Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

NENE TCHAKOU MCHARAZAJI WA SOLO DRC.

$
0
0
Na Moshy Kiyungi,Dar es Salaam

Nene Tchakou ni jina ambalo halijazoeleka sana kwa wapenzi wengi wa muziki wa dansi. Ni mkung’utaji wag it la solo aliyepitia katika bendi nyingi huko jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Jina lake halisi ni Nene Mbedi, kwa sasa ni mtu mzima wa umri wa miaka 57 hivi sasa. Alizaliwa Februari 1957, katika eneo lililojulikana kama Banana huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Vipaji vingi vya wanamuziki huibukia wakati wakiimba Kanisani au kupiga ala ya muziki na wengine hutokea kwenye Madrasa wakiimba Kaswida. Lakini kwa Nene Tchakou kwake ilikuwa tofauti kabisa.

Mbendi Tchakou yeye alianza kujihusisha na maswala ya muziki akicharaza gita kwenye kundi lililokuwa linaundwa na watoto wa Askari jijini Kinshasa.

Nuru njema ya mafanikio katika muziki ilianza kung’aa mwaka 1973 akiwa na bendi ya Bella Negrita. Mafanikio hayo yalipelekea kuanza safari ndefu ya kuzunguka kwenye bendi kadha wa kadha.

Weledi wake katika muziki alifanywa mithiri ya Kito cha thamani kwa kuwa kila alikotuwa, alikubalika vilivyo. Safari yake ya mwaka ya 1981, ilimfikisha katika kundi lililokuwa maarufu la ‘Langa Langa Stars mahali alikopewa jina la ‘Tchakou,’ likiwa na maana ya Parrot kwa lugha ya Kilingala. Kwa Kiswahili ni ndege ajulikanaye kama Kasuku.

Tchakou hakuwa mtu wa kukata tamaa wakati akitafuta mfanikio zaidi. Aliendeza safari mwaka 1983 alipojiunga katika bendi ya Grand Zaiko, ikiwa chini ya uongozi wa Pepe Manwaku.

Alitoa mchango mkubwa mno katika bendi hiyo hususani katika e kibao cha ‘Mbongo’. Baadaye akaamua kupiga muziki akijitegemea na kufanikiwa kufyatua wimbo wa ‘Niger’ mwaka 1987.

Ni kawaida kwa wanamuziki toka nchi za Afrika ya Kati pindi wanapokaribia mafanikio, hukimbilia kwenda nje ya nchi yao. Nene naye alifanya kwenda katika jiji Paris nchini Ufaransa mwaka 1988.

Alipokuwa katika jiji hilo aliandika historia kwa kutoa mchango mkubwa kwa nguli wa muziki barani Afrika, Kofi Olomide na kutoa albamu ya ‘Papa Bonheur’. 

Alipenda sana kushiriki na wanamuziki wakubwa hivyo baada ya muda alijiunga na kundi la Soukous Stars linaloongozwa na Lokassa ya Mbongo. Hapo walianza matayarisho ya albamu iliyokuja kutamba vilivyo ya ‘Lagos Knight’.

Utaratibu wa kushirikiana na wanamuziki wakubwa aliuendeleza ambapo kwa mara nyingine alishirikiana na mwanamuziki Lala Nomotoki (kutoka Togo) Shi Loving (Kutoka Nigeria), Papa Wemba (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, walitoa albamu ya ‘For idole.’

Ili atengeneze muziki mzuri Nene akashirikiana na mwimbaji mahiri Aurlus Mabele kutoka Congo Brazzavile, kwa pamoja wakaandaa albamu ya ‘Dossirr X’.

Nene Tchakou alitengeneza albamu yake ya kwanza akiwashirikisha Madame (Bongo), Patience Dabani (Kutoka Gabon), 3615 Code Niawu (Kutoka DRC.

Mwaka mmoja baadaye akiwa katika Jiji la California nchini Marekani, alirekodi albamu moja iliyotoka mwaka 2001.

Alimshirikisha mwimbaji wa Soukous Stars Shimmita mapema mwaka 2002, kuanzisha kundi la Afro Muzika.

Mwaka 2003 Nene Tchakou alijiunga na Lembo ya ‘Rowa Records’ kama msanii mkaazi. Huko ndiko alikotengeneza na kufyatua CD ya ‘Cesse Le Fou’ Pendin.

Tchakou vilevile anajishirikisha na kupiga muziki wa kiasili akishirikiana na wanamuziki wengine wa Kiafrika chini ya uongozi wa Injinia na Produza Rick Scott.

Nene Tchakou ameongeza idadi ya wanamuziki kwa Kiafrika wanaoishi nchini Marekani, na kwa idadi yao hadi sasa wamepatikana wanamuziki watatu.

Wanamuziki hao ni pamoja na Sam Mangwana, Diblo Dibala na yeye Nene Tchakou.

Amesema bado wanahitaji wanamuziki wengi ili waendelee kuutangaza muziki wa Kiafrika Ulimwenguni kote.

PICHA ZA NENE TCHAKOU.

SERIKALI YATOA ONYO KALI KUTANGAZA MILIPUKO YA MAGONJWA YA MIFUGO NCHINI

$
0
0


WAZIRI Mpina akishiriki katika zoezi la uogeshaji mifugo kwenye Josho la kwanza kujengwa na Wajerumani katika nchi za Afrika Mashariki liitwalo Nunge lililojengwa mwaka 1905 lililoko wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina wa kwanza kushoto mwenye koti jeupe kwenye picha ya pamoja na wadau mballimbali mara baada ya kutoa hotuba ya tathmini ya zoezi la uogeshaji kitaifa iliyofanyika kwenye josho la kwanza kujengwa na Wajerumani katika nchi za Afrika Mashariki liitwalo Nunge lililojengwa mwaka 1905 lililoko wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.



NA JOHN MAPEPELE, MPWAPWA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amepiga marufuku mtu yoyote kutangaza kuwepo magonjwa ya mifugo nchini isipokuwa yule aliyepewa mamlaka hayo kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na taratibu za nchi na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika.

Akizungumza hivi karibuni katika tathmini ya kampeni ya uogeshaji kitaifa iliyofanyika kwenye josho la kwanza kujengwa na Wajerumani katika nchi za Afrika Mashariki liitwalo Nunge lililojengwa mwaka 1905 lililoko wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina alisema Sheria za kimataifa na Sheria ya Magonjwa ya Mifugo Namba 17 ya mwaka 2003 inazuia kufanya hivyo.

Kwenye tathmini hiyo ya miezi mitatu kuanzia Novemba 2018 hadi Februari 2019 jumla ya Mifugo milioni 32 sawa na asilimia 56 ya mifugo milioni 57 iliyopo nchini iliogeshwa ambapo kati ya mifugo iliyoogeshwa ng’ombe milioni 19.9, mbuzi milioni 8.9, kondoo milioni 2.88, punda 224 na mbwa 229,000 huku majosho yanayofanya kazi nchini ni 1,197 kati ya majosho 2,300 lakini majosho 1,124 ni mabovu hayafanyi kazi vikundi 847 vimeundwa na kufungua akaunti vikundi 612


Aidha Mpina alisisitiza kuwa shabaha ya kuzuiwa kufanya hivyo kwa sababu baadhi ya watu wanaweza kujitokeza kupeleka hofu kwa wananchi na kusababisha kuharibu biashara hiyo na hivyo mwenye dhamana ya kufanya hivyo ni Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo na sio mtu mwingine yoyote yule.

Hivyo Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo ndiye aliyepewa dhamana ya kutangaza ugonjwa wowote wa mifugo kwa niaba ya watanzania na wala sio mtendaji yoyote yule wa Serikali

Alisema nchi yetu imejipanga vizuri kudhibiti magonjwa ya mifugo na ndio maana inazo kanda nane za uchunguzi wa magonjwa ya mifugo hivyo watanzania wako salama Tanzania iko huru na magonjwa na sasa tunazalisha chanjo 8 kufikia mwezi 9 hadi mwakani kutakuwa na chanjo 11 ili mifugo ichanjwe isipatwe tena na magonjwa.

Hivyo Waziri Mpina ilifakapo Julai mosi mwaka huu wizara yake itakuwa imeshatoa kanuni za namna ya uendeshaji wa zoezi la uogeshaji ili kila mmoja afahamu wajibu wake.

Pia Waziri Mpina alisisitiza agizo lake la ukarabati wa majosho na kwamba ifikapo Julai mosi mwaka huu halmashauri ambayo itakuwa hajakarabati majosho itazuiliwa kukusanya mapato huku akizindikia barua za kusudio la kuzizuia kukusanya mapato halmashauri hizo.

Majosho 132 kati ya majosho mabovu 1,124 yameshakarabatiwa ni asilimia 11 ya agizo hilo limetekelezwa leo miezi mitatu na kuupongeza Mkoa wa Kagera ambao wamekarabati majosho 34, Mkoa wa Mwanza wamekarabati majosho 19, Mkoa wa Arusha majosho 11 wengine hawajafanya hivyo

Mpina alisema halmashauri zote nchini zinakusanya zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa mwaka mapato yanayotokana na sekta ya mifugo lakini ni halmashauri chache zinazotenga fedha kidogo za kusaidia mifugo huku Mkoa wa Dodoma hadi sasa umekarabati majosho mawili tu

Alisema mwongozo unaelekeza asilimia 15 ya mapato yanayokusanywa kutoka kwa wafugaji iende kutoa huduma kwa mifugo ikiwemo ukarabati wa majosho, malambo na chanjo hivyo lazima fedha zitengwe kwenda kwa wafugaji.

Hivyo Waziri Mpina aliziagiza Mamlaka zote zinazosimamia zoezi la uogeshaji kusimamia mwongozo uliotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikiwa ni pamoja na kila josho kuwa na kikundi na kiwe kimefungua akaunti.

WAZIRI MWAKYEMBE AFANYA ZIARA MKOANI SINGIDA KUJIONEA MAENEO YA URITHI WA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA

$
0
0


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akisoma moja ya kaburi la wakoloni wa Kijerumani eneo la Kilima Tindewakati akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Singida kwa ajili ya kutembelea maeneo ya historia ya ukombozi wa Bara la Afrika ikiwa ni mikakati ya kuhamasisha viongozi na wananchi kutunza, kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo kwa matumizi ya kizazi cha sasa na kijacho.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiangalia eneo lilotumiwa na wakoloni wa Kijerumani eneo la Kilima Tindewakati wa ukoloni akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Singida kwa ajili ya kutembelea maeneo ya historia ya ukombozi wa Bara la Afrika ikiwa ni mikakati ya kuhamasisha viongozi na wananchi kutunza, kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo kwa matumizi ya kizazi cha sasa na kijacho.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia handaki lilotumiwa na wakoloni wa Kijerumani eneo la Kilima Tindewakati wa ukoloni akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Singida kwa ajili ya kutembelea maeneo ya historia ya ukombozi wa Bara la Afrika ikiwa ni mikakati ya kuhamasisha viongozi na wananchi kutunza, kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo kwa matumizi ya kizazi cha sasa na kijacho.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA UJENZI WA MAJENGO YA MAHAKAMA MBEYA

$
0
0
 Jengo la Mahakama ya wilaya ya Rungwe na Mahakama ya Mwanzo ya Rungwe mjini likiwa katika hatua za awali za ujenzi. jengo hili linajengwa na Mkandarasi M/S Moladi Tanzania Ltd na kusimamiwa na Chuo Kikuu cha Ardhi kama Mtaalam Mshauri. Ujenzi ulianza kutekelezwa mwaka wa fedha 2017/2018 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Aprili 2019. Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walitembelea na kukagua ujenzi wa jengo hili leo mkoani Mbeya.
 Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania Bwn Khamadu Kitunzi akiwaelezea waheshimiwa wabunge kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa majengo ya Mahakama.
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisikiliza ufafanuzi juu ya mradi wa ujenzi wa Mahakama kutoka kwa Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania Bwn Khamadu Kitunzi (hayupo pichani) walipoongozana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea mradi huo.


 Jengo la Mahakama ya Mwanzo Uyole likiwa katika hatua za ukamilishwaji (finishing) Jengo hili linajengwa na Mkandarasi M/S PIM Innovators na kusimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mkoa wa Mbeya. Ujenzi ulianza Desemba mwaka jana na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Aprili 2019. Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walitembelea na kukagua ujenzi wa jengo hili leo mkoani Mbeya.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea mradi wa ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Uyole.Lydia Churi Ntambi.




Na Lydia Churi- Mahakama-Mbeya


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wameanza ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa majengo ya Mahakama ya Tanzania inayoendelea nchini ambapo leo wajumbe hao wametembelea miradi iliyopo wilayani Rungwe pamoja na Uyole jijini Mbeya. 

Pamoja na wajumbe wa kamati hiyo, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Prof. Sifuni Mchome pia walikuwa ni miongoni mwa watu walioshiriki kwenye ziara hiyo. 

Katika ziara hiyo mkoani Mbeya, wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Katiba na Sheria walianza kwa kutembelea mradi wa ujenzi wa Mahakama ya wilaya ya Rungwe ambao bado uko katika hatua za awali. 

Mradi huu uliopangwa kutekelezwa mwaka 2017/2018 unahusisha huduma za mahakama ya wilaya na ya Mwanzo mjini Rungwe ambao unatekelezwa na Mkandarasi M/S Moladi Tanzania Ltd na kusimamiwa na Chuo kikuu cha Ardhi kama Mtaalamu Mshauri. 

Aidha, Mradi wa Ujenzi wa Mahakama ya wilaya na ya Mahakama ya Mwanzo Rungwe mjini ulianza kutekelezwa mwaka jana na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Aprili mwaka huu. 

Baada ya kutembelea ujenzi wa Majengo ya Mahakama wilayani Rungwe, wajumbe wa Kamati hiyo pia walitembelea ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Uyole ulioanza kutekelezwa Desemba 2018 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi April mwaka huu. 

Mradi huu unatekelezwa na Mkandarasi M/S PIM Innovators na kusimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mkoa wa Mbeya kama Mtaalamu Mshauri. Hatua iliyofikiwa sasa ni kuezeka na kuanza kazi za umaliziaji( finishing) 

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria pia wanatarajia kutembelea na kukagua ujenzi wa Mahakama katika mkoa wa Arusha na Manyara.

Prof. Kabudi apokea Salamu za Pongezi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China

$
0
0

Mheshimiwa Prof. Palamagamba J. Kabudi (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, leo tarehe 13 Machi, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa WANG Ke, Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China.

Mheshimiwa WANG Ke pamoja na masuala mengine amewasilisha kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki barua ya pongezi kutoka kwa Mheshimiwa Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China kufuatia Prof. Kabudi kuteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

Aidha Prof. Kabudi kupitia kwa Mheshimwa Balozi ameshukuru kwa salamu hizo za pongezi alizopokea.

Katika mazungumzo yao, Prof. Kabudi na Balozi WANG Ke, wameahidi kufanya kazi kwa pamoja ili kuimarisha ushirikiano wa kihistoria baina ya nchi hizo mbili. Na kwa pamoja wamesisitiza umuhimu wa kuendelea na jitihada za kuimarisha mahusiano ya kisiasa, kijamii, kiuchumi hususan kwenye maeneo la uwekezaji, biashara, utalii na miundombinu.
                                                                      
Prof. Kabudi ametumia fursa hiyo kuishukuru Jamhuri ya Watu wa China kwa misaada ya kimaendeleo wanayoendelea kuitoa na kwamba Serikali inafurahishwa na Jinsi China inavyounga mkono jitihada zake za kuwaletea wananchi maendeleo na kujenga uchumi.

Tanzania na China zimekuwa na mahusiano ya kidiplomasia tangu mwaka 1964 na mwaka huu zinatarajia kuadhimisha miaka 55 ya ushirikiano huo.

Mheshimiwa Wang amekuwa Balozi wa kwanza kuonana na Mhe. Kabudi tangu kuteuliwa kwake na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuiongoza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
13 Machi 2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akipokea barua ya pongezi kutoka kwa Balozi wa China nchini, Mhe. WANG Ke. Balozi wa China aliwasilisha barua hiyo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Mhe. WANG Yi ambapo anampongeza Prof. Kabudi kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mhe. Prof. Kabudi akisoma barua ya pongezi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambayo iliwasilishwa wizarani na Balozi wa China nchini.

Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China mara baada ya kupokea barua ya pongezi.

Prof. Kabudi na Dkt. Mahiga wakabidhiana majengo ya ofisi za Wizara zao na Ofisi

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akimkabidhi Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, mchoro wa jengo la Ofisi za Wizara ya Mambo ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zinazojengwa kwenye Mji wa Serikali uliopo Mtumba, Dodoma. Makabidhiano hayo yalifanyika tarehe 12 Machi 2019. Baada ya kukabidhiwa Prof. Kabudi alipongeza jitihada za Wizara chini ya usimamizi wa Mhe. Dkt. Mahiga kwa hatua kubwa iliyofikiwa kwenye ujenzi huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome akitoa maelezo mafupi kwa Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria walipofika  kwenye ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria zinazojengwa kwenye mji wa Serikali uliopo, Mtumba jijini Dodoma kwa ajili ya makabidhiano.
Mhe. Prof. Kabudi na Mhe. Dkt. Mahiga wakiwa kwenye moja ya chumba cha jengo la  ofisi za Wizara  zinazojengwa Mtumba


Mhe. Prof. Kabudi akisalimiana na mmoja wa Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alipotembelea ofisi za Wizara zinazojengwa Mtumba
Mhe. Prof. Kabudi akiongozana na Mhe. Dkt. Mahiga kuelekea kwenye jengo la Wizara, Mtumba
Mhe. Prof. Kabudi akisaini kitabu cha wageni na kutoa maoni yake kuhusu maendeleao ya ujenzi  wa ofisi hizo 
Mhe. Prof. Kabudi na Mhe. Dkt. Mahiga wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo na mafundi wanaojenga jengo la ofisi za Wizara zilizopo Mtumba
Muonekano wa jengo la ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki linalojengwa kwenye mji wa Serikali uliopo Mtumba, Dodoma



Waziri wa Katiba na Sheria ambaye awali alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akikabidhi Taarifa ya Makabidhiano ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.  Prof. Palamagamba Kabudi ambaye awali alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Makabidhiano hayo yalifanyika jijini Dodoma tarehe 12 Machi 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi (kushoto) akimkabidhi Taarifa ya Makabidhiano ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiweka saini Kitabu cha mahudhurio mara baada ya kukabidhiwa ofisi jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi mara baada ya makabidhiano ya ofisi.
Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakishuhudia makabidhiano ya ofisi kati ya Waziri wa Katiba na Sheria na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiongea na Wakuu wa Idara na Vitengo (hawapo pichani) baada ya kukabidhiwa ofisi na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga.
Wakuu wa Idara na Vitengo wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hayupo pichani).
Wakuu wa Idara na Vitengo wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiongea na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi Savera Kazaura akitoa maelezo kwa  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Waziri wa Katiba na Sheria kabla zoezi la makabidhiano kuanza.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akisalimiana na baadhi ya watumishi mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Anayemkaribisha  ni mmoja wa watumishi hao, Bw. Shaban Mtambo.
Bi. Chiku Kiguhe akisalimiana na Mhe. Prof. Kabudi.
Bw. Habibu Ibrahim akisalimiana na Mhe. Waziri.
Bw. Maulidi Mkenda akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiongea na baadhi ya watumishi waliojitokeza kumpokea mara alipowasili kwa mara ya kwanza katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje jijini Dodoma.
Bw. Caesar Waitara akisalimiana na Mhe. Prof. Kabudi

IRELAND HAILS PARTNER STATES' COMMITMENT TO EAC INTEGRATION

$
0
0
cid:image003.jpg@01D4D5C8.6F6284D0
EAC Secretariat
 The EAC Director of Trade, Alhaj Rashid Kibowa (right) in discussions with the Irish Ambassador to Tanzania and EAC, H.E. Paul Sherlock (second right), at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania. Also in the photo are Mr. Kenneth Gitonga of the Irish Embassy in Nairobi and Ms. Monica Mihigo of the EAC Trade Directorate.

                         The Irish Ambassador to Tanzania and EAC, H.E. Paul Sherlock (third left) with the EAC Director of Trade, Alhaj Rashid Kibowa, after bilateral discussions at the EAC Headquarters. Also in the photo are from left Mr. Stephen Analo and Ms. Flavia Busingye of the EAC Secretariat and Mr. Kenneth Gitonga of the Irish Embassy in Nairobi.

East African Community Headquarters, Arusha, 12th March, 2019:
 The Republic of Ireland has hailed the commitment of the six East African Community (EAC) Partner States to the EAC integration process.

Ireland’s Ambassador to Tanzania and the EAC, H.E. Paul Sherlock, further disclosed that his country would continue to promote trade and development cooperation between his country and the EAC.

Amb. Sherlock said that Ireland’s experience within the European Union was that every regional integration process has its challenges which can be surmounted through negotiations by the member countries.

Amb. Sherlock said that Ireland would continue to provide support to EAC integration initiatives through TradeMark East Africa, a not-for-profit company established in 2010 to support the growth of regional and international trade in East Africa. 

The Irish envoy was speaking when he paid a courtesy call at the EAC Headquarters where he held discussions with senior officers from the EAC Directorates of Customs and Trade. At hand to receive the Ambassador was Alhaj Rashid Kibowa, the Director of Trade at the EAC Secretariat.

In his remarks, Alhaj Kibowa informed the Amb. Sherlock that the Community was increasingly encouraging bilateral mechanisms among Partner States to resolve Non-Tariff Barriers (NTBs) to trade.

Alhaj Kibowa said that all EAC Partner States assented to the EAC Elimination of NTBs Act 2017, adding that NTBs were continuously being addressed by stakeholders at all levels of the Community.

Alhaj Kibowa further said that the Community had embarked on ambitious infrastructure development in the roads, railways, ports and energy sectors to spur economic growth and trade in East Africa.

Accompanying the Ambassador at the discussions were Mr. Robert Hull, Second Secretary at the Embassy of Ireland in Dar es Salaam and Mr. Kenneth Gitonga, Commercial Attaché at the Irish Embassy in Nairobi.  

With Alhaj Kibowa from the EAC Secretariat were Mr. Stephen Analo, Principal Customs Officer (Capacity Building), Ms. Flavia Busingye, Principal Compliance and Enforcement Officer, and Ms. Monica Mihigo, Principal Internal Trade Officer.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU NA KAMATI YA PAC YAKAGUA MIRADI YA UJENZI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Moshi Selemani Kakoso, akisisitiza jambo kwa  Naibu Mawaziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa na Atashasta Nditiye, wakati kamati hiyo ilipokagua ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Dodoma.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati kamati hiyo ilipokagua ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Dodoma. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Moshi Selemani Kakoso.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Atashasta Nditiye, akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Moshi Selemani Kakoso, wakati kamati hiyo ilipokagua ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Dodoma. 
 Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Dodoma,  Bertha Bankwa, akielezea mkakati wa uboreshaji wa kiwanja hicho kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati kamati hiyo ilipokikagua.
 Muonekano wa barabara ya kuruka na kutua ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Dodoma. Barabara hiyo imerefushwa kutoka mita 2,000 hadi mita 2,500.
 Mhandisi Kedrick Chawe kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS), akionesha ramani ya Kiwanja cha Ndege cha Msalato kitakavyokuwa mara baada ya awamu ya kwanza ya ujenzi wake kukamilika kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati kamati hiyo ilipokagua eneo ambalo kiwanja hicho kitajengwa.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akisoma taarifa ya mradi wa barabara ya Iringa-Dodoma (Km 260) kwa wajumbe wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), katika Ofisi za Bunge jijini Dodoma, leo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Naghenjwa Kaboyoka, akikagua ubora wa lami katika eneo la Nkulabi, barabara ya Iringa-Dodoma (Km 260), wakati kamati hiyo ilipokagua barabara hiyo leo.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi John Ngowi, akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), walipokagua barabara ya Iringa-Dodoma (Km 260).
Muonekano wa Barabara ya Iringa -Dodoma (Km 260) sehemu ya Migori- Fufu (Km 93.80) ambayo ujenzi wake umekamilika kwa kiwango cha lami.

KAIMU MKURUGENZI SHABANI MIRAO ALILIA MICHEZO KWENYE HALMASHAURI YA CHALINZE

$
0
0
Karim Juma Lugoba- Chalinze
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze  Shabani Mirao amefungua jukwaa la michezo kwenye halmashauri hiyo ambalo limeanzishwa kwa kutumia mapato ya ndani ambayo yanasimamiwa na idara ya elimu msingi na kuweza kutoa nia yake ya kujenga timu moja ambayo itakayofanya kushiriki kwenye ligi mbalimbali.Tamasha limefunguriwa lugoba kwenye uwanja wa msingi tarehe 13/03/2019 majira ya saa 10:00

 Mirao aonesha kilio chake kwa vijana kukosa ajira na kusubiria ajira na wakati tunatambua kwamba dunia nzima inachangamoto ya ajira kwasasa njia rahisi kutumia michezo kuweza kupunguza swala la ajira na kujenga afya mwili  na kuweza kupunguza changamoto za uwarifu kwenye jamii zetu .

Hata hivyo Mirao uamkuta kijana ana elimu nzuri tu ukiangaria nafsi zilizotoka na waliomba ni wengi waliomba kuliko nafsi kwanini sisi vijana tusitumie michezo kwa kupata kipato njie ya kutegemea ajira za serikalia tubadirike kulingana na mazingira yalivyo.

Afisa Elimu Msing Mwl. Zainabu Makwinya amesema kwamba idara ya elimu imejipanga kikamilifu kuanzisha ligi ambayo itakayoweza kutoa vijana na kuwa timu ya halmashauri ya chalinze na pia ni fursa kubwa kwa vijana kuweza kupata ajira.

Makwinya amesema kwamba uwamasishaji wa michezo upande kwa wanawake ni mkubwa na hata iyo ligi ikianza lazima wanawake  watashiriki kulingana na michezo yote itakayoanzishwa na tumeshapata wachezaji ambao wanauwezo mkubwa wakucheza kwa upande wa netball .

Makwinya amesema kwasasa jamii lazima ibadiriki kulingana na fikra tofauti za watu kwamba michezo ni burudani hapana kwasasa michezo ni ajira kubwa sana na hata ukiangaria mapato ya wachezaji ni makubwa , Hivyo wananchi naomba watumie fursa hii ambayo idara tunaianzisha.

Afisa  Utamaduni wa Halmashauri ya Chalinze Bi. Ester Kalale amesema kwamba kwasasa wananchi wasiogope kuwatumia wao maana wao wanafahamu aina mbalimbali za michezo na yupo tayari kupitia timu moja hadi nyingine kufundisha aina za michezo .

Kalale amesema fursa kubwa kwa tamasha hili la michezo ambalo limefunguliwa na kuonesha mwanga wa ajira kwa vijana .Pia michezo ndo njia rahisi sana kutambuana kwa haraka na njia ya kudumia amani ya nchi yetu na kuongeza upendo kwa kila mmoja wetu .naomba wananchi wanitumie mimi kwa michezo na kupandisha vipato vya ajira .

MIGOGORO YA ARDHI YAMRUDISHA WAZIRI LUGOLA MKOANI MOROGORO

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola anatarajia kuwasili kwa mara nyingine Mkoani Morogoro leo, kwa ajili ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imeibua mifarakano baina ya wananchi Mkoani humo.
Waziri Lugola, wiki iliyopita alimaliza ziara yake Mkoani humo iliyokuwa na lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi kuhusiana na utendaji kazi wa Taasisi za Wizara yake.
Lugola katika ziara yake Mkoani humo, alifanya mikutano ya hadhara ambapo alikutana na migogoro mbalimbali lakini kero kubwa kati ya hizo ni kuhusiana na ardhi ambayo inapelekea wananchi kuwekeana chuki, kujeruhiana, kufikishana Polisi pamoja na kuuana.
Kati ya Wilaya tatu alizozitembelea alipokuwa Mkoani humo, ni Morogoro, Mvomero na Kilosa, licha ya wananchi kutoa kero zao mbalimbali, mgogoro wa ardhi uliibuka kwa sehemu kubwa hasa katika Wilaya ya KIlosa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Waziri Lugola alisema alipokuwa Wilaya ya Kilosa, alikutana na mgogoro wa ardhi ambapo umeleta mgawanyiko miongoni mwananchi hivyo akawaahidi kurejea tena Wilayani humo kwa ajili ya kutatua kero zao baada ya kukutana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Lugola alisema mipango yote ipo sawa, hivyo anatarajia kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Kilosa Kesho Machi 15 Wilayani humo ili kuwapa majibu ya kero zao pamoja na kumaliza mgogoro wa ardhi unaowakabili. 
“Migogoro mingi inaletwa vituo vya polisi hasa Wilaya ya Kilosa, na wananchi katika mikutano yangu ya hadhara wanalalamika kuhusiana na ardhi, baadhi wanawalaumu polisi wangu kutokuwatendea haki na wengine pia wanawapongeza kwa kazi nzuri, na wengi wao wanalalamikia kuwa matajiri ndio wananyang’anya ardhi zao wakitumia fedha kwa wakiwahonga Polisi,” alisema Lugola.
Aliongeza kuwa, alipokuwa katika mkutano wake wa mwisho katika Tarafa ya Kimamba, Wilaya ya Kilosa Mkoani humo, kuliibuka na hoja nyingi za migogoro ya ardhi, kutokana na usugu wa tatizo hilo, aliwaahidi wananchi wa Wilaya hiyo atarejea tena kwa ajili ya kutatua mgogoro huo.
“Ziara yangu niliikatisha katika Mkoa huo, kwa ajili ya kwenda Dar es Salaam kuhudhuria kikao cha Baraza la Mawaziri, hata hivyo, niliwaahidi wananchi nitakutana na Waziri wa Ardhi, ili tushirikiane kutatua mgogoro huu ambao unaweza ukaleta vurugu kubwa pale Kilosa na Mkoa wa Morogoro kwa ujumla,” alisema Lugola.
Lugola anatarajia kufanya mkutano mwingine wa hadhara kuleta majibu ya ahadi alizowaahidi wananchi hao pamoja na kusuluhisha mgogoro huo ili wananchi waendelee kufanya shughuli zao za maendeleo. 
Waziri huyo alisema, hawezi kukaa ofisini huku wananchi wakiwa wanapata matatizo mitaani, hivyo atazunguka nchi nzima kuzungumza na wananchi na kupokea kero mbalimbali zinazowakabili.  
“Wananchi wanapojitokeza kwa wingi inasaidia kusikiliza matatizo yao yanayowakabili, ndio mana nimepanga kufanya ziara kama hizi nchi nzima, hii inasaidia sana kujua matatizo mbalimbali ya wananchi pamoja na kuangalia utendaji kazi wa Taasisi zangu zilizopo ndani ya Wizara hii, na hakika Serikali ya Dokta Magufuli inawajali wananchi wake ndio mana inawafuata mahali walipo, ili wazungumze na Serikali yao uso kwa uso,” Alisema Lugola. 
Lugola alisema Taasisi zilizopo ndani ya Wizara yake ambazo ni Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Idara ya Probesheni na Huduma kwa Jamii, zifanye kazi za kiweledi bila kuwaonea wananchi.

VIJANA WA UMRI CHINI YA MIAKA 25 HATARINI KUAMBUKIZWA VVU

$
0
0
UWEZEKANO wa Vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 kushindwa kutimiza ndoto zao za maisha ni mkubwa endapo hawatapata elimu sahihi ya afya ya uzazi na maambukizi ya Ukimwi (VVU) itakayowasaidia kufanya maamuzi sahihi kwa mstakabali wa maisha yao. Kundi hilo liko kwenye hatari hiyo kutokana na kukabiliwa na changamoto za ongezeko la maambukizi mapya ya VVU na mimba za utotoni kwa sababu ya uelewa mdogo (elimu) na upungufu wa huduma rafiki za afya ya uzazi na VVU kwa vijana.

Akizindua Jukwaa la Vijana ( SITETEREKI  Najifunza Kila Hatua ) kaimu Katibu Tawala wa msaidizi Mkoa wa Mwanza Emily Kasigara alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya wakishirikiana na Mradi wa USAIDI Tulonge Afya fhi 360 imeanzisha jukwaa hilo  la vijana ili kuwajengea uwezo katika masuala ya afya ya uzazi na Ukimwi, wajitambue na kubadilisha tabia zao. Alisema serikali, jamii na wadau wana kazi kubwa ya kuwaelimisha vijana kujitambua , wakijitambua na kujali afya zao kutakuwa na matokeo chanya kwao na watafanya maamuzi sahihi, hawatachezea afya zao na kuwahimiza waende vituo vya huduma za uzazi na kupima afya.

 “Jukwaa la SITETEREKI Najifunza kila hatua  litakuwa kimbilio la vijana kufikia maisha wanayoyahitaji kwani ni eneo muhimu ambalo ni nguvu kazi na taifa la kesho, watapata mahali pa kutoa dukuduku zao na watajengewa uwezo.Lengo la serikali wafikiwe ili wasijiingize kwenye changamoto zinazowaharibu na kuhatarisha maisha yao ya baadaye,”alisema Kasigara.

 Alisema serikali imeanzisha jukwaa hilo litakalowawezesha kuwa na maisha bora baada ya kujengewa uwezo  na kujitambua watatimiza azma ya serikali ya Tanzania ya uchumi wa kati wa viwanda kwani familia ikiwa duni kiafya haitakuwa na mchango kwenye uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake Mratibu wa Elimu Afya ya Uzazi Wizara ya Afya  Dk. Gerald Kihwele alisema licha vijana kuwa tegemeo kiuchumi wanakabiliwa na changamoto nyingi ambapo vijana wa umri wa miaka 15 hadi 24 sawa na asilimia 40 wana maambukizi ya VVU, kati ya hao asilimia 70 ni wasichana na ndio wanaokabiliwa na hatari ya maambukizi mapya. 

Alisema ni asilimia  41 tu ya vijana wa kiume wanaozingatia njia za afya ya uzazi na wanatumia kinga kwa usahihi wakati wa kujamiiana huku wasichana wanaopata huduma hizo wakiwa ni asilimia 37 na ndio wenye changamoto kubwa hivyo wakijengewa uwezo watajitambua na kusimama kwenye misimimo thabiti.  Dk. Kihwele alieleza kuwa serikali inafanya jitihada kubwa za kuweka mazingira bora ya huduma ya afya ya uzazi kwa vijana na kuwafanya wawe sehemu ya mipango yake, hivyo lazima kuwe na huduma za viwango vya  kuwavutia na kuchochea fikra zao waende kwenye maeneo ya kutolea huduma.

“Upatikanaji wa huduma rafiki za afya ya uzazi kwa vijana bado si za kuridhisha ni asilimia 30 hivyo hatuwezi kuwavutia vijana waende kupata huduma hizo ambapo  serikali zifikie asilimia 80 na ipo haja mitizamo ya watoa huduma ivutie na kuhamasisha vijana wazichangamkie,”alisema Dk. Kihwele.

 Naye Mshauri Mwandamizi wa SBCC Shahada Kinyanga alisema vijana hupewa  taarifa zisizo sahihi na wanakosa motisha ya kufikia malengo yao kimaisha  hivyo jukwaa la SITETEREKI  litajibu changamoto zao na kuibua hisia za kufikia matarajio na mahitaji yao,litawaongezea ukweli kabla ya kujiingiza kwenye uhusiano  na kufanya uamuzi sahihi.

“Tunalenga maeneo yatakayonyesha mafaikio makubwa  katika kuboresha afya za vijana wa Kitanzania wa umri wa miaka 15 hadi 24hasa huduma za afya ya uzazi kabla ya ujauzito,upimaji wa VVU na tohara ya hiari kwa wanaume.Baadaye tutahusisha vipaumbele vya jamii na kimaisha kwani takwimu zinaonyesha VVU na mimba za utotoni husababisha afya duni na vifo kwa vijana,” Kinyanga.

Alisema jukwaa hilo ambalo lipo  chini ya Wizara ya Afya,ndani ya mradi wa  miaka mitano wa USAID Tulonge Afya wanalenga kuwafikia vijana 22,800 kwa mwezi kwa kuwatumia wahamasishaji 520  katika Kanda ya Ziwa  na Magharibi na kati ya wahamasishaji hao 270 ni wasichana. 
 Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Emil Kasigara akizindua rasmi Jukwaa la “SITETELEKI” litakalozungumzi maswala ya Afya hususani Vijana chini ya mika 25 ili waweze kujitambua na kuwa na tabia chanya.Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza. 
 Mtaalamu wa maswala ya Afya kutoka Wizara ya Afya, Gerald Kihwele akiwakilisha maada ya “SITETELEKI” kwa wadau wa Afya(hawapo pichani) litakalozungumzia maswala ya Afya kwa Vijana chini ya miaka 25 mara baada ya uzinduzi wa Jukwaa hilo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza.
Wadau wa Afya kutoka sekta tofauti wakisiliza maada mara baada ya uzinduzi wa Jukwaa la “SITETELEKI” litakazungumzia maswala ya Afya haswa kwa Vijana chini ya miaka 25 uliofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Mwanza.

SHEIKH NURDIN KISHK NA WENZIE WAKWEA BOMBADIER KWENDA BURUNDI

TAARIFA ZA MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO

$
0
0


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu 14 kwa tuhuma za makosa mbalimbali.


MAUAJI

Mnamo tarehe 13.03.2019 majira ya saa 13:30 mchana huko Kitongoji cha Igadu, Kijiji cha Shuwa, Kata ya Iyunga – Mapinduzi, Tarafa ya Isangati, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya. TAMKA D/O MAMBA @ NGANGALE [28] Mkazi wa Kitongoji cha Masanga “A” aligundua kuuawa kwa mume wake aitwaye HADSON S/O HAIWOLE MWANGOKA [45] Mkazi wa Masanga “A” na mtu/watu wasiofahamika.


Marehemu aliondoka nyumbani tarehe 11.03.2019 saa 05:00 alfajiri kwenda shambani Kitongoji cha Igadu na hakurudi tena, harakati za kumtafuta zikaanza wakiwa wanamtafuta maeneo ya shambani kwenye korongo ndipo waliona kiganja cha mkono wa kulia kikiashiria kuna mwili wa marehemu umefukiwa.


Polisi walifika eneo la tukio na kukuta kiganja cha mkono korongoni na baada ya kufukua ulikutwa mwili wa marehemu aliyetambuliwa kuwa ni HADSON HAIWOLE MWANGOKA huku ukionekana kupigwa kitu kizito usoni. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali Teule ya Ifisi. Kiini cha tukio ni mgogoro wa ardhi/shamba la ukoo ambalo alikuwa analima marehemu ambalo linagombewa na wana ndugu baada ya baba yao kufariki dunia.


Watu nane wamekamatwa kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo ambao ni 1. PAULO HAIWOLE MWANGOKA [39] mchungaji na mkazi wa Kijiji cha Sanje 2. FREDRICK MOSES [36] Mkazi wa Iwindi 3. JOSHUA HAIWOLE [27] Dereva na mkazi wa Mlima reli 4. MICHAEL HAIWOLE [18] Mkazi wa Shuwa 5. ELIZABETH HAIBOLE [62] Mkazi wa Shuwa 6. JACOB S/O NOAH [51] Mkazi wa Izuo 7. ELIZA SHEYO [40] Mkazi wa Shua na 8. ERESIA HAIBOLE [64] Mkazi wa Shuwa. Upelelezi wa shauri hili unaendelea.



TAARIFA YA KIFO


Mnamo tarehe 12.03.2019 majira ya saa 13:45 mchana huko Kitongoji cha Uzunguni, Kijiji cha Idimi, Kata ya Ihango, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya. Watoto wawili waliofahamika kwa majina ya 1. CLAVERY MASHAKA [05] na 2. GIFT MASHAKA [03] wote wakazi wa Idimi walifariki dunia baada ya kusombwa na maji ya mvua yaliyopita kwenye mfereji uliopo karibu na nyumba yao.

Chanzo cha tukio hili ni mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha na kutiririsha maji mengi yaliyosababisha vifo vya watoto hao.


TAARIFA YA KIFO.


Mnamo tarehe 13.03.2019 majira ya saa 15:00 Alasiri huko maeneo ya Mtaa wa Lusungo, Kata ya Itende, Tarafa ya Iyunga, Mkoa wa Mbeya, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la EZEKIEL BONNY @ MWAKAPESA, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 28 – 30 na mkazi wa Itende alifariki dunia alipokuwa akiogelea kwenye mto Karabwe uliopo mtaa wa Lusungu.

Chanzo cha kifo chake inasemekana kuwa marehemu alikuwa na tatizo la ugonjwa wa kifafa ambacho kilimtokea akiwa anaogelea kwenye Mto huo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa uchunguzi zaidi wa kitabibu.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa tahadhari kufuatia matukio ya kufa maji yanayosababishwa na uzembe wa kutovaa maboya wakati wanapoingia majini, mtoni au ziwani. Aidha kufuatia mvua zinazonyesha nawasihi wazazi/walezi kuwa makini na watoto wao kwa kuweka uangalizi wa kutosha ikiwa ni pamoja na kuwapeleka watoto wadogo Shuleni na kuwapokea ili kuwalinda dhidi ya madhara ya kutumbukia katika maji au kusombwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali.


KUPATIKANA NA BHANGI.

Mnamo tarehe 13.03.2019 majira ya saa 10:45 asubuhi huko katika Kitongoji na Kijiji cha Matondo, Kata ya Matundasi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakiwa doria walimkamata JOHN RICHARD [24] Mkazi wa Kijiji cha Ifyenkenya akiwa na bhangi uzito wa gram 25. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa bhangi.

KUPATIKANA NA POMBE YA MOSHI NA MTAMBO WA KUPIKIA POMBE YA MOSHI.


Mnamo tarehe 13.03.2019 majira ya saa 12:00 mchana huko maeneo ya Sinde “B” Kata ya Sinde, Tarafa ya Iyunga ndani ya Jiji na Mkoa wa Mbeya, Polisi walimkamata ANATALIA MATUMLA [44] Mkazi wa Sinde “B” akiwa na pombe ya moshi lita 20 pamoja na mtambo wa kupikia pombe ya moshi. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo.


KUPATIKANA NA POMBE YA MOSHI NA MTAMBO WA KUPIKIA POMBE YA MOSHI

Mnamo tarehe 13.03.2019 majira ya saa 01:30 usiku huko maeneo ya Sinde, Kata ya Sinde, Tarafa ya Iyunga ndani ya Jiji na Mkoa wa Mbeya, Polisi walimkamata STELIA ANDALISYE [60] Mkazi wa Sinde akiwa na pombe ya moshi lita 04 pamoja na mtambo wa kupikia pombe ya moshi. Mtuhumiwa ni muuzaji/mtengenezaji na mtumiaji wa pombe hiyo.


KUPATIKANA NA POMBE YA MOSHI

Mnamo tarehe 13 03.2019 majira ya saa 11:30 asubuhi huko maeneo ya  Kata ya Ruanda, Tarafa ya Iyunga ndani ya Jiji na Mkoa wa Mbeya, Polisi  walimkamata MAGRET KENYA [45] Mfanyabiashara na Mkazi wa Mwanjelwa akiwa na Pombe ya moshi lita18. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo.


KUPATIKANA NA MTAMBO WA KUPIKIA POMBE YA MOSHI.

Mnamo tarehe 13.03.2019 majira ya saa 12:00 mchana huko maeneo ya Ilolo, Kata ya Isanga, Tarafa ya Sisimba ndani ya Jiji na Mkoa wa Mbeya. Polisi walimkamata DORICE GEORGE [16] Mkazi wa Ilolo akiwa na mtambo wa kupikia pombe ya moshi. Mtuhumiwa ni mtengenezaji na muuzaji wa pombe hiyo.


KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI NA POMBE YA MOSHI.

Mnamo tarehe 13.03.2019 majira ya saa 14:30 mchana huko Kitongoji cha Mamba, Kijiji na Kata ya Mamba, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, Polisi wakiwa doria walimkamata LUCY ISDORY [47] Mkazi wa Mamba akiwa na vipande15 vya nyama ya Pundamilia vyenye uzito wa kilogram 20 na Pombe Moshi lita 15 akiwa amehifadhi ndani ya nyumba yake. Upelelezi unaendelea ili kubaini mtandao wa wawindaji haramu na kuwakamata.

Watuhumiwa wote watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.


Imesainiwa na:

[ULRICH O. MATEI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA




SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UGENI KUTOKA TPB BENKI TAWI LA DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Meneja wa TPB Benki Tawi la Dodoma, Edward Mlowo (katikati) alipomtembelea leo tarehe 14 Machi 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Afisa Mikopo TPB Benki Tawi la Dodoma, Hamis Salehe
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Meneja wa TPB Benki Tawi la Dodoma, Edward Mlowo (katikati) walipomtembelea leo tarehe 14 Machi 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Afisa Mikopo TPB Benki Tawi la Dodoma, Hamis Salehe
Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati) katika picha ya pamoja na Meneja wa TPB Benki Tawi la Dodoma, Edward Mlowo (kulia), Afisa Mikopo TPB Benki Tawi la Dodoma, Hamis Salehe (kushoto) walipomtembelea leo tarehe 14 Machi 2019 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Acacia yazungumza na Serikali kunusuru Mgodi usifungwe

$
0
0
Na Issa Mtuwa, Dodoma 
Uongozi wa Kampuni ya Acacia kupitia Mgodi wa North Mara umezungumza na Serikali kuelezea hatua zilizochukuliwa hadi sasa kudhibiti maji yenye sumu ikiwa ni wiki moja tu ipite tangu Waziri wa Madini Doto Biteko, atangaze kufunga shuguli za mgodi huo endapo utashindwa kudhibiti maji ya sumu yanayotiririka kwenye makazi ya watu, ifike Machi 30 mwaka huu.
Tamko hilo la serikali limeifanya kampuni ya Acacia kuchukua hatua za haraka za kudhibiti maji hayo ili kukwepa rungu la serikali la kuufunga mgodi huo.  Machi 12, uongozi wa Acacia North Mara ulikutana na Waziri Biteko ofisini kwake jijini Dodoma kwa lengo la kueleza hatua iliyofikiwa ya kutekeleza agizo la serikali. 

Uongozi wa kampuni hiyo ukizungumza katika kikao hicho, ulieleza kuwa, tayari mgodi huo umechukua hatua za haraka tangu kutolewa kwa agizo na kwamba hadi sasa suala la kudhibiti maji yenye sumu limeshetekelezwa na hakuna maji yanayotiririka kuelekea kwenye makazi ya watu.
Aidha, ulimweleza kuwa, pamoja na kudhibiti maji hayo kupitia bwawa la kuhifadhia maji yenye sumu yajulikanayo kitaalam kama “topesumu” (Tailings Storage Facility- TSF) mgodi umeanza kuchukuwa hatua za kujenga TSF mpya. 

“Mhe. Waziri tumekuja kutoa mrejesho wa utekelezaji wa agizo lako, tunafurahi kukuambia kuwa tumetekeleza agizo hilo na kwa sasa hakuna maji yanayotiririka. Pamoja na hatua hiyo mgodi umeanza mchakato wa ujenzi wa bwawa jipya (TSF) la kuhifadhia topesumu,” walieleza.

Aidha, ulimweleza Waziri Biteko kuhusu hujuma za uharibifu wa miundombinu ya bomba la maji yenye sumu unaofanywa kwa maksudi na wakazi wanaozunguka mgodi ili kufifisha juhudi zao za kudhibiti maji hayo wakiwa na lengo la kuufanya mgodi uonekane haujachukuwa hatua kudhibiti jambo hilo, ambapo walionesha picha mbalimbali ya namna bomba lilivyo pasuliwa ili maji yatiririke kuelekeka kwa wananchi.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko alieleza kuwa, amepokea taarifa ya kampuni husika na kuwapongeza kwa hatua zilizochukuliwa na kusema kuwa, ukweli wa jambo hilo atauthibitisha mara baada ya kupata ripoti ya wataalam watakaokwenda kuhakikisha kuhusu utekelezaji wa agizo hilo na kuongeza,“katika hili sitanii juu ya kuufunga mgodi ikiwa utashindwa kudhibiti tope sumu,”.

 “Naomba nirudie tena katika hili sitanii, sitabadilisha msimamo wangu kama serikali na utaendelea kubaki pale pale dawa pekee ni kutekelezwa kwa agizo hilo. Lakini niseme ukweli, nasikitishwa sana na kitendo hiki cha wananchi kupasua bomba, kwa hili sikubaliani nao na siwaungi mkono.
 Pia, aliongeza kuwa, atawasiliana na Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya kuona namna ya kudhibiti hali hiyo ili wale watakao bainika wachukuliwe hatua.

Waziri Biteko alilitoa agizo hilo   Machi 6, alipoutembelea mgodi huo hapo kwa ziara ya kikazi  pamoja na kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyamongo wilaya ya Tarime.  
Waziri wa Madini Doto Biteko akiwa na viongozi wa Kampuni ya Acacia wa mgodi North Mara, ofisini kwake jijini Dodoma. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Mara, Agness Marwa. 


CONDOLENCE MESSAGE TO THE GOVERNMENT OF UGANDA AND THE FAMILY OF THE LATE AMB. JULIUS ONEN

$
0
0
cid:image003.jpg@01D4D5C8.6F6284D0
EAST AFRICAN COMMUNITY
                         East African Community Headquarters, Arusha, 14th March, 2019: 
The East African Community has learned with deep sorrow and grief of the passing on to glory of Amb. Julius Onen.

Amb. Julius Onen has been an instrumental player in EAC Affairs since it was re-established in 2000 until his death.

As a Permanent Secretary in the Ministry of Foreign Affairs, he was a very pro-active participant in the negotiations that led to the establishment of the EAC and the EAC Customs Union.

As Deputy Secretary General in the EAC Secretariat, he steered with zeal and selflessness the negotiations that led to the establishment of the EAC Common Market in 2010.

As a Permanent Secretary of Trade, he has been at the vanguard of trade integration in the EAC. When he was taken to India for treatment, he had just come from Arusha where he chaired a successful meeting of Permanent Secretaries of Trade.

EAC will remember Amb. Onen as an illustrious, selfless and avid integrationist, and above all, a distinguished international civil servant. 

Amb. Onen was an astute team leader wherever he worked and his legacy will remain in the minds of many of us.

The EAC extends its condolences to the family and Government of Uganda for this huge loss.

MAY HIS SOUL REST IN ETERNAL PEACE

Amb. Liberat Mfumukeko
SECRETARY GENERAL 

Arsenal matatani kufuzu robo fainali

$
0
0
Arsenal wana kazi kubwa mikononi mwao kama wanataka kuendelea kuuota ubingwa wa Europa mwaka huu. Arsenal walipoteza mchezo kwa mabao 3-1 dhidi ya klabu ya kawaida kabisa kutoka ligi ya Ufaransa kwenye mechi ya kwanza ya mzunguko wa 16 bora wiki iliyopita na kwa sasa sasa wanahitaji walau magoli mawili bila majibu ili kufuzu kwenda hatua ya Robo fainali.

Vijana wa Unai Emery walipata ushindi muhimu dhidi ya Manchester United jumapili na morali yao imeongezeka maradufu, hata hivyo Arsenal watakuwa bila beki wao Sokratis ambaye alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita. Kocha huyo anatarajia kumuanzisha mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Pierre Emerick Aubameyang ambaye alifunga kwa mkwaju wa penati dhidi ya Manchester United kwani anahitaji magoli zaidi ya kitu chochote ili aweze kufuzu.

Kwingineko Chelsea wako katika hali nzuri ukilinganisha na jirani zao wa jiji la London. Wao walifunga mabao 3-0 dhidi ya Dynamo Kyiv kwenye mchezo wa kwanza lakini walidondosha alama mbili siku ya jumapili walipokutana na Wolves kwenye ligi – matokeo ambayo yaliwafanya wasirejee katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi.

Kocha Maurizio Sarri anasema, “Ni kombe (Europa) la muhimu sana kwetu. Na kuna nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa kwa bingwa kwa hiyo lengo letu na ni muhimu kwetu kushinda.” Napoli ni timu nyingine iliyofanya vizuri wiki iliyopita baada ya kushinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Red Bull Salzburg, huku timu nyingine kutoka Serie A, Inter Milan ilitoka sare na Frankfurt walipokutana wiki iliyopita.

Ni StarTimes pekee ndio watakaokuonyesha ligi ya Europa kupitia chaneli zao za michezo. Arsenal vs Rennais saa 5:00 Usiku na utaonyeshwa LIVE kupitia ST World Football, Dynamo Kyiv vs Chelsea saa 2:55 Usiku nao pia utakuwa LIVE kupitia ST World Football.

RAIS WA TBF AKUTANA NA RC PAUL MAKONDA,WAPEANA MREJESHO UTEKELEZAJI MRADI WA UJENZI UWANJA WA NDANI KIKAPU.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akiwa na Rais wa Tanzania Basketball Federation (TBF) Phares Magesa, mara baada ya mazungumzo kuhusu maendeleo ya mpira wa Kikapu ambapo pia walipeana mrejesho kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndani wa kikapu katika mkoa wa Dar es Salaam, ujenzi wa uwanja wa ndani wa Kikapu na michezo mingine utaanza karibuni mara baada ya mazungumzo na wafadhili wa mradi kukamilika, TBF inamshukuru Mhe. 

Makonda kwa ushirikiano wake katika kuhakikisha mkoa wa Dar es Salaam unapata viwanja vya kisasa vya Kikapu na Michezo mingine na Shirikisho linaomba Wakuu wa Mikoa, viongozi wa ngazi mbalimbali na wadau wa maendeleo waige mfano wa Mhe. Makonda na Mhe. Anthony Mtaka katika kutatua changamoto ya miundombinu ya michezo nchini Tanzania, pia TBF inamshukuru sana Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli kwa kuwawezesha Makao Makuu Dodoma kupata mradi wa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo ambao nao utaanza karibuni kwa ufadhili wa Mfalme wa Morocco, www.tbf.or.tz

RC MWANRY AZINDUA JUKWAA LA SITETELEKI MKOANI TABORA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry akipiga makofi kwa kushirikiana na baadhi ya wadau wa Afya maya baada ya kuzindua Jukwaa la “SITETELEKI” litakalozungumzi maswala ya Afya hususani Vijana chini ya mika 25 ili waweze kujitambua na kuwa na tabia chanya.Uzinduzi huo ulifanyika jana Mkoani Tabora.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la “SITETELEKI” litakalozungumzia maswala ya Afya hususani Vijana chini ya mika 25 ili waweze kujitambua na kuwa na tabia chanya.Uzinduzi huo ulifanyika jana Mkoani Tabora.
Baadhi ya Vijana wa Mkoani Tabora wakimfuatilia Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry(hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la “SITETELEKI” litakazungumzia maswala ya Afya haswa kwa Vijana chini ya miaka 25 uliofanyika jana Mkoani Tabora.

WASHINDI 15 WAPATIKANA PROMOSHENI YA TIA KITU PATA VITUUZ NA DSTV

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
KAMPUNI ya Multichoice nchini  kupitia king'amuzi cha Dstv imechezesha droo ya tatu ya promosheni ya  tia vitu upate vituuzi jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa kitengo cha thamani kwa wateja Hilda Nakajumo wakati wa kutangaza washindi hao 15 waliopatikana katika kila vifurushi kama Compart plus, family,  premier pamoja na kifurushi cha bomba amesema ni wakati wa wateja kunufainika na na kuendelea kuuwasha kupitia king'amuzi hicho.

"Leo tumefanikiwa kupata washindi 15 kutoka mikoa mbalimbali kama vile Arusha, Kagera, Manyara pamoja na Dar es salaam na inaonyesha wazi kuwa  king'amuzi cha Dstv kinaendelea kutoa huduma nzuri na gharama nafuu, alisema Nakajumo"

Aidha amesema washindi hao wamezawadiwa malipo ya miezi miwili bure ili kuendelea kufaidika na vipindi mbalimbali kupitia King'amuzi cha Dstv.

Hata hivyo kwa upande wake Afisa Mwandamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha  Humud Abdulhussein amesema ni wakati wa wateja wa Dstv kulipia ving'amuzi vyao kwa wakati ili kupata ofa hiyo .

"Hakuna mtu ambaye anapangwa kwenye droo na pia inachezeshwa kwa haki bila ujanja wowote ambapo vigezo na masharti vinazingatiwa ipasavyo ," alisema  Abdulhussein.

Na Mshindi wa kifurushi cha Compart  mkazi wa jijini Mwanza Musa Juma mwenye umri wa miaka 24 amewapongeza Dstv kwa promosheni hiyo ya tia vitu pata vituuzi.

"Sikutegemea kama ningeweza kushinda katika droo hii ya tatu mara nyingi nasikia tu wenzangu wakishinda nikajaribu bahati yangu na nikaamua kulipia kwa wakati king'amuzi changu hatimae nimeibuka mshindi," alisema Juma

Pia amewapa ujasiri wateja wengine kulipa kwa wakati ili waweze kuingia kwenye droo hiyo na kushinda kabisa.
Mkuu wa kitengo cha thamani kwa wateja Kampuni ya Multichoice kupitia king'amuzi cha Dstv Hilda Nakajumo(katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi 15 waliopatikana katika droo ya tatu ya promosheni ya tia kitu pata vituuzi akiwa pamoja na  Afisa Mwandamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Humud Abdulhussein(kulia) .
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live


Latest Images