na Mjumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge, Magdalena Sakaya akizungumza kwenye Kikao cha Kupokea na Kujadili Waraka wa Spika kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya nyongeza ya Nane katika Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016 kilichofanyika 01 Aprili, 2019 katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
 Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akizungumza wakati wa Kikao cha Kamati ya Kanuni za Bunge kilicholenga Kupokea na Kujadili Waraka wa Spika kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya nyongeza ya Nane katika Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016 kilichofanyika 01 Aprili, 2019 katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
 Wajumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge wakiwa kwenye Kikao cha Kupokea na Kujadili Waraka wa Spika kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya nyongeza ya Nane katika Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016 kilichofanyika 01 Aprili, 2019 katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

SERIKALI YAKABIDHI NDEGE YAKE YA FOKKER 50 KWA ATCL

0
0
 Ndege aina ya Fokker 50 iliyokabidhiwa na serikali kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa ajili ya kubeba abiria wa kawaida kama ilivyoagizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo Aprili 1, 2019

 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akipeana mikono na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leonard Chamriho baada ya kumkabidhi ndege serikali aina ya Fokker 50 ili aikabidhi kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa ajili ya kubeba abiria wa kawaida kama ilivyoagizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye hafla fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo Aprili 1, 2019. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) Injinia Emmanuel Korosso.
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leonard Chamriho baada ya kukagua ndege aina ya Fokker 50 iliyokabidhiwa na serikal kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa ajili ya kubeba abiria wa kawaida kama ilivyoagizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye hafla fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo Aprili 1, 2019. Nyuma yao Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka


 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akipeana mikono na marubani wa ndege aina ya Fokker 50 iliyokabidhiwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa ajili ya kubeba abiria wa kawaida kama ilivyoagizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye hafla fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo Aprili 1, 2019. Nyuma yake ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leonard Chamriho, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) Injinia Emmanuel Korosso
Wafanyakazi wa ATCL wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya Ndege aina ya Fokker 50 iliyokabidhiwa na serikali kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa ajili ya kubeba abiria wa kawaida kama ilivyoagizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo Aprili 1, 2019

NDITIYE ASHUHUDIA SERIKALI IKISAINI MKATABA WA KUFUNGA RADA NYINGINE MBILI ZA HALI YA HEWA MKOA WA MBEYA NA KIGOMA

0
0
Serikali ya awamu ya tano imejizatiti katika kuhakikisha huduma za hali ya hewa nchini zinakuwa za viwango vya kimataifa na za usahihi wa hali ya juu. Katika kufanikisha hili Serikali ya awamu ya tano iliahidi kuendelea kuongeza mtandao wa Rada za hali ya hewa ili kufikia Rada saba (7) zinazohitajika kwa nchi nzima.

Serikali kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, imesaini mkataba wa ununuzi wa Rada mbili za hali ya hewa zitakazofungwa eneo la Kawetere katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya na eneo la Nyamoli katika barabara ya kuelekea Bulombora, Kigoma na hivyo kuifanya Tanzania kuwa na jumla ya mtandao wa rada tano (5). Ikumbukwe kuwa tayari Mamlaka imeishafunga rada mbili za hali ya hewa huko Kiseke Mwanza na Bangulo Dar es Salaam pia imeanza utaratibu wa ufungaji wa Rada Mtwara. Hii inaifanya Tanzania kuwa Taasisi bora kwa uangazi wa wa hali ya hewa kwa njia ya Rada katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Ununuzi wa Rada hizi mbili (ya nne na ya tano) kwa ajili ya Mbeya na Kigoma umegharimu kiasi cha Tshs. 5,715,971,148.45 (USD 2,497,125) kwa kila moja na pia utengenezaji na ufungaji wa rada zote mbili utachukua muda wa miezi kumi na nne hadi kukamilika kwake. Mtengenezaji wa Rada hizo ni Enterprise Electronics Corporation (ECC)

Rada hizi zina uwezo wa kuona hadi kilometa za mkato 450 (Aerial distance) huku zikizunguka (radius distance) na uwezo halisia wa kuona mpaka matone madogo sana ya mvua ni kilometa za mkato 250.  Rada za hali ya hewa ni moja ya mitambo inayotumika kufanya uangazi wa hali ya hewa wa masafa marefu. Mitambo hii husaidia katika kukusanya data za hali ya hewa zinazoonesha uhalisia wa anga kipindi Radar inapozunguka.

 Rada inasaidia; Kujua kwa wakati maeneo yenye mvua, aina ya mawingu yaliyopo na wakati mwingine hata kujua ni kiasi gani cha mvua kinachotarajiwa, Kufuatilia maeneo yenye mvua kubwa na za mawe zinazoambatana na radi na upepo mkali hivyo kuweza kutoa tahadhari kwa muda muafaka. Kufuatilia muelekeo wa mifumo inayosababisha hali mbaya ya hewa (mvua za mawe, upepo mkali na dhoruba). kufuatilia vimbunga baharini kadri ya upeo wake na hivyo kuweza kutoa tahadhari kutokana na mwenendo wa vimbunga hivyo.

Pia kufuatilia upepo unaoweza kuleta madhara kwa usalama wa usafiri wa anga (wind shear) na Kutoa ushauri kwa watumiaji wa huduma za hali ya hewa ili wachukue tahadhari wakati wa shughuli zao kiuchumi na kijamii ikiwemo kusaidia kutoa utabiri wa muda mfupi na wakati wa hali mbaya ya hewa.

Wito unatolewa kwa wananchi wote kutoa ushirikiano katika kulinda na kutunza mitambo hii ya Rada pamoja na vifaa vyote vya hali ya hewa kwa manufaa ya Taifa letu.

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akizingumza na waandishi wakati wa kusaini mikataba ya upatikanaji wa Rada mbili za hali ya hewa kwa mikoa ya Mbeya na Kigoma, kulia ni mwakilishi wa ECC kutoka Marekani Bw. Edwin Kasanga na kushoto ni mkurugenzi mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akishuhudia tukio la kusainiana mikataba ya upatikanaji wa Rada mbili za hali ya hewa kwa mikoa ya Mbeya na Kigoma, pamoja na mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TMA Dkt. Buruhani Nyenzi na wanasheria wa TMA na ECC.


Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya TMA Dkt. Buruhani Nyenzi akizungumza wakati wa kusaini mikataba ya upatikanaji wa Rada mbili za hali ya hewa kwa mikoa ya Mbeya na Kigoma.
Baadhi ya wafanyakazi wa TMA na wanahabari wakishuhudia tukio la kusainiana kwa mikataba ya upatikanaji wa Rada mbili za hali ya hewa kwa mikoa ya Mbeya na Kigoma.

MJASILIAMALI SOKO LA MACHINGA COMPLEX AJINYAKULIA KITITA CHA SHILINGI MILIONI TANO KUTOKA BIKO

0
0
 Mshindi wa sh milioni tano Omary Abdallah Kapungu, akifurahia fedha zake alizokabidhiwa kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko, katika droo kubwa iliyofanyika Jumapili, maarufu kama Jumadili Jenga. Kapungu ni mjasiriamali katika soko la Machinga Complex, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpigapicha Wetu.

DIWANI WA CHADEMA MTO WA MBU AJIUZULU KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS DKT MAGUFULI

RAIS DKT. MAGUFULI ATOA POLE KWA MBUNGE WA IRINGA MJINI MCHUNGAJI PETER MSIGWA ALIYEFIWA NA DADA YAKE JIJINI DAR ES SALAAM

0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha Maombolezo mara baada ya kuwasili Kimara kwa ajili ya kutoa heshma za Mwisho kwa mwili wa marehemu Tryphosa Simon Sanga ambaye ni Dada wa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshma za mwisho katika jeneza la marehemu Tryphosa Simon Sanga ambaye ni Dada wa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa Msibani pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakwanza kulia, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa wakwanza kushoto aliyekaa pamoja na ndugu zake kufatia kifo cha Dada yake marehemu Tryphosa Simon Sanga kilichotokea juzi jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili Kimara msibani huku akizungumza jambo na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa ambaye alifiwa na Dada yake marehemu Tryphosa Simon Sanga.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema wakati akitoka kutoa heshma za mwisho kwenye msiba wa marehemu Tryphosa Simon Sanga ambaye ni Dada wa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka eneo la msibani Kimara mara baada ya kutoa heshma za mwisho kufatia kifo cha wa marehemu Tryphosa Simon Sanga ambaye ni Dada wa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

KAMATI YA BUNGE YAMPONGEZA DC MURO.

0
0

Kamati ya Bunge, Mifugo, Kilimo na Maji imempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro kutokana na mkakati wake wa kukwamua miradi ya maji iliyokwama kwa muda mrefu katika wilaya hiyo.

Hayo yamejiri kwenye ziara ya kamati hiyo wilayani Arumeru Mkoani Arusha baada ya kamati ya Bunge Mifugo, Kilimo na Maji kufanya ziara yakukagua miundo mbinu ya miradi mikubwa ya maji ya vijiji 10 inayoendelea kujengwa yenye lengo la kuondoa changamoto ya uhaba wa maji safi na salama .

Akizungumza mara baada ya kukagua Miradi hiyo ya Maji Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Eng. Emmanuel Kalobelo amesema amefurahishwa na kitendo cha Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Muro ya kuwasaidia wakandarasi kupata vifaa vya ujenzi yakiwemo mabomba makubwa ya maji kwa dhamana ya ofisi yake kwa wenye viwanda uku taratibu za malipo zikiendelea hatua inayosaidia miradi hiyo kukamilika kwa wakati

"Nashukuru kwa maelezo ya Mhe. Mkuu wa Wilaya ambaye tangu asubuhi ameonyesha jinsi gani anavyofuatilia miradi yote ndani ya wilaya yake, na anafahamu takwimu zote za miradi na stegi zilizofikiwa hivyo Mimi kama mtu wa sekta ya maji nimefarijika kweli na uongozi wa Wilaya ya Arumeru." Alisema Naibu Emmanuel Kalobelo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo ya bunge Ndugu Mahamoud Mgimwa amesema DC Muro anaitaji pongezi na kuungwa mkono kutokana na juhudi zake anazoonyesha zakuwaletea wananchi wake maendeleo kwa kufuatilia miradi kila hatua , pamoja na kuhakikisha wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya miradi wananufaika kwanza *, hatua ambayo amesema inadhihirisha kuwa *Dc Muro hakai ofisini na badala yake anatumia muda mwingi katika kutembelea miradi

"Mhe Muro hapa anafanya kazi nzuri kuna kazi nyingine ambazo so za kwake lakini anajitolea,naomba tumpongeze sana, unawezajiuliza anafanya kwa ajili ya nani? Lakini ameamua kufanya kwa ajili ya kuwasaidia nyinyi ndugu zake, kwa zile juhudi anazozifanya mkuu wa wilaya na waombeni sana mumuunge mkono." Alisema Mahamoud.

Kamati hiyo pia ilipata fursa ya kutembelea Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji * mifugo kwa njia ya chupa NAIC Kilichopo Wilayani Arumeru. ambapo walijionea kazi zinazofanywa za kutengeneza mbegu za Ng’ombe wa kisasa wa maziwa na nyama .

KIKUNDI CHA GONGA GONGA WAFANYA UKARABATI NA USAFI ZAHANATI YA MJI MWEMA

0
0
Vijana wa Kikundi cha Gonga Gonga cha Mji Mwema, Kigamboni wakifanya usafi cha choo cha wagonjwa cha Zahanati ya Mji Mwema. Mwishoni mwa wiki (Picha na Andrew Chale
Vijana wa Kikundi cha Gonga Gonga cha Mji Mwema, Kigamboni wakikarabati mlango wa chumba cha leba cha Zahanati ya Mji Mwema. Mwishoni mwa wiki
Vijana wa Kikundi cha Gonga Gonga wakifanya usafi wa eneo la mtaro wa maji machafu kwenye Zahanati ya Mji Mwema, Kigamboni mwishoni mwa wiki.
Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Mji Mwema, Dk. Beno Constatino, akitoa mkono wa pongezi kwa Vijana wa kikundi cha Gonga Gonga, muda mfupi baada ya kumaliza shughuli za ukarabati na usafi wa mazingira wa Zahanati hiyo, mwishoni mwa wiki.

…………………………..


NA Andrew Chale


KIKUNDI cha Gonga Gonga kinachojishughulisha na shughuli za useremal, wamejitolea kufanya ukarabati na usafi katika Zahanati ya Mji Mwema, iliyopo wilayani Kigamboni, Dar es Salaam.

Kikundi hicho kiliweza kutengeneza milango iliyokuwa inasumbua ikiwemo ya vyoo, vyumba vya madaktari na maeneo mengine huku pia wakirekebisha vifaa vya umeme ikiwemo feni za majengo hayo.

Mbali na kufanya ufundi mdogomdogo pamoja na kuweka vifaa vipya, vijana hao walifanya usafi wa mazingira ikiwemo kufyeka majani na kuzibua mtaro wa maji machafu uliokuwa maeneo ya zahanati hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, Katibu wa Gonga Gonga, Ali Rajab Ali, alishukuru kwa nafasi waliyopewa na uongozi wa zahanati hiyo na kusema walichofanya ni kuonesha kuunga mkono juhudi mbalimbali katika jamii.

“Tunashukuru kwa kupewa nafasi ya kufanya tukio hili, kwani lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunawatoa kwenye msongo wa kufikiria kifaa fulani hakifanyi kazi ama mlango haifungi.

Kwa umoja wetu pia tumefanya usafi wa mazingira maeneo yote yanayozunguka zahanati” alisema Ali.Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Mji Mwema, Dk. Beno Constatino, alikipongeza kikundi hicho kwa namna walivyojitolea kufanya shughuli za kijamii kwenye zahanati hiyo huku akiwaomba kuwa na utaratibu huo mara kwa mara.

Dk. Beno alisema awali walikuwa wanapata changamoto kwenye hasa milango ukiwemo mlango wa leba.Dkt. Beno alibainisha kuwa, awali walikuwa wanapata changamoto kwenye mlango huo wa leba na hata walikuwa wakiamua kusafirisha mgonjwa kuhamishiwa kituo cha Vijibweni.

Nae Mwenyekiti wa Gonga Gonga, Seleman Omari amesema wameamua kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali hivyo kujitolea kwao huko ni kuungana na Rais katika kauli yake ya Hapa kazi.“Tunaungana na Serikali kuhakikisha kazi zinafanyika kwa ufanisi mkubwa kwa madaktari na wauguzi ama wagonjwa wanaofika hapa kuwa mazingira salama.

Kwa ujuzi wetu wa ufundi tumejitolea kufanya shughuli hii bure kabisa kwani inawasaidia ndugu zetu na pia hata sie wenyewe” alisema Omari.

Aidha, Omari aliongeza kikundi hicho cha Gonga Gonga kimesajiliwa kisheria na kipo toka mwaka 2005 wakiwa vijana sita na baadae kuhamasishana na sasa kufikia 22 ambapo wanashughulika na ufundi mkubwa wa useremala, Sanaa za vitu vya uselemala, Umeme, Kilimo na mambo mengine.

WAZIRI MHAGAMA AWAASA WANANCHI KUTUNZA MAZINGIRA NA VYANZO VYA MAJI

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Machifu wa Tamaduni za Asili na wakazi wa Ichenjeziya alipotembelea eneo kujionea chazo cha maji asilia kilichopo Ichenjeziya, Mkoani Songwe. (Kushoto) ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume, (Kulia) ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela
Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume akieleza jambo kwa Machifu wa Tamaduni za Asili na wakazi wa Ichenjeziya alipotembelea eneo kujionea chazo cha maji asilia Aprili 1, 2019 Mkoani Songwe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisikiliza jambo kutoka kwa mmoja wa Machifu wa Tamaduni za Asili kuhusu chanzo cha maji cha Ichenjeziya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akipanda mche wa mti karibu na chanzo cha maji asilia kilichopo Ichenjeziya, Aprili 1, 2019 Mkoani Songwe.
Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume akipanda mche wa mti karibu na chanzo cha maji asilia kilichopo Ichenjeziya, Mkoani Songwe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akicheza pamoja na wanakwaya wa JKT Mlale alipofanya ziara ya kukagua maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 katika uwanja wa Kimondo, Mkoani Songwe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akifurahia jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde wakati wakiangalia kikundi cha Ngoma Asili (hakipo pichani) walipotembelea uwanja wa Kimondo kukagua maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2019, Mkoani Songwe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akiangalia Vijana wakimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 (hawapo pichani) alipotembelea uwanja wa Kimondo kukagua maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Songwe. (Kushoto) ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akieleza jambo kwa Viongozi mbalimbali walihudhuria uwanjani hapo kujionea maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru.
ana wa Halaiki wakitengeneza umbo la Mlima Kilimanjaro kuashiria kupandisha Bendera ya Taifa katika mlima Kilimanjaro wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipotembea kukagua maandalizi hayo.PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENE ULEMAVU)




Na; OWM (KVAU), SONGWE

Wananchi waaswa kutunza rasimali mbalimbali katika mazingira yao na kuyapenda ili kuepuka kuathiri na kuharibu mazigira yaliyopo.

Kauli hiyo ameitoa leo Aprili 1, 2019 Mkoani Songwe na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Ichenjeziya alipotembelea eneo hilo lenye chanzo cha maji ya asili na kupanda mche wa mti ikiwa ni siku ya Kitaifa ya upandaji miti.

Waziri Mhagama alieleza kuwa Nchi yetu imeamua kutumia uchumi wa viwanda ili kutekeleza azma ya Serikali kuelekea uchumi wa pato la kati, hivyo hata upandaji miti na maliasili ya misitu inaendana na uchumi wa viwanda,” alieleza Mhagama.

Aliongeza kuwa kuelekea kwenye Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2019, ni vyema wananchi wakashiriki kauli mbiu ya upandaji miti ambayo inaendana na kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru isemayo “Maji ni Haki ya kila Mtu, Tutunze Vyanzo Vyake na Tukumbuke Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa”.

“Wanaichenjeziya mnatakiwa kuweka historia kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka huu kwa kupanda miti kwenye vyanzo vya Maji ili kupata maji safi na salama,” alisema Mhagama

Aidha, Waziri Mhagama alitoa wito kwa kila mwananchi kuhakikisha anakuwa msimamzi wa mazingira na anatunza vyanzo vya maji kwa kufuata sheria na taratibu ili kuhakikisha kila mtu anafikiwa na maji safi na salama kama haki ya msingi. 

Hata hivyo Mhe. Mhagama alitumia pia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi wa Songwe na Mikoa ya jirani kushiriki kwa wingi katika uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazozinduliwa Aprili 2, 2019 katika Uwanja wa Kimondo uliopo Kata ya Forest, Wilayani Mbozi. 

“Hii ni nafasi ya kipekee kwa wananchi na ni siku ya kuhamasishana kwa vijana kwa kujitathimini na kutambua mchango wa Baba wa Taifa na Mhasisi wa Mapinduzi ya Zanzibari katika kujenga Taifa,” alisema mhagama 

Naye Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Ali Karume alisema kuwa uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ni siku muhimu sana kwa wananchi kutambua historia ya Tanzania Bara na Zanzibar iliyopelekea Taifa katika mwanga.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRIL 2,2019

WIKI YA MAADHIMISHO JUMUIYA YA WAZAZI-CCM KITAIFA YAZINDULIWA MKOANI RUKWA

0
0
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya CCM ya Umoja wa Wazazi Tanzani Erasto Sima akishiriki kupanga matofali ya ujenzi wa hosputali ya Nkasi, katika mji mdogo wa Namanyere mkoani Rukwa, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya Jumuiya hiyo Kitaifa, leo. KWA PICHA NYINGI ZAIDI>>BOFYA HAPA

Na Bashir Nkoromo, Nkasi.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi ya Umoja wa Wazazi Tanzani, Erasto Sima leo amezindua kwa kishindo Maadhimisho ya Wiki ya Jumuiya hiyo Kitaifa katika mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa.

Uzinduzi huo ameufanya kwa mkutano maalum uliohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Jumuiya zote CCM ukitanguliwa na shuguli ya kukagua Zahanati ya Nyamanyere na ujenzi wa Hosoitali ya Wilaya ya Nkasi.

Manaibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Tija Magoma (Bara) na Othman Ali Maulid (Zanzibar) ni miongoni mwa viongozi walioshiki kwa karibu shughuli mbalimbali za uzinduzi wa maadhimisho hayo pamoja na viogozi wa Jumuiya zote za CCM tangu ngazi ya mkoa huo wa Rukwa.

Baada ya kuwasili Namanyere na ujumbe wake akitokea Mjini Sumbawanga, Nsima alizungumza na umati wa Wana CCM na viongozi mbalimbali katika viwanja vya Zahanati ya Namanyere ambako alikuta Kada wa CCM Mkuu wa Wilaya hiyo Saidi Mtanda akiongoza wana CCM hao na Wananchi kufanya kufanya usafi wa mazingira kwenye Zahanati hiyo.

Akizungumza. Nsima aliwataka wananchi kujenga tabia ya wanachi kwenda Kliniki wawapo wahawazito na kupeleka watoto  kwenye kliniki ya zahanati hiyo na pia kwenda kupata matibabu wanapougua kwa kuwa serikali imeijenga na kuiboresha kwa kuwa inajali afya za wananchi.

Aliwataka pia kujitolea damu mara kwa mara ili kusawiri lengo la serikali kuweka benki ya damu kwenye zahanati hiyo, akisema ni lazima wajivunie kwa kufanya hivyo kwa sababu ni zahanati chache nchini ambazo zina huduma ya benki ya damu kama ilivyo ya Namanyere.

Sima aliwataka wananchi kuunga mkono juhudi za kuboresha maisha ya wananchi zinazofanywa na Serikali CCM ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli ambapo Katibu Mkuu huyo wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania alieleza miradi ya kimaendeleo na huduma zilizokwisha tekelezwa na zinazoendelea kutekelezwa chini ya uongozi wa Rais Dk. Magufuli.

Baadaye Nsima aliikagua zahanati hiyo na kushudia ilivyoboreshwa hasa upande wa majengo ikiwemo chumba cha kisasa cha kuhifadhia maiti ambapo alihitimisha ukaguzi huo kwa yeye na msafara wake kupanda miti ya aina mbalimbali.

Nsima alimaliza ziara kwa kukagua ujenzi wa hopsitali kubwa ya Wilaya ya Namanyere ambayo itakuwa na uwezo wa kuhudumia wakazi wa wilaya hiyo na wa maeleneo ya wilaya jirani ambako alishiriki kupanga matofali yanayofyatulia hapo kwa ajili ya ujenzi huo.

Akizungumza na viongozi kwenye mkutano wa ndani wa kuzindua maadhimisho hayo, Nsima aliwataka wananchi kuwafichua watendaji au viongozi watakaokuwa wanazembea kushiriki kikamilifu utekelezaji wa ilani ya CCM.

Nsima ataendelea kuwepo Nkasi akishirikiana na wananchi kufanya shughuli mbalimbali za kijamii hadi Aprili 6, 2019, kabla ya jerejea mjini Sumbawanga ambako Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa atafunga kilele cha maadhimisho hayo kesho yake. TAZAMA PICHA KEMKEM ZA UDINDUZI WA MAAHIMISHO 

HAYO>>BOFYA HAPA

BEI ZA MATUNDA SOKO LA MWENGE,KINONDONI JIJINI DAR

0
0


Bei za matunda mbalimbali katika Soko la Mwenge wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,kama zinavyoonekana katika picha.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

Wafanyabiashara wa matunda katika soko la Mwenge jijini Dar es Salaam wakiendelea na kazi kama wanavyooneka pichani.


TUWATHAMINI NA KUWAPENDA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU KAMA WATOTO WENGINE

0
0
MEYA wa Temeke mkoani Dar es Salaam Abdallah Chaurembo amewataka wazazi kote nchini kuhakikisha wanawapatia huduma watoto walioko makambini na wale wa majumbani ili nao wajisikie kama vile wazazi wao wapo nao pamoja.

Rai hiyo ameitoa jana alipokuwa akizungumza na wazazi na wanafunzi wa shule ya secondari ya Joyland iliyoko kigamboni katika hafla ya kuchangia maendeleo ya watoto yatima katika shule hiyo. 

Alisema kuwa watoto yatima wamekuwa wakijisikia vibaya kutokana na wazazi walio wengi kuwatenga.

Hivyo Chaurembo amewataka wazazi kujitathimini juu ya jambo hilo kwani manyanyaso kwa yatima yamekuwa makubwa kutokana na sababu mbalimbali.

"Wazazi wezangu tujitolee ili kuwasaidia watoto yatima kote nchini ili nao wajisikie kama vile wazazi wao wapo hai hapa duniani, hata vitabu vya Mungu vinaimiza upendo kwa watoto hawa".alisema Chaurembo. 

Aidha meya huyo alifanikisha kupatikana kwa mamilioni ya fedha katika harambee hiyo ya kuwasaidia watoto yatima katika kituo hicho huku yeye akitoa milioni moja.

 Meya wa manispaa ya Temeke Mhe. Abdallah Chaurembo akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi katika shule ya sekondari ya Joyland iliyopo kigamboni,kwenye hafla ya kuchangia watoto yatima leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa shule ya sekondari ya Joyland,Fredrick Okuku akizungumza machache katika hafla ya kuchangia watoto yatima  leo jijini Dar es Salaam.
 Picha ya pamoja,

 Wasanii wa  mbalimbali wa Bongo Fleva wakitoa burudani.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

Wasanii wa  mbalimbali wa Bongo Fleva wakitoa burudani.

WAHANDISI WANAWAKE WASISITIZA WASICHANA KUCHANGAMKIA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI

0
0
Mhandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, Bi. Upendo Sanze, akielekeza jambo kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya KwaMtoro wilayani Chemba mkoani Dodoma, kuhusu umuhimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari KwaMtoro wilayani Chemba mkoani Dodoma, Bi. Neema Muna (mwenye miwani), akieleza changamoto zinazoikabili shule hiyo kwa Wahandisi wanawake kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, walipofika shuleni hapo kuhamasisha umuhimu wa usomaji wa masomo ya Sayansi na Hisabati kwa wasichana. 


Mwanafunzi Siminza Mambo, kutoka Shule ya Sekondari ya KwaMtoro wilayani Chemba mkoani Dodoma, akitoa maoni kwa Wahandisi wanawake kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) walipofika shuleni hapo kuhamasisha usomaji wa masomo ya Sayansi na Hisabati kwa wasichana.
Maabara ya Shule ya Sekondari ya KwaMtoro wilayani Chemba mkoani Dodoma licha ya kukamilika lakini bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa.
Wahandisi wanawake kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi pamoja na walimu wa Shule ya Sekondari ya Dalai, wilayani Kondoa mkoani Dodoma mara baada ya kutoa elimu ya umuhimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati kwa wanafunzi hao.
Picha na WUUM

…………………….

Na Siti Said

Wahandisi wa kike wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), kupitia Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, wamewataka wanafunzi wa kike mkoani Dodoma, kuchangamkia fursa za usomaji wa masomo ya Sayansi na Hisabati ili kuongeza wataalam katika fani ya Uhandisi.

Akizungumza kwa niaba ya wahandisi hao katika shule ya Sekondari ya KwaMtoro, Wilayani Chemba mkoani Dodoma, Mhandisi Rahma Mwinyi , amesema kuwa sekta hiyo bado ina uhaba wa wataalamu wa kike hivyo inahitaji wanafunzi kusoma masomo hayo ili kuongeza idadi ya wataalamu hao na kuweza kufikia uchumi wa viwanda ifikapo 2025.

“ Hakikisheni mnasoma masomo ya Sayansi na Hisabati kwa bidii, ufaulu wa masomo haya utategemea ufanyaji wa maswali na mazoezi ya kujipima mara kwa mara ambayo yatawajengea uelewa na kupelekea kufaulu vizuri, Serikali bado inahitaji wataalam wa fani hii na pia fursa za ajira kupitia fani hii zipo nyingi, kazi kwenu kujipanga ili mfikie malengo yenu”, amesema Mhandisi Mwinyi.

Aidha, Mhandisi Mwinyi amewataka wanafunzi hao kuachana na dhana potofu ya kuwa masomo hayo ni magumu na badala yake kutafuta njia mbadala ikiwemo ya kupanga ratiba ya masomo yao vizuri na kuzingatia yale wanayofundishwa na walimu darasani.

Kwa upande wake, Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya KwaMtoro, Bi. Neema Muna, kwa niaba ya walimu wenzake ameishauri Serikali kuhakikisha wanapeleka vifaa vya maabara kwa shule ambazo hazina vifaa hususan vijijini kwani ufaulu wa masomo hayo hutegemea sana kufanya mazoezi kwa vitendo.

Ameongeza kuwa ipo haja ya Serikali kuajiri na kupeleka walimu wa kutosha katika shule zilizopo vijijini kulingana na idadi ya wanafunzi na pia huduma za maji na umeme ziboreshwe ili kukidhi mahitaji ya ufanyaji wa mazoezi kwa vitendo kupitia katika maabara zao.

Naye, Mwanafunzi Siminza Mambo wa shule hiyo, ameiomba Serikali kuongeza walimu wa kike wa sayansi shuleni hapo kwani kwa sasa shule hiyo ina mwalimu mmoja tu wa jinsia hiyo hali inayowakatisha tamaa wanafunzi wa kike kujiunga na masomo hayo.

Pia, Mwanafunzi Lucy Isack, kutoka shule hiyo ameiomba Serikali kuongeza walimu wa sayansi na hisabati, vitabu na kuboreshea miundombinu ya maabara ikiwemo vifaa vya kupimia kemikali.

Ziara ya wahandisi hao katika shule mbalimbali za Sekondari za mkoa wa Dodoma inalenga kuhamasisha usomaji wa masomo ya Sayansi na Hisabati kwa wasichana ambapo leo wametembelea shule ya KwaMtoro, Dalai na Mondo.

TFS YAHAMASISHA WATANZANIA KUJENGA TABIA YA KUPANDA MITI KWA WINGI NCHINI

0
0
 Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki Zawadi Mbwambo aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo akiwa ameshika mche wa mti kabla ya kuupanda katika eneo la Kilongawima lililopo Kunduchi jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya kilele cha upandaji miti kitaifa. 
 Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki Zawadi Mbwambo kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) akipanda mti katika eneo la Kilongawima jijini Dar es Salaam jana  Aprili 1,2019 ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya siku ya upandaji miti kitaifa nchini.

 Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki Zawadi Mbwambo kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) akizungumza jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya upandaji miti kitaifa nchini ambapo ametumia nafasi hiyo kuhamasisha watanzania kupanda miti kwa wingi.
 Mkurugenzi wa Miradi wa Great Hope Foundation Noella Mahuvi  akipanda mti katika eneo la Kilongawimba lililoko Kunduchi jijini Dar es Salaam.

 Mmoja ya wakazi wa wa Kilongawimba akishiriki upandaji miti katika eneo hilo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya upandaji miti kitaifa ambayo yamefanyika leo Aprili Mosi mwaka huu.

 Baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) wakishiriki upandaji miti katika eneo la Kilongawima jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa waandishi wa habari kutoka Michuzi Blog na Michuzi TV Said Mwishehe akipanda mti katika eneo la Kilongawima ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya upandaji miti kitaifa nchini.







Said Mwishehe,Globu ya jamii 

WAKATI leo ikiwa ni Siku ya Maadhimisho ya kilele cha Upandaji Miti nchini kitaifa,Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umesema kuna kila sababu kwa Watanzania kuendelea kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu ili kukabiliana na kasi ya uharibifu wa mazingira inayoendelea kufanywa na baadhi ya watu. 

TFS katika kuhakikisha miti inaendelea kupandwa leo wameadhimisha siku hiyo kwa kupanda miti katika mikoa mbalimbali ukiwemo Mkoa wa Dar es Salaam ambapo wamepanda miti zaidi ya 1000. 

Akizungumza wakati wa upandaji miti katika eneo la Kilongawima lililoko Kunduchi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki Zawadi Mbwambo aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo amesema ni jukumu la kila Mtanzania kupanda miti iwe ya mbao, matunda au kivuli kwani kwa kufanya hivyo kutasaia uwepo wa misitu ambayo faida zake ni nyingi ikiwemo ya kuzalisha hewa safi kwa ajili ya binadamu. 

Amesisitiza kuwa ni kilele cha maadhimisho ya upandaji miti, hivyo TFS imeendelea na utaratibu wake wa kupanda miti katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba kwa mwaka huu wameamua kuweka utaratibu kila mkoa kupanda miti na wanaendelea kuhamasisha jamii ya watanzania kuwa na utamaduni wa kupanda miti kila siku na isiwe mara moja tu kwa mwaka. 

"Kupanda miti iwe ni jambo la kila siku bila kujali unapanda miti kiasi gani.Nitoe mfano hapa hapa Dar es Salaam kuna watu hawalali kwasababu ya joto ambalo msingi wake unatokana na kukosekana kwa miti kwenye maeneo hayo wakati kuna maeneo mengine ya Dar hakuna joto kwasababu tu wananchi wa maeneo hayo wamepanda miti kwa wingi na kufanya hali ya hewa kuwa tulivu na hakuna joto.Hivyo tunaendelea kuhamasisha watu kupanda miti kadri wanavyoweza. 

"Pia tunahimiza upandaji miti kwasababu itasaidia kuondoa athari 

mbalimbali zikiwemo za hewa ya ukaa.TFS pamoja na kuhimiza Watanzania kupanda miti tumebaliana kila mkoa upande miti.Tunafahamu kasi ya uharibifu misitu ni kubwa mno kulikoa kupanda, hivyo tunaendelea kupanda miti alau kuddhibiti uharibifu wa misitu na ukataji miti hovyo.Kwetu tunaamini upandaji huu wa miti malengo yake ni mawili moja kurudisha misitu ya asili na pili kukabiliana na uharibifu wa ukataji miti kwa kupanda miti,"amesema. 

Ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa waandishi wa habari nao kujenga utamaduni wa kupanda miti mbali ya kuhamasisha upandaji miti nchini kwani kwa kufanya hivyo nao watakuwa sahemu ya watanzania ambao wamepanda miti kwa maslahi ya nchi yetu na uhai wa misitu nchini. 

Kuhusu miti ambayo imepandwa Kilongawima amesema katika eneo hilo TFS imepanda miti 1000 ikiwemo ya mikoko ambayo moja ya kazi yake kubwa ni kulinda mmomonyo wa ardhi, inazuia mafuriko katika maeneo ya ukanda wa Pwani, pamoja kubadilisha hewa ukaa. 

Kwa upande wake Meneja wa Misiti wa TFS Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Dotto Tumbikwa amesema baada ya kupanda miti hiyo ni jukumu lao kuhakisha inalindwa, hivyo ametoa rai kwa wananchi kuhakiksha wanakuwa walinzi wa miti hiyo. 

"Miti ambayo imepandwa leo ni wajibu wetu TFS kuilinda , tutaendelea kushirikiana na wananchi wa maeneo haya kuwahakikisha tunasaidiana nao kuilinda.Tunafahamu faida za uwepo wa miti katika maeno yetu,"amesma na kuongeza kuwa wanaendelea kutoa mwito kwa Watanzania kote nchini kujenga tabia ya kupanda miti. 

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Miradi wa Great Hope Foundation Noella Mahuvi amesema wanatambua umuhimu wa misitu, hivyo wameona ni vema akaungana na TFS katika kupanda miti eneo hilo huku akitumia nafasi hiyo kueleza kuwa umedika wakati kwa wanafunzi katika shule mbalimbali nchini kupanda miti. 

"Ni wajibu wetu kuendeleza uwepo wa misitu nchini, na hii itatokana kwa sisi wenyewe kuamua kuilinda misitu iliyopo, kuzuia uharibifu wa misitu na kubwa zaidi kuendelea kupanda miti .Hivyo nitoe rai kwa wanafunzi nchini kushiriki kikamilifu katika kupanda miti,"amesema Mahuvi. 

WANANCHI WA KAGEZI,MLANGE WILAYANI KIBONDO WALALAMA MRADI WA MAJI WA SH.BILIONI MOJA KUTOKAMILIKA KWA WAKATI

0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma

WANANCHI wa vijiji vya Kagezi na Mlange wilayani Kibondo mkoani Kigoma, wanalazimika kutembea zaidi ya kilomita mbili kufuata maji katika Chanzo cha maji kutokana na mradi wa maji ulioghalimu zaidi ya Sh.bilioni moja kutokamilika tangu mwaka 2014 hadi sasa.

Wakizungumza jana kijijini hapo wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani kwa baadhi ya miradi ya Serikali uliofanywa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na Serikali ya Wilaya hiyo, baadhi ya Wananchi hao waliokuwa wakigombania maji katika chanzo cha mto Kagezi, walisema wanapata shida ya kuchota maji na hasa ukizingatia kilima kilichopo katika chanzo hicho kinawachosha.

Agnes Kunjira ni mmoja kati ya wananchi hao alisema wanalazimika kuamka asubuhi kuwahi kuchota maji ndipo waende mashambani, kutokana na kero hiyo wanashindwa kufanya shughuli zao za kiuchumi kwa wakati kwa kuwa maji ni uhai na wanahitaji maji.

Aidha aliiomba Serikali kufuatilia kwanini mradi huo hautoi maji kwa kuwa kero waliyonayo inawatesa sana na endepo mradi huo ukikamilika na wakaanza kuchota maji vijijini itawasaidia kwa kiasi kikubwa kufanya shughuli zao za maendeleo.

Akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa Kijiji cha kagezi mwenyekiti wa Kijiji Zabroni Ntimba, alisema tangu mradi huo uanze kujengwa ni muda mrefu na mpaka sasa ulitakiwa uwe umekamilika lakini mwaka 2018 wananchi walipata maji kwa muda wa miezi mitatu tu na baada ya hapo maji hayakutoka tena.

Alisema wananchi wanalalamika kwani katika mradi huo walichangia asilimia 20 ya mradi hali hiyo inayosababisha kushindwa kuchangia hata shughuli zingine za maendeleo, kwa kuwa wamechangia mradi wa maji lakini hawaoni mradi ukifanya kazi.

Akitoa ufafanuzi kuhusu mradi huo Mhandisi wa maji Wilaya ya Kibondo Michael Nguruwe alisema mkandarasi wa mradi huo aliingia mkataba ,wa Sh. 244,629,764, mradi ulitakiwa kuwa umekamilika 2014 lakini kutokana na changamoto ya fedha kulipa kwa wakati kwa mkandarasi mradi uliongezewa muda hadi 2018 lakini mpaka sasa haujakabidhiwa kwa wananchi.

Alisema tatizo kubwa lililopelekea mpaka sasa mradi huo kutokamilika kwa wakati, ni changamoto ya mfumo wa umeme, ambao mkandarasi alishindwa kuukamilisha na kama halmashauri wamezuia kiasi cha shilingi milioni 50 kwaajili ya umaliziaji wa mradi huo.

Alisema mpaka sasa wanaendelea kutafuta mkandarasi wa mfumo wa umeme katika mradi huo kwaajili ya kuweka kifaa kitakacho saidia kuongoza mfumo wa umeme katika mradi huo na mradi ukabidhiwe kwa Wananchi kwaajili ya kutumika.

Kutokana na changamoto zilizopo katika mradi huo na kero wanayoipata wananchi, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo Hamisi Tahilo alisema Chama kinaagiza mradi huo kukamilika kwa kipindi cha mwezi mmoja na baada ya mwezi mmoja watafika katika mradi huo kuangalia kama kweli Wananchi wameanza kupata maji.

Alisema Serikali imetoa zaidi ya bilioni moja kwaajili ya mradi wa Wananchi lakini hadi sasa mradi huo haujakamilika, Serikali iliahidi kuhakikisha wanamtua mama ndoo kichwani ni lazima watendaji kuhakikisha Wanasimamia miradi ya serikali inafanyiwa kazi.

" Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM na fedha zinatopewa kwaajili ya kukamilisha miradi Wananchi wataiamini Serikali bqada ya kuona miradi hii inakamilika niombe ndani ya mwezi huo mmoja mradi huu uwe umekamilika", alisema Tahilo.

Aiwaomba wananchi kuwa na subira na kuendelea kujenga imani na CCM kwa kuwa imejipanga kuhakikisha wananchi wote wa vijijini na mijini wanapata huduma sawa sawa na wanaondokana na changamoto zote.
 Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kagezi wakichota maji katika chanzo cha mto Kagezi baada ya kero kubwa ya  maji kijijini humo
 Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kibondo wakiwasaidia Wannanchi kubeba maji.
 Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kagezi wakichota maji katika chanzo cha mto Kagezi baada ya kero kubwa ya  maji kijijini humo
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kagezi wakichota maji katika chanzo cha mto Kagezi baada ya kero kubwa ya  maji kijijini humo
 Kifaa kinachodaiwa kusababisha maji yasitoke katika mradi wa Maji kagezi.

USHIRIKA UCHUKUE MIKOPO KWA AJILI YA WAKULIMA –MGUMBA

0
0


Naibu waziri Kilimo Mhe. Omari T. Mgumba (Mb) akiwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa arusha alipokutana na wataalamu wa kilimo ,ushirika na umwagiliaji kabla ya kuanza ziara ya kuzungukia maeneo mbalmbali mkoani hapo.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoani Arusha bwana Loata Erasto Sanare akieleza jambao baada ya kutembelewa na Naibu Waziri Kilimo Mhe. Omari T. Mgumba katika ofisi ya chama hicho hivi karibuni.


………………………….

Bashiri Salum,Wizara ya Kilimo Arusha

Vyama vya Ushirika vimeshauriwa kukopa fedha kwenye Mabenki kwa ajili ya wanachama wao kwa kuwa waliowengi hawakopesheki hivyo kufanya shughuli za kilimo kuwa ngumu.

Akizungumza katika kikao kilicho wakutanisha Maafisa Ushirika, umwagiliaji na afisa kilimo Mkoani Arusha Naibu Waziri Kilimo Mhe. Omari Mgumba amesema miundombinu mingi ya umwagiliaji inahitaji marekebisho makubwa ili kuweza kutumiwa na wakulima.

Aidha miundombinu hiyo imekosa ukarabati kutokana na wakulima kutokuwa na mitaji ya kutosha na kutoaminiwa na taasisi za fedha kusaidia ukarabati huo.

Ameshauri tume ya Ushirika kuvisimia vyama vya ushirika ili viweze kukopa fedha Benki Kwa ajili ya wanachama lengo likiwa ni kufanya ukarabati Wa miundombinu ya umwagiliaji ambapo kila mwanachama atawajibika kuchangia huduma hiyo.

Hatuwezi kufanya Kilimo cha kibiashara Kwa kutegemea mvua ambazo Nazo zimekuwa haziyabiriki nawashauri tume ya Ushirika na tume umwagiliaji kusimamia vyama hivyo kwenye skimu mbalimbali za umwagiliaji kukopa fedha ambazo zitatumika kurekebisha miundombinu ya umwagiliaji badala ya kutegemea serikali .alisema Mhe. Naibu Waziri

Naibu Waziri aliwataka maafisa ugani kuwafikia wakulima na kuelimisha namna ya kutumia na kutoa elimu juu ya matumizi bora ya viuatilifu vya mimea ili kupambana na visumbufu vya mazao ambavyo vimekuwa vikimsababishia mkulima hasara kubwa.

Naye afisa Umwagiliaji wa kanda mhandisi Juma Mdete amesema katika ukanda huo eneo ambalo linafaa kwa kilimo cha umwagiliaji ni hekta elfu 40 kati ya hilo linalotumika ni hekta elifu 24 tu

Amesisitiza kwamba pamoja na matumizi kidogo ya eneo la umwagiliaji lakini maeneo yanayomwagiliwa yanasaidia upatikanaji wa chakula wakati wa ukame.

Akichangia wakati wa mjadala huo Afisa Kilimo Mkoa wa Arusha Bwana Daniel Loiruck amethibitisha kwamba ukiondoa Magonjwa ya mlipuko na uvamizi wa visumbufu vya mimea maafisa kilimo wamekuwa wakijitahidi kuwafikia wakulima ili kutatua changamoto zinazowakabili.

Naye mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoani Arusha bwana Loata Erasto Sanare akamueleza Mhe. Naibu waziri kwamba hali ya ukame mkoani humo ni kubwa hivyo kuishauri serikali kuanza kufikiri njia mbadala ya kupambana na hali hiyo.

‘Msimu wa kilimo upo katikati lakini mpaka sasa hakuna mvua na tumezunguka sehemu mbalimbali hapa arusha mahindi yamekauka hata mvua ikinyesha haiwezi kuleta mabadiliko tunaishauri serikali kufikiri mbinu za kukabiliana na hali hiyo’. Alisisitiza bwana Loata Sanare

HALMASHAURI YA MJI IFAKARA YATOA MIKOPO YA SH.118 MILIONI

0
0


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akikabidhi Vikundi mfano wa hundi ya shilingi milioni 118 ambao ni mkopo kutoka Halmashauri ya Mji Ifakara. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara Mhe. Mashaka Mbilinyi na kushoto kwake aliyevaa tai ni Mkurugenzi Mtendaji wa hiyo Francis Ndulane.
Dkt. Kebwe akimkabidhi baiskeli Afisa Mwandikishaji wa mfuko wa Afya ulioboreshwa Shakila Limbega ili kumwezesha kufanya kazi hiyo kwa ufanisi zaidi. kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara Mhe. Mashaka Mbilinyi na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Francis Ndulane.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanavikundi ambao wamebahatika kupata mkopo wa jumla ya shilingi milioni 118. Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara Mhe. Mashaka Mbilinyi na kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Francis Ndulane.

…………………………..

Na . Andrew Chimesela

Halmashauri ya Mji Ifakara Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro imetoa Mkopo wa shilingi milioni 118 kwa vikundi vya akina mama, Vijana na watu wenye Ulemavu ambazo zimetokana na makusanyo ya vyanzo vya ndani kwa 2018/2019 ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kutenga asilimia kumi ya mapato ya ndani na kutoa mikopo kwa makundi hayo.

Mkopo huo umetolewa mwishoni mwa wiki katika Ofisi za Halmashauri ya mji wa Ifakara ambapo jumla ya vikundi 69 vimefaidika na Mkopo huo vikiwemo 52 vya wanawake sawa na 75%, 13 ni vya vijana sawa na 19% na Vikundi 4 ni vya watu wenye ulemavu sawa na 6% ya vikundi vyote vilivyopata mkopo huo.

Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Ifakara Francis Ndulane amesema katika kipindi cha Julai 2018 hadi Februari 2019 Halmashauri ya Mji Ifakara imekusanya jumla ya shilingi 1.1Bil kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato yake ya ndani.

Aidha amesema, katika kipindi hicho Halmashauri imetenga Tsh 110,000,000 ambayo inakaribia asilimia 10% ya makusanyo hayo kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye wenye ulemavu.

Hata hiyvo amesema milioni nane zimetolewa na Wahe. Wabunge kwa ajili ya mikopo hiyo ambapo Milioni tatu zimetolewa kutoka katika mfuko wa Jimbo la Kilombero na shilingi Milioni tano zimetolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Mchungaji Getrude Rwakatare na kufanya jumla ya mikopo iliyotolewa kuwa 118 Milioni.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akizungumza mara baada ya kukabidhi mfano wa hundi ya fedha hizo kwa wanavikundi, amewataka waliofaidika na mikopo hiyo kuwa waaminifu na kurejesha fedha wanazokopa kulingana na mikataba wanayoweka ili wengine nao waweze kufaidi mikopo hiyo na wasiorejesha wachukuliwe hatua za kisheria.

Sambamba na maagizo hayo Dkt. Kebwe amewataka Wakurugenzi wote wa Halmashauri kufanya uhakiki wa kina kabla ya kutoa mikopo hiyo kwa kikundi chochote kinachotaka kukopa, amesema engo ni kutaka fedha hizo za Serikali ziendelee kutoa tija kwa watu wengi kadri inavyowezekana badala ya wachache kuchukua fedha hizo na kutokomea kusikojulikana.

Aidha, Dkt. Kebwe ametumia fursa hiyo kuwakumbusha Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Mkoa wa Morogoro kutekeleza sharti hilo la kutenga asilimia kumi ya mapato yake na kukopesha makundi tajwa hapo juu kwa kuwa hilo sasa siyo hiari bali ni lazima kwa maelekezo ya Serikali ambapo kati ya asilimia kumi 4 ni za akina mama, 4 nyingine ni kwa ajili ya Vijana na asilimia mbili ni kwa watu wenye Ulemavu.

“Na ole wake Mkurugenzi ambaye atajivuta atazembea katika Mkoa wa Morogoro katika utoaji wa fedha hizi za vikundi, iatakula kwake” alisisitiza Dkt. Kebwe

Hata hivyo Dkt. Kebwe amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri wakishirikiana na Wahe. Madiwani kujaribu kubadili mtindo wa kukopesha fedha hizo. Amesema badala ya kukopesha fedha hizo vikundi vingi kwa fedha kidogo kidogo ni vema vikaunganishwa vikundi vingi pamoja na kupewa mkopo mkubwa ili waweze kuazisha hata kiwanda ambapo kitatoa ajira, kutakuwa na faida na kiwanda kitakuwa endelevu hivyo kuwa na tija zaidi.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Mhe. Mashaka Mbilinyi ametoa wito kwa vikundi vilivyopata mikopo kujiunga na mfuko wa Afya wa CHF ili kuwa rahisi kwao kupata tiba mara wanapopatwa maradhi huku akisisitiza kuimarisha usafi wa mazingira katika maeneo wanayoishi ili kuondoa mlipuko wa magonjwa na kusababisha watu kuwa na Afya dhaifu inayopelekea uchumi kudorola.

Tukio la utoaji wa Mikopo liliambatana na tukio la utoaji wa vifaa vya kufanyia kazi Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa (CHF) ambapo simu za viganjani tisa zenye thamani ya Tsh. 2,070,000/= zilitolewa huku baiskeli 11 zenye thamani ya shilingi 1,430,000/=pia zilitolewa kwa Maafisa Waandikishaji kuwawezesha kufika maeneo yaliyombali, kuhamasisha watu kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU UVCCM TAIFA JIJINI DODOMA

0
0
 Spika wa Bunge,Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Ndg. Raymond Mwangwala alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Ndg. Raymond Mwangwala alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Ndg. Raymond Mwangwala alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Wizara ya Maliasili na Utalii Kutangaza Utalii kupitia AFCON U17

0
0
Na Anitha Jonas – WHUSM
Serikali ya dhamiria kutumia jukwaa wa Mashindano ya AFCON U17 yatakayofanyika hivi karibuni kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kunufaika na wageni mbalimbali watakao kuja kushiriki michuano hiyo ya Kimataifa. Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda wakati wa kikao na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa lengo la kuhakiki mikakati itakayotumika kutangaza vivutio hivyo ambavyo ni tunu ya Taifa.

“Sisi Wizara ya Maliasili na Utalii tutahakikisha tunatumia jukwaa hili la michezo kuongeza idadi ya watalii katika vivutio vya utalii nchini na tumejipanga vizuri kwa matangazo mbalimbali ambayo yanamvuto wa ushawishi kwa watalii hawa wamichezo kuvutiwa kufika katika maeneo hayo tunafukwe nzuri,Mbuga za wanyama,majengo ya kale yenye hishoria mbalimbali,maporomoko ya maji na Mlima Kilimanjaro,”alisema Prof. Mkenda.

Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho Prof.Mkenda alisisitiza kuwa ujio wa mashindano hayo ya AFCON U17 nchini ni jambo lenye manufaa makubwa kwa taifa kwani kwa kujipanga vizuri huu ndiyo wakati wa kunufaika kwa watanzania wote kupitia wageni hao, wajasiriamali mbalimbali watanufaika kwa namna moja kwani wageni hao watahitaji huduma mbalimbali kwa kipindi chote watakapo kuwa hapa nchini hivyo ni vyema watanzania watumie fursa hii.

Kwa upande wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi alitoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa kiasi cha Shilingi Bilioni Moja kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo tunashukuru sana kwani fedha hizo zitasaidia kukamilisha uendeshaji wa shughuli mbalimbali katika kipindi cha mashindano.

 “Wizara yangu kama mlezi wa Sekta ya Michezo Nchi  mpaka sasa tumesha kamilisha mambo muhimu yote tuliyoagizwa CAF na vimebaki vitu vidogo sana ambavyo vitakamilika ndani ya muda mfupi hivyo naweza kusema tupo tayari kwa mashindano,”alisema Bibi.Mlawi.

Pamoja na hayo nae Bibi.Mlawi alieleza  kuwa mashindano hayo yanataanza Aprili 14, Mwaka huu na Mechi ya ufunguzi inatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivyo ni vyema wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na kujipanga kwa ugeni huu na watanzania nivyema kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hili la kihistoria kwa taifa letu kuandaa mashindano haya ya Kimataifa.

Halikadhalika nae Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) Bw.Wilfred Kidao alieleza kuwa katika mashindano hayo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani Gianni Infantino atakuja hivyo ujio wake katika mashindano hayo utakuwa ni fursa ya kutangaza nchi yetu, vilevile uongozi wote washirikisho la mpira wa Miguu Afrika  (CAF) nao utahamia Tanzania katika kipindi chote cha mashindano.

“Katika mashindano hayo ndipo wadau wa soka duniani wanakuja kusaka vijana wenye vipaji kwa ajili ya kuwaunga katika timu zao kubwa za kimataifa mfano mchezaji kama Neymar ni mmoja ya wachezaji waliyoibuliwa katika mashindano ya mpira kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 hivyo wapo wadau mbalimbali duniani watakuja kwa ajili ya hilo,”alisema Kidao.
Wito kwa watanzania ni kuwa tayari kwa ujio huu wa kimataifa na kujipanga vyema kunufaika na wageni hawa kwa kuhakikisha wanakuwa watulivu na wakarimu kwa ajili ya kuiletea nchini mafanikio katika uchumi. 
 Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawpo pichani) jana jijini Dodoma kuhusu namna ofisi yake imejipanga kutumia jukwaa la mashindano ya AFCON U17 kutangaza fursa za utalii zilizopo nchini katika kipindi cha mashindano hayo yatakayofanyika hivi karibuni nchini, kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi na Kulia ni Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Wilfred Kidao. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi akitoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha kiasi cha Bilioni Moja  za kuendesha mashindano ya AFCON U17  yatakayofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waaandishi wa habari (hawapo pichani) jana jijini Dodoma, Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda.
Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Wilfred Kidao (kulia) akizungumza  na waandishi wa habari (hawapo pichani) jana jijini Dodoma kuhusu aina ya wageni wanaotarajiwa kufika katika mashindano ya AFCON U17 yatakayofanyika nchini hivi karibuni ambapo alieleza Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani Gianni Infantino anatarajia kuja katika mashindano hayo, kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda.
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live




Latest Images