Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109934 articles
Browse latest View live

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YATOA MAFUNZO ARUSHA

$
0
0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. George Simbachawene akifungua mafunzo kwa Kamati hiyo kuhusu mbinu na utaratibu wa kufuatilia utekelezaji wa mipango na programu mbalimbali za Serikali. Mafunzo hayo yaliyofanyika Jijini Arusha yamedhaminiwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) chini ya Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo (LSP II).
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, wakifuatilia mada katika mafunzo kuhusu mbinu  na utaratibu wa kufuatilia utekelezaji wa mipango na programu mbalimbali za Serikali. Mafunzo hayo yaliyofanyika Jijini Arusha yamedhaminiwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) chini ya Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo (LSP II).

Airtel Divas washerehekea siku yao kwakushukuru wanaume wote

$
0
0
Airtel DIVAS Ikiwa ni siku ya wanawake inayoadhimishwa ulimwenguni kote wanawake wote wanaofanya kazi katika vitengo mbalimbali ndani ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel (Airtel Divas)  leo wamesherehekea kwa style ya kipekee ambapo wamewashukuru wanaume wote wanaofanya nao kazi kila siku kwa kuwapatia zawadi.

Akiongoza wanawake wenzie wote (Airtel Divas) katika maadhimisho hayo Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu Stella Kibacha alisema “leo ni siku yetu Wanawake, ambapo inaadhimishwa dunia nzima kila tarehe 3 Machi. Lakini style yetu sisi Divas  wa Airtel tumeamua kuwashuru kwa zawadi  mwanaume wote hapa Airtel, ni ukweli kuwa tunashinda nao kila siku wanatuonyesha ushirikiano wa kutosha, hawana ubaguzi tunafanya kazi kwa usawa na kusikilizana, kwa kweli tunawashukuru sana”

Kibacha alieleza kuwa “Mwaka huu kauli mbiu ya siku ya wanawake ni ‘#BalanceforBetter’ ikipambanua mambo mengi kati yao ni kujipanga na kupangilia kila jambo ili kuwa na mafanikio”

“Airte Divas Tumejipanga kisawasawa kuhakikisha kila jambo kazini au nyumbani yanakaa sawa kwa manufaa yetu na taifa kwa ujumla” alializa kwa kusema Kibacha
 Airtel Divas Mkurugenzi wa Airtel Rasilimali watu Stella Kibacha akimshukuru mmoja kati ya wafanyakazi wa airtel wakiume bw Dunia Yusufu leo walipoadhimisha siku ya wanawake Duniani yenye kauli mbiu ‘Balance for better’. Siku ya wanawake huadhimishwa kila mwaka tarehe 08 machi ikiwa na lengo la kutambua mchango wa wanawake katika jamii.
 Airtel Divas Meneja uhusiano Airtel Dangio Kaniki akitoa zawadi kwa Edward Mtingwa kwa lengo la kuwashukuru wanaume wote wanaofanya kazi nao. ‘Airtel Divas’ leo wameadhimisha siku ya wanawake Duniani yenye kauli mbiu ‘Balance for better’ kwa kutoa shukrani kw wanaume wote. Siku ya wanawake huadhimishwa kila mwaka tarehe 08 Machi ikiwa na lengo la kutambua mchango wa wanawake katika jamii
 Airtel Divas Mkurugenzi wa Airtel Huduma kwa wateja Adriana Lyamba akitoa zawadi kwa Ezekieli Mwakangata ikiwa ni ishara ya kushukuru wanaume wote wanaofanya kazi na wafanyakazi wa Airtel ‘Airtel Divas’ leo walipoadhimisha siku ya wanawake Duniani yenye kauli mbiu ‘Balance for better’ kwa kutoa shukrani kwa wanaume wote. Siku ya wanawake huadhimishwa kila mwaka tarehe 08 Machi ikiwa na lengo la kutambua mchango wa wanawake katika jamii. 
Airtel Divas wakiwa kwenye picha ya pamoja leo wakati wa  maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyobeba kauli mbiu ‘Balance for better’ Siku ya wanawake huadhimishwa kila mwaka tarehe 08 Machi kwa lengo la kutambua mchango wa wanawake katika jamii


AKUTWA AMEFARIKI DUNIA KWENYE KORONGO LA MAJI

$
0
0
Anaandika Dixon Busagaga.Hai.

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Diamon Munishi (87) amekutwa amefariki dunia katika Korongo la maji Makando lililopo katika kijiji cha Isawerwa kata ya Romu wilayani Hai.

Kwa mujibu wa mashuhuda wameeleza kuwa marehemu alikua na tatizo la uoni hafifu na kwamba alianguka kwenye korongo wakati mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali ikinyesha.

Mkuu wa Polisi wilaya ya Hai Lwelwe Luhaga Mpina alithibitisha kufariki dunia na kwamba kifo chake ni cha kawaida kutokana na  matatizo aliyokuwa nayo marehemu.

Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya alifika eneo la tukio na kutoa pole kwa familia iliyofikwa na msiba wa mzee wa huyo.
 Mwili wa Daimon Munishi ukitolewa kwenye Korongo la maji Makando lililopo katika kijiji cha Isawerwa kata ya Romu wilayani Hai.
 Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya (mwenye kofia) alitizama mwili uliokutwa katika Korongo la maji Makando lililopo katika kijiji cha Isawerwa kata ya Romu wilayani Hai.
 Mwili wa Daimon Munishi ukipandishwa kwenye gari la polisi mara baada ya kutolewa kwenye Korongo la maji Makando lililopo katika kijiji cha Isawerwa kata ya Romu wilayani Hai.
 
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya ( mwenye kofia) akitoa pole kwa wananchi waliofika eneo la tukio wakati wa kutoa mwili wa marehemu kwenye Korongo la maji Makando lililopo katika kijiji cha Isawerwa kata ya Romu wilayani Hai.
 Katibu tawala wilaya ya Hai,Upendo Wera akitoa pole kwa wananchi wa eneo hilo

RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU MBILI JIJINI DAR ES SALAAM NA KUREJEA NCHINI RWANDA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Teminal 1 wakati akijiandaa kurejea nchini Rwanda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame  wakipita kwenye Gadi ya heshma iliyoandaliwa na  Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Terminal 1 jijini Dar es Salaam.



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati akimsindikiza kwenda kupanda ndege katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na vikundi mbalimbali vya ushehereshaji katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kumsindikiza mgeni  wake Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na vikundi mbalimbali vya ushehereshaji  kwa kuwapungia mkono mara baada ya kumsindikiza mgeni  wake Rais wa Rwanda Paul Kagame. PICHA NA IKULU 

KIFO CHA KIBONDE NI PENGO KUBWA KWA TAIFA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema kifo cha aliyekuwa Mtangazaji Muandamizi wa kituo cha redio cha Clouds, Ephraim Kibonde ni pengo kubwa kwa Taifa, Clouds Media Group na tasnia ya habari kwa ujumla.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 8, 2019) alipokwenda kuhani msiba wa Mtangazaji Muandamizi kituo cha redio Clouds, Kibonde kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mbezi Beach Dar es Salaam.Kibonde alifariki dunia jana alfajiri Machi 7, 2019 jijini Mwanza.

“Msiba huu umetushtua sana na ni tukio ambalo hatukulitarajia ila ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Hivi karibuni sote tulimshuhudia akiongoza ratiba ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na alienda hadi Kagera kumzika.”

Waziri Mkuu amesema marehemuKibonde enzi za uhai wake ameshirikiana vizuri na Serikali katika shughuli mbalimbali, hivyo amewaomba wananchi waendelee kushikamana na kuifariji familia. “Tumuombee marehemu apumzike kwa amani.

Kadhalika, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wazazi, watoto wa marehemu pamoja na wananchi kwa ujumla waendelee kuwa na subira na watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mtangazaji wa Clouds FM, Efraim Kibonde wakati alipokwenda nyumbani kwao marehemu, Mbezi Beach jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia, Machi 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Samson Job Kibonde ambaye ni baba mzazi wa Mtangazaji wa Clouds FM, Ephrim Kibonde wakati alipokwenda nyumbani kwao marehemu, Mbezi Beach jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia, Machi 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimfariji Hilda Samson Kibonde ambaye ni mama mzazi wa Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde wakati alipokwenda nyumbani kwao  marehemu, Mbezi Beach jijini Dar es salaam, kutoa pole kwa familia, Machi 8, 2019. Katikati ni baba mzazi wa marehemu, Samson  Job Kibonde. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Samson Job Kibonde ambaye ni baba mzazi wa Mtangazaji wa Cloud FM, Ephrim Kibonde wakati alipokwenda nyumbani kwao marehemu, Mbezi Beach jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia, Machi 8, 2019. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Clouds Media, Joseph Kusaga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WASANII WA KIKE WA KIAFRIKA WAIMBAJI WA MUZIKI WA HIP HOP WAUNGANA KUSHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE

$
0
0


Wakati dunia ikijiandaa kutoa heshima kwa wanawake duniani kote katika Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, chapa ya bia ya kibunifu zaidi Africa, Castle Lite, imeanza safari ya kusherehekea wanawake katika bara zima kwa kuwezesha ushirikiano mkubwa uliopata kutokea wa wasanii wa kike katika muziki wa Hip-Hop kwenye ardhi mama. Lengo lilikuwa ni kuonyesha nguvu pale wanawake wanaposimama pamoja na kuimarisha umoja kwa kupitia muziki, hivyo chapa yetu ilishirikiana na kikundi cha wasanii wakubwa watano (5) wa muziki wa kufoka na kutengeneza tena nyimbo ya msanii malkia wa Hip Hop Queen Latifah iliyokuwa maarufu katika miaka ya 90 ya, U.N.I.T.Y.

 Afrika ya Kusini, Tanzania na Nigeria kwa pamoja waliungana kutengeneza wimbo huu, huku wasanii kama Moozlie (South Africa), Gigi Lamayne (Afrika ya Kusini), Rouge (Afrika ya Kusini), Rossa Ree (Tanzania) na Mz Kizz (Nigeria) wakiwa nyuma ya kipaza sauti. U.N.I.T.Y kutoka Castle Lite ni zaidi tu ya “wimbo mwingine unaoshirikisha wasanii wa kike wa Hip-Hop”, ni wimbo wa kusherekea na wito, sio tu kwa wanawake wote barani kote bali katika kila sehemu ya dunia, kuweka uhai katika nguvu ya wanawake katika muungano.

Wasanii watano kwa wakati mmoja waliimba U.N.I.T.Y mubashara asubuhi ya leo katika Instagram; Jambo la kwanza kabisa kufanyika kwa Castle Lite na kwa bara zima la Afrika kwa ujumla. Akizungumza baada ya onyesho (livestream), Mkurugenzi wa chapa ya Castle Lite Silke Bucker alisema: “Msingi wetu kama Castle Lite kila siku umekuwa ni kuvuka mipaka kwa kutumia ubunifu, na ili kuweka kumbukumbu katika siku hii ya kipekee, hakukuwa na njia nzuri zaidi kwetu kuunganisha wanawake zaidi bali kwa kutumia jambo ambalo kiukweli tunalolipenda – muziki.”

“Mshikamano wa kimuziki katika bara zima ulifanya jambo hili la wasanii kuja pamoja kufanya wimbo pamoja na chapa yetu kuwa la asili, na Castle Lite imebahatika imeamua kuwaweka wanawake katika hip-hop mbele. Leo sote tunasherekea nguvu ya wanawake katika UMOJA na

tunazidi kung’ara zaidi na kwa fahari kubwa tukisherekea na wanawake wote duniani kote katika siku hii ya kipekee na ya kimataifa,” Bucker alimalizia kusema. “Ni hesima kubwa sana kuwa sehemu ya harakati ambazo sio tu kwamba zinasherekea na wanawake, lakini zinachochea

UMOJA kwa kupitia muziki. Muziki una uwezo wa kuunganisha watu kutoka katika mazingira tofauti, na ni kwa kupitia suala hili tuliweza kufanya jambo la tofauti kwa namna yetu ya kipekee ili kutengeneza wimbo huu mzuri ukiwa na ujumbe wenye nguvu.” Moozlie Aliongeza Mwaka jana, chapa hii yenye bia ya baridi ilivunja mipaka ya kimuziki ilipokuwa mwenyeji wa onyesho la kwanza na la kipekee la wasanii wa kike wa Hip Hop lililoitwa Hip Hop Herstory, ambalo lilijikita katika kuonyesha nafasi ya wanawake katika mabadiliko ya Hip Hop.

Onyesho la Hip Hop Herstory kutoka Castle Lite lilifanikiwa na baada ya kujifunza kutokana na hilo ilimaanisha kwamba ushirikiano wa U.N.I.T.Y sio tu kwamba ulikuwa na mantiki lakini pia ni hatua kwenda mbele katika kuonyesha na kutoa heshima kwa vipaji na michango ya wasanii wetu wenyewe kutoka Afrika.

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MWANAMWEMA SHEIN MGENI RASMIN SIKU YA WANAWAKE GOMBANI PEMBA LEO

$
0
0
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania.(UWT) Bi.Gaudensia Kabaka, alipowasili katika uwanja wa gombani Kisiwani Pemba, kuhudhuria Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kitaifa zimefanyika Kisiwani Pemba katika Uwanja wa Gombani, leo 8-3-2019.(Picha na Ikulu)
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akihutubia wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani zilizofanyika Kitaifa Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba leo,8-3-2019.(Picha na Ikulu)
WANAWAKE kutoka sehemu mbalimbali Kisiwani Pemba wakifuatilia hutuba ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akihutuba wakati wa hafla hiyo ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani zilizofanyika katika Uwanja wa Gombani Pemba leo,8-3-2019.(Picha na Ikulu) 
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akitembelea Maonesho ya Wajasiriamali Wanawake Kisiwani Pemba yaliofanyika katika viwanja vya Gombani chakechake, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi.(Picha na Ikulu)
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiangalia Bidhaa za Wajasiriamali Wanawake wa Kisiwani Pemba wakati akitembelea maonesho hayo ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani zilizofanyika Kisiwani Pemba Uwanja wa Gombani, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Mama.Asha Suleiman Iddi.(Picha na Ikulu)
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwasalimia Vijana wa Madrasa kutoka Chakechake wakipiga dufu, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani zilizofanyika Kisiwani Pemba katika Uwanja wa Gombani.(Picha na Ikulu)

KIKWETE ARISHWA NA UTENDAJI WA BODI YA SHULE

$
0
0
Na Karim Juma - Mboga -chalinze
RAIS Mstafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekagua maendeleo ya shule ya sekeondari  Mboga na kujiridhisha kwa utendaji wa bodi ya shule hiyo na  bodi ya shule hiyo  kuhitajika kuachia madaraka kufuatia na waraka uliotolewa na Wizara ya elimu  kwa shule za sekondari .
Dkt. Kikwete amesema kwamba  uchagauzi wa bodi mpya  ufuate maelekezo kama yaliyotolewa kwenye waraka huo na sio kumchagua mtu kwa umarufu alionao, Hata hivyo  kikwete aliomba wanafunzi na walimu  watunze shule kwa kuwa ni ya kisasa sana na bado itaendelea kuwekezwa kwa kupata elimu ya kidato cha tano na cha sita.
 Amesema kuwa kwa wakati huu wakiendelea na utengenezaji wa majiko ya kupikia na wamepanga kujenga bwalo  la  chakula kwa wanafunzi pamoja na sehemu ya kuhifadhia chakula.

   Pia Mbunge wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete amesema ameridhishwa na  uwajibikaji, utendaji kazi kwa kuonesha kauli mbiu ya hapa kazi inatekelezwa hasa kwa  bodi ya shule kujinyima posho ili shule iweze kuwa salama na kuweza kukamilika pamoja  na kupata watendaji wa kufundisha vijana kwa ufasaha.
              Ridhiwani amesema ni wakati sasa kwa Halmashauri ya Chalinze kutumia pesa za ndani kuweza kuwapa posho walimu wa kujitolea kwa kuwa kuna uhaba wa walimu wasayansi na kwa hali ya sasa ya dunia inanyoendeleha lazima kupate wataalamu wa mambo ya teknolojia.

TBF YASIKITIKA KUMPOTEZA MWANAKIKAPU MAHIRI EPHRAHIM KIBONDE

$
0
0
Shirikisho la mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) linatoa salamu nyingi za pole kwa Wazazi, Watoto, ndugu, jamaa na wana familia wote wa Marehemu Ephraim Kibonde, salamu za pole kwa Clouds Media Group, Wanahabari na wanamichezo wote nchini kutokana na msiba mkubwa wa Mwanakikapu mwenzetu Ephraim  ambaye alikuwa ni Mtangazaji nguli wa habari na michezo nchini na muongozaji mahiri wa shughuli (MC). 

Marehemu Ephraim alianza kucheza kikapu akiwa mdogo, alikuwa mchezaji nyota wa kikapu katika Shule ya sekondari Mzizima na alipomaliza shule alijiunga na kituo cha vijana cha  Don Bosco ambapo alicheza katika timu ya Don Bosco Youth Centre Upanga na mnamo mwaka 1992 alikuwa katika timu iliyoshiriki daraja la pili na baadae mwaka huo alifanikisha timu hii kupanda daraja la kwanza.

Katika michezo aliyocheza marehemu mchezo muhimu ambao unakumbukwa sana timu yake ilicheza dhidi ya  timu ya Risasi ya Shinyanga ambapo Marehemu Ephraim alitoa pasi ya mwisho (assist) kwa mchezaji Dk. Peter Maro ambaye alirusha na kufunga point 3 na kuipandisha timu yao daraja.

Kwa sehemu kubwa safari ya mafanikio ya maisha ya marehemu Ephraim yalianza kwenye kikapu ambapo itakumbukwa kuwa Ephraim alishiriki katika kamati mbalimbali za maandalizi ya matamasha ya Don Bosco Youth festivals. Sehemu kubwa aliyoshiriki katika hizo kamati ni katika kitengo cha habari kama Muongoza shughuli (MC). 

Na hata safari yake yake ya utangazaji ilianzia katika mchezo wa kikapu, wakati ule akiwa pale Don Bosco alikuwa anafanya kazi ya kuwa MC na kwenye moja ya sherehe ya kufunga mashindano pale Don Bosco, mmoja wa wageni alikua ni Mkurugenzi wa kampuni ya Televisheni ya CTN ambapo alivutiwa sana na utangazaji wa Ephraim na ndipo aliongea na Fr. Peter Paul kumtaka Ephrahim kwenda ofisini kwake.

Hapo ndio ikawa mwanzo wa maisha ya utangazaji kwa Ephraim na yalitokana na mafanikio ya kituo cha Vijana cha Don Bosco Upanga kupitia matamasha na mchezo wa kikapu. 

Marehemu Ephrahim katika maisha yake licha ya kuwa mchezaji wa Kikapu wa timu za Sekondari Mzizima na baadae Kituo cha Don Bosco Upanga pia alishawahi kuwa mmoja wa Wakurugenzi katika chama cha Mpira wa Kikapu mkoa wa Dar es Salaam (BD) chini ya Rais wa wakati huo wa BD Simon Msofe na Mkurugenzi Mtendaji marehemu Mbamba Uswege. 

Marehemu Ephraim hadi anafariki alikuwa bado ni mchazaji wa kikapu kwa timu ya wachezaji wa zamani ambao walikuwa wakifanya mazoezi walau mara moja kwa juma, pia Marehemu Ephraim atakumbukwa mwaka jana mwishoni  alicheza mchezo wa Kikapu wa Tigo Fiesta Basketball Bonanza kati ya Wafanyakazi wa Clouds Media Group na Wasanii na alionyesha umahiri mkubwa katika mchezo huo uliofanyika katika viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam. 

Marehemu Ephraim anakumbukwa kwa uchambuzi mahiri wa mchezo wa kikapu nchini hasa ligi za RBA, NBL, Taifa Cup, NBA na utangazaji wa michezo mingine mbalimbali kama soka, masumbwi, riadha n.k. 

Kama shirikisho mpira wa Kikapu Tanzania tutaendelea kumuenzi Marehemu Ephraim Kibonde kwa kuhakikisha kuwa tunaundeleza mchezo huu wa kikapu nchini kote ili uweze kufungua fursa kwa Watanzania wengi zaidi kama ambavyo yeye Marehemu aliipata kupitia Kikapu. 

Tunaomba wadau wa maendeleo tushirikiane ili kuendeleza mchezo wa kikapu nchini Tanzania ili tufungue fursa zaidi kupitia mchezo wa kikapu ili kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Watanzania wengi hususani vijana nchini kote. 

Tunaomba wote tuendelee kuwaombea Wazazi wa marehemu na zaidi watoto wa Marehemu ili Mungu awe mfariji wao kipindi hichi kigumu cha kumpoteza Mpendwa wao Ephraim. 

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe, tunaomba Mungu amlaze mahala pema peponi Marehemu Ephraim Kibonde, Amina. 

Phares Magesa 
Rais, 
Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF) 

TSC yashiriki Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani

$
0
0
 Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) wakiwa katika hali ya furaha wakati wa Maandamano ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Machi 8, 2019 jijini Dodoma.
 Wafanyakazi wa TSC wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani jijini Dodoma.
 Watumishi kutoka Taasisi mbalimbali wakiwemo wa Tume ya Utumishi wa Walimu wakiwa katika Maandamano ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika  jijini Dodoma.

Wafanyakazi wa TSC wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma.

RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN, AZUNGUMZA NA MWENYEKITI WA KAMPUNI YA TOUCHROAD GROUP YA CHINA

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mwenyekiti wa Kampuni ya Touchroad Group ya China. Bwa.He.Liehui, aliupofika Ikulu Zanzibar, leo 8-3-2019, kwa ajili ya mazungumzo.kushoto Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Thomas Mihayo.(Picha na Ikulu) 
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwenyekiti wa Kampuni ya Touchroad Group ya China, kushoto  Bwa, He.Liehui, akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Thomas Mihayo.wakiwa katika mazungumzo hayo Ikulu Zanzibar,leo 8-3-2019.(Picha na Ikulu)

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Thomas Mihayo, akimtambulisha Mwenyekiti wa Kampuni ya Touchroad Group ya China, Bwa, He. Liehui, walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo,8-3-2019,(Picha na Ikulu) 


/RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Thomas Mihayo, wakitoka  katika ukumbi Ikulu baada ya kumaliza mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Touchroad Group ya China Bwa, He.Liehui,leo 8-3-2019.(Picha na Ikulu)

WAHAMIAJI HARAMU 12 WAKAMATWA NA WATU WENGINE 14 WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI PWANI KWA MAKOSA YA UHALIFU MBALIMBALI

$
0
0
 Na Mwamvua Mwinyi, Pwani 
WAHAMIAJI haramu 12 raia  kutoka Ethiopia , wamekamatwa mkoani Pwani, eneo la Mwidu porini, Chalinze kwa kosa la kutokuwa na kibali kinyume na sheria.  Aidha watu 14 wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa makosa mbalimbali ya kiuhalifu ikiwemo wizi wa pikipiki na kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bangi. 

Akielezea juu ya matukio hayo, kamanda wa polisi mkoa wa Pwani,ACP Wankyo Nyigesa, alisema usiku wa kuamkia march 8 ,askari polisi walipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu uwepo wa wahamiaji hao waliojificha kichakani eneo la Mwidu barabara ya Dar es salaam -Morogoro. 

Alieleza baada ya polisi kufika eneo hilo waliwakamata wakiwa safarini kutoka Ethiopia kuelekea Afrika ya Kusini.  :"Baada ya mahojiano ilionekana watu hao walifichwa hapo na mtu ama watu ambao bado hawajafahamika kwa lengo la kuwatafutia usafiri wa kuelekea nchini Afrika Kusini kutafuta ajira. "

Hata hivyo Wankyo alibainisha, afya ya wahamiaji haramu hao walikuwa wamedhoofika.  Wakati huo huo jeshi hilo linawashikilia watu nane kwa kufanya uhalifu mbalimbali ikiwemo wizi wa pikipiki. Pia watu sita wamekamatwa kwa kupatikana na dawa za kulevya ikiwemo bangi kete 172.

Wankyo alielezea kwamba, baada ya mahojiano na upelelezi kukamilika watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria. 

KOCHA EMMANUEL AMUNIKE ATAJA KIKOSI CHA TAIFA STARS KITACHOFUANA NA UGANDA CRANES JUMAPILI

$
0
0
Kocha Mkuu wa Taifa Stars Emmanuel
Amunike akiwa na Rais wa TFF Wallace Karia
Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti inakabiliwa na mchezo muhimu dhidi ya Uganda wa kufuzu kucheza Fainali za Afrika mwaka huu. Huu ni mchezo ambao kama Taifa Stars itashinda inaweza kukata tiketi ya kucheza AFCON mwaka huu itakayofanyika nchini Misri. 
 Mchezo dhidi ya Uganda utachezwa Jumapili Machi 24,2019 saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Taifa na leo  Kocha Mkuu wa Taifa Stars Emmanuel Amunike ametangaza kikosi kitakachopambana kuisaka tiketi hiyo kwenye Uwanja wa nyumbani. 
 Nahodha Mbwana Samatta anayecheza KRC Genk ya Belgium ataongoza kikosi katika mchezo huo uliobeba imani ya Watanzania.

Kocha Amunike amesema Kikosi alichokitaja kimezingatia mambo mengi kuhakikisha Taifa Stars inapata ushindi. Amewataka Watanzania kuiunga mkono Taifa Stars katika kuipeperusha bendera ya Tanzania. 

 Kwa upande wake, Afisa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), George Mango amesema kampuni hiyo imekuwa ikihakikisha kikosi hicho kinafanya maandalizi mazuri ili kufanya vema kwenye mchezo ujao na hatimaye iweze kuibuka na ushindi na kukata tiketi kucheza Afcon. 

 “Siku zote kinywaji cha Serengeti Premium Lager ni shabiki mkuu wa Taifa Stars na mdhamini mkuu pia. Katika mchezo huu tumejidhatiti kuhakikisha timu yetu inaibuka na ushindi ambao utakuwa fahari kwa Taifa letu na kwa kinywaji chetu cha Serengeti,” alisema Mango. 

 Mango aliwataka mashabiki wa soka nchini kufika kwa wingi siku ya mchezo huo ili kuwapa hamasa wachezaji kwaajili ya kuipa ushindi timu hiyo ya Taifa.

Kikosi cha Taifa Stars kilichoitwa:
1.Aishi Manula -Simba 
2.Feisal Salum -Young Africans 
3.Hassan Kessy-Nkana,Zambia 
4.Yahya Zayd-Ismaily,Misri 
5.Gadiel Michael-Young Africans 
6.Himid Mao-Petrojet,Misri 
7.Mudathir Yahya-Azam FC 
8.Shaaban Chilunda-Tenerife,Hispania 
9.Kelvin Yondan-Young Africans 
10.Shiza Ramadhan-ENPPI,Misri 
11.Simon Msuva-El Jadida,Morocco 
12.Rashid Mandawa-BDF,Botswana 
13.Jonas Mkude-Simba 
14.Mbwana Samatta-KRC Genk,Belgium 
15.Thomas Ulimwengu-JS Saoura,Algeria 
16.Mechata Mnata-Mbao FC 
17.Aron Kalambo-Tz Prisons 
18.Suleiman Salula-Malindi FC,Zanzibar 
19.Vicent Phillipo-Mbao 
20.Ally Mtoni-Lipuli 
21.Andrew Vicent-Young Africans 
22.Kennedy Wilson-Singida United 
23.Aggrey Morris-Azam FC 
24.John Bocco-Simba 
25.Farid Mussa-Tenerife,Hispania 

MZUNGUKO WA PILI LIGI KUU YA WANAWAKE KUANZA JUMAMOSI MACHI 9,2019

$
0
0
Mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Wanawake Tanzana Bara maarufu kama Serengeti Lite Women’s Premier League unatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya Jumamosi, Machi 9 2019.

Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake, Amina Karuma amesema wanatarajia kuona mzunguko wa pili unakuwa na ushindani kwa timu zote na hatimaye kupata bingwa anayestahili.

Karuma aliipongeza udhamini uliofanywa na Kinywaji cha Serengeti Premium Lite ambao pamoja na mambo mengine umewezesha kuifanya ligi kuwa na ushindani mkubwa na kuleta mvuto wa aina yake.

“Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Premier League imeweza kuleta ushindani mkubwa baina ya timu zinazoshiriki na hata ukitazama matokeo unaweza kuona ni jinsi gani ambavyo ligi hii imekuwa na msisimko wa aina yake,” alisema   

Aliongeza kuwa katika kuhakikisha mzunguko wa pili unakuwa bora Zaidi, imefanyika semina ya viongozi wa klabu na Waamuzi Wanawake ili kuwajengea uwezo zaidi.

Kwa upande wake, Ofisa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) ambao ni wadhamini wakuu wa Ligi hiyo, George Mango alisema kudhamini ligi hiyo kupitia kinywaji chake cha Serengeti Lite kumelenga kuongeza hamasa na kuleta ushindani wa ligi hiyo ya wanawake.

“Katika mzunguko wa kwanza tumeshuhudia hamasa na ushindani mkubwa miongoni mwa timu zinazoshiriki ligi hii hivyo ni matarajio yetu kwamba mzunguko huu wa pili utakuwa bora zaidi kwa timu zote ili kuongeza zaidi ari ya ushindani,” alisema.

Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kupitia kinywaji cha Serengeti Lite imeweza kuwekeza jumla ya Sh450 Milioni kama ufadhili wa ligi hiyo ya wanawake nchini kwa kipindi cha miaka mitatu kama sehemu ya kuendeleza michezo hususan mpira wa miguu nchini.

Aidha, SBL imekuwa ikitilia mkazzo uendelezaji wa michezo nchini hasa katika mpira wa miguu ambao mbali na kupendwa na watu wengi umekuwa chachu katika kuinua vipaji mbalimbali nchini.

TIMU ZA LIGI KUU YA WANAWAKE (SWPL) 

1. KIGOMA SISTERZ- KIGOMA 
2. SIMBA QUEENS – DSM
3. ALLIANCE GIRLS –MWANZA
4. BAOBAB QUEENS – DODOMA
5. MLANDIZI QUEENS – PWANI
6. JKT QUEENS – DSM
7. PANAMA – IRINGA 
8. EVERGREEN –DSM
9. MARSH ACADEMY – MWANZA
10. MAPINDUZI QUEENS – NJOMBE 
11. YANGA PRINCESS –DSM
12. TANZANITE – ARUSHA.

BOOMPLAY INASHEHEREKEA WANAMUZIKI WA KIKE KATIKA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0
Boomplay ni app nambari moja kwa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki barani Afrika, inasherehekea Siku Ya Wanawake Duniani 2019 ikiwa na kampeni mpya ya “Boom Queens”.
Vanessa Mdee, Rihanna, Tiwa Savage, Fena Gitu na wengine wengi, ni miongoni mwa  wanawake wenye vipaji ambao wameendelea kubadilisha tasnia ya muziki duniani. App ya Boomplay itakuwa na muonekano wa tofauti hasa katika Siku Ya Wanawake duniani tarehe 8 Machi, lengo likiwa ni kuonesha na kukuza kazi za wanawake katika muziki. App itapambwa na nyimbo, albamu pamoja na playlist za wanawake katika vipengele vyote kwenye ukurasa wa kwanza.
Boomplay pia itakuwa na kampeni kabambe ambayo itatoa fursa ya kukuza mauzo ya kazi za wanawake ambao nyimbo zao zitakuwepo kwenye playlist ya BOOM QUEENS. Playlist hiyo itakuwa na nyimbo za wasanii bora wa kike tu.
Katika kampeni hii, Meneja Mahusiano wa kampuni ya Boomplay, Bi Tosin Sorinola amesema, “majadiliano juu ya usawa wa kijinsia ni moja ya mambo ambayo ni muhimu kwetu kama jukwaa lenye nia kubwa ya kukuza wanawake katika muziki, katika njia njema kadri iwezekanavyo. Kampeni hii sio kwa mara moja tu, ni endelevu, na hili litadhihirishwa katika shughuli zetu za kila siku”.
Katika mwezi huu wa kuadhimisha Siku Ya Wanawake Duniani, watumiaji wa Boomplay kupitia simu zao za Android na iOS watapata fursa ya kujishindia simu mpya ya iPhone XS na zawadi nyingine kem kem nchini Tanzania, Kenya, Nigeria na Ghana. Ili kuonesha upendo kwa wasanii wa kike katika tasnia ya muziki, basi jishindie zawadi hizi kwa ku-subscribe kwenye app ya Boomplay kwenye vifurushi vinavyopatikana (vya siku, wiki na mwezi) na pia sikiliza playlist ya Boom Queens.
App ya Boomplay ambayo ina watumiaji zaidi ya milioni 42 dunia kote, hivi karibuni ilizindua app hiyo kwenye jukwaa la iOS. Hakika Boomplay inajivunia kuwa na nyimbo na video zaidi ya milioni 5 kutoka kwa wasanii wa Tanzania na wakimataifa.


IKULU YA MAREKANI YAMTUNUKU MKURUGENZI LHRC TUZO YA MWANAMKE JASIRI DUNIANI 2019

$
0
0
MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nchini Anna Henga ametunukiwa Tuzo ya Mwanamke jasiri duniani kwa 2019 kutokana na utetezi wa haki za binadamu. Tuzo hizo zilizotolewa na Ikulu ya Marekani zilitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo na kuhudhuriwa na Mke wa Rais wa Marekani Melania Trump.

Katika hafla hiyo Pompea alihimiza umuhimu wa kutambua mchango wa wanawake wanaoonesha juhudi zao popote duniani katika kupambana na changamoto zinazozaa matunda. Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu ya Marekani kupitia tovuti yake tuzo hizo hutolewa kwa ajili ya kutambua mchango wa wanawake  10  jasiri na wenye uthubutu katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao.

 Henga ni moja ya wanawake ambaye juhudi zake katika utetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania ni za  mfano. Wanawake wengine tisa waliotunukiwa tuzo hiyo wanatoka katika mataifa ya Bangladesh, Burma, Djibouti, Egypt, Jordan, Ireland, Montenegro, Peru na Sri Lanka.

Tuzo hizo zilianzishwa mwaka 2007 ni kutambua mchango wa wanawake wanaojitoa kwa nguvu na ujasiri kama viongozi katika kuleta mabadiliko chanya kwa jamii. Mpaka sasa kupitia tuzo za IWOC, Ikulu ya Marekani imetambua mchango kwa wanawake zaidi ya 120 kutoka nchi zaidi ya 65 katika kutetea haki za binadamu, kudumisha nafasi ya wanawake katika jamii na kudumisha amani na utawala bora katika nchi zao.
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga akionyesha tuzo yake baada ya kupokea tuzo hiyo ya Kimataifa ya Mwanamke Jasiri kwa mwaka 2019 katika hafla iliyoongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo na Mke wa Rais wa Marekani Melania Trump juzi jijini Washington, D.C. Anna Henga anakuwa ni Mtanzania wa pili kutunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya Mwanamke Jasiri, akifuata nyayo za Vicky Ntetema aliyepata tuzo hii mwaka 2016. (Picha: Ubalozi wa Marekani)

MWENYEKITI UVCCM TAIFA AFANYA ZIARA NA KUKAGUA UJENZI WA CHUO CHA CHAMA KIBAHA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MWENYEKITI wa UVCCM taifa Heri James leo amefanya ziara na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi chuo cha chama kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani. Mradi wa ujenzi wa chuo hicho uliwekwa jiwe la msingi na Rais Dkt. John Magufuli na hadi sasa umekamilika kwa asilimia 50 na hadi kufikia June 2020 mradi huo utakamilika.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo James amewataka vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali ya awamu ya tano na kueleza kuwa hadi sasa zaidi ya vijana 400 wameajiriwa kupitia miradi hiyo huku Katibu mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally akitoa fursa kwa vijana kutoa mawazo yao kupitia umoja wao wa vijana.

Makamu Mwenyekiti UVCCM, Subira mwita amewataka vijana kujiandaa kwa fursa Zitakazotokana na chuo hicho na ametoa mwito wa kuzingatia  usawa wa jinsia kwa kuhusisha na siku ya leo ya wanawake duniani. Kwa upande wake katibu mkuu UVCCM Mwalimu Mangwala amesema kuwa mradi huo umewalenga vijana na mafunzo yatakayotolewa ni kwa ajili ya kuwaandaa vijana katika kufahamu historia, itikadi na mwelekeo wa Chama.

Pia Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani Charangwa Makwillo ameushukuru uongozi wa UVCCM na serikali kwa ujumla kwa kutoa ajira zaidi ya 400 kwa vijana Mkoani humo. Imeelezwa kuwa Chuo hicho kitajenga wazalendo na viongozi wengi kutoka vyama dada vya MPLA, ANC,SWAPO na FRELIMO.
 Mwenyekiti wa UVCCM taifa Heri James (aliyesimama, mstari wa mbele)akizungumza na viongozi wa UVCCM Mkoa wa Pwani mara baada ya kuwasili Mkoani hapo na kukagua mradi wa ujenzi wa Chama, Leo Kibaha Pwani.
 Mwenyekiti wa UVCCM taifa Heri James akiwasikiliza wakandarasi wa mradi huo ambao umekamilika kwa asilimia 50, na amewataka vijana kuchangamkia fursa hizo zinazotolewa kwa ajili yao kupitia umoja wao wa vijana (UVCCM) leo Kibaha, Pwani.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani Charangwa Makwillo (aliyesimama kushoto) akitoa maelezo ya mradi kwa Mwenyekiti wa UCCCM taifa Heri James mara baada ya kukagua ujenzi wa mradi wa chuo cha Chama Mkoani humo, Makwillo amekishukuru Chama cha Mapinduzi kupitia umoja wa vijana kwa kutoa ajira 400 kwa vijana Mkoani humo, Leo Mkoani Pwani.

Sakata la Chuo cha Diplomasia lahamia Takukuru

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji K. Mnyepe (kulia) akikabidhi ripoti za ukaguzi za Chuo cha Diplomasia, kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (PCCB), Bw. Diwani Athumani kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa tuhuma za ubadhilifu wa fedha uliofanywa na baadhi ya viongozi wa chuo hicho. Makabidhiano hayo yalifanyika leo kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar Es Salaam. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia, Balozi Ombeni Sefue akishuhudia makabidhiano ya ripoti za ukaguzi ambazo zimeainisha ubadhilifu wa fedha katika Chuo cha Diplomasia. 
Balozi Sefue (kushoto), Dkt. Mnyepe na Bw. Diwani wakibadilishana mawazo kuhusu utendaji kazi wa Chuo cha Diplomasia. 
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Diwani Athumani akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia, Balozi Ombeni Sefue. 

Wanawake Watakiwa kubadili fikra kujikwamua

$
0
0
Wanawake wametakiwa wametakiwa kubadili fikra na kujikwamua kimtazamo, kiuchumi, kisiasa, kijamii pamoja na kuhakikisha wanazingatia upatikanaji wa lishe bora ili kuwa na taifa lenye afya bora kwa familia zao na jamii kwa ujumla

Rai hiyo imetolewa leo na Afisa Maendeleo ya Jamii, mkoa wa Arusha katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, yaliofanywa na halmashauri ya Arusha, kwenye viwanja vya shule ya sekondari Enaboishu kata ya Moivo 

Akizungumza wakati wa sherehe hizo, mgeni rasmi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii, mkoa wa Arusha, Irene Mateu amewataka wanawake hao, kubadili fikra na mitazamo yao, na kutumia fursa zinazotolewa na serikali na wadau mbalimbali ili kujikwamua wenyewe katika sekta zote na kutekeleza majukumu yao kama wanawake.

Wanawake wameaswa kutambua kuwa wao ndio msingi wa mabadiliko katika jamii na endapo watabadili fikra na mitazamo yao kuwa chanya, dhahiri kutakuwa na taifa bora lisilo na ukatili na udhalilishaji wa wanawake, na kutokomeza tatizo la ndoa na mimba za utotoni, na ukeketaji kwa wanawake

Amewataka wanawake kutumia majukwaa katika maeneo yao kubadilishana mawazo, katoka nyanja mbalimbali kusimama imara kupinga na kuwafichua watu wanaofanya ukatili wa kijinsia na wale waliofanyiwa ukatili, ili kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto na sio kuungana nao kuwaficha wahalifu hao.

" Inatupasa kutambua, wanawake ndio msingi wa mabadiliko kwenye jamii, kama wanawake tutabadili fikra zetu na kutekeleza majukumu yetu kwa usahihi, kuanzia ndani ya familia zetu, jamii zatu zitabadika pia, hakutakuwa na ukatili na udhalilishaji kwa wanawake na watoto, watoto wetu hawatakeketwa wala ndoa na mimba za utotoni hazitakuwepo" alisema

Kwa upande wake Diwani wa Viti Maalum, Mhe. Yasimin Bachu amesema kuwa, imefika wakati sasa wanawake kuchukua hatua la haraka kuhakikisha familia na jamii zao, zinapata lishe bora pamoja na ufanyaji wa mazoezi ya mara kwa mara ili kuimarisha afya na kuepuka magonjwa yasiyoambukiza. 

Getrude Darema akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, Afisa Maendeleo ya Jamii na Jinsia, Halmashauri ya Arusha, amesema kuwa, halmashauri hiyo imefanya maadhimisho hayo, huku ikiwa na mafanikio makubwa katika kuwawezesha wanawake kiuchumi, jumla ya wanawake wajasiriamali 395 kwenye vikundi 45, kwa kuwapatia mikopo ya bila riba, yenye thamani ya shilingi milioni 243, fedha zinazotokana na asilimia 4 za mapato ya ndani kwa mwaka huu wa fedha 2018/2019.

Hata hivyo Getrude, amesema kuwa halmashauri inatarajia kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 80 kwa vikundi nane zaidi hadi kufikia mwishoni mwa wiki hii na kuwahimiza wanawake kutumia vyema fursa hiyo kwa kuanzisha miradi ya kibiashara itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi na si vinginevyo.

Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ya "Badili Fikra Kufikia Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu" yamekwenda sambamba na maonesho mbalimbali ya biashara kwa wajasiriamali wanawake, upimaji wa afya kwa magonjwa yanayoambukizwa na yasiyoambukizwa bure, burudani mbalimbali, mashindano ya mchezo ya kuvuta kamba na kufukuza kuku, pamoja na mafundisho ya uandaaji wa chakula lishe.

Na. Vero Ignatus Arusha

WANAWAKE TANESCO WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0
Wafanyakazi wa Tanesco wakishiriki katika maandamano ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa jijini Dodoma.
MACHI 8 ya kila mwaka ni siku ya wanawake Duniani, wanawake wengi hasa wa mijini huadhimisha siku hii kwa maandamano na kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kusaidia wanawake wenzao katika jamii.

Maadhimisho ya mwaka huu yana kauli mbiu inayosema “Badili Fikra Kufikia Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu”
Rais John Magufuli wakati akiagana na mgeni wake Rais Paul Kagame wa Rwanda alituma salamu za heri kwa wanawake wote nchini.

Rais Magufuli amewatumia salamu za pongezi wanawake wote Tanzania na kusema serikali ina thamini na kutambua mchango mkubwa wa Wanawake wa Tanzania. 
Wanawake wa Shirika la Umeme nchini TANESCO ni miongoni mwa wanawake waliojitokeza kwa wingi katika kuadhimisha siku hii sawa na wanawake wenzao katika maeneo mbalimbali nchini na Duniani.

Tanesco makao Makuu jijini Dodoma ilishiriki maadhimisho hayo kwa kuanza na maandamano na kisha katika shughuli zingine zilizopangwa kufanyika katika maadhimisho hayo. 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira ,Anthony Mavunde amewaasa wanawake kudumisha upendo na umoja katika kushiriki shughuli za maendeleo nchini kwa kushikamana pamoja bila kujitenga.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 08, 2019 katika Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama.

Naibu Waziri alibainisha miongoni mwa changamoto zinazokwamisha maendeleo ya wanawake ni pamoja na kukosekana kwa umoja, upendo na ushirikiano ambao unawaga katika makundi na kusababisha wanawake kutokuwa na maendeleo ya pamoja.

“Niseme ukweli japokuwa hamtaupenda kwa leo, miongoni mwa sababu zinazowakwamisha katika kuendelea ni tabia ya chuki miongoni mwenu, umbeya na makundi yasiyoleta tija za kimaendeleo,”alieeza Mavunde

Aliongezea kuwa, wanawake wanapaswa kubalidi mitazamo na tabia ambazo zinawaga na kuondoa upendo kati yao na kujikuta wanajitenga hivyo, kupunguza nguvu kazi ya pamoja katika uzalishaji na kuchangia kusuasua kwa maendeleo yao.Aidha Mavunde alieleza kuwa, kwa kuzingatia mchango wa wanawake katika kuleta maendeleo nchini ni vyema wakaishi kwa upendo na umoja ili kufikia malengo ya kuwa na Tanzania ya Viwanda.

“Kimsingi wanawake ni nguzo imara inayotegemewa na Taifa kwa kuzingatia uthubutu na namna Mungu alivyowapa roho ya kuvumilia na kuwaamini katika utendaji wenye uadilifu,”alisisitiza Mavunde.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akihutubia wanawake walioshiriki wakati wa Maadhimishi ya Siku ya Wanawake Duniani Mchi 8, 2019 katia Viwanja vya Mashujaa Dodoma yenye Kauli mbiu isemayo “Badili Fikra Kufikia Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu”
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa katika maandamano ya kuadhimishi siku ya Wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Viwanja vya Mashujaa Dodoma. 
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho hayo. 

Kikundi cha bendi ya JUKIMSI wakionesha umahiri wao wa kuimba wakiwa katika gari maarufu kwa jina la “kijiko” wakati wa maadhimisho hayo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akiangalia moja ya mfuko ulioshoinwa kwa kitengo na kikundi cha Angel kutoka Dodoma wakati wa maadhimisho hayo.
Viewing all 109934 articles
Browse latest View live




Latest Images