Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live

MJADALA WA WANA -CCM WASIVAE SARE ZAO SHEREHE ZA UWASHAJI MWENGE KITAIFA WAIBUA MJADALA

$
0
0
MJADALA WA WANA -CCM WASIVAE SARE ZAO  SHEREHE ZA UWASHAJI MWENGE KITAIFA WAIBUA MJADALA KATIKA KIKAO CHA KAMATI YA MWENGE MKOA WA SONGWE,

Na Mashaka Mhando, Mbozi

KIKAO cha Kamati ya Mwenge mkoani hapa, umewapiga marufuku wana-CCM watakaohudhuria sherehe za kitaifa za uwashwaji wa Mwenge Kitaifa zitakazofanyika mjini hapa Aprili 2 mwaka huu, wasivae sare zao za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hoja hiyo iliwasilishwa na Mwenyekiti wa kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi na ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali Mstaafu Nicodemus Mwengela ambapo amedai sherehe hizo ni za kitaifa na watu wa CCM hawapaswi kuvaa sare hizo.

Kikao hicho kilichofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, baada ya Mkuu huyo kuwasilisha hoja katika agenda ya sare zitakazovaliwa kwenye uwashaji huo, aliungwa mkono na wajumbe waliohudhuria kikao hicho isipokuwa Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Kazimbaya Makwega.

Baada ya hoja kujadiliwa kwa kina na wajumbe, Mkuu wa mkoa aliomba mwongozo kwa Mratibu wa Mwenge wa mkoa wa Songwe Saida Mponjoli alieleza kwamba watu wote wanatakiwa wavae sare za kitenge kilichoandaliwa.

Kamanda wa polisi mkoani Songwe ACP George Kyando aliuliza kimasihara kwamba na wao pia wanalazimika kuvaa sare hizo mwenyekiti akamjibu wanatakiwa pia kuvaa.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Mbozi Makwega hakukubaliana na uwamuzi huo akieleza CCM ndiyo waliounda Serikali hivyo wana kila sababu ya kuvaa sare zao.

"Hii mwenyekiti si sawa sisi wengine tuvaeni sare, lakini wana-CCM tusiwapangie, mathalani amekuja mwenyekiti wao wa Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anaweza kutuacha sisi tuliovaa sare za Mwenge akaenda kuwasalimia ndugu zake waliovalia, tuwaache wavae sare zao," alisema Makwega.

Hata hivyo, akichangia mjadala huo Ofisa Usalama wa Mkoa Paulius Nansebwa ambaye vikao vingi vya mkoa amekuwa mchangiaji mzuri, alisema sherehe hizo ni za kitaifa na watu wa CCM wasivae sare zao ili kufanya uwashaji huo wa Mwenge usionekane wa kichama.

Katibu wa CCM mkoani Songwe Mercy Mollel alihamanika katika kikao hicho na akasema hawawezi kuchukua ushauri huo na badala yake watawahamasisha wanachama wao wavae sare za chama hicho.

"Mwenyekiti hatuwaelewi  hii hoja mmeileta hapa, sisi CCM tunajua faida na umuhimu wa Mwenge na hatuwezi kupangiwa tutawahamasisha wanachama wetu waje wakiwa wamevaa sare zao, kwanza vitenge vya Mwenge mlivyotoa sisi CCM hatuvikubali," alisema Mollel.

Hadi kikao kinamalizika saa 12:30 jioni uwamuzi wa mkoa uliopitishwa ni kwamba CCM wasije wakiwa wamevaa sare zao za chama.

Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu utawashwa mkoani hapa katika mji wa Mlowo uliopo katika halmashauri ya ya wilaya ya Mbozi Aprili 2 mwaka huu. 

Halmashauri ya Mbozi ina majimbo mawili ya uchaguzi ambapo jimbo la Vwawa mbunge wake ni Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga na jimbo la Mbozi ambalo mbunge wake ni Paschael Haonga wa Chadema.

Halmashauri hiyo ina kata 29 ambapo NCCR ilishinda kata 1 na Chadema ilishinda kata 10  ingawa mwishoni mwa mwaka ulioisha madiwani watatu wamerudi CCM na kufanya hadi sasa katika halmashauri hiyo wabaki wanane.

WAZIRI LUGOLA ATOA ONYO KALI KWA WANAOINGIZA WAHAMIAJI HARAMU NCHINI, AONGOZA KAMATI YA BUNGE KUKAGUA UJENZI MAKAO MAKUU UHAMIAJI DODOMA

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, wakati wajumbe hao walipotembelea eneo litakalojengwa Jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji, Jijini Dodoma, leo. Ujenzi wa jengo hilo ambao tayari umenza, unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 16. Katikati aliyevaa kofia ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Victor Mwambalaswa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   


Katibu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Ramadhan Abdallah, akitoa taarifa ya Kamati hiyo, katika kikao chao na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Kushoto meza kuu ni Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola. Katikati ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Victor Mwambalaswa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu (katikati), wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala, alipokuwa anawafafanulia jambo katika eneo la ujenzi wa Makao Makuu ya Idara hiyo, jijini Dodoma, leo.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, Jijini Dodoma, leo. Mara baada ya kikao hicho, wajumbe hao walitembelea eneo litakalojengwa Jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji, Jijini Dodoma. Ujenzi wa jengo hilo ambao tayari umenza, unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 16. Kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Victor Mwambalaswa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  


Madereva wa daladala jijini Mbeya watii agizo la serikali,warudi barabarani

ALIKOTOKA HUSSEIN JUMBE ‘MZEE WA KUCHECHEMEA’

$
0
0

Na Moshy Kiyungi,Dar es Salaam.

Mwanamuziki Hussein Jumbe anayo historia ndefu katika muziki hadi kuweza kumiliki bendi yake.

Wanamuziki wengi hapa nchini wamepitia mitihani mingi, ikiwemo ya taabu, mashaka na vikwazo kemkemu hadi kuyafika mafanikio.

Hapa uvumulivu wa mtu binafsi unachukua nafasi kubwa ya kuyafikia mafanikio hayo wala siyo kukata tamaa.Husseni Suleiman Jumbe 'Mzee wa Dodo' kama anavyojulikana kwa wengi, ni mifano unaoweza kuyakinisha hayo.

Ni mwanamuziki nguli aliyejaaliwa vipaji adhimu vya sauti ya uimbaji, utunzi uliojaa hisia na zinazosisimua zaidi, ambazo mara nyingi hugusa kila rika la watu.Jumbe alipata elimu yake ya msingi katika Shule za Uhuru Mchanganyiko na Sekondari ya Muslim, zote za Dar es Salaam.
‘Mzee wa Dodo’ aliwahi kutamka kuwa aliamua kujifunza muziki baada ya kuvutiwa na nyimbo za marehemu Marijani Rajab 'Jabali la muziki'."Nilikuwa natembea na radio yangu kwa ajili ya kusikiliza nyimbo za Marijani, enzi hizo akiwa na bendi ya Safari Trippers,” Jumbe alisema.

Vibao vya Marijani Rajab vilivyokuwa vikimpagawisha zaidi ni 'Roza nenda shule', 'Mwalimu Nyerere' na 'Nani mchokozi'.Hussein alisema kwamba kabla nyimbo hizo hazijatoka kwenye redio, alizijua na kwamba alikuwa akiziimba kila alipokwa ameketi, wakati huo ndio kwanza alikuwa bado yuko shule ya msingi.

Jumbe anakumbuka zaidi kuwa kutokana na mapenzi yake kwa Marijani, mara kwa mara alikuwa anatembelea maonyesho yake na kila Jumapili.
Alikuwa hakosi kwenda katika ukumbi uliokuwa ukijulikana kama Princess uliokuwa maeneo ya Mnazi Mmoja kwenye 'bugi dansi' dansi la mchana siku za Jumapili lililoisha saa kumi na mbili jioni, ambapo kiingilio chake kilikuwa shilingi tano tu.

Mnamo mwaka 1979, wakati akiwa darasa la nne, alijiunga kwa siri na kundi la Orchestra Siza, ambalo maskani yake yalikuwa Mtaa Ruvuma, Temeke, jijini Dar es Salaam ambako pia ndiko alikokuwa akiishi yeye.Katika kundi hilo Jumbe alisema kuwa ndiko kwa mara ya kwanza alikokutana na mwanamuziki Roshi Mselela.Roshi alikuwa mtunzi na mwimbaji katika bendi ya Super Matimila, aliyemuelezea kuwa walikuwa wakipatana kupita kiasi, akawa bado anaendelea na muziki kwa siri.

Waswahili wanasema “Siri haitambi mkono wa pili”, mwaka mmoja tu baadae wazazi wake wakagundua ‘janja’ yake ya kujiingiza katika muziki, na kuzembea masomo shuleni, wakamgombeza na kumpiga marufuku kufanya muziki. Hata hivyo, mwenyewe Jumbe anakiri kwamba kuishi bila kujihusisha na masuala ya muziki ilikuwa ngumu kwake.

Mwaka 1981 akajiunga tena kwa siri na kundi lingine la muziki wa dansi la Asilia Jazz, ambalo lilikuwa likimilikiwa na Baraza la Muziki Tanzania (BAMUTA)."Safari hii, baba alipokuja kugundua kuwa naendelea kujishughulisha na muziki, alinichukua na kunipeleka kufanyakazi katika kiwanda cha Plastiki," anasimulia Jumbe na kufafanua kuwa hapo aliajiliwa kama msimamizi wa uzalishaji (Production Foremen).

Huku akicheka, Jumbe akasema kuwa aliacha kazi kiwandani hapo, baada ya kuona anakosa muda wa kwenda kwenye mazoezi ya muziki. Matokeo yake familia yao yote ilimtenga na kumsusa kabisa."Nakumbuka katika kipindi hicho nilichosuswa na familia, nilitaabika kwa dhiki mpaka nilifikia hatua ya kuvaa nguo zenye viraka," anasema Jumbe. 

Alisema kuwa, katika jitihada zake za kuhakikisha hautupi mkono muziki, mwaka 1983 alilikimbia jiji la Dar es Salaam na kwenda Tabora kutafuta bendi atakayoitumikia kwa kujinafasi.Huko akapokewa na mkongwe Shem Karenga ndani ya bendi ya Tabora Jazz, ambako pia alikutana na mwimbaji Mohammed Gotagota ambaye kwa sasa ni marehemu.Aliitumikia bendi ya Tabora Jazz kwa miaka miwili, akachomoka akaenda katika mji wa Musoma, mkoani Mara.

Huko alikaa mwaka mmoja tu wa 1985 na ilipofika 1986 aliamua kurejea Dar es salaam baada ya kupokea taarifa ya msiba wa baba yake mzazi."Nilipowasili, nilikuta tayari baba amekwishazikwa," anaongea kwa huzuni kubwa Jumbe.Alisema kuwa baada ya hapo hakuona haja ya kuwa mbali na familia hivyo alimfuata Hamis Gotagota, aliyekuwa bendi ya Urafiki wakati huo.

Gotagota akamuunganisha kwa uongozi wa bendi hiyo, akakubali kuwa mwimbaji wa bendi hiyo.Bendi ya Urafiki Jazz 'Wana Chakachua' wakati huo ilikuwa ikiongozwa na Juma Mrisho 'Ngulimba wa Ngulimba', ndipo Jumbe alipoanza kudhihirisha makali yake katika utunzi na uimbaji, kwani aliporomosha kibao kizito kilichokwenda kwa jina la “Usia wa Mama”. 

Oktoba 17, 1987 aliitwa na mtu asiyemfahamu ambaye alimueleza kuwa amependezwa na uimbaji wake, hivyo siku hiyohiyo aende makao makuu ya Mlimani Park yaliyoko karibu na Chuo Kikuu Dar es Salaam.

Yule mtu alikuja kumtambua baadae kuwa kumbe alikuwa Hassan Rehani Bichuka 'Super Stereo'.“Wimbo wangu ya kwanza kabisa kutunga nikiwa na Wana Mlimani Park ni ule usemao 'Hisia za mwanadamu'.

Mwaka 1990 bendi ya Mlimani Park Orchestr ilishiriki mashindano ya nyimbo kumi bora, wimbo wake huo ukushika nafasi ya tatu. Nafasi ya kwanza ilinyakuliwa na bendi ya MK Group 'Ngoma za Magorofani’ na ya pili ikatwaliwa na Salna Brothers.Alidumu Mlimani Park kwa muda mrefu na kushiriki kuimba na kutunga vibao vingi vikali ambavyo baadhi yake ni ‘Epuka No2’, ‘Nuru ya Upendo’, ‘Shamba’, ‘Mtoto wa Mitaani’, ‘Chozi la Kejeli’, ‘Nachechemea’ na ‘Isaya Mrithi Wangu’ ambazo kila moja kwa wakati wake ilitikisa vilivyo. 

Mwaka 2002, aliondoka DDC na kujiunga na TOT Plus 'Achimenengule', ambapo kama kawaida yake, akiwa na kundi hilo lililokuwa chini ya Mbunge wa Mbinga Magharibi, Capt John Damian Komba, Jumbe aliporomosha vibao viwili moto wa kuotea mbali.Vibao hivyo ni 'Gunia la mazoezi' na 'Nani Kaiona kesho', ambavyo vyote viko katika albamu moja ya ‘Sarafina’ iliyofyatuliwa mwaka huohuo 2002, ambayo ilikuwa na jumla ya nyimbo sita.

Jumbe alidumu TOT kwa miaka miwili, akatoka na kwenda kujaribu upepo katika bendi ya Msondo Ngoma Music. Huko alikutana na wakongwe we dansi kama vile Muhiddin Gurumo, Suleiman Mbwembwe, Joseoh Maina, Athuman Momba na Tx Moshi William, wote ni marehemu.Akiwa na Msondo, Jumbe alifanya vitu vizito kwenye albamu iitwayo ‘Ajali’ aliposhiriki kuimba kwa takriban nyimbo zote akitumia ufundi wa njia ndogo ya sauti ujulikanao kitaalamu kama 'Minor' na kutunga vibao 'Transfer' na 'Sumu ya Ufukara'.

Tofauti na wanamuziki wengine wengi wanapohama bendi hukashifu alikotoka.Jumbe yupo tofauti kabisa kwa kuwa hadi leo anaisifu Msondo kwa kusema kuwa ni bendi ambayo wanamuziki wake hawana majungu, fitina wala nyoyo za chikichiki. 

"Msondo wenzetu wanapendana halafu lao moja, hawana majungu hata kidogo," anasema Jumbe anapoulizwa kuhusu bendi hiyo inayotumia mtindo wa 'Mambo Hadharani'. 

Hivi sasa, Jumbe ambaye ni baba wa familia mwenye watoto wanane na mkewe Zakhia Jumbe, anayekiri kuwa maendeleo katika muziki ni 'matokeo'. Juhudi zake binafsi ameweza kupata mafanikio makubwa hasa baada ya kuanzisha bendi yake.

Jumbe alisema kuwa tayari anamiliki bendi yake ya Talent, yenye albamu tatu, ambazo ni ‘Kwangu ni Wapi’, ‘Subiri Kidogo’ na ‘Kiapo Mara Tatu’.

Hussein Jumbe alisema hivi sasa wapo jikoni wanapika albamu nyingine itakayokusanya vibao vikali kama ‘Nyumba ya Urithi’, ‘Kaolewa Ramadhani Kaachika

Ramadhani’ na ‘Ukienda Kuomba Mboga’. 

Ndani ya vibao vyote kwenye albamu zilizotangulia za Talent Band, Jumbe ameonyesha ukomavu mkubwa kisanii kuanzia ujumbe hadi ala, kumemfanya afanikiwe kupata maendeleo makubwa zaidi ya alipokuwa mwajiriwa.

Hii ndiyo safari yake Hussein Jumbe katika muziki.



Kutana na Nuru Awadh mlemavu wa macho aliyetikisa tuzo za I CAN za Taasisi ya Dkt. Reginald Mengi

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AKEMEA VITENDO VYA UVUNJIFU WA SHERIA ZINAZOFANYWA NA BAADHI YA WANACHAMA WA CUF

TANZANIA YATOA MSAADA WA CHAKULA, DAWA NCHI ZA MALAWI, MSUMBIJI, ZIMBAMBWE ZILIZOKUMBWA NA MAFURIKO

IDARA YA UHAMIAJI MKOA WA KILIMANJARO IMEMFUKUZA RAIA WA KENYA ALIYEISHI NCHINI MIAKA 20 KINYUME NA SHERIA

$
0
0

Na Woinde Shizza-Globu ya jamii

IDARA ya uhamiaji mkoani Kilimanjaro imemfukuza nchini raia wa Kenya Magdalena Wavinya (43)ambaye ni Mkazi wa kijiji cha Ghona katika kata ya Kahe Mashariki wilayani Moshi Vijijini ,mkoani humo kwa kosa la kuishi nchini kwa zaidi ya miaka 20 kinyume cha sheria.

Aidha inamshikilia mumewe ,Steven Mrutu(45)kwa madai ya kuwa na mashaka na uraia wake, pamoja na Ofisa Mtendaji wa kijiji cha Mikameni wilayani humo Panaska Issa Manyi anayedaiwa kuishi na mwanamke ,Lyidia Nakiete raia wa Kenya ambaye alitoroka muda mfupi wakati maofisa wa uhamiaji wakimfuatilia kwa ajili ya vibali vya makazi.

Akizungumza leo Machi 19,2019 na ofisini kwake Ofisa Uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro Albert Rwelamira alisema idara hiyo imelazimika kumfutia kibali cha muda anachotumia mkazi huyo na kumpatia saa 24 awe ameondoka nchini tangu Machi 15,mwaka huu

"Tumelazimika kumfukuza nchini Magdalena kwa sababu kubwa mbili yakwanza amekuwa akiishi nchini kwa zaidi ya miaka 20 bila kuwa na kibali , tangu mwaka 2017 kwa maana amekuwa akikata paspoti ya miezi mitatu na pindi muda wake unapomalizika hurejea nchini Kenya na kukata nyingine ya muda huo na kurudi hapa nchini, ’’amesema

Aliongeza sababu nyingine ni kuidanganya idara hiyo kuwa ana cheti cha ndoa aliyofunga na mumewe, Steven Mrutu mwaka 2003 ,katika Kanisa Katoliki lililopo Himo mkoani humo, lakini idara hiyo ilifuatilia na kubaini kwamba hakuna jina hilo katika orodha ya watu waliofungwa ndoa kanisani hapo.

Pia alifafanua kushikiliwa kwa Mrutu ni kutokana na uraia wake kuwa na mashaka kwani mwaka 2017 alikamatwa na kutakiwa kuleta vielelezo vya uraia wake lakini hakuwahi kufanya hivyo,ila idara hiyo ilifuatilia mahala alipodai alisoma ikiwemo shule ya msingi kisimani aliyosoma mwaka 1986 ambapo uongozi wa shule hiyo ulitoa orodha ya wanafunzi waliotahiniwa mwaka huo jina lake halikuwepo.

Akizungumzia kadhia hiyo,Magdalena alilalamikia hatua ya kufukuzwa nchini kwani ameishi kwa zaidi ya miaka 20 na kufanikiwa kuzaa watoto watano wanaosoma katika shule mbalimbali nchini,hivyo kitendo cha kumfukuza na kuendelea kumshikilia mumewe ni kuwafanya watoto wake waishi maisha ya taabu na kuiomba serikali ya Tanzania imwonee huruma kwani maisha yake yote amewekeza hapa nchini.

Awali baba mzazi wa Mrutu,Awadhi Mrutu alidai kuwa Mkazi wa Makuyuni  wilaya ya Moshi vijijini,alisema wakati akifanya kazi za udereva wa malori makubwa kwenye nchi jirani na mikoani alibahatika kukutana na mama yake aitwaye Amina Rashird na kubahatika kupata ujauzito ambapo mwaka 1975 alijifungua mtoto huyo aitwaje Stivini .

Mzee huyo mwenye watoto nane aliowazaa nje ya ndoa ameilalamikia idara hiyo kwa kumtuhumu na kumkamata mara kwa mara mwanaye kwa madai kwamba si raia wa Tanzania jambo alilosema ni uonevu mkubwa kwani yeye kama baba mzazi bado yupo hai na kama wanahitaji vielelezo vyovyote ikiwemo kupima vina saba wamfuate yeye na yupo tayari muda wowote.

Ameitaka idara hiyo ya uhamiaji kumpeleke mahakamani mwanaye na kuacha kumkamata na kumshikilia kituo cha polisi huku wakimnyima dhamana kwa kuwa ni kinyume cha sheria.

 Afisa uhamiaji Wa Mkoa Wa Kilimanjaro Albert Rwelamira akizungumza na na waandishi Wa habari (Picha na Woinde Shizza globu ya jamii Arusha)

MAJALIWA AKABIDHI MATREKTA KWA WENYEVITI WA VYAMA VYA USHIRIKA VYA MSINGI MWANZA

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi ufunguo wa trekta aina Ursus, Mwenyekitiu wa Chama cha Msingi cha Mgundama, Bibi Getrude John katika hafla fupi ya kukabidhi matrekta 16 yenge hamani ya shiliüngi bilioni 1.8 kwa Vyama vya Ushirika vya Msingi iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwenye mtaa wa Posta jijini Mwanza, Machi 19, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi ufunguo wa trekta aina ya Ursus, Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Busisi wilayani Sengerema, Bibi  Amina Makone katika hafla fupi ya kukabidhi matrekta 16 yenge hamani ya shiliüngi bilioni 1.8 kwa Vyama vya Ushirika vya Msingi iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwenye mtaa wa Posta jijini Mwanza, Machi 19, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasha trekta aina ya Ursus  wakati alipokabidhi matrekta16 yenye thamni ya shillings bilioni 1.8  kwa wenyeviti wa baadhi ya  Vyama vya Ushirika via Msingi mkoani Mwanza    katika hafla fupi iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwenye mtaa wa Posta jijini Mwanza, Machi 19, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi ufunguo wa trekta aina ya Ursus, Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Ugata wilayani Magu, Bw. Enock Ng'ombe katika hafla fupi ya kukabidhi matrekta 16 yenge hamani ya shiliüngi bilioni 1.8  kwa Vyama vya Ushirika vya  Msingi iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo la Taifa  (NDC) kwenye mtaa wa Posta jijini Mwanza, Machi  19, 2019. 

Article 3

VIJIJI SITA WILAYA YA MEATU VYANUFAIKA NA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0

Vijana wa kikundi cha Nyati katika Kijiji cha Mwabulutago Kata ya Mwasengela wakikabidhiwa mashine ya kuchomelea itakayochangia uchumi wa jamii yao.
Wanakikundi cha uzalishaji mali Kijiji cha Makao wakikabidhiwa moja na Mkuu wa wilaya ya Meatu,Dk Joseph Chilongani.
Wanawake walionufaika kwa kujengewa uwezo wa kuweka na kukopa wakimpa zawadi Meneja wa Maendeleo ya Jamii wa kampuni ya FCFL,Nana Woodley.
Mkuu wa wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu,Dk Joseph Chilongani akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali kwa wananchi wake,kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Meatu,Juma Mwiburi na Meneja wa FCFL,Nana Woodley.
Mkuu wa wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu,Dk Joseph Chilongani(wa pili kushoto) akimsikiliza mkulima wa Kijiji cha Matale Kata ya Tindabuligi,Sayi Luchagula alipotembelea shamba lake lililowekewa uzio wa mizinga ya nyuki ili kuwazuia Tembo kushambulia mazao yao.
Mkuu wa wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu,Dk Joseph Chilongani(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Friedkin Conservation Fund Limited pamoja na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Meatu.


Vijiji Sita vinavyozunguka Pori la Akiba la Maswa na Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori ya Makao wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu vimenufaika kwa kuwezeshwa elimu ya kuweka na kukopa pamoja na ufugaji wa nyuki kwaajili ya kujikwamua kiuchumi.

Mkuu wa wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu,Dk Joseph Chilongani akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya kuwawezesha wananchi kiuchumi viliyotolewa na kampuni ya Utalii ya Friedkin Conservation Fund(FCF) vyenye thamani ya Sh 55 milioni aliwataka wananchi kuvitumia kujiletea maendeleo.

Alisema utaratibu uliofanywa na kampuni hiyo kuwapa elimu ya ujasirimali na kutoa nyenzo mbalimbali za kufanyia kazi zikiwemo mizinga ya nyuki,mashine za kuchomelea na vifaa vya kusindika asali utasaidia kuwapa wananchi fursa za kutumia mazingira yanayowazunguka kujiongezea kipato.

“Napenda kuwashukuru wadau wetu wa maendeleo kwa mchango mnaoutoa katika kusaidia jamii hii najua sio mara ya kwanza na mtaendelea kufanya hivyo kwasababu wananchi wetu wanaohutaji wa aina mbalimbali lakini wanashindwa namna ya kuanza ,”alisema Chilongani

Vijana Magese Donald na Koyo Ndimila kikundi cha Nyati katika kijiji cha Mwamhongo Kata ya Mwasengela waliopewa mashine ya kuchomelea yenye thamani ya Sh 6 milioni walisema itawasaidia kuongeza kipato na kupunguza ukataji miti kwaajili ya kutengeneza vifaa mbalimbali.

Ndimila alisema ujuzi walionao wa kutengeneza madirisha,milango na vitanda vya chuma utapunguza ukataji wa misitu ambao unaathiri vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla hivyo utatoa fursa kwao kujikwamua kiuchumi.

Afisa Maendeleo ya Jamii ya kampuni ya FCF,Alfred Mwakivike alisema vijiji zaidi ya 20 vinavyopakana na Pori la Akiba la Maswa pamoja na Hifadhi ya Jamii ya Makao mashamba ya wakulima yamekua yakivamiwa na wanyamapori wakubwa na kuwasababishia hasara.

Alisema wametoa mizinga 53 ya nyuki na kuweka uzio kwa mkulima Sailu Chagula kwenye shamba lake hatua iliyozuia wanyamapori wakubwa hasa Tembo kuacha kuvamia shamba hilo na mashamba yaliyo jirani.

“Tunapenda wakulima waendelee na shughuli zao na kupata tija bila kuwaona wanyamapori kama kikwazo kwao kwasababu wanao mchango muhimu katika kukuza pato la taifa,tumewapa mbinu ya kutumia mizinga ya nyuki kuwazuia Tembo kuvamia mashamba yao na wameipokea vizuri,”alisema Mwakivike

Vijiji vilivyonufaika na miradi ya maendeleo ni Matale,Sapa,Makao, Mwamhongo ,Mwabutulago na Mbushi ambavyo vimenufaika kwa kupewa mizinga ya nyuki,miradi ya elimu,Ujasiriamali na miradi ya maji.

AGAPE YAKUTANA NA VIONGOZI WA JAMII USANDA KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI ZINAZOKANDAMIZA WATOTO

$
0
0


Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Elizabeth Mweyo akizungumza katika kikao cha Viongozi wa Jamii kata ya Usanda.


Shirika la Agape AIDS Control Program la Mkoani Shinyanga limekutana na viongozi wa jamii katika kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya kutambua na kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia ukatili dhidi ya wanawake na watoto ili kupunguza mimba na ndoa za utotoni na maambukizi ya VVU na UKIMWI.

Kikao hicho cha siku moja kimefanyika leo Jumanne Machi 19,2019 katika shule ya msingi Shingida iliyopo katika kata ya Usanda na kukutanisha pamoja wenyeviti wa vitongoji 30 vya kata hiyo,viongozi wa kimila,dini,watu wenye ulemavu na vijana. 

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape, Lucy Maganga alisema viongozi wa jamii wanayo nafasi kubwa ya kuielimisha jamii kuachana na mila na desturi kandamizi ambazo zimekuwa zikichangia mimba na ndoa za utotoni. 

“Mila na desturi kandamizi zinachangia kwa kiasi kikubwa ukatili lakini pia maambukizi ya VVU na UKIMWI,ni jukumu letu sote kushirikiana kupiga vita mila na desturi hizi ili jamii yetu iwe salama”,alieleza. 

“Tuwaambie wananchi waache kufanya vitendo vya ukatili,mfano ukimnyanyasa mama nyumbani ni sawa na kwamba umenyanyasa familia nzima,mama atawaambia pia watoto jinsi anavyotendewa ukatili matokeo yake chuki inatawala katika familia”,aliongeza Maganga. 

Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Elizabeth Mweyo aliwataka wazazi na walezi kupeleka watoto shule badala ya kuwapa kazi ya kulinda ‘kuswaga’ mifugo na kuwaozesha wakiwa na umri chini ya miaka 18. 

“Lazima tuwalinde watoto wetu, pelekeni watoto shule, Kuswaga ng’ombe siyo kazi ya mtoto,jitahidini pia kuzungumza na kucheza na watoto wenu na kuwaeleza mambo mazuri na mabaya ambayo hawapaswi kuyafanya”,alisema Mweyo. 

Aidha aliwashauri akina mama kujiunga katika vikundi vya ujasirimali ili kuimarisha uchumi wa kaya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA). 

Nao wajumbe wa kikao hicho walizitaja baadhi ya mila na desturi zilizopitwa na wakati zinazoendelea kuwepo katika eneo hilo kuwa ni kurithi wajane,kutopeleka watoto shule, kuozesha watoto,kugawa mali kwa watoto wa kiume tu baba anapofariki na mwanawake kutorithi mali mme anapofariki dunia. 
Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape, Lucy Maganga akizungumza katika kikao cha Viongozi wa Jamii katika kata ya Usanda Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali kuhusu mila na desturi kandamizi zinachongia mimba na ndoa za utotoni sambamba na maambukizi ya VVU na UKIMWI - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape, Lucy Maganga akiwasihi wajumbe wa kikao hicho kushirikiana katika kupiga vita mila na desturi kandamizi katika jamii.
Wajumbe wa kikao hicho wakimsikiliza Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape, Lucy Maganga.
Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Elizabeth Mweyo akiwasilisha mada kuhusu Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) na kuwataka wajumbe wa kikao cha Viongozi wa jamii kuwa tayari kushirikiana na viongozi wa serikali na wadau mbalimbali kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni.
Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Elizabeth Mweyo akiwataka wanaume kubadilika na kuacha kuozesha watoto chini ya umri wa miaka 18 na wawapeleke shule badala ya kuwapa kazi ya kuswaga mifugo.
Wajumbe wa kikao hicho wakimsikiliza Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Elizabeth Mweyo (kushoto).
Mratibu wa Mradi wa Afya ya Uzazi na Ujinsia - Save The Children Sweden unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Sida la nchini Sweden,John Maliyapamba Komba akiwasihi viongozi wa jamii kushirikiana na shirika la Agape na serikali ili kutokomeza mila na desturi kandamizi katika jamii.
Afisa Ustawi wa Jamii kata ya Usanda,Halima Tendeja akizungumza katika kikao hicho.
Shimba Bundala akichangia hoja wakati wa kikao hicho kuhusu mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni.
Kijana Helen Mwita akieleza kuhusu mila na desturi zilizopitwa na wakati katika jamii. 
Mwanasheria wa Agape,Emmanuel Nyalada akiwasilisha mada kuhusu sheria zinazomlinda mtoto.
Paul Nkarangi akichangia hoja kuhusu suala la malezi ya watoto katika jamii.
Mzee wa mila, Shija Jimisha akichangia hoja kuhusu malezi ya vijana katika jamii.
Ashura Shija akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Shija Malundi akichangia hoja wakati wa kikao hicho. 


Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

RC MAKONDA ATIMIZA AHADI YA KUGHARAMIA MATIBABU YA PASCAL CASSIAN, AMKABIDHI TIKETI YA NDEGE NA PESA YA MALAZI KWA MUDA WOTE AKIWA INDIA.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametimiza ahadi ya kusaidia gharama za matibabu ya mshindi wa BSS 2009 Pascal Cassian kwa kumkabidhi Tiketi ya Ndege,Pesa ya Nauli, Chakula,Hotel na Pesa ya kujikimu kwa watu wote watatu watakaomsindikiza akiwemo Mke wake na Mkuu wa kitengo cha Urolojia Hospital ya Taifa Muhimbili.

RC Makonda amesema uamuzi wa kumpeleka Nchini India ni baada ya Jopo la madaktari bingwa wa Muhimbili kuridhia na kumtafutia Hospital ya kimataifa nchini India yenye uwezo wa kutibu tatizo hilo. 

Aidha RC Makonda amewashukuru watanzania wote waliochangia na kufanikisha safari hiyo na kuwaomba wazidi kuwa na moyo huohuo wa kusaidiana kwenye matatizo.

Kwa upande wake Pascal Cassian amemshukuru RC Makonda kwa kuona maumivu aliyokuwa akiyapata na kuamua kumsaidia ambapo ameeleza kuwa anaamini atarejea nchini akiwa amepona kwa uweza wa Mungu.

Itakumbukwa RC Makonda aliamua kumsaidi Pascal kwa kumtoa Nyumbani na kumpeleka hospital baada ya kuona kupitia mitandao ya kijamii maumivu aliyokuwa akiyapata baada ya kupata ajali iliyopelekea tatizo kubwa la kwenye mfumo wa figo.

MKUU WA CHUO DUCE AFUNGUA BONANZA LA MAZOEZI KWA WAFANYAKAZI WA CHUO HICHO.

$
0
0

Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha elimu DUCE Chang'ombe jijini Dar es salaam Profesa Bernadeta Killian akipiga mpira wa penati kuashiria ufunguzi wa bonanza la mazoezi ya wafanyakazi wa chuo hicho jana kwenye viwanja vya chuo hicho jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha elimu DUCE Chang'ombe jijini Dar es salaam Profesa Bernadeta Killian akizungumza na wafanyakazi wa chuo hicho wakati akifungua bonanza la mazoezi na michezo kwa wafanyakazi lililofanyika jana chuoni hapo jana jijini Dar es salaam na kushirikisha michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa Miguu, Pete, Bao na Drafti.

Lengo la Bonanza hilo la mazoezi ni kuwafanya wafanyakazi kujiweka sawa kwa afya ya miili yao ili kuwa tayari kutumikia chuo hicho kwa wakiwa na afya na miili iliyo yimamu kabisa kiafya.
Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bonanza Dk. Julius Mgunai, Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu DUCE Chang'ombe , Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishirki cha Elimu DUCE Taaluma Dk. Julius Mbuna na Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu DUCE Fedha Dk. Method Samwel wakielekea mahali ambapo bonanza hilo lilizinduliwa kwa kupigwa mpira wa penati na Mkuu wa Chuo hicho Profesa Bernadeta Killian.
Naibu Mkuu wa Chuo Fedha Dk. Method Samwel akiwa ameanguka chini baada ya kushindwa kudaka penati iliyopigwa na Mkuu wa Chuo hicho Profesa Bernadeta Killian wakati wa uzinduzi wa bonanza la mazoezi chuoni hapo jana.
Vikosi vya timu zilizoshiriki katika bonanza hilo vikiwa katika picha ya pamoja.
Vikosi vya timu za mpira wa pete vikiwa katika picha ya pamoja.
Wachezaji wa mpira wa miguu wakichuana vikali wakati wa mchezo wa mpira wa miguu.
Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha elimu DUCE Chang'ombe jijini Dar es salaam Profesa Bernadeta Killian akifurahia jambo kabla ya kupiga mpira wa penati wakati wa uzinduzi wa bonanza hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wakifurahia mara baada ya hotuba fuoi ya mkuu wa chuo hicho Profesa Bernadeta Killian.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 19.03.2019


MAGAZETI YA LEO JUMATANO MACHI 20, 2019

INNOVATION WEEK 2019

DC ARUMERU AANZA MKAKATI MAALUM WA KUKUZA UTALII HIFADHI YA WANYAMA ARUSHA

$
0
0

UTALII WETU ARUMERU 

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro ameanzisha mkakati Maalum wa kukuza utalii katika Hifadhi ya wanyama ya Arusha iliyoko wilaya ya Arumeru kwa kuvitumia Vyuo vikuu na taasisi za Elimu ya Juu , Shule za sekondari binafsi na za Umma pamoja na shule za msingi na za awali zilizoko katika wilaya ya Arumeru .

Dc Muro amebuni mkakati huo ikiwa ni mwendelezo wa kampeni yake ya kuhamasisha utalii wa ndani katika wilaya ya Arumeru ambapo safari hii ametoa maelekezo kwa wamiliki , viongozi , wakuu wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu pamoja na wakuu wa shule kuweka utaratibu utakaowawezesha wanafunzi na jumuiya za watu walio kwenye taasisi zao kutembelea hifadhi ya Wanyama Arusha.

Aidha kwa kuanzia mara mbili kwa mwaka, ambapo katika zoezi la mwanzo Dc Muro amewaongoza wanafunzi , walimu na wanajumuiya ya Shule ya Haradali Winners kutembelea hifadhi ya wanyama ya Arusha ambapo miongoni mwao ni wanafunzi walioapata alama ya ufaulu ya daraja la kwanza (division one ) kutoka kila darasa na mikondo ya shule hiyo kwa gharama za Dc Muro, ambapo mwezi ujao atapeleka kundi lingine la wananfunzi wa shule ya sekondari ya Ilboru iliyoko Halmashauri ya Arusha wilaya ya Arumeru .
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro akiwa na baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Haradali Winners ambao emeongozana nao kutembelea hifadhi ya wanyama ya Arusha,wakisoma maelezo kwenye vitabu vya utalii kuhusu hifadhi hiyo




KAMATI YA BUNGE YA UWEKEZAJI MITAJI YA UMMA KUIOMBA SERIKALI KUCHUKUA MADENI YA TANESCO

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, imeridhishwa na mabadiliko makubwa ya kiutendaji ndani ya Shirika la Umeme Nchini TANESCO, ambapo ndani ya kipindi kifupi limeondokana na utegemezi wa ruzuku ya serikali na sasa linajiendesha lenyewe. 
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Raphael M. Chegeni wakati wa hitimisho la ziara ya Kamati kwenye mradi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme utokanao na gesi asilia, Kinyerezi 1 (Kinyerezi I Extension) jijini Dar es Salaam, leo Machi 18, 2019.
“TANESCO ni Shirika ambalo limekumbwa na changamoto nyingi miaka ya nyuma, lakini tumefurahi kuona kwamba baadhi ya mambo yaliyokuwa mazito sana mmefanikiwa kuyatatua na hii ni dalili njema ni nzuri sana kwa sababu sasa hata serikali yetu ya awamu ya tano toka imeingia madarakani, TANESCO badala ya kuwa mtegemezi mkuu wa ruzuku ya serikali, hivi sasa Shirika halitegemei tena ruzuku ya serikali hili ni jambo jema sana.” Alisema.
Mmetoka kwenye ruzuku na sasa mnakua mnajitegemea haya ni mafanikio endeleeni kupunguza gharama, na mpanue wigo wa watumiaji wa umeme, watanzania wanahitaji umeme wenye gharama nafuu na haya ndio malengo ya serikali ya awamu ya tano, alisema Dkt. Chegeni na kuongeza
Mpango wa Serikali wa kujenga umeme wa maji kule Rufiji ni mpango sahihi kabisa na watanzania wote wazalendo lazima tuunge mkono juhudi hizo kwa sababu tunahitaji umeme ambao ni wa gharama ya chini ili  umeme umfikie kila mtanzania kwa gharama nafuu.
Aidha Mwenyekiti huyo ameahidi kuwa Kamati yake itaiomba serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina iangalie namna gani madeni yanayoikabili TANESCO kwa miaka mingi yanaondolewa ili iweze kujiendesha kikamilifu na kwa ufanisi zaidi.
“Madeni ambayo TANESCO inadaiwa huko nyuma Serikali iyabebe.” Alisisitiza.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO, Mhandisi Dkt. Alexander Kyaruzi ameiambia Kamati hiyo kuwa Kituo cha kuzalisha umeme wa gesi asilia cha Kinyerezi I kina uwezo wa kutoa Megawati 150 kwa sasa na upanuzi  unaoendelea hivi sasa utaongeza Megawati 185 na hivyo mradi utakapokamilika mwezi Agosti mwaka huu wa 2019, Kinyerezi I na I Extension itakuwa na jumla ya Megawati 335, huku Kinyeerzi II ambayo imekamilika ina uwezo wa kuzalisha Megawati 240 za umeme.
“Kinyerezi itakuwa complex kubwa sana ya kuzalisha umeme, tutaendelea na ujenzi wa Kinyerezi III na Kinyerezi IV.” Alifafanua.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka alisema Shirika limejiwekea mikakati endelevu ili kuhakikisha linaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ambapo baada ya kudhibiti deni ambalo Shirika limekuwa likidaiwa kwa muda mrefu, sasa wameanza kuwalipa wadai wa Shirika sambamba na kuondokana na kutegemea ruzuku ya kutoka serikalini.
"Kwa takriban miezi minane iliyopita deni ambalo TANSECO tumekuwa tukidaiwa limepungua kwa asilimia 3 naweza kusema limedhibitiwa." Alisema na kuomba sasa ni vema kama Serikali ingelichukua hilo deni au kututafutia mkopo ili tulimalize deni hilo kwani hii itapunguza uwezekano wa kuongezeka kutokana na interest maana tunashindana na deni lenyewe." Alifafanua Dkt. Mwinuka.
Alisema Kwa mwaka TANESCO ilikuwa ikipatiwa ruzuku ya serikali kati ya shilingi Bilioni 449 na bilioni 6 kwa mwaka, lakini hiyo sasa ni historia kwani Shirika linajiendesha lenyewe na kwa mwaka huu wa fedha tuna...project Shirika litatengeneza faida ya Shilingi Bilioni 9 

Aidha Mkurugenzi wa Uwekezaji kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina, Lightnes Mauki amesema, kwa sasa TANESCO imeanza kulipa madeni na tangu Mwezi wa Februari mwaka huu 2019 wamelipa bilioni 38.7 na ni hatua nzuri na wamekuwa wakitupatia nakala za malipo kila mwezi wanapolipa.” Alisema Lightnes
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, ambaye piamni Mbunge wa Busega, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni (kushotoO), akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara ya Kamati yake kutembelea mradi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme wa gesi asilia Kinyerezi I (Kinyerezi I Extension) jijini Dar es Salaam leo Machi 18, 2019.
 Wajumbe wa Kamati hiyo wakipatiwa maelezo ya utekelezaji wa mradi huo.
  Wajumbe wa Kamati hiyo wakipatiwa maelezo ya utekelezaji wa mradi huo.
 Mjumbe w aKamati Mhe. Charles Mwijage, akizungumza.
 Mbunge wa Kasulu Vijijini Mhe.Vuma Augustine ni miongozi mwa wajumbe waliotembelea mradi huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Mhandisi Dkt. Alexander Kyaruzi (aliyesimama), akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara ya kamati Machi 18, 2019. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka akizungumza.
Dkt. Mwinuka akimkaribisha Mbunge wa Karatu, Mhe. Willy Qambalo huku Mwenyekiti wa Bodi Mhandisi Dkt. Kyaruzi akishuhudia, wakati wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwkwzaji wa Mitaji ya Umma (PIC).

IFAHAMU ZAIDI KAMPENI YA TOKOMEZA ZERO YA WILAYANI KISARAWE, PWANI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo akiwa anazindua kampeni ya Tokomeza Zero.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo (wa pili kutoka kushoto) akipata maelekezo katika  moja ya mahabara wilayani Kisarawe
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwigelo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi katika mahafali ya kidato cha nne.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo (Kulia) akigawa vifaa vya  shule ikiwa ni sehemu ya kampeni ya   Tokomeza Zero Kisarawe.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo akiwa picha ya pamoja na wanafunzi wa shule yaMakurunge
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi katika mahafali ya Darasa la Saba.

Tokomeza zero Kisarawe ni kampeni maalum kwa ajili ya kuongeza ufaulu na kuondoa kabisa zero Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani. Changamoto wanazopitia walimu na wanafunzi ni nyingi.  Elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo wana kisarawe wameona  ni vyema  kuwekeza katika Elimu

"Ukimsaidia mtoto akaweza kupata elimu unakuwa umeweza kusaidia Tanzania nzima,na mimi kuanzia sasa nataka tuanze  na kidato cha nne na sita tufute hizo zero na zisiwepo kabisa. Katika kuhakikisha hii linatimia kuna mambo mengi ambayo tutafanya kwa kushirikiana na wadau wote wa elimu nchini ." Alisema Mhe. Jokate Mwegelo

TUMEFANYA 
Mwaka jana kampeni hii ya tokomeza Zero  ilifanyika kwa wanafunzi wa kidato cha nne kwa kuongeza ufaulu ikiwa ni kupunguza zero kutokea 455 mpaka 259 na kuondoa zero kabisa kwa kidato cha sita.  

Kwa kuona hili Mhesimiwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo alizindua Kampeni dada ijulikanayo kama Tokomeza Zero Kisarawe ikijumuisha wanafunzi kuwekwa kwenye kambi kwa ajili ya mafunzo maalum, uboreshwaji wa miundo mbinu mashuleni na  Elimu na kozi kwa walimu ili kuinua kiwango cha Elimu Wilaya ya Kisarawe

Utafiti unaonyesha wanafunzi wengi wa kisarawe hutembea umbali mrefu sana kwenda shule (Zaidi ya km 15 kwenda pekee) hali inayofanya wanafunzi kufika shuleni wakiwa wamechoka, mtoto wa kike ambaye atahitajika kufanya usafi nyumbani kisha aende shule kwa kutembea huchoka zaidi.

Miundo mbinu ya shule  ni changamoto na hata idadi za shule Wilayani ni chache kwa kulitambua hilo kuna ushirikishwaji wa wadau wa Elimu ili kuwezesha ujenzi wa shule kwa ajili ya wana Kisarawe na mkazo unawekwa zaidi ili kufanikisha kampeni ya Tokomeza Zero


"Wanafunzi wote wa Kisarawe wa kidato cha nne na cha sita watapata mafunzo ya ziada ili kujiandaa na mitihani yao ya taifa, ili kuwaepusha na kazi za kila mara wanafunzi hawa watakuwa kwenye kambi maaum kwa muda miezi miwili kabla ya muda wa mitihani yao ya taifa." Alisema Mhe. Jokate Mwegelo 

Sambamba na hilo walimu wanapatiwa mahitaji yote muhimu ili kufanikisha zoezi lao la ufundishaji na pia kuboresha miundo mbinu ya shule ili kuweza kukidhi mahitaji ya wanafunzi na walimu.

Katika kufanikisha kampeni hii inaenda sawa imeandaliwa Dinner Gala tarehe  30/03/2019 Ukumbi wa Mlimani City, katika jitihada za kukusanya fedha ambazo zitatumika katika ujenzi ya mabweni, shule hiyo itakuwa na madarasa ya kutosha, maktaba pamoja na maabara za kisasa. Shule hiyo itakuwa ya kwanza ya aina yake Kisarawe na kama mdau wa Elimu unaweza kushiriki kwa kuchangia Tsh 100,000  au kununua meza moja kwa shilling million moja . 

Fedha zote hizi zitaelekezwa katika ujenzi wa shule hiyo ya kwanza ya aina yake yenye lengo la kuwa shule ya mfano ambapo shule zitakazofuatia zitaundwa kwa mfano huo.

Unaweza kushiriki kwa kuwasiliana nasi kwa namba hii ili kupata ticket yako 0677062070 au 0656132676

Asanteni


Viewing all 110104 articles
Browse latest View live




Latest Images