Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110115 articles
Browse latest View live

WAAMUZI WAONYWA VITENDO VYA UVUNJIFU WA NIDHAMU VIWANJANI

$
0
0
   *Ili kufanikiwa ni lazima nidhamu ipewe kipaumbele
 *Muamuzi afungiwa Msimu mzima kutokana na utovu wa nidhamu
     
       Na.Khadija seif,Globu ya jamii

CHAMA cha soka visiwani Zanzibar (ZFA) kupitia kamati ya kusimamia mashindano ya soka na ligi ya Zanzibar kitaifa, imemfungia kwa mwaka mmoja, mwamuzi, Ramadhan Keis, kutokana na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu.

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hussein Ahmada, ameeleza kuwa kama kamati ilijaribu mara kadhaa kumuonya mwamuzi huyo, lakini, alionekana kutokuwa na nia ya kubadilika katika uchezeshaji wake pamoja na kutokuwa na nidhamu kwa wakuu wake wa kazi.

“Tumemuonya mara kadhaa, lakini, hakuonyesha kubadilika, tumeona bora tumsimamishe”, alisema Ahmada.Aidha ahmada amesema katika tukio la hivi karibu, mwamuzi huyo alikataa kuchezesha mechi kati ya Negro na Zantex kwa madai kuwa kamishna aliyepangiwa hakukubaliani nae.

Na pia kitendo hicho kilikuwa cha utovu wa nidhamu jambo ambalo kama kamati imeona bora wamfungie na kumuangalia kwa msimu ujao kama atabadilika waweze kumsamehe.

“kimsingi muamuzi huyo hayuko tayari kubadilika, hivyo tumemfungia msimu mzima na mbali na hayo pia huwa ni mgumu wa kuandika hata ripoti wakati anapomaliza kuchezesha mechi zake”, alisema Ahmada.

Na ameitaka  kamati iliyopo kwa sasa kuwa na nidhamu michezoni na kuheshimu viongozi wa kila nyanja hususani kwa viongozi wa juu ,ili kufanikiwa ni lazima kuipa kipaumbele nidhamu kwa watu wote wanaokuzunguka ndipo utafanikiwa.

NYANZA BOTTLERS YAKABIDHI ZAWADI ZA PROMOSHENI YA ‘KUNYWAAH NA USHINDE'

$
0
0
1049889
Meneja mauzo wa Kampuni ya Coca Cola ya Nyanza Bottlers, Samwel Makenge (kulia) akikabidhi zawadi ya TV kwa Mkazi wa Mwanza Saduni Rashid (kushoto) katika hafla ya kuwakabidhi washindi wa Promosheni ya Coca Cola ya ‘Kunywaaah na Ushinde’ iliyofanyika jana jijini humo. Promosheni hiyo ya miezi mitatu inaenda sambamba na msimu huu wa Coke Studio ambapo imedhamiria kuwatunuku wateja wake wapendwa kwa majuma 12 ambapo watu mbalimbali wanajinyakulia fedha taslimu, runinga na bidhaa nyingine nyingi kutoka Coca Cola.
1049890
Meneja mauzo wa Kampuni ya Coca Cola ya Nyanza Bottlers, Samwel Makenge (kulia) akikabidhi zawadi ya TV kwa Mkazi wa Mwanza Said Masoud (kushoto) katika hafla ya kuwakabidhi washindi wa Promosheni ya Coca Cola ya ‘Kunywaaah na Ushinde’ iliyofanyika jana jijini humo. Promosheni hiyo ya miezi mitatu inaenda sambamba na msimu huu wa Coke Studio ambapo imedhamiria kuwatunuku wateja wake wapendwa kwa majuma 12 ambapo watu mbalimbali wanajinyakulia fedha taslimu, runinga na bidhaa nyingine nyingi kutoka Coca Cola.
1049892
Meneja mauzo wa Kampuni ya Coca Cola ya Nyanza Bottlers, Samwel Makenge (kulia) akikabidhi zawadi ya TV kwa Mkazi wa Mwanza Wilhad Shirima (kushoto) katika hafla ya kuwakabidhi washindi wa Promosheni ya Coca Cola ya ‘Kunywaaah na Ushinde’ iliyofanyika jana jijini humo. Promosheni hiyo ya miezi mitatu inaenda sambamba na msimu huu wa Coke Studio ambapo imedhamiria kuwatunuku wateja wake wapendwa kwa majuma 12 ambapo watu mbalimbali wanajinyakulia fedha taslimu, runinga na bidhaa nyingine nyingi kutoka Coca Cola. 
1049893
Washidi wa Promosheni ya Coca Cola ya ‘Kunywaaah na Ushinde’ wakionyesha zawadi za TV walizojishindia wakati wa hafla ya kuwakabidhi zawadi hizo jana jijini Mwanza. Promosheni hiyo ya miezi mitatu inaenda sambamba na msimu huu wa Coke Studio ambapo imedhamiria kuwatunuku wateja wake wapendwa kwa majuma 12 ambapo watu mbalimbali wanajinyakulia fedha taslimu, runinga na bidhaa nyingine nyingi kutoka Coca Cola.
1049894
Washidi wa Promosheni ya Coca Cola ya ‘Kunywaaah na Ushinde’ wakionyesha zawadi za TV walizojishindia wakati wa hafla ya kuwakabidhi zawadi hizo jana jijini Mwanza. Promosheni hiyo ya miezi mitatu inaenda sambamba na msimu huu wa Coke Studio ambapo imedhamiria kuwatunuku wateja wake wapendwa kwa majuma 12 ambapo watu mbalimbali wanajinyakulia fedha taslimu, runinga na bidhaa nyingine nyingi kutoka Coca Cola. Pamoja nao ni wafanyakazi wa Kampuni ya Nyanza Bottlers, Samwel Makenge (wa pili kushoto) na Deus Kadiko (kulia).

DKT. MWANJELWA AWATAKA WAAJIRI SERIKALINI KUZINGATIA UBUNIFU KATIKA UJUMUISHWAJI WA MASUALA YA KIJINSIA SEHEMU ZA KAZI ILI KULETA TIJA KIUTENDAJI

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amewataka waajiri serikalini kuzingatia kigezo cha ubunifu wanapotekeleza zoezi la ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi ili kuleta matokeo chanya na yenye tija katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa (Mb) amesema hayo mapema leo, alipokuwa akifungua kikao kazi cha siku mbili kinachohusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia mahala pa kazi kilichofanyika mjini Morogoro.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, endapo waajiri watazingatia kigezo cha ubunifu na kuacha kufanya kazi kwa mazoea serikali itapata watendaji kazi bora watakaoleta matokeo chanya katika maendeleo ya nchi kwani watafanya kazi kwa uadilifu na kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa (Mb) ameongeza kuwa, ubunifu katika utendaji kazi utawezesha watumishi kuondokana na mitazamo hasi juu ya dhana ya jinsia ya kike kutegemea kupata kazi kutokana na jinsi yao badala yake watambue kuwa vigezo na sifa za kiushindani ndiyo vinazingatiwa. 
“Tunapodai haki zetu kama wanawake tuwe na hoja zenye mashiko zitakazoendana na sifa na vigezo husika, tusiseme kuwa sisi ni wanawake hivyo tupewe nafasi” amesema Dkt. Mwanjelwa.
Dkt. Mwanjelwa amewataka waajiri kuzingatia vigezo vya ubunifu wanapoajiri wanawake na kutenga bajeti kwa ajili ya ujumuishwaji wa masuala ya jinsia mahala pa kazi ili kuboresha  utendaji kazi. 
Aidha, Dkt. Mwanjelwa amewaagiza watendaji katika Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kuwa kioo katika utekelezaji wa masuala ya kijinsia mahala pa kazi ili kuepuka vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, rushwa ya ngono, ubaguzi wa aina yoyote, upendeleo, ubadhilifu wa mali za umma na uvujishaji wa siri za serikali.
Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Agnes Meena amesema kuwa, ofisi yake kama mratibu wa masuala ya anuai za jamii imeona umuhimu wa kuandaa kikao cha ujumuishaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kwa kushirikiana na wakurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi Rasilimaliwatu kwa kuwa wao ndio wahusika katika usimamizi wa mipango ya rasilimaliwatu na masuala yote ya kiutumishi.
Bi. Meena amesema kuwa, kikao hicho kimefanyika kutokana na kuwapo kwa mwitikio wa wastani katika utekelezaji wa masuala ya jinsia sehemu za kazi unaosababishwa na kukosekana kwa utayari wa taasisi , mipango katika taasisi, mitazamo hasi, unyanyapaa na ufinyu wa bajeji.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa kikao hicho, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala, Mahakama ya Tanzania, Bi. Wanyenda Kutta amekiri kuwapo kwa changamoto katika utekelezaji wa masuala ya kijinsia mahali pa kazi na kuahidi kuwa kikao hicho kitatoa maazimio yatakayoiwezesha serikali kutekeleza masuala ya kijinsia ipasavyo mahali pa kazi.
Lengo la kikao hicho ni kujadili fursa za masuala ya kijinsia katika utumishi wa umma na kuweka mikakati itakayofanikisha Usawa wa Jinsia kwa Maendeleo Endelevu.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akifungua kikao kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia mahali pa kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.
 Mkurugenzi Msaidizi Idara wa Utawala, Mahakama ya Tanzania, Bi. Wanyenda Kutta akitoa neno la shukrani katika kikao kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia mahali pa kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.
 Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora , Bi. Agnes Meena akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb)  (hayupo pichani) kufungua kikao kuhusu Ujumuishwaji wa masuala ya ya kijinsia mahali pa kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.
Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ,Bi. Leila Mavika akiwasilisha mada katika kikao cha ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia mahali pa kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.
 Baadhi ya washiriki wa kikao kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya Kijinsia mahali pa kazi kutoka katika Wizara na Taasisi za serikali wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) wakati akifungua kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia mahali pa kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.

WADAU WAJADILI CHANGAMOTO ZA MITANDAO YA KIJAMII KUPITIA FILAMU YA THE CLEANERS

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KATIKA kushereheka wiki ya Lugha ya Kifaransa ubalozi wa Uswizi nchini Tanzania umefanya mdahalo na wadau wa mitandao ya kijamii kwa ajili ya kufahamu changamoto wanazokutana nazo pamoja na sheria za makosa ya Kimtandao inavyotumika.

Mdahalo huo ulifanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliweza kuwakutanisha wadau mbalimbali akiwemo Wanasaikolojia, mawakili, wamiliki wa mitandao ya kijamii na jamii husika inayotumia mitandao hiyo.

Kabla ya kuanza kwa mdahalo huo, iliwekwa Filamu ya ‘The Cleaners’ iliyofanikiwa kupata tuzo ya The Geneva International Film na Forum on Human Rights kwa mwaka 2018 nchini Uswizi ambayo imekuwa inazungumzia namna mitandao ya kijamii inavyotumiwa vibaya na wale wanaohusika na kusafisha picha au video chafu wanakuwa kwenye mazingira ya aina gani.

Balozi wa Uswizi nchini Florence Tinguely Mattli amesema kuwa, filamu ya The Cleaners imeweka wazi namna watu walionyuma ya mitandao ya kijamii wanavyofanya kazi kubwa ya kuweza kusafisha yale yote ambayo hayafai kuonekana kwa jamii kimaadili au kitaaluma.

Amesema, wadau wanapokutana katika midahalo ya wazi itasaidia kwenye kubadilisha njia ya mawasiliano ikiwemo na kufahamu haki za binadamu na jinsi mitandao ya kijamii inavyoweza kubadilisha maisha ya watu ikiwemo Kutoa elimu kwa nchi ya Tanzania.

“Kuna kazi kubwa inafanywa na wasafishaji walio nyuma ya maudhui mbalimbali ya Mitandao ya Kijamii na wanakutana na picha za aina tofauti kwa siku na wanazifuta na hilo linasaidia kulinda maadili ndani ya jamii”, amesema Mattli.

Mmiliki na Mwanzilishi wa Jamii Forum Maxence Melo amesema kuwa watu wamekuwa wanatumia mitandao ya kijamii vibaya na hata kwa nchini kwetu namna wanavyopambana kulinda maudhui ya Kiswahili kama kinachofanyika kwenye filamu ya The Cleaners.

Maxence amesema, watumiaji wa zamani wa mitandao walikuwa ni wasomi na kabla ya kuiweka mtandaoni wanafikiria maudhui ila kwa sasa hivi watumiaji wa mktandao ya kijamii wamekuwa wengi na kila mmoja anaweka kile anachojisikia kwa muda huo.

Mwanasaikilojia Araika Mkulo amesema, filamu ya the Cleaners imeonesha kiasi gani walio nyuma ya mitandao ya kijamii wanapata changamoto kubwa sana ukilinganisha na namna watu wanavyofikiria. “Takribani kwa siku mtu anakutana na picha zisizo na maadili 25,000 na kujiuliza je wanapata stahiki zao kama inavyotakiwa kwani wamekuwa wanakutana na changamoto za kisaikilojia kutokana na kuona picha chafu na zisizo na maadili mara kwa mara,”amesema .

Wakili wa kujitegemeaBenedict Ishabakaki amesema kwa serikali ya Tanzania imeweka sheria ya makosa ya kimtandao Kipengele cha 12 kikielezea adhabu ya mtu atakayeweka picha au taarifa isiyo na maadili kwenye mtandao wa kijamii ambapo anaweza kufungwa kifungo kisichopungua mwaka mmoja au faini isiyopungua Milion 5 au vyote kwa pamoja.

Filamu ya The Cleaners inaonesha namna jamii inavyotumia mitandao ya kijamii pasi na kufuata maudhui au maadili na watu walionyuma ya mitandao hiyo wakiwa wanafanya jitihada za kusafisha picha chafu na zisizo kwa dunia nzima.
Balozi wa Uswis nchini Tanzania Florence Tinguely Mattli akizungumza na wadau mbalimbali waliojitokeza kwenye mdahalo kuhusiana na matumizi ya mitandao, wanaosafisha picha zisizo na maadili mtandaoni pamoja na kuangalia Filamu ya The Cleaners iliyoshinda tuzo ya The Geneva Internationla Film and Forum on Human Rights.
Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Jamii Forum Maxence Melo akitoa hoja kuhusu matumizi ya mtandaoni pamoja na changamoto wanazokutana nazo wanaosafisha picha au taarifa zisizo za kimaadili na kuangalia Filamu ya The Cleaners iliyoshinda tuzo ya The Geneva Internationla Film and Forum on Human Rights. Pembeni ni Mwanasaikolojia Araika Mkulo na Wakili Benedict Ishabakaki

Tanzania Mwenyeji Tamasha la JAMAFEST 2019.

$
0
0
Na Shamimu Nyaki-WHUSM 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe amesema kuwa Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linatarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 21-28 mwaka huu. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Dkt.Mwakyembe ameeleza kuwa Tamasha hilo linaloongozwa na Kauli mbiu “Uanuai wa Kitamaduni;Msingi wa Utengamano wa Kikanda,Maendeleo ya Kiuchumi na Kushamiri kwa Utalii. Lengo lake ni kulinda na kuendeleza Urithi wa Utamaduni na kukuza utambulisho wa Afrika Mashariki. 

Ameendelea kueleza kuwa Tamasha hilo litawezesha uhamasishaji wa Sanaa na Utamaduni kwa kutangaza vivutio vya kitalii na utamaduni vilivyopo nchini,kutangaza fursa za kiuchumi na kijamii pamoja na mandhari mazuri ya upigaji picha na filamu kwa wadau wa kitaifa kikanda na kimataifa. 

“Tamasha litaunganishwa na matamasha mengine ya Utamaduni nchini ikwemo Usiku wa tuzo za Serengeti International Film Festival pamoja na tukio la watu sita watakaopanda Mlima Kilimanjaro na kupeperusha bendera za nchi zao juu ya kilele cha Mlima huo kuashiria uzinduzi wa Tamasha hilo la JAMAFEST”alisema Dkt.Mwakyembe. 

Mhe. Mwakyembe ameendelea kueleza kuwa Tamasha hilo litakuwa na maonesho mbalimbali ya kiutamaduni ikiwemo mavazi asili, sanaa ya uchongaji,wabunifu wa vifaa vya mapambo,michezo ya kuigiza watunga riwaya na mabingwa wa lugha ya Kiswahili,watengenezaji wa vyakula na michezo mbalimbali ya Jadi. 

Aidha Dkt. Mwakyembe ameisitiza Watanzania kushiriki katika tamasha hilo kwa kuuza na kutangaza kazi zao za Sanaa na Utamaduni kwani nchi yetu mwaka huu imebahatika kuwa na matukio makubwa yenye fursa ya kuitangaza nchi ikiwemo Sekta ya Michezo kwani timu ya Taifa Stars na Serengeti Boys zinatarajiwa kuiwakilisha nchi katika mashindano makubwa ya Afrika ya AFCON. 

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu ambaye ndiye mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Bibi.Joyce Fissoo amesema kuwa Tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini ambapo nchi sita za Jumuiya ya Afrika Mashariki za Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi Sudan Kusini na Mwenyeji Tanzania zinatarajiwa kushiriki. 

Bibi Fissoo ameendelea kueleza kuwa Tamasha hilo lilifanyika kwa mara ya kwanza nchini Rwanda mwaka 2013 ambalo lilihudhuriwa na washiriki17,500 Kenya ikafuatia mwaka 2015 kwa kuwa na washiriki 21,000 na Uganda mwaka 2017 ambapo washiriki 42,600 walijitokeza. 

“Tamasha hili linafanyika kwa mzunguko miongoni mwa nchi hizo wanachama wa Jumiya ya Afrika Mashariki kwa kila baada ya miaka miwili kwa mujibu wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki la mwaka 2012”.aliongeza Bi Fissoo. 

Tamasha hilo linaratibiwa na Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara nyingine,pamoja na Kamati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojumuisha nchi wanachama. 
.Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (Katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 20/2019 Jijini Dar es Salaam kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalotarajiwa kufanyika septemba 21 -28 2019.Wa Kwanza kulia  ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara hiyo Bibi Leh Kihimbi.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo(katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 20/2019 Jijini Dar es Salaam kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalotarajiwa kufanyika septemba 21 -28 Kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe na Kulia ni Katibu Mtendaji wa BASATA Bw.Godfrey Muingereza.

ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA AFYA YA KINYWA NA MENO DUNIANI

$
0
0
Na Miza Kona Maelezo Zanzibar
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed amewataka Madaktari kufanya utafiti wa kina ili kujua kiwango cha maradhi ya kinywa na meno na namna ya kupunguza maradhi hayo katika jamii.

Waziri Hamad ameyasema hayo katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Kinywa na Meno duniani iliyofanyika Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge mjini Zanzibar.

Amesema utafiti huo utaweza kusaidia kutoa taaluma zaidi kwa Walimu wanaofundisha watoto wakiwa skuli na hivyo kuwajengea uwezo wa kujikinga na matatizo ya kutoboka kwa meno na kuvimba fizi.

Amefahamisha kuwa kufanyika kwa utafiti huo kutasaidia kupatikana kwa takwimu sahihi na kuweza kujua ukubwa wa maradhi hayo na kupatiwa ufumbuzi wake.

Aidha amewataka wananchi kuvitumia Vituo vya afya na hospitali za serikali kupata huduma zilizobora ili kuondoa matatizo yanayowakabili.

“Nia ya Serikali ni kuwa na taifa la watu wenye afya ni vyema kupima afya zetu angalau mara mbili kwa mwaka katika Vituo vya afya vilivyokaribu nasi,” alieleza Wazri Hamad

Aidha Waziri huyo wa Afya aliwaomba wananchi kufanya usafi wa kinywa pamoja na kuwafundisha watoto namna ya kupiga mswaki ili kuepuka matatizo kutoboka kwa meno na kutoa harufu katika kinywa.

“Asilimia 90 ya matibabu ya maradhi haya tunayo wenyewe, tiba zaidi ni kuwa wasafi, hivyo nawaomba sana kuzingatia usafi maana afya ni usafi” alisisitiza Waziri Hamad.

Waziri Hamad alitumia fursa hiyo kuwasisitiza Wananchi kuchangia damu kwa lengo la kusaidia jamii na kuokoa maisha ya wagonjwa ambao wanakabiliwa na tatizo la kupoteza damu.

Aidha amewasisitiza madaktari na wahudumu wa afya kuwa Wazalendo na kufanya kazi kwa bidii pamoja na lugha nzuri wakati wa kuwahudumia wananchi.

Nae Mkuu wa Kitengo cha Meno na Kinywa Hospitali ya Mnazimmoja Dk Semeni Shaaban Mohamed kuwa amesema asilimia 90 ya wananchi wana matatizo ya meno ni vyema kwa jamii kuwa na utamaduni wa chunguza afya ya meno ili kuepuka madhara ya kutoboka na kung’oka.

Aidha ameeleza kuwa kitengo chake kinakabiliwa na upungufu wa vifaa vya upasuaji pamoja na kuiomba serikali kupeleka huduma za meno katika vituo vidogo vidogo vya afya ili kuondoa usumbufu kwa wananchi kufuata huduma katika hospitali hiyo.
 Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akizungumza na wananchi na Madaktari katika maadhimisho ya siku ya kinywa na meno Duniani yaliyofanyika Mapinduzi Square Michenzani Mjini Zanzibar, (kushoto) Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Sleiman na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Meno na Kinywa Hospitali ya Mnazimmoja Dkt. Semeni Shaban Mohd.
 Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akiwa na mmoja wa madaktari wa kujitolea kutoka Finland Prof. Ana Pucar akionyesha jinsi ya kupiga msuwaki katika maadhimisho ya siku ya kinywa na meno Duniani.
 Daktari bingwa wa meno Zanzibar Iddi Suleiman akifanyia uchunguzi wa meno mtoto Rashid Msote.
 Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya siku ya kinywa na meno Duniani wakiwa kwenye foleni kwa ajili yakwenda kufanyiwa uchunguzi wa kinywa na meno.
Timu ya madaktari wa kujitolea kutoka Finland wakiwa na furaha katika siku ya afya kinywa na meno Duniani iliyoadhimishwa Mapinduzi Square Michenzani Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga

MENEJA RASILIMALI WATU TPDC AIAMBIA MAHAKAMA HAJUI NI SHTAKA GANI LINALOWAKABILI VIGOGO WATANO WA SHIRIKA HILO

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MENEJA Rasilimali watu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mary Samson, ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, haelewi ni shtaka gani ambalo vigogo watano wa shirika hilo wanashtakiwa nalo. 

Pia amedai hajui kama bodi ya Wakurugenzi ya TPDC ndio waliopeleka tuhuma zinazowakabili vigogo hao Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) au la.

Mary ambae ni shahidi wa upande wa mashtaka katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka ameeleza hayo leo Machi 21, 2019 wakati akijibu swali la Wakili wa utetezi Emmanuel Makene lililomtaka aieleze Mahakama kama anafahamu washtakiwa wanakabiliwa na kesi gani mahakamani hapo na kama shirika hilo ndilo lililowashtaki ama la.

Katika keai hiyo, vigogo wanaoshtakiwa ni, Mkurugenzi Mtendaji James Mataragio, Kaimu Meneja wa Uvumbuzi, George Seni, Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Utawala Wellington Hudson, Mkurugenzi wa Mkondo wa Juu, Kelvin Komba na Edwin Riwa ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa mipango.

Akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kelvin Mhina, shahidi Mary amedai

mshtakiwa James Mataragio aliteuliwa na Rais lakini hajawai kupokea barua kutoka kwa Rais ya kumsimamisha kazi mshtakiwa huyo wala hajawai kupokea barua kutoka kwa Rais ya kumuelekeza Mwenyekiti wa bodi ya TPDC kumsimamisha kazi mshtakiwa huyo. 

Amedai, washtakiwa hao mpaka leo bado ni watumishi wa TPDC isipokuwa walisimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazowakabili ambazo yeye hazijui. 

Akiongozwa na Wakili wa Serikali kutoka Takukuru Aneth Mavika kutoa ushahidi wake shahidi Mary amedai kuwa nyaraka za watumishi wa shirika hilo zipo katika majalada yanayotunzwa kwenye masijala ya siri na kuongeza anawafahamu washtakiwa kwa kuwa ni watumishi wenzie na ni mabosi zake ila kwa sasa wamesimamishwa kazi.

Amedai majalada ya washtakiwa hao, yalichukuliwa ofisini kwao Januari mwaka huu na kuyapeleka Takukuru baada ya taasisi hiyo kuyahitaji kwa ajili ya uchunguzi.

Amedai, Januari mwaka huu, shirika lilipokea hati kutoka Takukuru iliyoelekeza kuhitaji majalada hayo agizo ambalo walilitekeleza kwa kukabidhi majalada hayo kwao.

Akifafanua kuhusu jalada la mshtakiwa mmoja mmoja, amedai mshtakiwa James jalada linaonesha kuwa mtumishi huyo aliajiriwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Desemba 15,2014 ambapo alidumu katika nafasi hiyo hadi Agosti 24,2016 aliposimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili. 

Mshtakiwa George Seni yeye inaonesha aliajiriwa TPDC Februari ,2014 na kutakiwa kuendelea na wadhifa aliokuwanao kutoka ofisi za Bunge ambapo alikuwa Mhasibu Mkuu hata hivyo alipofika TPDC hakukuwa na cheo hicho hivyo kupewa cheo cha Mkurugenzi wa Fedha. 

Kwa upande wake, mshtakiwa Wellington Hudson aliajiliwa TPDC Mei 23, 1989 kama Mtaalamu wa Jiolojia na Juni, 2015 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Utawala ambapo alidumu katika cheo hicho mpaka Julia 14, 2017 aliposimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili. 

Pia Mary amedai, mshtakiwa Kelvin Komba aliajiriwa TPDC, Mei 23, 1989 na April 2014 aliteuliwa kukaimu nafasi ya Mkurugenzi wa mipango aliyodumu nayo hadi Agosti 24, 2016 aliposimamishwa kazi kupisha uchunguzi. 

Kuhusu mshtakiwa Edwin Riwa naye aliajiriwa Desemba 12, 2009 kwa nafasi ya Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi baadae cheo hicho kilibadirishwa jina na kuitwa Meneja Manunuzi, baada ya mchakato Januari, 2015 alikuwa Meneja Manunuzi na alikaa katika nafasi hiyo hadi Agosti 24, 2016 aliposimamishwa kazi kupisha uchunguzi.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na shtaka la matumizi mabaya ya madaraka na wanadaiwa kuwa walitenda kosa hilo kati ya April 8, 2015 na June 3,2016.

Inadaiwa wakiwa watumishi wa umma na waajiriwa wa TPDC kwa nafasi zao, wakati wakitimiza majukumu yao kwa makusudi walitumia madaraka vibaya.

Inadaiwa walibadilisha na kupitisha bajeti na mpango wa mwaka wa manunuzi wa mwaka 2014/2015 na 2015/2016 kwa kuingiza ununuzi wa kifaa cha utafiti cha airborne gravity gradiometer survey ndani ya ziwa Tanganyika bila ya kupata kibali cha bodi ya wakurugenzi ya shirika.

Inadaiwa kitendo hicho kinakiuka kifungu cha 49(2) cha sheria ya manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 kwa lengo la kujipatia manufaa yasiyohalali ya dola 3,238,986.50 ambazo ni sawa na Sh7.2 bilioni kwa Bell Geospace.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 16, itakapokuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.

Tanzania Mwenyeji Tamasha la JAMAFEST 2019

$
0
0
Na Shamimu Nyaki-WHUSM
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe amesema kuwa Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linatarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 21-28 mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Dkt.Mwakyembe ameeleza kuwa Tamasha hilo linaloongozwa na Kauli mbiu “Uanuai wa Kitamaduni;Msingi  wa Utengamano wa Kikanda,Maendeleo ya Kiuchumi na Kushamiri kwa Utalii. Lengo lake ni kulinda na kuendeleza Urithi wa Utamaduni na kukuza utambulisho wa Afrika Mashariki.
Ameendelea kueleza kuwa Tamasha hilo litawezesha uhamasishaji wa Sanaa na Utamaduni kwa kutangaza vivutio vya kitalii na utamaduni vilivyopo nchini,kutangaza fursa za kiuchumi na kijamii pamoja na mandhari mazuri ya upigaji picha na filamu kwa wadau wa kitaifa kikanda na kimataifa.
“Tamasha litaunganishwa na matamasha mengine ya  Utamaduni nchini ikwemo Usiku wa tuzo za Serengeti International Film Festival pamoja na tukio la watu sita watakaopanda Mlima Kilimanjaro na kupeperusha bendera za nchi zao juu ya kilele cha Mlima huo kuashiria uzinduzi wa Tamasha hilo la JAMAFEST”alisema Dkt.Mwakyembe.
Mhe. Mwakyembe ameendelea kueleza kuwa Tamasha hilo litakuwa na maonesho mbalimbali ya kiutamaduni ikiwemo mavazi asili, sanaa ya uchongaji,wabunifu wa vifaa vya mapambo,michezo ya kuigiza watunga riwaya na mabingwa wa lugha ya Kiswahili,watengenezaji wa vyakula na michezo mbalimbali ya Jadi.
Aidha Dkt. Mwakyembe ameisitiza Watanzania kushiriki katika tamasha hilo kwa  kuuza na kutangaza kazi zao za Sanaa na Utamaduni kwani nchi yetu mwaka huu imebahatika kuwa na matukio makubwa yenye fursa ya kuitangaza nchi ikiwemo Sekta ya Michezo kwani timu ya Taifa Stars na Serengeti Boys zinatarajiwa kuiwakilisha nchi katika mashindano makubwa ya Afrika ya AFCON.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu ambaye ndiye mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Joyce Fissoo amesema kuwa Tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini ambapo nchi sita za Jumuiya ya Afrika Mashariki za Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi Sudan Kusini na Mwenyeji Tanzania zinatarajiwa kushiriki.
Fissoo ameendelea kueleza kuwa Tamasha hilo lilifanyika kwa mara ya kwanza nchini Rwanda mwaka 2013 ambalo lilihudhuriwa na washiriki17,500 Kenya ikafuatia mwaka 2015 kwa kuwa na washiriki 21,000 na Uganda mwaka 2017 ambapo washiriki 42,600 walijitokeza.
“Tamasha hili linafanyika kwa mzunguko miongoni mwa nchi hizo wanachama wa Jumiya ya Afrika Mashariki kwa kila baada ya miaka miwili kwa mujibu wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki la mwaka 2012”.aliongeza Bi Fissoo.
Tamasha hilo linaratibiwa na Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara nyingine,pamoja na Kamati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojumuisha nchi wanachama.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (Katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 20/2019 Jijini Dar es Salaam kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalotarajiwa kufanyika septemba 21 -28 2019.Wa Kwanza kulia  ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara hiyo Leh Kihimbi.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo(katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 20/2019 Jijini Dar es Salaam kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalotarajiwa kufanyika septemba 21 -28 Kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe na Kulia ni Katibu Mtendaji wa BASATA Bw.Godfrey Muingereza.

Medie Kagere akabidhiwa tuzo na Bikosports ya mchezaji bora

$
0
0

 Msemaji wa bikosports nchini Tanzania, Geofrey Lea kushoto akiwa na mshambuliaji wa klabu ya Simba, Medie Kagere, aliyetwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi February, tuzo inayodhaminiwa na Kampuni ya michezo ya kubashiri matokeo nchini ya Biko Sports, ambapo mbali na tuzo hiyo, pia alikabidhiwa sh milioni moja.
Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Medie Kagere, akiwa ameshika tuzo yake aliyokabidhiwa na waendeshaji wa mchezo wa kubashiri matokeo wa bikosports, ambapo mbali na tuzo hiyo, pia Kagere alipokea zawadi yake ya sh milioni moja kutoka Biko Sports, ambao ndio wadhamini wa tuzo hizo.

 

FAMILIA NCHINI NEWZEALAND ZAANZA KUPOKEA MIILI YA WAPENDWA WAO

$
0
0
* Waziri Mkuu kutangaza sheria mpya ya umiliki wa silaha ndani ya siku 10
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
LEO Machi 20 ndugu wa familia za waliopoteza maisha katika shambulio la kigaidi katika misikiti ya Wood na Al Nool katika mji wa Christchurch nchini Newzealand.

Kwa mujibu wa mtandao wa Dailymail miili hiyo imekabidhiwa kwa ndugu zao huku polisi wakieleza kuwa uchunguzi umekamilika ambapo miili 12 ikiwa imetambulika na tayari miili 6 imekabidhiwa kwa ndugu zao.

Waziri Mkuu nchini humo Jacinda Ardern amesema kuwa kufikia jumatano miili yote itakuwa imekabidhiwa kwa ndugu zao.

Aida Jacinda amesema kuwa ndani ya siku 10 kuanzia sasa sheria mpya ya umiliki wa silaha itatangazwa na wanaamini taifa hilo litakuwa salama zaidi.

Shambulio hilo la kigaidi lilitokea ijumaa wiki iliyopita na tayari mtuhuma wa mauaji hayo Brenton  Tarrant (28)raia wa Australia alifikishwa mahakama mapema Jumamosi.

KAMATI YA PIC YASHAURI TAASISI ZA UMMA KUTUMIA HUDUMA ZA TTCL

$
0
0



Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) Dk. Raphael Chegeni (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kamati yake kufanya ziara kutembelea miradi inayoendeshwa na kusimamiwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omari Rashid Nundu pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Ndugu Waziri Waziri Kindamba (kulia).
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) Dk. Raphael Chegeni (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kamati yake kufanya ziara kutembelea miradi inayoendeshwa na kusimamiwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omari Rashid Nundu pamoja na Mjumbe wa Kamati ya PIC, Zainab Vullu.
Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omari Rashid Nundu (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kufanya ziara kutembelea miradi inayoendeshwa na kusimamiwa na TTCL leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) Dk. Raphael Chegeni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Waziri Kindamba.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakiwa katika mkutano na wanahabari mara baada ya kufanya ziara yao kutembelea miradi inayoendeshwa na kusimamiwa na TTCL leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakiwa katika mkutano na wanahabari mara baada ya kufanya ziara yao kutembelea miradi inayoendeshwa na kusimamiwa na TTCL leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakiwa katika mkutano na wanahabari mara baada ya kufanya ziara yao kutembelea miradi inayoendeshwa na kusimamiwa na TTCL leo jijini Dar es Salaam.



MWENYEKITI Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) Dk. Raphael Chegeni amezitaka Taasisi za Umma na Ofisi za Serikali ambazo bado hazijaanza kutumia huduma za Mawasiliano zinazotolewa na Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL kuanza mara moja kutumia Huduma hizo.

Dkt Chegeni amesema, Taasisi za Umma zina wajibu mkubwa wa kutumia Huduma za TTCL ikiwa ni kuunga mkono Jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kufufua Mashirika ya Umma.

Dk Chegeni ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya kamati yake kufanya ziara kwenye miradi inayoendeshwa na kusimamiwa na TTCL iliyopo jijini Dar es Salaam.

"..Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na Kituo cha kutunza kumbukumbu 'Data Center' vinafanya kazi vizuri sana, Mkongo unawezesha Mawasiliano bora kwa Nchi nzima na Majirani zetu huku taarifa mbalimbali zikihifadhiwa katika kituo cha Data Centre lakini Miundombinu hii haitumiki ipasavyo. "Sisi kama Kamati tumebaini kwamba taasisi nyingi za Serikali bado hazijalitumia vizuri Shirika letu la TTCL na huduma zinazotolewa.

Hali hii inaonesha wazi kwamba bado hatujatoa msisitizo wa kutosha kwa Wizara, Idara za Serikali na Taasisi zote kwa ujumla kuwa Wateja wa TTCL ili Shirika letu liweze kujiendesha kwa Tija na Taifa kufaidika.

Aidha Kamati hiyo imeshauri taasisi hizo kutumia sasa mitandao na huduma za data za TTCL jambo ambalo ni muhimu kuliunga mkono shirika hilo la Umma. "...Kamati inaona ni vizuri taasisi za Serikali kutumia huduma hizi vizuri, kwani uwekezaji uliofanywa unatumika chini ya matarajio. Serikali imefanya uwekezaji mkubwa sana na kama tunashindwa kutumia huduma hizo tunapasa hasara" alisisitiza Mwenyekiti huyo.

Kamati pia imeshauri gharama za uwekezaji unaofanywa na Shirika la TTCL ichukuliwe na Serikali kwa lengo la kuiondolea mzigo shirika. Uwekezaji huu mkubwa unapoachiwa katika shirika linashindwa kufanya kazi kwa ufanisi na kujikuta linabeba mzigo mkubwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omari Rashid Nundu alisema Mwaka 2019, TTCL Corporation imejipanga vyema kuhakikisha kuwa Huduma za Shirika ina sambaa zaidi kote Nchini huku tukisimamia ubora na unafuu wa gharama kwa Wananchi wote.

"Tumekusudia kuendelea kufanya mageuzi makubwa ndani ya Shirika ili kuli wezesha kushindana kikamilifu katika Soko la Huduma za Mawasiliano Nchini sambamba na kutimiza wajibu wa kimsingi wa kuwa mchangiaji muhimu katika Pato la Taifa," alisema Mhandisi Rashid Nundu.
Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omari Rashid Nundu (wa pili kushoto) pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakiwa ziarani kutembelea miradi inayoendeshwa na kusimamiwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakiwasili eneo la mapokezi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo jijini Dar es Salaam kutembelea shirika hilo.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya TTCL.

PROF. KABUDI AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UAE NCHINI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi alipomtembelea katika ofisi ndogo za Wizara zilizopo Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Machi 2019. Mazungumzo hayo yalijikita katika kujadili masuala mbalimbali ya namna ya kudumisha na kukuza uhusiano baina ya Tanzania na UAE. 
Waziri Mhe. Kabudi akimsikiliza Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Mhe.Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi walipokutana kwa Mazungumzo Jijini Dar es Salaam 
Mazungumzo yakiendelea.



Mhe. Prof. Kabudi akutana kwa mazungumzo na Balozi wa UAE nchini

Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Khalifa Abdulrahman Al-Marzooqi, Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) nchini. 

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika tarehe 20 Machi 2019 kwenye ofisi ndogo za Wizara zilizopo Dar es Salaam, Prof. Kabudi alimshukuru Mhe. Balozi Al-Marzooqi kwa kupata fursa ya kukutana naye na kwamba, Tanzania inathamini mahusiano na ushirikiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu. 

Aidha, alimweleza Balozi huyo kuwa, Wizara chini ya uongozi wake itaendelea na jitihada za kuhakikisha kuwa, mahusiano yaliyopo kati ya nchi hizi mbili yanaimarishwa.Kwa upande wake, Mhe. Balozi Al-Marzooqi ametumia mazungumzo hayo kumpongeza Mhe. Prof. Kabudi kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kumhakikishia ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha mahusiano yaliyopo yanaimarishwa.

Mhe. Balozi Al-Marzooqi aliongeza kuwa, Umoja wa Falme za Kiarabu una nia ya kuimarisha mahusiano yaliyopo na umepanga kufungua Ubalozi mdogo (Consulate General) Zanzibar. Pia, Mhe. Balozi alimuarifu Mhe. Waziri kwamba ana mpango wa kuutembelea Mkoa wa Dodoma ili pamoja na masuala mengine, kujionea eneo walilopewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za ubalozi na makazi kwa lengo la kujipanga kuliendeleza.

Kadhalika, Prof. Kabudi na Mhe. Balozi Al-Marzooqi wamekubaliana kuendeleza ushirikiano kwenye maeneo ya uwekezaji ambapo Balozi huyo ameonesha nia ya kuendelea kushawishi wawekezaji kutoka nchini kwake kuja kuwekeza nchini hususan kwenye sekta za utalii, hoteli, viwanda na utoaji wa huduma. Pia ameahidi kuwashawishi wafanyabishara wakubwa na wadogo kutoka UAE kuja nchini ili kujionea fursa za biashara zilizopo.

Prof. Kabudi amemuhakikishia Balozi Al-Marzooqi kuwa, Tanzania ni eneo bora la uwekezaji na biashara na kwamba, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Wizara zingine zitaendelea kuweka mazingira mazuri ya kupokea wawekezaji na wafanyabiashara kutoka maeneo yote duniani.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
20 Machi 2019

Majadiliano mradi wa LNG kuanza mwezi Aprili

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, ameeleza kuwa, Serikali imeamua kuanza rasmi majadiliano ya mradi wa uchakataji na uuzaji gesi iliyo katika hali ya kimiminika (Liquefied Natural Gas-LNG project) mwanzoni mwa mwezi wa Nne mwaka huu. 

Dkt Kalemani ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kikao chake na watendaji wa kampuni ya Equinor ambayo ni moja ya kampuni zitakazotekeleza mradi huo. 

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Charles Sangweni na watendaji kutoka Wizara ya Nishati.

Watendaji wa kampuni hiyo walifika kuonana na Waziri wa Nishati jijini Dodoma ili kujadiliana namna bora ya kuharakisha majadiliano ya mkataba wa uwekezaji kati ya Serikali ya Tanzania na wawekezaji wa mradi huo.

“Serikali imeamua kutekeleza mradi huu kutokana na na umuhimu wake katika ukuaji wa uchumi wa nchi, hivyo tumeshapanga kuwa majadiliano ya mradi huo yaanze mwezi wa Nne na yakamilike mwezi wa Tisa mwaka huu,” alisema, Dkt Kalemani.

Dkt. Kalemani alitoa angalizo kuwa, majadiliano hayo yalenge katika kuhakikisha kuwa pande zote mbili zinafaidika na mradi huo na kwamba kila upande ulenge katika kufanikisha mradi huo na si kuukwamisha.

Kwa upande wake, Makamu Mwandamizi wa Rais wa kampuni ya Equinor, Dkt. Mette Halvorsen Ottoy alisema kuwa, kampuni hiyo kutoka nchini Norway imedhamiria kutekeleza mradi huo ambao pamoja na kuendeleza gesi asilia nchini utaendelea kudumisha uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi ya Norway na Tanzania.

Mradi wa uchakataji na uuzaji gesi iliyo katika hali ya kimiminika (Liquefied Natural Gas-LNG project) unatarajiwa kutekelezwa mkoani Lindi ambapo kampuni ya Equinor inatarajiwa kuingia Mkataba na Serikali katika Mradi huo. Kampuni nyingine zinazotarajiwa kutekeleza mradi huo ni Shell, Pavillion na Ophir.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) na Makamu Mwandamizi wa Rais wa kampuni ya Equinor, Dkt. Mette Halvorsen Ottoy wakijadiliana kuhusu mradi uchakataji na uuzaji gesi iliyo katika hali ya kimiminika (Liquefied Natural Gas-LNG project).
 Watendaji wa kampuni ya Equinor wakiwa katika kikao na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kilicholenga kujadili namna bora ya kuharakisha majadiliano ya mkataba wa uwekezaji kati ya Serikali ya Tanzania na wawekezaji wa mradi uchakataji na uuzaji gesi iliyo katika hali ya kimiminika (Liquefied Natural Gas-LNG project).

TEMESA YAALIKA WADAU KUJADILI RASIMU YA MUONGOZO WA MATENGENEZO YA MAGARI

$
0
0
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle akizungumza wakati akifungua kikao cha wadau kujadili Rasimu ya Muongozo wa Matengenezo ya magari, pikipiki, mitambo, usimikaji na matengenezo ya mifumo ya umeme, elektroniki, viyoyozi, majokofu na kangavuke pamoja na ushauri wa kiufundi kilichohudhuriwa na Wazabuni, wamiliki wa gereji teule, maafisa usafirishaji na wadau kutoka taasisi za Umma na binafsi walioko mkoa wa Dar es Salaam. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Mt. Depot Keko Dar es Salaam.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle akizungumza na wadau kutoka taasisi za Umma, wazabuni, wamiliki wa gereji teule, maafisa kutoka halmashauri ya mji na maafisa usafirishaji kutoka taasisi za serikali na binafsi walioko mkoa wa Dar es Salaam  wakati wa kikao cha kujadili Rasimu ya Muongozo wa Matengenezo ya magari, pikipiki, mitambo, usimikaji na matengenezo ya mifumo ya umeme, elektroniki, viyoyozi, majokofu na kangavuke pamoja na ushauri wa kiufundi  kilichofanyika katika ukumbi wa Mt. Depot Keko jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wadau kutoka taasisi za Umma na binafsi, gereji teule, ofisi za halmashauri na wizara mbalimbali kutoka mkoa wa Dar es Salaam wakifuatilia kwa umakini hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa kikao cha kujadili Rasimu ya Muongozo wa Matengenezo ya magari, pikipiki, mitambo, usimikaji na matengenezo ya mifumo ya umeme, elektroniki, viyoyozi, majokofu na kangavuke pamoja na ushauri wa kiufundi  kilichoandaliwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Mt. Depot Keko jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Sylvester Simfukwe akitoa ufafanuzi wakati akijibu swali la mmoja wa wadau wakati wa kikao cha kujadili Rasimu ya Muongozo wa Matengenezo ya magari, pikipiki, mitambo, usimikaji na matengenezo ya mifumo ya umeme, elektroniki, viyoyozi, majokofu na kangavuke pamoja na ushauri wa kiufundi kilichoandaliwa na Temesa. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Mt.Depot Keko jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Maafisa usafirishaji, wazabuni, wamiliki wa gereji teule, maafisa tawala na wadau kutoka taasisi mbalimbali za Umma na binafsi zilizopo mkoani humo.

RC MAKONDA KUUNDA MFUKO WA KUWASOMESHA WASICHANA 100 BURE KUANZIA KIDATO CHA TANO HADI SITA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda katika kuwawezesha watoto wa kike waliokuwa wanafaulu vizuri masomo ya sayansi lakini wanashindwa kuendelea na masomo, kwasababu ya ugumu wa maisha ameamua kuunda mfuko maalumu utakaokuwa na jukumu la kusomesha wasichana 100 Bure kila mwaka kuanzia kidato cha tano hadi sita.

RC Makonda amesema walengwa wa Mfuko huo ni watoto wa kike waliofaulu vizuri masomo ya sayansi licha ya kutokea kwenye familia duni ambazo ni yatima, watoto wa Mamantilie, kondakta,wavuvi na ombaomba.

Aidha RC Makonda lengo la kujikita kwenye masomo ya sayansi ni kuzalisha Madakrari bingwa wanawake, Marubani, wabobezi wa computer, wataalamu wa gesi na fani nyinginezo ambazo anaamini ukimkomboa mwanamke umeikomboa jamii.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema waliopata fursa hiyo watagharamiwa kuanzia Ada, Madaftari, Bag,Vitabu na pesa ya kujikimu ili wabaki ni jukumu moja la kusoma na kufaulu. 

Mhe. Makonda amesema hatua hiyo inaenda sambamba na kuunga mkono jitiada za Rais Magufuli kupambana na umaskini kwa kuhakikisha watoto wa maskini wanasoma bure ili waje kuzisaidia familia zao.

RC Makonda anaamini kuwa kama mtoto wa kike ameweza kufaulu masomo na kuvishinda vishawishi vya mafataki wanaotumia pesa au lifti kuwarubuni na kuwapa ujauzito, basi mtoto huyo akiendelezwa anaweza kuwa mtu mkubwa nchini na nje ya nchi.
RC Paul Makonda

PAC YASHAURI UJENZI WA HUDUMA ZA KIJAMII KATIKA MIRADI YA NYUMBA KIGAMBONI, BUNJU B

$
0
0
*Mradi wa Nyumba Kigamboni, Gezaulole umegharibu kiasi cha Tsh. Bilioni 21.7
*Mradi wa Bunju B umegharimu Tsh. Bilioni 4.1.


Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeshauri kujengwa huduma za kijamii ikiwemo miundombinu katika ujenzi wa miradi ya nyumba iliyopo Gezaulole, Kigamboni na Bunju B jijini Dar es Salaam.

Miradi ya Ujenzi wa Nyumba hizo unatekelezwa na Watumishi Housing Company, ambapo PAC imefanya ziara maeneo hayo kuangalia ubora wa nyumba hizo, Uuzaji na upangishaji pamoja na kuhakikisha pesa hizo za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii hazitapelekea kufirisi Mifuko hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada yakutembelea miradi hiyo, Mwenyekiti wa PAC, ambaye ni Mbunge wa Same Mashariki, Mhe. Nagy Livingstone Kaboyoka amesema nyumba hizo zinaridhisha kutokana kiasi cha Pesa kilichotumika.

Mhe. Kaboyoka amewashauri Watumishi Housing kuhakikisha Miundombinu bora zikiwemo Barabara, Shule, Zahanati pamoja na Masoko zinapatikana maeneo hayo kwa urahisi ili kuleta kichocheo kutokana na umbali wa nyumba zilipo. 

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Aesh Hillary ameungana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo kuridhishwa na Bei za nyumba, Soko licha ya Watumishi wangi kuhamia Dodoma, amesema ujenzi wa nyumba hizo umelenga zaidi Watumishi wa hali ya chini ambapo ameomba mradi huo kuenezwa sehemu mbalimbali nchini. 

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company, Dkt. Fredy Msemwa amesema mradi wa huo umekamilika kwa 95%, Kigamboni, Gezaulole ukikamilika utakuwa na nyumba 795, amesema awamu ya kwanza utakuwa na nyumba 329, ambapo 268 ni Ghorofa na 61 nyumba za chini, 50% ya nyumba hizo tayari zimeuzwa.

Amesema mradi wa ujenzi Bunju B umekamilika kwa 98%, una nyumba 64 pamoja na Miundombinu yote kukamilika ambapo nyumba 20 tayari zimeuzwa.

Dtk. Msemwa amesema Mardi huo utafungua fursa ya mauzo kwa Watumishi wa Umma kwa nyumba hizo, Pia itafungua fursa kwa Sekta binafsi wakiwemo Waandishi wa Habari pamoja na Wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Mwenyekiti wa PAC, ambaye ni Mbunge wa Same Mashariki, Mhe. Nagy Livingstone Kaboyoka (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea miradi ya nyumba zilizopo Gezaulole, Kigamboni na Bunju B jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa (wa kwanza kulia) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa PAC, Mhe. Nagy Livingstone Kaboyoka (wa pili kulia) wakati wa ziara ya Kamati hiyo ilipotembelea mradi wa ujenzi wa nyumba wa Gezaulole, Kigamboni jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Mssaka,MMG)
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali wakitembelea Miradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Gezaulole wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa majengo ya Mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Gezaulole wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam. 
Muonekano wa majengo ya Mradi Nyumba za Watumishi Housing Company zilizopo Bunju B wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

TBS YATOA SEMINA KWA WAAGIZAJI WA BIDHAA NA MAWAKALA WA FORODHA MKOANI TANGA

$
0
0
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu kwa waagizaji wa bidhaa mbalimbali na wakala wa forodha katika mpaka wa Horohoro na bandari ya Tanga  juu ya utaratibu na mifumo ya ukaguzi wa bidhaa mbalimbali kabla hazijaingia nchini " Pre- shipment Verification of Conformity (PVoC)", ukaguzi wa bidhaa baada ya kuwasili nchini "Destination Inspection (DI)", uthibitishaji wa bidhaa na matakwa ya viwango.

Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa ofisi za Bandari na  washiriki 33 walihudhuria. Semina hii ilifunguliwa na Thobias Mwilapwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, ambaye alisisitiza washiriki kusikiliza kwa makini taratibu zinazotakiwa kufuatwa ili kuepuka gharama ya kupoteza muda na pesa, kwa kutokufuata taratibu au kuingiza bidhaa zilizochini ya kiwango.
 
Baadhi ya washiriki wakati wa majadiliano, waliomba TBS kuhakikisha majibu ya sampuli yanatoka kwa haraka ili kuepuka gharama za ziada ya kuhifadhi mizigo yao. Kwa upande wake Gladness Kaseka, Afisa Masoko Mwandamizi (TBS), aliwasisitiza washiriki kuwa na hulka ya kutuma malalamiko yao rasmi kwenye dawati la huduma kwa mteja, kupitia namba ya bure ambayo ni 0800110827, ili yaweza kushughulikiwa kuliko kubaki nayo na kusubiri mikutano au semina.

TBS imeendelea kutoa semina kama hizi kwa waagizaji bidhaa mbalimbali na mawakala wa forodha mkoani Mwanza na Dar es Salaam, na hivi karibuni itatolewa pia katika mkoa wa Arusha.
 Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa akifungua Semina kwa waagizaji wa bidhaa mbalimbali na mawakala wa forodha katika Bandari ya Tanga na Horohoro, katika ukumbi wa Bandari , Machi 20, 2019. Kushoto ni Bw. Cunbert Kapilima, Afisa Udhibiti Ubora Mkuu(TBS) na kulia ni   Bw. Faustine January, Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kaskazini (TBS).
Afisa viwango mwandamizi (TBS), Stephen Rwabunywenge akiwasilisha mada ya matakwa ya msingi wa viwango kwa waagizaji wa mizigo na mawakala wa forodha  katika bandari ya Tanga na Horohoro.
Afisa Udhibiti Ubora (TBS), Emmanuel Kiwango akiwasilisha mada juu ya utaratibu wa kufuatwa kwa mizigo inayoingizwa bila kukaguliwa inapotoka na kukaguliwa nchini " Destination Inspection" kwa waagizaji na mawakala wa forodha katika bandari ya Tanga na Horohoro.
 Waagizaji mizigo na mawakala wa forodha katika bandari ya Tanga na mpaka wa Hororo, wakiwa pamoja na watoa mada wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Thobias Mwilapwa(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi.
 Afisa Udhibiti Ubora (TBS), Bi. Janeth Kakuru akiwasilisha mada ya ukaguzi wa bidhaa katika nchi zinakotoka kabla hazijasafirishwa kuja hapa nchini (PVoC),kwa waagizaji na mawakala wa forodha mkoani Tanga

MWANAHABARI WA ITV AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAKOSA YA KUSHAMBULIA NA KUDHURU MWILI.

$
0
0
 Mwandishi wa kituo cha Habari cha ITV na Readio One Mkoani Kagera Bwn. Audax Mtiganzi amefikishwa katika mahakama ya mwanzo Wilayani  Bukoba mapema Machi 20, 2019, kwa kosa la kushambulia na kudhuru mwili. 

Akisomewa maelezo ya kosa,hakimu wa mahakama hiyo Owemilembe Ishabakaki amesema, mshitakiwa alitenda kosa hilo katika mtaa wa Kashenye (anapoishi) Januari 21,2019 saa tatu usiku.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 255/2019 Mtuhumiwa kwa kumpiga na kumdhuru  bila halali mlalamikaji Bwn. Phinias Bashaya Mwandishi Wa Habari Wa Mwananchi Communications Ltd, Mkoa Wa Kagera.

Baada ya kusomewa shitaka mlalamikaji alihoji kutokuwepo kwa shitaka la kuharibu mali,na madai ya mshitakiwa kuwa mlalamikaji alijaribu kumpa sumu na mahakama imeagiza hati ya mashitaka ibadilishwe.

Mtuhumiwa huyo yupo nje kwa dhamana, baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ambapo mdhamini amesaini bondi ya shilingi laki mbili na kesi itatajwa tena March 25 mwaka huu

SIMBA SC YAZOA MILIONI 50 SPORTPESA

$
0
0
Klabu ya Soka ya Simba yenye maskani yake Msimbazi jijini Dar es Salaam imepongezwa na Kampuni yakubashiri nchini ya SporPesa baada yakufanya vyema kwa kufuzu Robo Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika. 

Simba SC kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, imethibitisha kuwa SportPesa kutoa kiasi cha pesa cha 50,000,000/= kama pongezi baada yakutinga hatua ya Robo Fainali ya Michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa ngazi ya klabu.

Taarifa hiyo imesema: "Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa Sportpesa, Tarimba Abbas ameipongeza timu hiyo kutinga hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya CAF ambapo amethibitishwa kuwa Kampuni hiyo itakabidhi kiasi cha Tsh 50,000,000/= kama zawadi Kimkataba".

Simba SC  ilifuzu hatua hiyo baada yakuifunga AS Vita lub bao 2-1 kwenye dimba la Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, hata hivyo Mnyama atasubiri droo ya Robo Fainali ya Michuano hiyo itakayopangwa majira ya Saa 2 Usiku, nchini Misri kujua anakabitiana na nani katika Robo Fainali.

PANITA, ASASI ZA KIRAIA WAIOMBA SERIKALI KUENDELEA KUWEKA MIKAKATI KUBORESHA UPATIKANAJI WA LISHE BORA NCHINI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WADAU wa masuala ya lishe nchini zikiwemo asasi za kiraia nchini Tanzania wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli kwa kutambua lishe bora ni jambo muhimu katika kuboresha afya za wananchi huku wakitoa maombi na ku[endekeza mambo gani yafanyike kuhakikisha eneo la lishe linapewa kipaumbele.

Wameyasema hayo Machi 19,2019 wakati wa mkutano wa tathmini ya pili ya utekelezaji wa mkataba wa lishe.Mkutano huo ulifanyika ukumbi wa Kambarage Hazina katika Jiji la Dodoma.

Akizungumza kwa niaba ya Asasi za kiraia, Mkurugenzi Mtendaji wa PANITA Tumaini Mikindo ametumia nafasi hiyo kueleza kuna mambo muhimu katika kuboresha hali ya lishe nchini Tanzania.

Amefafanua Serikali ilitenga fedha katika bajeti kwa mwaka wa 2017/18 zipatazo Sh.bilioni 11 na mwaka 2018/19 zimetengwa kiasi cha Sh. bilioni 14 kwa ngazi za mikoa na wilaya kwa kigezo cha Sh.1000 kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano na kwamba hilo ni jambo jema na linapaswa kupongezwa.

Amesema utekelezaji wa bajeti hii unaonesha mambo kadhaa ambapo ameyataja ni sehemu kubwa ya bajeti hiyo ilitoka kwenye Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund) ikifuatiwa na ruzuku ya Serikali Kuu kwenda halmashauri na kwa kiwango kidogo toka kwenye mapato ya ndani ya halmashauri. 

Aidha mikoa ambayo inapata fedha za wafadhili au wadau wa maendeleo imekuwa haiweki fedha za vyanzo vya ndani katika bajeti za lishe au zikiweka basi ni kwa kiwango kidogo sana.

Pia wanaona bado utekelezaji wa matumizi ya fedha zilizotengwa, hasa zinazotoka vyanzo vya ndani vya halmashauri ni hafifu, na kwa baadhi ya halmashauri hazitoi fedha hizo kabisa.

"Hii inamaanisha nini? Kwa kipindi cha kati tutapata matokeo chanya kwa sababu fedha za wafadhili zipo. Lakini mafanikio haya hayatakuwa endelevu pindi miradi ya wafadhili itapomaliza muda wake. 

"Hivyo basi mwito wetu kwa serikali kuu ni kwamba kupitia halmashauli ijenge tabia ya kutenga na kutoa fedha kulingana na mipango waliyoipitisha.Aidha tunatambua kuwa vipaumbele ni vingi; lakini kwa hizo fedha kidogo zinapatika kutoka vyanzo vyetu vya ndani, basi kuwe na uwiano wa mgawanyo katika vipaumblele ikijumilisha kipaumbele cha lishe,"amesema. 

Amesema kuwa utaratibu huo utasaidia kuweka mfumo thabiti na endelevu katika kuboresha hali ya lishe ambao utajengeka juu ya msingi bora unaowekwa na fedha za wafadhili pindi miradi hiyo itakapokwisha.

"Vile vile matumizi ya hadidu za rejea za kamati za lishe za Mikoa na Halmashauri ni hafifu, hivyo kushindwa kufikia malengo ya NMNAP 2016/21. Hivyo ni mwito wetu kuwa Mikoa na Halmashauri zitilie mkazo matumizi ya hadidu hizo za kamati za lishe zinazolenga kuimarisha uratibu wa kazi za lishe katika ngazi za mikoa na halmashauri,"amesema.

Pia Mikindo amesema kuwepo na sera jumuishi ya kisekta ya lishe ni jambo muhimu, ili kuweka msingi bora zaidi wa kuratibu na kusimamia mukhtadha mzima wa kuboresha hali ya lishe kwa haraka ziadi. Aidha ametumia nafasi hiyo kueleza waamshukuru Makamu Rais Mama Samia Suluhu kwa kuwashirikisha katika mkutano huo adhimu cha kujadili utekelezaji wa mkataba wa lishe.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwamo mawaziri, wakuu wa mikoa, manaibu makatibu wakuu, wadau wa maendeleo wa kitaifa na kimataifa, watendaji wa Serikali kutoa Ofisi pamoja na TAMISEMI.

"Nitoe shukrani za dhati kwa niaba ya asasi za kiraia kwa Serikali wa kutualika katika mkutano huu; na si hivyo tu na pia kutupa fursa ya kutoa salamu katika hadhara hii. Hii ni uthibitisho tosha Serikali ya awamu ya tano inavyothamini na kutambua mchango wa wadau ikiwemo Asasi za Kiraia katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya taifa hili kuelekea uchumi wa kati kupitia viwanda ifikapo 2025."amesema.

Viewing all 110115 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>