Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

RC MAKONDA AZINDUA KAMPENI YA KUZUIA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI, AKABIDHI BILION 3 ZA UJENZI HOSPITAL ZA WILAYA.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya tukio la kihistoria la uzinduzi wa Kampeni ya kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na kukabidhi hundi ya Shilingi Bilioni 3 alizotoa Rais Dkt.John Magufuli kwaajili ya ujenzi wa Hospital za Wilaya ya Kigamboni na Ilala eneo la Kivule ambapo ametoa muda wa Miezi 3 kuhakikisha ujenzi umekamilika.

Akizungumza katika Uzinduzi huo RC Makonda amesema serikali imejidhatiti kuhakikisha inapunguza na ikiwezekana kumaliza kabisa vifo vya Mama na Mtoto kwa kujenga Hospital za kutosha, Zahanati, Vituo vya Afya, Ununuzi wa Magari ya kubebea Wagonjwa pamoja na vifaa tiba ili wananchi wasipate tabu.

RC Makonda amesema katika Fedha hizo Wilaya ya Kigamboni imepokea Shilingi Bilion 1.5 na Ilala Bilioni 1.5 ambapo Hospital zitakazojengwa zitakuwa na watumishi zaidi ya 500 na kuongeza kuwa mbali na Ujenzi wa Hospital hizo za Wilaya pia Serikali inaendelea na ujenzi wa Hospital nyingine ya kisasa eneo la Mabwepande.

Aidha RC Makonda amewataka wanaume kuwasindikiza wake zao Clinic ili kujua maendeleo ya Afya zao jambo litakalosaidia kuepusha vifo vya mama au mtoto wakati wa kujifungua.

Pamoja na hayo RC Makonda amewataka mabinti kuhakikisha wanaepuka Mimba za utotoni ambazo zimekuwa chanzo cha ongezeko la vifo na hata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Uzinduzi wa Kampeni ya kuzuia Vifo vitokanavyo na Uzazi JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA inaenda na kaulimbiu isemayo kila mmoja anao wajibu wa kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi "MANENO BASI SASA NI VITENDO"


Jukwaa la Utu na Mtoto laandaa kongamano kujadili ya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

SHIRIKA la Jukwaa la Utu na Mtoto (CDF) limeandaa kongamano la kitaifa kujadili hali ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kutokomeza na kuboresha upatikanaji wa viwango vya huduma kwa waathirikia wa vitendo vya ukatili.

Kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika Machi 21 na22 linatarajia kujadili namna ya kutokomeza vitendo vya ukatili yakidhaminiwa na Ubalozi wa Uswidi.

Mkurugenzi wa CDF Koshuma Mtengeti amesema kuwa Kongamano hilo litafungiliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  na kuhudhuriwa na wageni takribani 600 kutoka mataifa mbalimbali.

Mtengeti amesema, lengo kuu la kongamano hilo ni kuwapatia fursa viongozi wa kitaifa, watafiti, asasi za kiraia, wanataluma, viongozi wa dini, wanaharakati wa haki za binadamu, wadau wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi kujadili hali halisi ya ukatili pamoja na namna ya kuimarisha mikakati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

“ Kongamano hili litaangazia mada kuu sita ambazo ni halinya ukatili kwa watoto katika familia na mashuleni, ukatili wa kijinsia na unyanyasaji, mimba na ndoa za utotoni, ukeketaji, malezi katika ulimwengu wa kisasa, ukatili wa kingono, ukatili dhidi ha watoto kwenye mitandao na namna ya kuwapatia msaada wahanga wa vitendo hivyo,” amesema Mtengeti.

“Tanzania inakabiliwa na kiwango cha juu cha ukatili kwa wanawake na watoto ikiwemo vipigo, mimba na ndoa za utotoni, ukeketaji, unyanyasaji na hata ukatili wa kingono licha ya juhudi  kubwa zinazofanywa kupingana na vitendo hivyo na nchi yetu imekuwa ikijaribu kutekeleza mpango wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ,”amesema.

Mtengeti ameeleza kuwa kwa mujibu wa demografia ya afya mwaka 2015/16 inaonyesha kuwa idadi ya wasichana wanaopata watoto katika umri wa miaka 15-19 imeongezeka na kufikia asilimia 27 kutoka asilimia 23 mwaka 2010, asilimia 40 ya wanawake wa umri wa miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15.

Ameeleza, kwa mujibu wa ripoti ya ukatili dhidi ya watoto iliyotayarishwa na UNICEF 2011 ilibainisha kuenea kwa aina za ukatili wa kijinsia, kimwili na kiakili nchini Tanzania dhidi ya watoto na kuonyesha kuna asilimia 28 ya wasichana na asilimia 13 ya wavulana wamefikiwa na ukatili wa kijinsia kabla ya kutimiza miaka 18, na zaidi ya asilimia 70 ya wasichana na wavulana wamefanyiwa ukatili wa kimwili na zaidi ya robo wametndewa ukatili wa kiakili.

Mhadhiri Chuo Kikuu Kishirikishi (DUCE) Dr Mabula Nkuba amesema kongamano hili litatoa mwanga wa namna ya kupambana na kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto na wao kama wazazi, walezi na walimu wameamua kushirikiana na CDF kuunga mkono jitihada hizo na ukiangalia matukio ya ukatili wa kimwili ni mengi zaidi kuliko ukatili wa kijinsia kulingana na tafiti ya mwaka 2011.

Ripoti mbalimbali za haki za binadamu zimeweza kuonyesha kuna ongezeko kubwa la ukatili dhidi ya watoto kwa kipindi cha mwaka 2018 ukilinganishwa na mwaka 2017 nchini.

Aidha, kongamano hilo litatoa fursa kwa washiriki kudadavuabukubwa wa sura za ukatili yanayowasibu wanawake na watoto  na litasaidia juhudi za kuweka mikakati madhubuti ya kuzuia, kukabili na kuanzisha utaratibu wa kuboresha huduma kwa watoto na wanawake waathirika wa ukatili.
 Mkurugenzi wa Shirika la Jukwaa la Utu na Mtoto CDF Koshuma Mtengeti akizungumza na waandishinwa habari kuelekea kongamano la kitaifa la kujadili hali ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto  litakalofanyika Machi 21-22 Mwaka huu Jijini Dar es Salaam na Mgenj rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishirikishi DUCE Dr Mabula Nkuba akielezea kongamano la kujadili hali ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na namna wadau watakavyodadavua  kwa ukubwa wa sura za ukatili unavyowasinu wanawake na watoto katika jamii inayotuzunguka hapa nchini, kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Jukwaa la Utu na Mtoto CDF Koshuma Mtengeti.

FURSA YA MASOKO YA MATUNDA NA VIUNGO

Balozi Mgaza aahidi kuandaa mafunzo zaidi kwa wataalam wa afya nchini

$
0
0
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto, Abdulhakiem Kattan wa Saudia Arabia akizungumza kabla ya shughuli ya utoaji vyeti kwa washiriki wa mafunzo ya kusimamia upumuaji kwa wagonjwa wa ICU.
 Daktari Bingwa wa Watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Evelyne  Assenga akikabidhiwa cheti na Balozi wa Tanzania nchini Saudia Arabia, Hemedi Iddi Mgaza baada ya kumalizika kwa mafunzo ya kusimamia upumuaji kwa wagonjwa wanaolazwa ICU. Wengine katika picha ni wataalam wa afya kutoka Saudia Arabia. 

Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo leo, balozi huyo amesema wataendelea kuandaa mafunzo ya huduma za afya kwa wataalam mbalimbali nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo. 

Kauli hiyo imetolewa leo na balozi huyo wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili kuhusu upumuaji kwa wataalam kutoka hospitali mbalimbali nchini ikiwamo Bugando, Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Hospitali ya Benjamini Mkapa na Hospitali ya Mkoa wa Dodoma. 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru amesema kwamba Muhimbili itaendelea kutoa ushirikiano kwa wataalam wa afya kutoka Saudia Arabia ili kuhakikisha wataalam wabadilisha uzoefu na wenzao kutoka  Saudia Arabia. 

Mafunzo hayo yameandaliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Al balsam Cure and Care International Charity Organization
 Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo leo.
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto, Dkt. Martha Mkony akipokea cheti baada ya kumaliza mafunzo ya kusimamia upumuaji kwa wagonjwa wa ICU kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Saudia Arabia, Hemedi Iddi Mgaza.
 Daktari Bingwa wa Huduma za Usingizi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dkt. Amos Zakharia akifurahia baada ya kuwa miongoni mwa washiriki waliokabidhiwa cheti.
006: Baadhi ya wataalam walioshiriki mafunzo ya kusimamia upumuaji kwa wagonjwa wanaolazwa ICU.
Sehemu ya washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo leo.
 Mtaalam wa wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), Peter Bahati akikabidhiwa cheti na Balozi wa Tanzania nchini Saudia Arabia, Hemedi Iddi Mgaza.
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto, Dkt. Jenifa Metodi akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru baada ya kumaliza mafunzo hayo leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa afya kutoka Saudia Arabia na wenzao kutoka hospitali mbalimbali nchini.

(TAA yatoa misahafu 29 kwa Madrasat-ul-Istiqama ya Buguruni

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA  ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), leo imetoa ya misahafu 29 kwa Madrasat-ul-Istiqama ya Buguruni, Mtaa wa Ghana, jijini Dar es salaam kwa ajili ya watoto wanaosoma elimu ya dini ya Kiislam.
Akikabidhi vitabu hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Kaimu Mkurugenzi wa Uhandisi na Huduma za Ufundi, Mhandisi Mbila Mdemu amesema mbali na kazi za kuendesha, kusimamia na kuendeleza Viwanja vya Ndege Tanzania Bara, TAA imekuwa ikishirikiana na jamii katika masuala mbalimbali yanayohusu jamii.
Mhandisi Mdemu amesema pamoja na kwamba Madrasat hiyo ina watoto takribani 230, lakini anaamini wataweza kupokezana vitabu hivi na kupata mafunzo yaliyo sahihi, yatakayowajengea malezi bora yenye msingi wa amani na mshikamano.
Amesema msaada huu wa vitabu vya dini utasaidia kuanza kuwaandaa watoto hao, ambao baadaye wakiwa wakubwa wanakuwa ni sehemu ya jumuiya na sehemu ya Mamlaka na jamii nzima ya Kitanzania, ambapo watakuwa waadilifu na wenye maadili mema kwa taifa kwa kuwa wamepata msingi mzuri wa elimu ya dini, ambao ndio chimbuko la uadilifu na amani.
“Hii ni kawaida ya Mamlaka kutoa misaada kwa jamii, na ninaamini msaada huu pia utasaidia kufanya kitu kikubwa katika jamii yetu, kwa kuwa watoto hawa ndio watakuja kuwa watumishi wa miaka ijayo, hivyo watakuwa mfano wa kuigwa katika jamii,” amesema Mhandisi Mdemu.
Pia Mhandisi, amewakaribisha kutembelea TAA kwa ajili ya kujifunza na kuwa na ari ya kufanya kazi na Taasisi hii, ambayo ipo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi).
Naye Katibu wa Madrasat hiyo, Hemed Suleiman ameishukuru TAA kwa kujitoa kwao kwa kutoa msaada huo, ambao ni moja ya vitu muhimu kwao.
“Nawashukuru sana tena sana kwa msaada huu, hatuna cha kuwalipa ila Mungu awazidishie pale mlipotoa, muendelee kuwasaidia watu zaidi ya sisi” ameshukuru Bw. Suleiman.

 Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Uhandisi na Huduma za Ufundi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Mbila Mdemu (kushoto), leo akimkabidhi Katibu wa Madrasat-ul-Istiqama, Ustaadh Hemed Suleiman misahafu 29, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa wa Mamlaka hiyo, Richard Mayongela.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakishughudia Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Uhandisi na Huduma za Ufundi, Mhandisi Mbila Mdemu (kushoto) akikabidhi Katibu wa Madrasa ya Istiqama ya Buguruni, Ghana, Ustaadh Hemed Suleiman moja ya misahafu 29 waliyotoa msaada leo.  

Mhe. Suluhu Awataka Viongozi Afrika Kuwapa Kipaumbele Vijana

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 13.03.2019

WATAFITI WAAGIZWA KUTAFSIRI TAFITI ZAO KWA LUGHA YA KISWAHILI KUWASAIDIA WAKULIMA

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha

Naibu waziri wa kilimo Mh Inocent Bashungwa amewaagiza watafiti wa kilimo kuhakikisha wanatafsiri matokeo ya tafiti kwa lugha ya kiswahili ili iweze kueleweka kwa wakulima, badala ya kutumia lugha ya kiigireza ambayo mwisho wa siku haiwanufaishi wakulima.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza katika uzinduzi wa teknolojia ya kilimo hifadhi ijulikanayo kwa jina la CASI iliyofanyika mjini hapa.

Alisema kuwa,tafiti nyingi ambazo zimekuwa zikifanyika zimekuwa zikiandaliwa kwa lugha ya kiingireza hali ambayo imeshindwa kuwafikia walengwa wengi ambao ni wakulima ,hivyo lazima pawepo na mabadiliko hayo ili ziwafikie walengwa kwa wakati.

Alisema kuwa,teknolojia hiyo inajikita katika kuleta mabadiliko makubwa kwa wakulima hususani katika kuongeza uzalishaji zaidi kutokana na teknolojia hiyo kustahimili ukame kwa kiwango kikubwa.

Kwa upande wake mkuu wa mradi wa SIMLESA ,Dkt John Sariah amesema kuwa,mradi huo umewafikia zaidi ya wakulima elfu hamsini ,ambao wamefikiwa moja kwa moja huku zaidi ya wakulima zaidi ya elfu kumi na tano wakiwa wamepata taarifa juu ya mradi huo.

Alisema kuwa ,mradi huo ulianza kufanya kazi mwaka 2010 ambapo walifanya tafiti katika katika wilaya mbalimbali na kugundua manufaa ya mradi huo kwani unafanya kazi katika maeneo yote hasa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi huku ukiokoa muda wa mkulima kwa asilimia 50.

Nae Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania TARI ,dokta Geoffrey Mkamilo,amesema kuwa,utafiti unaonyesho kuwa teknolojia hiyo ina manufaa makubwa kwa wakulima na tayari imeshaonyesha matunda kwa baadhi ya wakulima ambao wameshaitumia teknolojia hiyo .

Dokta Mkamilo amesema kuwa,watahakikisha teknolojia hiyo inawafikia wakulima wote ili waweze kunufaika na kuongeza uzalishaji zaidi ,ambapo watahakikisha wanaingiza utaratibu wa kuhaulisha teknolojia hiyo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa utafiti kituo cha selian ambao ndio walioibua teknolojia ya kilimo hifadhi dokta Joseph Ndunguru amesema wanahitaji teknolojia hiyo iwafikie wakulima wengi ili iweze kuongeza uzalishaji wa chakula ,hata kuongeza malighafi kwenye viwanda.

Bi Rehema hasan ni mkulima kutokea mviwata morogoro ambao ni mmoja wa walionufaika na mradi huo amesema baada ya simlesa kuwapelekea mradi huo wamenufaika kwa kiwango kikubwa cha uzalishaji wa mazao kufuatia elimu waliyopatiwa.
 Naibu waziri Wa Kilimo Innocent Bashugwa  akizungumza na waandishi Wa habari mara baada ya kuzindua rasmi teknologia ya Kilimo hifadhi .
 Katibu tawala  Mkoa wa Morogoro Clifford Tandari akizungumza namna wananchi wa mkoa wake walivyoelimishwa wakati wa utafiti huo
 Mwenyekiti Wa kamati ya kudumu ya  Bunge Kilimo ,mifugo na maji Mohammed mkiwa akito ufafanuzi wa jambo katika katika uzinduzi huo 
 Mkurugenzi wa kituo cha utafiti seliani Josephy Ndunguru akizungumza na  waandishi kuhusu mipango yao mbalimbali baada ya uzinduzi

MATUKIO YA PICHA ZA WAZIRI MKUU AKISHIRIKI MAZISHI YA MAREHEMU KAKA YAKE MZEE SAID MAJALIWA

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki ibada ya kumsalia marehemu kaka yake Mzee Said Majaliwa aliyefariki Machi 12, 2019 katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa Machi 13.2019 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu kaka yake Mzee Said Majaliwa aliyefariki Machi 12, 2019, ambaye amezikwa machi 13.3.2019 katika makaburi ya familia, Nandagala Wilayani Ruangwa. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa mkono wa pole wa marehemu kaka yake Mzee Said Majaliwa aliyefariki Machi 12, 2019 na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa, kijijini kwake Nandagala Wilayani Ruangwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

STARTIMES KURUSHA TAMTHILIYA MPYA KWA LUGHA YA KISWAHILI

$
0
0
KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd leo Machi 13, imetangaza rasmi  ujio wa tamthiliya mpya ya kihindi iliyotafasiriwa na kuingiziwa sauti za Kiswahili hapa nchini.

Tamthiliya ya Waaris ikiwa na maana ya  Mrithi kwa kiswahili  inakuwa  tamthiliya ya kwanza kwenye kingamuzi cha StarTimes kwa kuingizwa sauti za Kiswahili hapa nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Meneja masoko wa Startimes Davis Malisa amesema kuwa katika kuhakikisha wateja wao wanapata burudani wanayostahili, StarTimes kupitia chaneli ya ST Swahili wataanza kuonyesha tamthiliya hiyo siku ya Alhamisi tarehe 14 Machi mwaka huu.

“Tunaendelea kujipambanua kama wafalme wa burudani za kifamilia, na tamthiliya hii mpya ina maudhui ambayo yanaweza kuangaliwa na familia na itaanza kuonekana kwenye chaneli yetu ya StarTimes Swahili siku za Alhamisi na Ijumaa kuanzia saa 2:30 hadi saa 3:30 Usiku" ameeleza David.

Imeelezwa kuwa tamthiliya ya Waaris inazungumzia masuala ya malezi na matokeo ya malezi hayo pamoja na mambo mengine. Pia inaonyesha unyanyasaji wa kijinsia ambao pia bado ni changamoto katika jamii zetu, bila kusahau uhalisia wa ambavyo kina mama wanawalinda watoto wao. 

Baadhi ya waigizaji walioshiriki  kuingiza sauti za Kiswahili katika tamthiliya hiyo ya Warris ni pamoja na  Yvonne Cherry (Monalisa), Godliver Gordian, Sophie na Rakheem David ambao wameonesha uwezo wa hali ya juu katika kuingiza sauti na kwa ujumla wameitendea haki Waaris.

Tamthiliya hiyo itaonyeshwa na chaneli ya ST Swahili pekee ambayo inapatikana katika kifurushi cha Nyota kwa gharama ya shilingi 8000 na kwa watumiaji wa Antenna na gharama ya shilingi 11,000 kwa watumiaji wa dikoda za Antenna.

Meneja masoko wa Startimes Davis Malisa  akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kuonesha tamthiliya mpya ya kihindi iliyotafasiriwa na kuingiziwa sauti za Kiswahili itakayokuwa inaoneshwa kupitia kwenye kingamuzi cha Startimes leo uliofanyika katika ukumbi wa sinema uliopo mlimani City jijini Dar es Salaam.

DC MURO AWAPA RAHA WAFUGAJI WA OLDONYO SAMBU

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro amekabidhi mabwawa manne makubwa  yenye uwezo wa kuhifadhi na kuvuna maji ya Mvua Milioni Thelathini na nane za maji ya mvua   kwa Viongozi wa kata ya OLDONYOSAMBU ambao wengi wao wanatoka katika maeneo ya Wafugaji kwa ajili ya matumizi yao na mifugo katika kijiji cha LEMANDA.
Dc Muro amekabidhi Mabwaya hayo , mara baada ya kuyapokea kutoka kwa wadau wa maendeleo Shirika la OIKOS la nchini Italia  kwa ufadhili wa Umoja wa Mataifa ( EU  ) Pamoja na ushirikiano wa nguvu za ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arumeru pamoja na wananchi wa Halmashauri ya Arusha Dc.
Awali Mabwawa hayo yalikuwa na uwezo wa kukusanya ma kuhifadhi maji lita milioni sita tu na sasa yamekarabatiwa  na kutengenezwa kuweza kumudu kuhifadhi maji lita million 38, pamoja na ujenzi wa Mapalio ya kisasa ya kunyweshea maji mifugo inayotoka katika maeneo mbalimbali mkoani Arusha
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro akiongea na Wafugaji katika kijiji cha Lemada.
  Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro akijumuika kucheza ngoma  na Wafugaji katika kijiji cha Lemada.
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro akijumuika kucheza ngoma  na Wafugaji katika kijiji cha Lemada.
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro akifurahia zawadi alizopata  katika kijiji cha Lemada.


 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro akikagua moja ya mabwawa manne  katika kijiji cha Lemada.
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro akikagua moja ya mabwawa manne  katika kijiji cha Lemada.
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro na ujumbe wake wakitembelea miradi ya wafugaji  katika kijiji cha Lemada.
Moja ya mabwawa manne  katika kijiji cha Lemada.

ULEGA ATATUA CHANGAMOTO YA DARAJA KITONGOJI CHA CHURWI KATA YA TAMBANI, MKURANGA

$
0
0
MBUNGE wa jimbo la Mkuranga Mkoani  Pwani na  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega  ametembelea katika Kitongoji cha  Churwi, Kata ya Tambani na kukaguwa mradi wa kivuko ambapo amefanikiwa kutatua changamoto  ya kivuko hicho chenye historia ya kuuwa watoto wawili.

Akizungumza na wananchi wa eneo hilo, Ulega alisema kuwa ameridhishwa na kitendo cha wananchi kuweza kujichangisha na kuanza ujenzi wa kivuko ili kukabiliana na changamoto zilizokuwa zikiwakabili za kukosa kivuko kwa muda  wa miaka mingi.


Katika hali hiyo  imempelekea Naibu waziri huyo kuchangia mifuko ya saruji 60  na milioni moja na nusu  kuongeza nguvu katika ujenzi wa kivuko hicho.

Aidha  amewataka wananchi hao  kuongeza ushirikiano zaidi katika masuala  ya maendeleo kwani wananchi wanapoanzisha miradi ya maendeleo serikali  ni lazima iweke mkono  wake ili kuongeza nguvu.


"Tushirikiane ili kuokoa maisha ya watoto wetu  pia kivuko hiki  kitasaidia kufungua fursa  mbalimbali za maendeleo kutokana na  uwepo wa uhakika wa njia"Alisema Ulega.Kwa upande  wake diwani wa kata hiyo Ally Mtamirwa amempongeza mbunge  Ulega kwa juhudi zake anazozifanya katika kuhakikisha mkuranga ina kuwa ya kuigwa kwenye maendeleo.

Aliongeza  kuwa bado  wananchi wanaendelea kujitolea katika mambo mbalimbali ya maendeleo ili kuhakikisha wanafanikiwa katika upatikanaji wa huduma za jamii.
Mbunge  wa jimbo la Mkuranga mkoa Pwani,  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akimkabidhi diwani wa kata  ya Tambani, Ally Mtamiwa mifuko 80 ya saruji kwaajili ya ujenzi wa kivuko katika kitongoji cha Churwi kata ya Tambani  wilaya ya Mkuranga.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Mbunge wa jimbo la Mkuranga mkoa Pwani,Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiweka jiwe la msingi ujenzi zahati ya kijiji cha Tipo  ambapo  alichingia amifuko 50 ya saruji na shilingi milioni moja.

 Mbunge  wa jimbo la Mkuranga mkoa Pwani,  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa ameongoza na niongozi wa chama cha (CCM) wa wilaya hiyo wakigangua mradi wa Zahanati ya kijiji cha Tipo ambapo alichangia mifuko 50 ya saruji na shilingi milioni moja.
Muuguzi wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga ,Grace Msemwa akisisitiza jambo katika mkutano uliofanyika katika kijiji cha Tipo wilaya ya hiyo.











Muonekano wa kivuko kinachoendelea kujengwa katika kitongoji cha Churwi kata ya Tambani  wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

WFP NA TRC Wasaini Mkataba wa ukarabati wa mabehewa 40 ya mizigo,WAZIRI KAMWELE AWAPONGEZA

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK, MAREKANI

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUTOKA MKOA WA MBEYA LEO

$
0
0


AJALI YA MOTO KUUNGUZA NYUMBA NA KUSABABISHA MAJERUHI NA UHARIBIFU WA MALI.

Mnamo tarehe 12.03.2019 majira ya saa 20:00 usiku huko katika Kitongoji cha Mapogoro, Kijiji cha Kapunga, Kata ya Itamboleo, Tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya, CATHERINE MFIKWA [32] Mkazi wa Kapunga pamoja na mtoto wake aitwaye PRISCAN PIUS @ MWAFWALO [14] Mkazi wa Kapunga walijeruhiwa kwa kubabuliwa na moto sehemu za miguu yao kutokana na moto uliozuka ghafla kwenye duka lao.
Katika tukio hilo moto huo ulisababisha uharibifu wa bidhaa zilizokuwa zinauzwa kwenye maduka ya (1) PIUS AIDAN @ MWAFWALO [41] Mkazi wa Kapunga, aliyekuwa anauza vinywaji baridi (2) JOMBAA @ RAS aliyekuwa anauza vitu vya jumla (3) JUMA MWAMJINGA aliyekuwa anauza bidhaa za dukani na mahindi. 

Majeruhi wamelazwa na wanapata matibabu katika Hospitali ya Misheni Chimala na wanaendelea vizuri. Bidhaa zote zilizokuwa zipo stoo zimeokolewa na zimekabidhiwa kwa wamiliki. Chanzo cha ajali hiyo ya moto ni kulipuka kwa jiko la gesi lililokuwa linatumiwa na CATHERINE MFIKWA (mke wa PIUS AIDAN @ MFIKWA) na kushika kwenye bidhaa za dukani na kusambaa kote. Moto huo umezimwa na kikosi cha zimamoto na uokoaji Wilaya ya Mbarali, Polisi na wananchi. Thamani ya mali iliyoungua bado kufahamika.


AJALI YA GARI KUGONGA UZIO NA NYUMBA NA KUSABABISHA MAJERUHI.

Mnamo tarehe 12.03.2019 majira ya saa 14:00 mchana huko maeneo ya Inyala, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya katika barabara ya Mbeya/Iringa, gari no. T. 608 DNP/T. 214 DNW aina ya FAW iliyokuwa ikitokea mkoa wa Songwe kuelekea Dar-es- Salaam ikiwa inaendeshwa na dereva asiyefahamika iliacha njia na kugonga uzio na nyumba inayotumika kwa huduma ya vipimo vya magonjwa mbalimbali ya binadamu [kliniki] na kusababisha majeruhi kwa 1. ZAKARIA CHINA [24] Mkazi wa Uyole ambaye ni mhudumu katika kliniki hiyo, 2. ELIUD FUNGO [38] Mkazi wa Inyala

ambaye ni Daktari wa kliniki hiyo 3. MAGRETHI HASSAN [32] Mkazi wa Inyala aliyekuwa anapata huduma 4. PILI MWANGAMBA [28] Mkazi wa Tunduma na alikuwa abiria kwenye gari hilo. Majeruhi wote wamepata majeraha ya kawaida mwilini na wamelazwa Kituo cha Afya Inyala. Chanzo cha ajali ni ubovu wa gari. Gari hiyo ilikuwa imebeba mzigo aina ya shaba. Msako mkali wa kumtafuta Dereva na mmiliki wa gari unaendelea.


KUFANYA SHUGHULI ZA UGANGA BILA KIBALI (LAMBALAMBA)

Mnamo tarehe 12.03.2019 majira ya saa 07:00 asubuhi huko katika Kijiji na Kata ya Sangambi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, Askari wakiwa katika msako waliwakamata 1. PETER DAUDI [37] Mkazi wa Mlimanjiwa 2. SIMON PAMBO [44] Mkazi wa Sangambi 3. AZOLE MWANAHELA [31] Mkazi wa Sangambi na 4. MASUMBUKO CHARLES @ MWANAHELA [36] Mkazi wa Sangambi wakiwa wanafanya shughuli za uganga wa lambalamba isivyo halali. Watuhumiwa walikamatwa wakiwa na madawa mbalimbali ya kienyeji, manyanga na ngoma mbili. Watuhumiwa wengine walitoroka kabla ya kutiwa nguvuni na juhudi za kuwasaka zinaendelea.

TAARIFA YA KIFO – RUNGWE.
Mnamo tarehe 07/03/2019 saa 12:30 mchana huko katika Mto Kiwira uliopo Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya Mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu Tukuyu Mwaka wa Tatu aitwaye SAMWEL JAMES CHACHA [25] alikufa maji akiwa anaogelea kwenye Mto huo na mwili wake kutoonekana baada ya kusombwa na maji.

Kutokana na tukio hilo zilifanyika jitihada za kuutafuta mwili wa mwanafunzi huyo ambapo tarehe 11/03/2019 majira ya saa 16.00 jioni huko katika Kijiji cha Mboyo, Kata ya Lupepo, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe na Mkoa wa Mbeya kwenye mto kiwira mwili wa mwanafunzi huyo ulipatikana. 

Chanzo cha tukio ni uzembe wa marehemu kutaka kuogelea kwenye mto huo bila kuchukua tahadhari. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Rungwe – Makandana kusubiri uchunguzi wa kitabibu. Upelelezi unaendelea.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa tahadhari kufuatia matukio ya kufa maji yanayosababishwa na uzembe wa kutovaa maboya wakati wanapoingia majini, mtoni au ziwani. Aidha kufuatia mvua zinazonyesha nawasihi wazazi kuwapeleka watoto wadogo shuleni na kuwapokea ili kuwalinda dhidi ya madhara ya kutumbukia katika maji.

KUZINI NA MAHARIMU.

Mnamo tarehe 09.03.2019 saa 21:00 usiku huko Mtaa wa Ghana, Tarafa ya Sisimba, Jiji na Mkoa wa Mbeya TUMAINI MWASOMI, Mkazi wa Mama John aligundua kubakwa kwa binti yake aitwaye CAREEN BONIPAHCE [14] Mkazi wa Ghana, Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari LEJIKO na baba yake mzazi aitwaye BONIPHACE JULIUS [42] Mkazi wa Ghana.

Aidha CAREEN BONIPHACE anaishi Ghana na baba mzazi baada ya kutengana na mama yake na ndipo baba yake akaanza kumbaka mara kwa mara tangu Septemba, 2018 bila kumwambia mtu yeyote na ndipo juzi tarehe 09.03.2019 majira ya saa 21:00 usiku baba yake alitaka kumbaka tena na ndipo binti huyo alikataa na baba yake alianza kumpiga na kumsababishia maumivu makali mwilini na hivyo kupelekea kumsimulia shangazi yake aitwaye LUCY MWASUMBULE juu ya vitendo vya kubakwa anavyofanyiwa na baba yake.

Chanzo cha tukio ni tamaa za kimapenzi. Mtuhumiwa amekamatwa na yupo mahabusu. Mhanga anaendelea na matibabu Hospitalini.


KUPATIKANA NA MICHE YA BHANGI.

Mnamo tarehe 10.03.2019 saa 07:00 asubuhi huko eneo la Mapanga, Kijiji cha Stamiko, Kata ya Mkola, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walikamata miche 30 ya bhangi ikiwa imelimwa kwenye shamba la mahindi lenye ukubwa wa robo heka mali ya NDUSHI SHIJA. Mtuhumiwa alikimbia na juhudi za kumtafuta zinaendelea lakini GUMBA ZALA [32] mkazi wa mapanga-stamiko ambaye ni mke wa mtuhumiwa na LUHENDE SHIJA [18] ambaye ni mtoto wa mtuhumiwa wamekamatwa kwa mahojiano. Mtuhumiwa ni mkulima na muuzaji wa bhangi. Upelelezi unaendelea.

MALI YA KUOKOTA.

Mnamo tarehe 10.03.2019 saa 21:30 usiku huko Kitongoji cha Lubele, Kata ya Ikimba, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakiwa doria pamoja na kikundi cha ulinzi shirikishi waliona gari aina ya Toyota Ractics rangi nyeupe ikiwa imeegeshwa maeneo ya uchochoroni kwenye pagala na watu wasiofahamika ambapo msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa unaendelea. Watuhumiwa waliacha gari hilo.
Baada ya kulikagua iligundulika kubomolewa kioo kidogo cha mbele upande wa dereva na pia kuharibika mfumo wa kuwashia gari, hivyo kuunganisha nyaya kwa urahisi wa kuliwasha. Gari hilo lilikuwa limebandikwa namba za kitanzania T 512 DCL na ndani ya gari hilo kumekutwa nyaraka zinazoonyesha kuwa ni IT iliyokuwa ikielekea Blantyre nchini Malawi. Ufuatiliaji unaendelea

KUPATIKANA NA MALI ZIDHANIWAZO ZA WIZI.

Mnamo tarehe 10.03.2019 saa 10:00 asubuhi huko maeneo ya ZZK Mbalizi na maeneo mbalimbali ya Mbalizi Wilaya ya Kipolisi Mbalizi. Askari Polisi wakiwa katika msako wa wahalifu na uhalifu na matukio ya uvunjaji walimkamata GOODLUCK JOSHUA [21] mkazi wa Nsalala akiwa na speaker mbili kubwa aina ya Dynamic Ailiong na Equalizers 1 aina media com na baada ya mahojiano alikiri kuhusika katika matukio mbalimbali ya uvunjaji na kutaja washiriki wenzake ambao ni JOHN MBEMBEJA, RAMADHANI, BONKE JIRANI na EMMANUEL MAPUNDA wote wakazi wa Mbalizi.

Makazi yao yamefanyiwa upekuzi na kupatikana mali mbali mbali ambazo ni:-
Mashine ya kuchezea bahati nasibu ya kichina 1,
Monitor aina ya dell 1,
CPU aina ya hp 1,
Radio za aina ya sub woofer zenye majina mbalimbali 5 na speaker zake 8,
King’amuzi cha kampuni ya startimes 1,
Mashine za kunyolea nywele aina home cut 2,
Cable ya umeme aina tronic 1,
Deck ya cd aina singsung 1,
Keyboard na mtungi mdogo wa gas kampuni ya Orexy,
Burner, pamaoja na stand yake mali zote zikidhaniwa kuwa za wizi.
Baadhi ya mali zimetambuliwa katika matukio ya uvunjaji. Mbinu ni kuvunja makufuri ya maduka na sehemu za biashara nyakati za usiku na kuiba.

Imesainiwa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

KUPATIKANA NA MALI ZIDHANIWAZO ZA WIZI.

Mnamo tarehe 10.03.2019 saa 10:00 asubuhi huko maeneo ya ZZK Mbalizi na maeneo mbalimbali ya Mbalizi Wilaya ya Kipolisi Mbalizi. Askari Polisi wakiwa katika msako wa wahalifu na uhalifu na matukio ya uvunjaji walimkamata GOODLUCK JOSHUA [21] mkazi wa Nsalala akiwa na speaker mbili kubwa aina ya Dynamic Ailiong na Equalizers 1 aina media com na baada ya mahojiano alikiri kuhusika katika matukio mbalimbali ya uvunjaji na kutaja washiriki wenzake ambao ni JOHN MBEMBEJA, RAMADHANI, BONKE JIRANI na EMMANUEL MAPUNDA wote wakazi wa Mbalizi.

Makazi yao yamefanyiwa upekuzi na kupatikana mali mbali mbali ambazo ni:-
Mashine ya kuchezea bahati nasibu ya kichina 1,
Monitor aina ya dell 1,
CPU aina ya hp 1,
Radio za aina ya sub woofer zenye majina mbalimbali 5 na speaker zake 8,
King’amuzi cha kampuni ya startimes 1,
Mashine za kunyolea nywele aina home cut 2,
Cable ya umeme aina tronic 1,
Deck ya cd aina singsung 1,
Keyboard na mtungi mdogo wa gas kampuni ya Orexy,
Burner, pamaoja na stand yake mali zote zikidhaniwa kuwa za wizi.
Baadhi ya mali zimetambuliwa katika matukio ya uvunjaji. Mbinu ni kuvunja makufuri ya maduka na sehemu za biashara nyakati za usiku na kuiba.

Imesainiwa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

Shirika la chakula Duniani WFP waungana na TRC kusafirisha chakula nje ya nchi

$
0
0


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwele na Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRC Profesa John Kondoro wakishuhudia Meneja Mkazi wa WFP Tanzania , Bw. Michael Dunford (kulia) na Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Bw. Masanja Kadogosa (kushoto) wakitia saini mkataba wa makubaliano ya ukarabati wa Mabehewa 40 ya treni yatakayofanya kazi ya kubeba mizigo ya WFP kwenda nchi mbalimbali za ukanda wa Afrika mashariki na Maziwa Makuu, Mkataba huo umetiwa saini leo katika Karakana ya TRC.


……………………………………………………………………

*Kwa mwaka huu wamejipanga kununua zaidi ya tani laki 1 za mahindi

*JPM atoa Bil 5/- kukarabati mabehewa 200, WFP kukarabati 40 kwa Bil 1.1/-

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwele amesema hawezi kuwa tayari kuona baadhi ya masuala yanasshindwa kufanikiwa katika taasisi zilizo chini ya wizaaraa yake kwa kisingizio cha kubanwa na sheria.

Alisema hayo jana wakati wa hafla yaa kutiliaanaa saini mkaataba wa kutengenezaa mabehewa 40 kati ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Shirika la Mpango wa Chaakulaa Duniani (WFP) kwenye karakana ya treni jijini Dar es Salaam jana.

Mhandisi Kamwele alisema, uwiano wa mizigo inaayosafirishwaa hailingani na uwezo wa maamlaaka ya bandari na TRC kutokana na uwekezaji mkubwa uliowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano na fursa ya kupakana na nchi zisizo na baahari.

“TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania), TPA (Mamlaka ya Bandari Tanzania) na TRC zinakwamisha uwezo wa bandari yetu kupakua naa kupakia mizigo. Tutafanya hiki kwa pamoja maaana nimebaini tatizo kubwa lipo TRA,” aalisema Mhandisi Kamwele na kuongezaa:

“Nimeshamwandikia baruaa Waziri wa Fedha na Mipango tukutane kwa ajili ya maazungumzo, maana sheria za fedha zipo lakini kama zinatukwamisha tuzifanyie marekebisho. Kwa mfano Uganda inazalisha tani laki 7.5 kwa mwaka lakini uwezo wa bandari yetu hadi sasa ni tani laki tatu kwa mwaka, tunakwama wapi. Tutataajana naani anakwamisha kupaata hii mizigo.”

Aidha, katika hafla hiyo TRC na WFP walikubaliana kusafirisha mizigo yaa chakula kutoka shirika hilo la kimataifa linalosambaza chakulaa ndani na nje ya nchi.

Ambapo katika kuimarisha uhussaano wao WFP wameamua kutoaa kiasi cha Dola za Kimarekani 600,000 sawa na Sh Bilioni 1.1 kwa ajili ya kukarabati mabehewa 40 ya shirika hilo.

“Napenda kutumia furssa hii kuwashukuru WFP kwa msaada huu ambao utaenda kukuza uwezo wa shirika la reli katika kuhudumia mizigo hususan unaopita bandari ya Dar es Salaam kwenda mikoa mingine na nchi jirani kama Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Zambia, Rwanda na Burundi. Tunashukuru WFP kwa kuungaa mkono juhudi za serikali iliyojielekeza kuleta mageuzi ya kiuchumi chini kwa kukuza biashara na kujenga uchumi wa viwanda,” alisema Mhandisi Kamwele.

Kaatika kuimarisha shirika hilo, hivi karibuni Rais Dk. John Magufuli alitoaa kiasi cha Bil 4 kwa ajili ya ukarabati wa maabehewa ya mizigo, ambapo lengo ni kukarabati mabehewa 200 hadi kufikia sasa TRC wameshakarabati mabehewa 40.

Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa alisema kwa kiasi kikubwa mabadiliko yametokea ndani ya shirika hilo tangu kuingia madarakani Rais Magufuli, ambaye aliapa kuinua uchumi wa watanzania kupitia viwanda na miundombinu imara.

“Miaka 15 iliyopita TRC ilikuwa na uwezo wa kusafirisha hadi tani milioni 1.4 kwa mwaka, lakini katikati tulipata misukosuko tukapoteza uwezo wetu. Tulipolibinafsisha tulizifunga njia nyingi katika reli ya kati na ya Tazara.

“Tunafanya ukarabati mkubwa katika reli ya kati, tunakarabati kilomita 970. Tayari kipande cha Tanga hadi Mombo kimeshakamilika viwanda vya saruji vimeanza kusafirisha mizigo yao kwa njia ya reli,” alisema Kadogosa.

Alibainisha, uhusiano wao na WFP unafikia mwaka mmoja sasa na kwa kuwa hilo ni shirika la kimataifa kuna uwezekano mkubwa wakapata wateja wengi zaidi kwa kuwa vigezo wanavyotumia kutaka kusafirisha mizigo hadi vimekubaliwa maana yake TRC wanaweza kufanya kazi na shirika lolote duniani.

“Mkakati huu wa kukarabati mabehewa una lengo la kukarabati mabehewa zaidi ya 500, kwa sasa tunaanza na haya 200 kwa fedha iliyotolewa na Rais Magufuli. Tunafanya kazi usiku na mchana ili tumalize mapema, mpango huu utasaidia kutoa ajira za moja kwa moja 30 na za muda mfupi 32,” alisema Kadogosa.

Kwa upande wake Meneja Mkazi wa WFP, Michael Dunford alisema walianza kutoa kazi za muda mfupi ili kuangalia uwezo wa TRC lakini ndani ya kipindi kifupi wamevutiwa na uwezo wao na ndiyo maana wameamua kufanya nao makubaliano.

“Mpango wa chakula kazi yake si lishe tu bali kusafirisha mizigo pia, tangu mwaka 2010 katika ardhi ya Tanzania tumenunua kiasi cha tani 500,000 za chakula, kwa mwaka jana 2018 tumenunua zaidi yaa tani laki moja na mwaka huu tuna mpango wa kununua zaidi ya tani laki moja na nusu, hii mizigo yote inahitaji kusafirishwa.

“Ndiyo maana tukaamua kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa mabehewa 40 yatakayosaidia kusafirisha mizigo yetu ndani na nje ya nchi kwenda DRC, Uganda hadi Sudan. Si tu tutaongeza ajira lakini pia tutachangamsha uchumi kwa masuala mbalimbali ya usafirishaji na miundombinu,” alisema
Dunford.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedith Kakoko ambaye pia alihudhuria hafla hiyo alisema kuimarika kwa shirika la reli kuna faida kubwa kwa TPA kwa sababu kazi zao zinategemeana.

“Hakuna reli bila bandari na hakuna bandari bila reli, lazima kazi zetu tuzifanye kwa pamoja. Nafikiria pia TPA tuingie mkataba kama huu na WFP kwa sababu ya kurahiisisha kuvusha mizigo mipakani. Na TRA vilevile wanahitaji kuhusishwa kwa kuwa yapo mambo mengi yanakwama au kuchelwa kwa kukosa maelewani,” alisema Kakoko.

Ushirikiano huu utaakuwa na tijaa kwa wakulima na wafanyakazi wa kubeba na kupakua mizigo kuanzia bandarini hadi kwenye maeneo ya reli, kwa kuwa WFP wamepanga kuwa watanunuaa chakula kutoka Tanzania ambayo ni faida kwa wakulima na watasafirisha kwa kutumia miundombinu ya reli na wakifika maeneo ya maziwa makuu watavusha kwa kutumia Ziwa Victoria kwenda nchi jirani.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwele na Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRC Profesa John Kondoro wakishuhudia wakati Meneja Mkazi wa WFP Tanzania , Bw. Michael Dunford wa pili (kulia) na Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Bw. Masanja Kadogosa (kushoto) wakionyesha mkataba wa makubaliano ya ukarabati wa Mabehewa 40 ya treni yatakayofanya kazi ya kubeba mizigo ya WFP kwenda nchi mbalimbali za ukanda wa Afrika mashariki na Maziwa Makuu Mkataba huo umetiwa saini leo katika karakana ya TRC

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwele na Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRC Profesa John Kondoro wakishuhudia Meneja Mkazi wa WFP Tanzania , Bw. Michael Dunford (kulia) na Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Bw. Masanja Kadogosa (Kushoto)wakibadilishana mkataba wa makubaliano ya ukarabati wa Mabehewa 40 ya treni yatakayofanya kazi ya kubeba mizigo ya WFP kwenda nchi mbalimbali za ukanda wa Afrika mashariki na Maziwa Makuu Mkataba huo umetiwa saini leo katika Karakana ya TRC.

Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Bw. Masanja Kadogosa akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwele (kulia),Meneja Mkazi wa WFP Tanzania , Bw. Michael Dunford (katikati) na Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Bw. Masanja Kadogosa Kushoto wakiwasili katika karakana ya TRC kwa ajili ya utiaji saini mkataba huo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwele (kulia),Meneja Mkazi wa WFP Tanzania , Bw. Michael Dunford (katikati) na Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Bw. Masanja Kadogosa Kushoto wakijadili machache kabla ya utiaji saini mkataba huo.
Meneja Mkazi wa WFP Tanzania , Bw. Michael Dunford akizungumza katika hafla hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwele akitoa hotuba yake kabla ya utiaji saini wa mkataba huo.
Meneja Mawasiliano wa TRC Jamila Mbarouk akitoa ratiba fupi na kukaribisha wageni katika hafla hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwele akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya TRC na wadau mbalimbali walioshiriki katika hafla hiyo.

COURT HEARS CASE CHALLENGING THE ELECTION OF THE CURRENT EALA SPEAKER

$
0
0


 Mr Nestor Kayobera representing the Attorney General of the Republic of Burundi (Applicant) in Court
 Honourable Judges of the First Instance Division during hearing session
 Dr Anthony Kafumbe Counsel To the Community representing the Secretary General (Respondent) in Court
Mr Donald Deya representing Hon Fred Mukasa Mbidde (Intervener) in Court

East African Court of Justice Arusha 12th March, 2019: The First Instance Division on Monday heard the case filed by the government of Burundi (Applicant) challenging the process of electing the current Speaker of the East African Legislative Assembly (EALA) which was held on 19th December, 2017.

The Applicant argues that the elections that were held in the absence of the Honourable Members of the Republic of Burundi and the United Republic of Tanzania are in violation of the fundamental Principles of the Community under Articles 6 (d), 7 and 57 (1) and Rule 12 (1) of EALA Rules of Procedure.

The matter came before Honourable Judges Lady Justice Monica Mugenyi (Principal Judge), Justice Dr Faustin Ntezilyayao (Deputy Principal Judge), Justice Fakihi A. Jundu, Justice Dr. Charles Nyawello and Justice Charles Nyachae. 

Mr. Nestor Kayobera, the Counsel representing Burundi, submitted to court that the election of the Speaker of EALA is governed by the EAC Treaty and the Assembly’s Rules of procedure and that Article 9 (4) of the Treaty obligates Organs and Institutions of the Community to perform the functions and act within the limits of the powers conferred upon them by the Treaty.

Mr. Kayobera also contended that the issue of quorum is a Treaty obligation under Article 57 and rule 12 (1) of EALA Rules of Procedure which provides that; The quorum of the House or of the Committee of the Whole House shall be half of the elected Members and such quorum shall be composed of at least one third of the elected Members from each Partner State”.  He argued that, violation of the rule on quorum entails violation of the Treaty.

Counsel further submitted that on 19th December, 2017, the Speaker of EALA was elected without the Members from Burundi and Tanzania hence a violation of the principles of good governance and Rule of Law. Mr. Kayobera also argued that Article 23 of the Treaty provides powers to the Court as the judicial organ to ensure adherence to law in the interpretation and application of and compliance of the Treaty.

Summing up his submissions, Mr. Kayobera said that the Speaker of EALA was not elected in accordance with the Treaty and the Rules of the Assembly and therefore asked the Court to order re election in accordance to the Treaty and rules of the Assembly. Mr Kayobera appeared with Mr Vyzigiro Diomede, State Attorney in the Attorney General’s Office Burundi.

Dr Anthony Kafumbe, representing the Secretary General (Respondent), on his part, submitted that the election of the Speaker was done under Part III of the Rules of Procedure of the Assembly. He further submitted that under Part III of EALA Rules of procedure, Rule 6 (9) (c) on the election of the Speaker, it is not mandatory for every member to vote, hence the Members of Burundi and Tanzania had liberty not to vote. Rule 6 (9) (c) states that; “After all Members who wish to vote have voted, the Clerk shall in full view of the Members present, empty the ballot box and immediately count the ballot paper contained in it”.

He also argued that the issue of quorum does not apply, that it only applies when the house is duly constituted. He therefore submitted that there was no illegal election process, that the Speaker was elected under relevant provisions of the Rules of procedure of the Assembly and that the election process did not violate the Treaty.

Dr. Kafumbe further submitted that as Article 9 of the Treaty obligates the Organs and Institutions of the Community, the Assembly acted within its mandate and in accordance with its rules of procedure.

Dr. Kafumbe also contended that Members of the Assembly have accepted the Speaker and a lot of business is going on and therefore, it would not be helpful to nullify the election and order fresh election.

Dr. Kafumbe also took issue with the Affidavits sworn by the Applicant’s Counsel on the basis of information relayed to him by EALA’s Members from the Republic of Burundi and submitted that the Court should reject the said affidavits as evidence since Counsel was not a witness and could not even have been a witness and a Counsel at the same time; the impugned affidavits ought to have been sworn by the Burundi’s Members of EALA, he argued.

In light of his submissions, Dr. Kafumbe prayed that the Reference be dismissed with costs to the Respondent. Dr Kafumbe was accompanied by Ms. Brenda Ntihinyurwa, a Legal expert in the Office of the Counsel to the Community.

The Intervener, Hon. Fred Mukasa Mbidd,e represented by Mr Donald Deya, Mr. Justin Semuyaba and Mr Nelson Ndeki in court, associated their submissions with the Respondent and asked the Court not to grant the orders sought by the Applicants.

The Court will deliver the judgment on notice.

The current Speaker of the East African Legislative Assembly is Rt Hon Martin Ngoga from the Republic of Rwanda, he was elected on 19th December 2017. The position of the Speaker is rotational and serves a period of five years.

The East African Court of Justice (EACJ or ‘the Court’), is one of the organs of the East African Community established under Article 9 of the Treaty for the Establishment of the East African Community. Established in November 2001, the Court’s major responsibility is to ensure the adherence to law in the interpretation and application of and compliance with the EAC Treaty.

Arusha is the temporary seat of the Court until the Summit determines its permanent seat. The Court’s sub-registries are located in the respective National Courts in the Partner States.



MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS YOWERI MUSEVENI JIJINI KAMPALA

$
0
0
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Africa Now Summit 2019 katika hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort mjini Kampala, Uganda. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MACHI 14,2019

MAKAMU WA RAIS AKICHANGIA MADA MKUTANO WA AFRICA NOW SUMMIT 2019

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akichangia mada katika masuala ya kuboresha biashara huria barani Afrika wakati wa hitimisho la mkutano wa Africa Now Summit 2019 jijini Kampala, Uganda. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)




Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images