Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

KAMATI YA MAENDELEO YA WANAWAKE,HABARI NA UTALII YA BARAZA LA WAWAKILISHI YAFANYA ZIARA SEHUMBALIMBALI ZANZIBAR.

0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake,Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi Mwantatu Mbaraka Khamis(katikati) akizungumza katika Mkutano maalum na Jumuiya ya Wawekezaji katika Sekta ya Utalii(ZATI)katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Zanzibar.
 Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake,Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi wakiteremka katika Pango la Gonga(GONGA CAVE)lililopo Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja baada ya kufanya ziara maalum kutembelea Sehemu hiyo .

 Muonekano sehemu ya wa Pango la Gonga(GONGA CAVE)lililopo Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja lililotembelewa na Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake,Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

 Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake,Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi wakipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Pango la  Gonga(GONGA CAVE) Issa Abdalla Ali  Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja.
 Msimamizi wa Pango la  Gonga(GONGA CAVE) Issa Abdalla Ali akionesha Mifupa ya Binaadamu iliokutwa ndani ya Pango hilo lililopo  Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja.
 Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake,Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi wakitembelea Msikiti wa Kizimkazi uliojengwa mwaka 1184 na Washirazi kutoka Pashia katika ziara maalum katika sehemu za Makumbusho na Mambo ya kale.
 Msikiti wa Kizimkazi uliojengwa mwaka 1184 na Washirazi kutoka Pashia namna Unavyoonekana kwa Ndani sehemu ya Kibla .
Mtunzaji wa Msikiti wa Kizimkazi kutoka Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale Yussuf Rakib Ashkina akitoa maelezo kuhusu maandishi yaliomo ndani ya Msikiti huo kwa Kamati ya Maendeleo ya Wanawake,Habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA YAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, YAPONGEZA VYOMBO VYOTE VYA ULINZI NA USALAMA

0
0


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola wa kwanza kushoto akitoa maelekezo kwa Watendaji Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kabla Watendaji hao hawajaingia kwenye Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kilichoketi leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma leo, ili kupitia utekelezaji wa Mpango wa Bajeti kwa mwaka 2018/2019 na Makadirio ya Mapato, Matumizi ya Kawaida na Miradi ya Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Jacob Kingu, akifuatiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara hiyo Wanja Mtawazo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Katibu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje , Ulinzi na Usalama, Ramadhani Abdallah wa kwanza kulia akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola wa kwanza kushoto pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Jacob Kingu katikati, muda mfupi baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kupitisha Makadirio ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola wa kwanza kushoto akizungumza na watendaji Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pichani baada ya kumalizika kwa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kilichoketi leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mjini Dodoma, ili kupitia Utekelezaji wa Mpango wa Bajeti kwa mwaka 2018/2019 na Makadirio ya Mapato, Matumizi ya Kawaida na Miradi ya Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, wa pili kulia, akifuatiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, wa kwanza kulia, pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo wakimsikiliza kwa makini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola wa kwanza kushoto wakati akiwapa maelekezo mbalimbali baada ya kumalizika kwa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kilichoketi leo katika ukumbi wa Mikutano wa Bunge la Mjini Dodoma na kupitisha Makadirio ya Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2019/2020. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola, wa pili kushoto akiwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamadi Masauni, wa kwanza kushoto, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Faustine Kasike wa pili kulia na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala wa kwanza kulia, wakielekea katika Ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma, kwa lengo la kushiriki katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kilichoketi leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mjini Dodoma ili kupitia utekelezaji wa Mpango wa Bajeti kwa mwaka 2018/2019 na Makadirio ya Mapato, Matumizi ya kawaida na Miradi ya Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ya Wizara hiyo. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

RIDHIWANI KIKWETE AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA SHULE NA ZAHANATI JIMBONI KWAKE

0
0
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akikagua maendeleo ya ujezi wa madarasa katika Shule ya Sekondari ya Mboga, iliyopo Msoga Mkoani Pwani, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali inayoendelea Jimboni kwake, mwishoni mwa wiki iliyopita. 
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza jambo na baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari ya Mboga, wakati alipotembelea eneo kisima cha maji chenye uwezo wa kusambaza maji shule hapo na maeneo ya jirani.
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete pamoja na ujumbe wake wakifatilia ngonjera za wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mboga, muda mfupi kabla ya kuzungumza nao pamoja na kufungua rasmi mabweni mawili ya washichana katika shule hiyo.
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akipokea moja ya taarifa za wanafunzi kutoka kwa Mwanafunzi, Yasinta John.
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akifatilia risala ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mboga, Mwalimu George Mwakihaba.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akitoa kitambaa katika jiwe la msingi kuashiria ufunguzi rasmi wa mabweni mawili ya wasichana ya Shule ya Sekondari ya Mboga, iliyopo Msoga Mkoani Pwani.
 Baada ya kutoka shule ya Sekondari Mboga, Mbunge Ridhiwani Kikwete alielekea moja kwa moja katika Shule ya Sekondari ya Lugoba ambayo nayo inaendelea na ujenzi wa madarasa pamoja na uchimbwaji wa visima vya maji kwa ajili ya matumizi ya Shule hiyo.
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Lugoba, Mwalimu Mbaga wakati alipotembelea karakana ya shule hiyo kuona maendeleo ya utengenezaji wa meza za walimu pamoja na wanafunzi.
 Ukaguzi wa moja ya Madarasa.
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Lugoba, Yussuf Kikwete wakikagua maendeleo ya Ujenzi wa Shule hiyo, ambayo ujenzi wake unaelekea ukikoni na hivi karibuni wanafunzi wataanza kuyatumia madarasa hayo.
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete kwa pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Lugoba, Yussuf Kikwete wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi ikiwa ni sehemu ya ufunguzi rasmi wa madarasa matatu ya shule ya Shule ya Sekondari ya Lugoba huku wakishuhudiwa na wajumbe wa kamati ya ujenzi wa Shule hiyo.


Ujenzi wa Zahanati katika eneo la Lugoba.

Jafo ataka ushirikiano zaidi na WFP

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo amewataka Shirika la Chakula Duniani (WFP) kuendelea kutoa ushirikiano katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ili kuendelea kuboresha masuala ya Lishe katika jamii.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa kikao na Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid cha kujadili masuala mabalimbali yanayohusiana na Lishe sambamba na miradi inayofadhiliwa na fedha za Umoja wa Ulaya kupitia Shirika la chakula Dunia.
Waziri Jafo amesema tunawashukuru kwa ushirikiano mnaotupatia katika miradi mbalimbali ya Lishe na hakika mmekua na mchango mkubwa katika kuboresha Lishe Tanzania; Kwa kuwa Lishe ni suala endelevu na mtambuka tunaomba muendelee kutoa msaada zaidi wa kifedha na kitaalamu ili  Lishe izidi kuboreshwa katika  jamii.
‘Hatuwezi kufikia Taifa la Uchumi wa Kati endapo  watu wetu hawatakuwa na lishe bora, ili watu wafanya kazi kwa bidii, waweze kuzalisha na kulipa kodi inavyotakiwa ni lazima wawe na Afya bora wakati wote hivyo kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha lishe bora ni vitu muhimu sanakatika kufikia lengo la Kitaifa” alisema Jafo. 
Katika kikao hicho Jafo alizungumzia suala la kuanzisha Siku ya Lishe kitaifa itakayozimishwa kila mwaka ili kuendelea kutoa Elimu kwa Umma kuhusu umuhimu wa Lishe katika maisha ya kila siku ya mtanzania.
Alimtaka Binti Mfalme wa Jorda Sarah Zeid kuendelea kutoa ushirikiano katika kufanikisha siku hii muhimu ya kitaifa itakayoanza kuazimishwa mwaka huu wa 2019.
Naye Binti Mfalme Sarah Zeid amesema amefurahishwa sana na utekelezaji wa miradi ya Lishe inayotekelezwa katika Halmashauri nne Nchini na ameridhishwa na matokeo aliyoayaona kuptia miradi ya wananchi.
Ameahidi kupitia Shirika la Chakula Duniani (WFP) kuendelea kutoa ushirikiano katika miradi mingine itakayoendelea kutekelezwa ila kuhakikisha Lishe inaboreshwa katika Jamii.
Naye Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Chakula Duniani Michael Dunford ameshema watashiriki kikamilifu katika kuadhimisha siku la Lishe Kitaifa na watatoa ushirikiano unaohitajika katika kufanikisha siku hiyo.
Shirika la Chakula Duniani (WFP) linaratibu mradi wa Boresha Lishe unaotekelezwa katika Halmashauri nne Nchini ambazo ni Bahi, Ikungi, Singida Dc pamoja na Chamwino.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (kushoto) akisalimiana na Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid wakati wa ziara yake Nchini kukagua miradi ya Lishe inayotekelewa na Shirika la Chakula Duniani (WFP).
 Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid akizungumza na Waziri wa Nchi OR- TAMISEMI Selemani Jafo (Mb) wakati wa ziara yake Nchini kukagua miradi ya Lishe inayotekelewa na Shirika la Chakula Duniani (WFP).
 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani Michael Dunford akizungumza wakati wa kikao.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (katikati) akiwa na  Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid (kushoto) pamoja  na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani Michael Dunford .
Katika Picha ya Pamoja ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (katikati) akiwa na  Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani Michael Dunford pamoja na watalaamu wa OR-TAMISEMI pamoja na WFP.

BI JACQUELINE MKINDI AONGOZA KIKAO CHA BODI YA WAKURUGENZI WA BARAZA LA KILIMO

0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Bi Jacqueline Mkindi akiongoza kikao cha bodi hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Baraza la Kilimo Machi 27,2019  Jiji Dar es Salaam.

 Sehemu ya wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania wakifuatilia kwa umakini agenda za kikao hicho cha kawaida cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi za Baraza la kilimo, Machi 27, 2019  Jiji Dar es Salaam.

 Mratibu Taifa wa Ubia wa Kilimo Tanzania Bw Mark Magila, Bw. Omary Mwaimu Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi na wajumbe wengine wakifuatilia kikao hicho cha Bodi ya wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Bi Jacqueline Mkindi akiongoza kikao cha bodi hiyo, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Bi Janet Bitegeko, kikao hicho cha siku moja kimefanyika  katika Ofisi za Baraza la Kilimo Machi 27,2019  Jiji Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Kilimo Tanzania Bi Jacqueline Mkindi (mwenye gauni la kitenge)  kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la kilimo Bi Janet Bitegeko wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wengine  baada ya kumalizika kwa kikao cha kujadili mpango mkakati wa ACT kwa mwaka 2019 hadi 2023, kikao hicho kilifanyika Machi 26,2019 Jijini Dar es salaam..

TUKIKUGUNDUA NA TUKIKUMATA , TUTALALA NAWE MBELE- RC RUVUMA

0
0
Baadhi ya wakulima wa Korosho Kijiji cha LINGUSANGUSE Wilaya ya NAMTUMBO Mkoani RUVUMA wameulalamikia uongozi wa Chama cha Msingi cha MJIMWEMA kwa kuwaibia kilo za korosho na kutowalipa stahiki zao. Malalamiko hayo wameyatoa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa RUVUMA, CHRISTINA MNDEME alipotembelea kijijini hapo kwa lengo la kusikiliza kero zinazowakabili.

NCHI ZA SADC ZIMEAHIDI KUSHIKAMANA NA SAHARAWI

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akiwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Pretoria Afrika Kusini tarehe 25 na 26 Machi 2019. Mkutano huo ni maalum kwa ajili ya kuonesha mshikamano na nchi ya Saharawi, ambapo washiriki walielezea dhamira yao ya kusimama pamoja na Saharawi. 
Dkt. Damas Ndumbaro akisalimiana na Rais wa Saharawi, Mhe. Brahim Ghali katika ukumbi wa mikutano jijini Pretoria. 
Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC na wawakilishi wa Wakuu Nchi na Marafiki wa Sharawi walioshiriki mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja. 

MZEE WA MIAKA 80 AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA MKUKI UBAVUNI,NA WENGINE WATATU WAJERUHIWA

0
0
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

MZEE mmoja aliyetambulika kwa jina la Visu Urembo (80),amefariki dunia baada ya kuchomwa mkuki kwenye sehemu ya ubavuni mwa mwili wake, katika mgogoro wa wakulima na wafugaji, uliotokea Lukenge, tarafa ya Ruvu, Kibaha Vijijini ,mkoani Pwani. 

Akithibitisha kutokea kwa tafrani hiyo, kamanda wa polisi mkoani Pwani ACP, Wankyo Nyigesa alisema tukio limetokea majira ya saa 12 alasiri, march 26 mwaka huu. 

Alieleza, mzee Urembo kabla ya kufikwa na umauti alikimbizwa kituo cha afya Mlandizi, ambapo baadae alikimbizwa hospital ya Tumbi kwa matibabu zaidi lakini kabla ya kupatiwa matibabu madaktari waligundua kuwa umati umeshamfika. 

Hata hivyo, Wankyo alibainisha, wafugaji hao waliingiza mifugo yao (ng'ombe) kwenye bwawa linalotumika katika shughuli za binadamu ikiwemo kunywa, kufulia, kupikia na kadhalika. 

"Kwa kuona hivyo ndipo wakulima wakaenda kwa mhemko kuwazuia watoe ng 'ombe wao lakini wafugaji walianzisha tafrani, ambapo walianza kurusha mikuki ,vitu vyenye ncha kali na kusababisha kifo cha mzee huyo na kujeruhi watu watatu "alifafanua Wankyo. 

"Polisi tulifika eneo la tukio alfajir March 27 ,na kutuliza tafrani hiyo na sasa hali ni shwarii". Wankyo aliwataja waliojeruhiwa ,kuwa ni pamoja na John Kisukari Urembo (50) ambae ni mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Lukenge. 

Wengine ni mtendaji wa kijiji cha Lukenge Maximillian Evarist (34) na Adam Onesha ambae ni mwenyekiti wa kamati ya maji kijijini hapo .Kamanda huyo alitoa wito, jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi ili kuepukana na madhara kama hayo yaliyojitokeza. 

Wankyo,alisema kila mtu katika nchi hii ana haki ya kuishi, kutumia ardhi hii, na hakuna mwenye mamlaka juu ya mwenzie ila inabidi kuacha kuingiliana mipaka iliyotengwa kwa ajili ya kundi jingine ili hali kukabiliana na migogoro hasa ya wakulima na wafugaji"alisisitiza Wankyo. 

Mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama aliyataka makundi hayo yaheshimiane na kujenga upendo badala ya kujiona kundi moja ni zaidi ya kundi jingine. 

NCHI ZA SADC ZIMEAHIDI KUSHIKAMANA NA SAHARAWI

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akiwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Pretoria Afrika Kusini tarehe 25 na 26 Machi 2019. Mkutano huo ni maalum kwa ajili ya kuonesha mshikamano na nchi ya Saharawi, ambapo washiriki walielezea dhamira yao ya kusimama pamoja na Saharawi.

Dkt. Damas Ndumbaro akisalimiana na Rais wa Saharawi, Mhe. Brahim Ghali katika ukumbi wa mikutano jijini Pretoria.

Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC na wawakilishi wa Wakuu Nchi na Marafiki wa Sharawi walioshiriki mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja.

Dkt Kalemani aahidi fidia kwa wananchi waliopisha mradi wa umeme Kidahwe, Kigoma

0
0
Na Teresia Mhagama, Kigoma

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, amesema kuwa wananchi waliopisha mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme katika Kijiji cha  Kidahwe wilayani Kigoma watalipwa fidia kabla ya ujenzi kuanza.

Alisema hayo jana wakati za ziara ya kikazi wilayani Kigoma na Uvinza ambapo alikagua eneo kutakapojengwa kituo cha kupoza umeme wa gridi ambao utatoka Tabora hadi Kigoma kwa msongo wa kV 132.

“ Tunawapongeza wananchi kwa kupokea mradi huu kwa mikono miwili, lakini tunajua kuna wananchi wanaopaswa kulipwa fidia, ni haki yao ya msingi, hivyo hatutaweza kuanza ujenzi mpaka mtakapolipwa kwanza.” Alisema Dkt Kalemani.

Aliongeza kuwa, Serikali imetenga shilingi milioni 722 kwa ajili ya malipo ya fidia kwa wananchi na kwamba makadirio yameshafanyika na taratibu za uhakiki zinaendelea ili wananchi wapate kile wanachostahili.

Alisema kuwa,  wananchi watakaopisha njia hiyo ya umeme pia watalipwa fidia na kwamba ujenzi utaanza wakati wowote baada ya malipo ya hayo kukamilika.

Akiwa wilayani Uvinza, Waziri wa Nishati alikagua kazi ya usambazaji umeme vijijini katika Kijiji cha Kazuramimba na Nyanganga ambapo mkandarasi kampuni ya CCCE Etern anaendelea na kazi.

Katika Kijiji cha Kazuramimba alikuta mafundi wakiendelea na kazi ya ufungaji wa transfoma ambapo msimamizi wa mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) alimweleza kuwa, kazi hiyo inakamilika tarehe 27 Machi, 2019 na baada ya hapo wataanza kuunganishia umeme wananchi.

Akiwa katika Kijiji cha Nyanganga, Dkt Kalemani alimwagiza mkandarasi kuhakikisha kuwa, Kijiji hicho kinapata umeme tarehe 31 Machi, 2019 ambapo pia aliiagiza TANESCO kutoa elimu kwa wananchi ili wahamasike kuunganisha umeme kwenye nyumba zao.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Tatu kutoka kulia) akizungumza na wanachi katika Kijiji cha Kidahwe wilayani Kigoma (hawapo pichani) wakati alipofika kijijini hapo kukagua eneo kutakapojengwa kituo cha kupoza umeme. Wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson Renard.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Tatu kutoka kushoto) akikagua miundombinu ya umeme katika Kijiji cha Kazuramimba wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma.
 Wananchi katika Kijiji cha Nyanganga wilayani Uvinza wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati alipofika kijijini hapo kukagua kazi ya usambazaji umeme.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa pili kushoto) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mwanamvua Mlindoko wakati alipofanya ziara ya kukagua kazi ya usambazaji umeme katika Kijiji cha Nyanganga wilayani humo.

COURT DECIDES THAT UGANDA’S EXCISE DUTY IMPOSED OVER GOODS IMPORTED WITHIN EAST AFRICA IS A VIOLATION OF THE TREATY

0
0


 East African Court of Justice, Arusha, 26th March, 2019: The First Instance Division decided that the government of Uganda violated the East African Community Treaty and the Customs Union and Common Market Protocols by imposing extra excise duty law over imported cigarettes within East Africa. This was a decision in the case filed by the British American Tobacco (BAT) Ltd Uganda, challenging the Government of Uganda over the Excise Duty (Amendment) Act of 2017, that was assented to by the President of Uganda on 13th June 2017,with a commencement date of 1st July 2017 and the Act was published in the Uganda Gazette on 30th June 2017.   The government of Uganda through the Uganda Revenue Authority issued tax assessment notices on the basis of the above amendments requiring the BAT (Applicant) to pay excise duty for its cigarettes manufactured in Kenya and imported to Uganda. The tax assessment initially categorised the cigarettes as locally manufactured but subsequently re categorised the same as imported attracting excise duty at the higher rate for imported cigarettes, i.e. Ushs 75,000 per 1000 sticks of ‘soft cup’ and Ushs 100,000 per 1000 sticks of ‘hinge lid’.

The court further ordered that implementation of the provisions of Sec 2(a) and (b) of the Excise Duty  (Amendment) Act No.11 of 2017 by misconstruction and wrongful re-classification of the British American Tobacco Ltd Uganda’s Cigarettes as ‘imported goods”, contravene and infringe on Articles 1 and 75 (6) of the Treaty as well as Articles 1 (1) and 15 (1) (a) and (2) of the Customs Union Protocol and Article 6 (1) of the Common Market Protocol.

The Court further ordered that the government’s misapplication of the provisions of the said Act by issuance of the payment registration slips for additional taxes in the sum of Ug shs 325,208,000 for the BAT’s 1,170 packages of soft cap cigarettes is illegal, null and void and the court ordered the gov’t with immediate effect to rescind and withdraw the payment registration slips.

In addition the court ordered the government to ensure the interpretation and application of Excise Duty Act with due regard and in compliance with applicable Community Law and to align the Ugandan tax laws with Community Law applicable to goods from EAC Partner States.

The court exercising its discretion ordered each party to bear its own costs on the basis that this case has canvassed matters of grave importance to the advancement of Community law and EAC intra-regional trade, which would be of significant public interest to across section of stakeholders within and beyond the EAC regional bloc.

The court however did not find any infringement of Articles 6 (d) and (e), 7 (1) (c) 75 (1) and (4) or 80(1) of the Treaty, neither was the alleged infringement of article 4 (5)(2) or 32 of the Common Market Protocol as alleged by the Applicant against the government of Uganda.

The judgment was delivered by Honourable Judges: Lady Justice Monica Mugenyi (Principle Judge), Justice Dr Faustin Ntezilyayao (Deputy Principal Judge), Justice Fakihi A. Jundu, Justice Audace Ngiye and Justice Charles Nyachae. 

Notes for Editors:

On 30th June 2017, on 30th March 2017, the Government of Uganda published the Excise Duty (Amendment) Bill No.6 of 2017 in the Uganda Gazette proposing an increase in the rate of excise duty on cigarettes (soft cup) from Ushs. 50,000 per 1000 sticks to Ushs. 55,000 per 1000 sticks. The said rate was to apply uniformly to all applicable tobacco products manufactured within the EAC. The Bill was laid before the Parliament and referred to the Committee on finance, Planning and Economic Development. 
The Committee held meetings and prepared a report where it was recommended that the Bill be passed into law subject to a proposed amendment introducing different excise rates for locally manufactured and imported cigarettes. On 10th May 2017, the Bill was brought before the plenary, debated upon by Members of Parliament and subsequently passed by the Parliament. 
The Bill introduced amendments of excise duty on locally manufactured cigarettes (soft cup) to an amount of Ushs. 55,000 per 1000 sticks and Ushs. 75,000 per 1000 sticks for imports. While introducing Ushs 80,000 per 1000 sticks for hinge lid locally manufactured and Ushs. 100,000 per sticks for imported. 
The Act was assented to by the President of Uganda on 13th June 2017,with a commencement date of 1st July 2017 and the Act was published in the Uganda Gazette on 30th June 2017.   The government of Uganda through the Uganda Revenue Authority issued tax assessment notices on the basis of the above amendments requiring the BAT (Applicant) to pay excise duty for its cigarettes manufactured in Kenya and imported to Uganda. The tax assessment initially categorised the cigarettes as locally manufactured but subsequently re categorised the same as imported attracting excise duty at the higher rate for imported cigarettes, i.e. Ushs 75,000 per 1000 sticks of ‘soft cup’ and Ushs 100,000 per 1000 sticks of ‘hinge lid’.
 Representatives of the British American Tobacco Ltd Uganda (seated in front) in court to receive the judgment.

 Judges of the First instance Division delivering the judgment.
Lawyers in court receiving the Judgment.

WALIOKUWA WAFANYAKAZI BANDARI KAVU WATUPWA JELA KWA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA YA BILIONI 12.7

0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

MAHAKAMA Kuu divisheni ya Rushwa na uhujumu uchumi imewahakumu wafanyakazi wawili wa zamani wa bandari kavu ya Azam ICD kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya kughushi na kuisababishia serikali hasara ya sh. Bil.12.7 na kuachiwa kwa makosa ya kutakatisha fedha na kukwepa kodi.

Pia mahakama imemuhukumu Benson Malembo mfanyakazi wa Region Cargo Service kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani kwa kukutwa na hatia ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya sh. Bilioni 12.

Aidha Mahakama imewaamuru washtakiwa hao mara baada ya kumaliza kifungo chao kulipa fidia  ya sh. Bilioni 6.35 ambayo ni nusu ya fedha  waliyoisababishia taasisi hasara, bilioni 12.7.
 Mbali na Malembo, washtakiwa waliotiwa hatiani na kusomewa Hukumu yao  leo Machi 28.2019 na Jaji Winifrida. Korosso ni Raymond Adolf Louis ambaye ni Meneja wa oparesheni za usalama, Khalid Yusufu Louis.

Washtakiwa hao wamesomewa hukumu yao leo baada ya Machi 25.2019 (jumatatu) mahakama hiyo kuwakuta na hatia.

Katika kesi hiyo, washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na mashtaka 110 yakiwemo ya kula njama, utakatishaji wa fedha na kukwepa kodi.

Akisoma adhabu hiyo, Jaji Koroso amesema, katika shtaka la 2 hadi la 106 ambayo ni ya kughushi, washtakiwa Raymond na Khalid wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani katika kila shtaka huku katika shtaka la kusababisha hasara washtakiwa wote wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani.

Upande wa mashtaka uliita jumla ya mashahidi 34 mahakamani hapo  kutoa ushahidi wao ambapo Jaji Korosso amesema  kupitia ushahidi huo, upande wa mashtaka umethibitisha kesi dhidi ya washtakiwa hao.


Hata hivyo, mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa  waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka hayo  baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.
Washtakiwa walioachiwa ni, Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara TRA, Hamis Omary, Haroun Mpande wa kitengo cha mawasiliano na kompyuta ICT TRA

Jaji Korosso amesema amepitia maelezo ya upande wa mashtaka na yale ya washtakiwa pamoja na mawakili wa utetezi ambapo wamedai washtakiwa ni wakosaji wa kwanza na kwamba wanafamilia zinazowategemea kwani wote wana wake na watoto ambao wanawategemea.

Jaji Korosso amesema, amezingatia maombi yote ya washtakiwa kuwa wanajutia makosa yao na pia mshtakiwa Raymond na Khalid wameiomba mahakama iangalie kipindi cha zaidi ya miaka mitatu walichokaa gerezani. Aidha katika utetezi wao waliiomba mahakama kuzingatia kuwa katika kipindi chote wakiwa waajiriwa wa Azam  hakukuwahi kutokea upotevu wowote na mara zote walikiwa wakionyesha nidhamu na kufika mahakani bila kukosa.

Washtakiwa Raymond na Khalid wanadaiwa kutoa makontena kwenye Bandari kavu ya Azam ICD iliyopo maeneo Sokota na kujaribu kuonesha yalitolewa kihalali na TRA Dar es Salaam.
Kwa upande wa washtakiwa 
Pia wanadaiwa walisababisha hasara ya Sh 12, 618,970,229 kwa kutoa makontena 329 bila ya kulipia ushuru na malipo mengine.
 Watuhumiwa Raymond Adolf Louis wa kwanza kushoto mwenye shati Jeupe,  Khalid Yusufu Louis  wa kati kati na Benson wakiwa katika ukumbi wa wazi wa Mahakama kuu devisheni ya rushwa na uhujumu uchumi, wakisuburi kusomewa  hukumu yao baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya uhujumu uchumi kwenye makosa ya kughushi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya bil. 12.7
Wshtakiwa hao wakijadiliana jambo na mawakili wao baada ya Jaji Winfrida Korosso kuwasomea hukumu yao ambapo Raymond mwenye shati jeupe na Khalid shati la bluu wamehukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani hukumu Mulembo kushoto akihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani.

TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA VYA MAKURUNGE KITALU "N" BAGAMOYO MJINI

0
0
VIWANJA VYA MATUMIZI MBALIMABALI VINAUZWA ENEO LA MAKURUNGE BAGAMOYO MJINI. VIWANJA  HIVYO VIPO UMBALI WA KILOMITA 3.5 KUTOKA BARABARA KUU YA MSATA-BAGAMOYO INAYOTUMIWA NA MAGARI YAENDAYO MIKOA YA KASKAZINI KUTOKA DAR ES SALAAM. 

PIA VIWANJA VIKO MITA 500 KUTOKA BARABARA YA KUELEKEA PANGANI NA TANGA INAYOENDELEA KUJENGWA  KWA KIWANGO CHA LAMI NA KUWEKEWA MIUNDOMBINU YA MAJI NA UMEME.  

VIWANJA VIPO MPAKANI  MWA ENEO LA RAZABA AMBALO SEHEMU YAKE INA SHAMBA LA MIWA LA  BAKHARESA NA KIWANDA CHA SUKARI KINACHOENDELEA KUJENGWA KM 7 KUTOKA MAHALI VIWANJA VIPO. ENEO LINALOPAKANA NA VIWANJA HIVI LIMEPIMWA NA VIWANJA VYOTE VIMESHAUZWA  NA VIMEISHA. HUDUMA ZOTE ZA JAMII ZIMETENGEWA MAENEO HAYO.

VIWANJA HIVI VINAUZWA KWA GHARAMA ZA MITA ZA MRABA YA SH. 3900 KWA VIWANJA VYA MAKAZI NA T.SHS 4500 KWA VIWANJA VYA BIASHARA  NA SHUGHULI ZINGINE ZA KIUCHUMI IKIJUMUISHA NA HOUSING ESTATES . VIWANJA HIVI VINA UKUBWA WA KATI YA MITA ZA MRABA WA 450 HADI 11000. 

BAADHI YA VIWANJA VINA HATI TAYARI NA VINGINE MNUNUZI ATATENGENEZEWA HATI NA HALMASHAURI KATIKA MKATABA  WA MANUNUZI UTAKAOFANYWA MBELE YA HALMASHAURI.  MALIPO YA KIWANJA YANAWEZA KUFANYWA KWA AWAMU NDANI YA MIEZI SITA. 

 KWA MAHITAJI NA KUCHAGUA KIWANJA PIGA SIMU 
NAMBA 0765751517 AU 0653461126 
AU FIKA OFISI YA AFISA ARDHI MTEULE BAGAMOYO


 Ramani ya site na 
inayoonyesha viwanja


DJ MWANAMKE MWENYE MIAKA 83 ANAYEPIGA MUZIKI KATIKA KLABU ZA USIKU

0
0
Leandra Gabriel, Globu ya jamii
SUMIKO Iwamura mwanamke(83) kutoka nchini Japan ndiye Dj wa klabu mzee zaidi duniani aliyetambulika na Guiness World Record ambaye hadi sasa anafanya shughuli hiyo.

Sumiko Iwamura maarufu kama Dj Sumirock alizaliwa Januari 23, 1934 na alikuwa na ndoto za kuwa mtu maarufu duniani kote lakini baada ya baba yake kufungua mgahawa alienda kusaidia hapo mara baada ya kumaliza shule.

Dj Sumirock alienda shule na kujifunza fani hiyo akiwa na miaka 77 na kuanza kufanya kazi hiyo mara mbili kwa mwezi huku akiendelea na kazi ya kuuza mgahawa.

Akiwa na ndoto za kusafiri duniani kote Dj Sumirock amesafiri katika nchi mbalimbali zikiwemo Paris na Newzealand huku akieleza kupendezwa za muziki wa Jazz na Rock.

Alipoulizwa na jarida la Guiness World Report kuhusiana na fani hiyo alieleza kuwa, "Ninafikiri  nilizaliwa na kipaji hiki na huwa sifanyi mazoezi kwa ajili ya afya ila ninapopiga muziki naona nafanya kitu cha  tofauti, nahisi nna nguvu" ameeleza Dj. Sumirock.

Kuhusiana na vijana wanaopambana kutimiza ndoto zao  Dj. Sumirock alinukuliwa akisema kuwa, "Nafasi  zipo kila siku, wasikate tamaa na daima wasisite kujaribu kitu" alieleza.

Dj. Sumirock ana ndoto za kusafiri duniani kote kwa kazi yake ya kupiga muziki.

MABORESHO KATIKA MAHAKAMA YA TANZANIA YAZINGATIA UTUNZAJI BORA WA KUMBUKUMBU

0
0
Na Mary Gwera, Mahakama
Ikiwa katika maboresho mbalimbali ya huduma zake, Mahakama ya Tanzania inaendelea kufanya jitihada kadha wa kadha katika kuhakikisha kuwa huduma zake zinaboreka zaidi.
Katika awamu hii tunaangazia maboresho katika suala la utunzaji bora wa Kumbukumbu ndani ya Mahakama. Katika Mhimili wa Mahakama suala la utunzaji wa kumbukumbu ni la muhimu kwani kwa asilimia kubwa Mahakama inafanya kazi kwa kutumia kumbukumbu ambazo huhifadhiwa kimaandishi, na hivyo kwa umuhimu huu Masjala ndio kitovu kikuu katika uendeshaji wa Mahakama kwakuwa baadhi ya  kumbukumbu huhifadhiwa huko.
Katika mahojiano maalum na Mkurugenzi wa Kumbukumbu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Malimo Manyambula anaeleza kwa upana kuwa neno kumbukumbu linatokana na neno la Kilatin lijulikanalo kama ‘recordum’ ikiwa na maana ya ushuhuda wa shahidi (testimony of witness).
Mkurugenzi, analielezea zaidi neno kumbukumbu kuwa ni taarifa ya kimaandishi inayopokelewa au kuzaliwa na taasisi husika kwa lengo la kusaidia taasisi hiyo kutoa maamuzi yaliyo sahihi na kwa wakati mfupi iwezekanavyo.
Katika kuendeleza  utunzaji bora wa kumbukumbu, Mahakama ya Tanzania kwa kuzingatia umuhimu wa suala hili, imeanzisha Kurugenzi maalum ya kumbukumbu  ili kuwa na usimamizi na utunzaji bora wa kumbukumbu toka inapozaliwa/kufunguliwa hadi inapofungwa. Pia, kutoa ushauri, Mafunzo na kuweka mifumo kwa kutumia viwango vya ndani na vya kimataifa.
Hivi karibuni Mahakama ya Tanzania kupitia Kurugenzi hii iliendesha zoezi maalum la kuchambua, kuorodhesha na kuweka katika maboksi mafaili yaliyofungwa (closed case files) kwenye jumla ya Mahakama 12 zilizopo mkoani Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Bw. Manyambula, kwa Dar es Salaam, zoezi hilo lilifanyika katika Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu, Masjala Kuu, Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi.
Nyingine ni Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Mahakama ya Hakimu Mkazi Jiji/Kivukoni na vilevile Mahakama za Wilaya Temeke, Ilala na Kinondoni.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa Mahakama imekuwa ikizalisha kumbukumbu nyingi kutokana na utendaji kazi wake, hivyo mashauri yanapokuwa yameisha/yamefungwa kunakuwa na mlundikano wa mafaili yaliyomaliza muda wake.
“Mlundikano wa majalada una changamoto kadhaa, ikiwa ni pamoja na kutumia muda mrefu na nguvu kubwa katika kutafuta majalada, kujaza nafasi za ofisi ambavyo vyote kwa ujumla husababisha kuchelewa kwa matokeo chanya katika utendaji kazi,” alieleza Bw. Manyambula.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya zoezi hilo lililoanza rasmi Januari 14 na kukamilika Februari 09, 2019, jumla ya majalada 225,150 yalichambuliwa na kufungwa katika maboksi 5,574.
Taarifa inaonesha idadi ya majalada yaliyochambuliwa na kufungwa huku kwa upande wa Mahakama ya Rufani jumla ya majalada 16,516 yalichambuliwa, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam majalada 31,628 yalichambuliwa, Mahakama Kuu Masjala Kuu majalada 270 yalichambuliwa.
Kwa upande wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Biashara jumla ya majalada 2,798 yalichambuliwa, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi  majalada 6,135, Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi majalada 13, 213 huku Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikiwa na jumla ya majalada 38,606 yaliyochambuliwa.
Aidha; kwa upande wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni ambapo zoezi hili pia lilifanyika jumla ya majalada 35,520 yalichambuliwa, Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine Drive jumla ya majalada 20,448 yalichambuliwa, Mahakama ya Wilaya Kinondoni  majalada 4,320, Mahakama ya Wilaya Ilala, majalada 28,838 na Mahakama ya Wilaya Temeke majalada 26,858.
Bw. Manyambula aliongeza kuwa majalada yaliyochambuliwa na kufungwa katika maboksi yalipelekwa katika kituo cha Taifa cha kuhifadhi kumbukumbu za Serikali (National Archives) kilichopo jijini Dodoma.
Akizungumzia kuhusu faida za zoezi hilo, Bw. Manyambula alisema kuwa linasaidia kutoa nafasi kwa majalada yanayotumika kuhifadhiwa vizuri, kupata majalada yanayohitajika kwa haraka na kwa wakati, kupunguza upoteaji wa majalada usio wa lazima na kuokoa nafasi katika ofisi iliyokuwa inachukuliwa na mlundikano wa mafaili.
Faida nyingine ni pamoja na kutambua kumbukumbu zitakazokuwa sehemu ya urithi andishi ‘written heritage’ na kujenga imani kwa wateja na Wadau wengine wa Mahakama.
Aidha; baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya kazi hiyo, Kurugenzi ya Kumbukumbu imejipanga kufanya zoezi hili katika Kanda nne (4) za Mahakama Kuu ambazo ni Dodoma, Mwanza, Arusha na Tanga.
“Matarajio tuliyonayo kwa mwaka ujao wa fedha ni kuendesha zoezi hili katika Kanda zote za Mahakama na mikoa. Idara itaendelea kutoa ushauri kwa Mahakama ili kuendelea kutunza vizuri kumbukumbu na kuweka mifumo ya uendeshaji na udhibiti,” alisema Bw. Manyambula.
Mbali na hayo, Idara pia imejipanga kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wa masjala kwa kuwapa mafunzo ya muda mfupi na mrefu ili wawe na weledi wa kutosha katika kusimamia vyema suala la utunzaji wa kumbukumbu.
“Kuhusu mafunzo watumishi 20 wamehudhuria kongamano la Watunza Kumbukumbu lililofanyika mkoani Tanga mwezi Oktoba, 2018, aidha watumishi 13 wameshikizwa (attachment) kwenye Taasisi saba (7) ili kupata uzoefu wa utunzaji wa kumbukumbu na menejimenti ya masijala,” alieleza Mkurugenzi huyo.
Vilevile kuendesha vikao/semina kwa Watendaji na watumiaji wa kumbukumbu ili waelewe matakwa ya sheria, kanuni, taratibu na miongozo katika usimamizi wa kumbukumbu.
Mahakama ya Tanzania kupitia Mpango Mkakati wake wa miaka mitano (5) (2015/2016-2019/2020) imelenga kuboresha huduma zake katika nyanja mbalimbali lengo likiwa ni kutoa haki sawa kwa wote na kwa wakati kama isemavyo dira yake.
Utunzaji sahihi wa Kumbukumbu (Mahakama Kuu-Tabora): pichani ni muonekano wa Maboksi ambayo ndani yake yamepangwa majalada ya kesi zilizoisha, majalada hayo yamepangwa kulingana na mwaka, utunzaji sahihi wa majalada ya kesi na mengineyo hurahisisha upatikanaji wa kumbukumbu na hatimaye kurahisisha kazi ya utoaji haki nchini kufanyika kwa ufasaha kutokana na kwamba hutegemea ushahidi wa nyaraka ili kesi iweze kusonga mbele na hatimaye kukamilika kwa wakati.
Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wakiendelea na uchambuzi wa majalada, anayezungumza (mwenye shati la bluu bahari) ni Mkurugenzi wa Kumbukumbu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Malimo Manyambula na aliyesimama ni Mkurugenzi Msaidizi-Kumbukumbu za Mahakama, Bi. Agnes Bulyota.

KIKWETE AMALIZA CHANGAMOTO YA MAJI KWA WALIMU NA WANAFUNZI WA MBOGA SEKONDARI.

0
0

Na Shushu Joel,Chalinze.
MBUNGE  wa jimbo la chalinze  katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete amefanikiwa kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama iliyokuwa ikiwakabili walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Mboga iliyodumu takribani kwa kipindi cha miaka zaidi ya 10 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo.
Akizungumza mara baada ya kukagua na kujirizisha kwa ujenzi wa mradi huo wa maji ya kisima kirefu kwa ajili ya walimu na wanafunzi wa shule hiyo,mbunge huyo alisema kuwa Jimbo la chalinze kwa ujumla linachangamoto kubwa ya maji lakini juhudi za uchimbaji wa visima virefu kwa ajili ya taasisi kama shule na za afya zinafanyika ili kutokomeza uhaba huo kwenye maeneo hayo.
“Maji ni uhai kwani kila kiumbe hai kilichopo   hapa duniani kinahitaji maji safi na salama ili kiweze kuishi hivyo ni jukumu langu kama kiongozi kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana kwa asilimia kubwa katika jimbo la chalinze”Alisema Kikwete.
Aliongeza kuwa ni kipindi kirefu walimu na wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakikumbwa na changamoto ya ukosekanaji wa maji lakini kwa kuanzia tumeanza na upatikanaji huo wa kisima kirefu ili pampu zitakuwa zinasambaza maji kwenye pointi zilizotengwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali shuleni hapo.
Pia amemtaka mkuu wa shule hiyo kuhakikisha miundombinu ya maji hayo yanalindwa ili kisima hicho kiweze kudumu kwa muda mrefu na si kukiharibu kwa makusudi ili mbunge aweze kutoa hela ya kukarabati.
Aidha Ridhiwani Alisema kuwa huduma hiyo ya upatikanaji wa maji si tu kwa ajili ya walimu na wanafunzi wa shule ya mboga bali itakuwa ni mkombozi wa upatikanaji wa huduma hiyo ya maji katika eneo hilo hivyo wananchi nao wanapaswa kupata nafasi ya uchotaji wa maji  kijijini humo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo ya Mboga sekondari Lunge Mwalaba amempongeza mbunge Kikwete kwa juhudi zake anazozifanya katika jimbo la chalinze kwa ujumla katika shughuli za ukamilishaji wa maendeleo kwa wananchi,kwani kilio cha upatikanaji wa maji katika jimbo la chalimze  ni mkubwa lakini shule yetu ya mboga imekuwa ni kipaumbele sana kutokana na mazingira.
Aliongeza kuwa kutatuliwa kwa changamoto ya maji kutapelekea juongezeka kwa ufaulu kwa wanafunzi kwani maji yalikuwa yakiumiza vifwa vya watumishi wa shule kutokana na kuwatuma wanafunzi kwenda sehemu mbalimbali kutafuta maji ili waweze kupata huduma ya chakula,hivyo maji hayo yatarahisisha shughuli za usimamizi na uendeshaji wa shule pia ogezeko la ufanisi wa ufundishaji kwa walimu kutokana  na kipindi cha nyuma walimu walikuwa wakiwazia maji kwa ajili ya matumizi ya familia zao.
Aidha amemhakikishia mbunge huyo kuwa hakuna yeyote Yule atakayehalibu miundombinu ya maji hayo kwani si muda mrefu walikuwa wakilia kwa tatizo la kukosa maji hivyo kila mtu katika eneo hili ni mlinzi wa mwenzake katika mradi huu.
Naye Mjumbe wa kamati ya bodi ya shule Muhamed Mzimba amempongeza mbunge huyo kwa kufanikisha lengo lake la kuhakikisha taasisi za serikali zote katika jimbo la chalinze zinakuwa na visima virefu kwa kusudi la kutatua changamoto za maji,taasisi hizo ni pamoja na mashuleni,vituo vya afya na sehemu mbalimbali zenye kutoa huduma za kijamii zinapata visima vya maji.
Aliongeza kuwa uwepo wa kisima hicho katika shule hiyo kutafanikisha mambo mengi ya shule kuweza kusonga mbele kutokana na upatikanaji wake.

Kwa upande wake mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo Juma  Ally amempongeza mbunge wa chalinze kwa kuichaingia shule yao misaada  mbalimbali katika harakati zake za kuisaidia shule yao

WAZIRI MHAGAMA HAMIZA VIJANA KUWA WAZALENDO KWA NCHI YAO

0
0
Na OWM – KVAU, Kilimanjaro

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewahimiza vijana kuwa wazalendo na kuithamini nchi yao.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga vijana waliopanda Mlima Kilimanjaro jana tarehe 26 Machi, 2019 Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni kuaadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Waziri Mhagama alisema kuwa, Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere alikuwa kiongozi mzalendo kwa nchi yake na alijali utu na usawa, hivyo ni vyema vijana na vizazi vijavyo wakarithishwa falsafa za Baba wa Taifa.

“Vijana mna kila sababu kuyaenzi matendo ya Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere na Mhasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Abeid Amani Karume kwa vitendo kwa kuwa ninyi ndio nguzo ya Taifa na mnaelewa vema tulipotoka, tulipo na tunapoenda,” alisema Mhagama

Aliongeza kuwa, Viongozi hawa hawakuwa wabinafsi kwa kujilimbikizia mali na hawakubagua mtu kwa rangi wala kabila bali walijenga Taifa na kudumisha amani na moja.

Aliendele kwa kuwapongeza vijana kwa azma yao ya kuenzi historia na mazuri yaliyofanywa na viongozi hao kwa kupanda mlima Kilimanjaro na kuwatakia baraka waende na kurudi salama.

“Kitendo hiki ni cha kishujaa na uzalendo wa hali ya juu kwa Taifa ikiwa ishara ya kumuenzi Baba wa Taifa,” alieleza Mhagama

Aidha Waziri Mhagama alitoa rai kwa vijana kuwa wazalendo na kuwasihi wafanye kazi kwa bidii ili kujenga Taifa kupitia uchumi wa viwanda utakao ifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Alifafanua kuwa uzalendo lazima ujengwe sambamba na ujenzi wa uchumi wa Taifa, ulinzi na usalama wa Taifa na utunzaji wa tunu za Taifa.

Pamoja na hayo, aliwapongeza na kuwashukuru Viongozi wa Mkoa wa Songwe na Lindi pamoja na uongozi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) kwa ushirikiano mkubwa na Ofisi yake katika kuwashirikisha vijana kwenye suala hilo.

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba alisema kuwa tukio hili ni muhimu kwa vijana kutambua historia na mchango wa Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere katika Taifa.

“Tumieni fursa hii kupitia vitabu mbalimbali vya kihistoria ili mjifunze mipango, mwenendo na malengo ya Baba wa Taifa itawasaidia na kuwajengea nafasi nzuri ya kujitambua na kuelewa historia ya Taifa,” alisema Warioba.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Bw. James Kajugusi alieleza kuwa Baba wa Taifa alianza harakati za kulikomboa Taifa akiwa kijana na aliendelea kufanya hivyo kwa kuwa hamasisha vijana kujenga Taifa lao baada ya kupata uhuru.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akivishwa skafu na vijana wa skauti mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe. John Palingo mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, Mkoani Kilimanjaro.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Viongozi na wakazi wa Marangu wakati wa hafla ya kuwaaga vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
 Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba akieleza jambo kwa vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi akufafanua jambo kuhusu ushiriki wa vijana hao watakaopanda Mlima Kilimanjaro, Machi 26, 2019.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akimsikiliza Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Betrita Loibooki (aliyesimama kulia) alipokuwa akiwasilisha taarifa fupi kuhusu Hifadhi hiyo. (Kushoto aliyekaa) ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba.
 Baadhi ya watumishi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara ya kuwaaga vijana hao.
 Vijana wanaotarajiwa kupanda Mlima Kilimanjaro wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama kabla ya kuanza safari ya kupanda mlima huo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akikabidhi Bendera ya Taifa kwa vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akifurahia jambo wakati wa kuwaaga vijana kabla ya kuanza zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali, Uongozi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro.



PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

Vodacom yazindua huduma mpya ya kurahisisha biashara inayoendana na mabadiliko ya kidijitali

0
0


 Hisham Hendi, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vodacom, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitengo maalum kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya wateja wanaofanya biashara kuanzia makampuni madogo-ofisi ndogo za nyumbani(Soho), wafanyabiashara wa kati (SMEs) na makampuni makubwa jana jijini Dar es salaam. 
Hisham Hendi, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vodacom, na Arjun Dhillon, Mkurugenzi wa Kitengo maalum cha Biashara wakizungumza wakati wa uzinduzi wa kitengo hicho maalum kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya wateja wanaofanya biashara kuanzia makampuni madogo-ofisi ndogo za nyumbani(Soho), wafanyabiashara wa kati (SMEs) na makampuni makubwa jana jijini Dar es salaam. 
Farid Seif (wa pili kushoto) na timu ya kitengo cha biashara wakimsikiliza moja kati ya wateja wao aliehudhuria uzinduzi wa kitengo hicho maalum kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya wateja wanaofanya biashara kuanzia makampuni madogo-ofisi ndogo za nyumbani(Soho), wafanyabiashara wa kati (SMEs) na makampuni makubwa jana jijini Dar es salaam.

 Katika jitihada za kuhakikisha biashara zinaenda sambamba na mabadiliko ya masoko ya kisasa, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC, leo imezindua kitengo kwa ajili ya kushughulikia huduma zinazoenda sambamba na mahitaji ya wateja wake wanaofanya biashara kuanzia makampuni madogo-Ofisi ndogo za nyumbani (Soho's), Wafanyabiashara wa kati (SMEs) na Makampuni makubwa. 

Lengo kuu la huduma hii ni kuwawezesha kufanya biashara kwa ufanisi zaidi, kuhimili ushindani, kujenga mtandao wa kibiashara na kuwawezesha kupata huduma zote za kurahisha biashara zao bila kuhangaika na masuala yaliyo nje ya biashara zao za msingi.

“Ulimwenguni kote kumetokea mabadiliko ya njia za kufanya biashara kutoka njia za zamani kwenda njia za kidijitali, kutumia mitandao na teknolojia za kisasa kama cloud ,tunatarajia wateja wetu kwenda sambamba na mabadiliko haya ili kufanya biashara zao kwa ufanisi na kuhimili ushindani katika masoko nasi tunaamini ni wabia wao muhimu katika kuleta ufumbuzi wa kufanikisha biashara zao”, alisema Hisham Hendi, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC.

Makampuni makubwa kama mabenki na sekta ya umma yanatafuta ufumbuzi wa ubunifu ambao utarahisisha shughuli za uendeshaji, kuhimili ushindani na kuhakikisha mali zake ziko salama. Vodacom Tanzania PLC kampuni kinara inayoongoza kutoa huduma za ubunifu wa kidijitali inawezesha kupata huduma za utambuzi wa maeneo, huduma za kompyuta kutumia teknolojia ya kisasa ya Cloud, data MPLS, huduma za simu ambazo mpigaji hatotozwa gharama za kupiga simu na biashara kutumia M-Pesa ili kuwezesha makampuni makubwa kufanya kazi kwa tija na ufanisi.

Msukumo wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda umepelekea kuanzishwa kwa biashara ndogo na za kati ambazo uendeshaji wake kwa ufanisi unahitaji huduma za ubunifu wa kiteknolojia za kisasa ili kuzipunguzia gharama za uendeshaji

"Vodacom inayo dhamira ya kufanikisha ukuaji wa biashara nchini Tanzania kupitia ubunifu wake wa huduma za teknolojia ya kidijitali za kuwarahisishia wafanyabiashara kufanikisha malengo yao na kujiandaa kwa siku zijazo na ndio maana tumewaletea huduma hizi” alisema Bw, Hendi.

Biashara zenye ukubwa wa kati kama asasi zisizo za Kiserikali (NGO’s) ambazo zimejipanga kuendesha shughuli zake kwa njia za kisasa na ambazo zinatoa kipaumbele kutumia teknolojia za kisasa yatafaidika na huduma kama IoT (Internet of Things) , SIM Manager na utumaji wa ujumbe wa maneno kwa watu wengi kwa wakati mmoja (bulk SMS).

Kwa upande wa biashara ndogo na Ofisi ndogo za nyumbani (Soho's) zitanufaika kwa kubana matumizi na kujenga mtandao wa biashara kupitia huduma ya M-Pesa, huduma za kurahisisha biashara na utumaji wa ujumbe wa maneno kwa watu wengi kwa pamoja wataweza kubadilisha biashara zao na kuzifanya kukua zaidi.

Kupitia ubunifu huu mkubwa ambao unabadilisha mbinu za kufanya biashara, Vodacom Business imeonyesha dhamira kuwa ni mbia katika kuleta teknolojia zinazorahisisha biashara na kuwezesha kuhimili ushindani, huku wakiongeza ufanisi na kuwezesha kujenga mtandao katika uendeshaji.

“Sisi ni kampuni ya huduma za simu inayotoa huduma kupitia ubunifu wa kiteknolojia zinazoweza kurahisisha biashara, shughuli za viwanda na kuleta mabadiliko “alimazia kusema Bw. Hendi.

WAZIRI MKUU AIPONGEZA OFISI YA RAIS - UTUMISHI KWA KUKAMILISHA UJENZI WA OFISI YAKE KWA WAKATI KWENYE MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA

0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) amewapongeza viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa usimamizi mzuri uliopelekea kumalizika kwa ujenzi wa ofisi hiyo  kwa wakati iliyopo mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Pongezi hizo amezitoa mapema  leo, alipotembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo kwenye mji wa serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Mhe. Majaliwa amesema kuwa, ameridhishwa na kiwango cha ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliyojengwa ndani ya kipindi cha miezi mitatu na kwa gharama nafuu ya kiasi cha shilingi bilioni moja iliyotengwa na serikali.
 “Serikali imekuwa ikifuatilia hatua zote za ujenzi katika mji wa serikali ili kuhakikisha ujenzi unafanywa kwa viwango, na jengo la Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora limekuwa likienda vizuri sana katika hatua zote” amesema Mhe. Majaliwa.
Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa, anatambua kwamba Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora imeshafanya uzinduzi wa jengo lake, jambo ambalo ni jema na limeonyesha namna ambavyo ofisi hiyo imetekeleza vema maelekezo ya serikali.
Aidha, Mhe. Majaliwa ameweka bayana kuwa, uzinduzi rasmi wa Ofisi zote zilizojengwa kwenye mji wa serikali utafanywa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika tarehe rasmi atakayoipanga.
Mhe. Majaliwa ametoa wito kwa ofisi hiyo kuboresha mandhari ya nje ya  ofisi ili iweze kupewa kipaumbele na serikali kuwa ofisi itakayotumika kwa ajili ya  uzinduzi wa ofisi zote  zilizojengwa kwenye mji huo wa serikali. 
Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amemshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) kwa kutenga muda wake kuitembelea Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora katika mji wa serikali, na kumshukuru kwa namna alivyowahimiza mawaziri kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa ofisi zao kwenye mji wa serikali ili ukamilike kwa wakati.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, amemuahidi Mhe. Majaliwa kuwa, ofisi yake itatekeleza maelekezo aliyoyatoa na itaendelea kutekeleza maagizo anayoyatoa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Awali, Kaimu Meneja wa Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Bw. Herman Tanguye amesema kuwa, Wakala ya Majengo Tanzania imekamilisha ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa asilimia 99.5% kwa muda uliopangwa na kwamba hatua iliyobakia ni kukamilisha mandhari ya nje ya ofisi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa ameitembelea Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za serikali kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma, kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuzindua ofisi hizo rasmi hivi karibuni.
 Muonekano wa jengo jipya  la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) na ujumbe wake wakiwasili katika jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) akiwa ndani ya ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) iliyopo kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma. Kulia kwake ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) akizungumza  na baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kwenye mji wa serikali, mara baada ya kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) akifurahia jambo mara baada ya kuzungumza na baadhi ya viongozi na watumishi wa umma kwenye mji wa serikali, mara baada ya kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitoa neno la shukrani kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb), mara baada ya Mhe. Majaliwa kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael wakifurahia jambo na viongozi wengine mara baada ya kukamilika kwa ziara ya Mhe. Kassim M. Majaliwa ya kutembelea jengo jipya la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora lililopo kwenye mji wa serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KONGAMANO LA 7 LA AFYA NA SAYANSI AFRIKA MASHARIKI

0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasha mwenge kama ishara ya ufunguzi wa Kongamano la 7 la Afya na Sayansi la Afrika Mashariki lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 7 la Afya na Sayansi la Afrika Mashariki lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

6
Sehemu ya Wataalamu waliohudhuria ufunguzi wa  Kongamano la 7 la Afya na Sayansi la Afrika Mashariki lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).



=====  ===============  ===============


SPEECH BY H.E. SAMIA SULUHU HASSAN, VICE PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA  AT THE OFFICIAL OPENING OF THE  7TH EAST AFRICAN HEALTH AND SCIENTIFIC CONFERENCE, HELD AT JULIUS NYERERE INTERNATIONAL CONVENTION CENTER (JNICC)
DAR ES SALAAM, THE 27TH MARCH 2019

·       Hon. Chairperson of the EAC Council of Ministers and Minister of Foreign Affairs and International Cooperation, Republic of Rwanda;
·       Hon. Chairperson of the EAC Sectoral Council of Ministers of Health and Minister of Health, Republic of Rwanda;
·       Honourable Ministers of Health from the EAC Partner States;
·       Honorable Ministers;
·       Amb. Liberat Mfumukeko, Secretary-General of the East African Community;
·       Honourable Members of Parliament from the East African Legislative Assembly and National Assemblies of the EAC Partner States;
·       Permanent Secretaries of EAC Partner States;
·       Members of the Diplomatic Community;
·       Professor Gibson Kibiki, Executive Secretary of the East African Health Research Commission;
·       Representatives of Development Partners;
·       Researchers, Scientists and Practitioners;
·       Conference Participants;
·       Members of the Press;
·       Distinguished Guests;
·       Ladies and Gentlemen;
A very goodmorning to you all.

At the outset, allow me to express my profound gratitude and appreciation to the organizers for inviting me to such an auspicious occasion of the 7thEast African Health and Scientific Conference. We are all aware that no country/region can achieve meaningful and sustained economic growth without advancement in Digital technologies especially in the critical health sector.
In this regard I wish to commend the organizers for holding this biennial conferences successfully and consistently over the past years. The interest of the region’s health researchers and scientists in discussing the gains and setbacks in Health Sector and the role of Science and Technologies in developing the sector is clearly reflected in the extensive preparatory work that has gone into the conference, and at the range of expertise gathered here today.
I am witnessing firsthand the enthusiasm of this community to drive efforts to promoterapid technological and digital transformation to support the implementation of health sector interventions and programmes. This is surely a step in the right direction towards the attainment of SDG 3 and universal health coverage and am in full support of this.
We are grateful that you chose Tanzania as the venue.  Indeed we are extremely privileged to host you. Let me take this opportunity to welcome you all, I trust that the organizers have  done  everything  within  their means to make you feel at home KARIBUNI SANA TANZANIA.

Chairperson, Hon. Ministers, Distinguished Delegates;
Investing in Health Sector and relevant digital technologies is key for our development that we need to pursue more aggressively as a region.  I am pleased with the region’s continued efforts towards operationalizing the EAC Treaty, particularly Article 118 that calls for collaboration in Health Sector as well as other relevant provisions of the EAC Common Market Protocol.

I am delighted to see that this conference is not only graced by Scientists coming from EAC but also brings together participants and delegates from all over Africa and beyond the Continent.I have no doubt thatyou will find the selected topics interesting and enriching. I believe this conference will provide you with yet another opportunity to exchange information on current development and deployment of potential approaches to scaling up innovative technologies that will accelerate the attainment  of the SDGs

Chairperson, Hon. Ministers, Distinguished Delegates;
Science and technology is an important and vital tool in addressing fundamental gaps in the health sector. I wish to commend the organizers for the timely and relevant selection of the theme, “Technology for health systems transformation and attainment of the UN-Sustainable Development Goals”. This theme comes atan opportune moment as the world is in its fourth industrial revolution where science and technology is taking the lead in all aspects.
You will all agree with me that sustainable development is elusive if we do not invest in fit-for-purpose technologies in order to help our countries to generate answers and solutions to many public health problems and challenges.
I wish to underscore that the need to invest in Digital Health Technology cannot be understated if we are to fully implement the Sustainable Development Goals and address all aspects of poverty.We can no longer ignore the direct correlation of poverty and social vulnerability in aggravating poor health. Therefore, in order to address these vulnerabilities we need to invest inDigital Health Technology as a way of strengthening regional healthcare services.


We in Tanzania have been able to identify that and we have already embarked in digitizing our healthcare system through our Ministry of Health and the several agencies under them such as the MSD ( whereby the digitized technology helps us in tracking the consignement from purchase point to delivery point), the NHIF (management of the client membership, claim and contribution) and the TFDA (online reporting of import and exports under TFDA and online reporting of the adverse effects of the use of medicine and cosmetics) . In addition to what is happening at our Agencies level we have installed Hospital Management System in all Government Hospitals. This system gives real time data and you can track the movement of the patient and the medicine stock.

We have recorded positive impact of our healthcare sector since we embarked on digitizing our sytems. A number of gains have be made which among other things include;
         i.          Improved quality of healthcare services – For instance; having EMR in place, improved availability of patient history (medical records), enhance continuity of care, Today No Record Loss, Appointments are made by the Doctors right away, improved medication etc.
       ii.          Improved efficiency and time saving
     iii.          Availability of real- time data for better decision making
     iv.          Improved resource (health commodities, HRH) tracking and allocation based on the demand
      v.          Improved accountability (internally and externally)
     vi.          Improved data security, privacy, confidentiality, transparency and internal controls.
One of the gains that is dear to me is the  Reduced post-natal mortality rate through telemedicine e.g. Digital Village located in Ngorongoro – Ololosokwan.

Our challenges still remain in having adequate manpower to support these ICT initiatives and funds to train  new manpower and come up with new initiatives. I believe the discussions you will have today will share on your best practises and how you can cooperate with each other in scaling up digitized transformation in the region’s healthcare sector




Chairperson, Hon. Ministers, Distinguished Delegates
Am made  aware that today, in addition to the East African Health and Scientific Conference, the East African Health Research Commission Commission has established new platforms meant to share research findings in the region, to build research capacity and to create a better environment for research on health matters. Allow me to mention a few of them:
1.     The Commission has developed a new concept note of the conference, approved by the 15th Sectoral Council of Ministers of Health, which makes the conference a biennial event instead of being an annual one as it was before. This gives time to implement the recommendations of the conference and to prepare for the next one.
2.     The Commission has established an official comprehensive compendium of health information in East Africa, which is a One-Stop Center for Health Information. It is operational through a web portal (www.eahealth.org), which will be launched during this ceremony.
3.     The Commission operationalized two (2) scientific Journals that are contributing to share with the global scientific community the scientific work part of the EAC region;
4.     The Commission established the Young East African Health Research Scientists’ (YEARS’) Forum which is an initiative aiming to empower East African Community (EAC) young researchers to be able to shape the future of research for health in the region; this initiative was approved by the 15th EAC Council of Ministers; YEARS’ Forum will also launched during this ceremony.
5.     The Commission initiated a number of other regional programs and projects that are running.

I therefore, take this opportunity to congratulate all members of the Commission from Partner States and the East African Health Research Commission Secretariat for these tremendous achievements and encourage them to keep up the speed and the commitment.
Chairperson, Hon. Ministers, Distinguished Delegates;
The approval of the Digital Regional East African Community Health (Digital REACH) 10 years strategic plan by the Sectoral Council of Ministers of Health held in Kigali on 26thOctober 2018 is an important step  towards achieving transformation in the sector.  

I expect that Digital REACH will support the development and implementation of regional health programme, within existing EAC Regional policies and legal frameworks as provided by the Treaty Establishing the East African Community and as desired by each of the EAC Partner States.

I am informed that this initiative will build infrastructure and other digital health assets that can be used directly, by each country, for their own national programme implementations. It has been developed based on collaboration and inputs from representatives of the EAC Partners and is supported by respective Organs of the EAC.

However,  effective implementation of this regional initiative depends not only on  good coordination from the East African Health Research Commission but also on strong commitments of EAC partners States, Development Partners and every Health Sector Stakeholder in Partner States. I take this opportunity therefore to call upon our Development Partnersto continue their support to the East African Health Research Commission, and Partner States to implement and coordinate this initiative.

Chairperson, Hon. Ministers, Distinguished Delegates;
As we discuss the above mentioned revolutionary and innovative initiative we must strive to put up  mechanisms that support and accelerate its implementation in the Health Sector. I am informed that all EAC Partner States are now implementing digital health initiatives that need to be supported. We should not forget however, that for effective integration of the EAC partner states they need to be regionally interoperable.

Digital health is proved as one of the enablers of Sustainable Development Goals in developed countries and a lot of pilot projects all over the world are confirming the same to be the case in low- and middle-income country settings.Digital solutions are used to strengthen all the core building blocks of health systems which are: service delivery; health workforce; health information systems; access to essential medicines;financing; and leadership/governance.

I therefore encourage Partner States to support the new development in EAC partner states and call upon them to work together through Digital Health Technology and I reiterate the commitment of the United Republic of Tanzania to take advantage of Digital Health technology to improve implementation of health sector interventions, with the aim of accelerating attainment of the Universal Health Coverage and SDGs.

Chairperson, Hon. Ministers, Distinguished Delegates;
We realize however that, digital healthcare initiatives to achieve the SDGs have inherent challenges that go beyond the implementation of technology.These  challenges include among others the need for a trained workforce skilled in using digital health solutions and the need for proper governance and funding, among others.

To overcome these barriers, we need to take an interdisciplinary and inter-sectoral approach, bringing together all the main actors in the digital health ecosystem such as international organizations, health service institutions, academia, research centers, and public and private industry.

We need to align our digital health approaches and solutions with the specific needs of the country’s health system and the region. We need to define and implement digital health strategic plans which consider governance mechanisms in digital health.  Our national strategies and policies need to be developed and aligned together to ensure inter-sectoral cooperation.

Therefore, our Academia and research centers and institutions are expected to continuously develop and produce primary evidence that helps decision makers identify the best, most cost-effective solutions from the wide range of options available in digital health.

The public and private industry, which is revolutionizing the digital health sector, should consider national and regional health realities and priorities, and offer sustainable needs-oriented solutions in specific sociocultural and social health realities in line with resources available in the context.

This underlines the urgency of supporting the Digital REACH Initiative which is designed to complement, improve, and strengthen EAC Partner States specific work in digital health. Let us not lose this opportunity to boost the attainment of SDGs for our Community.

As for our experts gathered here today, the Community expects from you concrete, simple and cost effective actions, with high impact that EAC Partner States can undertake at national level or collectively at regional level.

Chairperson, Hon. Ministers, Distinguished Delegates;
Before I conclude my Remarks, let me once again welcome you all to Tanzania and thank Hon Ministers of Health from our Region and Your Country delegations for having decided to stay and attend this Conference after you concluded the Meeting of the EAC Sectoral Council on Health, which just ended on 26th of March 2019 in Dar es salaam. This is a testimony of how you value East African Cooperation in Health, Research and Science.

My appreciation would not be replete if do not thank all Members of the Diplomatic Community, Development Partners Members of The East African Legislative Assembly, Presenters of various scientific papers invited to the Conference and all those who have put in time and effort to ensure the success of this Conference.

I wish to conclude my remarks by thanking you all for attending, for those who are coming outside Tanzania and will get few days to rest, hope you will enjoy exploring the beauty of our country. I particularly recommend our sandy beaches in Zanzibar; our picturesque Kilimanjaro Mountain not forgetting our renowned Serengeti National Park.
I wish you fruitful deliberations.

IT IS NOW MY SINGULAR HONOR AND PLEASURE TO DECLARE THE 7THEAST AFRICAN HEALTH AND SCIENTIFIC CONFERENCE, OFFICIALLY OPENED.

I THANK YOU FOR YOUR KIND ATTENTION.

   
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images