Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live

Ujenzi majengo katika Mji wa Serikali mjini Dodoma wakamilika kwa asilimia 99

$
0
0
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Ujenzi wa majengo ya Wizara kwenye Mji wa Serikali uliopo Ihumwa jijini Dodoma umekamilika kwa asilimia 99 ambapo wizara 20 zinatarajia kuhamia ifikapo mwezi Aprili mwaka huu.
Akizungumza leo mara baada ya kufanya ziara  katika mji huo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa ujenzi kwenye mji huo umekamilika kwa asilimia 99, aidha amezitaka wizara hizo kukamilisha sehemu ndogo zilizobaki kabla ya mwezi Aprili mwaka huu, ikiwa ni baada ya kupata hati kutoka Wakala wa Ujenzi (TBA).
Waziri Mkuu Majaliwa amesema, “kwa ujumla kazi ni nzuri na imefanywa kwa umakini mkubwa, jukumu lililobaki ni kuhakikisha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wanaweka umeme wenye nguvu na wakutosha, barabara zote zipitike kwa urahisi, na lazima kuwepo na huduma muhimu ikiwemo kituo cha afya, hoteli, stendi ya daladala na maduka ili watumiaji wa majengo haya waweze kupata huduma hizo”.
Vile vile ameagiza Makatibu Wakuu wa wizara zote kuhakikisha wanajenga uzio, ikiwa ni  sambamba na kuweka mageti yatakayowarahisishia wananchi kufikia ofisi hizo kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali. Huku akiwapongeza TBA, pamoja na  wakandarasi mbalimbali walioshiriki katika ujenzi huo.
Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa aliongeza kuwa “watanzania wengi wamenufaika kwa kuwepo kwa miradi hii, kwa vile ujenzi huu  na mingine inayoendelea imesaidia kupanua wigo wa fursa kwa Watanzania”.
Naye, Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Wazee na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema kuwa huduma mbalimbali zinaendelea kuimarishwa katika mji huo wa Serikali ikiwemo ujenzi wa barabara ambapo Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARULA) na Halmashauri ya Jiji wanaendelea na ujenzi wa kilomita 18 kati ya kilomita 39 zi;izopo  ndani ya mji huo wa Serikali.
Maeneo mengine ni usafiri na mgahawa, ambapo Halmashauri zimeshaanza zoezi la kukamilisha viwango vya nauli kutoka maeneo mbalimbali kuelekea mji wa  Serikali.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Wazee na Wenye Ulemavu, Mhagama, alisema kuwa “tayari Wizara ya Fedha imeshatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya pamoja na ununuzi wa gari la wagonjwa litakalotoa  huduma kituoni hapo”
Kwa upande wake, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alisema kuwa wizara yake kupitia TANESCO itafunga transfoma yenye ukubwa wa KVA 300 katika mji huo wa Serikali  ili kuweza kutoa huduma ya umeme kwa wizara mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupitisha nyaya za umeme ardhini badala ya nyaya hizo kuonekana juu ya ardhi.

Ujenzi wa Mji wa Serikali ni moja ya agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambapo alizitaka wizara zote kujenga ofisi zake katika mji huo na kuhamia mapema iwezekanavyo ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma zote za Serikali katika eneo moja.
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akizungumza na uongozi na watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (hawapo pichani) baada ya kukagua ujenzi wa jengo la wizara hiyo kwenye mji wa Serikali Ihumwa, Dodoma. Waziri Mkuu Majaliwa amewapongeza watumishi na viongozi wa wizara hiyo kwa kukamilisha ujenzi ndani ya muda. Pembeni ya Waziri Mkuu ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa na katikati ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Francis Michael.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenister Mhagama, akiwasilisha ripoti ya mwenenendo wa ujenzi wa majengo mbalimbali ya wizara kwenye Mji wa Serikali Ihumwa, Dodoma mbele ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa. Leo Waziri Mkuu Majaliwa amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa majengo hayo na ameeleza kuridhishwa na hatua iliyofikiwa.


 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisikiliza maelezo kutoka kwa msimamizi wa ujenzi wa majengo ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizara ya Katiba na Sheria kwenye eneo la Mji wa Serikali Ihumwa, Dodoma wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo leo. Waziri Mkuu amempongeza mkarandasi SUMA JKT kwa kukamilisha majengo ya wizara hizo tatu ndani ya muda kama ilivyoainishwa kwenye mkataba wa ujenzi.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akifurahia jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya wizara mbalimbali kwenye Mji wa Serikali Ihumwa, Dodoma. (Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 27.03.2019

AFRICAN COURT ON HUMAN AND PEOPLES’ RIGHTS TO DELIVER SIX JUDGMENTS

$
0
0
Arusha, 26 March 2019: The African Court on Human and Peoples’ Rights will deliver five Judgments on Thursday (28 March 2019) and one on Friday (29 March 2019) at the close of its four-week sitting of the 52nd Ordinary Session at its Seat in Arusha, Tanzania.

The Judgments scheduled for 
Thursday are on the following matters:

1. Application 009/2015 – Lucien Ikili Rashidi v. United Republic of Tanzania  http://www.african court.org/en/images/Cases/Case%20Summaries/Website%20summary.%20Ikili%20Rashidi.pdf 

2. Application 025/2016 - Kenedy Ivan v. United Republic of Tanzania

3. Application 042/2016 - Collectif des Anciens Travailleurs du Laboratoires ALS v. Republic of Mali 

4. Application 016/2017 - Dexter Eddie Johnson v. Republic of Ghana


Judgment scheduled for 
Friday is on the following matter:

1. Application 013/2017 - Sebastien Germain Ajavon v. Republic of Benin 

The delivery of the Judgments will begin at 10H00 (East African Local time) and will be live streamed via the following link: 

1.  The Court is composed of eleven Judges, nationals of Member States of the African Union elected in their individual capacity. 
2. The Court meets four times a year in Ordinary Sessions and may hold Extra-Ordinary Sessions.
Further information on the Court can be obtained from the Court’s website 

atwww.african-court.org.

Asks 15-year-old Abby Chams... Can teenagers make a change?

Tanzania’s new e Passport shine at Banknote and ID Excellence Prestigious Awards in Malta

$
0
0
Reconnaissance, the organisers of High Security Printing EMEA, revealed the 2019 winners of the Regional ID Documents and Banknotes of the Year awards at a special ceremony during the conference in Malta on 26 March 2019.
EMEA-2019-Awards
The ID document awards, of which there are three, recognise outstanding achievement and technical sophistication of a document and promote the best in system infrastructure and implementation of a government passport or national identity card scheme.
The banknote awards, meanwhile, recognise excellence in design, technical sophistication and security of a banknote or banknote series, and again there are three categories – Best New Series, Best New Banknote and Best New Commemorative Banknote.
Tanzania’s new ePassport, Estonia’s new national eID card and the new EU Visa project were the winners of the ID awards. Switzerland’s new banknote series, the new Bulgarian 100 lev and South Africa’s commemorative series celebrating the centenary of Nelson Mandela’s’ birth have all been recognised as best in their class in the banknote awards.

Best New ePassport

Tanzania-passport
The first award went to the Immigration Department of the Ministry of Home Affairs of Tanzania for the new Tanzanian ePassport.
Tanzania has moved from an MRP booklet to a phased implementation of a complete eImmigration system in January 2018, with the first stage of the project, including the issuance of the first ePassports, being only four months from contract award to completion.
The new ePassport features a polycarbonate datapage incorporating laser engraving technology, an optically variable feature and positive and negative embossing incorporating an MLI lens. The datapage also carries an ICAO compliant secure RFID microcontroller chip and operating system with ICAO LDS 1.7 as well as BAC, EAC and the latest SAC/PACE security mechanisms, certified up to EAL6+.
The design of the booklet captures local themes and cultures across the visa pages, datapage and end papers, helping to engender a sense of national pride in the carrier.
Notable features include end papers with duplex security patterns and rainbow split duct printing, and two colour Intaglio printing incorporating a latent image and an optically variable print feature. Among the security features on the visa pages are rainbow split duct printing in both visible and invisible inks, Foredge registration feature and hidden page identifiers.
One of the benefits of the new ePassport solution is that the holder can have an emergency passport on their smartphone, if their passport is stolen or lost in another country. This passport, verifiable electronically by the embassy, allows the traveller to obtain the necessary document to return home or request a replacement passport without the need for further online checks, filling out forms or other time-consuming tasks. The mobile emergency passport has been developed using HID’s mobile goID solution. The new ePassport will, at the same time, make travel easier for the country’s citizens, through the use of automated border control stations.
The passport booklet is one component of an end to end system solution to support the enrolment, adjudication, personalisation, issuance and authentication of the ePassport, plus border control and eVisa systems.
The transformational project has been instigated by the Department of Immigration of the Ministry of Home Affairs, Tanzania and delivered by HID Global, their local partner Softnet with booklet manufacture by DLRS Security Concepts (now Smurfit Kappa Security Concepts) and design by Absolute Graphics.
The award was presented to Tanzania’s Commissioner of Immigration for Passports and Citizenship Gerald Kihinga and Henry Mkuzi of HID Global.

Best New National eID Card

eID-Card-Estonia
The second award went to the Police and Border Guard Board of Estonia, part of the Ministry of Interior for the new national eID card.
The new national eID cards with upgraded design and security features in December 2018. It took 18 months to prepare. Both internal and external experts were consulted when drawing up the new card’s design and choosing the security elements including the Estonian Forensic Science Institute and Enterprise Estonia.
The new cards utilise Estonia’s own font and elements of its brand, and feature a colour photo, a transparent window and an invisible secondary photograph that will only appear when viewed from an angle. One new detail is the inclusion of a QR code, which will make it easier to check the validity of the ID card.
The new eID card also integrates a new chip that allows contactless use in the future, once service providers start offering corresponding solutions – validating public transport trips for example. The new chip will retain the traditional interface and can still be used in ID card readers. The chip fits more information and is compatible with new applications, like electronic public transport tickets or other kinds of electronic certification. Giving and reading digital signatures will be possible using the traditional interface only.
Estonia is considered to have one of the most highly-developed national ID card system in the world. Much more than a legal photo ID, the mandatory national card also provides digital access to all of Estonia’s secure eServices. Nearly 5,000 separate eServices enable people to run their daily errands without having to get off their computers at home. They can enter into agreements, sign documents, submit various applications, use digital channels and means to communicate with various state authorities and service providers and so on.
The chip on the new card carries embedded files, and using 2048-bit public key encryption, it can be used as definitive proof of ID in an electronic environment. Thanks to the ID card, Estonia has one of the world’s most advanced digital signature systems. As of January this year, there are approximately 1.3 million ID cards being used in Estonia, which constitutes nearly 98% of the entire population of the country.
The award was presented to Eliisa Sau, Chief Expert of the Police and Border Guard Board of Estonia and Michal Grochowski, Area Sales Director at IDEMIA who supply the new document.

Best New ID Document


The final award went to Germany’s Bundeskriminalamt, the Federal Criminal Police Office and Bundesdruckerei, the country’s state printer and manufacturer of banknotes, passports and ID cards for the new EU Visa sticker project.
As part of the EU Commission Action Plan to strengthen the EU response to travel document fraud, all EU member states will be introducing the new EU Visa sticker in 2019. The project was a result of the collective work done at EU Article 6 Committee and associated subgroup with regard to the development of an improved uniform format visa.
Following a contest and the presentation from each member state and subsequent voting on points for seven different categories regarding the visa (Substrate, DOVID, Features, Personalisation etc), Germany was chosen as having the best concept and it had also won six of the seven categories outright.
It was decided by the member states not just to write the technical specification but also to improve the quality of the Visa Stickers and limit variation by running a Development Project to produce a Zero Series/Pilot Project – which would then be used as the baseline for the member states and the producers to adhere to. The project, funded by the EU, was awarded to and run by the Bundeskriminalamt and the Bundesdruckerei together.
The development project lasted about 11 months and was finished within time and on budget with a successful outcome and the issuance of a “Best Practice” Visa Kit and Technical Specification for 31 EU member and associate States. The Visa Kit and Technical Specification would then also be used as Best Practice for the basis of the subsequent eResidence Permit Card Project.
The Visa development project involved the integration of some additional ideas of the other member states as well, in order to create a project involving all concerned – which created team spirit. Suggestions came from a number of countries including Italy, Hungary and the UK. The approval at the production stage also involved an invitation for the subgroup to come to Berlin to sign off the progress.
This collaboration increased the level of the security features, the security concept specification, the design and quality of the document. The new sticker integrates improved chemical sensitisers, high level security background design, completely re-designed DOVID with improved features, improved intaglio inks and latent images, rip cuts and advanced UV elements. The sticker also has a “quiet zone” reserved for a 2D barcode in order to upgrade and secure the personalisation of the sticker, which is seen as a good next step to incorporate digital security into the security document world.
The project is a good example of the concept of Europe working together on an issue which concerns all Member States driving through the necessary factors for the good of all whilst taking into account the compromises needed and involved in successful partnerships.
The award was presented to Dr. Anna Wandschneider of Bundeskriminalamt, Duncan Faulkner of Bundesdruckerei and Francis Deschrijvere of the European Commission.

Best New Banknote Series

SNB_9S_BN1000_pack_020_web
The award for the Best New Series went to the Swiss National Bank for the ninth banknote series, entitled ‘The Many Facets of Switzerland’, which has broken new ground in terms of design and security.
Each note in the new series depicts a typically Swiss characteristic (creativity, scientific expertise, communication etc), which is illustrated via an action, a Swiss location and various graphic elements.
The respective themes are time for the CHF 10, light for the CHF 20, wind for the CHF 50, matter for the CHF 200 and, for newly-issued CHF 1,000, language. The CHF 100, which will be released this autumn to complete the series, will have water as its theme, reflecting Switzerland’s humanitarian tradition.
The banknotes have been designed and printed by Orell Füssli Security Printing on a three-layer banknote substrate – Durasafe® – provided by Landqart. The substrate consists of two outer layers of cotton paper and a polymer core for reinforcement that provides greater stability and durability than traditional banknote papers, as well as variety of transparent and semi=transparent windows.
One of the main security features is the innovative two-colour KINEGRAM® Volume stripe, combined with a partially metallised KINEGRAM provided by KURZ incorporating the denomination numbers in two colours (red and green)., a map of Switzerland, its language region and the names of all the Swiss cantons.
Another key feature is the SICPA’s SPARK® feature printed as a shimmering globe.
Other features include a window, two watermarks, a see-through feature, UV and IR features, microprint, intaglio, security thread, security fibres and Microperf®.
In addition, the new banknotes have been designed to assist the visually impaired to distinguish between the various denominations via a series of short, raised lines along the notes’ long edges.
The award was received by Peter Kuenzli of the SNB.

Best New Banknote – Bulgaria

Bulgaria
The award for the Best New Banknote was made to the Bulgarian National Bank for the new 100 lev, the first note in the country’s new series which was issued last December. While the design themes and colours of the existing series have been retained, the new series is being upgraded with a variety of innovate new features.
The Bulgarian National Bank has earned a reputation for innovation in banknotes, having been the first adopter of a number of new security features in the past. The 100 leva is no exception.
It features a dynamic RollingStar® LEAD stripe, synchronised to a dynamic ‘rectangular checkered field’ (like a moving chessboard) in a RollingStar® security thread (both technologies developed by Louisenthal) and to the SPARK® Live feature from SICPA.
Other security features of the paper note (which is post-print varnished for durability with Oberthur’s Fiduciare’s Securicoat Ultra™) include new tri-coloured paper embedded security fibres which can be seen in white, green, red under UV light, microprint, and a three-dimensional watermark portrait of Aleko Konstantinov (the Bulgarian writer and social activist) that is the combined with the highlight inscription ‘BNB’, visible on both sides in transmission view.
The note is intaglio printed and the use of the intaglio portrait of Aleko Konstantinov, together with the portrait in the watermark and LEAD stripe, is designed for ‘cross-referencing’, making it easy to check the authenticity of the notes.
In addition, the notes feature Simultouch ™, also from Oberthur Fiduciaire, namely intaglio-printed thick and thin lines along the short sides as an aid for the visually-impaired. And they include its interactive UV feature Avalon ™.
The whole project represents an example of impressive collaboration between the BNB, Oberthur Fiduciaire AD (the printworks in Sofia jointly owned by BNB and Oberthur Fiduciaire) and Papierfabrik Lousienthal.
The award was presented to Stefan Tzvetkov of the BNB.
Commenting on the award, Georgi Simeonov, Managing Director of Oberthur Fiduciaire AD, said: ‘OFAD sends its congratulations to the Bulgarian National Bank for this great award and is proud to have played its part in designing and producing the new 100 Lev which combines some of the most modern printed banknote security features as well as showcasing Bulgaria ‘s 21 century outlook and perspective.

Best New Commemorative Banknote

Rand Mandela series
The third award, for the Best New Commemorative Banknote, was made to the South African Reserve Bank (SARB) for the commemorative series commissioned to celebrate the centenary of the birth of Nelson Mandela. This is the first time a complete series of commemorative notes have been issued.
The new notes (in denominations of R10, R20, R50, R100 and R200) were launched last July at a special ceremony at the historic Freedom Park in Pretoria, and were issued on 18 July (Mandela’s birthday).
The front of the commemorative notes is the same as the existing series, with Nelson Mandela’s portrait and watermark, colour shifting thread and a large denomination numeral in either OVI or SPARK depending on the denomination.
On the reverse, however, the images of the iconic Big 5 animals have been replaced with different scenes and accompanying themes on telling the story of Mandela’s life from young boy to president, marking key passages and historic milestones.
The R10, for example features the village where he was born (Birth), and the R20 the home in Soweto where he began both his career and his campaign against apartheid (Life). The background to the R50 is the place where he was taken prisoner (Capture), and the R100 Robben Island, where he was incarcerated for 18 of the 27 years he spent in captivity (Struggle). The highest denomination R200 depicts the Union Building where he was inaugurated as President in 1994 (Destiny).
The notes were designed by De La Rue and printed by the South African Banknote Company. Deon van Zyl of the latter collected the award on behalf of the SARB.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MACHI 28, 2019

SERIKALI YAZINDUA MFUMO WA MATIBABU KWA MTANDAO

$
0
0
Na WAMJW - DOM

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo imezindua Mfumo mpya wa utoaji huduma za afya kwa njia ya mtandao utaosaidia kurahisisha utoaji wa huduma za Afya ikiwemo huduma za matibabu ya kibingwa kwa wananchi.
Uzinduzi huo umefanyika leo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 7 wa masuala ya Sayansi na Afya uliowakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi za Afrika Mashariki kujadili kwa pamoja juu ya njia ya kufanikisha malengo ya Afya ya umoja wa mataifa.
Mhe. Samia alisema kuwa nchi za Afrika Mashariki zikijikita katika utoaji huduma kwa mfumo huo kwa ushirikiano wa pamoja, itakuwa ni njia sahihi kwa nchi hizo kufikia malengo ya milenia na huduma za afya kwa wote.

“Tunapaswa kufikia malengo tuliyojiwekea kama bara la Afrika na nchi za Afrika mashariki, mkutano huu si tu wa watafiti kutoka Afrika Mashariki bali ni muhimu kwa wadau wote katika sekta ya afya tufanye kazi kwa pamoja kukamilisha malengo haya,” alisema Mhe. Samia.

Mhe. Samia aliendelea kusema kuwa tiba mtandao itawezesha na kuongeza ufanisi katika kufanya uchunguzi, utoaji wa tiba na dawa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali, hivyo kurahisisha utoaji huduma za Afya kwa Wananchi.

Aidha, Mhe. Samia Aliongeza kuwa tiba mtandao itapunguza gharama za wagonjwa na wanaowahudumia kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za matibabu katika Vituo vyakutolea huduma na Hospitali.

Nae,Waziri wa Afya na mapambano dhidi ya VVU kutoka Burundi Dkt. Thaddee Ndikumana alisema programu hiyo itakuwa ikitumika kwa nchi za Afrika Mashariki itakuwa chachu katika kuleta Mapinduzi ya utoaji huduma za Afya kwa Wananchi wa Afrika Mashariki.

 “wananchi wa Burundi watakuwa wanaweza kupatiwa matibabu na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa nchini kwao bila kuja Dar es Salaam hiyo ni kitu muhimu tutakuwa tunabadilishana uzoefu raia wa Burundi walikuwa wanakuja kila siku sasa safari zitapungua, watabaki Bunjumbura na huduma watapata.” Amesema Dkt. Thaddee Ndikumana

Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa daktari atakuwa na uwezo wa kuwasiliana na madaktari wenzake katika mtandao na madaktari bingwa wa nchi nzima wanaona lile tatizo jambo litalosaidia katika kutoa huduma bora kwa Wananchi wan chi za Afrika Mashariki.
Waziri Ummy Mwalimu, aliendelea kusema kuwa tayari Tanzania ilishaingia katika mfumo wa matumizi ya kidijitali katika utoaji wa huduma kwenye maeneo mengi, na umekuwa na msaada mkubwa sana katika Sekta ya Afya.

“Nchini Tanzania miezi mitatu iliyopita madaktari walianzisha mfumo mawasiliano kupitia dijitali ambao unawawezesha madaktari bingwa kuwasiliana moja kwa moja na madaktari waliopo pembezoni na umeweza kuokoa maisha ya kinamama sita ambao walikuwa wanajifungua,” amesema Ummy.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Nimr Profesa Yunus Mgaya alisema kuwa mfumo huo utapunguza gharama za utoaji wa huduma za afya na itaongeza ufanisi katika utendaji wa kazi wa wahudumu wa afya.

“Italeta utaalamu wa hali ya juu wa kibingwa katika maeneo ambayo hauwezi kufikika kwa mfano wataalamu wanaweza kuwepo Muhimbili na mgonjwa akawa mbali ambako hapafikiki kirahisi na hiyo ni msaada mkubwa sana kwa kuwa hizi huduma kama ingetakiwa wataalamu wawepo kule gharama yake ingekuwa kubwa sana,” alisema Prof. Mgaya.

Nae, Waziri wa Mambo ya Nje, Palamagamba Kabudi amesema kuwa nchi ya Tanzania itanufaika zaidi katika mfumo huo katika kulifikia lengo namba tatu la malengo ya milenia, pia itasaidia kufanikisha lengo la afya kwa wote ifikapo 2030.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akibofya batani, ikiwa ni ishara ya kuzindua Mfumo mpya wa utoaji huduma za afya kwa njia ya mtandao,  katika Mkutano wa 27 wa masuala ya Sayansi na Afya uliowakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi za Afrika Mashariki katika Kituo cha mikutano ya Kimataifa cha J.K Nyerere Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akinyanyua juu kitabu cha Mwongozo wa Mfumo mpya wa utoaji huduma za afya kwa njia ya mtandao utaosaidia kurahisisha utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi. Wakwanza kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje, Palamagamba Kabudi na Watatu kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akitoa hotuba yake katika  Mkutano wa 27 wa masuala ya Sayansi na Afya uliowakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi za Afrika Mashariki katika Kituo cha mikutano ya Kimataifa cha J.K Nyerere leo jijini Dar es salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Wakulia) akipata maelekezo, wakati alipita katika mabanda ya maonesho baada ya kumaliza Mkutano wa Kimataifa wa 7 wa masuala ya Sayansi na Afya uliowakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi za Afrika Mashariki, mkutano huo umefanyika katika Kituo cha mikutano cha Kimataifa cha J.K Nyerere Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  (watatu kutoka kulia)akipata maelekezo katika banda la (TFDA) wakati alipita katika mabanda ya maonesho baada ya kumaliza Mkutano wa Kimataifa wa 7 wa masuala ya Sayansi na Afya uliowakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi za Afrika Mashariki, mkutano huo umefanyika katika Kituo cha mikutano cha Kimataifa cha J.K Nyerere Jijini Dar es salaam.

 Wadau wa masuala ya Afya, kutoka nchi mbali mbali wakifuatilia ufunguzi wa wa mkutano wa 7 wa masuala ya sayansi na Afya uliowakutanisha mawaziri wa Afya kutoka nchi za Afrika Mashariki, mkutano huo ulifunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (Hayupo kwenye picha)

PASIPOTI YA TANZANIA KIDEDEA KWA UBORA DUNIANI

$
0
0
Passport ya kielekroniki ya Afrika Mashariki inayotolewa na Tanzania imeshinda tuzo ya ubora na usalama duniani kwa mwaka 2019. 
Tuzo hiyo hutolewa na Taasisi ya Kimataifa ya kupima ubora na usalama wa nyaraka zikiwemo Pasipoti, vitambulisho, noti za fedha na nyinginezo  iitwayo EMEA. Hongera Idara ya Uhamiaji ya Tanzania kwa kazi nzuri.

WAZIRI MHAGAMA AWAHIMIZA VIJANA KUWA WAZALENDO KWA NCHI YAO

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akikabidhi Bendera ya Taifa kwa vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akifurahia jambo wakati wa kuwaaga vijana kabla ya kuanza zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali, Uongozi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akivishwa skafu na vijana wa skauti mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe. John Palingo mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, Mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Viongozi na wakazi wa Marangu wakati wa hafla ya kuwaaga vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba akieleza jambo kwa vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi akufafanua jambo kuhusu ushiriki wa vijana hao watakaopanda Mlima Kilimanjaro, Machi 26, 2019.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Betrita Loibooki (aliyesimama kulia) alipokuwa akiwasilisha taarifa fupi kuhusu Hifadhi hiyo. (Kushoto aliyekaa) ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba.
Baadhi ya watumishi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara ya kuwaaga vijana hao.
Vijana wanaotarajiwa kupanda Mlima Kilimanjaro wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama kabla ya kuanza safari ya kupanda mlima huo.PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)





……………………..


Na; OWM – KVAU, Kilimanjaro


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewahimiza vijana kuwa wazalendo na kuithamini nchi yao.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga vijana waliopanda Mlima Kilimanjaro jana tarehe 26 Machi, 2019 Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni kuaadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Waziri Mhagama alisema kuwa, Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere alikuwa kiongozi mzalendo kwa nchi yake na alijali utu na usawa, hivyo ni vyema vijana na vizazi vijavyo wakarithishwa falsafa za Baba wa Taifa.

“Vijana mna kila sababu kuyaenzi matendo ya Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere na Mhasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Abeid Amani Karume kwa vitendo kwa kuwa ninyi ndio nguzo ya Taifa na mnaelewa vema tulipotoka, tulipo na tunapoenda,” alisema Mhagama.Aliongeza kuwa, Viongozi hawa hawakuwa wabinafsi kwa kujilimbikizia mali na hawakubagua mtu kwa rangi wala kabila bali walijenga Taifa na kudumisha amani na moja.

Aliendele kwa kuwapongeza vijana kwa azma yao ya kuenzi historia na mazuri yaliyofanywa na viongozi hao kwa kupanda mlima Kilimanjaro na kuwatakia baraka waende na kurudi salama.“Kitendo hiki ni cha kishujaa na uzalendo wa hali ya juu kwa Taifa ikiwa ishara ya kumuenzi Baba wa Taifa,” alieleza Mhagama

Aidha Waziri Mhagama alitoa rai kwa vijana kuwa wazalendo na kuwasihi wafanye kazi kwa bidii ili kujenga Taifa kupitia uchumi wa viwanda utakao ifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.Alifafanua kuwa uzalendo lazima ujengwe sambamba na ujenzi wa uchumi wa Taifa, ulinzi na usalama wa Taifa na utunzaji wa tunu za Taifa.

Pamoja na hayo, aliwapongeza na kuwashukuru Viongozi wa Mkoa wa Songwe na Lindi pamoja na uongozi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) kwa ushirikiano mkubwa na Ofisi yake katika kuwashirikisha vijana kwenye suala hilo.Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba alisema kuwa tukio hili ni muhimu kwa vijana kutambua historia na mchango wa Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere katika Taifa.

“Tumieni fursa hii kupitia vitabu mbalimbali vya kihistoria ili mjifunze mipango, mwenendo na malengo ya Baba wa Taifa itawasaidia na kuwajengea nafasi nzuri ya kujitambua na kuelewa historia ya Taifa,” alisema Warioba.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Bw. James Kajugusi alieleza kuwa Baba wa Taifa alianza harakati za kulikomboa Taifa akiwa kijana na aliendelea kufanya hivyo kwa kuwa hamasisha vijana kujenga Taifa lao baada ya kupata uhuru.

BABA MZAZI WA JOHN BUKUKU AZIKWA KIJIJI CHA IWEZI,MBOZI MKOANI SONGWE

$
0
0
3
Baadhi ya wanakijiji pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa wamebeba jeneza la Marehemu Marehemu Angolwisye Mwambande Bukuku(101) tayari wakiupeleka kwenye makazi ya milele
4
John Bukuku ambaye ni Mmiliki wa Blogu ya Fullshangwe ,Baba mzazi wake Marehemu Angolwisye Mwambande Bukuku(101), aliyefariki usiku wa kuamkia , Machi 24, 2019.
2
Jana alihifadhiwa katika nyumba ya milele katika kijiji cha Iwezi,wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria mazishi hayo wakiwemo viongozi wa CCM mkoa wa Songwe pamoja na mkoa wa Mbeya.
1
index
John Bukuku ambaye ni Mmiliki wa Blogu ya Fullshangwe akiwa na baadhi ya ndugu zake baada ya kumaliza shughuri za kumzika ,Baba yake mzazi Marehemu Angolwisye Mwambande Bukuku(101), aliyefariki , Machi 24, 2019. na kuzikwa jana Machi 26 katika kijiji cha Iwezi,wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria mazishi hayo wakiwemo viongozi wa CCM mkoa wa Songwe pamoja na mkoa wa Mbeya.
Bwana alitoa na sasa ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Ameen.

VIJANA TUKILINDA AMANI TUKAWA WAMOJA MAENDELEO YATAKUJA - RC GAGUTI

$
0
0

Anaandika Abdullatif Yunus - Kagera.

Katika kuhakikisha Amani na Usalama Wa Taifa la Tanzania iliyoasisiwa na Viongozi waliotangulia inazidi kudumishwa, Vijana Mkoani Kagera wametakiwa kuwa wazalendo, wamoja, wabunifu, na wajasiliamali ili kuondokana na Umaskini.

Akizungumza na Mamia ya Waendesha pikipiki Mkoani hapa wakati Wa Droo ya Kupanga Timu za Vijana hao ambao Jumamosi ijayo wanatarajia kuanza mashindano ya Ligi ya mpira Wa Miguu maarufu kama JPM BODABODA CUP, Mkuu Wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti mnamo 26, Machi 2019 amesema.

Vijana wana dhima na jukumu kubwa la kulinda Amani ya Nchi yetu kupitia shughuli wanazozifanya kikubwa ikiwa ni matumizi bora ya Vyombo vya Moto, na kupitia mashindano hayo ya JPM BODABODA CUP Vijana wataelimishwa zaidi masuala ya Usalama barabarani.

Kwa upande Mwingine Mh. Gaguti amekaririwa akisema kuwa Tayari Serikali Mkoani Kagera imekwishatenga Zaidi ya Milioni 20 kwa ajili ya Vijana kujiendeleza katika shughuli za Ujasiliamali, ambapo anetumia fursa hiyo kuwataka Vijana Wa bodaboda kuimarisha Vikundi vyao kwa ajili ya kupatiwa fedha ambazo zitawasidia kufanya shughuli nyingine za uzalishaji.

Mashindano ya JPM CUP yanayoratibiwa na Ofisi ya Mkuu Wa Mkoa Kagera kwa Kushirikiana na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama barabarani yanaanza kutimua vumbi rasmi Jumamosi ya Tarehe 30, Machi kwa kuzishirikisha Timu 16 za Waendesha Bodaboda Manispaa ya Bukoba, huku zawadi zikitajwa kuwa ni pamoja na Kombe kwa Washindi Tatu Bora, pamoja na pesa Taslimu Sh. Milioni 6.
Picha ni RC Gaguti akionesha uwezo wake wa kumiliki mpira wakati wa kuelekea kuanza kwa mashindano ya JPM BODABODA CUP 2019 KAGERA, yanayoratibiwa Chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Jeshi la Polisi Kitengo Cha Usalama Barabarani.

 Sehemu ya Vijana wa Bodaboda walohudhuria Uwanjani Kaitaba katika Shughuli ya Kupanga makundi ya Timu zitakazoshiriki Ligi ya Kombe la JPM 2019 KAGERA.
 Mmoja kati ya Viongozi wa Timu za Waendesha pikipiki akiokota karatasi ya Droo ya Upangaji Timu na Makundi katika Mashindano ya JPM BODABODA CUP 2019 KAGERA.
 Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti akizungumza na Vijana Waendesha Bodaboda Uwanjani Kaitaba, katika kuelekea Kuanza kwa Mashindano ya JPM BODABODA CUP Jumamosi ya wiki hii.

JPM amteua Dkt. Richard Faustine Sambaiga kuwa Mwenyekiti wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali

HESLB yaweka mikakati ya utoaji elimu kwa wanafunzi wa kidato cha sita.

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) iko katika mkakati wa utoaji wa elimu kwa wanafunzi wa kidato cha sita ili kuweza wanafunzi hao waelewe namna ya kujaza fomu kwa usahihi wakati wa kuomba mikopo katoka bodi hiyo.

Wakizungumza na wanafunzi katika shule za Sekondari za St.Anthony, Kisutu na Zanaki wamesema kuwa wakati wa kuomba mikopo wanafunzi wamekuwa wanafanya makosa ambapo Bodi imeona kuna umhimu wa kuwapa elimu wanafunzi.

Afisa wa Bodi hiyo Daud Elisha amesema elimu wanayoitoa kwa wanafunzi ni kutokana na kuwepo kwa makosa baadhi ya wanafunzi wakati wa uombaji wa mikopo.

Elisha amesema lengo la bodi kuona wanafunzi wa kidato cha sita wanapata uelewa mapema namna ya kuomba mikopo ya bodi kwa vigezo vilivyowekwa.

Aidha amesema elimu wanayoitoa ni mwendelezo kwa nchi nzima katika kuhakikisha kila mwanafunzi anajua kinagaubaga kuhusiana na bodi inavyofanya kazi katika utoaji mikopo kwa wanafunzi wahitaji wa kitanzania.

"Tumedhamiria kutoa elimu kwa wanafunzi wa kidato cha sita pindi wanapohitimu na kujiunga na elimu ya juu wakiomba mkopo wa wasiwe na changamoto ya kufanya ashindwe kuomba mkopo huo"amesema Elisha.

Nae Afisa Mikopo wa Bodi Christina Chacha amesema kuwa licha ya kuwapa elimu ya wanafunzi kuhusiana na uombaji mkopo pia wanatoa elimu ya namna ya kurejesha mkopo huo kwa wale watakaonufaika.

Amesema mkopo wanayotoa kwa wanafunzi kwa ajili ya elimu ya juu lazima ilipwe kwa ajili wengine kukopeshwa.

Aidha maswali ya wanafunzi wengi yalijikita endapo mwanafunzi atapohitimu shahada yake na akawa hajaajiriwa ataulipaje mkopo ambapo bodi hiyo imesema kukosa kazi sio kigezo cha kutolipa mkopo kwani elimu hiyo anaweza kufanya kazi nyingine na kuweza kulipa mkopo huo.
 Afisa wa HESLB Daud Elisha akizungumza na wanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari kisutu kuhusiana na vigezo vya uombaji mikopo katika bodi hiyo.
 Wanafunzi wa kidato cha sita  Shule ya Sekondari Zanaki wakisikiliza maelezo ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) .
 Afisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Daud Elisha akizungumza na wanafunzi wa kidato cha Sita Shule ya Sekondari Kisutu wakati Bodi hiyo ilipokwenda kutoa elimu ya masuala mbalimbali ya namna wanafunzi wanavyoweza kuomba mkopo katika Bodi hiyo.
 Afisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Christina Chacha akitoa maelezo kwa wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari Kisutu kuhusu vigezo vya uombaji mikopo na masharti ya mkopo.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari Zanaki Julieth Matowo akitoa maelezo wakati Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ilipokwenda kutoa elimu katika shule hiyo.
Wanafunzi wa Kidato cha Sita  Shule ya Sekondari Kisutu wakisikiliza mada kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)

JK AWAKA WATENDAJI CHUO CHA UDSM-MCHAS KUSIMAMIA NIDHAMU NA UBORA WA ELIMU ILI KIWE BORA BARANI AFRIKA

$
0
0
Na  Emmanuel Madafa.

MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Rais Mstaafu  awamu ya nne, Dk.Jakaya Mrisho Kikwete, amewataka watendaji wa chuo hicho kusimamia nidhamu na ubora wa elimu ili kiwe chuo cha mfano Barani Afrika.

Rais, Kikwete aliyasema hayo jana wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa chama na serikali, baada ya kutembelea na kukagua eneo la ardhi lililotengwa na serikali ya Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho Ndaki ya Afya na Sayansi Shiriki (MCHAS).

Amesema, shabaha yao nikuongeza nguvu ya wataalamu nchini, hivyo watendaji wanawajibu wa kusimamia kiwango cha elimu kinachotolewa hakishuki na kamwe hatapenda kuona watu wa bora liende wakikiendesha  chuo hicho.

“Sipendi kuona sifa hii ya elimu bora ikishukia Mbeya,  sipendi kuwaona watu wanaosema bora liende tu, madaktari ni watu muhimu sana kwani wanashindana na uhai wa mtu usiondoke, hivyo sitaki kuona mchezo ukifanyika,”alisema.

Aidha, akijibu agizo hilo Naibu Makamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Bonaventure Rutinwa, amesema kamwe hatakubali mtumishi au mwanafunzi yoyote kuharibu sifa ya chuo  chuo hicho ambacho kimebahatika kutoa viongozi wakubwa watano wa  Afrika.

“Chuo hiki kimewatoa viongozi wakubwa akiwemo Rais Magufuri, Rais wa Uganda Yower Kaguta Museven, Rais wa sasa wa Malawi, Bingu wa Mutarika, Rais Mstaafu wa Tazania awamu ya nne, Jakaya Kikwete, Rais wa awamu ya tatu Tanzania, Benjamin Mkapa na Rais wa zamani wa Sudan Kusini Dr. John Mabior,”alisema.
Rais mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha (UDSM ) akizungumza kwa msisitizo na uongozi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam  Ndaki ya Afya na Sayansi shiriki (UDSM -MCHAS) katika ziara yake ya kutembelea na kukagua eneo kitakapo jengwa Chuo katika eneo la Tanganyika Pekers nje kidogo ya Jiji la Mbeya .
 Rais mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha (UDSM ) akiwa na Shangazi yake Marehemu Efraemu Kibonde Elinelia Kibonde baada ya kumkuta akiwa katika foleni ya kusubiri Matibabu katika dirisha la dawa la Bima ya Afya katika Hospital  ya rufaa ya Kanda Mbeya .Picha na Emanuel Madafa Mbeya.
 Rais mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha (UDSM ) akiwa na wanafunzi wa udaktari kitengo  afya ya meno Chuo kikuu cha Dar es Salaam  Ndaki ya Afya na Sayansi shiriki (UDSM -MCHAS) katika ziara yake ya kutembelea na kukagua eneo kitakapo jengwa Chuo katika eneo la Tanganyika Pekers nje kidogo ya Jiji la Mbeya .

 Rais mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha (UDSM ) katikati walioketi akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam  Ndaki ya Afya na Sayansi shiriki (UDSM -MCHAS) mara baada ya kuzungumza nao .
 ais mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha (UDSM ) aliyeweka mkono mfukoni akiwa na uongozi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam  Ndaki ya Afya na Sayansi shiriki (UDSM -MCHAS) wakiwa eneo la  chuo katika ziara yake ya kutembelea na kukagua eneo kitakapo jengwa Chuo katika eneo la Tanganyika Pekers nje kidogo ya Jiji la Mbeya nyuma yake ni Mwenyekiti wa baraza la hicho Jaji Mstaafu Damian Luguva.

EMIRATES YATANGAZA OFA KWA WATANZANIA ZA KWENDA DUBAI

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SHIRIKA la Ndege la Emirates limeamua kutoa ofa kwa Watanzania kutembelea Dubai ambapo ofa itapatikana katika daraja la biashara na uchumi ikiwa ni pamoja na mzigo wa tatu kuwa bure.

Taarifa ya Emirates iliyoitoa leo Machi 28,2019 kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam imesema kuwa ofa hiyo ni kwa tiketi ya daraja la uchumi kutoka Dar es Salam hadi Dubai inaanza $ 489 na daraja la biashara ya kuanzia $ 1,499 na kwamba ofa hizo zitatolewa kwa muda maalum na tiketi zinatakiwa kukatwa kuanzia Machi 26, 2019 na Aprili 9, 2019, safari zitaanza kati ya kati ya 26 Machi 26,  2019 na Septemba 30, 2019. Gharama ya tiketi ni pamoja na kodi ya uwanja wa ndege.

Pia Emirates inatoa ofa ya mzigo wa tatu bure mpaka kilo 23 kwa daraja la uchumi na kilo 32 kwa daraja la biashara huku ikifafanua watakaopata ofa hiyo watapata nafasi ya kuitembelea Dubai  ambapo kuna jua mwaka mzima, kuna maduka makubwa ya kutembelea, fukwe nzuri na majengo ya kipekee kwa familia nzima. 

"Wageni wa Dubai wanaweza kufurahia maeneo mengine ya jiji kwa kuona na kutembelea Hifadhi ya Kijiji cha Kimataifa - tamaduni mbalimbali na maeneo ya shopping - pamoja na viwanja vya mandhari kama Wild Wadi Waterpark na IMG World of Adventures,"imesema taarifa hiyo.

Emirates imesema kuwa katika Mji wa Dubai watatoa aina mbalimbali za malazi kukidhi bajeti zote na katika ndege zote za Emirates, wateja wanaweza kufurahia muda wa burudani kwenye mfumo wa burudani unaoweza kushinda tuzo inayoitwa ICE, ambayo inaonesha zaidi ya  vituo 4,000 vya burudani na ya kusikiliza na ya kuona, kutoka kwenye filamu za hivi karibuni na mziki.

Pia vitabu vya sauti na michezo, pamoja na bidhaa zinazopendwa na wanafamilia na huduma kwa watoto, ikiwepo ni pamoja na michezo ya kupendezwa, chakula cha watoto na sinema,familia zitapewa kipaumbele katika kutumia gari ya kumsukumia mtoto akifika uwanja wa Ndege wa Dubai.

Imesisitiza pamoja na huduma nzuri za kuingia na bidhaa, wateja wataweza kupokelewa vizuri na wafanyakazi wa kimataifa wa Emirates ambao hutokana na zaidi ya mataifa135 na ambao wanazugumza lugha zaidi ya 60, huku wakifurahia vyakula vya kikanda na kimataifa, kwa kutumia viungo vingi, ikifuatana na aina mbalimbali za mvinyo na vinywaji vingine.

"Tunawaomba Watanzania kuchangamkia ofa hii ambayo imekuja wakati muafaka , kikubwa ni kuhakikisha wananunua tiketi za Emirates kulingana na muda ambao umetolewa wa kipindi cha ofa.Kwa anayehitaji mawasiliano tafadhali anaweza kutembelea tovuti yetu ya www.emirates.com/tz au tembelea ofisi za Emirates au wakala wa usafiri,"imesema taarifa hiyo.


FAHAMU ILIKOTOKA FM ACADEMIA

$
0
0
Na Moshy Kiyungi, Dar es Salaam
Bendi ya FM Academia ni kongwe katika tasnia ya muziki wa dansi humu nchini. Wanamuziki wa bendi hiyo kwa pamoja wanao uwezo mkubwa wa kumudu kuwaridhisha wapenzi na mashabiki wake popote wapandapo jukwaani kupiga muziki. Safu ya waimbaji na wanenguaji wake huwa kivutio kikubwa ndani ya ukumbi.

Baadhi ya watu yawezekana wakawa hawajuwi historia ya bendi hiyo iliyojizolea sifa lukiki ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu. Kwa miaka 16 mfululizo zimekuwa zikitajwa bendi zinazoshika nafasi tatu juu, moja wapo ni bendi ya FM Academia, iliyoitambulisha Tanzania kwa muziki wa dansi wa kizazi kipya.

Chanzo cha bendi hiyo ililianzia kwa Wasanii ambao walikuwa wakifanya kazi katika bendi ya MK Sound, iliyokuwa bendi dada ya MK Group, zikiwa chini ya umiliki wa ndugu ambao hivi sasa ndiyo wanaomiliki kampuni ya African Stars Twanga Entertainments (ASET) Kampuni hiyo hadi sasa inamiliki bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ MK Sound enzi hizo, ilikuwa chini ya uongozi wa ndugu wawili, akiwamo mwenyekiti wake wa ASET, Baraka Msiilwa, ambaye ni kaka wa Asha Baraka ´Iron Lady´ ambaye ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo.

Aliyekuwa rais wa bendi ya FM Academia, Nyoshi El Saadat, alianza kuelezea safari yao, ambapo aliwataja baadhi ya wasanii waliounda MK Sound kuwa ni pamoja na Credo, Liver Hassan, Depichu, Willy Amuli, King Dodoo Le Bouche, Bibie Alembi Moseka, Elystone Angai, Bakunde Desine, Lesave, John Mary na Louis 14.

Alisema, wakiwa na MK Sound, walipewa mkataba wa mwaka mmoja, 1991 hadi 1992. Baada ya mkataba kumalizika 1992, walitimka na kuipa kisogo bendi hiyo na kwenda jijini Nairobi nchini Kenya. Wakiwa jijini humo wakaunda bendi iliyofahamika kwa majina ya Bogoss Musica.

“Tukiwa Nairobi, tuliongeza wasanii katika nafasi za rapa, ambapo tulimchukua Sege Mwila. Katika safu ya waimbaji tulikuwa na Aristote Emerite, Jose Muzungu, Opicha Cloude, King Blase, Nicco Kasongo, Lwigi B52 na Balleaterve.”

Nyoshi alisema mwaka 1997, walirejea nchini huku wakiwa na baadhi ya wanamuziki, ambapo walichukuliwa na mfanyabiashara Felician Mutta. Wakiwa na Mutta, waliongezeka wanamuziki wengine ambao ni Mulemule FBI, wakaongeza safu ya wacheza shoo, wakamchukua mpiga kinanda, Saidi Comorean na rapa Papii Nguza Viking ‘Papii Kocha’.

Mwaka 1999, wakaingia mkataba na Felician Mutta, ambako alianzisha bendi ya FM International. Wakiwa chini ya Mutta, walitamba na albamu za ‘Khadija’, ‘Atomic’ na ‘Omba omba’ ambazo ziliwapa heshima mjini. Mara baada ya mkataba kumalizika, wakabadili jina la bendi kutoka FM International na kuwa FM Academia the Dream Team, wakampata mmiliki mpya kwa wakati huo ambaye ni Hussein Macheni.

Tangu kuanzishwa kwa bendi ya FM Academia mwaka 1997 bendi hiyo imepata kutoa albamu 10, huku ikileta changamoto mbalimbali kwa bendi nyingine za muziki wa dansi nchini ikiwemo Twanga Pepeta ambayo imekuwa ikisuguana na kunyang’anyana mashabiki na FM Academia kwa muda mrefu.

Albamu ya mwisho ya bendi hiyo ilizinduliwa Desemba 2013, huku ikiwa imebeba jina la Chuki ya Nini, katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mzalendo Pub Kijitonyama jijini Dar es Salaam, huku ikisindikizwa na bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa Musica.

Rais wa bendi hiyo Nyoshi El-Saadat aliwahi kuzitaja nyimbo za albamu hiyo mpya kuwa ni ‘Fataki’, ‘Otilia’, ‘Ndoa ya Kisasa’, ‘Neema’, ‘Dai Chako Ulaumiwe’, ‘Maisha’, ‘Madudu’, ‘Miraessa’ na ‘Intro’ ambazo zote zimeshatengenezewa video.

Meneja wa bendi hiyo Kelvin Mkinga alisema bendi hiyo imekumbana na misukosuko mingi kwa kipindi chote, lakini haikuwahi kutetereka. “Tumekutana na misukosuko mingi lakini mpaka leo FM Academia imekuwa ni bendi bora na imejitahidi kuwapa burudani mashabiki wake ipasavyo.” Alisema Mkinga.

Mkinga anasema bendi ya FM Academia ilizindua albamu ya kwanza ya ‘Hadija’ mwaka 1998 kisha ikafuatia ya pili iitwayo ‘Atomic’ mwaka 1999 na mwaka uliofuata wa 2000 bendi hiyo ilizindua albamu ya tatu iliyopewa jina la ‘Prison’.

“Tulizindua albamu tatu kwa mpigo. Lakini tulivyofika mwaka 2001 tulizindua nyingine pia hii ilikuwa ni katika kuhakikisha kwamba tunaufanya muziki wa dansi wa kizazi kipya ukubalike tofauti na ilivyokuwa mwanzo, pia muziki wetu ulikuwa na asili ya Congo hivyo ulikuwa na mashabiki wengi.” Alitamka Mkinga

Mwaka 2001 walizindua albamu ya nne iitwayo Freedom na kufuatiwa na ya tano ya ‘Mpambe Nuksi’ iliyozinduliwa mwaka 2001 na kisha ikafuata ya sita iitwayo ‘Dotnata’ mwaka 2003 kabla ya ‘Dunia Kigeugeu’ iliyozinduliwa mwaka 2006. “Mwaka 2006 tulipozindua albamu ya Dunia Kigeugeu ilifanya vizuri sana, hatukuamua kutoa nyingine haraka kwa kuwa tulikuwa bado tunalinda ubora wa albamu yetu iliyofanya vizuri kuliko zote sokoni,” anasema Mkinga.

Mkinga alisema baada ya hapo bendi hiyo ilikaa kimya kidogo hadi mwaka 2010 ilipozindua albamu mbili kwa mpigo ambazo ni ‘Vuta Nikuvute’ na ‘Heshima kwa Wanawake’, huku mwaka 2013 ikiumaliza kwa kuzindua albamu ya ‘Chuki ya Nini’.

Alisema bendi hiyo ilikutana na vikwazo vingi kutokana na baadhi ya wanamuziki kuondoka na kwenda kujiunga katika bendi nyingine, lakini iliweza kuendelea kusimama kutokana na waasisi wa bendi hiyo kama Nyoshi El Saadat kuendelea kuitumikia bendi hiyo.

“Miaka ya hivi karibuni tulipoteza wanamuziki wengi ambao waliondoka na kwenda kujiunga na bendi nyingine kutokana na kuhitaji masilahi huku wengine wakihitaji kujisimamia wao wenyewe. Wapo wengi walioondoka katika bendi hii lakini mpaka sasa hatuna mpango wa kusajili wanamuziki wapya.

“Uongozi wa bendi hii hauna mpango wa kusajili wanamuziki wapya hivi karibuni, kwani kulikuwa na pengo katika bendi lakini kwa sasa limefunikwa na wanamuziki haohao hivyo limejitosheleza.

Licha ya juhudi kubwa alizozifanya kwa kipindi kirefu za kuweka katika chati ya juu bendi hiyo ya FM Academia, aliyekuwa rais wake Nyoshi El Saadat, hivi karibuni ametangaza kujing’atua katika bendi hiyo.

FRED NDALA KASHEBA ILIZICHARAZA NYUZI DAZANI

$
0
0
Na Moshy Kiyungi, Dar es Salaam
Historia ya muziki humu nchini haiwezi kumuweka kando aliyekuwa bingwa wa kulicharaza gita la nyuzi 12 Fredy Ndala Kasheba.

Alionesha makali yake hususa alipokuwa katika bendi ya Orchestra Safari Sound (OSS) na baadaye kwenye benzi ya Zaita Muzica. Pamoja na kulikung’uta gita hilo la nyuzi dazeni, alikuwa kiongozi wa bendi pia alibarikiwa vipaji vya kutunga na kuimba.

Akiwa katika bendi hiyo ya OSS, alibuni mtindo wa Dukuduku aliokuja kuwa maarufu kila pembe za jiji hilo la Dar es Salaam. Baadhi ya nyimbo zake alizotamba nazo ni pamoja na ni Marashi ya Pemba na Kesi ya Khanga.

Kasheba hatunaye tena humu duniani kawa kuwa ni kama ada kwa kila mwanadamu kuiacha dunia. Alipatwa na maradhi yaliyopelekea kifo chake Oktoba 22, 2004 jijini Dar es Salaam akiwa na miaka 58.

Wasifu wake.

Fred Ndala Kasheba aliyeyaanza maisha baada ya kuzaliwa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka 1946. . Wasifu wa Kasheba unaeleza kuwa alianza kufundishwa gita na baba yake wakati akiwa na umri wa miaka 12.

Baba yake alikuwa anajuwa kupiga gitaa japo hakuwa mwanamuziki. Alikuwa akipiga gita nyumbani kwake baada ya saa za kazi. Moja ya bendi maarufu ambazo zilimtambulisha sana Fredy Ndala Kasheba ilikuwa Orchestra Fauvette.

Bendi hiyo ilikuwa na watunzi na waimbaji mahiri akina Baziano Bwetii na Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’. Wakati wa uhai wake, Kasheba aliwahi kueleza kuwa bendi ya Orchestra Fauvette ilianza Juni 07, 1964 katika jiji la Lubumbashi huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Afafanua maana ya jina hilo Fauvette kwa Kiswahili ni ndege aina ya Chiriku aimbae. Bendi hiyo ilikuwa na mwimbaji ambaye waliamini alikuwa anaimba mithiri ya Chiriku, hivyo wakaamua kuipa bendi jina hilo.

Wimbo wa uliotamba wakati huo ulijulikana kwa jina la Camarade ya Nzela, ambao Fredy aliwahi kusimulia kuwa ni wimbo uliokuwa ukizungumzia rafiki wa kukutana nae barabarani au njiani. Jirani huyo mwenye roho iliyofananishwa na sanduku la nguo, ambalo ndani yake huwezi kujua kuna nini.

Pia ulipigwa wimbo Jacqueline ambao ulitungwa na mwenyewe Freddy na kuimbwa kwa umahiri mkubwa na Baziano Bwetii, ambao alieleza kuwa alimtungia mpenzi wake aliyempenda Jacqueline. Wimbo mwingine uliopigwa katika kipindi hicho ni Nono na Kalemie.

Wimbo huo ulitungiwa binti aliyeitwa Nono mkazi wa Kalemie, ambaye alikuwa mpenzi mkubwa wa bendi ya Fauvette. Fauvette iliwahi kufanya ziara hapa nchini na kujikita kwa kipindi kifupi katika ukumbi wa White House Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Miaka hiyo Ubungo ilikuwa mbali sana na mji, hivyo kulikuwa na ajali nyingi za magari na pikipiki zikiwapata wapenzi wa bendi hiyo wakisafiri kutoka kwenye muziki. Busara zikatumika wakati uongozi wa bendi ulipoamua kuhamishia bendi kwenda katika ukumbi wa Mikumi Tours. Ikiwa huko walikuwa wakiporomosha burudani katika siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.

Fauvette walikuwa na ndoto ya kuwa bendi bora Afrika, japo hawakufikia huko lakini waliweza kuweka alama kubwa katika historia ya muziki wa Afrika mashariki na Kati. Ndala Kasheba aliweza kuimarisha jina lake zaidi alipolifanya maarufu kupiga gita la nyuzi kumi na mbili, mwenyewe akiliita nyuzi dazani, hasa alipoanza kulipiga kwa mtindo wa Dukuduku akiwa Safari Sound Orchestra.

Baadaye Fauvette ilirejea kwao ambako bendi hiyo ikabadilishwa jina na kuitwa Safari Nkoy. “Safari Nkoy” ina maana ya ‘Chui msafiri’ kwa lugha yetu ya Kiswahili.

Baadea Kasheba alirejea hapa nchini ambako alipitia bendi nyingi hapa nchini zikiwemo za Orchestra Safari Sound, Maquis du Zaire na Tancut Almasi. Ya mjini Iringa. Alikuwa mmoja wa waanzilishi wa bendi iliyowajumuisha wanamuziki toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Tanzania, wakaiita Zaita Muzika.

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam hawezi kumsahau Ndala Kasheba, kwa jinsi alivyokuwa akipita katika hoteli kubwa za Kitalii, nyakati za usiku akiwa na kofia kubwa aina ya Pama, akipiga gitaa lake meza baada ya meza akitoa burudani. Baadae akanzisha kundi lake la wanamuziki likaitwa Kasheba group.

Mpenzi msomaji utakuwa unazikumbuka baadhi ya tungo za nyimbo zake zikiwemo za Umbea, Nimlilie nani, Happy Birthday, Cocoa na Dezo dezo. Ubora wa wimbo wa Dezo dezo ulipelekea mwimbaji wa wa bendi ya Soukous Stars Tshala Mwana, kuimba katika mtindo wa aina yake.

Kasheba ‘aliachia’ nyimbo nyingine za Ziada, Chunusi, Takadiri, Marashi ya Pemba, Kimbunga na Yellow Card ambao ulikuwa kama akijitabiria kifo chake. Tutaendelea kukukumbka daima, Mungu aiweke roho yako pahala pema peponi, Amina.

UNAFAHMU KUWA WANAWAKE WALIKUWA NA BENDI YAO HAPA NCHINI?

$
0
0
Na  Moshy Kiyungi Dar es Salaam
 Kwa kawaida watu wamezoea kuona muziki wa dansi ukipigwa na wanaume na kuchezwa na watu wa jinsia zote. Kama ilivyo historia kwamba huwa haifutiki, inaeleza kuwa mwaka 1965, kundi jipya la aina yake lilianzishwa la ni bendi ya akina mama watupu, likapewa majina ya Women Jazz.

Akina mama hao wengine walikuwa ni wafanyakazi wa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali (Government Press), walichaguana wenyewe kuunda bendi hiyo. Kina mama hao walipokuwa wakianza shughuli hiyo walikuwa hawana ujuzi wowote wa katika muziki, wakaanza kuhudhuria mafunzo ya muziki chini ya yule mwanamuziki mahiri Mzee Mayagilo.

Mayagilo kipindi hicho alikuwa kiongozi wa kitengo cha muziki Brass band katika Jeshi la Polisi, waanza mazoezi kwa nguvu. Bendi hiyo ilikuwa chini ya Umoja wa Vijana wa TANU (TANU Youth League) wakati ule. Sasa ni UVCCM.

Kutokana na jitihada zao wakajitengenezea utaratibu wa kuanza kufanya maonyesho yao hasa kwenye hafla za serikali na Chama tawala cha TANU wakati huo. Dhamira yao ilitimia Mei 31, 1966 ambapo bendi yao iliingia katika studio za RTD zilizopo jijini Dar es Salaam na kurekodi nyimbo zao sita.

Nyimbo hizo zilikuwa za Tumsifu mheshimiwa, Leo tunafuraha, Mwalimu kasema, Women Jazz, Sifa nyingi tuwasifu viongozi na TANU yajenge nchi. Women Jazz alikuwa ikiundwa na akina Mary Kilima, Juanita Mwegoha, Rukia Hassan na Siwema Salum ambao walikuwa waimbaji katika bendi hiyo.

Wengine ni Kijakazi Mbegu aliyekuwa akilicharaza gitaa la solo, Mwanjaa Ramadhani alikuwa akiliungurumisha gitaa zito la besi na Chano Mohammed, aliyekuwa akipiga gitaa la kati la rhythm. Kwa upande wa ‘mdomo wa bata’ walikuwepo Tatu Ally na Anna Stewart waliokuwa wakipuliza Alto Saxophone, wakati Mina Tumaini na Rukia Mbaraka wakipuliza Tenor Saxophone.

Mama aliyejulikana kwa jina la Lea Samuel alikuwa akichangaya Bongos, wakati huohuo Josephine James alikuwa akidunda drums. Miaka hiyo kulikuwa na zana nyingi za muziki tofauti na miaka hii. Kulikuwepo na chombo kikiitwa Maracass kilichokuwa kilichezwa na Zainabu Mbwana wakati kile cha Timing alikuwepo Tale Mgongo.

Kwa wale wasioijuwa ama kukumbuka historia ya chama cha TANU, kirefu chake ni Tanganyika African National Union. Hicho ndicho kilikuwa chama kilichotawala Tanganyika na Tanzania hadi muungano wa chama hicho na Chama cha Afro-Shirazi cha Zanzibar, vilipounda Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977.

Chama cha TANU kilianzishwa 7 Julai, 1954, kabla yake kulikuwepo na chama cha Tanganyika African Association (TAA). TAA ilikuwa na mwelekeo wa kitamaduni zaidi ya siasa. Mwenyekiti wa kwanza wa TANU alikuwa Julius Kambarage Nyerere. TANU ilikuwa ikishinda kila uchaguzi chini ya utawala wa kikoloni ikawa chama cha kuongoza Tanganyika hadi ilipopata uhuru wake mwaka 1961.

Katiba ya Taifa ya mwaka 1962 ilifanya TANU kuwa chama cha pekee nchini, ikifuata mfano wa nchi za kijamaa zenye muundo wa siasa ya chama kimoja. Bendi ya Women Jazz ilipata umaarufu kiasi cha kuanza kufanya safari nje ya Tanzania, na kuweza kufanya maonesho katika miji ya Nairobi na Mombasa, baada ya kutembelea miji kadhaa hapa nchini.

Baada ya waaamuziki wa bendi hiyo kujiona hawapati faida yeyote kutokana na mapato ya bendi yao, wakiwa katika maandalizi ya kufanya ziara ya kwenda nchini China, bendi hiyo ilisambaratika. Nathubutu kutamka kwamba nyimbo za akina mama hao hazifahamiki kwa kizazi hiki kwa kuwa hakuna anaye jail kazi ya akina mama hawa. Hazichezwi katika kituo cha redio chochote hata TBC taifa iliyo na Maktaba kubwa ya muziki! 

WAZIRI BITEKO AZINDUA BODI YA GST,AITAKA KUIWEZESHA GST KURAHISISHA MAISHA YA WACHIMBAJI

$
0
0
Asteria Muhozya na Samwel Mtuwa, Dodoma
Bodi ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), imetakiwa kuiwezesha taasisi hiyo kurahisisha maisha ya Wachimbaji Wadogo, wa Kati na Wakubwa kwa kuhakikisha wanapata taarifa za tafiti zinazofanywa na taasisi hiyo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini Doto Biteko wakati akizundua Bodi ya GST na kueleza kuwa, shughuli za utafiti ni moja ya maeneo muhimu katika sekta ya madini kutokana na kutoa uhakika kwa wachimbaji na hivyo kukidhi matarajio ya wadau.
Pia, ameitaka bodi kuiwezesha taasisi hiyo kutoa ubunifu mpya utakaowezesha taasisi hiyo kuongeza mapato kwa serikali kutokana na shughuli na huduma zinazotolewa na GST.
Katika hatua nyingine, Waziri Biteko ameitaka bodi hiyo kuhakikisha GST inapata Ithibati ya maabara yake ikiwemo kutangaza huduma zinazotolewa na maabara hiyo ili kuwawezesha wadau kuifahamu na kuitumia.
Aidha, ameitaka bodi husika kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sera, sheria na taratibu zilizowekwa na kueleza kwamba, taasisi hiyo inao watendaji wazuri wa kuiwezesha kutekeleza majukumu yake kiamilifu na kutumia fursa hiyo kumpongeza Kaimu Mtendaji Mkuu wa GST Yokberth Myumbilwa, kwa kusimamia vema utendaji wa GST.
Naye, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema taasisi hiyo ni kitovu cha sekta ya madini nchini na kwamba ndiyo imeshikilia mstakabali wa wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa.
Ameongeza kuwa, bado yapo majukumu ya taasisi hiyo ambayo hayajafanikiwa na hivyo kuitaka bodi hiyo chini ya Prof. Ikungula kuhakikisha yanafanikiwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. Justinian Ikingura amesema bodi hiyo inatambua umuhimu wa rasilimali madini katika kuchangia pato na kukuza uchumi wa taifa ikiwemo kutambua nia na lengo la Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.
Amesema ili kufikia lengo hilo, ni muhimu GST ikawezeshwa ipasavyo kupitia wizara ili iongeze kasi na tija zaidi katika kutekeleza majukumu yake, hususan katika maeneo ya kufanya utafiti na kukusanya taarifa muhimu za kijiosayansi za kubaini maeneo yenye miamba yenye vishiria vyakuwepo madini ya kimkakati yanayohitajika zaidi katika matumizi ya teknolojia ya viwanda vya kielekitroniki, zana za utafiti wa mawasala ya anga na matumizi maalum katika viwanda vingine, ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchini katika maeneo hayo. 
“Kwa mfano madini lithium, cobalt na palladium yanazidi kupata umuhimu wa pekee katika matumizi ya viwanda vya kimkakati. Hivi majuzi takriba wiki moja iliyopita bei ya Palladium ilifikia kiasi cha dola za kimarekani 1,600 kwa wakia na kuzidi hata dhahabu ambayo ikiwa karibu dola 1,300 kwa wakia moja. Lakini si wengi wanatambua madini ya Palladium ambayo yako katika kundi la metali za Platinum, yaani Platinum Group Metals (PGM),” amesisitiza Prof. Ikingura.

Ameongeza kuwa, eneo jingine ni uboreshaji wa huduma za maabara za uchunguzi na upimaji wa miamba na madini yake ili zikidhi viwango vya kimataifa, na hivyo kuvutia wawekezaji katika sekta ya madini kutumia zaidi maabara za ndani ya nchini badala ya kupeleka sampuli katika maabara za nje ya nchi, na hivyo kupoteza fedha za kigeni.

Vilevile, amesema ipo haja ya kuboresha na kuongeza thamani taarifa za jiofikizia na jiokemia zilizo katika hifadhi au kanzidata ya GST ili ziweze kuwa na thamani kubwa zaidi  kwa taifa na kwa wawekezaji katika sekta ya madini, suala ambalo  litaiweesha GST kuongeza maduhuli ya serikali kupitia wizara.

Mbali ya Mwenyekiti, wajumbe wa bodi hiyo ni Abdulkarim Hamisi Mruma, Emanuel Mpawe Tutuba, Bibi Bertha Ricky Sambo, Shukrani Manya, David R. Mulabwa na Bibi Monica Otaru.

Bodi hiyo imezinduliwa Machi 27, 2019 Makao Makuu ya GST, jijini Dodoma.
 Waziri wa Madini Doto Biteko (kushoto) akizungumza na jambo wakati wa uzinduzi wa bodi ya GST .kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya GST Prof. Justinian Ikingula.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Wajumbe wa  Bodi ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti  wa  Madini Tanzania (GST), Watendaji wa wizara  pamoja na watumishi  mbalimbali kutoka  GST wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini Doto Biteko (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Bodi ya GST uliofanyika jijini Dodoma tarehe 27/3/2019.
 Waziri wa Madini Doto Biteko,  akimkabidhi  kitendea kazi mmoja wa wajumbe wa Bodi ya GST , Kamishna wa Madini, David Mulabwa wakati wa uzinduzi wa bodi. Anayeshuhudia kulia ni Mwenyekiti wa Kamati  ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dustan  Kitandula.
Waziri wa Madini Doto Biteko akimkabidhi moja a kitendea kazi mjumbe wa Bodi ya GST Prof. Shukran Manya wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya GST uliofanyika tarehe 27/3/2019 katika ukumbi wa mikutano wa wizara , pembeni anayeshuhudia makabidhiano hayo ni mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. Justinian Ikingula.
 Waliokaa kutoka kushoto ni  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya  Bunge ya Nishati na Madini  Dustan  Kitandula, Waziri wa Madini Doto Biteko , Mwenyekiti wa Bodi ya GST Prof. Justinian Ikingula, na Naibu waziri wa Madini Stanslaus Nyongo. Wengine katika picha waliosimama ni Wajumbe wa Bodi ya GST na baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya GST. 

Tanroad mkoa wa Ruvuma yafanya zoezi la uchunguzi wa Afya kwa hiari kwa watumishi wake

$
0
0
Na Amri Mmanja, Ruvuma.

WAKALA wa Barabara (Tanroad) mkoa wa Ruvuma imefanya zoezi la uchunguzi wa Afya kwa hiari kwa watumishi wake. Meneja wa Tanroad mkoani Ruvuma Mhandisi Razak Alilanuswe alisema, zoezi hilo mbali kuwa litasaidia watumishi kutambua hali zao, litahamasisha watumishi kupenda kupima Afya zao mara kwa mara na kutumia kadi za Bima ya Afya kupata matibabu.

Alisema,huu ni mkakati uliowekwa na Tanroad kupitia vikao vya Baraza la wafanyakazi ambalo limeagiza kila mtumishi kuhakikisha anapima Afya na kupata muda kwa ajili ya mazoezi ili kuwa na utimamu wa kimwili. Kwa mujibu wake,mtumishi akitambua Afya ataweza kujitunza na hata wale watakokutwa na maradhi itakuwa rahisi kwao kuanza matibabu na kuendelea na majukumu yake ya kawaida.

Aidha,amewapongeza wafanyakazi kwa kujitokeza kwa wingi kupima Afya na kusisitiza kuwa, hatua hiyo itasaidia sana kuongeza ufanisi na hivyo kushiriki vema kuchochea kukua kwa uchumi wa Nchi yetu. Mmoja wa Wafanyakazi Geofrey Mwakalebela, amepongeza zoezi hilo na kushauri lifanyike mara kwa mara kwani litasaidia sana watumishi kutambua Afya zao.

Ameiomba Tanroad kuendelea kuboresha suala la wafanyakazi wake kushiriki na kufanya mazoezi angalau mara mbili kwa Mwezi kwani Mazoezi ni sehemu ya kipimo cha Afya.

Alisema, mtumishi mwenye Afya njema ana mchango mkubwa sehemu ya kazi tofauti na mgonjwa ambaye kimsingi hawezi kutoa mchango kwa sababu lmuda mwingi atalazimika kupumzika nyumban.

Kwa Upande wake Afisa lishe wa Manispaa ya Songea Anna Nombo alisema, kwa siku mbili ambazo zoezi hilo limefanyika walifanya uchunguzi wa Ini,HIV,Uzito,Urefu,Sukari pamoja na shinikizo la Damu(PB).

Nombo alisema, wale ambao wamekutwa na matatizo ikiwemo uzito uliokithiri wamepewa ushauri na namna ya kufanya ili kuzuia kuongezeka kwa maradhi na ambayo yanaweza kupelekea matatizo makubwa kiafya.
Mganga wa kituo cha Afya Mjimwema Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Dkt Grace Ndumbaro kulia akimpima Presha(BP)mmoja wa wafanyakazi wa Wakala wa Bara bara Tanroad mkoa wa Ruvuma ambaye hakufahamika jina lake mara moja,wakati wa Zoezi la uchunguzi wa Afya kwa Watumishi wa Tanroad mkoani Ruvuma.
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live




Latest Images