Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live

WAWILI KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
Wakazi wawili wa Chanika jijini Dar es Salaam, Abdallah Hamis (30) na Adam Kawambwa(35)  wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na tuhuma za kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya zaidi Sh  bil.moja na utakatishaji.

Akisoma hati ya mashtaka, mbele ya Hakimu Mkazi, Augustine Rwizile Wakili wa serikali Candid Nasua amedai, washtakiwa wametenda makosa yao Februari 11.2019 huko Chanika kwa Zoo katika Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Imedaiwa siku ya tukio washtakiwa walikutwa na vipande 47 vya meno ya tembo vyenye thamani ya USD 465,000 ambayo ni sawa na Sh. 1,081,375,500 mali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mkurugenzi wa wanyama pori.

Katika shtaka la pili imedaiwa Siku na mahali hapo, washtakiwa hao walikutwa na vipande hivyo vya meno ya Tembo huku huku wakijua kuwa wamepata vipande hivyo kutokana na kutenda kosa la ujangili. Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo  kwa sababu Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida zinasikilizwa Mahakama Kuu au mpaka pale itakapopata kibali kutoka kwa DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na imeahirishwa hadi Machi 25,2019 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.
 Watumiwa Abdala Hamis na Adam Kawabwa wakiingia mahamani kisutu kwa kosa la kukutwa na meno ya Tembo yenye thamani ya thamani ya USD 465,000 thamani ya Sh. 1,081,375,500  na utakatishaji.
Washtakiwa Abdallah Hamis (30) na Adam Kawambwa(35) wakitoka katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo wanakabiliwa na tuhuma za kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya USD 465,000 thamani ya Sh. 1,081,375,500  na utakatishaji.

Prof. Kabudi akutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Prof. Palamagamba J. Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mikhail Bogdanov, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Urusi katika Ofisi Ndogo ya Wizara Jijini Dar es Salaam. Wamezungumzia masuala mbalimbali yaliyolenga kuboresha na kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya mataifa haya mawili, hususan, katika Nyanja ya kidiplomasia, nishati, biashara na uwekezaji. Naibu Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Mawaziri wanaendelea na mazungumzo hayo, huku ujumbe aliofuatana nao Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi ukifuatilia mazungumzo hayo 
utoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mej. Jenerali mstaafu Simon Mumwi, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Jestas Nyamanga, Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Yuri Popov na Afisa wa Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania wakifuatilia mazungumzo ya Mawaziri. 

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU RAIS WA KENYA MH RUTO.

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Rais wa Kenya Mhe. William Ruto katika hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, Kampala nchini Uganda ambapo kuna mkutano wa Africa Now Summit 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Rais wa Kenya Mhe. William Ruto kabla ya kufanya mazungumzo yao katika hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, Kampala nchini Uganda ambapo kuna mkutano wa Africa Now Summit 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Prof. Kabudi akutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Prof. Palamagamba J. Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Mikhail Bogdanov, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Urusi katika Ofisi Ndogo ya Wizara Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Waheshimiwa Mawaziri wamezungumzia masuala mbalimbali yaliyolenga kuboresha na kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya mataifa haya mawili, hususan, katika Nyanja ya kidiplomasia, nishati, biashara na uwekezaji. Naibu Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. 
Waheshimiwa Mawaziri wanaendelea na mazungumzo hayo, huku ujumbe aliofuatana nao Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi ukifuatilia mazungumzo hayo .
Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mej. Jenerali mstaafu Simon Mumwi, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Jestas Nyamanga, Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Yuri Popov na Afisa wa Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania wakifuatilia mazungumzo ya Waheshimiwa Mawaziri. 

NAIBU WAZIRI MABULA AHIMIZA UPIMAJI VIJIJI KUONDOA MIGOGORO YA ARDHI

$
0
0
Na Munir Shemweta, KATORO
Serikali imehimiza  halmashauri nchini kupima maeneo ya vijiji ili kuwamilikisha wananchi ardhi kwa nia ya kuwapatia hati za kimila na wakati huo kupanga matumizi bora ya ardhi katika maeneo hayo kwa lengo la kuepuka migogoro ya ardhi na kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Kauli hiyo imetolewa jana tarehe 12 Februari 2019 na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa kutoa hati 21 kwa wananchi wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Katoro uliopo wilaya ya Geita mkoa wa Geita pamoja na kutoa Ramani za Urasimishaji kwenye wilaya za Chato na Geita wakati wa ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi.

Alisema suala  la kupima vijiji ni la lazima na halmashauri zinapaswa kuchukua  hatua za kuwapimia wananchi kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi lakini pia kuleta salama ya miliki ya maeneo yao kwa kuwa kutofanya hivyo kutasababisha kuwepo migogoro ya mipaka pamoja na kiwanja kimoja kumilikishwa kwa watu wawili    (double allocation).

Akigeukia suala la urasimishaji, Dkt Mabula alizitaka halmashauri za wilaya ya Geita kuhakikisha zinarasimisha maeneo yaliyojengwa kiholela na kusisistiza kuwa salama ya eneo la mtu haliishii kuwekewa vigingi bali kinachotakiwa ni mtu kumilikishwa ili aweze kuitumia ardhi hiyo kujiinua kiuchumi kwa kuwa anaweza kuitumia hati yake kwa ajili ya kukopea fedha benki,

Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  alikabidhi ramani za urasimishaji kwa wakurugenzi wa halmashauri  mbili za wilaya ya Geita pamoja na ile ya Chato kwa nia ya kuendesha zoezi la urasimishaji katika maeneo ya halmashauri hizo.

Sambamba na hilo Dkt Mabula alishuhudia utiaji saini  makubailiano ya kupatiwa kiasi cha shilingi milioni 180 kwa halmashauri ya wilaya ya Geita kwa ajili ya kutwaa maeneo mapya ya halmashauri hiyo ambapo alieleza kiasi hicho cha fedha kitumike  kuepuka kero wakati wa kutwaa maeneo hayo.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  fedha zilizosainiwa ni kama mkopo na halmashauri husika inatakiwa kuuza viwanja na kurejesha fedha hizo ndani ya miezi mitatu na kubainisha kuwa Wizara imetengewa  shilingi bilioni 7 kwa ajili ya kuzikopesha halmashauri mbalimbali nchini ili kutwaa maeneo.

Alisisitiza kuwa ni marufuku kuchukua eneo la mtu bila kulipa fidia na kubainisha kuwa sheria ya mwaka 2016 inaweka wazi kuwa ukitwaa eneo ndani ya miaka miwili kama hujalipa fidia basi mwenye eneo anaruhusiwa kubaki na eneo lake na kiasi cha riba kinaongezeka kila baada ya miezi sita.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Ally Kidwaka alisema pamoja na Halmashauri yake kuwa na miji midogo yenye wakazi 50,000 lakini Mji Mdogo wa Katoro ndiyo unaokuwa kwa kasi na sasa umefikia wakazi wapatao laki moja. Alisema kutokana na mji huo kukuwa kwa kasi wataalamu wa upimaji wanatakiwa kuongezwa katika mji huo ili kuepuka changamoto za urasimishaji maeneo ya mji huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halamashauri ya Wilaya ya Geita Elisha Lupuga alisema Mji wa Katoro pamoja na kukuwa kwa kasi kwa muda mrefu lakini  ulichelewa kupatiwa mamlaka ya Mji  jambo lililochelewesha maendeleo katika mji huo. Hata hivyo, alisema  pamoja na wananchi wa Mji wa Katoro kuwa na uwezo wa fedha na nyumba nzuri lakini wamekuwa wazito kutoa fedha kwa ajili ya kupimiwa maeneo yao jambo linalosababisha mji kutopangika vizuri.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro katika mkoa wa Geita wakati wa kutoa hati za ardhi kwa wananchi wa mji huo kwenye ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi. Kulia kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Ntemi Musafiri na kushoto ni Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Geita Ally Kidwaka.
 Mkuu wa wilaya ya Chato Mhandisi Ntemi Musafiri akizungumza wakati wa zoezi la kutoa hati za ardhi kwa wananchi wa Mji Mdogo wa Katoro mkoani Geita uliofanywa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati akihamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi. Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo.
 Baadhi ya wananchi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro mkoani Geita wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati akihamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chato mkoa wa Geita Eliurd Mwaiteleke alipomkabidhi ramani kwa ajili ya zoezi la urasimishaji katika halmashauri hiyo wakati Naibu Waziri akiwa katika ziara  ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi hati ya ardhi mmoja wa wakazi katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro mkoani Geita Dohoi Shimiyu wakati alipotoa hati 21 kwa wakazi wa Mji huo akiwa katika kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro mkoani Geita waliopatiwa hati za ardhi wakati Naibu Waziri akiwa katika ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi. Wa tatu kushoto aliyekaa ni Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Ntemi Musafiri na wa tatu Kulia aliyekaa ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita Elisha Lupuga
 Mkuu wa idara ya Ardhi na Maliasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoa wa Geita Deogratias Matiya akimuonesha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula eneo la uwekezaji la Lubambagwe (Chato Beach) wakati Naibu waziri akiwa katika ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi mkoani Geita, Kulia ni Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Kagera Benit Masika.
 Mkuu wa wilaya ya Chato Mhandisi Ntemi Musafiri  akimuonesha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula eneo lililopangwa kwa ajili ya makazi katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita wakati Naibu waziri alipotembelea eneo hilo  kwa nia ya kuhamasisha mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuzuia ujenzi holela eneo linalozunguka uwanja huo.

Mganga mkuu ashauri kujengwa kwa hospitali kubwa nchini

$
0
0
Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohamed Kambi ameiomba Serikali ya Uarabuni kundelea kutoa misaada mbalimbali ukiwamo wa kujenga hospitali kubwa nchini ili kuwasaidia wagonjwa mbalimbali nchini. 
Kauli hiyo imetolewa na Prof. Kambi wakati akifungua mafunzo ya siku mbili yalioandaliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Al balsam Cure and Care International Charity Organization kwa ajili ya kuwawezesha wataalam wa afya kusimamia upumuaji kwa wagonjwa waliolazwa ICU.
“Natambua kwamba Serikali ya Uarabuni imekuwa ikitoa misaada mingi ya kuboresha huduma za afya, hivyo naomba wajenge hospitali kubwa nchini kwa ajili ya kutoa huduma za afya nchini,” amesema Prof. Kambi.
Prof. Kambi amewataka wataalam wanaopata mafunzo hayo kuyatumia vizuri katika sehemu za kazi pamoja na kuwaelimisha wataalam wengine.
Pia, Mganga mkuu ameishukuru Serikali ya Uarabuni kwa msaada wa matibabu ambao wamekuwa wakitoa kwa hospitali mbalimbali nchini ikiwamo Muhimbili na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Naye Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Muhimbili, Bw. Makwaia Makani amesema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwa kuwa MNH imepanua huhuduma za vyumba vya kulaza wagongonjwa wanaohitaji uangalizi maalamu pamoja na kununua vifaatiba.
Leo, watalaam walikuwa wakifundishwa jinsi vifaa tiba vya ICU vinavyopunguza maumivu kwa mgonjwa na jinsi kudhibiti hewa wakati mgonjwa akipatiwa matibabu ICU. Mafunzo hayo yanawashirikisha wataalam kutoka Hospitali ya Muhimbili, Mbeya, Hospitali ya Benjamini Mkapa, Bugando, Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
 Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohamed Kambi akizungumza kwenye mafunzo ya  kuwawezesha wataalam wa afya kusimamia upumuaji kwa wagonjwa waliolazwa ICU. Mafunzo hayo yanafanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
 Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohamed Kambi wakati akifungua mafunzo hayo.
 Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Muhimbili, Bw. Makwaia Makani akizungumza leo kwenye mkutano huo. Bw. Makani alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru.
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Homoni katika hospitali hiyo, Dkt. Faraja Chiwanga akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo kwa wataalam wa ICU nchini.
 
Wataalam kutoka Hospitali ya Bugando, Hospitali ya Benjamini Dodoma, Mbeya na Hospitali ya Mkoa wa Dodoma wakifuatilia mafunzo hayo
 Bw. Alaa Almqatieb akitoa mafunzo kwa  wataalam mbalimbali wa hapa nchini wakiwemo washiriki kutoka Hospitali ya Bugando, Hospitali ya Benjamini Dodoma, Mbeya na Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
 Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohamed Kambi akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa afya pamoja wataalam wengine.

RAIS WA ZANZIBAR DKT.SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA HIVI KARIBUNI

$
0
0
 /RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Bi. Hamida Mussa Khamis, hafla hiyo imefanyika leo 13-3-2019, Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimpongeza na kumkabidhi Hati  yake ya Kiapo Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja, Mkoa wa Kusini Unguja, hafla hiyo imefanyika leo 13-3-2019 Ikulu Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.Ndg. Khalid Abdallah Omar, hafla hiyo imefanyika leo 13-3-2019, katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimpongeza Naibu Katibu Mkuu Anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Ndg. Khalid Abdallah Omar, wakati wa hafla hiyo iliofanyika Ikulu Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Katibu Mtendaji Tume ya Utangazaji Zanzibar Ndg. Omar Said Ameir, hafla hiyo imefanyika leo 13-3-2019, Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduziu Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisaini hati ya Kiapo ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Ndg. Omar Said Ameir, hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar. 
 BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya M,apinduzi Zanzibar wakihudhuria hafla ya kuapishwa Viongozi walioteuliwa hivi karibuni, hafla hiyo imefanyika leo Ikulu Zanzibar
 BAADHI ya Wanafamilia wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakihudhuria hiyo ya kuapisha iliofanyika leo Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
  BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakihudhuria hafla ya kuapishwa Viongiozi walioteuliwa hivi karibuni, kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Saleh Kabi
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali kushoto Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid, Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja. Hamida Mussa Khamis na Naibyu Katibu Mkuu Anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.Ndg Khalid Abdallah Omar na kulia Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Said Hassan Said,Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Saleh Kabi na Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Ndg.Omar Said Ameir..(Picha na Ikulu)

SAM MANGWANA ASIYEKATA TAMAA KATIKA MUZIKI

$
0
0
Na: Moshy Kiyungi, Dar es Salaam

Machi, 2019.

Majina ya Sam Mangwana siyo mageni masikioni mwa wapenzi wa muziki wa dansi Afrika Mashariki na Kati. Ni mwanamuziki mwenye vipaji vya utuzi na kuimba nyimbo za muziki wa dansi.

Wasifu wa Sam Mangwana unaeleza kuwa alizaliwa Februari 21, 1945, katika mji wa Kinshasa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wazazi wake walikuwa wahamiaji ambapo baba yake alikuwa raia toka nchini Zimbabwe, wakati mama yake raia wa  Angola. Mangwana aliwahi kuwa mwanachama, mtunzi na mwimbaji katika bendi ya T.P. OK Jazz, iliyokuwa ikiongozwa na Franço Luambo Makiadi.

Nguli huyu alipitia kupiga muziki katika bendi zilizokuwa zikiongozwa na Tabu Ley Rochereau za African Fiesta, African Fiesta National na Afrisa Internationale.

Weledi wake katika muziki ulijulikana zaidi mwaka 1963, alipokuwa akipiga muziki wa rhumba katika bendi ya African Fiesta, iliyokuwa ikimilikiwa na na kuongozwa na Tabu Ley Rochereau.

Baadae Sam Mangwana alivuka mto Kongo akaingia katika mji wa Brazzaville, nchini Kongo Brazzaville.

Nchi hizo mbili za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Kongo Brazzaville, zinapakana na kutenganishwa na mto Kongo. Sam alipofika katika jiji hilo, aliunda bendi ya Los Batchichas, ambayo haikudumu kwa kipindi kirefu.
Aliwahi kufanya kazi katika bendi zilizoanzishwa za Negro Band na Orchestra Tembo mjini Brazzaville. Baadae akarejea kwao DRC katika jiji la Kinshasa, ambako aliungana na Tabu Ley, kupiga muziki katika bendi ya African Fiesta National.

Mwaka 1967, Mangwana kwa mara nyingine tena aliamua kuunda bendi yake akaipa majina ya Festival des Maquisards. Bendi hiyo ilisheheni wanamuziki wakiwemo mwimbaji Dalienst, mpiga  gitaa Dizzy Mandjeku na Michelino  aliyekuwa akipiga gitaa la solo.

Miaka miwili baadae, Sam Mangwana aliondoka tena akaenda kujiunga na mpiga gitaa maarufu aliyekuwa akiitwa Jean Paul "Guvano" Vangu, hadi mwaka 1972.

Mwaka huohuo wa 1972, alikwenda kujiunga katika bendi ya  T.P.OK. Jazz iliyokuwa ikiongozwa na Franco Luambo Makiadi. Mwaka 1973 Sam Mangwana alifuatana na bendi ya T.P.OK Jazz, walikuja katika jiji la Dar es Salaam kuporomosha burudani.
Yaelezwa kwamba Mangwana alifanywa mkarimani wa muda, akiwasaidia sana wanamuziki wenzake ambao walikuwa hawafahamu lugha yya Kiswahi.

Aidha alishirikiana vyema kuimba nyimbo zilizotungwa na mpiga gitaa wa bendi ya T.P. OK. Jazz, Lutumba Simaro Massiya, ambapo umaarufu wake ukapanda haraka wakati huo. Ushirikiano wake na Simaro, waliweza kuachia vibao vikali vya"Ebale ya Zaire", "Cedou", "Mabele" na nyingine nyingi.

Mangwana aliicha bendi ya T.P. OK. Jazz na kurudi tena kwenye bendi ya Tabu Ley ya Afrika Interantionale. Hata hivyo hakudumu kwa kipindi kirefu katika bendi hiyo, ya  Leyu, akaenda katika mji wa  Abidjan, nchini Ivory Coast, Afrika ya Magharibi.

Mwaka 1978 Mangwana pamoja na wanamuziki wengine waliunda bendi  iliyoitwa African All Stars. Mwaka mmoja baadaye bendi hiyo ilisambaratika mwaka 1979, Mangwana akaamua kuwa mwanamuziki wa kujitegemea.

Aliweza kurekodi na kufanya ziara nchi mbalimbali akiwajumuisha wanamuziki wenye vipaji mchanganyiko.
Akiwa na wanamuziki hao, alirekodi wimbo za  "Maria Tebbo" mwaka 1980, "Cooperation wa mwaka 1982, akiwa na Franco, "Canta Moçambique" wa mwaka 1983, akishirikiana na Mandjeku.

Baadhi ya nyimbo za nguli huyu ni Suzana, Fati Mata, Kabibi, Lokolo ya mwaka 1989, For Ever ya mwaka 1984, Aladji ya 1987, Waka Waka ya 1978, Bonne Anne ya mwaka 1983, Tchimurenga Zimbabwe, Maria Tebbo  na Matinda za mwaka 1979 na nyingine nyingi.

Sam Mangwana bado yu hai akipiga muziki wa kujitegemea.

Nafasi za masomo na ajira

$
0
0

Nafasi za masomo na ajira


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuwahimiza Watanzania wenye sifa kuomba fursa za masomo na ajira zinazotolewa na wadau mbalimbali duniani. Fursa zilizopokelewa mwezi Machi 2019 ni kama ifuatavyo:


i.       Mafunzo ya Shahada ya Uzamili yanayotolewa na Chuo Kikuu cha British nchini Misri (British University – Egypt) kwa kipindi cha mwaka wa masomo 2019/2020. Fursa hizi zinaratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, na maombi yanafanyika kwa njia ya  mtandao kupitia tovuti, http://www.bue.edu.eg/;


ii.    Mafunzo ya Shahada ya Kwanza na Uzamili yanayotolewa na Taasisi ya Elimu ya Urusi (Russian Education Institute)                                               kwa kipindi cha mwaka wa masomo 2019/2020 na 2020/2021. Fursa hizi zinaratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Maelezo ya namna ya kuomba fursa hizo yanapatikana katika Wizara zinazoratibu mafunzo hayo. Mwisho wa kufanya maombi kwa mwaka wa masomo 2019/2020 ni tarehe 25 Machi 2019 na tarehe 25 Juni 2020 kwa mwaka wa masomo 2020/2021;


iii.Mafunzo ya Shahada ya Uzamili katika fani ya Usuluhisihi katika Mchakato wa kutafuta Amani (Mediation in Peace Processes) yatakayotolewa nchini Ujerumani katika kipindi cha mwaka wa masomo 2019/2021.  Fursa hizi zinaratibiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki, na maombi yanafanyika kwa njia ya mtandao kupitia tovuti, http://www.mas-mediation.ethz.ch/.  Mwisho wa kufanya maombi ni tarehe 21 Aprili 2019;


NAFASI ZA AJIRA

iv.Nafasi ya ajira ya Afisa Tathmini (Evaluation Officer, P-3) katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Kudhibiti Matumizi ya Silaha za Kemikali (The Secretariat of the Organization for the Prohibition of Chemical Weapons-OPCW). Maelezo ya jinsi ya kuomba yanapatikana katika tovuti, https://opcw-career.talent-soft.com/job/job-officer-industry-p-3_11.aspx. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 15 Machi 2019; na


v.    Nafasi ya ajira ya Afisa Usalama wa Masuala ya Habari (Information Security Officer, P – 3) katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Kudhibiti Matumizi ya Silaha za Kemikali (The Secretariat of the Organization for the Prohibition of Chemical Weapons-OPCW). Maelezo ya jinsi ya kuomba yanapatikana katika tovuti, https://opcw-career.talent-soft.com/job/job-information- security-officer-industry-p-3_18.aspx. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 26 Machi 2019.

         


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Dodoma.

13 Machi 2019


DC MURO AWAPA RAHAA WAFUGAJI

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Cornel Muro amekabidhi mabwawa manne makubwa yenye uwezo wa kuhifadhi na kuvuna maji ya Mvua Milioni Thelathini na nane za maji ya mvua (38,000,000) kwa Viongozi wa kata ya OLDONYOSAMBU ambao wengi wao wanatoka katika maeneo ya Wafugaji kwa ajili ya matumizi yao na mifugo katika kijiji cha LEMANDA.

Dc Muro amekabidhi Mabwaya hayo , mara baada ya kuyapokea kutoka kwa wadau wa maendeleo Shirika la OIKOS la nchini Italia kwa ufadhili wa Umoja wa Mataifa ( EU ) Pamoja na ushirikiano wa nguvu za ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arumeru pamoja na wananchi wa Halmashauri ya Arusha Dc.

Awali Mabwawa hayo yalikuwa na uwezo wa kukusanya ma kuhifadhi maji lita milioni sita tu na sasa yamekarabatiwa na kutengenezwa kuweza kumudu kuhifadhi maji lita million 38, pamoja na ujenzi wa Mapalio ya kisasa ya kunyweshea maji mifugo inayotoka katika maeneo mbalimbali mkoani Arusha.









RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA URUSI MIKHAIL BOGDANOV IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov kabla ya kuanza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaa
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov ambaye aliambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov zawadi ya Kinyago cha Mpingo kabla ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro kabla ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuonesha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov picha ya Mlima Kilimanjaro ambayo alimkabidhi kama zawadi kabla ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Kitabu chenye Mambo ya Urusi  alichopewa zawadi na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mikhail Bogdanov watano kutoka kushoto, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi watano kutoka kulia, Balozi wa Tanzania nchini Urusi Meja Jenerali Simon Mumwi watatu kutoka kulia, Balozi Zuhura Bundala wapili kutoka kushoto pamoja na Maofisa wengine kutoka nchini Urusi Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

BAADHI YA WANANCHI WADAI VIGUTA MAMILIONI YA FEDHA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

WANANCHI zaidi ya 200 mkoani Pwani,wanadai kutapeliwa fedha milioni 185 ,kwa ajili ya kupatiwa viwanja na kujengewa nyumba kwa gharama nafuu kupitia kampuni ya Vicoba group union Tanzania (VIGUTA). 

Aidha Chamwino huko Dodoma wanadai kuidai kampuni hiyo milioni 61 huku wakikosa kupatiwa nyumba walizolipia kujengewa kwa gharama nafuu.

Aliyekuwa meneja wa Viguta mkoani Pwani,Iddi Kanyalu alikiri kuwepo kwa tetesi hizo na kudai taarifa hizo tayari amezifikisha kwenye vyombo vya sheria ili kufanya uchunguzi na sheria kufuata mkondo wake. 

Alisema,ni kweli walikuwa wananchi wanalipia viwanja kwa bei nafuu na nyumba walikuwa wakilipia kwa asilimia 25 mfano ukitaka kujengewa nyumba ya milioni 25 unalipia milioni 7.5 ambapo wengi walishalipia asilimia 25 na wengine fedha zote kisha kuingizwa mkenge. 

Kanyalu alieleza, utapeli huo umegusa watu ambao wameuziwa viwanja hewa na nyumba ambazo hawajakabidhiwa hadi sasa. 

"Wamenisababishia doa, kwanza mimi ni diwani wa kata ya Kongowe, kutokana na aibu hii na mimi kutohusika, nimeshachukua hatua ya kulifikisha suala hili polisi ili kuchukua hatua zaidi "alifafanua Kanyalu. 

Alipoulizwa kuwa kwanini asigutuke toka alipopewa kazi hiyo hadi kufikia hatua ya kuleta kero na ubabaishaji kwa jamii, Kanyalu alijitetea kuwa kama utapeli ulikuwa wa kimataifa hadi kufikia hatua ya kujitangaza kwa wabunge na kuingia mkataba na baadhi ya taasisi za kifedha hivyo haikuwa rahisi kwake kutambua ubabaishaji huo. 

Baadhi ya wananchi wa Kibaha akiwemo Aidan Mndewa na Kisaken ,walibainisha, kutokana na kudai fedha zao kutokana na kutopatiwa viwanja wala nyumba wanaiomba serikali ifuatilie kampuni hiyo na kuwasaidia kurejeshewa fedha zao. 

Wakati huo huo, msimamizi wa VIGUTA Chamwino huko Dodoma, Hilda Kadunda, ambae pia ni diwani viti maalum alisema wananchi walioingia katika mpango huo Dodoma wanadai milioni 300 na Chamwino wanadaiwa milioni 61 ambapo wapo watu waliouziwa viwanja mara mbili mbili. 

"Ninasimamia Chamwino pia kuna wakati nilikuwa katika mkoa wa Dodoma, mkurugenzi Christina na Mwenyekiti Salmin Dauda wao ndio watia saini lakini tukidaiwa wakipigiwa simu wanazima ama kudai hawapo wanashughulikia masuala mengine "

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, ACP Wankyo Nyigesa alipoulizwa juu ya tuhuma hizo kama wahusika akiwemo Mkurugenzi wa VIGUTA Christina Rwebangila na mwenye kampuni hiyo Salmin Dauda kama hatua zozote zimeshachukuliwa kufuatia malalamiko hayo, amedai hajapata taarifa hizo. 

Wankyo alielezea, atafuatilia kwa watendaji wake ili kujua kama wamepata taarifa hizo ili waweze kufanya uchunguzi na kuchukua hatua .
Baadhi ya picha zikionyesha nyumba za sampo zilizokuwa zikidaiwa kujengewa wananchi kwa gharama nafuu

IDARA YA UHAMIAJI YAANZA ‘KUWAFUNDA’ WANANCHI MAENEO YA MIPAKANI

$
0
0
Idara ya Uhamiaji Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Uhamiaji la Kimataifa (IOM) limeanza kutoa mafunzo ya Ushirikishwaji wa Wananchi katika Ulinzi na Usimamizi wa Mipaka katika Kijiji cha Horohoro, mpakani mwa Tanzania na Kenya kwa siku tatu kuanzia leo tarehe 13-15 Machi, 2019.

Warsha hiyo ya Mafunzo ambayo imefunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Mhe. Yona Maki, inashirikisha wananchi waishio mpakani wenye ushawishi katika jamii pamoja na viongozi wa dini, wakulima, mgambo, viongozi wa vijiji na waendesha bodaboda.

Awali akifungua warsha hii, Mkuu wa Wilaya ya Mkinga aliipongeza Idara ya Uhamiaji kwa kuamua kutoa mafunzo yenye lengo la kuwashirikisha wananchi wa kawaida katika suala zima la ulinzi na usimamizi wa mipaka.

“Kwanza niwashukuru sana Idara ya Uhamiaji pamoja na watu wa IOM kwa kuamua kutoa mafunzo kwa wananchi wa kawaida. Ninaamini baada ya mafunzo haya, washiriki kwa kuwa ni watu wenye ushawishi katika jamii ya vijiji vya kata hii, watasaidia sana kufikisha ujumbe. Naona kuna viongozi wa bodaboda, hawa bodaboda ndio wanaosafirisha watu, miongoni mwa watu hao kuna wahamiaji haramu pia, naamini wakipewa elimu basi hawa bodaboda watakuwa ni sehemu muhimu katika Ulinzi na Usimamizi wa mipaka yetu”.

Mkuu huyo wa Wilaya alieleza kuwa Baba wa Taifa aliwahi kusema kuwa jukumu la ulinzi wa Taifa ni letu sote na hasa wazalendo. Hivyo jukumu hili la ulinzi si la vyombo vya ulinzi na usalama pekee, bali ni la kila Mtanzania.

Wakati akitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Afisa Uhamiaji Wilaya Mkinga alisema kwamba jumla ya wahamiaji haramu 216 kutoka mataifa ya Ethiopia, Somalia na Kenya walikamatwa katika wilaya ya Mkinga katika Mwaka 2018.

Warsha hii ya siku tatu imelenga katika kuwajengea uwezo washiriki juu ya Uhalifu wa Kimataifa, Makosa ya kiuhamiaji, Biashara ya Magendo ya Binadamu, Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Uraia wa Tanzania na mambo yanayohusiana na Uhamiaji nje ya Mfumo rasmi.
Mkuu wa wilaya ya Mkinga, Yona Maki akizungumza wakati wa mafunzo ya Ushirikishwaji wa Wananchi katika Ulinzi na Usimamizi wa Mipaka katika Kijiji cha Horohoro, mpakani mwa Tanzania na Kenya.
Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanda akitambulishwa kwa wajumbe wakati wa mafunzo ya Ushirikishwaji wa Wananchi katika Ulinzi na Usimamizi wa Mipaka katika Kijiji cha Horohoro, mpakani mwa Tanzania na Kenya

Diwani kata ya Lemara Profesa Raymond Mosha akabidhi baiskeli ya walemavu kwa mkazi wa kata hiyo George Makinda

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud,Arusha.
Diwani wa Kata ya Lemara ,Profesa Raymond Mosha ameanzisha mpango wa kuwafikia watu wenye ulemavu na kuwapatia mahitaji yao pamoja na nyenzo wanazohitaji ikiwemo baiskeli maalumu za walemavu.
Akizungumza katika zoezi la kukabidhi baiskeli ya mlemavu mwenye umri wa miaka zaidia ya sitini mkazi anayeitwa Mzee George Makinda  wa kata ya Lemara katika eneo la Njiro jijini Arusha amesema kuwa  baiskeli  hiyo  itamsaidia kujishughulisha na kazi zake kama kawaida.
Msaada wa baiskeli hiyo  imetolewa na Professa Raymond Mosha ambae ni diwani wa kata hiyo ya Lemara baada ya kuona familia ya Mzee George Makinda haina uwezo wa ununuzi wa baiskeli hiyo,
Professa Mosha alisema kuwa alihuzunishwa sana na maisha ya mlemavu huyo kwani George Makinda  miaka ya nyuma alikua mzima lakini alikubwa na ugonjwa wa kupooza uliomfanya kua mlemavu wa kushindwa kuongea wala kutembea.
alisema hali hiyo ndio iliomgusa yeye na marafiki zake nakuamua kujitolea baiskel ambayo itamsaidia kwa namna moja au nyingine kutembelea na kujiona kama watu wengine.
Hata hivyo Mke wa Mzee George Makinda  Bi Estar Makinda  pamoja na kutoa shukurani  ya  msaada wa Baiskel hiyo ambayo anataja kua sababu ya kumfanya kumpa ahuweni kwakua ameteseka kwa muda mrefu katika kumlea mumewe,
Estar alisema hata muda mwingine alishindwa kujishughulisha na kazi za kiuchumi nakubaki kumhudumia mumewe  kutokana na  muda wote ni mtu wa kuhudumiwa kila kitu,
“ sasa amepatiwa msaada wa Baisekel itakayomsaidia kutembea naamini sasa mabadiliko ya familia yataonekana”  Alisema Estar Makinda.
Diwani wa kata ya Lemara Profesa  Raymond Mosha akikabidhi baiskeli ya walemavu kwa mkazi wa kata hiyo George Makinda ambaye ni mlemavu wa miguu baada ya kupata ugonjwa wa kupooza .picha zota na Mahmoud Ahmad Arusha

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA MOROCCO HAPA NCHINI ALIYEAMBATANA NA UJUMBE KUTOKA NCHINI KWAO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kiongozi wa Ujumbe kutoka nchini Morocco Balozi Mohamed Methqal ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa Wakala wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Morocco  mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. katikati  ni Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah Benryane akishuhudia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao na Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah Benryane ambaye aliambatana pamoja na Kiongozi wa Ujumbe kutoka nchini Morocco Balozi Mohamed Methqal ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa Wakala wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Morocco,  Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini Patrick Mfugale pamoja na wajumbe wengine.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo kuhusu ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu utakaokuwa na uwezo wa kuingiza watazamaji zaidi ya  85,000 mkoani Dodoma huku Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah Benryane wanne kutoka (kushoto) pamoja na Kiongozi wa Ujumbe kutoka nchini Morocco Balozi Mohamed Methqal watatu kutoka kushoto pamoja na ujumbe huo wakisikiliza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mfano wa Uwanja mkubwa wa mpira wa miguu utakaojengwa jijini kwa ufadhili wa Mfalme wa Morocco Mohamed VI. Uwanja huo utakuwa  na uwezo wa kuchukua watazamaji 85,000 (normal capacity) waliokaa kwenye viti lakini pia utaweza kubeba washabiki  hadi105,000 kama walivyopanga. Kwa nje uwanja huo utakuwa na muonekano kama mlima Kilimanjaro hivyo kuzidi kupamba madhari ya mjii mkuu wa Tanzania mkoani Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah Benryane wasabi kutoka kushoto akifatiwa na Kiongozi wa Ujumbe kutoka nchini Morocco Balozi Mohamed Methqal ambaye ni  Mkurugenzi mkuu wa Wakala wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Morocco pamoja na Ujumbe wao. Wengine katika picha ni  ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi wasabi kutoka kulia, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale wasita kutoka kulia, Balozi Zuhuru Bundala wakwanza kulia  pamoja na wajumbe wengine Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU



Prof. Kabudi apokea Salamu za Pongezi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Kabudi akisoma barua ya pongezi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambayo iliwasilishwa wizarani na Balozi wa China nchini.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Prof. Kabudi apokea Salamu za Pongezi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China

Mheshimiwa Prof. Palamagamba J. Kabudi (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, leo tarehe 13 Machi, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa WANG Ke, Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China.

Mheshimiwa WANG Ke pamoja na masuala mengine amewasilisha kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki barua ya pongezi kutoka kwa Mheshimiwa Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China kufuatia Prof. Kabudi kuteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

Aidha Prof. Kabudi kupitia kwa Mheshimwa Balozi ameshukuru kwa salamu hizo za pongezi alizopokea.

Katika mazungumzo yao, Prof. Kabudi na Balozi WANG Ke, wameahidi kufanya kazi kwa pamoja ili kuimarisha ushirikiano wa kihistoria baina ya nchi hizo mbili. Na kwa pamoja wamesisitiza umuhimu wa kuendelea na jitihada za kuimarisha mahusiano ya kisiasa, kijamii, kiuchumi hususan kwenye maeneo la uwekezaji, biashara, utalii na miundombinu.

Prof. Kabudi ametumia fursa hiyo kuishukuru Jamhuri ya Watu wa China kwa misaada ya kimaendeleo wanayoendelea kuitoa na kwamba Serikali inafurahishwa na Jinsi China inavyounga mkono jitihada zake za kuwaletea wananchi maendeleo na kujenga uchumi.

Tanzania na China zimekuwa na mahusiano ya kidiplomasia tangu mwaka 1964 na mwaka huu zinatarajia kuadhimisha miaka 55 ya ushirikiano huo.

Mheshimiwa Wang amekuwa Balozi wa kwanza kuonana na Mhe. Kabudi tangu kuteuliwa kwake na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuiongoza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
13 Machi 2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akipokea barua ya pongezi kutoka kwa Balozi wa China nchini, Mhe. WANG Ke. Balozi wa China aliwasilisha barua hiyo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Mhe. WANG Yi ambapo anampongeza Prof. Kabudi kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China mara baada ya kupokea barua ya pongezi.

Taasisi Zinazohusika na TEHAMA Zatakiwa Kushirikiana Kuendeleza Vipaji

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Taasisi zinazohusika na Masuala ya TEHAMA nchini zimetakiwa kuendelea kushirikiana katika kuinua vipaji vya wanafunzi wanaosoma masomo yahusuyo TEHAMA na kuviendeleza ili viweze kuondoa changamoto zilizopo katika jamii.

Hayo yamesemwa jana jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako alipokuwa akifunga mafunzo na mashindano ya siku ya Kimataifa ya Wasichana na TEHAMA yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote.

Prof. Ndalichako amesema kuwa nia ya Serikali ni kuona mchango wa Sayansi na Teknolojia ukiongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za jamii na kuongeza tija katika uzalishaji hususani katika sekta zinazogusa wananchi moja kwa moja zikiwemo za uchumi, kilimo, mifugo na viwanda.

“Hadi sasa tunaona mafanikio mengi ya matumizi ya TEHAMA ambapo hata wajasiriamali wamekuwa wakikuza biashara zao kupitia mitandao, pia mapato ya serikali yameendelea kuongezeka baada ya kuingia kwenye mfumo wa matumizi ya TEHAMA hivyo kutokana na mafanikio hayo, natoa rai kwa wadau wote wa TEHAMA kushirikiana na Serikali sio tu kuinua vipaji bali na kuviendeleza,” alisema Prof. Ndalichako.

Prof. Ndalichako amefafanua kuwa Serikali imeendelea kutoa msisitizo katika masuala ya TEHAMA ambapo hivi karibuni imetoa  jumla ya Kompyuta 300 na Projekta 100 kwa ajili ya kuendeleza mafunzo ya teknolojia, habari na mawasiliano kwenye Vyuo vya Walimu pia zimeanzishiwa maabara za kompyuta kwa baadhi ya shule ili kuendeleza mafunzo ya teknolojia hiyo.

Ametoa rai kwa wanafunzi kuacha kuitumia vibaya TEHAMA na badala yake kusoma masomo hayo kwa kuwa fursa za masomo ya Sayansi na Teknolojia ni nyingi pia zinatoa nafasi kwa watu kujiajiri kwa kutengeneza programu mbalimbali ambazo zinaweza kuuzwa kwa gharama kubwa.

Akiongelea kuhusu mafunzo hayo, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, (UCSAF) Mhandisi Peter Ulanga amesema kuwa siku ya Kimataifa ya Wasichana na TEHAMA ilianzishwa kwa lengo la kumuhamasisha mtoto wa kike kuchagua masomo ya TEHAMA na kuweza kupata fursa katika sekta hiyo.

“Kama Taifa tunajiandaa kuelekea katika uchumi wa kati ambao ni uchumi wa viwanda hivyo hatuna namna yoyote ya kuufikia uchumi huo kama hatutowaelimisha wananchi kuhusu masuala ya TEHAMA, Sayansi na Teknolojia, tunaamini kuwa ukimuwezesha mtoto wa kike basi umeelimisha familia na Taifa ndio maana tunawahamasisha kusoma masomo hayo,” alisema Mhandisi Ulanga.

Akiwakilisha wanafunzi wenzie, Khatija Saphy ameishukuru Serikali kwa kutoa motisha hiyo ya wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi, ameiomba Serikali kuendelea kutoa fursa hizo mpaka vijijini kwa sababu maeneo hayo yana wanafunzi wengi wabunifu ambao hawapati nafasi hiyo.

Juhudi za Mfuko huo juu ya kuhamasisha watoto wa kike kupenda masomo ya Sayansi zilianza tangu mwaka 2016 ambapo kila mwaka wanafunzi 248 wa kidato cha tatu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani hasa wanaopata daraja la kwanza kwenye mitihani ya  kidato cha pili wanapata fursa ya kupata mafunzo ya TEHAMA hasa namna ya kutengeneza mifumo ya komputa.

Vile vile ili kuongeza hamasa, wanafunzi 31 wanapewa medali na wanafunzi sita kati ya hao wanapata zawadi za kikombe, kompyuta mpakato na safari ya kwenda nchini Ethiopia kwa ajili ya kushiriki fainali za mashindano hayo ya watoto wa kike ulimwenguni.
.Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akizungumza  na wadau pamoja na wanafunzi wa kike (hawapo pichani) jana jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo na mashindano ya siku ya Kimataifa ya Wasichana na TEHAMA yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akimvalisha medali mwanafunzi Monica Cleophance ambaye ni kati ya wanafunzi 6 waliopata nafasi ya kwenda nchini Ethiopia kwa ajili ya kushiriki fainali za mashindano hayo ya watoto wa kike ulimwenguni.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akifurahi pamoja na mwanafunzi Khatija Saphy baada ya mwanafunzi huyo kuwa mmoja kati ya washindi sita na kupokea zawadi ya kikombe, kompyuta mpakato na kupata safari ya kwenda nchini Ethiopia kwa ajili ya kushiriki fainali za mashindano hayo ya watoto wa kike ulimwenguni.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote na wanafunzi wa kike 31 waliopata mafunzo hayo. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo, Mhandisi Peter Ulanga

IGP SIRRO AKUTANA NA KUWAPONGEZA ASKARI WALIOSHIRIKI KATIKA MICHEZO YA MAJESHI TANZANIA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa michezo mbalimbali walioshiriki katika mashindano ya michezo ya majeshi (BAMMATA). IGP alikutana na wanamichezo hao Makao Makuu ya Polisi kuwapongeza na kuwatia moyo ili wafanye vizuru zaidi katika michezo ijayo. PICHA NA JESHI LA POLISI.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akimvisha nishani ya dhahabu SGT Kenya wa kikosi cha kutuliza ghasia alioipata wakati wa mashindano ya majeshi (BAMMATA) hivi karibuni katika uwanja wa Uhuru jijini dare s salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akikabidhiwa moja ya makombe yaliyopatikana katika michezo ya majeshi (BAMMATA) katika mashindano yaliyomalizika hivi karibuni katika uwanja wa taifa jiji Dar es Salaam. Anayemkabidhi kombe ni Mrakibu SP Mtafi, Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Kutuliza.

WAZIRI KAIRUKI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke mapema hii leo Machi 13, 2019 katika ofisi zake Jijini Dodoma.

Lengo la mazungumzo hayo ilikuwa ni kujadili maeneo muhimu yanayohusu masuala  ya uwekezaji ambapo Waziri Kairuki alieleza vipaumbele muhimu vya uwekezaji  vitakavyochangia adhma ya Serikali ya kuwa na uchumi wa viwanda ikiwemo kuwekeza katika maeneo ya kilimo, elimu, afya, viwanda vya nguo pamoja na ujenzi wa Miundombinu ya barabara.

“Ninafarijika kwa ujio wako na ni ishara nzuri ya mahusiano mazuri yaliyopo  baina ya nchi hizi mbili naamini yatasaidia katika fursa za uwekezaji hasa kwa namna Uingereza ilivyochangia katika maeneo muhimu nchini ikiwemo elimu,”alisema Kairuki

Waziri aliongezea kuwa, Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji kwa kuzingatia mchango unaotokana  na wawekezaji hasa katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo nchini.

Waziri Kairuki alieleza kuwa, kuwepo kwa Idara ya uwekezaji katika Ofisi ya Waziri Mkuu ni hatua muhimu kwani itasaidia kuongeza nguvu ya ufuatiliaji na utekelezaji wa masuala hayo na kuendelea kuleta mabadiliko katika kutatua changamoto zilizozikabili sekta hiyo.

Aidha alimshukuru balozi huyo kwa hatua ya mazungumzo yenye tija pamoja na kuendelea kuunga mkono nchi ya Tanzania na kuwataka kuendeleza urafiki huo kwa kuwekeza zaidi katika maeneo aliyoyaainisha ikiweko yale ya vipaumbele.

Naye Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Sarah Cooke aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa na sera zinazovutia wawekezaji pamoja na maboresho yanayofanywa kuwavutia wawekezaji nchini ikiwemo maeneo ya ulipaji wa kodi.

“Tunaelewa kuwa Serikali inafanya jitihada kubwa katika kuboresha mazingira ya biashara ikiwa ni pamoja na mazingira ya ulipaji wa kodi tunaahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili kuwa na mchango katika maendeleo ya nchi pamoja na kuimarisha mahusiano yaliyopo,”alisisitiza Cooke.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke, ofisini kwake Jijini Dodoma Machi 13, 2019 alipokutana naye na kufanya mazungumzo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki akizungumza na balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke pamoja na wenyeji alioambatana nao wakati wa kikao cha mazungumzo  na Waziri Kairuki kuhusu masuala ya fursa za uwekezaji nchini.
 Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke akizungumza jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki alipomtembelea Ofisini kwake Machi 13, 2019 Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki akizungumza jambo na balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke wakati wa kikao hicho.
 Mwakilishi wa masuala ya Biashara Afrika Bw.Martin Kent akizungumza jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki (Hayupo pichani) wakati walipomtembelea katika Ofisi zake Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki akiteta jambo na balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke mara baada ya kumaliza mazungumza yao, kulia ni Beth Arthy aliyeambatana na balozi huyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke (wa pili kutoka kushoto) pamoja na wajumbe alioongozana nao.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TRA YAWAHIMIZA WAFANYABIASHARA, WAMILIKI WA MAJENGO KULIPA KODI KWA WAKATI

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewahimiza wafanyabiashara na wamiliki wa majengo kote nchini kulipa kodi kwa wakati hususani Kodi ya Mapato awamu ya kwanza, Kodi ya Majengo na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambapo huu ndio muda muafaka wa kulipa kodi hizo. 

Akizungumza na walipakodi katika Ofisi za TRA Vingunguti jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo amesema kodi ya ongezeko la thamani inatakiwa kulipwa ifikapo Machi 20 mwaka huu, kodi ya mapato inatakiwa kulipwa kabla ya tarehe 30 Machi, 2019 wakati mwisho wa kulipa kodi ya majengo ni mwezi Juni, 2019.

“Ninachukua fursa hii kuwahimiza wafanyabiashara na wamiliki wa majengo mliopo hapa na wale watakaosikia taarifa hii kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuwahi kulipa kodi hizi kwa wakati ili kuepuka usumbufu na hatimaye kujikuta mnatozwa faini na riba," alisema Kayombo.

Amesema kuwa, viwango vya kodi ya majengo ni shilingi 10,000 kwa nyumba za kawaida, shilingi 50,000 kwa kila sakafu ya ghorofa na shilingi 20,000 kwa nyumba za ghorafa zilizoko vijijini.

"Tunaona serikali imepunguza kiwango cha kodi ya majengo, hivyo hakuna sababu ya watu kuchelewesha na kusubiri dakika za mwisho, tulifanye suala la ulipaji kodi kuwa utamaduni wetu kwa lengo la kuleta maendeleo ya nchi yetu,” alisisitiza Kayombo.

Wakati huo huo, Mkurugenzi Kayombo amewatahadharisha walipakodi kuhusu uwepo wa watu wanaotumia jina la mamlaka hiyo kufanya utapeli kwa kujitambulisha kuwa ni maofisa wa TRA wakidai kwenda kukagua ulipaji wao wa kodi.

“TRA ina utaratibu wake wa kuwasiliana na wafanyabiashara na kuwajulisha siku rasmi ambazo maofisa wetu watakwenda kufanya ukaguzi na unafanyika kwa uwazi bila vitisho na si kwa taratibu nyinginezo,”alisema Kayombo

Ameongeza kuwa, "kama mtu atapigiwa simu au kama una mtu una wasiwasi nae tafadhali toa taarifa kwa ofisi zetu zilizopo karibu nawe au toa taarifa Kituo cha Huduma kwa Wateja namba 0800 780 078 au 0800 750 075 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa moja usiku na utupe namba ya mhusika ili tuweze kufuatilia.

“Pia kuna namba ya Whatsapp ambayo unaweza kutoa taarifa au kuuliza chochote kupitia namba 0744 233 333 ambayo ni maalum kwa ajili ya kutatua changamoto za wananchi na kuwawezesha kulipa kodi kwa wakati,” alisema Kayombo.

Richard Kayombo amesema kuwa, tangu mwezi Desemba mwaka jana, TRA imekuwa ikipata malalamiko kutoka kwa watu tofauti tofauti ambao wamekuwa wakitapeliwa fedha na maofisa feki wanaodai kufanya kazi Mamlaka ya Mapato Tanzania.
 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akizungumza na walipakodi katika Ofisi ya TRA Vingunguti jijini Dar es Salaam kuhusu wito wa kujitokeza kulipa kodi za mapato, majengo na kodi za ongezeko la thamani kwa wakati ili kuepuka usumbufu, riba na faini.
 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akizungumza na mmoja wa walipakodi katika Ofisi ya TRA Vingunguti jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea ofisini hapo kuwahimiza walipakodi kulipa kodi za mapato, majengo na ongezeko la thamani kwa wakati ili kuepuka usumbufu, riba na faini.
Mkazi wa Mwanagati, Nyamizi Mgawe akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya TRA Vingunguti jijini Dar es Salaam wakati Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo Richard Kayombo alipotembelea ofisini hapo kuwahimiza walipakodi kulipa kodi za mapato, majengo na ongezeko la thamani kwa wakati ili kuepuka usumbufu, riba na faini.

Viewing all 109973 articles
Browse latest View live




Latest Images