Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

KIWANDA CHA BORA CHAWAKA MOTO JIJINI DAR

$
0
0

Kiwanda cha Bora kilichopo barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam kimetetea kwa moto, uliowaka tangu saa 10 alfajiri leo. Jeshi la Zima Moto linaendelea na jitihada za kuzima moto huo, lakini chanzo cha moto huo bado  hakijafahamika. 
 Baadhi ya Wananchi wakishuhudia tukio hilo


PROF. KABUDI AFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA WA HAKI ZA BINADAMU WA UMOJA WA MATAIFA BI. MICHELLE BACHELET JERIA

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi na ujumbe wake katika picha ya pamoja na Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Bi. Michelle Bachelet Jeria na ujumbe wake baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika Mjini Geneva nchini Uswisi Februari 27, 2019.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi na ujumbe wake (kushoto) wakizungumza na Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Bi. Michelle Bachelet Jeria na ujumbe wake (kulia). Mazungumzo hayo yalifanyika Mjini Geneva nchini Uswisi Februari 27, 2019
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi na ujumbe wake katika mazungumzo na Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Bi. Michelle Bachelet Jeria na ujumbe wake Mjini Geneva nchini Uswisi Februari 27, 2019


Waziri wa Katiba na Sheria,Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Bi. Michelle Bachelet Jeria Mjini Geneva, Uswisi.

Prof. Kabudi amekutana na Kamishna wakati akihudhuria Kikao cha 40 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kinachoendelea Mjini Geneva-Uswisi. 

Katika mazungumzo yao Kamishna Bachelet alitaka kujua kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu haki za binadamu nchini hususan haki za kina mama na watoto, makundi maalum na kwa jinsi gani Baraza hilo la Mataifa linaweza kuisaidia Tanzania kuendelea kukuza, kudumisha na kulinda haki za binadamu nchini.

Akizungumza katika mazungumzo hayo Prof. Kabudi alisema licha ya Serikali kuendelea na mikakati mbalimbali ya kulinda na kukuza haki za wanawake, imeendelea kutoa fursa kwa wanawake kupata nafasi za uongozi wa juu Serikalini na kwenye taasisi mbalimbali za umma ambazo zinawawezesha kushiriki katika utoaji wa maamuzi yenye manufaa kwa nchi. 

Prof. Kabudi alisema Tanzania inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari na uwepo wa vyama vya siasa na demokrasia nchini na kuongeza kuwa mwaka huu inatarajia kufanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utafuatiwa na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2020. 

Prof. Kabudi alimhakikishia Kamishna Bachelet kuwa Tanzania itaendelea na jitihada za kukuza, kuheshimu na kulinda haki za binadamu nchini pamoja na kutekeleza wajibu wake na ahadi zake mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa. 

Aidha Prof. Kabudi alielezea jitihada zinazofanwa na Serikali kwenye maeneo ya elimu, afya, mapambano dhidi ya rushwa na dawa za kulevya pamoja na malengo ya kuleta maendeleo nchini. 

Prof. Kabudi alisema Serikali imeboresha mfumo wa ukusanyaji kodi na hivyo kuiwezesha Serikali kutoa huduma za kijamii kwa wananchi wake bila ubaguzi. 

Mhe. Kabudi alimshukuru Kamishna Bachelet kwa ushirikiano uliopo kati ya Ofisi yake na Wizara ya Katiba na Sheria na Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Mjini Geneva-Uswisi na kwamba Serikali kwa ujumla itaendelea na mazungumzo kuhusu maeneo ambayo wataweza kushirikiana.

Ofisi ya Kamishna ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu iliundwa mwaka 1993 ili kusimamia ukuzaji na ulinzi wa haki za binadamu duniani. Ofisi ya Kamishna wa Haki za Binadamu pamoja na mambo mengine inazisaidia Serikali za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa kutoa mafunzo na utaalamu kwenye maeneo ya upatikanaji wa haki, mabadiliko ya sheria na masuala ya uchaguzi. Vile vile inazisadia Serikali za Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kutekeleza wajibu walionao kimataifa wa kulinda, kuheshimu na kukuza haki za binadamu.

WAAJIRI WANAOKWAMISHA USHUGHULIKIAJI WA RUFAA ZA MASHAURI YA WATUMISHI WA UMMA KUCHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi kati yake na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma, kilichofanyika Ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji Mstaafu, Dkt. Stephen Bwana.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akizungumza  na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma kabla ya kuanza kikao kazi kati yake na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma, Ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.


Naibu Katibu, Tume ya Utumishi wa Umma, Bi. Rosy Elipenda akitoa neno la shukrani kwa niaba ya watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma wakati wa kikao kazi kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma, kilichofanyika Ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.


 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akisalimiana na Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bi. Immaculate Ngwale alipowasili Ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam kuzungumza na watumishi wa Tume hiyo.

 Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji Mstaafu Dkt. Stephen Bwana akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) kuzungumza na watumishi wa Tume wakati wa kikao kazi kilichofanyika Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Katibu, Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Richard Odongo.

 Kaimu Katibu, Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Richard Odongo akitoa neno la utangulizi wakati wa kikao kazi kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma kilichofanyika Ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.






Serikali ya Awamu ya Tano kuendelea kulinda na kutetea Haki za Binadamu-Prof. Kabudi aliambia Baraza la Haki za Binadamu la UN

$
0
0

Waziri wa katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akihutubia Kikao cha 40 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kinachofanyika jijini Geneva nchini Uswisi
Mhe. Prof. Kabudi alipata fursa pia ya kuzungumza na Kundi la Mabalozi kutoka nchi za Afrika waliopo Geneva kama anavyoonekana pichani
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (wa nne kulia) akiwa katika picha  ya pamoja na baadhi ya maafisa wa Tanzania mara baada ya kuhutubia kikao hicho cha Baraza la Haki za Bianadamu kinachofanyika Geneva, Uswisi.

=====================================================

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amesema Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kukuza na kulinda haki za binadamu na ustawi wa jamii kama kipaumbele chake na  itaendelea kushirikiana na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuhakikisha haki za binadamu nchini na duniani kote zinadumishwa.

Prof. Kabudi amesema hayo jana alipohutubia Kikao cha 40 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kinachofanyika jijini Geneva nchini Uswisi. Prof. Kabudi amesema Serikali ya Tanzania imelenga pamoja na mambo mengine kuimarisha haki za binadamu, utawala bora na utii wa sheria nchini na kuondoa ukatili dhidi ya wanawake, watoto na watu wenye ulemavu. 


Serikali imelenga kuimarisha haki za binadamu, utawala bora, utii wa sheria na kuondoa ukatili dhidi ya wanawake, watoto na watu wenye ulemavu, kwa sasa tunatekeleza mpango mkakati wa kitaifa wa kuondoa ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa mwaka 2017/18 - 2021/22, lengo likiwa ni kulinda na kudumisha haki za wanawake, watoto na watu wenye ulemavu,” alisema Prof. Kabudi.

Amesema Serikali pia inazingatia suala la kuwapatia haki kwa haraka wananchi wasio na uwezo kwa kutolea maamuzi kwa haraka mashauri yanayowahusu watu wasio na uwezo na kuwapatia msaada wa kisheria kupitia utekelezaji wa Sheria ya Msaada wa Kisheria ya mwaka 2017 ili wananchi hao waweze kupata haki zao kwa wakati. 

Aidha, Prof. Kabudi amelihakikishia Baraza hilo kuwa Serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na vyombo vya habari nchini na imeendelea kuhakikisha uhuru wa vyombo hivyo unalindwa huku jumla ya vituo vya redio 152, televisheni 34, magazeti 172  nchini kote yamesajiliwa na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira stahiki yatakayowezesha vyombo vya habari kufanya kazi zao kwa uhuru.

Ameongeza kuwa Serikali imedhamiria kuleta ustawi wa jamii kwa kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo ikiongozwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 na kunadi kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuhakikisha kuwa haki ya kupata elimu, afya na maji zinawafikia wananchi wote. 

“Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuhakikisha kuwa haki ya kupata elimu, afya na maji zinawafikia wananchi wote na kuongeza kuwa Serikali inatumia zaidi ya Shilingi Bilioni 23 kwa mwezi kutoa elimu pasipo malipo na hivyo kuongeza udahili wa watoto wanaojiunga darasa la kwanza kwa asilimia 35.2 na asilimia 20.1 kwa wanaojiunga na kidato cha kwanza,” alisema. 

Prof. Kabudi pia amesema Serikali imedhamiria kufikisha huduma za afya karibu na watanzania wote ambapo imeongeza bajeti ya afya kutoka Shilingi bilioni 31 mwaka 2015/2016 hadi Shilingi bilioni 269 mwaka 2017/2018 na kuongeza kuwa Serikali inatekeleza mikakati ya kujenga vituo vya afya ambapo hadi sasa imejenga vituo 304, na nyumba za watumishi wa afya 578 zimejengwa nchini kote.

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ni chombo cha Umoja wa Mataifa chenye jukumu la kukuza na kulinda haki za binadamu duniani kote na kushughulikia uvunjwaji wa haki za binadamu unaotokea katika nchi wanachama wa umoja huo na kushauri hatua za kuchukuliwa ili kuboresha haki za binadamu duniani. 

Baraza hilo pamoja na mambo mengine linatarajia kupokea taarifa mbalimbali kuhusu haki za binadamu duniani na kutoa nafasi kwa viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kutoa maelezo yao kuhusu utekelezaji wa wajibu wao wa kulinda na kukuza haki za biandamu katika nchi zao.

MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI ATEMBELEA MRADI WA RELI YA KISASA SGR KUTOKA KITO CHA ILALA HADI KILOSA

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) jijini Dar es salaam, kabla ya kuanza ziara ya kutembelea Mradi huo kutoka kituo cha Ilala hadi kituo cha Kilosa mkoani Morogoro. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiangalia sehemu ya reli ya Kisasa SGR iliyokamilika wakati alipofanya ziara ya kutembelea mradi huo kutoka kituo cha Ilala hadi kituo cha Kilosa mkoani Morogoro. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiwasilia katika kituo cha Soga kilichopo mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuona namna mataluma ya reli yanavyotegenezwa katika kituo hicho wakati alipofaya ziara ya kutembelea Mradi wa Reli ya Kisasa SGR kutoka kituo cha Ilala hadi kituo cha Kilosa mkoani Morogoro. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa (kushoto) akimuelezea jambo Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, kuhusiana na Mradi wa Reli ya kisasa SGR, wakati alipofanya ziara ya kutembelea Mradi huo unaojegwa na Kampuni ya Yapi Merkezi. Picha na Jeshi la Polisi.


SHINDA MTAJI NA BIKO ,MAMILIONEA SITA NA BODA BODA

Hatima ya Rufaa ya Mbowe na Matiku kujulikana kesho Machi Mosi

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
MAHAKAMA ya Rufani kesho Machi Mosi, 2019 inatarajia kutoa uamuzi wa rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko.

Katika uamuzi huo, mahakama inatarajiwa ama kukubali Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kuendelea kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mbowe na Matiko, kutokana na kufutiwa dhamana katika kesi ya uchochezi iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu au kuitupilia mbali rufaa hiyo.

 Mapema Leo Februari 28.2019  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kesi  ya uchochezi  inayowakabili vigogo hao na  wenzao saba wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), iliitwa kwa ajili ya kutajwa na
 Wakili wa Serikali, Wankyo Simon akadai kuwa bado wanasubiri hatua za rufaa zilizopo Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu.

Hata hivyo, Wakili wa Utetezi, Profesa Abdallah Safari alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi kuwa ni muhimu mahakama ikapewa taarifa ya maendeleo ya rufaa zote na kwamba wao wamepata taarifa kuwa kesho  Mahakama ya Rufaa itatoa uamuzi dhidi ya rufaa hiyo

Wakili Wankyo alipoulizwa  alidai kuwa yeye bado hajapata taarifa kuhusu uamuzi huo na kwamba hata kama isingekuwa hivyo bado wanaomba tarehe ya kutajwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 14, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Uamuzi huo wa rufaa  utatolewa na jopo la Majaji watatu likiongozwa na Mwenyekiti wao, Jaji Stella Mgasha, Mwanaisha Kwariko na Gerald Ndika  kutoa uamuzi huo baada ya Februari 18, mwaka huu kusikiliza rufaa hiyo iliyokatwa na DPP kupinga Mahakama Kuu kusikiliza rufaa ya kupinga kufutiwa dhamana iliyokatwa na wakina Mbowe.

Katika kesi hiyo, washitakiwa wengine ni Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu.

Katika kesi ya msingi, washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16, mwaka jana maeneo ya Dar es Salaam.

MSIBA WA RUGE WASABABISHA KESI YA HALIMA MDEE KUPIGWA KALENDA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  imeshindwa kuendelea na usikilizwaji wa kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kwa sababu shahidi abdu Chemba aliyetarajiwa kutoa ushahidi wake leo, ambaye ni mfanyakazi wa clouds amepata msiba.

Wakili wa Serikali, Ashura Mzava amedai hayo leo, Februari 28, 2019  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati  kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Amdedai katika kikao kilichopita mahakama ilimuonya shahidi  huyo Abdu Chemba, na kumtaka leo kuja mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi wa shauri hilo lakini tangu juzi aliomba udhuru kwamba  wanamsiba.

"Niliwasiliana na Chemba mimi mwenyewe hivyo tunaomba baada ya wiki mbili shahidi huyu aje kuendelea na usikilizaji pia tunaomba hati ya wito kwa mashahidi wengine," alidai Mzava.

Kufuatia taarifa hizo, Hakimu Simba amesema sababu zilizotolewa ni za msingi na ni udhuru ambao hauepukiki hivyo shahidi afike  na wengine ili kesi iishe.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 12 mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa na wito kwa mashahidi wote ili wafike kutoa ushahidi wao umetolewa.

Mpaka sasa  mashahidi watatu wa upande wa mashitaka wameshatoa ushahidi katika kesi hiyo akiwamo  Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Urafiki, Mrakibu wa Polisi (SP) Batseba Kasanga.

Katika kesi ya msingi imedaiwa, Julai 3, 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema zilizopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Mdee alitamka maneno dhidi ya  Rais John Magufuli kuwa,  ‘anaongea hovyo, anatakiwa  afungwe breki,’ kitendo kinachodaiwa kuwa ni kumdhalilisha Rais na kusababisha uvunjifu wa amani.

DStv yaja na ofa ya kuwapandisha wateja wake daraja

$
0
0
Kampuni ya MultiChoice Tanzania kupitia huduma zake za DStv imetangaza tena ofa mpya na kabambe kwa wateja wake inayojulikana kwa jina la  “Step Up”  ambapo mteja wa DStv atatakiwa kufanya malipo ya mwezi ya kifurushi cha juu ya kile anachotumia  na kisha kupatiwa  kifurushi cha juu zaidi ya kile alicholipia kwa kipindi cha mwezi mzima bila malipo ya nyongeza.

Akizungumza wakati wa kutangaza ofa hiyo Meneja Uendeshaji wa kampuni ya MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo alieleza kuwa Ofa ya‘Step Up’ ni kampeni maalum kwa wateja wa DStv yenye lengo la kuwatunuku wateja wanaolipia kifurushi cha juu ya kile anachotumia.  Wateja wa vifurushi vya Bomba, Family na Compact watakaolipia kifurushi kinachofuatia juu yake watatunukiwa kufurushi cha juu zaidi. Kwa mfano, mteja wa Bomba akilipia kifurushi cha Family atazawadiwa kifurushi cha Compact. Mteja wa Family akilipia Compact anapata kifurushi cha Compact+ na yule wa Compact akilipia Compact+ anapewa kifurushi cha Premium”, alisema Shelukindo.

Aliongeza kuwa” Kampeni hii ya “Step Up” itadumu kwa kipindi cha muda wa miezi miwili kuanzia tarehe 1 March 2019 hadi tarehe 30 Aprili 2019 na itawahusisha  wateja wa Wateja wote ambao akaunti zao hazijakatika vifurushi vya Bomba, Family pamoja na kile cha Compact.
 Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo akitangaza rasmi promosheni maalum ya kuwapandisha daraja wateja wa DStv ambapo mteja akilipia kifurushi cha juu yake huzawadiwa kifurushi cha cha juu ya kile alicholipia. Promosheni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi miwili itaishia mwisho wa mwezi wanne.
  Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria akielezea  promosheni maalum ya kuwapandisha daraja wateja wa DStv ambapo mteja akilipia kifurushi cha juu yake huzawadiwa kifurushi cha cha juu ya kile alicholipia. Promosheni hiyo itaanza inaanza rasmi tarehe 1 Machi na itaendelea kwa muda wa miezi miwili.  Kulia ni Meneja Uhusiano Johnson Mshana na katikati ni Meneja Uendeshaji Ronald Shelukindo.
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana akieleza kuhusu promosheni maalum ya kuwapandisha daraja wateja wa DStv ambapo mteja akilipia kifurushi cha juu yake huzawadiwa kifurushi cha cha juu ya kile alicholipia. Promosheni hiyo itaanza inaanza rasmi tarehe 1 Machi na itaendelea kwa muda wa miezi miwili

Dkt. Amani Abeid Karume ahutubia mkutano wa amani wa Global Peace Convention jijini Seoul, Korea

$
0
0
  Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume akihutubia katika mkutano wa  amani uitwao Global Peace Convention jijini Seoul.
Mkutano huu unaofanyika  kila baada ya miaka 2, umekuwa ukizunguka nchi mbalimbali duniani. Mwaka huu mkutano huo umefanyika nchini Korea ili kuhamasisha Korea Kusini na Korea Kaskazini waondoe tofauti zao na kuwa wamoja (OneKorea).

Dkt. Karume, ambaye ni moja wa wazungumzaji wakuu katika kujadili maswala ya violent extremism and radicalisation (misimamo mikali inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani, ameeleza matumaini yake kwamba iko siku kutakuwa na Taifa la Korea Moja.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkazi wa Global Peace Tanzania Bi. Martha Nghambi, Watanzania mbalimbali wanashiriki kwenye mkutano huo akiwema mke wa Dkt. Karume, Mama Shadya Karume, ambaye ameongozana naye. 
Bi. Nghambu amesema Mkutanio huu unatarajiwa kufungwa Februari 1, mwaka huu.

 Mama Shadya Karume akiwa na washiriki wengine kwenye mkutano huo
 Sehemu ya wshiriki wa mkutano wa amani wa Global Peace Convention jijini Seoul.
 Sehemu ya wshiriki wa mkutano wa amani wa Global Peace Convention jijini Seoul.
 Sehemu ya wshiriki wa mkutano wa amani wa Global Peace Convention jijini Seoul.
 Sehemu ya wshiriki wa mkutano wa amani wa Global Peace Convention jijini Seoul.
Mkurugenzi Mkazi wa Global Peace Tanzania Bi. Martha Nghambi akiwa katika mkutano huo wa amani wa Global Peace Convention jijini Seoul.
 akiwa katika mkutano huo wa amani wa Global Peace Convention jijini Seoul.
Bi Shamira Mshangama  akiwa katika mkutano huo wa amani wa Global Peace Convention jijini Seoul.
Bi Emma Kawawa akiwa katika mkutano huo wa amani wa Global Peace Convention jijini Seoul.

Jumia na Xiaomi kushirikiana kukuza ueneaji simu janja Afrika

$
0
0
 Kushoto ni Makamu Mkuu wa Rais wa Jumia, Bw. Romain Christodoulou pamoja na Bw. Wang Xiang (kulia), Makamu Mkuu wa Rais wa kampuni ya Xiaomi wakiweka sahihi wakati wa makubaliano ya biashara katika Kongomano Kuu la Simu Duniani lililofanyika jijini Barcelona, Hispania mnamo Februari 27, 2019. 
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Vifaa vya Kielekroniki vya Wateja wa Jumia, Sandeep Narayanan, Makamu Mkuu wa Rais wa Jumia, Bw. Romain Christodoulou, Makamu Mkuu wa Rais wa kampuni ya Xiaomi, Bw. Wang Xiang, pamoja na Makamu wa Rais wa Xiaomi, Wang Lingming wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuingia makubaliano katika Kongomano Kuu la Simu Duniani lililofanyika jijini Barcelona, Hispania mnamo Februari 27, 2019.


· Ushirikiano huu unaifanya Xiaomi kuingia rasmi kwenye soko la mtandaoni barani Afrika kupitia Jumia, na kuwapatia fursa ya kipekee mamilioni ya wateja kuzifikia bidhaa za Xiaomi.

kampuni inayoongoza barani Afrika kwa kuuza bidhaa mtandaoni, imesaini mkataba muhimu wa ushirikiano wa kibiashara na kampuni inayoongoza kiteknolojia ya Xiaomi katika Kongamano Kuu la Simu Duniani (the Mobile World Congress) jijini Barcelona nchini Hispania, na kuwapatia fursa ya kipekee mamilioni ya Waafrika kuzifikia kwa urahisi bidhaa za Xiaomi.

Kupitia ushirikiano huu, Jumia itafungua duka maalum la Mi mtandaoni kwake na kuipatia Xiaomi fursa ya kuwafikia mamilioni ya wateja walioko mtandaoni katika nchi takribani 14 barani kote, wakati huo huo Jumia itaitambulisha rasmi simu aina ya Redmi Go (1GB + 8GB) mahsusi kwa Afrika na bidhaa nyinginezo nyingi ndani ya mwaka huu. Ushirikiano huu utapewa nguvu na juhudi za pamoja baina ya pande mbili za shughuli za kimasoko kwa mwaka wote wa 2019, kwa kutumia uwezo wa Jumia kwa kidigitali pamoja na wa kimasoko wa Xiaomi, ikijumuisha jamii ya mashabiki wa Mi. Hii ni hatua ya kwanza muhimu yenye kutia matumaini katika ushirikiano wa karibu baina ya makampuni haya mawili kwa miaka mingi ijayo.

“Ushirikiano huu ni muhimu sana kwetu, kwa kuwa ni dhahiri utakuza matumizi ya simu janja Afrika na kusaidia kuenea kwa manunuzi ya njia ya mtandaoni. Jumia na Xiaomi zote zina vinasaba sawa vya mtandao wa intaneti hivyo basi zitakuwa na kusudio moja: kutoa simu za kisasa zenye ubora wa hali ya juu na gharama nafuu huku ikiwapatia wateja namna ya kipekee ya kufanya manunuzi. Hii itazinufaisha kampuni zote mbili na zaidi ni wateja wote barani Afrika,” amesema Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok Prescott, akielezea juu ya ushirikiano huo.

“Tunaamini kwenye kufanya kazi na makampuni ambayo yana maadili sawa nasi na tunayofuraha kushirikiana na Jumia kuwafikia mashabiki wengi zaidi wa Mi Afrika nzima,” amesema Wang Xiang, Makamu Mkuu wa Rais wa Xiaomi. “Mfumo wa kuuza bidhaa kwa njia ya mtandaoni ni sehemu ya Xiaomi na tunaamini ya kwamba kufanya kazi na Jumia kutatusaidia kuleta ubunifu kwa kila mtu barani Afrika.” 

Afrika imeshuhudia kukua kwa kuingia bidhaa za kiwango cha gharama nafuu kutoka kwa makampuni ambayo yamejikita zaidi katika bei hususani kutokea China, kitu pekee ambacho ni muhimu katika kukuza matumizi ya simu za kisasa barani. Takwimu zinaonyesha kuwa ueneaji

wa simu za kisasa Afrika ulikuwa 36% kwa mwaka 2018, huku idadi hiyo inatarajiwa kufikia 66% kufikia mwaka 2025.

Balozi wa Tanzania nchini Oman Mhe. Abdallah Kilima alonga

BASATA LATEKELEZA AGIZO LA MWAKYEMBE, DUDUBAYA AONJA JOTO OYSTERBAY POLISI

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
MWANAMUZIKI wa miondoko ya Bongofleva  Godfrey Tumaini a.k.a ‘Dudu Baya' anashikiliwa na  jeshi la polisi katika kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Michuzi Blog Kamanda wa polisi Kinondoni, Mussa Taibu ameweka wazi kwa sasa Dudubaya anashikiliwa kwa mahojiano.

Hii ni kufatia agizo alilolitoa jana  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa (BASATA) kuhakikisha linamchukulia hatua kali Dudu Baya.

Pia Mwakyembe aliweka wazi sababu za kumchukulia hatua mwanamuziki huyo kutokana na makosa ya kumkashifu, aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji (Clouds Media Group) Marehemu Ruge Mutahaba.

Baada ya amri hiyo, Basata na jeshi la polisi limeweza kumfikisha Dudu Baya kituo cha polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Sanjari na hilo Mwanamuziki huyo anakabiliwa na kwa makosa ya matumizi mabaya ya mtandao.

H-TOWN OLD SCHOOL REUNION USIPIME MTANANGE WA SIMBA NA YANGA KUPIGWA JUMAMOSI

$
0
0

HOTELS HOUSTON KARIBU NA UKUMBI
-Palace Inn                                         
9317 W Sam Houston Pkwy   
Houston, TX 77099
Ph # 713 777 4622

-Holiday Inn
11160 South Fwy
Houston, TX 77031
Ph # 281 530 1400

-Scottish Inns & Suites
9610 W Houston Pkwy S,
Houston, TX 77099
Ph # 281 564 9100

-Frontier Inn
11230 Southwest Fwy,
Houston, TX 77032
Ph # 281 496 9000

-Symphony Inn & Suites
11744 Southwest Fwy,
Houston, TX 77031
Ph # 281 933 5550

-Comfort Inn Southwest
11230 Southwest Fwy,
Houston,TX 77031
Ph # 281 498 9000

Courtyard By Marriott
12655 Southwest Fwy,
Stafford,TX 77477
Ph # 281 491 7700

Comfort Suites
7707 W Sam Houston Pkwy S,
Houston, TX 77072
Ph # 713 774 7707

-Hilton Garden Inn
6855 W Sam Houston Pkwy S,
Houston, TX 77072
Ph # 713 270 6100

-Home 2 Suites by Hilton
11121 Fountain Lake Dr,
Stafford, TX 77477
Ph# 346 309 2240

-Comfort Inn & Suites
11050 Southwest Fwy,
Houston, TX 77074
Ph # 281 568 6969

-Crowne Plaza Houston
9090 Southwest Fwy,
Houston, TX 77074
Ph# 713 995 0123

JK AHANI MSIBA WA RUGE MUTAHABA MIKOCHENI JIJINI DAR LEO

$
0
0
Rais wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Kikwete akitia saini daftari la waombolezaji katika msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji Vipindi wa Clouds  Media Group Ruge Mutahaba aliyefariki Nchini Afrika Kusini,Pichani kushoto ni Mke wa Rais Mstaafu Salma Kikwete na kulia ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza na 
Rais Dkt Jakaya Kikwete akiingia katika Msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji Vipindi wa Clouds Ruge Mutahaba aliyefariki Nchini Afrika Kusini.
 Baadhi ya wabunge na viongozi wa kisiasa waliofika siku ya leo katika Msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi wa Clouds Ruge Mutahaba aliyefariki Nchini Afrika Kusini.
 Baadhi ya vijana wa THT wakiimba wimbo wa uombolezaji katika msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi wa Clouds Ruge Mutahaba aliyefariki Nchini Afrika Kusini
 Picha ya vijana wa THT wakiimba wimbo wa uombolezaji katika msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Ruge Mutahaba aliyefariki Nchini Afrika Kusini.

Nimemjua Ruge miaka 20 iliyopita Dkt.Kikwete

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Rais wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete amesema kuwa alikuwa karibu sana kati ya Ruge Mutahaba pamoja na Joseph Kusaga.

Kikwete ameyasema hayo alipokuwa katika msiba wa uombolezaji wa Ruge Mutahaba aliyefariki juzi nchini Afrika Kusini alipokuwa anapatiwa matibabu.

"Nimekuwa karibu kati ya Ruge na Joseph Kusaga "Zaidi ya miaka 20 nimekuwa nao karibu kama mshauri nimewaunga mkono katika shughuli mbalimbali"amesema Kikwete.

Amesema angekuwa na uwezo wa kifedha ningewapa ili waende haraka.Dkt Kikwete Wakati akianzisha THT tulikuwa pamoja kwa sababu ya kuwa Rais niliwaunga mkono.

Aidha amesema alikuwa akifuatilia kwa karibu sana akiwa Hospitali.
Katika shughuli za siasa vyombo vya habari ni muhimu.Nilivyoandika kuwa kupoteza mzalendo limetoka kwa dhati kwa ajili ya Ruge

Ruge alifanya kwa kunufaisha wengi na tujitahidi kuishi kwa mfano wake alikuwa yu tayari kujitolea kwa ajili ya wengi tuwaombee ndugu na wanae waishi kama baba yao.Mwenyezi Mungu amjalie mapunziko mema amina.Hata walipokuwa wakitofautiana kati ya Ruge na Joseph Kusaga walikuwa wanakuja na kuwasuluhisha.
Rais wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Kikwete akizungumza na waandishi habari kuhusu Maisha aliyoyaishi aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi wa Clouds Ruge Mutahaba

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS MTENDAJI MWANDAMIZI WA JICA KAZUHIKO KOSHIKAWA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais Mtendaji Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan (JICA) Bw. Kazuhiko Koshikawa (wa tatu Kushoto) na ujumbe wake walipokutana  Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 28, 2019. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya picha ya kuchora ya wanyama wakuu watano (Big Five)  Makamu wa Rais Mtendaji Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan (JICA) Bw. Kazuhiko Koshikawa alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 28, 2019. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya kinyago ja UJAMAA  Makamu wa Rais Mtendaji Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan (JICA) Bw. Kazuhiko Koshikawa alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 28, 2019. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na  Makamu wa Rais Mtendaji Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan (JICA) Bw. Kazuhiko Koshikawa (wa tatu Kushoto) na ujumbe wake baada ya kukukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 28, 2019. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Mtendaji Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan (JICA) Bw. Kazuhiko Koshikawa (wa tatu Kushoto) na ujumbe wake baada ya kukukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 28, 2019. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro.
PICHA NA IKULU

SOKO LA WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO LINALOWASAIDA WALAJI WA KAWAIDA.

$
0
0
Wafanyabiashara ndogo ndogo wakiendelea na biashara zoa zinazo wasaidia kujipatia riziki ya kila siku katika makutano ya Mtaa wa Utete na Uhuru Ilala jijini Dar es Slaam, Soko hilo limekuwa maarufu kwa uuzaji wa vyakula mbalimbali kwa bei nafuu kwa mlaji wa kawaida.
Wafanyabiashara ndogo ndogo wakiendelea na biashara zoa zinazo wasaidia kujipatia riziki ya kila siku katika makutano ya Mtaa wa Utete na Uhuru Ilala jijini Dar es Slaam, Soko hilo limekuwa maarufu kwa uuzaji wa vyakula mbalimbali kwa bei nafuu kwa mlaji wa kawaida.

DAVIDO KUIBEBA TENA BENDERA YA AFRIKA TUZO ZA NICKELODEON

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
MWANAMUZIKI nchini ya Nigeria David Adeleke, maarufu kama Davido amechaguliwa kushiriki kwa mara nyingine katika Tuzo za kimataifa  za Nickelodeon kwa mwaka huu.

 Miongoni mwa  wanamuziki wanaoshindanishwa na Davido katika tuzo hiyo kwenye kipengele cha Mwanamuziki anaependwa wa kimataifa ni pamoja na Taylor Swift, David Guetta na J Balvin kutoka amerika ya kusini 

Davido akiwa msanii mwenye umri wa miaka 26 kwa mwaka huu imekua fursa kwake kwa mara ya pili kushiriki katika tuzo hizo  kutoka Afrika huku akishindanishwa na wasanii kutoka mataifa mbalimbali.

Na usiku wa Tuzo hizo utapambwa Na Msanii djKhaleed ambae kwa msimu uliopita alijizolea  tuzo tatu ikiwemo tuzo ya rapa bora wa mwaka pamoja na Msanii bora wa mwaka kimataifa huku wimbo wa No brainer aliomshirikisha Msanii Justin Bieber kuibuka wimbo bora wa mwaka.

Pia wasanii ambao wamebahatika kuwepo kwenye vipengele tofauti tofauti katika tuzo ni Cardi B, Ariana Grande, Maroon 5, Camila Cabello ambao wanafanya vizuri kwa sasa kimataifa kwenye soko la muziki.

DKT NDUGULILE AMEITAKA JAMII KUTOWANYAYAPA WAGOJWA WA RARE DISEASE

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amewataka  wananchi kuacha kunyanyapaa wahanga wa magonjwa ya (rare disease), magonjwa yanayoathiri watu wachache ambayo ni Kuathirika kwa  ubongo,kuathirika kwa misuli inavyofanya kazi,uti wa mgongo na mengine mengi.

Dkt Ndugulile ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam  katika kumbukumbu ya siku ya siku ya Rare disease  duniani kote inayoadhimishwa kila ifikapo februari 28 kila mwaka, ambayo ilianza kuadhimishwa barani Ulaya na kuungwa mkono na nchi nyingi,  ambapo nchini Tanzania ilianza kuadhimishwa rasmi mnamo mwaka 2016.

Dkt Ndugulile amesema kuwa lengo la kuadhimisha siku hiyo ni kuhamasisha jamii  kuelewa kuhusu magonjwa hayo na athari zake, maana yake ni nini, na kutohusisha magonjwa hayo  na masuala ya kishirikina

Aidha naibu huyo amesema kuwa changamoto katika magonjwa hayo adimu duniani utambuzi wake kwa wakati umekuwa mgumu, matibabu yake pia ni magumu,vile vile matunzo mabovu ndani ya familia na jamii kwa ujumla.

"Serikali itaendelea kushirikiana na wananchi tutajadili yale muhimu, na niwapongeze wazazi ambao wanaendelea kusimamia haki za watoto"amesema Dkt Ndugulile.

Vile vile Sharifa Mbarak mzazi wa mtoto Ally ambaye ni mhanga wa magonjwa hayo amesema kuwa mwanae alianza kuumwa akiwa na miaka miwili na nusu lakini hakukata tamaa na matatizo ya mtoto wake,pia amekuwa akifuata ushauri  wa madaktari mpaka sasa alipofikia.

Sharifa amesema kuwa Matatizo hayo ya kupooza mwili yamepelekea Ally asiende shule ikiwa ana ndoto  nyingi sana Kama watoto wengine.

"Kutokana na uzoefu wangu nimepata msukumo na kuamua kujitoa kwa jamii ili wagonjwa walio na magonjwa haya na rai wenye mapenzi mema tujenge uelewa muhimu ili tuweze  kupaza sauti kwa pamoja"amesema bi Sharifa .

Hata hivyo Daktari  mfumo wa ufahamu kwa watoto MUHAS Edward Kija amesema kuwa  takwimu za magonjwa mengi yanayoathiri watu wachache katika 60,000 mmoja ndio ameathirika, na huweza kurithishwa  magonjwa hayo kutoka kwa wazazi wakati mtoto akiwa tumboni kwa mama katika hatua za ukuaji tatizo linapotokea mtoto anaweza akazaliwa na magonjwa hayo.

"Ili kuepuka magonjwa haya katika jamii ni kuhakikisha uelewa wa haya maradhi, kuhakikisha watu wanafahamu dalili za athari pamoja na kuboresha ufahamu na uelewa katika vituo vyetu vya afya"amesema Dkt Kija.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na  wadau mbalimbali leo wakati wa mahadhimisho ya siku ya ( Rare disease)  ni magonjwa mengi ambayo yanawapata watu wachache duniani Jijini Dar es Salaam.
 Sharifa Mbarak mzazi wa mtoto Ally ambaye ni mhanga wa magonjwa hayo akizungumzia leo Jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya rare disease  duniani jinsi ugonjwa huo alivyoupokea kwa kumuuguza mtoto wake ambapo ameonyesha kupambana bila kuchoka
Picha ya pamoja
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images