Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

WAZIRI KABUDI AMVUTIA KASI MWANAMKE ALIYETOROKA NCHINI TANZANIA BAADA YA KUTAFUTWA NA TAKUKURU

$
0
0

*Ni yule anatuhumiwa kwa utakatishaji fedha, kumiliki majumba ya kifahari

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WIZARA wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema itahakikisha inashirikiana na nchi nyingine ili kumpata Magreth Gonzaga aliyetoroka nchini Tanzania na kutokana na tuhuma zinazomkabili za utakatishaji fedha.

Gonzaga kwa sasa anatafutwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) ambapo mbali ya tuhuma za utakatishaji fedha anatuhumiwa kujipatia mali kupitia Kampuni ya Superior Financing Solution Limited inayodaiwa kufanya biashara bila kulipa kodi ya Serikali.

Akizungumza leo Machi 27 ,2019 jijini Dar es Salaam Wizara hiyo kupitia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amesema Sheria za kimataifa ambazo Tanzania nayo imesaini hakuna mhalifu anayeweza kutoroka nchini na asipatikane kwani kuna ushirikiano mkubwa kwa nchi mbalimbali duniani kusaidiana kutafuta wahalifu popote alipo.

"Ipo sheria maalumu ya kimataifa ambayo inahusika katika eneo la kusaidiana kutafuta wahalifu.Nchi yoyote ambaye mhalifu atakwenda atapatikana na kurejeshwa nchini na hivyo hivyo mhalifu akiwa wa nje nyingine kwa kukimbia chini atarudishwa nchi husika kwa utaratibu uliopo kisheria,"amesema Profesa Kabudi.

Hivyo amesema  mtuhumiwa Magreth Gonzaga atapatikana na atarejeshwa nchini na kwa sasa kinachoendelea ni kufuatilia kujua amekimbilia nchini gani na baada ya hapo Mkurugenzi wa Mashtaka kwa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria watachukua hatua zinazostahili kwa mujibu wa sheria na baada ya hapo Wizara ya Mambo ya Nje itachukua jukumu la kumfuatilia.

Ameongeza kwa dunia hii yenye ushirikiano katika maeneo mbalimbali hakuna mhalifu anayeweza kukimbia nchini na asipatikane, hivyo Magreth ni vema akarudi nchini na kujisalimisha Takukuru  ili sheria ichukue mkondo wake.

Alipoulizwa kama tatizo na mtuhumiwa ni kutolipa kodi ya Serikali kwanini badala ya kuhangaika kutamfuta isizungumze naye alipe kodi na kisha kuachwa akaendelea na maisha yake, Waziri Kabudi amesema kinachotakiwa mtuhumiwa huyo kutafutwa na kurejeshwa nchini na kisha hatua nyingine za kisheria zifuatwe.

"Kuna dhana kuwa kosa la kutolipa kodi ni la kawaida kwa hapa nchini kwetu, ukweli kwa nchi za wenzetu ikiwemo Ujerumani kutolipa kodi ni kosa kubwa sana na ni bora uwe na kosa la kuua kuliko kulipa kodi.Kosa la kuua unaweza hata kusamehewa lakini la kutolipa kodi halina msamaha.Hivyo badala ya kukimbia nchi ni bora akarudi tu na sheria ichukue mkondo wake,"amesema Profesa Kabudi.

Jana Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Diwani Athuman alitangaza kuwa wanamtafuta Magreth ambaye ametoroka nchini wakati akitambua anatafutwa kutokana na tuhuma kwa makosa mbalimbali likiwemo la utakatishaji fedha.

Magreth Gonzaga ambaye ni Mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam anatafutwa ili kujibu tuhuma za utakatishaji fedha haramu kinyume cha kifungu namba 12(d) na 13 (a) cha sheria ya utakatishaji fedha haramu ya mwaka 2006.

Hivyo Takukuru inamsaka mwanamke huyo kupitia tangazo ambalo wamelitoa kwa vyombo vya habari.Pia inaelezwa mbali ya makosa hayo , inaeleza wakati wa uchunguzi unaendelea mtuhumiwa alitoroka nchini.

Inadaiwa kwa nyakati tofauti mtuhumiwa huyo kwa kutumia fedha ambazo ni zao la ukwepaji kodi alinunua viwanja vilivyoko ufukweni mwa Bahari ya Hindi na nyumba tatu. Pia anamiliki viwanja vitatu vilivyopo Temeke jijini.

Takukuru inasema si mara ya kwanza mtuhumiwa huyo mali zake kutolewa uamuzi wa kutaifishwa ambapo katika kesi namba CC.92/2016 alikutwa na hatia  na mali zake yakiwamo magari manne na nyumba saba zenye thaman ya Sh.milioni 486 zote zilirejeshwa serikalini .


CRDB BANK CEO HOLDS TALKS WITH CHIEF SECRETARY JOHN KIJAZI, PROMISE TO ENHANCE BUSINESS RELATIONS

$
0
0
The Chief Secretary, Engineer John Kijazi urged CRDB Bank to push for more Public-Private Partnership and financial inclusion endeavors to spur economic growth. Ambassador Kijazi made the remarks during a meeting with CRDB Bank's delegation led by the Chairman of Board of Directors Ally Laay and Managing Director Abdulmajid Nsekela who visited his office in Dar es Salaam recently.

In his remarks, Chief Secretary Kijazi pointed out that commercial Banks are the fundamental partners in complementing the government's drive towards industrialization and financial inclusion.

"The Government is keen on fostering the Public-Private Partnership as well as the financial inclusion drives, commercial Banks are our essential partners in the area of capacity building, network and projects financing through credit facilities. May I take this opportunity to applaud CRDB Bank for taking a lead role in supporting and offering financial solutions to various governments’ infrastructural projects. The Government strongly encourages other banks to take an active role in spearheading these projects as they are of fundamental benefits to the country’s economic growth” said the Chief Secretary.
Ambassador Kijazi also congratulated Mr. Nsekela on his appointment as the new Managing Director and CEO of CRDB Bank stating that the government is confident in his capabilities. “We have a lot of faith in you, the government being amongst the largest shareholders of the Bank, is expecting you to spearhead taking CRDB Bank into new milestones. You have our support”.

On his part, CRDB Bank Managing Director, Mr. Abdulmajid Nsekela thanked ambassador Kijazi on behalf of the government for continued support and vowed to continue strengthening business relations for mutual benefits. “We at CRDB have a motto that says “Tupo-Tayari,” which elucidates our readiness in embarking and providing financial solutions to all viable projects from both public and private sectors. We recognize the significance in financing development projects as they contribute to our economic growth through trickledown effects” said Mr. Nsekela.
CRDB Bank is one of the significant players in the project financing business, having taken an active role in issuing performance guarantees, bonds and working capital, as well as other banking services to various high profile projects in the country.

Mr. Nsekela also said that CRDB Bank has recently put major emphasis on retail and SMEs taking into consideration that more than 5 million Tanzanians are self employed or own small business entities which is probably one third of country’s economy. “We are most interested in retail and SME banking because we see that as an engine for growth and employment,” added Mr. Nsekela.
During the courtesy call, the CRDB Bank CEO was accompanied by Chairman of the Board of Directors Ally Hussein Laay, who exuded confidence in the bank’s new strategic direction. The Chairman also affirmed to the Chief Secretary that, CRDB Bank is on course to employ a number of initiatives to improve productivity and as a result increase returns to shareholders.

MEYA WA CUF MANISPAA YA MTWARA MIKINDANI AJIUNGA NA CCM.

$
0
0
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Godfrey Mwanchisye (CUF) na Diwani wa kata ya Chikongola Mussa Ismaili ‘Fashion’ (CUF) wamejiuzulu nafasi zao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA PRINCESS SARAH ZEID

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Binti wa Mfalme wa Jordan Sarah Zeid (katikati) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa WFP Bw. Michael Dunford (kushoto) ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Binti wa Mfalme wa Jordan Sarah Zeid (kushoto) ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa maelezo ya viungo vya chai vya Zanzibar wakati wa kumkabidhi zawadi  Binti wa Mfalme wa Jordan Sarah Zeid (kushoto) ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

LAUNCH OF CALL FOR PAPERS FOR THE EAST AFRICAN JOURNAL OF SCIENCE, TECHNOLOGY AND INNOVATION

$
0
0
East African Science and Technology Commission, Kigali, Rwanda, 27th March, 2019: The East African Journal of Science, Technology and Innovation (EAJSTI) will launch its first call for papers for publication on 3rd April, 2019 in Kampala Uganda.

EAJSTI is designed as a multidisciplinary, open access and peer review journal, publishing original research of relevance to the East African Community (EAC) region, covering basic and applied research in science, technology and innovation.

The goal of the Journal is to enhance, advance and disseminate scientific, technological and innovative knowledge that supports regional socio-economic development. The objectives of the journal include:

Supporting the development of evidence based policies;
Providing an avenue for disseminating scientific research and technological findings to researchers, professionals, industry and other stakeholders in the EAC and beyond;

Increasing the number and quality of scientific publications from the EAC Partner States;
Advancing and opening up the new frontiers for further research in science, technology and innovation domains;
Enhancing visibility of the regional scientific and technological research, and;
Promoting international recognition of local researchers and professionals.

It is anticipated that EAJSTI will, among other things, provide a strong forum, linkage and network for exchange of scientific knowledge, technology and innovations that are being generated from Universities, Research Institutions and Industry in East Africa and globally. The EAJSTI will further enhance the sharing of knowledge to its readership as it continues to increase and develop a rich database of research output in science, technology and innovation in a wide thematic area. 

Given the scarcity of regular and reliable scientific journals in production within the East African region, the EAJSTI will fill this gap and void which is created by the of absence of research outputs available from well recognized and reputable peer-reviewed journals. The EAJSTI will endeavour to support the world-renowned scientists, upcoming scientists and graduate students from both the East African region and globally to continue to publish scientific outputs, new technologies, and innovations.

The journal will invite articles in the areas of: Agriculture; Food Security and Rural Development; Natural Resources and Environmental Management; Health and Wellbeing Science; Infrastructure; Energy and Industrial Development, and; Information Communication Technology. The journal has been established through collaboration between the East African Science and Technology Commission (EASTECO), the Inter-University Council for East Africa (IUCEA), and the Nelson Mandela African Institute for Science and Technology (NM-AIST). The call for papers will be published in major newspapers in Partner States, and on the websites of the partnering institutions.

The launch will be preceded by inauguration of the editorial board, which comprises senior scientists from academia, research institutions and the industry. The ceremony will be attended by senior officers from Ministries of East African Community Affairs (MEACAs) in the Partner States, Ministry of Science Technology and Innovation of Uganda, members of the EASTECO Governing Board, and other stakeholders in Science, technology and innovation ecosystem in the region.

FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO KWA WATANZANIA

$
0
0

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO KWA WATANZANIA


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za ufadhili wa masomo ya muda mrefu katika fani mbalimbali kutoka Serikali ya Thailand.


Kozi hizo zitakazotolewa kwenye Vyuo mbalimbali nchini humo, zitajikita katika fani za Filosofia ya Uchumi Timilifu; Mabadaliko ya Tabianchi, Usalama wa Chakula; Afya ya Jamii na Malengo ya Maendeleo Endelevu.


Wizara inawahimiza Watanzania wenye sifa kuomba nafasi hizo za mafunzo zilizotangazwa na Serikali ya Thailand kwa mwaka 2019.


Mwisho wa kuomba nafasi hizo ni tarehe 31 Machi 2019. Kwa maelezo zaidi kuhusu kozi hizo na namna ya kuomba, tafadhali tembelea tovuti  ifuatayo: http://www.tica.thaigov.net



Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje Na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Dar es Salaam

27 Machi 2019

Mji wa Serikali Ukamilike Ifikapo Aprili 15-Majaliwa

VIONGOZI YANGA WAJIUZULU KUPISHA UCHAGUZI MKUU.

$
0
0
Na Ripota wa blogu ya Jamii. 

KAIMU Mwenyekiti wa klabu ya Yanga SC Samuel Lukumay na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika wametangaza rasmi leo kujiuzulu nafasi zao.

Viongozi hao wameamua kuachia ngazi mapema ili kupisha mchakato mzima wa uchaguzi mkuu wa klabu  unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Nyika pamoja na mwenzake Lukumay wameamua kujiondoa ili kutoa mwanya mzuri kwa mchakato wa uchaguzi kwenda vizuri ili kuja kupata warithi wa nafasi hizo.

Aidha hata hivyo licha ya kujiuzulu, Nyika amewaomba  msamaha wale wote aliowakosea pindi akiwa madarakani ndani ya klabu hiyo. 

''Ninajiuzulu nafasi zangu zote nikiwa kama Mjumbe wa kamati ya utendaji. "Lakini pia Mwenyekiti wa kamati ya usajili na kamati ya mashindano na niombe msamaha kwa wale niliowakosea katika utekelezaji wangu wa majukumu''. Amesema Nyika

Ikumbukwe hivi karibuni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Yanga, George Mkuchika, alitangaza kuwa watakuwa na mkutano mkuu maalum utakaoenda kuamua kama klabu inahitaji kufanya uchaguzi mkuu ama wa kujaza nafasi.


MAKAMU WA RAIS AZINDUA KONGAMANO LA 7 LA AFYA NA SAYANSI AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 7 la Afya na Sayansi la Afrika Mashariki lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasha mwenge kama ishara ya ufunguzi wa Kongamano la 7 la Afya na Sayansi la Afrika Mashariki lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Sehemu ya Wataalamu waliohudhuria ufunguzi wa Kongamano la 7 la Afya na Sayansi la Afrika Mashariki lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema teknolojia ni zana muhimu katika kushughulikia mapungufu ya msingi katika sekta ya afya.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la 7 la Afya na Sayansi la Afrika Mashariki lililofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.“tunahitaji kuwekeza katika teknolojia ya afya ya kidijitali kama njia ya kuboresha na kuimarisha huduma ya afya za kikanda” alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais ametanabaisha kuwa Tanzania imeweza kutambua na kuanza kujenga mfumo wetu wa huduma za afya kupitia Wizara ya Afya na mashirika kadhaa kama vile MSD (ambayo teknolojia ya kidijitali inasaidia kufuatilia usambazaji kutoka hatua ya ununuzi hadi utoaji kwa uhakika), NHIF (usimamizi wa uanachama wa mteja, kudai na mchango) na TFDA (taarifa ya mtandaoni ya kuagiza na kuuza nje chini ya TFDA na taarifa ya mtandaoni ya madhara mabaya ya matumizi ya dawa na vipodozi) pia kuna Mfumo wa Usimamizi wa Hospitali haswa katika Hospitali zote za Serikali. Mfumo huu hutoa taarifa halisi ya muda na unaweza kufuatilia harakati za mgonjwa na za dawa.

Mkutano huo unaofanyika kila baada ya miaka miwili unawakusanyisha wadau wa sekta za afya kutoka Afrika Mashariki na Wataalamu kutoka sehemu mbalimbali duniani ambao una lengo la kuangalia namna ya kutumia utaalamu wa kisasa katika huduma ya afya kwa kutumia mfumo wa kidijitali.

Kwa upande wake Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema Kongamano hili linafanyika wakati ambapo kanda hii, na Afrika nzima, inahitaji mabadiliko ya teknolojia ya haraka hasa katika teknolojia ya kidijitali ili kusaidia utekelezaji wa hatua za sekta za afya na mipango na kuongeza kasi ya kufikia Ufikiaji wa Afya wa Ulimwengu (UHC) ili kufikia kufikia Lengo la Maendeleo Endelevu (SDG) 3 kwa ujumla.

Wakati huohuo Makamu wa Rais amekutana na kufanya mazungumzo na Binti wa Mfalme wa Jordan Sarah Zeid ambapo walizungumzia masuala mbali mbali ya kuboresha lishe na afya kwa Mama na Mtoto.

Binti huyo wa Mfalme aliambata na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani Bw. Michael Dunford.

AGAPE YAENDESHA WARSHA KWA WASIMAMIZI WA SHERIA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA KWENYE MASOKO

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Agape,John Myola.

Shirika la Agape AIDS Control Program la mkoani Shinyanga limeendesha warsha kwa Wasimamizi wa Sheria ili kutambua haki za binadamu kwa lengo la kuondoa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye masoko ya Manispaa ya Shinyanga. 

Warsha hiyo ya siku mbili imeanza leo Machi 27,2019 katika ukumbi wa Katemi Hotel Mjini Shinyanga na kukutanisha pamoja wasimamizi wa sheria wakiwemo polisi,migambo,maafisa masoko,maafisa maendeleo ya jamii,wenyeviti wa kamati za masoko na wafanyabiashara sokoni. 

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo,Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Agape,John Myola alisema warsha hiyo ni sehemu ya kutekelezaji wa Mradi wa “Mpe Riziki Si Matusi” unaofadhiliwa na shirika la UN WOMEN kupitia Shirika la kitaifa la Equality for Growth (EfG). 

“Agape tunatekeleza huu katika Manispaa ya Shinyanga,katika warsha hii tumekutana na wasimamizi wa sheria na wafanyabiashara kutoka masoko kwenye masoko sita tunakotekeleza mradi ambayo ni Soko Kuu Mjini Shinyanga,Kambarage,Nguzo Nane,Ibinzamata,Ngokolo Mitumbani na Majengo Mapya”,alisema Myola. 

Kwa upande wake,Meneja Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda alisema lengo la warsha hiyo ni kuwajengea uwezo wasimamizi wa sheria ili waende wakasaidie kutokomeza ukatili wa kijinsa unaotokea kwenye masoko yaliyopo katika Manispaa ya Shinyanga. 

“Tafiti mbalimbali zimekuwa zikionesha kushamiri kwa matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni,mfano wanatolewa lugha chafu,wanadhulumiwa,wanabaguliwa katika nyadhifa za uongozi sokoni lakini pia kufanyia mashambulio ya aibu ikiwemo kushikwa shikwa bila idhini yao”,alieleza Isabuda. 

“Baada ya kutoa elimu kwa wasaidizi wa sheria pia tutatoa elimu kwa wasaidizi wa sheria sokoni ambao watakuwa na kazi ya kutoa elimu kwa wafanyabiashara,kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili sokoni na kutoa rufaa kwa wahanga wa ukatili na usuluhishi”,aliongeza. 

Kwa upande wao wafanyabiashara sokoni walikiri kufanyiwa vitendo vya kikatili kama vile kudhulumiwa malipo,kubaguliwa katika uongozi kwenye masoko,kutukanwa na wateja,wasichana kutongozwa kwa lazima na kushikwashikwa ovyo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Agape,John Myola akifungua Warsha ya siku mbili kwa Wasimamizi wa Sheria ili kutambua haki za binadamu kwa lengo la kuondoa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye masoko ya Manispaa ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde - Malunde1 blog. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Agape,John Myola akiwasisitiza wasimamizi wa sheria kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye masoko unatokomezwa. 
Wasimamizi wa sheria wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Agape,John Myola. 
Meneja Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda akielezea lengo la Mradi wa “Mpe Riziki Si Matusi” unaolenga kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana wafanyabiashara kwenye masoko. 
Meneja Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabda akizungumza wakati wa warsha hiyo. 
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini. 
Mwanasheria Martha Masalu kutoka ofisi ya Masalu Law Attoneys akitoa mada ya 'Uelewa wa Jumla wa Kisheria kuhusu haki za wanawake na wasichana'. 
Warsha inaendelea. 
Mwanasheria Martha Masalu akiendelea kutoa elimu kuhusu sheria mbalimbali. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

PROF KABUDI ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO ZIMBABWE

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi amesaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Zimbabwe ulioko jijini Dar es Salaam na ambapo mpaka sasa takribani watu 179 wamepoteza maisha na wengine wakiwa hawajulikani waliko kutokana na kimbunga Idai kilichosababisha mafuriko nchini humo.

Akizungumza katika Ubalozi wa Zimbabwe jijini Dar es Salaam mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ubalozini hapo,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi amemtaka Kaimu Balozi wa Zimbabwe hapa Nchini Bw Martin Tvenyika kufikisha salam za rambirambi kwa serikali na watu wa Zimbabwe kwa maafa yaliyotokea na kwamba serikali ya Tanzania iko pamoja na wananchi wote wa Zimbabwe katika kipindi hiki kigumu cha maafa.

“Msiba wenu ni msiba wetu na matatizo yenu ni matatizo yetu na kama nilivyosema ninyi na sisi chimbuko letu ni moja na tumekuwa pamoja tangu katika harakati za kutafuta uhuru kwa hiyo mioyo ya mababu zetu ambayo imetuweka pamoja kwa miaka yote hii iendelee kuwatunza,kwani ziko hadithi na mapokeo kwamba washona na wabena ni walewale hivyo sisi ni ndugu na Mwenyezi Mungu awasaidie wale wote waliopatwa na misiba”

Kaimu Balozi wa Zimbabwe Nchini Tanzania Bw Martin Tvenyika ameishukuru serikali ya Tanzania chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na kubainisha kuwa hadi kufikia jana taarifa zinasema takribani watu 179 wamethibitika kufariki dunia na wengine wakiwa hawajulikani walipo huku kukiwa na uharibifu mkubwa wa miundo mbinu.

“Maji yanapozidi kupungua ndivyo miili mingi inavyozidi kupatikana na kwa kweli tunashukuru sana kwa msaada mnayotupatia kwani imekuwa ya manufaa sana. Ni ukweli kuwa Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Barani Afrika kutoa msaada wa haraka wa kiutu ikiwemo chakula na dawa na Rais wetu Comrade Emmerson Mnangagwa anatoa shukrani zake za dhati kwa Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwa hatua hii ni moja ya mifano mingi ya mahusiano mazuri ya muda mrefu na ya kindugu yaliyopo baina ya Tanzania na Zimbabwe”

Kaimu Balozi wa Zimbabwe Bw Martin Tvenyika ameyataja maeneo yaliyoathirika zaidi na kimbunga cha Idai kuwa ni Chimamani na Manica land lililoko Mashariki mwa nchi ya Zimbabwe.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba Joh Kabudi akisaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Zimbabwe uliopo jijini Dar es Salaam,Tanzania
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba Joh Kabudi akisaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Zimbabwe uliopo jijini Dar es Salaam,Tanzania huku kaimu Balozi wa Zimbabwe hapa Nchini Bw. Martin Tvenyika akishuhudia.
Kaimu Balozi wa Tanzania hapa nchini Bw Martin Tvenyika akimuonesha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba John Kabudi katika ramani maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko yaliyotokana na Kimbunga Idai nchini humo.

TFDA YAJIVUNIA KUSHIKA NAFASI YA KWANZA BARANI AFRIKA KATIKA KUDHIBITI UBORA WA DAWA, VIFAA TIBA, VIPODOZI NA VITENDANISHI

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JITIHADA za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli za kuhakikisha inadhibiti ubora wa dawa na vifaa tiba umeiwezesha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kushika nafasi ya kwanza Barani Afrika na kwa duniani kuwamo kwenye orodha ya nchi 50 tu ambazo zipo kwenye levo ya tatu katika udhibiti wa ubora wa dawa, vifaa tiba, vipodozi na vitendanishi .

Kwa mujibu wa TFDA, mchakato wa kufikia levo ya tatu ni mrefu na unahatua mbalimbali zikiwemo za wataalam wa Shirika la Afya Duniani kufuatilia mifumo, maabara, kuhoji na kufanya uchunguzi kwa lengo la kujiridhisha ambako kote huko mamlaka hiyo ilifanikiwa na hatimaye mwaka jana ikafikia hatua hiyo na kuifanya Tanzania kuwa nchi pekee kwa nchi za Bara la Afrika kufikia levo tatu.

Ifahamike leo Machi 27,2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuna mkutano mkubwa wa wanasayansi ambao umeshirikisha nchi za Afrika Mashariki na kuhudhuriwa na watalaam na wadau mbalimbali . TFDAimeamua kuweka banda lake katika mkutano huo kwa lengo la kutoa elimu kwa umma na kubwa zaidi kuzifahamisha nchi za Afrika Mashariki kuwa Mamlaka hiyo imepiga hatua kubwa na Shirika la Afya Duniani(WHO) inatambua uwezo wake wa kimifumo katika kudhibiti ubora.

Wakizungumza na Michuzi Blog, Ofisa Mkuu Uelimishaji Umma James Ndege na Ofisa Mwandamizi Uelimishaji Umma Roberta Feruzi wote kutoka TFDA wamesema Tanzania imefanikiwa kupiga hatua kubwa katika eneo la udhibiti wa ubora wa dawa na vifaa tiba na hiyo imetokaa na jitihada ambazo zinafanywa na Serikali katika kuweka mifumo ya kisasa katika maabara mbalimbali za TFDA pamoja na utoaji wa mafunzo ya mara kwa mara kwa watalaam.

"Mwaka jana ndio tulifanikiwa kufika levo ya tatu na kwa Afrika ni Tanzania pekee kupitia TFDA ndio tumefikia hatua hiyo.Kwa maana nyingine TFDA ilikofikia haina tofauti na mataifa makubwa yakiwamo ya nchi za Ulaya ambayo nayo yapo hatua hiyo hiyo ambayo nasi tunayo.

"Kwa duniani kote kuna nchi 50 tu ambazo zipo levo ya tatu na Tanzania ni miongoni mwao.Kwa maana rahisi ni kwamba katika mifumo bora ya udhibiti wa dawa na vifaa tiba ni kumhakikisha mlaji anachotumia tunakifahamu, tunajua kinakozalishwa, kinatumika vipi, na tunafuatilia hatua kwa hatua kwa lengo la kumhakikisha usalama mlaji,"amesema Ndege.

Ndege amesema ilipofikia TFDA ni jambo la kujivunia kwa nchi zote za Bara la Afrika kwani inatoa tafsiri kuwa Bara la Afrika linaweza kufanya mambo makubwa na hivyo kikubwa ni kuweka mikakati na malengo ya kusonga mbele."Tuko hapa kuiambia jamii ya Afrika Mashariki TFDA tunaweza na tunasonga mbele."

Kwa upande wake Feruzi amesema mafanikio ya TFDA yametokana na jitihada ambazo Serikali inazifanya kwa kuijenga uwezo, kununua vifaa vya kisasa kwa ajili ya maabara pamoja na kuwajengea uwezo watalaam wa TFDA na hatimaye kwa pamoja kufikia lengo ambalo ni kuhakikisha mamlaka hiyo inatimiza majukumu yake kikamilifu.

Feruzi amesema uamuzi wa Serikali kuijengea uwezo TFDA, imekuwa na uwezo mkubwa katika ufanya uchunguzi na kufuatilia hatua kwa hatua mambo ambayo wanayasimamia huku akitolea mfano katika eneo la dawa kabla ya kuingia nchini TFDA kupitia watalaam wake inakwenda eneo ambako dawa inazalishwa na kujiridhisha na ubora wake.

Pia amesema si tu kuzifuatilia maeneo ambayo dawa zinazalishwa bali wamekuwa na mfumo kwa kutumia maabara zake zinafanya uchunguzi wa kujiridhisha kwa kina na ubora wa dawa kabla ya kufika kwa mtumiaji na hawaishi hapo kwani wanafuatilia hata baada ya kuingia nchini.

"TFDA kupitia watalaam wetu na maabara zetu pia tunafanya majaribio ya dawa kabla haijaingia sokoni.Lazima tujiridhishe kwanza na ndipo sasa turuhusu, pale ambapo tunabaini kuna kitu hakiko sawa tunatoa taarifa kwa wahusika ambao ndio wazalishaji ili watoe ufafanuzi na tukiridhika tunaendelea na hatua zinazofuata.Kutokana na ufuatiliaji makini ambao TFDA tunao, ndio umetuwezesha kuaminika na kufikia levo ya tatu,"amesema .

Amefafanua kabla ya kufika levo ya tatu, kuna levo ya kwanza ambayo hiyo ni kwa ajili ya nchi ambazo zinaanza , kisha kuna levo ya pili na baada ya hapo ndio levo ya tatu ambayo hiyo ni safi zaidi na ni nchi chache tu ambazo imefikia mahali hapo.

Feruzi amesema TFDA kufikia levo hiyo imewezesha nchi nyingi Afrika na nje ya Afrika kutumia maabara za  TFDA na watalaam wake katika kufanya uchunguzi na tafiti mbalimbali kwani majibu yanayopatikana hapo yanaweza kutumika kokote duniani.

Pia amesema kwa nchi za Afrika Mashariki, Mamlaka kama TFDA ipo Tanzania tu kwani nchi nyingine nao ndio sasa wameanza mchakato na kwa maana hiyo TFDA imekuwa ikitumika katika kushauri na kutoa maoni yake kwa nchi hizo.

"Nchi za Afrika Mashariki ukiondoa Tanzania hakuna mamlaka ya udhibiti wa ubora na usalama.Kupitia mkutano huu unaondelea jijini Dar es Salaam watalaam wetu na wadau mbalimbali katika eneo hilo watabadilishana uzoefu na kujengana uwezo kati ya nchi moja na nyingine kuhusu udhibiti wa ubora na usalama,"amesema Feruzi.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Kissa Mwamwitwa akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Mkuu Uelimishaji Umm James Ndege baada ya kutembelea banda la TFDA lililopo ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ambako kuna mkutano wa wanasayansi unafanyika leo 
Ofisa Mkuu Uelimishaji Umma James Ndege (kushoto) na Ofisa Mwandamizi Uelimishaji Umma Roberta Feruzi (kulia) wote kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) wakifafanua jambo wakiwa kwenye bandao lao la kuelimisha umma lililopo Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

WAZIRI LUGOLA AWAONGOZA WATENDAJI WAKUU WA WIZARA YAKE KATIKA KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA, JIJINI DODOMA, LEO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akifafanua jambo katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Phaustine Kasike.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akifurahia jambo wakati alipokua anazungumza na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Victor Mwambalaswa, na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini, Prosper Mbena, wakati walipokua wanatoka katika kikao cha Kamati hiyo, kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mussa Zungu (kushoto meza kuu), akiwa na wajumbe wa kamati hiyo, wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (hayupo pichani) alipokua akifafanua jambo katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma leo. Waziri Lugola aliambatana na Watendaji Wakuu wa Wizara yake katika kikao hicho.
Naibu Katibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (kushoto) akifurahia jambo na Mbunge wa Viti Maalum, Amina Mollel, mara baada ya Naibu Katibu Mkuu huyo kutoka katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKAGUA OFISI ZA WIZARA MJI MPYA WA SERIKALI

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kukagua ofisi mpya za wizara ambazo zimejengwa katika mji mpya wa Serikali jijini Dodoma Machi 27.2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ofisi za wizara zilizojengwa katika mji mpya wa Serikali jijini Dodoma Machi 27.2019
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mhandisi Valentino Chaffu,wakati alipo kagua jengo la Ofisi ya Rais (TAMISEMI) katika mji mpya wa Serikali jijini Dodoma Machi 27.2019
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, katika mji mpya wa Serikali jijini Dodoma Machi 27.2019 kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis Michael, katikati ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Marry Mwanjelwa.

UJENZI MJI WA SERIKALI WAKAMILIKA KWA 99%-MAJALIWA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema nia ya dhati ya Rais Dkt. John Magufuli ya kujenga upya mji wa Serikali imetekelezwa baada ya mji huo kukamilika kwa asilimia 99.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Machi 27,2019) alipotembelea mji mpya wa Serikali unaojengwa katika eneo la Mtumba, Jijini Dodoma. Majengo ya wizara 20 yamekamilika.

Katika ziara yake hiyo, Waziri Mkuu ametembelea na kukagua majengo ya Wizara 13, ambapo amesema ameridhishwa na hatua za ujenzi zilizofikiwa katika maeneo mengi.Hata hivyo katika maengo hayo ya wizara 13 aliyoyatembelea, Waziri Mkuu, alibaini kasoro kwenye mlango wa kuingilia katika Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu amemuagiza mkandarasi anayejenga jengo hilo auondoe na aweke mwingine kwa kuwa mbao zilizotumika zipo chini ya kiwango na haupendezi.Kadhalika, kuhusu ujenzi wa Ofisi ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ambayo bado haikamilika, Waziri Mkuu amemuongezea siku 10 mkandarasi na kumtaka akamilishe.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewaagiza Mawaziri na Makatibu Wakuu wahakikishe kazi iliyosalia ambayo ni ya kuboresha mazingira ya nje ya ofisi hizo iwe imekamilika ifikapo Apriri 15, mwaka huu. Mji huo unatarajiwa kuzinduliwa na Rais Dkt. Magufuli.

Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema ujenzi wa mji huo ulianza Desemba mwaka jana na ulitarajiwa ukamilike Februari mwaka huu lakini utakamilika Mei mwaka huu.

Waziri Jenista alisema ujenzi wa majengo ya wizara tatu ambayo hayajakamilika ikiwa ni pamoja na OR-TAMISEMI na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi na Wenye Ulemavu yatakamilika Mei mwaka huu.

WAZIRI WA AFYA AELEZEA UMUHIMU WA KUTUMIA TEKNOLOJIA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuna faida nyingi ambazo zinapatikana katika utoaji wa huduma za afya nchini kwa kutumia mifumo ya teknolojia iliyopo.

Ameyasema hayo leo Machi 27,2019 wakati anazungumza na waandishi wa habari baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa Afrika Mashariki ambao unazungumzia utoaji huduma za afya kidigitali ambapo kupitia mkutano huo watalaam wa kada mbalimbali wanatangalia jinsi gani teknolojia inaweza kutatua changamoto katika sekta hiyo.

Waziri Ummy Mwalimu amesema kukua kwa teknolojia kumesaidia katika utoaji wa huduma za afya nchini ambapo ametumia nafasi hiyo kuelezea kupitia uwepo wa teknolojia madaktari bingwa katika masala ya uzazi wameanzisha kundi lao kwenye WhatsApp na wanalitumia kwa ajili ya kusaidiana katika mambo yanayohusu uzazi.

"Kundi hilo limewaunganisha madaktari wote waliobobea katika eneo la huduma zinazohusu  uzazi, kupitia kundi hilo madaktari wanapohitaji msaada wowote kwa mama anayejifungua inakuwa rahisi kuupata.

"Kupitia kundi hilo tunayo taarifa kuwa imesadia kuokoa maisha ya mama na mtoto.Hivyo kwetu sisi tunaiangalia teknolojia kama sehemu sahihi ya kuimarisha utoaji wa huduma za afya nchini,"amesema.

Pia amesema kupitia uwepo wa teknolojia hivi sasa katika maeneo mengi ya utoaji wa huduma za afya mifumo mingi inatumia teknolojia akitolea mfano kwa sasa taarifa za mgonjwa zinawekwa katika kompyuta badala ya kuweka kwenye mafaili kwa kuandikwa kwenye karatasi.

"Tunaendelea kuhamasisha watoa huduma za afya kwenda sambamba na kasi ya ukuaji wa teknolojia, wapo baadhi bado wanaweka taarifa za mgonjwa kwenye faili na matokeo yake baada ya kuandika anaanza tena kuhamisha kwenye kompyuta na hivyo kujipa kazi mara mbili,"amefafanua Waziri Ummy

Pia amesema  kwa Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha kunakuwa na mifumo imara ya kidigitali inayorahisha utoaji wa huduma za afya.

Kuhusu mkutano huo  ulioanza leo jijini Dar es Salaam na kuendelea kwa siku tatu katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere, Waziri Ummy amesema umezikutanisha nchi tano za Afrika Mashariki na kwa sehemu kubwa wanaangalia sekta ya afya na uwepo wa mfumo wa utoaji huduma za afya kidigitali.

"Katika mkutano huu kuna mambo mengi yatajadiliwa kuhusu kutumia mifumo ya digitali katika kutoa huduma za afya. Tutaangalia uwepo wa changamoto zinazopatikana wakati wa utoaji huduma za afya kwa kutumia mifumo ya kidigitali na kisha kutafua ufumbuzi wake,"amesema.

Kupitia mkutano huo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amezindua mfumo wa kidigal katika utoaji wa huduma za afya ambapo amesema utasaidia kurahisisha utoaji huduma kwani madaktari watakuwa wakitoa huduma hata kama hawapo eneo husika ilimradi wapo kwenye mfumo huo.

"Mfumo huu wa kidigitali tuliouzindua leo utakuwa na manufaa makubwa kwa nchi zetu za Afrika Mashariki kwani madaktari watakuwa na uwezo kuwa kumtibu mgonjwa kwa kutumia mfumo huu,"amesema Mama Samia na kuongeza Tanzania inapaswa kwenda kasi zaidi katika kuutambulisha mfumo huo na kuutumia.

Wakati huohuo Waziri wa Afya kutoka nchini Burundi Thadde'e Ndikumana amesema mfumo wa kidigitali umekuja wakati muafaka na kufafanua katika nchi yao wamekuwa wakitumia zaidi Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Nairobi nchini Kenya pindi raia wao wanapohitaji kutibiwa.

Hivyo baada ya kuzinduliwa mfumo wa kidigital katika kutoa huduma za afya watakuwa na nafasi ya kuwatibu wagonjwa walioko kwenye nchi yao bila kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili au Nairobi."Kwa kutumia mfumo huu sasa watu wetu watabiwa na madaktari wa Muhimbili au Nairobi bila ya kwenda huko."

BENDI YA MAQUIS ILIYOTIKISA ANGA YA MUZIKI

$
0
0
Na Moshy Kiyungi,TABORA

Miaka ya 1970 baadhi bendi toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) zilivamia soko la muziki humu nchini zikiporomosha muziki.

Ikumbukwe mwaka 1973, Franco Luambo Luanzo Makiadi akiwa na bendi yake ya T.P. OK. Jazz alikuja hapa nchini na akafanya onyesho kamambe katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mwaka mmoja baadae wa 1972 bendi ya Maquis du Zaire, nayo ikaingia kwa mbwembwe na kuweka makazi yake ya kudumu katika jiji la Dar es Salaam.
Makala hii inaizungumzia bendi hiyo ambayo ‘iliwatesa’ baadhi ya Watanzania wapenda muziki wa dansi kwa kuwaporomoshea burudani ya muziki katika kumbi mbalimbali hapa nchini. 

Bendi hiyo ni Maquis du Zaire, iliyotokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ikafia humu nchini miaka 1990.Ili kuipata historia kamili ya bendi hiyo mwaka 1981, nilifanikiwa kufanya mahojiano maalum na mmoja wa waliokuwa viongozi wa bendi hiyo Chimbwiza Mbangu ‘Nguza Vicking’.

Alisimulia kwa kina wasifu wa bendi hiyo akisema kwamba mwaka 1960, vijana wa wakati huo katika mji wa Kamina huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), waliungana na kuunda bendi yao wakaiita Super Theo.


Nguza alisema kuwa bendi hiyo ilikuwa ikitoa burudani tosha kwa wapenzi wa muziki wa mji huo wa Kamina na vitongoji vinavyouzunguka mji huo.Alisema baadae wakaibadilisha majina ya bendi ikawa Super Gabby. Lakini uongozi wa Super Gabby ulitaka kuleta mageuzi katika muziko, mwaka 1972, wakabadilisha majina rasmi kuwa Maquis du Zaire.

Mwaka huohuo bendi hiyo iliingia hapa Tanzania wakapitia nchini Uganda.
Walipofika katika jiji la Dar es Salaam walipata mkataba wa kupiga muziki katika ukumbi wa Mikumi Tours, uliokuwa maeneo la Tazara Buguruni jijini Dar es Salaam.

Baada ya kumaliza mkataba wao waliondoka wakaenda kupiga muziki katika Klabu ya Hunters kwa kipindi kifupi.

Kisha viongozi wa bendi hiyo wakafanya mazungumzo na mfanyabiashara Hugo Kisima, aliyekuwa akimiliki wa ukumbi wa Safari Resort maeneo ya Kimara, jijini Dar es Salaam. Wakaanza kupiga muziki kwa mkataba na mfanyabiashara huyo.

Februari 1977 viongozi wa bendi hiyo ya Maquis du Zaire, waliamua kukiongezea nguvu kikosi chao. Hivyo walimtuma Tchibangu Katayi ‘Mzee Paul’ aliyekuwa mwanamuziki wa bendi ya Maquis du Zaire. Pia alikuwa mmoja kati ya viongozi wa bendi hiyo.Mzee Paul aliwachukua baadhi ya wanamuziki ili kuja Tanzania kuongeza nguvu katika bendi ya Maquis du Zaire.

‘Mzee Paul’ alibahatika kuwachukuwa wanamuziki akina Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’, mtunzi na mwimbaji, Kanku Kelly kwa upande wa tarumbeta., Ilunga Banza ‘Mchafu’, aliyekuwa akiungurumisha gitaa la besi, Mutombo Sozy aliyekuwa akizicharanga drums, na mnenguaji Ngalula Tshiandanda.

Wakati huo Maquis du Zaire walikuwa wakicheza muziki wakitumia mtindo wa ‘Chakula Kapombe’, ambao kwa Watanzania ulikuwa mpya na ukapendwa mno na mashabiki.

Kufika kwa wanamuziki hao kulileta changamoto kubwa katika muziki. Tungo nzuri za Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’, zilikuwa chachu masikioni mwa wapenzi wa muziki wa dansi. Kiki pia yaelezwa kuwa ndiye aliyeleta Mapinduzi makubwa ya muziki hapa nchini Tanzania.

Maquis du Zaire wakaazisha mtindo mwingine wa ‘Kamanyola’ uliowapagaisha wapenzi na wadau toka pembe zote za jiji la Dar es Salaam.

Mwishoni mwa 1977, Marquis du Zaire, walimaliza mkataba kwa Hugo Kisima, wakaondoka.Bahati nyingine ikawadondokea tena baada kuingia mkataba mwingine wa kupiga muziki kwa mzee Makao, aliyekuwa akimiliki ukumbi wa Savannah, maeneo ya Ubungo.Wakiwa Savannah, walianzisha mitindo ya ‘Sanifu’ na ‘Ogelea piga mbizi’.

Lakini ukumbi huo ukabadilishwa jina ukaitwa White House. Ikumbukwe kwamba Maquis pia ilikuwa ikipiga kwenye ukumbi wa Mpakani, maeneo ya Mwenge.Mwishoni mwaka Maquis du Zaire 1978 waliamua kuimarisha tena kikosi chao kwa kuwaleta wanamuziki wengine wapya kutoka DRC.Iliwaleta akina Kabeya Badu, Kalala Mbwebwe, Ngoyi Mubenga na Khatibu Iteyi Iteyi.

Bendi hiyo ilikuwa ikiongozwa na wanahisa akina Chinyama Chiyaza ‘Chichi’, Chibangu Katayi ‘Mzee Paul’, Chimbwiza Mbangu Nguza ‘Nguza Vicking’, Mutombo Lufungula ‘Audax’ na Mbuya Makonga ‘Adios’.

Chini ya uongozi huo, miaka ya 1980 mafanikio makubwa yalionekana, mojawapo ni lile la kuanzisha Kampuni iliyofahamika kama Orchestra Maquis Company (OMACO).

Kampuni hiyo iliweza kumiliki shamba la matunda, wakalima kwa kutumia treka zao maeneo ya Mbezi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.Mazao yao walikuwa wakiyapeleka na kuuza katika Soko Kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam.OMACO pia ilimiliki mradi mwingine wa viwanja tisa na nyumba kadhaa, maeneo ya Sinza, jijini Dar es Salaam.

Aidha iliwahi kuingia mkataba wa kuitangaza kampuni ya magari makubwa ya SCANIA.Vijana wa wakati huo watakumbuka jinsi ukumbi wa White House ulivyokuwa ukifurika watu kila siku za Jumamosi.Waliwashuhudia wanamuziki wa bendi hiyo waliokuwa watanashati, nidhamu ya hali ya juu hususan wakiwa jukwaani wakifanya vitu vyao.

Enzi hizo ilikuwa ukiingia katika ukumbi huo wa White House, mbele yako macho lazima yakutane na mbao zilizokomelewa juu ya mwembe uliokuwa ukumbini hapo, zikiwa zimenakshiwa kwa maandishi ya majina ya wanamuziki wote.

Maquis du Zaire ambayo ilikuwa ikipiga muziki mara moja kwa wiki, ilikuwa ikifika usiku wa manane, wanasisitisha muziki kwa muda na kusikika kipaza sauti kikiuliza “Wapenzi mumekuja na miswakii? Wapenzi walikuwa wakijibu “ndiyooo…” Wanaelezwa dawa ya meno ipo hapo.

Watu wengi hawakuwa na haja ya kuchukua teksi kurudi nyumbani kwani muziki wa Maquis du Zaire, ulikuwa unarindima hadi alfajiri. Muda ambao mabasi ya UDA ya Ikarus yalikuwa yameanza kazi. Wakati huo hazikuwepo ‘Dala dala’, Bajaji wala Pikipiki.

Kupitia ubunifu waliokuwa nao wanamuziki hao waliweza kubadilisha mitindo mbalimbali kwa nyakati tofauti. Mitindo hiyo ilikuwa ya ‘Chakula kapombe’, ‘Kamanyola’, ‘Sanifu’, ‘Bishe Bishe’, ‘Zembwela’, ‘Chekecha’ na Ogelea Piga mbizi.

Mpulizaji wa Tarumbeta Mwema Mudjanga ‘Mzee Chekecha’ alikuwa akiwahamasisha wapenzi wake ukumbini humo akitoa

Alikuwa Mwema Mudjanga ‘Mzee Chekecha’ aliyekuwa akinogesha zaidi mitindo hiyo ukumbini. Licha ya kazi yake ya kupuliza tarumbeta, aliweza kuwainua vitini wapenzi kwenda kucheza, akitumia vibwagizo vya “Chekeee…. Chekechaaa” “Cheza Kamanyola bila jasho…”, “Tusangalaa”, “Aima imaa”, ‘Bishe bishee”, “Saa… Sanifuu”, “cheza Kamanyolaa” “cheza kwa maringo”, “ Cheza ukijidai” na mengine mengi.


Maquis du Zaire wakati huo ilikuwa imesheheni wanamuziki takriban 40, wenye talanta zinazopishana.Kwa idadi hiyo, laiti kama wangelikuwa na tamaa, wangeliweza kupiga muziki katika kumbi tatu tofauti kwa wakati mmoja.Mpendwa msomaji naomba nikujuze au kukumbusha kikosi kamili kilichokuwa kinatengeneza bendi hiyo kwa nyakati tofauti.

Safu ya waimbaji walikuwepo akina Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’, Mbuya Makonga ‘Adios’, Mutombo Lufungula ‘Audax’, Mukumbule Lolembo ‘Parashi’, Kabeya Badu, Kalala Mbwebwe, mapacha Kassalo Kyanga na Kyanga Songa.

Wengine walikuwa Kiniki Kieto, Abubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’, Mbombo wa Mbomboka, Tshimanga Kalala Assosa, Masiya Radi ‘Dibakuba kuba’, Issa Nundu na waimbaji wa kike Tabia Mwanjelwa, Rahma Shaari na Anna Mwaole.

Wapiga gitaa la solo alikuwepo Chimbwiza Nguza Mbangu ‘Nguza Vicking’, ambaye kwa umahiri wake wa kulicharanza gita hilo, wapenzi walimpachika cheo cha juu kabisa jeshini cha ‘Field Marshal’.Wengine katika gitaa hilo walikuwa akina Ilunga Lubaba, Dekula Kahanga ‘Vumbi’, na Mbwana Suleiman ‘Mbwana Cox’.

Gitaa la rhythm walikuwepo Mulenga Kalonji ‘Vata’, Omari Makuka na Steven Kaingilila Mauffi. Halikadharika walikuwepo akina Mbambu Kazadi, Mondo Mondonde na Nawayi Kabwila.

Kwa upande wa uungurumishaji wa gitaa zito la besi walikuwa akina Ilunga Banza ‘Banza Mchafu’ ambaye aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa kulimudu gitaa hilo akiwa kajitwisha kwenye upara uliozungushiwa simbi kichwani kwake. Wengine walikuwa Ibrahimu na Mujos wa Bayeke.

Kwa upande wa wapuliza Saxophone ‘mdomo ya bata’ walikuwepo akina Mafumu Bilali ‘Bombenga’ au‘Super Sax’, Khatibu Iteyi Iteyi, Kalamzoo, Alex Kanyimbo, Akulyake Suleimani ‘King Mallu’, Roy Mukuna ‘Mukuna wa Mukuna’, Chibangu Katayi , Comson Mkomwa na Majengo Selemani.

Wapulizaji tarumbeta walikuwepo akina Mwema Mudjanga ‘Mzee Chekecha’ Nkashama Kanku Kelly, Mioma wa Mwamba ‘Mzee Tito’, Kayembe Ndalabuu ‘Trumbloo’, Mpoyo Kalenga, Berry Kankonde, Kaumba Kalemba, Ngoi Mubenga, Ilunga Ngoi ‘Bizos’, Morgan Machege na Ngenda Kalonga.

Pamoja na uimbaji Mbuya Makonga ‘Adios’ alikuwa anabofya kinada, huku Mutombo Sozzy akizicharaza drums akisaidiana na Matei Joseph.

Tumba zilikuwa zikigongwa na Siddy Morris ‘Super Konga’ na Pulukulu Wabandoki Motto.Kwa upande wa wanenguaji walikuwa akina ‘Washa Washa’, Dulla ‘Panga Panga’, Wandema Rashid, Anna Mganga, Kinacho, Mwajuma, Frida Shirima, Zuwena na Ngalula Tshiandanda, wakiongozwa na Nkulu Wabangoi.

Ikiwa katika ukumbi huo wa White House, bendi hiyo ilitoka na vibao vingi vikiwemo vya Double double, Clara, Kyembe, Maiga, Mpenzi Luta, Ngalula, Nasononeka, Nimepigwa ngwala, Promotion, Ngalula, Karubandika na Noelle Bonane. Wimbo huo ulikuwa ukipigwa mahsusi nyakati za Krimasi na mwaka mpya.

Zingine zilikuwa Dora mtoto wa Dodoma, Balimwacha, Malokelee, Promotion, Seya, Sophia, Sumu ya mapenzi, Sababu ya nini, Zowa, Uba, Safari ya Mbeya, Wakati nikiwa mdogo na nyingine nyingi zisizo idadi.

Kuna msemo usemao “Cha kuazima hakistiri maungo” msemo huo uliisibu bendi ya Maquis du Zaire baada ya kutokea sintofahamu kati ya mmiliki wa ukumbi na uongozi wa bendi. Hatma yake Maquis du Zaire ikasambaratika, wakaacha ukumbi huo uliokuwa jirani na kona ya kwenda Msewe, ukabadilishwa kuwa gereji hadi leo.

Baadhi ya wanamuziki hao walijikusanya na kuisuka upya bendi hiyo, kwa jina jingine la Maquis Original.Ikaanza kupiga muziki katika kumbi za Wapiwapi’s uliopo Maduka mawili, Chang’ombe na CCM Kata ya 14 Temeke.
Baadae wakahamia ukumbi mpya kwa wakati huo wa Lang’ata, Kinondoni walipopafanya kuwa makao yao makuu.

Baadhi ya wanamuziki hao ni pamoja na Mutombo Lufungula ‘Audax’, Tshimanga Kalala Asossa, Dekula Kahanga ‘Vumbi’, Mukumbule Lolembo ‘Parashi’, Mukuna Roy, Ilunga Banza ‘Mchafu’, Mujos wa Bayeke, Kaumba Kalemba, Mulenga Kalondji ‘Vata’ na wengine wengi.

Maquis Original iliongeza nguvu zaidi kwa kuwaleta wanamuziki wengine toka DRC, muda mfupi kabla ya kuondoka mpiga gitaa la solo, Dekula Kahanga ‘Vumbi’ kwenda Stockholm nchini Sweden.

Wanamuziki hao walikuwa Kivugutu Moto na Chatcho, aliyekuwa akilicharaza gitaa la solo, waimbaji Freditto Butamu na Luhembwe Mwahitwa ‘Bobo Sukari’.

Safu hiyo ya Maquis Original ilitikisa wapenzi na mashabiki wake katika ukumbi wa Lang’ata kwa nyimbo zao kali za Mangolibo, Mayanga, Makumbele na nyingine nyingi.Wimbo wa Ngalula ulikuwa ukitia fora mbapo wakati wa ‘chorus’, Tshimanga Assosa, alikuwa akimpandisha mori mpiga gita la solo Dekula Kahanga ‘Vumbi’ akimwita “vumbiii… Vimbiiii… Vumbiii…”

Nyimbo za Maquis Original ziliweza kukonga nyoyo za wapenzi wao kwa mitindo waliyobuni hapo ya ‘Washawasha’ na ‘Sendema’.Aidha Maquis Original walikuwa shabiki wao mkubwa aliyejulikana kwa jina la ‘Magoma moto’. Alikuwa akiachiwa uwanja akionesha uhodari wake wa kucheza mtindo hiyo, huku akiwa kajitwisha chupa yenye bia kichwani chake.

Waswahili wanasema kuwa “ Lakuvunda halina Ubani” Maquis Original nayo ikaondoka katika medani ya muziki, ni zaidi ya miaka 27 sasa toka jina la Maquis Original,liliposambaratika katika miaka ya 1990.
Mwanamuziki mahiri Tshimanaga Kalala Assosa ‘mtoto mzuri’, alijitoa Kimasomaso kwa kutumia weledi wake, akalienzi jina la Maquis.

Alianzaisha bendi ya ‘Bana Maquis’ ambayo hupiga na kukumbushia nyimbo zilizopigwa na Maquis du Zaire, Maquis Original na za kwao.Mpenzi msomaji kwa mapenzi yake Mungu, idadi kubwa miongoni mwa wanamuziki wanaotajwa katika makala hii, wameshatangulia mbele zake.

Wengine wanaumwa maradhi mbalimbali akiwemo Mbombo wa Mbomboka.
Mungu aziweke roho zao pahala pema peponi waliotangulia mbele zake na awape tahfifu wanaoumwa, amina.

SHONZA AKUTANA NA WADAU WABUNIFU WA MITINDO NA USHONAJI

$
0
0



Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akizungumza na wabunifu wa mitindo na ushonaji (hawapo pichani), baada ya kufungua kikao kusikiliza changamoto zao, kikao hicho kilifanyika katika Uwanja wa Mpira wa Taifa (National Stadium ) Jijini Dar es Salaam, kulia ni Rais wa TAFCA, Adrian Nyangamalle na Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa, Bi. Leah Kahimbi.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akitoa afafanuzi wa jambo kwa wabunifu wa mitindo na ushonaji ( hawapo pichani ), baada ya kufungua kikao kusikiliza changamoto zao, kikao kilifanyika Uwanja wa Mpira wa Taifa (National Stadium ) Jijini Dar es Salaam, kulia ni Rais wa TAFCA, Adrian Nyangamalle na Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa, Bi. Leah Kahimbi.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akijibu swali la mmoja ya washiriki katika kikao cha Wabinifu wa mitindo na ushonaji, kilichofanyika katika Uwanja wa Mpira wa Taifa (National Stadium ) Jijini Dar es Salaam, kulia ni Rais wa TAFCA, Adrian Nyangamalle na Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa, Bi. Leah Kahimbi na kushoto ni katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfery Mngereza.
Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa, Bi. Leah Kahimbi (aaa na Michezo, Juliana Shonza (kushoto) kuhusu changamoto zilizotolewa na Wabunifu wa Mitindo katika kikao kilichofanyika Uwanja wa Mpira wa Taifa (National Stadium ) Jijini Dar es Salaam, kulia ni Rais wa TAFCA.
Mbunifu wa Mitindo Airinda Sawe (Afrika sana), akichangia hoja mbele ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Juliana Shonza katika kikao cha Wabinifu wa mitindo na ushonaji kilichofanyika Uwanja wa Mpira wa Taifa (National Stadium ) Jijini Dar es Salaam.
Mbunifu wa Mitindo na Mshonaji kutoka Chuo cha Ufundi(VETA) Athanasia Kisyeli akitoa mawazo yake kuhusu sanaa ya mitindo na ushonaji mbele ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Juliana Shonza(hayupo pichani) aliyeitisha kikao cha kuwasikiliza Wabunifu wa mitindo na ushonaji, kilichofanyika katika Uwanja wa Mpira wa Taifa (National Stadium ) Jijini Dar es Salaam.
Mwenyeketi wa Chama cha fashion Association Tanzania (FAA) ambaye pia ni Mbunifu wa mitindo, Mustafa Hassanali akieleza changamoto ambazo wanakumbana nazo katika kazi zao.
Mbunifu wa mitindo na Mshonaji kutoka Speshoz, Jeff akitoa mchango wa mawazo wa kuinua tasnia ya ubunifu na ushonaji katika kikao cha Wabunifu na Washonaji kilichofanyika Uwanja wa Mpira wa Taifa (National Stadium ) Jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa kikao cha Wabunifu na washonaji wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (hayupo pichani) wakati wa kikao, kilichofanyika Uwanja wa Mpira wa Taifa (National Stadium ) Jijini Dar es Salaam.

BILIONI 50 ZAWANUFAISHA WANANCHI KATIKA UJENZI WA MJI WA SERIKALI-IHUMWA- DODOMA

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akieleza kuhusu Sh.  bilioni 50 ambazo zimetumika na wakandarasi katika shughuli mbalimbali na kuwanufaisha wananchi waliopata ajira katika ujenzi wa Mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma. Kulia ni  Waziri  Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.
 Muonekano wa  Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango katika Mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma ambazo zinajengwa na  Mkandarasi, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na zimekamilika kwa asilimia 99.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akipata maelezo kuhusu uwekaji wa Transfoma ili kupata umeme wa uhakika kutoka kwa Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Elisante Ulomi, wakati Waziri huyo alipotembelea  na kukagua ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango katika Mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma.

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu, akimsikiliza kwa makini Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Elisante Ulomi alipokua anatoa maelezo kuhusu miundombinu ya Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango katika Mji wa Serikali Ihumwa, Jijini Dodoma.
Waziri  Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (wa tatu kushoto),  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) pamoja na viongozi wengine wakisikiliza maelezo ya jumla ya ujenzi wa ofisi katika Mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma.(Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango).
 Waziri  Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akipeana mkono na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alipotembelea na kukagua ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango katika Mji wa Serikali, Ihumwa Jijini Dodoma.
 Waziri  Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (wa pili kulia) akikagua ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango katika Mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma. Watatu kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).

 Waziri  Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto), akipongeza kazi nzuri ya ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango katika Mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma ambazo zimekamilika kwa asilimia 99 na kuagiza Mkandarasi ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kuhakikisha anamalizia kasoro ndogondogo zilizoonekana kabla ya Ofisi hizo kuzinduliwa rasmi.

Na Peter Haule, WFM, Dodoma
Serikali imeeleza kuwa takribani Sh. bilioni 50 zimewanufaisha wakandarasi na wananchi wa hali ya chini wakati wa  ujenzi wa ofisi za wizara mbalimbali katika Mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa, Jijini Dodoma.
Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, wakati Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, alipotembelea na kukagua ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango katika Mji wa Serikali uliopo eneo la Ihumwa.
Dkt. Mpango alisema kuwa katika eneo la ujenzi kulikuwa na mafundi kutoka kila pembe ya nchi, wafanyabiashara wadogo wa chakula (mama lishe) na wakandarasi ambao wamenufaika na uwekezaji mkubwa wa majengo ya ofisi za Serikali katika eneo hilo la Ihumwa.
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, amepongeza maendeleo ya ujenzi wa Ofisi hizo ambao umekamilika kwa asilimia 99.
Waziri Mkuu Majaliwa alimeagiza Wizara ya Fedha na Mipango kuhakikisha inatengeneza  Bustani nzuri, kusawazisha eneo hilo na kuweka samani katika ofisi hizo ili ziweze kutumika.
Aidha, alimtaka mkandarasi ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kurekebisha kasoro alizozibaini wakati akikagua jengo hilo hususan mlango mkuu wa kuingia ofisi hizo kabla ya kuzinduliwa rasmi na Mhe. Rais hivi Karibuni.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhe. Dkt. Khatib Kazungu, alisema kuwa Wizara imepokea maelekezo ya Waziri Mkuu na kuahidi kuyatekeleza kwa haraka ili watumishi waanze kutumia ofisi hizo.
Mhandisi kutoka NHC, anayesimamia ujenzi huo Bw. Elisante Ulomi ameishukuru Wizara ya Fedha na Mipango kwa ushirikiano waliompa katika kufanikisha ujenzi huo ulioanza Desemba 29, 2018 na kuahidi kurekebisha kasoro zilizobainishwa wakati wa ukaguzi huo.

DEFAO ATIMIZA ZAIDI YA MIONGO SITA.

$
0
0
Mwanamuziki maarufu Defao Desemba 03, 2018, alikuwa ni mwenye furaha ya kutimiza miaka 60 tangu azaliwe.

Licha ya umri huo kuwa mkubwa, ukimuona jukwaani ama kwenye Luninga hauwezi kuamini kama ana uwezo wa kulichezesha tambo lake lililojaa minofu kila sehemu.

Defao alizaliwa Desemba 03, 1958 katika jiji la Kinshasa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Baada ya kuzaliwa akapewa majina ya Mutomona Defao Lulendo.

Ni mwanamuziki mwenye talanta za kutunga na kuimba kwa sauti nyembeba na nyororo.Defao aliaza kujishughulisha na muziki mwaka 1976, akiwa katika bendi ya Orchestra Suka Movema. Baadae akaenda kujiunga katika bendi ya Fogo Stars.

Mwaka 1978 Defao akaenda kupiga muziki katika bendi ya Korotoro huko Somo, Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).Alikuwa mmoja kati ya wanamuziki waliounda bendi mpya ya Grand Zaiko Wawa mwaka 1981, ikiongozwa na mpiga gitaa mashuhuri Pepe Felix Manuaku.

Katika kile kilichoitwa mbinu za kujitafutia maisha, Defao aliungana na mwanamuziki Ben Nyamabo kuunda kikosi kipya cha Choc Stars.Bendi hiyo ya Choc Stars na Orchestra Shakara Gagna Gagna, zilikuwa chini ya uongozi wa Jeanpy Wable Gypson, zilimfanya General Defao kuwa maarufu kwa mara kwanza kitaifa.

Akiwa na wanamuziki akina Ben Nyamabo, Debaba, Carlito, Bozi Boziana na Djuna Djunana, bendi ya Choc Stars ikajizolea umaarufu mkubwa kupitia tungo zao.Uimbaji na uwajibikaji jukwaani wa General Defao aliweza kuonesha kuwa kipaji chake siyo cha kubahatisha.

Defao Mutomona kwa kawaida hucheza sambamba na wanenguaji wake, ambapo huwa kivutio kikubwa cha wapenzi na mashabiki wake akicheza mitindo mbalimbali ukiwemo ule wa ‘Ndombolo’ pasipo kuchoka.

Mutomona ilipofika mwishoni mwa mwaka 1990, aliiacha bendi hiyo ya Choc Stars, akiwa na madhumuni ya kuunda bendi yake.Dhamira yake alitimia baada ya kuunda bendi yake iliyopewa jina la Big Stars.

Katika bendi hiyo hupiga muziki kwa kushirikiana na mwimbaji mwingine Djo Poster, aliyetokea katika bendi ya Grand Zaiko.Defao aliomuongeza katika safu ya wanamuziki mpiga solo chipukizi Jagger Bokoko, ambaye alitokea kuwa kipenzi chake kikubwa.

Bendi ya Big Stars ilikuwa na wanamuziki wengi wenye uwezo mkubwa wa kutengeneza muziki.Kulikuwa na waimbaji akina Djo Djo Bayenge, Debleu Kinanga na Adoli Bamweniko.Kwa upande wa wapiga magitaa, kulikuwa na Mogus aliyekuwa akilicharaza gitaa la solo, gita la besi likiungurumishwa na Guy wa Nzambi.

Tumba zilikuwa zikidundwa na Richa Cogna Cogna. Mbofya kinanda alikuwa ni Sedjo Kavanda.Katika kipindi cha miaka mitano ya bendi ya Big Stars, Defao alionesha ubunifu uliomletea mafanikio makubwa baada ya kufyatua album zisizopungua 17. Kati ya hizo, sita ziliingia katika soko la Ulaya mwaka 1995.

Mifarakano katika sehemu za kazi huwa hazikosi. Big Stars iliteteleka kwa kipindi kifupi mara baada ya kuondoka Djo Djo Bayenge na kumuacha Defao akiwa kiongozi wa bendi hiyo.Defao akiwa na wanamuziki wake wa Big Stars, walikarabati upya bendi yao na kuweza kutengeneza kikosi kipya chenye wanamuziki mahiri. Walimuongeza Roxy Tshimpaka.

Roxy kabla ya kujiunga na Big Stras alikuwa katika bendi ya Choc Stars. Aidha alimpata mwimbaji mpya Azanga.Siku zilivyokuwa zikiiendela, mpigaji gitaa la solo Jagger Bokoko akawa kuwa kipenzi kikubwa cha Defao.
Umaarufu wa General Defao ulizagaa maeneo mengi Afrika Mashariki na Kati kwenye miaka 1990.

Wapenzi na mashabiki wake waliulingaisha umaarufu wake na ule wa wanamuziki akina Papa Wemba, Koffi Olomide, Bozi Boziana na Kester Emeneya.Hapana ubishi kwamba Defao Mutomona ni mwanamuziki aliye na umaarufu mkubwa miongoni mwa wanamuziki toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mpenzi msomaji utakubaliana nami iwapo utasikiliza nyimbo za Georgina, Fammilie Kikuta, Nadine, Bana Kongo, Oniva na Filie.Nyimbo hizo ziko katika kiwango cha juu na zimepigwa katika mitindo miwili ya rumba na sebene mold.Kufuatia uangalizi wa uzalishaji wa kazi toka kwa meneja wake kuwa mbovu, Defao hulazimika kubadili maprodyuza na kampuni za kurekodia.

Wakati mwingine alikuwa akitoka na matoleo ya kazi zake zilezile kwa lebo tofauti.Defao alilivunja kundi zima la Big Stars mwaka 2000 wakiwa katika jiji la Kinshasa.Yeye akaamua kwenda ‘kutanua’ katika jiji la Paris nchini Ufaransa wakati wa kipindi cha joto.Lakini akiwa katika jiji hilo, alirekodi album ya Nessy de London, akiwashirikisha wanamuziki nyota waishio katika jiji hilo la Paris.

Wanamuziki hao walikuwa akina Nyboma Mwandido, Luciana de Mingongo, Wuta Mayi, Ballou Canta na Deesse Mukangi, walioshirikiana na Defao kufanya onesho kubwa lililo wavutia watu wengi.Defao kwa kuwatumia waimbaji hao waalikwa, walipelekea album yake ya De London kupanda chati zaidi.

Aliachia album nyingine nyingi zikiwa na nyimbo za Mandova, Ya Gege, Copinnage, Sam Samita, Salanoki Guerre De1, Animation na Nessy of London.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Defao baadae akawa kimya katika anga ya muziki.Hali hiyo yasemekana kuwa ilitokana na sintofahamu ya kisiasa nchini mwake iliyopelekea kufungiwa kupiga muziki huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa uongozi wa Rais Lauler Kabila.

Defao alifika nchi za Afrika ya Mashariki ikiwemo Tanzania.Katika ziara yake ya humu nchini iligubikwa na matatizo lukuki mwaka 2000, uliokuwa mwaka mpya wa Millenium.Baada ya kumaliza kufanya maonyesho kadhaa, Defao alizidiwa akili na ‘Mapromota’ waliomleta, matokeo yake alifikia hadi kukosa pesa ya kujikimu pamoja na kulipia Visa yake kuwa mushkeri.

Nguli huyo ‘alifulia’ hata nauli ya kumrejesha kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hakuwa nayo.Bahati njema ilikuwa upande wake kwa kuwa alifanikiwa kurejea kwao baada ya kupewa ‘lift’ katika ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC), aliyokuwa ikizindua safari zake kati ya Dar es Salaam na Lubumbashi nchini DRC.

“Kimya kingi kina mshindo mkuu” usemi huu ulijionesha wazi kwa gwiji hilo lililosubiriwa na wapenzi kwa kipindi kirefu hadi mwaka 2006, ndipo alipotoka na album yake mpya yenye Lebo ya Nzombo le Soi.

Baada ya miaka minne mingine alifyatua CD yake yenye Lebo ya Pur Encore mwaka 2010.Mwaka 2012 Defao kwa bahati nzuri alirudi uliongoni akiwa na album ya The Undertaker.Defao pamoja na kuadhimisha miaka yake 60, amekuwa kimya hadi leo bila ya kutoka na album nyingine mpya licha ya kushughulika na muziki akiwa katika nchini kwao DRC na Ulaya.

Mwanamuziki huyo mwaka jana 2018, alikuwa akisikika akifanya maonyesho katika jiji la Nirobi nchini Kenya.
GENELA DEFAO (WA PILI KUSHOTO),AKIWA NA WAANDISHI WA HABARI WA TANZANIA, WAKIWA SAFARINI KWENDA LUBUMBASHI KONGO. WAKWANZA KUSHOTO NI MOSHY KIYUNGI, MAKARANGA NA VEDASTO MSUNGU.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images