Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

WAFANYAKAZI WA DAWASA WASHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

0
0

Wanawake ambao ni Wafanyakazi wa Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka Dar es Salaam (DAWASA) leo wameungana na akinamama wa jijini Dar es Salaam kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City. Wafanyakazi hao waliingia na bango lenye ujumbe wa kumshukuru rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuweza kumtua mama ndoo kichwani huku wakiwa wamebeba ndoo ya maji ikiwa ni ishara.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo katika ujumbe wake aliishukuru Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka kwa kuweza kufika asilimia 60 ya utoaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani. 
Pia katika salamu zake Mhe Makonda amewataka akinamama wote kuacha kuwa mstari wa nyuma katika kufanyakazi bali wajitokeze katika kupigania haki zao kwa usawa bila kujali jinsia yao. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wafanyakazi wa DAWASA wakifuatilia hotuba ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.
Wafanyakazi wa DAWASA wakifuatilia hotuba.
 Akinamama wa jiji la Dar es Salaam walifurika katika ukumbi wa Mlimani City kuhudhuria katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
 Mwimbaji Stara Thomas akitoa burudani
 Akinamama kutoka nchini Kenya ambao waliungana na wenzao katika maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani.
 Msanii Mrisho Mpoto akitoa ujumbe kwa akinamama wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

KUELEKEA MIAKA 25 AZIMIO LA BEIJING,WADAU WAKUTANA KUTATHIMINI MUSTAKABALI WA JUHUDI ZA UKOMBOZI WA MWANAMKE NCHINI

0
0
Sehemu ya washiriki wa warsha ya siku moja iliyolenga kutathimini mustakabali wa juhudi za ukombozi wa mwanamke nchini kuelekea miaka 25 ya mkutano wa Beijing hapo mwakani.

Mwenyekiti wa TGNP Mama Assen Muro akitoa rai kwa wadau wote kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi wa changamoto zinazosimama kama vikwazo ili wanawake waweze kupiga hatua katika kufikia maendeleo endelevu. Mwenyekiti wa TGNP Mama Assen Muro akimueleza jambo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa alipowasili kwenye warsha hiyo.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa akizungumza na washiriki wa warsha hiyo ambapo aliwahimiza kutorudi nyuma katika jitihada za kutetea haki na nafasi ya mwanamke katika jamii.

Na Mwandishi Wetu,

Ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kilele ni tarehe 8 ya mwezi Machi kila mwaka,wadau mbali mbali wamekutana jijini Dodoma kujadili na kutathimini mustakabali wa juhudi za ukombozi wa mwanamke nchini kuelekea miaka 25 ya mkutano wa Beijing hapo mwakani.


Warsha hiyo siku moja ambao iliyowakutanisha washiriki zaidi ya 100 kutoka kote nchini  wakiwemo wadau mbalimbali likiwajumuisha wanawake wakiwakilisha  makundi mbalimbali,wabunge,madiwani,wanasheria,waandishi wa habari pamoja na wanafunzi wa vyuo na sekondari,iliandaliwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na TAWLA, Landesa, Msichana Initiative, Haki Ardhi, Haki Elimu, Care International na TAMWA.

Mkutano huo wa Beijing uliofanyika mwaka 1995 ulilenga kuwashirikisha na kuwawezesha wanawake katika maendeleo ili kuimarisha mapambano dhidi ya umaskini na hiyo yote ni kwa wanawake kushiriki katika shughuli za kimaendeleo.

Katika kuhakikisha kila mshiriki anachangia mawazo,ilitumika njia ya kuwagawa katika makundi na kujadili maana,uelewa,umuhimu,mitizamo pamoja na changamoto la azimio la Beijing katika jamii na nchi kiujumla ambapo miongoni mwa hoja zilizoibuliwa katika kuboresha jitihada za kuleta usawa wa kijinsia  ni pamoja na elimu juu ya azimio bado inahitajika sambamba na ushirikishwaji wa jamii yote kwa ujumla sambamba na kueleza faida ya usawa wa kijinsia kuanzia ngazi ya familia ili kutengeneza kizazi chenye kuelewa manufaa yake.

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yanasimamiwa na kauli mbiu inayosema Badili fikra kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu”.

Wawakilishi wa wanawake wa jamii ya wafugaji wilayani Mvomero wakiongozwa na mwenyekiti wa umoja huo Bi. Mariam Simango (wakwanza kushoto) wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika warsha hiyo.

 Akifafanua lengo la warsha hiyo, Mary Ndaro kutoka Care International aliwaambia washiriki kwamba warsha hii ni fursa kwa wanawake kurejea azimio la Beijing imefanikiwa kwa kiasi gani na kujua ni zipi jitihada za kuongeza ili kuendelea kuikwamua hali ya mwanawake katika jamii . Kundi liliojumuisha wanafunzi katika ngazi zote pamoja na vijana likiwa makini kujadili mitazamo na uelewa juu ya azimio la Beijing ambapo kufikia 2020 litatimiza miaka 25 ya maazimio. Akichangia wakati wa majadiliano ya katika makundi,mbunge wa Mtera Mhe.Livingstone Lusinde alisisitiza kuwa azimio la Beijing halina azma ya kuwafukuza wanaume kutoka nafasi zao katika jamii, bali ni juu ya kuinua wanawake kwa hali ya juu ili waweze kupata haki zao kama wanaume na kufanya kazi pamoja kwa maendeleo ya nchi. Anna Marwa kutoka Pelum Tanzania akichangia jambo wakati wa majadiliano ya makundi yaliyolenga kupima umuhimu,mitazamo na uelewa juu ya azimio la Beijing miongoni mwa washiriki wa warsha hiyo.   Zawadi Kondo mwanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha majibu kwa niaba ya kundi lililojumuisha wanafunzi katika ngazi zote pamoja na vijana.

Washiriki wakifuatilia kwa karibu mawasilisho.

Mdau wa masuala ya wanawake ambaye pia ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Rachel Chibwete akiwasilisha majibu kwa niaba ya kundi lililojumuisha wabunge,madiwani pamoja na waandishi wa habari. Wanafunzi kutoka shule ya sekondari Manchali iliyopo Chamwino jijini Dodoma wakicheza kuashiria furaha yao kutokana na fursa ya kushiriki katika warsha hiyo. 

Washiriki wakishikana mikono kama ishara ya umoja na mshikamano ambayo kwa pamoja waliafiki kuwa ni nguzo muhimu katika kufanikiwa kuitetea nafasi ya mwanamke katika jamii.



     Sehemu ya washiriki wakipata picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa 
    Waandaaji nao hawakuwa nyuma kupata kumbukumbu na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa 

    MAAGIZO YA WAZIRI UMMY MWALIMU ALIPOSHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MKOANI MWANZA

    CRDB-TAWI LA MLIMANI CITY WASHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

    0
    0
    Mwanadiplomasia,Gertrude Mongella akizungumza machache na wafanya kazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City leo siku wanawake duniani ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka ambapo amewaasa kufanya kazi kwa bidii na kujitambua katika jamii inayowazunguka. 
    Kaimu Mkurugenzi benki ya Benki ya CRDB tawi la Mlimani City,Adelphina Barongo akizungumza na wafanyakazi benki hiyo katika siku wanawake duniani ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka. 
    Mwanadiplomasia,Gertrude Mongella akikata keki pamoja na wafanya kazi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam kwaajili ya kusherekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka. 
    Mwanadiplomasia,Gertrude Mongella akimlisha keki Kaimu Mkurugenzi benki ya Benki ya CRDB tawi la Mlimani City,Adelphina Barongo 
    Mwanadiplomasia,Gertrude Mongella akiwa katika picha na wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi Mliman City leo katika maadhimisho siku ya wanawake duniani.
    Mwanadiplomasia,Gertrude Mongella akiwa katika picha na wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi Mliman City leo katika maadhimisho siku ya wanawake duniani.
    Afisa wa benki ya CRDB tawi Mliman City,Maureen Mwanda kulia akimkabidhi zawadi Mwanadiplomasia,Gertrude Mongella 
    wafanya kazi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakiwa katika picha ya pampoja mara baada ya kudhimishi siku ya wanawake dunia katika tawi lao jijini Dar es Salaam.

    Wafiziotherapia wajengewa uwezo huduma ya mfumo wa uzazi, nyonga na mkojo

    0
    0
    Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na wataalam wa Fiziotherapia wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu yalioandaliwa na Chama cha kitaaluma cha Wafiziotherapia Tanzania (APTA). Kushoto ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Scomt nchini Uholanzi, Prof. Willy Smeets na Rais wa APTA, Remla Mramba Shirima.
    Baadhi ya wataalam wa Fiziotherapia wakimsikiliza Prof. Museru.
    Mtaalam wa Fiziotherapia, Bi. Ellie Sawayael kutoka Hospitali ya DC Oltrumet mkoani Arusha, akimkabidhi zawadi mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Fiziotherapia nchini Uholanzi Liesbeth Westerih baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo leo.
    Hivi ndivyo mmoja wa wataalam wa Fiziotherapia akifuatilia matukio mbalimbali leo.
    Mtaalam wa Fiziotherapia wa Muhimbili, Bi. Eliela Kaaya amkimpatia keki Prof. Museru ikiwa ni siku ya kuzaliwa kwa Prof. Willy Smeets (kulia).
    Rais wa APTA, Remla Mramba Shirima akimlisha keki, Prof. Willy Smeets kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.
    Mtaalam wa Fiziotherapia, Bi. Neema Tuwa kutoka Hospitali ya WAJA mkoni Geita akipokea cheti kutoka Prof. Museru baada ya kumaliza mafunzo hayo leo.
    Mtaalam wa Fiziotherapia, Bi. Zamia Ladha wa Hospitali ya Gemsa Polyclinic jijini Arusha akipokea cheti kutoka Prof. Museru.
    Prof. Museru akimkabidhi cheti mtaalam wa Fiziotherapia, Bi. Christabella Mugeu kutoka Hospitali ya Aga khan jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza mafunzo hayo leo.
    Prof. Museru akiwa katika picha ya pamoja na wataalam hao leo.




    Mafunzo ya siku tatu kwa wataalam wa Fiziotherapia nchini yamemalizika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), huku wataalam wakitakiwa kutumia elimu walioipata kuwasaidia wanaume na wanawake wenye matatizo kwenye mfumo wa uzazi, nyonga na mfumo wa mkojo

    Pia, wanachama wa Chama cha kitaaluma cha Wafiziotherapia Tanzania (APTA) wametakiwa kutoa mchango wao katika shughuli mbalimbali zinazofanywa na chama hicho kama vile kushiriki mara kwa mara katika shughuli za chama hicho.

    Mkuu wa Chuo Kiku Cha Scomt nchini Uholanzi, Prof. Willy Smeets amemshukuru Mkuregenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru kwa kushiriki kikamilifu katika uandaji wa mafunzo hayo na kwamba ushiriki wake umeonyesha nia ya thati ya kuwajengea uwezo wataalam hao kutoka hospitali mbalimbali nchini.

    “Mafunzo haya yamekuwa ya manufaa makubwa kwa wataalam hawa, ni imani yangu kuna mambo wamejifunza. Pamoja na kwamba tumetoa mafunzo kwenu, Prof. Museru napenda kukujulisha kwamba vifaatiba tulivyokuja navyo tunawapatia, tuwanawaachia ili mvitumie kutoa matibabu,” amesema Prof. Smeets.

    Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Museru amewataka wataalam kuvitunza vifaa hivyo kwa kuwa vitakuwa msaada mkubwa kwa hospitali hiyo pamoja na wagonjwa.

    Pia, Prof. Museru ametaka kuendelezwa kwa mazungumzo ya kuanzishwa kwa kozi ya shahada ya Fiziotherapia katika Chuo Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) ili kuandaa watalaam wengi zaidi na mkurugenzi huyo ameahidi kuunga mkono juhudi za kuanzishwa kwa shahada hiyo.

    Washiriki wanatoka hospitali mbalimbali nchini ikiwamo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), CCBRT, Physiocare Arusha, London Health Centre, Police Barracks, Dar group Hospital, The Aga Khan Hospital -Dar es Salaam, GEMSA Polyclinic, Waja Hospital Geita na International Rescue Committee CBR ya mkoani Kigoma.

    wanafunzi shule ya Sekondari kisutu waaswa kuzingatia masomo

    0
    0
    Meneja wa kampeni ya Binti ya Kitaa David George akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya wasichana Kisutu katika maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani, leo jijini Dar es salaam na kuwahimiza mabinti hao kuishi katika ndoto zao ili kuweza kufikia malengo
     Balozi wa kampeni ya Binti wa kitaa Salama Salim maarufu kama Sandra akiongea na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya wanawake Kisutu katika maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani, na kuwahimiza kuzingatia masomo yao ili waweze kutimiza malengo yao, leo jijini Dar es salaam.
    Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya wanawake Kisutu wakimsikiliza Meneja wa kampeni ya Binti ya Kitaa David George. 
    Picha ya pamoja

    TFDA KANDA YA KATI YAANZA KUTOA ELIMU KUHUSU MADHARA YA VIPODOZI KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI

    0
    0
      Na Jumbe Ismailly SINGIDA

    MAMLAKA ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Kati Dodoma imeanza kutoa mafunzo ya namna ya kudhibiti natumizi ya vyakula,dawa,vipodozi pamoja na vitendanishi kwa lengo la kutoa elimu kwa shule 30 za sekondari zenye jumla ya wanafunzi 12,000.

    Mkaguzi wa TFDA Kanda ya Kati,Abeli Daule aliyasema hayo alipokuwa akitoa elimu juu ya bidhaa ambazo Mamlaka ya Chakula naa Dawa inadhibiti zikiwemo bidhaa za chakula,dawa,vifaa tiba na vitenganishi katika shule nane za sekondari za Halmashauri ya wilaya ya Singida.

    Aidha Daule ambaye pia ni Afisa elimu kwa umma wa TFDA aliweka bayana lengo la kutoe elimu katika shule za sekondari kuwa ni sehemu za kazi ya Mamlaka hiyo kutoa elimu na kwamba sekondari ni wanafunzi wengi ambao tayari wanajitambua, kukiwepo watumiaji.

    “Lakini pia sekondari wanafunzi ambao wengi tayari wanajitambua kwa maana kwamba wengine ni watumiaji lakini na wengine majumbani kwao wanatumwa,lakini pia ni muda ambao wakipewa elimu wanaweza kujua kufanya uchaguzi sahihi lakini pia watapeleka elimu hiyo nyumbani.”alisisitiza Mkaguzoi huyo.

    Kwa mujibu wa Daule endapo wanafunzi hao wa sekondari watapatiwa elimu itasaidia pia kwa namna moja au nyingine kuwadhibiti wafanyabiashara wasio waaminifu wenye utamaduni wa kuikwepa serikali wanapobaini Mamlaka hiyo inafanyakazi, huamua kufunga biashara zao kutoweka kabisa.

    “Kwa hiyo utaratibu huo ni wa taasisi kwa maana kwamba Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati katika utekelezaji wa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2018/2019 basi tumeona tupite katika hizi shule ili tuweze kuwapitia.”alibainisha Daule.

    Naye Kaimu Afisa elimu sekondari wilaya ya Singida,Wolta Jenaeli aliweka bayana manufaa ya mpango huo utasaidia kwa akiasi kikubwa sana kwenye shule 30 zilizopo katika Halmashauri hiyo kupunguza madhara yatokanayo na vipodozi hususani kwa wanafunzi wa kike ni makubwa sana.

    “Kwa hiyo ina maana tunapunguza zinazotokea kwenye mashule yetu kwa sababu umri wa watoto wetu walionao kutumia kila kitu bila kujua madhara yake ni yapi.”alisema kaimu afisa elimu wilaya ambaye pia ni afisa elimu sekondari wa wilaya hiyo.

    Alizitaja baadhi ya shule za sekondari zilizopatiwa elimu hiyo kutoka TFDA kuwa ni pamoja na Ntonge,Amana,Mrama,Kijota, Kijota Hull,Mtinko,Singitu na Mikiwu.

    Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi walionufaika mpango huo kutoka shule ya sekondari Kijota,Hajra Juma alisema mpango huo utawasaidia baadhi ya wanafunzi walioanza kutumia vipodozi hivyo endapo wataendelea kutumia vipodozi hivyo.
     Mmoja wa Maafisa wa TFDA Kanda ya Kati akielezea madhara ya vipodozi vilivyopigwa marufuku kutumika kutokana na muda wake wa matumizi kwisha alipokuwa akitoa elimu ya madhara hayo kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Ntonge,wilaya ya Singida Vijijini.  
     Mkaguzi wa TFDA Kanda ya Kati,Abeli Dauli akitoa elimu katika shule ya sekondari Singitu,Halmashauri ya wilaya ya Singida juu ya madhara ya matumizi ya vipodozi vilivyokwisha muda wake. 
    Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kijota wakiwa katika viwanja vya shule hiyo wakiwasikiliza  maafisa wa TFDA kutoka Kanda ya Kati walipokuwa wakitoa elimu juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya vipodozi vyenye viambato vyenye sumu.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)

    UNAYAKUMBUKA MASHAIRI YA PATRICK BALISIDYA?

    0
    0
    Na Moshy Kiyungi,

    Mashairi ya nguli Patrick Balisidya aliyokuwa akitunga na kuimba katika nyimbo zake, kamwe hayatachuja kufuatia ujumbe uliomo.

    Alikuwa kiongozi wa bendi ya Afro70, ambapo alijizoea umaarufu mkubwa humu nchini hata nje ya mipaka yetu.

    Hata hivyo historia ya muziki haiwezi kumuweka pembeni mwanamuziki huyu Balisidya, aliyezaliwa katika kijiji cha Mvumi mkoani Dodoma Aprili 18, 1946.

    Alikuwa ni wa kabila la Wagogo, ambalo limetoa wanamuziki wengi maarufu akiwemo marehemu Dk. Hukwe Zowose.Mama yake alikuwa mpiga Kinanda Kanisani, kwa mantiki hiyo vikichanganywa na asili ya kabila lake, pasipo shaka muziki ulikuwa ndani ya damu yake.

    Patrick Balisidya wakati akiwa mwanafunzi katika sekondari ya Dodoma, alipewa nafasi ya kuwa kiongozi wa bendi ya shuleni, baada ya kugundulika kuwa na kipaji cha muziki.

    Baada ya kumaliza elimu yake, alikwenda kujiunga na Chuo cha Ufundi jijini Dar es Salaam, kisha alkapata ajira ya muda.Mwaka 1967 Balisidya alichukuliwa kwenda kupiga muziki katika bendi ya Dar es Salaam Jazz B. Nyakati hizo bendi za muziki hata klabu za mpira wa miguu nyingi zilikuwa A na B.

    Baada ya kipindi kupita, mwaka 1970 Patrick alianzisha bendi yake mwenyewe aliyoipa majina ya Afro70.Bendi hiyo ilianza kupiga muziki maridadi na kuonekana kama tishio kwa bendi zingine kubwa zilizokuwapo wakati huo.

    Bendi hiyo alikuwa ikitumia mtindo wa Afrosa, uliobuniwa na nguli huyo.
    Balisidya alikuwa mbunifu katika muziki, kwa muda mrefu alikwepa sana kuingia katika wimbi la kufuata mapigo ya Kikongo.Mwaka 1979, alipata fulsa ya kwenda nchini Sweden, huko alishirikiana na kikundi cha Archimedes, wakatoa album nzuri sana iliyoitwa ‘Bado Kidogo’.

    Kuna wakati Patrick alijiunga na bendi ya Orchestra Safari Sound, (Masantula), aliweza kupiga Piano katika wimbo maarufu wa ‘Unambie siri’.
    Balisidya alikuwa na talanta nyingi za ziada katika muziki. Licha ya kutunga na kuimba, pia alikuwa na uwezo mkubwa wa kubofya kinanda.
    Baadhi ya nyimbo walizotunga na kupiga wakiwa na bendi ya Afro70, ni pamoja na Harusi, Dirishani, Weekend, Tausi, Pesa, Nakupenda kama Lulu, Ni mashaka na Mahangaiko.

    Patrick Balisidya na bendi yake ya Afro70, iliwahi kuteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika maonesho ya mtu mweusi yaliyofanyika katika jiji la Lagos, nchini Nigeria yaliyojulikana kama (FESTAC Festival 1977).
    Kabla ya kuondoka wakati huo serikali ilikuwa imemtaarifu kuwa ndiye atakuwa mwakilishi.

    Kwa bahati mbaya pamoja na kuteuliwa huko, vyombo vyake vyote vya muziki vilikuwa vimeharibika katika ajali ya gari.Kwa bahati njema Serikali ilikuwa tayari imenunua vyombo vipya kwa ajili ya bendi yake ya Wizara ya Utamaduni wakati huo.Balisidya na bendi yake wakaenda Lagos kwenye maonesho hayo wakiwa na vyombo muziki vipya.

    Mara nyingi alikuwa akitamka kuwa aliaahidiwa kuwa vyombo hivyo vitakuwa vyake baada ya maonesho hayo ya Nigeria.Lakini waliporejea nchini, kiongozi mwingine wa serikali aliamumuru vyombo hivyo kurudisha serikalini.Taarifa hiyo haikuwa njema kwa Balisidya, aliyekuwa na imani kubwa kwamba atakabidhiwa yeye.

    Alitumia muda mwingi kujaribu kudai haki aliyokuwa akidhani yake, lakini uongozi wa serikali wakati huo ukawa unamkwepa.Hata hivyo vyombo vilitumika kuanzisha bendi ya Asilia Jazz iliyokuwa ikimilikiwa na Wizara ya Utamaduni na Vijana.Kitendo hicho cha kunyang’anywa vyombo hivyo, Balisidya na wanamuziki wenzake wakawa hawana la kufanya, na ndipo ikiwa mwazo wa kifo cha bendi hiyo ya Afro70.Patrick Balisidya kwa mapenzi yake mungu, alifariki Agosti 07, 2004 na kuzikwa Agosti 12, 2004 katika makaburi ya Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam.

    Daima atakukumbukwa Patrick Balisidya, Mungu ailaze roho yako pahala pema peponi, Amina.


    Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa namba:

    0713331200, 0736331200, 0767331200 na 0784331200.

    PICHA ZA PATRICK BALISIDYA.


    MWANZO MWISHO WA MAISHA YA SHAKILA BINT SAID.

    0
    0
    Ni zaidi ya miaka miwili tangu atutoke Shakila Bint Said, aliyekuwa nguli katika miondoko ya muziki wa taarabu humu nchini na Afrika Mashariki na Kati kwa ujumla.

    Wakati wa uhai wake, aliweza kuonesha umahiri wake wa uimbaji wa taarabu katika bendi zote alizowahi kuzitumikia.

    Shakila alifariki ghafla ambapo Binti yake wa mwisho aitwaye Shani, alisikika kupitia vyombo mbalimbali vya habari akisema kuwa mama yake Bi. Shakila alianguka gahfla alipokuwa akifagia muda mfupi mara baada ya kufanya ibada ya magharibi nyumbani kwake Charambe jijini Dar es Salaam Agosti 19, 2016.

    Alikuwa na Weledi wa kujuwa jinsi ya upangiliaji wa sauti kupitia maneno ya lugha adhimu ya Kiswahili katika nyimbo zake zote alizoimba.

    Shakila hakuimba nyimbo za mapenzi pekee, alikuweza kuimba nyimbo zinazoigusa jamii, za siasa na Ukombozi. Wasifu wa Bi. Shakila unaeleza kuwa alizaliwa mnamo Juni 14, 1947, Wilayani Pangani, mkoa wa Tanga.

    Miaka ya nyuma zao la Mkonge lilikuwa na soko kubwa ulimwenguni, Tanganyika wakati huo ikiuwa ni nchi mojawapo iliyokuwa ikizalisha kwa wingi zao hilo.Wamiliki wa mashamba ya Mkonge walikuwa wakiwachukua watu ‘Manamba’ kuwapeleka kufanya kazi ya vibarua katika mashamba hayo.

    Manamba hao walipofika huko waliamua kuoa wake akiwemo Mzee Said Hamis baba yake aliyekwenda Tanga akitokea wilayani Kiomboi mkoani Tanga. Mzee huyo alifuatana na vijana wenzake kutafuta vibarua katika mashamba ya Mkonge.

    Mzee huyo alioa mwanamke aliyekuwa wa kabila la Zigua toka mkoani Tanga wakaweza kumpata mtoto wakampa majina ya Tatu bint Said.Alikulia katika malezi mema ya baba na mama yake, na alipofikisha umri wa kwenda shule, aliandikishwa kuanza masomo katika shule ya Msingi Pangani mkoani humo.

    Tatu bint Said aliolewa na mume wake wa kwanza Khatibu Akida akiwa na umri wa miaka 11, wakafanikiwa kupata mtoto mmoja.Mume huyo alikuwa mbofya Kinanda maarufu ambaye ndiye aliyemshawishi kuingia katika tasnia hiyo ya muziki wa taarabu.

    Tatu alikubali ushauri wa mumewe akaanza kufanya mazoezi makali ya kutunga na kuimba nyimbo za taarabu.Baada ya kuonekana kuwa ana uwezo mkubwa, mumewe Khatibu alimshawsihi kujiunga katika kundi la Kijamvi taarabu lililokuwepo mjini Pangani mkoani Tanga.

    Hakudumu kwa kipindi kirefu na kikundi hicho akalazimika kuhamia mjini Tanga kumfuata mumewe Khatibu Akida.Alipofika huko alijiunga katika kundi la Al Watan, lakini kwa sababu ambazo hazikuelezwa, Tatu akiwa katika kundi hilo hakupewa nafasi ya kuimba mbele ya kadamnasi.

    Kitendo hicho kilisababisha yeye na mumewe baada ya muda mfupi wakahamia katika kundi la lililokuwa likimilikiwa na mzee Kiroboto la Young Novelty mwaka 1961.Msomaji wa makala hii itakumbukwa miaka ya 1960 hadi 1980 Sinema za Kihindi zilichukuwa nafasi kubwa katika kumbi nyingi hapa nchini.

    Katika sinema hizo watu walimshuhudia mwimbaji wa nyimbo za Kihindi aliyekuwa akiitwa Shakila.Hivyo wapenzi na mashabiki wa miondoko ya taarabu wa wakati huo walilinganisha na sauti ya Tatu Saidi kuwa haitofautiani sana na ya Shakila, wakampachika jina hilo

    Shakila bint Said alikuja kuwa miongoni mwa waanzilishi wa kundi la taarabu la Black Star, ambako alionesha cheche zake baada ya kuachia tungo yake ya “Duniani nakupenda wewe”.

    Aidha alifanikiwa kuimba wimbo mwingine unaoitwa “Jogoo acha makuu”, ukiwa ni utunzi wa Awadhi Seif, walishirikiana kuimba na mwimbaji Hamadi Mrisho.Yaelezwa kuwa wimbo huo uliwavutia mamia ya mashabiki waliokuwa wakijazana kwenye kumbi ambazo Black Star ilikuwa ikitoa burudani.

    Hiyo ilielezwa kuwa ilitokana na uwezo mkubwa wa Bi. Shakila kuweza kucheza na sauti katika nyimbo za taarabu.Ndani ya kundi hilo ambalo lililokuwa likimilikiwa na Soud Saidi, Shakila aliweza kufanya makubwa katika uimbaji wake uliokuwa ukiwavutia watu wengi.

    Ndani ya mwaka mmoja alifanikiwa kuimba nyimbo kali kama vile Kitumburi, “Macho yanacheka” na “Kifo cha mahaba”.Black Star walimpa majukumu mazito Bi Shakila, karibia nyimbo zote za kundi hilo, sauti yake ilisikika na kuweza kuipandisha chati bendi hiyo.

    Alidumu ndani ya Black Star kwa miaka kumi, tangu mwaka 1961 mpaka 1971, baadaye alihama na kwenda kutafuta maisha bora sehemu nyingine.

    “…nikiwa Binti wa umri wa miaka 18, niliondoka Black Star baada ya kuitumika kwa kipindi kifupi, nikaenda kujiunga katika kundi la Lucky Stars lililokuwa mjini Tanga…” alisema Bi. Shakila.

    Shakila alifanya ‘kufuru’ akiwa katika kundi hilo kwa kuimba nyimbo nyingi zenye maudhui maridhawa kwa jamii.Nyimbo hizo ni pamoja na Mapenzi ni kama donda, Mapenzi yamepungua, Bunduki bila risasi, ’Viva Frelimo, Viva Samora, Kitanda kuwekwa pembeni na nyingine nyingi.

    "Nilianza muziki mwaka 1960 kabla ya nchi yetu haijapata Uhuru na nimekuwa huko kwa miaka mingi. Wakati nikianza muziki, nilimkuta marehemu Saada Binti Saad na Fatuma Binti Baraka ‘Bi Kidude’ yeye akiwa tayari amejiunga na ngoma za Unyago.

    Alikuwa bibi yangu na mtu wa karibu sana na mimi wakati huo nilikuwa na miaka sita...” Shakila aliwahi kutamka.Akiyaelezea maisha yake ya ndoa, alisema kuwa aliolewa na mume wa kwanza akiwa na umri wa miaka 11.

    Katika ndoa yao waliweza kupata mtoto mmoja lakini ndoa hiyo ilidumu kwa kipindi kifupi cha mwaka mmoja wakahitilafiana hadi kuachana.
    Shakila aliyekuwa na haiba yenye mvuto, aliolewa tena na mume mwingine aliyepata naye watoto watano.

    Kwa bahati mbaya mnamo mwaka 1975 mume huyo alifariki baada ya miaka 18 ya ndoa yao. Akakaa Eda kwa mujibu wa taratibu ya dini ya Kiislamu.

    “…baadaye niliolewa na mume mwingine huyo nilizaa naye watoto watano baadaye tukaachana. Nikaolewa tena kwa mara ya nne nikaza watoto wawili. Nilipokuwa na mimba ya mtoto wangu wa mwisho Shani mwaka 1993, mume wangu akaniacha…” alisema Shakila.

    Rais wa awamu ya kwanza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alikuwa ni mmoja wa viongozi waliokuwa wakivutiwa na uimbaji wa Tatu bint Said ‘Shakila’, hata marehemu mzee Rashid Mfaume Kawawa.

    Baadhi ya mikutano ya hadhara Bi. Shakila alikuwa akialikwa kutumbuiza kabla ya Mwalimu Nyerere ama Kawawa kuhutubia.

    Kwa Weledi wake mkubwa ulipelekea mwaka 1987 kukubali ushawishi wa aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo Dk. Salim Ahmed Salim, pamoja na makada wa Chama Cha Mapinduzi Moses Nnauye na Abdurahman Kinana, kumuondoa Tanga kwenda kuwa mkufunzi wa kikundi cha taarabu cha Jeshi la Kujenga Taifa Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

    Bi Shakila akiwa na kundi la hilo la JKT kati ya miaka 1980 na 1990, aliendeleza wigo wa umaarufu ndani ya nchi hata Afrika Mashariki na Kati kwa ujumla.

    Akiwa na kundi hilo alifyatua wimbo wa ‘Kitanda kukaa Pembeni’ ambao alikiri kuwa ulikuwa ukimkuna sana hususan baada ya kukosa majibu akaonekana kuwazidi uwezo wa utunzi wasanii wenzake.

    Shakila aliwahi kutamka kuwa aliimba kibao hicho mwenyewe kikiwa na nia ya kuuliza swali hilo ili apatiwe jibu toka kwa wasanii wenzake, hasusan wale wa muziki wa taarab.Alisema kuwa tangu aimbe kibao hicho ni miaka 25 imekwishapita, lakini hakuna msanii yeyote wa taarab au mwimbaji wa muziki mwingine aliyethubutu kumjibu swali lake hilo.

    “Niliimba kibao hicho nikiwa na nia ya kujibiwa swali langu, lakini cha kushangaza hadi leo hii, bado swali langu hilo halijajibiwa na mimi sijakata tamaa bado nasubiri jibu litakaloniridhisha…” alisema Bi. Shakila aliyeacha wajukuu 20.

    Wakati wa uhai wake Tatu Said Khamis maarufu kwa jina la Bi. Shakila, alikuwa mmoja wa waasisi wa muziki wa taarabu nchini na Mwenyekiti wa Chama cha Waimbaji wa taarabu Tanzania.

    Akielezea taarabu ya wakati huu alisema “….mwanzoni taarab haikuimbwa bali ilighaniwa, na ndiyo maana waimbaji wake walikuwa wanakaa `kitako` na kutulizana huku wakifikisha ujumbe.

    Miaka inavyokwenda na ndivyo taarab inavyozidi kupoteza mwelekeo na kuichafua jamii badala ya kuijenga kama ilivyoasisiwa kufikisha ujumbe na kukuza lugha ya Kiswahili…”

    “Tumebaki na Taarab inayokwenda kama Kuku aliyokatwa shingo, taarab isiyotazamwa na watoto na wazazi wao…” alilalama Shakila.Pamoja na sifa zote hizo alitamka kuwa hakufaidika na jasho lake na hata kama alifaidi siyo faida inayolingana na jasho lake alilotumia.

    Shakila aliwahi kutamka kuwa yeye ni miongoni mwa Wasanii ambao hawakunufaika kwa jasho lao kama ilivyo kwa wasanii wengi wa zamani kutokana na mfumo mbovu.

    Sauti yake nyororo alikuwa hatofautiani sana na ya Bi. Aisha Abdul maarufu ‘Malika’ anayeishi hivi sasa nchini Marekani hata Bi. Mwanahela anayeishi mkoani Tanga.

    Bi. Shakila alistaafu muziki akiwa katika bendi ya Jeshi la Kujenga Taifa mwaka 2009.Licha ya kustaafu kwake, alikuwa aikiitwa kwenda kuimba na kundi lake hilo la JKT ambapo alikuwa akilipwa ujira wa sh. 3,000 wakati akifanya onesho moja.

    Tatu Said ‘Shakila’ alikuwa akilalamika kuwa baada ya kustaafu, hakuwa na pesa za kujikimu kimaisha kwa kuwa kiwango alichokuwa akipokea kama kiinua mgogo cha sh. 80,000 kwa mwezi toka NSSF, kilikuwa hakimtoshi kabisa. Alilazimika kuishi kwa kupika na kuuza visheti na vitumbua.

    Bi. Shakila alikuwa mbioni kumalizia albamu yake ya ‘Mama na Mwana’ ambayo ingelikuwa na nyimbo nane na kati ya hizo, tano zilikuwa zimekamilika ukiwamo wa ‘Mama na Mwana’

    Aidha katika mikakati ya kuimba tena wimbo wa “Kifo cha Mahaba” alikuwa amedhamiria kumshirikisha mwanamuziki wa kizazi kipya Naseeb Abdull ‘Diamond Platnumz’.Katika maisha yake Bi. Shakila alibahatika kupata watoto 15, 12 kati yao bado wapo hai.

    Binti yake anayejulikana kwa jina la Mape, ndiye pekee aliyetajwa kwa aliyerithi mikoba ya taarabu ya mama yake.Shani ambaye ni binti yake wa mwisho, alionesha ujasiri mkubwa katika kipindi kigumu cha msimba wa mama yake kwa kuweza kueleza chanzo cha kifo cha mama yake mbele ya vyombo vya habari.

    Alisema kuwa mama yake hakuwa anaumwa ila baada ya kumaliza kuswali sala ya Magharibi, alianguka ghafla na alipofikishwa hospitali alielezwa kuwa tayari amekwisha fariki.Bi. Shakila Saidi alizikwa Agosti 20, 2016 katika makaburi ya Uwanja wa Ninja huko Mbagala Charambe jijini Dar es Salaam. 

    Bi. Shakila, hatutakusahau kamwe, mungu uipumzishe roho yako pahala peponi, Amina.


    Imeandaliwa na Moshy Kiyungi

    EXTRA MUSICA ILIVYOTIKISA KONGO BRAZAVILLE.

    0
    0
    Na Moshy Kiyungi,Dar es Salaam.

    Muziki wa dansi umeshika nafasi kubwa katika burudani katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Kongo Brazzaville.

    Watu wa nchi hizo wanaongea lugha moja ya Lingala pia wamepakana. Aidha sehemu ya mipaka yao imetenganishwa na mto Kongo.

    Katika makala hii inaizungumzia bendi ya Extra Musica, iliyoko Kongo Brazzaville.

    Bendi hiyo ilianzishwa mwaka 1993 jijini Brazzaville, ikiasisiwa na wanamuziki akina Ibabi Okambi Rogatien ‘Roga Roga’, ambaye ni mahiri kwa kulicharaza gitaa la solo. Aidha Roga Roga ndiye kiongozi wa kundi hilo hadi sasa. Muasisi mwingine ni Espe Bass, ambaye ni muungurumishaji wa gitaa la besi.

    Mwaka 1995, wanamuziki wa bendi hiyo waliachia albamu yao ya kwanza ya Nouveaux Missiles, iliyowatambulisha vyema kwenye ulimwengu wa muziki.

    Albamu hiyo ilipambwa na nyimbo nyingi kali hususani ule Fred Nelson. Wanamuziki walioshiriki kwenye albamu hiyo mbali na Roga Roga na Espe Bass, ni pamoja na Guy Guy Fall, Quentin Moyascko, Oxygen Mbon Slyvain, Dou Dou Copa ‘Elenga Laka Bienvenu’, Dominique, Christian na Herman Nagasaki ambao wote ni waimbaji pamoja na kunengua.

    Wanamuziki wengine walikuwa akina Killa Mbongo aliyekuwa ‘rapa’, Durell Loemba, ambaye ni mcharazaji wa gitaa la rhythm, kwa upande wa uchanganyaji drums, yupo Ngolali G’Ramatoulaye na Christian Kingstall alikuwa anabofya kinanda.

    Wanamziki wa bendi hii ya Extra Musica walijizolea sifa lukuki, wakapendwa na wapenzi wengi kwa jinsi walivyo wajuzi katika kulishabulia jukwaa wakinengua katika maonesho yao yote ikiwahusisha wanamuziki wenyewe kunengua, tofauti na bendi nyingine ambazo hutumia wanenguaji wa kike.

    Ndiyo sababu wao walipenda kujiita wao ni ‘La Difference’ (wa tofauti).
    Kwenye albamu hiyo ya kwanza, kulikuwa na wanamuziki wengine ambao hawakupata nafasi ya kurekodi wakiwemo akina Pinochet Thierry, Regis Touba, Cyrille Molanga na Arnaud Luguna.

    Albamu hiyo ya Nouvoeaux Missiles, ilisababisha wanamuziki wengine nje ya bendi yao kuvutiwa nayo mmojawapo alikuwa ni Samba Brice ‘Abillissi’, aliyeamua kujiunga nao.

    Albamu ya pili ya Confirmation ya mwaka 1996, ilipelekea kundi hilo kuzidi kutikisa vilizvyo hadi wakapata mialiko mingi barani Afrika na Ulaya.
    Yaelezwa kuwa albamu hiyo ya Confirmation iliuza nakala nyingi mno kuzidi ile ya mwanzo.

    Lakini mafanikio hayo yalisababisha kuzuka kwa mgogoro mkubwa wa kimasilahi. Hali iliyofanya baadhi ya wanamuziki wake wakiwamo akina Christian na Guy Guy Fall, kujiondoa kundini japokuwa kuondoka kwa wanamuziki hao, Extra Musica iliendelea kuwa imara.

    Ilipotoka albamu ya tatu ya Ouragan mwaka 1997, wanamuziki Herman Nagassaki na Samba Brice ‘Abilliss’, waliziba vilivyo mapengo ya Guy Guy Fall na Christian .

    Mgogoro wa chini kwa chini ulikuwa ukifukuta miongoni mwa wanamuziki wa bendi hiyo na uongozi.Baadhi ya wanamuziki walishindwa kuvumilia wakaihama bendi hiyo.Wanamziki hao walikuwa ni Arnaud Laguna, Quentin Mayascko, Durell Loemba, Cyrille Malonga, Regis Touba na Pinochet Thierry.

    Wakaenda kuunda kundi lao jingine walilolipa majina ya Z.I. International, chini ya uongozi wa Cyrille Malonga, Regis Touba, Pinochet Thierry na Durrell Loemba.

    Baada ya bendi ya Extra Musica kukimbiwa na wanamuziki hao, walikaa chini na kuamua kuwatafuta wanamuziki wengine vijana wenye vipaji vikubwa.

    Walifanikiwa kuwapata vijana hao akina Gildas Pozzi, na Emery Mboma. Wakati huohuo Sonor alichukua nafasi ya ucharazaji wa gitaa la rhythm, lilokuwa likishikwa na Durell Loemba.

    Mara baada ya kuwaingiza vijana hao kundini, mwaka 1998 waliachia albam yao ya nne ya Extra Major.Albamu hiyo ilivunja rekodi ya mauzo ya albamu zote za awali na kuwaletea tuzo nyingi barani Afrika, ikiwemo ya Kora kwa kuteuliwa kuwa bendi bora ya muziki kwa bara la Afrika.

    Mwaka uliofuatia waliachia albamu nyingine tano zilizokuwa kali mno.
    Kati ya albamu hizo ile ya Shalai ilisababisha kuwapata wanamuziki wengine wakali akina Papy Batin Maboulango na Boudouin Massipi.

    Rapa wao wa kutumainiwa Killa Mbango, alijitoa kundini akaachana na muziki. Lakini baadaye alirejea tena kundini.Extra Musica ilichukuam kipindi kirefu kutoa albamu ya sita ya Trop C’Est Trop ya mwaka 2001.

    Rapa mwingine alijulikana kwa jina la Arafat, nae alijiunga na bendi hiyo, akichukua nafasi iliyoachwa wazi kwa mara nyingine tena na Killa Mbongo.
    Baada ya kutoka na albamu hiyo, waliamua kubadilisha kidogo majina ya bendi yao ikaitwa Extra Misica Zagul.

    Mara baada ya kutoa albamu ya saba ya Obligatoire mwaka 2004, mwimbaji wao Dou Dou Copa naye akajiondoa kundini akafuatiwa na Oxygene mwaka 2005.Kuodoka kwa wanamuziki hao hakukuithiri Extra Musica Zagul, kwani waliachia albamu ya nane ya La Main Noire mwaka 2006 na nyingine ya tisa ya Sorcellirie ‘Kindoki’ ya mwaka 2011.

    Pamoja na kukimbiwa na vijana wake wengi, kiongozi wao Roga Roga, bado anaendelea kuamsha muziki mkali akiwa na vijana wengine wenye vipaji vikali.Hili ndilo kundi la Etra Muzica Zagul kutoka Kongo Brazzaville, japo sasa kuna makundi mengine kadhaa yamezaliwa kutokea ndani ya bendi hiyo.

    THTU:Mkakati unahitajika katika kupunguza idadi ya watoto wenye kichwa kikubwa na Mgongo wazi.

    0
    0

    Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

    Chama cha wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu (THTU) kimesema katika kupunguza vifo vya Watoto chini ya miaka mitano nchini, lazima jitihada za kimkakati zichukuliwe katika kupunguza ongezeko la kuzaliwa Kwa watoto wenye ugonjwa wa kichwa kikubwa na mgongo wazi.

    Akizungumza na wazazi wa Watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi waliopo katika kituo cha Uzima Mission Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake THTU Taifa Salma Fundi amesema katika kusherekea siku ya wanawake wameona kuna umuhimu wa kujua hali ya Watoto wenye matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi na kueleza jamii juu ya tatizo hilo na kutaka wadau kuongeza nguvu katika utaoaji wa elimu kwa wanawake pindi wanawake wanapokuwa wajawazito lakini pia utoaji huduma Kwa watoto wenye hali hiyo kwani wanamahitaji mengi. 

    Fundi amesema kuwa matatizo ya ugonjwa huu kwa Watoto wakati mwingine hutokana na kukosa elimu juu ya matumizi ya vidonge vya Folic acid, hivyo kama elimu ikitolewa kwa msisitizo tatizo hili linaweza kupungua kuliko ilivyosasa.

    Taasisi mbalimbali na Jamii kwa ujumla, lazima tubadilike na kuweka mkakati juu ya Watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi ili kufikia malengo yakupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano, kupunguza gharama za matibabu kwa serikali pamoja na umaskini kwani mama mwenye mtoto wa ugonjwa huo huwa hawezi kuzalisha na kubaki tegemezi kipindi chote cha kuuguza.

    Katika kuadhimisha siku hiyoTHTU kwa kushirikiana na wadau wengine ( NMB Bank Tawi la Morogoro Road na kampuni ya HQ wamepeleka msaada wa kadi za bima ya Afya kwa Watoto 12, vipima Joto kumi na katoni Moja ya pampers ikiwa ni kuchangia huduma za Afya kwa watoto hao. 

    Nae Mratibu wa Chama cha Wazazi wenye Kichwa kikubwa na Mgongo Wazi Hidaya Alawi amesema chama kinawatoto zaidi 1200 ambao hao wamefikishwa katika sehemu za huduma za Afya. Alawi anasema japo kundi kubwa la watoto wenye tatizo hili bado hawajafikishwa kwenye huduma.

    Nae Mkurugenzi wa Youth With A Mission Tanzania Jeremiah Kiwinda amesema kuwa baada ya kuona wazazi wanaotoka mikoani na kuja Hospitali ya Muhimbili kwa watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wakaona kuna umuhimu wa kuwapatia malazi na chakula ili kuwaokolea gharama kwa huduma hizo katika Kituo cha Uzima Mission ni Bure.

    Amesema kuwa wakiwa katika kituo hicho wanapatiwa mazoezi kwani bila kufanya hivyo kutokana na gharama mbalimbali akiruhusiwa wazazi wengi ni vigumu kurudi.
     Kaimu Katibu wa Kamati ya Wanawake THTU  Roselyne Massam akimkabidhi bima ya afya mmoja ya wazazi wenye watoto wenye Kichwa na Mgongo Wazi katika kituo cha Uzima Mission wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
     Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake THTU Taifa Salma Fundi akipeana na Mkona na mmoja wazazi wenye kichwa kikubwa na Mgongo Wazi ikiwa shukrani ya msaada katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
     Picha ya pamoja ya wadau waliojitokeza kutoa msaada wakiwa na viongozi wa Kituo cha Uzima Mission na wazazi wenye watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi waliokaa chini katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

     Mratibu wa Chama cha wazazi wa watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi Hidaya Alawi akizungumza kuhusiana na malezi ya watoto hao na mahitaji wanayotakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
    Wazazi wenye watoto wa kichwa kikubwa na mgongo wa wazi wakipokea msaada wa pampers  ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

    JEZI ZA MTANANGE WA SIMBA NA YANGA HOUSTON ZAWASILI

    0
    0
    Jezi za Yanga
    Jezi za Simba

    Mtanange unaosubiliwa kwa hamu Houston na vitongoji vyake, pambano la watani wa jadi Yanga na Simba litakalochezewa katika viwanja vya Cullen Park anuani ni 19008 Saums Rd, Houston, TX 77084. Kila mwaka jezi za timu hizo hudhaminiwa na DELINA GROUP kampuni ya Davis Mosha yenye makao makuu Sinza.

    Mpambano huo ambao huchezwa mara mpja kila mwaka na timu ya Yanga ikiwa ikizidiwa ujanja na timu ya Simba, mara zote timu hizi zinapokutana mpambano unakua mkali sana na huwezi kutabili mshindi mpaka dakika ya 90. Mechi ya kwanza Columbus, Ohio Simba iliibuka mshindi kwa kuifunga Yanga 2-1 na mechi iliyochezwa DMV na kuchezeshwa na refarii Kazi kutoka Tanzania, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 na katika mikwaju ya penati Simba ilipata penati 4 na Yanga ilipata penati 3 na hivyo kukubali kipigo kingine kutoka kwa Simba.

    Mechi hizi za Yanga na Simba ni sehemu ya kusherehekea Old School Reunion ambayo mwaka huu inafanyika Houston, Texas ambayo safari hii itakua ya aina yake na si ya kukosa.

    Old School Reunion ilianzishwa kwa lengo la kuwakutanisha vijana wa enzi zilee katika kukumbuka enzi zao, kwa michezo na burudani inayowakumbusha miaka hiyo walipokua vijana.

    Tamasha hili la Old School Reunion lilianzia Columbus, Ohio mwaka 2017, na mwaka uliofuata lilifanyika DMV na sasa mwaka huu mwezi March tarehe 22 na 23 litafanyika Houston, Texas.

    Mwitikio ni mkubwa wadau mbalimbali ndani na nje ya Marekani hujitokeza kuhudhuria onyesho hili la vijana wa zamani linalo waunganisha madj wakongwe na madj wenyeji wa jimbo linakofanyikia.

    Old School Reunion hii ya mwaka huu, 2019 ni ya aina yake kwa jinsi ya mwamko ulivyokua mkubwa kutoka kila pembe, wadau wengi wameipania sana na hasa inavyokuja mechi ya Yanga na Simba huvutia wachezaji wengi husafiri kutoka kila jimbo ikiwemo Canada na Sweden. Inakua mechi ya kukamiana sana, hakuna timu inayotaka kupoteza mchezo. 

    Michezo mingine inayokuwepo ni mpira wa kikapu ambayo hukutanisha wachezaji wa zamani waliochezea timu za Pazi, Vijana Don Bosco na timu nyingine za mchezo huo nchini Tanzania.

    Old School Reunion itaanzia Ijumaa March 22, 2019 kwa usiku utakaotawaliwa na nyimbo zinazotamba sasana usiku huo utaitwa KARIBU NIGHT na siku ya Jumamosi saa kumi kamili jioni utachezwa mpambano wa Simba na Yanga na baadae usiku ndio siku inayosubiliwa kwa hamu OLD SCHOOL REUNION usiku utakaowakutanisha vijana wa zamani kukumbuka enzi zao.

    Yote haya yatafanyika kwenye paa moja CRYSTAL PALACE PARTY HALL anuani ni 12450 Bissonet # 220, Houston, TX 77099. KARIBU HOUSTON UANDIKE HISTORIA

    ZENJ TV NA ZENJ FM ZAMLILIA EPHRAIM KIBONDE

    RAIS MSTAAFU KIKWETE, RC MAKONDA NA WAZIRI MWAKYEMBE WAHANI MSIBA WA KIBONDE

    0
    0
    Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mtangazaji wa Clouds FM, Efraim Kibonde wakati alipokwenda nyumbani kwao marehemu, Mbezi Beach jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia, leo Machi 9, 2019.
    Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili nyumbani kwa alieyekuwa mtangazaji wa Clouds FM, Merehemu Efraim Kibonde leo Mbezi Beach jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia, Machi 9, 2019. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe na kushoto ni Mkurugenzi wa Clouds Media, Joseph Kusaga
    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitoa pole kwa Mkurugenzi wa Clouds Media, Joseph Kusaga alipowasili nyumbani kwa alieyekuwa mtangazaji wa Clouds FM, Merehemu Efraim Kibonde leo Mbezi Beach jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia, Machi 9, 2019. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.
     Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na  Samson Job Kibonde(kushoto) ambaye ni baba mzazi wa aliyekuwa Mtangazaji wa Clouds FM, Marehemu Ephrim Kibonde wakati alipokwenda nyumbani kwao marehemu, Mbezi Beach jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia, Machi 9, 2019. Kulia ni Mkurugenzi wa Clouds Media, Joseph Kusaga

    TCRA YATOA UFAFANUZI KUHUSU KUPUNGUZA GHARAMA ZA KUSAJILI MITANDAO YA KIJAMII 'BLOGS & ONLINE TV"

    0
    0
    Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo 

    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema haiwezi kuzungumzia chochote kuhusu gharama za usajili wa mitandao ya kijamii inayotoa maudhui mtandaoni kwa sababu ni sheria na ili kupunguza gharama hizo lazima mchakato wa kisheria ufuatwe kwa kupitia bungeni.

    Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya utangazaji kupitia Televisheni na Redio za kawaida na mitandaoni (Blogs & Online Tv) kutoka Kanda ya Ziwa Victoria uliofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

    Mhandisi Mihayo alitoa kauli hiyo akijibu swali la Mmiliki wa Malunde Media (Malunde 1 blog), Kadama Malunde aliyeiomba TCRA kupunguza gharama za usajili wa Mitandao ya Kijamii ili kuwasaidia vijana walioamua kujiajiri kupitia mitandao waendelee kutoa huduma za maudhui mtandaoni.

    "Hizi gharama wanazotozwa hawa watoa huduma za maudhui mtandaoni ni ndogo ukilinganisha na zile gharama zinazolipwa na watu wa Televisheni na Radio, kwanza watu wa Mtandaoni wana leseni ya kimataifa, anapochukua habari anaenda kuzipakia kwenye mtandao zinaonekana dunia nzima lakini nyinyi (Tv na Radio) mna leseni kulingana na eneo husika",alisema Mhandisi Mihayo.

    "Kwa hiyo Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) hatuwezi kuzizungumzia chochote hizi gharama za usajili kwa sababu ni sheria,sisi tunatekeleza sheria,kwa hiyo hizi gharama nafikiri ukitaka zipungue ni lazima mchakato wa kisheria ufuatwe kwa sababu lazima upitie bungeni",alieleza Mihayo.

    Awali akitoa taarifa ya vituo vya utangazaji wa maudhui Kanda ya Ziwa, Mhandisi Mihayo alisema mpaka sasa TCRA inasimamia vituo 36 vya Redio, Televisheni 3 na watoa huduma wanne wa maudhui mtandaoni waliosajiliwa kwa mujibu wa sheria ambao ni Mohab Online Tv, Geita Online Tv, Binagi Blog na Malunde Media. 

    "TCRA inaendelea na zoezi la kuwabaini watoa huduma mtandaoni ambapo mpaka sasa Kanda ya Ziwa tulishawatambua 24 na kuwatahadharisha kuacha kuvunja sheria kati yao wapo waliotii agizo la Mamlaka kwa kusitisha kwa muda upakiaji wa habari mtandaoni na wanaendelea na taratibu za usajili",alisema. 

    "Wengine wameendelea kukaidi agizo la mamlaka na kuendelea kuvunja sheria kwa kisingizio eti wanaandika habari za viongozi mbalimbali wa mikoa na wilaya,niwakumbushe viongozi hao kuwa sheria ya usajili wa watoa huduma mtandaoni za Online Tv, Blogs,Online radio,simulcasting online Tv na Radio,Weblogs ipo kwa ajili ya wote zikiwemo taasisi za serikali. 

    Hivyo basi TCRA inawashauri viongozi waache kusaidia kuvunja sheria ama kwa kujua au kwa kutojua kwa kuwatumia waandishi wanaopakia habari za matukio mbalimbali yanayowahusu kwenye mitandao ya kijamii inayotakiwa kusajiliwa,tutaendelea kuwachukua hatua za kisheria ili kila mtoa huduma mtandaoni anafanya kazi kwa kufuata sheria" 

    "TCRA inawafahamu watu wote wanaopakia maudhui mtandaoni hivyo wale wanaoendelea kutoa maudhui mtandaoni ni lazima wafuate taratibu za kisheria ikiwemo kujisajili,tunaendelea kuwafuatilia na watashughulikiwa na vyombo vya kisheria",aliongeza.

    "Kuna wale ambao wameamua kuhamishia kazi za blogs Instagram na Facebook, hawa nao tutawashughulikia",alisema Mhandisi Mihayo.

    AGA KHAN FANYENI MAPITIO YA GHARAMA ZENU-MAJALIWA

    0
    0


    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Binti Mfalme Zahra Aga Khan (wapili kushoto) wakifungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi, 9, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamaii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zaynab Chaula, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa, (Agence Francaise de Developpment)

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Binti Mfalme Zahra Aga Khan baada ya kufungua awamu ya pili ya hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019.
    Baadhi ya waalikwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpokea mtoto Claribel Mwakatumbula (1) kutoka kwa mama ya Delfina Audax wakati alipotembelea wodi ya watoto katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam kabla ya kufungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali hiyo, Machi 9, 2019. Mtoto Claribel amelazwa hospitalini hapo kwa matibabu.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amembeba mtoto, Claribel Mwakatumbula (1) wakati alipotembelea wodi ya watoto kabla ya kufungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019. Mtoto Claribel amelazwa hospitalini hapo kwa matibabu
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimfariji mtoto Ilham Ally wakati alipotembelea wodi ya watoto kabla ya kufungua awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019. Mtoto Ilham amelazwa hospitalini hapo kwa matibabu.
    Wazari Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Jackline Vicent aliyejifungua mtoto Lois Ladislaus katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Machi 9, 2019. Mheshimiwa Majaliwa alitembelea wodi ya wazazi kabla ya kufungua awamu ya pili ya upanuzi wa haospitali hiyo
    ……………………………

    SERIKALI imeutaka Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), ufanye mapitio ya gharama za afya katika hospitali ya Aga Khan ili wananchi wa kawaida waweze kumudu na kunufaika na huduma za tiba wanazozitoa.

    Imeelezwa kuwa pamoja na jitihada za Serikali za kuboresha huduma za afya, pia inatambua mchango unaotolewa na taasisi zisizo za Kiserikali ikiwemo Hospitali ya Aga Khan katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za kisasa.
    Hayo yamesemwa leo (Jumamosi, Machi 9, 2019) na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.

    Amesema upanuzi wa hospitali hiyo ni miongoni mwa jitihada za kuwafikishia Watanzania huduma za afya katika maeneo yao na kwa ngazi zote na kwa gharama nafuu, hivyo amewataka watoa huduma wote nchini waangalie upya gharama zinazotozwa katika huduma mbalimbali hususan za matibabu.

    “Mtakubaliana nami kuwa gharama zikiwa kubwa hazitawanufaisha wananchi hususan wa kipato cha chini na wananchi hawataona unafuu wa kutibiwa nchini na nje ya nchi, hivyo fanyeni mapitio ya gharama hizo.”

    Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua gharama kubwa za uwekezaji na uendeshaji wa shughuli za afya nchini hususan kwa sekta binafsi. “Lengo la Serikali kutoa misamaha ya kodi kwa baadhi ya taasisi zisizo za kiserikali kama Aga Khan ni kuwezesha huduma zinazotolewa kuwa nafuu.”

    Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema Serikali imeanzisha na kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na mwitikio wa ni mkubwa na lengo lake ni kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa ya matibabu tena kwa uhakika.

    “Nitoe wito kwa taasisi zote zisizo za Serikali kuunga mkono jitihada hizi za Serikali na kuhakikisha wananchi wote wananufaika na huduma zenu kupitia mfumo huu bila kubaguliwa.”

    Pia ameutaka uongozi wa Hospitali ya Aga Khan na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakamilishe majadiliano yao katika matumizi ya NHIF kwenye hospitali hiyo ya rufaa. “Dr. Konga Mkurugenzi Mkuu wa NHIF upo hapa kamilisheni mjadala.”

    Amesema nia ya Serikali ni kuona wananchi wanakwenda hapo kwenye jengo hilo zuri na wanapata huduma kupitia bima ya afya. “Ni matumaini yangu kwamba jambo hili litafanyiwa kazi kwa kuzingatia maslahi mapana ya pande zote mbili.”

    Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuhakikisha uwepo wa mazingira mazuri ya uwekezaji, kuimarisha amani na utulivu, ambapo ametoa rai kwa sekta binafsi ziendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo nchini kwa kuzingatia sheria za nchi, utamaduni na mila za Watanzania.Awali, Waziri Mkuu alitembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma katika jengo hilo ikiwemo maabara, chumba cha upasuaji, wodi ya watoto, wodi ya wazazi. Ujenzi wa hospitali hiyo umegharimu sh. bilioni 192, kati yake sh. bilioni 134 ni mkopo wa muda mrefu wenye masharti nafuu kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).

    Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameupongeza Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan kwa upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kwani unakwenda kuboresha huduma za afya nchini.

    Amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya kutolea huduma za afya ambapo kwa sasa imeanzisha ushirikiano na sekta ya umma na binafsi kwenye mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza.

    NayeBalozi wa Ufaransa nchini, Balozi Frederic Claiver amesema awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali hiyo utasaidia kuboresha utoaji wa huduma za afya Tanzania.

    Pia Balozi huyo amesema Ufaransa itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha inatimiza mkakati wake wa kukuza uchumi kutoka wa chini kwenda wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025.

    TCRA YABAINI MADUDU MAKUBWA VITUO VYA REDIO

    0
    0
    Mamlaka Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa miezi minne kwa Vituo vya Redio Kanda ya Ziwa kurekebisha mapungufu mbalimbali yaliyopo ikiwemo wafanyakazi kufanyishwa kazi bila mikataba ya ajira,vituo kukosa ubunifu wa kutafuta habari na matukio na kuwa watangazaji wa darasa la saba.

    Akizungumza wakati wa Mkutano wa Watoa huduma za maudhui zikiwemo Redio,Tv na Mitandao ya Kijamii uliofanyika Machi 8,2019 jijini Mwanza, Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Injinia Francis Mihayo alisema vituo vya Redi vinatakiwa kufanya marekebisho vinginevyo vituo hivyo vitaamuriwa kusitisha huduma mpaka watakapojirekebisha.

    Alisema hivi karibuni Kamati ya Maudhui ya TCRA ilifanya ukaguzi kwenye vituo vya Redio takribani 36 vilivyopo Kanda ya Ziwa na kubaini kuwa vingi vina hali mbaya ya kiundeshaji na kiutendaji.

    Aliyataja mapungufu yaliyopo kwenye vituo vya utangazaji vya Redio kuwa pamoja na wafanyakazi kutokuwa na mikataba ya ajira ambao baadhi ya vituo hakuna hata mmoja mwenye mkataba ajira lakini pia vituo vingine Watangazaji ni wa darasa la saba,Kidato cha Pili au Kidato cha Nne pamoja na kazi kutolewa kiukoo.

    "Mapungufu mengine ni vituo kukosa vyoo na kama vipo basi ni vichafu lakini cha kushangaza kwenye ratiba yao ya vipindi wana vipindi vya afya,pia baadhi ya studio hazina Sound Proof,viyoyozi hali inayopelekea watangazaji kufungua madirisha pale wanapozidiwa na joto",

    "Baadhi ya vituo vimekosa ubunifu wa kutafuta habari na matukio kunakopelekea ku kubadilisha ratiba ya vipindi bila kutoa taarifa TCRA,Mfano vipo vituo vya redio Wamiliki wake huamua kwa matakwa yao wenyewe kubadilisha vipindi kwa kuwaamrisha wakuu wa vipindi bila kufuata taratibu",alieleza.

    Alisema mapungufu mengine ni baadhi ya vituo vya redio kutokuwa na mlinzi hata mmoja,vituo kutokuwa na mazingira rafiki ya kufanyia kazi, vituo kutolipia leseni kwa mujibu wa sheria na kushindwa kutoa taarifa za kweli pale TCRA inapoomba taarifa kutoka kwa watoa huduma.

    Kutokana na mapungufu hayo,Mhandisi Mihayo alisema baada ya miezi minne iliyotolewa kujirekebisha wataamury vituo vifungwe.

    "Ni bora tuwe na vituo vichache vya redio vinavyofuata taratibu. Kuhusu mapungufu ya sifa (CV) za waajiriwa lipo kwa mujibu wa sheria ambapo serikali ilitoa muda mpaka ifikapo Desemba 2019 kila kituo lazima kiwe kina Wanahabari wenye kima cha chini cha elimu ya Diploma na si vinginevyo",aliongeza Mkuu huyo wa TCRA Kanda ya Ziwa.

    Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui TCRA, Bi Valerie Msoka alivitaka vyombo vya habari na waandishi wa habari kuzingatia maadili na sheria,kanuni za utangazaji na taratibu za nchi.

    "Wasimamizi na Wamiliki wa vituo vya utangazaji lazima mtimize wajibu wenu ipasavyo,jitahidini kusimamia vipindi na ni vyema watangazaji wawe na Mwongozo wa Vipindi 'Script'",aliongeza. Mkuu wa Mamlaka Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Injinia Francis Mihayo akizungumza katika mkutano wa Watangazaji wa maudhui kutoka vituo vya Redio,Televisheni na Mitandao ya Kijamii Kanda ya Ziwa Machi 8,2019 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza. Mkuu wa Mamlaka Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Injinia Francis Mihayo akizungumza katika mkutano wa Watangazaji wa maudhui kutoka vituo vya Redio,Televisheni na Mitandao ya Kijamii Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui TCRA, Bi Valerie Msoka akizungumza katika mkutano wa Watangazaji wa maudhui kutoka vituo vya Redio,Televisheni na Mitandao ya Kijamii Kanda ya Ziwa Machi 8,2019 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza. Wajumbe wa Kamati ya Maudhui TCRA wakiwa ukumbini. Wajumbe wakiwa ukumbini Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde akiuliza swali wakati wa mkutano huo.

    WANAWAKE MSD WATOA MSAADA WODI YA KANGAROO HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

    0
    0


    Wanawake wa Bohari ya Dawa (MSD), wakishusha vitu mbalimbali walivyotoa kwa wanawake wenzao na watoto waliozaliwa kabla ya wakati waliopo wodi ya Kangaroo Hospitali ya Taifa ya Muhili jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
    Aneth Moshi wa MSD, akimkabidhi Maria Mzee Ali msaada huo.
    Meneja Jengo la Wazazi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Stellah Rushagara, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kupokea msaada huo.
    Mwenyekiti wa Wanawake MSD, Rehema Mosha, akizungumza. Kushoto ni Selwa Hamid.
    Misaada ikitolewa.
    Mama akipokea msaada.
    Dada Selwa Hamid wa MSD, akikabidhi msaada.
    Msaada ukitolewa



    Na Dotto Mwaibale

    JAMII imetakiwa kujenga tabia ya kuwasaidia wenzao wenye changamoto mbalimbali za maisha ikiwemo magonjwa.

    Mwito huo umetolewa jana na Mwenyekiti wa Wafanyakazi Wanawake wa Bohari ya Dawa (MSD) Rehema Mosha wakati wanawake hao walipokuwa wakitoa msaada ya vitu mbalimbali kwa akina mama ambao wamelazwa na watoto wao waliozaliwa kabla ya kutimiza miezi tisa wodi ya Kangaroo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)

    "Ni vizuri jamii ikabadilika na kuwa na moyo wa kusaidia makundi yenye changamoto kama hawa wakina mama wenzetu ambao wapo katika hospitali hii kwa muda mrefu wakiwa na watoto wao" alisema Mosha.

    Alisema wao kila mwaka katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani wamejijengea utaratibu wa kuchangishana na kununua vitu mbalimbali kwa ajili ya kusaidia kundi fulani watakaloona linahitaji msaada ambapo kwa mwaka huu wakaona waende katika wodi hiyo ya Kangaroo.

    Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt. Faraja Chiwanga alitoa shukurani kwa wanawake wa MSD kwa msaada huo na kueleza kuwa ni wa muhimu ukizingatia kuwa wakina mama wengine wanatoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam hivyo hawana jamaa wa kuwasaidia.

    Alisema watoto hao waliozaliwa kabla ya wakati wanakuwa kupitia joto la kifua cha mama zao ambapo wakati wote wanatakiwa kukumbatiwa na wanakuwa bila ya wasiwasi wowote."Hawa watoto kama mnavyowaona wanatakuwa kama kawaida kupitia joto la mama zao na kesho mtasikia kuwa ndio viongozi wa baadae" alisema Dkt. Chiwanga.

    Mama ambaye alijifungua mapacha kabla ya wakati, Mariam Salum mkazi wa Kitunda, alitoa shukurani kwa MSD kwa niaba ya wenzake kwa msaada waliowapatia na kusema upendo huo wauendeleze na kwa watu wengine.

    UJUMBE WA JOSEPH KUSAGA KWENYE MAZIKO YA KIBONDE WAIBUA HISIA NZITO ,WAACHA TAFAKARI KWA WAOMBOLEZAJI

    0
    0
    *Azungumza maneno mazito, asema kifo cha Kibonde kimemuachia funzo kuwa umaarufu,fedha havina nafasi

    *Asema kama umaarufu basi Kibonde alikuwa maarufu kuliko msanii yoyote lakini bado alikuwa mnyenyekevu


    Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

    MWILI wa aliyekuwa Mtangazaji maarufu nchini marehemu Ephraim Kibonde umepumzishwa kwenye nyumba yake ya milele katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam huku ujumbe mzito uliotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group ukigusa mioyo ya waombolezaji.

    Wakati wa kuupumzisha mwili wa Kibonde mamia ya waombolezaji wakiwamo viongozi wa ngazi mbalimbali, familia,ndugu,jamaa na marafiki wameshiriki kwenye maziko hayo.Huzuni ilikuwa imetawala wakati wote wa maziko.

    Mwili wa Kibonde ulianza kushushwa kaburini saa saa 10:02 Alasiri ya leo Machi 9,2019 baada ya kutolewa neno la faraja ambapo pamoja na kuelezea majonzi ya msiba huo waombolezaji waambiwa kifo ni adui na sio mpango wa Mungu.

    SALAM ZA FAMILIA

    Baada ya mwili wake kuwekwa kaburini,Msemaji wa familia ya Kibonde kupitia Frank Chagula imetoa shukrani kwa waombolezaj wote ,viongozi wa Serikali huku ikielezewa miongoni kwa walioguswa na msiba huo ni Rais Dk.John Magufuli ambaye kutokana na majukumu aliyonayo amemwagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumuwakilisha.

    Chagula amesema wanatoa shukrani kwa kila mtu ambaye ameshiriki kwenye mazishi na maziko ya marehemu Kibonde."Kwa umati huu ambao umejitokeza nyumbani na hapa makaburini familia tunatoa shukrani kwa wote,ukweli kutaja jina la kila mtu mmoja hatutaweza ,hivyo tunatoa shukrani kwa wote."

    Baada ya familia kutoa shukrani ikafuata hatua ya kufukia kaburini. Wakati kaburini lenye mwili wa Kibonde linafukiwa kimya kilikuwa kimetawala makaburini hapo kulikuwa na umati mkubwa watu.


    ALICHOSEMA RAFIKI WA KIBONDE 

    Wakati huo huo salamu za Mtangazaji wa kipindi cha Jahazi Garda G Habashi amemueleze Kibonde enzi za uhai wake alivyoingia kwenye utangazaji na safari yake ilianza ya utangazaji mwaka 1990 baada ya kupata kazi kituo cha CTN na baadae mwaka 1999 alijiunga Clouds Media Group.

    Aliingia Clouds Media Group baada ya kuanzisha kipindi cha michezo na burudani. Uwepo wa Clouds Media Group alionesha umahiri mkubwa Garza alimuomba wawe wote kwenye kipindi cha Jahazi.

    "Kibonde alikuwa pacha wangu kabla ya kazi na baada ya kazi.Hata kwenye mambo ya familia walishirikiana.Na hata katika mambo ya starehe kwa kweli tulifanya starehe zetu vizuri,niamini mimi.

    "Kibonde leo huyo ametangulia ,sipo naye tena. Sitalia kwasababu nikilia nitamsikitisha,nikilia naye atalia na wote tutalia wakati wote," amesema Garda G Habashi na kuongeza ucheshi wa Kibonde alionesha kwa kila mtu kwani hata wakiwa wanaongoza alikuwa anamuacha nyuma kutokana na kupenda kusalimia kila tena kwa kumshika mkono.

    Hata hivyo amesema kuwa ni wiki iliyopita wamempoteza Mkurugenzi wao wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba na sasa Kibonde lakini ametoa ahadi ya kwamba wafanyakazi pamoja na kuondokewa na wapendwa wao watafanya kazi ili hata huko waliko wafarijike.

    UJUMBE MZITO WA KUSAGA 

    Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group Joseph Kusaga amesema ni pigo kubwa kwa Clouds Media Group kwani ndani ya wiki mmoja wameondokewa na watu muhimu.

    "Machozi niliyonayo moyoni yatachelewa kukauka , ni pigo kubwa sana kwetu.Hata hivyo nitoe shukrani kwa Rais Dk.John Magufuli kwani baada ya taarifa kifo cha Kibonde alinipigia simu ya kunipa pole," amesema Kusaga.

    Hata hivyo amesema kwamba kifo cha Kibonde ambaye baada ya kupata matatizo lakini baada ya kupata huduma za matibabu alipata nafuu lakini baadae akafariki.

    "Fundisho ambalo nimelipata baada ya kifo cha Kibonde ni kwamba tuache nyodo,Kibonde alikuwa maarufu kuliko wasanii wowote lakini ameondoka,kama fedha zinaokoa maisha tungeweza kumuokoa kutokana na jitihada.Tuache nyodo kwani duniani tunapita tu.

    " Umaarufu na fedha sio chochote mbele ya kifo,Kibonde nenda tunakuaga,tunajua utakutana na mzee Kusaga ambaye alikupenda sana,utakutana na Ruge ambaye mlishirikia naye kikamilifu .Nenda Kibonde ,uliniheshimu nami nilikiluheshimu sana.

    "Niombe kila mmoja wetu hapa atambue anayo fursa ya kuonesha upendo kwa kila mtu,onesha upendo kadri unavyoweza.Hapa duniani tunapita tu.Tushikane mikoni kuonesha ishara ya kusameehana na kuanza upya," amesema Kusaga.

    Hata hivyo baada ya Kusaga kutoa ujumbe mzito ambapo ulisababisha watu kushindwa kuvumilia na kuwafanya wapige makofi kumppngeza ilifuata hatua ya kuweka mashada ya maua katika kaburi la marehemu Ephraim Kibonde.
    Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akizungumza jamo wakati wa Mazishi wa Mtangazaji wa kituo hicho cha redio,Marehemu Ephraim Kibonde

    Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP Media Reginald Mengi akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group Joseph Kusaga wakati wa mazishi ya Ephraim Kibonde,leo makaburi ya Kinondoni jijini Dar
    Rafiki na Myanyakazi mwenzake Marehemu,Gadna G Habash akiwa na majonzi makubwa kufuatia msiba wa Ephraim Kibonde ,wa pili kati ni Mtoto wa Marehemu.
    Wazazi wa Marehemu wakihuzunika kuondokewa na mtoto wao mpendwa
    Sanduku lenye mwili wa maerehemu Ephraim Kibonde ukiwasili katika makaburi ya Kinondoni jioni ya leo kwa maziko
    Watoto wa Marehemu wakiweka udongo kwenye kaburi la Baba yao

    WANAWAKE MSINYAMAZIE RUSHWA YA NGONO

    0
    0
    Wanawake Mkoani Songwe wameaswa kutonyamazia vitendo vya rushwa ya ngono ili waweze kujikomboa kifikra, kiuchumi na kisiasa katika harakati za kufikia usawa wa kijinsia kwa ajili ya maendeleo endelevu.

    Akisoma hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika Kimkoa Wilayani Ileje, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi John Palingo amesema rushwa ya ngono inapaswa ithibitiwe kwa nguvu zote

    “Nawasihi sana wanawake wanaokumbana na udhalilishaji huu wa kuombwa rushwa ya ngono watoe taarifa katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) pia wananchi wengine watoe taarifa mara tu wanapokutana na matatizo ya rushwa ili taasisi husika ziweze kushughulikia”, amesema Palingo

    Ameongeza kwa kuziagiza halmashauri za Mkoa wa Songwe kuhakikisha zinaendelea kupiga vita unayanyasi na ukatili wa kijinsia, taasisi zote zinazohusika na mapambano hayo ikiwa ni pamoja na dawati la jinsia kuwachukulia hatua wote wanaofanya vitendo hivyo.

    Palingo ameelekeza kuwa halmashauri ziweke mazingira mazuri ya masoko ya bidhaa na mazao yanayozalishwa na wanawake, kutenga fedha kwaajili ya kuwawezesha wanawake kuwa na uwezo wa kumiliki viwanda na kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake.

    Akisoma risala kwa niaba ya wanawake Afisa Maendeleo ya Jamii Roida Kyomo amesema wanawake wamekuwa wakizalisha kidogo kutokana na ukosefu wa masoko, elimu na mitaji wakti uwezo wa kuzalisha bidhaa na mazao mengi wanayo.

    Kyomo ameongeza kuwa uwepo wa mashauri 442 ya unyanyasaji wa kijinsia unaonyesha kuwa tatizo hilo bado lipo hivyo ameiomba serikali kuendelea kuhamasisha jamii kuachana na mila kandamizi kwa wanawake ili muda unaotumika katika kusuluhisha matatizo hayo utumike katika kuzalisha mali ili kukuza uchumi.
     Mkuu wa Wilaya ya Mbozi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani akionyesha Bidhaa zinazozalishwa na Kikundi cha wanawake wilayani Ileje
     Maafisa kutoka katika Dawati la Jinsia Wilayani Ileje wakiandamana katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mapema leo
    Viewing all 109570 articles
    Browse latest View live




    Latest Images