Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

WAHAMIAJI HARAMU 12 WAKAMATWA NA WATU WENGINE 14 WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI PWANI KWA MAKOSA YA UHALIFU MBALIMBALI

$
0
0


NA MWAMVUA MWINYI, PWANI

WAHAMIAJI haramu 12 raia kutoka Ethiopia ,wamekamatwa mkoani Pwani, eneo la Mwidu porini, Chalinze kwa kosa la kutokuwa na kibali kinyume na sheria.

Aidha watu 14 wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa makosa mbalimbali ya kiuhalifu ikiwemo wizi wa pikipiki na kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bangi.

Akielezea juu ya matukio hayo, kamanda wa polisi mkoa wa Pwani,ACP Wankyo Nyigesa, alisema usiku wa kuamkia march 8 ,askari polisi walipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu uwepo wa wahamiaji hao waliojificha kichakani eneo la Mwidu barabara ya Dar es salaam -Morogoro.

Alieleza baada ya polisi kufika eneo hilo waliwakamata wakiwa safarini kutoka Ethiopia kuelekea Afrika ya Kusini. :”Baada ya mahojiano ilionekana watu hao walifichwa hapo na mtu ama watu ambao bado hawajafahamika kwa lengo la kuwatafutia usafiri wa kuelekea nchini Afrika Kusini kutafuta ajira. “

Hata hivyo Wankyo alibainisha, afya ya wahamiaji haramu hao walikuwa wamedhoofika. Wakati huo huo jeshi hilo linawashikilia watu nane kwa kufanya uhalifu mbalimbali ikiwemo wizi wa pikipiki.Pia watu sita wamekamatwa kwa kupatikana na dawa za kulevya ikiwemo bangi kete 172.

Wankyo alielezea kwamba, baada ya mahojiano na upelelezi kukamilika watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria

.


Wanawake Wizara ya Habari waadhimisha Siku ya Wanawake kwa kutoa misaada Kituo cha Afya Chamwino.

$
0
0


 Mwenyekiti wa Wanawake Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Prisca Shewale akikabidhi vitu mbalimbali kwa  niaba ya wanawake wa Wizara hiyo kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Chamwino Dkt.Zipora Mfugale  kwa ajili ya wanawake, watoto na wenye uhitaji maalum waliolazwa kituoni hapo ikiwa ni kuamdhimisha Siku ya Wanawake Duniani leo Wilayani Chamwino.
PIC 2
Afisa Utumishi Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Jacquiline Kalua akimpa vifaa mbalimbali Bibi Marietha Maiko alielazwa Kituo Cha Afya Chamwino wakati wanawake wa Wizara hiyo walipotembelea kituo hicho katika kuamdhimisha Siku ya Wanawake Duniani leo Wilayani Chamwino.
PIC 3
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Lorietha Laurence akitoa vifaa mbalimbali kwa Bibi Regina Balabaido alielazwa Kituo Cha Afya Chamwino wakati wanawake wa Wizara hiyo walipotembelea kituo hicho katika kuamdhimisha Siku ya Wanawake Duniani leo Wilayani Chamwino.
PIC 4
Afisa Habari wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi.Lilian Lundo akitoa vifaa mbalimbali kwa Bibi Molen Mwaiko alielazwa Kituo Cha Afya Chamwino wakati wanawake wa Wizara hiyo walipotembelea kituo hicho katika kuamdhimisha Siku ya Wanawake Duniani leo Wilayani Chamwino.
PIC 5
Baadhi ya Wanawake Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Kituo Cha Afya Chamwino mara baada ya kutembelea Kituo hicho na kutoa misaada mbalimbali kwa wagojnwa waliolazwa kituoni hapo ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU POLISI JAMII KUKAMATA BODABODA, ASKARI POLISI KUKAMATA VYOMBO VYA MOTO BILA KUVAA SARE ZA JESHI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimfafanulia jambo Katibu wa Umoja wa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Morogoro, Juma Bega, alipokuwa akilalamika kuhusu Polisi Jamii kuwanyanyasa waendesha bodaboda, katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Mafisa B, Mwembesongo, mjini humo, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimfafanulia jambo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Regina Chonjo (katikati), mara baada ya kumaliza Kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, SACP-Wilbroad Mutafungwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akifurahi jambo wakati Mkuu wa Nidhamu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, Marko Nehemia, alipokuwa anajibu maswali yake kwa ufasaha katika Kikao cha Askari na Watumishi raia wa Wizara yake, kilichofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Umwema, mjini Morogoro, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Na Felix Mwagara, MOHA-Morogoro. 


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku Polisi jamii kukamata bodaboda zinazofanya makosa ya usalama barabarani nchini. 


Pia Waziri huyo amepiga marufuku polisi wa usalama barabarani kukamata vyombo vya moto wakiwa hawajavaa sare za Jeshi. 

Akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Mafisa, Kata ya Mwembesongo, mjini Morgoro, jana, Lugola alisema Polisi Jamii hawana ujuzi wa kijeshi wa ukamataji wa bodaboda hivyo kuendelea kuifanya kazi hiyo ni kuwanyanyasa wananchi. 

“Nimepata malalamiko mengi ninapofanya ziara zangu hapa nchini, wengi wanawalalamikia Polisi Jamii kuwaonea, kuwaomba rushwa na kuwakamata pasipofuata utaratibu unaotakiwa kijeshi, hapa Morogoro pia, katika mkutano huu wa hadhara mnayasema yale yale, sasa natangaza kuanzia leo, marufuku Polisi Jamii kukamata bodaboda,” alisema Lugola. 

Waziri Lugola pia alipiga marufuku baadhi ya Polisi wa Usalama barabarani ambao wenye tabia ya kutovaa sare za Jeshi na kuingia barabarani au mitaani na kuyakamata magari na bodaboda. 

Lugola alisema lazima polisi wafate sheria za usalama barabarani hasa wanapokamata magari yanayofanya makosa, uvaaji wa sare za Jeshi ni muhimu na unapaswa kufutwa. 

Waziri Lugola aliongeza kuwa, bodaboda au vyombo vingine vya moto, zinazovunja sheria za usalama barabarani zinapaswa kukamatwa bila kuwaonea huruma, ila ni kosa Polisi kuwanyanyasa vijana hao ambao wanapata ridhiki kupitia biashara hiyo. 

“Mnapaswa kukamata hizi bodaboda zinapofanya makosa, tabia ya kukurupuka huku mkitafuta fedha zisizo halali, huko ni kuwaonea waendesha bodaboda,” alisema Lugola. 

Lugola alifafanua kuwa, bodaboda zinazotakiwa kuwepo kituo cha polisi ni zile zilizopo katika makundi matatu ambayo ni Bodaboda zilizohusika kwenye uhalifu, zilizotelekezwa au zilizookotwa na zilizohusika katika ajali. 

“Bodaboida hizo ndizo zinapaswa kuwepo vituoni, lakini kuziweka bodaboda ambazo hazipo katika makundi hayo, napiga marufuku na hii nataka Polisi nchi nzima munielewe,” alisema Lugola. Pia Lugola aliwataka waendesha bodaboda mjini Morogoro na Tanzania kwa ujumla wafate sheria za usalama barabarani zikiwemo kuvaa kofia ngumu, kutokubeba abiria zaidi ya mmoja na pia wakiendesha wanapaswa kuwasha taa. 

Lugola ameanza ziara yake ya siku tatu mkoani humo akitembelea Wilaya za Morogoro, Mvomero, Kilosa na Gairo akisikiliza kero za wananchi pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake. 

Lugola mwaka jana alitoa maagizo kwa makamanda wa mikoa nchini ambayo ni dhamana zitolewe saa 24 katika vituo vyote vya polisi nchini, na pia kupiga marufuku tabia ya baadhi ya Polisi kubambikizia kesi wananchi, na pamoja na agizo la pikipiki zote zilizopo vituoni ziondolewe. 

Waziri Lugola amemaliza ziara Wilaya ya Morogoro na leo ataanza ziara yake katika Wilaya ya Movemero, na Machi 10, 2019 atamalizia Wilaya ya Gairo ambapo katika Wilaya hizo pia atazungumza na wananchi pamoja na watumishi waliopo ndani ya Wizara yake ambao ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Magereza, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Idara ya Probesheni.

TSC yashiriki Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani

$
0
0

 Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) wakiwa katika hali ya furaha wakati wa Maandamano ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Machi 8, 2019 jijini Dodoma.
2
Wafanyakazi wa TSC wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani jijini Dodoma.
3
Watumishi kutoka Taasisi mbalimbali wakiwemo wa Tume ya Utumishi wa Walimu wakiwa katika Maandamano ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika  jijini Dodoma.
4
Wafanyakazi wa TSC wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma.
5
Wafanyakazi wa TSC wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma.

TUKIMALIZA SIKU YA MWANAMKE, TUTAFAKARI MAISHA YA HOUSE GIRL

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MACHI 8 ya kila mwaka Tanzania huungana na mataiafa mengine duniani kusherehekea Madhimisho ya Siku ya Wanawake.
Hongereni wanawake wote  Tanzania.Machi 8 ya kila mwaka ni siku muhimu katika maisha yenu.Ndio siku ambayo hutumika kutafakari maisha ya wanawake waliko katika nyanja mbalimbali.Ndio siku ambayo hutumika kuweka mipango na mikakati ya kumkomboa mwanamke.
Ni jambo nzuri, ni jambo lenye tija na kubwa zaidi ni jambo lenye kuleta usawa kati ya wanawake na wanaume.Siku ya leo hutumika kuangalia haki sawa kati ya wanawake na wanaume.Ndio siku ambayo wanawake hukutana na kufanya mijadala, makongamano na mikutano ambayo kimsingi inaangalia changamoto zinazomzunguka mwanamke na kisha kutafuta ufumbuzi wake.
Ukweli wanaume wamefika mahali wamekubali na kumtambua mwanamke kama kiumbe mwenye thamani kubwa katika maisha ya mwanadamu.Mwanamke kimaumbile ndiye aliyepewa jukumu la kuleta mtanzania mpya duniani.Ndio mama zetu, ndio dada zetu, ndio bibi zetu, ndio shangazi zetu, ndio wake zetu.Hata wifi anapatikana humo humo katika kundi la wanawake.
Kwa kutambua thamani yao , Tanzania kama ambavyo zipo chini nyingine duniani waliamua kutumia Machi 8 ya kila mwaka kama sehemu ya kuadhimisha siku ya Wanawake ambayo huadhimishwa kwa njia mbalimbali lakini msingi mkuu ni kuona wametoka wapi, wako wapi na wanakwenda wapi.
Kwa Ujinga wangu najaribu kuitazama siku hii kwa jicho la aina yake sana.Ndio ambayo wanawake wakiitumia vizuri watatoka na muelekeo ambao utahitimisha kila aina ya unyanyasaji dhidi yao.Wakiitumia siku ya leo itatoa fursa ya kuwa na sauti kwenye jamii inayowazunguka.Wakiitumia vizuri maadhimisho ya siku ya wanawake watakuwa na nafasi pana ya kupigania na kutetea maslahi yao.
Nimeona na kushuhudia taasisi , masharika ,kampuni na maeno mbalimbali wakijadiliana namna ya kumkomboa mwanamke hasa kwa yale mambo ambayo bado wanaona hana nafasi.Ni ukweli usiopingika kuna baadhi ya sheria ambazo zimekuwa changamoto kwa mwanamke.Sheria kandamizi dhidi ya mwanamke zimekuwa zikipigiwa kilele.Ni wakati sahihi wa kuhakikisha yanafayika marekebisho kwa zile sheria ambazo zinalalamikiwa.
Sitaki kuzungumzia Sheria ya Ndoa ambayo nayo kwa muda mrefu inapigiwa kelele.Sitaki kuizungumzia maana mjadala wake ni mpana na unahitaji muda.Ninachotaka kumaanisha bado kuna sheria ambazo zinatumika nchini lakini kiuhalisia si rafiki kwa mwanamke na huenda zikawa chanzo cha kurudisha maendeleo yake nyuma.
Wakati naitafakari Siku ya Wanawake Duniani , ghafla nikaanza kuwaza na ule msemo usemao katika mafanikio ya mwanaume nyuma yake kuna mwanamke.Sikatai, ndio ukweli.Nipo kwenye jamii hii hii, natambua mchango mwanamke katika kuleta maendeleo kwa ngazi mbalimbali.Ukiona familia imefanikiwa na kupiga hatua ukifuatilia utabaini mchango mkubwa wa mwanamke.Iko hivi mwanamke akiyumba na nyumba lazima itayumba.Akiwa imara na nyumba itakuwa imara.
Hivyo hivyo katika ngazi nyingine za kimaamuzi.Katika maeneo ambayo wanawake wameamianiwa utaona mambo yanavyokwenda vizuri.Kinachonifurahisha mimi wanawake wengi ni waaminifu, wachapakazi na hodari katika kutekeleza majukumu yao.Hivyo wakati mnaitafakari siku ya mwanamke ni vema mkatafakari  namna nzuri ya kuendelea kuunganisha nguvu ambayo mwisho wa siku itamuacha mwanamke akiwa huru kwa kila kitu.
Kwa nchi yetu ya Tanzania, tumepiga hatua kutokana na jitihada ambazo zinaendelea za kuhakikisha mwanamke anakuwa na nafasi sawa na mwanaume.Tunakwenda vizuri na ndio
maana si ajabu kumuona Makamu wa Rais wa Tanzania ni mama .Tena ni mama shupavu na hodari.Huwa namuangalia Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan kisha napata somo kubwa kwamba Wanawake wanaweza.Hongereni.
Ushauri wangu, wanawake wakati mkienddelea kudai usawa, ni wakati sahihi pia wa kuangalia kama mwenendo wenu uko sahihi au laa.Naeleza hivyo kwasababu huwa naona kuna baadhi ya maeneo wanawake wanakwamishana wao kwa wao.Huwa natamani kusema adui wa mwanamke ni mwanamke.
Hivyo wakati mnajadili mengi kuhuu mfumo dume na changamoto nyingine, ni wakati sahihi wanawake wakabadilika na kutambua kabla ya kunyoosha vidole wanaume wakajinyooshea na wao wenyewe.Nikiri si wanawake wote lakini kwa sehemu kubwa wamekuwa na tabia ya kupigana vijembe, kuchongeana na baya zaidi hawataki kuona mwanamke mwenzao anafanikiwa.Hili ni tatizo ambalo linahitaji kupata ufumbuzi kwa mustakabali wa mwanamke wa Tanzania.
Yote ambayo nimeandika hapo juu na wewe ukaamua kuyasoma tena kwa hiari yako ni muhimu lakini la kuzingatia zaidi na ambalo limesukuma kuandika maelezo hayo ni maisha ya 'House Girl' (Mfanyakazi wa kike wa ndani ya nyumba). Maisha ya House Girl ambaye kimsingi naye ni mwanamke na leo ni siku yake pia yametawaliwa na changamoto lukuki.Kwa bahati mbaya sana wanaomsemea House Girl ni wachache sana ukilinganisha na changamoto ambazo zimewazunguka.
House girl ni muhimu sana katika maisha ya familia na hiyo ni kutokana na majukumu waliyokabidhiwa na baadhi ya familia.Kuna nyumba ambazo House Girl anakuwa wa kwanza kuamka na mwisho kulala.Familia ya watu sita au nane wote wanamtegemea House Girl ndio afanye kila kitu.Hakuna mwenye kuwaza kumsaidia .Sawa wanawalipwa kwa kazi anayofanya lakini lazima kuangalia aina ya maisha yake.
Ni mwanamke ambaye anahitaji huruma, anahitaji kusaidiwa, anahiti kupata furaha mahali anakoishi.Chakula ambacho familia inakula muandaaji wake ni House Girl,usafi wa nguo, nyumba, watoto , kuteka maji, kusikindikiza watoto shule yote ameachiwa yeye.Hana muda wa kumpumzika na anayesababisha hivyo ni mwanamke mwenzake (Mama Mwenye nyumba).
Nitoe rai ni vema Siku ya Mwanamke ikatoa nafasi ya kujadili maisha ya House Girl.Wengi wao wanateseka na hawana pa kwenda.Kazi kubwa wanayoifanya haiendani na mshahara ambao anautapa kwa mwezi.Akidai kuongezewa mshahara utasikia anaambiwa kwani unakula wapi?
Jamani house girl ni mwanamke na anastahili thamani yake kama mwanamke.Hivyo wakati leo hii wanawake mmeungana kujadili changamoto ambazo mnakabiliana nazo, tumie nafasi hii kujadili namna ya kumuondolea changamoto mfanyakazi wa ndani.
Kutoishi vizuri na mfanyakazi wa ndani madhara yake ni makubwa.Unajua kwanini?Iko hivi
mama unapoamua kumchukia dada wa kazi, kumnyanyasasa, kutomthamini na hata kutomjali yeye anachokifanya anarudisha hasira kwa watoto.Mama ukiondoka kwenda kazini anasema afadhali sasa nami ni zamu yangu kulipiza kisasi.
Tukiishi na house girl vizuri hata familia itakuwa salama.Hivyo leo hii iwe chachu ya kumuondolea changamoto.Ni mwanamke kama walivyo wanawake wengine.Kufanya kazi kwenye nyumba yako si kigezo cha kumuona hana thamani anayostahili kupewa mwanamke.Nimewaza tu kwa Ujinga wangu kama vipi achana nayo.

MKAZI WA MOSHI MJINI AJISHINDIA BODA BODA YA BIKO,PIA AKABIDHIWA KITITA CHA MILIONI MOJA

$
0
0
Mkazi wa Moshi Mjini, Prosper Andrea Massawe wa Moshi, mkoani Kilimanjaro, akifurahia baada ya kuibuka mshindi wa bodaboda na sh milioni moja aliyokabidhiwa kutoka kwenye bahati nasibu ya Watanzania ya Biko, mchezo wa kubahatisha unaotoa nafasi kubwa ya kushinda nchini Tanzania. Droo kubwa za Biko hufanyika kila Jumatano na Jumapili.

KIKAO CHA 40 CHA BODI YA TAIFA YA PAROLE CHAFANYIKA LEO UKONGA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0



Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(kushoto) akiongoza Kikao cha 40 cha kujadili Wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole. Kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Kamishna wa Magereza, Uwesu Ngarama ambaye pia ni Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole. Kikao hicho cha siku moja kimefanyika leo Machi 8, 2019, katika Bwalo la Maafisa Magereza, lililopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
PIX 2
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Kamishna wa Magereza, Uwesu Ngarama ambaye pia ni Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole akitoa taarifa fupi ya Sekretarieti kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(hayupo pichani)afungue rasmi kikao hicho.
PIX 3
Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole wakifuatilia majadiliano ya wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole leo Machi 8, 2019, katika Bwalo la Maafisa Magereza, lililopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
PIX 4
Ujumbe kutoka Zanzibar wakishiriki mazungumzo maalum yenye lengo la kubadilishana uzoefu na Bodi ya Taifa ya Parole Tanzania katika ziara yao ya kikazi leo Machi 8, 2019. Wa kwanza kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Said Hassan(katikati) ni Waziri wa TAMISEMI na Vikosi Maalum vya Zanzibar, Mhe. Haji Omari na Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Polisi kutoka Zanzibar, Hasina Ramadhani.
PIX 5
Sekretarieti wakifuatilia kwa makini majadiliano katika kikao hicho.
PIX 6
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(wa nne toka kushoto walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole pamoja na Viongozi Waandamizi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, leo Machi 8, 2019, katika Bwalo la Maafisa Magereza, lililopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam baada ya ufunguzi wa Kikao cha Bodi ya Taifa ya Parole(Picha zote na Jeshi la Magereza).

WAZIRI MBARAWA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA MAJI WA KISARAWE

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa amefurahishwa na kasi ya maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Kisarawe unaoendelea Kwa sasa unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Julai.

Katika ziara yake aliyoifanya leo kwa kutembelea ujenzi wa tanki la Kisarawe na Kibamba, Mbarawa amesema kuwa kukamilika kwa mradi huu kutasaidia katika utaoji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Kisarawe pamoja na viwanda vilivyopo.

Mbarawa amesema kuwa mradi wa Kisarawe unajengwa kwa fedha za ndani za Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA  na unagharimu takribani Bilioni 10 za kitanzania.

Amesema, adhma ya serikali ni kuhakikisha 2020 wananchi wa mijini wanapata maji wka asilimia 95, Wilaya ni asilimia 90 na vijjjni asilimia 85.

“Malengo ya serikali ni kuona wananchi wote wanapata maji ifikapo 2020, na Mamlaka zote zinatakiwa kuhakikisha malengo hayo yanafanyika kwa jitihada kubwa sana,” amesema Mbarawa.

Akizungumzia siku ya wanawake duniani inayoadhimishwa kila Machi 08, Waziri Mbarawa amesema kuwa mwanamke ndiyo mtu anayeiangalia familia na malengo ya kumtua mama ndoo chumbani yatafikia ifikapo 2020 na hilo linawezekana kama Mamlaka za Maji zitafanikisha miradi yote ya maji inayotekelezwa kwa sasa.

Msimamizi wa mradi wa Kisarawe Mhandisi Kakwezi Ishmael amesema kuwa muda uliopo kwa sasa ni utekelezaji tu kama maagizo ya Waziri alivyoyatoa.

Baada ya kumaliza kutembelea miradi hiyo, Waziri Mbarawa ameutaka uongozi wa DAWASA kusimamia miradi ili iweze kumalizika kwa wakati ili wananchi waliokaa kipindi kirefu bila kuwa na maji safi na salama.

 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akiwa anakagua maendeleo ya mradi wa maji wa Kisarawe unaoendelea kwa kasi ukiwa unatarajiwa kukamilia mwishoni mwa mwezi Julai. 
 Msimamizi  wa Mradi wa Maji wa Kisarawe kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Mhandisi Kakwezi Ishmael akielezea mradi mzima wa Kisarawe kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akizungumza na wanahabari baada ya kumaliza kutembelea mradi wa maji wa Kisarawe  na kasi ya ujenzi unaoendelea, kushoto ni Msimamizi wa Mradi wa Kisarawe kutoka DAWASA Mhandisi Kakwezi Ishmael.


KASONGO MPINDA ALIYEKUWA GWIJI WA MUZIKI.

$
0
0
Na: Moshy Kiyungi,Dar es Salaam.


Desemba 02, 2018 ilitimia miaka mitatu tangu mwanamuziki Kasongo Mpinda ‘Clayton’, aliyefariki Desemba 02, 2015 akiwa nyumbani kwake Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa maradhi ya Kisukari.

Mwanamuziki huyo alitamba katika bendi mbalimbali za muziki wa dansi humu nchini zikiwemo za Maquis du Zaire na baadaye MK Group, kabla ya kujiunga kufanya kazi ya muziki na gwiji la muziki nchini, Kikumbi Mwanza Mpango Mwema Kyembe ‘King Kiki’ na kundi lake la La Capitale ‘Wazee Sugu’.


Kasongo aliingia nchini Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 1970 akiwa na bendi ya ‘The Wings Brother’s’ aliyoianzisha mwenyewe akiwa huko kwao Jamhuri  ya Kidemokrasia ya Kongo.

Akiambatana na wanamuziki wa bendi hiyo walisafiri wakitoka katika nchi za Zambia, Botswana na Zimbabwe hadi humu nchini kutoa burudani.

Mwaka 1979 akaangukia mikononi mwa bendi ya Maquis du Zaire iliyokuwa ikiungurumisha muziki katika ukumbi wa White House, Ubungo jijini Dar es Salaam.

Kasongo aliweza kuzikumbuka baadhi ya nyimbo alizotunga au kushiriki kuimba akizitaja nyimbo alizotunga na kuimba akiwa Maquis du Zaire za Angelo, Mwana Malole, Nasononeka, Baharia, Siri ya Mkoko na zingine kibao.

Kasongo Mpinda  ‘Clayton’ akisaidiana na Mbombo wa Mbomboka,  walikuwa waanzilishi wa bendi ya MK. Group iliyokuwa ikifanya vitu vyake katika ukumbi wa Bandari Grill aliyopo katika hoteli ya New Africa, katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Akiwa na bendi hiyo iliyokuwa ikitumia mtindo wa ‘Ngulupa’ alifanikiwa kuifanya kuwa ya kipekee kuanzia upigaji hadi utaratibu wa kimahudhurio kwa upande wa wapenzi na mashabiki.

Mpinda kuna wakati aliwahi kutetea kuwa muziki wa dansi umeshuka akisema kwamba  kuwa muziki huo hauwezi kushuka kutokana na kwamba una tabaka lake mahususi kiushabiki.

Alisema hata vijana wa sasa wanaoonekana kuishabikia Bongo fleva, itafikia kipindi watalazimika kuwa mashabiki wa dansi kutokana na umri wao kuwaruhusu.

Aidha Kasongo Mpinda aliweza kuonesha makali yake akiwa na bendi ya Zaita Muzika aliyojiunga nayo baada ya miaka minane ya kuitumikia MK Group.

Wakati akiwa hai  wake aliwahi kufanya mazungumzo na mwandishi wa habari hizi, akaeleza kuwa alizalliwa Februari 2, 1945 Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,  akiwa ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto wanane unaotokana na ukoo wa ki Chifu.

Baba wa Babu yake alikuwa akiitwa Chifu Kasongo huko Kasai, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Baba yake mzazi mzee Boniface Mpinda Kasongo, alikuwa mfanyabiashara maarufu katika mji wa Lubumbashi, wakati mama yake Kanku wa Mokendi, alikuwa muumuni na mwimbaji mashuhuri katika  Kanisa la kikatoliki mjini humo.

Mpinda alibainisha kwamba mama yake ndiye aliyekuwa chanzo cha yeye kupenda kuimba kwa kuwa kila mara alikuwa akifuatana nae kwenda Kanisani kuimba.

 ‘Clayton’ hakuweza kuendelea na masomo ya  sekondari baada ya wazazi wake wote  kufariki dunia akiwa kidato cha kwanza.

Safari yake ya muziki ilianza katika bendi ya Ode Jazz na baadae akajiunga katika bendi ya Lupe Jazz, zilizokuwa Lubumbashi.
Mwaka 1965 Kasongo alikwenda katika jiji la Kinshasa kutafuta bendi ya kujiunga nayo, ambapo alikutana na Dokta Nico Kasanda, aliyekuwa mmiliki wa bendi ya L’Africa Fiesta Sukisa.

Alipiga muziki na bendi  hiyo hadi mwaka 1968,  alipoachana na Dokta Nico akaamua kuvuka mpaka akaingia mji wa Lusaka nchini Zambia.

Mwaka uliofuatia wa 1969 na kuanzisha bendi yake ya The Wings Brother’s,  mjini Lusaka.

The Wings Brother’s ilijumuisha vijana toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waliokuwa wamechipukia katika  muziki wakati huo.

Aliwataja kuwa ni akina Kibambe Ramadhani, Lomani, Jozee, Lushiku wa Lushiku na Kayembe Trumbloo.

Chini ya uongozi  wake bendi, hiyo ilisafiri kwenda kupiga muziki katika nchi za Botswana, Zambia hatimaye wakatua hapa nchini Tanzania mwaka 1979.

Haikuchukua kipindi kirefu ambapo yeye na baadhi ya wanamuziki wenzake walijiunga na bendi ya Maquis du Zaire, huku wanamuziki wengine wakijiunga na bendi ya Orchestra Safari Sound (OSS).

Baada ya ujio wa vijana hao kukawa na ushidani mkali kati ya bendi ya Orchestra Safari Sound (OSS) iliyokuwa ikipiga muziki wake kwenye ukumbi wa Kimara resort na Maquis du Zaire iliyokuwa imejikita ukumbi wa White House Ubungo.


Kasongo alifunga ndoa ya kiisilamu na Bi. Habiba mwaka 1984, jijini Dar es Salaam. Kabla ya kufunga ndoa hiyo, alilazimika kuingia dini ya kiislamu,  hivyo alisilimishwa na kupewa jina la Abubakar.
Katika maisha ya ndoa yao walifanikiwa kupata watoto wanne ambao ni Johari, Kiloman, Mpinda na Idd.

Kati yao wawili ndiyo waliofuata nyao za baba yao ambapo  Idd ‘Clayton’ yupo katika kikosi cha Twanga Pepeta Academy akifanya vizuri katika muziki wa dansi na  Kiloman anapiga muziki wa kizazi kipya.

Kwa muda mrefu Clayton hakuwa vizuri kiafya kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya Kisukari na ngazi yaliyohitimisha safari yake ya kuishi duniani.

Kabla ya hatma yake kimuziki alikuwa akifanya kazi ya muziki katika bendi ya La Capitale ‘Wazee Sugu’ akiwa pamoja na Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kikii’ na  baadae alijiunga na bendi ya Bana Maquis inayoongozwa na Tshimanga Kalala Assosa.

Boubakar Kasongo katika mazunguzo yake aliwahi kutamka kuwa alikuwa akiona raha kuimba pamoja na marehemu Issa Nundu ‘Prince’.

Alisema kuwa ukiwaondoa Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kikii’ na Tshimanga Assosa, mwimbaji pekee aliyekuwa akimpa changamoto kubwa enzi za Marquis na MK Group ni mtunzi na mwimbaji mahiri Hassan Rehani Bitchuka.

 “Nasikitika nimekuwa masikini licha ya kutumika sana huko nyuma, hii ni kutokana na kuchelewa kwa mafanikio ya kimuziki hapa nchini, lakini ingekuwa ni kama sasa, muda huu mimi ningelikuwa tajiri kama msanii Diamond…” alisema Clayton enzi za uhai wake.

Akiwa kama mkongwe katika tansnia ya muziki wa dansi Aboubakar Kasongo Mpinda aliwahi kutoa usia kwa wanamuziki wa dansi kutokata tamaa pamoja na kushirikiana.

Alisema kuwa mawazo ya wengi kwenye ushirikiano huzaa kitu kizuri na kwamba ubinafsi ndio unaosababisha nyimbo nyingi za sasa kuwa na ubora muda mfupi.
ABOUBAKAR KASONGO MPINDA 'CLYTON' (L)AKIIMBA SAMBAMBA NA ISSA NUNDU

MBARAKA MWINSHEHE UKOSEFU WA DAMU KUONGEZEWA KULISABABISHA KIFO CHAKE.

$
0
0
Na: Moshy Kiyungi,Tabora.

Kifo cha mwanamuziki Mbaraka Mwinshehe Mwaruka, kilisababishwa na ukosefu wa damu ya kumuongezea muda mfupi baada ya kupata ajali mjini Mombasa.

Ajali hiyo ilitokea Januari 12, 1979, wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Makadara mjini Mombasa nchini Kenya.
 MBARAKA MWINSHEHE ENZI ZA UHAI WAKE

Baadhi ya Watanzania kwa mapenzi yao makubwa, kila ifikapo Januari 12, kila mwaka, hufanya kumbukizi ya nguli huyo aliyeliletea sifa kubwa taifa letu kupitia muziki.

Mbaraka alikuwa nchini humo kwa ajili ya safari ya kikazi pamoja na kurekodi nyimbo zake wakati huo akiwa kiongozi wa bendi ya Super Volcano ya mjini Morogoro.

Wasifu wa nguli huyo unaeleza kuwa alizaliwa Juni 27, 1944 mjini Morogoro.
Mbaraka alikuwa na vipaji vingi vikiwemo vya kutunga na kuimba nyimbo ambazo zilikuwa zikiburudisha, zikielimisha na kutoa maonyo kwa jamii.

Mbaraka alikuwa bingwa wa kupiga gitaa la solo ambalo alilimudu hadi kufikia kuitwa ‘International Soloist’.Aidha aliweza kuongoza kwa ufanisi mkubwa bendi za Morogoro Jazz kwa bendi yake ya Super Volcano kwa miaka tofauti.

Mwinshehe alikuwa mtoto wa pili kuzaliwa kati ya watoto 12, kati yao ni yeye na wadogo zake Zanda na Matata ndio waliokuwa wanamuziki.Zanda alikuwa mwimbaji wa nyimbo za kizungu katika bendi ya Morogoro Jazz na Matata alikuwa akichanganya drums katika bendi hiyo hiyo.

Baba yake Mzee Mwinshehe Mwaruka alikuwa wa kabila la Waluguru, msomi aliyekuwa Karani katika mashamba ya Katani. Mama yake alikuwa wa kabila la Ngoni.

Kwa mujibu wa maelezo ya familia, babu yake Mbaraka alikuwa wa kabila la Wadoe kutoka Bagamoyo. Alipelekwa na Wakoloni kijiji cha Mzenga Kisarawe, mkoani Pwani akawe Chifu wa huko.

Baada ya kutawazwa kuwa Chifu, alioa wake tisa na kupata watoto zaidi ya 50 akiwemo baba yake Mbaraka, Mzee Mwaruka.

Tungo za nyimbo za Mbaraka zimejaa maudhui mema, ambazo zilimpandisha ‘chati’ hadi kuchaguliwa kuwa mmoja kati ya wasanii waliokwenda kuiwakilisha Tanzania katika mji wa Osaka nchini Japan mwaka 1970, ambako kulifanyika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Expo70.

Tanzania iliwakilishwa na wasanii kadhaa akiwemo mzee Morris Nyunyusa, mlemavu wa macho, aliyekuwa na kipaji cha kupiga ngoma zaidi ya kumi kwa wakati mmoja.

Wengine walikuwa Wanasanaa toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kundi la Blass Band toka jeshi la Polisi lililokuwa likiongozwa na Mzee Mayagilo.

Aliporejea toka Japan, Mbaraka alitunga wimbo uitwao ‘Maonesho Japan’ akisimulia jinsi mafanikio makubwa yaliyopatikana katika maonesho hayo.

Kwa upande wa elimu Mbaraka Mwinshehe aliipata huko Kisarawe Middle School mwaka 1963.

Baadaye akaenda mjini Morogoro kuendelea na masomo. Mbaraka yaelezwa kwamba aliamua kuacha shule akiwa darasa la kumi ili awe mwanamuziki.

Kisa cha kuacha shule ilitokea siku moja mwaka 1965 wanamuziki wa Morogoro Jazz wakiwa wamepumzika nje ya Klabu yao, Mbaraka Mwinshehe alipita karibu yao akiwa kabeba begi kubwa. Walipomuuliza anaenda wapi muda ule ambao anatakiwa kuwa darasani?

Aliwajibu kuwa hataki tena shule, ameamua kwenda Dar es Salaam kutafuta maisha.

Wanamuziki hao walitumia busara wakamkalishi chini na kumsihi alale pale klabuni. Madhumuni yao ni kwamba waltaka Mabraka aweze kufikiria kwa utulivu juu ya uamuzi yake ya kuacha shule.

Kesho yake wanamuziki hao walishikwa na bumbuwazi baada ya kumkuta Mbaraka akifanya mazoezi ya kupiga gitaa. Kabla ya hapo walimfahamu kuwa yeye ni mpulizaji wa filimbi.

Kwa kuwa walikuwa na shida ya mpiga gitaa la rhythm, walimshauri aache safari ya kwenda Dar es Salaam, abaki kwenye bendi yao kama mpiga gitaa hilo naye alikubali.

Mbaraka alijikuta amekubaliwa kujiunga katika bendi hiyo pasipo kutarajia.
Wakati huo ni wapiga tarumbeta, saxophone na gitaa la solo pekee ndio waliokuwa wakilipwa mshahara kwa mwezi.Wengine wote walikuwa wakipata posho kidogo kila lilipopigwa dansi.

Siku moja wanamuziki wa bendi hiyo ya Morogoro Jazz walialikwa kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya mashindano kati yao dhidi ya bendi ya Kilwa Jazz.Kabla ya kuondoka Mwinshehe ‘alitikisa kiberiti’ kwa kugoma kwenda Dar es Salaam kwa kuwa alikuwa halipwi chochote.

Kwa mara nyingine tena busara na hekima za viongozi wa bendi hiyo zilitumika, wakakubali kumlipa mshahara wa shilingi 120 kwa mwezi.

Mpiga solo ambaye aliyekuwa akilipwa shilingi 150, naye akatunisha misuri kwa kugoma kwenda Dar es Salaam kwa hoja kwamba mpiga rhythm hastahili kupata mshahara.

Mbaraka akawatoa hofu viongozi hao juu ya mgomo wa mpiga solo huyo, akasema kuwa yeye ataweza kupiga pia gitaa hilo.

Bendi ya Morogoro Jazz ikaenda Dar es Salaam huku ikiwa imejawa na tashwishiwi juu ya ushindani uliokuwa ukiwakabili kati yao na bendi ya Kilwa Jazz.

Wakati huo bendi ya Kilwa Jazz ilikuwa tishio ukizingatia wanamzuki wakubwa waliokuwepo katika bendi hiyo akina Ahmed Kipande, Kassimu Mapili, Juma Mrisho ‘Ngulimba wa Ngulimba’ na Duncan Njilima.

Viongozi hao wa Morogoro Jazz wakamkabidhi gitaa la solo Mbaraka Mwinshehe Mwaruka, naye bila ajizi siku hiyo ‘Nyota ya Jaha’ ilimuangazia upande wake. 

Alilicharaza gitaa hilo kwa umahiri mkubwa katika nyimbo zote zilizokuwa zimepangwa, hadi mwisho wa mashindano bendi yao ikaibuka kidedea kwa ushindi.

Baada ya tukio hilo ambalo halikutegemewa na wengi, Mbaraka Mwinshehe akapandishiwa mshahara hadi ukafikia shilingi 250 kwa mwezi, ambazo zilikuwa ni kiwango cha juu sana miaka hiyo.

Mwinshehe alikuwa na kipaji cha ziada ambacho wanamuziki wengi wamekosa. Alikuwa na uwezo wa kuimba huku akilikung’uta gitaa la solo.

Aliwahi kutunga, kuimba na kushiriki kikamilifu kupiga gitaa la solo nyimbo nyingi za bendi hiyo. Baadhi ya nyimbo hizo ni kama Shida, Nateseka, Safari siyo kifo, Dina uliapa, Maudhi, Penzi la mashaka, Heshima kwa Vijana , Harusi imevunjika , Mshenga No.1 na Nisalimie Zaire.

Wimbo huo Nisalimie Zaire aliutunga kwa ajili ya kumuaga rafiki yake mpigaji gita la rhythm na kuimba sauti ya pili, Koko Malalii aliyekuwa raia wa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambaye alikuwa akipiga gitaa katika bendi hiyo.

Walikuwa marafiki ‘walioshibana’ sana na mara alipoondoka, ndipo akamtungia wimbo huo. Nyimbo zingine zilikuwa Baba mdogo, Mwese, Kibena, Naogopa utanisumbua, Ni siku nyingi, Regina, Kwa ajili yako na Dr. Kreluu.

Wimbo huo aliutunga mahsusi kwa ajili aliyekuwa mkuu wa mkoa Iringa wakati huo, Dk. Kreluu aliyeuawa na mkulima aliyejulikana kwa jina la Mwamwindi, ambaye baadae yaelezwa kuwa alihukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Nyimbo zingine alizotoka nazo Mbaraka ni za Harusi imevunjika, Mapenzi shuleni na Sembuli. Wimbo huo wa Sembuli ulikuwa wa maombolezo ya kifo cha marehemu Gibson Sembuli, aliyekuwa mzaliwa wa Morogoro na mcheza kandanda katika mkoa huo baadaye alijiunga na klabu ya Yanga ya Dar es Salaam na timu ya Taifa.

Zingine ni za Matilda, Nalilia raha, Nikupendeje, Mapenzi yanitesa Jogoo la Shamba na nyingine nyingi.Mfano mwingine ni pale alipotunga wimbo ukiwa ni ‘kijembe’ mahsusi kwa hasimu wake mkubwa kimuziki, Juma Kilaza aliyekuwa akiongoza bendi ya Cuban Marimba.

Bendi ya Morogoro Jazz alikuwa na wanamuziki mahiri ambao waliifikisha katika mafanikio hayo. Kwa uchache nakutajia majina ya baadhi yao.

Walikuwa ni akina Mzee Seif Ali, Tosi Malekela, Suli Bonzo, Kilongola, Lazaro Bonzo na Mpalanje. Wengine walikuwa Kazingoma, Simaro Kasansa, Kasinde, Matata, Zanda Ngokoko, Athumani na Paschal.

Kipindi hicho Wapenzi wa muziki waliweza kuondoka Dar es Salaam kwenda mjini Morogoro kuvinjari siku za mwisho wa wiki, katika bendi ya Cuban Marimba au Morogoro Jazz.

Baadaye mwaka 1973 Mbaraka Mwinshehe alijitoa toka katika bendi ya Morogoro Jazz, iliyokuwa ikipiga katika mitindo ya Masika, Likembe, Zolelanga, Sululu na Mahoka.

Akaunda bendi ya Super Volcano akisaidiana na Charels Kasembe, yeye akaendelea kuwa kiongozi wa bendi hiyo hadi mauti yake yalipomfika.

Nguli huyu alikumbwa na mauti baada ya kupata ajali ya gari iliyoyafupisha maisha ya mwanamuziki huyo Januari 12, 1979.

Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo aliyejulikana kwa majina ya Zebedee Japhet Kinoka, maarufu kama Super Zex, alieleza kuwa kifo cha Mbaraka Mwinshehe kilitokea majira ya saa 7 mchana Januari 12, 1979 alipokuwa anatoka maeneo ya Kisauni, jirani na mji wa Mombasa.

Alisema kuwa mwanamuziki huyo alikuwa ameenda kumtembelea mtanzania mwenzake aliyekuwa akimiliki hoteli huko.

Kinoka alisema alipofika karibu na kanisa la Kongoya, aliliona gari aina ya Peugot 404, lenye rangi nyeupe likitoka upande wa Bush bar. Gari hilo lilikuwa katika mwendo mkali likaligonga roli moja lililokuwa likitokea upande mwingine. Watu walokuwa karibu wakakimbilia kungalia ajali akiwemo yeye.

Mara moja akamtambua Mbaraka na kuwambia watu kuwa huyo ni mwanamuziki Mtanzania anaitwa Mbaraka Mwinshehe.Iliwalazimu kuanza kukata mabati ili kumuondoa Mbaraka aliyekuwa amebanwa miguu katika gari lile akiwa bado yu hai.

Wakati kazi hiyo inaendelea Zebedee alikimbilia kwenye baa ya Kengeleni, ambako bendi ya Jamhuri Jazz ya Tanga ilkuwa ikitoa burudani ya muziki. Akawambia kuwa mwenzao kaumia sana, nao wakatoka mbio kwenda kushuhudia.

Walifanikiwa kumtoa Mbaraka kwenye gari hilo, akakimbizwa hadi katika hospitali ya Makadara, mjini Mombasa.Zebedee pia akatumwa kuwafuata wanamuziki wa bendi ya Super Volcano ambao wakati huo walikuwa wameanza kupiga muziki wa mwanzo wakimsubiri Mbaraka katika ukumbi wa baa ya Zambia.

Wanamuziki walipofika hospitalini hapo, wakaambiwa watoe damu ya kumuongezea kiongozi wao Mabaraka Mwinshehe.Kila mmoja akaanza kukwepa kutoa damu kwa visingizio mbalimbali. Baada ya muda mchache Mbaraka Mwinshehe akafariki dunia akiwa na umri mdogo wa miaka 34 tu!.

Mwili wa Mbaraka akasafirishwa hadi mpakani mwa Tanzania na Kenya ukapokewa na ndugu, jamaa, marafiki na maofisa wa Wizara ya Utamaduni.
Baadae mwili wa Mbaraka Mwinshehe akazikwa katika nyumba yake ya milele kijijini kwake Mzenga Wilayani Kisarawe, mkoa wa Pwani.

Mwaka huu umetimia mwaka wa 40 tangu Mbaraka Mwinshehe Mwaruka kufariki dunia, tungo za nyimbo na sifa za kazi zake zitaendelea kudumu vizazi kwa vizazi.

Nyimbo nyingi za bendi ya Morogoro Jazz na Super Volcano bado zinapendwa na kurindima kwenye baadhi ya vituo vya redio na sehemu zingine za burudani hadi leo.

Binti yake Taji Mwaruka, ndiye aliyefuata nyayo za baba yake, ambapo alikuwa akiimba na kuliungurumisha gitaa zito la besi katika bendi ya marehemu baba yake ya Super Volcano. Taji kwa taarifa za hivi karibuni zimeeleza kuwa ameachana na mambo ya muziki, ameamua kuwa mfanyabiashara huko Aghaibuni.

Mungu aipumizishe roho yake pahala pema peponi, Amina.

Mwisho.

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa namba: 08713331200, 0767331200 na 0784331200.



TUGHE yatoa zawadi kwa kina mama Mloganzila.

$
0
0
: Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Redemptha Matindi (aliyevaa nguo ya rangi ya bluu) akiwakaribisha viongozi kutoka TUGHE makao makuu (kamati ya wanawake) ambao wametembelea hospitalini hapo leo.
Naibu Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa Bi. Jane Mbula (kulia) akizungumza kabla ya kugawa zawadi katika wodi ya kina mama katika Hospitali ya Mloganzila. 
Bi. Stella Apolo kutoka TUGHE makao makuu akimpatia mzazi zawadi ya kanga, sabuni na sukari.
Baadhi ya wanawake wa Hospitali ya Mloganzila leo wameungana na wanawake wengine duniani katika kusheherekea siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa imefanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.
1 Baadhi ya wanawake wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Upanga na Muhimbili-Mloganzila wakiwa katika picha ya pamoja katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.


Viongozi kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) makao makuu, leo wametembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili -Mloganzila na kuwapatia zawadi mbalimbali wanawake waliojifungua na wale waliolazwa na watoto hospitalini hapo. 

Ujumbe wa viongozi hao umeongozwa na Naibu Katibu Mkuu TUGHE Taifa Bi. Jane Mbula ambapo amesema lengo la kutoa zawadi kwa kina mama hao ni kuungana nao katika kusheherekea siku ya wanake duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka. 

‘’Tumekuja kuwatembelea kina mama na kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwemo kanga, sabuni na sukari kwani lengo letu ni kugusa jamii na kuhakikisha wanawake waliopo mahospitalini nao wanafurahia siku hii ambayo huadhimishwa mara moja tu kwa mwaka’. amesema Bi Mbula. 

Pamoja na mambo mengine kiongozi huyo wa TUGHE ametumia fursa hiyo kuwataka wanawake nchini kuendelea kufanya kazi kwa bidi kwakua mwanamke ana mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa familia na taifa kwa ujumla. 

Kauli mbiu ya siku ya mwanamke duniani kwa mwaka 2019 inasema “badili fikra kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu”

Tigo kuwawezesha wasichana kujiendeleza kiteknolojia

$
0
0


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tigo Tanzania, Simon Karikari, akipata maelezo kutoka kwa wasichana wanaojengewa uwezo kwenye sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano muda mfupi baada ya uzinduzi wa mradi wa ‘TECH IS FEMALE’ ambao Tigo imeufadhili katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Wasichana wanaojengewa uwezo kwenye sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na taasisi ya Apps and Girls wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafadhili wao ikiwamo Kampuni ya Tigo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tigo Tanzania, Simon Karikari, akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam ambapo kampuni ya Tigo ilitoa msaada kwa ajili ya kuwajengea uwezo wasichana na wanawake kwenye sekta ya Habari na Mawasiliano. Wa kwanza kulia ni Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Imni Patterson, na anayefuatia ni mwanzilisi wa taasisi ya Apps and Girls, Caroline Ekyariisma.
Halima Okash kutoka Kitengo cha Uwajibikaji kwa Jamii cha Tigo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ufadhili wa kampuni ya Tigo kwa mradi wa ‘TECH IS FEMALE’ unaolenga kuwajengea wanawake na wasichana uwezo kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Wa kwanza kulia ni mwanzilishi wa taasisi ya Apps and Girls, Caroline Ekyariisma, akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tigo Tanzania, Simon Karikari


Kampuni ya mawasiliano ya Tigo, imeelezea dhamira yake ya kusaidia kuwajengea uwezo wasichana na wanawake kwa ujumla kwenye eneo la teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kupitia taasisi ya hapa nchini inayojulikana kama Apps and Girls.

Akizungumza mbele ya wasichana wenye ndoto za kuwa wajasiriamali kwenye sekta ya TEHAMA wakati wa uzinduzi wa mradi wa ‘TECH IS FEMALE’, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Bw. Simon Karikari alisema, Tigo inatambua mchango wa wasichana na wanawake kwenye maendeleo na kuelezea utayari wa kampuni hiyo kuunga mkono jitihada za kuwawezesha kutoa mchango wao.

“Uwezeshaji unaofanywa na Tigo kwa wasichana na wanawake, unalenga kuwezesha utekelezaji wa miradi ya kigunduzi kwenye TEHAMA kwa makundi ya wasichana waliofanyiwa mchujo na ambao watapewa mafunzo maalum kabla ya kuwekwa chini ya uangalizi maalum wakati wakifanya miradi waliobuni wenyewe ya kibunifu,” alisema Karikari.

Karikari aliongeza kuwa, mradi huo wa ‘TECH IS FEMALE’ unalenga kutoa fursa sawa kwa wasichana wote wenye umri kati ya miaka 14 na 24 (wanafunzi na sio wanafunzi) nchini Tanzania ili kuwawezesha kiuchumi na kidijitali, waweze kuwa vinara katika ulimwengu huu wa kidijitali unaokwenda kwa kasi kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia ya kila siku.

Kwa upande wake, Muasisi wa Apps and Girls, Caroline Ekyariisma, alisema kwamba kampeni hiyo itakuwa ni ya mwaka mzima. “Lengo letu ni kutoa mafunzo ya kutengeneza programu kwa wasichana katika shule 61 za sekondari zilizo chini ya mpango wa Tigo E-schools nchi nzima. Mpango huu pia utahusisha makundi ya wasichana ambao hawapo mashuleni, hivyo wasichana ambao sio wanafunzi pia watapata fursa sawa ya kushiriki na kunufaika,” alisema.

“Tunapenda pia kutoa shukrani zetu kwa Mpango wa Uvumbuzi kutoka Afrika ya Kusini (SAIS 2) pamoja na Mfuko wa Uvumbuzi kwa ushirikiano na uwekezaji wao katika kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupata ujuzi kwenye TEHAMA,” alishukuru Ekyarisiima.

Mchakato wa kuwapata wasichana watakaoshiriki katika mradi huu utafanyika nchi nzima na utakuwa na mchujo mkali ambapo wasichana 30 bora ndiyo watakao fuzu. Wasichana hawa ambao watakuwa mchanganyiko wa wanafunzi na sio wanafunzi, wataingizwa katika mpango maalumu ya mafunzo na uangalizi. Wengine watafanya mafunzo kwa vitendo katika idara ya TEHAMA ya Tigo kwa ajili ya kujiendeleza na kujifunza zaidi, huku wengine wakishughulika na miradi mengine. Wakati huo huo tutakuwa tunawajengea uwezo na kuwasaidia kupata kazi na kuwapatia mazingira bora ya wao kujiajiri,” alifafanua Ekyarisiima.

“Tigo inaendelea kutengeneza kizazi cha kidjitali. Ushirikiano wetu na Apps and Girls ni kuwekeza katika vijana wanawake ambao wanaonesha dalili nzuri za kuwa wajasiriamali, wavumbuzi, viongozi na mifano mizuri katika sekta ya teknolojia nchini Tanzania na Kusini mwa Jangwa la Sahara. Tunaamini kwamba katika siku za usoni ‘TECH IS FEMALE’ na tunaahidi kujitolea kupunguza tofauti za kijinsia kwenye sekta ya kidijitali nchini Tanzania,” alisisitiza Karikari.

Kwa miaka kadhaa sasa Tigo imekuwa ikishirikiana na kampuni ya Apps and Girls ili kuweza kupunguza tofauti ya kijinsia katika sekta ya kidijitali hususani katika eneo la Dar es Salaam. Ushirikiano huu kwa Apps and Girls umefanikiwa kuwafikia wasichana zaidi ya 3000 mashuleni na kwenye maeneo mengine ya jamii nje ya shule, na kuwezesha kuzaliwa kwa wajasiriamali, wavumbuzi, vioo kwa jamii na viongozi katika sekta ya teknolojia ambao wanaleta mabadiliko chanya katika nchi ya Tanzania.

RC MAKONDA AJITOLEA KUWASOMESHA HADI KIDATO SITA WATOTO 100 WA KIKE WALIOFAULU MASOMO YA SAYANSI.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametoa ahadi ya kuwasomesha kuanzia kidato cha tano hadi cha sita bure wasichana 100 waliofanya vizuri kwenye masomo ya sayansi katika matokeo ya mtihani wa kidato nne ili kuongeza idadi ya wanawake wataalamu na wabobezi wa nyanja mbalimbali.

RC Makonda amesema amegundua kuwa wapo mabinti wengi waliofaulu vizuri masomo yao lakini kutokana na wazazi wao kutokuwa na uwezo wa kuwaendeleza kielimu wameishia kupoteza ndoto zao hivyo ameona ni vyema akawaendeleza.

Aidha RC Makonda ameeleza kuwa wasichana hao watagharamiwa kila kitu kuanzia ada,mabegi,vitabu na sare za shule ili wabaki na kazi moja pekee ya kusoma na kufaulu.

Hayo yote yamejiri leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika ukumbi wa Mlimani City na kuhudhuriwa na Maelfu ya wanawake.

SHIRIKA LA DHWYT YATOA ELIMU KWA WANAFUNZI MTWARA

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mlango wa matumaini kwa wanawake  na Vijana Tanzania DHWYT Clemence Mwombeki akitoa mafunzo kwa Wanafunzi waliohudhulia Mafunzo Juu ya Usawa wa Kijinsia ,Ukatili na Rushwa ya Ngono maeneo ya kazi na Shuleni.
 Baadhi ya wanafunzi wa Vyuo mbalimbali wakisikiza Mafunzo kuhusiana na Afya ya Uzazi pamoja na Ujasiliamali katika kuadhimisha siku ya wanawake Dunia Mkoani Mtwara.
 Mratibu wa Huduma za Afya ya uzazi Baba,Mama na Mtoto Mkoa wa Mtwara Bi.Rosalia Arope akitoa mafunzo juu ya Afya ya Uzazi kwa wanafunzi wa Vyuo katika siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Mkoa wa Mtwara.
Blandina Emanuel Nguli  Mwanafunzi wa Kozi ya sekretari chuo cha Utumishi Mkoani Mtwara akiuliza swali juu ya Afya ya Uzazi katika mafunzo yaliyofanyika siku ya wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Shirika la Mlango wa Mtumaini Tanzania.

NA JOSEPH MPANGALA,MTWARA
Katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani shirika lisolokuwa la kiserikali la Mlango wa matumaini kwa wanawake na Vijana Tanzania DHWYT limetoa elimu kwa Wanafunzi wa Vyuo kuhusiasna na elimu ya afya ya uzazi pamoja na Ujasiliamali Mkoani Mtwara.

Mafunzo hayo yamehudhuriwa na jinsia zote huku wanafunzi wengi wakitaka kujua juu ya afya ya uzazi baba,mama na Mtoto hasa katika taratibu za upatikanaji wa mimba na umuhimu wa Baba kuhudhulia kliniki pamoja na Athari zake iwapo hata hudhulia.

Akizugumza katika mafunzo hayo Mratibu wa huduma za afya ya uzazi Baba,Mama na mototo Mkoani Mtwara Bi.Rosalia Arope amesema wanawake wengi wamekuwa wakiwatumia madereva wa Boda boda kama waume zao na kwenda nao Kliniki kwa kuwalipa kiasi kidogo cha pesa kutokana na taratibu zilizowekwa kliniki za kuja na baba wa Mtoto.

“Kuna wanawakewanapokuja Kliniki unabaini kuwa sio mwenza wake halisi anamchukua tu dereva wa bodaboda ili aweze kukidhi kwa sababu kuna baadhi ya wilaya wamejiwekea sheria ndogo kila mwanamke lazima aje na mume wake kwahiyo anaamua kumchukua Dereva Boda boda ili kuepukana na Kero hiyo”amesema Bi.Rosalia.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Mlango wa Matumaini Tanzania amewataka Vijana kushiriki katika maswala mbalimbali ya kijamii kama moja ya njia ya kufatilia maendeleo katika jamii inayowazunguka kuanzia ngazi ya mtaa kata mpaka wilaya.

MAMA WA MITINDO ASYA IDAROUS NDANI YA TANZANITE WOMEN'S DAR

$
0
0
Mama wa mitindo Asya Idarous Khamsin  Jumamosi hii ya Machi 9, ataingia na  Wanawake wa Tanzania kusherehekea siku ya Wanawake Duniani kwa kuonesha Mitindo yake katika jukwaa hilo maalum litakalo wakutanisha pia wabunifu mbalimbali. 

Hii itakuwa ni fursa ya kipekee kwa watu mbalimbali watakaojitokeza kushuhudia Mama wa mitindo ambaye kwa muda mrefu amekuwa akishiriki kuonesha mitindo yake nchini Marekani pamoja na mataifa ya Ulaya. 

"Mitindo mipya ya Ubunifu ya mavazi nitaonesha katila katika jukwaa la Tanzanite Women's hapa Dar.  Lakini pia tutauza karibuni sana" alieleza Mama wa mitindo Asya Idarous Khamsin  

Tanzanite Women's Forum & Runch ni jukwaa kubwa la Wanawake ambapo ufanyika kila mwaka huku Wanawake wenye ushawishi wakipata nafasi ya kuzungumza katika nyanja mbalimbali za kufikia malengo ya kibishara.

Tukio hilo linatarajia kufanyika katika ukumbi wa Double tree by Hilton hotel Masaki Jijini Dar Es salaam.

Wabunifu wengine mbali na Mama wa Mitindo Asya Idarous,  ni pamoja na Mustafa Hassanali, Vivya shaa, Abdul Mwene,Mgeci Cici, Zamda George.

Wabunifu wengine ni Irada Style, Katty Collection, Malika  Designer. 

Aidha, watoa mada na wazungumzaji wakuu kwenye tukio hilo ni pamoja na Mwanahamisi Singano, Smart Money Decisions  na Lavie Makeup artist. 



SIKU YA WANAWAKE YAACHA ALAMA RUBALE, BUKOBA .

$
0
0

Anaandika Abdullatif Yunus - Bukoba Kagera.

Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, ambayo huadhimishwa Machi 08 kila Mwaka, Wanawake wa Kata Rubale wamejitokeza kwa wingi na kujitolea Vifaa vya Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto katika Kituo cha Afya Rubale Wilaya ya Bukoba, Wodi inayotarajiwa kuanza kujengwa mara moja.

Kufuatia Sherehe hizo zilizohudhuriwa pia na Viongozi mbalimbali, Taasisi, Mashirika na Wadau wa Maendeleo, Mgeni Rasmi katika Shughuli hizo Mwenyekiti wa Halmasahuri ya Bukoba Murshidi Ngeze amelishukuru Shirika La World Vision Rukoma AP kwa kukubali kusaidia kiasi cha Fedha Shilingi Milioni 67 kwa ajili ya Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto, itayojengwa katika Kituo cha Afya Rubale ambapo gharama za Shughuli nzima za Ujenzi huo, ni Shilingi Milioni 22, Mbali na pesa hiyo kutoka shirika la World Vision tayari Kuna vifaa vya Ujenzi ambavyo vimekwisha tolewa na wadau pamoja na wananchi huku wengine wakiahidi kuleta.

Aidha Mh. Ngeze ameeleza nia ya Serikali ya Kuendelea Kuboresha Afya kwa akina mama hao na jamii kwa ujumla na kuwakumbusha umuhimu wa Kuwa na Bima ya Afya kwa kila kaya na faida zake, lakini pia Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayojengwa Eneo la Bujunangoma Kata Kemondo Wilayani Humo.

Mh. Ngeze akitoa ujumbe wake kwa Akina Mama hao amewaomba kuendelea kuwa walezi bora kwa familia zao hususani mabinti zao, kuwajenga katika misingi bora na kuwalinda dhidi ya Vishwawishi wanavyokumbana navyo vinavyopelekea mimba za Utotoni na mimba zisizotarajiwa na hatimae kukosa Elimu..
Kikundi cha Akina mama toka Kijiji Migara wakiwa wamebeba tofali za Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto, tofali hizi na mawe ni Vifaa  walivyobeba kutoka Majumbani kwao.
 Pichani ni sehemu ya Akina mama waliohudhuria Sherehe za Siku ya Wanawake Duniani ambapo Kwa Wilaya ya Bukoba sherehe hizi Kiwilaya zimeadhimishwa Katika Kata ya Rubale
 Pichani Ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Murshidi Ngeze akipokea Vifaa vya Ujenzi Kutoka kwa Akina Mama wa Kata ya Rubale kama ishara ya uzinduzi wa Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto, pembeni ni Diwani wa Kata Rubale Rutta Kitale.

 Pichani ni Bi. Penina Petro Meneja toka TADEPA akitoa salaam za Shirika lao, TADEPA wamekuwa wadau wakubwa wa Maendeleo ya Akina Mama Kata Rubale kwa Kuviwezesha Vikundi vya Ujasiliamali Mikopo midogo midogo.
 Pichani ni Bwn. Gratian Rwezaula Afsa mwezeshaji wa Shirika la World Vision Rukoma AP, akizungumza na Wananchi (hawapo pichani) waliohudhuria Sherehe za Siku ya Wanawake Duniani Iliyofanyika Kiwilaya Kata ya  Rubale, Rukoma Kama wadau wa Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto wametoa Shilingi Milioni 67.
 Pichani ni Bi. Celina Willbard Mwwnyekiti wa Kikundi cha Muungano, akiwakilisha Wanakikundi wenzake kwa kuleta Jiwe kutoka Nyumbani kwake, kama mchango wake wa Ujenzi wa Wodi ya Akina Mama na Mtoto katika Kituo cha Afya Rubale

WAZIRI UMMY ANG’AKA MIKOPO KIDUCHU KWA WANAWAKE

$
0
0


 Baadhi ya wanawake na wakazi wa mkoa wa Mwanza wakiwa katika maandamano katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2019 ambayo yalifanyika katika Viwanja vya Bujora Kisesa.
????????????????????????????????????
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.ummy Mwalimu akijadiliana jambo na Msanii Nurdin Bilal “Shetta” mara baada ya kuzindua kampeni ya SAWA ya Kupambana na Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto inayomshirikisha Msanii Nurdin Bilal “Shetta” wakati wa kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambapo Mhe Ummy aliungana na wanawake na wananchi wa mkoa wa Mwanza kuienzi siku hiyo.
????????????????????????????????????
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiangalia bidhaa zinazozaliswa na wanawake  mbalimbali katika moja ya banda lililokuwepo katika viwanja vya Kisesa Bujora  wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Mwanza.
????????????????????????????????????
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.ummy Mwalimu akijadiliana jambo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja Wa Mataifa Bw. Alvaro Rodriques na  Balozi wa Anders wa Sweden wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Mwanza.
????????????????????????????????????
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza  na wanawake na wananchi wa mkoa wa Mwanza katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake yaliyofanyika mkoani humo katika viwanja vya Bujora Kisesa.
????????????????????????????????????
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  Dkt. Philis Nyimbi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana akitoa  salamu za mkoa katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake yaliyofanyika mkoani humo katika viwanja vya Bujora Kisesa.
 Mwakilishi Mkazi Umoja wa Mataifa Bw. Alvaro Rodriguez akielezea ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha usawa wa kijinsia unapatikana nchini wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Mwanza.
????????????????????????????????????
Mwakikishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake UN Women Bi. Hodan Addou akisisitiza ushirikishwaji wa mwanamke katika masuala ya kimaendeleo ili kufikia usawa wa kijinsia wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Mwanza.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.ummy Mwalimu akiserebuka mziki pamoja na wanawake wa mkoa wa Mwanza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Mwanza.
Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Mwanza wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoani Mwanza.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW


……………….


Na Mwandishi Wetu Mwanza

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amepiga marufuku mikopo ya laki tano kwa wanawake nchini bali wawezeshwe kupata mikopo yenye tija ili kuwa na uwezo wa kujikwamua kiuchumi.

Ameyasema hayo leo mkoani Mwanza alipokuwa akizungumza na Wanawake na wananchi wa Mkoa wa Mwanza katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Waziri Ummy Mwalimu amesema lengo la kuadhimisha Siku ya Wanawake katika nagzi ya mikoa kwa miaka mitano ni kutoa nafasi ya kujitathimini katika utekelezaji wa masuala mbalimbali kuhusu hali ya ka Maendeleo ya mwanamke.

Amesema kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2019 inasema “Badili Fikra Kufikia Ustawi wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu” Kauli mbiu hii isaidie kubadili fikra katika kuhakikisha tunafikia uchumi wa viwanda kwa kutoa umuhimu kwa mwanamke, mwanaume na taifa zima ili kuona ni kwa jinsi gani ataweza kushiriki katika kulifanikisha hilo.

Amemuagiza Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi kuhakikisha Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wanatoa taarifa za kila robo mwaka za utoaji wa mikopo inayotolewa kwa vikundi mbalimbali katika kila mkoa husika.

“Nimesikitishwa na utoaji mikopo kwa wanawake maana nimetembelea kikundi cha Wanawake kwenye mabanda chenye watu 30 lakini wamepatiwa mkopo wa milioni moja ambao hauna tija kulingana na idadi ya wanachama hao” alisema.

Amesema kuwa ushiriki wa wanaume ni muhimu katika kufikia suala la kijinsia na maendeleo endelevu katika Taifa letu kwani wanaume ni sehemu kubwa katika kuwezesha mwanamke kiuchumi.

Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano iliandaa na kutekeleza Mpango Mkazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto zikiwemo mimba na ndoa za utotoni ambazo ni kikwazo kwa Maendeleo ya wanawake na Mtoto wa kike nchini.


Serikali imeendelea kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutoka Bilioni 8 mwaka 2015 hadi Bilioni 16 kwa mwaka 2017/18 kiasi ambacho ni mara mbili zaidi hivyo kuongeza nguvu katika kumuwezesha mwanamke kiuchumi.

Amewataka wanawake kundokana na unyonge uliopo na kusimama na kujitoa na kupambana hasa katika kugombea nafasi za maamuzi katika uongozi na pia kupendana na kuinuana katika kupeana taarifa na fursa mbalimbali za kimaendeleo.

Aidha ameitaka jamii katika maeneo ya kazi kuondokana na rushwa za ngono jambo ambalo ni tatizo katika upatikanaji wa haki za wanawake na waajiri wa Sekta za Binafsi ni muhimu kuzingatia usalama na haki za wanawake wafanyakazi.

Akimkaribisha mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Philis Nyimbi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana amesema mkoa unatekeleza mikakati mbalimbali katika kumuwezesha Mwanamke na Mtoto wa kike kwa kumuweka mbali na Vitendo vya Ukatili dhidi yao ili kuwawezesha kupata fursa zitakazowezesha kufikia usawa wa kijinsia.

Ameongeza kuwa Mkoa unaendelea na Kampeni za kutoa elimu kwa wananchi katika suala zina la kupinga Ukatili dhidi ya wanawake na watoto ikiwa ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kutokomeza vitendo hivyo.

“Katika kutekeleza Mpango Mkakati wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kwa kuanzisha Kamati za ulinzi wa Mwanamke na Mtoto kuanzia ngazi ya Mkoa, Halmashauri, Kata, Mitaa na Vijiji na kuimarisha utendaji wake ili zisaidie kupambana na Vitendo vya Ukatili katika sehemu zao” alisema.

Akitoa Salamu kwa Wanawake Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula amesema kuwa katika Siku hii mwanamke anatakiwa kujitambua na ni wakati wa wanawake kusimama na kufanya Maendeleo na mwanamke asiyesimama imara mambo mengi huharibika na wanayofursa za kuunga mkono juhudi za mapambano ya kumuwezesha mwanamke.

“Tushikamane mikono wenyewe kwa wenyewe tujikombe sisi kama wanawake ili kuondokana na ukandamizaji na kusisimama na kuwa na sauti moja ili kujiletea Maendeleo yenye fikra chanya” alisema


Naye Mwakilishi Mkazi Umoja wa Mataifa Bw. Alvaro Rodriguez amesema kuwa Umoja wa Mataifa unataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kuhakikisha kunakuwepo na usawa wa kijinsia na kuondoa vikwazo vyote vinavyosababisha kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia kama vile mimba na ndoa za utotoni ambazo zimekuwa zikiwanyima fursa watoto wa kike kutimiza ndoto zao.

Ameongeza kuwa mapambano ya usawa wa kijinsia yatafanikiwa pale yatakaposhirikisha wanaume na wavulana katika kuhakikisha wasichana na Wanawake wanapata fursa sawa katika kutikiza ndoto zao.

Kwa upande wake Mwakikishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake UN Women Bi. Hodan Addou amesema kuwa Shirika hilo linashirikiana na Serikali na Mashirika ya kitaifa kuhakikisha elimu inatolewa na usawa wa kijinsia unakuwa suala la kipaumbele katika Jamii zetu.

Akizungumzia kuhusu Kampeni ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto msanii Nurdin Bilal maarufu kama Shetta amesema lengo la Kampeni hiyo ni kubadili fikra wanaume ambao ni watendaji wakubwa vitendo vya Ukatili Dhidi ya wanawake na Watoto.

Ameongeza kuwa Ukatili wa kijinsia hauathiri wanawake pekee bali hata wale ambao wanaowazunguka hasa Watoto hivyo amewaasa wanaume kuachana na vitendo vya kikatili kwa wanawake.

“Mimi nina amini ukimthamini Mwanamke unaleta maendeleo katika Taifa kwani mwanamke ni nguzo ya Maendeleo kwa Taifa” alisema.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Wanawake Mkoa wa Mwanza Bi. Grace Bunyinyiga amesema kuwa bado mwanamke ana vikwazo vingi katika kuleta chachu ya Maendeleo na kuna haja ya kuwakomboa wanawake wenyewe kifijra wawe mabadiliko katika Jamii husika.

“Wanawake wa Mkoa wa Mwanza wawe kipaumbele katika kuhakikisha uwepo wa usawa wa kijinsia katika Jamii zao na ushiriki wa wanaume na kuondokana na mila na desturi zilizopitwa na wakati ili kuondokana na vitendo vya kikatili” alisema

Katika Maadhimisho hayo Waziri Ummy Mwalimu alizindua Kampeni ya Kupambana na kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto ijulikanayo kama SAWA inayoratibiwa na Msanii SHETTA.

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI SHEREHE ZA MWAKA MPYA 2019 NA MABALOZI WANAOWAKILISHA NCHI ZAO HAPA NCHINI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini katika Sherehe za Mwaka mpya 2019 kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini katika Sherehe za Mwaka mpya 2019 kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza hotuba iliyokuwa ikitolewa na Kiongozi wa mabalozi haonekani pichani wakati wa Sherehe za Mwaka mpya 2019 kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini kabla ya chakula cha jioni alichowaandalia Mabalozi hao katika Sherehe za Mwaka mpya 2019 kwa Mabalozi hao (Diplomatic Sherry Party) zilizofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

FARU 12 KUINGIZWA NCHINI

$
0
0
Katibu Mkuu wizara ya maliasili na utalii Prof.Adolf Mkenda amesema kuwa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Grumeti Fund inatarajia kuingiza faru 10 nchini kwa ajili kuongeza idadi ya wanyama hao hapa nchini.

Kuagizwa kwa Faru hao kutaongeza idadi yao kutoka 2 walioagizwa na taasisi hiyo hapo awali hadi kufikia 12.

Akizungumza katika kikao kilichowahusisha wadau hao wa uhifadhi kilichofanyika katika chuo cha Uhifadhi wa Wanyamapori cha Pasiansi jijiji mwanza, Prof. Mkenda amewashukuru wadau hao kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuimarisha shughuli za uhifadhi nchini.

Amesema Serikali itaendeleza mahusiano mazuri yaliyopo baina yake na wadau wote wapenda maendeleo kwa lengo la kulinda na kukuza shughuli za uhifadhi wa wanyamapori nchini.

Prof. Mkenda amesema kuwa kuletwa kwa faru hao kutaongeza idadi ya wanyama hao hapa nchini na kuongeza kuwa taasisi ya Grumeti imesaidia kuwaleta watu maarufu kutoka katika mataifa mbalimbali kuja kutembelea hifadhi za Taifa na hivyo kuchangia kutangaza utalii na kuongeza pato la Taifa.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa idara ya wanyamapori Tanzania Canisius Karamaga akizungumzia kuhusu ujio wa Faru hao amesema kuwa jitihada zinazofanywa na taasisi hiyo zinalenga kuwaongeza Faru hao hapa nchini.

Ameongeza kuwa Faru hao wataingizwa nchini kwa lengo la kuboresha kizazi cha wanyama hao waliokuwa hatarini kutoweka ikiwa ni moja ya juhudi za kuwafanya waongezeke kwa kuzaliana na wale waliopo nchini.

Amesema kikao hicho kati ya wizara na wadau hao ni muhimu sana kwa kuwa kimejadili na kuangalia kwa utalaam Zaidi namna Faru hao watakavyoingizwa nchini, kutunzwa na kulindwa kwa kuwa wanyama hao ni adimu na muhimu kwa utalii.

Amewataka watanzania kuwa mstari wa mbele kulinda rasilimali za nchi ili ziwe na faida kwa vizazi vijavyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda akisalimiana na watumishi wa Wizara hiyo kutoka katika taasisi za Uhifadhi wa Wanyamapori na wadau kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya Grumeti Fund inayotarajia kuingiza faru 10 kwa ajili kuongeza idadi ya wanyama hao hapa nchini.
Wadau wa Uhifadhi kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya Grumeti Fund wakifuatilia kikao cha pamoja kilichowahusisha viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na watumishi wa Wizara hiyo kutoka katika taasisi za Uhifadhi wa Wanyamapori, kikao hicho kimefanyika katika Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori, Pasiansi jijini Mwanza.
Baaadhi ya Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoka katika taasisi za Uhifadhi wa Wanyamapori wakiwa katika kikao cha pamoja na Wadau wa Uhifadhi kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya Grumeti Fund kilichofanyika katika Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori, Pasiansi jijini Mwanza.PICHA/ Maliasili na Utalii-Mwanza.
 

MPINA AJA KIVINGINE KUONDOA UVUVI HARAMU BAHARI YA HINDI

$
0
0
Wananchi wa Kilwa Kivinje wakishangilia na kusalimiana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina (Mb), mwenye koti la bluu mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara. Picha na John Mapepele
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina (Mb), mwenye miwani akiwasili katika eneo la Kilwa Kivinje kuongea na wavuvi hivi karibuni. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Emil Ngubiagai na kushoto ni diwani Ali Mohamed Yusufu.Picha na John Mapepele
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina (Mb) akiwahutubia wananchi wa Somanga Kilwa. Picha na John Mapepele



Na John Mapepele, Kilwa


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ametangaza kuundwa kanda kuu mpya ya ulinzi wa rasilimali katika Bahari ya Hindi ili kukabiliana na uvuvi haramu ulioshamiri kwa muda mrefu. 

Amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano ina nia thabiti ya kulinda rasilimali hizo ili ziweze kulinufaisha Taifa.

Mpina alitangaza uamuzi huo hivi karibuni wakati akizungumza na wavuvi wilayani Kilwa mkoani Lindi kuhusiana na juhudi zinazofanywa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika kulinda rasilimali hizo na kutolea ufafanuzi wa baadhi ya maombi ya wavuvi ikiwemo kuomba kuruhusiwa kutumia majenereta na taa za sola kaatika shughuli zao za uvuvi wawapo baharini baada ya Sheria ya Uvuvi ya mwaka 2003 kukataza za vifaa hivyo.

Akizungumza kwa nyakati tofauti na wavuvi katika maeneo ya Kivinje na Somanga wilayani Kilwa Waziri Mpina alisema Serikali ya awamu ya tano haina nia kumuonea mwananchi yeyote bali kinachofanyika ni kulinda rasilimalli hizo kwa mujibu wa sheria ili ziwe enedelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Mpina alisema katika kuwasikiliza wavuvi nchini Serikali imeamua kufumua Sheria ya Uvuvi na kanuni zake za mwaka 2009 ili kuondoa maeneo ambayo yanakwaza shughuli za uvuvi ikiwemo kufuta vipengele vilivyokuwa vinalalamikiwa kwa muda mrefu.

Hata hivyo Mpina alikubali ombi la wavuvi nchini kurusiwa kutumia taa za sola na majenereta huku akitaka wavuvi ha kutokamatwa kwa makosa ya kutokuwa na leseni hadi hapo kanuni mpya zitakapotoa Julai mwaka huu.

Pia aliwaomba wavuvi kuwa na subira kuhusiana na ombi la kutaka kuruhusiwa kutumia nyavu za chini ya milimita nane kwani kwani sheria iliyopo ya uvuvi ya mwaka 2003 na Kanuni yake ya mwaka wa 2009 imeweka masharti kuzuia matumizi ya nyavu hizo kwenye ukanda wa bahari hivyo kuwataka kuwa watulivu na kusubiri sheria hiyo ifanyiwe marekebisho.

Mkuu wa wilaya ya Kilwa christopher Ngubiagai alimshukuru Waziri Mpina kwa kufika kuzungumza na wananchi hao kwani ametoa ufafanuzi utakaoondoa sintofahamu iliyokuwa imetanda miongoni mwa wavuvi wa wilaya hiyo huku akiwaomba kuunga mkono juhudi za serikali za kulinda rasilimali za uvuvi.

Mmoja wa wavuvi wa Somanga Mohamedi Kimbwembe aliomba radhi Serikali ya awamu tano kutokana na wavuvi wengi kujihusisha na uvuvi haramu na kuua mazalia ya samaki na kwamba wengi walifanya hivyo baada ya serikali zilizopita kushindwa kuchukuwa hatua dhidi ya waalifu hao.

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Lindi Hamida Abdalha alimshukuru Waziri Mpina kwa kuruhusu matumizi ya jenereta na taa za mwanga wa jua pamoja na kuruhusu wavuvi kutumia leseni moja mambo ambayo yalikuwa yakiwaumiza wavuvi wa Lindi.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images