Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

ELIMU MUHIMU KWA UHIFADHI :JE WAJUA ADHABU NA FAINI YA KUGONGA WANYAMAPORI HIFADHINI?.

$
0
0

Muhimu kufahamu kwamba adhabu na faini ya kugonga wanyamapori  hifadhini

1: Tembo = USD  15,000 au shilingi Milioni 34.6
2: Twiga = USD 15,000 au shilingi Milioni 34.6
3: Simba = USD 4,900 au shilingi Milioni  11.3
4: Chui = USD 3,500 au shilingi Milioni 8
5: Nyati =USD 1900 sawa na shilingi milioni 4.2
6 :Pundamilia = USD 1200 au shilingi milioni 2.7
7: Fisi = USD 550 au shilingi milioni 1.2
8: Ngiri = USD 450 au shilingi milioni 1
9: Swala = USD 390 au shilingi Laki 9
10: Nyani = USD 110 au shilingi Laki 254

11: Ukipata ajali hifadhini shilingi 200,000 na ukizidisha mwendo faini yake shilingi 30,000

Ni muhimu kuwa na tahadhari pindi uingiapo au upitapo kwenye maeneo ya hifadhi,  Day speed ni 70km/h na night speed ni 50km/h.

Kuwa makini, chukua tahadhari

CHAKA CHAKA NA ALI KIBA WAACHIA AKILI YA MAMA

$
0
0

Na Moshy Kiyungi,Dar es Salaam
Msanii mkongwe Afrika Kusini Yvonne Chakachaka akishirikiana na msanii wa nchini Tanzania Ali Kiba, waliachia rasmi wimbo wao mpya unaoitwa ‘Akili ya Mama’.
 Wimbo huo waliurekodi mwishoni mwa mwaka 2016 jijini Johannesburg, nchini Afrika ya Kusini, ambako Kiba alikuwa ameenda kutumbuiza kwenye tuzo za Mkhaya Migrants Awards.
Akiongea  jijini Dar es Salaam, mapema mwezi huu wa Mei, 2018, Chakachaka alisema wimbo huo ambao amefanya na Ali Kiba,  unawatetea akina mama.
 “Mimi na Ali tumeandika wimbo pamoja, una vibe ya “Mkomboti na tumeimba kwa lugha ya Kiswahili, Ali yupo Comfortable sana kuimba kwenye Kiswahili na amenifundisha kiasi kidogo cha Kiswahili” alisema Chakachaka.
Yvonne aliongeza akisema kuwa “Wimbo huo unawatukuza akina Mama,  Ali anaonekana ni kijana mzuri sana na namshukuru sana kwa kuimba wimbo wa kunitukuza mimi kama Mama na wanawake wengine Afrika.”
Msanii huyo mkongwe wa muziki kutoka Afrika Kusini, amemmwagia sifa lukuki mtunzi na mwimbaji Ali Kiba ‘Mvumo wa Radi’ kwa madai kuwa ni msanii mwenye kipaji cha hali ya juu.
Chakachaka alikuwepo nchini Tanzania kwa ajili ya shughuli za kijamii.
 Yvonne Chaka Chaka ni nani?

Wasifu wa Yvonne Chaka Chaka unaeleza kuwa alizaliwa mwaka 1965 nchini Afrika ya Kusini, akapewa majina ya Yvonne Machaka.
Ni msanii anaye heshimika zaidi nchini humo,  kwa akijihusisha na masuala ya misaada ya kibinadamu na ualimu.Chaka Chaka alipewa jina la ‘Princess of Africa’ kwa mafanikio makubwa kimuziki aliyoyapata kwa miaka 27.
Nyimbo zake zilizotamba ni pamoja na I’m Burning Up, Thank You Mister DJ, I Cry for Freedom, Makoti, Motherland na Umqombothi ambao ulitumika kwenye filamu ya mwaka 2004, Hotel Rwanda.Sifa za Yvonne katika muziki zilivuma zaidi mnamo miaka ya 1980. Kwa juhudi zake, hivi sasa ni mtangazaji na mwendesha kipindi katika kituo cha New Millennium.

Vilevile Chakachaka ni mburudishaji maarufu wa Afrika Kusini na Afrika kwa ujumla.Kwa mara ya kwanza alitikisa katika muziki wa Afrika Kusini, akiwa kijana mnamo mwaka 1984 kwa wimbo wa “I’m in Love with a DJ”.

Muziki wa disko uliotengenezwa na Sello ‘Chicco’ Twala ambao ulikuwa kama muziki wa asili ya Mbaganga, lakini ukiwa na mashairi ya Kiingereza.
 Mtindo huo Mbaganga uliweza kujulikana kama ‘Bubblegum’.
Yvonne Chakachaka sambamba na Brenda Fassi, walibaki wakitamba kwa miaka hiyo ya 1980.

Licha ya kuwa na umri mkubwa, haiba yake yenye mvuto wa pekee bado ipo vilevile.Aidha sauti yake nyororo ilijidhihirisha katika albamu ya Umqombothi mwaka 1988, ambayo ilipendwa na watu wengi.

Albamu hiyo ambayo ilikuwa inasifia pombe ya Kiafrika inayotokana na mtama ilikuwa katika mtindo wa Pop. Ingawa ilifuata kwa karibu desturi za Mbaganga na Singalong katika kiitikio, ambapo iliweza kuwavutia watu wa Afrika Kusini na Afrika kwa ujumla.

Aidha kulikuwa wimbo uliokuwa na jina lilelile la “I’m Love with a DJ”.


Alifanya ziara katika Afrika kwa kufanya matamasha katika viwanja vya Nigeria, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (zamani Zaire).

Chaka chaka mekuwa msanii wa muziki wa Afrika nzima na anaendelea kufurahia hadi leo.Alitambulika kama “Malkia wa Afrika” kutokana na kutembelea Bara la Afrika na uvaaji wake wa kilemba kichwani.

Kwenye miaka ya 1990, Yvonne  aliendelea kufanya ziara na kuuza albamu katika kila nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.Ikumbukwe kuwa aliwahi kutumbuiza katika kundi la viongozi  wa nchi za Afrika pamoja na tukio la kihistoria la kuzaliwa kwa nchi ya Afrika Kusini. 

Mwanamama huyo pia ni mlezi wa mradi wa ‘Giving and Sharing’ ambao unajishughulisha na kusaidia maskini wenye uhitaji, pia inajihusisha ukusanyaji wa mapato ili kupambana na gonjwa la Ukimwi,mfano ni kituo cha Orlando Children’s Home.
  
Aliachia albamu ya ‘Yvonne and Friends’ mwishoni mwa mwaka 2000, ambayo iliwashirikisha wasanii wa kigeni kama vile Tsepo Tshola ambaye alikuwa Sankomota.

Mwaka 2002 alifanya kazi ya kuwa mtangazaji katika radio na Televisheni, hii ilipelekea yeye kuhama kutoka kuwa ‘Malkia wa Afrika’ mpaka kuwa mfanyabiashara maarufu, mburudishaji na muelimishaji.

Yvonne Chaka chaka ameolewa na mwanafizikia kutoka Soweto na ni mama wa watoto wanne.

ZAINABU VULU AFUNGUWA OFISI YA UWT KISARAWE

$
0
0

Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani,Zainabu Vulu akifungua ofisi ya kata UWT Kisarawe mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani,Zainabu Vulu akizungumza na wajumbe wa kata ya Kisarawe ,ambapo alisema Msingi wa kuwa na maisha bora ni kufanya kazi kwa bidii na ameahidi kuendelea kuwaunga mkono ili kuhakikisha wanasonga mbele bila kurudi nyuma.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani,Zainabu Vulu akikabidhi viti kwa Katibu wa UWT kata ya Kisarawe,Moshi Litatilo kwa ajili ya ofisi ya kata hiyo.

Introducing "Goligota" by Gnox john

WAZIRI MKUU AZINDUA MRADI WA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KOROMIJE

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Ujenzi na Ukarabati Mkubwa wa Kituo cha Afya cha Koromije wilayani Misungwi Machi 19, 2019. Kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa, wa pili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Misungwi, Gambadu Samwel.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kukata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua Ujenzi na Ukarabati Mkubwa wa Kituo cha Afya cha Koromije wilayani Misungwi, Machi 19, 2019. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Misungwi, Juma Sweda na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Misungwi, Samwel Gambadu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua Ujenzi na Ukarabati Mkubwa wa Kituo cha Afya cha Koromije wilayani Misungwi, Machi 19, 2019. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Misungwi, Juma Sweda na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Misungwi, Samwel Gambadu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Grace Fabian aliyejifungua mtoto wa kiume katika Kituo cha Afya cha Koromije wilayani Misungwi wakati alipofungua Ujenzi na Ukarabati Mkubwa wa Kituo hicho, Machi 19, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua mradi wa ujenzi na ukarabati mkubwa wa kituo cha afya cha kata ya Koromije wilayani Misungwi na amewahakikishia wananchi kuwa Serikali imejipanga vizuri kuboresha huduma za afya.

Amesema uboreshaji huo unahusisha ujenzi wa chumba cha upasuaji, maabara, chumba cha kujifungulia, wodi ya mama na mtoto na wodi ya wanawake na wanaume pamoja na chumba cha kuhifadhia maiti.Uboreshaji huo unagharimu sh. milioni 500.

Waziri Mkuu alifungua mradi huo jana (Jumanne, Machi 19, 2019) akiwa ziarani Misungwi, ambapo aliwataka wananchi waendelee kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo.

“Hapa zamani kulikuwa na zahanati yenye jengo moja, tumeamua kuboresha na kupandisha hadhi na kuwa kituo cha afya. Rais Dkt. John Magufuli anataka wananchi wapatiwe huduma muhimu zikiwemo za afya karibu na makazi yao”.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema hakuna kijiji chochote nchini kitakachoachwa bila ya kuunganishiwa umeme katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA), vikiwemo na vya wilaya ya Misungwi tena kwa gharama nafuu.

“Rais wetu Dkt. John Magufuli anajali sana wananchi wake, hivyo ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote vikiwemo na wilaya yenu hii ya Misungwi. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu.”

Waziri Mkuu aliongeza kwamba lengo la Serikali ni kufikisha umeme kwenye vijiji vyote Tanzania na vile ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi ya taifa vitafungiwa sola, jambo ambalo litafungua fursa za ajira na kukuza uchumi.

GEO Company ya China yapiga jeki shule za msingi na sekondari wilayani Ileje

$
0
0
Wakati ujenzi wa barabara ya Mpemba hadi Isongole Ileje mkoani Songwe ukiendelea shule za Msingi na Sekondari tayari zimeonja matunda ya mradi huo kwa kumwagiwa vifaa vya michezo,madawati pamoja na redio za kisasa kwajili ya matumizi ya wanafunzi.
Kampuni ya Kichina GEO Company iligawa vifaa hivyo ikiwa ni kujibu kwa vitendo ombi la Mkuu wa Wilaya hiyo Ndugu Joseph Mkude baada ya kuendelea kupokea kero ya kukosekana kwa vifaa hususani vya michezo kwa shule zake.

Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Mwangela aliishukuru kampuni hiyo na akiwataka wanafunzi kujua mataifa rafiki yenye nia njema kwa nchi yetu kwa manufa ya vizazi vijavyo.

Mkuu wa Wilaya hiyo aliwataka wananchi kutobwaga manyanga katikakufanya shughuli za maendeleo wakitegemea kuendelea kupata misaada kama hiyo,bali mipango waliyojiwekea iendelee kutekelezwa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Mhe. Ubatizo Songa Songa akizungumza kwa niaba ya wananchi aliwataka wazazi na walezi kufanya vitu vingine vyenye manufaa kwa elimu baada ya pengo la madawati na vifaa hivyo vingine kuzibwa kwa  msaada huo.

Wanafunzi wa shule hiyo kupitia nyimbo na mashairi waliweza kuonesha furaha jinsi watakavyoongeza bidii katika masomo na michezo.

Hotuba ya kampuni hiyo  ilihimiza umuhimu wa kuwekeza katika elimu ili kufikia malengo mbalimbali ya kitaifa ambayo yakisimamiwa vema huleta maendeleo na kulipa taifa heshima mbele ya mataifa mengine.


Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kakoma Wilayani Ileje mkoa wa Njombe wakifurahia vifaa mbalimbali vilivyokuwa vimewasilishwa hapo shuleni kwao tayari kwa makabidhiano.

Sehemu ya vifaa vya michezo iliyopokelewa na baadaye vitagawiwa kwa shule za Msingi na Sekondari wilayani Ileje

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Mwangela (aliyevaa skafu) akipokea madawati na viti 200 toka kwa mmoja wa wakilishi wa kampuni ya Kichina ya 

GEO Company 

WAFANYABIASHARA NCHINI WAFURAHIA HUDUMA YA VISA KATIKA KUFANYA MALIPO KWA SIMU

$
0
0

*Maofisa Kampuni ya VISA watoa neno kwa Watanzania ...

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii. 
 
WAFANYABIASHARA wanaouza bidhaa mbalimbali nchini na hasa wa Jiji la Dar es Salaam wamepongeza uwepo wa huduma ya VISA katika kufanya malipo ya fedha kwa kutumia simu kwamba si tu umewafanya wawe na usalama wa fedha zao lakini kubwa zaidi imeongeza mauzo. Wamesema kuwa mteja anapotumia huduma ya VISA katika kufanya malipo haoni shida kuchukua fedha kwenye akaunti yake na kulipia anachotoka kuliko anapoamua kulipia kwa fedha aliyonayo mkononi.

Baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema hayo jijini Dar es Salaam kwa nyakati tofauti baada ya maofisa wa Kampuni ya VISA wa ndani na nje ya Tanzania kufanya ziara ya kuwatembelea katika maeneo ya biashara yakiwemo maduka ya nguo, vituo vya mafuta na maduka makubwa na baa ya Samaki samaki kwa lengo la kuangalia namna huduma hiyo ya VISA inavyofanya kazi na ilivyopokelewa na watoa huduma. Kwa mujibu wa maofisa wa VISA ni kwamba biashara zaidi ya 6,000 malipo yake yanaweza kufanywa kwa kutumia huduma ya VISA ambapo kwa kutumia simu ya mkononi mteja atalipia bidhaa aliyonunua.





Mmoja ya maofisa wa Kampuni ya VISA ambao ndiyo wanaotoa huduma ya VISA kupitia simu za mkononi Henry Thuku (aliyeshika simu), akitoa maelezo machache kwa mfanyakazi wa kituo cha mafuta cha Puma na Wanahabari. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA - KAJUNASON/MMG. Wakizungumza na Michuzi Blog jijini Dar es Salaam kwa nyakati tofauti wafanyabishara hao wamesema tangu kuwepo na huduma ya kufanya malipo ya fedha kwa kutumia VISA kumeongeza mauzo yao kwani mteja anapolipia kwa VISA haoni tatizo kuchukua fedha yake iliyoko benki na kisha kulipia bidhaa aliyochukua. 
"Tunao uzoefu, mteja anaponunua bidhaa na kisha akaamua kulipa kwa fedha kwa kutumia huduma ya VISA huwa haowani tabu kununua bidhaa zenye thamani ya fedha nyingi. Uzuri ni kwamba anakuwa na fedha yake benki na anapotajiwa bei anatoa fedha kutoka akaunti yake. "Iikitokea mteja akaja na mfukoni kwake au mkono anayo Sh. 20,000 kwa mfano, ukimwabia bei ya bidhaa anayotaka na ikawa zaidi ya hapo hawezi kununua au ataomba apunguziwe lakini akitumia VISA kwake inakuwa rahisi kuingia kwenye simu yake na kuchukua fedha benki na kisha akalipa,"amesema Meneja Maendeleo wa Kampuni ya Samakisamaki Saum Wengert.
Mkurugenzi Mkuu wa VISA Afrika Mashariki Kevin Langley na Mkurugenzi Mwandamizi wa Mauzo ya Biashara Kennedy Luhombo (mwenye tai) wakinywa Juisi pamoja na ujumbe wao mara baada ya kutembelea duka la Mak Juice lililopo Sinza, Dar es Salaam. Amefafanua kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa wanayo hiyo huduma ya VISA na waliweka utaratibu kwa wafanyakazi ambao wataongoza kwa kuuza bidhaa zao na kisha malipo kufanywa kwa njia ya VISA wanalipwa bonasi. 
"Kwetu hapa anayeuza zaidi na kisha malipo kufanyika kwa VISA tunampa bonasi kama sehemu ya kumtia moyo maana fedha ikilipwa kwa mfumo huo inakuwa salama zaidi na inakwenda moja kwa moja katika akaunti ya kampuni yetu,"amesema. Kwa upande wake Msimamizi wa Kituo cha Mafuta Puma Energy kilichopo Upanga jijini Dar es Salaam Mohamed Omari amesema VISA imerahisisha sana katika kufanya malipo kwani idadi ya wateja ambao wanalipa fedha kwa kutumia VISA imeongezeka. "Wapo wanaokuja kununua mafuta kwenye kituo chetu na malipo ya fedha wanalipa kwa kutumia huduma ya VISA.Tunawapongeza kampuni ya VISA kwa uamuzi wake wa kuleta hii h


Mkurugenzi Mkuu wa VISA Afrika Mashariki Kevin Langley akizungumza na mwanahabari Benard Lugongo (kushoto) wakati wakifanya ziara ya kutembelea maduka yanayotumia huduma ya VISA jijini Dar es Salaam. Mfanyabishara wa duka la nguo JS lililopo Sinza jijini Neema Charles amesema kutokana na malipo mengi kufanyika kwa huduma ya VISA ,kumesaidia kuondoa usumbufu wa kutafuta chenji kwani mteja atatoa fedha kwenye akaunti yake ile ambayo ameambiwa tu. 
 
Pia anasema zamani ilikuwa mteja akitajiwa bei anakwenda nje kutafuta fedha katika Tigo pesa, M-Pesa au Airtel Money ili kupata fedha ya kulipa lakini kwa sasa hakuna usumbufu kwa kutumia VISA ataingia kwenye simu yake na kufanya malipo. Wakati huo huo Meneja wa Shoppers Plaza Maheshi Venktatesh amesema uwepo wa VISA kumesababisha uwepo wa unafuu mkubwa katika kufanya malipo kwani huchukua muda mchache na kupunguza msongamano kwa wateja.
Pia imefanya kuwe na usalama wa fedha , mteja ananunua bidhaa na kulipa kwenya akaunti moja kwa moja, hivyo hakuna hasara ambayo inaweza kujitokeza tofauti na awali kabla ya huduma hiyo. Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Engen Paul Mhato- Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya VIVO Energy Tanzania Limited ambayo inamiliki vituo vya mafuta vya Engen Paul Mhato amesema kwa malipo ya fedha kwa kutumia VISA kumsaidia kukaa na fedha nyingi kwenye eneo la biashara.
 
"Mnapokuwa na fedha nyingi eneo la biashara usalama unakuwa mdogo na wenye tamaa ni rahisi kushawishika na kufanya uporaji wa fedha." Meneja Biashara wa Kadi kutoka Benki ya CRDB Fadhili Mollel amewahamasisha Watanzania kutumia huduma ya VISA katika kufanya malipo mbalimbali na kwamba benki ya CRDB imetambua hilo na hivyo wenye akaunti CRDB wanayo nafasi ya kuifurahia huduma hiyo. "Maduka zaidi ya 2000 yanahudumiwa na CRDB kupitia VISA."

Mkurugenzi Mkuu wa VISA Afrika Mashariki Kevin Langley akizungumza kulea ufafanuzi jinsi VISA inavyoweza kufanya malipo kwa haraka alipofika katika kituo cha mafuta cha Engen Msasani Dar es Salaam. Wakizungumza baada ya kuwatembelea wafanyabiashara hao, maofisa wa Kampuni ya VISA wamesema ni jambo la faraja kuona namna ambavyo huduma hiyo imepokelewa vema na kushika kasi huku wakitumia nafasi hiyo kuwahamasisha Watanzania kuitumia VISA katika kufanya miamala ya malipo. Pia wamesema wataendelea kutoa elimu ya kuufahamisha umma kuhusu umuhimu wa kutumia huduma ya VISA katika kufanya malipo katika simu ya mkononi ."Ni jukumu letu kuwaambia watanzania kwanini huduma hii ya VISA ni muhimu kwao,"amesema mmoja wa wakurugenzi wa VISA Henry Thuku.

Meneja Maendeleo wa Kampuni ya Samakisamaki Saum Wengert (kwanza kushoto) akieleza machache mbele ya wanahabari walitembelea kiota hicho cha maraha cha SamakiSamaki ili kujionea wateja wanavyoweza kunufaika na utumiaji wa huduma ya VISA kupitia siku ya Mkononi. Pembeni yake ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya VISA Afrika Mashariki Kevin Langley.

KING KIKI ALIAPA KUFIA KATIKA MUZIKI

$
0
0
Na Moshy Kiyungi, Dar es Salaam

King Kiki ni mwanamuziki mwenye historia ndefu yenye mvuto wa kipekee, hajawahi kufanya kazi nyingine tofauti na muziki katika kipindi chote cha maisha yake.Licha ya kuonekana bado ana nguvu, mtanashati mwenye tabasamu wakati wote, amefikisha umri wa miaka 72.

Kiki amejijengea umaarufu kwa wapenzi wa muziki wa dansi, kila kona hapa nchini kwa kutoa burudani katika sherehe mbalimbali zikiwemo za Kitaifa.
Kiki aliingia hapa nchini kwa mara ya kwanza mnamo miaka ya 1970, alipofuatana na bendi ya Orchestra Fouvette toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati huo ilikuwa ikitwa Zaire.

Bendi hiyo iliyofanya maonesho yake ya muziki humu nchini ikiwa ya uongozi wa Fred Ndala Kasheba. Mwandishi wa makala hii alifanikiwa kufanya mahojiano maalum na nguli huyo nyumbani kwake Mtoni kwa Azizi Ali, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Katika mahojiano hayo King Kiki alieleza kwa undani historia ya maisha yake, ikiwamo ya muziki, mafanikio na njia alizopitia hadi kufikia hapo alipo. Akiwa na tabasamu tele usoni mwake, alianza kuelezea Wasifu wake akitamka majina yake kuwa anaitwa Kikumbi Mwanza Mpango.

Kiki alisema kwamba alizaliwa Januari 01, 1947 katika mji wa Lubumbashi uliopo katika mkoa Katanga huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). “Mimi ni mtoto wa tano kwa kuzaliwa toka kwa wazazi wangu mzee Katambo Wabando Paulino na mama yangu Mwanza Jumban Elia Maria…” alisema Kiki.

Alieleza kwamba akiwa na umri wa miaka sita akisoma shule ya awali mwaka 1952, kundi la muziki kutoka Afrika Kusini likiwa limeambatana na mwanamuziki mahiri Miriam Makeba ‘Mama Afrika’, lilifanya ziara nchini mwao. Kiki aliendelea kusimulia kwamba wakati huo alikuwa na kaka yake aliyemtaja kwa majina ya Koroumba Joseph.

“Kwa bahati nzuri kaka yangu alikuwa akinipenda sana, hivyo muda mwingi nilikuwa nikiongozana naye kwenye dansi, hususan mwishoni mwa wiki, hata kwenye onesho la Miram Makeba alinipeleka...” alisema King Kiki. Licha ya miaka mingi kupita hajamsahau kiongozi wa kundi hilo aliyekuwa anaitwa Dambuza Mulele.

Wanamuziki wengine wa kundi hilo walikuwa akina Sekena Kolaye, Tigizi Kwankwa, Dolira Jebe na mwenyewe nguli Miriamu Makeba. Miriam Makeba aliyekuwa akiongoza safu ya uimbaji kwa pamoja na wanamuziki wa kundi hilo, waliimba na kucheza kama vile hawana mifupa kwenye miguu na mwili kwa ujumla.

Kiongozi wao Dambuza Mulele, alikuwa na sauti nzito hivyo alikuwa ‘akichombeza’ maneno walipokuwa wakiimba kama afanyavyo Koffi Olomide katika baadhi ya nyimbo zake. Kiki alisema kwamba mwimbaji Miriam Makeba alipokuwa anaimba, alikuwa anaona kama jina hilo halikumstahili kuitwa.

Akawaza kama angelipewa fulsa ya kumtafutia jina linaloendana na hadhi yake. Kwa bahati nzuri wakati akiwaza hivyo, akasikia kiongozi wa bendi hiyo akipaza sauti akisema anapenda kumwita mwanamama huyo ‘Chocolate girl’. “Kwa kweli nimezunguka nchi nyingi kufanya muziki, nimeona shoo nyingi za Kimataifa, hakuna aliyewahi kuvunja rekodi ya kile nilichokiona siku hiyo kwa Miriam Makeba...” alisisitiza King Kiki.

Mwaka 1953 alipelekwa kwenda kuanza masomo ya awali akiwa na umri wa miaka sita. Baadae aliendelea na elimu ya msingi katika shule ya Officialle Laique de Kolwezi, ambako alimaliza darasa la saba mwaka 1959. Kikumbi alitamka kuwa wakati akiwa darasa la nne, baba yake aliyekuwa mfanyakazi katika kampuni ya madini inayotambulika kwa majina ya Gecamiou Athenee Royale kwa sasa, alipata uhamisho na kuhamia katika mji wa Likwasi huko DRC.

Wakati huo kampuni hiyo ilikuwa ikijulikana kama Union Miniere Du Hut Katanga. Kiki tangu zamani alikuwa anapenda sana kuimba, ambapo mwalimu wake akaliona hilo akamjumuisha katika vikundi vya ngoma na muziki shuleni hapo. Akawa anachukua utaalamu wa kucheza mitaani na kuupeleka shuleni, akawaunganisha wanafunzi wenzake watatu na kuanzisha kikundi cha muziki wa dansi wakiwa darasa la tano.

Walimu wake waliupenda muziki wao na jinsi walivyokuwa wakiimba na kucheza. Hivyo kila sherehe za shule waliitwa kutoa burudani. Sifa za umahiri wa kundi hilo zikavuma ikizingatiwa kwamba walikuwa vijana wadogo wanaofanya mambo makubwa. “Haikuishia hapo hata katika sherehe za watu wa karibu na shule yetu, wanafunzi waliokuwa na sherehe majumbani mwao walikuwa wanatualika tunakwenda kuimba na kucheza bure…” alisema King Kiki.

Alifafanua kuwa mbali na kupenda muziki, pia alikuwa mahiri katika masomo darasani. Kikumbi alijigamba kwamba hakuwahi kuwa mtu wa tatu kila anapofanya mtihani na akifeli sana alishika nafasi ya pili. Akiwa shuleni hapo, alikuwa akipendekezwa kufanya fani mbalimbali zikiwemo za maigizo, ngoma kuimba na kucheza.

Kiki wakati akiwa bado masomoni mwaka 1958, alijiunga na kikundi cha watoto wenzake cha Bantu Negro, waliweza kubadili muziki huo kwenda kwenye muziki wa rumba. Bendi ya Bantu Negro ilikuwa ikifanya maonesho ambayo watazamaji walikuwa wanaketi wakiwatazama na kusikiliza jinsi vijana hao wanavyo poromosha muziki wakitumia ala.

Mwanza Mpango alijiunga na masomo ya sekondari kidato cha kwanza katika shule ya Attene Iwayala, mwaka 1960. Kwa kuwa Kiki muziki ulikuwa umemtawala sana, mwaka 1962 ilimlazimu kuacha shule akiwa kidato cha tatu, akaanza kuimba rasmi mwaka huo. Hata hivyo alikuwa akikumbana na kizingiti kikubwa toka kwa wazazi wake ambao hawakupenda kabisa awe mwanamuziki, walimtaka aendelee na masomo shuleni.

King Kiki anakiri kuwa muziki ulikuwa umemuingia ndani ya damu, akawa akipigwa na wazazi wake ili aende shule, lakini hakubadili msimamo wake.
 “Kaka yangu alikuwa akinifunga kamba kwenye baiskeli huku akinikimbiza umbali wa Kilometa takriban 20, kama adhabu ya kutokwenda shule lakini yote hayo haikusaidia…” alitamka Kiki huku akitabasamu.

Alisema ukali wa kaka na wazazi wake alilazimika kutoroka nyumbani na kwenda kujihifadhi kwa marafiki zake. Usemi usemao kwamba “Uchungu wa mwana ajuwae mzazi” ulijidhihirisha pale wazazi wa Kiki kuaona kwamba kijana wao mwenye akili sana darasani ameshindikana. Baba yake alimuweka chini akamuuliza iwapo atakuwa tayari kufanya kazi nyingine yeyote tofauti na muziki.

Pasipo woga mbele ya baba huyo, Kiki alimjibu kwamba muziki umemteka sana na kwamba atakufa nao. Kwa majibu hayo baba yake akawa hana jinsi, ila alimbariki na kumtakia mafanikio mema katika muziki. “Baba aliposema hivyo, niliruka ruka kwa furaha, nikajihisi kama nilikuwa naelea katika dunia ya wapenda muziki…” anasema Kiki.

Mwaka 1964 akaenda mkoa wa Kasai ambako alijiunga na bendi ya Norvella Jazz. Katika mazungumzo hayo, Mwanza Mpango aliwataja wanamuziki wakongwe waliomfanya kubadili mfumo wa muziki akiwa katika bendi hiyo. Aliwataja akina Tchamala Joseph Kabasele ‘Grand Kale’, Tabu Ley na Fanco Luambo Makiadi.

Yeye pamoja na wanamuziki wenzake wa bendi ya Norvella Jazz, walilazimika kutafuta vyombo vingine vizuri vya muziki. Wakapita katika vikundi mbalimbali hadi wakafika mkoa wa Kasai (Mbudji Mai). Huko walikutana na vikundi mbalimbali kutoka mkoa wa Kinshasa vya African Jazz, Conga Success, Negro Success, Eco Bantu, African Fiesta vita na vingine mbalimbali, vilivyomfanya kupata uzoefu zaidi katika muziki wa rumba mwaka 1965.

Kiki alipiga muziki na bendi hiyo hadi mwaka 1967, lakini mara alipoondoka bendi hiyo ikasambaratika naye mwaka 1968 akarudi mkoa wa Katanga. Akiwa mkoani humo, alikutana na wanamuziki wa bendi ya Videt Jazz, iliyokuwa ikitoka nchini Zimbabwe. Mwanza Mpango alisimulia Kaka yake aliyekuwa na bendi yake, ilimzidishia hamasa katika muziki.

Aliwakumbuka baadhi ya wanamuziki waliokuwa wakifanya kazi na kaka yake ambao ni Zapta Mfana, Kumaro Kadima, Andre Kaka na Joseph Kolomba. “Naweza kusema hao walinipa ujuzi mkubwa kwani nilijifunza kupiga vyombo pamoja nao, hapo ndipo nilipopenda kucheza, sikuwa mnene kama nilivyo sasa ungeniona ungefurahi…” alisema Kikii akiyatikisa maungo yake yaliyojaa minofu.

Alieleza kuwa ipo picha ya video iliyorekodiwa wimbo wa ‘Kasongo rudia’ wanaonekana yeye, Chinyama Chiyaza, Mtombo Lufungula, Mbuya Makonga, Kanku Kelly wakicheza kwa kupishana huku na kule wakati huo bado vijana. Kuna wakati Kikumbi alikuwa akipata mialiko ya huku na kule kiasi cha kutambuliwa na Wakurugenzi wa makampuni ambao walimuahidi kumpatia vyombo vya muziki.

Kwa ujasiri wa aina yake alikuwa akikataa. Hakuwa tayari kufanya kazi chini ya kampuni ya mtu, akijielekeza katika kutafuta njia ya kujikwamua mwenyewe kwa kutumia jasho lake.  “Nikiwa napiga muziki kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo, baadhi ya pesa nilizokuwa nikizipata nilipelekea kwa baba yangu kumuonesha kuwa muziki unalipa…” Kiki alitamka.

Hata hivyo wazazi wake pamoja na kuzipokea pesa hizo, bado walikuwa wakimshauri kwamba anayo nafasi ya kurudi shule kuendelea na masomo. Kauli hizo za wazee wake akaona bora awe mbali na nyumbani. Alikuwa mwanamuziki Fred Ndala Kasheba aliyemkaribisha King Kiki kujiunga katika bendi ya Orchestra Fouvette.

Alipojiunga na bendi hiyo Kiki alianza kuimba nyimbo mbili zilizotamba sana, nazo ni ‘Jacqueline’ na ‘Kamarade ya Nzela’ ambazo ndizo zilizompa nafasi ya kufuatana na bendi ya Fouvette kuja nchini Tanzania. Ikiwa hapa nchini bendi hiyo iliweza kuzikonga nyoyo za wapenzi na mashabiki wa muziki wa dansi katika maonesho yao kadhaa.

Bendi hiyo baada ya kufanya maonesho hayo, ilirejea kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako waliamua kubadili majina, ikaitwa Safari Nkoi.
Mwaka 1977 Kikumbi Mwanza Mpango akiwa kwao DRC, alifuatwa na Chibangu Katayi ‘Mzee Paul’, aliyekuwa mmoja kati ya viongozi wa bendi ya Maquis du Zaire iliyokuwa tayari ipo katika jiji la Dar es Salaam.

Kiki hukukurupuka kukubali bali alianza kumhoji Mzee Paul iwapo Wanamuziki waliopo Maquis du Zaire wanakidhi viwango? Majibu ya Mzee Paul yalionesha wasiwasi, ndipo yeye akapendekeza wachukuliwe wanamuziki wengine toka huko DRC.

Kiki aliwapendekeza wanamuziki wa kuondoka naye kuja nchini Tanzania akiwemo Nkashama Kanku Kelly, aliyekuwa akipuliza tarumbeta, Mutombo Sozy, aliyekuwa akizicharanga drums, Ilunga Banza ‘Banza Mchafu’na aliyekuwa akipiga gitaa la besi.

Wakiwa safarini kuja nchini, walipitia mji wa Kamina, ambako walimpata mwanadada Ngalula Tshiandanda, aliyekuwa mnenguaji katika bendi ya Sakayonsa ya mjini humo. Bendi ya Maquis du Zaire wakati huo ilikuwa chini ya uongozi wa mwanamuziki Chinyama Chiaza ‘Chichi’.

Baada ya kutua Maquis, Kiki alianza kuonesha cheche zake baada ya kubuni mtindo wa Kamanyola, ambao baadaye ukawa gumzo katika jiji la Dar es Salaam na viunga vyake. Alieleza maana halisi ya Kamanyola akisema Kamanyola ni mji huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

“Nilitunga mtindo huo baada ya kujiunga na bendi hiyo mwaka 1977, niliongeza maneno ya ‘bila jasho’. Kwa maana mchezaji wa muziki huo atacheza taratibu kwa raha zake huku akijidai…” Kiki alifafanua. Mwaka huohuo  kulifanyika sherehe za sikukuu ya Wakulima kitaifa mkoani Mbeya. Bendi ya Maquis du Zaire ilialikwa kwenda kutoa burudani. Baada ya kurejea Dar es Salaam, walitunga wimbo wa ‘Safari ya Mbeya’.

Kwenye wimbo huo, sauti ya King Kiki inasikika akianza kwa kughani. Umahiri wa kutunga na kuimba Kiki aliedelea kuachia vibao vya ‘Nimepigwa Ngwala’, Kiongo na ‘Kyembe’. Baadhi ya nyimbo nyingine alizoshiriki kutunga na kuimba ni pamoja na Kasongo, Kibwe Mutondo, Sofia, Mokili, Yoka Mateya Babote, Dora mtoto wa Dodoma, Sababu ya Nini, Usinifiche siri, Noele Krismas na nyingine nyingi.

Bendi ya Maquis du Zaire iliingia nchini mwanzoni mwa miaka ya 1970 kwa mbwembwe nyingi ikipiga muziki kwa mtindo wa ‘Chakula chakula Kapombe’. Lakini ilikuja kusambaratika ikiporomosha muziki maridadi katika ukumbi wa White House, Ubungo jijini Dar es Salaam.

Safu ya waimbaji wenzake wakati huo walikuwa ni akina Mbuya Makonga ‘Adios’, Mutombo Lufungula ‘Audax’, Mukumbule Lolembo ‘Parashi’,  Kiniki Kieto, Abubakar Kasongo Mpinda ‘Clyton’, Mbombo wa Mbomboka, Tshimanga Kalala Assosa na Masiya Radi ‘Dikuba Kuba’. Safu hiyo ilikamilishwa kwa waimbaji Issa Nundu na Tabia Mwanjelwa.

Waswahili wanasema “Chema Chajiuza” Usemi huo ulijidhihirisha baada ya miaka miwili, akatafutwa na mfanyabiashara maarufu katika jiji hilo la Dar es Salaam, Hugo Kisima. Kisima alikuwa mmiliki wa ukumbi wa Safari Resort na bendi ya Orchestra Safari Sound (OSS), iliyokuwa na makao yake katika huko Kimara, jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo yao waliafikina kuondoka katika bendi ya Maquis du Zaire, akajiunga na OSS, baada ya ‘kumegewa’ kitita cha fedha. Baada ya kuingia OSS, alishirikiana vyema na waimbaji wa bendi hiyo akina Skassy Kasambula, Monga Stani Liki, Dingituka Molay, Mobali Jumbe, Kalala Mbwebwe, Tshibanda Sony na Kabeya Badu.

Aidha Kiki alitambulisha mtindo mpya wa ‘Masantula Ngoma ya Mpwita’. Pamoja na tungo zake nyingi kuna kumbukumbu zisizosahaulika katika enzi za mtindo wa Masantula. Kikumbi alipotunga na kuimba nyimbo za Mimi msafiri, Mama Kabibi na Kitoto kaanza tambaa, zilimletea sifa nyingi sana kwa wapenzi wamuziki wa dansi wakati huo.

Wimbo wa Mimi msafiri, alikuwa akijibashiria kuwa bendi hiyo ndiyo ingelikuwa ya kuzeeka nayo. Lakini mambo hayakuwa hivyo kwa kuwa aliamua kujikwamua badala ya kuajiriwa.

Mwaka 1982 alipata ufadhili toka kwa Dk. Alex Khalid, ambaye alisafiri naye kwenda Ujerumani kununua vyombo vya muziki. Aliporejea na vyombo hivyo vipya, ndipo alipoanzisha bendi yake ya King Kiki Double O’ iliyokuwa ikitumia mtindo wa ‘Embalasasa shika breki’. Baadhi ya nyimbo walizotamba nazo ni  za ‘Kitoto kaanza tabaa, Dodoma Capitale , Pilikapilika Mtaa wa Samora, Lamanda , Malalamiko  Njigina, Salamule, Mtoto wa Elia, Sababu ya Nini na Malalamiko.

Mwaka 1997 bendi hiyo ilikufa kufuatia uchakavu wa vyombo vya muziki. Baada ya kusambaratika bendi hiyo, Kiki aliitumia talanta yake katika muziki akawa msanii mgeni au mwalikwa katika bendi mbalimbali. Moja kati ya bendi ambazo alikuwa akishiriki maonesho yao bila kuajiriwa, ilikuwa ni ya Orchestra Sambulumaa ‘Wana Zuke Muselebende’.

Bendi hiyo ilikuwa ikiongozwa na mfanyabiashara Emmanuel Mpangala pamoja na mwanamuziki Chimbwiza Mbambu Nguza ‘Vicking’, aliyekuwa ameiacha bendi ya Maquis du Zaire. Kiki alifanya shughuli hiyo kwa takribani miaka minne, akaondoka kwenda kuungana na Fred Ndala Kasheba.

Kwa umoja wao wakaunda bendi ya Zaita Musica mwaka 1994, iliyokuja kuwa maarufu hususani baada ya kuachia wimbo wa ‘Kesi ya Kanga’. Hapo ndipo mtindo wa ‘Kitambaa Cheupe’ ulipozaliwa. Mwaka 2003 akiwa na Ndala Kasheba walianzisha bendi ya La Capitale ‘Wazee Sugu’.

“Lakini kwa mapenzi ya mungu mwenzangu Kasheba akafariki dunia mwaka mmoja baadaye, yaani 2004…” alisema Kiki. Bendi hiyo bado inauendeleza mtindo wa Kitambaa cheupe ambao umeiletea bendi yake wateja wengi wanaopenda muziki wa kistaarabu wakicheza na vitambaa vyeupe mikononi.

Alifafanua kitendo cha kuweka Kitambaa Cheupe ni kama ishara ya upendo na amani. Kikumbi alishirikana vyema na mtunzi na mwimbaji mahiri Baziano Bwetti, ambaye pia walikuwa wote katika bendi ya Orchestra Fouvette. Baada ya kuishi kwa muda mrefu humu nchini, aliamua kuomba Uraia wa Tanzania.

Kiki alizifuata taratibu zote za Idara ya Uhamiaji, hadi mwaka 1997, alipokubaliwa kuwa raia halali wa Tanzania. Kiki na bendi yake hiyo miaka ya 2000, walifanikiwa kwenda katika jiji la London nchini Uingereza, ambako waliporomosha muziki maridadi kwa Wantanzania waishio huko. Baada ya kurejea nchini, akatunga wimbo uliopewa jina la ‘Safari ya London’.

Katika wimbo huo uwalielezea jinsi safari yao ilivyofana wakiwataja baadhi ya watu waliofanikisha ziara hiyo wakiwemo baadhi ya maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza. Ukisikiliza mirindimo ya wimbo huo, hataitofautisha sana na ile ya wimbo wa ‘Safari ya Mbeya’. Baada ya kukongwa na nyoyo za baadhi ya mashabiki na wapenzi wake walimpachika majina ya ‘Bwana Mukubwa’.

King Kiki anayo imani kwamba bendi ya La Capitale ‘Wazee Sugu’ iliyoundwa mwaka 2003, ndiyo bora kwa muziki wa dansi kwa sasa. Alipoulizwa nini  kilichomshawishi zaidi kuwa mwanamuziki. Kiki alieleza kuwa alishawishika kuingia kwenye muziki akiwa na miaka sita, baada ya kumshuhudia mwanamama Miriam Makeba, toka Afrika ya Kusini alipofanya maonesho nchini mwake.

Kikumbi ‘aliifagilia’ bendi yake ya La Capitale iliyoundwa mwaka 2003, kuwa ndiyo bora kwa muziki wa dansi kwa sasa, na huenda ikawa ndiyo atakayozeekea nayo. Aidha Kiki aliweza kusimulia siri ya mafanikio ya kung’ara kwake akisema “…inawezekana kung’aa kwangu katika muziki kunatokana na nyota njema iliyojionyesha mapema, kwani nilizaliwa Januari Mosi, saa 11 alfajiri…” 

Akiainisha baadhi ya mafanikio aliyokwisha yapata katika muziki kuwa ni pamoja na kuweza kusafiri kwenda kufanya maonesho katika mataifa mbalimblai makubwa duniani likiwemo la Marekani. Kiki alitamka kuwa alipokuwa huko Marekani, aliweza kukidhi kiu ya Waafrika waishio huko alipoporomosha ‘bonge la shoo’ akiwashirikisha wanamuziki wa kundi la Soukuos Stars Lokassa ya Mbongo na Ngouma Lokito.

Aidha alisema ameweza kumudu maisha yake na familia kwa ujumla pia kumiliki bendi mbili nyingine ipo katika jiji la Mwanza. Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’ ni baba wa familia ya mke na watoto kadhaa. Kati yao ni binti mmoja pekee aliyefuata nyayo za baba yake katika uimbaji. Nguli huyo alionesha kujali ukweni kwake mkoani Mbeya, alipotunga na kuimba wimbo wa Barua.

Katika wimbo huo anaagiza kufikishiwa salamu afikapo Igulusi, Uyole, Makambako na kwingineko. Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’ bado anaendeleza talanta yake ya muziki katika jiji la Dar es Salaam na kwingine anako alikwa.

TSHIMANGA KALALA ASOSSA ASIYECHUJA

$
0
0
Na Moshy Kiyungi, Dar es Salaam
Tshimanga Kalala Assosa ni mwanamuziki maarufu aliyewahi kupiga muziki katika bendi kubwa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo za Negro Success, Les Kamalee, Lipua Lipua na Fuka Fuka. Akiwa katika bendi hizo alishirikiana wanamuziki nguli akina Bavon Marie Marie, Nyboma Mwandido, Pepe Kalle na Georges Kiamuangana Mateta Wazela Mbongo ‘ Verckies’.

Asossa hata leo utakapokutana nae mitaani au ukimuona awapo jukwaani, hauwezi kudhani kuwa ni mzee wa miaka 68 hivi sasa. Ni mtanashati, mcheshi asiye na majivuno pia hupenda kuongea na watu wa rika zote. Tshimanga Asossa ana vipaji vya kutunga na kuimba nyimbo za muziki wa dansi pia ni hivi sasa ni kiongozi wa bendi ya Bana Maquis.

Mwandishi wa makala hii alimtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, ambapo alisema kuwa alizaliwa katika mji wa Kamina uliopo Jimbo la Shaba huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mnamo tarege Aprili 04, 1949. Asossa alipata elimu ya Sekondari katika shule iliyojulikana kama Charles Ruangwa hapo Kamina.

Alianza kuimba akiwa bado mdogo na kwamba alijipeleka mwenyewe katika kwaya ya Kanisa la Mtakatifu Baram huko Kamina ambako Mapadri walimsaidia kumfunza muziki. Pamoja na juhudi zake hizo, Baba yake mzazi kamwe hakutaka mwanaye ajitumbukize katika muziki,  alimtaka afuate masomo yake shuleni.

Baada kumaliza kidato cha nne, baba yake alimpeleka Chuo cha Ufundi cha Kamina. Asossa muziki ulikuwa ndani ya damu yake, hivyo kila siku baada ya kutoka Chuoni alikuwa akienda kuangalia mazoezi ya bendi iliyokuwepo hapo Kamina ya Super Gabby.

Ikumbwe Super Gabby ndiyo ilikuja kubadilishwa majina hatimaye ikaitwa Orchestra Maquis du Zaire, iliyoingia humu nchini mwaka 1972. Mazoezi hayo yalimtia hamasa kubwa ya kupenda muziki.

Siku moja aliomba apewe nafasi kujaribiwa kuimba katika bendi hiyo. Asossa alikubaliwa akaingia stejini kuimba, lakini kabla hajamaliza kuimba ghafla baba yake alitokea ukumbini humo na kumcharaza viboko. Pamoja na makatazo yote hayo, hatimaye baba yake alikubali ombi la mwanaye baada ya kubaini kuwa hashikiki wala habadiliki kitabia.

Mwaka 1969, Tshimanga alikwenda Kinshasa kutafuta maisha. Kwa bahati nzuri alikutana na mwanamuziki Bavon Marie Marie akampeleka kwa mmiliki wa bendi moja katika jiji hilo aliyejulikana kama Didi Kalombo.

Asossa aliitumia vyema nafasi hiyo ya kujaribiwa sauti ambapo mmiliki huyo alimkubali, hapo ikawa chanzo kuanza kutimiza ndoto zake kwa kupata ajira katika bendi hiyo. Asossa anazikumbuka changamoto alizokutana nazo za kuwakuta wanamuziki wa bendi hiyo wakiwa watanashati kuliko yeye, mavazi mazuri zikiwemo suti na wote walikuwa wang’aavu usoni wakitumia vipodozi (mkorogo).

Pamoja na hayo, sauti yake ndiyo iliyomuokoa na kupewa heshima kama wanamuziki wengine. Kiongozi wa bendi ya Negro Success Bavon Marie Marie alipofariki kwa ajali ya gari, bendi hiyo iliteteleka na hatimaye ikafa. Mwaka 1974 Assosa alikutana na Nyboma Mwandido na kumueleza kwamba anatakiwa na mmiliki wa bendi ya Lipua Lipua, aliyejulikana kwa majina ya Kiamuangana Mateta Wazela Mbongo "Vickie’s".

Alipofika huko alitakiwa kujaribu kuimba sauti ya Pepe Kalle, ambaye alikuwa amekwisha ondoka. Hata hivyo, hakujua ujasiri aliupata wapi siku hiyo pale alipomtamkia mmiliki huyo kwamba hayuko tayari kuimba sauti ya mtu, bali aachiwe aimbe sauti yake halisi ambayo baadaye uongozi ulimkubali.

Akajiunga na bendi ya Orchewstra Lipua Lipua ambako aliungana na wanamuziki wengine wakali. Wakiwa na Lipua Lipua waliibuka na vibao vikali vilivyotisa jiji la Kinshasa vya Mombasa, Nikibwe na Amba. Mwaka 1975 bendi hiyo iliingia katika mgogoro kati ya mmiliki wa Bendi hiyo na wanamuziki. Asossa aliamua kuondoka na kwenda kujiunga na Bendi ya Les Kamale.

Akiwa na Les Kamale walitoka na nyimbo ambazo hadi hivi sasa bado zinatamba katika ulimwengu wa muziki za Abisina, Masuwa, Aigi na nyingine nyingi. Wanamuziki wa Bendi hiyo baada ya mafanikio yao ya ghafla, walilewa sifa na kujiamini kupita kiasi. Hiyo ilitokana na kitendo cha kulipwa maslahi murua, walinunua vyombo vyao vya muziki na magari ya kubebea vyombo hivyo.

Mbwembwe zikazidi na kusababisha kusahau wajibu wao katika kazi, zilizopelekea bendi ya hiyo kufa mwishoni mwaka 1975. Baada ya hapo Asossa alikaribishwa kujiunga katika bendi ya Fuka Fuka iliyokuwa ikiongozwa na Mule Chibauma. Akiwa na Bendi hiyo mwaka 1978 ilifanya ziara hapa nchini Tanzania.

Fuka Fuka ilipoingia Dar es Salaam ilikuwa na nyimbo zake mpya za Bitota, Lomeka, Baba Isaya, Papii na Funga Funga ambazo alizielezea kwamba zailiwaduwaza wapenzi wa muziki wa jiji la Dar es Salaam wakati huo. Bendi hiyo baadaye iliingia mkataba wa kupiga muziki kwa miezi sita na Chama cha mateksi Dereva cha Tanzania Transport, Tax and Services (TTTS) ambacho pia kilikuwa kikimiliki ukumbi wa Mlimani Park.

Baada ya kumaliza mkataba Fuka Fuka waliondoka kurejea kwao wakipitia Nairobi nchini Kenya na Kampala huko Uganda. Wakiwa Kampala kwa bahati mbaya nchi hiyo ilikuwa imeingia vitani, ikipigana na Tanzania mwaka 1979.

Vita hivyo viliiwaathiri kwa kiasi kikubwa kwani wakiwa Uwanja wa ndege wa Entebbe wakisubiri kurejea kwao, vurugu za vita ziliwakaribia, wao wakakimbia wakiviacha vyombo vyote vya muziki uwanjani humo ilihali kila mmoja akitafuta njia ya kunusuru maisha yake. Mwaka 1981 akiwa kwao Kongo, Assosa alifuatwa na mfanyabiashara toka Tanzania aliyemtaja kwa jina la Joseph Mwakasala ili kuja Tanzania kupiga muziki katika bendi ya Mlimani Park Orchestra kwa mkataba wa miezi sita. Akiwa Mlimani Park Orchestra alikutana na wakali wa muziki wa Tanzania, akina Muhidini Maalim Gurumo, Michael Enoch, Abel Balthazar, Joseph Bartholomew Mulenga na Cosmas Tobias Chidumule.

Baada ya kumaliza mkataba mwaka 1982, Tshimanga Kalala Asossa alichukuliwa na mzee Kitenzogu Makassy katika bendi yake ya Orchestra Makassy alikodumu hadi mwaka 1986. Akiwa hapo alitoa wimbo ulioshika chati wa Athumani. Mwaka huo huo aliamua kuanzisha bendi yake ya Orchestra Mambo Bado, akatoka na wimbo wa ‘ Bomoa Tutajenga kesho’ Wimbo huo ulitafsiriwa vibaya na baadhi ya watu kwamba haukuwa na maadili mema.

Bendi hiyo ilijengewa mizengwe na kusababisha kasambaratika baada ya muda mfupi. Assosa alichukuliwa na bendi ya Maquis du Zaire iliyokuwa ikiongozwa na Chinyama Chiyaza kwa wakati huo mwaka 1987. Alipigia bendi ya Maquis hadi ilipo sambaratika. Baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo akiwemo yeye walijipanga na kuisuka bendi kwa jina jipya la Maquis Original.

Wakaaza kupiga muziki katika ukumbi wa Wapi Wapi’s na baadaye wakaenda Kata ya 14 huko Temeke jijini Dar es Salaam. Maquis Original ikafanya makao yake makuu katika ukumbi mpya wakati huo wa Lang’ata uliopo Kinondoni mano miaka ya 1990. Akiwa hapo wapenzi wa Maquis Original walimpa jina la ‘mtoto mzuri’ kufuatia utanashati wake.

Baadaye alichukuliwa na mfanyabiashara wa Jijini Dar es Salaam, Paul Kyala kuimarisha bendi ya Legho Stars. Akiwa na bendi hiyo alifyatua vibao vya Francisca, Afra, Moseka na vingine vingi. Baada ya kumaliza mkataba aliungana na wanamuziki aliokuwa nao Maquis du Zaire ambao walikuwa wameanzisha bendi ya Bana Maquis. Anawataja akina Kasongo Mpinda ‘Cryton’, Mukumbule Lulembo ‘Parashi’, Mbuya Makonga ‘Adios’, Mutombo Lufungula ‘Audax’ na Ilunga Banza ‘Banza Mchafu’.

Tshimanga Kalala Asossa licha ya kufaya muziki, pia mtunzi wa vitabu. Ameweza kutunga kitabu cha ‘JIFUNZE LINGALA KWA KISWAHILI’, ambacho kipo sokoni nchi nzima. Aidha husikika akitafsiri na kuuelezea muziki na wanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo cha Cavacha Time kila Jumamosi asubuhi kupitia TBC FM.

Assosa ana familiya ya mke na watoto kadhaa. Mkewe ni binti wa aliyepata kuwa na nyadhiza nyingi zikiwemo za ubunge na  Uwaziri Bwana Paul Kimiti.

TSHALA MUANA MWENYE VITUKO JUKWAANI

$
0
0
Na Moshy Kiyungi, Dar es Salaam
Tshala  Muana ni mwanamuziki maarufu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mwenye vituko visivyolingana na umri wake awapo jukwaani. Mama huyo hivi sasa ni mtu mzima mwenye umri wa miaka 61 sasa, alizaliwa Mei, 13, 1958 katika mji wa Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Majina yake halisi anaitwa Elizabeth Tshala Muana Muidikay. Ni mama mwenye sura na umbile la kuvutia kwa mtu yeyote atakayemuona.Tshala Muana anavyo vipaji vingi kikiwemo cha kutunga na kuimba pamoja na uwezo mkubwa kunengua jukwaani.

Mama huyo alianza muziki mwaka 1977 akiwa katika bendi iliyokuwa na majina ya Tsheke Tsheke Love. Elizabeth Tshala Muana Muidikay maarufu kama ‘ Malkia wa Mutuashi’  au ‘Kasa wa Mutshanda’ ni bingwa  wa miondoko ya mtindo wa Mutuashi ulio na sili ya utamaduni wa kabila la Baluba toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mwaka 1982 aliamua kuwa mwanamuziki wa kujitegemea na akaweza kupata mafanikio makubwa kwa kazi zake. Katika kipindi cha miaka 20 ya kuvuja jasho, Tshala alifyatua album 19 mnamo mwaka 2002. Tshala Muana ameunda kikundi chake kiitwacho Dynastie Mutuashi. Baadhi ya nyimbo ambazo bado zinaendelea kutamba ni pamoja na Dezo dezo, Karibu yangu, Kokola, Tshbola, Seli Pere, Mutuashi, Amina, Chena, Nasi Nabali, Benga na Na respect.

Zingine ni pamoja na Baba Nima, Vundula, Sukisa, Mpokolo, Golgotha na Lekela Muadi. Tshala ameachia ngoma nyingine za Malu Parole, Tshaza, Dinanga, Nkashama, Dikeba, Tshikuna Fou, Cicatrice d’amour, Viluka Dilolo, Burkina Faso, Nguma Yanyi na Luadia Bombo

Muana amekwisha shida zawadi katika mashindano ya Kora Award mwaka 2003 kama mwanamuziki bora wa kike toka nchi za Afrika ya Kati. Katika sherehe hizo za Kora Award, Muidikay hakuweza kuhudhuria kufuatia hali ya uchumi ulokuwa ukimkabiri wakati huo. Muana baadaye katika mahojiano na vyombo vya habari alikiri kwamba yeye pamoja na wanamuziki wake  walitakiwa kuwa na Pauni 4,000 kwa ajili ya usafiri wa ndege  wa kwenda Afrika ya Kusini  kuhudhuria na kupokea zawadi yake.

Wakati huohuo mwanamuziki mwanamuziki mwenzake Charls Antonie Kofi Olomide, alikuwa amepata bahati ya ya kupata tiketi kumi toka kwa waandaji wa Tamasha hilo. Wasanii wengine toka nchi mbalimbali walihudumiwa na serikali zao, bingwa huyu wa Mutuashi aliwahi kukiri katika mahojiano kushindwa kwake kuhudhuria sherehe hizo akisema zilihitajika Dola za Kimarekani 4,000 kwa ajili tiketi za ndege kwa yeye na wanamuziki wake kwenda Afrika ya Kusini.

Akiwa kama mwimbaji bora wa Mutauashi, Afro- Cuban aliyoitambulisha huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Tshala Muana anajulikana mno kwa umahiri wa kulimiliki jukwaa akicheza kwa kujiachia na wakati mwingine huwaduwaza wapenzi na mashabiki wa muziki pale anapoamua kucheza wa asili ya Baluba na kuachia ‘Nyeti’ zake zikiwa wazi.

Wanamuziki wake nyota anaowahusudu anawajumuisha kina Emedo Wabafike, Jojo Kashama na wengine wote wanaotoa mchango kuendeleza muziki wa KiKongo.
Fikra zake kubwa ni kuwa Produza mkubwa, kuwa na Studio kamambe katika jiji la Kinshasa ya kurekodia muziki kwa ajili ya kuendeleza vipaji vya vijana wanaochipukia katika muziki.

Tshala Muana alijipatia umaarufu mkubwa hapaTanzania pale alipokopi na kuimba wimbo wa Dezo dezo kwa umahiri wa aina yake. Awali wimbo huo ulipigwa na Orchestra Safari Sound chini ya Supreme Fred Ndala Kasheba. Pia alitoka na wimbo mwingine aliouimba kwa lugha ya Kiswahili unaoitwa Karibu yangu. Nyimbo nyingine ni pamoja na Malu, Mbombo na Menteur.

MAFUMU BILALI ATIMIZA MIAKA 46 KATIKA MUZIKI

$
0
0
Mafumu Bilali ni kati ya wanamuziki wachache waliopo katika tasnia ya muziki aliyeanza kupiga muziki mwaka 1973 hadi leo. Vipaji vya mwanamuziki huyo ni vya pekee ambapo anamudu kupuliza Saxophone ‘mdomo wa bata’ anao umahiri mkubwa katika kulicharaza gitaa la solo na rhythm.

Halikadhalika Mafumu ni mtunzi na mwimbaji mzuri wa nyimbo licha ya yeye kuchelewa kugundua kipaji hicho. Amepata mafanaikio makubwa kupitia vipaji vyake hivyo ambavyo amekuwa akivitumia ipasavyo na kupelekea kuweza kuzuru nchi nyingi za bara la Ulaya na Asia kwa nyakati tofauti.

Mafumu hivi sasa ni mzee wa miaka 60, aliyezaliwa mjini Kigoma eneo la Mwanga, barabara ya Legeza Mwendo mwaka 1958. Alipata kupata elimu ya msingi katika shule ya H.H. Aga Khan. 

Alipofika darasa la sita ndipo alipong’amua kuwa anapenda muziki. Hii ilitokana na yeye kumshuhudia mjomba wake Shem Karenga, aliyekuwa akipiga gitaa la besi katika bendi ya Lake Jazz wakati huo.

Umahiri wake wa kupuliza saxophone ulipelekea kupewa jina la ‘Super Sax’. Mafumu alidhamiria moyoni kuwa aje mwanamuziki kama mjomba wake huyo, licha ya kuwa na vikwazo kutoka kwa baba yake aliyekuwa hapendi kabisa mambo hayo.

“Nikafaulu kuingia kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Kazima iliyopo mjini Tabora ambako nilikosoma hadi kidato cha nne…” anasema Mafumu Bilali. Akiwa shuleni hapo alisema walikuwa pamoja na aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya Simba na mbunge wa Tabora mjini, Alhaj Ismail Aden Rage. 

Mafumu alisema baada ya kumaliza shule alikwenda Makutupora Dodoma jeshini kwa mujibu wa Sheria na mwaka 1973, huko ndiko alikojifunza kuimba na kupuliza Saxophone. Yakatangazwa majina ya vijana walipata ajira, jina  lake halikuwepo lakini aliambiwa asubiri orodha nyingine.

Super Sax akaamua kutoroka kwenda Morogoro  kujiunga katika bendi ya Morogoro Jazz. “Nilikwenda kujiunga na Morogoro Jazz bila kuwa na ndugu katika mji huo, yaani nilikwenda moja kwa moja kwenye bendi na nikapokewa wakati huo ndio hayati Mbaraka Mwinshehe wakati huo alikuwa katika harakati za kuondoka kwenda kuunda bendi yake ya Super Volcano…” alitamka Mafumu.

Alisema kwamba hakukaa sana na bendi hiyo akaamua kwenda katika jiji la Dar es Salaam kwa kaka yake. Mwaka uliofuata wa 1973, aliingia katika bendi ya Western Jazz alikoshiriki vyema kupiga Saxophone. Akiwa na bendi hiyo waliokuwa wakitumia mtindo wa ’Saboso’, ikiwa chini ya uongozi wa Shamba Ramadhani.

Aliutaja mshahara wake wa kwanza kupokea akiwa na bendi ya Western ni Sh. 275, ambazo alizitumia zote kununua nguo.  “Nilikuwa naishi kwa kaka yangu kila kitu bure ‘kula kulala’, nilikuwa napenda sana kuvaa, hivyo nikautumia mshara wote kununulia nguo. Wakati huo sikuwa mnene kama leo nilinunua suruali za mtindo wa bugaluu, viatu virefu vilivyokuwa vikiitwa  raizoni na mashati ya kubana ‘slim fit’ ya kutosha.

Hapo ndipo nilianza kuona umuhimu wa kuwa mwanamuziki na jinsi gani natakiwa kung’ara…” Mafumu alisema huku akicheka. Anaeleza kuwa wakati huo hakuwa akiimba bali alikuwa anapuliza mdomo wa bata na kupiga rhythm gitaa. Mwanamuziki huyo ameeleza kuwa wakati akiwa katika bendi ya Western Jazz, wapinzani wao wakubwa ilikuwa ni bendi ya Dar Jazz, waliokuwa wakijiita  ‘majini wa bahari’, wakitumia mtindo wao wa ‘Mundo’.

Bendi hizo wakati huo pamoja na kupiga muziki, pia zilikuwa ni wapinzani wa jadi katika soka. Western Jazz ilikuwa ni mashabiki wa Klabu ya Yanga ingawa yeye hashabikii timu hiyo na Dar Jazz ni  ilikuwa na wakishabikia klabu ya Simba. Hivyo bendi hizo zilijigawa katika mtindo huo.

Ilikuwa marufuku na haikutokea bendi ya Western kupiga kwenye tafrija za Simba halikadhalika kwa Dar Jazz vile vile kwenye shughuli za Yanga.
“Mamluki kama mimi wasiokuwa wanachama au mashabiki wa timu inayoshabikiwa na bendi husika, tulikuwepo lakini mashabiki na wapenzi wa bendi hizi walijigawa katika mtindo huo Western Yanga na Dar Jazz Simba, ilikuwa wenyewe huwaambii kitu hasa matajiri wa Western na ushabiki wa soka wa zamani ulikuwa wa kweli…” alifafanua Mafumu.

Akiwa katika bendi hiyo ya Western Jazz, nyimbo ambazo zilitamba wakati huo zilikuwa za Jela ya mapenzi, Rosa, Vigelegele, ‘Kazi ni Kazi’ na Hakika. Mafumu hakusita kutaja baadhi ya vibao kadhaa alivyoshiriki katika bendi hiyo kuwa ni pamoja na ‘Hakika’, na ‘Sadaka’.

Ameutaja ukumbi mkuu wa bendi hiyo kuwa ulikuwa Community Centre, ambao kwa sasa Makao Makuu ya Wilaya ya Kinondoni, maeneo ya Magomeni Mapipa. Mafumu aliaeleza safari yake ya muziki ilivyoanza kwa kusema kuwa kama siyo moyo wa dhati wa kupenda muziki, wala asingefika hapo alipo. Baba yake mzazi aliyekuwa mganga maarufu mkoani Kigoma, alikuwa hataki ajiingize kwenye muziki.

 “Baba mzee Bilali hakutaka kabisa kusikia muziki alipenda nisome sana dini, lakini nilikuwa kila nikipata nafasi nilikuwa natoroka kwenda kwenye muziki…” alieleza Mafumu. Hivi sasa ni baba wa familia na watoto wake saba katika makazi yao maeneo ya Vingunguti, jijini Dar es Salaam.

Historia yake katika muziki Mafumu alieleza kuwa inaanzia mwaka 1972 nilipojiunga na bendi ya Morogoro Jazz iliyokuwa ikiongozwa na Mbaraka Mwishehe Mwaruka, akitokea JKT Makutupora. Alianza rasmi kujiingiza kwenye tasnia ya muziki mwaka 1973, lakini hadi leo ni moto wa kuotea mbali kutokana na kuwa maahiri wa kufanya kazi hiyo ambayo kwa mujibu wake atakufa akiifanya.

Mwaka 1978 aliamua kwenda katika jiji la Dar es Salaam. Alipotinga jijini humo, mwaka uliofuatia wa 1979 ‘alitua’ katika bendi ya Vijana Jazz. Hapo akatunga kibao ‘Taabu’ na pia kushiriki kukiimba. Halikadhalika akipuliza Saxophone kwenye vibao kama ‘Chiku’ na ‘Matata Ndani ya Nyumba’.

Ilipotimu mwaka 1980, Mafumu alihamia katika bendi ya Maquis du Zaire. Huko alikutana na miamba mingine wa kupuliza Saxophone akiwemo Chinyama Chiyaza, Suleiman Akulyake ’King Maluu’, Alex Kanyimbo, Mukuna Roy na  Khatib Itei Itei kwa nyakati tofauti.

Akiwa na bendi hiyo alipuliza ‘mdomo wa bata’ kwenye vibao vingi, baadhi yake ni ‘Zoa’, ‘Sina Ndugu’, ‘Noel Christmas’ pamoja na ‘Mage’. “Nilikaa Maquis hadi mwaka 1984, nilipochomoka tena na kuhamia katika bendi Bima Lee Orchestra iliyokuwa ikimilikiwa na Shirika la Bima la Taifa. Huko nilikokutana na wakali wengine katika muziki kama Jerry Nashon ‘Dudumizi’, Shaaban Dede Kamchape ‘Super Motisha’, ‘Joseph Mulenga ‘King Spoiller’…” alisema Mafumu.

Mwaka 1985 alikuwa mmoja wa waanzilishi wa bendi ya MK Group ‘Ngoma za Maghorofani’, iliyokuwa ikiporosha muziki wake katika ukumbi wa Bandari Grill, ulipo katika hotel ya New Africa. Bendi hiyo ilikwa ikiongozwa na Abubakar Kasongo Mpinda ‘Clyton’. Hapo alikutana na wanamuziki wengine akina Andy Swebe, Asia Darwesh, Kayembe Ndalabu ‘Trumblo’ Omari Makuka na wengine wengi.

Mwaka 1986 alikwenda Iringa akawa tena mmoja wa waanzilishi wa bendi ya Tancut Alimasi ya mjini humo. Mwaka 1987 alirejea tena MK Group ambapo wimbo wake wa kwanza kupuliza Saxophone awamu hiyo ya pili ilikuwa ni ‘Utakuja kuanguka kwenye matope’.Mwaka 1989, kaka yake Adam Kinguti alirudi nchini akitokea Sudan, alipokuwa akifanyakazi kwenye ofisi za Ubalozi.

Wakaanzisha bendi ya Bicco Stars, yeye akashiriki kupuliza Saxophone kwenye vibao kadhaa kama vya ‘Magret Mage’, ‘Wapangaji’ na Kisamvu’. Mwaka 1991 Mafumu alitoka katika bendi hiyo ya Bicco akiwa na mpapasaji kinanda mahiri wa kike Asia Daruweshi, baada ya kutokea hali ya kutoelewana kati yake na Kinguti. Wakaamua kuanzisha bendi yao ya Zanzibar Sound.

“Tukiwa na Zanzibar Sound, tulipata mkataba katika Hoteli ya Mount Meru, Arusha na mwaka mmoja baadaye mwanamuziki mwenzetu kwenye bendi hiyo, Kanku Kerry Nkashama, alipata mkataba nchini Japan. Tukaondoka naye kwa sharti la sasa kujiita Kilimanjaro Connection…” anasema Mafumu Bilali.

Walizunguka nchi nyingi za bara la Asia wakiwa na bendi hiyo ya Kilimanjaro Connection. Waliporudi mwaka 1994, alijitoa katika bendi hiyo na baadae kidogo Asia Darwesh nae alijitoa, akairudisha upya bendi yake ya Zanzibar Sound na kurejea mkataba wake Bahari Beach Hotel.

Mafumu yeye alibaki bila bendi, ambapo muda si muda, Asia Darweshi alipata kazi nchini Bahrain na kumuachia Super Sax mkataba wake wa kupiga muziki katoka hoteli ya Bahari Beach. Baada ya kuona ameachiwa mkataba wakati hana bendi, Mafumu ndipo alipomfuata Baraka Msirwa na kumuomba vyombo vya muziki ambapo alimpa kwakuwa havikuwa na kazi kutokana na kufa kwa bendi za MK Group, MK Beat na MK Sound walivyokuwa wakivitumia.

Bendi ya African Beat ilianzishwa mwaka 1998, baada ya Mafumu Bilali kujiengua kutoka katika bendi ya African Stars ambayo nayo ilianzishwa mnamo mwaka 1994 kwenye Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam, huku yeye akiwa ndiye mwanzilishi. Mafumu anakumbuka kuwa, wakati akiwa na African Stars ambayo hata jina lake alilibuni yeye, walitamba na vibao kama ‘Sakatu Sakatu’, ‘Mayanga’, ‘Maya’, ‘Afrika’ na ‘Dance Dance’.

Baadhi ya wanamuziki waliokuwa wakiunda kundi hilo la African Stars linalojulikana zaidi hivi sasa kama ‘Twanga Pepeta’, ni Bob Gady, Andy Swebe, Alfa Nyuki, Palmena Mahalu, Pamela pamoja na Hamisi Kayumbu ‘Amigolas’. “Hicho ndio kilikuwa chanzo cha bendi ya African Stars niliyoibuni mwenyewe hadi jina, lililoniletea uhasama mkubwa na dada yangu Asha Baraka baada ya kujitoa,” anasema Mafumu Bilali.

Akiwazungumzia wanawe amesema ana wawili  ambao wanaoonekana kufuata vyema nyayo zake, ambao ni Feruzi, anayepapasa kinanda na Aziza ambaye ni mwimbaji. Aidha Mafumu Bilali amekuwa mmoja kati ya wanamuziki wachache humu nchini walioamua kuunda bendi zao binafsi. Wengine wanaomiliki bendi zao ni akina Hussein Jumbe anayemiliki bendi yake ya Talent, Banana Zorro na Matei Joseph anayemiliki bendi yake ya African Minofu.8m

Na Moshy Kiyungi, Dar es Salaam

ZANZIBAR KUADHIMISHA SIKU YA AFYA YA KINYWA NA MENO DUNIANI KESHO MACHI 20

$
0
0
Na Miza Kona  Maelezo Zanzibar
Zaidi ya asilimia 50 ya watoto wanaugua  maradhi ya kutoboka kwa meno jambo ambalo hupelekea kuathirika kwa kinywa na afya ya meno.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na siku ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani huko ofisini kwake Mnazi Mmoja.

Amesema jamii imekuwa ikiathirika na kutoboka kwa meno hasa watoto kutokana na kula vyakula vyenye sukari na kutofuata mambo muhimu katika kujikinga na usafi wa kinywa.

Amesema mabadiliko ya tabia na ulaji wa vyakula vya sukari kwa wingi ni ongezeko la maradhi ya kinywa na meno na kupelekea kuongezeka kwa kiasi kikubwa kutoboka kwa meno.

Alieleza kuwa ni muhimu kutunza afya ya kinywa ili kuepukana harufu mbaya ya kinywa na meno kutoboka kwa kujikinga na kupata matibabu kabla ya kuathirika zaidi.

“Maradhi haya ya kinywa na meno sio maradhi madogo ni maradhi makubwa duniani kwani maradhi haya husabisha kansa mbalimbali ni lazima kufanya kinga ya usafi na kuwaelimisha vijana na watoto skuli,” alifahamisha  Waziri Hamad.

Aidha Waziri Hamad aitaka jamii kudhibiti ulaji wa vitu vya sukari mara kwa mara na kuboresha mbinu za upigaji mswaki kwa kutumia dawa ili kuweza kujikinga na maradhi hayo.

Waziri huyo wa Afya ameeleza kuwa serikali imekuwa ikitoa elimu juu ya uhifadhi na kinga ya kinywa na meno katika skuli mbalimbali mjini na vijijini  pamoja na kuboresha huduma za afya katika vituo kwa kuweka vifaa na wataalamu ili kuepukana na maradhi hayo.

Amewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kufanya uchunguzi wa meno katika vituo vya afya angalau mara mbili kwa mwaka ili kuepukana na madhara ya kinywa na meno kwa lengo la kupata afya bora.

Waziri Hamad Ameeleza katika kudhimisha siku hiyo Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wataalamu wa meno kutoka   Chuo Kikuu cha Belgrade kesho inatarajia kutoa huduma mbalimbali za matibabu ya meno huko katika Mnara wa Kumbukumbu Kisonge.

Nae Daktari Bingwa wa Meno Idd Suleiman Idd amewasisitiza kinamama wajawazito kufika mapema katika vituo vya Afya  kupima afya ya kinywa na meno ili kuepuka madhara kwa mtoto.

Ameeleza kuwa madhara ya kinywa na meno kwa wajawazito huweza kumuathiri mtoto na kupelekea kuzaa watoto wasiotimia umri.

Siku ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani  huadhishwa kila ifikapo tarehe 20  Machi ambapo ujumbe wa mwaka ni “Tunza Afya ya Kinywa”
 Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) kuelekea maadhimisho ya siku ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani yatayofanyika kesho tarehe 20/03/19 Mapinduzi Square Michenzani Mjini Unguja.
 Baadhi ya wandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakifuatilia Mkutano wa Waziri wa Afya alipokutana nao kuzungumzia maadhimisho ya siku ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani yatayofanyika Mapinduzi Square Michenzani.
 Daktari bingwa wa meno Zanzibar Iddi Sleiman Iddi akijibu baadhi ya maswali yalioulizwa na wandishi wa habari katika kuelekea madhimisho ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani.
Mkuu wa Madaktari wakujitolea kutoka Chuo Kikuu cha Belgrade Prof. Ana Pucar akielezea juu ya umuhimu wa kutoa elimu ya Afya ya kinywa na meno kwa watoto walio shuleni katika Mkutano wa Waziri wa Afya uliofanyika Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga.

UHAMIAJI WAFANYA WARSHA YA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI KATIKA ULINZI NA UDHIBITI WA MIPAKA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Charles Kabeho amefungua warsha ya siku tatu wa ushirikishwaji wa wananchi katika ulinzi na uthibiti wa mipaka kuanzia  tarehe 19 hadi 21 Machi, 2019. Ufunguzi huo umefanyika katika ofisi za kituo cha Uhamiaji Sirari, Wilayani Tarime Mkoa wa Mara.

Kabeho amewataka washiriki kuzingatia yale yote watakayofundishwa na kwenda kuyafanyia kazi katika maeneo wanayoishi. Pia alieleza kwamba maeneo ya mpakani kuna changamoto nyingi ambazo vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na taasisi nyingine za serikali zilizopo mpakani haziwezi kuzimaliza peke yake bila ya ushirikishwaji wananchi.

“Ndugu washiriki, kwanza napenda kuwapongeza kwa kuchaguliwa kwenu kushiriki, wengi wenye sifa kama ninyi hawakuipata hii nafasi. basi naomba nafasi hii muitumie vizuri katika kujifunza na mafunzo mtayopata  mkawaelimishe wana jamii wengine ambao hawakupata fursa hii.” Ameeleza Kabeho.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya kufungua warsha, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mara Naibu Kamishna Fredrick Kiondo ameishukuru Idara ya Uhamiaji Makao Makuu na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji(IOM) kwa kuwafikia wananchi moja kwa moja ili kuwapatia elimu juu ya changamoto zinazokabili maeneo ya mipakani.

“Nawashukuru Uhamiaji Makao Makuu na IOM kwa juhudi zao kubwa kuelimisha jamii ya mipakani. Tunazo changamoto nyingi kwenye masuala ya wahamiaji haramu, magendo ya binadamu, usafirishaji haramu wa binadamu, magendo ya bidhaa, madawa ya kulevya (Mirungi) na uhalifu mwingine wa Kimataifa. Ni imani yangu kuwa jamii ikipata uelewa itashirikiana vyema na Idara ya Uhamiaji na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika kufichua maovu hayo.”

Warsha hiyo ya siku tatu inashirikisha viongozi kuanzia kitongoji hadi kata, viongozi wa dini, wadau wa mpaka, viongozi wa bodaboda na mabasi ya abiria kwa upande wa Tanzania na Kenya kwa siku ya kwanza, na siku ya pili na siku  ya tatu ni mikutano ya hadhara na wananchi wa Kata zinazozunguka mpaka wa Sirari. Ni imani kubwa kwa idara ya Uhamiaji Tanzania kuwa wananchi wengi watapata elimu katika masuala ya Uhamiaji, Uraia, Taratibu za Kuingia, Ukaazi na Utokaji nchini, Wahamiaji Haramu, Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Uhalifu wa Kimataifa, Magendo ya Binadamu na masuala yote ya Ulinzi na Udhibiti wa Mpaka katika maeneo yao.
Wawezeshaji wa Warsha, Ally Mtanda na David Lukiru wakitoa somo kwa washiriki wa warsha  ya ushirikishwaji wa wananchi katika ulinzi na udhibiti wa mipaka iliyofanyika katika ofisi za kituo cha Uhamiaji Sirari, Wilayani Tarime Mkoa wa Mara.
Washiriki wa kiwa kwenye warsha ya ushirikishwaji wa wananchi katika ulinzi na udhibiti wa mipaka iliyofanyika katika ofisi za kituo cha Uhamiaji Sirari, Wilayani Tarime Mkoa wa Mara.

UVUVI HARAMU WA MABOMU TUMEUTOKOMEZA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 98-MPINA

$
0
0
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza na wavuvi wa Kasera eneo la Sahare Jijini Tanga wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani hapa ambapo alisikiliza changamoto zinazowakabili ili kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi wa haraka 
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga akizungumza wakati wa ziara hiyo 
Mkurugenzi Msaidizi Ulinzi wa Rasilimali za Uvuvi Mchira Wamarwa akitoa taarifa yake katika ziara hiyo
Diwani wa Kata ya Mnyanjani (CUF) Thobias Haule akizungumza katika ziara hiyo 
Sehemu ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali wakifuatilia mkutano huo wa Waziri Mpina na Wavuvi eneo la soko la Samaki la Kasera Jijini Tanga 
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina kushoto akisisitiza jambo kwa mmoja wa wavuvi waliopo eneo hilo mara baada ya kuzungumza nao 
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiagana na wavuvi wa eneo la soko la Kasera Jijini Tanga mara baada ya kumaliuza kusikiliza kero zao zinazowakabili wakati wa ziara yake 
Mmoja wa wavuvi Jijini Tanga akiuliza swali kwa WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina


WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amesema serikali imefanikiwa kuutokomeza uvuvi haramu kwa kutumia mabomu kwa kiwango kikubwa cha zaidi ya asilimia 98 huku wakiendelea kupambana kuhakikisha unakwisha kabisa kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini. 

Mpina aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani Tanga iliyokuwa na lengo la kukutana na wavuvi kwenye soko la Sahare Kasera Jijini Tanga na Moa wilayani Mkinga ikiwa ni kusikiliza kero zinazowakabili na kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi. 

Ziara hiyo inatokana na wito wa viongozi waliotaka afike kwenye eneo hiloi ili kuweza kubaini changamoto zinazowakabili wavuvi hao na kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi wa kina. Alisema baada ya kufanikiwa kuutokomeza uvuvi wa mabomu hivi sasa wanageukia kwenye nyavu haramu kwa kuhakikisha zinaondolewa majini ili wananchi waendelee kuvua kwa njia endelevu itakayokuwa na tija kwa vizazi vya sasa na vijavyo. 

“Niwaambie kwamba nyavu haramu zilizokamatwa kwenye ukanda wa bahari kuu ukizibadilisha ni zaidi ya km 773 zimekamatwa zilzokuwa zinavua kwa njia haramu…leo hii watu walipokuwa wanavua na sumu samaki wanateketea, watanzania wanapoteza maisha kutokana na uvuaji wa namna hii na tusipojipanga vizuri kuzilinda rasilimali za bahari zitatoweka “Alisema Waziri Mpina 

Aidha alisema kutokana na uvuvi huo haramu leo hii zaidi ya bilioni 56 ya fedha za kitanzania wanazitumia kuagiza samaki kutoka nje wakati nchi ina maziwa mengi na bahari kubwa, mito mingi mikubwa ambayo ingeweza kutosheleza mahitaji. “Haiwezekani kuagiza samaki kutoka nje hata kwenye nchi ambazo hazina mabwawa wala mito kutokana na sisi samaki wetu tunawavua kwa mabomu na sumu, makokoro hivyo kwa pamoja lazima tubadilike na tukubaliane kuzilinda rasilimali zetu”Alisema Waziri Mpina. 

“Lakini pia niwaambie kwamba serikali ya awamu ya tano ipo pamoja na wananchi wake ndio maana leo hii waziri nimekuja hapa na watendaji wengine wa serikali kuwasikiliza mnachangamoto gani pamoja na hayo niwaambie mnapoona serikali inachukua hatua kwa ajili ya rasilimali hizo mjue ni kwa ajili yenu”Alisema. 

Alisema serikali inapochukua hatua mbalimbali za kukabiliana na uvuvi haramu mtambue inafanya hivyo kwa ajili ya nia nje ya kuhakikisha rasimali zilizokuwepo majini zinalindwa ili kuepusha zisitoweke. “Wapo wavuvi wanavua kwa nyavu halali na wapo wengine wanavua kwa nyavu haramu ukienda kuvua kwa mabomu na nyavu haramuni hatari kubwa kutokana na kuharibu mazalia ya samaki na viumbe vyengine vilivyopo majini lakini pia kuhatarisha afya za walaji kutokana na kwamba wanaweza kupata saratani”Alisema 

Awali akizungumza katika ziara hiyo, Mkurugenzi Msaidizi Ulinzi wa Rasilimali za Uvuvi Mchira Wamarwa alisema katika operesheni ya biashara haramu ya samaki na mazao yake uliofanyika ukanda wa pwani ya bahari ya hindi kwa siku 29 kutokana na ukanda huo kuna matukio mengi 

Alisema uendelevu wa rasilimali za uvuvi bahari ya hindi unatishiwa na uwepo wa uvuvi unaofanyika kinyume cha sheria ya uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni za mwaka 2009 pamoja na sheria nyengine za nchi ikiwemo wa sheria za mazingira namba 20 ya mwaka 2004. 

Alisema uvuvi haramu unaofanyika kwenye bahari ya hindi ni matumzi ya zana haramu na mbinu haramu za uvuvi, matumizi ya milipuko,kuvua bila leseni ,matumizi ya nyavu zenye macho chini ya nchi tatu, vyavu za timber,njavu za dagaa zenye macho chini ya milimita 10,uvuvi wa katubi ,kutumia vyombo visivyoisajiliwa na kuvua kwenye maeneo yasiyosajiliwa 

Awali akizungumza Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji alisema katika Jiji hilo wanachokiwanda kiwanda kimoja kinachochakata samaki ambacho kinakabiliwa na changamoto ya kutokupata samaki wa kutosha wanakusanya kidogo kidogo hali inayopelekea kufanya kazi mara moja kwa wiki au wiki mbili ndio wanachakata. 

Alisema kutokana na kuwepo kwa hali hiyo siku nyengine wanakusanya kidogo kidogo lakini changamoto iliyopo kwenye uwezekazaji wa kiwanda hivyo wanafanya utafuti kubaini kama wanaweza kupata samaki wa kutosha. 

Mkurugenzi huyo alisema hilo linatokana na kwamba wanaopatikana kwa sasa hawatoshelezi kuendesha kiwanda ndio maana bado wawekezaji wanasita kuwekeza huko lakini kikubwa maboresha yanayoendelea kufanywa na serikali ni ya muhimu kwa sababu yatawezesha upatikanaji wa samaki kwa wingi kama uvuvi utakaofanyia utazingatia sheria za uvuvi. 

Alisema jambo hilo litakuwa na tija kwao na wafanyabiashara huku akieleza kikubwa kinachowathiri wakati kunapotokea uvuvi haramu wanaua samaki ambao hawastahili kwenda sokoni matokeo yake viwanda havipati mzigo wa kutosha. 

Balozi Seif afanya mazungumzo na Uongozi wa Wizara ya Kilimo ya Cuba

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Tanzania ina kila sababu ya kuimarisha Sekta ya Kilimo kutokana na kubarikiwa kuwa na Rasilmali za kutosha zinazoiwezesha kujikita zaidi katika eneo hilo muhimu kwa Uchumi wa Taifa na Ustawi wa Wananchi wake.

Balozi Seif alieleza hayo wakati akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo ya Cuba Mjini Havana mwanzoni mwa Maonyesho ya Siku Nne ya Kimataifa ya Kilimo (FIAGRO - 2019) yanayofanyika kila Mwaka Nchini humo na kuhudhuriwa na wadau wa Sekta hiyo kutoka Mataifa mbali mbali Duniani.

Alisema Sekta ya kilimo inayochukuwa asilimia kubwa ya Watu wake hasa katika Maeneo ya Vijijini inaweza kuwa mkombozi mkubwa wa Ajira hasa kwa kundi kubwa la Vijana wanaomaliza masomo yao.

Balozi Seif  alisema yapo mazao ya asili hasa Muhogo Majimbi, Viazi na mboga mboga yanayoendelea kuzalishwa na Wakulima mbali mbali Nchini Tanzania, lakini kinachokosekana kwa kiasi kikubwa ni ile Taaluma ya kutosha ya kuendeleza uzalishaji wa mazao hayo Kitaalamu zaidi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushauri Uongozi huo wa Wizara ya Kilimo wa Cuba kuendelea kuiunga mkono Tanzania na Zanzibar kwa ujumla kwa vile Taifa hilo limeshapiga hatua kubwa Kitaalamu kwa miaka mingi sasa katika kuendeleza Sekta hiyo.

Alisema hatua hiyo muhimu itaweza kusaidia zaidi kuongeza chachu ya uhusiano wa muda mrefu uliyopo baina ya Mataifa hayo mawili yanayoendelea kushirikiana Kidiplomasia tokea yapate  Uhuru na ukombozi wao kutoka katika makucha ya kikoloni.

Akizungumza katika ufunguzi wa Maonyesho hayo Naibu Waziri wa Kilimo wa Cuba Bwana Jose Migeil Rodriguez De Armas alisema Cuba imekuwa na Utamaduni wa kuwalika Wadau wa Sekta ya Kilimo kutoka Nchi Rafiki kushiriki Maonyesho hayo.

Alisema Maonyesho hayo huambatana na utolewaji wa Taaluma inayolengwa kupewa wakulima hatua iliyowezesha kuzalishwa Matunda na Mpunga Kitaalamu na kusafirisha nje ya Nchi tokea Mwaka 1933.

Bwana Jose aliwaeleza washiriki wa Maonyeshao hayo wakiwemo Mabalozi wa Nchi rafiki pamoja na wale 26 wa Mataifa ya Bara la Afrika kwamba Cuba imeanza kufungua milango ya uimarishaji wa Seka za Maendeleo ikilenga kujetegemea yenyewe kwa kila nyanja.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alipata fursa ya kutembelea mabanda mbali mbali ya maonyesho na kuridhika na hatua kubwa iliyofikiwa na wazalishaji wa mazao tofauti yenye ubora wa kiwango kinachokubalika Kimataifa.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia na kupata maelezo ya utengenezaji wa sigara zinazopendwa zaidi na Watalii na matajiri maarufu (Siga) kwenye maonyesho ya Kilimo Mjini Havana Nchini Cuba.
 Mtaalamu wa Kilimo cha Migomba na vyakula vya Mizizi akimpatia maelezo balozi Seif  taalum inayotumika katika kulima maazo hayo Kisasa zaidi.
- Balozi Seif akifurahia na kuridhika na ubora wa bidhaa za Mapapai na Mananasi zilizopo kwenye Maonyesho ya Kilimo Mjini Havana Nchini Cuba. Picha na – OMPR – ZNZ.

OFISI YA BUNGE YAWASILISHA BAJETI YAKE MBELE YA KAMATI YA BAJETI

$
0
0
 Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai (wa pili kushoto) akitoa taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2018/2019 na makadirio ya mapato na matumizi ya Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa fedha 2019/2020 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akifafanua jambo kuhusiana na makadirio ya mapato na matumizi ya Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa fedha 2019/2020 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti George Simbachawene akichangia jambo mbele ya Kamati hiyo ilipokutana ili kupokea taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2018/2019 na makadirio ya mapato na matumizi ya Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma hii leo.  (Picha na Ofisi ya Bunge)
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2018/2019 na Makadirio ya mapato na matumizi ya Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma hii leo.  (Picha na Ofisi ya Bunge)

Tumewekeza nguvu katika huduma ya afya ya uzazi ya Mama na Mtoto-Dkt.Ndugulile

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Serikali imesema kuwa imewekeza katika huduma za  Afya ya Mama na Mtoto katika kuhakikisha wanawake  wa wote wanajifungua katika sehemu salama.

Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipokutana na Mtandao wa Utepe Mweupe Kitaifa wenye kampeni ya Mwanamke anataka Nini, Ndugulile amesema kuwa hali ya upatikanaji wa huduma za afya nchini zimeboreshwa ikiwemo huduma ya uzazi kwa kujenga vituo vya afya 350 ambapo huduma za uzazi zinatolewa.
Amesema kuwa tatizo la wanawake kujifungulia koridoni katika vituo vya zimepungua na mwisho wa siku zitaisha kabisa kutokana na jitihada za serikali zinazofanywa.

Amesema kuwa serikali imeajiri wafanyakazi 11000 wa sekta ya afya ili kuweza kutoa huduma zenye ufanisi  katika Hospitali na vituo vya afya nchini. Dkt.Ndugulile amesema  kuwa katika katika uwekezaji huo wameboresha Hospitali 67 nchini kwa kuwa na huduma zote kwa kuzingatia huduma za uzazi ya Mama na mtoto.

Amesema kuwa vifo vya wa Mama na Watoto wanategeemea katika twakimu zijazo zitakuwa zimepungua kutokana na uwekezaji uliofanywa katika sekta ya afya. Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mtandao wa Utepe Mweupe Kitaifa Rose Mlay amesema kuwa katika kampeni hiyo mwanamke anataka Nini baada ya kuwahoji wanawake wamekuwa wakitaka huduma ziboreshwe katika huduma ya uzazi huku wakitaka zitolewe bure pamoja na vifaa mbalimbali.

Mlay amesema kuwa katika mahojiano baadhi wanataka serikali iongeze vituo vya afya vya kufanya kila mwanamke aweze kufikia.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na Mitandao wa Kuratibu wa Utepe Mweupe katika ofisi Wizara ndogo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Utepe Mweupe Kitaifa Rose Mlay akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile kuhusiana na Kampeni ya wanataka nini inayoratibiwa na mtandao huo.

AZANIA BENKI YAONGEZA MATAWI MARA BAADA YA KUUNGANA NA BENKI M

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Azania ,Charles Itembe akizungumza na Waandishi wa Habari mara  baada ya kukamilika Kusaini Mkataba wa kukubali kuchukua mali zilizokuwa zinamilikiwa na Banki, Mara baada ya kupatiwa majukumu hayo na Benki Kuu ya Tanzania kufuatia Benki M kuishiwa Ukwasi na kushindwa kujiendesha kwa ufanisi na taratibu za kibenki zinavyotaka.
  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Azania ,Charles Itembe akizungumza na Waandishi wa Habari mara  baada ya kukamilika Kusaini Mkataba wa kukubali kuchukua mali zilizokuwa zinamilikiwa na Banki Mara baada ya kupatiwa amajukumu hayo na Benki Kuu ya Tanzania kufuatia Benki M kuishiwa Ukwasi na kushindwa kujiendesha kwa ufanisi na taratibu za kibenki zinavyotaka.

 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Azania ,Charles Itembe akiwa katika picha na Watendaji Wakuu wa Idara kutoka Benki ya Azania.
Sehemu ya Waandishi wa Habari walioshiriki katika Mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es Salaam

JKCI yatoa zawadi kwa mfanakazi bora wa robo mwaka

$
0
0
 Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni moja mfanyakazi bora wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2018/2019 (Novemba 2018 – Januari 2019) Afisa Uuguzi Prisca Kiyuka wakati wa hafla fupi ya kumpongeza iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Prof. Mohamed Janabi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi Afisa Uuguzi Prisca Kiyuka cheti cha kutambua utumishi wake baada ya kuwa mfanyakazi bora wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2018/2019 (Novemba 2018 – Januari 2019) katika hafla fupi ya kumpongeza iliyofanyika leo katika ukumbi wa taasisi hiyo uliopo Jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi Robert Mallya na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Fedha Mohamed Songoro.
 Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye ni mfanyakazi bora wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2018/2019 (Novemba 2018 – Januari 2019) Prisca Kiyuka akitoa neno la shukrani wakati wa hafla fupi ya kumpongeza ilioyofanyika leo katika ukumbi wa taasisi hiyo uliopo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Yeyeye akimpongeza mfanyakazi bora wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2018/2019 (Novemba 2018 – Januari 2019) Afisa Uuguzi Prisca Kiyuka wakati wa hafla fupi ya kumpongeza iliyofanyika leo katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Utawala Joachim Asenga. Picha na: JKCI

MJUMBE WA MCHEKESHAJI DULLYZO WA ZANZIBAR KWA VIJANA WANAOTAKA KUFANIKIWA HARAKA

$
0
0

Na Khadija Seif, Globu ya jamii

MCHEKESHAJI chipukizi visiwani  Zanzibar, Abdulnadhif Shaka Hassan ‘Dullyzo’, ametoa ujumbe kwa vijana ambao wanataka mafanikio ya haraka.

Akizungumza leo Dullyzo amesema umaarufu na mafanikio alioyapata hayakuja kimiujiza kwani aliamini ndoto zake pamoja na kujishugulisha na kazi mbalimbali za kijamii.

"Kabla sijawa mchekeshaji nilikua nacheza ngoma na ndio kilikuwa kipaji changu ambacho kilikua kinaniingiza fedha za kujikimu kiuchumi na kuendesha familia," amesema

Hata hivyo ameeleza nini kilimvutia na kuingia kwenye tasnia ya vicheko huku akimtaja Dullivan kama mtu anayefata nyayo zake katika kazi.

“Wakati naanza kumuiga Dullvani, nilitamani siku nikutane naye ili anifundishe baadhi ya njia anazotumia na nashukuru Mungu tumeweza kuonana katika tamasha lililofanyika siku chache zilizopita lililoandaliwa na Zanzibarglamr la mavazi na vipodozi visiwani Zanzibar," amesema Dullyzo

 Amewaasa vijana wa visiwani humo kuchakarika na kujihusisha na kazi yoyote ile ya hali ili kujikwamua kiuchumi na kujiepusha na vitendo viovu vinavyoiathiri jamii kiujumla kama ubakaji,uporaji na uhalifu.

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images